Tangazo kwa kanisa: Wanawake mliokoka, kanisani ni mahali pa kuabudu sio maonesho!

Naona kanisa linajisahau kila inapoitwa leo. Shukrani kwa kanisa la Roman Catholic kukataza mavazi yasiyofaa kanisani, makanisa ya kiroho sikuhizi yanashangaza sana, watu wamekuwa huru kweli kweli, wachungaji wa kike angalieni mnavyovaa, mavazi mengine yanawaingiza wengi katika mitego ya dhambi. 

–TN

Advertisements

9 thoughts on “Tangazo kwa kanisa: Wanawake mliokoka, kanisani ni mahali pa kuabudu sio maonesho!

 1. HATA WATUMISHI WANACHANGIA KWANI WAPO AMBAO HUSEMA ,UTAKASO WA MTU SIO KATIKA MAVAZI BALI NI KATIKA SADAKA UMTOLEAYO MUNGU,NA MOYO WA UKUNJUFU.BILA KUJUA KWAMBA PIA UENDAPO MBELE ZA BWANA MUNGU WAKO MWILI NA ROHO NA MAVAZI YENYE HESHIMA VYOTE UENDA MBELE ZA BWANA.TUWE MACHO NA WATUMISHI KAMA HAO KWAI WATATUINGIZA JEHANAM, KWA WAO KUOGOPA KUWAKOSA WAUMINI NA KUACHA KUKEMEA UOVU

 2. Mabinza,
  Heri ya mwaka mpya.

  Sikuwa nineona comment yako.

  Tatizo lako wewe ni moja; unashindwa kutulia vema kwenye mada. Focus yako kubwa unaielekeza kwenye wanawake kuwa wachungaji wakati mada haiko huko.

  Nilikuuliza maswali kadha wa kadha huko juu, lakini umeyapotezea.

  Ni vema ukatofautisha kanisa kwa maana ya mwili wa kristo na kanisa kwa maana ya jengo.

  Jengo halilazimiki kuwa takatifu ili kufanya Mungu atende kazi. Bali mtu kama kanisa ndiye hupaswa kuwa mtakatifu.

  Hujawahi kuona watu wanasalia kwenye kumbi za sinema na baa na Mungu anafanya mambo makubwa!!? Hizo kumbi si takatifu

  Kuna kitu mleta mada kakisema Kwa wanawake kuwa kanisani si mahali pa maonesho.
  Sasa suala la maonesho ni suala la nia. Kuna wanaovaa vazi fulani kwa nia ya kujionesha kwa watu, na kuna wanaovaa vazi hilohilo kwa nia ya kuvaa tu kupendeza.

  Kundi la kwanza likemewe la pili halina shida.
  Nabinza tafsiri ya vazi fulani huwa haitokani na vazi lenyewe, bali utamaduni wa jamii lilimovaliwa.

  Wanawake wakristo wakija siku moja wamevaa hijab nyeusi na kujifunika kininja sidhani kama ibada itaenda sawasawa kwa walio wengi, pamoja na kwanba vazi hilo hufunika mwili wote kabisa.

  Nikasema kuwa ni vema wanawake wavae mavazi yanayokubalika na jamii yetu, na mavazi hayo si lazima yawe marefu ama nafupi, bali ni yale yanayokubalika yawe marefu au mafupi.

  Halafu sidhani kama wanaume wanaosumbuliwa na mavazi ya kina mama kanisàni huwa hayawasumbui kazini, na mtaani kwa ujumla.

  Ifike mahali mwili na hisisia zake zisitutawale, bali tuvitiishe. Haiwezekani nitoe focus yangu kwenye ibada kanisani na kuipeleka kwa dada/ mama aliyevaa akaacha maziwa au mapaja nje. Nikiwa hivyo huko ni kutawaliwa na mwili.

  Mabinza pamoja na wanaume wenzangu wote, tuache uzembe na kasumba ya kuuacha mwili utupeleke unavyotaka wenyewe.

  We are the boss over the flesh, not the flesh over us!!!

 3. Sungura,

  Sidhani kama iko haja ya kubishana, jambo liko wazi, mwandishi anasema mambo mwawili, moja, kutovaa mavazi ya staa kwa wanawake huko makanisani; Lakini la pili ni kuwa, kuna wachungaji wa kike wanaovaa nusu uchi, ambapo kwa kitendo hicho wanasababisha majaribu. Soma mada mpaka mwisho bro; kwa hiyo, hicho ndicho kilichonifanya kusema kama nilivyosema katika mchango wangu uliotangulia hapo juu.

  Nikirudi kwako juu ya mchango wako “ukimwadress” Furaha, nakuona wazi kuwa unaongelea ushabiki, au kama sivyo, basi huenda hujui kabisa kinachoendelea Duniania kati ya wana wa Mungu na wana wa shetani! Mtu mwelewa hawezi kusema “Kanisani” si pahali pa takatifu, labda hulijui “Kanisa” ni nini. Mugonjwa huenda hospital, hapo ndipo mahali pa wagonjwa kwenda kupata ondoleo la tatizo lao, huwezi kusema, eti Hospital ni pachafu kwakuwa unaenda kutumbuliwa usaha pale! Vivyo hivyo, Mwnye dhambi ili apate ondoleo la dhambi, lazima aliendee kanisa, kwa hiyo huwezi kupaita Kanisani ni pachafu, eti kwasababu wanaokwenda pale ni wachafu kwa dhambi! Kanisani ndipo wanapopaswa waliojaliwa kujitambua kuwa wanadhambi waende, mtu mchafu akiata kuwa safi, huenda palipo safi akajisafi mwili wake!

  Kichwa cha Kanisa ni Kristo, basi kanisa ni mwanamke, maana Bibi harusi hawi mwanamme. Tunapomtazama mwanamke ndipo tunarudisha akili nyuma katika kulitafasiri Kanisa! Mavazi hayo yasiyofaa yanalitambulisha kanisa la leo, waliouchi hujidhania wamevaa, hata kanisa linaweza kujiona limevaa kumbe lipo uchi mbele za Mungu. Kuukemea upunguani huu wanaojitia kuwa nao wanawake ni sahii kabisa, kwani mwenendo wa mwanamke ndiyo mwenendo wa kanisa kiroho!

  Ukisoma maonyo ya Yesu Kristo katika lile kanisa la Laodikia katika kitabu cha ufunuo, ni mfano halisi wa Kanisa la leo. Lakini mimi kama mimi, sikukatazi kuwa chini ya mchungaji wa Kike wanaopenda kuwa uchi mbele za waumini wao, ila tu mara zote mme ndiyo kichwa cha mwanamke na Kristo ndiye kichwa cha Mwanamme. Sasa unapobadili cha mbele kuwa nyuma, hata kwa maelezo mazuri namna gani unakuwa unaupotosha ukweli! Mchungaji humwakrisha Kristo, ndiyo maana iko sehemu Kristo anajulikana kuwa yeye ni “Mchungaji mwema” sasa Kristo si mwanamke, yeye ni Mwanamme!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 4. Furaha,

  Kanisani si mahali patakatifu kama unavyojaribu kujishawishi.
  Mahali patakatifu huwa hawaendi wenye dhambi.

  Badala yake, kanisani ni mahali pa kimbilio kwa wenye matatizo, wenye mizigo, wenge dhambi ili wakapate msaada wa Mungu.

  Anaetakiwa kuwa mtakatifu ni wewe ambaye kimsingi ndo kanisani. Jengo kimsingi according to New Testament siyo kanisa.

  Roho mt hakai kwenge jengo la matofali anakaa kwenye hekalu ambalo ni mtu au mwili wa kristo.

  Sasa kama unadhani kuwa unaweza ukaikimbia dunia kwa kwenda kwenye jengo unaloliita kanisa, hii ni habari mbaya kwako kwamba hata huko kwenye jengo dunia iko imejaa.

  Huko kwenye jengo huwa tunakaa si zaidi ya masaa matano kisha tunatoka kurudi ambako unapaita duniani. Kwa hiyo wewe mwenye kujaribu kuikimbia dhambi kwa kwenda jengoni asilimia 90 ya maisha yako kwa wiko yako hatarini.

  Kinachoongezekaga tukikutanika huwa ni kule kujengana ktk umoja ambao huudhihirisha uwepo wa kristo.

  Kinyume cha hapo unatakiwa mkamilifu tangu ukiwa huko unakopaita duniani mpaka huko unakopaita kanisani.

  Huwa hatuendi kanisani kujipumzisha na dhambi, tunapaswa kuwa tumepemzika na dhambi 24/7.

  Mariam Magdalena alimfuata Yesu katikati ya fellowship akiwa bado amekaa kikahaba hivyohivyo, akamfanyia ibada na kuwaacha wenye kwenda kuangalia watu wamevaaje wakiendelea kushangaa.

  Hakuna anayeshabikia wanawake kuvaa isivyokubalika kwenye kusanyiko. Lakini ha muhimu zaidi si wao kuvaa mnavyotaka bali ni ninyi kupona kwanza huo udhaifu.
  Maana huwa hauwapati tu nkiona wamevaa hivyo kanisani, bali hata mkiwa huko unakopaita duniani.

  Vinginevyo Yesu akirudi na kuwakuta hamko mjengoni bali mko Kariakoo, basi lazima muachwe.

  Mwenye tatizo si aliyevaa hayo mavazi, bali ni anayeshindwa kujiweza anapomwona aliyevaa!

  Unadhani Yesu angeona mtu amevaa nguo ya kubana angepoteza muda kuhangaika na hiyo nguo!!!?

  Na kama huyo mtu angekuwa amevaa kwa dhamira ya kutamanisha wanaume, Yesu angedeal na dhamira yake.

  Kamuulize yule msamaria kisimani, kama mavazi yake yalimsumbua Yesu!

 5. Kanisani Ni mahali patakatifu ambapo mambo yote yanahusiana Na ushawishi wa dhambi yanatakiwa yakae pembeni kabisa,watu wanaenda kanisani kukutana Na Mungu,kumwomba Mungu Na hata kutubu dhambi zao Na poa kujifunza neno,Sasa inakuwa haiingii akilini mtu mwingine anakwenda kanisani matiti yako nje,mapaja wazi,nguo za kubana halafu tunaambiana eti tuvumilie hata Luthu alivimilia hii haiingii akilini,Inakuwa inachanganya Sana vishawishi vibaya vya uasherati ulivyovikimbia duniani unaenda kukutana navyo kanisani wakati mtu ulitegemea kanisani ndio sehemu salama lakini inakuwa baraa zaidi bora ubakie nyumbani.Ndugu msomaji naomba ifahamike wazi kujistiri Ni mambo la muhimu Sana Na chemchem hiyo lazima ianzie kanisani ambako mafundisho mema hutotewa.tukiendelea kushabikia hivi watu wanaovaa nusu uchi kwenye nyumba za ibada upo siku wataingia uchi kabisa kwenye mikesha nafikili hapo ndio mtakapofunguka,Kwa mwanaume kupenda au kutamani kunatokana Na kuona, Kuna umuhimu WA kudhibiti hivi vitu ambavyo vinawezekana kudhibiti,sijajua itakuwaje siku mwanakwaya au praise team wanaimba halafu mmoja Wao kitovu kipo nje sijui mtasema hata Luthu alivumilia.Tusiruhusu sumu kumwagwa kwenye chemchem manake waathirika watakuwa Ni wengi Sana.Huo ndiyo mchango wangu

 6. Mabinza,

  Mada haiongelei suala la wanawake kuwa maaskofu wala wachungaji.

  Unataka tu kuipeleka mada kusiko,wakati iko wazi kabisa.
  Suala la la wanawake luwa wachungaji nakumbuka tulishalijadili kwa sana tu.

  Tusipende kurudia vitu tena kwa mgongo wa mada nyingine.

  Hapa tuongee suala la jinsi wanawake wanavyovaa katika nyumba za ibada.

  Lakini pia unatala kutuambiaje, kwamba katika roho na kweli alipopasema Yesu ni pahala fulani au ndo kwenye nyumba za ibada?

  Kwa hiyo mavazi ya katika roho na kweli yakoje?

  Nafikiri suala la mavazi yenye staha si kanisani tu,kwa mkristo halisi ni kila mahali alipo anatakiwa kuvaa mavazi yenye staha.

  Lakini pia bado nitazidi kuwashangaa tu ninyi ambao mnaingia ibadani badala ya kufanya kilichowapeleka huko mnaanza kuangalia mavazi ya wanawake mpaka ibada yenu inageuka kutoka kwa Mungu kwenda kwa mwanamke aliyevaa mavazi fulani. Mna matatizo makubwa.

  Naomba mtiwe changamoto na Luthu aliyeweza kuishi katikati ya zinaa za Sodoma na Gomora na akaendelea kumpendeza Mungu.

  Wanaume mnaotatizwa sana na mavazi kanisani naamini njiani kazi yenu ni kuangalia maumbile ya wanawake kwa sana.

  Nendeni kanisani mkafanye ibada bhana, acheni hiyo kazi ya kuchungulia chungulia wanawake!

 7. TN,

  Usemalo ni kweli. Mungu atupe ujasiri kukemea na sio wawapo kanisani tu. bali hata huku mtaani kwani uwakili wao kwa Mungu sio kanisani bali zaidi huko ulimwenguni ambapo ndipo walipo Muda mwingi.

  Ukweli ni huu, dhambi isipokemewa hatimaye uzoeleka na kuchukuliwa kama ni kawaida. nakumbuka mara ya kwanza kuona mwanamke aliyevaa mavazi yasiyositiri kila mtu alikuwa akimshangaa lakini leo, Mhhh. wala.. imekuwa kawaida. kinachoendelea ni uzinzi kushamiri.

  Tulio na mamlaka kanisani tusiwe waoga kukosa watu kwa sababu tunakemea dhambi. tukumkuke shetani uleta wawakilishi wake kama hao ndani ya kanisa, sio ili waabudu bali kwa mitindo hiyo ya mavazi wawaangushe hata yumkini waliowateule.

  Tuwafundisheni wanawake kanuni hizi kuhusu mavazi kwa kifupi kwa mujibu wa neno la Mungu;

  1.Kila mmoja avae mavazi ya jinsia yake
  2.Mavazi hayo yawe yenye kusitiri-kufinya uchi
  3.Tusivae kujionyesha-kiburi cha moyo.

  Msisitizo wangu wavae hivyo popote walipo-wasijekutufariji wawapo kanisani kumbe huko nje ni mawakala wa bwana mwingine.

  wanawake msifanye mioyo kuwa migumu

 8. Ndg. Yangu N. na wengine wote, salaam,
  Maandiko yapo wazi, mwanamke hawezi kuwa Mchungaji, wao walidanganywa na shetani Biblia inasema hivyo kupitia kinywa cha Paulo! Kama mwanamme ambaye ndiye mtawala ameacha dalaka lake unategemea nini? Unawapongeza Mapadri? Ndiyo ni sawa, wao ni wanaume tupu katika upadri wao, hivyo wanatenda na kuamua kama watawala halisi katika zamu yao, utajilinganishaje nao, wakati kwenu kuna utawala wa kike kinyume na Biblia?

  Mungu huliheshimu Neno lake, naye kila mara hulichunguza apate kulitimiza. Unataka alitimize pahala lisipo? Unataka kuwe na Adabu, unataka kuwe na staha ya kutoingizana majaribuni? Biblia inasema mwenye uwezo wa kuwaingiza watoto wa Mungu majaribuni ni shetani, na shetani huishi akilitizama Neno la Mungu apate kuligeuza ili lifae kwa upotofu kama apendavyo. Unaposema, mwanamke awe Asikofu, wakati Biblia haimpi mwanamke nafasi hiyo, unategemea anayehubiri humo atakuwa nani na maneno yanayofundishwa humo yatakuwa yanatokana na nani kama si shetani mpotoshaji?

  Mwisho ukiona pahala watu wanaingia nusu uchi kuabudu, ujue hapo si pahala pa kuabudia kabisa. Pahala panapofaa kuabudia ni pale Bwana Yesu Kristo, alipopataja akimwambia yule mama msamalia siku ile pale kisimani, kama inavyotajwa katika kile kitabu cha Yohana.

  Sasa jiulize, pale ulipopaona wanachunga wanawake, au unapopaingia ili kuabudu unakuta staha ni ziro, bado pahali pale panakuwa panafanana na pale pakuabudia alipopataja Bwana Yesu Kristo? Kama hapafanani, wewe unaenda kufanya nini hapo? Kujaribu kulikataza Jambo la kubakia wanawake nusu uchi pahali kama hapo, ni kama kufanya Biblia isiseme kweli!
  EFATHA yaani funguka!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s