Nimeokoka lakini nakandamizwa na majinamizi!

jinamiziNaombeni mnisaidie ni miaka zaidi ya 10 toka niokoke lakini ninatatizo moja la kukandamizwa pindi nilalapo, saa nyingine nahisi kabisa mtu amenikalia mgongoni, mara nyingine nkilala kifudifudi nahisi kitu kinaingizwa katikati ya makalio,pia kuna kipindi nilikuwa naamka usiku saa 9 kusali kila siku ndio mambo yakazidi yaani nkimaliza kusali sitolala ntafanyiwa hivyo vituko mpaka kunakucha, nisaidieni jamani nimechoka sana, hali hii ikinitokea nakuwa sina hata uwezo wakujitingisha hata kidole..mbarikiwe

— NS

Tafadhali popote ulipo tamka Neno juu ya ndugu yetu na hali hiyo ikamwache mara. Katika jina la Yesu!

Advertisements

31 thoughts on “Nimeokoka lakini nakandamizwa na majinamizi!

 1. Nimependa NS ulivyoshauri, na ni short and clear, suluhu ni kuacha DHAMBI … kwisha habare yake. Mbarikiwe!

 2. kwa Jina La Yesu, pokea uwezo ushindi wa kushinda pepo wabaya. Funikwa kwa Damu ya Yesu Kristo. Amen  Siaka S. Nyanchiwa    Internet cafe and College Controller        P.o Box  70 Serengeti, Mara, Tanzania.           P.o Box 417 Tarime,Mara, Tanzania.    Contacts: sianchwa@yahoo.com/sianchwa@gmail.com. Mobile:            +255755527476.

 3. Hakuna mwema ila mmoja ndiye MUNGU.
  Ndugu yangu kila mtu ametoa idea na experience zake lakini katika yote mtegee Roho Mtakatifu yeye achunguzaye hadi ndani. Siwezi kujudge kuwa dhambi ,inawezekana kabisa ni roho za mizimu ya kwenu,inawezekana ni maagano kama alivyosema dada Faith.
  hatumfati Mungu kikawaida na kwa experience ya mtu au ya jana. tafuta uso wa BWANA naye atakuvusha.
  mimi nimeokoka na nilipoanza kuomba kuhusu mizimu nilipata vita ya maana so nakuelewa sana.

  Mungu aliyemwamuru Farao awaache watu wake waliokaa utumwani kwa miaka 400…akukomboe kwa ile damu ya Yesu iliyomwagika pale msalabani.

 4. Ns. Shalom, mpaka umefikia kulitoa hili neno hadharani maana yake umechoka hali unayopitia na unahitaji msaada, wanafunzi walipomuuliza Yesu mbona wameshindwa kumtoa pepo aliwaambia namna hii haitoki ila kwa kuomba. Nakushauri neno moja tu “OMBA” pale umeamua kuomba Yesu atakuonyesha mlango wa kutokea hapo kupitia roho wake, anaweza akasema nawe au akatumia mtu mwingne. Kwa wanajukwaa neno linatushauri tuombeane kwanini kila mmoja asitamke neno mbele za Yesu kwa ajili ya ns? Unapoombea wengne nawe wapo wanaokuombea.

 5. Daaaaah!ndugu nadhani umeshindwa kutambua mamlaka na thamani uliyonao,ukilijua Neno la Kristo na likakaa ndani yako!hakika cheche ni ngurumo za shetani utazishinda!Neno la Kristo likikaa kwa wingi ndani yako hakika utamshinda shetani kwa neno.maana shetani haogopi kwa kusema umeokoka maana alimjaribu hata Yesu,lakini Yesu alimshinda kwa neno.Ukiijua kweli hakika utakuwa huru kwelikweli!

 6. UNYENYEKEVU WA YESU UNAENDELEA KUPANDA MBEGU
  INAYOZAA UPENDO WA MUNGU!!

  Unyenyekevu wa Yesu ndiyo Roho Ya upendo wa Mungu aliye hai.
  Yesu ni mnyeyekevu kwahiyo na wafuasi wake wanaitwa wanyenyekevu wanaoishi duniani(ISAYA 11:4).Hawa ndiyo watu ambao
  wako tayari kwa roho,moyo,akili na nguvu zao zote KUPOKEA HABARI
  NJEMA kuhusu UPONYAJI WAO(ISAYA 61:1-11).Ni habari njema kwamba unyenyekevu wa Yesu uko tayari;

  1.Kuwaganga waliovunjika moyo

  2.Kuwatangazia mateka uhuru wao

  3.Kuwatangazia wafungwa habari za kufunguliwa kwao

  4.Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa

  5.Kutangaza siku ya KISASI cha Mungu wetu

  6.Kuwafariji wote waliao

  7.Kuwapa wateule taji ya maua badala ya majivu

  8.Kuwapa wateule mafuta ya furaha badala ya maombolezo

  9.Kuwavika wateule vazi la sifa ili kuondoa uzito wa roho zao

  10.Kuwafanya wateule waitwe MITI YA HAKI iliyopandwa na Yesu
  ili Mungu aliye hai atukuzwe.

  11.kuwawezesha wateule kujenga mahali pale palipoharibiwa ambako
  palikuwa ukiwa zamani na kuachwa kizazi baada ya kizazi.

  12.Kuwafanya mbwamwitu wawatumikie wateule

  13.kuwawezesha wateule kula utajiri wa mataifa na kujisifia utukufu wao

  14.kuwafanya wateule wapate wafuraie utajiri wa milele na mbwamwitu wapate aibu na fedhea ya milele

  15.kuwaingiza wateule ndani ya agano la unyenyekevu wa milele
  ili wapokee malipo ya kweli na kusimamia hukumu ya haki ambayo
  inachukia wivi na uovu wote.

  16.Kuwalazimisha mbwamwitu wakiri kwa vinywa vyao kwamba wateule
  ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA YESU KRISTO.

  17.kuwavalisha wateule wote MAVAZI YA WOKOVU na KUWAFUNIKA
  na VAZI LA HAKI maana ndivyo Bwana Mungu atakavyootesha haki na
  sifa mbele ya mataifa yote.

  SIRI ILIYOKUWA IMEFICHIKA NDANI YA MAKALA NINAZOONGOZWA
  NA ROHO MTAKATIFU KUANDIKA!!!

  Ilikuwa ni siri lakini sasa si siri tena ni mambo ambayo yako wazi sana
  na pengine kwa namna moja au nyingine yameleta USUMBUFU WENYE
  FAIDA KUBWA KWA WATEULE.Ni ukombozi wa kutisha kwa wateule
  hasa katika nyakati hizi za hatari.Hizi ni nyakati za mafumbo ya Yesu
  kueleweka sana alafu mafumbo ya shetani kufichuliwa kwa uwazi sana(LUKA 12:2).

  Makala zangu zote ni zinazungumzia VITA KALI KULIKO ZOTE CHINI
  YA JUA katika ulimwengu wa roho ambayo tunaweza kuziona athari
  zake nyingi katika ulimwengu wa mwili.Ni vita ambayo inaendelea
  kuwaangamiza wateule wengi.NI VITA KATI YA UZAO WA YESU NA
  UZAO WA NYOKA(MBWAMWITU).Ni vita ambayo Yesu mwenyewe
  kwa kinywa chake ALITUONYA KWAYO MAPEMA SANA.Tunaweza kuuona UHALISIA WA VITA HII ndani ya MATHAYO 24:24,25.Hebu
  tumsikilize YESU kwa mara nyingine tena akitupa ONYO KALI
  KUHUSU UHALISIA WA VITA HII
  “KWA MAANA WATATOKEA MAKRISTO WA UONGO, NA MANABII WA
  UONGO, NAO WATATOA ISHARA KUBWA NA MAAJABU WAPATE
  KUWAPOTEZA KAMA YAMKINI HATA WALIO WATEULE.TAZAMA NIMEKWISHA KUWAONYA MBELE”

  Makala yangu ya kwanza inayoitwa TUNATAKIWA KUTAZAMA KWA
  MACHO YA ROHONI,ilikuwa imeficha MAARIFA na HEKIMA ya Yesu
  kwa namna ya ajabu sana na kuiendea ilihitaji umakini wa hali ya juu
  sana.Ni makala ambayo iliyuacha uchi kabisa ndani ya mioyo yetu.
  Mtumishi Lwembe alichangia kwa tahadhari kubwa huku akijaribu
  kuutupa mpira kwa wengine ambao walikataa kuupokea!Mtumishi Sungura aliuliza swali la moja kwa moja ambalo liliitikisa dunia ya wajinga na wapumbavu.Kwa kweli lilikuwa swali la msingi mno!HII ILIKUWA NI MAKALA AMBAYO ILIMZUNGUKA SHETANI BILA YA YEYE
  KUTAMBUA AMEZUNGUKWA VIPI INGAWA ALISTUKIA TU GAFLA YESU
  YUKO NYUMA YAKE AMEMFUNGA MIKONO!!!

  Sasa ninaona wazi kwamba Yesu anatupenda zaidi ya upeo!Na amekusudi kwa kudhamiria haswa KULIKOMBOA KANISA LAKE LA
  TANZANIA NA ULIMWENGUNI KOTE KWA KISHINDO CHA KUTISHA.

  CK LWEMBE , SUNGURA pamoja na wachangiaji wengine inawezekana
  hatujui ni kwa kiwango kipi tunamsaidia Yesu katika mapambano
  haya kati ya wateule na mbwamwitu.Mimi siwezi kuacha mpaka nimefia mikononi mwa Yesu.

  HARAKATI ZA MAARIFA YA YESU ZINAENDELEA NA HAKUNA WA
  KUZIZUIA.

  Wateule wa BWANA tunatakiwa tuwe kikazi zaidi muda wote usiku
  na mchana.Yesu anatuambia “KESHENI”

 7. Mrs Christina,

  Achana na maneno ya vitisho na kujihesabia haki, hayatakusaidia. Tumekuwepo kwenye kanisa la SG miaka mingi tu tukijadili kwelu ya Kristo.

  Unapotutisha kuwa kuna watu wanakufuru Roho mt.naona unaropoka tu, labda hata maana ya kumkufuro Rohi hujui.

  Na tena usitudanganye kuwa kwa shetani nako kuna wokovu, hajawahi shetani wala mtumishi wake kufa msalabani ili kuleta wikovu.

  Wokovu ni mmoja tu wa Yesu kristo, huo wokovu wa upande wa pili ni upi kama si kupenda kuongea mambo yasyo na maana?

  Nilishasema ninyi watu wenye kujifanya mko rohoooni ndo mara nyingi mnadanganya watu Mungu, kwa kujifanya kuwa kila kitu mnafunuliwa.

  Naamini hata imani Sloam ilianza kinamna hiihii, kuhukumuhukumu kuwa wengine wanamtumikia shetani na ninyi tu ndo mnamtumikia Mungu.

  Tumeokoka na tunaujua msingi wa imani yetu, dont dare to touch the diode!

  Wewe kama umeishiwa maneno ya kuongea juu ya mada basi kaa kimya tu, huo nao ni uungwana, kuliko kujaribu kutuongelea maneno mengiii ya kirohoroho na kuhukumu wengine.

  Usijaribu kujihesabia haki kwamba wewe unalijua sana neno, na kumbe ulichonacho ni kule kukariri maandiko basi.

  Kujua neno ni kule kujua nini kinamaanishwa katika andiko ulilolikariri.

  Mjema mwenyewe unayesema umeungana nae hana credentials za kumshauri mtu aliyeokoka maana yeye haamini katika kuokoka sasa hivi, na kwenye mada inayohusu kuokoka amemsimanga huyu ndugu yetu tunayemshauri hapa.

  Halafu huyo ndo unataka kutushawishi kuwa ushauri wake uchukuliwe na huyu ndg yetu!! Hebu acha utani aise.

  Mara oh manabii wa uongo, mara uzao wa nyoka, mara waliookoka wa upande wa pili.
  Kwani manabii wa uongo wameanza leo kuwepo?

  Kanisa la kristo limejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, milango ya kuzimu hailiwezi!

  Ongea vitu vya maana, siyo kujaza miparagrafu ya mambo mepesi na kuhukumu wengine!

 8. Ndugu NS

  Yote niliyoongozwa na Roho Mtakatifu KUKUANDIKIA wewe pamoja
  na wateule wote NIMEKAZIA na KUFAFANUA KWA UNDANI maelezo
  ya watumishi wafuatao;

  Nanukuu,

  W.H. MJEMA 22/11/2014 at 8:06 pm
  Jamani tusimseme sana inategemea ameokoka upande gani(halisi au bandia).Siku hizi kuna wengi wameokoka upande wa pili.

  JOHN 20/11/2014 at 5:12 pm
  ……………Ila pia inawezekana hata kanisa unaloabudu na lenyewe ni
  style ya mauza mauza.Si yote yenye misalaba na yanayosema tumeokoka ni makanisa ya kiroho.BWANA YESU kupitia Roho wake Mtakatifu akusaidie kutambua ni eneo gani kuna udhaifu ili uweze
  kutoka!

  …………….mwisho wa kunukuu………………………..

  Sasa hebu twende taratibu, na hapa nazungumza na wateule sizungumzi na wanaoendelea kumkufuru Roho Mtakatifu(mbwamwitu).

  W.H. MJEMA anasema KUNA WENGI WAMEOKOKA UPANDE WA PILI.
  Alafu JOHN anasema KUNA MAKANISA YENYE MAUZA MAUZA NA SI
  MAKANISA YA KIROHO.Haya ni maneno mazito ambayo yanahitaji
  ufafanuzi wa kina wa kimaandiko.Si suala la kanisa tu hata ndani ya hii
  blog tunajadiliana na kizazi cha nyoka na pia kizazi cha Yesu.JOHN anasema inabidi Roho Mtakatifu atusaidie kuwatambua.Kwa wale wenye macho ya rohoni kila kitu kiko wazi sana KULIKO VAZI
  LA KAHABA MZOEFU anayeuza roho yake.

  Changamoto ya wateule katika nyakati hizi za hatari ambayo inazuia
  UPONYAJI WAO NA BARAKA AMBAZO MUNGU amewakusudia ni
  wingi ‘Makanisa’ ya MANABII WA UONG0 MIJINI NA VIJIJINI.Na wateule wengi
  WANAENDELEA KUDANGANYWA.Yesu anaeleza kweli hii inayotisha
  katika MATHAYO 24:11 “NA MANABII WENGI WA UONGO WATATOKEA,
  NA KUDANGANYA WENGI”. Mimi, MJEMA na JOHN tumeungana na
  unabii huu wa Yesu ambao umeshatimia na zaidi ya kutimia!Mbwamwitu wanajaribu kudhibiti mafundisho YANAYOFICHUA SIRI
  ZAO BILA MAFANIKIO.Ni nani aliwahi kushindana na Yesu na akashinda?
  Kadiri manabii wa uongo WANAVYOENDELEA KUJIFICHA KATIKA
  MITANDAO YA KIJAMII(Blog za injili), Tv,Radio, kwenye UIMBAJI na VIKUNDI VYA MAOMBI ndivyo Yesu anavyoendela KUWAVUA NGUO
  ZOTE NA KUWAACHA UCHI KABISA.Tunapoishi maisha matakatifu ndani
  ya neno la Mungu, hawa manabii wa uongo ni chakula chetu kama
  ilivyokuwa kwa shujaa Yoshua na Kalebu, waliyatafuna yale majitu na
  kufanikiwa kutawala na kumiliki KAANANI.TABASAMU LA MOTO WA YESU NI LA MILELE KATIKA NYUSO ZA WATEULE WANAOJITAMBUA
  KIROHO(LUKA 12:49).

  MANABII WA UONGO WANADHANI WANAWEZA KUMCHEKA MUNGU
  ALIYE HAI NA WAKABAKI SALAMA!!!

  Hiki ni zaidi ya kituko!
  Shetani anaendelea kuandaa mazingira mazuri ya KUWANYONGA
  watumishi wake wanaomtumikia kwa ujasiri na uaminifu wote!!!Si tu
  kwamba tunasikia lakini pia tunaona kwa macho ya rohoni jinsi anavyowafua nguo watumishi wake mwenyewe! CHEZEA SHETANI
  WEWE, UNADHANI ANA URAFIKI NA MWANADAMU.Unamcheka Yesu
  au unajicheka mwenyewe?! Hii miale ya moto wa Yesu HAIZUILIKI na ni
  MPAKA KIELEWEKE.

  IBRAHIMU baba wetu wa imani alimcheka Mungu kwa ujinga wa
  kutokujua tu na Mungu alilitambua hilo akamsamehe(soma MWANZO
  17:17-18).Mbwamwitu anapomcheka Mungu anajicheka mwenyewe
  na hata akiomba msamaha kamwe hawezi kusamehewa.Manabii wa
  uongo walifundishwa UONGO na KUFUZU tangu wakiwa tumboni
  mwa mama zao.Walishamdhihaki Mungu na kumcheka tangu wakiwa tumboni mwa mama zao.Walishakataliwa tangu wakiwa tumboni
  mwa mama zao na infact tangu kuanzishwa kwa misingi ya dunia(ZABURI 58:3, MITHALI 16:4).Alafu mteule unapoabudu kwenye
  ‘makanisa’ ya wauaji kama hawa UNATEGEMEA KUPATA UPONYAJI?
  Kwanza ukifika tu wanafunga baraka zako zote na kuchukua UMILIKI
  WA MACHO NA MASIKIO YAKO YA ROHONI.Asanteni ndugu JOHN na
  MJEMA kwa mchango wenu wa kuwafungua wateule ufahamu.

  HIZI NI NYAKATI ZA HATARI kama ambavyo Mtume Paulo
  allimueleza kijana TIMOTHEO(soma 1 TIMETHEO 4:1-3).Mtume Paulo
  alilia na kutokwa machozi alipoonyeshwa jinsi mbwamwitu watakavyo
  livamia kanisa la Yesu na akawaonya sana wateule wenzake USIKU
  NA MCHANA KWA MUDA WA MIAKA 3, AKIWASISITIZA SANA KUHUSU
  KUZITUNZA NAFSI ZAO(MATENDO 20:28-31).VITA TULIYONAYO
  NDANI YA WOKOVU NI VITA KATI YA UZAO WA YESU NA UZAO
  WA NYOKA(soma MWANZO 3:15).

  MTEULE AMKA KUTOKA USINGIZINI. EZEKIELI 34:1-31 INAONYESHA
  JINSI WATEULE WANAOJITAMBUA KIROHO WANAVYO WAGALAGAZA
  MANABII WA UONGO.

  SHETANI HAKUJUA YESU NI NANI MPAKA WALIPOKUTANA
  USO KWA USO KUZIMU.NA WAKATI HUO YESU ALIKUWA KIKAZI ZAIDI
  HACHEKI NA KIMA.

  KWA MBEGU KAMA HII NINAYOIPANDA HAKIKA NAFSI ZA WATEULE ZINAENDELEA KUWA SALAMA.

 9. Haya yote ni kwa ajili ya nini ktk mada hii?

  Huku si sawa na kutupa lulu mbele ya nguruwe?

  What is so difficult to narrate things within the armpit of the topic?

  ?????????????

 10. SEKUNDE CHACHE ZILIZOKUWA ZIMEBAKI ZIMEISHA!!

  NENO LA MUNGU LIMESHINDA KWA KISHINDO CHA KUTISHA!

  WAEBRANIA 4:12-13
  “Maana Neno la Mungu li HAI, tena lina NGUVU, tena lina UKALI
  kuliko upanga wowote ukatao kuwili,tena LACHOMA hata KUZIGAWANYA nafsi, roho, na viungo na mafuta yaliyo ndani yake,
  tena li jepesi KUYATAMBUA MAWAZO NA MAKUSUDI YA MOYO,
  wala hakuna KIUMBE KISICHO KUWA WAZI MBELE YAKE,lakini
  vitu vyote vi UTUPU NA KUFUNULIWA MACHONI PAKE YEYE
  ALIYE NA MAMBO YETU”

  Miale ya moto wa MAARIFA YA YESU imeshasambaa kila mahali.
  Mashetani wote wamechanganyikiwa! Neno juu ya neno.Maarifa juu ya
  maarifa.Hekima juu ya hekima.Busara juu ya busara.Miujiza ipo ili tujifunze na kutengeneza misuli ya imani,miujiza ni ya maisha ya jagwani na baraka ni za maisha ya kaanani.Maisha ya Misri na jangwani
  ni ya kupita(ni mapito).Maisha ya Kaanani ndiyo maisha ya baraka au
  mafanikio yanayotokana na maarifa yaliyo ndani ya neno la Mungu.
  KUISHI KWA IMANI MAANA YAKE NI KUISHI KWA KULITENDEA KAZI
  NENO LA MUNGU.Kuna neno,miujiza ,maarifa,mafunuo na baraka za shetani zinazotolewa na mashetani(manabii wa uongo).

  Kulitendea kazi neno la Mungu ni kuweka katika matendo yale Maarifa(mafunuo na hekima) yanayopatikana ndani ya neno la Mungu.
  Haya yote chanzo chake ni kuwa na neno la kutosha mioyoni mwetu.
  Tunaweka neno la Mungu kwa wingi mioyoni mwetu kwa kusoma na
  kutafakari Maandiko pamoja na kusoma vitabu vyenye pumzi ya Mungu.Kuna vitabu vingi ambavyo vimeandikwa HAVINA PUMZI YA MUNGU ndani yake.Kuna vitabu vya Mungu na vitabu vya mashetani.Kuna uponyaji wa Mungu na uponyaji wa mashetani.Namshukuru Yesu,Bwana wa vita ameshakomesha maangamizi yote.Uzao wa shetani UNATEMBEA UCHI HAUNA JINSI
  YA KUJIFUNIKA TENA.Mamilioni ya wateule kote duniani WANAENDELEA KUJITAMBUA KIROHO.Wachungaji wazembe na wale
  wanaoshirikiana na mbwamwitu KULIPOTOSHA NENO LA MUNGU
  WANAENDELEA KUFUKUZWA KAZI!

  UNABII HUU WA MUNGU KWA WATEULE WA TANZANIA UMETIMIA MAPEMA KULIKO ILIVYOTARAJIWA!!!(EZEKIELI 34:1-31)

  Mteule ni vyema ukausoma na kuutafakari unabii huu ambao
  ni ushindi na zaidi ya ushindi.Mimi nitanukuu mistari michache
  kama ifuatavyo;
  Mistari yote ni mizito nashindwa niandike upi niache ipi na sitaki
  niandike yote, OK! Ngoja niandike mstari wa 11, 28 na 29.
  “Maana Bwana MUNGU asema hivi.Tazama mimi mwenyewe, naam,
  mimi, NITAWATAFUTA KONDOO ZANGU NA KUWAULIZIA….Hawatakuwa
  MATEKA YA MAKAFIRI TENA,WALA MNYAMA WA NCHI HATAWALA,
  BALI WATAKAA SALAMA SALIMINI, WALA HAPANA MTU ATAKAYE
  WATIA HOFU.Nami nitawainulia MICHE iwe sifa njema, WALA HAWATAANGWAMIZWA KWA NJAA KATIKA NCHI YAO TENA, WALA HAWATACHUKUA TENA AIBU YA MAKAFIRI ”

  Mungu akubariki sana mteule.

  UNYENYEKEVU(MAARIFA) WA YESU NI ZAIDI YA USHINDI(HABAKUKI 2:14)

 11. Mh, things are never complicated like this.
  Wapendwa tunaongea mno mpaka tunakosa kueleweka ni nini hasa tunachowasilisha.

  Watu mna-complicate mambo utadhani wanatoa masharti ya waganga wa kienyeji.
  Mambo hayako complicated kiasi hicho bhana.

  Huyo ndugu aliyeokoka miaka kumi na anasumbuliwa na nguvu za giza hiyo ni ishara kwamba bado ni mchanga mwenye kuhitaji maziwa.

  Ukomavu(maturity) katika kristo hauji kwa idadi ya miaka, ispokuwa unakuja kutokana na bidii ya mtu kumjifunza Mungu.

  Anasema Paul ktk Waebrania 5:11-14 habari za uchanga kwa sababu ya uvivu wa kujifunza.
  Uwanja wa vita wa shetani kwetu ni akiki zetu. Huwa akipata nafasi anahakijisha akili zetu zinabaki njinga ili tukose maarifa ya neno la Mungu, ili apate nafasi ya kutuchezea.

  Kwa hiyo huyo ndugu anatakiwa kuongeza tu bidii ktk kujifunza, maarifa ya Mungu yakimjaa hayo mambo ya nguvu za giza hatayaona.

  Kukiwa na giza huhitaji kupambana nalo hilo giza, unachotakiwa kufanya ni kuleta nuru hapo palipo na giza, hilo giza litakimbia lenyewe.

  Baada ya mtu kumpokea Yesu na kujazwa Roho mt.anachotakiwa ni kujifunza neno la Mungu ili limjae kwa wingi.

  Hakuna cha maombi maalum ya ukombozi wala nini.
  Ukombozi ni subset ya wokovu, which means huwezi kuwa umeokoka halafu ukawa hujakombolewa.

  Labda kama mtu hujui maana ya neno kuokoka ndo unaweza kuwaza hivyo.

  Kwa hiyo huyo ndugu aongeze bidii ya kujifunza na aangalie pia hapo alipo kama anapata mafundisho sahihi, kama ni mafundisho manyonge atafute sehemu nzuri ya kufundishwa neno la Mungu. Akishamfahamu vizuri na kwa usahihi mwana wa Mungu hakuna mchawi, pepo wala jini wa kumgandamiza.

  Hakuna malango wala laana wala chochote kinachoweza kuushinda ufahamu wa neno la Mungu ndani ya mwamini!

 12. Ndugu NS

  Naomba tuwasiliane.Kama uko tayari naomba uwasiliane na SG
  wakutumie email yangu kupitia email yako.Yesu atakapokaa meza moja
  na mimi pamoja na wewe KILA KITU KITAWEKWA WAZI(LUKA 12:2).Hii ni
  fursa ambayo si vyema tukaikosa na inategemea unyenyekevu wetu.

  BARUA YA MOTO WA UPENDO WA YESU KWA WATEULE NA
  MBWAMWITU WOTE POPOTE PALE WALIPO DUNIANI!!

  kuna watu ndani ya hii blog sihitaji kukutana nao uso kwa uso kwa sababu NINAWAONA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO(2 WAKORINTHO
  4:18).Yesu amenifundisha kuangalia mambo katika ulimwengu wa roho
  na kuachana ana mambo ninayoyaona katika ulimwengu wa mwili ambayo
  bila ya hekima na maarifa ya Mungu HUTUFANYA TUSHINDWE KUUKOMBOA WAKATI(WAEFESO 5:15-21).Ulimwengu wa roho ni halisi zaidi kuliko ulimwengu huu tunaoishi tukiwa na miili hii ya udongo.UNAWEZA UKAWA
  UNAJADILIANA NA MTU NDANI YA HII BLOG, MUNGU AKAKUONYESHA
  MAHALI ALIPO,SURA YAKE , JINSI ALIVYOVAA NA UHALISIA WAKE
  KIROHO YAANI KAMA NI MTEULE AU MBWAMWITU!!!Uweza wa Yesu
  ulio ndani yetu UNATISHA MNO.Kuna wateule wanao tembea katika
  viwango hivi vya KIROHO.Mteule wa Mungu si mwanadamu wa kawaida,ni vyema tukaanza KUJITAMBUA KIROHO.Jambo hili huwa
  linanifanya NITOE TABASAMU LA MIALE YA MOTO WA YESU(LUKA 12:49).Ni bora kumuita mtu kwa jina la MTUMISHI bila kujalisha kwamba
  ni mtumishi wa nani.Ndugu CK LWEMBE upo hapo?Na hii ndiyo maana
  ya Mungu KUTUUMBA KWA SURA YAKE (SOMA MWANZO 1:26-27).Sisi ni roho kama alivyo Mungu.Miili yetu ni nyumba zetu za udongo.Ninapotaka nijue wewe ni nani sihitaji kutafuta picha yako na kuulizia historia yako au kanisa unalosali.NITAKACHOFANYA NI KUKUTAFUTA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO.

  Mwanadamu yeyote ameumbwa kwa namna ambayo ANATAKIWA KUISHI KWENYE ULIMWENGU WA ROHO na ULIMWENGU WA MWILI
  KWA WAKATI MMOJA.Mtume Paulo aliwaambia wakolosai kweli ya
  kutisha kwamba pamoja na kwamba alikuwa mbali nao kimwili LAKINI
  ALIKUWA ANAONA KILA KITU WANACHOKIFANYA KILA SIKU NA JINSI
  WANAVYOENDELEA NA WOKOVU,kwahiyo hakuna jambo ambalo
  wangeweza kumficha kwasababu ALIKUWA ANAUONA UTARATIBU WAO WOTE WA MAISHA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO(WAKOLOSAI 2:5-6).Paulo aliwaambia naona mnaendelea vizuri songeni mbele.
  Sikiliza, uweza huu wa rohoni UMO NDANI YA KILA MTEULE WA MUNGU ni vyema tukautumia ILI TUSIANGAMIZWE NA MBWAMWITU.

  Mungu wangu awabariki wateule wote.

  ………………………ZIMEBAKI SEKUNDE CHACHE……………………………..

 13. TUNAANGAMIZWA KWA KUKOSA UNYENYEKEVU!!

  Ndivyo ilivyo na huu ni zaidi ya ukweli!Unasema Mrs CHRISTINA K. Una maana gani kusema hivi? Sikiliza mpendwa,Unyeyekevu ni Maarifa(Hekima),kwahiyo Maarifa siku zote yamefichwa ndani ya unyenyekevu(MITHALI 11:2).Tusipoingia ndani ya unyeyekevu wa Yesu hatuwezi
  kuyapata Maarifa ya Mungu na katika hali hii KUANGAMIZWA ni lazima.Je tunawajua wanaotuangamiza?Maarifa ni nini na tunayapataje ili
  tusiangamizwe? Naona Roho Mtakatifu kuna mahali anatupeleka na ili tupokee kile ambacho Mungu ametukusudia inahitaji unyeyekevu(utii).
  UNYENYEKEVU wa kweli ni kumuogopa Mungu katika kila jambo tunalofikiri,kunena na kutenda.Na hapa ndipo ulipo MTIHANI WA MAISHA
  YA WOKOVU.

  Hebu tumsikilize Mungu anasema nini juu ya hili;
  HOSEA 4:6 ” Watu wangu WANAANGAMIZWA kwa kukosa MAARIFA.Kwa kuwa wewe umeyakataa Maarifa, mimi nami NITAKUKATAA wewe usiwe KUHANI kwangu mimi.Kwa kuwa UMEISAHAU sheria ya Mungu wako .Mimi nami nitawasahau watoto wako”.Neno kukataa linauhusiano wa moja kwa moja na kukosa unyenyekevu.Katika MITHALI 28:14 Limetumika neno USHUPAVU WA MOYO,ndilo jambo ambalo wengi linatutesa.

  Kumbuka tulikotoka kwamba unyenyekevu ni Maarifa ya Mungu.Sasa
  tuisome HOSEA 4:6 Kwa mafunuo ya Roho Mtakatifu kama ifuatavyo;
  Mungu anasema “Watu waliookoka wanaangamizwa kwa kukosa
  unyenyekevu.Kwa kuwa wewe umeukataa unyenyekevu, mimi nami
  nimekukataa wewe usiwe mtumishi wangu.Kwa kuwa umeuacha upendo wangu.Mimi nami nitawaacha watoto wako”

  Kumbe suala la kuuacha upendo wa Mungu(sheria yake) linaleta athari
  kutoka kizazi hadi kizazi.KUTOKA 20:3-6 inakazia jambo hili kwamba ni kuanzia kizazi cha kwanza mpaka cha nne cha wale wasio na Maarifa ya kuvunja maagano,malango na madhabahu za miungu(mizimu).Mstari
  wa 6 unasema tiba ni KUFANYA MAOMBI YA REHEMA.Kila mtu aliyeokoka anayo changamoto hii na kwahiyo anatakiwa apate maarifa ya
  namna ya kujikomboa ili ASIANGAMIZWE na shetani na manabii wa uongo
  ambao wanatumia majeshi ya pepo wabaya.Mapepo wabaya uvaa sura za
  ndugu zetu waliokufa katika DHAMBI(mizimu) na kuja duniani kututesa wakitutaka tumtumikie shetani.Wanatuingiza katika makafara ya damu na
  ngono(uzinzi na uasherati).Kama akutokea mtu wa kusimamia damu na maarifa ya Yesu katika ukoo ili kuvunja maagano,malango na madhabahu
  ambazo zilitumikiwa na kizazi kilichotangulia,KUANGAMIZWA HUWA KUNAENDELEA kutoka kizazi hadi kizazi.Wakati Mungu anamuita GIDEONI
  alimuongoza KUJITENGA na KUVUNJA MAAGANO,MALANGO NA MADHABAHU ZA MIZIMU(MIUNGU) YA UKOO WA BABA YAKE(WAAMUZI 6:14-16,24-29).Unapovunja maagano,madhabahu na malango
  ya miungu unatakiwa kujenga maagano,madhabahu na malango ya Mwana
  wa kondoo(YESU KRISTO).Na hii inahitaji MAARIFA MAALUM,si makanisa
  mengi ya walokole yanafundisha haya maarifa lakini pia manabii wa uongo
  huwa wanayafundisho ili kuwaunganisha wateule na maagano,madhabahu na malango ya KUZIMU.Wengi wanaendelea kuangamizwa kwa staili hii ndani ya madanguro(huduma) za manabii
  wa uongo ambazo zimejaa kila kona kuanzia mijini mpaka vijijini.Tatizo
  wateule wengi hawana macho na masikio ya rohoni na ndiyo maana
  wanaendelea kufanywa mateka(ISAYA 42:18-22) na juhudi za kuwarudisha(kuwatoa katika hayo madanguro) bado HAZITOSHI.

  Ngoja tuliweke vizuri zaidi hili jambo.MAARIFA ni mafunuo na hekima
  inayopatikana kwa kutafakari neno la Mungu na kisha kulitenda(kuliishi).Ni mafunuo na hekima ya neno la Mungu ambayo imewekwa
  katika matendo.Unaweza ukapata mafunuo na hekima lakini kama hukuweka katika matendo uwe na uhakika hayo Maarifa yamekufa.

  Kuna tofauti kati ya KUOKOKA(kuzaliwa mara ya pili) na KUKOMBOLEWA.Wateule wengi baada ya kuzaliwa mara ya pili huwa
  hawaingii hatua inayofuata ya KUKOMBOLEWA(hatua ya kukubali kuingia ndani ya unyenyekevu wa Yesu).Tusikilize kwa makini hapa,tukimiss hii point tutakwama.UKOMBOZI ambao Yesu aliukamilisha
  pale msalabani na akasema imekwisha, ULIFANYIKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ili uje uthibitike katika ULIMWENGU WA MWILI.
  Pale msalabani Yesu alitukomboa kwa kutukabidhi BARAKA ZOTE
  TUNAZOSTAHILI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.WAEFESO 1:3 inaeleza
  wazi jambo hili ” ATUKUZWE MUNGU BABA WA BWANA WETU, YESU
  KRISTO,ALIYE TUBARIKI KWA BARAKA ZOTE ZA ROHONI, KATIKA
  ULIMWENGU WA ROHO, NDANI YAKE KRISTO”
  Kwahiyo ni jukumu letu kusimama katika MAOMBI YA MAARIFA
  YA YESU ili kuzichukua/kuzitoa hizo baraka zetu zote zilizopo katika
  ulimwengu wa roho ili TUTAWALE NA KUMILIKI katika ulimwengu wa mwili.

  YAFUATAYO NI MAARIFA AMBAYO TUMEYAPATA KUTOKA KWA WATUMISHI WALIOCHANGIA.

  W.H.MJEMA, JOHN na RTUO
  Wamesisitiza kwamba Maarifa ya kwanza ni kuutambua mlango
  wa DHAMBI na MAOVU ili kuushughulikia.Mlango huu unaweza ukawa
  ni Hofu,kukosa imani na dhambi nyingine zilizofichika.Infact,hafichae dhambi kuangamizwa ni LAZIMA(MITHALI 28:13-14).HAPA BILA SHAKA LENGO KUU NI
  KUHAKIKISHA TUNAZIJUA KWA JINSI YA ROHONI MADHABAHU
  ZA MAKANISA TUNAYOSALI.Mtumishi John umenifanya nitokwe na
  machozi ya ushindi.Mungu wangu akukumbuke na kukamilisha mahali
  ulipopungua katika maisha yako.(MITHALI 22:4)

  PETRUS GEORGIY
  Ametupa Maarifa ya jisnsi ya kuzitubia dhambi ambazo wakati mwingine si rahisi kuzijua.Ameeleza vizuri na kutupa na maandiko.USHUHUDA WA MAISHA YAKE BINAFSI unatupa picha halisi
  ya namna roho za miungu zinavyoweza kumtesa mtu na kuharibu maisha
  yake kabisa.Pia ameeleza njia na namna ya kutafuta maarifa kama vile
  kuudhuria semina za neno la Mungu.Ameeleza mambo mazito ambayo
  tunatakiwa tuyasome kwa kuyatafakari sana na yatatuweka mahali pazuri.Mungu wangu anakwenda kukufunulia ile MANA iliyo kuwa imefichwa na JIWE JIPYA JEUPE ambalo jina lake analijua Yesu na wewe tu!(UFUNUO 2:12-17).

  FAITH na MUKAMA MAGAFU
  Niko makini sana na ujasiri wa Faith katika kujieleza.Watumishi hawa
  wametupa Maarifa kwamba TUNAPOFANYA MAOMBI YA REHEMA
  ni lazima tufunge na kuvaa SILAHA ZOTE ZA MUNGU sawa na WAEFESO
  6:10-17.Maombi ya Rehema ya kujitenganisha na mizimu yanatakiwa
  yafanywe kwa siku 7 mfululizo.Siku 3 za mwanzoni kufunga na kuomba
  bila kula wala kunywa chochote,hapa tunatakiwa kuomba msamaha kwa ajili yetu na wengine katika ukoo lakini pia kusamehe(kuwaachilia) waliotukosea,ni maombi ya kujidhili na kulala chini.Siku 4 zinazofuata tunatakiwa kufunga kwa masaa 12 tu na kuomba.Hapa tunatakiwa kufanya maombi ya vita kwa kuvunja maagano,madhabahu,na malango
  ya mizimu alafu kisha tunaweka na kujenga maagano,madhabahu na malango ya Yesu.Kabla ya kuanza maombi tunatakiwa kujifiweka wakfu na kujifunika na DAMU YA YESU
  kwa ajili ya hayo maombi ili tuweze Mungu atulinde na kutuongoza tuweze kuyamaliza salama.Wengine huwa wanajikuta wanaishia njiani.

  MATHEW TAMBUKA
  Ametupa Maarifa ya kufanya haya maombi ya Rehema chini
  ya uangalizi wa mtumishi wa Mungu.Hili suala ni muhimu hasa pale
  tunapopata mtumishi ambaye amewahi kufanya haya maombi.Kuna maelekezo ya namna ya kufungulia baada ya zile siku tatu kavu za
  mwanzoni na pia namna ya kufungulia baada ya kuanza kufunga kwa
  masaa 12.Kuna maelekezo ya kiwango cha maji unachotakiwa kunywa
  kabla ya kuanza mfungo na maandiko ya kujiweka WAKFU.Pia Maelekezo ya maandiko ya kusimama katika zile siku 3 za mwanzoni
  na zile siku 4 za kumalizia.Pia kuna maelekezo ya mazingira mazuri
  yanayopaswa kufanyia haya maombi na namna ya kuepuka makwazo
  au dharula zinazolenga kukuharibia maombi.KUNA MAMBO MENGI HAPA KADIRI MTUMISHI ATAKAVYOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  Kabla ya maombi ni lazima aombe kibali kwa cha Mungu ili akufanyie
  USHAURI WA AJABU.Wakati mnaongea ROHO YA MAARIFA itaanza
  kufichua mambo yaliyo kuwa yamefichika katika maisha yako ili muweze kujua jinsi ya kuomba.KIMSINGI NI KWAMBA NI LAZIMA NA YEYE AFUNGE NA KUOMBA NA WEWE KWA AJILI YAKO KWA SIKU HIZO SABA!Si lazima afunge zile siku tatu kavu lakini ni lazima afunge
  kwa masaa 12 kwa siku zote 7.

  MAGRETH na AYOUB JL
  Wametoa ushauri mzito kuhusu kuzikiri kwa vivywa vyetu ahadi za
  Mungu katika maandiko.kwa mfano tunatakiwa kufunga laana zote
  katika ulimwengu wa roho na kufungulia baraka zote katika ulimwengu
  wa roho ili zitujilie(MATHAYO 16:19).Pia jambo lingine la muhimu wakati tunafanya hivyo
  NI LAZIMA TUHAKIKISHE TUNAISHI MAISHA MATAKATIFU NA KUACHA
  KUISHI MAISHA YA KINAFIKI(MATHAYO 15:7-9).

  ANGALIZO
  Ukifanya haya maombi chini ya muongozo wa mtumishi wa shetani
  huwe na uhakika atakuunganisha na maagano,madhabahu na malango
  YA KUZIMU.Kama wengi walio katika huduma za manabii wa uongo
  wanavyoendelea kuunganishwa ILI KUWAFANYA WAWE MASIKINI KWA
  SIRI.Na wanaofanikiwa ni wale wanaotembea ndani ya BARAKA ZA SHETANI.Si wateule wengi wanaojua kutofautisha kati ya BARAKA ZA
  MUNGU na BARAKA ZA SHETANI.Kuna AMANI YA KRISTO na AMANI
  YA SHETANI.KWA SABABU YA KUTOKUJUA AU KUPUUZA HAYA MAMBO WATEULE WENGI WANAISHI MAISHA AMBAYO MUNGU HAKUWAKUSUDIA ALAFU WANATEMBEA VIFUA MBELE!!!MAFUMBO
  YA MUNGU, MTU MJINGA HAWEZI KUYATAMBUA NA MTU MPUMBAVU
  HAYAFAHAMU.USITAMANI SANA MAJUMBA NA MAGARI WANAYOENDESHA WAPENDWA.SI KILA MPENDWA ANAISHI NDANI YA MAFANIKIO
  YA YESU.ISHI NDANI YA KANUNI ZA YESU ILI AKUPONYE NA KUKUINUA.ZABURI YA 92 MSTARI WA 5-7 inaeleza haya mambo
  kwa uwazi sana.

  Nitaendelea kadiri Mungu anavyonipa kibali…………………….

  ………………………..ZIMEBAKI SEKUNDE CHACHE…………………………………

 14. Jamani tusimseme sana inategemea ameokokea upande gani (halisi au bandia). siku hizi kuna wengi wameokokea upande wa pili.

  Rafiki pokea ushauri hapo juu dozi ya kufunga siku tatu kavu kavu. kwani ” Namna hii haiwezekani ila kwa kufunga na kuomba”.

  Na utakapowekwa huru maneno ya Yesu kwako ni…wala mimi sikuhukumu bali endenda zako nawe usitende dhambi tena….

 15. Kama ni hofu ya kipepo ujue itavuta nguvu za kipepo kukufuata na kama ni hofu ya Mungu ujue itavuta uwepo wa Mungu kuwa pamoja na wewe na kukufunika. Sijajua umemkabidhi nini adui mpaka akapata nafasi ya kukushambulia. Hiyo nguvu shetani anaitoa wapi kumshambulia mtu aliyeokoka namna hii

 16. Naungana na wachangiaji wengi. Kuna kitu ambacho kinakuunganisha na kutoa nafasi kwa mapepo kukusumbua au haujajua mamlaka uliyopewa katika kristo Yesu kama umeokoka. Pili kwasababu ni miaka 10 unasumbuka inawezekana ndani yako hofu imejengeka na kuota mizizi. Na hofu huwa inavuta nguvu za Giza. Ukilala na hofu kukujia ghafla inatengeneza mlango wa mashambulizi kupita halo. Ayubu anasema ” lile linitialo hofu ndilo unijia na kunipata”

 17. Pole sana ndugu yangu,mambo hayo ni ya kuhuzunisha,jitahid kuongeza ibada yenye imani thabit kwa mwokozi.Nawe utawekea huru ukimkiri Yesu moyoni na sio mdomoni

 18. Ndugu,
  Kwanza Pole sana ila ninaongezea mchango wa mwenzangu hapo juu kuwa shetani hababaishwi na kuwa umeokoka lini hata ikawa miaka 100 kama hujajiweka vizuri na Yesu na hujafunguliwa bado atakuchezea. Lakini ukumbuke kuwa Yesu mwenyewe alifunga siku 40 na aliongozwa na roho kwenda nyikani kuomba lakini bado shetani alimfuata huko huko na kumjaribu pamoja na maombi yake.Ila shetani alimshindwa Yesu kwa sababu aliyajua maandiko na kujua namna ya kuyatumia kwa sababu nguvu zote za kumshinda shetani alikuwa nazo na alijua uongo wote wa shetani.
  Ninachomaanisha kukuambia kuwa jiweke vizuri kwa Yesu na tambua hila zake kila wakati.
  Herry.
  Mtwara.

 19. dada faith si kuhusu kuhukumu…dhambi muda mwingine si kwamba umeitenda wewe wakati mwingine yapo makosa tuliingizwa na waliotutangulia ivyo ukaribu na kukua kiroho ndio suluhisho….ni wachache sana wanaopata nehema ya mapepo yote kuondoshwa siku ambayo anamkataa shetani na kumkubali YESU kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yake….formula ya mungu utaifahanu kweli na kweli ndio itakayokuweka huru…na kweli na nuru ya kufunua ya gizani ni mungu tu (ushuhuda wangu binafsi mwingine niliteswa sana na mapepo ilikuwa ikifika siku nafanya mitihani ya taifa anakuja mwanamke ndotoni usiku ambao asubuhi naingia kwenye chumba cha mtihani tunafanya tendo la ndoa na nilikuwa nimeokoka tayari na lazima mtihani hiyo nianguke ivyo nimereseat mtihani ya form six mara 3….mpaka wadogo zangu wakawa wananifikia…lakini nilikuja angaziwa nuru ya mungu na kweli yapo masuala yalifanyika wakati nazaliwa tu ivyo ukoo wetu hakuna aliewahifika chuo kikuu aliyejitahidi alifika form six…baada ya kuongezeka (kutoka 23:29) ndipo siri ikawa wazi inamaana miaka miwili yote ya mwanzo ilikuwa ni namna flani nikue nifikie kiwango flani ambacho mungu amekusudia ndipo niwekwe huru. baada ya hapo nikafaulu vizuri sana chuo na wandugu zangu walionifuata wakafaulu vyuo.. na si hapo amenifanya kuwa kichwa chuoni….muhimu ufahamu dhambi ni chanzo cha matatizo mengi sana mungu. ndugu NS utafute ufalme wa mbinguni na haki yake kwanza….rudisha maombi ya usiku uliyoyazima kama umeacha….miaka 10 ni mingi sana kwa ka experience kangu kadogo.

 20. pole sana miaka kumi ni mingi sana katika wokovu……………mara nyingi sana ni kuna mambo tunakuwa
  (1)tunayatenda pasipo kujua ni AMBAYO ni dhambi Ayubu 34:32 ” Nisiyoyajua nifundishe wewe kama nimefanya uovu sitafanya tena”
  (2)kuna dhambi ambayo haikutubiwa hii mara nyingi ubaki mlango wa shetani daima zaburi 19:12-14 ” ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? unitakase na mambo ya siri. umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi…..”
  (3)Kuna majira ambayo umekwama maana mungu huwa anaachilia majira kwa kila wakati na neno lake ili mtu huyo azidi kukua kiroho kuwa mpya kila siku…..YAPO MAMBO AMBAYO MUNGU AMESEMA NA WEWE LAKINI UMEKATAA KUYAACHIA AU KUBADILIKA. (SHETANI ANAPENDA TESA WAKRISTO WASIOKUA) unapookoka na kumkubali yesu kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yako unaanza safari ya maisha yenye uvumbuzi wa mambo mbalimbali yanayokuhusu wewe na jamiii yako..uvumbuzi huo unaupata vipi?
  (a)Maombi hasa muda wa usiku wakati watu wanalala tenga saa moja kutafakari neno na maombi…(ndio maana ulikuwa unashambuliwa sababu ulikuwa unauvuta uwepo wa mungu maishani mwako kwa karibu na mapepo yalikuwa yanachomwa na nuru ya mungu)
  b)Jitahidi anza huzulia semina na ibada kuzidi kujifunza na mungu ndipo anazidi waondosha adui zako kutoka 23:29-30 ….”Sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja; nchi isiwe ukiwa, na wanyama wa bara wakaongezeka kukusumbua. Nitawafukuza kidogo kidogo mbele yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi”…..hapa kadili ushirika wako na mungu utakapoongezeka yaani mahusianao ndipo kukua na adui zako wanaondoshwa mmoja baada ya mmoja…(Ushuhuda wangu binafsi sikujua kama kufanya ibada ya shukrani kwa MUNGU kila mwaka ni jambo la lazima kwa wakristo. ivyo nilikuwa natoa tu matoleo ya shukrani mara kwa mara mungu aliponitendea jambo jipya. hivyo siku nilipopata mafunuo nilipewa maono katika ulimwengu wa roho mapepo yalivyolipuka)
  (4)Mazoea hili ni jambo ambalo linatusumbua wakristo wengi kuuzoea wokovu na neno la mungu hivyo kupeleka maisha ya wokovu kwa namna na jinsi tulivyozoea siku zote uleta shida na hii ni roho kabisa ya kuikemea….ndio maana hata daudi mara kwa mara alipopigana na adui zake wafiristi alimuuliza MUNGU na hii ilimsaidia kupewa mbinu mpya za kupambana na adui zake..

 21. Pole sana Mpendwa..nakusalimu katika Jina la YESU..Jina lipitalo maina yote..
  Mimi siwezi kukuhukumu na kusema kwamba kuna dhambi unafanya eti ndo inasababisha ukandamizwe..NO WAY. Mi mwenyewe niliokoka nikiwa mdogo sana lakini bado nilikuwa nakandamizwa. mara nyingi hii huwa nimizimu inayotoka either upande wa baba yako au mama yako. Ni pepo wachafu wanaitwa jinamizi…huwa yanafatilia sana maagano ya ukoo mfano labda wazazi wako walikuwa wanatambika lakini wewe hautambiki. Pili ibilisi anapenda sana kukatisha tamaa wale ambao anajua wakiijua kweli wakasimama watakuwa threat kwake…something great is ahead of you….na ndo maana hata ukiomba bado anakuja kukukandamiza anajaribu kukuvunja moyo tu uone kwamba MUNGU hawezi. huu ndo uongo wake maana yeye ni baba wa waongo.

  Usikate tamaa mpendwa..tenga cku chache..funga na kuomba ili kutubu kwa ajili yako na vizazi vingine vya nyuma. Vunja mikataba yote ya damu au kuabudu wanyama iliyofanywa na wazazi wako au vizazi vingine vya nyuma. Simama na huu mstari wa Isaya 53:5..kwa kupigwa kwa YESU msalabani tumepona…tafuta vifungu kwenye bibilia ambavyo vionaonyesha promises za MUNGU kwetu…simama navyo mpendwa. Usikate tamaa kabisaaa Omba..omba…omba…mi nimemuona MUNGU mpendwa..anajibu..we maanisha tu. Muite atakuitikia kama alivyosema kwenye Yeremia 33:3. Mwambie ibilisi mwili wako ni hekalu la ROHO MTAKATIFU na HANA LEGAL RIGHT YOYOTE MAANA WE NI MWANA WA MUNGU…Waefeso 5:30 inasema sisi ni viungo vya kristo. Yohana 15: 5 inasema yeye ni mzabibu wa kweli na sisi tu matawi.

  Pia jifunze kuvaa silaha za wokovu wakati woote. Chepeo ya wokovu kichwani, dirii ya haki kifuani,mkanda wa haki kiunoni, viatu ya utayari wa injili, upanga wa ROHO MTAKATIFU na ngao ya Imani. yaani fanya ishara kama unavaa kweli…Pia jifunike kwa damu ya YESU wakati wote…na unapoenda kulala. Shusha malaika wa ulinzi na vita..sema kabisa nakusha malaika Michael..huyu ni malaika wa vita.,.afanye vita na wanaokutafuta…awakamate..awatupie kwenye shimo kuu la giza na wafungie huko kwa Mathayo 18:18 wasitoke wasubiri hukumu yao.

  Kumbuka kwenye Yohana 16 kuanzia mstari wa 23 YESU aliwaambia wanafunzi wake waombe lolote kwa Jina LAKE na BABA atafanya…so mkumbushe. Maana alisema tumkumbushe kwenye Isaya 23;46. MUNGU ni Mwaminifu..atakujibu.

 22. NS,
  pole sana.
  Kwanza, Mimi nikwambie kuwa, hujaokoka wewe!! Saa ya kuokoka bado!! Sasa hivi umemwamini Yesu tu, lakini kuokoka bado. Na unapomwamini Yesu, sharti la kwanza ni kuchunguza njia uliyo (mapito unayoyapitia kumfuata Yesu), iko sahihi?? Hapa ndipo watu wengi wanashindwa kuelewa!! Wanatoka kwenye ulimwengu wa shetani, wanaingia kwenye ulimwengu mwingine wa shetani uleule japo huu wa pili, unatumia jina la Yesu tu!! Kwani wewe hujawahi kusikia watu wanaombewa na kupata watoto majoka? unafikiri kama waliombewa kweli kwa Mungu, ilitokeaji mtoto akawa joka?? Tafakari sana!!
  Pili, amua sasa kumtafuta Mungu. Unapomwamini Kristo, vita kati yako na nguvu za giza huongeza sana kuliko ulipokuwa muasi. Mapambano huwa ni makali mno! Ndiyo maana, nikakwambia hapo mwanzo kuwa, WEWE HUJAOKOKA bado!! Waliookoka, huwa hawapatwi na misukosuko hii ya shetani. Waliokoka, huondolewa kwenye dunia hii ya taabu -misukomisuko ya kila siku. Ndiyo maana nakwambia kama uko kwenye makanisa ya wale wanaosema wameokoka ilhali bado wako kwenye dunia hii, wanaendelea kupambana na nguvu za giza kila siku, na wengine kudondoka kabisa dhambini nk, tafakari njia zako.
  Bado hauko salama na hayo majinamizi, hayatatoka. Mtafute Mungu wa kweli kwanza. Naye huwezi kumpata popote. Anapatikana kwenye Biblia tu. Isome, umjue Mungu wa kweli ni yupi halafu mfuate huyo na mapepo yote yatakuacha muda huohuo!!
  Siyi

 23. Pole sana kwa tatizo hilo.Haihitaji utafiti wa gharama kubwa kugundua kinachokusumbua,unasumbuliwa na mikataba ambayo uliingia au kufungamanishwa bila kujua.Ninakushauri ufanye maombi ya toba kukataa kila aina ya uonevu toka kwa shetani.Katika hili unapaswa kumaanisha (maisha ya utakatifu ni msingi wa yote.).Nyunyiza damu ya YESU kila mahali unapohisi linaweza kuwa tatizo limeanzia.Nina uhakika na jina la YESU utapona maana andiko linasema “Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli” Yoh 8:36
  AYOUB JL
  FROM MWANZA

 24. mkabidhi Yesu madaraka ya kuwa insurance na daktari wa maisha yako, na mruhusu afunge milango iliyokuwa imefunguliwa na kufungua milango iliyofungwa .endelea na sehemu zote kama unavyoijua shida yako. kumbuka maneno unayotoa kutoka kinywani ya kumkiri na kumruhusu aingilie kwenye shida yako , ni dawa kubwa. kwa jina linguine tunaita kufanyiwa deliverance.
  safina redio ni shida kama hizo wanajaribu kuifundisha watu na kusaidia sana, maana watu wengi hawajui adui anatokea mlango gani.

 25. NS
  Mimi kwa ufahaamu wangu una “mume wa kipepo” ninakushauri ukafanyiwe “Deliverence” na mtu wa Mungu mwenye karama hiyo. Na nikwambie wapo wachahche wa namna hiyo. Naamini ukiingia kwenye maombi ya kumaanisha Roho Mtakatifu Atakuongoza au atakupa ufumbuzi.
  Mimi nilikuwa na mkew wa kipepo miaka kumi baada ya kuokoka na kwa neema ya Mungu nimekwisha funguliwa. Usikate tamaa Bwana Yesu Yu Hai kazana ushindi wako upo karibu.

 26. Mpendwa katika Bwana, Kama ni kweli wewe umeokoka na bado mambo hayo yanakukuta, kuna mambo mengine ya sirini ambayo ama haujayasema au kuna kitu ndani mwako kinakufunga ambacho haujakisamehe au kukisahau. Hebu chukua dose hii. Funga siku tatu kavu huku ukiwa unaomba na kusoma neno la Mungu kila unapokuwa una nguvu, Na unapoingia kulala kitandani jifunike na damu ya Yesu Krusto ili iwe kinga kwako.Ukiona bado ongeza tena siku tatu.Mambo hayo yote yatakuacha. Mungu akubariki sana

 27. Umenena W.H. Mjema!

  Ndugu NS, Ili kuondokana na tatizo ulilo nalo ni kujikita zaidi kwa YESU ikiwa ni pamoja na maombi yako binafsi yaliyo ya dhati kwake YESU!

  Lakini pia unaposema umeokoka miaka 10 au zaidi, si kigezo cha kumtisha shetani au ukomavu kiroho. Yawezekana kabisa kuna mzigo ambao bado unakuzinga ambao unatakiwa kuachiliwa kabisa na kumtwika Kristo ashughulike nao. Ila pia inawezekana hata kanisa unaloabudu na lenyewe ni la style ya mauza mauza. Si yote yenye misalaba na yanayosema tumeokoka ni makanisa ya Kiroho. BWANA YESU kupitia Roho wake Mtakatifu akusaidie kutambua ni eneo gani kuna udhaifu ili uweze kutoka!

  Barikiwa rohoni na mwilini. Natamka kwa imani ktk Jina la YESU, ufunguliwe toka tatizo linalokukabili toka sasa! AMEN!

 28. NS,

  Ubarikiwe kusema ukweli. Ninachoona mimi kuna kitu bado kinachokuunganisha na shetani yaani dhambi aidha unaijua au la. Haiwezekani useme “NIMEOKOKA MIAKA 10″ iliyopita alafu bado shetani aendelee kukuchezea. Lazima kuna dhambi unayoendelea nayo na unaipenda au una dhambi pengine usiyoijua. Ushauri wangu ili uweke huru kweli kweli ni lazima uweke mbali kila mzigo ukuzingao na ndipo watumishi wa Mungu watakapoomba utawekwa huru vinginevyounawasumbua tu.

  Kumbuka Yesu alipowaweka watu huru aliwaambia ” enenda zako na usitende dhambi tena…” pia alisema tunapompokea Yesu nusu nusu…. Hali yetu itakuwa mbaya kuliko awali.

  Haiwezekani wakati unapoamka kwenye maombi then shetani naye ndo ajihudhurishe kukuchezea ni lazima na wewe kuna dhambi utendayo inayokufanya akuone wewe unamchezea Mungu…

  Kwa Jina la Yesu ACHA IYO DHAMBI ata kama niya siri nawe Utakuwa Huru Kweli Kweli.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s