Nina maswali kuhusu Marehemu Nabii Elia!!

munuoBwana Yesu Asifiwe.

Biblia inasema kwamba ili kutambua nabii wa kweli ni lazima unabii wake uweze kutimia. Hii inamaanisha kwamba kama unabii haujatimia basi nabii yule atakuwa ni nabii wa uongo. Juzi tumeshuhudia kifo cha aliyesema yeye ni nabii wa kizazi kipya, Eliya AD2,.

Kama mnavyojua kuna mada iliwahi kuwekwa mezani kwa SG kuhusu mafundisho ya nabii huyu, watu walijaribu kujieleza, wengine kwa jazba, wengine kwa kutetea nk nk, sasa kitu ambacho kinaumiza akili yangu ni kwamba je ni kweli Munuo alikuwa nabii wa ukweli? ni kweli kwa jinsi alivyowaaga waumini wake kwamba Mungu amemwandalia gari la moto liweze kumbeba? ni kweli kama alivyodai kwamba Mungu amemwita kwa sababu hapa duniani amezungukwa na maadui wengi sana? hebu wana SG tutumieni muda kidogo kujaribu kujibu haya ambayo yamezagaa mitaani.

Kwa taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinasema kwamba Munuo alikuwa amefunga mkataba na lucifa, kwa kawaida lucifa huwa anatoa vibali vyake ambavyo yeye anaona kwamba vinafaa kwako kama ukivihitaji. kumbukeni wakati wa majaribu ya Yesu Kristo, shetani alitaka kumhonga Yesu ili amwabudu. Sasa inasemekana kwamba jamaa aliingia kingi, at the end of the day, mkataba wake umeisha, alipokuwa ameenda kurenew, jamaa alikataa kata kata akamwambia kwamba ‘sasa nataka sadaka yako wewe mwenyewe’ hakuwa na ujanja kabisa na ndiyo maana inasemekana alijua atakufa tarehe ngapi.

Niliwahi kusoma gazeti lake la NEEMA KUBWA alikuwa akielezea kwamba yeye hatakufa, bali ataenda tu sehemu Fulani na kukaa huko maisha yake yote kwa sababu yeye ndiye Adamu wa pili alidai Adamu aliyetarajiwa kuwa wa pili ni Yesu, lakini hakufanya yale aliyopaswa kuyafanya, na hivyo alilalamika sana na kudai kwamba si vizuri katika kipindi hiki kutumia jina la Yesu kwa sababu alishindwa kutimiza makusudi ya Mungu.

Hebu watumishi naomba tujadili kidogo juu ya jambo hili ili tuweze kufufua mioyo ya watu pengine labda sisi ndiyo tuna matatizo siku moja nilisikiliza CD ya Munuo alidai kuwa ‘watu wengi hawaelewi mafundisho yangu kwa sababu wapo gizani’ labda pengine tuko gizani hebu naomba udadavuzi na uchanganuzi yakinifu kama kuna member wa hapo ajaribu kutusadia kama anajua ukweli wa jambo hili

–Mchungaji Dani Seni

Advertisements

60 thoughts on “Nina maswali kuhusu Marehemu Nabii Elia!!

 1. Jacob, utazipima hizo roho kwa kipimo gani ilhali kipimo chenyewe ni hilo Neno la Mungu ambalo umenyang’anywa? Kweli mtu anayethubutu kumwita mwenzake kwamba ni “mungu wa majeshi, Adamu wa pili”, huyo aweza kukudanganya kwamba eti anaiamini Biblia hata iwe kipimo? Huyo ana tofauti gani na na huyu mwingine aliyeamua kumwita mwenzake, “Baba Mtakatifu”? Unaona, ni wahuni wa injili tu hao, watu walioandikiwa Hukumu ….!!!

 2. Mungu asimame mwenyewe maana yeye anahukumu kwa haki.Lakini maandiko yasema zipimeni hizo roho muone kama zinatokana na MUNGU.1YOHANA 4:1

 3. jamani,hata tusemeje,maandiko yanatimia,eti ADAM wapili? wapi Bible imetaja hayo?

 4. MUNGU ALISEMA MJUE SANA BWANA MUNGU WAKO ILI MEMA YAKUIJILIE ,PASIPO KUMJUA MUNGU NAZUNGUMZA NENO,UTABAKI UNANUNG’UNIKA TU KAMA WANA WAISRAEL HATA MUNGU ALIPOWAVUSHA KWENYE BAHARI YA SHAM BADO WALIENDELEA KUNUNG’UNIKA NACHOTAKA KUSEMA ELIYA HAJAMKATAA YESU KWA SABABU YESU YEYE NDIE ALIE SEMA ELIYA ATAKUJA KUTENGENEZA KUREJESHA NA KUPATANISHA NA KUJENGA KAMA YESU NAYE ALIVYOTABIRIWA NA WALIOMTANGULIA , ILA KUMJUA MTAKATIFU NI UFAHAM NDANI YAKE MITH9:10 NACHOTAKA KUSEMA YESU ALIKUJA KUKOMBOA ULIMWENGU ILI WOTE TUSIHESABIWE MAUT .BAADA YA ADAM KUACHA AGIZO mw 2:15 ,mw 3:1 ADAM ALIPEWA NAFSI HAI INAYOTENDA MAPENZ YA MUNGU mw 2:19 NAFSI HY IKAIBIWA AKABAKI MAVUMBI YAANI MWILI .KWASABABU MWILINI DHABI UOVU NA UAS TUNASHUHUDI BAADA YA ANGUKO HAKUNA AMBACHO KILIFANYWA NA ADAM KKMRIDHISHA MUNGU MW 6:1-8 HAD GHARIKA LK 1:26 .YESU alizaliwa kama wanadam mariam alivikwa neema tu ya mungu iliazalie kama sisi ili aje kufuta dhambi mwilin yoh 1:14 neno alivikwa mwili rum 8:2 -5 MUNGU KWA KUMTUMA MWANAWEKATIKA MFANO WA MWL

 5. Binafsi siwezi sema sana kwani nimesali kila kanisa ili ikiwezekana nipone magonnjwa nilio kuwa nayo ilailishindikana ,hivyo nilipo fika siloamu nimepona saizi namienzi 3 sijanywa dawa nahakuna kitu kingine nilichokipokea zaidi ya uponyaji .kimsingi naogopa kusema uongo zaidi yanilicho kiona nakukipokea.

 6. Grace David nakupa pole, mie kilimba nitasema ukweli hata kama unanigharimu. Elia alikuwa tapeli kwa vigezo vyote ukilinganisha mafundisho yake na neno la Mungu. Na kama hakutubu wakati anakufa anasubiri moto wa jehanamu huko aliko.
  Soma uelewe acha kuiishi kwa habari za kufikishiwa Grace.
  Mnadanganywa damu ya haki kweli na hukumu ya kutoka wapi, na nani aliitoa. Yesu alimaliza yote pale kalvary. Hiyo yenu inaweza kuwa ya makafara.

 7. YAANI WHATEVER MUMUITE MJUMBE, ,, HATA MKIMWITA SHETANI KINYESI MIMI NAMPENDA TU!!!! YAANI YOU CHANGE ME NOTHING,, , HAJATOKEA MUNGU KAMA MUNGU WA ELIYA! !!!

 8. Siloam tumeshinda milele, wachangiaji kazaneni kutengeneza Njia zenu.kumtukana ELIYA mnapoteza mda hasa we kilimba.si tumetofautishwa kabisa kitendo cha jua kumtii ELIYA ni heshima na fahari kwetu.toka yesu apae hakuna aliyewahi kuonyesha ishara ya ushindi SK ya harusi yake zaidi ya ELIYA.

 9. Duh!
  Viapo ninavyovisoma humu, vinawakilisha kutawaliwa na roho kandamizi za kichawi; vikilidhihirisha lile Andiko ktk Efe 6:12, kwamba hizi ndizo zile falme za giza; “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

  Kweli hii ni siku ya Uovu; Bwana na akukemee Vai!

  Mungu aliye mwingi wa Rehema, akulinde Kilimba kwa kuipigania Haki yake, makala ulizoziandika, zisimame kuwa ushuhuda wa Kweli iliyohubiriwa kwao, ile Lulu; tena ziko roho zilizoponyeka kwa kuyasoma hayo, wakafunguliwa kutoka vifungo hivyo, ndio sababu amepandwa na hasira, ngome inaporomoka; “… ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara,..” (‭ZAB.‬ ‭7‬:‭14‬) Na amezaa Viapo!!!!

  Ukimbieni uovu; hakuna aliyepaa kutoka sandukuni (coffin), nabii wenu atakuwa ndiye wa kwanza, na sioni utukufu wowote ule kwa Mungu, sana naona ni ujinga uliokithiri! Shetani kawachezeshea phenomena, nanyi kwa kukosa “Mafuta”, ndio mkaaminishwa kuwa amepaa!

  Kupaa kwa aliyekufa huwa kunaanza na kufufuka kwake, Sipendi kumsemea vibaya bwana Munuo, maana ninaamini kabisa kwamba alikuwa ni mtumishi wa Mungu ktk kuyakusanya magugu kwa ajili ya moto; na wala sishangazwi saana nanyi, kwani najua uongo mnaoutukuza wa kumwita yeye Adamu wa pili mungu wa majeshi, ni kijisehemu tu cha ule Uongo kabambe wa mkora anayesubiri kifo kisicho na ufufuo, bali akijiita “Baba Mtakatifu”!! Ni roho yule yule, bali kabadili kanzu tu!

  Siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya yaja; inawaka kama tanuru; kaeni mkao wa “kula” wote mlio ktk kufuru!!!

 10. Bwana asifiwe,yaani huyu nabii eliya tumepoteza muda kumjadili,kwanza alikuwa anatumia kitabu gani

 11. Tunajivunua mungu anayejibu kwa moto.ELIYA ni baba yetu.Hekima yake,na ufunuo wake umepimwa na umedhibitika.Nani aliyewahi kusimamisha jua zaidi ya dk75?Mungu ametudhihirishia ELIYA live kwa live.wakamilifu msiogope Maneno ya mabaal maana hao SWAPO tu!!! Yesu kiz kile mpaka anapaa aliwapata wanafunzi12 tu.ndani ya uumbaji wote.sisi tumeshinda wakamilifu.hakuna hata mmoja ajuaye SK ya kuondoka.lkn ELIYA aliijua na mungu alimtukuza mbele yetu.

 12. HONGERA MKAMILIFU KIBALI ELIYA KWA UFAHAMU WA ELIYA KIZAZI CHA NNE KWA KIAPO KIZURI AMBACHO TUNAJUA HAWAWEZI KUAPA KWA SABABU HAWANA MADHABAHU YA VIAPO ACHANANAO HAO HAWANA UFAHAMU WA ELIYA KIZAZI CHA NNE KANISA TUNATUBU KWA AJILI YAO KWA MAANA HAWAJUI WAYATENDAYO NDIO MAANA MUNGU WA ELIYA AMETUPA UPENDELEO WA KUWA NA MSINGI WA TOBA YA KWELI KUTUBU KWA AJILI YA YOTE VYOTE NA WOTE NAJUA HATA WEWE KILIMBA UKO MFU KWENYE UFALME WA MUNGU NDIO MAANA UNALOPOKA VITU USIVYOVIJUA TUNAKUSAMEHE TU KWA DAMU MOJA NA TUNAKUPENDA KWA SABABU UNAPENDA KUJIFUNZA UFUNUO WA NENO NA TUNAJUA ATUWEZI KUBISHANA NA MAUTI NA KUANZIA SASA HIVI TUNAKUAPIA KUWA WEWE KAMA UNASEMA KUWA NABII ELIYA AMEKUFA KWA SISI KITUO CHA UNABII TUMEAMA TUKO KWENYE KITUO CHA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU KIZAZI CHA NNE AU MJUMBE WA HAKIKAZI KWA TAARIFA YAKO UJUE YA KUWA MJUMBE WA HAKIKAZI YUPO NA ATAENDELEA KUWEPO HADI UNYAKUO WA KANISA NA HAJAFA BALI AMEPAA NA KAMA ULIKUWA UJUI BASI JUA H ILO NA UKITAKA KUJUA ALIE SIMAMISHA JUA DAKIKA 75 NI NANI BASIJUA NI MJUMBE WA HAKIKAZI NDIYE ALIESIMAMISHA JUA NA KUANZIA SASA HIVI UKIENDELEA KULITUKANA KANISA KWA AJILI YA HABARI ZA UONGO BASI NAKUAPIA KUWA KAMA WEWE KILIMBA UNAUHAKIKA KAMA MJUMBE WA HAKIKAZI AMEKUFA BASI NAKUAPIA KUWA MIMI NIFE NA KAMA HAJAFA BASI WEWE NAKUPA SIKU 7 KUANZIA LEO TAREHE 30/01/2015 HADI TAREHE 08/02/2015 KABLA YA TAREHE HIYO NAKUOMBA UJISALIMISHE KWA MUNGU WA ELIYA KABLA HUJALAZWA MAHALI PEMA PEPONI AMBAPO PAMEJAA MAPEPO MUNGU WA ELIYA ANAKUPENDA TUMECHOKWA NA MANENO YAKO TUNAMSHUKURU MUNGU WA ELIYA KWA AJILI KUTUVUSHA MWEZI ZIVU NA KUTUINGIZA MWEZI SIWANI HONGERENI WAKAMIFU KWA KUVUKA MWEZI TUKU JUU NA DUNIA BAI BAI

 13. kibali uweza eliya Ukiona kichaa anajinadi anaweza piga kila mtu ukaenda kupigana naye. Wewe utakuwa na level kubwa zaidi ya ukichaa kuliko kichaa aliyejinadi. Munuo alikuwa mwabudu shetani hata Yesu alisha mkataa na hakuwa anataka kumtaja unashindania nini naye, wakati yeye alishashindwa tayari kumfuata Yesu mtoa uzima. Tunajua nia ya siloam ni kujaza watu kuzimu, ndio maana hata Roho mtakatifu mwalimu na kiongozi wetu ambaye Yesu alimwachia kanisa hamumtaki.

  Mnatupotezea muda kujadili mambo yetu maana ni purely upotofu ambao hauhitaji hata kujadiliwa maana uko wazi kwa kipimo cha neno la Mungu. Hapo ulipo huna kibali labda kwa hayo mashetani ya Munuo na huna uwezo wowote labda wa kubabaisha waliokosa maarifa ya neno la Mungu.

  Pole sana.

 14. Kibali Uweza Eliya. Wewe una Matatizo katika Akili na roho yako.Usifikiri kula KIAPO ni sifa.Hata Biblia ilisema ‘USIAPE KWA MBINGU WALA KWA NCHI’.Unasema Umekula KIAPO,hiyo inamaanisha kuwa mapepo yaliyokuwa ndani ya Munuo hata wewe unayo.Pia hicho KIAPO humaanisha kuwa Hutatoka Mpaka Ulipe senti ya mwisho.Kuhusu VITISHO VYA KUJA MADHABAHUNI unavyowatisha WACHANGIA mada unapoteza muda bure!KUTHIBITISHA IMANI haihitaji kuja madhabahuni ila IMANI NI MATENDO hata kwa KUNENA hutendeka.MUNUO kawajaza MAPEPO sasa mnalipuka!!Eti Munuo ni Adamu wa pili mungu wa majeshi na ninyi mnakubali kama mmelaaniwa. Pia Munuo Kawaambia 2008 alimuua shetani na ninyi mnakubali! Ndio maana Munuo Kauawa na shetani.KWELI MMELOGWA NA SHETANI ambaye mnadai aliuawa na huyo Mchaga wenu hata hamna ufahamu wa kawaida!

 15. Nashukuru sana kwa kupata neema hii ya kusema hili mjumbe wa mapenziyamungu alishawahi kutoa viapo vingi tena madhabahuni lkn acha niseme kiapo chake 1
  Nanukuu
  Wamlete mungu wao naye amwombe mungu wake kisha waone ni mungu yupi ni wa kweli akafafanu waje manabii na wachungaji wa kila kona ya dunia dini na madhehebu wamwombe huyo mungu wao kama anachofanya si sahihi na afe mbele yao na wakishidwa wamruhusu mungu wake awauwe haktokea hta 1 mpk leo hii sasa mnajinadi nn huku
  Nawaruhusu hta sasa kama mnajiamin mungu mnayemwomba n wakweli ksanyikeni muombe kwa huyo mungu wenu watuuwe kwa kuwa tunapotosha watu wake la mkishidwa mturuhusu sisi sihitji kuendelea wwkama unajiona upo sahhi fanya hivy tunakukaribisha madhabahini au mumuite popote kuhni kiongozi aliyekabidhiwa mskani wa kuongoza kanisa awaonyeshe mungu tnayemwabudu n yupi msiangaike na ambaye haonekani

 16. Kila tulifanyalo tulifanye kwa jina la Yesu. Colossi 3:17 “And whatsoever ye do in WORD OR IN DEED do all in the name of the Lord Jesus….” kwa nini walijitofautisha ktk salaam za watakatifu? Lengo ni kutolitaja jina hili linaloheshimika mbinguni duniani hata chini ya ardhi. Jina linawakera. Bwana Yesu asifiwe sana. Shika neno lipi!!? Nimekuja mkoa wa kilimanjaro kijana mmoja wa hiyo dini akaanza kunishuhudia kwamba mjumbe alipaa na Mungu wa eliya wao alidhibitisha kwa ishara zilizoshangaza dunia. Vyombo vya habari vilitangaza ndani ya nchi na nje hata chombo mashuhuri CNN ilitangaza hayo maajabu. Kweli sikusikia Tz Meteorology Dept . au CNN ikitoa habari hizo. Labda TBC iligusia juu ya upinde wa mvua. Jambo lingine lililonishangaza waumini wao wote wamekatazwa kusikiliza habari za mahubiri ya mtumishi wa Mungu Christopher Mwakasege ; pia wasisikilize Radio Safina au mafundisho yoyote nje ya imani yao ya Mungu wa eliya. Namshukuru Mungu aliye baba wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo kwa kuniokoa kunijaza na Roho Mt. ambaye amenisaidia kugundua upinzani wa elimu ya Mungu Mt. Kipitia NENO lake. Kuna ujanja iliojificha wa kutaka kuondoa jina la Yesu na kupachika lingine. Nafurahi nikiitwa Mlokole; au mtu wa dini au dhehebu. Mungu anajua mimi ni wa Yesu Kristo na makao yangu ameniandalia mbinguni. Ukiniita mbwa siwezi kuwa hivyo unajiridhisha mwenyewe. Kanisa la kweli atakalochukua Yesu Adam wa Pili halisi si siloam ni kanisa la kristo lililo chini ya uangalizi wa Roho Mt. La siloam labda atakuja kuchukua Ad2 wao feki. Kama sina ufahamu wa mafunuo yao, ya Yesu Kristo aliyenifilia akanikomboa yanatosha kunipa uzima wa milele soma lsaya 35:8.-9. Nina kazi ya ziada kuwaombea hawa wapendwa ili wafunguke maana vifungo walivyogungwa vinatisha. Lakini Mungu anaweza. Praise the Lord Jesus Christ. Beloved Remain Blessed.: AMEN.

 17. Grace David kama utapeli unampa Mungu utukufu basi Mungu wenu atakuwa Lucifer. Kiwanja cha makao ametapeli akamlazimisha mzee kimambo kuoa kumbe ilikuwa gia ya kuteka ufahamu wake na baadae kumhadaa kuwa Mungu kasema kiwanja chake kijengwe kanisa.

  Kwa taarifa yake siandiki kwa kuhisi, ninauhakika na ninachokiandika Munuo hakuwa na Mungu, ndio maana alijaa kuwatisha tu kama vile ananguvu kumbe tapeli tu. WEWE USIPOGEUKA NA IMANI YENU HIYO BANDIA KWA HUYO TAPELI JEHANAMU HALALI YAKO KAMA ILIVYO KWA WAISLAMU NA WOTE WAFANYAO MACHUKIZO MBELE ZA BWANA.

 18. Nikweli kabisa alishaonywa lakini hakusikia kwa hiyo baada ya kufa kazi iliyobaki nikumwachia Mungu sisi kama watumishi wa Mungu hawa aliowaacha chini ya huduma yake kwa sasa bado wanaendeleza upuuzi hasa kama ulivyomsikia mjane wakea alishatangaza kufuta baadhi ya mistari ya biblia huyu sasa ni saizi yetu kumkemea na kumuonya kwa nguvu zetu zote

 19. mtu hunena yaujzayo moyo wako,mi naona ni heri kuangalia safu yako mbele za mungu kuliko kutukana kitu usichokijua.eliya anakazi mbele za mungu wa majeshi.na kazi zake zimesimama kwa haki ya mungu.kama kweli umeokoka kaa kwenye maombi muulize mungu kuwa huyu eliya wa siloam ni nani mbele zako?nahakika mungu atakujibu.kwa miaka 12 amefanya kazi kubwa inayompa mungu heshima.we una kazi gani au matunda gani ndani ya ufalme wa mungu?na je leo mungu akiamua uondoke au ufe unachakuonyesha kwake?kuwa makini usije ukawa unamtukana mungu bila mwenyewe kujua kwa ushabiki wa hekima ya dunia.

 20. Mi nimekuwa msomaji kwa muda mrefuu lakini nimeona nami nichangie tena hapa.

  Japo sifahamu jina lako ni UWEZA wa kufanya nini lakini uliyoandika hapa yamenigusa mno:

  “4)NITAMWOMBA MUNGU PIA ATUPE MACHO ILI TUONE KAMA HUYU ELIYA TULIEMTUKANA ALIKUWA MWONGO AU MKWELI?
  Ahsante kwa leo na mungu asiye mwanzilishi wa dini wala dhehebu AYATHIBITISHE HAYO”

  Ni maneno yanayoonyesha KIU ya Mungu wa kweli alete jibu. Lakini je, akileta jibu tutafahamu? Nabii Eliya alimuomba Mungu na kumwambia kuwa AJIBU KWA MOTO ili watu wajue. Sasa sijuwi ndugu yangu utamuomba Mungu athibitishe vipi ili akithibitishsa wote tujue kuwa Mungu ndiye kathibitisha?

  Yehova Mungu atusaidie sana kwa katika jambo hili.

 21. Mungu wa eliya akusamehe kaka,mmmh kama unaweza kumtukana mungu kiasi hicho onamaanisha we ni mpagani.!!!!!! MUNGU WA ELIYA HASHINDANI NA HEKIMA ZA WATU NA WANADAMU WALA DUNIA.HIVYO WAKAMILIFU TUSISHINDANE NA WASIOFUNULIWA.NDIO MAANA TUNA NEEMA KUBWA!!!!!.NI NEEMA KUBWA KWELI SIO MCHEZO.ELIYA NI MJUMBE WA KIZ 4 KWA SISI AMBAO ROHO AMETUHUISHA.KWA MLIOZOEA MAPOKEO NA RITURUJIA SIO RAHISI KUMKUBALI MJUMBE ALIYETUMWA!!!!!

 22. UWEZA usipoteze muda wako wa thamani eti kumwomba huyo Mungu aliyemtuma Munuo kumdharau Yesu na Damu yake. Hana majibu ndio maana alishindwa kumponya mtumishi wake na TETENAS TU. Elia wa siloam alikuwa mwongo na tapeli, unaweza kuwa huyajui mengi. Niliwahi sema huko nyuma tutayajua mengi sana akiondoka muhusika maana aliwatia hofu watu hawawezi sema hata kama wataona tatizo kama ulivyo wewe. Pamoja na hilo ni vigumu wewe kuona maana ulisha jiungamanisha na maroho hayo ya udanganyofu kupitia viapo mlivyolishwa huku mkichekelea.

  Google mada hii halafu angalia kilichopo: Kifo Cha Nabii Eliya Munuo,Mungu amesikia sala ya mnyonge wake.
  MAKAO NI ENEO LILILOTAPELIWA KUTOKA KWA MZEE KIMAMBO, LABDA ILIKUWA NI MAFUNUO, SASA INAKUWAJE MZEE ANALALAMIKA.

  Wengi wenu ukiwepo wewe mmeumia sana kimaisha kwa udanganyifu wa huyo nabii. Tamaa ya mafanikio imewaingiza wengi kwani mlidanganyika kuwa kwa neno la nabii MTATAWALA NA KUMILIKI.

  Ninajirani yangu mke wake anasali huko, mjumbe wa shetani akatoa unabii kwa neno la Nabii wafuasi wakalime watafanikiwa sana. Mama kachukua neno lama lilivyo akamshawishi mumewe, hakukubali kwa kuwa tayari walikuwa na malengo mengine. Mama akalazimisha na akachukua na mkopo, jumla alitumia karibu milioni mbili, mavuno hata gunia moja la mhindi hakupata.

  Narudia tena mimi sio mchungaji na sijasikia wito wa kuwa mchungaji, hivyo sina masilahi ya moja kwa moja kwa kuwaambia ukweli mkatoka huko, wala sijawahi hata kusema naabudu wapi, maslahi yangu yanabaki katika kusema kweli ya yeye aliyeniokoa ili mpone.

  UWEZA MUNGU BADO NI WA REHEMA, MRUDIE YEYE UTAPONA, NA KAMA UTASHUPAZA SHINGO MUNGU HANA HASARA, ANAO WENGI HASARA IKO KWAKO WEWE NA WAFUASI WENZIO. NA MKIKUTANA NA MUNUO HUKO ATAWASUTA VIZURI KWANI NILIWALAZIMISHA SIMLINIFUATA WENYEWE.

  UONGO WA HUYU MTU UMEELEZWA KWA WINGI NDANI YA BLOGU HII HUTAKUWA NA SABABU YA KUJITETEA.

  MMEINGIZIWA UTAPELI MWINGINE TENA ROHO YA MTU HAIKAI KWENYE MAITI, LEO MNADANGANYWA ROHO YA HUYO TAPELI ILIPAA SIKU MNAZIKA (SIKU NEE BAAYA YA KUFARIKI). SHETANI AMEWANYANYASA AMEPITILIZA NA BADO MNAMCHEKEA. ACHA UBISHI AMBAO HAUTAKAA UKUSAIDIE MFUATE YESU. KIMBILIA KWA YESU HUFI NA HAYO MADUDU HAYATA KUDHURU NG’O.

 23. Namshukuru Mungu wa Kweli atendaye yote kwa ukamilifu wa Moyo, Roho, na Nafsi yake.
  Namshukuru pia kwa ajili ya kila mmoja aliyejaribu kukieleza kile alichojifunza na anachokijua.
  Kwanini nasema hivyo?
  Kwasbb huwezi kusema usichokifahamu au kikijua!
  Mi nadhani mila mmoja amejaribu kutamka kile alichonacho, na kwahiyo NI rahisi sana kumjua mila mmoja ana ufahamu UPI kuhusu Mungu.
  Mimi nachokiona hapa NI wengi kutokujua hasara za kuhukumu wengine, au kutokukubali kwenda mahali panaposemwa vby ili sao wenyewe wasikie waone na wawe mashahidi wa ama mambo mby au mazuri yasemwayo kuhusu sehemu husika.
  Hii NI dhahiri kuwa wasiomjua Mungu wana Akili kuliko sisi tushindao makanisani mila Leo.
  Kvp? Mpelelezi akisikia tuhuma fulani inayokuhusu huwa haji akakukamata eti kiss amesikia.
  Ila atatumia muda, gharama, na hata anaweza hata kukutana na mambo mengine ya hatari Ali mradi aupate ukweli. Kilichonipa kushinda na kuogopa hata Kimnyooshea kidole yoyote NI ile hali ya kutaka kujifunza na ktaka kupata ukweli wa mambo yasemwayo pasipo walakini.
  Kwa njia hii nimefanikiwa kukaa na wengi pasipo hata kulumbana. Lkn pia niliowaona wako kando ya njia sikupata tabu kuwarejesha kwa SBB nilipata neema ya kuongea nao vzr pasipo kuwalaumu au kuwatisha.
  Nikirudi ktk hili ninaona wakristo wa sasa tukiwa na makundi ambayo yanaonekana yakipigana rohoni japo hayajashika silaha zionekanazo kwa jinsi ya mwili.
  Nimeshangaa wengine wanajiita apostle lkn walivyochangia ktk mada hii wanajidhihirisha hekima japo kdg tu ya Kiungu kwao haipo.

  MIMI NIKIFANYACHO KUANZIA LEO,
  1) ZABURI YA 100:4, ZABURI 92:1-2
  Nitamshukuru Mungu kwajili ya wachngiaji wote mliochangia
  2) NITATUBU PIA KWAJILI YENU

  3)NITAMWOMBA MUNGU ATUPE NEEMA YA KUFUNGULIWA MACHO ILI TUJUE NI WAPI PALIPO SAHIHI KUMBUKUMBU 12:5-7
  4)NITAMWOMBA MUNGU PIA ATUPE MACHO ILI TUONE KAMA HYU ELIYA TULIEMTUKANA ALIKUWA MWONGO AU MKWELI?
  Ahsante kwa leo na mungu asiye mwanzilishi wa dini wala dhehebu AYATHIBITISHE HAYO.
  AMINA AMINA AMINA…….

 24. Bwana Yesu Asifiwe!
  Nafurahi kuona wakristo wenye ujasiri kukemea uovu na kuwajulisha wengine iliyo kweli, Kilimba nakuomba uendelee vema na kwa hekima yote. Lakini nashangaa ni kwa jinsi gani shetani amefunga mioyo ya watu kiasi cha kutoona kabisa, imefikia wakati kinyesi kinaitwa ‘keki’, haina maana ya kuhukumu lakini ndugu zangu ni uwazi kabisa kwamba Imani potofu sasa zinatenda kazi waziwazi na sisi Wakristo ni muda wa kuzisema na kuzikemea waziwazi. Kama shetani anaffanya kazi waziwazi kuiba na kuua hata waliokuwa viongozi wazuri wa imani za kweli kwa nini tulio nuruni tusimulike?
  Binafsi naomba huu uwe ni mwanzo tu, inapotokea nabii mwingine au mchun gaji au mtumishi yeyote ambaye bila shaka tunajiridhisha kwamba ni wakala wa shetani tusisite kuwajulisha wengine ambao muda wa kuchambua Biblia hawana wanasubiri ‘manabii hao wawape sumu’. Mwisho nawaomba wakristo wenye mapenzi mema kwa wale wanaopotea tuungane katika maombi kama yale aliyoomba mtume Paulo kwa waefeso akiomba mioyo yao itiwe nuru. Soma Waefeso 1:15-18. Naamini Roho Mtakatifu atatufundisha na kutusaidia jinsi ya kuomba ipasavyo.
  Yesu Kristo, mwana wa Mungu, Alfa na Omega ashukuriwe!

 25. Amani ys Kristo Yesu iwe kwenu katika utimilifu wote!
  Ndugu Bariki kadhi,
  Kwanza nasikitika uliyoyaandika na kwa bahati mbaya yakaruhusiwa kuwekwa hapa kanisani; LUGHA YAKO si lugha nzuri unayoweza kusema na jirani yako wala mpita njia wala ndugu yako wala mzazi wako UNLESS “uko kwenye upako husika”. Nadhani kama utaweza kukaa, ukatafakari na neema ya Mungu ikakutembelea juu ya hilo utaingiwa na hekima na kuja kuomba msamaha wa kuwatukana watu kuwa wao ni mapepo nk.

  Sikuwahi kumsikia Yesu akimtukana mtu kuwa pepo mdogo, ama mkubwa ama shetani, hili naona ni tatizo la kukosa “nguvu ya Mungu ndani” na hatimaye “nguvu itendayo kazi huko ndani ya mtu” ikajibu sawa na matakwa yake. Yesu alizitaja na ali-deal na roho zilizokuwa ndani ya watu. Mfano alimkemea Shetani ndani ya Petro na wakati mwingine akikitaja kizazi cha nyoka lakini hakuwaita wao kuwa nyoka wala Petro kuwa ni Shetani (Re-read your Holy Bible).

  Watu hawawezi kuaminishwa jambo la kimungu kwa nguvu za kimwili, kwa matusi na majidai WALA watu wenye dhambi na waasi dhidi ya Mungu hawawezi kuitwa ama kukaribishwa kwenye neema ya wokovu wa Mungu kwa matusi na jazba.
  Ngoja nitoe mfano hapa; Uko na njaa sana na unapita karibu na hoteli, fedha unayo na hamu ya kula unayo, ukifika mlangoni unakutana na mkaribishaji wateja anakuambia “KARIBU SANA WEWE NJAA KALI, ULIYECHOSHWA SANA NA NJAA, USIYEJITAMBUA KAMA CHAKULA KIZURI KIKO HAPA NA HUKO KOTE UMEWAHI KULA HAKUNA CHAKULA KAMA HAPA. MWANGALIE KWANZA ALIVYOLEGEA HUYU PUNGUANI, HATA KUTEMBEA HAWEZI….mwishoni anaendelea NGOJA TUKUACHE KWENYE NJAA YAKO ILI IKUFUNZE ADABU ili siku nyingine usitukane tena chakula chetu. Mwisho anamalizia ndimi mhudumu na mkaribishaji mwaminifu na wa haki aipendaye hoteli hii.

  Je mtu huyo Mwenye njaa hata kama anakaribia kufa atakuja hapo kula?

  Swali lingine: Je unajua maana ya KADHI? Unajua jinsi kadhi anavyotakiwa kuishi kulielewa kwa kina, marefu na mapana kila neno analotakiwa “KUTAMKA” na madhara/athari zake?

  Please please, tusifanye hapa ni kijiwe cha wabeba zege pamoja na wabeba mizigo mizito wa bandarini na viwandani wa Tanzania wa miaka ya 1980 wa Dar-es-Salaam Tz, waliosifika kwa matusi ambapo hata wakipewa salamu na “mtoto mdogo asiyejua kitu” waliporomosha matusi kama fataki za vita.

  Yesu Kristo awabariki!

 26. Bariki kadhi huyu alikuwa freemason mwenzako, hatukushangai ndio maana umejaa lugha ya matusi, huna lolote wewe ulikuwa mfuasi wa marehemu Munuo, tapeli mkubwa, endelea mwisho wake utauona, mwenyewe alishauona, bado zamu yako.

 27. Wapendwa tumuombe Mungu atupe neema ya kuelewa kweli yake ili ituweke huru.Manabii wa uongo tayari wapo hivyo unabii unatimia.Jambo la msingi ni mahusiano mazuri na Roho Mtakatifu.Kamwe tusiwe wepesi wa kusema unless tumefunuliwa na Mungu mwenyewe.Pili kila jambo tulipime kwa mzani wa neno la Mungu.Mbarikiwe

 28. Hahaaaaaaa! Hahaaaaa! Namshukuru MUNGU sana kwani leo kanipa kicheko chake mwenyewe kile kinachoangamiza maadui (mashetani) wote-Zaburi 2: 4.
  Sasa nimeamni kwamba ukiwa na nafsi ya shetani ndani yako (nafsi iliyokufa) kamwe huwezi kuyajua mambo ya ufalme wa MUNGU, na wala huwezi kumjua MUNGU wa KWELI wala Kumkubali.

  Wengi mnajiita, na kuamini kwamba ninyi ni wakristo na kwamba mnamuabudu Mungu, lakini kumbe ninyi siyo wa -wakristo bali ni ‘wakristu’ ambao mnamuabudu mungu shetani yule mwanzilishi wa dini na madhehebu yote aliyoandikwa kaika kitabu cha 2 Wathesalonike 2: 4.
  Kweli ninyi ni vipofu na wajinga (wapumbavu) wa mambo ya ufalme wa MUNGU, na pia mko kando ya njia kabisaaaa! Mmepofushwa fikra na ufahamui kwa elimu ya dini na madhehebu (ambayo imeanzishwa na shetani) yenye kujaa madanganyo matupu ( Kolosai 2: 8)
  Hamstuki? Hamjasoma? hata MUNGU mwenye amezikataa hizo dini zenu zilizo, na zinazo enedelea kuwatia giza na ujinga (soma Amosi 5: 21-23)

  Lakini shingai kwani hata YESU mwenyewe ambaye pia alitoka kwa MUNGU mlimkataa (na mpaka sasa mnamkataa) na mnamchukia kwa sababu hamyatendi aliyowaagiza (Yohana 14:21)

  Sasa hata huyu ambaye MUNGU amemleta kwa ajili yenu ambaye YESU mwenyewe alitabiri kuja kwake (Mathayo 11: 13-14) na Malaki 3: 1-2, Malaki 4: 4

  Kiukweli, japo mimi siyo mwana SILOAMU, lakini ninaujasiri wote wa kukubali na ninauthibitisho kwamba huyu aliyekuwa anaiywa NABII ELIYA, AD2 MUNGU WA MAJESHI ni NABII wa kweli na aliyoka kwa MUNGU

  Nawashangaa namna ambavyo mnafungua vinywa vyenu na kunena mambo machafu juu yake, huku mkiwashangilia manabii wenu wengine wa UONGO ambao kila siku wanafumaniwa na mabinti gesti, wachawi, walevi na wengi tunawashuhudia mitaani wakifanya mambo machafu, ikiwamo kuwapa wanafunzi mimba na kuzukumu pesa za waumini wao.
  Kama mnajua kweli kwamba Biblia imesema nabii wa kweli mtamjua kwa matunda yake, JE? hayo ndiyo matunda yaliyowapa majibu kwamba hao manabii wenu na hayo makanisa yenu ni ya kweli.

  Nani kati yenu akihojiwa hivi leo anauthibitisho wowote wa kashfa yeyote mbaya juu ya NABII ELIYA WA KANISA LA SILOAMU?

  Wengi mnamuhukumu kwa sababu ya mambo ambayo alikuwa anayazungumza madhabahuni (mafundisho yake) pasipo kujua kwamba ndani yenu mna nafsi ya giza na umauti ambayo haiwezi kuyafamu yanayotoka kwa MUNGU . Shishangai lakini, kwani hata YESU mwenyewe walimshangaa kwa aliyokuwa akiongea na wengine kwa akili zao za kijinga (kama za kwenu) wakafikia hatua ya kumwambia kwamba ana MAPEPO (Yohana 8: 49-52)
  Kwa hiyo mnavyosema kwamba ELIYA WA KANISA LA SILOAMU alikuwa agent wa shetani , shiwashangai kwani hayo ndiyo mnayofundishwa na baba yenu SHETANI ( Mapepo wakubwa niniyi)

  YESU alizaliwa kama wanadamu wengine wanavyozaliwa, na akafanya kazi kama wengine, akala chakula wanachokula wengine, akavaa kama wengine, lakini majira yalipofika ya MUNGU kuanza kumtumia, MUNGU akamtia mafuta ( Luka 4: 18-19) na mafuta yale yakambadilisha na kumpa mamlaka yote ya MUNGU.

  Sasa mlitegemea ELIYA aliyetabiriwa na YESU kwamba atakuja majira haya ya mwisho aje kwa njia gani? Na ungo toka kuzimu? ama na saani ya dhahabu toka Mbinguni? (MAPEPO NINYI)
  Eti wengine mnasema alikuwa anawadanganya waamini wake kwamba kuna kizazi channe na kumbe hakipo, yote haya ni kwa sababu ya ujinga wenu wa kufananisha mambo ya ufalme wa MUNGU na siasa (someni basi Mwanzo 15: 16) au hapo hakijatajwa kizazi cha nne?

  Kumbukeni mambo ya ufalme wa MUNGU yanahitaji utakatifu na usafi wa moyo ili uweze kuyafahamu na kuyapokea, na shangaa wengine mkishakunywa pombe zenu mnaanza kuongea na kupost kwenye mitandao mambo ya kijinga kwa
  mpakwa mafuta wa MUNGU (Hii ni tabia ya asili ya mwanadamu na shetani—Yakobo 3: 15)

  KANISA LA SILOAMU MTAKE MSITAKE NDILO KANISA LA KWELI, NABII ELIYA NDIYE NABII PEKEE ALIYEKUWA WA KWELI, NA AMBAYE MPAKA SASA ANAISHI AKIWA NENO LA UFUNUO KIZAZI CHA NNE

  Ha! jamani haya maana ya ukristo hamjui kweli ninyi ni ‘punguani’ tena wa kuzimu na ndani yenu mmerithishwa nafsi, moyo na roho ya baba yenu lucifer aliyemuasi MUNGU toka pale kwenye Mlima mtakatifu (Ezelieli 28: 13—)

  Aaa wala msinichoshe kwa leo, ninyi nawaweka fungu moja na baba zenu ambao walijifanya wasomi na wakawaingizi elimu ya dunia (yenye asili ya shetani) ambayo imewapofusha macho na wala hamna adabu mbele za MUNGU wa KWELI .

  Sasa ngojeni niwaache katika mikono ya shetani mnaempenda ili awafundishe adabu siku nyingine msimtukane MUNGU (1 Timotheo 1:20)

  Wakubarikiwa, mbarikiwe, na wale wa kulaaniwa, mlaaniwe milele ninyi na baba yenu shetani marehemu

  Na, Kadhi mwamanifu, ampendaye MUNGU

 29. haihitaji uwezo mkubwa kiroho kumtambua nabii wa uongo, kwani kila roho inayofundisho kuwa kuna bwana mwingine tofauti na yesu hiyo si ya mungu bali ya shetani, ahsanteni wapendwa

 30. Shalom Aleichem!
  Kama walivyochangia baadhi ya washiriki, ni kweli kazi ya kuhukumu mtu yeyote awe mtumishi wa madhabahu ama mshirika wake ama mtu wa kawaida haituhusu, kinachotuhusu ni kukemea fundisho/ imani potofu tukilinganisha na maandiko ili kuwaelekeza hao wapoteao / wapotezwao na mafundisho husika kuijua kweli.

  Mimi ninapenda niwaambie hapa kuwa imani hii ya Siloam ya hapo Tanzania inafanana sana tena kwa karibu na dini nyingine iliyoanzishwa mwaka 1956, dini hii inaitwa “BROTHERHOOD OF CROSS AND STAR”. Nadhani baadhi ya watu wenye FTA (Free to Air) television systems watakua wanaona channel yao BCS yenye nembo ya nyota na mwezi.
  Kifupi dini hii inaamini;-
  1. Yesu hakuwa na muda wa kumaliza kazi yote aliyotumwa (alikufa haraka sana) hivyo OBU (Olumba Olumba) ndiye aliyekuja “KUJAZILIZA” kazi hizo na “KUZIREKEBISHA”. Hadi sasa huyo OBU…. anasemwa kwamba ameshafanya makubwa kuliko yale Yesu alifanya.
  2. Obu aliyezaliwa mwaka 1918 (sasa anaiongoza mwanawe) amekuwa akiabudiwa kama Mungu japo yeye mwenyewe amekuwa akikiri si Mungu ama Yesu Kristo wakati mafundisho ya dini hiyo yakikiri kuwa yeye ni “MFALME WA WAFALME” na roho mtakatifu.
  3. Msingi wa imani yao hauko kwenye Agano la kale na lile jipya la Biblia kikamilifu na hivyo yameongezewa na vionjo vya mila na desturi za Kiafrika.
  4. Huvaa mavazi meupe na LAKINI kiongozi wao mkuu huvaa mekundu…..
  5. Hawaamini dawa za mitishamba wala miti ulaya (si hospitali wala tiba yeyote).
  6. Hawaamini katika kufa kimwili (Mkuu wao alisemekana kufa na wakamzika kwa siri, hadi leo wanaficha kwamba amekufa).
  7. Wanaamini Dini (kanisa lao) linatawala dunia pasipo magonjwa wala taabu….

  Kwa leo niishie hapo, ukiwa na muda waweza kusoma zaidi kwenye mtandao na kulinganisha na Siloam ya Tanzania ufanye ulinganifu.
  Ref:
  http://en.wikipedia.org/wiki/Brotherhood_of_the_Cross_and_Star
  http://www.naijarchives.com/olumba-olumba-obu/
  Na nyingine nyingi

 31. Tumaini ni kweli unalosema lakini sio wote wanaupeo wa kuona unavyoona ndio maana wako watu mpaka leo bado wanaenda kwenye utapeli huu ambao sasa uko hadharani. Eti gazeti lao la NEEMA KUBWA la wiki iliyopita linasema nabii alipaa, wakati huohuo wanazika mwili wake kaburini. Elia Mtibishi hakuzikwa wangekuwa na uwezo wa kufanya mazingaombwe wangefanya ilikuendeleza uwadanganyifu, lakini shetani mtaji wake ni mdogo, ndio maana kafilisika mapema na mambo yote hadharani. Vinganganizi watakuwepo kwani hata waislamu siwanajua kuwa hawana Mungu wa kweli ndio maana wakawekewa sheria ngumu ili wasitoke, kwani ilibadilikuwa sasa wana Mungu wa kweli.

  Siloam church you are proving openly now that you are the access of evil with your shameless lies. You buried your fake prophet in Mapinga, and yet you are claiming that he ascended to heaven. EVEN POLITICIANS HAVE NOT COME TO SUCH AN EXTENT OF BLACK AND WHITE LIES.

 32. Daaaaah!Hakika mtawatambuwa kwa matunda yao!je watu huchuma zabibu ktk miiba au tini ktk mibaruti?Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mema;na mti mwovu huzaa matunda mabayaa.Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya,wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa,ukatupwa motoni.Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.Si kila mtu aniambiaye Bwana,Bwana atakayeingia ktk ufalme wa mbinguni,bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.Wengi wataniambia siku ile Bwana,Bwana,hatukufanya unabii kwa jina lako kutoa pepo,na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?Ndipo nitawaambia dhahiri sikuwajua ninyi kamwe;ondokeni kwangu ninyi mtendao maovu.daaaaah!mbona matunda yake yameonekana?C.K,Mjema,Haule, Kaka Mkubwa Edwin,Sungura,Siyi, Kilimba, Faith, Mrs Christina, Bishop Yuda.Kuna hoja tena hapa wandugu?mbona mambo yote hadharani?hakuna ubishi wa kutunisha misuli hapa.

 33. Bishop uko sahihi kuwa hakuna haja na kuongea habari za marehemu kwani yeye hayupo lakini hatujaanza kujadili upotofu huu baada ya kufa kwake kunamijadala ambao inamuda mrefu saana some Mjadala juu ya Shetani amekufa na Kanisa la siloam wanaamini nini utaona, kuwa kumekuwa na mijadala hii muda mrefu. Shida ni kuwa huyu hakuwa na sikio la kusikia maana kuburi kilimpanda na hata kujiona yeye ni ADAM WA PILI.

 34. UJUMBE WA YESU KWA WATEULE WA KANISA LA TANZANIA!

  Ujumbe huu mzito kuliko uzito wa dunia unatoka katika kitabu
  cha MITHALI 1:10-33.Tunapaswa kusoma na kutafakari mistari
  yote kwa muongozo wa Roho Mtakatifu.Kwa sasa mimi nitaandika
  kile ninachoongozwa kwa njia ya hekima na mafunuo ya Roho wa
  Kristo.Huu ni ujumbe uliobeba UNABII na ONYO kwa wateule wa
  Tanzania ambao wako tayari kutumia hekima na maarifa ya Yesu
  kupambana na uzao wa nyoka(manabii wa uongo).Kwa sasa hawa
  manabii wa uongo si tu kwamba wamejipenyeza kwa siri ndani ya
  makanisa yetu lakini pia wanatufutilia kwa karibu sana mashuleni,
  vyuoni, makazi na majumbani .Katikati ya makazi tunayoishi wamesha
  anzisha ‘makanisa’ yao pia tunatakiwa kuwa makini na hawa mabinti
  wanaofanya kazi za ndani katika majumba yetu.

  Hebu sasa tusikilize kwa kutafakari sana kile ambacho Yesu
  anatuambia;

  Tunaanzia Mithali sura ya kwanza mstari ule wa 10 na kuendelea
  ” Mteule , manabii wa uongo wakikushawishi wewe usikubali.
  Wakisema njoo katika ‘makanisa’ yetu tushirikiane pamoja kutoa
  kafara za kumwaga damu na kuwashusha kuzimu watu wasio na hatia,
  na kukuvuta na injili za mafanikio ya miujiza ya shetani kwa ahadi
  za kukutajirisha na mali za kishetani. Wewe tafuta macho na hekima
  kutoka kwangu ili uuzuie mguu wako usiingie katika hila zao”

  “Mteule sikiliza, kazi ya manabii wa uongo ni kuongeza bidii katika
  kufanya maovu na kumwaga damu za wenye haki. “Makanisa ” yao
  ni mitego ya kuwanasa ndege(wenye haki) wanao tanga tanga katika
  kutafuta kila chakula kinachowavutia.Manabii wa uongo walishamkufuru
  Roho wangu,kwahiyo siku zote hujiotea damu yao wenyewe,hujinyemelea nafsi zao wenyewe na kuuondoa uhai wao
  wenyewe kwa tamaa ya baraka za shetani”

  “Mimi ni Hekima ya Mungu, napaza sauti katika njia kuu na katika
  viwanja na mahali penye mikutano mikubwa ya watu wangu.Enyi
  wajinga hata lini mtapenda ujinga wa kuchukuliwa mateka na manabii
  wa uongo? Upumavu wenu wa kutokubali kunyenyekea umewafanya
  mchukie Maarifa yangu na kuyadharau.Geukeni kwa ajili ya maonyo
  yangu.Tazama mnae Roho Mtakatifu ambaye anawajulisha kweli
  yote kuhusu manabii wa uongo na hila zao”

  “Wale wote walionikataa na mimi nimewakataa.Kwa maana niliwaita
  na kuwapa mkono wangu lakini wakajifanya kama hawauoni.Wamebatilisha Neno langu na kukataa maonyo yangu.Tazama
  sasa NINAWACHEKA SIKU YA MSIBA WAO na KUHIDHIHAKI HOFU YAO.DHIKI NA TAABU ZITAENDELEA KUWATAFUNA.HOFU YAO ITAKUWA KAMA TUFANI NA MISIBA YAO KAMA KISULISULI. NA HATA
  WATAKAPONIITA, MIMI SITAITIKA. WATANITAFUTA KWA BIDII LAKINI
  HAWATANIONA, KWA KUWA MIMI NI MAARIFA NA HEKIMA YA MUNGU
  AMBAYE NIMEJIFICHA NDANI YA UNYENYEKEVU WA MUNGU.KWA KUWA WAMEUKANA UNYENYEKEVU WA MUNGU BASI INA MAANA
  WAMEYAKATAA MAARIFA YANGU.KWAHIYO KUANGAMIZWA KWAO
  SI JAMBO LA KUSHANGAZA.MTEULE YEYOTE ASIYE NA MAARIFA
  YANGU, KUANGAMIZWA NA MANABII WA UONGO NI LAZIMA”

  “Waliokataa maarifa yangu WATAKULA MATUNDA YA NJIA ZAO
  NA WATASHIBA MASHAURI YAO WENYEWE.MAANA KURUDI NYUMA
  KWAO WAJINGA KUTAWAUA.NA KUFANIKIWA KWAO WAPUMBAVU
  KUTAWAANGAMIZA. BALI KILA MTEULE ATAKAYEKUBALI KUISHI
  NDANI YA UNYENYEKEVU WANGU ATAKAA SALAMA NA ATAYAJUA
  MABAYA YOTE YA MANABII WA UONGO NA KUYAEPUKA”

  MAOMBI YANGU KWA YESU.

  Bwana na Mungu wangu Yesu,ninaomba uturehemu sisi wanao
  tunaojihesabia haki na kuasi maagizo yako kwa kutokutii.Ninajua
  kwamba pasipo wewe hatuwezi jambo lolote.Tunaomba uturehemu
  ili hasira na ghadhabu yako isiendelee kuwaka na kutuangukia.Ninaomba ututie nguvu ya kukubali kunyenyekea chini
  ya mkono wako ulio hodari ili tupate maarifa yalio hai ili tusiendelee
  kuangamizwa mbele ya macho yako.Baba wa milele na mshauri wa
  ajabu ninaomba utukumbuke kwa ajili ya jina lako na kazi ambayo
  uliianzisha hapa duniani.

 35. SOMA EZEKIELI 18:20-31 Ndipo mtakapo oona huu sio wakati wake kabisa na kumpa ibilisi nafasi kwenye mioyo yetu.

 36. Ninachosema mimi ni kuwa kwanini hamkumuonya mapema angali hai ili tuone kama atatii au ataendelea kuwa na roho ya ugaidi kwa sasa mmechelewa kwa hakuna ajuae pumzi yake ya mwisho ilitokaje uko uwezekano pumzi ya mwisho ikawa imetoka wakati amejutia na kutubu.Haipaswi kumpinga mtu aliyemaliza kazi yake na anangojea kuvuna alichopanda.

 37. @ Kilimba,
  Duh! Huyo Bishop atakuwa haelewi maana ya HUKUMU, hukumu zote zimo ndani ya Neno, sisi tunazirejea tu hizo kutoka humo, yaani Injili licha ya kuwa ni Habari kwa wanaoipokea, ni Hukumu kwa wasio ipokea au wanaoibishia au wanaoipoza kwa kuwashutumu wanaoihubiri, wakiwaita ni wenye kuhukumu!

  @ Siyi,

  Nakuona ulivyopandisha “mzuka” wa kisabato!

  Aliyekudanganya kwamba kila anayekufa anakwenda mbinguni ni nani huyo?

  Kwa UHAKIKA, kila aliye ONGEZA au KUPUNGUZA ktk Neno la Mungu, haijalishi mnampamba vipi, huyo hatasimama ahukumiwe maana hana hata kitabu cha matendo baada ya kuwa AMEFUTWA jina lake ktk Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, maana siku alipofutwa, ndipo alipokelewa Kuzimu; kwahiyo hata kama unamuona akitembea hapa duniani, labda ni nabii mwenye maono au huduma iliyotukuka, huyo ni sehemu ya jeshi la Kuzimu linalofanya kazi ya kuwakufurisha wote walio na masikio ya utafiti!

  Ndio maana tunajaribu kuwaonya kuhusu mambo hayo, sio mnashangilia tu bila ufahamu; mtu anajiita Adamu wa Pili, hata hamsimami kidogo kujiuliza, au mtu anazihamisha koma kwenye Maandiko mnachekelea tu, kumbukeni kuna “kulia na kusaga meno” huko mbele, hata ukiwa kibogoyo, unapewa meno yote 32 ili Neno likutimilie!!!

 38. Bishop, naomba kupingana nawewe, la sivyo tutakuwa tumekuwa wanasiasa, umewahi msikia nabii wa pombe unamsemaje huyu. Neno limetuonya kwa habari za manabii wa uongo, na vielelezo vyote vinaonyesha mtu anafika mahali pa kujiita mungu wa majeshi, na alikuja kutawala na kanisa miaka 1,000, leo amekufa washirika wanbadili kauli alijiita kwa ubini wa Mungu wa majeshi. Askofu nikishindwa kumwambia mtu huyu, sina ujasiri wa kusema a changudoa au kibaka au polisi anayetaka rushwa barabarani.

 39. Iwapo viongozi wengine walibaini chembechembe za upotoshaji wa mafundisho haya kwa nini hawakuchukua hatua hata ya kutoa tamko la pamoja. Haya ni matokeo ya kupuuza mambo madogo. Leo hii ninasoma kwenye magazeti kwamba CNN yatumika kuthibitisha kuhusu suala la miale ya jua kama alivyotabiri nabii huyo, mara mamlaka ya hali ya hewa imesema vile. Ipo haja ya kuwa na chombo kinachosimamia maudhui yatolewayo kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia bila kujali ni dhehebu gani. Nina amini katika jina la Yesu Kristo aliye hai.

 40. @ Faith,

  Ha ha ha ha ha ha ha kumbeee, kumbe kitu Nail ndio ilifanya kazi siyo? yaaani nacheka mpaka basi. Hata nimesikia kua alikataa kwenda Hospitali kuwahi iyo effects maana hawaendagi wala kuamini Madaktari au kutibiwa kibinadamu.

  Angela,

  Yaani Umevaa Sketi na unajua kabisaa umevaa sketi kisha Mtu anakuuliza, ”’eti Dada umevaa sketi au la? unaweza mjibu kua ngoja ukaaombe kuuliza mbingu au Roho Mt kujua kwa hakika kua umevaa sketiiii au kaputuura? Aisee iyo mbingu ni ya Kimanzichana na huyo atakua ”roho” si ”Roho” wakumsumbua-sumbua ivyo na mambo so peanut and mere humanistic foolishness.

  Press on,

  Edwin

 41. Wajoli,
  Nashangaa tulio wengi, tunaamini kuwa, mtu akifa anaenda mbinguni. Anakuwa ameitwa na Mungu!!! Sijui wamelipata wapi fundisho hili kwenye Biblia. Mbaya zaidi, juzijuzi, Masanja Mkandamizaji kwenye Whatsap, alirusha kichekesho kimoja kuwa yeye hataki kwenda mbinguni kwa sababu, kwenda huko, ni sharti ufe. Likuwa nawatolea mfano kwaya ya ambassadors of Christ-Rwanda. Na watu wazima,wenye akili zao, fedha zao, na wengine ni waheshimiwa fulani kwenye nyadhifa fulani serikalini/makampuni binafsi, walishangilia ufedhuli huo!!
  Hata hapa, kifo cha nabii, Eliya, wengine wameamini kuwa ameenda mbinguni. Hata watumishi wengine waliokufa kama Musa Kulola nk, ambaye hakuwa na kashfa kama hii ya nabii Eliya, watu waliamini kuwa kaenda mbinguni. Huu ni ufedhuli na watu wanapaswa kuufahamu kuwa ni efedhuli uliovuka mipaka!!
  Biblia haifundishi kuwa mtu akifa anaenda mbinguni!! Hakuna aya ya namna hiyo!! Mtu anapokufa, anakuwa amepumzika kaburini na siku ya mwisho, Bwana atamfufua ktk wafu ili alipwe sawasawa na kile alichokitenda wakati wa uhai wake. Sasa kama mtu akifa anaenda mbinguni, wale walioenda huko sasa, siku Yesu akirudi, atawatoa huko mbinguni tena ili awapatie uzima wa milele/maangamizi ya milele? Tafakari sana!! Huo ni uefdhuli na unapaswa kuachana nao maramoja.
  Nabii Eliya ni nabii wa uongo. Yote aliyoyafanya, yanatosha kumdhihirisha kuwa yeye alikuwa ni nabii wa uongo. Na thawabu yake (mauti ya milele), inamgonja kama hakutubu wakati amekaribia kufa, maana alifahamu tarehe hizo.
  Changamkeni wapendwa. Mtaishia pabaya na falsafa za kuzimu, na hatimaye mpotee milele. Hasara iliyoje!!
  Siyi

 42. Huyu hakuwa mtumishi wa Mungu. Alikuwa mjumbe wa shetani kabisa.. Ni nani anaweza kuedit kazi ya Yesu duniani.. Akakafie mbali huko, coz angeliharibu na kupotosha kanisa zaidi

 43. Angela
  Ndugu ninanena nawe kama mtu wa mwilini/mtoto mchanga

  2Cor11.4 Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!

  Mungu anesema nasi kupitia neno lake,hakuna habari ya kusikia kimesemwa hiki,nimesikia hiki hapa,

  kuna kazi nyingi tu za kumpigia goti Bwana wa mavuno na kuomba kupeleka watenda kazi ktk mavuno yake lakini si hii ya ndugu wa uongo. wa siloam.

  iHakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine badala ya ule uliokwisha wekwa, yaani Yesu Kristo.

  Mtu anakuja na ku hubiri injili tusiyoikubari kwamba yeye ni Adamu wa pili,Amekuja kuweka msingi

  Halafu unataka tupige goti la nini kutafuta kujua habari hipi!!,vinginevyo tuliamini bure na wala hatuja hekimishwa na hatuna ujuzi wowote wa maandiko wa kuzipima roho. na kuzipambanua.

  Yesu hakurithi hali ya dhambi kutoka kwa Adamu. Kwa hivyo, anaitwa Adamu wa pili Marehemu munuo alirithi dhambi toka kwa Adamu anaye baba wa kimwili,au unataka na sisi tuamini kama siloam wanavyoaminishwa kuwa marehemu munuo alitoka mbingu ya saba.

  Teka nyara kila fikra zimtii Yesu Kristo na kila ngome/mawazo/kitu kilichoinuka/ kinachojiinua kinyume na elimu ya Mungu kiangushe chini kwani silaha zetu zina nguvu ktk Mungu.tuache kupofushwa fikra.

  Hatuwezi kuwaonea wao shauku hata kidogo,tunamwonea shauku na kiu Kristo Yesu peke yake.

  Mjoli Haule

 44. Mrs CHRISTINA K kwa maoni yangu umeongea ukweli unaothibitishwa na neno la mungu. Kristo hapendi wala ktk mafundisho yake hakuwa anafurahia watu wanaokimbilia miujiza. ingawa alifanya miujiza mingi tu. alifahamu shetani atatumia udhaifu wetu wa kupenda miujiza ili atuangamize

 45. Kwa kweli hakuna maneno mengi sana kujua hili kwa sababu maneno ya Mungu wetu yapo hai na wazi kwa eneo la unabii, nabii yeyote atakaye tabiri na unabii usitimie ,basi ni yeye na sio Mungu wetu, Pia hakuna neno la ushahidi linalothibitisha kwa habari ya kuchukuliwa yeye kwa gari moto.Watumishi wa Mungu NENO LA MUNGU ni kioo chetu na biblia ndicho kisoma ramani chetu waenda mbinguni, kila mmoja anajua anayemtumikia na ndiye atakayemlipa mshahara wa hapa dunia na hata wa mbinguni. Zaidi ya yote mwachieni Mungu aweze kuhukumu kwqa haki na kweli.
  Toka Bishop,Burton Saulo Yuda

 46. Shalomu,

  Kama alivyosema Mjema hapo juu, uongo wa mtu huyu uko dhahili kabisa. Mtu akijifananisha na Mungu, huyo ni mwongo. Anaposema kuwa yeye ni Adamu wa Pili wakati neno la Mungu limeshatamka kuwa Yesu ndiye adamu wa pili maana yake nini? si muongo huyo? Mtu akisema kuwa Yesu hakumaliza kazi, maana yake nini kama si mpinga mkristo? Mtu akisema kuwa watu wasiombe kwa Jina la Yesu bali kwa jina lake maana yake nini kama si nabii wa uongo na mpinga Kristo?

  Wapendwa, ukweli uko wazi, lakini tatizo kubwa linalowasumbua watu wengi hasa waliookoka ni kusikia kuwa kulikuwa na miujiza mingi pamoja na mafanikio ikiwemo wengine kupata ndoa, fedha n.k. Naomba tuangalie Mathayo 24:5 Yesu mwenyewe anasema wengi watakuja kwa jina langu, wakisema Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. Sasa huyu amesema ni zaidi ya Kristo, maana anasema Kristo hakumaliza wala Jina lake lisitumike kwa sala. Soma pia Mathayo 24:24 inasema watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule.

  Hivyo wapendwa, miujiza si tatizo wala kipimo cha kuwa mtu fulani ni mtumishi wa Mungu, biblia inasema mtawatambua kwa matunda/matendo yao. 1Yohana 4: 1-3 inasema wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.

  Dada Angela ametoa ushauri mzuri kuwa watu wamuombe Mungu, ni sawa na muhimu sana katika siku za leo kumuomba Mungu. Hata hivyo, Biblia imetupa wajibu wa kuzipima roho ili tujue kama zinatoka wapi. Tutazipima roho kwa kuliangalia neno la Mungu kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, huku tukimwomba Mungu atusaidie, lakini pia si vibaya kujadiliana kuhusu jambo linaloonekana kuwa na utata, maana hata kwa njia ya majadiliano Mungu husema na watoto wake. Ukisoma katika Matendo 15, utaona kuwa Mitume waliamua kufanya Baraza/kikao kujadili jambo lililokuwa likiwatatiza, na kupitia kikao hicho, Roho Mtakatifu aliwapa majibu na mwongozo.

  Mungu awabariki

  Maran Atha

 47. Ni bahati mbaya kwamba mimi nilikuwa sijawahi kusikia habari zake. Lakini kama ulichoandika ni sahihi basi twafwa. Ni lazima nikiri ya kwamba nguvu za giza zipo tena hasa makanisani mwetu. Na wako viongozi wa madhehebu ya kikristo/ makanisa makubwa makubwa sana wako huko unakodai. Lakini mimi nikwambie kitu kimoja unachotakiwa kufanya wewe mwenyewe binafsi mwamini Mungu wako na ni yeye pekee atakayekuokoa. Kwani kwenda mbinguni unakwenda kwa ticketi ya nabii au mtume au mchungaji? Hapana. ni imani yako wewe mwenyewe. waache wafanye wayafanyayo. sana sana tuwaombee tu kwa Mungu wapate rehema ya Bwana ya kuujua ukweli ili wakatubu na kumrudia Mungu wao wa kweli

 48. Watu Wangu Wanaangamia kwa kukosa Maarifa, Kuna Mambo hata hayaitaji PHD kuyadadavua ni akili ndogo tuuu lakini nashangaa watu wasivyoweza kufikiri kabisa sijui tumefungwa na nini jamani, Mungu Atusaidie..

 49. WAPENDWA MUNUO ALIKUWA NABII WA UONGO NA TAPELI HILI HALINA MAJADALA MTOA MADA UMENUKUU KUWA ALISEMA HAKUNA SABABU YA KUTUMIA JINA LA YESU KWA KUWA HAKUFANYA VYEMA, SASA KAMA YESU HAKUKAMILISHA KAZI UKRISTO UKO WAPI.

  NILIWAHI SIKIA PIA AKIIWAPONDA MITUME ETI WALIUAWA KWA KUWA WALIRUDI NYUMA. HUYU ALIKUWA NI KITI CHA SHETANI MWENYEWE.

  MIMI SIELEWI KWA NINI WAKRISTO WA LEO HATUNA UJASIRI WA KUWAAMBIA MATAPELI WANAOKUJA KWA NJIA YA KANISA LA YESU UKWELI. CHA AJABU TUNAUJASIRI WA KUWAAMBIA MAKAHABA, WAVUTA BANGI NA VIBAKA UKWELI, UJASIRI HUU TUNAUPATA WAPI.

  AMEWAJAZA MAPEPO WAUMINI WAKE NA NDIYO YALIYOTENGUA UFAHAMU WAO NA KUWAFANYA NIWABISHI TU. HATA SIMPLE LOGIC HAWANA, THEY ARE DEMON POSSESSED.

  MAPEPO YA UTAMBUZI YALIMWEZESHA KUTABIRI MAMBO YA MAISHA YA WATU TU KWA AJILI YA PSYCHOLOGICAL MANIPULATION.

  HAKUJUA MAPEMA KUHUSU KIFO CHAKE, ANGEKUWA AMETOA KWENYE NEEMA KUBWA, HILI ALISHTUKIZWA. SASA NIMEANZA KUHISI WALE WATU WA BUKOBA ILIKUWA NI KAFARA, NA YAWEZEKANA SIO MASHARTI ALIYOKUWA AMEPEWA.

 50. UJUMBE KWA MANABII WA UONGO WANAOJIHUSISHA NA UTAFITI
  KUHUSU UELEWA WA WATU JUU YA SIRI ZAO!!!

  Naona wateule walio kufa wanafufuka!
  Yesu ameikamata Tanzania kwa mikono yote miwili!!
  Wajumbe wa shetani wamechanganyikiwa.Kazi zao zimekuwa majivu.
  Hii ni MIALE YA MOTO ULAO kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu aliye hai(UFUNUO 5:6,ISAYA 11:2).
  Mungu ndiye muamuzi wa mwisho wa kila jambo linalotokea au ambalo
  halitokei katika mfumo mzima wa dunia ambao siri zake zote zinapatikana
  katika ULIMWENGU WA ROHO.Watu wasioona au kuelewa yale wanayoyaona na kuyasikia katika ulimwengu wa roho wako katika mateso makali(ISAYA 42:18-22).
  Ndiyo maana Mtume,mwalimu na nabii Paulo aliwaombea Waefeso ili
  waone katika ulimwengu wa roho na wapewe roho ya hekima na mafunuo
  kutoka kwa Mungu(WAEFESO 1:17-18).Hii ndiyo changamoto ya wateule
  wengi ambayo TAYARI imeshapatiwa ufumbuzi kupitia Maarifa ya Yesu
  ndani ya mashujaa wake akiwemo Nabii na Mwalimu Mwakasege.TUNATAKIWA TULIFAKARI NENO LA MUNGU MCHANA NA USIKU KWA MUONGOZO WA ROHO WA KRISTO.Neno la Mungu limewavua
  nguo manabii wa uongo na kuwaacha UCHI KABISA,limetuonyesha undani
  wa roho,nafsi na miili yao(WAEBRANIA 4:12-13).

  Manabii wa uongo ni wachawi na waganga.Mganga kazi yake ni kuwashirikisha watu wafanye uchawi bila ya kujua.Na mchawi kazi yake ni
  kushirikiana na mganga kuua watu au kuharibu maisha yao.Sasa manabii wa
  uongo ni wachawi na waganga ambao wamejificha nyuma ya pazia la NENO
  LA MUNGU ili wasijulikane!!Lakini sasa uchawi na uganga wao uko wazi sana
  kuliko vazi la kahaba mzoefu na fedhea kubwa imewakumba.Tutaendelea
  kushuhudia jinsi wananyongwa na shetani ambaye hana urafiki na mtu japo
  wao wanadhani anawapenda!!(EZEKIELI 13:7-23,ISAYA 47:1-15).Hakikisha
  unasoma kwa makini kila maandiko UTAUONA UTUPU wa manabii wa uongo
  ambao kimsingi wanatoka ndani ya CHUO KIKUU CHA SHETANI kinachoitwa FREEMANSONS UNIVERSITY!Matawi ya hiki chuo yamesambaa ulimwenguni kote.

  UKWELI WA KUTISHA KUHUSU YALE WANAYOTABIRI!
  Manabii wa uongo huwa wanatoa unabii wa yale ambayo wameshayanga na kukubaliana katika VIKAO VYAO VYA KICHAWI!
  Wanatoa unabii wa mambo ambayo huratibiwa na majeshi ya pepo
  wabaya katika ulimwengu wa roho.
  Kwa mfano wanapomuandaa mtu wao awe RAIS WA NCHI fulani,wanampa kibali nabii fulani wa uongo ya kutoa unabii kuhusu huyo
  mtu kushinda nafasi ya URAIS!!Mungu anapoamua kuuacha mpango huo
  utimie kwa malengo yake maalum,ndipo watu wa kawaida wanaposhangalia na kusema unabii umetimia na nabii huyo kuonekana
  kwamba ni wa kweli!!Wakati mwingine shetani huwapa manabii hawa
  uhakika ambao anajua hautatimia ili kuwaaibisha.Ndiyo maana unaweza kukuta mtumishi anatoa unabii kwa ujasiri wote ya kwamba fulani ni chaguo la Mungu na ndiye atakaye kuwa Rais wa nchi alafu mwisho wa
  siku unabii hautimii na mbaya zaidi wafuasi wa huyo mtumishi bado
  wanaendelea kuwa vipofu na kumwamini zaidi!!!Maandiko yako wazi kwamba manabii wa jinsi hii ni manabii wa uongo na HATUTAKIWI KUWAOGOPA kwa jinsi ya rohoni !(KUMB 18:22).

  Kuna wanabii wa uongo ambao wameingia mkataba maaluma na shetani
  wa kutabiri makafara yanayofanyika katika vikao vya siri.Kwa mfano wanaweza kuandaa kafara ya ajali ya ndege alafu wakishahakikishiwa kuwa hiyo kafara itafanikiwa,ananyanyuka nabii fulani anatibiri kuhusu
  kutokea kwa hiyo ajali na kuwataka watu ‘waombe ili isitokee’ wakati katika vikao vyao vya kichawi walishakamilisha kila kitu.MARA NYINGI
  WANAOTOLEWA KAFARA KATIKA MATUKIO YA NAMNA HII NI WATU AMBAO WAMEINGIA MAAGANO NA SHETANI KWA KUJUA AU KUTOKUJUA!!Kila siku watu wanatolewa kafara kwa staili hii.HATA HIVYO UNABII UTOLEWA KWA MATUKIO AMBAYO NI MAARUFU au kwa watu maarufu ambao kiukweli wengi wao wameingia maagano
  na shetani.Hawa ni watu ambao huwa WAMEINGIA KATIKA MAAGANO
  YA UTAJIRI NA KUPEWA MUDA MAALUM WA KUISHI HAPA DUNIANI.
  KWA HIYO MUDA WAO UNAPOISHA SHETANI ANAWACHUKUA.Ni mara chache sana mtu anaweza kukubaliwa kuongeza mkataba tena kwasababu maalum kwa ajili ya makusudi ya shetani.

  MAKUBALIANO KATI YA MUNGU NA SHETANI NI FUMBO ZITO
  KWA WATEULE WENGI!!!
  Moja kati ya makubaliano kati ya shetani na Mungu ni kwamba
  MANABII WA UONGO watamtangulia shetani katika lile ZIWA LA MOTO!
  Manabii wa uongo watatupwa kwanza alafu shetani atafuata baadae!(UFUNUO 19:20, UFUNUO 20:7-10).

  Pia makubaliano mengine ni kwamba shetani anatakiwa kumpelekea
  Mungu mashitaka kuhusu dhambi tunazofanya mchana na usiku.Lakini
  pia shetana hana mamlaka ya kuua au kugusa roho zetu,yeye shetani
  chakula chake ni miili (udongo/mavumbi) ya watu wanaomuasi Mungu
  na kazi yake kubwa ni KUUDANGANYA ULIMWENGU WOTE NA KUHAKIKISHA SIRI ZA WAFUASI WAKE ZINAFICHUKA NA KUWA WAZI MBELE ZA WATEULE WA MUNGU(UFUNUO 12:7-10,MATHAYO 10:26-28).

  Makubalino yako mengi sana ambayo kimsingi yanalenga kuwafanya
  wateule washinde na zaidi ya kushinda wakati wajumbe wa shetani
  na shetani mwenyewe wakishindwa na zaidi ya kushidwa!!!MAKUBALIANO KATI YA MUNGU NA SHETANI AMBAYO YALIFANYIKA
  BAADA YA UASI ULIOTOKEA MBINGUNI NI KWA FAIDA YA MUNGU NA
  WATU WAKE.

  ……………ZIMEBAKI SEKUNDE CHACHE…………………………..

 51. ukiangalia kwa makini picha za huyu jamaa (nabii eliya)huwa anapendelea kunyoosha mikono yake miwili juu alama ambayo ni ishara ya pembe za kucifa yan frmaso ambaya ni sawa 2 na ile alama vidole wiwili!amekufa mwez wa 11 na huduma yake ilianza mwaka 2003 mpaka 2014.ukichukua mwaka 2014 ukitoa 2003 unapata exactly 11.hzi ni namba ambzo masoniki wanazitumia angli tukio la septmber 11.huo ndo mda aliopewa na lucif kuish duniani

 52. Yaani jamani kwa nini watu wanajadili kwa kusikia kimesemwa hiki,nimesikia hiki,kama yuko Mungu na roho wa kweli ndani yako,jambo rahisi piga magoti muulize Mungu utapata majibu bila kuuita baraza la kujadili mtu.Mungu atusaidie ufahamu maana wengi wetu tunaingi dhambi ya kujadili watumishi wa Mungu badala ya kupiga magoti nakuomba Mungu akufunulie lililo la kweli.

 53. Mch. Dani,

  Mbonas huyu Jamaa uongo upo wazi kabisa tu. Kwa kusema kuwa Yeye ni Adamu wa Pili eti kwa kuwa Yesu kila Jambo hakukamilisha ni Uongo mtupu. Yesu alikamilisha kazi yake kabisa na ndio maana kwa jina lake tunawekwa huru.

  Yeye kafa kifo cha kishenzi kweli. Yesu alikufa na kufufuka na leo yupo mbinguni anatuombea, na alimwombea hata yeye mwenyewe.
  Wala sioni haja ya Kuumiza kichwa hapa. Yesu alisha maliza kazi kwani yeye ni Alfa na Omega. Amen.

 54. Bwana Yesu asifiwe,
  Hii mada mwenyewe inanikanganya sana,na ninaogopa kua mwepesi kwenye kuongea. Nataman kusikia maoni ya wengine.
  Pamoja na yote haya,siku zote mwongozo wetu ni bibilia Roho mtakatifu akiwa mwalimu wetu. Naamini hakuna ambacho hakija hakijasema kwenye bibilia.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s