Je, Mungu Ana Upendeleo?

OLYMPUS DIGITAL CAMERA


Je, Mungu ana Upendeleo?

 • Kwa nini watu wengine Mungu hukutana nao katika Ndoto na kusababisha WAOKOKE wakati wengine wakiendelea katika maisha ya dhambi pasipo udhihirisho wowote wa ki-Mungu katika maisha  yao?
 • Kwa nini maeneo Mengine Wainjilisti hupokezana VIWANJA VYA MIKUTANO, akitoka mmoja anaingia mwingine wakati sehemu zingine inaweza kupita miezi kadhaa bila kuona Mkutano hata mmoja wa Injili?
 • Je, ni kwamba Mungu anapendelea baadhi ya watu ili wamjue yeye huku wengine anawaacha tu waangamie?

Kwa kuwa kuna watu ambao wakiwa wangali dhambini Mungu huwatokea katika ndoto/maono na kuanzia hapo maisha yao yanabadilika, Kwa nini basi asiwatokee watu wengi tuu katika ndoto/maono ili hatimaye wamgeukie yeye? Nini maana yake mambo haya?

Advertisements

39 thoughts on “Je, Mungu Ana Upendeleo?

 1. Ahsante Ndugu Milinga,

  Umetuanzisha mwaka mupya na fundisho zuri.

  Ubarikiwe.

 2. WOTE, HERI YA MWAKA MPYA 2015?

  UPENDO, UPENDELEO, MAPENZI, MAPENDELEO, KUCHAGULIWA, NI KWA NEEMA TU, KWA BAHATI NZURI, WENYE MAPENZI MEMA, nk…….Hayo ni maneno yanayowachanganya wapendwa Wengi Kila kona kama siyo Tanzania na dunia yote.

  Je, Mungu ana UPENDELEO? Ndiyo Mungu ana UPENDELEO!!!!!!

  Tatizo la wapendwa wengi wanachanganya UPENDELEO wa Mungu na UPENDELEO wa mwanadamu. Au NEEMA ya Mungu na UPENDO wa Mungu.

  UPENDELEO wa Mungu kusema ukweli huchanganywa na NEEMA YA MUNGU.

  Yaani mtu akipendelewa na MUNGU anasema ni NEEMA TU
  Mwingine alifikia kutunga wimbo usemao ……Siyo kwa ujanja wangu ni Kwa neema ya Mungu. Kubarikiwa kwangu siyo kwa sababu mimi ni mwombaji sana, siyo kwa sababu mimi natoa sadaka sana, Utasikia wakisema nimepata wokovu siyo kwa sababu mimi ni mzuri sana bali ni kwa Neema ya Mungu, nk…..nk

  Mfano, Binti Bikra Mariam alipopata mimba ya Yesu, tunasoma kwamba alipewa neema, mwingine aweza kusema alipendelewa na MUNGU miongoni mwa mabinti mabikra maelfu waliokuwepo duniani wakati ule..

  Mfano huo siyo UPENDELEO WA KIBINADAMU ni UPENDELEO WA KIMUNGU kwa ajili ya kutimiza kusudi lake kwa watu wake. Ilikuwa lazima Yesu aje na avae mwili wa mwanadamu kwa kupitia tumboni mwa mwanamke.

  Mfano mwingine, mpendwa akiokoka kwenye ajali mbaya ya barabarani au akapona yeye tu kwenye ajali mbaya iliyoteketeza mamia ya watu, utasikia watu wakisema, Ni Mungu tu, Ni Mungu tu , au ni kwa neema tu ya Mungu,

  Swali la kujiuliza ni je, Mungu alimpendelea au alikuwa ana makusudi gani kumwacha?

  UPENDELEO wa Kimungu siyo ule wa kibinadamu ambao unafanya kwa NIA MBAYA jambo lolote. UPENDELEO wa KIMUNGU hutokea kwa ajili ya kutimiza kusudio fulani……ambalo ni jema kwa watu wake.

  Kwa mfano uliwahi kujiuliza kwa nini Mungu alichagua TAIFA la Israel kuleta mwokozi duniani na siyo taifa la TANZANIA? Hii ilikuwa lazima Mungu aokoe ulimwengu kupitia Taifa lolote. Kwa hiyo taifa lolote ambalo angepitisha mwokozi huyo, bado inaweza kutafsiriwa kuwa MUNGU ALILIPENDELEA TAIFA HILO kwa kusudi la kuokoa mataifa yote.

  Maswali haya ya mpendwa wetu yanaonesha kuwa watu wanashindwa kumwelewa Mungu na utendaji wake wa kazi. Hebu tafakari maswali yake tena,

  “1…………………….Kwa nini watu wengine Mungu hukutana nao katika Ndoto na kusababisha WAOKOKE wakati wengine wakiendelea katika maisha ya dhambi pasipo udhihirisho wowote wa ki-Mungu katika maisha yao?

  2…………………..Kwa nini maeneo Mengine Wainjilisti hupokezana VIWANJA VYA MIKUTANO, akitoka mmoja anaingia mwingine wakati sehemu zingine inaweza kupita miezi kadhaa bila kuona Mkutano hata mmoja wa Injili?

  3…………………. Je, ni kwamba Mungu anapendelea baadhi ya watu ili wamjue yeye huku wengine anawaacha tu waangamie?

  Wapendwa wenye maswali kama haya ni wengi. Lakini itoshe tu kusema kwamba Mungu hafanyi kazi kwa kutumia “FORMULA MOJA” Duniani kote. Ukiona Mungu ametenda jambo fulani Tanzania kuwafanya watanzania wamwamini USITARAJIE kwamba formula hiyo hiyo ndiyo itakayotumika KENYA, BURUNDI, UGANDA, nk. Soma maandiko vyema utaelewa Mungu anavyotenda kazi.

  Inawezekana kabisa mikutano mingi ikafanyika VIWANJANI na Wainjilisti wakawa wanapishana kila mara kuhubiri, lakini ikawa siyo kila mkutano wenye KIBALI CHA MUNGU.

  TAFAKARI SANA, CHUKUA IMANI

 3. Lwembe,

  Sasa umekwenda katika…”deep things of God…” Natafakari………hasa kusudi la Mungu la kuchagua…….!Ubarikiwe

 4. ……. inaendelea:

  Basi, Neno la “Haki ya mzaliwa wa kwanza” lilipomfikia Yakobo, yeye aliijua Siri iliyofichika ndani ya Neno hilo, lakini kaka yake hakuijua Siri hiyo, hakuona ni kwa jinsi gani mdogo anaweza kuichukua Haki hiyo ilhali yeye aliye mkubwa yupo, Haki ya Mungu hakuijua, yeye alidhania hilo ni jambo la mila na desturi, kama ambavyo wengi wetu tunavyoyachukulia mambo ya Mungu, tukijidhanisha kwamba Mungu anaheshimu mawazo yetu kuhusu Yeye!
  1 Cor. 2:7, “but we speak God’s wisdom in a mystery, the hidden wisdom, which God predestined before the ages to our glory.”
  Hili ladhihirisha jambo hilo, kwamba Mungu ali predestinate Neno lake, hiyo Hekima yake iliyofichwa ndani ya hilo Neno, ambayo hufunuliwa kwetu wenye kulipokea hilo Neno la wakati, lenye kuificha hiyo hekima!

  Basi hilo Neno lililokuwa predestined, unapolipokea kama lililvyokusudiwa, hilo hukufanya kuwa hilo Neno, ndipo kwa kigezo hicho wewe huonekana kama mtu aliyekuwa predestined ktk kuishi jinsi hiyo, ndipo kifungu kama hiki cha Rom 8:30, “and whom He predestined, …” kingekupeleka ktk wazo hilo.

  Tafsiri ya neno “predestinate” inachanganya kidogo hata kuzalisha wazo la kwamba Mungu HUIPANGA hatma yetu sisi kama watu. Lakini ukweli ni kwamba hatma yetu iko ktk jinsi tutakavyolipokea Neno lake. Nao upendeleo uko kwa wale aliowaona wakilipokea Neno lake, ndipo akawatayarishia Neno hilo lenye huo Upendeleo na kuliweka ktk vizazi vyao ili liwafanyie huo Upendeleo. Kule Misri walipelekewa neno la kuwatoa hicho kizazi kilichopaswa kutoka, ambalo kwa leo hii ni neno lililokwisha kutumika, hivyo sisi hulitumia tu kama rejea ktk kumjua Mungu.

  Lakini, ukiliangalia kwa kina ktk background ya Injili, ndipo tunaweza kufika ktk ufahamu kwamba Mungu aliliweka Neno lake ndani ya hao wote waliokuwa Wazo lake, maana Yeye ni Neno lake, nalo Neno twafahamu ndiyo Mbegu ya Asili, hivyo yapaswa iwemo ndani yetu, imelala kama mbegu zilalavyo ardhini zikiisubiri nguvu ya Jua ili zichipue; ndivyo ilivyo kwetu, ile mbegu aliyoipanda Mungu tangu kabla ya kuwekwa misingi ya dunia, ikiwamo ndani yetu imelala, basi nguvu ya Injili, ile Nuru halisi inapoifikia hiyo mbegu, huchipua haraka na kuipasua ardhi itoke juani ikue, ndio ile imani ambayo huja kwa kusikia ambako huja kwa Neno la Kristo!

  Ndipo Yeye Mungu, alituita kwa Injili, ile Mbegu iliyomo ndani yetu, akatuhesabia Haki na kututukuza kulingana na Nguvu na Utukufu wake, ambavyo amevihifadhi ktk hilo Neno tulilolipokea!!

  Mtazame yule mwanamke wa Kisamaria, alikuwa na Neno la Masihi ndani yake, ile Mbegu. Kristo akiwa ndilo hilo Jua, hivyo ilimpasa apite kisimani hapo ili akutane na yule mwanamke, yaani Kristo akiwa ndilo hilo Neno lililokuwa predestined kuihuisha hiyo Mbegu iliyomo ndani ya huyo mwanamke, ilimpasa AMTAFUTE huyo mwanamke; nayo Nuru ilipompiga, akainuka ktk Uzima! Mungu ndiye anayetutafuta, zile Mbegu zake, hakuna kati yetu anayeweza kumtafuta Mungu na akampata; “Mtu haji kwangu asipovutwa na Baba”, hii ndiyo Haki ya Mungu inayoambatana na Upendeleo wake!!!

  Mungu anasema, ktk Mt 22:14 “Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache”. Tunafahamu kwamba Mungu alimuita mpaka Kaini; hata Esau aliitwa pia na kupewa ile Haki ya mzaliwa wa kwanza, lakini hawakuweza kulijua Kusudi la Mungu, wakayaamini mawazo yao!!

  Kulijua Kusudi la Mungu ktk kuwapo kwako hapa duniani, ni kujua kuhusu jina lako kuwamo katika Kitabu cha Uzima. Upendeleo wa Mungu ni kwa ajili ya hao tu, hao ambao Mbegu ya Mungu imepandwa ndani yao, hawa ndivyo vyombo vya utukufu!

  Ngoja nikomee hapa kwa leo, maana kama ni “depth”, well mambo haya ndio hayo the Deep things of God, yale mafumbo ya Mungu; Mungu na atusaide kuyafumbua mambo hayo kwa ajili ya Utukufu wake!

  Gbu!!

 5. Ndg Orbi,

  Nimefurahi kukuona!

  Ninaamini kwa mchango huu uliouleta, umeupindisha mjadala kuelekea huko kwenye UHALISI wa jambo hili la Upendeleo, na iwapo tutaweka kando mambo yetu ya dini, basi kiwango chetu cha ufahamu kitapanda hata kufikia kujitambua sisi ni nani; yaani vile “vyombo”!

  Kwa kadiri nilivyojaribu kuyatafakari hayo uliyoyaleta, naweza kusema kwa uhakika kwamba Upendeleo wa Mungu umejikita katika hayo mambo mawili, “Election” yaani “Uteule”, na “Predestination”.

  Lakini pia twafahamu kwamba Mungu ni mwenye Haki, kwahiyo hatuwezi tukasema juu juu tu kwamba “Mungu Ana Upendeleo na Hana Upendeleo”, ilmradi jambo la Haki li mbele yetu, tutakuwa tunabahatisha. Haki ya Mungu ndio inayouleta Upendeleo, na ndiyo inayoamua “Uteule” na “Predestination” hata kuufanya Ukristo wetu kuwa Halisi kulingana na jambo hilo.

  Ili kulielewa vizuri jambo hili ni lazima turudi huko Mwanzo, huko ktk kitalu cha mbegu, huko yalikoanzia yote, ili yanapofunuliwa huku mbele ktk Agano Jipya, tuwe tayari tumejengeka ktk msingi imara. Mfano ulio bora ktk hili ni wa Esau na nduguye Yakobo:
  “Mwa 25:22-23 “… Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA. BWANA akamwambia, Mataifa mawili yako tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.”

  Jibu la Mungu kwa Rebeka kuhusu hao wanae humo tumboni, linatoa tamati ya watoto hao bila kutoa vigezo vinavyopelekea jambo hilo kuwa hivyo. Lakini mbele tunamuona Esau akiiuza Haki yake aliyopewa na Mungu. Hapa ndipo kuna jambo la kulitazama zaidi; kwanini Yakobo aliitaka Haki hiyo? Bila shaka aliijua Thamani yake kulingana na Neno la Mungu na hivyo shauku yake ya kulipata jambo hilo ikawaka moyoni mwake, na Esau aliiona ni kitu kidogo kisichoweza kumuondoka!

  Sasa ukija ktk kile kifungu ulichokinukuu, Rom. 8:29, “For whom He foreknew, He also predestined to become conformed to the image of His Son…”; Tunapolitazama hili neno ” For whom He FOREKNEW”, hili linatuambia kwamba Mungu alitujua kabla hata hatujazaliwa na mahali pengine anasema kabla ya misingi ya dunia kuwekwa. Basi ni dhahiri kutujua kwake huko ni hapo tulipokuwa Wazo lake kabla hatujadhihirika kwa Neno lake; kwani Neno ni wazo lililodhihirika, ndiko huko kuumbwa kwa Neno kukiwa ndiko kudhihirika kwa Wazo la Mungu!

  Huko ktk Mawazo yake ndiko alituona jinsi ya mwenendo wetu kuhusu Neno lake; nani atalipokea na kulithamini na nani atawatupia nguruwe! Wenye kulipokea, aliwaona katika ukamilifu, pamoja na mapungufu watakayoyapitia, kuanguka kwao nk, ndipo akali PREDESTINATE Neno la KUWAINUA, hilo litakalo wafanya WAMFANANIE Mwanae, huyo ambaye ni Neno; ndiko huko ” to become conformed to the image of His Son”, which is The Word allotted for every age; yaani Neno la Mungu ndilo linalotugeuza nia na si kwamba Mungu alitupangia tugeuke nia bali alituwekea hilo Neno ambalo tutakapokutana nalo basi tutalipokea na litatubadilisha nia zetu, maana kwa asili ni letu tangu hapo tulipokuwa Wazo lake!!! Nayo Nguvu ya kutubadilisha, Mungu ameihifadhi ktk Neno lake.

  Nitaendelea……..

 6. shalom labda mtoa mada angefafanua msingi wa swali lake, lakini kama msingi unaendana na majibu yanayotolewa na wachangiaji wengine nami nichangie kama ifuatavyo naamini namimi pia ninaye roho wa kristo kama paulo, hapa ndipo ninapojikuta kila wakati nampigia saluti muumba, Mungu anao upendeleo na wala hapaswi kuulizwa maswali kwanini kampenda Yakobo akamchukia Esau kabla hata hawajazaliwa warumi 9:11-33. kwanini Petro apate nafasi ya kutubu yuda asiipate na wote wamekosa, kwani kuna tofauti ya kusaliti na kukana kiutendaji? maana yake wote walimgeuka Yesu. kwanini Miriam aadhibiwe amrehemu hajiri. kwanini esta anatii vashti anakaidi. kwanini hakumuua shetani pale ameasi. kwanini achague Israel kuwa taifa takatifu kati ya mengi. kwanini utukufu wake hatompa mwingine. kwanini wenye haki kama ayubu nao huteswa na shetani. kwanini ampandishe huyu na kumshusha huyu. kwanini asiwaonye sodoma kwanza kabla hajawaadhibu kama alivyowaonya ninawi kupitia Yona. kwanini wengine wanaanza vizuri na wanamaliza vibaya kama sulemani na wengine wanaanza vibaya wanamaliza vizuri kama Paulo. tukitaka kufukunyua kila kitu basi tuwe na utayari wa kuyakubali majibu toka kwa muumba kama yalivyo maana yanaweza yakatuchanganya. yeye anatenda sawa na inavyompendeza yeye. vingine havichokonoleki jibu rahisi ni mapenzi yake na Mungu atabaki kuwa Mungu. lakini kama msingi wa swali la mtoa mada ni sawa na maneno ya Paulo au petro basi Mungu hana upendeleo kwa myunani wala kwa myahudi in generalization lakini katikati ya wayunani au katikati ya wayahudi hao hao wapo wenye haki anaowapendelea (kina yakobo) na wapo wapumbavu asiowapendelea (kina Esau) hapa anafanya specification sasa. warumi 11:33-36. tunapomwangalia Petro anaposema Mungu hana upendeleo ni lazima tuangalie msingi wa usemi wake ni nini; yaani kwanini Petro alifikia hatua ya kutamka maneno Yale na msingi huo tunauona katika matendo 10:1-43; hapo mwanzo petro alidhani wayahudi tundio wanaoweza kupatana naMungu Si wayunani wala wasamaria ni wao tu wayahudi kama vile walokole wengi tunavyodhani kwamba WARC au walutheri au waanglikana wanaosema wameokoka lakini bado wanaendelea kuabudu kulekule kwenye makanisa yao basi hawajaokoka vizuri hadi wamehamia pentekoste, na hawawezi kumsikia Mungu, ni sawa na wengine wanapoangalia wengine ambao bado hawajamjua kristo mienendo yao wanapigia mstari kwamba hata iweje hawawezi kuokoka kutokana na wanayoyafanya ndipo Mungu anapobadilisha mitazamo yetu tunastukia mlevi sugu kaokoka kaacha pombe, mchawi kiboko kasalimisha vitendea kazi vyake madhabahuni, petro alikuwa na fikra finyu na za kibaguzi ndipo Mungu akaamua kumbadilisha fikra zake hadi akafikia kutamka alitoyatamka, Si Petro pekee anayeyatamka maneno haya Bali Paulo pia anayarudia anapowaandikia warumi barua mlango wa 2:11 hapa Paulo alikua akimaanisha kwamba tofauti na mahakim wa dunia hii Mungu anapohukumu anatoa haki sawasawa na inavyomstahili mhukumiwa. kwanini hivyo? kwasababu kuna tofauti kati ya hukumu ya Mungu na ya mwanadamu. Mungu pamoja na kwamba anahukumu lakini yeye mwenyewe ni shahidi namba moja maana huona yote ayafanyayo mtuhumiwa tofauti na wanadamu ambao huwa hawapo kwenye tukio hivyo wanategemea ushahidi wa wengine ili kutoa hukumu, pia Mungu hapokei rushwa umeua kwake ni umeua no discussion, mwanadamu anaweza akapindisha hukumu lakini sio Mungu. hizi ndizo maana Paulo na petro walizimaanisha. baraka za kristo na ziwafate.

 7. Mjema,

  Mungu anaaminika lakini hashabikiwe.Unaposema Petro alitambua kama Mungu hana upendeleo usisahau kama Ayubu na wengine walisema anao. Ndo maana Mungu huwezi kumfahamu kama unavyoweza fahamu kitu. Mungu iko huru na hakuna anayeweza mhukumu. Akipendelea siyo kusema hahukumu kwa haki kwani haki ni yake. Ndio maana tumeambiwa tushukuru kwa kila jambo. Hii ina maana hata likiwa libaya huwezi kwa nguvu zako ligeuza kama jinsi huwezi hesabu njwele zako.
  Ukitaka mfahamu Mungu kwa vigezo vya binadamu utakwama. Kwake Mungu kuwa na upendeleo siyo dhambi kwani hatendi dhambi. Angalia tu jinsi aliteua Israeli ndipo utafakari kama taifa nyingine zimeachwa kwa nini. Hata Israeli ilipotengeneza ndama Mwenyezi Mungu hakuwaacha. Utakaposema Mungu akipendelea amefanya dhambi utakua umekufuru. Ni sawa kumhukumu kwani alitolewa damu au pombe au kutofautisha watu kwa rangi au kushusha na kuinua au kuua na kuponya, … Iko huru na hiyo yatosha kwetu. Ni Mtakatifu… full stop. Pia kwa mambo kama yale hakuna kujiuliza mengi. Utaumiza kichwa chako kwa bure. Wapi uliwai sikia chombo kikijifunza matendo ya mfinyanzi. Na kama mfinyanzi anapendelea au hapendelei chombo fulani where is the problem?

  Asante.

 8. wapendwa,

  Tunaposema Mungu anaupendeo ni sawa na kusema kuwa Hukumu yake sio ya haki.kwa kuwa wengne anawatokea ktk ndoto na wengne usikia injili kila siku wakati wengne hawana fursa hzo.

  Naomba tuzingatie yafuatayo,

  1.Wakati Mungu utoa fursa tofauti kati ya mtu vs mtu,au watu vs watu. Wote tuna nafasi sawa ya wokovu ila fursa tofauti. Tutawajibishwa tofauti kulingana na fursa Mungu anazotupa. Yaani, Yuda Iskariote atawajibika zaidi ya yule mwizi aliyemkataa Yesu pale msalabani kwa kuwa Yuda alikuwa na fursa Tele kwa miaka kadhaa tofauti na yule mwizi. -yaani uo tunaoutaja kuwa ni upendeleo waweza kuwa laana! Fursa zaidi,kuwajibika zaidi!

  2.Wakati sisi tunaangalia leo na kwa nje tu,Mungu yeye uona hadi mwisho uusoma moyo. Kwa iyo kwa mapana haya ya Mungu tujue Hukumu zake niza haki na hana upendeleo.

  Jamani hata mitume walifikiri kuwa Mungu ana upendeleo,lakini ilifika mahali Petro akasema, ” ….Hakika natambua ya kuwa Mungu HANA UPENDELEO, bali ktk kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.” Mdo10:34-35.

  Sijui tunataka ushahidi gani mwingne.

  **akawafungua akili zao wakaelewa na maandiko. Luka24:45**

 9. John Bethania,

  Napenda ufikiri tofauti.Hebu jiulize,

  Swali: Kati ya Miriam na Haruni, ni yupi Mungu alimpendelea?

  Zingatia: Mungu kuturudi ni kwa kuwa anatupenda. Ivyo ni sawa na kusema aliyependelewa ni Miriam kwa kurudiwa kwa kutiwa ukoma!

  Karibu.

  **akawafungua akili zao wapate kuelewa na maandiko. Luka 24:45**

 10. Nadhani Mungu ana upendeleo! mbona Miriam na haruni walimkosea Mungu lakini ukoma akapigwa Miriam peke yake? kama si upendeleo ni nini? Soma Hesabu 12:1-12

 11. For More reading…..

  What is predestination and election?
  by Matt Slick

  Predestination and election are both biblical teachings. The English “predestination” is translated from the Greek word proorizo which means 1) to predetermine, decide beforehand; 2) in the NT, of God decreeing from eternity; 3) to foreordain, appoint beforehand.1 Predestination, then, is the biblical teaching that God predestines certain events and people to accomplish what He so desires. The word proorizo occurs six times in the New Testament–each time demonstrating that God is the one who is foreordaining and bringing about certain events:

  Acts 4:28, “to do whatever Your hand and purpose predestined to occur.”

  Rom. 8:29, “For whom He foreknew, He also predestined to become conformed to the image of His Son, that He might be the first-born among many brethren;

  Rom. 8:30, “and whom He predestined, these He also called; and whom He called, these He also justified; and whom He justified, these He also glorified.”

  1 Cor. 2:7, “but we speak God’s wisdom in a mystery, the hidden wisdom, which God predestined before the ages to our glory.”

  Eph. 1:5, “He predestined us to adoption as sons through Jesus Christ to Himself, according to the kind intention of His will.”

  Eph. 1:11, “also we have obtained an inheritance, having been predestined according to His purpose who works all things after the counsel of His will.”

  You must also note that God predestines people as Rom. 8:30 and Eph. 1:5, 11 demonstrate. There is, however, controversy as to the nature of this predestination. In the Reformed (Calvinist) camp, predestination includes individuals. In other words, the Reformed doctrine of predestination is that God predestines whom He wants to be saved; and that without this predestination, none would be saved. The non-Reformed camp states that God predestines people to salvation but that these people freely choose to follow God on their own. In other words, in the non-Reformed perspective God is reacting to the will of individuals and predestining them only because they choose God where by contrast the Reformed position states that people choose God only because He has first predestined them.

  Election

  The word “election” or “elect” comes from the Greek word, eklectos, and occurs about 25 times in the New Testament. It signifies “to pick out, choose, to pick or choose out for one’s self, a choosing one out of many.”1 The one who does the choosing–the electing–is God.

  John 13:18, “I do not speak of all of you. I know the ones I have chosen; but it is that the Scripture may be fulfilled, ˜He who eats My bread has lifted up his heel against Me.”

  Eph. 1:4,”He chose us in Him before the foundation of the world, that we should be holy and blameless before Him.”

  1 Tim. 5:21, “I solemnly charge you in the presence of God and of Christ Jesus and of His chosen angels, to maintain these principles without bias, doing nothing in a spirit of partiality.”

  Again, there is debate within Christianity as to the means and purpose of God’s election. Some say that God elects individuals, and others say He only elects nations and/or groups of people. If God elects individuals, this means that God is predestining them and electing them into salvation; and He is not electing others. This does not sit well with many Christians. On the other hand, some Christians state that God elects based upon a foreknowledge of what an individual will do.

  Whichever side you believe, remember that predestination and election are biblical concepts. You must also remember that how you believe or not in predestination and/or election does not affect your salvation. Therefore, you should be gracious to other Christians who differ with you on this subject.

 12. Wapendwa,

  Wakati mwingine lazima tukubali kuna mengi kuhusu Mungu tusiyoyafahamu…! Na vile vile naona wengi tunajaribu kumweleza Mungu kwa vigezo vyetu vya ufahamu wa kibinadamu….! What is is fair kwa vigezo vyetu vya kibinadamu inawezekana kabisa ni tofauti kwa upande wa Mungu…..”Oh, the depth of the riches and wisdom and knowledge of God! How unsearchable are his judgments and how inscrutable his ways!”R0m 11:33) Aliyeyazungumza haya ni Paulo….! Na ni Kweli Njia zake hazichunguzi……..Sina muda wa kulifikisha somo hili mbali, lakini ukisoma Biblia utaona kuna vyombo( watu) kuanzia awali Mungu aliviumba kuwa vyombo vya uharibifu……”vessels prepared for destruction” Pharao (Exodus 4:21)….Mungu alisema ataufanya moyo wa Pharao kuwa mgumu…..na kweli aliufanya ili kutimiza kusudi lake…….! Na kuna vyombo ambavyo toka awali Mungu alivichagua toka awali kwa ajili ya Utukufu wake…..! Fanyeni homework na Maandiko mtaona hivyo….! Na kwa vile mimi na wewe hatujui i ni vipi vyombo vya uharibifu na vipi ni vyombo vya utukufu…….anayejua ni Muumba (Mfinyanzi) (Potter) ambaye anajua chombo hiki au kile kiko kwa makusudi yapi…….mimi na wewe tuna kazi moja tu….kwanza kutetemeka kwa nini amenichagua au ametuchagua kuwa Chombo cha Neema……! Na vile kulipeka Neno lake kwa wale wengine ambao amewachagua……ambao mimi siwafahamu…..! Yeye anawafahamu…….

  Kama nilivyosema awali unavyozidi kumfahamu Mungu na njia zake, ndio ambavyo unatambua kwamba Humfahamu kabisa…..! Hasa anavyotenda Kazi……Kwa mtazamo wangu……kwa akili za kibinadamu…..na ufahamu wangu wa Maandiko, naona vyote viwili….Mungu Hana Upendeleo….Na Vile Mungu anaupendeleo……Lakini mimi naangalia kwa wigo wa Macho ya Mwili na nyama tu….Mungu anaangalia….jana, juzi, milele….miaka elfu kutoka sasa…..na anajua anachokifanya………kwa mimi nayeangalia leo….Naweza Kusema Mungu ana Upendeleo……au Hana Upendeleo…..!

  Nikipata muda tutaendelea na mjadala

 13. sungura,

  Una maana gani kwa sentensi hii, “God is not Fair, but He is Just!”???

  Kwangu mimi najua God is Fair and Just. Na ndio maana atamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.! Na pia B inasema atahukumu ulimwengu kwa haki.

 14. Lwembe, Mjema,

  Kinachoongelewa ni maandiko, Biblia ikiwa na lugha yake, inaposema Mungu hana upendeleo ina maana hana. Na inaposema ana upendeleo ina maana anao. Hivi yote iko ndani ya Biblia ina maana kinachotakiwa kufahamu ni mantiki ya lile neno” upendeleo” kuliko kujifanya bingwa kuliko Biblia.

  Mjema, usimshangae Christina kwani alichotambulisha ni hiyo mantiki wala hakuenda mbali. Si unafahamu kama “Yesu ilifika kwa ajili ya waliyo wake…”? Pia si unàfahamu jinsi ule mwanamke muyunani alipata muujiza wa kuponyeshwa mwanae kama mbwa?
  Huo ulimwengu unaousema nao una mantiki yake.

  Lwembe, uko sahihi kabisa. Kinachobaki ni kufahamu kwa nini wengine hawakuandikwa na gharama ipi inahitajika kwao kwa kuokolewa kwani wao imewapasa kwanza kujiandikisha baadaye kulinda huo wakovu.

  Mungu awabariki.

 15. Dah,
  Naona tunachanganya sana kati ya Neema (Grace) na Upendeleo ( Favouritism)

  Upendeleo kwa sehemu kubwa kimatumizi ni ubaguzi katika kutoa haki kati ya watu au jamii wenye kustahili haki sawa.

  Upendeleo ni kutoa hisani kwa mtu/kundi la watu na kuliacha au kulibagua kundi jingine lenye sifa sawa na lile ulilolipa hiyo hisani!

  Kwa hiyo Mungu hana upendeleo!

  God is not Fair, but He is Just!

 16. RUMI 9.6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.

  7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa;

  8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.

  9.14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!

  9.19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?

  9.20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?

  9.23 tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;

  9.24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa Mataifa pia?

  Rumi10.20 Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia.

  10.21 Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi.

  11.33 Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!

  11.34 Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?

 17. …inaendelea…

  wasiojua kusoma wala kuandika!Ila nafasi ya wokovu ni sawa,kwani tutaokolewa au hukumiwa kwa kile tukijuacho tu.

  Pia wanawaisrael walipata fursa ya ziada kuwa taifa teule ila nafasi yao na yetu ktk wokovu ni sawa.

  Nini maana ya Upendeleo?

  Ina maana watu wawili au zaidi wenye hadhi/sifa/vigezo sawa kuchukuliwa/kutendewa tofauti ktk jambo au huduma fulani!

  Sasa fikiri, Imani .. Iliyotajwa hapo juu..inayoufanya upendeleo wa Mungu alioutoa kwa wanadamu wote ufanye kazi maishani mwa yeye aaminiye Je ndo tuuite upendeleo? Sio kweli, kila mtu ana nafasi sawa ya kuufaidi upendeleo uo iwapo tu atatimiza vigezo-Imani.

  Mrs Christina: umedai kuwa Mungu aliwaombea Wanafunzi tu na sio ulimwengu Yoh17:9,ivyo ni sawa na kusema biblia inajichanganya ukizingatia Yoh3:16-upendo wa Mungu nikwa ulimwengu wote!

  Pia,umesahau kusoma Yohana 17:20,. Anaposema,onawaombea sio wanafunzi tu bali na wengne watakaoamini (ulimwengu).mbona hujasoma hii.!

  Ninachotaka kusema ni kuwa, izo aya zote mlizotoa, Mithali, Ayubu, Esau vs Yakobo, wana wa Mungu vs Wanadamu- zote uonyesha kuwa pasipo IMANI upendo/upendeleo wa Mungu kwa watu wote hauwezi kutunufaisha.na huu tunaousema hapa ni tofauti kabisa na ule wa kibinadamu anaopewa mtu asiyestahili.

  ***tufunguliwe akili,tuelewe na maandiko***

 18. Kama kupendwa na Mungu kunanigharimu mimi kumpenda, je kule kupendwa kwangu na yeye hapo bado ninasema huo ni upendeleo?

  Ndio maana kuna umuhimu wa kuelewa maana ya neno upendeleo kwanza!

 19. Shalom. Kama alivyosema ndg Lwembe,Upendeleo wa Mungu umejikita juu Ya Msingi wa Neno lake.Hebu tafakari hii mistari; MITHALI 8:17 “Nawapenda wale wanipendao, Na wale nitafutao kwa bidii wataniona”. Kumpenda Mungu ni kulishika NENO LAKE (YOHANA MT. 14:15 ” Mkinipenda, mtazishika amri zangu”.

 20. Lakini si neno linasema kuwa Mungu hana upendeleo?

  Au neno upendeleo lina maana gani hasa?

 21. Wandugu maswali ni mazuri na ya msingi sana maana yanatatanisha kwakuwa Mungu anasema na hawa wanaokoka lakini wengine hawaokoki je Mungu ana upendeleo? Cha msingi sana uyafahamu majibu ya maswali haya.
  (i) Je Mungu husema na watu gani katika ndoto anabagua?
  (ii) Je Mungu anasema na watu hao katika ndoto ili kusudi iweje?
  1.0 Kwa nini watu wengine Mungu hukutana nao katika Ndoto na kusababisha WAOKOKE wakati wengine wakiendelea katika maisha ya dhambi?
  (i) Je Mungu anabagua anaposema na watu?
  Mungu hunena na watu wote katika ndoto bila kujali ni mkristo, muisilamu, mpagani, mhindu, Myahudi, Mwarabu, mkurya, mnyamwezi mototo au mtu mzima. Yaani ndoto unazoota ni Mungu anazungumza na wewe. Yeye hunena na watu wote kwa sababu yeye ni Mungu wa wote wenye mwili. (Yeremia 32:27. Katika Ayubu 33:14- inasema, Kwakuwa Mungu hunena mara moja naam hata mara ya pili ajapokuwa mtu hajali (hatii ufahamu), katika ndoto na katika maono ya usiku usingizi mzito uwajiliapo ndipo huyafunua masikio yao (ya rohoni) na kuwafundisha sheria yao. Kwahiyo hakuna mtu ambaye Mungu hasemi naye katka ndoto. Tatizo ukiona Mungu ameleta ndoto mbaya (hakuna ndoto mbaya kwa Mungu zote ni nzuri hata kama unaota unazini, unaua, unatukana hiyo ni nzuri tu maana inataka utoke huko dhambini), unadhani hiyo ndoto imeletwa na Shetani. Kumbuka ulimwengu wa roho (katika ndoto) uko chini ya utawala wa Roho Mtakatifu, shetani hana mamlaka nao.
  (i) Mungu anasema katika ndoto kusudi iweje?
  Mungu husema katika ndoto akupe taarifa ili ujue
  o Mbinguni wanakuwazia nini , wamekukasirikia au la!
  o Kuzimu wanakuwazia nini
  o Mazingira ( wanaokuzunguka) wanakuwazia nini baba,mama,rafiki,jirani,watoto nk.
  Mungu hukutana na watu wote katika ndoto. Wengine wanaokoka wengine hawaokoki!! Tatizo liko wapi?
  (i) Uamuzi wa kwenda mbinguni au jehanamu ni wa mtu mwenyewe, soma Yoshua 24:15-16 Uchaguzi ni wako kuokoka au kutokuokoka.
  (ii) Wajibu wa kumtafuta Mungu ni wa mwanadamu usipomtafuta huokoki Mithali 8:17 ukimtafuta kwa bidii utampata (utaokoka), tatizo watu hawamtafuti Mungu.
  (iii) Wako watu ambao Mungu ana kazi nao hawa huwa anawatafuta kokote waliko hata kama ni machungani (Daudi), Kwa matasa (Samweli, Yohana, Isaka nk)
  (iv) Wako watu ambao Mungu amekwisha kuwahukumu kwenda jehanamu tangu tumboni mwa mama zao hao omba mpaka upate vidonda vya tumbo hawataokoka soma Zaburi 58:3 umewahi kusikia mimba ikisema uongo? Maana yake wanazaliwa wakiwa wamehukumiwa kwenda jehanamu.
  (v) Mtu hawezi kuokoka kama Mungu hajamridhia Soma Yohana 6:44, lazima Mungu atake ndipo uokoke kama asipotaka mtu atakaa gizani mpaka kifo. Kwa maana nyingine kuokoka ni kwa neema tu siyo kwa maamuzi ya mtu.
  2.0 Kwa nini maeneo Mengine Wainjilisti hupokezana VIWANJA VYA MIKUTANO, akitoka mmoja anaingia mwingine wakati sehemu zingine inaweza kupita miezi kadhaa bila kuona Mkutano hata mmoja wa Injili?b HILI LINAHUSIANA NA MAMBO YALIYO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO AMBAKO KUNA VITA KUBWA. KWA SABABU HIYO KUMILIKI NCHI AU MAHALI NI LAZIMA MUWE MMEPIGANIA SANA. KWAHIYO HAPO AMBAPO WATU HAWAENDI SANA KUFANYA MIKUTANO PANAMILIKIWA NA VIUMBE VINGINE PANAHITAJI KUKOMBOLEWA.

  • Je, ni kwamba Mungu anapendelea baadhi ya watu ili wamjue yeye huku wengine anawaacha waangamie?
  Kwanza ufahamu si kila mtu atakwenda mbinguni kutokana na ukweli kwamba watu wamepewa uchaguzi wa kwenda kwa Yesu au Mungu mwingine. Chagueni hivi leo mtakayemtumikia). Kwahiyo wana uhuru, Mungu hataki kumlazimisha mtu, ni wachache tu aliwalazimisha sababu alikuwa na kazi nao. (akina Yeremia, Isaya, Ezekieli, Musa nk ) walikuwa hawataki lakini akawalazimisha)
  Soma haya maandiko uone kama Mungu ana upendeleo Matendo 10:34-35; 1Samweli 16:7; wengine anawakataa; Warumi 9:14-33
  MBARIKIWE SANA

 22. Wapendwa Mbarikiwe,

  mrs christina.Nashangaa jinsi unavyojaribiwa kwenda mbali zaidi hata kusema Yesu akuja kwa ajili ya watu wote.pia kudai kuwa anaupendeleo,Neema ni Neema kwa 7 na zaidi sana kudai kuwa ibabu inapendeleanjili inayodai ivyo ni mfu na mazoea tu! Pole sana.

  Soma vizuri mchango wa magreth hapo juu.ameyaweka haya vizuri tu.

  Tafakari haya:

  Kwanza kabisa tujue kwamba neno upendeleo limetokana au ni mnyumbulisho wa neno upendo. Then , tafakari mantiki iliyopo kwny maneno haya,

  1.Yoh 3:16″.kwa maan jinsi hii Mungu ALIUPENDA ULIMWENGU, hata akamtoa mwanae wa pekee,ili KILA MTU amwaminie awe na uzima wa milele”

  2.Ebr11:”..maana pasipo IMANI haiwezekani KUMPENDEZA MUNGU”

  Point za kuzingatia:

  1.Hebu fikiri Neno, ALIUPENDA ULIMWENGU-hv unafikiri aya hii inawahusu nani hasa? Wote au baadhi

  2.Pia, “..Ili KILA MTU AMWAMINIE..” mbona hata hii aibagui km unavyofanya wewe.

  3.Waebrania 11 – inatwambia ingawa yoh3:16 inaonyesha kuwa Kila mtu anapendwa na Mungu, ila mrejesho wetu kwake kwa njia ya Imani kunatufanya TUMPENDEZE. Yaani tunakuwa wanufaikaji wa upendeleo alioupatia ulimwengu wote.

  Kwakuzingatia mafungu aya, kila mtu ana nafasi sawa ya kujitwalia upendo,upendeleo aliotupa Mungu!

  Nina maana kuwa ktk suala la wokovu, wote tuna NAFASI sawa ila FURSA tofauti(equal chances vs unequal opportunities)!. Nina maana kuwa Wanafunzi wa Yesu walikuwa na fursa kubwa zaidi yetu ila tuna nafasi sawa ktk wokovu. Sisi tunaosoma hapa SG michango fursa kubwa ukilingnisha na wale wazee wetu kule vijiji

 23. Upendeleo wa Mungu umejengeka katika Haki yake. Ili kuitimiza Haki hiyo, sote hupewa fursa sawa ktk uhuru wa maamuzi kuhusu Neno lake.

  Naye Mungu ndiye Muinjilisti wa kwanza, tunamuona akimuinjilisha Kaini kuhusu dhambi, Mwa 4:6 “6BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.”

  Hii ndiyo jinsi ya Haki ya Mungu inayozalisha Upendeleo kwa wenye kuutafuta Moyo wake, na Hukumu kwa wenye kiburi. Mungu anapokuambia jambo fulani, labda anakuambia “Usiwe na miungu mingine”, usijipokelee tu miungu bila ya kuitafiti kujua kama ndiye huyo Mungu wa Kweli? Yapime mambo yote yanayomhusu Mungu kwa Neno lake na si hadithi za dini!

  Kwa mfano, kiongozi wako anajipachika u “Adamu wa Pili”, halafu anakuchanganya na maneno ya kusisimua kama “Damu ya Haki na Hukumu”, nawe unakaa hapo kama kuku wa kizungu anayemkimbia panzi, umejijaza uvivu unaokusababishia kushiriki kufuru bila kujua, Je, kuna mpumbavu atakayesamehewa? Kamuulize Esau yaliyomfika, na wengi wetu tutapotea kwa dengu! Naye Mungu anakuona unavyoiuza Haki yako ya Mzaliwa wa Kwanza kwa tumiujiza tusito dumu, ndio maana alimchukia Esau!

  Jambo jingine la muhimu sana, ni kwamba tunapaswa tujue kwamba hapa duniani kuna makundi yapatayo matatu. Kundi la kwanza ni hao waliondikwa majina yao ktk Kitabu cha Uzima, ambalo ndani yake kuna ambao majina yao yatafutwa, haswa hao watakaojiingiza ktk kulikufuru Neno la Mungu, hilo ambalo ndilo Roho, Yn 6:63 “Maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.”

  Na kundi jingine ni la hao ambao majina yao hayajaandikwa ktk Kitabu cha Uzima, yaani ni kundi la kupotea!

  Sasa hatari kubwa ni pale kati ya hao wasiondikwa majina yao na hao waliofutwa, anapotokea kuwa kiongozi wako wa kiroho, nawe kwa upumbavu uliokutia uvivu, hujisumbui kumkagua ktk Neno ili uone kama ametumwa kweli?! Je, anachokifundisha, ndicho walichofundisha mitume?

  Basi Roho akiwa ndiye atiaye uzima, tunapaswa tuutazame huo Mwili uliotiwa uzima kwa huyo Roho, nao Mwili huo ndio Mwili wa Kristo ambao unalo hilo Neno ambalo ndilo Roho, Mwili huo ni wale mitume wake. Basi unapokutana na mkristo, ukamuonesha hilo Neno linalonenwa na mitume, akiona linapishana na mafundisho ya nabii wake, ndipo angetaharuki na kukuambia “Tumfuate nani, Yesu Mwalimu au mitume wanafunzi? Kisha akakusisitizia kwamba “role model wetu ni Kristo!” Unaona! Sasa, ukiisha kulitilia shaka Neno la Mungu, usitegemee kupata Upendeleo wake, kwa maana ukiisha kukombolewa kwa Damu yake, halafu ukajirudisha ktk kumtilia shaka, hilo ni sawa na KUMTUSI!

  Upendeleo wa Mungu uko kwa wenye kulipenda Neno lake!

  Gbu all!

 24. Salaam,
  Katika hii site, kuna uwezekano wa kuongezaea sehemu ya ‘ku-sapoti’ au kukataa yaani ikawa sio lazima kuandika chochote bali ukaunga mkono hoja fulani au ukaididimiza (dole juu dole chini!!)?? Hebu ongezeeni ‘kipengele’ hicho! Kuna maoni yanavutia sana na mengine yanavutia kidogo na mengine yanaboa sana na mengine afadhali!!
  Shukran. 🙂 🙂 🙂

 25. Mrs Christina,

  Nashukuru sana kwa makala yako. Mim nawapendaga sana wanaosema kweli. Nadhani ni mwalimu kama wewe nilikuwa nikitafuta.

  Ubarikiwe.

 26. MUNGU HANA UPENDELEO NA HAJIPINGI KAMA ASEMAVYO KTK NENO LAKE PIA HUFANYA VITU KAMA APENDAVYO YEYE MAANA ANASEMA ANATUJUA TANGU TUKIWA TUMBON MWA MAMA ZETU. KUHUSU KUFANYA MIKUTANO MAHALI FLANI HATA KUFUNGUA HUDUMA SEHEMU HIZOHIZO HII INATOKANA NA MASLAHI BINAFSI MARA NYINGI, MAANA AGIZO KUU LA BWANA YESU LASEMA ” ENENDENI ULIMWENGUNI KOTE MKAWAFANYE MATAIFA KUWA WANAFUNZI WANGU……..” KWAKUWA BAAZ YA WATUMISHI KUPENDA PESA WANAELEKEZA HUDUMA ZA KIROHO MIJINI KWENYE MAKAMPUNI,WIZARA NA TAASISI MBALIMBALI, KIJIJINI WATAPATA NN???????????

 27. TUKIIKATAA KWELI , UONGO UTATUANGAMIZA!!!
  Ni kweli kwamba Mungu HANA UPENDELEO kwa wateule wake
  yaani wale aliowachagua kabla ya kuanzishwa kwa misingi ya dunia
  na hawa ndiyo waliofanyika kuwa WANA WA MUNGU.MWANZO 6:1-2
  inaeleza wazi kabisa kuwa duniani kuna WANA WA MUNGU na
  WANADAMU.Si kila mtu anaweza akapata NEEMA ya wokovu na ndiyo
  maana inaitwa Neema!Moja kati ya mafundisho ya uongo ni hili suala
  la kwamba Yesu alikuja duniani kwa ajili ya WATU WOTE.Yesu mwenyewe aliliweka jambo hili wazi sana wakati AKIWAOMBEA WANA
  WA MUNGU WAWE NA UMOJA.Yesu akuomba UMOJA WA WATU
  WOTE ULIMWENGUNI bali umoja wa wateule yaani wale ambao
  Mungu alimpa awachunge.
  Sikiliza kwa makini sana na tena utafakari kile ambacho Yesu
  anasema hapa katika YOHANA 17:6,9 “Jina lako nimewadhihirishia
  WATU WALE ULIONIPA katika ulimwengu,walikuwa wako, ukanipa mimi
  na neno lako wamelishika. Mimi NAWAOMBEA HAO, SIUOMBEI
  ULIMWENGU, BALI HAO ULIONIPA kwa kuwa HAO NI WAKO”
  Unasikia maneno haya ambayo Yesu anamwambia Baba yake!

  ZABURI 58:3 inatuthibitishia kwamba kuna watu wanaletwa duniani
  ili KUTUMIKIA KUSUDI LA SHETANI.Wanazaliwa ili kuja kupanda mbegu
  za UONGO na MITHALI 16:4 inakazia wazi kabisa kuhusu hili.Inabidi tusome haya maandiko kama kweli tuna nia ya kujifunza alafu tuyatafakari.

  TUUNGANE NA BAADHI YA MAANDIKO ALIYOTUPA MTUMISHI
  ZIRAGOZA!

  Mtumishi ZIRAGOZA
  Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo.

  MITHALI 14:9 inasema “Wapumbavu huidharau hatia bali UPO UPENDELEO kwa WENYE HAKI”
  Hapa tunaona wazi kabisa kwamba kuna UPENDELEO kwa WENYE
  HAKI na WASIO HAKI wanaitwa WAPUMBAVU.Mungu hana upendeleo
  miongoni mwa WENYE HAKI kama kina Mtume Petro ambao walikuwa
  ni wayahudi na kina Kornelio ambao walikuwa ni watu wa mataifa.
  Petro alidhani wayahudi tu peke yao ndiyo waliopewa NEEMA ya wokovu na Mungu akamueleza kwa njia ya maono kwamba wateule
  wa Mungu wako katika kila kabila, rangi na lugha duniani kote.Hata hivyo ndani ya familia ya watu sita, tunaweza tukaona mtu mmoja
  anapata Neema ya wokovu na waliobakia watano wasipewe neema
  ya wokovu!!Kama unadhani natania soma LUKA 12:51-53,unakuta mtoto amepewa Neema ya wokovu lakini wazazi hawajapata matokeo
  yake wanaishia kufarakana nae!Katika kila familia au ukoo kuna wenye
  haki na wasio haki.Yawezekana haya yasiwe mepesi sana kuyaelewa
  kwa sababu ya mafundisho yaliyo kufa tuliyoyazoea!

  ISAYA 60:10 inaelezea jinsi Mungu alivyolipendela Taifa la ISRAEL
  ambalo ni taifa lake teule!Kwa wale wasiojua ni kwamba ISRAELI
  ni taifa la wayahudi ambalo Mungu aliamua kuliteua ili kumpitisha
  Yesu yaani azaliwe kupitia taifa hilo kama myahudi.Kwahiyo MUDA
  NA BARAKA ZOTE za mataifa yote duniani ZIMEFICHWA ndani ya taifa
  la ISRAELI!!Taifa lolote lisilotaka kuitumikia ISRAELI lazima liangamie.
  Kaiulize MAREKANI na UJERUMANI juu ya hili.Na kwa uhakika zaidi
  soma ISAYA 60 yote.Neema ya wokovu iliyotufikia sisi ilianzia ISRAELI.
  Watu wote tuliopewa neema ya wokovu TUNA UPENDELEO dhidi ya
  WATU WASIO HAKI(uzao wa nyoka).

  AYUBU 10:12 Tunaona namna ambavyo mteule wa Mungu Ayubu
  anakiri kwamba Mungu AMEMJAZA UHAI NA UPENDELEO.Ndivyo
  ilivyo hata leo watu wote ambao wamepewa neema ya wokovu
  wamejazwa uhai na upendeleo.Duniani kuna watu ambao wanatokana
  na mbegu ya kizazi cha Israeli(Yakobo) ambao baba yao ni Mungu aliye hai na watu wanaotokana na kizazi cha Esau(Edom) ambao baba
  yao ni shetani!Na hii haina maana ya kwamba hakuna wateule
  wanaokwenda kuzimu.Kama tusipoishi maisha ya kujitakasa na tukajisahau katika dhambi KUANGAMIZWA na wajumbe wa shetani
  ni lazima kwahiyo ni vema tukautumia vizuri upendeleo tuliopewa!
  kama unadhani nakutania soma WAEBRANIA 6:4-6.Kumbuka hili na
  ulishike, HAKUNA UZAO WA NYOKA AMBAO UNAWEZA KUPEWA
  KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU,wao wanaongozwa na Roho ya shetani na kunena kwa lugha za kipepo!

  HAYA NI MAFUNDISHO AMBAYO MBWAMWITU WANAFANYA JUU
  CHINI ILI WATEULE WASIYAJUA…………..

  Mtumishi ZARAGOZA tuko pamoja, Roho Mtakatifu ataendelea
  kuzama ndani zaidi mpaka kieleweke.

 28. Wapendwa,

  Ninaposoma Biblia naona shairi nyingi sana zinazosema Mungu hana upendeleo.
  Lakini pia kuna nyingine zinazoonyesha kama anaupendeleo kama Ayubu 10:12,Mithali 12:2, Mithali 13:15, Mithali 14:9, Mhubiri 9:11, Isaya 60:10.

  Sasa inaomba kimantiki tufahamishwe kama huo upendeleo ni upi anao pia ni upi ambao hana.

  Karibu walimu kwa kutufundisha.

  Asante.

 29. Ndugu yetu,

  Matendo 10:34-35- ” Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. ” aya inaonyesha hata mtume aliye kabidhiwa kanisa la mitume alikuwa na fikra kama zako

  Rafiki, Mungu ana namna yake ya kufanya kazi na kujifunua kwa mtu mmoja mmoja. Usitake afanya kazi kama unavyofikiri wewe. Katika suala la wokovu wote tuna nafasi sawa ya wokovu.

 30. God is Fair & So is His Favor

  I heard a sermon once in which the preacher made the statement that “God is not fair”. The words bothered me so much immediately. I have since really struggled with that ‘claim’. As it depicts God in a light that I personally feel, is so false.

  Since the sermon that I heard, God has shown me continuously, verse after verse, there’s a reason that message has bothered me so much. I have read scriptures that say otherwise.

  God IS fair.

  Some definitions of ‘Fair’: Free from bias, dishonesty, or injustice: a fair decision; a fair judge. Free from self-interest, prejudice, or favoritism.

  I think about how as a parent I attempt to make things fair for my children. How it’s my job as a parent to bring about that “fairness” and do things in a “just” manner. Because, Life is not fair. People are not fair. Situations are not fair. Hardships are not fair. Circumstances are not fair. There are more things on earth that are NOT fair, than fair. So it’s my job to keep things in my home as fair as I can. As a parent I love my children equally. Not one more than the other. They are each so different from one another. Each with her own strengths and weaknesses. Talents & gifts. Each with her own endearing ways. I could never love one more than the other. They are each so precious in their own ways. They each brings something no one else ever could to our little family. And in my raising them, I believe in treating each one fairly, free from bias, prejudice or favoritism.

  Through life & all the unfairness it brings I believe we can have peace in the fact that we serve an incredibly fair God. We serve a just God. When life and all it throws at us is unfair, we can rest in knowing our God is righteous and just, good and FAIR. Our God loves His children equally and counts us as precious in our own ways. He sees what we each bring to the table.

  Here take a look at the proof I found. (There are many verses that talk about God being fair and how we should be fair like him, these are only a portion.)

  Genesis 18:19 I have chosen him so that he would command his children and descendants to live the way the Lord wants them to, to live right and be FAIR. Then, I, the Lord will give Abraham what I promised him.

  Leviticus 19:15 Be fair in your judging, you must not show special favor to poor people or great people, but be fair when you judge your neighbor.

  Deuteronomy 32:4 He is like a rock; what he does is perfect, and he is always fair. He is a faithful God who does no wrong, who is right and fair.

  1 Kings 9:4 But you must serve me as your father David did; he was fair and sincere. You must obey all I have commanded and keep my laws and rules.

  Job 34:17 Can anyone govern who hates what is right? How can you blame God who is both fair and powerful?

  Psalm 9:8 and he will judge the world in fairness; he will decide what is fair for the nations

  Psalm 9:16 The Lord has made himself known by his fair decisions

  Psalm 33:5 He loves what is right and fair; the Lord’s love fills the earth.

  Psalm 89:14 Your kingdom is built on what is right and fair. Love and truth are in all you do.

  Psalm 103:6 The Lord does what is right and fair for all who are wronged by others.

  Proverbs 21:3 Doing what is right and fair is more important to the Lord than sacrifices.

  Isaiah 30:18 The Lord wants to show his mercy to you. He wants to rise and comfort you. The Lord is a fair God, and everyone who waits for his help will be happy.

  Jeremiah 9:24 But if people want to brag, let them brag that they understand and know me. Let them brag that I am the Lord, and that I am kind and fair, and that I do things that are right on earth. This kind of bragging pleases me,” says the Lord.

  Ezekiel 18:25 But you say, ‘What the Lord does isn’t fair.’ Listen, people of Israel. I am fair. It is what you do that is not fair!

  John 5:30 By myself I can do nothing; I judge only as I hear, and my judgment is just, for I seek not to please myself but him who sent me.

  2 Thessalonians 1:6 God is just: He will pay back trouble to those who trouble you

  Hebrews 6:10 God is fair; he will not forget the work you did and the love you showed for him by helping his people. And he will remember that you are still helping them.

  I believe favor comes from God. I believe His Favor is fair because God is fair and favor is available for all of us who love Him. Favor can be bestowed upon all of God’s children. Anyone who loves God can pray for favor and should pray for favor.

  God rewards. God gives. God takes away. God is fair. God will be fair.

  Life isn’t fair. Circumstances are not fair. But God is fair and we can find favor with Him.

  Favor = (noun) an attitude of approval or liking (verb) feel or show approval or liking

  Fact is God loves us all. When we strive to do what pleases the Lord we can find favor with him. Though we all fall short, God still approves of us. Like when our children fall short, nothing they do or don’t do could ever make us love them less. If God didn’t love us, He wouldn’t have sent His son to die in our place. God created each of us. We are loved even when we fall short.

  Favor as a form of favorite would imply that God has favorites, which Romans 2:11 says For God does not show favoritism.

  Therefore, God does NOT have favorites or favor certain children. God does not bestow his favor upon only certain followers like some game of chance or by a lottery system.

  If salvation is available for all of us and Jesus died for ALL mankind wouldn’t that mean we all have favor available to us? Proverbs 8:35 For those who find me find life and receive favor from the LORD. Are you following? Favor IS for all of us who love God.

  We shouldn’t brag about our blessings or things we receive or have. To speak in a way such as to say “Favor ain’t fair” is an ‘in someone’s face’ statement which sounds like ‘I am more spiritual than you or God favors me more because of this or that’.

  And this isn’t how God works. Favor IS fair. We all can be blessed. Anyone who loves and serves God can receive God’s favor. Being blessed with this or that, while the person next to us has something less at the moment doesn’t mean they are less than us as a person or christian. It doesn’t mean you have done something that warrants a bigger amount of favor. Someone having more money or less, a higher social standing or less, a job or a loss, a family or striving to have a family, etc. doesn’t mean more or less “favor.”

  We can ALL count our blessings and should NEVER compare our blessings or favor to anyone else’s.

  Sure, favor can come in different forms. We don’t all receive the same rewards and blessings in life. Because we’re all different. We all have different talents, strengths, weaknesses, struggles, needs, wants, desires, etc.

  God is fair. So I believe His favor lines up with His fairness.

  And that favor is absolutely available to all of us.

  Psalm 5:12 Surely, LORD, you bless the righteous; you surround them with your favor as with a shield.

  Psalm 30:5 For his anger lasts only a moment, but his favor lasts a lifetime; weeping may stay for the night, but rejoicing comes in the morning.

  Proverbs 3:34 He mocks proud mockers but shows favor to the humble and oppressed.

  Proverbs 11:27 Whoever seeks good finds favor, but evil comes to one who searches for it.

  I know I sound like a broken record, but I really believe this! God truly is fair and anyone can find favor with Him!

  Count your blessings. Don’t compare your life to anyone else’s. We have all been created as equal and are loved equally by God. Embrace your salvation. Strive to follow the example set before us and live a life of righteousness by being fair in your day to day interactions with others. Find peace in God’s ability to be fair when all else isn’t

 31. Mtumishi ORBI

  Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo.

  Nimeyatafakari sana maelezo yako katka paragraph ya mwisho.
  Hebu tusome na kufuatilia kwa pamoja Maandiko yafuatayo;

  MATENDO 16:6-10
  “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, WAKIKATAZWA NA ROHO
  MTAKATIFU, WASILIHUBIRI LILE NENO KATIKA ASIA.Walipofika kukabili
  Misia wakajaribu kuenda Bithinia,Lakini ROHO WA YESU AKUWAPA
  RUHUSA……..Paulo akatokewa na maono usiku, alimuona mtu wa Mekadonia amesimama, akamsihi na kumwambia, vuka uje Mekadonia
  utusaidie.Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka
  kutoka kwenda Mekadonia, kwa kuwa tuliona HAKIKA KWAMBA
  MUNGU AMETUITA TUWAHUBIRI HABARI NJEMA”

  ZABURI 58:3-4
  “WASIO HAKI wamejitenga tangu kuzaliwa kwao tangu tumboni
  WAMEPOTEA, WAKISEMA UONGO.Sumu yao mfano wake ni sumu
  ya nyoka.Mfano wao ni fira kiziwi azibaye masikio yake ”

  MITHALI 16:4
  “BWANA amefanya kila kitu kwa KUSUDI LAKE.Naam, hata WABAYA
  kwa siku ya ubaya”

  MARKO 4:11-12
  “Akawaambia ,NINYI MMEJALIWA KUIJUA SIRI YA UFALME WA MUNGU,
  bali kwa WALE WALIO NJE yote hufanywa kwa mifano,ili WAKITAZAMA, WATAZAME WASIONE NA WAKISIKIA, WASIKIE, WASIELEWE, WASIJE WAKAONGOKA NA KUSAMEHEWA”

  WARUMI 11:13-14
  “Lakini nasema na nyinyi mlio watu wa Mataifa.Basi kwa kadiri nilivyo
  mtume wa watu wa Mataifa,naitukuza huduma iliyo yangu, NIPATE
  KUWATIA WIVU WALIO DAMU MOJA NA MIMI NA KUWAOKOA
  BAADHI YAO”

  WARUMI 10:13,16,18
  “Kama ilivyoandikwa NIMEMPENDA YAKOBO bali ESAU NIMEMCHUKIA.
  Basi kama ni hivyo, SI KATIKA UWEZO WA YULE ATAKAYE WALA
  WA YULE APIGAYE MBIO, BALI WA YULE AREHEMUYE, YAANI
  MUNGU.Basi kama ni hivyo atakaye kumrehemu, HUMREHEMU
  na atakaye kumfanya MGUMU humfanya MGUMU”

  MWANZO 6:1-2
  ” Ikawa WANADAMU walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike
  walizaliwa kwao, WANA WA MUNGU waliwaona HAO BINTI ZA WANADAMU kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wo wote waliowachagua”

  MAFUNUO TUNAYOYAPATA NDANI YA MAANDIKO HAYA

  1.MWANZO 6:1-2 inatuambia kwamba duniani kuna WANADAMU
  na WANA WA MUNGU!

  2.WARUMI 10:13,16,18 Inasema Mungu alimchagua Yakobo na kumkataa Esau! Mungu alimrehemu Yakobo na kumchukia Esau!
  Soma UNABII kuhusu maisha ya Yakobo na Esau ambao Mungu
  alimpa mama yao alipokuwa mjamzito ndani ya MWANZO 25:21-23
  “………..BWANA akamwambia MATAIFA MAWILI YAKO TUMBONI
  MWAKO, NA KABILA MBILI ZA WATU WATAFARAKANA TANGU
  TUMBONI MWAKO.KABILA MOJA LITAKUWA HODARI KULIKO
  LA PILI, NA MKUBWA ATAMTUMIKIA MDOGO”

  3.ZABURI 58:3 inasema kuna WATU WASIO HAKI ambao walishapotea
  tangu wakiwa tumboni mwa mama zao!

  4.MITHALI 16:4 inasema duniani kuna WATU WABAYA na WATU
  WAZURI na wote wameubwa kwa makusudi maalum!

  5.MATENDO 16:6-10 inasema kuna mahali tunweza kutamani sana
  kwenda kupeleka injili ya Yesu lakini Yesu mwenyewe akatuzuia
  tusiende!!

  HITIMISHO
  Mungu hana upendeleo kwa wateule wake, kila mteule ni mbarikiwa
  unaweza ukazaliwa na mtu tumbo moja lakini asiteuliwe.Ndiyo maana
  MWANZO 3:15 inatueleza wazi kabisa kwamba MAISHA YA DUNIANI
  NI VITA KATI YA UZAO WA YESU NA UZAO WA NYOKA.Uzao wa nyoka kamwe hawawezi kumpokea Yesu( Rudia kusoma MARKO 4:11-12).HABAKUKI 1:4 inasema WENYE HAKI(WATU WAZURI) wamezungukwa na WATU WABAYA(UZAO WA NYOKA).

  BIBLIA ni neno la Mungu lenye majibu yote ya maisha yetu
  ya hapa duniani na kule mbinguni.Ndiyo maana shetani na watoto
  wake wanafanya juu chini ILI KUHAKIKISHA WATEULE HAWAELEWI
  NENO LA MUNGU.Mafundisho yaliyo kufa yamekuwa mengi hasa
  katika SEMINA ZA UJASIRIAMALI na SEMINA ZA NDOA.TUWE MAKINI
  SANA NA MAFUNDISHO YANAYORUSHWA KATIKA TV NA RADIO.BILA
  YA MUONGOZO WA ROHO MTAKATIFU TUTAENDELEA KULISHWA
  SUMU ZA NYOKA.

  Mtumishi PANDAEL SIMON twende kazi……….Nimekupa pande hilo
  ushindwe mwenyewe kumalizia.Nataka upige shuti kali ambalo
  mabeki na kipa wa timu ya uzao wa nyoka wataona tu nyavu za
  golini zikiwacheka……………

  Yesu ni mshambuliaji ASIYEZUILIKA MILELE.

 32. Naungana na mchangiaji wa kwanza hapo juu. Kwanza Mungu hana Upendeleo maana yeye si mwanadamu maana wanadamu tuna mamo mengi.Pia kutomsikiliza Roho Mtakatifu pia kunafannya watumishi wengi wasihubiri injili wanakoambiwa wahende kuhubiri injili bali wanamuwekea Mungu mipaka na masharti na Sharti kubwa wanaangalia PESA kwanza.
  Mtumishi mmoja wa Mungu alisema wainjilisti wa sasa wanataka injili ya Rami(Tarmac Roads) na sio makorongo na mashimo yaani pesa mbele ila pia tukumbuke kuwa mahali ambapo maasi yamezidi ndipo Neema inaongezeka zaidi ili kuweka uwiano.
  Pia kuna kitu kinahitwa UTUKUFU WA MUNGU.Yako maeneo Mungu anataka ajitukuze yaani Mungu akionekana katika kitu fulani mahali hapo basi wengi uokolewa.
  Pia tukumbuke kuwa kazi ya kuokoa ni ya Mungu mwenyewe(Majira na Jinsi ya kuokoa) na si ya mwanadamu.Sisi si kazi yetu bali kazi yetu ni kupanda Neno tu(Kuhubiri habari njema za ufalme wa Mungu.

 33. Ndugu yangu,

  Mungu hana upendeleo, maandiko mengi yanasema hivyo sina haja ya kuyanukuu hapa, na vile vile Makusudi ya Mungu hayachunguziki….akili zetu haziwezi kabisa kuyachunguza makusudi yake…..

  Lakini mambo mengine uliyoeleza haya uhusiano na Mungu….Je kama wainjilisti wetu hawaendi sehemu ambayo haijafikiwia na Injili ila wanapenda kwenda mahali fulani tu, inawezekana kabisa, labda hawajaitii sauti ya Mungu inayowataka kwenda na kuanza kazi ambako wengine hawajaweka msingi, lakini pia labda wakati wa Mungu kupeleka Injili sehemu hiyo haujafika…..Yesu hakumaliza vijiji vyote Israeli……na hakuponya wagonjwa wote waliokuwepo katika Israeli….! Kumbuka yule mgonjwa aliyeponywa na Petro kwenye mlango wa Hekalu, Yesu alipita mara nyingi katika mlango huo……! Inawezekana huyo mgonjwa hakuweko hapo……! Au wakati wake ulikuwa bado…..hatujui…….Lakini alipokuja ponywa na Petro, uponyaji wake ulisababisha mlipuko wa kuhubiri Injili hadi watu 5000 wakaongeza katika kanisa……!

  Kuhusu kuokoka kwa ndoto……hata ndani ya Agano jipya ni wachache…..Paulo…..Kornelio kama nakumbuka kwa haraka. Nakumbuka pia ratiba nzima ya kusambaza Injili iko chini ya Roho Mtakatifu…..Paulo alitaka kupeleka Injili baadhi ya sehemu….Roho Mtakatifu akamzuia….akataka kwenda sehemu nyingine Roho akamkataza……na baadaye akaona Maono kwenda sehemu aliyotakiwa Kwenda……!

  Mungu na kubariki…

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s