Ni ELIMU hii hii ya Darasani au Ni ELIMU kitu kingine?

vitabu

Mara nyingi tumekuwa tukitumia Maneno kutoka katika Kitabu cha Mithali 4:13 yasemayo:

Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.

Maneno haya yamekuwa yakitumika katika kusindikiza jitihada au harakati za kielimu, kuwahamasisha watoto/watu kujisomea au kusoma. Tena hata kwa wale wasiozingatia mambo ya Mungu nao sasa wanatumia maneno hayo katika matangazo ya shule zao au vyuo vyao.
Swali lililopo hapa ni  Je, maandiko hayo yanatumika sawa sawa au yamepelekwa kutumika isivyo sahihi?
Kiinachozungumziwa katika Mithali 4:13 ni elimu hii ya Biolojia na Hisabati ndizo mtu anatakiwa kuzishika kwa kuwa ni UZIMA wake au kuna maana tofauti na ya ELIMU tunayoifahamu sisi, iliyoko chini ya Wizara ya Elimu?

Advertisements

13 thoughts on “Ni ELIMU hii hii ya Darasani au Ni ELIMU kitu kingine?

 1. Biblia ya kiingereza imetumia neno instructions ikimaanisha maelekezo na haiku specify kuwa maelekezo yawe ya kiroho tuu au ya kimwili hivyo hili neno latumika kote mfano unaposoma biology kuna maelekezo ambayo unajifunza kuhusu mwili wa mwanadamu namna ya kuutunza na kadhalika na ukiyafuata utajikuta unaepukana na magonjwa mengi ni hivyo kuleta uzima. Pia katika ulimwengu wa roho neno hili lafanya kazi pia kwa maana kunayo maelekezo mbalimbali ambayo MUNGU ametoa kwa watoto wake na pasipo kuyafuata roho zetu hazitakuwa na uzima mana tutadumaa kiroho

 2. Hii niwazi kuwa, fungu hili linatumiwa vibaya, kama ilivyo kwa mafungu mengi katika biblia yanayotumiwa vibaya,
  Tukiangalia neno hili, “maana yeye ndie uzima wako” nasi sote twajua kuwa, elimu ya duniani haina uzima wowote, katika neno “elimu” na neno “mushike/mukamate” haya maneno yanaweza kumaanisha hivi, kusoma, kuchunguza na kutafuta sana ukweli wa MUNGU, kisha baada ya kuujua ukweli huo, ndipo kuushikiria kikamilifu, ili kupata huo uzima.

 3. Petrus Georgiy,
  Unasema ” ….ni hatari sana wakristo wenye misimamo au aina kama yako sababu anakuwa hana tofauti na wale jamaa wa upande wa pili (wa ishmael)”
  WA ISHMAEL unawajua vizuri au unautafuta UMAARUFU?
  Bwana Yesu Kristo na ahirehemu nafsi yako yenye DHAMBI.

 4. “HOLD ON TO INSTRUCTION, DO NOT LET IT GO”
  “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake …”

  Instruction: 1 mafunzo, mafundisho. 2 (pl) maagizo; mwongozo, maelekezo

  Mdo 2:41- 42 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika FUNDISHO la mitume…”

  Mambo ya kusoma shule ni mkanganyiko wa watafsiri tu; tunapaswa kudumu ktk Fundisho la mitume, humo ndimo Uzima ulimohifadhiwa, nalo Neno hilo ktk mithali linatuongoza huko.

  Maagizo hubadilika kulingana na wakati, usikivu ni wa muhimu sana ili kwenda sawa na Maagizo. wengi tutapotea kwa kushikilia mambo yaliyopita, waliyoagizwa vizazi vingine, kwa ujinga tukiyaacha yale Maagizo yanayotuhusu!!

  Tufungueni masikio yetu ya kiroho ili tuyaelewe Maagizo tunayopewa, hayo ambayo tunapaswa kuyashika yasituponyoke!

  Gbu!

 5. Bwana Petrus. Unaujua Vizuri ‘Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya?’ELIMU YA HESABU,FIZIKIA,KEMIA’HISTORIA……nk, imetoka kwenye MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA (IBILISI) Mbona unakuwa Umeweka Yakini kwa wanadamu unaposema Sungura amenyamaza hivihivi, akinyamaza na Mungu amenyamaza? Unafikiri Luka aliitwa kuwa Mkristo kwa Sababu alikuwa amesoma?Hayo ni maoni yako.Mbona hutuambii Petro,Yohana Bwana Yesu walisoma mpaka darasa la ngapi?Kwani Adamu na Hawa walisoma mpaka darasa la ngapi?Edeni kulikuwa na Shule,chuo au hospitali?Umenukuu maandiko ukayatafsiri kwa kutumia mtazamo wako (personal attitude), unajua maarifa gani mwanadamu aliikataa au unafikiri ni kukataa kwenda shule? Unajua KWELI NI NENO LA MUNGU PEKE YAKE na si elimu ya IBILISI iliyoleta mauti? YOHANA MTAKATIFU 17:17 “Uwatakase kwa ile Kweli; neno lako ndiyo Kweli”. Hujui Kuwa mwanadamu anaweza akawa hata na Phd lakini bado akawa ni mjinga?Ni heri kuwa mjinga katika Kristo kuliko kuwa mjanja katika Elimu ya Ibilisi. ISAYA 35:8 “Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa,Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo”. Wanaopita njia hii ni WATEULE tu na si WAJUAJI. BWANA YESU KRISTO NDIYE ELIMU YA KWELI, UHAKIKA na Ya UZIMA WA MILELE nyingne ni KIINI MACHO TU.

 6. Kwako Ndugu
  Wewe ndugu mbona Luka mwandishi wa INJILI YA LUKA…….alikuwa msomi wa elimu wewe unayoiita kiini macho….fuatilia alikuwa ni daktari(TABIBU) wa wanadamu na vilevile mwanahistoria….wakolosai 4:14..”14 Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu”
  ma mara nyingi sana mtume paulo alipopigwa kutokana na kueneza injili alitibiwa na luka ambayo wewe mara nyingi sana comment zako zimeisema vibaya sana…..ndio maana hata ndugu sungura kanyamaza sasa hivi……..katika ukristo ndugu yangu kuna umwanana (calm, tranquil.) (2 timotheo 2:24) huwa hakuna fanatic (mtu ashikiliaye sana jambo bila akili)….ni hatari sana wakristo wenye misimamo au aina kama yako sababu anakuwa hana tofauti na wale jamaa wa upande wa pili (wa ishmael)….kama ukisoma historia ya Tanzania bara na visiwani baada ya ukristo kukataliwa kule zanzibar ndipo wamishenari walihamia bara wakafikia kwa wingi maeneo ya kaskazini mwa tanzania ndio maana kuna shule nyingi sana kanda za kaskazini hapa Tanzania na leo hii uwezi fananisha Elimu ambao wanazo sisi wa Isaka na wao wa ishmael ni tofauti kabisa na kile walichokikataa wao leo hii kinawatoa kwao na kuvuka mipaka kuingia bara kuitafuta……Hosea 4:6…”Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; KWA KUWA WEWE UMEYAKATAA MAARIFA, MIMI NAMI NITAKUKATAA WEWE………(Maarifa ni elimu au ujuzi aupatao mtu kwa kusoma au kutenda )……..sasa kifupi ukikataa KWELI hapo utadumkia kwenye UROHKOREE ambao ni tofauti na ULOKOLE…sifa za UROHKOREE ndio moja wapo kanisa liloibuka kule kigoma wazazi wakaambiwa waawachishe watoto shule eti ni elimu kiini macho…na bado kutaka kwenda kuhubiria injili Ulaya na asia kwa kupanda ndege bila VISA wala nauli….Kukataza wafuasi wao wasitumie madawa ya Hospitali matokeo wengi wanapoteza maisha……kuna mwingine alikunywa sumu mbele za watu akisema hata mkila kitu cha kufish akitawadhuru ameshazikwa tiyari……na majuzi kuna mmoja kafa maji huko Nigeria alitaka kutembea juu ya maji…….Maombi yangu kwa mungu wa israel akufungue leo utoke kwenye mtego huo

 7. mm naamini elimu iliyokuwa inazungumziwa hapa ni kwa ujumla elimu ya rohoni na hii ya kawaida ya mwilini kwasababu hata elimu ya ulimwengu wa mwili ni ya muhimu pia kwaisha ya mwanadamu .leo ususani katika nchi zetu za kiafrika tunashuhudia ongezeko kubwa la uovu kama vile wizi, ujambazi, uchangudoa iyo yote sababu kubwa ni watu kukosa elimu ya.kimwili na kiroho mm nadhani sis waafrika tungepata elimu yakutosha jinsi ya kutumia rasilimali zetu vizuri mimi naamni ingesaidia kupunguza watu kupiga madili haramu

 8. Ni elimu ya neno la MUNGU liwezalo kumpa mtu maarifa namna ya kuishi akimpendeza Mungu.

 9. Kwa watu wenye hekima ya kutosha jambo hili si la kukurupuka na kusema chochote.

  Ukitaka kujua hii inayoongelewa hapa ni elimu ipi, soma sura nzima.

  Ila nidokeze kuwa suala la falsafa ktk dunia hii leo hata halina nguvu kama ilovyokuwa wakati wa utawala wa Kiyunani, nfio maana biblia inasema wayahudi wanataka ishara na wayunani wanataka hekima.

  Kwa hiyo Falsafa na wanafalsafa wamekuwepo tangu zamani lakini hawajawahi kuwa juu ya hekima ya kristo!

  Take care!

 10. Ubarikiwe Kwa mada NZURI.
  HAKIKA UMEGUSA MOYO WA MAFANIKIO & UMAARUFU KWA WASOMI WA KIZAZI HIKI CHENYE UKAIDI.
  “Mithali 4:13 Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.”
  Mstari huu umetafsriwa vibaya,na leo MADHEHEBU mengi yameanzisha Shule Hospitali,Vyuo vya Biblia na Vyuo Vikuu na hata BAADHI ya MADHEHEBU huweka MSTARI HUU kama TANGAZO LA BIASHARA ZAO ZA TUMBO. HUU NI UJANJA WA ibilisi.
  Katika kuzungumzia mada hii kwa Kutumia tafsiri hii ya Kiswahili kama ilivyotumika ,hebu tuangalie ELIMU hii inayozungumziwa ni ipi.
  Sentensi hii kama inavyojieleza “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.” haina UHUSIANO na kitu (Elimu ya kwaida-FIZIKIA,BIOLOJIA NA HISABATI) BALI Sentensi hii humzungumzia MUNGU .
  MANENO “Mkamate,yeye & Usimwache” hayahusiani au hayana upatanisho na kitu (yaani elimu ya kawaida kama Biolojia,Hisabati,nk).MANENO, “mkamate,yeye, &usimwache yana uhusiano na MUNGU (YESU KRISTO)
  ” UZIMA” kama ilivyotumika hapa ni BWANA YESU. YOHANA MTAKATIFU 14;6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi .”
  UZIMA wote UNATOKA KWA BWANA YESU KRISTO. YOHANA MTAKATIFU 1:1-3 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.”
  ELIMU hii ya darasani ni mbinu ya kutafuta kazi TU iliyoletwa na WAZUNGU.
  MUNGU hapo mwanzo alimpa mwanadamu KAZI MBILI TU (KULIMA na KUFUGA)
  ELIMU hii ya Kwenda SHULE au CHUO ni KUTIMIZWA kwa UNABII WA DANIELI 12:4 “4 Lakini wewe, Ee Danielii, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.”
  BWANA YESU NDIYE MWANZILISHI WA UZIMA NA UZIMA WA MILELE.
  SHETANI NDIYE MWANZILISHI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA (SAYANSI USTAARABU na MAUTI)
  KAMA ELIMU YA FIZIKIA,BIOLOJIA,FALSAFA, nk, NI UZIMA mbona WASOMI Wengi wakiwemo WACHUNGAJI,MAPROFESA,MADAKTARI HUKANA NENO LA MUNGU?
  WASOMI NDIO WANAOONGOZA Kwa Kusema HAKUNA MUNGU,UPONYAJI WA KIUNGU,UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU,..
  ELIMU YA BIOLOJIA,THEOLOJIA HISTORIA,HISABATI,UHANDISI,BIASHARA HAINA UZIMA BALI NI KIINI MACHO TU.
  MITHALI 1:7 “Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.”

 11. Pro 4:13

  HOLD ON TO INSTRUCTION, DO NOT LET IT GO:

  GUARD IT WELL, FOR IT IS YOUR LIFE: ” ‘Grab the lifeline, and don’t let go! You can make it! You can live!’ If you were drowning at sea, would you obey these words from a sailor in a rescue boat? You would, for the consequences of not obeying would be certain death. You would, for holding a line is a very cheap price to pay, and easy effort to make, to save your life.

  “You may never face drowning at sea; but you will face drowning in the sea of life, when the storms of a sinful world come against you. Only by keeping instruction will you be able to survive the storm. The Lord instructs us by parents, pastors, and His Word. Have you grabbed hold of this teaching to save your life (Pro 3:18,22; Ecc 7:12; Deu 32:45-47)?

  “Our proverb teaches us how to listen to instruction. We must grasp with understanding what we hear and not let it slip away. The instruction of wisdom is what will save us from the perplexities and dangers of life. We must hold it tight and not let it go. We must retain what we learn. Don’t sell it for any price (Pro 23:23)!

  “Jesus described good hearers as those who took His sayings and built their lives on them (Mat 7:24-27). He told of two men, one who built his house on the sand, one who built his house on a rock. The storms of life destroyed the house built on sand, but the one built on a rock easily withstood the storm” (LGBT).

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s