Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini katika Yohana 10:9?

mlango

 

Unayaelewaje maneno haya ya Yesu katika Yohana 10:9 ?

 

Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.

 

Anaposema ‘ataingia na kutoka‘ maana yake ni nini?

 

Advertisements

7 thoughts on “Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini katika Yohana 10:9?

 1. Hii ni kauli iliyo katika rejesta ya ufugaji.

  Kwa hiyo mtu ambaye amewahi kuwa mfugaji wa asili anaweza akaelewa kiurahisi zaidi suala la kuingia na kutoka.

  Na ieleweke kuwa Yesu hakuwa anaongelea suala la kurudi nyuma na kurejea kwake tena.

  Yeye ni mlango, kwa kuwa kuna suala la malisho, inamaana panapotokwa ni zizini.

  Mifugo hutoka zizini kwenda kupata malisho na kisha hurudi tena zizini.

  Kwa hiyo huo mfano umetumia maneno kutoka na kuingia kwa sababu rejesta yake ni ya kifugaji, na ili mantiki ya ufugaji ikamilike lazima suala kwenda kupata malisho na kurudi tena zizini limetumika.

  Lakini zizi na malisho vyote viko ndani ya himaya ya mtu mmoja, ispokuwa kuna section ambazo lazima tu ziwepo ili circle ya ufugaji wa asili ukamilike.

  Kwa hiyo Yesu ndiye zizi, ndiye mlango, na ndiye malisho!
  Alisemea mlango zaidi kwa kuwa ndio unaounganisha zizi na malisho; kuwa ili kondoo atoke zizini kwenda maslishoni lazima apite mlangoni, ili kondoo arudi zizini toka malishoni lazima apite mlangono.

  Amen

 2. Asanteni kwa Michango yenu mizuri, imeufunua sana ufahamu wangu!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 3. amen wapendwa habarini,
  mlango ni nini? wanalugha ya kiswahili kupitia kamusi wanaelezea mlango kuwani 1. uwazi au nafasi maalum iliyoko ili kuingilia na kutokea penye uwazi zaidi, 2. kizuizi kilichotengenezwa kwa ubao, chuma au kitu kingine chochote ili kuziba uwazi wa kuingilia na kutokea kwenye ukuta au kiambaza cha jengo, chumba au gari, 3 ni kikundi cha watu wanaotokana na nasaba moja (ukoo, uzawa) 4. ni sehemu iliyogawanywa katika kitabu (sura). kuingia na kutoka ni tendo ambalo MTU anafanya kwa wakati mmoja, ninapoingia ndani maana yake nakuja ndani kutokea nje, mlango unatenganisha ndani na nje sasa Yesu ndiye anayetenganiaha kati ya nuru na Giza, Yesu alimaanisha kwamba MTU anapooka maana yake anaingia uzimani, nuruni, rahani, mbinguni na wakati huohuo anatoka mautini, gizani, shidani, kuzimu, kupitia mlango Yesu. MTU anapookoka kupitia mlango Yesu anatoka kwenye ukoo wa shetani ibilisi na kuingia ukoo wa Mungu kupitia mlango Yesu, unapookoka kwa kuwa Yesu ni kizuizi basi atazuia vya kuzimu visikuguse na ataruhusu vya mbinguni vikutumikie, akisema ndiyo hakuna wa kusema hapana na akisema hapana hakuna wa kusema ndiyo yaani akishazuia hakuna wa kuruhusu. Yesu ni mlango yaani mzaliwa wa kwanza wa ukoo wa Mungu wetu na sisi tupo kwenye orodha ya ukoo wa Mungu.

 4. Yesu alipokuwa anasema “ataingia na kutoka alikuwa anamaanisha uhuru ambao mtu anaupata anapokuja kwake. ukitafakari huo msatari unaweza kujifunza mengi sana. sometime tunapita ktk wakati mgumu ktk maisha haya tunayoishi na inafikia mahali kila unalifanya halifanikiwi na inakuwa ni kama milango yote imejifunga kabisa na huoni pa kupitia na ndo maana Mungu ameweka neno lake na kama ni msomaji mzuri wa neno mojawapo ya majibu ya magumu unayopitia ni huu mstari ambao pale ambapo milango yote imejifunga na huoni pa kutokea Yesu anasema mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. kwa hiyo Yesu ni mlango wa kutokea kwenye magumu tunayopitia lakini vilevile ni mlango wa kuuingia kupokea majibu ya magumu tunayopitia na hii ndo sababu anasema, ‘ataingia na kutoka‘ akimaanisha uhuru ambao mtu anaupata kupitia yeye ambaye ni MLANGO!

 5. Umeivuta hisia yangu kwa kweli,acha nibaki kimya nijifunze kutoka kwa walimu wa kundi hili.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s