Makundi ndani ya Watu waliookoka

 

msalabaniMtu akimpokea Yesu huingia kwenye familia ya watu waliookoka, watu waliosafishwa kwa damu ya Yesu Kristo. Anakuwa mwanachama wa Kanisa la Mungu lililo hai. Anaanza kuishi kwa kufuata mafundisho ya Bwana Yesu Kristo. Anakuwa Mkristo!

Lakini kadri watu wanavyoendelea kuokoka kutoka katika dini na madhehebu mbali mbali kunajitokeza makundi ya watu hao. Wale wanaookoka toka katika dini fulani hutengeneza kikundi chao cha waliookoka toka dini hiyo. Huwa na kanuni na taratibu zao ambazo zinawafunga au zinatofautiana na wale wa kutoka dini au dhehebu fulani.  Na pengine huendelea kutekeleza baadhi ya maagizo ya dini/madhehebu walikotokea hata kama mambo hayo yanaweza kuwa yana mgongano wa kimaslahi na Imani ya Kikristo!

Je, huku kuokoka halafu mtu akawa anajiita kwa jina la dini au dhehebu aliyotoka mfano Muislamu aliyeokoka, Mkatoliki aliyeokoka au Mpentekoste aliyeokoka inaashiria nini hasa? Kwa nini tu mtu asiseme Mimi nimeokoka? Huo utambulisho wa dhehebu/dini una umuhimu gani kwenye Wokovu?

Maoni yako tafadhali!

Advertisements

39 thoughts on “Makundi ndani ya Watu waliookoka

 1. Frankly speaking!!! There is nothing like religious in the Bible. These are from humans perceptions so that they can abide to what that at least is seems to be right in accordance to what that is in the Bible. Sasa sioni maana ya kulaumu au kuhukumu au kunyooshea kidole kundi fulani la imani. Hakuna kikundi chochote cha waamin ambacho hakiitwi dini na ndani yake lazma Kuna vitu wamevishikilia kama kanuni ya imani Yao.

 2. Bwana yesu asifiwe wote kwanza mimi niseme wanaotaja udhehebu wako sawa hata nyie mnaopinga mimi sielewi mnasimamia wapi au mnasema tu kujifulahisha kweli nimechelewa kuchangia sasa nianze kusema hivi
  kazi ya Yesu alikuja kutafuta na kuokoa wote ambao wamepotea katika dhambi sasa kubwa hapa ni hili ulipotea katika dhambi,au umepotea katika dhambi ni kugeuka na kumpa Yesu maisha yako
  Yesu aliacha kazi kwa mitume kuwa waende ulimwenguni mwote wakawafanye mataifa yote,watu wote, wakawafanye kuwa wanafunzi wa Yesu (mathayo 28:-19) na hapa naomba nieleze machache ili nijenge hoja kwanza sharti ujue ujue wakati Yesu anakuja zilikuwepo dini kama dini za kiyahudi
  sasa mtu anaposema nimeokoka niko romani,PAG,EAGT,Anglikani,lutherani nk unajua kuna madhebu yanajitaja ni ya kristo lakini ukweli wa mambo yanamkataa yesu ndio maana watu wote ni wakristo kama mlivyonukuu katika matendo ya mitume mko sawa leo utakuta mtu anajiita ni mkristo yeye ni mzinzi,mlevi,mvuta sigara,ana mke zaidi ya mmoja,fisadi,mchawi,na wengine kwa ajili ya kutetea dhambi wanathubutu kusema huwezi kuokoka ukiwa duniani hata hawaju neno lolote kwani ukisema wewe ni mkiristo uwe kama Yesu alivyo kuwa yeye alipigwa,alitukanwa,alitemewa mate,pamaoja na maudhi mengi bado biblia inasema hakutenda dhambi yoyote aliendelea kumpendeza Mungu na wanadamu
  sasa kuna madhehebu ambayo kweli yenyewe ni nuru ya ulimwengu kama kanisa la kakobe huwezi kuwakosoa kwa lolote wanaishi sawa na neno la Mungu linavyo sema.ndio maana watu wanajitambulisha kwa madhebu ili ukiwafatilia uweze kuelewa wameokoka au hawajaokoaka kwani nyakati za leo kila mkristo asema Bwana asifiwe hata kama ni mtenda dhambi wakati biblia inasema kila alitajaye jiana la Bwana na aache uovu
  kwa leo niishie hapo nasubili mchango wako wewe unayebisha bila maana
  balikiwa

 3. Wapendwa;
  SHALOM.
  YEREMIA
  2:13 ” Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha
  mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika,
  mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.”
  MADHEHEBU YOTE wamemfanyia BWANA YESU makosa MAWILI.
  1.KOSA LA KWANZA; Madhehebu WAMEMUACHA Yeye ( BWANA YESU), aliye CHEMCHEMI ya MAJI ya UZIMA.
  -Madhehebuni hakuna NENO LA UZIMA bali kuna MAPOKEO,MAFUNDISHO YA SHARTI na KANUNI ZA IMANI.
  2.KOSA LA PILI ; MADHEHEBU wamejichimbia Mabirika (wanajiita,
  TAG,ANGLLIKANA,EAGT,LUTHRAN,HOLINESS,KLPT,KATOLIKI,….nk.
  Unaweza Kuthibitisha kwa kumuuliza mmoja “wewe ni Mkristo?” utasikia
  “Mimi ni MKATOLIKI, MUANGLIKAN,MPENTEKOSTE, M-TAG, M-EAGT, M-BAPTISTI,
  ……nk.”
  -Mabirika yenyewe yanavuja na hayaweki maji (MAFUNDISHO YANAYOFUNDISHWA
  ni ya MASHETANI, 1TMOTHEO 4:1-5 ” Basi Roho anena waziwazi ya kwamba
  nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho
  zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;
  kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
  wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo
  Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua
  hiyo kweli.
  Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa,
  kama kikipokewa kwa shukrani;
  kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.”
  MAFUNDISHO MENGINE YA MASHETANI yanayofundishwa MADHEHEBUNI ni Mungu ana NAFSI TATU, UBATIZO WA WATOTO,KUBATIZA KWA VYEO VYA MUNGU ( BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU),WANAWAKE WANAPEWA KUWA
  WACHUNGAJI,WAINJILISTI,MASHEMASI,…..nk”
  MATENDO 11:25-26 ” Kisha akatoka akaenda Tarso kumtafuta Sauli;
  hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka
  mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na
  wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.”
  Mtu yeyote anayemuamini YESU huitwa MKRISTO si M-TAG,M-EAGT,MPENTEKOSTE,MWANGILIKANA,WALA MKATOLIKI hayo ni MAJINA YA MAKUFURU.
  **** NA WANAFUNZI WALIITWA WAKRISTO KWANZA HAPO ANTIOKIA****

 4. HAKUNA NENO LILILOSITIRIKA AMBALO HALITAFUNULIWA WALA
  LILILOFICHWA AMBALO HALITAJULIKANA!!!(LUKA 12:2)

  Huu ni unabii wa Yesu mwenyewe ambao umeshatimia na unaendelea
  kutimia.Utimilifu wa unabii huu unaleta AFYA YA KIUNGU kwa wateule
  hasa wale wanaojitambua kiroho.Roho Mtakatifu naomba utufafanulie
  una maana gani kusema haya.

  Hii mada ni nyeti mno hasa katika nyakati hizi za mwisho.CK LWEMBE
  ametoa maelezo ya kina kwa sehemu na yanaleta nuru ya ajabu.Ukiya
  soma kwa utulivu unaweza ukaiona tofauti kati ya kanisa na madhehebu.Kupitia blog hii, nilipata neema ya kusoma mafundisho
  ya Mwalimu Mwakasege yanayohusu tofauti kati ya KANISA na DHEHEBU.Roho Mtakatifu alimuongoza Mwakasege kueleza KWA KINA
  TENA KWA UNDANI SANA kuhusu makundi ya watu walio ndani na nje
  ya WOKOVU.Maelezo hayo yanapatikana katika mada inayosema
  KWANINI BWANA YESU ALITUOMBEA UMOJA.Wewe mwenye nia njema
  itafute ili UWE HURU KWELI KWELI.Ni mafundisho ya Roho Mtakatifu
  ndani ya Mwakasege na siyo mafundisho ya Mwakasege!Huwezi kuyatambua mafundisho ya Roho Mtakatifu kama huongozwi na Roho
  Mtakatifu.Unaweza ukawa umeokoka lakini hujampa Roho Mtakatifu
  nafasi ya kukuongoza katika mambo yote(Soma 1YOHANA 2:20,27).

  KANISA ni mwili wa Kristo.Mwili wa kristo ni watu wanaoongozwa na Roho Mtakatifu kwa kuwa walizaliwa mara ya pili kwa uweza wa Roho
  wa Kristo.DHEHEBU ni watu au kusanyiko la watu ambao hawajazaliwa
  mara ya pili na kimsingi wanaongozwa na mapokeo ya wanadamu.Katika
  MATHAYO 15:3-9, Yesu anazungumza wazi kuhusu MADHEHEBU ya kwamba ni UNAFIKI wa kufuata MAFUNDISHO na MAAGIZO ya
  wanadamu.WARUMI 8:12-17 inaelea maana halisi ya KANISA kuwa ni
  mikusanyiko ya wana wa Mungu wale ambao HAWAONGOZWI NA
  ROHO YA UTUMWA ILETAYO HOFU.Kuna madhehebu ya wanadamu
  na madhehebu ya shetani(1 TIMOTHEO 4:1) ambayo kimsingi yote
  chimbuko lake ni shetani,kwa sababu yote yanafanya UNAFIKI kwa kupotosha MAFUNDISHO na MAAGIZO ya Mungu aliye hai.

  Ni muhimu sana tukatambua kwamba ndani ya MADHEHEBU wapo
  wana wa Mungu na wana wa Ibilisi.Na pia ndani ya KANISA kuna wana
  wa ibilisi ambao wamejiingiza kwa siri.Hata katika hii blog wapo
  mbwamwitu ambao wanachangia mada mbalimbali sambamba na wana
  wa Mungu na kila mmoja analinda maslahi ya ufalme wake.Wateule
  ni LAZIMA wafike mahali pa kuyatambua mambo haya na kuwabaini
  WAPOTOSHAJI.Nisikilize kwa makini hapa,Roho Mtakatifu anapigilia
  misumali ya moto ulao.SI KILA ANAYEPOTOSHA NI MBWAMWITU
  WENGINE NI WATEULE WASIOJITAMBUA KIROHO LAKINI KWA MUONGOZO WA ROHO WA KRISTO TUNAYATAMBUA MAFUNDISHO
  YANAYOPOTOSHWA PAMOJA NA UHALISIA WA WALE WANAYOYAPOTOSHA.Si lazima nionane na Lwembe uso kwa uso
  ili kujua anafananaje au kuujua uhalisia wake wa kiroho.Roho Mtakatifu
  anaweza kunionyesha uhalisia wa Sungura katika ULIMWENGU WA ROHO.Kama unadhani natania katafakari kile ambacho Mtume Paulo
  anasema katika WAKOLOSAI 2:5.Unaweza kumtambua mtu na mafundisho yake kwa kumchungulia katika ulimwengu wa roho.USIPOTEZE MUDA WAKO KUBISHANA NA KUSHINDANA NA MTU.
  Katika MADA HII NENO LA MUNGU LIMEWAACHA UCHI WALE WOTE
  WANAOPINGANA NA MAFUNDISHO YA ROHO MTAKATIFU.Soma WAEBRANIA 4:12-13 UONE JINSI NENO LA MUNGU LINAVYOWEZA
  KUTOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA MASHETANI NA YA ROHO
  MTAKATIFU.

  Mtumishi Pandaeli utakuwa umeelewa sana kile ambacho ROHO WA
  KRISTO anadhibitisha.Watumishi JOHN PAUL,SUNGURA NA ASHERI
  ENDELEENI KULETA CHANGAMOTO.KUSUDI LA MUNGU NI LAZIMA
  LITIMIE HAIJALISHI ANAYELITIMIZA NI MWANA WA MCHANA AU USIKU.Ninawaomba wateule mfatilie hii mada kwa KUMSHIKA MKONO
  ROHO MTAKATIFU.MTAONA MAMBO MAKUBWA NA MAGUMU AMBAYO HAMKUYAJUA KUHUSU KANISA NA MADHEHEBU.Yesu alikuja
  kuvunja madhehebu na kuanzisha KANISA LAKE.HATA LEO KUNA MADHEHEBU MENGI SANA YA MAFARISAYO NA MASADUKAYO.

  Ni lazima tutofautishe kati ya JINA LINALOBEBA MAONO YA KANISA(kusanyiko la wana wa Mungu) fulani na DHEHEBU fulani.Roho Mtakatifu ataendelea kuwaelewesha wateule wake.KWA HABARI
  YA MAFUNDISHO POTOFU, VITA KATI YA WANA WA MUNGU NA IBILISI
  INAENDELEA KUWA TAMU ZAIDI.MWAKA 2015 WATEULE WENGI ZAIDI
  WATAENDELEA KUJITAMBUA NA KUONDOKA KATIKA MADHEHEBU
  YA MASHETANI.KWA SABABU YA UTANDAWAZI WA MAFUNDISHO
  YALIYO KUFA NDIYO MAANA KUNA MAKANISA YA KRISTO AMBAYO
  YAMEGEUZWA KUWA MADHEHEBU!!

  KARIBUNI WAPOTOSHAJI NA WENYE NIA NJEMA ILI ROHO
  MTAKATIFU AMALIZE KABISA HII BIASHARA.

 5. asanten kwa wote mliochangia kwan

  baadh ya michango yenu imenibariki sana.

 6. Siyi,

  Hahahaha..!!!
  Swali uliloniuliza kwamba, “Je, kanisa la Kristo nalo lipo????” ni swali la zamani saaana!! Elia aliwahi kuwa na swali kama lako kichwani mwake, ndipo akamwambia Mungu kuwa amebaki peke yake, yaani Kanisa lote limekengeuka, limejiingiza ktk ibada ya miungu, kama ilivyo leo hii, yule mungu wa kale, Baali, amejibadilisha jina, sasa hivi anajiita UTATU MTAKATIFU!!!

  Bali Mungu alimhakikishia kwamba anao watu 7,000 ambao hawajampigia magoti Baali, 1 Ki 19:18 “Yet I have left me seven thousand in Israel, all the knees which have not bowed unto Baal, and every mouth which hath not kissed him.”!

  Ndio hivyo, Kanisa lipo, hilo ambalo halijajichafua na wanawake, Ufu 14:4-5 “Hawa ndio wasiotiwa unajisi pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo. 5Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.”

  Na wengine hawa hapa, Efe 1:3-5:
  “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.”

  Gbu!

 7. …….. inaendelea:

  Tunafahamu kwamba duniani kuna roho mbili tu zinazofanya kazi, kuna Roho ya Kristo, ambayo ndiyo Kichwa cha Kanisa, huo Mwili wake; na kuna roho ya Mpinga Kristo, hiyo inayojiwakilisha kama Roho ya Kristo, ndiyo hiyo roho ya Ibilisi itendeyo kazi ndani ya wana wa uasi, ambayo tunafunuliwa hapo kwamba inajitambulisha kama Wayahudi, bali ni sinagogi la Shetani, ndilo hilo “kanisa” laghai, kwa maneno mengine!

  Kimsingi tumekuwa na miaka 2000 ya Teolojia, yaani miaka ya kuitafsiri Injili, ile interpretation. Matokeo ya miaka hiyo, yanapimika katika tafsiri za Maandiko zinazojiwakilisha ktk idadi ya madhehebu yetu kiasi kwamba kwa mtu mwenye kujiuliza kuhusu hali hiyo, ni lazima abaki na maswali mengi sana kichwani yasiyo na majibu.

  Ukirudi ktk Maandiko unaweza kuuona mzizi wa jambo hili, Maandiko yanasema ni FITINA; 1Kor 1:11-12 ” … ya kwamba iko fitina kwenu. Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu kusema, Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?” Hebu jaribuni kulipima jambo hili na madai yetu ya leo, kwamba mimi ni Mlutheri, au ni Muanglikana au ni mTAG au ni Mkatoliki nk, Leo Paulo akituuliza maswali hayo aliyowauliza Wakorintho, binafsi ningependa niyasikie majibu yake kutoka kwenu wapendwa! Kama jambo hilo Roho alilikemea ktk siku hizo, sioni ni kwa vipi atalikubali leo hii!

  Kuwa kwetu Wakristo si jambo la “lele mama”, ni wito unaoambatana na jinsi ya mwenendo ili kulitimiza kusudi la wito wetu, Efe 4:1-6
  “Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.”

  Jamani, Roho ANATUSIHI! Tunapaswa kuuhifadhi umoja wa Roho, tukiwa sote tu chini ya huyo Roho, huyo ndiye anayeweza kutufikisha ktk kuwa Mwili mmoja maana ni Roho mmoja. nayo imani itakuwa ni moja inayoambatana na Tumaini moja kutoka kwa huyo Roho!

  Labda ili kuliweka ktk kueleweka vizuri, tumatazame huyo “Roho” anaye tuongoza ili tuuone mfano ulio hai kuhusu jambo hili: Tuchukulie Dhehebu la Katoliki. Ibada inayoendeshwa ktk kanisa la dhehebu hilo lililoko Songea, itakuwa iko sawa sawa na ibada inayoendeshwa huko London au Beijing au ktk vijiji vya Brazil au Vatican na sehemu yoyote nyingine duniani, tofauti itakuwa ni lugha tu, lakini content ya Ibada ni moja, kwa sababu wanaongozwa na roho mmoja nao ni mwili mmoja, na Tumaini lao ni moja na imani yao ni moja nk! Vivyo TAG, EAGT, SDA, Lutheran nk kila kundi likiwa ni tofauti na jingine hivyo roho pia zikiwa ni tofauti, lakini zote zikiwa zimejizalisha kutoka ktk Injili hiyo hiyo, na wote wakidai kwamba Roho Mtakatifu ndiye anaye waongoza, ndiye mwenye kuwapa mafundisho yooote waliyonayo; mpaka fundisho la kwamba Ishara na Miujiza vilikwisha na mitume!!!

  Ngoja nikomee hapa kwanza, kisha nitamalizia wazo nililonalo kuhusu haya makundi ya waliookoka kutoka ktk mauti za kidhehebu, halafu mwendo kidogo wanarudi tena humo kujitambulisha na kifo, tuone wamepatwa na nini??!!!

  Gbu all!

 8. Wapendwa,

  Kuna wakati fulani katika majadiliano, ilionekana kana kwamba tuko ktk mitazamo tofauti, lakini mwenzangu alipoyaangalia kwa kina tunayoyazungumzia akaniambia, “May be we have the same perspective but we miss how to describe and come to common ground”, huyo alikuwa ni Eucalyptos; ni kweli, wakati mwingine shida inakuwa ndio hiyo!

  Katika majadiliano haya, yamejitokeza mambo mengi kama ambavyo mijadala inavyoweza kuzalisha mikondo mingi, lakini yote huwa ni kutoka ktk ile Tie Post moja, Yesu Kristo, yaani lile Neno!

  Mshangao alionao mleta mada ni halisi sana tena una changamoto ya Uzima kwa wote ambao mioyo yao huridhika na mambo yaliyo halisi, kama ni Kweli ya Mungu, basi kiu yao iko ktk hilo na si ule wepesi wa ku compromise hiyo Kweli na kubakia umelishikilia jambo ambalo unajua kabisa kwamba si Halisi, bali unaendelea nalo ukijidanganya kwamba ni halisi!

  Mleta mada anazungumzia ukweli wa maisha anaouona kuhusu makundi yetu ya Kikristo. Anasema “Mtu akimpokea Yesu huingia kwenye familia ya watu waliookoka, watu waliosafishwa kwa damu ya Yesu Kristo.” Kwa kadiri ya jambo la Wokovu, huo unaoletwa kwa Injili, binafsi ninaamini kwamba kauli yake hii ni sahihi kwa asilimia 100; Mk 16:15-16 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Nao udhihirisho wa jambo hili ndio huu hapa, Mdo 2:40-41 “Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.”

  Sasa kundi hilo la watu 3000 waliookoka siku hiyo, ni hao waliotoka ktk dini, huo Ufarisayo na Usadukayo na Waandishi nk, yale madhehebu ya wakati huo, hayo yaliyojizalisha kutoka ktk Torati. Kundi kubwa zaidi lilibaki ktk madhehebu yao, wakaendelea na taratibu zao za ibada, wakikataa KUMPOKEA Kristo, yaani kulingana na hicho kifungu cha Marko 16:16, ni kwamba wote wameingia ktk Hukumu, na hivyo hawawezi kuwa sehemu ya Mwili wa Kristo!!!!

  Kwa kadiri ya hali hiyo iliyokuwapo ktk siku hizo, tunaweza kusema ndicho kinachojirudia leo hii tena. Tazama anachokisema mleta mada, “Lakini kadri watu wanavyoendelea kuokoka kutoka katika dini na madhehebu mbali mbali…” Basi, iwapo kuna watu wanaookolewa kutoka ktk madhehebu yetu ya Kikristo, hili ndilo linaloashiria kwamba huko wanakookolewa hakuko salama, maana tunaokolewa kutoka ktk Hukumu ya Jehanamu! Ndio kusema kwamba hayo madhebu ambamo watu wanaokolewa, licha ya kwamba yanadai kwamba wao ni Kanisa, yaani ule Mwili wa Kristo, kwa jambo hilo la watu kuokolewa kutoka humo, hilo laonesha kwamba madhehebu hayo yanaelekea kuzimu! Maelezo yake ya ki Maandiko ndiyo hapa: Ufu 2:9 “… najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.”

  Nitaendelea…..

 9. shaloom……samahan si mahali pake Mtumishi wa mungu John Paul ni wewe pia unatumia jina John F paul ktk Vitabu kama Uponyaji wa Mti wa famila & weka ufahamu wako huru

 10. Pendael, wow bravo!

  Asante sana kwa maneno mazuri yaliyojaa neema na kukolea munyu yanayomfaa msikiaji.

  John Paul alikwambia kitu kimoja kuwa unaweza ukasema lolote kwa ujasiri kwa sababu tunajadili katika uwanja ambao hatuonani wala kusikiana kwa sauti zetu.

  Lakini as God lives kuna siku tutakutana na kuonana uso kwa uso, ndipo utajua Sungura huyu unaemwita mwana wa ibilisi ni nani hasa.

  Huwezi kunishawishi kuwa wewe unamfahamu Mungu sawasawa,huwezi kunishawishi kuwa anayeongea ndani yako kuniita mimi ni mwana wa ibilisi kuwa ni Roho mtakatifu, no way!

  Pamoja na hayo yote, hebu tuonyeshe sasa andiko lipi linasema kuwa dhehebu ni mwili wa ibilisi.

  Na hebu thibitisha kuwa wewe hauko chini ya dhehebu lolote. Maana najua ktk nchi hii huwezi kukusanyika mahali popote kwenye public bila kujulikana jina la hilo kusanyiko.

  Kuthibitisha kwako hayo uliyoyasema ndio kitu cha msingi kuliko kumwita Sungura kuwa ni mwana wa ibilisi.

  Na ashukuriwe Mungu kuwa damu iliyonikomboa si yako ila ya kwake mwenyewe. Huyo ndiye anayeujua uchungu wa kunipata mimi.

  Kwa naana hiyo, huyo ndiye atakayekuhold responsible kwa maneno yasiyo maana. Shetani hawezi kuwa na mtoto mzuri kama mimi rafiki.

  Pendael, nakuona kabisa kuwa wewe unachokiona ni kujua maandiko ni kule kuyanukuu kama ulivyonukuu
  Ufunuo 3:17 hapo juu na kuitumia kwa matakwa yako. Mtu yeyote anayejua neno la Mungu akiangalia jinsi unavyoyatumia hayo maandiko uliyonukuu atajua pasi na shaka kuwa uelewa wako wa neno uko so limited.

  Mara nyingi unaongea mambo mengi ambayo huna ujuzi nayo wa kutosha, lakini kwa sababu wewe unadhani unaowaandikia nao ujuzi wao ni kama wa kwako, basi unajiona u mwerevu kweli.

  Pole, mimi huwezi kunidanganya, ila kuniita nwana wa ibilisi hilo unaweza!

  Thibitisha niliyokuuliza inatosha!

  Thank u!

 11. Sungura. Nishakuambia ni Haki Ya Msingi KUNENA YALIYOUJAZA MOYO. Hayo ndiyo MATANGO MWITU ULIYOLISHWA NA IBILISI. Unadai kwamba Huwezi kudanganywa wakati tayari uko Kwa BABA WA UONGO UKITUMIKA KWA MOYO WOTE. Unaniambia ‘believe me’! How can I believe unbeliever like you?Mara nyingi nimesoma Michango yako ni UPOTOSHAJI TU wa MAANDIKO kwa kutumia ‘techniques’ za Ibilisi ikiwemo teminolojia za THEOLOJIA. Mtumikie Adui vizuri kwa sababu kuna Mshahara pia. UFUNUO 3:17 ” Kwa kuwa wasema, mimi ni tajiri,nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na uchi”.Umeshasema “akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa,huwezi kunifundisha….nk” nawe hujui kuwa u mnyonge(weak spiritual muscles) na mwenye mashaka (huna IMANI), maskini ( kiroho uko tupu),na kipofu (huoni chembe ya Neno la Mungu zaidi ya Kukariri mapokeo ya DHEHEBU lako na INJILI Chotara “Hybrid Gospel” ya Theolojia ) na Uchi (Neno la Mungu ni vazi kwaku Neno huna,uko uchi Mbele za Mungu). Kama unataka Mungu akusaidie hebu ZINGATIA HUU USHAURI ULIOPO KWENYE “UFUNUO 3:18-22”. **Mungu Na Ahirehemu Nafsi Yako Yenye DHAMBI**

 12. Pendael,

  Acha maneno rejareja, jibu hoja!

  Kunukuu maandiko siyo kuelewa maandiko.

  Wewe tuambie imeandikwa wapi kwamba dhehebu ni mwili wa ibilisi?

  Bila shaka wewe umezoea mijadala fulani ya kujadili na watu wenye reasoning ndogo, ndio maana unaongea vitu ambavyo havina substance, vinaelea.

  Ati bila aibu unasema uongo kuwa wewe huna dhehebu. Halafu unataka tusikwambie kuthibitisha hilo!

  Please, elewa kuwa unaongea na watu wenye ufaham, huvyo ongea vitu ambavyo vina ukweli usiotia shaka.

  Believe me, unaweza kuongea chochote lakini huwezi kunidanganya jambo linalohusu kweli ya kristo.

 13. Asheri. Haihitaji UFAFANUZI Kulifahamu jambo fulani isipokuwa Inategemea UNA NIA ipi.Ungekuwa na NIA ILIYOKUWA NDANI YA KRISTO na USINGEKUWA NA ROHO YA KUPINGA MAANDIKO Usingediriki Kusema MAANDIKO niyokupa HAYAHUSIANI na MADHEHEBU.Pia kumbuka Kuwa Kisicho na MAANA kwako kina MAANA kwa mwingine.Usipate Shida kuwa na DHEHEBU lako kwana Bwana Yesu anasema kwenye MATHAYO 19:11 ” Lakini yeye akawaambia, Si Wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.”

 14. Pendael,

  Ni kweli kuwa akili ndogo haiwezi tawala akili kubwa.
  Huwezi wewe kutawala akili yangu kwa issues kama hizi, maana unaongea vitu kwa kukurupuka tu rafiki.

  Sijakuuliza hayo maswali ili unifundishe ktk majibu yako, nimekuuliza ili uthibitishe ulichokisema.

  Kujaribu kuyasema kuwa ni ya kipuuzi ni kutafuta tu kichaka cha kujificha.

  Huwezi ukathibitishe kwenye maandiko kuwa dhehebu ni mwili wa ibilisi. Umeitumia hiyo term kutoka kwenye wazo la mwili wa kristo, kwa akili nyepesi tu ukadhani kuwa kuna na mwili wa ibilisi pia.

  Ona pia umeamua kusema uongo wa wazi kabisa kuwa wewe hauko kwenye dhehebu. Maneno kama hayo kawaambie mabaladhuli ndo pekee unaweza ukawa-fool!

  Jana kama ulisali ulikusanyika wapi, chumbani kwako?
  Lakini kama hukukusanyika chumbani kwako ila ulikusanyika haraiki baso kuanzia leo jua kuwa hilo ndio dhehebu lenyewe.

  Vipi kuhusu dini na yenyewe huna au unayo?

  Halafu ati unasema kuwa Yesu hakuanzisha dhehebu! Ulitaka aanzishe dhehebu kwani dhehebu linamhusu Mungu au watu?

  Kwani Yesu aliwahi kujenga jengo la kuabudia,lakini kwa nini leo sisi tunajenga majengo, kwa mfano?

  Pendael, umeniambia mimi ati nina kiburi cha uzima, ivi unaelewa maana ya kiburi cha uzima kweli?

  Kama mimi nina kiburi cha uzima sijui wewe una kiburi cha nini sasa, labda cha ujinga!
  Maana unadhani kunukuu maandiko ndio kujua maandiko, lakini kumbe kutokujua maana ya andiko ni zaidi ya ujinga, hata kama umekariri biblia nzima!

  Uko biased big time!

 15. Ndugu Pendael Simon
  Shalom,

  Ndugu yangu, mimi ningefurahi na ungekuwa umenisaidia kama ungenifafanulia hayo maandiko uliyoyaandika. Nilisema katika mchango wangu wa mwisho kuwa maandiko uliyoyaandika hayahusiani na dhehebu, ulichopaswa ni kuyafafanua ili mimi nisiye na ufahamu basi nifahamu. Cha kusikitisha unaniambia nataka mashindano yasiyo na tija! Mimi nilitaka kufahamu si kushindana. Tija kwangu ni kujua kile ambacho ndugu yangu unakijua ili kinisaidie.

  Naomba ufahamu kuwa mimi haijaniuma kwa kuwa umesema madhehebu ni mabaya/ makufuri, hilo kwangu si tatizo. Tatizo langu ni watu wanaosema vitu halafu wakiombwa kufafanua wanaruka ruka na kuwa wakali. Hapa ni mahali pa mjadala, ukisema kitu uwe na uwezo wa kukifafanua na kama ulikuwa hukijui vizuri basi wengine watakusaidia kwa maana kupitia majadiliano haya tunajifunza mambo mengi. Lakini pia lazima tukumbuke kuwa tunasomwa na watu wengi, tusipokuwa makini tunaweza kuwa sababu ya kupoteza wengine, ndiyo maana ni lazima tuwe wapole tunapoulizwa kile tulichokisema.

  Hivyo mpendwa Pendael Simon, narudia tena kusema kuwa ninaamini huna jibu ndiyo maana una ruka ruka badala ya kujibu hoja. Ushauri wangu kwako ni kama unaotushauri sisi, unahitaji kujifunza neno la Mungu na kujifunza si kunukuu tu maandiko, ni kuyaelewa hayo maandiko katika usahihi! Mungu akubariki!!!!

  Maran Atha!

 16. Bwana John Paul,
  Hivi, Kwa MAELEZO YAKO hayo uliyoyatoa NDIYO UKO CHINI? Hiyo ndiyo namna ya kushuka au una jambo lingine ZAIDI YA KUJIFUNZA?
  Kama Unatka nikujibu unavyotaka UNGENIULIZA ungenieleza na NAMNA YA KUKUJIBU.
  Ushupavu wa Dini, mashindano wa anayejua kuliko mwenzake na Mapokeo Ya Wazee Hayatusaidii kitu.
  HASIRA ya MWANADAMU haitendi Haki ya MUNGU.Ninajua unataka Nikutajie JINA kama LA KWAKO, nilishakuambia HAYO ni MAJINA ya MAKUFURU kulingana NA BIBLIA.
  Mimi ni MKRISTO tu na sina mojawapo ya Majina hayo ya kidhehebu.
  Nilishakuambia TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD ni DHEHEBU na wala si KANISA.
  Hayo MAJINA Ya KUJIITA ndiyo MAJINA YA MAKUFURU ( UFUNUO 17:3-5)
  KUKUJIBU naabudu KANISANI ndio kumekufanya UKASIRIKE?
  Wanafunzi WA YESU WALIKUTANIA KANISANI kule YERUSALEMU.
  FILEMONI 1:1 Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi,
  na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako.”
  SEHEMU nyingi kwenye BIBLIA zinasema kuhusu WAKRISTO na KANISANI (MATENDO 8:1 “Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.”)
  BIBLIA inasema katika UFUNUO 2-3: Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Na kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika; Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika;”
  Mbona Kinachozungumziwa hapa ni KANISA na si DHEHEBU?
  Hivyo kuna KANISA lililoko Dar es Salaam,Mtwara,.Arusha.Kigoma,Tabora,….n
  Unaweza Kuchagua KANISA au DHEHEBU Utambulishwe kwalo,
  LAKINI huwezi kuwa na KANISA na DHEHEBU kwa wakati mmoja.

 17. @ Pendael Simon

  Kunukuu Biblia siyo tatizo wala siyo sababu. Hilo lisikutie moyo. Nami Naweza sana tuu kunukuu maandiko lakini yasipoambatana na Upendo ni maneno tuu sawa na maneno mengine. Mbona hata wapagani wanatumia tuu maneno ya Biblia?

  Kama ungekuwa unayafahamu hayo maandiko ULIYOYANUKUU kama ninavyoyafahamu mimi USINGENIJIBU HIVYO kama vile unaongea na hayawani. Kwani mimi sijui wanapokutana wakristo panaitwa KANISANI? Hicho ni kiburi tuu ndugu. Au hukuona nilivyokuuliza kwa upendo na unyenyekevu? Unataka kusema kanisani kwako kunaitwa kanisani? Serious? No! Ni lazima kuna JINA la Kanisa Lako. Hakuna kanisa duniani linaloitwa tuu Kanisa! Tuache hiki kiburi hasa kwa kuwa hapa hatufahamiani live. Bora angalau ukiwa unamfahamu mtu live unaweza ukam-rate na hivyo ukamjibu unavyojisikia. Lakini hata kama mnafahamiana haifaikuleta mazoea binafsi hapa. Sasa hapa hatufahamiani. Tumekutana hapa kama wakristo ili tubadlishane ujuzi wa Neno la Mungu. Sasa mtu anapojiona yupo juu sana; kila mtu anamparamia tuu, siyo sawa. Ni lazima kunyenyekea. Kushuka chini. Yesu ainuke. Sisi tuwe chini. Hata kama mtu amekosea kuuliza unajibu kwa upendo siyo kwa KEJELI, japo swali langu liko wazi na sahihi kabisa.

  Kwa hiyo nasisitiza tena kuwa umejiinua sana na kufikiri kiiiiiiila kitu unakijua. Hapana! Kuna vingi tuu huvijui. Tena mimi kuna ninavyovijua zaidi yako na wewe kuna unavyovijua zaidi yangu kwa hiyo TUNAHITAJIANA kila mmoja kwa mwenzake.

  Neno la Mungu ndilo linatufundisha KUWATAMBUA WATU KWA MATUNDA YAO. Kile ulichojibu swali langu la msingi pale juu ndicho kimesababisha niku-rate kutokana na Neno. Bible inasema HATA MPUMBAVU AKIKAA KIMYA HUONEKANA MWENYE BUSARA. Kwa sababu ya Neno nimekuona unakiburi. Umejiinua saaana. Na hapa siyo NAKUHUKUMU bali nakuelezea ulivyo. Mungu ndiyo mwenye KUHUKUMU.
  Ni Neno linatufundisha KUWAIGA WALE WALIOTUTANGULIA katika imani, kwa kutazama mwenendo wao. Utamuigaje mtu bila KUMFAHAMU? Mtume Paulo aliandika NIFUATENI MMI KAMA NINAVYOMFUATA KRISTO. Utamfuataje bila kumfahamu NI MTU WA NAMNA GANI? Sasa kuna ubaya gani mm nikikufahamu kuwa wewe ni mtu wa namna gani na hasa kwa jinsi UNAVYOTOA KILE KILICHOUJAZA MOYO WAKO?

  Nashukuru lakini kwa majibu yako ambayo yananifundisha kitu kingine kuwa dhehebu lako ni tofauti na la kwangu. Wewe umekataa kutaja dhehebu lako kwa kufikiri kuwa dhehebu lina tatizo. Tatizo siyo dhehebuu bali ni watu. Mimi nimekutajia la kwangu na ambalo HALINIZUWII KUMTAFUTA MUNGU KWA KADRI NIWEZAVYO. Sasa wewe endelea kuficha la kwako!

  Nakusihi tu kwamba shuka chini brother. Tuongee kwa upole, upendo na katika hali ya kumuinua Yesu na siyo vichwa vyetu hivi ati mtu labda ana kadigree ka Theology au sijuwi Professor au gari au nyumba 20 mjini au whatever. Hayo yote si kitu tunapokuwa tumepata fursa ya kujifunza maneno ya Mungu!

  Si unaona unavyoendelea kuandika “Pia sijafunga MILANGO kama ulivyodai na hata ningetaka nisikujibu ningekuwa mwungana kukuambia.na sababu ya kutojibu.”

  Haya! Wewe endelea kuwa juu lakini mimi niko chiiiini kabisa. Nimekuja hapa kujifunza ili nitoke na kitu kipya chenye kunisaidia. Sijuwi wewe mwenzangu!

 18. Ndugu yangu ,
  Umenihukumu pasipo haki. UKIHUKUMU kwa kuhisi utakosea sana. Nimejiinua Kwa Kukuambia “Unapaswa KULIJUA na KULIFAHAMU hasa NENO LA MUNGU kwa Hakika na kwa Mapana na Marefu yake.”?
  Nilichomaanisha ni UMJUE BWANA YESU zaidi kuliko kunijua mimi NA SI VINGINEVYO.
  YEREMIA 9:23-24 ” Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana, ”
  Pia sijafunga MILANGO kama ulivyodai na hata ningetaka nisikujibu ningekuwa mwungana kukuambia.na sababu ya kutojibu.

 19. Baada ya kujibu kwa kejeli hata baada ya kuwa nimekuuliza kwa upendo na unyenyekevu UMEFUNGA MILANGO YOTE AMBAYO NILITAKA NIPITE ILI NIJIFUNZE KITU TOKA KWAKO. Siwezi pokea chochote tena toka kwako unless umeshuka chini. Umejiinua juu mno!
  @ Pendael Simon

 20. John Paul,
  Unapaswa KULIJUA na KULIFAHAMU hasa NENO LA MUNGU kwa Hakika na kwa Mapana na Marefu yake.
  Ahsante.

 21. Nashukuru kwa jibu hilo ambalo nalo limenisaidia pia kufahamu kwamba wewe ni mtu wa namna gani.

  Asante. @ Pendael Simon

 22. Ndugu,John Paul.
  Mahali ninapokutana na Wakristo Wenzangu Panaitwa KANISANI.

 23. Mi naomba tu kukuuliza ndg Pendael Simon, kwa unyenyekevu kabisa, kwamba ina maana wewe mahali unapokutana na wakristo wenzako PANAITWA JINA GANI? Mimi ninapokutana na wakristo wenzangu panaitwa TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD. Wewe kwako panaitwaje?

 24. Sungura.Ulishawahi kuniambia ‘akili ndogo haitawali akili kubwa’.Kama una ‘akili kubwa’ kama unavyojiita hayo maswali uliyoniuliza ni ya nini?Kutokana na KIBURI CHAKO cha Uzima ndio maana nimekuwa napuuzia maswali yako.

 25. Bwana Asheri. Usipende mashindano yasiyo na tija.Naona Dhehebu kuwa Mwili wa Ibilisi limekuuma sana! Kanisa na Dhehebu ni kitu kimoja?HAYO MENGINE niliyozungumzia kuhusu DHEHEBU mbona kimya? Hayo MAANDIKO niliyokuandikia ni ya UONGO?Kama hujasoma Hayo maandiko hutasaidika kwa namna yoyote.EPUKA KUTETEA DHEHEBU KWANI MADHEHEBU YOTE NI YA IBILISI.HAKUNA DHEHEBU LA YESU mahali popote.Kama unatamani kujua zaidi,Hii mada ya ‘tofauti kati ya KANISA na DHEHEBU ilishachangiwa hapa SG. Mimi sina DHEHEBU kwa sababu YESU KRISTO,MANABII na MITUME hawajawahi kuwa nalo.WAEFESO 2:2O-22.

 26. Well done Asheri!

  Kuna wakati hawa jamaa mimi naamua kuwaangalia tu, sijui kwenye vichwa vyao wanadhani wanawasiliana na watu wa namna gani hapa.

  They just say anything wanachojisikia wao kusema, bila kuwa na uwanda wa kutosha wa kimtazamo!

  Ngoja tungoje majibu ya Pendael!

 27. Ndugu Pendael Simon na wasomaji wenzangu wote,

  Shalomu,

  Nilipochangia hapo juu, nilitaka kupata majibu ya swali ambalo na ndugu Sungura ameliuliza pia kuhusu kauli ya ndugu Pendael, lakini ndugu Pendael hajannisaidia. Nilitegemea angenijibu kwa kuonyesha maandiko, lakini ameanza kwa kusema kuwa kama una Roho wa Kristo jibu liko wazi!!!. Lakini naomba sote tukumbuke kuwa, tunapoandika hapa wanasoma watu wa aina mbalimbali, wakiwa na viwango tofuati vya kiroho, hivyo ni vema kuwa makini sana na kile tunachokiandika ili kiweze kuwasaidia wanaojifunza

  Ndugu Pendael, niseme tu ukweli kuwa mimi hujanisaidia wala hujajibu swali la kuwa dhehebu ni mwili wa shetani. Maandiko yote uliyoyaandika hayahusiani na dhehebu au madhehebu. Hii nayo ni hatari kwa kuwa wapo watu waliotamani kujua maana ya maandiko hayo, hivyo unaweza kuwa umewapotosha. Kwa mantiki hiyo, mimi nachukulia kuwa huna jibu la kimaandiko linalosema kuwa dhehebu ni mwili wa shetani, kama unalo jibu basi utatupatia.

  Kwanza naomba niseme kuwa, si lazima mtu awe kwenye dhehebu fulani ndipo ahubiri uongo! mtu anaweza aseme yeye hana dhehebu/dini na bado akawa mhubiri wa uongo. Kwa sababu shetani hawaogopi wenye madhehebu au wasiyo nayo! Lakini ndugu Sungura alikuuliza kama wewe huna dhehebu, hukutaka kujibu swali hilo. Mimi nadhani tunahitaji pia kupata tafsiri ya neno dhehebu ili tuone nini maana yake? Maana kuna wengine wanaweza wakadhani kuwa hawana madhehebu, kumbe wanayo.

  Aidha, niseme wazi kuwa si nia yangu kutetea madhehebu, lakini pia si sahihi kuyasema madhehebu bila kuwa na hoja za msingi? Kwangu mimi najiuliza, tatizo ni uwepo wa madhehebu? mbona tunaposoma nyaraka za Paulo tunaona kuwa makanisa yalikuwa na shida? hata kama hayakuwa yakiitwa madhehebu? Ukiangalia Wakorintho, utagundua kuwa kanisa hilo lilikuwa na mambo mengi ikiwemo ugomvi, migawanyiko, kushtakiana, uzinzi, n.k., lakini tukiulizana je Wakorintho walikuwa dhehebu? Si Wakorintho tu, angalia Wagalatia, huko hata waalimu wa uongo walikuwepo lakini biblia haijasema kuwa Wagalatia walikuwa dhehebu, bali inasema ni kwa makanisa ya Galatia (Gal. 1:2).

  Katika Ufunuo wa Yohana mlango/sura ya pili na ya tatu, Yesu anazungumza na makanisa saba ya Asia Ndogo ambapo tunaona kuwa makanisa mengi yalikuwa na shida mbalimbali ikiwemo mafundisho ya uongo, kupungua upendo, uzinzi, waliokuwa na majina ya kuwa hai lakini wamekufa n.k. ni kutokana na matatizo hayo Bwana wetu Yesu Kristo anayaonya na kuyaambia yatubu!! Hapo biblia haikusema madhehebu, inasema makanisa!! Ndiyo maana mimi naona kuwa ipo haja ya kuangalia hoja ya msingi kuliko kuyasema madhehebu bila kuwa na tafsiri ya neno dhehebu. Lakini cha muhimu zaidi ni kuangalia tatizo liko wapi? Ni dhehebu au watu?

  Maran Atha.

 28. Hahahaa,

  Jibuni hoja, la mtakalia hayohayo ya msiogope maneno ya wanatheolojia.

  Mnajifanya mna ujuuuzi, lakini mnakwepa kujibu mambo ya msingi na kubaki kusifiana wenyewe kwa wenyewe!

  Suala la theolojia linatoka wapi kwenye hii mada kama si kuongea tu maneno ya vivihivi?

  Semeni hapa kama ninyi hamtoki kwenye madhehebu.

  Pendael sema hapa umepata kwenye andiko gani mwili wa ibilisi.

  Jibuni hoja!!!

 29. WAPENDWA,
  SHALOM.
  Kama una ROHO WA KRISTO kujua kuwa DHEHEBU NI MWILI WA IBILISI iko wazi kabisa.
  ILI Uweze kuona mambo ya ROHONI ni LAZIMA MACHO YATIWE NURU.
  Hapa dhana ya “MWILI” imetumika KUDHIHIRISHA SIFA FULANI.SIFA za MUNGU au za IBILISI.
  Kama MNAKUBALI kuwa KANISA ni MWILI WA KRISTO mbona MNAKATAA kuwa DHEHEBU si MWILI WA IBILISI?
  Mbona KIMOJA ni KINYUME cha KINGINE?
  Mwanzilishi WA KANISA NI BWANA YESU ( MATHAYO 16:18 ” Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”
  Mwanzilishi wa DHEHEBU ni IBILISI. (KJV BIBLE 1 Corinthians 14:33 ” For God is not the author of confusion, but of peace, as in all churches of the saints.”
  -Kwa maana Mungu si mwanzilishi wa machafuko,lakini wa amani,kama ilivyo katika makanisa yote ya Watakatifu.
  Mwanzilishi wa MACHAFUKO ni IBILISI
  MAKANISA YOTE YA WATAKATIFU YANA AMANI,
  Madhehebu ni MACHAFUKO. MADHEHEBU YOTE YANA MACHAFUKO ( Hawa wote HUPINGANA; TAG,EAGT,KLPT,PEFA,FPCT,CALVARY,HOLLINESS,JESUS ONLY,LUTHERAN,KATOLIKI,SABATO,ANGLIKANA,SALVATION ARMY, AIC,,,,,,nk,,)
  JE, HUU NI MWILI WA YESU?
  1 WAKORINTHO 6:15-17 ” Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
  Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. ”
  UDHEHEBU KWA MUNGU NI UKAHABA (UFUNUO 17:3-5 ” Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.”
  Majina ya MADHEHEBU ni Majina ya MAKUFURU.Madhebu ndio chimbuko la Mafundisho potofu.
  -Kukufuru ni KUNENA DHIDI YA..
  BWANA YESU ALIANZISHA KANISA na SHETANI ALIANZISHA DHEHEBU,
  HEBU MNIJIBU MASWALI HAYA;
  1.BWANA YESU na MITUME wake pamoja na WAKRISTO wa BIBLIA walikuwa DHEHEBU GANI?
  2,MADHEHEBU WANAHUBIRI KITU KIMOJA?
  3.DHEHEBU LIPI LINASEMA UKWELI?
  4.MADHEHEBU wanahubiri KAMA MITUME WALIVYOHUBIRI?
  5,HAMUONI MADHEHEBU YAMELAANIWA?
  -WAGALATIA 1: 8-9 ” Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. ”
  >>>NIONESHE DHEHEBU LAKO KWENYE BIBLIA NAMI NITAKUONESHA KANISA LANGU KWENYE BIBLIA>>>

 30. Ndugu,
  Jackson Zebedayo Mulele .
  Ubarikiwe na BWANA YESU KRISTO.
  Usiogope MANENO ya WANATHEOLOJIA.

 31. Mulele,

  Acha ubabaishaji kwa kusema mambo ambayo kimsingi ni misemo ya kubuni wala hayapo.

  Unaposema kuna neno na maneno tofauti yake ni ipi nje ya kwamba neno ni umoja na maneno ni wingi?
  Huu si msemo tu wa rejesta ya kilokolelokole ambao hauna ukweli wowote wa kimantiki!

  Halafu unasema kuacha mipasho; nani anayeongea mipasho kama si wewe mwenyewe? Kwenye hiyo komenti yako mbona kuna maneno ya vivihivi mengi tu!!

  Halafu unaanzia wapi kuiamini biblia ambayo uliletewa na wazungu, una uhakika gani kuwa yaliyoandikwa humo ni maneno ya Mungu?
  Huoni kuwa hata kilichoandikwa kwenye hicho kitabu walichotuletea wazungu ni mawazo yao tu?

  Na kitu kingine mnachokosea sana ni kuyajadili mambo kwa ujumlajumla.

  Mnapotukana suala la madhehebu naona kama mnajitukana wenyewe, maana hapo mlipo nanyi mna madhehebu. Kama hamna madhehebu mtuambie hapa hadharani ili tujue ninyi kwenye hayo makusanyiko mnayotoka mkoje!

  Kuna tofauti kubwa kati ya dhehebu na udhehebu, kwa hiyo msiunganishe hayo mambo mawili mkadhani ni jambo moja.

  Na Pendael nae atuambie suala la mwili wa ibilisi amelitoa kwenye andiko gani, maana ni rahisi sana kuona kuwa kuna neno mwili wa kristo ukadhani kuwa basi kuna na mwili wa ibilisi!

  Lazima kila mtu tumwajibishe kwa maneno anayosema, huwezi kusema tu chochote tukanyamaza!

  Take care (sijaedit)

 32. Shalomu wapendwa,

  Nimefurahishwa na mada, ina changamoto za msingi sana, hata hivyo nimeshangazwa kidogo na mchango wa mchangiaji wa kwanza kuwa madhehebu ni mwili wa Ibilisi, naamini kuwa ana maana yake katika hili, lakini ningemuomba afafanue kuhusu mwili wa ibilisi. Kulingana na kumbukumbu zangu, biblia inasema kuwa Kanisa ni mwili wa Kristo, lakini sikumbuki kama biblia imesema juu ya mwili wa ibilisi (shetani).

  Aidha, nadhani kuwa ipo haja ya kukubaliana na baadhi ya mambo yanayotokea kutokana na uwepo wa sheria na nyakati tulizo nazo hivi sasa. Yapo mambo ya kisheria yaliyosababisha kuwepo kwa madhebebu, na pia kuna tofauti za kiimani zilizosababisha kuwa na misingi tofauti ya kiimani iliyosababisha watu wawe na madhehebu tofauti, maana, kama watu wametofautiana masuala ya msingi ya imani, hawawezi kuwa na kusanyiko moja. Mfano, wapo wanaosali siku ya Jumamosi, wengine Jumapili, hapa lazima iwepo tofauti. Wapo wanaokubali wokovu, wapo wanaoukataa, wapo wanaoukubali wokovu, lakini wanasema kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, na wapo wanaoukubali wokovu, lakini wanasema ni Yesu Pekee. Wapo wanaomkubali Roho Mtakatifu, wengine wanakataa kuhusu Roho Mtakatifu, sasa katika mazingira hayo, ni lazima watu wawe tofauti.

  Ni hayo tu kwa sasa, ila nitafurahi kupata ufafanuzi kutoka kwa mchangiaji wa kwanza.

  Maran atha

 33. Amani iwe juu ya yeyote ataesoma!
  Kwa mtazamo wangu: Hata huyu ‘Mtoa mada’ nae ni mmoja wa hao waliokuja na ‘madhehebu yao’ kwenye kuokoka, maana nikiangalia hii mada bado haina ‘mishiko’.

  Kwani hasa KUOKOKA ndio nini?? Hivi ni Kweli kwamba mtu akisema au akidai kuwa ameokoka ndio ameokoka?? Hivi nii Kweli kwamba alie okoka na asie okoka tofauty yao ni kusema na kukiri kwao tu, lakini kuumwa, kushindwa, kuchoka, hasira, faraka, fitina zao ni sawasawa?? Mroman ni mtu wa asili ya Italia, je Mnyamwezi wa Shinyanga akijiita Mroman kama sio wazimu ninini!? Lini Mu-Anglicana (Muengereza) atajiita M-Chagglian ( Mchaga ) kama sio kuwa na mawazo ya kitumwa ktk Neno ni nini?? Wa-Lutheran ni Wajerumani walio kuja na kufanya vita na mababu zetu na kuwaua kwa kuwanyonga na kisha kumiliki migodi na mashamba ya Katani, kama walivyofanya waingereza! (Anglicans)

  Nimewahi kuandika hapa SG jinsi wazungu walivyo ‘tuletea’ Injiri na utapeli wao mwingi tuu! Lakini nikasema kuwa, Mungu na awabariki kwa kuwa wametuletea NENO ambalo ndani yake tunaweza jifunza na kuhojiana ‘wenyewe’ nae Bwana ameahidi kutufunulia ‘siri’ zake zilizofichwa ndani ya hilo NENO Lake !!

  SG yaani Straight Gospel inapaswa ku-hit straight ktk NENO na wala sio mipasho! Tunazo ahadi nyingi ktk NENO kwamba Mungu atatuinua na kutuweka mahali pa JUU, lakini hapo hatutapafikia kamwe bila kuzama ktk NENO.

  “Mtu akimpokea Yesu huingia kwenye familia ya watu waliookoka, watu waliosafishwa kwa damu ya Yesu Kristo. Anakuwa mwanachama wa Kanisa la Mungu lililo hai” Haya ni mafundisho ya Chekechea, yaani wiki ya kwanza darasani ktk safari ya kuelekea Primary, Secondary, High Level na hatimae kuuendea utimilifu yaani University!!
  Hebrania 5:11-14 Inatuamsha kwamba tuondokane na mipasho (story na itikadi za wazungu na u-kindergaten) na tuingie kwenye NENO Hebrania 6:1-2 kwa namna ya ‘ajabu kabisa’ NENO lina tuainishia ni jambo gani tunapaswa KULIENDEA na mambo gani ambayo “tutayafanya Mungu akitujalia”

  Tunapaswa kujifunza na kuelewa kuwa kuna NENO na maNENO, wazungu wametuletea maNENO ambayo ndani yake kuna NENO ambalo ndilo linapaswa kujadiliwa hapa SG (Straight to NENO!!!!)

  Tuulizane/tujadiliane/tufundishane kuhusu NENO tukiachilia mbali maNENO !! Pendaeli wa Simon, wewe ni mjasiliamali wa NENO la Mungu, hongera kwa kuthubutu kuyasema uliyoyasema ndugu! Walisemaga mababu zetu: Msema Kweli, ni mpenzi wa Mungu. Uko vizuri na salama ndugu na ahsante sana kwa “Udhehebu kwa Mungu ni Ukahaba” 🙂 🙂 Hilo ni NENO wala sio maNENO !!

  Soma majibu yangu ya swali: Kwanini ndoa nyingi za leo zina migogoro!?? Hapa SG ili tujifunze NENO.

  Wa-Asalaam

 34. ukimuuliza mlutheran kuwa je? umeokoka, atakuambia hapana. lakini misingi ya hilo dhehebu ni kuwa kila jumapili kuna sala ya pamoja ya kuukiri wokovu. hapa ninaona kuwa wakristo wengi hawajui kwa undani hasa wokovu ni nini? fanya research utaniambia kuwa ninachosema ni kweli. wape karatasi na kalamu waandike wanavyoufahamu, utashangaa mitazamo yao

 35. ukimuuliza mlutheran kuwa je? umeokoka, atakuambia hapana. lakini misingi ya hilo dhehebu ni kuwa kila jumapili kuna sala ya pamoja ya kuukiri wokovu. hapa ninaona kuwa wakristo wengi hawajui kwa undani hasa wokovu ni nini? fanya research utaniambia kuwa ninachosema ni kweli. wape karatasi na kalamu waandike wanavyoufahamu, utashangaa mitazamo yao.

 36. SHALOM;
  KANISA NI MWILI WA KRISTO na DHEHEBU ni MWILI WA IBILISI.
  WANAFUNZI au WALIOMWAMINI BWANA YESU waliitwa WAKRISTO ( MATENDO 11:26)
  MADHEHEBU yanakua kama UTITIRI MPAKA MAJINA YAMEKOSEKANA wanayaita kwa majina YAO hasa MADHEBU YA PENTEKOSTE MPAKA YANATIA AIBU.
  MADHEBHEBU yamekuwa KWAZO katika KUSHUHUDIA Injli KUTOKANA na TOFAUTI ZAO KIMAANDIKO.
  Hivi vikundi vimesababishwa na IBILISI. SHETANI si mjinga kama watu wanavyofikiri alijua namna ya kuwatala WATU WASIOLIFUATA NENO.
  VKUNDI HIVI VIMEJIKITA KATIKA MIRADI YA TUMBO badala ya KUHUBIRI INJILI; MFANO, KUJENGA SHULE,VYUO,HOSPITALI nk.
  IBILISI aliweza kutumia mtindo wa WAGAWE na UWATAWALE”DIVIDE & RULE” Kutengeneza MADHEHEBU Mengi na YOTE YANAPINGANA KWANI KILA MOJA LINAFUNDISHA TOFAUTI NA LINGINE.
  -MADHEHEBU wanaunga mkono WANAWAKE KUHUBIRI mimbarani na kuongoza wanaume? 1 WAKORINTHO 14:34-38, 1TIMOTHEO 2:8-15
  -MADHEHEBU HUWAPINGA MITUME (mfano; KAKOBE hufundisha kuwa MITUME walifundisha kinyume cha MAAGIZO YA YESU- kuhusu Ubatizo) ? LUKA 10:16, WAEFESO 2:20, WAGALATIA 1:8-9
  -MADHEHEBU wanapinga UBATIZO KATIKA JINA LA YESU KRISTO? (MATENDO 2:38-39, 8:14-16, 10:48, 19:1-5)
  *Mengine hubatiza WATOTO!
  – BWANA YESU na MITUME wake pamoja na WAKRISTO wa BIBLIA hawajawahi kuwa na DHEHEBU?
  * UDHEHEBU KWA MUNGU NI UKAHABA (UFUNUO 17:3-5). Majina ya MADHEHEBU ni Majina ya MAKUFURU.Madhebu ndio chimbuko la Mafundisho potofu.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s