KUTIMILIZA TORATI

 

law2

 

UTANGULIZI

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nawe mdau wa SG. Tunaishi katika kipindi ambacho kuna namna nyingi za injili, na usipokuwa makini unaweza kufikiri kuwa uko katika injili ya Yesu Kristo kumbe mtu ulishahama – kwa wale wanamuziki, wanasema umetoka “nje ya key”! Hata enzi za Kanisa la kwanza, jambo kama hili lilipata kutokea kule Galatia (soma Wagalatia 1:6-9).

Ukisoma Mathayo 5:20 unakutana na maneno haya toka katika kinywa cha Bwana wetu Yesu Kristo:

“Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.”

Andiko hili limekuwa likitumiwa na wengi kusisitiza kwamba, ili kuingia ufalme wa mbinguni hatuna budi kufanya matendo mema au mazuri na mengi zaidi ya vile ambavyo mafarisayo walikuwa wanafanya. Je mafarisayo walikuwa wanafanya nini?

“Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.” (Luka 18:11-12)

Hivyo, hoja hiyo husisitiza, tunapaswa kufunga zaidi ya mafarisayo na kutoa zaka na kufanya mambo mengine zaidi yao vinginevyo haki yetu haitazidi ile haki ya mafarisayo na hivyo hatutaweza kuingia ufalme wa mbinguni.

Je, ni kweli Bwana Yesu alimaanisha hivyo? Twende pamoja. Kanuni yetu, kama kawaida, ni kujenga hoja na kujadili kwa kuzingatia kile ambacho Maandiko Matakatifu yanasema.

BWANA YESU NA TORATI

Ili kuelewa ujumbe wa Bwana Yesu alipowaambia watu waliokuwa wakimsikiliza kuwa haki yao isipozidi ya mafarisayo hawataingia katika ufalme wa mbinguni, inabidi kusoma mstari huo katika muktadha wake.

“Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali KUTIMILIZA. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata YOTE YATIMIE. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu ISIPOZIDI hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, USIUE, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila AMWONEAYE ndugu yake HASIRA itampasa hukumu; na mtu AKIMFYOLEA ndugu yake, itampasa baraza; na mtu AKIMWAPIZA, itampasa jehanum ya moto.” (Mathayo 5:17-22, SUV, msisitizo wangu)

Yesu alikuwa akiongea na makutano (Mathayo 5:1), katika kipindi ambacho torati ilikuwa imeshika hatamu maana bado kilikuwa ni kipindi cha agano la kale. [Kuzungumzia kwa undani maswala ya agano la kale na lile jipya haiko katika lengo (scope) la mjadala huu, ila kwa ufupi sana niseme tu kuwa agano la kale Mungu aliliweka na wana wa Israeli pale alipowatoa kule Misri (soma Waebrania 8:8-9), na katika kipindi hicho wana wa Israeli walipewa torati waishi kwa hiyo. Agano jipya lilikuja kuanza Bwana Yesu alipotolewa dhabihu pale msalabani (soma Waebrania 9:11-15).] Bwana Yesu aliweka bayana kuwa alikuwa amekuja duniani “kutimiliza” torati. Je “kutimiliza” huku kulikuwa ni kufanya nini hasa, na hayo “yote” ambayo Yesu alisema kwamba yalikuwa hayana budi “kutimia” yalikuwa ni yapi?

Yesu alikuja KUTIMILIZA yale YOTE yaliyokuwa yamenenwa na torati na manabii. Yesu alilifafanua jambo hilo kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka maana katika kitambo chote alichokuwa nao hawakumwelewa.

“Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu NILIYOWAAMBIA nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba NI LAZIMA YATIMIZWE YOTE niliyoandikiwa katika TORATI YA MUSA, na katika MANABII na ZABURI. Ndipo AKAWAFUNULIA AKILI ZAO wapate kuelewa na maandiko. Akawaambia, NDIVYO ILIVYOANDIKWA, KWAMBA KRISTO ATATESWA NA KUFUFUKA SIKU YA TATU; na kwamba MATAIFA YOTE WATAHUBIRIWA KWA JINA LAKE HABARI YA TOBA NA ONDOLEO LA DHAMBI, kuanza tangu Yerusalemu.” (Luka 24:44-47, SUV, msisitizo wangu)

Kwa hivyo, Yesu aliposema kuwa hakuja kuitangua torati na manabii bali kuitimiliza, alikuwa anamaanisha kuwa alikuwa amekuja duniani ili YALE YOTE YALIYOTABIRIWA katika torati na manabii kuhusu kuteswa, kufa na kufufuka kwake, na hatimaye injili ihubiriwe duniani kote YATIMIE. Ni vema tukumbuke kuwa torati ilikuwa ni kiongozi wa kutuleta kwa Yesu Kristo, maana tunasoma, “Lakini KABLA ya kuja ile IMANI tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa. Hivyo TORATI IMEKUWA KIONGOZI kutuleta kwa Kristo, ILI TUHESABIWE HAKI KWA IMANI. Lakini, IWAPO IMANI IMEKUJA, HATUPO TENA CHINI YA KIONGOZI.” (Wagalatia 3:23-25, SUV, msisitizo wangu)

HAKI YA MAFARISAYO NA HAKI ANAYOITAKA MUNGU KWETU

Baada ya kuona kile ambacho Bwana Yesu alimaanisha aliposema kuwa hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza, tunaweza sasa kuelewa kile alichomaanisha alipozungumzia kuwa haki ya mtu inapaswa kuizidi ile ya mafarisayo ili kuingia katika ufalme wa mbinguni. Neno lililotafsiriwa kama “haki” katika Mathayo 5:20 limetokana na neno la Kiyunani “dikaiosune¯” linalomaanisha “the character or quality of being right or just”, yaani, ile hali au tabia ya kuwa sawa (bila kosa lolote) au mwenye haki.

Tafsiri ya Kiingereza ambayo inafafanua zaidi maana za maneno inasema:

“For I tell you, unless your righteousness (your uprightness and your right standing with God) is more than that of the scribes and Pharisees, you will never enter the kingdom of heaven” (Matthew 5:20, Amplified)

Mafarisayo na waandishi walikuwa wakijihesabia haki (yaani, walijihesabu kuwa wako sawa) mbele za Mungu kwa kujipima ni kwa jinsi gani walikuwa wanafanya yaliyoandikwa katika torati. Ndio maana tunasoma:

“Akawaambia mfano huu watu WALIOJIKINAI YA KUWA WAO NI WENYE HAKI, WAKIWADHARAU WENGINE WOTE. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa MIMI SI KAMA WATU WENGINE, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza shuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, HUYU ALISHUKA KWENDA NYUMBANI KWAKE AMEHESABIWA HAKI KULIKO YULE; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.” (Luka 18:9-14, SUV, msisitizo wangu)

Bwana Yesu katika hotuba yake ya mlimani alifafanua kuwa, katika torati iliandikwa “usiue” (yaani wasifanye tendo ambalo linaonekana kwa macho – kuua – na ambalo lilikuwa limeandikwa katika torati) lakini yeye akawatajia mambo ambayo mtu akiyafanya itampasa adhabu – kumwonea hasira mwenzake, kumfyolea, au kumwapiza. Hayo aliyowatajia hayakuandikwa katika torati yao, lakini yalikuwa ni mwanzo wa hasira ambayo mtu anakuwa nayo kabla ya kufikia hatua ya kumwua mwenzake. Nitatoa mfano mwingine.

“Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” (Mathayo 5:27-28, SUV)

Yesu aliwaambia mafarisayo waliokuwa wakijihesabia haki kwa kuwa hawakuzini kwamba, hata kama hawakuzini lakini kama waliwaangalia wanawake kwa kuwatamani kingono tayari walikuwa wamezini nao. Tamaa ya kutaka kufanya ngono na mwanamke ndiyo hupelekea mtu kutafuta fursa ya kuzini naye (soma pia Yakobo 1:13-15). Mafarisayo walijihesabia haki kwa kuwa hawakufanya lile tendo la ngono, lakini Yesu akawasisitizia kuwa kutamani kufanya ngono na mwanamke – hata bila ya kufanya tendo lenyewe – tayari ilikuwa ni uzinzi.

Kupitia mifano hiyo, Bwana Yesu alikuwa anawaeleza kiwango cha juu cha haki ambacho Mungu alikuwa anakitarajia kwa wanadamu – si tu kufuata vile torati ilivyokuwa ikisema (usiue, usizini, usiibe, nk), bali kwenda kushughulikia kwenye MZIZI wa hayo maovu, yaani kwenye moyo ambako mawazo ya kufanya maovu hayo huanzia. Huko kukishashughulikiwa, mtu hatahitaji tena kuwa na orodha ya mambo ya kutokufanya bali atajikuta anaenenda katika njia iliyo sawa na hafanyi yasiyopasa. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa anawaeleza namna ya haki ambayo ilikuwa ni ya KIWANGO CHA JUU, iliyozidi kwa mbali sana namna ile ya haki ambayo mafarisayo walikuwa wanajihesabia.

Mahali pengine Yesu aliwaambia mafarisayo, ambao walijihesabu kuwa ni wenye haki mbele za Mungu kwa zile jitihada zao za kutii torati (japo walichanganya na mapokeo yao ambayo hayakuwemo katika torati (angalia, kwa mfano, Mathayo 15:6)), maneno haya:

“Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya MIOYO ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu YATOKA NDANI, nayo yamtia mtu unajisi.” (Marko 7:20-23, SUV, msisitizo wangu)

Mafarisayo walijihesabia haki kwa kujitahidi kukwepa kufanya matendo maovu na kufanya matendo mema yanayoonekana (angalia Mathayo 6:1-6), lakini Yesu aliweka bayana kwao kuwa walitakiwa kushughulika na mioyo yao ambako matendo yote huanzia huko. Ndiyo maana aliwaambia:

“Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa MNASAFISHA NJE ya kikombe na chano, na NDANI YAKE vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza NDANI ya kikombe, ILI NJE YAKE NAYO IPATE KUWA SAFI.” (Mathayo 23:25-26, SUV, msisitizo wangu)

Kama haki ya mtu itaishia katika kutii torati au orodha ya makatazo (prohibitions), kwamba usifanye hiki au kile, itakuwa sawa na ile waliyojihesabia mafarisayo na waandishi. Hiyo haitasaidia kitu.

“Basi ikiwa MLIKUFA PAMOJA NA KRISTO mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, KWA NINI KUJITIA CHINI YA AMRI, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata MAAGIZO NA MAFUNDISHO YA WANADAMU? Mambo hayo YANAONEKANA KANA KWAMBA YANA HEKIMA, katika namna ya IBADA MLIYOJITUNGIA WENYEWE, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini HAYAFAI KITU kwa kuzizuia tamaa za mwili.” (Wakolosai 2:20-23, SUV, msisitizo wangu)

Haki yetu inatakiwa izidi hiyo – itokane na kushughulikia kule ndani kabisa, kwenye moyo, ambako maovu huanzia. Na hilo haliwezekani pasipo kumpokea Kristo Yesu na kuzaliwa upya, na kujifunza kuongozwa na Roho Mtakatifu katika kufisha mwili pamoja na tamaa zake.

“Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.” (Wagalatia 5:24)

NAFASI YA MATENDO MEMA

Baada ya kusema hayo, hebu tuangalie nafasi ya matendo mema katika maisha ya mtu aliyemwamini Kristo Yesu.

Ni muhimu kutambua kuwa Mungu alituumba ili tutende yaliyo mema kwa wengine:

“Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende MATENDO MEMA, ambayo TOKEA AWALI MUNGU ALIYATENGENEZA ILI TUENENDE NAYO.” (Waefeso 2:10, SUV, msisitizo wangu)

Kama wana wa Mungu, tunatarajiwa kufanya yaliyo mema (soma pia Mathayo 5:16, 1 Timotheo 2:8-10, Tito 2:7-14; 3:14), lakini SI MATENDO HAYO yanayotufanya tuhesabiwe haki mbele za Mungu (angalia Warumi 3:23-24, Waefeso 2:8-9, Warumi 11:6, Wagalatia 2:21, ). Tukitarajia au kutafuta kuhesabiwa haki kwa sababu ya matendo yetu mema tunarudi kule kwenye torati na kuachana na neema.

Matendo mema tunayoyatenda ni matunda ya mabadiliko yanayotokana na utendaji au uhai wa ile imani katika Kristo Yesu iliyo ndani yetu. Ndiyo maana Yakobo aliandika:

“Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini? Vivyo hivyo na imani, ISIPOKUWA INA MATENDO, IMEKUFA NAFSINI MWAKE. Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami NITAKUONYESHA IMANI YANGU KWA NJIA YA MATENDO YANGU.” (Yakobo 2:14-18, SUV, msisitizo wangu)

Uhai wa imani yetu katika Kristo Yesu unaonekana kwa nje kupitia matendo yetu. Kama hakuna mabadiliko, Maandiko yako wazi kabisa kuwa imani hiyo imekufa.

KWA KUMALIZIA

Nisisitize kuwa, Bwana Yesu alikuja duniani akafa msalabani na kupata mateso mengi, damu yake ikamwagika, ili ashughulikie mzizi wa dhambi unaotufanya tuwaze na hatimaye kutenda maovu. Kama tutang’ang’ania kutaka kuishi kwa kufuata mlolongo wa sheria na kujihesabia haki kwa umahiri wetu wa kuzifuata, tutakuwa tumetoka nje ya mstari na kuifanya kazi yote ya Mwokozi kuwa haina maana. Tunapomwamini, imani ile inapotenda kazi ndani yetu inapelekea sisi kutenda matendo mema yanayoonekana kwa nje na kudhihirisha badiliko lililotokea katika maisha yetu.

Mungu wa mbinguni akubariki.

Joel Msella

Advertisements

291 thoughts on “KUTIMILIZA TORATI

 1. Sungura,
  Unaweza kudhani kuwa unajua na/au kukiamini unachokisema! Najua unaamini hivyo! Na akili yako inakuaminisha hivyo! Hata mimi nilikuwa huko uliko na nilikuwa mbishi kama wewe!! Kwa kweli sikujua asili na maana ya wokovu hasa! Nilikuwa napokea miujiza kama wewe, nanena kwa lugha kama wewe! Nilidhani niko kwenye njia sahihi kabisa! Mara nyingine niliwatukana walioniijia na injili mpya tofauti na ile niliyokuwa nayo! Sikuwa na staha. Neema ya Mungu iliponifungukia, nilijuta na kutubu sana! Siku yaja Mungu atakufungua tu! La msingi, angalia usije ukachelewa!
  Baada ya kupokea NURU mpya, ndipo nilianza kuijua kweli iliyoniweka huru! Ndipo nilipogundua kuwa, kuwa kumbe wokovu ni PROCESS! Kama Paulo, nimekuja kugundua kuwa, nina safari ndefu ya kufikia hatua ya kutamka kuwa “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake”. Paulo anatoa kauli hii katika kipindi chake cha mwisho katika historia ya maisha yake. Jiulize kwa nini kipindi cha mwanzoni alipompokea Kristo, hakusema ‘dhambi imekoma maishani mwake’? na badala yake anaonekana kulalamika(warumi 7:20-25) kuwa dhambi inamtesa kila iitwapo leo japo alikuwa akifanya jitihada za kuishinda kwa jina la Kristo?!!
  Hata sasa najua unaweza usinielewe ndugu yangu. Kama sasa “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu”. Ndugu yangu Sunugura, Kila siku tunatenda dhambi ama ya kimwili, kifikra, kuona, kusikia, kutowajibika na pengine tunatenda dhambi bila ya kujua kuwa tutendacho ni dhambi! Ni kwa Neema ya Mungu tu ndio maana tupo! Si kwa sababu hatutendi dhambi!! Hasha!! Sisi ni wadhambi wakubwa, tena wa kwanza wao, lakini kwa neema tu ya Kristo, Mungu bado anatuvumilia katika makuzi yetu ya ya kiimani kama Paulo. Ipo siku tutakayotamka kama Paulo alivyotamka (hapo juu) –tamko la ushindi. Kwa sasa bado sana. Tuna safari ndefu ya kwenda.
  Mimi nasikitika kukuona ukikiri kuwa una shetani mzuri!! Hii nayo ni mpya! Shetani ni mbaya siku zote ndugu yangu! Kamwe hajawa mzuri hata siku moja! Kama wasabato tunatumia hekima au akili (yoyote ile), fahamu kuwa Mungu hujifunua katika vitu hivyo! Maana kwa vitu hivyo, Mungu huwasiliana na binadamu. Ndiyo mafunuo yenyewe hayo! Nguvu ya Mungu hutuijia baada ya kupata hekima/akili itokayo JUU! Tofauti na hapo ni ukengeufu tu –huo unaouamini wewe! Ndio maana una negative pre-conceived ideas kuwa wasabato hatujazwi na roho takatifu ya Mungu! Nani alikudanganya?! Tunawezaje kuzijua siri za Mungu kama hatujazwi na roho takatifu??!! Acha kubweteka kijana! Changamka aisee!
  Usikatae wala kukana kuwa ni kwa sababu ya miujiza ndiyo maana umeng’ang’ana kubaki jinsi ulivyo. Uko hivyo kwa sababu ya miujiza!! Kazi za Mungu katika maisha ya mwanadamu, ndiyo miujiza yenyewe hiyo bro! Hata unapoamka asubuhi toka usingizini, huo nao ni muujiza. Kwa maneno mengine, ni kazi ya Mungu pia! Ndiyo maana ndege na viumbe wengine wa asili, humsifu Mungu (kwa nyimbo) kila asubuhi na jioni kwa sababu ya kazi/matendo yake makuu –miujiza kwa viumbe hao. Kwa ujumla, maisha ya mwanadamu, naam hata viumbe vyote, yamegupikwa na kazi/miujiza ya Mungu japo na shetani naye yupo kwa upande mwingine! Ndiyo maana nakwambia, hatuwezi kukimbilia miujiza tu badala ya ukweli kwanza! Adamu alipooumbwa, hakupewa muujiza ili amwamini Mungu na aamini kile alichoambiwa! Isipokuwa alipewa neno la Mungu (SHERIA YA MUNGU) tu. Tunaanza na neno kwanza, then miujiza inafuatia! Ukiwa kinyume na NENO la MUNGU, miujiza ya Mungu hutaipata kamwe na badala yake ibilisi ataleta ya kwake! Na watu wengi walio kinyume cha Neno la Mungu, wanapoona miujiza, huamini kuwa inatoka kwa Mungu kumbe inatoka kwa yule muovu. Pole zao!
  Wale waliaminilo neno la Mungu na kuliishi, miujiza ya Mungu itaambatana nao pia. Mungu akusaidie kukufungua ndugu yangu. Usitangulize miujiza, anza na neno la Mungu kwanza ndipo miujiza ije baadaye. Hapo ndipo utakuwa salama kwenye safariya wokovu!
  Neema yake ikufunike
  Siyi

 2. Siyi,

  Umejaa majibu ya kukariri kuwa watu wa aina fulani huwa mnawajibu hivi au vile, ndio maana mara nyingi huwa unakosa kuona mantiki za mambo katikati ya maandishi.

  Katika comment yangu hakuna mahali nimetaja neno ‘miujiza’, na hakuna mahali nimetaja neno ‘ akili’. Wewe kwa kukariri kwako ulipoona neno ‘kazi’ ukadhani ni neno miujiza. Mimi siyo kama uliozoea kubishana nao ambao ni waprotestant kama mimi. Mimi ninakijua vizuri ninachokisema.

  Nilisema ‘kwa yale ambayo nimemuona Mungu akitenda’.
  Siyi, kitu cha kwanza ambacho Mungu katenda kwangu ni kule kuniwezesha kushinda dhambi. Hapo nyuma nilijaribu sana lakini sikuweza kabisa. Hata nisiposema mengine, hilo tu moja lilinitosha kujua Mungu niliyempata ni wa kweli.

  Na kama huyo aliyenipa nguvu ya kushinda dhambi, ni shetani, basi ni shetani mzuri sana kuliko niliyekuwa nae mwanzo.

  Kitu kingine nilichokisema ni ‘human wisdom’, sikusema akili. Nilikwambia kuwa wasababto mnasumbuliwa sana na kutafsiri maandiko, kwa sababu mnatumia sana hekima ya kibinadamu. Kama wewe ni msomi mzuri basi utakuwa unaelewa kuwa kuna tofauti kati ya akili na hekima.

  Lakini pia nilikwambia kuwa ufalme wa Mungu si katika neno tu, bali ni katika nguvu pia.

  Usitake kunidanganya Siyi, wasabato labda siku hizi ndo mmeanza kuamini habari za kujazwa Roho mtakatifu, lakini siku zote mmekuwa mkipinga habari za kujazwa na Roho. Lakini mimi sitashangaa kuona mmebadilika, Mungu hana upendeleo.

  Kwa habari ya miujiza, ni kwamba ninaamini miujiza, lakini simwamini kristo kwa sababu tu ya miujiza. Ndo maana nimekushangaa kuona unaniambia ati naamini ‘tu’ kwa kwa sababu ya miujiza ( zingatia matumizi ya neno tu).

  Ysu aliwaambia kama hawamwamini yeye basi wayaamini matendo ya miujiza anayofanya ili wajue kuwa Baba yuko ndani yake.

  Siku zote watu wasiokuwa na uwezo sawia wa Mungu ndani yao, wakiona muujiza wazo la kwanza linalokuja ndani yao ni kwamba muujiza huo ni wa shetani. Wanamwamini shetani kwa haraka zaidi kuliko wanavyomwamini Mungu. Hata Siyi nakuona uko miomgoni mwa hao.

  Ni kweli miujiza kwa waprotestant/wapentekodte kama mimi ni sehemu ya maisha yetu: ukimwi kupona, kansa kupona, viwete kutembea, vipofu kuona, wafu kufufliliwa, waliofungwa na mapepo kufungulia, watu kujazwa Roho mt, n.k, ni part and parcel ya ibada zetu. Lakini hayo ni matokeo ya nguvu ya Kristo itendayo kazi ndani yetu.

  Asante sana.

 3. Sungura!!
  Unaona sasa??!! Ndiyo maana nimekwambia wewe huoni japo wadai kuona!! Hatuwezi kuamini tu kwa sababu ya miujiza!! Hata huku kwa wasabato miujiza ipo, lakini Siyi na wasabato wengine makini, hawawezi kuamini tu kwa sababu ya miujiza hiyo. Ni kweli Mungu ana miujiza. Na shetani naye ana miujiza pia!! Yote hiyo utaipimaje? Maana kote kuna miujiza!!
  Bila ya kukaa chini ukatafakari kwa kumuomba Mungu akupatie nguvu yake itokayo juu, huwezi kumuona Mungu! Utadhani unaye kumbe una ibilisi tu! Maana hata na yeye (ibilisi), aliasi mbinguni kwa sababu ya kukosa heshima ya kuabudiwa. Naye anapenda sana kuabudiwa. Na anapoabudiwa, sharti na yeye atende miujiza ili watu wamwamini pia kama alivyokwishafanya katika historia. Kama uliona muujiza katika maisha yako, umebakiza jambo moja; UHAKIKI huo muujiza kama kweli ulitoka kwa Mungu.
  Tofauti na hapo, utapotea tu pamoja na kupokea muujiza huo. Hatuokolewi kwa sababu tulipokea miujiza. Ila ni kwa sababu tuliishi sawasawa na Neno la Mungu.
  Mambo ya kiroho ni sharti utumie AKILI pia maana AKILI ndiyo ROHO!!
  Ubarikiwe
  Siyi

 4. Siyi,
  Asante sana kwa kupita.

  Naweza kuwa na matatizo mimi kama mimi,lakini kusema kuwa wanaokusanyika kusali Jumapili ati wamepotea na wasabato ndo mko vizuri,huko ni kukosa hoja ya kusema juu ya tunachojadili hapa.

  Hata kama ningekuwa kipofu wa kimwili kabisa nisiweze kusoma kwenye maandiko ukweli wa Kristo, kwa yale ambayo nimeona Mungu akitenda kwa hao unaowaita wa Jumapili,mimi nikiwa wa kwanza wao,yanatosha kabisa kunihakikishia kuwa waliye nae ni Yehova aliye hai.

  Kuna wakati hufika ikabidi watu tuangalie kazi zinazofanyika ili tukiamini kinachofanya kazi ndani ya wanaotenda hizo kazi kuwa ni Mungu aliye hai.

  Ufalme wa Mungu si katika neno tu,bali na katika nguvu pia.

  Tafsiri ya maandiko inawateseni sana wasabato, nafikirii mnajaribu sana kutumia human wisdom,kwa sababu kimsingi hamumkubali Roho mtakatifu.

  Kama nina kiburi cha maisha basi ninacho ktk kumjua kristo

  Amen.

 5. Sungura,
  Unasikitisha sana rafiki yangu. Mimi nakuangalia kama mtu uliyejawa na kitu kiitwacho ‘KIBURI CHA UZIMA’! Hapo ulipo unajua kuwa na una uzima…!! Na “kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”. Ushauri wangu kwako;
  1. “Mtafute Bwana, maadamu anapatikana, Mwite, maadamu yu karibu”
  2. Njoo “ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona”.
  3. “Wote niwapendao mimi (Mungu) nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu”.
  4. “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”
  U ‘re an educated person, p’se don’t be easily cheated! Sunday worshiping churches are front organizations of the Illuminati which are carbon copies of the Jesuits methods and techniques running the entire world into desolation! Watch on!

  Nilikuwa napita tu!! Unaweza kudhani kuwa unaona kumbe huoni rafiki yangu!! Wewe huoni!! Na hujui kama huoni kweli!! Hiyo ndiyo shida kwako!

  Siyi

 6. Siyi,
  Umenichekesha sana,kwamba unabii wa kweli ni wa wasabato, this is a big joke indeed.

  Kuna miaka kadhaa iliyopita wasabato walishatoleana unabii kuwa Yesu anarudi, wakakesha kwenye mawe milimani wakingoja. Mwishoe wakaamua kurudi majumbani wao wenyewe,maana hakurudi.

  Wala sijakujibu comments nyingi ati kwa sababu kulikuwa na hoja nzito umeandika.
  Moderator amekuwa anachelewa kurelease comments, kwa hiyo kwa sababu ya mambo mengi kama mara mbili hivi nikadhani sijakujibu,kumbe zilikuwa zimechelewa tu.

  Maswali mengi unaniuliza wakati unatakiwa kuiuliza biblia. Unataka nikubali tafsiri zako ati kwamba kilichotumika ni lugha ya kinabii, this is rediculous. Iko very clear kwenye hiyo mistari kuwa New Jerusalem na mbingu mpya na Nchi ni vitu viwili tofauti.

  U dont wanna agree with scriptures, bt to rely on yo religious interpretation, we call it a day. It’s nobody’s business.

 7. Eliy
  Binafsi nakushukuru kwa maoni na mawazo yako mazuri. Ubarikiwe sana.
  Mimi nina swali moja kwako:
  Je, Mungu akikufunulia mambo yake (siri zake zilizo ndani ya Biblia), mafunuo hayo huwekwa wapi? Akilini au moyoni/rohoni? Je, kuna tofauti yoyote au mfanano wowote wa vitu hivi viwili (akili na moyo/roho)?
  Nasubiri majibu yako ili yanibariki pia kama mchango wako huu ulivyonibariki.
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 8. Wakristo huwa hawalumbani na kila mmoja kujifanya mjuaji. Naona kuna malumbano kama ya waislamu kati ya Siyi na Sungura, mmepotea sana kila mmoja anajifanya anaielewa Biblia. Nimewaona jinsi kila mmoja anavyojaribu kutumia akili zake kuelezea jambo la kiroho, tena zito kuliko mnavyodhani. Mashindano na kujiona ndivyo vitu vilivyomfanya shetani atupwe duniani. Inatosha kuelewa kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, na ukimwamini umekwisha kuokolewa. Tulieni na kujifunza kwa upole, na kamwe hamtaweza kuielewa kwa utimilifu Biblia mpaka Kristo atakaporudi na kutufunulia siri zote.

 9. Sungura,
  Nakushukuru kwa kukuona tena. Naona pachiko langu la safari hii limekushughulisha kwelikweli hadi ukaliandaalia majibu matatu ya siku tatu tofauti!! Ha ha ha ha!! Kimsingi nakushukuru maana umeanza kuuona ukweli sasa.
  Siku ile nilikwambia kuwa “Yerusalemi Mpya = Mbingu na Nchi Mpya”. Hii ni lugha ya kinabii tu iliyotumika kaka. Wewe unasema kuwa Yerusalemi ni mji ndani ya mbingu mpya na nchi mpya, haya, hao mataifa watakaoukuja keleta heshima na utukufu watatokea wapi? Kumbuka moto ulishailamba dunia na waovu wote!! Je, kuna mataifa gani tena watakaokuja kuleta heshima kwenye mji wa Yerusalemi kama unavyodai wewe!!? Ukiisoma Biblia kama MZALENDO, utakesha!! Mimi nilikwambia Kitabu cha ufunuo ni kitabu cha unabii. Unakataa na kusema ni sawa na vitabu vingine. Haya!! Hebu niambie sasa maana ya nyota saba, roho saba, malaika saba. n.k. zilizomo kwenye kitabu hicho!! Na kama ni wasabato tu tunaojifunza unabii, akili yako ina shida!! Mungu ni Mungu wa unabii kijana!! Mambo yoote huyafanya kiunabii!! Hakuna jambo ambalo alishawahi kulifanya bila ya kulitolea unabii. Hakuna!! Bisha na hapa!! Wewe sema, unabii mnao ila wa kwenu ni matangopori tupu ndio maana unapiga chenga hapa kuusema!!
  Kristo ataushusha mji wake uje ukae ilipokuwa dunia baada ya dunia hii kuunguzwa kwa moto na wadhambi wake wote na kasha kuondolewa. Jiulize sasa, dunia imewekwa wapi? Jibu utapa!!
  Ukisema kuwa “mji wa Yerusalem mpya utakuwa ndani ya Mbingu mpya na nchi mpya”, una matatizo!! Unadhani ndani ya mbingu mpya na nchi mpya, mataifa hao watatokea wapi tena? Hao mataifa watakuwa ni wacha Mungu au? Au mbinguni kuna mataifa tayari yatakayokuja kutoa homage kwa Kristo na mji wake?. Narudia kukwambia, jifunze unabii kijana. Unaaibisha sana!!
  Unabii sahihi unaweza kuupata kwa wasabato tu!! Kwingine utalishhwa matangopori tu! Pamoja na kuupuza na kuubeza, unabii wa wasabato ndio wenyewe!! Kama unataka kuuhakiki unabii wa Wasabato, usome kwanza, halafu uulinganishe na historia za matukio ya dunia as per Bible itself!! History doesn’t lie!! Hakiki tu kwanza uone!!
  Naona bado unarudia tu hii hoja. “Uliuliza swali kuwa kama Yerusalem mpya ni mji,nje ya Yerusalem mpya kutakuwa na nini? Nikakuonesha jibu katika Ufunuo 21: 24 (Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
  26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.)”
  Hebu nisaidie kujibu maswali yangu hapo juu kwa mujibu wa hii hoja yako!! Ukishindwa, njoo tukufundishe unabii kwanza!! Maana unadhani tunakuuliza maswali ya kitoto kumbe wewe mwenyewe una shida kubwa ya kiufahamu kuhusu jambo hili kuliko unavyofikiri.
  Mungu akubariki sana
  Siyi

 10. Siyi,

  Jaribu kuwa makini zaidi.

  Tanh\gu mwanzo nilikuambia kuwa mbingiu mpya na nchi mpya siyo mji, bali ni ulimwengu.
  Yeusalem mpya ndo mji, ambao kimsingi utakuwa ndani ya mbingu mpya na nchi mpya.

  Sasas sijui mimi na wewe nani mwenye fikra ya kwamba mbingu mpya na nchi mpya ni kimji.

  Una akili ndogo sana ya kuona mantiki ya jambo katikati ya mistari.

  Uliuliza swali kuwa kama Yerusalem mpya ni mji,nje ya Yerusalem mpya kutakuwa na nini? Nikakuonesha jibu katika Ufunuo 21: 24 (Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
  26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.)

  Ulivyo kichwa maji, hutaki ku-concentrate katika majibu ya ulichouliza, unaanza kurukia vitu vingine ili kuhama kwenye suala la msingi.

  Hatuna huo muda wa kuendelea kuongea jambo lilelile ambalo kimsingi limeshaeleweka.

  Unaniuliza kama huwa kwetu tunajifunza hivi vitabu vya unabii; ili iweje sasa?
  Vitabu vya unabii ni vitabu tu kama vitabu vingine vya biblia, sihitaji kwenda shule maalum kuvielewa. Hakuna mtume ambaye aliwahi kuvifundisha exceptionally ati kwa kuwa ni vitabu vigumu sana.

  Hiyo kazi mnafanya ninyi wasabato kwa sababu kwanza hamna Roho mtakatifu akiwaongoza ndani Yenu, maana yeye ndiye mwalimu.
  Na matokeo yake mnalishana matango mwitu(yaani mafundisho ambayo yako fabricated na akili tu za watu fulani) mpaka macho yenu yanapofuka kabisa.

 11. Siyi,

  Kati ya mimi na wewe nani kasema kuwa mbingu mpya na nchi mpya ni kimji kidogo, na ni wapi ambapo nimedhani kuwa mbigu na nchi mpya ni kimji kidogo?

  Ivi kati ya Jerusalem mpya na mbingu na nchi mpya kipi ambacho ni mji?

  Yeyote mwenye akili timamu atajibu kuwa Jerusalem mpya ndo mji, na mbingu mpya na nchi mpya ni ulimwengu.

  Sasa jaribu kupitia machapisho yetu uone kati ya mimi na wewe nani hasa aliyekuwa amekazana kusema kuwa mbingu mpya na nchi mpya ni mji.

  Tangu mwanzo nimekwambia mji wa Yerusalem mpya utakuwa ndani ya Mbingu mpya na nchi mpya.

  Unaniambia habari za kujifunza vitabu vya unabii,sijui ni kujifunza kwa nanmna gani huko unakokutaka. Vitabu vya unabii vina ugumu upi mpaka vifanyiwe shule yake binafsi, ni mtume yupi ulishamsoma kwenye maandiko alifanya madarasa maalum ya kujifunza vitabu vya unabii?

  Hizo shule maalaum za kujifunza vitabu vya unabii fundishaneni ninyi wasabato kwa maana hamna Roho mtakatifu ambaye ndo katumwa kwa kusudi la kulifundisha kanisa.

  Vitabu vya unabii navijifunza kama ninavyojifunza vitabu vingine, mmeambiwa kuwa ni vigumu sana ndo maana mmedanganywa.

  Hakuna chochote cha maana unachokijua kuhusu hivyo vitabu vya unabii, ni uongo tu.
  Take care!

 12. Siyi wewe ni sikio la kufa aise!

  Nilikuwa nakusubiri tu maana ukilemewa huwa unakaa kimyaaa, lakini nilijua hii shule mahali ilipofika hauiwezi!

  Huwezi kuanza kuniauliza maswali ya kitoto yasiyo na msingi wowote kwa kitu ambacho tunatakiwa kukiainisha hapa, wakati mimi nilikuuliza swali very specific kuwa:
  ” Hao mataifa wanaosemwa watatembea kwa nuru ya hilo jiji wenyewe yatakuwa wako kwenye nini,
  na hao wafalme watakaoleta fahari zao katika huo mji watakuwa wanatokea wapi.?”

  Nikunukuu na kingine umekisema, ” Kristo ataushusha mji wake ili aishi na wateule wake pamoja ili kutimiza ahadi yake ya sisi kuishi sehemu aishipo na YEYE”

  Unaposema kuwa Kristo ataushusha mji wake, ataushusha wapi, baharini au?

  Ukijibu hilo swali utakuwa umepata jibu la tunacholumbana hapa!

  Siyi, don’t take me lightly,read between the lines carefully!

 13. Sungura,
  Wewe una shida rafiki yangu!! Shida kubwa kweli!! Biblia inapozungumzia habari za nchi mpya na mbingu mpya, ina maanisha hivyo –ulimwengu mpya!! Haina maana kuwa mbingu mpya na nchi mpya ni kimji kidogo kama vile unavyodhani wewe. Kitabu cha Ufunuo ni kitabu cha kiunabii. Ni vyema ukakielewa kabla ya kuanza kukipinga!! Naomba usome kwa makini aya hizi zifuatazo za Ufunuo 21.
  10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
  11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;
  12 ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.
  13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu.
  14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
  15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
  16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
  17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.
  18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.
  19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi;
  20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.
  21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
  22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.
  23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo.
  24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
  25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
  26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake.
  27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

  Nataka umakinike zaidi na hizi aya mbili kwanza;
  16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
  17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.

  Maswali kwako ya tafakari!!
  a. Unaujua urefu na upana wa mji wa Yerusalemi ya zamani ulikuwa ni kiasi gani??
  b. Je, Yerusalemi hii mpya inafanana na ile ya zamani kwa ukubwa au kuna utofauti?
  c. Kuna ufanano/utofauti wowote kwenye vipimo vya ukutua vilevile??
  d. Biblia inaposema “… maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa” Danieli 7:10. “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka. Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele”- Ufunuo wa Yohana 5:11-13.
  Unadhani hawa watu woote na viumbe woote wa mbinguni watakaokuwa wakisifu, watakuwa wameenea ndani ya mji huo Yerusalemi mpya na vipimo vyake vidogo hivyo??

  Nidokeze kuwa, Ufunuo wa Yohana na Daniel ni vitabu vya kiunabii. Sina uhakika kama mnajifunza unabii huko kwenu!! Yohana alioneshwa Yerusalemi mpya kwa maana ya mbingu na nchi mpya itakayokuja baada ya dunia hii na anga lake kuondolewa!! Yerusalemi mpya inawakilisha mbingu mpya na nchi mpya ambayo kimsingi ni mji wa Yesu Kristo. Kristo ataushusha mji wake ili aishi na wateule wake pamoja ili kutimiza ahadi yake ya sisi kuishi sehemu aishipo na YEYE. Jifunze unabii kaka, ndipo utaelewa mambo hayo.
  Neema ya Bwana ikufunike kijana.
  Siyi

 14. Siyi,

  Labda chunguza vizuri kwenye maandiko unaweza kupata majibu ya hicho ulichouliza.

  Thanks!

 15. Sungura,
  Nikuulize swali kabla sijajibu pachiko lako.
  Kwa hiyo, baada ya mbingu na nchi za zamani (za sasa) kuondolewa, Yerusalemi mpya itakayoshuka, itaenda sehemu ilipokuwa Yerusalemi ya zamani (kama sijakuelewa vibaya). Je, maeneo mengine ya nchi kama huku Tz, Amerika n.k. (ambayo kwa wakati huo hayatajulikana kwa majina hayo tena), yatakaliwa na nani kwa vile watakatifu wa Mungu watakuwa Yerusalemi tu? Au watasambaa baadaye? Hebu nisaidie kuleta utondoti wa maana.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 16. Siyi,

  Unataka nikukugundue ili inisaidie nini sasa?

  Unaesma Ufunuo 21 haiongelei vitu viwili tofauti, bali mbingu mpya na Jerusalem mpya ni kitu kilekile.

  Hebu tuinukuu tena Rev 21:saw the Holy City, the new Jerusalem, coming down out of heaven from God, prepared as a bride beautifully dressed for her husband.

  Mji mtakatifu Yerusalem mpya, unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu, halafu Siyi anasema kuwa kinachoshuka na kinakotoka hicho kinachoshuka ni kitu kilekile- lazima huyu mtu hayuko sawa kiufahamu.

  Hii inaitwa Yerusalemu mpya kwa vile sasa hivi kwenye hii nchi ya sasa kuna Yerusalem ya zamani.
  Hii inaitwa nchi mpya maana kuna nchi ya sasa hivi (dunia) ambayo ni ya zamani.
  Na hii inaitwa mbingu mpya maana kuna ya sasa ambayo ni ya zamani.

  Kuna swali uliuliza, ngoja nilinukuu nikujibu;
  ”Kama Yerusalemi mpya itashuka, je, itaijaza hiyo mbingu mpya na nchi mpya?? Au sehemu zingine za mbingu mpya na nchi mpya kutakuwa na nchi gani zingine (mpya)??”

  Kabla sijakupa andiko, jiulize kama Yerusalemu ya sasa imeijaza nchi yote na mbingu, na jiulize kama Yerusalem ya sasa iko mbinguni au duniani (nchi)

  Soma hii, Rev 21: 22 I did not see a temple in the city, because the Lord God Almighty and the Lamb are its temple. 23 The city does not need the sun or the moon to shine on it, for the glory of God gives it light, and the Lamb is its lamp. 24 The nations will walk by its light, and the kings of the earth will bring their splendor into it. 25 On no day will its gates ever be shut, for there will be no night there. 26 The glory and honor of the nations will be brought into it.

  Halafu niambie hayo mataifa yanayosemwa yatatembea kwa nuru ya hilo jiji yenyewe yatakuwa yako kwenye nini,
  na hao wafalme watakaoleta fahari zao katika huo mji watakuwa wanatokea wapi.

 17. Sungura
  Hata mimi najua kuwa huwa unauliza mambo mengine ukiyajua kabisa. Ila nilivyokuona, mambo mengine unayoulizaga huwa huyajui totally, unayajua kiasi au unayajua ndivyo sivyo!! Ndiyo maana huwa ninakujibu kwa kuzingatia hayo!! Kwa hiyo, na wewe uwe makini kunisoma ninapokujibu!! Kwa mfano ukisoma majibu yangu huwa unagundua nini? Je, ukinisoma huwa unaona ninajibu mtu anayeelewa anachokiuliza? Au anaelewa kidogo tu? Au anaelewa ndivyo sivyo? Jitahidi unigundue sasa. Kama ulikuwa bado, mimi nakupa pole.!!
  Mengi ya mambo unayoyaelewa ndivyo, huwa unataka nijibu kama uelewa wako ulivyo!! Ndiyo maana mtu atakusikia ukisema sijajibu maswali….. sijajibu maswali!!! Hiyo ndiyo shida yako!! Mimi Mungu ananiongoza sawia kulielewa NENO, hivyo siwezi kukujibu sawasawa na ulivyolishwa falsafa na wanatheolojia wako!! Kamwe sitafafana nao!! Nikushauri jambo moja, unapokuwa unajadili mambo na watu, jaribu kujiempty kichwani ili usikie wengine wanasemaje kwanza. Halafu, baadaye changanya na uelewa wako. Ukiona haviwiani, weka mawazo yote mawili, matatu mezani then Omba na kummuliza Mungu kuhusu jambo hilo kwa kulisoma NENO lake. “Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo” – Isaya 28:10. Utagundua tu ni nani yuko sahihi? Tofauti na hapo, unaweza kung’ang’ana na jambo ukidhani ni fundisho la Biblia kumbe ni fundisho la dini tu –Lwembe alisema siku ile!! Acha kutumia akili zako mwenyewe kijana!! Utaishia hewa!!
  Leo nitarudia kujibu swali lako dogo la nyongeza kuhusu idadi ya Sayari. Sayari ziko nyingi sana sana. Kwa akili yangu ya kibinadamu siwezi kuzihesabu. Ila wanasayansi, wamezibaini chache hizo –unazozijua wewe!!
  Kama wewe uelewa wako ni kwamba Mungu ataleta mbingu mpya na nchi mpya, halafu ndani ya mbingu hiyo mpya na nchi hiyo mpya alete Yerusalemi mpya, akili yako ndiyo ina shida rafiki!! Kama Yerusalemi mpya itashuka, je, itaijaza hiyo mbingu mpya na nchi mpya?? Au sehemu zingine za mbingu mpya na nchi mpya kutakuwa na nchi gani zingine (mpya)?? Leo ukiambiwa kuwa Tanzania mpya itashuka ndani ya mbingu mpya na nchi mpya, unaelewaje? Pole sana. Uelewa wako hauna tofauti na ule wa mashahidi wa Yehova!! Jiandae na wewe kuja kurithi majumba na maghorofa yaliyopo leo. Ha ha ha ha!!
  Ushauri, Ufunuo 21:1-2, haiongelei vitu viwili tofauti!! Inaongelea kitu kilekile kimoja!! Mbingu mpya na nchi mpya, tayari ni nchi hiyohiyo -Yerusalemi!! Kwani Mungu alipoiumba dunia hii, aliiumba na kasha Yerusalemi akaiumba tofauti? Je, na Tanzania iliumbwa nayo? Kenya, Uganda, Zambia, Marekani n.k.? Sungura, Mungu alipoziumba mbingu na nchi, alitengeneza mazingira ya viumbe kuishi! Ndio eneo hili leo tunaliita Tanzania, Marekani, Uganda , Bahari n.k. -dunia nzima. Hakuna ubarishaji, uinchiishaji wala ukijijishaji!! Mbingu Mpya na nchi mpya, ndiyo Yerusalemi hiyohiyo kijana. “Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo” – Isaya 28:10. Ukisoma Biblia tofauti na kufuata kanuni hii, nimekwambia utaishia hewa!!
  Ngoja nikupe mfano kidogo. Soma mwanzo 1: 6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. 7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo.

  Nenda tena mistari hii ya kitabu na sura hiyohiyo!!
  20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. 21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

  Enhee, umegundua nini hapa ambacho wewe ndicho kinachokusumbua mpaka leo? Angalia mwanzo 1:6 Mungu anaonekana kutamka tu. Lakini mstari wa 7, Mungu anaonekana kutenda!! Je, tuseme kuwa Mungu aliumba vitu viwili tofauti hapo? Hapana!! Hebu soma na aya zingine kadhalika!! Unapata nini? Jibu ni kwamba Mungu aliumba kitu kilekile!! Shida inatokea wapi sasa kwenye ufunuo 21:1-2?? Shida ni wewe mwenyewe na hao walimu wako wa dini!! Rafiki, acha kusoma Biblia kama gazeti la udaku!! Neno la Mungu halisomwi hivyo!! Ni lazima uzingatie kanuni ya “.. amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo” ndipo utafaulu. Tofauti na hapo, utakesha!!

  Mungu akufungue!

  Siyi

 18. Siyi,

  Nikikuuliza jambo usidhani kuwa nakuuliza kwa sababu mimi sijui, utakuwa umepotea sana ukiwa na mawazo hayo.

  Mambo niliyokuuliza hujayatolea majibu, ila umeongea tu maneno yako.

  Nilikuuliza hivi:

  1.Kwanza, hiyo imani kuwa kuna sayari nyingi zilizoumbwa na Mungu, umeitoa kwenye andiko gani au unaamini from which source?”

  – Hakuna andiko hata moja ulilonipa ambalo limetamka neno sayari, umeongea tu maneno yako mengiii kama kawaida yako.

  Ivi ulisoma shuleni kuwa sayari ziko ngapi, halafu mwalimu wako alikuambia pia nyota ziko ngapi? Sasa kwa kuwa ulifundishwa kuwa nyota nazo ni sayari halafu ukafundishwa pia idadi ya sayari, sasa niambie sayari ziko ngapi jumla.

  2. Nipe andiko ambalo linasema kuwa dunia ndo sayari pekee inayokaliwa na viumbe walioasi”.

  Ulichokisema katika hili kinanipa wasiwasi sana kama unajua sayari hasa ni kitu gani.
  Lakini hapo napo hujanipa andiko linalosema kuwa dunia ndo sayari pekee inayokaliwa na viumbe walioasi.
  Zaburi 8:3-9 – Haijasema kuwa dunia ndo pekee inakaliwa na viumbe walioasi. Na sijajua kwa nini umeunukuu huu mstari hapa.
  Ufu 21:1 – Nayo haisemi hivyo
  Kwa hiyo hapa napo hujajibu swali, umeongea tu maneno yako.

  La mbingu mpya na Yerusalem mpya;

  Ivi siyi, do u really think properly brother or something is out of place in your brain?

  Ufunuo 3:12- imekwambia kuwa Yerusalem mpya unashuka kutoka mbinguni kwa Baba. Hapo tu penyewe ameshakuonesha kuwa mbingu ni kitu kingine na Yerusalemu mpya ni kitu kingine. Halafu ukidikia neno mpya ujue kina ya zamani. Ya zamani ni hii Yerusalem iliyopo.

  Ufunuo 21:1 – anasema akaona mbingu mpya na nchi mpya…
  Ufunuo 21:2- anasema akauona mji mtakatifu, Yerusalem mpya unashuka kutoka mbinguni kwa Mungu.

  Tayari kesha kuonesha kuwa mbingu mpya ni kitu tkimoja na Yerusalem mpya ni kitu kingine. Yerusalem mpya inashuka kutoka kwenye mbingu – Halafu wewe kwako Yerusalem mpya ndo mbingu mpya.

  Sikia, kama ambavyo Yerusalem ya zamani iko ndani ya mbingu ya zamani na nchi ya zamani, ndivyo ambavyo Yerusalem mpya itakuwa ndani ya mbingu mpya na nchi mpya.

 19. Sungura,
  Kwanza, pamoja na kusema kuwa uko makini kufuatilia kila niandikacho, ukweli unaonesha kuwa, hauko makini!! Kwa nini? Hauko makini kwa sababu unapigwa chenga na mambo madogomadogo sana. Kama haya madogomadogo tu huyaelewi, itakuwaje kwa mambo makubwa? Si ndo utaambulia negative sifuri kabisa!! Hebu twende tuone…
  a. Swali lako: 1. “Kwanza, hiyo imani kuwa kuna sayari nyingi zilizoumbwa Mungu, umeitoa kwenye andiko gani au unaamini from which source?”

  Jibu
  Kwanza inabidi uelewe maana ya Sayari. Sayari maana yake ni gimba kubwa linaloelea angani (agh. kwenye njia yake maalumu) kulizunguka jua! Hata JUA lenyewe, ni sayari vilevile. Mwezi ni Sayari pia! Kabla ya uumbaji Mungu alikuwepo (usiniulize alikuwa anakaa wapi!). The entire universe had nothing, except Mungu na maji (ambayo hatuambiwi yaliumbwa lini, japo mimi naamini kuwa na menyewe yaliumbwa tu!). Katika mwanzo 1 Biblia inasema, “Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi” –mstari 14-17.
  Zingatia:
  – Jua, Mwezi na Nyota hazikuumbwa kama vyanzo vya NURU juu ya nchi/mbingu! Hasha! Mungu alikuwa alishaumba tayari NURU hata kabla ya kuziumba sayari hizi –Jua, Mwezi, na Nyota! Rejea uumbaji wa siku ya kwanza –mwanzo 1:3-5. Kwa hiyo sayari hizi ziliumbwa kwa makusudi maalumu (mengine kabisa –ishara ya nyakati na majira) pamoja na kwamba kazi ya kutia nuru juu ya nchi/mbingu zilipewa!

  Kwa hiyo, nikiisoma Biblia yangu, huniambia kuwa, kuna sayari (nyota) nyingi sana zilizoumbwa na Mungu. Hizo ni miongoni mwa aya za Biblia zinazonifanya niamini hivyo! Kama wewe unabisha, leo kataa hapa kuwa Jua, mwezi, na nyota siyo sayari!! Kataa hapahapa na watu wakuone!!

  Swali lako: 2. “Pili nipe andiko ambako ambalo linasema kuwa dunia ndo sayari pekee inayokaliwa na viumbe walioasi”.
  Jibu
  Ndiyo! Kama hili nalo linakupa shida, nazidi kukupa pole tu! Mungu alipoiumba sayari dunia na sayari zingine, Biblia inasema kuwa, “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha; Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. Kondoo, na ng’ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini. Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!” Zaburi 8:3-9.
  Zingatia:
  Kabla ya uumbaji, the universe, ilikuwa bahari tu –maji tu yasiyo na kiumbe chochote kwa ndani! Sasa hapa kwenye mstari wa 8, Biblia inasema mwanadamu alipewa kuvitawala vyote hata vile vinavyozidi njia za bahari, -‘Na kila kipitacho njia za baharini’. Sayari zote, zilikuwa chini ya mamlaka ya Adamu. Ndiyo maana Adamu alipoasi, sayari zote na viumbe wengine waliokuwa kwenye sayari dunia, nao walihesabiwa uovu huohuo!! Ndiyo maana kwenye Ufunuo Biblia inasema, “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena” –Ufunuo 21:1. Kwa maneno mengine, ‘When Adam sinned, ALL of CREATION was affected—the entire universe’.

  Pili, umeniambia nani kaniloga kwa kuiita Yerusalemi kuwa ndiyo mbingu mpya na nchi mpya!! Hadi nimeshangaa!! Lakini nimemshangilia Bwana maana leo nitakwambia aliyeniloga!! Hebu muone aliyeniloga anavyosema –
  Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. Isaya 65:17

  Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Isaya 66:22

  Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. 2 Petro 3:13

  Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya. Ufunuo wa Yohana 3:12

  Mbingu mpya na nchi mpya ni zile alizoenda kuandaa Kristo huko mbinguni. Makao ambayo nabii Isaya, mtume Petro na Yohana, waliziona katika njozi zao. Baada ya kakamilika kwa ujenzi wa mji huo (yohana 14:1-3), Kristo ataushusha chini mji huo, ndiyo mji ambayo Yohana anauita Yerusalemi mpya! “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe” – Ufunuo wa Yohana 21:1-2. Nchi/Mbingu Mpya na Yerusami Mpya, ni kitu kilekile. Hivi siyo vitu viwili tofauti. Mungu haleti mbingu mpya na nchi mpya, halafu akaleta na Yerusami mpya tena!! Mungu hana miji miwili aliyoenda kuandaa! Ameenda kuandaa mji mmoja tu. Mji ambao nchi (ardhi yake), na anga (mbingu yake), vitakuwa ni vipya, tofauti na na hivi vilivyopo leo. Na mji huo wenye vitu vipya, unaitwa Yerusalemi Mpya!! Acha kuchanganyikiwa kijana!!

  Hata mimi sijasema kuwa tutaishi mbinguni milele. Mbinguni tutaenda tu kwa miaka 1000 na baada ya hapo, mji wetu (Yerusalemi Mpya), tutashuka nao. Tutashuka wapi? Sehemu ambapo hapo zamani sayari dunia ilikuwepo!

  Kwa hiyo Sungura, usitafute mchawi wangu. Ni huyu –Biblia!!
  Ni rahisi kiasi hicho!

  Siyi

 20. Siyi,

  Niko makini sana kufuatilia kila neno, kwa hiyo ukiandikaandika tu utapata shida sana kudadavua na mimi hii mada. Nikutake kwanza uache kuandika kiswahiliswahili na kipashkuna.

  Kwanza, hiyo imani kuwa kuna sayari nyingi zilizoumbwa Mungu, umeitoa kwenye andiko gani au unaamini from which source?

  Pili nipe andiko ambako ambalo linasema kuwa dunia ndo sayari pekee inayokaliwa na viumbe walioasi.

  Halafu wewe inaonekana hata katika elimu tu ya kawaida hauko makini sana. Ngoja nikuoneshe kitu cha kijinga ulichosema.

  ”Mbingu mpya na nchi mpya itakayokuja baada ya sayari dunia kuondolewa, yenyewe inaitwa Yerusalemi Mpya kwa mujibu wa Biblia”

  Kwamba kwa akili yako ndogo Yerusalem mpya wewe ndo unaiita mbingu mpya na nchi mpya.
  Wewe Siyi usiye na akili ni nani kakuloga, pamoja na biblia kukonesha wazi kuwa mbingu mpya na nchi mpya ni kitu kimoja, halafu Yerusalem mpya ni kitu kingine?

  Ona Ufunuo 21 inavyosema: – 1 Then I saw a new heaven and a new earth; for the first heaven and the first earth passed away, and there is no longer any sea. 2 And I saw the holy city, new Jerusalem, coming down out of heaven from God, …

  Andiko liko wazi linakwambia kuwa Yerusalem mpya itashuka kutoka mbinguni, halafu wewe unasema Yerusalemu mpya ndio mbingu mpya na nchi mpya. Huo ni ujinga uliochanganyika na uzembe.

  Jambo jingine la kizembe ulilosema ni hili hapa:

  ” Mungu hakuiumba Earth ili akae humo, bali aliiumba Earth kwa ajili ya wanadamu tu. Sasa hivi ameandaa makao yetu kwenye makao yake, sehemu ambayo na sisi atatukaribisha. Sehemu hiyo siyo Earth tena wala dunia!! Ni Mbingu mpya na nchi mpya”

  Unachokisema kuwa Mungu alikiumba ili akae mwanadamu kinaitwa nchi (Earth), na unachosema kuwa Mungu amekiandaa sasa hivi ili sisi tukae nae umekiita ‘mbingu mpya na nchi mpya’ ukidhani kuwa chenyewe siyo earth.

  Lakini mbingu mpya na nchi mpya kwa Kiingereza ni ‘New heaven and new Earth’. Ndo maana nikakuambia Mwanzo Mungu aliumba mbigu na nchi(Heaven and Earth), na atakapoziondoa hizo mbingu na nchi za kwanza, bado atazireplace na mbigu na nchi, lakini hizi zitakuwa mpya ( New heaven and new Earth).

  Hautaishi mbinguni, usijidanganye.

  Simple like that

 21. Sungura,
  Unaona sasa? Unaona akili yako inavyofikiri kidogo kwenye jambo hili!!!? Sidhani kama nitakuwa na muda wa kutosha kukuelekeza ukaelewa!! Kwa ufupi na ili tusiendelee kutoka nje ya mada kama unavyosema, mimi naamini kuwa, kuna sayari nyingi sana zilizoumbwa na Mungu. Mojawapo ya Sayari hizo, ni sayari yetu –dunia; sayari ambayo kwa mujibu wa Biblia ndiyo pekee yenye viumbe walioasi!! Na hii ni lazima iondolewe/ifutiliwe mbali sayari yenyewe na viumbe vyake vyote vilivyomo –isipokuwa kwa wale wanaomfuata Kristo kila aendako!!
  Ndani ya Biblia kuna aya 409 zinazotaja neno ‘dunia’. Mbingu mpya na nchi mpya itakayokuja baada ya sayari dunia kuondolewa, yenyewe inaitwa Yerusalemi Mpya kwa mujibu wa Biblia –mji wa Mungu, makao ya Mungu. Sehemu ambayo Mungu anakaa, nasi tutakaa hapo!! Kwa hiyo ni ukweli usiopingika kuwa, dunia ni jina tu la waswahili (Kiingereza Earth). Mungu hakuiumba Earth ili akae humo, bali aliiumba Earth kwa ajili ya wanadamu tu. Sasa hivi ameandaa makao yetu kwenye makao yake, sehemu ambayo na sisi atatukaribisha. Sehemu hiyo siyo Earth tena wala dunia!! Ni Mbingu mpya na nchi mpya –Yerusalemi kwa jina la Biblia!! Kama wewe unasubiri kuja kuishi tena duniani, nakupa pole sana.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 22. Siyi,

  Kunavitu vingi sana tunabishana mimi na wewe, ila kuna vingine hunibidi tu nicheke, kama hiki cha mbingu na nchi.

  Lakini ngoja twende hivi:
  Mwanzo 1:1 inasema hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.

  Ufunuo 21:1 inasema nikaona mbingu mpya na nchi mpya, maana ya mbingu na nchi ya kwabza zimeondolewa.

  Zote hizi ni mbingu na nchi, tofauti ni kwamba moja ni mpya na nyingine ni kuukuu.

  Neno dunia na neno nchi ktk Biblia ya Kiswahili yametumika ‘ interchangeably’. Pia mahali pengine pa world biblia ya Kisw.imesema dunia badala ya ulimwengu

  Nikakwambia tutaishi kwenye nchi/ dunia ambayo lakini ni mpya.

  Sasa wewe nioneshe kwenye maandiko kuwa hatutaishi duniani, ili uthibitishe ufedhuli wangu!

  Suala la maana ya ufalme wa Mungu mioyoni mwetu, is too pet to concetrate on. Ndo huko tunakolalamikiwa kuwa tunatoka nje ya mada.

 23. Sungura
  Sehemu tunayoishi leo ni sayari dunia!! Mbingu mpya na nchi mpya siyo sayari dunia!! Inabidi utambue hilo!! Hatutaishi duniani tena bro!! Wewe vipi!!? Sisemi mimi kuwa nina ufahamu zaidi ya wasabato wengine. Hasha! Ila ninakuonesha ni ukweli wa Maandiko. Kama unabisha fasiri yangu ya ufalme wa Mungu kuwa mioyoni mwetu kuwa maana yake ni amani ya mioyoni. Wewe tupe fasiri sasa. Ulimaanisha nini!??
  Acha falsafa za kifedhuli za kudanganyana kuwa duniani ni mahali pazuri pa kuishi hata baada ya Yesu kuja!! Huo ni uongo uliokubuhu! Jinasue mapema
  Siyi

 24. Sungura
  Sehemu tunayoishi leo ni sayari dunia!! Mbingu mpya na nchi mpya siyo sayari dunia!! Inabidi utambue hilo!! Hatutaishi duniani tena bro!! Wewe vipi!!? Sisemi mimi kuwa nina ufahamu zaidi ya wasabato wengine. Hasha! Ila ninakuonesha ni ukweli wa Maandiko. Kama unabisha fasiri yangu ya ufalme wa Mungu kuwa mioyoni mwetu kuwa maana yake ni amani ya mioyoni. Wewe tupe fasiri sasa. Ulimaanisha nini!??
  Acha falsafa za kifedhuli za kudanganyana kuwa duniani ni mahali pazuri pa kuishi hata baada ya Yesu kuja!! Huo ni uongo uliokubuhu! Jinasue mapema

 25. Siyi,

  Ivi wewe ndo mwenye ufahamu wa juu kati ya wasabato wote au wewe ndo mjinga kuliko wote?

  Hapa umeongea nini sasa:

  ”Sasa kama mbingu zitaondolewa, bado dunia itaendelea kuwepo? Usijidai kijana. Wote tunatambua kuwa Makao ya Watakatifu yatakuwa ndani ya mbingu mpya na nchi mpya”

  Ivi kama unajua kuwa makao ya watakatifu yatakuwa ndani ya mbingu mpya na nchi mpya, kwa nini nikikwambia kuwa watakatifu hawataishi mbinguni bali duniani unakataa? Au hujui kuwa hata sasa tunaishi kwenye mbingu na nchi, na zinazokuja nazo ni mbingu na nchi ila zenyewe ni mpya?

  Au niliponukuu hili andiko hukuelewa?:

  ” Rev 21: – Then I saw a new heaven and a new earth; for the first heaven and the first earth passed away, and there is no longer any sea. 2 And I saw the holy city, new Jerusalem, coming down out of heaven from God, made ready as a bride adorned for her husband.…”

  Unaelewa kinachosemwa kwenye mstari wa pili, Kwamba Jerusalaem mpya itashuka kutoka mbinguni imeandaliwa?
  Kwa nini nikikwambia kuwa hayo makao aliyokwenda kuandaa Yesu yatashushwa toka mbinguni, which means hayatakuwa mbinguni bali duniani huonekani kuelewa, nini kigumu hapo? Imetengenezwa mbinguni, inaletwa kutumika ( kukaliwa duniani)

  Acha ubishi wa kijinga, ukiwa huna kitu cha maana cha kuongea si lazima kuongea.

  Hakuna mahali nimekwambia kuwa ufalme wa Mungu maana yake ni amani ya mioyoni, hayo ni maneno yako ya kuropoka tu.

  Nilichokwambia ni kwamba ufalme wa Mungu uko mioyoni mwetu!
  Halafu sijafasiri kitu bali nimenukuu tu ambacho biblia imesema.

  Wewe ndo uniambie hii fasiri umeitoa wapi:
  ” Ufalme wa Mungu uko mioyoni mwenu maana yake ni kwamba, tuna uhakika wa wokovu tukikaa (tukiwa na matumaini) ndani ya Kristo”

  Onesha ulikoitoa hii fasiri yako.

  Makao aliyokwenda kutuandalia yatashuka kutoka mbinguni, hayatakuwa mbinguni!!

 26. Lwembe,
  Nadhani hukuliona sharti langu nililokupa siku ile. Naomba uthibitishie kama mtu wa rohoni anaweza kuzungumza na mtu wa mwilini, basi! Hebu niambie kama leo Spiritual mind imefanana na carnal mind, kwamba vyote vinaweza kufungwa kwenye nira moja!!
  Tafadhali hebu njoo rafiki yangu!!
  Siyi

 27. Sungura,
  Wewe ndo unatia huruma sana rafiki yangu. Unasema makao mapya Yesu atayaleta duniani?? Fanatics!!! Una matatizo nini!!
  Hebu soma aya hii “Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake” – Ufunuo 6:14.
  Sasa kama mbingu zitaondolewa, bado dunia itaendelea kuwepo? Usijidai kijana. Wote tunatambua kuwa Makao ya Watakatifu yatakuwa ndani ya mbingu mpya na nchi mpya! Sehemu hiyo, ndiyo makao ya Kristo mwenyewe, maana alisema, “…niwakaribishe kwangu…, ili nilipo nanyi muwepo…”.
  Mimi sijui mbingu ilivyoumbwa. Kama kuna sehemu ya Yesu kuishi, hiyo ndiyo sehemu yetu pia –Biblia imesema. Ufalme wa Mungu si kama unavyoufasiri wewe –amani ya mioyoni!! Ufalme wa Mungu uko mioyoni mwenu maana yake ni kwamba, tuna uhakika wa wokovu tukikaa (tukiwa na matumaini) ndani ya Kristo. Tujapolala leo, tuna uhakika wa kuja kuishi milele kutokana na matumaini hayo!! Wewe vipi??
  U masikini sana wa maarifa rafiki yangu japo u mtaalamu wa kutuhumu wengine!! Pole sana.
  Mungu akusaidie kukufungua.
  Siyi

 28. Siyi,
  Unalalama bure, acha kuandika kiujanjaujanja, sijui kama unaandika ili wasomaji wakuhurumie. Usipoteze muda kunijadili mimi, jadili mada!

  Katika hilo ulilolilalamia sana nilichokwambia kimsingi ni hiki hapa, najinukuu; ”Hebu imagine mtu anayesema anayaelewa maandiko, anausubiria kuuona ufalme wa Mungu siku akifika mbinguni. Ni ujinga ulioje huo. Hujui ufalme wa Mungu ni kitu gani Siyi.”

  Nilisema hivyo nikikurejerea wewe uliiposema unasubiri kwenda kuuona ufalme wa Mungu mbinguni.

  Nikakwambia hujui maana ya ufalme wa Mungu.

  Siyi ungejua maana ya ufalme ungekuwa unajua kuwa ufalme wa Mungu siyo sehemu, bali ni mfumo wa utendaji wa Mungu. Na biblia inatuambia kuwa ufalme wa Mungu uko mioyoni mwetu.

  Na hakuna sehemu biblia imesema kuwa tutaenda kuishi mbinguni, mwanadamu hajaumbiwa kuishi mbinguni Siyi, ndio maana kuna suala la nchi mpya na mbingu mpya. Unatakiwa kuelewa hayo.

  Usichukulie mambo kirahisi kumbe unaingiza mawazo yako ukidhani kuwa ni maandiko.
  Yesu kwenda kwa Baba na kwenda kutuandalia makao, hakusema kuwa hayo makao yatakuwa mbinguni, wewe kwa kutumia common sense yako unadhani makao aliyokwenda kutuandalia yatakuwa mbinguni.

  Siyi ndege huwa zinatengenezwa Ulaya kisha tunaletewa sisi huku kuzitumia, mtu akikwambia naenda Ulaya kukutengenezea ndege usidhani kuwa akimaliza kuitengeneza atakuchukua akupeleke Ulaya, ataichukua ndege aliyokutenezea na kukuletea huku uliko.

  Ni hivi; makao kweli Yesu kaenda kuyaandaa mbiguni, lakini yakikamilika yatawekwa duniani ambako binadamu aliumbwa kuishi.

  Ona haya maandiko: Rev 21: – Then I saw a new heaven and a new earth; for the first heaven and the first earth passed away, and there is no longer any sea. 2And I saw the holy city, new Jerusalem, coming down out of heaven from God, made ready as a bride adorned for her husband.…

  Siyi, hayo makao yaliyokwenda kuandaliwa yatashushwa kutoka mbinguni kuja duniani!

  Punguza kulalama, lete facts!

 29. @ Mhina
  Umenena neno ndugu yangu. Sina uhakika kama tunastahili kuwa na sifa ya ushujaa, isipokuwa Neema ya Kristo inayotuzunguka kila wakati. Kimsingi tuko nje ya mada. Hii ilitokana na machipukizi madogomadogo yanayojitokeza wakati wa mjadala wa mada husika, ambayo na menyewe ni ya muhimu pia kuyafahamu/kuwekana sawa. Ndiyo maana hata moderators wetu, waliyaona ni ya muhimu ndiyo maana wakawa wanayaruhusu ili watu wayasome. Hatuna budi kuwashukuru sana kwa kazi yao kubwa, nzito na nzuri. Mungu awabariki sana.
  Tuko duniani japo sisi si watu wa duniani!!
  Neema ya Bwana iwafunike.
  Siyi

 30. hongereni kwa moyo wa kishujaa usiochoka wala kukata tamaa….ijapokuwa mmetoka kabisa nje ya “maada husika jadiliwa!!.. jitahidini kuandika injili ya kristo yenye kudumisha upendo na tumaini, kuliko kutafuta ukamilifu wenu.thax

 31. Sungura,
  Zamani kwetu kulikuwa na group la vijana waliokuwa wakisema kinyumenyume!! Ulikuwa ni mtindo wao!! Sungura naye ni mmoja wao!! Anashangaza kwa wale wasiomfahamu vizuri!! Kwa watu kama mimi, sina shida naye, maana siandiki kwa ajili yake tu, bali kwa wasomaji wote!! Kila mtu ana akili, akisoma michango yetu, ataamua mwenyewe. Mimi ni nani? Sungura ni nani? Ni bora Mungu akatawala fikra zetu.
  Moja, Ninakushukuru kama umesema kinyume cha “Unatia huruma ndg!” kwa maana ya ‘Unachangamsha ndg’, unaleta vitu vya maana n.k. Nimefarijika kwelikweli, maana ni dhahiri kabisa kuwa message delivered unto you in depth!! Glory to God!!
  Pili, kuhusu hoja ya kumwelewa Mungu, mimi sijamwelewa Mungu sawasawa kama ulivyosema (kinyume chake). Na sitamwelewa Mungu vilivyo hadi nitakapooanza kuishi naye kwenye makao mapya! Maana wakristo wa kawaida tu kama mimi, wanaoisoma Biblia, wanaamini kuwa Yesu aliwaahidi wafuasi wake akiwaambia “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” –Yohana 14:1-3. Mkristo yeyote anayemwamini Kristo na mafundisho yake, anaamini kuwa ahadi hii ni amini na kweli. Kwa vile alisema “naenda kuwaandalia mahali”, na hakwenda kwingineko kokote isipokuwa mbinguni kwa Baba yake, tuamini wapi sasa kuwepo kwa makao hayo mapya kama siyo mbinguni? Pachiko lililopita, nilikwambia kuwa, sisi si watu wa ulimwengu huu maana tu wafuasi wa mtu (Kristo) asiye wa ulimwengu huu. Kama wewe ni mjuvi wa maandiko, kwa nini usingepangua hoja hizo kimaandiko? Ndugu yangu Sungura, mambo mengine unaandika kama kujiaibisha tu, kimsingi unajidhalilisha!! Wakristo tunaoisoma Biblia, tunaamini kuwa kuna ahadi ya kwenda mbinguni, mahali tulikoandaliwa na Kristo. Na huo ndio werevu wa maandiko –wewe unauita ujinga!! Ha ha ha haa!! Kazi kweli!

  Mungu azidi kukupa mafunuo zaidi ya neno lake. Maana kwa mwendo huo, mmh!
  Hekima ni tunu isiyogharimiwa kwa chochote, ni zawadi toka kwa Mungu tu. Huwezi kuipata kwa kupata elimu dunia. Hilo inabidi ulitambue!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 32. Wana wa Mungu , ninapita tu na kuwasalimu wote, natumaini wote ni wazima, tunaendelea kujifunza. nafarijika ninapoona michango na hoja za ndugu zangu kama Kaka Sungura. Ni miaka mingi imepita toka tuwe katika hili group,

 33. Siyi,
  Unatia huruma ndg!

  Huwa unadhani unamwelewa Mungu sawasawa, na unajeuri kweli juwa unamwelewa,lakini hujui vitu vingi sana vya msingi.
  Hebu imagine mtu anayesema anayaelewa maandiko, anausubiria kuuona ufalme wa Mungu siku akifika mbinguni. Ni ujinga ulioje huo. Hujui ufalme wa Mungu ni kitu gani Siyi.
  Ya mbinguni yanakuhusu nini wewe, kwani umeahidiwa kwenda kuishi mbinguni?-Rediculous!

  A coward will always dodge to answer heavy questions!

  Kwa hiyo sihitaji majibu yako Siyi, maana huna hata uwezo wa kujibu moja ya hayo maswali, coz unajua yatakuumbua maana umeshasema uongo, hivyo majibu sahihi ya hayo maswali yataumbua uongo wako juu ya mwaka unaosema ndio wa Mungu!

  Endelea kushindwa jujibu hivyohivyo!

 34. Sungura,
  Kwanza, Shalom! Ukitii masharti, nitajibu maswali yenu nyote. Usipotii, ngoma imepita hiyo!! Wala usiishangalie!! Iache tu iende zake…
  Pili, ni rahisi kufikiri kama unavyofikiri wewe, lakini siyo rahisi kuishi kama mkristo. Kuna watu wengi hufikiri kuwa wao ni wakristo, japo hawaishi sawasawa na Kristo. Halikadhalika Sungura!!!

  Tatu, mnashangaza sana watu kama ninyi mnapobisha kwa mambo ya wazi kiasi hiki. Sisi ni wafusi wa mtu asiye wa ulimwengu. Na ufalme wake (ambao na sisi tunatarajia kukaribishwa kwa huo), sio wa ulimwengu huu!! Japo tunaishi duniani, Kristo alituombea akisema, “Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli” – Yohana 17:14-17. Zingatia mstari wa 16 –“ Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu”.

  Nne, tunapaswa kutumia kalenda za duniani kwa mambo ya duniani. Kwa mambo ya mbinguni, sharti tutumie kalenda ya mbinguni. Na tukiitumia kalenda hiyo tu, ndipo kutimia kwa neno la Kristo kutakuja –“ Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu”, kwa sababu tutakuwa tofauti na ulimwengu kwa mambo mengi sana. Wakristo wote wa kweli, wanapaswa kuishi kwa mujibu wa neno la Kristo, kama Paulo alivyofundisha kwenye wakol 3:2… Tofauti na hapo, ni sawa na -wanawake saba watakaomshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu. – Isaya 4:1. Ni aibu iliyoje, maana watakuwa wamechelewa ajabu!!

  Tano, mwisho, bado ninaishi duniani. Ninafuata kalenda ya duniani kwa mambo ya duniani tu. Ukija kwa habari ya mbinguni, nina kalenda yangu mwanaume! Kalenda ya Biblia. Wewe ukiamua kuchanganya yote kwa mpigo –yaani kalenda ya Mungu na ile ya duniani, poa tu. Nayo ni maisha vilevile, ila sidhani kama utakuwa salama kiroho, maana Biblia imeonya!
  “Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia” –Yohana 15:19
  “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu” –Rumi 12:2.
  Sita, mimi (Siyi), ya Kaisari ninayafanya kama Kaisari alivyosema. Na ya Mungu, ninayafanya kama Mungu alivyoagiza. Sitaki kucnganya yote kwa pamoja!! Hiyo ndiyo habari ya mbinguni!!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 35. Hahaa, Siyi!

  Maneno mengiii, bt zero substance!

  Suala la nani anakwenda jehanam na nani mbinguni kutokana kila mmoja wetu anavyoamini nilishakwambia usubiri wakati ukifika nani atamkuta/atamtangulia mwenzake wapi!

  Ni ujinga sana kuanza kumshambulia mtu kwa kitu ambacho wewe mwenyewe unakiishi.

  Ati unanukuu Kolosai 3:2 -kwamba tuyafikiri yaliyo juu. Unaelewa maana yake au unafurahia tu kunukuu andiko? Yesu akiwa juu unadhani chini hayupo?

  Paul akasema kuwa tusifungiwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa(zingatia maneno ‘kwa jinsi isivyo sawasawa’) -Maana yake ni kwamba kuna kufungiwa nira na wasioamini kwa jinsi ilivyo sawasawa, ndio maana bado tuko duniani.

  Siyo kila kitu hapa duniani ni dhambi, ndio maana jana nikakwambia hapa duniani kuna falme mbili zinafanya kazi, na ufalme mmoja(wa Mungu) unafanya kazi by force.

  Mwaka jana ilikuwa 2015 na mwaka huu ni 2016, hata wewe hilo unalijua, na kwenye madafutari na nyaraka zako umeandika hivyo, hata jana uliandika tarehe za jana(14/01/2016). Kama hujafanya hivyo sema ukweli hapa na useme uliandikaje jana.

  Siyo kila kitu cha kibinadamu ni dhambi, kama ni dhambi mbona watoto wako wanahama madarasa shuleni kwa mujibu wa mpangilio huu wa miaka?
  Ukisema kuwa huu ni mwaka 2016 inakudhuru nini wewe kama msabato labda, je inakulazimisha usisali J’mosi, au inamzuia Mungu kufanya chochote katika majira yake?
  Jifunze kufikiri vizuri, siyo kutokwa mishipa ukikomalia kitu ambacho haki-add value yoyote kwenye maisha ya kitaua

  Kama hutaki kujibu maswali ya msingi acha – who cares, hakuna wa kukubembeleza kujibu, ila msomi mwenye akili atajua tu kuwa unakwepa kuumbuka. Na sidhani kama Lwembe amekuuliza ili kwa kujibu kwako apate kitu cha kumsaidia.

  Tena mengine haya hapa:
  -Ulizaliwa tarehe ngapi?
  -Ulimaliza shule ya msingi mwaka gani?
  -Ulioa mwaka gani?

  Hebu sema huo mwaka wa kimungu yalipotokea hayo matukio kwako!

  15 January,2016

 36. Sungura,
  Kwanza, kwa mtu asiyefikiri sawasawa, anaweza kufikiri kama ulivyofikiri wewe, kuwa nilichokiandika hakihusiani na mada na ni upotezaji wa muda –ujinga! Mara nyingi, nimekuwa nikikwambia kuwa, mambo mengine, huibuka ndani ya safari. Nilipokuona umeniambia “heri ya Mwaka Mpya 2016”, nilijua kuwa pamoja na kujiita mjanja, lakini bado ndume (ibilisi), imekushikilia vizuri na unaendelea kuzienzi sera zake. Kama kukusaidia kwangu ili ujinasue unakuita ni ujinga, basi msemo wa waswahili haukukosewa –‘Shukrani ya Punda ni mateke’!!
  Pili, kama unafikiri kuwa wakristo nao wanapaswa kufikiri kama ulimwengu ufanyavyo, bado una safari ndefu ya kwenda. Tambua kuwa tuko duniani, lakini KIROHO, hatupaswi kutenda na kuwaza kama wafanyavyo walimwengu. Sungura, tunapaswa kuyafikiri yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi –Kolos 3:2. Hatupaswi kutenda kama walimwengu -wala kuifuatisha namna ya dunia hii; bali tugeuzwe kwa kufanywa upya nia zetu, tupate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu warumi 12:2. Walimwengu hufanya mambo yao machoni pa watu, kusudi mtazamwe na walimwengu wenzao kuwa hawana tofauti nao. Kwa Mkristo wa kweli, inabidi iwe ni tofauti, kwa maana akifanya kama hayo, hapati thawabu kwa Baba yake aliye mbinguni. Mathayo 6:1.
  Tatu, kusema “ee mfalme uishi milele na heri ya 2016”, havina uhusiano kabisa! Kwetu huko, mwanamke akiitwa na mtu yeyote, huitika ‘lama’ maana uishi (milele). Unataka kusema kuwa lakabu hii –lama inafanana na heri ya 2016 kwa Mkristo? Ee mfalme uishi milele na lama, havina athari yoyote kwa maisha ya Mkristo. Na haviwezi kumfanya mtu ashindwe kumjua Mungu na taratibu/sheria zake. Kimsingi maneno/lakabu hizi, zili/zinazonesha kuwa, mwanadamu kwa kuiasi sheria ya Mungu, sharti afe. Ila suala la kutakiana maisha marefu ni jambo jema tu lakini halina maana ya kwamba, wanaoitwa hivyo au wanaoitikiwa hivyo, huishi milele kweli! Hii ya heri 2016, inakuondoa kwenye kalenda sahihi ya Mungu -Biblia! Na kimsingi, Mkristo hupaswi kuishikia bango kuuuubwa eti mwaka mpya/mwisho wa mwaka kwa kalenda hizi za kidunia! Tukifanya hivyo, tunatimiza unabii wa Biblia unaosema “… naye (ibilisi) ataazimu kubadili majira na sheria…”. Majira alishabadilisha, ndiyo maana nakupigieni kelele hapa ili mzinduke. Kwa fikra rahisi tu, mjiulize, kwa nini saa moja inaandikwa 7? Saa mbili inaandikwa 8? Au kwa nini kila penye utaratibu wa Mungu, shetani ameugeuza miguu juu kichwa chini?, miezi nayo je? Cheki hiyo maana nilikundolea japo kidogo.
  Nne, sheria kashabadilisha, ndiyo maana leo wakristo wengi, wanasali jumapili, bila ya hata kujua masikini! Na cha ajabu ukiwaambia, wengine ni wabishi sana kama Sungura! Kupona kwenu ni mpaka Mungu aingilie kati tu, vinginevyo, subirini jehanamu ya moto! Na mbaya zaidi, tumeshawaambia mapema lakini mkashupaza shingo tu! Kimdingi mmejipalia mkaa ninyi wenyewe!! Kazi kwenu!!
  Tano, Kaisari yeyote akienenda kinyume na taratibu za Mungu, mtupilie mbali! Heshima na haki zake tutampa kama Kaisari. Lakini akianza kutuongoza kinyume cha neno la Mungu kisa yeye ni Kaisari, akafie mbali na ukaisari wake!
  Sita na mwisho(si kwa umuhimu), maswali yako na matusi yako sishughuliki nayo kwa kweli!! Kama unadhani kuwa rohoni ni mambo halisi na kuwa mwilini si mambo halisi, endelea na uelewa huo! But mimi najua, Carnal mind is always against Spiritual mind! Sasa siwezi kujadili mambo ya rohoni kwa kuyahusianisha na yale ya mwilini! Kama una ubavu huo, wewe fanya!
  Swali la Lwembe kama na wewe unataka ujifunzemo, tii sharti nililompa, then nitakujibuni! Au tii sharti hilo kwa niaba yake, ndipo nitakujibuni! Upo hapo?
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 37. Siyi,
  Kuna vitu vingine unafanya kwa kuwa tu unapungukiwa hekima. Ivi kuandika mkeka mrefu hivyo wa maelezo kuhusu majira, wakati ni kitu kilicho nje ya mada maana yake nini kama si kukosa utija kwenye kufikiri!!

  Haya mambo ndo mimi huyaita ya kijinga na kipuuzi halafu unanilaumu kuwa nimekutukana, lakini unapaswa kuwa mtu mwenye fikra yakinifu kabla hujafanya jambo.

  Kama unadhani kuwa huku ni kuunga mkono sera ya shetani, kesho nenda ofisini kwenu au kokote au bank ukitakiwa kujaza form yoyote kwenye sehemu ya tarehe na mwaka andika tarehe na mwaka unaojua wewe usiandike 2016 kisha submit hiyo document usubiri huduma.

  Mkristo yeyote mwenye kujitambua anajua kuwa tunaishi katika ulimwengu ambao mkuu wake ni ibilisi, lakini bado ndani ya giza la ibilisi umeingizwa ufalme wa Mungu,na nuru ya ufalme( wa Mungu) inaangaza, na ndio maana Yesu akasema ufalme wa Mungu unatekwa kwa nguvu. Ni kwa nguvu kwa sababu kuna upinzani.

  Akina Daniel walikuwa wanasema maneno ya kumtukuza Nebkadneza (ee mfalme uishi milele) maana ndo mfumo walioukuta na haukuwa na madhara yoyote kwao.

  Mimi nikisema kuwa huu ni mwaka 2016 inanidhuru nini, au wewe ukiulizwa kuwa huu ni mwaka gani huwa husemi kuwa ni 2016? Acha unafiki na figisu za kitoto. Ongea mambo yenye hoja za maana.

  Ya Kaizari mpe Kaizari na ya Mungu mpe Mungu (sijui kama unaelewa nini maana yake maneno hayo ktk hili tusemalo)

  Mnafiki wewe, swali la Lwembe liko wazi sana lakini umempa maelezo ya kinafiki na kipuuzi, halafu unajaribu kujenga picha kuwa umemjibu kwa hekima!

  Unamwambia mambo ya rohoni ni ya kufikirika tu,kwamba yeye yuko kwenye ulimwengu halisi (wa mwili), na wewe uko kwenye ulimwengu wa roho.

  Excuse me, wewe Siyi ulitoka lini mwilini ukaenda rohoni, tena kwa usafiri upi? Wewe uko mwilini typical na kuwaza kwako kote kuko mwilini, ndo maana unaleta hoja ya kupinga majira ambayo mwenyewe unayatumia.

  Muongo wewe, nani kakuambia kuwa ulimwengu wa roho ni wa kufikirika na wa mwili ni halisi?

  Hujui kuwa ulimwengu wa roho ni halisi kuliko ulimwengu wa mwili, tena hujui kuwa mambo yote yanayoonekana mwilini yalikuwapo tangu siku zote rohoni? Je hujui ulimwengu unaoonekana ulitokana na usioonekana (wa roho)? Mambo yote ktk ulimwengu wa roho ni halisi!!

  Anyway, jibu swali la Lwembe, acha figisu za rasharasha!

  14 January, 2016

 38. Lwembe,
  Shalom.
  Sina uhakika kama ni busara kujibiwa swali lako na mtu aliye kwenye ulimwengu wa kufikirika tu, maana utapewa majibu ya kufikirika pia. Mambo ya Rohoni ni mambo ya kufikirika tu, japo viashiria huonekana mbashala! Wewe uliye kwenye ulimwengu halisi (wa mwili), nitakujibuje mimi niliye kwenye ulimwengu wa kufikirika (rohoni)? Kazi kweli!
  Anyway, nithibitishie kama inawezekana kwa wewe kuambiwa chochote na mtu aliye rohoni huku wewe ukiwa mwilini!
  Ubarikiwe ndugu!
  Siyi

 39. Siyi,
  Asante kwa kuliweka vizuri swali langu jepesi! ila naona umeamua kujizungusha badala ya kunijibu, jambo ambalo linaonesha kwamba unaishi ktk dunia ya kufikirika!!!

 40. Sungura,
  Siandiki ili kuendeleza mjadala ulioutaka uishe na mimi nikashadidia! Nimevutwa tu kuandika kidogo kutokana na maneno yako. Mimi sijivunii kwa kuwa msabato. Najivunia kwa kumjua Mungu na Mwanaye Yesu Kristo! Nikimjua Yesu tu au Sabato tu bila ya hawa wawili, ni kazi bure!! Kazi bure kwelikweli!!! Najivunia kwa kumjua Mungu japo nazidi kumtafuta zaidi kila iitwapo leo!
  Zaidi, nakushangaa zaidi kunipa heri ya mwaka mpya! Mwaka upi Sungura? 2016 au? Kama ulimaanisha 2016, mimi nakupa pole rafiki yangu. Mimi (BINAFSI) huwa sihesabu miaka kama wanavyohesabu walimwengu!

  Kwani Mwaka Una Siku Ngapi??
  Ukisoma historia ya mambo ya kale kabisa(kipindi cha miaka 3000’s BC,), kumbukumbu nyingi za mambo hayo, zinaonesha kuwa, dunia hadi leo ina miaka zaidi ya 6,000 tangu kuumbwa kwake. Na tangu mwanzo, miaka ilikuwa ikihesabiwa kutoka juu kushuka chini hadi kipindi cha Kristo. Mabadiliko mengi ya wakati na majira katika ulimwengu huu, yalianza kuonekana kushika kasi kuanzia karne ya nne japo mipango ilikuwepo hata kipindi cha kuzaliwa kwa Kristo. Mpaka leo, mabadiliko makubwa yamefanyika, kiasi kwamba wanadamu wasiomjua Mungu wamebaki njia panda . Na wengine, wamebaki kuunga mkono sera ya ibilisi, jambo ambalo ni hatari sana.

  Biblia Mwongozo Wetu
  Kama wafuasi wa Kristo, Biblia itakuwa ndiyo msingi wetu mkuu kwa mafunuo ya mambo haya ili tuyajue. Tangu uumbaji, nyakati(mida) zilikuwa zikipimwa kwa kutumia mianga ya nuru (mwz 1:14-19) na vizazi vya Adamu. Kibiblia, miezi tunaambiwa ilikuwa na siku 30(mwz 7,8 na ufu 11). Na hakuna msatari ndani ya Biblia unaosema kuwa mwezi una wiki nne tu (yaani siku 28). Biblia iko wazi kwa saa za siku nzima kuwa ni 24(Yohana 11:9), Juma siku 7 na mwezi siku 30 tu na siyo idadi ya wiki ndani ya mwezi bali siku tu.

  Swali la kujiuliza, kwa nini leo kuna tofauti??
  Shetani kupitia mawakala wake(wanadamu waovu) alibadilisha mpango mzima wa Mungu wa majira na sheria ili litimie neno lililotabiriwa na nabii Daniel 7:25( “….naye ataazimu kubadili majira na sheria…..”) . Ndani ya Biblia, mwaka mzima una miezi kumi na mbili tu. Mimi sijaona sehemu ambayo tunaarifiwa kuwa miaka ilikuwa na na miezi zaidi ya hiyo. Mungu aliwafundisha watu kuhuesabu miezi kuanzia mwanzo mpya wa mwezi(mwonekano wa mwezi mpya) hadi mwanzo mwingine. Mungu aliita miezi wa kwanza, pili, tatu nk. Majina ya miezi hii, waliita wanadamu kwa sababu walizoziona wao. Angalia miezi ndani ya Biblia…

  Mwezi wa Kwanza – Nisani au Abibu (Esta 3:7, Nehemia 2:1, kutoka 12:2, torati 16:1)
  Mwezi wa Pili – Zivu au Iyari (1 Falme 6:1, 37)
  Mwezi wa Tatu – Siwani au Sivani (Esta 8:9)
  Mwezi wa Nne – Tamuzi (2 Falme 25:3, Jeremia 52:6, Ezekiel 8:14)

  Mwezi wa Tano – Abi au Av (2Falme 25:8, Hesabu 33:38, Ezra 7:8-9)

  Mwezi wa Sita – Eluli au (Nehemia 6:15, Hagai 1:1, 15)

  Mwezi wa Saba – Ethanimu (1Falme 8:2)

  Mwezi wa Nane – Buli au Cheshvani (1falme 6:38, 12:33)

  Mwezi wa Tisa – Kisleu (Zekaria 7:1, Nehemia 1:1)

  Mwezi wa Kumi – Tebethi (Esta 2:16)

  Mwezi wa Kumi na Moja – Shebati (Zekaria 1:7)

  Mwezi wa Kumi na Mbili – Adari (Esta 3:7, Ezra 6:15)
  Hii ndiyo miezi ya Biblia ambayo hata watakatifu wa zamani waliifahamu vizuri. Shetani aliibadilisha tu na kuichanganya sana ili wanadamu wachanganyikiwe na kufuata mawazo yake ya kuudanganya ulimwengu. Tunamshukuru Mungu ametupatia NURU, nuru ambayo ni neno lake. Nasi tunaotembea katika hiyo NURU, sharti tuuone udanganyifu wake(ibilisi) huo na kisha tuukatae kabisa. Angalia alivyochanganya mianzo na miisho ya miezi. Mwezi wa shetani(kalenda ya mfumo wa Kirumi) ulianzia katikati ya mwezi wa kibiblia na kuishia katikati ya mwezi mwingine wa kibiblia. Angalia…
  Mwezi wa Kibiblia Urefu wake Kalenda ya Kirumi
  1. Nisani Siku 30 March-April
  2. Zivu/ Iyar Siku 30 April-May
  3. Siwani/ Sivan Siku 30 May-June
  4. Tammuzi Siku 30 June-July
  5. Abi/ Av Siku 30 July-August
  6. Eluli Siku 30 August-September
  7. Ethanimu/ Tishri Siku 30 September-October
  8. Buli/ Cheshvan Siku 30 October-November
  9. Kisleu Siku 30 November-December
  10.Tebethi/ Tevet Siku 30 December-January
  11. Shebati/ Shevat Siku 30 January-February
  12. Adari Siku 30 February-March

  Hadi kufikia kipindi cha kuzaliwa kwa Kristo, vuguvugu la kubadilisha miezi hii lilikuwepo japo lilikuwa halijashika kasi. Baada ya Yesu na mitume wake (thenashara) kupita, mabadiliko rasmi ya miezi hii yalifanyika miaka ya 300’s AD(karne ya 4). Kipindi hiki ndipo tunawaona akina Julias Caesaria na wengine wengi waliofuata (utawala wa Rumi), wakibadilisha taratibu nyingi sana(majira na sheria za Mungu) ndani ya Neno la Mungu. Ukisoma Katheksimu ya Waumini kipengele cha sheria za Mungu, utaelewa ninachokisema hapa. Hawakubadilisha miezi tu. Walibadilisha Saa(ndiyo maana leo ukiambiwa ni saa 1:oo asubuhi, itasomeka 7:oo asubuhi), Mianzo ya siku (Badala ya siku kuanza jua linapochwea, wao wakaamua siku ianze usiku wa manane), Siku za juma(ya kwanza ikawekwa ya mwisho na ya mwisho ya kwanza), Siku za miezi(badala ya mwezi kuwa na siku 30, wakaamua miezi mingine iwe na siku 28, 29, 30 na 31).
  Shetani amefanya haya yooote kwa makusudi kabisa. Ameiba miaka mingi ya Mungu ili tusifikiri kuwa muda umekwisha sana na Yesu yu karibu kuja kulichuka kanisa lake. Kwa mf. Ukichukua ile miaka 5 (kwenye idadi yake ya siku kwa mwaka ambayo ni 365¼) na ukazidisha na mwaka wa leo kuanzia karne ya nne, utapata miaka mingi sana aliyoiba shetani. Sasa tufanye kidogo..

  Tuanze na miaka 2016AD-300AD= 1716
  Chukua miaka 1716 x siku 5¼ = 9009. Hizi ni siku (9009) zilizopotea! Tukizichukua na kuzigawa kwa siku 360, tutapata miaka 25.025. Sasa tuchukueu mwaka tuliopo 2016+25.025 = 2041.025. Ajabu!! Shetani ametupumbaza saana! Kwa sasa tulipaswa kuwa kwenye mwaka huu wa 2041.025, badala ya 2016 tu. Hii ni kwa mujibu wa Biblia na historia yeyenyewe! Mungu atusaidie kubaini udanganyifu huu wa ibilisi!!
  Ukiangalia historia ya wenzetu wa Gharika, ilikuja miaka 2000 tangu kuumbwa kwa dunia. (Sodoma, Gomora na ile miji mingine mitatu), waliangamizwa miaka 2000 baada ya gharika. Na miaka 2000 ilipita hadi kipindi cha Yesu kuzaliwa. Tangu hapo hadi leo, ni miaka 2000 tena na zaidi…(miaka 13 ya rehema).

  Sherehe ya Mwaka Mpya
  Je, tunaweza kusema sasa kwa miaka hii kuwa leo ni mwisho wa mwaka au mwanzo wa mwaka? Kwa misingi ipi? Je, tunaweza kuikokotoa ile miaka yoote aliyoiba shetani, halafu tukafahamu miisho na mianzo ya miaka mipya kwa leo?? Inawezekana kweli? Tukiweza, na tufanye hivyo kama Wakristo. Tukishindwa kuipata vizuri na kwa usahihi wake, NI HERI TUKAKAA KIMYA KULIKO KUENDELEA KUDANGANYA WATU kuwa leo ni mwisho au mwanzo wa mwaka mpya. Mungu anatushangaa sana wengine tunapotangaza hadi makanisani, eti sabato/ibada ya mwanzo wa mwaka au mwisho wa mwaka. Ni lazima tuwe tofauti na wengine(wasiomjua Mungu). Na wakituuliza sababu, tuwaambie tu!! Hakuna haja ya kuwapigia watu filimbi ya shetani ya kuwapeleka watu jehanamu. Heri tuendelee kung’ang’ana na Bwana wetu. Tuko kwenye kipindi cha mwisho sana. Ni muda wa kumtafuta Mungu tu. Si muda wa kuchezacheza na kutaka kufanana na dunia. Moto anaouzungumzia Mtume Petro(2 Petro 3:7) u karibu kuichoma dunia na dhambi zake. Utakuwa wapi wewe. Mtafute Mungu!! Tafuta kweli ya Neno lake ukaokolewe!!
  Be, a different person plz!
  Ukifanya kama wafanyavyo walimwengu, wewe siyo wa Kristo, japo wajidai kuwa!
  Jitahidi!
  Siyi

 41. Sawa Siyi,

  Wewe jivunie usabato wako, mimi sina cha kujivunia ila Yesu, kanitoa mbali sana mpaka kuja kuwa huyu mtu niliye leo, najua nilikuwaje na leo nikoje.

  Ukiwa na akili iliyo sawa ukijua kitu utajua kuwa unajua, na usipojua utajua kuwa hujui!

  Happy new year!

 42. Sungura,
  Mpaka sasa nakuelewa vizuri sana rafiki yangu! Hata kama ukielewa jambo jipya, huwa hutaki kuappreciate!!! Ni tabia yako hiyo!! Tangu mwanzo, kila unapopata jambo jipya, mimi huwa nakusoma vizuri sana!! Sina uhakika na hicho unachokisema kwa sasa. Binadamu hutazama kwa nje, bali Mungu huuchunguza moyo!!
  Kijana, wasabato wengi, huwa hawabahatishi kuhusu mambo ya imani yao!!! Tuko makini kiasi hicho!
  Siyi

 43. Siyi,

  Nilivyokuwa naelewa ndo hivyo nimeendelea kuelewa, sijaanza kuelewa jana au leo. Najua unaujua msimamo wangu juu ya hilo, nami naujua wa kwako!

  Niko thabiti.

  Ubarikiwe!

 44. Sungura,
  Nashukuru kwa kulitambua hilo! Nina imani utakuwa umeelewa vyema! Mungu akuongoze katika yote yenye kibali mbele za macho yake. Amina.
  Siyi

 45. Sungura,
  Samahani rafiki yangu. Siku hizi nimekuwa nikichelewa sana kujibu mapachiko yako. Hadi nafedheheka mara nyingine! Nisamehe bure ndugu yangu. Kuna mambo fulani yalinibana. Tuombeane tuzidi kujadili neno la Mungu.
  Nimesoma majibu yako nikahuzunika tena., kwamba ulikataa kusoma kitabu. Sina maana kwamba ungepata majibu yote kwenye kitabu hicho. Hasha! Lakini kingekusaidia kupata uelewa fulani. Hata hivyo, hatuwezi kuvipuuza vitabu, maana ndivyo vinavyotupa maarifa. Hata walimu wetu, wachungaji wetu na wainjilisti hutufundisha kwa kutumia vitabu! Hivyo hatuwezi kuvikwepa vitabu rafiki yangu. Vipo ili tuvisome na kuvichambua!! Jitahidi kusoma kwa umakini ili unielewe rafiki yangu.
  Agano jipya nalijua kidogo. Kwa kweli silijui saaana! Hata Agano la Kale nalo, nalijua kidogo tu, na si saana kama unavyodhani!! Kwa hiyo nuru ndogo niliyonayo kwenye maagano haya, ndiyo inayonisukuma kushare na ninyi mambo haya! Na dhana kubwa kuliko zote kuhusu maagano haya, ni ile dhana ya AGANO LINALOHUSU WOKOVU WA MWANADAMU!! Hili ndilo msingi wa maagano yote aliyowahi kuyafanya Mungu na watu wake (anuai) ndani ya Biblia. Nje ya kujadili agano la wokovu, tunacheza sindimba tu na tutaishia kutoka na majeraha!!
  Nimeona niseme maneno hayo maana huenda tunajadili vitu viwili tofauti na wewe! Mimi najadili Agano la wokovu alilolifanya Mungu na Adamu pale Bustanini kabla ya dhambi na likaendelea kwenye vipindi tofautitofauti mpaka sasa hivi. Mungu anamwambia Adamu asiwe na miungu mingine ila YEYE –asisikilize sauti au mamlaka ya kiumbe kingine tofauti na Mungu. Kimsingi kwa kipindi hicho halikuonekani kuandikwa popote japo lilikuwepo. Uzima au maisha ya Adamu, yalitegemea kwenye utii wake kwa maagizo ya Mungu. Na Mungu angeendelea kumtimizia yote kama Adamu angetii!
  Baada ya dhambi, Mungu analitengenezea/kuliongezea by laws zingine. Agano bado ni lilelile, lakini linaongezewa kanuni tu ambazo kimsingi, zilionekana kuwa ngumu na nzito. Zingatia, si Agano lililoonekana kuwa zito/gumu, bali ni zile by laws tu –makafara ya wanyama n.k, japo zenyewe hazikuwa sehemu za Agano hilo maana lilikuwepo hata kabla ya hizo by laws. Haukuwa mpango wa Mungu kumpa mwanadamu by laws nzito na ngumu kuzitekeleza kwa ajili ya wokovu/usalama wake, bali by laws zilikuwa ni habari njema (Injili), ambayo ingekuja kudhihirika baadaye, jambo ambalo watu wengi huwa wanapingwa chenga hapo. Mwandishi mmoja anasema, namnukuu,
  “Hebrews 9:1 is a text that hinders many from seeing that all God’s blessings to man are gained by virtue of the second covenant, and not by the first. That text reads: “Then verily the first covenant had also ordinances of divine service, and a worldly sanctuary.” This, together with the fact that when men complied with these ordinances of divine service, they were forgiven (Leviticus 4), seems to some conclusive evidence that the old covenant contained the gospel and its blessings. But forgiveness of sins was not secured by virtue of those offerings; “for it is not possible that the blood of bulls and of goats should take away sins.” Heb. 10:4. Forgiveness was obtained only by virtue of the promised sacrifice of Christ (Heb. 9:15), the mediator of the new covenant, their faith in whom was shown by their offerings. So it was by virtue of the second or new covenant that pardon was secured to those who offered the sacrifices provided for in the ordinances of divine service connected with the old or first covenant.
  Moreover, those “ordinances of divine service” formed no part of the first covenant. If they had, they must have been mentioned in the making of that covenant; but they were not. They were connected with it, but not a part of it. They were simply the means by which the people acknowledged the justice of their condemnation to death for the violation of the law which they had covenanted to keep, and their faith in the mediator of the new covenant.
  In brief, then, God’s plan in the salvation of sinners, whether now or in the days of Moses, is: The law sent home emphatically to the individual, to produce conviction of sin, and thus to drive the sinner to seek freedom; then the acceptance of Christ’s gracious invitation, which was extended long before, but which the sinner would not listen to; and lastly, having accepted Christ, and being justified by faith, the manifestation of the faith, through the ordinances of the gospel, and the living of a life of righteousness by faith in Christ”
  Ndani ya New Testament, hatukuti Agano Jipya! Hasha! Agano ni lilelile likiwa limetenegenezewa daraja –Kristo aliye mpatanishi kati yetu na Mungu. Ili tuwe sehemu ya watekelezaji wa Agano hilo(la zama na zama), sharti tumpokee Kristo kwanza kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu. Kimsingi hii nayo inaonekana kama ni by law mpya lakini ni udhihiriisho wa by laws za makafara ya huko –Old Testament. Tukimpokea huyo, kauli yake ni moja tu – “Mkinipenda, mtazishika amri (AGANO) zangu” Yohana -14:15, kauli ileile aliyoitamka Mungu mwenyewe kwa Israel ya zamani akiwahubiri “ agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe…” -Torati 4:13. Kwa hiyo kile ambacho kimekuwa kikifanyika, si Mungu kuleta Agano Jipya (kama ambavyo watu wengi hufikiri), bali amekuwa akilibadilishia by laws tu (renewing it), Agano likiendelea kubaki lilelile. Mwandishi mmoja anasema, namnukuu
  “The concept of covenant renewal, as demon¬strated by the various covenants in the Old Testament, is not such a strange one as it is often portrayed…. God’s covenant is like a house that He has rented out to His people, giving them a rental contract that stipulates the conditions of occupation. However, the renters, God’s Old Testament people—Israel—disregarded the contract and began to demolish the house.
  Through the centuries, God sent His prophets, and at various moments, He renewed the contract, not because the contract was deficient but because the occupants did not adhere to it and even tried to change it. Eventually, God had to make a new contract, the new covenant, which is still based on the same conditions, but it is now ratified by Christ’s blood; and thus, it is the most complete manifestation of the eternal covenant. What the Old Testament covenant phases were anticipating, the New Testament covenant completes in Christ. This is just an analogy (with some limitations), but it can help to illustrate to the class the idea of the eternal covenant in its phases”.
  Hata leo bado Mungu anawatumia akina Siyi kuwajulisheni habari za Agano la wokovu kati ya Mungu na watu kuwa halijabadilika!! Takayetii masharti ya Agano hili, ataokolewa. Atakayekaidi, moto unamgonja!!
  Hiyo ndiyo habari ya mjini kaka.
  Siyi

 46. Siyi,

  Sorry, sms yangu ina makosa mengi ya kisarufi, hata kimaana pia. Kwa mfano nimekosea hata jina lako, badala ya Siyi nikasema Siyo.

  Kwa hiyo naedit na kutuma tena:

  Sihitaji kusoma hicho kitabu kujifunza kitu ninachokijua tayari. Kama unadhani sijui na nimekosea kitu kwenye majibu yangu wewe thibitisha huko kutokujua kwangu, au sema ambacho hicho kitabu kimekufundisha.

  Siyi agano jipya hulijui, na huna ujasiri wa kulichambua. Ulichonacho ujasiri wewe ni agano la kale.

  Ni uelewa ndogo sana kufikiri kuwa agano linaweza kutekelezwa na upande mmoja tu kati ya pande mbili zilizoingia hilo agano.

  Mimi nimekwambia agano hutekelezwa na Mungu pamoja na wanadamu kila upande kwa kufanya lililo upande wake, wewe unasema Mungu tu ndo hutekeleza agano. Ni akili kweli hiyo!?

  Ndo maana hufika wakati naona napoteza muda kujadili ishu zenye akili na wewe.

  Kingine usichokijua ni neno Milele. Kasoma maana yake kwa upana ili uondokane na maana finyu ya hilo neno mahali mbalimbali lilipotumika kwenye maandiko.

  Asante

 47. Siyo,

  Sihitaji kusoma hicho kitabu kujifunza kitu ninachokijua tayari. Kama unadhani sijui na nimekosea kitu kwenye majibu yangu wewe thibitisha huko kutokujua kwangu, au sema ambacho hicho kitabu kimekufundisha.

  Siyo agano jipya hulijui, na hina ujasiri wa kulichambua. Ulichonacho ujasiri wewe ni agano la kale.

  Ni uelewa ndogo sana kufikiri kuwa agano linaweza kutekelezwa na upande mmoja tu kati ya pande mbili zilizoingia hilo agano.

  Mimi nimekwambia agano hutekelezwa na Mungu pamoja na wanadamu kila kwa kufanya lililo upande wake, wewe unasema Mungu tu ndo hutekeleza agano. Ni akili kweli hiyo.

  Ndo maana hufika wakati naona napoteza muda kujadili ishu zenye akili na wewe.

  Kingine usichokijua ni neno Milele. Kasoma maana yake kwa upana ili uondokane na maana finyu ya hilo neno mahali mbalimbali lilipotumika kwenye maandiko.

  Asante

 48. Sungura,
  Nakushauri usome kitabu hiki; Calvary at Sinai by Paul Penno. Kitakusaidia sana kuelewa jambo hili rafiki yangu. Maana unadhani unaelewa kumbe sivyo!
  Mungu akubariki sana.
  Siyi

 49. Siyi,

  Nafikiri umeelewa vizuri ukweli niliouweka bayana kuhusu tofauti ya Covenant na Testament!

  Hilo ndo la msingi!

 50. Sungura,
  Nashukuru sana kwa majibu yako mazuri kuhusu COVENANT na TESTAMENT. Kimsingi umejibu kwa jinsi unavyoelewa wewe, ya kwamba, msemaji wa Convenat huwa ni Mungu na mtekelezaji wa Testament ni wanadamu, kama ulivyosema “Kwa hiyo tunaposema Old Testament tunaongelea mambo mawili; kwanza tunaongelea Agano (Covenant) lenyewe na ushuhuda wa jinsi hilo Agano lilivyotekelezwa na pande zote mbili, yaani Mungu na watu wake.”
  Kimsingi, sidhani kama ulikuwa sahihi sana. Mimi ninavyoelewa, Mungu ndiye anayetoa Convenant na ndiye anayetestify pia, maana hakuna tofauti kati ya mambo hayo mawili kwa maana ya maandiko. Ni kweli kuwa kuna maagano mengi ndani ya Biblia kati ya Mungu na watu wake mbalimbali. Agano tunalilongelea sisi ni agano la milele alilolifanya Mungu na Israel pale mlimani Sinai. Hili ndilo agano ambalo limetajwa ndani ya Biblia zaidi ya mara 158 idadi ambayo ni kubwa zaidi ukilinganisha na maagano mengine.
  Hili lilijulikaana kama ni Agano la milele (amri kumi ikiwemo Sabato ya siku ya Saba –Jumamosi) Kutoka 31:16. Kumbuka kuwa maagano mengine Mungu alifanya na mtu mmojammoja. Hili agano la milele alilifanya na taifa zima la Israel. Hivyo ilimaanisha kuwa, lilikuwa ni agano la milele kwa Israel ya kimwili pamoja na Israel ya kiroho, maana Biblia inasema, “Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu” – Wagalatia 3:7.
  Zingatia:
  a. Agano hili kwa mara ya kwanza(old convenant), lilijikita kwenye utendaji (uzingatiaji) wa hukumu –lilikuwa ni agano la vitendo zaidi vya uchinjaji wa wanyama na upondwaji mawe/uuaji wa wadhambi!
  b. Agano jipya, limejikita kwenye imani tu –kwa maana kwamba Yesu aliondoa uchinjaji wa wanyama na upondwaji mawe, japo msingi wa agano ni uleule, yaani utii wa sheria ya Mungu!
  c. Kilichobadilika si agano wala testament, isipokuwa ni kuondolewa kwa utekelezaji wa hukumu tu na makafara! Kwa maana Convenant (Kiebrania –oth, diatheke au berith) ndiyo Testament (Kigriki- diatheke).
  Old Convenant na Old Testament aliyoifanya Mungu kati yake na Israel mlimani Sinai ni sawa na New Convenant na New Testament iliyoko katika Israel ya kiroho ya leo! Hivyo agano takatifu na la milele kati ya Mungu na watu wake ni (kuanzia zamani na hata leo) ni Sheria ya Mungu – Amri 10 za Mungu. Mtu yeyote anayepanga kuja kuishi na Mungu kama mwana wake, hawezi kulikwepa agano/testament hili. Piga ua kaka!! Liko vile na litaendelea kuwa vile siku zote.
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 51. Sungura,
  Kwa niaba ya Siyi napenda kukushukuru saaana kwa majibu mazuri na ya kina yenye kuufunua msingi imara wa wokovu uliojengeka juu ya ufahamu wa mambo hayo kulingana na Programu ya Mungu kwa kadiri alivyojifunua ktk Covenant na kujidhihirisha wktk Testament!!!

  Nafahamu kwamba haya ni mambo mazito, yaani the Deep things of God, ambayo dini nyingi haziyafahamu zaidi ya kuendelea na mambo yao, hivyo jitihada yako ina faida kubwa sana capo unapowaondolea wapendwa pazia la dini na kuwafunulia ile Kweli!

  Gbu!

 52. Siyi,

  Kule kusema kuwa Testament iko ndani ya Covenant, lakini Covenant haiko ndani ya Testament nilimaanisha hivi;

  Testament huja tu kuthibitisha Covenant, hivyo bila kuwepo kwanza Covenant, Testament haiwezi kutokea.

  Kwamba, Mungu alipomwambia Nuhu atengeneze safina utaona kuwa suala zima la Agano liko kwenye Mwanzo 6 kuanzia verse 13. Hapo Mungu anampa Nuhu msingi wa agano, Kitu cha kufanya, jinsi ya kufanya, na kumwahidi atakachomfanyia akitekeleza alichomwagiza.

  Testament inakuja kuanzia sura ya 6:22 na kuendelea, ya kitabu cha Mwanzo, ambapo tunaona jinsi Nuhu alivyotekeleza alichotakiwa kufanya, na jinsi Mungu alivyotekeleza alichoahidi atafanya, pia jinsi tukio zima lilivyofanyika.

  Kwa mfano ukiangalia Mwazo 6: 20, utaona Mungu anamwambia Nuhu aingize kwenye safina viumbe vya kila aina +ke na +me.

  Lakini ukisoma sura ya 7: 2, unaona utekelezaji wa hilo una mambo ya ziada ndani yake. eg; wanyama safi wawe pair sabasaba, wasi safi ndo wawe waili tu( pair moja), ambapo kimahesabu utagundua kuwa kama kulikuwa na ng’ombe kwenye safina walikuwa ng’ombe 14 jumla, njiwa nao walikuwa 14. Lakini mbwa walikuwa wawili tu!

  Kwa hiyo bila Covenant hakuna Testament!

 53. Sungura,
  Nashukuru ndugu yangu. Najua ubusy ni jambo la kawaida sana. Na kuwa busy ni muhimu pia. Nimejitahidi kusoma mchango wako, kidogo nielewe lakini mwishoni nikapotea njia. Umesema,
  “Testament iko ndani ya Agano, lakini ndani ya Agano hakuna Testament maana Testament huja kuthibitisha utekelezaji wa Agano!”
  Hapa kimsingi umeniacha. Kama utapata muda, nitashukuru ukija na substantials zenye rejea za uga husika. Maana secular references, kwa kweli zinaweza kukupoteza, lakini bahati nzuri, kuna religious references kama vile Kamusi za Biblia, Ensaiklopidia za Biblia, Biblia yenyewe n.k., tafadhali onesha huko kwa ajili ya kuthibitisha hoja zako. Aidha, kama ni uelewa wako, wewe sema tu vilevile maana hata mawazo yako, nayaheshimu pia.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 54. Siyi,

  Hivi ndivyo ninavyoweza kuiweka: Sintazungumzia usheria wa hayo maneno kama yalivyo kwenye kamusi, maana ni maneno yaliyo katika rejesta ya kisheria. Kwa hiyo sintatumia hiyo misamiati ya kisheria maana iko ki-secular zaidi. Lakini nitajikita kwenye application zake kibiblia.

  Covenant: Ni agano kati ya Mungu na watu (watu wake), lenye kuonesha vile ambavyo Mungu atafanya kwao, na ambavyo anawataka wao wafanye.
  Mfano: Agano la Mungu na Nuhu, Agano la Mungu na Ibrahim, Agano la Mungu na Israel kupitia Musa.

  Testament: Ni ushuhuda, uthibitisho au udhihirisho wa utekelezaji wa yale ambayo Mungu alisema atatenda kwenye agano (Covenant), na jinsi ambavyo mtu anayehusika kwenye hilo agano alitekeleza yale ambayo Mungu alimtaka atende.

  Kwa hiyo tunaposema Old Testament tunaongelea mambo mawili; kwanza tunaongelea Agano (Covenant) lenyewe na ushuhuda wa jinsi hilo Agano lilivyotekelezwa na pande zote mbili, yaani Mungu na watu wake.

  Halikadhalika tunapoongelea New Testament, tunaongelea Agano (Covenant) ambalo linaambatana na kuzaliwa, kufa na kufufuka kwa Yesu ( Mt26:27). Lakini pia tunaongelea habari za mambo yaliyofanyika kwa mikono ya mitume na wengine, katika kutekeleza yale ambayo Yesu aliagiza kama sehemu ya Agano.

  Naweza kuhitimisha hivi;

  Testament siyo agano, ila ni ushuhuda, udhihirisho, au uthibitisho wa jinsi Agano, yaani Covenant lilivyo/ linavyo – tekelezwa na pande mbili zinazohusika, yaani Mungu na mtu (watu).

  Testament iko ndani ya Agano, lakini ndani ya Agano hakuna Testament maana Testament huja kuthibitisha utekelezaji wa Agano!

  Ngoja nikomee hapo!

 55. Sungura,
  Sina uhakika kama ulinielewa kaka. Naomba nirudie tena. Nakuomba unifundishe tofauti iliyopo kati ya Convenant na Testament, basi! Mijadala na maswali mengine kwenye mada hii, yataendelea baada yaw ewe kutoa lecture. Sawa mzee?! Nakungoja.
  Siyi

 56. Lwembe,
  Ha ha ha ha haa!!
  Mmmnh, na wewe ndugu yangu, kila ukiibuka huachi kuja na vijembe! Mimi sina akili ya kusoma, kuona, kuonja, kusikia, kuhisi au kunusa nikapa ufahamu hadi nidese toka kwa watu wengine? Aliyekwambia kuwa mimi huwa nahubiri nilichokisikia kwa mchungaji wangu ni nani? Au unabashiri tu? Una matatizo kweli kaka.
  Nimekusoma vyema lakini safari hii umeongea hoja ambazo haziwiani na aya ulizokuwa unanukuu. Sina uhakika kama uliandika ukiwa sawa. Hebu rudia tena kukisoma ulichoandika ili uone kama ulikuwa fit.
  Injili ya Kristo, huwezi kuielewa kama bado unaamini kuwa Hawa na Nyoka walikula tunda kwa kufanya uzinzi! Kama unapigwa chenga kwa mambo madogo kiasi hiki, sembuse mambo makubwa yahusuyo wokovu…. si ndo basi kabisa!!?? Nakupa pole. Nenda ukaoge mtoni mara saba, nawe utapona, ukoma wa kiroho. “Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.” Ufunuo 3:18.

  Neema ya Bwana ikufunike
  siyi

 57. Ndg Siyi,

  Ebr. 13:8 “YESU KRISTO NI YEYE YULE, JANA NA LEO NA HATA MILELE.”

  Tukimfuata mtume Paulo, tutajua alifikaje hata kumsema Bwana Yesu hivyo!
  Kielimu ya Torati, hakusoma ktk shule za kata au ktk “vyuo” vya upenuni mwa nyumba kama hivi vya madrasa tulivyo navyo leo hii; yeye alisomeshwa ktk shule bora chini ya mwalimu aliyetukuka nchi nzima ktk ukufunzi wa Torati.
  Mdo 22:3
  ” Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi”

  Kupitia elimu hiyo, yeye alimjua MUNGU ya kwamba ni Roho, na hata jinsi alivyojifunua alipowaongoza Israeli kutoka Misri akiwa ktk nguzo ya wingu na nguzo ya moto:
  Kut 13:21
  ” BWANA naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na usiku, ndani ya moto mfano wa nguzo”

  Ndipo alipopigwa kwa ile nuru kutoka mbinguni yeye alliitambua hiyo kuwa ni BWANA, lakini alipaswa kujua kwa uhakika ndipo akaiuliza ile nuru:
  Mdo 9:3-5
  ” Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.”

  Na alipofikia KUOKOKA, Injili aliyohubiriwa na mtumishi wa kweli ndo hii hapa:
  Mdo 9:17, 20
  “Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.”
  Mdo 22:14-16
  ” Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, na kumwona yule Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake. Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia. Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina la Bwana.”

  YESU KRISTO JANA – Kut 13:21 ikijitambulisha na Mdo 9:5

  YESU KRISTO LEO – Mdo 22:14-16 ongeza juu yake Injili iliyokuwa ikimuudhi sana anapoisikia kutoka kwa akina Petro, Mdo 2:36, 38 ” Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. … Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”

  YESU KRISTO MILELE – Mdo 9:18-20 “… Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; … Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu”

  Ukihubiriwa Injili ya kweli, ukaipokea, ukabatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo ukiziosha dhambi zako, hapo ndipo unajazwa Roho Mtakatifu wa kweli na mambo yote haya utayajua ktk ukamilifu wake. Kinyume cha hapo utakuwa unakariri tu mistari ya Biblia pasi kujua lolote, sana sana uta repeat alichokisema mchungaji wako tu na ukiulizwa ni nini hicho, basi lazima uchapie chapie na kuwa mkali ili kuficha umbumbumbu wako!!!

  Nakutakia “sabato” ya Kiyahudi njema!

 58. Siyi,

  Asante kwa kukubali kuwa hujui tofauti ya COVENANT na TESTAMENT!

  Nijibu na lile swali ambalo nilikwambia uwe specific, please. Wewe ukiitwa mjinga unaona ni tusi wakati ni kivumishi kinachoweza kuthibitika!

 59. SSungura,
  Kwanza nashukuru kwa kuniita mjinga. Hilo halinisumbui hata kama ungelisema mara 1000000000000000…. soma hiyo namba!! Tatizo lako hujui kama hujui, na hii ndiyo shida kubwa kwako kaka yangu.
  Pili, niliyekuuliza habari za Convenant vs Testament ni mimi! Haya hebu ngoja niwe na subira unifundishe tofauti yake, huenda kweli siijui! Karibu unifundishe sasa. Nakusubiri sana. Huenda utanisaidia!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 60. Siyi,

  Get specific, unaposema ” Bila ya fundisho hili la Kibiblia, utaendelea kupiga kelele tu na mapepo ukidhani una nguvu ya Mungu kumbe huna!”
  ulimaanisha kusema kuwa mimi nina mapepo au ulimaanisha nini brother?

  Unajua kuongea na mtu mjingi mara nyingi inasumbua sana, wewe Siyi nishakwambia kwambia ni mjinga mno katika hii anga ya ufahamu wa mambo haya. Ndio maana unajikuta unatumia nguvu nyingi zaidi kuliko maarifa ya kweli ya Kristo.

  *Be open here; Je unakubali kuwa hujui tofauti kati ya COVENANT na TESTAMENT unataka nikufundishe?*

  Maswali yako yote uliyoniuliza yamejificha kwenye jibu utakalojibu hapa!

  Mambo ya Sanctuary unayoyaita kuwa ni fundisho hayapo kwenye maandiko. Ni mapokeo yenu wasabato na ndio maana mmebaki IKABODI, kama mafarisayo vile, ambao walikuwa wanajidai kuwa wanamjua sana Mungu jymbe wamekariri maandishi tu pasipokujua maana ya kilichoandikwa.

  Ndio maana unajaribu kujinadi kwa mafundisho mengi ya watu; mara wanamatengenezo, mara Sanctuary. Ni mstari gani wa maandiko ambako kuna neno ‘wanamatengenezo’, kama siyo man made doctrines ambazo hazina uzima ndani yake!

  Halafu, hakuna fundisho la Yesu ambalo tumelibadili, wala sifa ya Yesu ambayo tumeibadili, ufinyu wako wa kuelewa issues ndo unakupa fikra hiyo hohehahe. Hauna tofauti na waliokuja na magombo yao mkononi wakionyesha mahali ambapo imeandikwa atatokea, wasijui huyo wanayemsonga kwa hila kila siku ndiye, na yaliyoandikwa juu yake yametimia kama inavyotakiwa – Wajinga
  Yesu ni mmoja tu milele yote wala hatakuja mpya.

  Haya niambie sasa kama hujui tofauti ya Covenant na Testament!!

  Wasalaam!!

 61. Sungura,
  Kwanza, nashukuru kwa mara ya kwanza kuonesha kuwa kumbe una kaunyenyekevu Fulani!! Sikujua hilo mapema! Nilidhani wewe ni mtu wa jino kwa jino tu na … Hii nayo ni hatua nzuri kwako. Kazana zaidi!!
  Pili, mimi ndiye niliyekuuliza habari za Agano, toka mwanzo! Nikakuuliza hivi, hebu nieleze maana ya CONVENANT na NEW TESTament!! Ulilala mbele hadi leo. Badala yake unakuja na hoja za mitume kutumia Agano jipya kwenye mafundisho yao, tena unauliza swali eti Agano Jipya liliandikwa lini!!! Sasa, lililoandikwa ni Testament, Convenant au vyote viwili?!! Kimsingi mwanzoni nilikustahi tu rafiki yangu kwa namna jinsi nilivyokujibu kwa kukuuliza vimaswali nikidhani kuwa ungegutuka!! Hata sasa, bado unakuja na hoja ileile tena kwa kunishangaa!! Sasa, nikuulize wewe, hilo ambalo (wewe unadhani) ni new convenat, unajua liliandikwa lini? Na wapi? Na lilianza lini kutumika hasa? Enzi za Mitume, zama za giza, enzi za wanamatengenezo au enzi zako hizi? Kumbuka kuelezea habari za watu ambao walikufa agano la kale dhambi zao zikifunikwa tu na damu za wanyama, je hao pia wanaguswa na agano hili jipya la damu ya Yesu? Hebu fafanua!!
  Tatu, nikushauri tu tena kwa mara nyingine, licha ya kuupuuza mfumo nilioupendekeza kwako ili umjifunze Mungu, kimsingi unapaswa uujifunze tu mfumo wenyewe, maana nje ya huo, hakuna WOKOVU! Kile unachokipaparikia sasa hivi, msingi wake ni SANCTUARY doctrine! Na kwa wooote wanaoukiri wokovu, SANCTUARY ni barabara kuelekea kwa Kristo. Bila ya fundisho hili la Kibiblia, utaendelea kupiga kelele tu na mapepo ukidhani una nguvu ya Mungu kumbe huna! Nisisitize tena kwako kwa mara nyingine, habari za SANCTURY, zimeanzia Mwanzo 3 na kuendelea hadi siku Kristo anakufa msalabani; na bado sasa hivi zinaendelea mbinguni zikifanywa na Kristo mwenyewe kama Kuhani wetu mkuu anayeupatanisha ulimwengu kwa damu yake. “Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu; tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, ALIMOINGIA YESU KWA AJILI YETU, MTANGULIZI WETU, AMEKUWA KUHANI MKUU HATA MILELE KWA MFANO WA MELKIZEDEKI.” Ebrania 6:17-20. Wewe kama unaendele kubisha, endelea kubisha kaka, lakini ukweli ndio huo!

  Tatu, kama Yesu habadiliki, hatakuja mwingine ila YEYE na sifa zake hazibadiliki, kwa nini ninyi mnambadilisha kwa mafunishao yenu? Unaona unavyojigonga sasa?!! Kimsingi unahitaji msaada zaidi ya mtu aliye ICU!!

  Nakuombea tu.
  Ubarikiwe
  Siyi

 62. Siyi..,

  Yesu ni yeye yule jana na leo hata milele,hayo maneno yako kitabu cha Waebrania 13:8

  Nafikiri unachotaka hasa nifafanue ni suala la panga(sword), ambalo halikikuwa ni moja ya vitu ambavyo aliwaambia wanafunzi wasiwe navyo wakati anawatuma kwenda kuhubiri, lakini katika bustani ya Gethsemane akawaambia sasa wanatakiwa kuwa navyo.

  Pointi yangu kubwa ilikuwa ni kufafanua jinsi ambavyo Yesu anafanya kazi kwa mwanadamu ndani ya wakati. Kwamba wakati aliokuwa nao pale Gethsemane haukuwa wakati wa kuendelea kutokuwa na hivyo vitu (mfuko, mkoba, viatu) Luka 22:35-36

  Msisitizo wangu ni kwamba, inposema Yesu ni yeye yule jana leo na milele, kinachosemwa hapo kwa kifupi ni kwamba hatakuja Yesu mwingine, wala sifa zake hazitabadilika.

  Ndo hivyo Siyi!

 63. Siyi,

  Kuwa busy ni sehemu ya maisha, usijali!

  Nikianza na kile ulichoniambia katika paragrafu yako ya mwisho, kwamba kama ninataka kumfahamu vyema Mungu, nianzie Agano la Kale na kisha nimalizie na agano jipya, na kujijifunza mambo sijui ya Sanctuary.

  Kwa unyenyekevu mkubwa kabisa nikwambie kuwa wewe huwezi kunifundisha jinsi ya kumjua Mungu, maana wewe ndo humjui Mungu. Na humjui kwa sababu ya kumjifunza kwa kutumia huo mfumo unaojaribu kuniambia mimi niutumie.

  Swali langu ambalo hukulijibu hapo nyuma, leo ndo nimejua kuwa kumbe kweli lilikuwa swali, maana majibu yako yameonesha kuwa hujui. Ndio maana kumbe ulikuwa umeleta janjajanja kulijibu, mimi bila kujua nikadhani tu umeamua kulipuuza.

  Siyi hujui maana ya Agano( Covenant), ndio maana unadhani kuwa mitume walitumia Agano la kale katika kumhubiri kristo. Kwa akili yako wewe unadhani Agano ni hayo maandishi yaliyoandikwa kwenye magombo, ambayo yamekuja kuunganishwa(compile) na kufanyika kuwa Agano jipya ( New Testament). Pole sana rafiki.

  Hujui hata tofauti iliyopo kati ya COVENANT na TESTAMENT, unadhani Testament ndio Covenant. Soma hivyo vitu utaelewa na bila shaka inaweza kukusaidia usiendelee kusema uongo.

  Ona hapa Testament inavyokwambia; Hebrews 8:13 By calling this covenant “new,” he has made the first one obsolete; and what is obsolete and outdated will soon disappear.

  Anayeyasema haya si yule aliye-discover na ku-compile hii Testament, bali ni yule aliyeiishi na kuitenda hiyo Covenant inayoitwa ‘New'( inasdikiwa ni Paul mtume). Kwa hiyo New Covenant inaanza rasmi wakati Yesu amekamilisha kilichopaswa kukamilishwa (Methew 26:28 This is my blood of the covenant, which is poured out for many for the forgiveness of sins.

  Unachokisema wewe kuwa ”Agano Jipya limekuja kukompailiwa katika kipindi cha kuanzia miaka 100+AD” siyo COVENANT, bali ni ushuhuda wenye kuthibitisha yale yaliyoaganwa kwenye hilo agano (Covenant), na jinsi mitume walivyoyatekeleza.

  Moja ya utekelezaji wa hayo mambo yaliyoaaganwa ni hii hapa: Acts 15: 28 It seemed good to the Holy Spirit and to us not to burden you with anything beyond the following requirements: 29 You are to abstain from food sacrificed to idols, from blood, from the meat of strangled animals and from sexual immorality. You will do well to avoid these things.Farewell.

  Kumbuka debate kubwa hapa ilikuwa ni suala la tohara kama requirement ya lazima katika Agano la kale

  Hujui operations za Mungu katika kitu kinachoitwa nyakati, bali u mbishi tu !!

 64. Sungura,
  Nipo ndugu yangu. Sema tu mara nyingine mambo yanabana hivi, hadi nakosa muda wa kukutana na ninyi katika mijadala maridhawa kama hii. Yote kwa yote, hatuna budi kumshukuru Mungu daima.
  Kwanza, nakuona umelishwa sana doctrine ya jamaa mwanatheolojia niliyemtaja huko juu kuwa ndiye mwansisi wa Dispensationalism! Na utakesha tu na mawazo hayo potovu. Ni vyema ukaelewa kuwa, wakati Mungu anaumba ulimwengu, aliumba kwa lengo gani? Baada ya mwanadamu kuasi, kingefuata nini kwa agizo la Mungu? Matokeo ya kile ambacho kingefuata, yangekuwaje baadaye? Je, hapo nyuma ya wakati, katikati ya nyakati na hata wakati huu, umeshaona Mungu anahukumu kifo cha milele kwa mtu yeyote aliyevunja sheria zozote isipokuwa sheria za maadili? Kuteuliwa kwa taifa la Israel kuwa wafikisha nuru kwa walimwengu wote, kunakuchanganya nini leo na vile alivyoumbwa Adamu na mkewe na kuambiwa zaeni mkaijaze nchi? Kwani Mungu alishindwa nini kuumba wanadamu wengi tu na badala yake anawapatia wanadamu jukumu la kuzaana? Au Yesu kilimshinda nini kuja duniani kwa wanadamu wote –akaonekana amezaliwa, kukua, kuuwawa, kufufuka na kupaa mbinguni na badala yake anakuja kwa kitaifa kimoja tu? Ndiyo maana wewe rafiki yangu, nilikwambia tangu mwanzo kuwa, huwa unaisoma Biblia kama Gazeti. Nakupa pole tu maana una safari ndefu sana ya kwenda! Tuombeane!
  Pili, naomba unithibitishie kimaandiko kauli yako hii. Nakunukuu, “Maandiko yanaposema kuwa Yesu ni yeye yule jana leo na milele huwa hayamaanishi kuwa Yesu ni static. Maana kama ni hivyo, basi alijichanganya sana kwa wanafunzi alipowakataza wasiwe na panga wala kitu chochote, lakini baadae tena Gethsemane akawaambia asiye na panga atafute.” Nakungoja.
  Tatu, swali lako nililijibu kwa maswali kwa sababu, ninajua unajua kuwa, enzi za mitume, hakukuwa na agano jipya! Wao walitumia Agano la kale tu. Injili zao zooote, walizihubiri kwa kutumia agano la kale. Nyaraka na makabrasha (vyuo) ya mitume na waandishi wengine wa Biblia katika agano jipya, zimekuja kukusanywa baadaye sana. Agano Jipya limekuja kukompailiwa katika kipindi cha kuanzia miaka 100+AD. Huko nyuma –yaani baada ya Yesu kupaa 34AD, hadi 99 AD, na hata na zaidi kidogo, mitume walifanya kazi ya kuhubiri injili na kuandika nyaraka/vitabu vyao. Nilijua unajua walao kijisehemu kidogo cha habari hizi ndiyo maana nilikujibu kwa maswali. Nadhani umenielewa.
  Mwisho, jitahidi kumjua Mungu. Na kama unataka kumfahamu vyema Mungu, anzia Agano la Kale na kisha umalizie na agano jipya. Kuhusu habari za wokovu kwa mwanadamu baada ya dhambi, jifunze habari za SANCTUARY, utaelewa vizuri na hautachanganyikiwa juu ya kafara ya Kristo na sheria zake (kivuli chake) pamoja na sheria takatifu ya Mungu –aliyoitoa kabla ya dhambi na itakayodumu milele zote.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 65. Siyi, kumbe upo!!

  Kuna wakati huwa naufurahia sana huu uhuru wa kujadili mambo na kila mtu kusema vile anaona ni sawa!

  Mtu anayeuliza swali kama hili lifuatalo, kwa mimi namwona ni mtu ambaye hajui jinsi Mungu anavyofanya kazi kulingana na wakati/nyakati.

  Swali hili hapa ” Kama Yesu huyo ndiye muumbaji na mtoa sheria pale bustanini kabla ya dhambi, inakuwaje sheria zake ziishie kwenye kifo chake tu kilichotokana na uasi wa mwanadamu?”

  Hii mimi inanionesha kuwa huyu mtu hata hajui tunapoongea habari za Torati na sheria tuongea kitu gani, tunapoongea habari za nyakati tunaongea nini.
  Mwanadamu mwenyewe ktk maisha ya duniani yuko kwenye reli inayoitwa wakati.

  Kuna wakati Siyi uliwahi kuniambia kuwa kifo cha Kristo kiliondoa zile sheria za kulinda amri tu, lakini zile amri kumi zenyewe zinaendelea kama kawa. Sijui kama unakumbuka hicho kitu.

  Tunapoongelea nyakati tunaongelea mambo kama haya; kuna wakati Mungu alikuwa ni Mungu wa binadamu wote.
  Lakini kuna wakati akaamua kujitengea jamii fulani toka kwa wanadamu wengine na kuiita taifa lake (Ibrahim, Isaka, na Israel). Wengine waliobaki nje ya taifa hilo wakaitwa wa mataifa.

  Lakini kuna wakati Mungu akaamua kuwachanganya tena hao taifa lake na wale wa mataifa kutengeneza kitu kinaitwa Kanisa (mwili wa Kristo).

  Hizo ni nyakati tofauti ambazo Mungu kaamua kufanya mambo kitofauti, yaani wakati wa Mungu wa watu wote, Mungu wa Israel, Mungu wa Kanisa.

  Sasa usipoelewa hizo dynamics, unaweza ukajikuta unalazimisha kuishi wakati wa kwanza(Mungu wa binadamu wote), katika kipindi cha wakati wa pili (Mungu wa Ibrahim, Isaka ,na Israel), au kuishi wakati wa pili ndani ya wakati wa tatu( Kanisa).
  Ukifanya hivyo lazima ukwame.

  Siyi suala la Mungu kubadilika nalo niliwahi kukwambia vizuri kuwa Mungu siyo static,ila ni dynamic. Sasa sijui kama Mungu kuwa dynamic maana yake ni kwamba hubadilika kwa maana hiyo ya Kiswahili.

  Maandiko yanaposema kuwa Yesu ni yeye yule jana leo na milele huwa hayamaanishi kuwa Yesu ni static. Maana kama ni hivyo, basi alijichanganya sana kwa wanafunzi alipowakataza wasiwe na panga wala kitu chochote, lakini baadae tena Gethsemane akawaambia asiye na panga atafute.

  Lakini Mungu tunasema habadiliki kwa maana ya ATTRIBUTES zake hazibadiliki.

  Mwisho, nakubali kuna maswali ya kujibiwa kwa swali katika mijadala, lakini swali langu la ‘Agano jipya lilitolewa lini’ halikuwa la kujibiwa kwa swali(tena kwa maswali mawili)

  Asante

 66. Lwembe,
  Kwanza habari za siku kaka? Nilipotea kiasi chake; nitawaomba mniwie radhi! Sasa nimerudi tena. Nimekusoma jinsi unavyohangaika na mafundisho ya wanadamu ndugu yangu. Huna tofauti na Sungura! Mafundisho ya dispensationalism, yamewateka mno! Hamuwezi kumwelewa Mungu ndugu zangu, ni mpaka mtakapoondoa mawazo kuwa, Mungu anabadilika, anafanya tofautitofauti kwa watu tofautitofauti na kwa nyakati tofautitofauti! Hili likiwatoka mioyoni mwenu, mtamwelewa Mungu! Lakini kwa sasa, itakuwa ni vigumu sana kwenu kumwelewa Mungu.
  Pili, kile alichokifanya Yohana, hakina tofauti na kile walichokifanya manabii wa Agano la Kale k.v. Isaya, Yeremeia, Musa na wengine wengi! Hakina tofauti! Ila kwa watu kama ninyi (msioelewa), itakuwa kazi kwelikweli kuwaelewesha. Unabii alioutoa Musa katika vitabu vyake kuhusu ujio, kifo na kufufuka kwa Kristo, ndio unabii huohuo alioutoa nabii Isaya, Yeremia, Yohana mbatizaji n.k. Hata hili nalo linaonekana kuwa ni gumu kwenu! Akili zenu zimetekwa kabisaa. Mimi nawaombea tu Mungu awafungue ndugu zangu, maana mko nyuma mno! Kazi imebaki kuimba tu ‘Kristo ni mwisho wa sheria’, bila ya kujua maana yake! Kama Yesu huyo ndiye muumbaji na mtoa sheria pale bustanini kabla ya dhambi, inakuwaje sheria zake ziishie kwenye kifo chake tu kilichotokana na uasi wa mwanadamu? Kwani Mungu anaweza kufanya jambo na binadamu akalipindua au likamfanya Mungu atangue alichokisema? Iweni makini!!
  Tatu, saa imefikwa kwako kujifunza kwa undani habari hizi za Neno la Mungu. Wewe ni miongoni mwa watu wanaochanganya kuhusu Sheria za Mungu kama Neno lote, Msingi wa Sheria hizo kama Amri 10 na Sheria zinazohusu wokovu baada ya dhambi –sheria zilizokuwa ni kivuli cha Kristo! Hapa ndipo kuna shida kwa wakristo walio wengi hasa wa makanisa ya kij2! Natoeni wito kwenu mjifunze habari hizi! Vinginevyo, mtachelewa, jambo ambalo ni hatari sana kwenu na watoto wenu! Aidha, tafuteni muda mjifunze habari za Sanctuary! Somo hilo linaweza kuwafungua baadaye!
  Neema ya Bwana ikufunikeni
  Siyi

 67. Siyi,
  Nilikuambia siku nyingi sana kwamba ili mradi umeukataa Wokovu, HUTALIELEWA Neno la Mungu tena, umejiingiza Gizani kwa hiari yako mwenyewe huko ambako hakuna Injili ya kuwatoa akina Esau waliouza haki yao ya Wokovu kwa dengu!

  Tazama mwenyewe ulichokiandika hapa, nakunukuu:
  “”Sasa Biblia inaposema kuwa, Torati imekuwepo mpaka kwa akina Yohana mbatizaji, ina maana gani? Kumbuka akina Yohana wanaotajwa wako Agano Jipya!? Kwa maelezo mengine, tungeweza kusema kuwa, Torati imekuwepo kuanzia agano la kale hadi agano jipya! Ina maana, mwisho wa agano jipya, ndio mwisho wa torati, labda uanze kutuuzia mbuzi kwenye gunia ya kwamba, enzi za akina Yohana mbatizaji si sawa na enzi za akina mitume 12 wa Yesu –uligawe agano jipya ktk vipindi tofautitofauti! Kimsingi tutazidi kukushangaa na kuvunja mbavu! Maana jambo hilo haliwezekani!””

  Haya ni maelezo ya mtu asiyejua chochote kuhusu Biblia, au mtu aliyenyang’anywa ufahamu!

  Hivi hao waliohudumiwa na Yohana, walikuwa ni hao waliompokea Kristo au ni watu wa Musa waliokuwa wakitayarishwa kumpokea Kristo? Changamsha akili hiyo kaka, Yohana Mbatizaji huduma yake ilikuwa ni kuwatayarisha ndugu zake wa Musa sasa wamgeukie Kristo. Nayo Biblia inaposema kuwa, Torati imekuwepo mpaka kwa akina Yohana mbatizaji, haina maana iliyo tofauti na hivyo inavyojieleza. Kutokuamini kwenu ndiyo mnajipokelea mafundisho ya mashetani yanawapofua zaidi! Yohana ndiye aliyeifunga Torati kwa wote walioipokea Huduma yake! Hawa ndio walioipokea Injili wakabatizwa kwa Jina la Yesu Kristo wakapata Ondoleo la Dhambi na Kujazwa Roho Mtakatifu ambaye kwaye Sheria ile Torati ikakoma baada ya kuwafikisha kwa Kristo, Rm10:4 “Kristo ni mwisho wa sheria.” Hiki ndicho kiwango cha Ukamilifu wanachokifikia hao watakatifu kupitia zile Huduma Tano.

  Kwahiyo, kutokana na kutokuyajua kwako Maandiko, kwa kule kumkosa Kiongozi, ndio huijui hata Huduma ya Yohana ilifanya nini, ile nguvu ya utenganisho iliyokuwa ndani yake, ambayo ndiyo hii hapa uliyoinukuu hapo Kristo anapolidhihirisha na kulitia muhuri jambo hilo la utenganisho, hata limekubeba mpaka wewe ktk kizazi hiki ktk maana kamili ya kifungu hiki:
  “For truly I tell you, until heaven and earth disappear, not the smallest letter, not the least stroke of a pen, will by any means disappear from the Law (TORATI) until everything is accomplished” –Matthew 5:18.

  Huduma ya Yohana iliwatenganisha Israeli ktk makundi mawili. Wale walioipokea huduma hiyo, walipelekwa kwa Kristo na kuingizwa ktk maisha mapya kulingana na utu mpya walioupokea baada kuzaliwa kwa Roho wa Mungu na hivyo kuwa wana wa Ufalme, ndio hawa hapa, Lk 7:29:
  ” Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.”Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye.
  Na kundi jingine ni la hawa ambao hawakuipokea Huduma ya Yohana. Hawa walibakia huko ktk Sheria na mambo yake yote, haijalishi wanajidanganya vipi, hawa watahukumiwa kwa Sheria , maana hata ufahamu wao wa mambo ya Wokovu ulifungwa siku walipoukataa wokovu, hawa ndio hili kundi hapa Lk 29:30:
  “Lakini, Mafarisayo na wana-sheria walilipinga shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye.”

  Ufahamu unapofungwa, basi maisha yako yote utaishia kupingana na Neno la Mungu! Usichokijua ni kwamba nje ya wokovu, unaangukia ktk Sheria, na unapaswa uitimize yoooote, kama kifungu cha kauli ya Kristo kinavyowaonya, hakuna hata yodi moja inayoondoka; huo uongo wa sheria za maadili na za kafara ni michezo ya mapepo ya dini yanapokuweka sawa kwa Hukumu; maana wewe mwenyewe umesoma na kunukuu kwamba hakuna kinachopungua ktk sheria, halafu leo yanakudanganya unakubali, kama sio uzezeta wa dini huo ni nini basi?!!!

  Dogo, changamsha akili hiyo kabla ya kiberiti!

 68. Sungura,

  Katu usipuuze kitu! Acha kupiga chenga kujibu hoja! Kama una hoja zenye proof, jibu with Biblical evidences!

  Suala la aya nalizingatia sana. Sema tu aya zangu huwa ni ndefu. Kwenu ninyi wavivu wa kusoma na kuandika, mtachemsha tu! Naomba nijibu maswali yako.

  Swali 1.
  hebu niambie,Agano jipya lilitolewa lini(yaani ni kipindi gani lilianza kuwa kazini)?

  Jibu
  Wewe unadhani, wakati wa Yesu au mitume, kulikuwa na Agano jipya? Unajua ni lini Biblia iliandikwa, particulary new testament!

  Na mwisho, Biblia niliyotumia kufananua neon MPAKA ni SUV na KJV na nilionesha kwenye pachiko langu! Inavyoonekana, hukusoma pachiiko langu between lines! Nikushauri urudie kulisoma tena.

  Neno la Mungu lipo siku zote. Naam hata mbingu na nchi zitoweke, lenyewe halitaondolewa hata nukta moja! Kaa ukijua hivyo!

  Neema ya Bwana ikufunike sana.
  Siyi

 69. Siyi,

  Mengine yasiyo ya maana sana acha niyapuuze.

  Niseme matatu tu. La kwanza, weka paragrafu unapoondika, wewe siyo std two.

  Pili; hebu niambie,Agano jipya lilitolewa lini(yaani ni kipindi gani lilianza kuwa kazini)?

  Tatu; Neno mpaka uliyotafsiri na kusema mfano wa mwisho wa shamba n.k., haina kabisa muktadha wa ‘mpaka’ tunayoiongelea, ambayo kwa Kiingereza ni ‘until’ . Huo ndo udogo wa IQ ninaousema sasa.

  Kwa nini kwenye Mt 5:18 kuna until mbili? Na ni version gani ya biblia uliyotumia!

 70. Sungura,
  Samahani kwa kuchelewa kujibu pachiko lako. Hii imetokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Mjadala unaendelea…
  Kila mtu anamshangaa mwenzake kuwa ana akili ndogo! Hii ni ajabu sana! Anyway, mwenye akili ndogo atabainika tu. Hebu tuendelee….
  Kwanza,unadai kuwa sizingatii njeo! Hiyo siyo kweli! Njeo mbalimbali zimetumika ndani ya Biblia. Ni kweli kuwa kuna njeo zinazoonekana ni za wakatti ujao, lakini zilitimia. Kwa mf. “Bikra atachukua mimba….” Ndani ya Biblia, ni kweli muda ulipofika, jambo hilo lilitokea, -Yesu alizaliwa. Kwa hiyo ndani ya Biblia kuna mambo mengine yaliyosemwa kwa njeo zijazo na tunaendelea kuyasoma katika njeo hizohizo, lakini yalitimia na mengine hayajatimia. Aidha, yapo yaliyosemwa kwa njeo zilizopo, na bado yanaendelea kuaapply hadi leo! Ndiyo maana huwa nakwambia, usiisome Biblia kama mwananchi au habarileo!! Kanuni ya usomaji wa Biblia ni “For precept must be upon precept; line upon line; here a little, and there a little…- Isa 28:10, 13 KJV. So you must take an ample time to study the word of God, otherwise, akili yako itaendelea kuwaza na kuishia hapohapo unapoishia sasa!
  Pili, uchambuzi wako kwa IQ yangu hadi unatia huruma! Unazidi kujionesha kiasi gani ulivyo! Umeniita msumbufu na punguani, kwa kuniambia sijui maana ya neno “MPAKA” kiingereza “UNTIL”. Mimi nikushukuru tu kwa matusi maana moyo wako ndio uliokusukuma uyatamke kwangu! Kwangu hilo halina shida hata kama ungetamka mara 100. Ukweli utaendelea kuwa palepale! Ngoja nikuoneshe maana ya neno ulilosema silijui…
  Maana ya kwanza ya neno “MPAKA” (nm) ni sehemu inayotenga sehemu moja na nyingine mf. shamba au kiwanja kimoja na kingine au eneo la nchi moja na nchi nyingine. Na maana ya pili ya neno hili ni kielezi ‘hadi’ chenye maana ya ukomo wa kitu au jambo! Kimsingi maana zote mbili (za nomino na kielezi) zinashabihiana tu. Sasa Biblia inaposema kuwa, Torati imekuwepo mpaka kwa akina Yohana mbatizaji, ina maana gani? Kumbuka akina Yohana wanaotajwa wako Agano Jipya!? Kwa maelezo mengine, tungeweza kusema kuwa, Torati imekuwepo kuanzia agano la kale hadi agano jipya! Ina maana, mwisho wa agano jipya, ndio mwisho wa torati, labda uanze kutuuzia mbuzi kwenye gunia ya kwamba, enzi za akina Yohana mbatizaji si sawa na enzi za akina mitume 12 wa Yesu –uligawe agano jipya ktk vipindi tofautitofauti! Kimsingi tutazidi kukushangaa na kuvunja mbavu! Maana jambo hilo haliwezekani!
  Sasa, ndugu yangu, unaujua wewe mwisho wa agano jipya utakuwa lini??? Jibu linapatikana katika kauli ya Yesu mwenyewe aliposema, “For truly I tell you, until heaven and earth disappear, not the smallest letter, not the least stroke of a pen, will by any means disappear from the Law (TORATI) until everything is accomplished” –Matthew 5:18. Nadhani mpaka hapa, jibu unalo tayari kaka, kwa maana kile kilichofanywa na akina Yohana mbatizaji, Yesu mwenyewe, ndicho kilichofanywa na mitume na ndicho tunachopaswa kukitenda sisi leo. Mitume hawakufanya jambo jipya na lile walilofundishwa na Bwana wao. Hoja yangu ya kusema kuwa, TORATI itaendelea kuwepo siku zote, ilitokana na kauli ya Yesu mwenyewe pamoja na mitume wake! Hakuna suala la uzoba hapo kaka, isipokuwa kama utasoma kwa makengeza kama ulivyofanya! Na mimi sikushangai, maana una misimamo yako usiyotaka kuiachia kamwe! Shauri yako….
  Yesu aliposema, “For truly I tell you, until heaven and earth disappear, not the smallest letter, not the least stroke of a pen, will by any means disappear from the Law (TORATI) until everything is accomplished” –Matthew 5:18, alimaanisha kwa neno lake lote maana Biblia ni SHERIA. Neno la Mungu ni SHERIA kijana! Ni TORATI ile! Acha kudanganyika kabisaa!! Mifano uliyotoa, haifanani kabisaa na hoja yenyewe! Kama ndiyo uaIQ huo, basi nakupa pole na IQ yako!! Ishughulishe upya aisee!! Bado sana sana! Kama una hoja, thibitisha kutetea hoja yako hiyo!, Kama kupita kwa mbingu na nchi ulikuwa ni msemo tu, thibitisha pia!! Maana huwezi kutuletea hoja ya kidhanifu hapa kuwa eti ulikuwa ni msemo tu huku vizazi hivyo vilikuwa vinatambua fika historia ya dunia juu ya ghariba na madhila yaliyozipata baadhi ya nchi kama vile Sodoma na Gomora walipozidi katika uasi wa sheria/neno la Mungu! Kama mambo haya waliyasoma katka hisoria, inawezekanaje mbingu na nchi kupita likawa gumu kwao tena, hadi walitengenezee msemo?! Acha kutudanganya bwana! Kama una ushahidi, thibitisha mwanaume! Vinginevyo, porojo hapa, mimi sitaki bana!
  Tatu, suala la Sabato, liko clear sana. Biblia inaposema kuwa, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu na si mwanadamu kwa ajili ya sabato”, ukisoma kwa makengeneza vilevile, utasema kuwa sisi tuna uwezo wa kulibadili neno la Mungu! How? Kama Sabato itakuwa chini ya mamlaka yetu, ina maana tunaweza kuirekebisha! Au sivyo?! Na ndicho mlichokifanya ninyi waj2! Neno la Mungu ni katiba ya Mungu tuliyopewa sisi wanadamu iili tuifuate. Hatuna uwezo wa kuifanyia marekebisho, ni mpaka Mungu mwenyewe aliyeiandika! Kwa mujibu wa katiba ya Mungu (Biblia), tulipewa Sabato kama ibara mojawapo inayobainisha madhumuni ya Mungu kumuumba mwanadamu –kumwabudu Mungu. Wewe sungura ukiiona leo ibara ya sabato haifai, mwambie Mungu airekebishe not you!! Maana sisi ametuagiza tusiongeze wala tusipunguze chochote kwenye neno lake! Ndio maana sisi Wasabato, tulishagundua kuwa, Mungu anahitaji kutiiwa tu kama matokeo ya upendo wetu kwake. Na kwa maana hiyo, ndiyo maana tunaitunza Sabato kama mwasisi mwenyewe alivyoagiza!
  Nne, kwa habari ya miujiza, bado nakupa ushauri wa bure, chunguza miujiza hiyo kama halisi au la! Nashukuru kwa ukaribisho kanisani kwenu, japo hata nikija, siwezi kukufahamu maana sidhani kama unatumia jina la Sungura kwenye huduma yako. Wewe niambie jina lako halisi, na sehemu lilipo kanisa lenu ili siku nikija, nikiyaamuru hayo mapepo yakutoke, yatakutoka mbashala -mbele za watu! Acha mchezo wewe …!! Mimi nataka nianze na wewe kwanza! Habari ya wewe kusikia, siitaki. Nataka uone kwanza! Wewe niambie jinalo halisi, na sehemu lilipo kanisa lenu. Naja huko…
  Tano, suala la Torati na Neema, tulishaliongea sana rafiki yangu. Inasikitisha kukuona tena unarudia matapishi yaleyale eti kuwa Torati ilianzia kwa akina Ibrahimu tu hadi kuzaliwa kwa Yesu… Huzuni iliyoje!! Mimi naona katika hili, nikuache na uelewa wako huo wa wagala 3. Acha mimi niendelee na huyo Neema aliyefunuliwa kwangu, ambaye ili nionekane kuwa nampenda, sharti nizishike sheria (torati) zake! Mungu akubariki sana.
  Siyi

 71. Siyi, inaendelea..

  Kwa kuwa na wewe unakiri kuwa kuna mambo Yesu alisema yakatimia yakiwemo hayo tuliyoyabainisha, kwa nini unashindwa kuelewa kuwa suala la kusema mbingu na nchi zitapita, lilikuwa linatumika kama msemo, japokuwa ni kweli kuna siku mbingu na nchi zitapita?

  Kwa mfano hapa kwenye Luka 21 : 32 “Truly I tell you, this generation will certainly not pass away until all these things have happened. 33 Heaven and earth will pass away, but my words will never pass away).

  Hiyo sentensi ya mstari wa 33 alikuwa anamaanisha nini kwenye hayo maneno? Maneno yake yapi ambayo yenyewe yatabaki wakati mbingu na nchi zikishapita?

  Mbona yalishapita mengi tu aliyoyasema kama tulivyoona huku nyuma!!

  Maneno haya yalitumika kama msemo pamoja na ukweli kwamba mbingu na nchi zitapita.
  Watu walikuwa wanaona kuwa suala la mbingu na nchi kupita ni gumu sana kuliko jambo lolote, ndiposa Yesu anawambia ni ngumu zaidi neno lake kupita bila kutimia, kuliko ilivyo ngumu kwa mbigu na nchi kupita.

  Umesema kwamba Adamu hakuambiwa akatawale na siku, ni kweli hiyo sentensi ya hivyo hakuambiwa, lakini Yesu anaweka bayana kuwa sabato iliumbwa kwa ajili ya mwanadamu na si mwanadamu aliumbwa kwa ajili ya sabato. Hapa inaonesha nani ni boss wa mwingine. Ni kama ilivyo kwa mwanamke na mwanaume aliyeumbwa kwa ajili ya mwingine ndiye anayetawaliwa. Sijui kama haya yanakuelea!

  Kwa suala la miujiza/ ishara usiongee sana, nimekwisha kwambia kuwa kwa sababu unadhani simwabudu Mungu aliye hai lakini nina nguvu ndani yang, kwa hiyo nguvu itakuwa ya shetani, wewe unayedhani una nguvu ya Mungu njoo ukemee huyo shetani aliyemo ndani yangu.

  Kama hujui mahali nilipo nitakwambia; niko Dar es Salaam, nafanya huduma kanisa linaitwa Nchi ya Ahadi. Karibu sana.

  Lakini ukishindwa hilo, basi nenda hospitali ukaombee wagonjwa, ukiweza uende na mohwari ukafufue hata mfu mmoja, habari zitatufikia ndani ya muda mfupi sana.

  But as long as nawajua wasabato, ni ujuzi wa kuongea porojo tu, lakini kwa habari ya karama za nguvu, hamna kitu.

  Lakini pia nataka uone utofauti unaofunuliwa na maandiko kati ya Torati na Neema, kwamba ni vitu viwili tofauti, lakini wewe mara nyingi tu nakuona unalazimisha kusema kuwa hata wakati wa Torati neema ilikuwepo, na sasa wakati wa neema Torati inaendelea kushika hatamu

  Tuangalie hiki kitabu cha Wagalatia 3: 17This is what I am trying to say: The agreement God made with Abraham could not be canceled 430 years later when God gave the law to Moses. God would be breaking his promise. 18For if the inheritance could be received by keeping the law, then it would not be the result of accepting God’s promise. But God graciously gave it to Abraham as a promise.
  19Why, then, was the law given? It was given alongside the promise to show people their sins. But the law was designed to last only until the coming of the child who was promised. God gave his law through angels to Moses, who was the mediator between God and the people. (NLT)

  Mstari wa 17 unaonesha kuwa Torati ilianza wakati wa Musa, huko nyuma wakati wa Ibrahim hapakuwa na Torati.

  Mstari wa 18 unasema kuwa ahadi haikuja kwa kushika Torati.( Ahadi yenyewe inayosemwa ni Mwokozi Yesu Kristo)

  Mstari wa 19a unaonesha sababu za Torati kuja, na 20b inaonesha muda wa torati kuendelea kuwepo (duration), ambapo imesema muda wa uhai wa torati ulifikia tamati siku ahadi ilipokuja( Yesu Kristo) – Lakini wewe bila aibu unalazimisha tu kwamba mpaka leo ipo na kesho itakuwepo. – silly!

  Kuja kwa ahadi kunadhihirisha kuwa Torati haikuweza kutuletea maisha mapya ambayo tulitakiwa kuwa nayo – 21b If the law could give us new life, we could be made right with God by obeying it. 22But the Scriptures declare that we are all prisoners of sin, so we receive God’s promise of freedom only by believing in Jesus Christ.

  Ona maandiko yanavyomalizia kwa habari za uhai wa Torati: – 24Let me put it another way. The law was our guardian until Christ came; it protected us until we could be made right with God through faith. 25And now that the way of faith has come, we no longer need the law as our guardian.

  Siyi, hatuhitaji tena Torati kuendelea kuwa kiongozi wetu – period!

  Sasa sijui wewe Torati inaendelea kukuongoza kwenda wapi!!!!

 72. Siyi,

  Nafikiri una IQ ndogo sana , kwa hiyo inakugharimu sana katika kuyaelewa mambo, hususani suala la Lugha.

  Kwa akili yako ndogo unadhani kuwa kila kilichosemwa kwenye biblia kama kilisemwa kwa wakati ujao, uliopita, uliopo kitabaki hivyohivyo kikimaanisha wakati huohuo! What a misery!!!

  Kwa hiyo kwa akili yako hiyo ndogo ungetaka tuendelee kuhubiri kuwa ‘bikira atachukua mimba nae atamzaa mwana na jina lake ataitwa Imanuel,n.k? Ina maana wewe ukimkuta mtu anasema bikira alichukua mimba akamzaa mwana….., utamwambia kuwa anasema kitu ambacho biblia haijasema?

  Wewe ni msumbufu kwa sababu uwezo wako wa kuelewa ni mdogo kiasi hicho!

  Ngoja nikuonesha udogo wa IQ yako kutoka kwa yale umesema, nakunukuu:
  ”Tuanze na mastari wa 16 unaosema, “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”-SUV. Kwanza, hata mimi nakubali kuwa, Torati imekuwapo tangu mwanzo hadi kipindi cha Agano Jipya, zama za akina Yohana, Yesu mwenyewe, mitume n.k. Torati imekuwapo muda wote na itaendelea kuwapo milele”

  Ngoja nichambue ufinyu wako wa kuelewa toka kwenye hii nukuu:

  Umekubaliana na hilo andiko kuwa Torati na manabii vilikuwepo mpaka Yohana, halafu hapo mwishoni unakuja kusema kuwa Torati imekuwepo muda wote na itaendelea kuwapo milele. Anayeweza kusema tungo za hivyo ni punguani tu, mwenye busara lazima ajue kuwa hizo tungo mbili zinakinzana.

  Nafikiri hujui maana ya neno ”MPAKA”

  Kwa mfano ukisema kuwa ‘mfumo wa chama kimoja nchini Tanzania ulikuwepo mpaka mwaka 1992, kuanzia mwaka huo mfumo wa vyama vingi ulianza.Kwa hiyo mfumo wa chama kimoja umekuwepo na utaendelea kuwepo siku zote’

  Hapo lazima uonekani kuna kitu kichwani mwako hakiko sawa!

  Sasa hicho ndicho ulichokisema Siyi!

  Neno ‘mpaka’ linamaanisha ukomo! Na sijui kwa nini huwezi kuelewa kuwa kwenye maandiko kuna nyakati.Eg; Wakati wa waamuzi siyo sawa na wakati wa wafalme. Hizi ni zama mbili tofauti kabisa kiutendaji! Kwa mfano uliwahi kusikia kwenye Torati ya Musa watu wanaambiwa wabatizwe kwenye maji?

  Nyingine hii hapa: ” Zingatia hapa; Biblia haisemi kuwa ‘ilikuwa ni vyepesi zaidi mbingu na nchi zotoweke kama torati ingekuwa ya agano la kale tu…’, bali inasema, ‘ni vyepesi (present time) mbingu na nchi vitoweke inaonesha mwendelezo usiokoma”

  Haya, kuna mwendelezo gani hapo, kwani mbingu na nchi vilikuwa vinatoweka wakati hayo maneno yanasemwa?

  Inaposema kuwa TANGU wakati huo habari njema za ufalme zinahubiriwa, kama Torati na Habari njema za ufalme ni kitu kimoja basi kusingekuwa na neno ‘mpaka,Tangu’. Lakini huo mpaka unakuonesha kuwa kilichokuwa kinafanyika wakati wa Torati na manabii ni tofauti na kinachofanyika wakati wa habari njema ya ufalme. Na hiyo tofauti iko katika operation ya hivyo vitu viliwil na kanuni zinazotumika.
  Hivyo neno Mpaka linamaanisha mwisho wa jambo, na neno ‘Tangu linamaanisha mwanzo wa jambo jingine!

  Kwamba Torati na Injili ni sawa na pande mbili za shilingi, nakubaliana na wewe, na hiyo ilitakiwa kukusaidia kujua kuwa pande mbili za shilingi hazifanani, lakini malengo yake yanafanana. Ndipo nikakwambia Torati na Injili zilitoka kwa mmoja lakini kanuni za utendaji wake ziko tofauti, japo lengo ni moja.

  Mwisho, Yesu alikuwa haongelei neno lake lote Siyi, ispokuwa ni lile neno la kinabii alilowaambia wanafunzi wake kwa habari ya siku za mwisho!

  Kama lingekuwa ni neno lake lote, mbona mengi tu aliyosema yalishatimia wakati mpaka sasa mbingu na nchi bado zipo!!
  Eg; Alisema kuwa atakamatwa na kusulubiwa- ilishatimia
  Alimwambia Petro kuwa atamkana mara tatu kabla ya jogoo kuwika- ilishatimia
  Alisema atamtuma msaidizi (Roho mtakatifu) – ilishatimia, n.k

  Ifanyishe kazi zaidi IQ yako ili uwe unaongea sense zaidi!

  Ntaendelea….

 73. Inaendelea…

  Nne, suala la Sabato, mimi sijalitafsiri vibaya kama unavyodai. Kama umeona nimetafsiri visivyo, hebu onesha wewe inavyotakiwa kuwa. Aidha, mtu aliyesema kuwa ‘anachokumbuka yeye ni kwamba alikuwa mgonjwa na wasabato walikuwepo na hawakumponya isipokuwa alipoona muujiza kwa kanisa alimo sasa’ siyo Siyi bali ni Sungura. Miujiza ndiyo inayokufanya uendelee kuivunja Sabato ya Bwana kwa kudhani kuwa, na huko uliko, miujiza hiyo inatendwa na Mungu! Ukasema akina Siyi tuko dhaifu sana spiritually ukilinganisha na ninyi! Nami nikakwambia kuwa, Mungu hutenda mambo yake kupitia vitu au watu wadhaifu kama Siyi. Kwa hili hakuna cha uwenda wa wazimu wala kupungukiwa na akili. Acha janjajanja!! Kama una Mungu kweli, kwa nini usimdhihirishe?

  Ninashangaa unapolalamika siasa hivi kama unaonekana tena kunitupia kibao! Alah!! Wewe vipi bwana?
  Tano, Kama unaelewa maana ya Agano Jipya na Agano la Kale, siku moja nilishawahi kukuuliza utofautishe kati ya New Testament vs Old Testament na New Convenant vs Old Convenant! Uliingia mtini mpaka leo!! Narudia tena kukwambia, Mungu wa Agano la Kale, ndiye Mungu wa Agano Jipya. Siku utakapoelewa tofauti ya phrases nne hizo hapo juu (New Testament vs Old Testament na New Convenant vs Old Convenant), ndipo utaelewa kuwa ulikuwa unaogelewa dimbwini, sasa unapaswa kuingia kwenye bahari yenyewe. Sina haja ya kukupatia kila kitu! Tafuta na wewe!
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 74. Sungura,
  Kwanza, acha kuchekesha rafiki yangu! Huwezi kuwa bosi wa siku ilhali maisha yako yanategemea mamlaka ya siku! Huko ni kuhalalisha uasi uliokubuhu! Mungu hakumwambia Adamu akatawale na siku zote. Aliambiwa akawe bosi wa viumbe tu basi! Ungekuwa bosi wa siku, ungeyajua pia ya kesho! Huo ni moto ungeni! Ndio maana nauita ni UASI ULIOKUBUHU! Wewe kama umeamua kuasi –kuivunja Sabato ya Bwana, endelea na uasi huo, lakini ujue kabisa kuwa, hakuna sababu yoyote unayoweza kujitetea kwayo! Hakuna!

  Pili, wewe ni fundi wa kucheza na maneno tu, lakini kwa mtu wa IMEANDIKWA, unaelea kama boya la mtego maana kila neno sharti lithibitike. Umesema kuwa, “Torati & Manabii ni tofauti na Injili ya ufalme katika operation zake”. Aidha umenukuu Luka 16:16-17 ukasema kuwa mimi nimeitafsiri visivyo ila wewe. Haya hebu twende tuione inasemaje kwa mara nyingine tena…
  “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati”.
  Tuanze na mastari wa 16 unaosema, “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”-SUV. Kwanza, hata mimi nakubali kuwa, Torati imekuwapo tangu mwanzo hadi kipindi cha Agano Jipya, zama za akina Yohana, Yesu mwenyewe, mitume n.k. Torati imekuwapo muda wote na itaendelea kuwapo milele. Pili, kishazi cha pili kinasema, “tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”. Hoja inabaki tangu wakati huo, wakati upi? Wa agano la kale au wa agano Jipya? Kwani Injili imeanza kuhubiriwa tangu lini? Ni tangu Agano la Kale au Agano Jipya tu? Biblia inasemaje kwa hili? Tafakari! Jenga tabia ya kujiridhisha kwanza kabla hujasema lolote!

  Twende kwenye aya ya 17 “Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati”-SUV. Zingatia hapa; Biblia haisemi kuwa ‘ilikuwa ni vyepesi zaidi mbingu na nchi zotoweke kama torati ingekuwa ya agano la kale tu…’, bali inasema, ‘ni vyepesi (present time) mbingu na nchi vitoweke inaonesha mwendelezo usiokoma….’. Mtu mwingine anaweza kufikiri kuwa labda ni tatizo la Kiswahili, ngoja tuangalie KJV inasemaje. “And it is easier (not it WAS…) for heaven and earth to pass, than one tittle of the law to fail”. Hii ina maana gani? Sasa ili kujibu hoja hii vizuri kwa ujumla wake (Luka 16:16-17), ni vyema tukaanza kuangalia maana ya TORATI, MANABII na INJILI kama ni vitu viwili/vitatu tofauti, vinafanya kazi tofauti na kila kimoja kilianza kufanya kazi lini!! Biblia inayo majibu.
  TORATI; Nilishawahi kulitolea maana hapa. Torati kwa wanadamu inaanzia kitabu cha mwanzo hadi Kumbukumbu la Torati. Aidha, kwa maana pana, Torati ni Biblia nzima.
  MANABII: Hawa ni waandishi wa Biblia japo Biblia nzima haikuandikwa na manabii tu. Katika Biblia, wanaanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Katikati humo utawakuta wengi (manabii wakubwa na wadogo) tu na wala hawapishani kwa maandiko yao. Hadi leo, nabii wa Mungu anaweza kuwepo, lakini kigezo kikuu cha kumpima, ni kusema sawasawa na manabii wengine wote waliotangulia, maana chanzo chao wote ni kimoja –Mungu. Hivyo hawawezi kubishana.

  INJILI; Kwa ufupi ni neno lenye maana ya ‘habari njema’ . Maneno ‘habari njema’ inayohusu wokovu wa mwanadamu, yameanza kutumika tangu agano la kale mf. Mwanzo3, Isaya 40:9, Isaya 61:1, n.k. Yohana mbatizaji alipokuja, hakuhubiri jambo jipya -Injili. Alichokifanya yeye, ni kuitengeneza njia ya Bwana tu, ambaye kiunabii, alianza kutajwa tangu kitabu cha mwanzo kama uzao wa mwanamke…. Hivyo, habari njema (injili kuhusu ufalme wa Mungu), ilianza kusikika tangu bustanini Edeni.

  Hivyo, TORATI, MANABII na INJILI, huwezi kuvitenganisha kiutendaji au kimaudhui! Kamwe huwezi! Natambua kuwa ndani ya Agano la kale kulikuwa na nakala za baadhi ya mambo ambayo katika Agano Jipya, yamewekwa bayana –halisi. Paulo anaposema kuwa Kristo ni muumbaji, japo hakuonekana moja kwa moja kufanya hivyo katika agano la kale, hiyo haimfanyi Kristo wa agano la kale awe tofauti na Kristo wa Agano Jipya. Kazi za Kuhani Mkuu wa Agano la Kale (ambaye kimsingi alikuwa ni nakala ya Kristo mwenyewe), haziwi tofauti leo katika Agano Jipya zinapofanywa na Kristo mwenyewe katika hekalau la mbinguni! TORATI na INJILI, huwezi kuvitofautisha pamoja na waandishi wake, hata ufanyeje!

  Neno la Mungu ni TORATI au ni INJILI. Torati inazungumzia habari wa uchaji Mungu na wokovu wa bure kwa njia ya kutii sheria za Mungu, na Injili nayo inazungumzia habari za uchaji Mungu na wokovu wa bure kwa njia ya kuzitii sheria zilezile za Mungu. Kwa maneno mengine, Torati na NEEMA ni pande mbili za shilingi moja. Yesu alisema, neno lake (ZIMA) halitapita kamwe hadi yote hayo yatimie. Hayo yepi? Mambo yoooote yaliyotabiriwa kutokea baadaye likiwemo lile la kuzaliwa kwake, kufa kwake, kufufuka kwake, kupaa kwake, kurudi kwa mara ya pili na lile la mbingu na nchi kupita. Mbingu na nchi kupita haukuwa msemo wa Yesu kijana. Yesu alimaanisha! Dunia imetabiriwa kuwa itaondolewa kama kurasa. Watakatifu wakishaenda zao mbinguni, bado wataenda kuendelea na ibada maana hata kule nako kuna hekalu –ufunuo 11:19. Mfumo wa kufuata taratibu, kanuni, sheria katika kumwabudu Mungu, utadumu milele hata baada ya dunia hii kuondolewa. Usidanganyike na mbingu na nchi eti ulikuwa ni msemo tu. Hilo ni jambo halisi, na ni sharti litimie. Acha mchezo kijana! Ukisoma Biblia kama gazeti utaishia na fasili potovu siku zote. Kuna mambo ambayo Yesu aliyasema kwa wakati ule na yalitokea na wakati uleule, mengine miaka michache baadaye na mengine yanaendelea kutokea leo na mengine yatakamilika mwisho wa wakati. Kwa mfano, Yesu alitabiri habari za kifo chake. Kimsingi hazikupaita siku nyingi akafa. Alitabiri habari za kubomolewa kwa ukuta wa Yerusalemi, miaka 30+ baada ya Kristyo kupaa kwake (mnamo miaka ya 70 AD), majeshi ya Titus yaliizingira ngome ya mji huo. Kilichotokea, tunakijua sote. Mambo mengine aliyoyatabiri, leo yanaendelea kutokea na mengine yataendelea kutokea. Kwa hiyo, kuna yale yaliyokuwa yamepangwa kutimia wakati wake, kwa kizazi cha zama zile na mengine ambayo yangekuja kutimia baadaye.
  Tatu, sheria ya Mungu iko palepale hata katika Agano Jipya. Hii ni kwa sababu, tunapohubiriwa injili (habari njema), habari njema hiyo ina masharti/sheria/kanuni za kuzingatia ili mtu anufaike na habari njema hiyo. Miongoni mwa sheria hizo, ni amri 10 za Mungu na zingine nyingi. Ndio maana leo tukiwa wakristo, ulimwengu utatushangaa kutuona tunaiba, tunazini, tunasema uongo, tunavunja sabato n.k. Utatushangaa sana, maana ni kinyume cha matakwa na Neno la Mungu lote! Biblia inaposema usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, ni sawa na inaposema usizini! Kanuni ni moja kwa kila muumini, TII (Biblia) UISHI, ASI UFE, full stop!

  Inaendelea…..

 75. Siyi naendelea,

  Kama ulikuwa unajua kuwa andiko la Ezekiel linaongelea sabato za jumla kwa nini ulikuwa unalinukuu, kama siyo kutukujua kutumia maandiko kwa haki? Haijasema itakaseni sabato yangu bali zitakaseni sabato zangu, kwa hiyo hapo umejaribu kutumia mstari usio ili kujaribu kuhalalisha matakwa yako- usijaribu kurahisisha tafsiri ya maandiko ukadhani uko sawa tu Siyi!

  Wajinga fulani walimtaka Yesu afanye muujiza ati ndipo wamwamini,akawagomea, akawaita ni kizazi kikaidi. Lakini pia kutaka uone muujiza ndipo umwamini Mungu ni utoto wa hali ya juu.

  Siyi ukidhani kuwa ati nimeogopa uliponiambia habari ya kutaka kudhihirisha mimi na wewe nani anamwabudu Mungu kiusahihi au nani ana Mungu aliyehai. Kunitaka nifanye hivyo ili nijue kuwa Mungu niliyenae ni Mungu alie hai naona ni kama kupungukiwa akili.

  Sihitaji ishara yoyote, I already know that the God in me is the living God, nilikwambia vitu vichache tu alivyonitendea ambavyo kwavyo najua niko na Yehova ndani yangu.

  Wewe fanya hivi, njoo uniombee mimi ambaye unadhani simwabudu Mungu aliye hai ispokuwa naabudu miungu, maana mwabudu miungu lazima ana mashetani ndani yake. Kwa hiyo njoo uyakemee halafu uone yatatoka mashetani mangapi.

  Ndivyo biblia inavyosema kuwa waaminio ishara zitafuatana nao, lakini katika ishara hizo ishara ya sabato haipo, ispokuwa ishara kutoa pepo, kuponya wagonjwa, kusema kwa lugha impya, kutokufa wakila kitu cha kufisha.

  Halafu sikia, mimi huwa sipumziki Jumapili wala Jumamosi wala siku yoyote, siku zote mimi napiga kazi, na siku zote mimi napumzika. Pole yako wewe ambaye kupumzika kwako ni mpaka Jumamosi

  Kitu kingine ambacho si kweli umesema ni kule kusema kwamba huwezi ukalielewa agano Jipya pasipo kulielewa la kale. Agano jipya linajitosheleza kwa kila kitu. Usidhani kuona biblia yako umeunganisha vitabu vya agano jipya na la kale ukadhani ilikuwa ni lazima iwe hivyo. (Prove me wrong)

  Tha fact kwamba Mungu wa Agano jipya ndiye Mungu wa agano la kale, haiithibatishi kuwa utendaji au kanuni za kuenenda za Agano jipya ni sawa na kanuni za Agano la kale!

  Ndio mana hili ni Jipya na lile ni la Zamani

  Take care

 76. Siyi,

  Achana na maneno yako ya kitoto ya kusema ”changamka kijana”, am not a teenager katika kuifahamu kweli ya Mungu. Suala la uungu wa Yesu hapa SG tulishalijadili tena kwa undani mkubwa tu. Kama akili yako inakwambia kuwa ni fundisho geni kwa wale unaotuita wa Jumapili (japo nilishakwambia mimi si wa siku yoyote, napiga kazi siku zote maana Mungu mwenyewe anapiga kazi siku zote, mimi ni boss juu ya siku, natawala siku, wala siku hazinitawali mimi!), basi ufahamu wako ni mchanga bado. Liwe geni kwa kipi hasa?

  Siku zote nakwambia kuwa shida huwa siyo nini kimeandikwa kwenye maandiko, ispokuwa shida ni hicho kilichoandikwa kina maana gani(Tafsiri). Huna tofauti na wale ambao ungewaambia kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu, nao wakakuuliza swali kuwa Mungu alimuoa Mariam? Maana akili ya hao imekomea tu kwenye wazo la kwamba ili mtoto apatikane lazima kuna tendo la ndoa, au lazima yai la kike likutane na mbegu za kiume.

  Lakini naamini wangekuuliza hilo swali na kukupa huo msimamo wao ungewacheka kuwa ufahamu wao ni mdogo kwa kufikiri ndani ya boksi kiasi hicho. Nami ndivyo navyokuona wewe kwa habari za kuelewa uungu wa Yesu.

  Ukisikia mtu anasema usitumie hoja ya nguvu, ila nguvu ya hoja ni kama hivi wewe unavyofanya. Nakunukuu ” habari za kutolitaja bure jina la Mungu iko palepale. Haina cha Agano la Kale wala Jipya! Habari ya Amri 10 za Mungu, ziko palepale, hakuna cha Agano la Kale wala Jipya. Yesu alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu (Sheria zake) hayatapita kamwe”

  Hapo umeamua kutumia hoja ya nguvu. Ukinukuu maandiko bila kuangalia vizuri katikati ya mistari uliyonukuu unaweza ukadhani umesema kitu sahihi sana kumbe la.
  Umenukuu Luka 21:33, na Luka 16:17, na ukaongeza na mbwembwe kuwa hayo mambo yanaeleweka kwa akili ya ugali na mlenda tu. Hebu ngoja tuone sasa kinachosemwa:

  Luke 16:16 “The Law and the Prophets were proclaimed until John. Since that time, the good news of the kingdom of God is being preached, and everyone is forcing their way into it. 17 It is easier for heaven and earth to disappear than for the least stroke of a pen to drop out of the Law.

  Wewe umenukuu tu mstari wa 17, bila kuona kilichosemwa mstari wa 16. Keshakwambia tayari kuwa torati na manabii vilifanya kazi mpaka wakati wa Yohana mbatizaji, baada ya hapo Injili ikaanza kuhubiriwa. Mpaka hapo keshakuonesha kuwa Torati & Manabii ni tofauti na Injili ya ufalme katika operation zake.

  Kinachosemwa katika mstari wa 17 ni kitu cha kweli kwamba haingewezekana torati hata nukta moja ya torati ipite bure, which means, mpaka torati inapokuja kupata ukomo wake kwenye enzi za Yohana mbatizaji, yote yaliyokuwa yanapaswa kutimia kwa habari ya torati yalikuwa yametimia.(Enzi za Yohana ni pamoja na enzi aliyofanya kazi Yesu)

  Ndipo unapoyaangalia maneno ya Yesu katika Mathew 5: 18 unajua kilichokuwa kinamaanishwa ( For truly I tell you, until heaven and earth disappear, not the smallest letter, not the least stroke of a pen, will by any means disappear from the Law until everything is accomplished) – Zingatia sentensi ‘Until everything is accomplished’ ndiyo iliyobeba maana ya tungo nzima

  Kwa mpangilio mzuri zaidi alichokisema ni hiki – For truly I tell you, until everything is accomplished, not the smallest letter, not the least stroke of a pen, will by any means disappear from the Law, even if (until) heaven and earth disappear.

  This is conditional statement, kufika mwisho kwa torati hakuko under condition kwamba mpaka mbingu na nchi zipite, ila iko under condition kwamba mpaka yote yaliyoandikwa kuhusu torati yatimie ndipo torati itafika mwisho wake, hata kama kutimia kwake kutachukua muda mpaka siku mbingu na nchi zinatoweka.

  But the good news ni kwamba yaliyoandikwa katika Torati na manabii yalishatimia.

  Mstari wa Luka 21: 33 unaongelea kitu kingine. (32 “Truly I tell you, this generation will certainly not pass away until all these things have happened. 33 Heaven and earth will pass away, but my words will never pass away).

  Mstari huu unaongelea habari za maneno ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake walipomuuliza kwa habari ya mambo ya siku za mwisho, akisema kuwa lazima mambo hayo aliyowaambia yatatimia katika kizazi hiki. Hakuwa anaongelea torati hapa.

  Na kama wewe ni msomaji mzuri utagundua kuwa maneno ‘mbingu na nchi kupita’ yalikuwa ni msemo tu katika nyakati za Yesu, msemo wenye kuonesha uhakika wa kutimia kwa jambo fulani ambalo msemaji amelisema. Kwa sababu ukiangalia sentensi hiyo ilivyotumika hapa haioneshi kuwa hayo maneno ambayo Yesu aliyasema kutimia kwake ni mpaka mbingu na nchi zifike mwisho, maana tayari ameshasema lazima yatime kwenye kizazi hiki, na siku mbingu na nchi zinafika mwisho hakitakuwa kinaendelea kuwepo

  Nimeandika sana, nitaendelea…..

 77. Sungura,
  Kwanza, Mungu akubariki sana kwa vile umezikubali facts zangu, japo kwa kuzipunguzia hadhi ya kuziondoa kwenye reli ya ukristo. Niseme tu kuwa, kulielewa Agano la Kale ni muhimu kuliko unavyodhani, maana huwezi kulielewa Agano Jipya usipolielewa kwanza Agano la Kale. Huwezi!! Utaendelea kubisha na kubisha weee hadi kunakucha tu!
  Pili, kumwelewa Mungu ndio msingi wa wokovu kwa mwanadamu yeyote! Natambua kuwa hatuwezi kumfahamu Mungu kwa 100% maana akili zetu zina ukomo. Lakini kwa kile kiwango alichojifunua kwetu, tunapaswa kumwelewa kwa namna ile. Kuanzia Agano la Kale hadi Agano Jipya, Biblia inamtaja Kristo kama mzaliwa wa kwanza wa Mungu. Siyi amamwamini Mungu mmoja –YEHOVA mwenye mtoto wake Yesu Kristo. Natambua hili ni fundisho geni kwa wakristo walio wengi hasa wa kijumapili!Lakini ukweli wa Maandiko ndio huu, kwamba kuna Mungu mmoja aliye na mtoto mmoja –Yesu Kristo, full stop! Ukiendelea kulishwa unga wa ndele kuwa Mungu Baba ndiye Yesu Kristo, utakesha tu! Changamka! Haya siyo ya fikra kijana, bali ni uhalisia wenyewe wa maandiko!
  Tatu, habari za kutolitaja bure jina la Mungu iko palepale. Haina cha Agano la Kale wala Jipya! Habari ya Amri 10 za Mungu, ziko palepale, hakuna cha Agano la Kale wala Jipya. Yesu alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu (Sheria zake) hayatapita kamwe”- Luka 21:33. Kwa maneno mengine, “… ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati”- Luka 16:17. Kwa kutumia akili ya kawaida tu (ya kula ugali wa dona na mlenda), mbingu na nchi havijaondoka, vitu ambavyo ni rahisi kuondolewa kuliko TORATI yenyewe! Wewe unasemaje leo kuwa torati imeondolewa hata kabla ya mbingu na nchi? Daah! Na watu wanakufundisha hivyo na wewe unaendelea tu kuwasikiliza pamoja na akili yako yoooote hiyo Sungura? Unasikitisha sana rafiki yangu wewe!! Mungu akusaidie aisee!
  Nne, Ezeliel 12;20, na 20:20, inatoa taarifa za jumla kuhusu Sabato za majuma yote. Sabato ambayo ishara au alama ya Mungu muumbaji ni Sabato ya Amri ya Nne tu. Hii ndiyo Sabato inayomtambulisha Mungu kuwa Yeye ni Muumbaji wa mbingu, nchi na vyote vilivyomo. Uumbaji, utawala, umiliki, n.k., ni alama au ishara inayomtambulisha Mungu –YEHOVA dhidi ya miungu wengine wote wa dunia. Na alama au ishara hii, inaonekana kwenye amri ya nne –Ikumbuke siku ya Sabato uitakase, Kutoka 20:11. Hata kitabu cha mwisho wa Biblia –ufunuo, kinatoa wito wa kumwabudu Mungu mmumbaji na siyo miungu wengine… “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. MSUJUDIENI YEYE ALIYEZIFANYA MBINGU NA NCHI NA BAHARI NA CHEMCHEMI ZA MAJI”.- Ufunuo wa Yohana 14:7. Mungu anayepaswa kuabudiwa kaka ni Mungu muumbaji! Wewe kama unamwabudu mungu asiyetajwa kwa sifa hizi ambazo kimsingi ndio utambulisho wa Sabato, shauri yako. Utaliwa usipoangalia!!

  Tano, kuhusu habari za wanamatengenezo kusali jumamosi, kama msingi wako wa kuhalalisha watu kusali jumapili, inabidi uelewe tu kuwa, hawakuwa na uelewa wote kuhusu mpinga Kristo na alama yake! Walichokuwa wakikipinga zaidi wao kilikuwa ni baadhi ya man made creeds vs the Bible teachings. Hata hivyo, hizo creeds hawakuzimaliza kuzisema ndiyo maana Warumi waliwaua kikatili. Hata sasa, wapo wajumapili wanaopinga man made creeds zinazoingizwa makanisani mwao, japo hawajazielewa creeds hizo zote! Wana sifa ya kuitwa wanamatengenezo tu japo hawajawa sahihi kwa asilimia 100. Pamoja na wao kuwepo, ukweli wa Biblia leo ndio unaomfanya Siyi, na wengine wote kusimama katika huo hata kama kuna watangulizi/wanatamatengenezo ambao hawakuwa na nuru ya Biblia 100%. Hatutaenda mbinguni kwa sababu ya jitihada za wanamatengenezo, bali kwa njia ya KWELI itakayotuweka huru.
  Sita, habari za kumdhihirisha Mungu wa kweli, siyo jambo la konfuu kaka! Ni jambo ambalo limekuwepo tangu zamani. Na siyo kwamba watu wenye maradhi au mapepo hawakuwepo; walikuwepo lakini ilipofika hatua ya kumdhihirisha Mungu wa kweli, matukio ya namna hiyo yalifanyika tu na mambo yakawa bayana! Leo naweza kumwombea mtu akapona na kwa upande mwingine bado akafa tu kama Mungu atakuwa karuhusu hivyo. Lakini kwa habari ya mapepo, hayo ni lazima yatoke. Hapo hakuna mjadala! Yote haya nikiyafanya, hakuna haja ya kutaka nijulikane. Kama wewe unaamini kweli kuwa unayemwabudu ni Mungu, sidhani kama ungepata kigugumizi cha kwenda kumdhihirisha huyo Mungu wako! Unamwonea aibu Mungu?! Pole sana, jua unaabudu kinyago rafiki yangu. Toka huko mapema!
  Saba, nashukuru kama umekiri kuwa miujiza siyo kigezo pekee cha kukufanya uamini hiki na kile uache, kama ulivyodai siku ile! Miujiza hata kwa wapagani ipo na ilikuwepo tangu agano la kale mpaka leo na itaendelea kuwepo hadi Yesu atakaporudi! Lakini pamoja na hayo, Mungu na neno lake, are unchangeable! They are there to stay for ever! Mungu wa Agano Jipya ndiye Mungu wa Agano la Kale. Ukifundishwa tofauti na hivyo, imekula kwako! Nami nakupendekezea kuwa, usidanganyike! Changamkoa bado kungali mapema!
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 78. Siyi,
  Facts zako unazotoaga huwa ni facts lakini katika mwelekeo fulani ambao ambao hauko sawasawa kwenye reli ya Ukristo.
  Unajaribu sana kuuelewa ukristo kwa Agano la kale, hivyo unajikuta facts unazotoa haziko relevant sana na ukweli wa Agano jipya ambalo ndo msingi haswa wa Ukristo. Na matokeo yake unabaki kunishangaa na kutokunielewa sawasawa.

  E.g; Kujaribu kusema kuwa neno Bwana humrejerea Kristo na BWANA humrejerea Mungu Baba,tena kwa sababu za waandishi wa Biblia fulani ni kutaka kujenga msingi kwamba Mungu ni kitu kimoja, Yesu ni kitu cha pili, tena kwa mtazamo kwamba Mungu ni mkubwa, halafu Yesu anafuatia!
  Hapo kuna fikra fulani haiko sawa!

  Ulishawahi kujiuliza kwa nini wa agano la Kale waliambiwa wasilitaje bure jina la Bwana Mungu, na unajua inahusikaje hiyo na Agano jipya?

  Ivi unajua Mungu alisema zamani kuwa mwanadamu hawezi kumwona uso akaishi, ivi unafikiri mpaka kwenye Agano jipya hiyo iko hivyo?

  Tena, Sabato alizotoa Mungu ziwe ishara zilikuwa ngapi, na ninyi mnashika ngapi? Maana hilo andiko la Ezekiel limesema ”sabato zangu” siyo sabato yangu!

  Nikikunukuu, umesema ”kuhusu Papa kuwa ni mpinga Kristo, hiyo siyo sera ya wasabato bali sera ya Biblia. Hata wanamatengenezo wa zamani akina Martini Luther, John Wisley, John Huss, Latmer, Tindely na wengine wengi, walisema kuwa Papa ndiye mpinga Kristo, mtu wa kuasi! Na alama yake ni Jumapili –Sunday”
  Kuwataja hao unaowaita wanamatengenezo kunamaanisha unakubali kazi zao na kuwakubali wao wenyewe.

  Sasa niambie, Je Martin Luther alikuwa msabato (hakusali J2), John Wisley alikuwa msabato ( hakusali J2)?

  Mpiga nkung fu wa uhakika ukimwambia kuwa uwezo wake ni mdogo, huwezi kumsikia anakwambia kuwa hebu njoo tujaribu kupigana ili tuone nani zaidi, ukisikia anasema hivyo ujue huyo ni kanjanja, hajui hata kanuni za huo mchezo.

  Siyi kukusikia unaniambia kuwa tukashindane kutoa mapepo au kuponya wagonjwa ili kujua nani ana nguvu ya Mungu ni upunguani wa hali isiyo ndogo. Hii Tz siyo kubwa na imejaa nguvu ya media siku hizi, ungekuwa ulishawahi kuponya hata mmoja au kuangusha chini wachawi wawili tungeshasikia mbona!

  Na hata sasa hujachelewa, kuna wagonjwa wengi hospitali wamekaa miaka nenda kadhihirishe nguvu zako huko, Sungura atasikia tu habari.

  Sijui kama umegundua kuwa sija-initate wazo la kwamba Miujiza na maajabu hutoka kwa Mungu tu, sasa sijui hiyo habari ulikuwa unamjibu nani.

  Miujiza inayotoka kwa shetani nafikiri ni pamoja na hiyo anayotaka Siyi akashindane na Sungura.

  Kwa kujaribu kusema kuwa kusali au kutofanya kazi siku ya sabato ndio msingi wa ukristo unaokufanya ujaribu kusema kuwa wako ni Mungu wangu ni mungu, ni kuwa na akili ndogo isiyojitambua. Kwenye makala yangu nilikwambia kuwa Mungu wangu yu afanya kazi mpka Jumamosi, na Jumapili, na Jumatatu na siku zote, hivyo nami nafanya kazi!

  Mjue Mungu wa agano Jipya Siyo ili ufahamu wako upate kufunguliwa. Hujawahi kumjua huyo Mungu, ndo maana hata rejea zako zote ni za agano la kale tu, ispokuwa hiyo ya miujiza uliyomnukuu Mark, ambayo lakini si msingi sana wa mada yetu!

 79. Sungura,
  Kwanza, mara nyingine huwa unachekesha saaana rafiki yangu. Yaani huwa hutaki kuona jambo jipya kwako likisemwa na mtu mwingine hasa asiye wa imani yako! Lakini pia, huenda ni tabia nzuri hiyo ya kutaka kujua zaidi habari ya jambo hilo jipya ulilolisikia/kuliona! Na pengine, huenda unayajua vizuri mambo mengi, ila huwa unataka kujua tu kama na watu wengine wanayafahamu kama unavyoyajua wewe! Kimsingi, wewe ni mtu wa ajabu sana! Pamoja na hayo, Mungu anakupenda saaana, yaani hadi nashangaaga!
  Pili, habari za maneno BWANA na Bwana haya ni majina mawili ya Mungu (cheo). Jina Mungu ni cheo tu ndugu yangu. Majina halisi ya Mungu ndiyo hayo niliyokutajieni siku ile. Amri ya 3 inasema, “Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure”- Kutoka 20:7, Kumbukumbu la Torati 5:11. Kumbuka nilisema kuwa, “MARA NYINGI” katika Biblia neno BWANA, humrejelea Mungu –YEHOVA na neno Bwana humrejelea Kristo. Pamoja na hayo, bado kwa kiasi fulani maneno haya katika tafsiri ya Kiswahili SUV yametumiwa interchangeably! Lakini katika Biblia ya KJV, wafasiri wa Kiingereza wameyaweka vizuri kwa kiasi fulani. Kwa sehemu kubwa, neno BWANA (LORD), limetumika kumrejelea Mungu –YEHOVA. Kwa mfano, rejea aya tajwa hapo juu katika Biblia ya KJV. Na Neno Bwana (Lord), limetumika kumrejelea Kristo. Kwa mfano rejea Mathayo 17:4 katika Biblia ya KJV/SUV. Hivyo, neno lenye herufi kubwa (BWANA), hutumika kumrejelea Mungu Baba na neno (Bwana) lenye herufi ndogo, hutumika kumrejela Mungu Mwana. Kwa maana hiyo, YEHOVA ni Mungu na Yesu ni Mungu. Haya mambo yako bayana kiasi hicho ndugu yangu.

  Tatu, jambo lingine la msingi hapa, ambalo hata mimi mwenyewe huwa najikuta naanguka kila mara hasa wakati wa maombi ni uvunjaji wa amri ya 3, -“Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure”- Kutoka 20:7, Kumbukumbu la Torati 5:11. Watu wengi sana huwa tunaivunja amri hii wengine bila ya kujua na wengine kwa makusudi kabisa! Na kwa isivyo bahati, huwa hatukumbuki hata kutubu kwa dhambi ya uvunjaji wa amri hii. Mtu mwingine anaweza kujiuliza, jina la Bwana ni lipi? Ndani ya Biblia, Mungu ameonekana kujitaja mwenyewe. Jila lake halisi ni YEHOVA! Biblia inasema katika;

  Kutoka 6:2 Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA;
  Kutoka 6:3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
  Kutoka 6:6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
  Kutoka 6:7 nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwatoaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.
  Kutoka 6:8 Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo naliinua mkono wangu, niwape Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA. n.k.

  Hili ndilo jina ambalo huwa hatupaswi kulitaja ovyoovyo!! Kwa mujibu wa The Online Bible Encyclopedia, jina hili lilikuwa likitajwa mara moja tu kwa mwaka tena na Kuhani Mkuu kunako siku kuu ya upatanisho. Insaiklopidia hiyo inasema, “The name YHWH occurs 6,828 times in the Hebrew Bible, including all books but Ecclesiastes, Esther, and Song of Songs.1 This name, the Tetragrammaton of the Greeks, was held by the later Jews to be so sacred that it was never pronounced except by the high priest on the great Day of Atonement, when he entered into the most holy place”. http://www.christiananswers.net/dictionary/jehovah.html. Hivyo ndugu yangu Sungura, ni vizuri ukaelewa na ukajitambua kama mkristo asiyebahatisha mambo, vinginevyo, utaishia kuitwa mkristo tu, halafu ukaja kupotea bure!

  Nne, mimi sina ubavu wa kujihesabia haki ndugu yangu! Na wala sina ubavu wa kujiweka juu yako! Sina kabisa! Hizo ni tafsiri zako tu. Nilichokisema siku ile na ninachoendelea kukisema hata leo ni hiki, kwamba, Mungu wangu ninayemwabudu, si sawa na mungu wako unayemwabudu! Si sawa kabisa! Mimi namwabudu Mungu, jina lake ni YEHOVA/YAHWE ambaye keshaweka ishara ya utambulisho wake mwenyewe na watu wake –Sabato. Biblia inasema, “Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye”- Ezekieli 20:12. “zitakaseni sabato zangu; zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu”- Ezekieli 20:20. Wewe na wenzako mliojitafutia sabato zenu bandia –za kijumapili, mmeshaikataa ishara ya Mungu –Sabato. Kama mmeshakataa utambulisho wake, bado unaendelea kulalamika kuwa mungu unayemwabudu si sawa na Mungu wangu? Haya endelea kubisha, lakini ukweli ndio huo! Kama usabato ni udhaifu wa imani, Mungu ndio ameamua kuutumia kujitambulisha kwetu.

  Tano, kuhusu Papa kuwa ni mpinga Kristo, hiyo siyo sera ya wasabato bali sera ya Biblia. Hata wanamatengenezo wa zamani akina Martini Luther, John Wisley, John Huss, Latmer, Tindely na wengine wengi, walisema kuwa Papa ndiye mpinga Kristo, mtu wa kuasi! Na alama yake ni Jumapili –Sunday! Haya si maneno ya wasabato, ni maneno ya Biblia na wanamatengenezo wa zamani. Kama umewaona wasabato wameshaanza kukaa kimya kutosema kuwa Papa ni mpinga Kristo na alama yake ni jumapili, wanapika siku ya sabato n.k. jua kuwa wameshaanza kupoteza mwelekeo. Siyi hajaanza kupoteza mwelekeo huo! Wapo na wengine wachache ambao hawajaanza kupoteza mwelekeo wao sahihi.

  Tano, kuhusu uwezo wa wasabato spiritually kuwa ni dhaifu, nadhani kwa mawazo yangu unaweza kuwa uko sahihi. Sisi wenyewe (Wasabato) kama binadamu tu, hatuna uwezo wowote spiritually. Hatuwezi kitu isipokuwa tumekaa ndani ya Pendo la Kristo. Yesu alituambia kuwa, “Ninyi (wasabato) mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”. Hivyo ukiona wasabato wanafanya jambo lolote spiritually, fahamu kabisa, wanatenda si kwa uwezo wao wenyewe bali wanatenda kwa uwezo wa Kristo pekee. Na kwa uwezo huo wa Kristo, ndio maana akina Siyi tunao ujasiri mkubwa wa kusimama kinyume na nguvu za giza, wachawi, shetani na mapepo yote. Ukibisha, wewe niite hata mimi tu (mtu mdogo kabisa) na wewe ili twende popote pale kwa mgonjwa au mwenye pepo, tukadhihirishe nani anamwabudu Mungu wa kweli! Hata kipindi fulani, nilikwambia maneno haya ukadhani ni utani. Narudia kusema tena, usiandikie mate na wino upo kaka!

  Sita, wengi hudhani kuwa wakiona miujiza, maajabu, maponyo n.k., hutoka kwa Mungu tu. Hii ni ajabu sana! Hata wewe mtu mwenye akili zako, bado una akili zilezile! Mungu hufanya miujiza na shetani pia hufanya! Hivyo Mungu hatumpimi kwa miujiza tu ndugu yangu. Kama unategemea miujiza tu, imani yako iko mashakani sana. Jitahidi (soma) kungali mapema! Biblia inasema, “kwa maana wataondoka Makristo wa uongo, na manabii wa uongo, watatoa ishara na maajabu, wapate kuwadanganya, kama yamkini, hata hao wateule”- Marko 13:22. Biblia ilishakuonya mapema, jitahidi kujua ni miujiza ipi hutoka kwa Mungu na ni ipi hutoka kwa ibilisi na mawakala wake! Changamka Sungura aisee!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 80. Siyi,

  Kwamba neno Bwana mara nyingi linapoonekana kwenye Biblia humrejelea Kristo Mwenyewe! Neno BWANA, humrejelea Mungu Mwenyewe –YEHOVA.
  Hii nayo siyo kweli, lazima ni mawazo ya mtu fulani tu amekulisha, otherwise prove me wrong!
  Unaposema Mungu mwenyewe kichwani mwako una picha gani, kwamba Yesu siyo Mungu mwenyewe au?

  Halafu kujaribu kuniambia kuwa simwabudu Mungu, ni wazo la kipuuzi sana na kujaribu kuijihesabia haki kusiko na msingi wowote, au nisemae ni kuyakufuru usiyoyajua.
  Je ni kwa sababu nimekwambia kuwa mbuzi wa Bwana,mbuzi wa azazeli, ng’ombe wa kuhani, na kondoo wa kafara wote walimwakilisha kristo, au ni kwa sabau mimi sikusanyiki Jumamosi au ni kwa sababu ipi ndo unajaribu kujihesabia juu yangu?

  Kati ya imani ambazo ni dhaifu kabisa kwa habari ya uwezo wa rohoni ni pamoja na usabato. Tena afadhali sasa hivi kwa sababu kuna facts angalao mmeanza kuzikubali, zamani ndo mlikuwa wajinga kabisa. Habari za Roho mt., habari za kutoa mapepo, ndo mmeanza kuzielewa siku hizi tu.

  Eg;Mmepunguza juzi tu kuwadanganya watu kuwa papa wa wakatoliki ndo mpinga kristo, ndo mnyama, lakini tangu na tangu mmekuwa mkiaminishwa hivyo na walimu wenu wenye kujaribu kutafsiri unabii wa biblia kwa akili, mlikuwa mnakula vipolo Jumamosi, siku hizi mmeacha – Je huko ndiko unakoniambia kua wewe unamwabudu Mungu wa kweli?

  Wasabato hamna uwezo wowote spiritually, hamwezi hata kumtisha mchawi, ninyi ni ichabodi kabisa, japokuwa mnajaribu kujitutumua siku hizi, lakini bado. Ninyi ni imani dhaifu sana kwa habari ya kutembea na Mungu, mmekalia kulazimisha ku-apply agano la kale leo (kuweka divai mpya ndani ya kiriba cha zamani), lakini nyakati si zenyewe, matokeo yake torati humwiwezi na kanuni za agano jipya mnazihalifu.

  Je kusali Jumamosi huko ndiko kumwabudu Mungu, kutokula nguruwe huko ndiko kumwabudu Mungu, who told u Mungu huwa hafanyi kazi Jumamosi? Hujui Yesu alichowajibu wasabato wenzako – John 5: 17 – In his defense Jesus said to them, “My Father is always at his work to this very day, and I too am working.”
  Na mimi kwa kujua kuwa hata sasa Mungu hufanya kazi hata Jumamosi, na mimi nafanya kazi Jumamosi, hata Jumapili pia Siyi!

  Mambo ya kujaribu kusema mimi simwabudu Mungu, ofcourse hayawezi kunipunguzia chochote, lakini nataka tu ujue kuwa matukano ya namna hiyo ni hatari kwa roho yako. You better be careful!

  Najua kitu kimoja kuwa sikuwa tu mwenye dhambi, bali nilijaribu sana kuacha dhambi sikuweza, nilikuwa na maradhi hayakuweza kupona kwingine kokote, ispokuwa siku nilipokutana na Yesu mahali, haya yaliisha na kukoma kabisa.

  Lakini kwa taarifa yako sikukutana na Yesu kwa wasabato japokuwa nilikuwa nao siku zote, wala sikukutana na Yesu kwenye kusanyiko la Jumamosi!

  I think you’ve got that clear!

 81. Sungura,
  Kwanza samahani kwa kuchelewa kukujibu mapachiko yako.
  Pili, nashangaa kuona bado unaendelea na hoja zilezile nilizokujibu siku ile. Nilikwambia kuwa, mbuzi wa azazeli si sawa na na mbuzi wa Bwana. Mbuzi wa azazeli, hakuangikwa msalabani, lakini mbuzi wa Bwana aliangikwa (kwenye madhababu ya mawe) nje ya hema. Kumbuka, hiki kichanja (kimadhabahu), kilikuwa nje ya patakatifu! Hii inaashiria kuwa, Yesu angekuja kusulubiwa nje ya mji wa Yerusalemi juu ya kilima (kimadhabahu). Upatanisho wa sikukuu (Yom Kippur), uliashiria mwisho wa wakati! Mbuzi wa Bwana (ndiyo maana anaitwa mbuzi wa Bwana (Masihi), huyu alimwakilisha Kristo. Kumbuka neno Bwana mara nyingi linapoonekana kwenye Biblia, humrejelea Kristo Mwenyewe! Neno BWANA, humrejelea Mungu Mwenyewe –YEHOVA. Mbuzi wa azazeli (asiyefaa, mwenye kusababisha matatizo, shida, n.k.), huyu alimwakilisha shetani. Na ili kukiondoa chanzo cha matatizo katika jamii, baada ya toba (upatanisho wa mwaka), chanzo hicho (mbuzi wa azazeli), kilipelekwa mbali jangwani kikafie huko kama ishara ya kuyafutilia mbali mabaya, maovu, shida, matatizo n.k. katika jamii. Ukiona bado hunielewi rafiki yangu, wewe jifunze polepole Biblia. Omba sana, utaelewa tu.
  Tatu, unaweza kudhani kuwa unamwabudu Mungu muumbaji –YEHOVA; nasikitika kukwambia kuwa sivyo!! Najua utaudhika na kuniita mjinga, lakini ukweli ndio huo!! Kutumia herufi ndogo kumwita mungu wako, nilikuwa sahihi na niko sahihi mpaka sasa!! Unachopaswa kukifanya ni wewe kujiuliza kama uko sahihi na hicho unachokiamini bila ya kuhusisha hisia zako binafsi, aibu n.k. Maana kumbuka Biblia inasema kuwa, “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote” Efeso 4:4-6. Kama imani ni moja tu kama Mungu alivyo mmoja, je unafikiri wewe binafsi unamwabudu Mungu huyo? Je, makanisa mengine, yanamwabudu Mungu huyo vilevile? Kama jibu ni ndiyo, basi Biblia inaongopa! Lakini kama Biblia iko sahihi, ni wakati wa wewe kujiangalia kama unafiti kwenye vigezo vya uchaji Mungu kwa mujibu wa Biblia na si mapokeo!!

  Nne, katika kujibu maswali yako on the serious note; umeuliza,
  1. A. sasa niambie wapi biblia inakwambia kuwa shetani atakuja kubebeshwa furushi la dhambi?
  Jibu;
  Lawi 16, 33

  B. na wapi pia inakwambia kuwa siku ya kiyama shetani atauliwa!
  Jibu;
  Ufunuo 20: 9-10 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

  2Petro 3:7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. (wewe Sungura unafikiri, Ibilisi anamcha Mungu?)

  Ufunuo 12:9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

  Ufunuo 19: 20-21 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.

  Ufunuo 20:15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. (na unafikiri Ibilisi naye ameandikwa kwenye kitabu cha uzima?)

  Nafikiri aya hizi chache zinakutosha…

  Tano, nikikwambia una akili ndogo sana rafiki yangu, bado unajustify udogo wa akili yako kwa kuihafifisha mada kuwa si jambo zito lenye kuhitaji kusugua kichwa. Wewe ni talanje kwelikweli rafiki yangu! Mtu aliye sawa kifikra, hawezi kusema hivi, nakunuu, “Nilikwambia kuwa kusema kwamba Kristo, yeye anabebeshwa dhambi na kila mtu anayeamini leo- hii siyo sawa.” Unaona sasa??!!
  Kama Yesu alishabeba dhambi za wanadamu wote miaka 2000 iliyopita, unafikiri kuna mtu atachomwa moto siku ya mwisho kama Biblia inavyosema? Rejea aya chache za Biblia hapo juu. Kama na wasiomcha Mungu dhambi zao zilishabebwa na Kristo, huoni kuwa hakuna haja kwa yeyote sasa kuwa muumini au mfuasi wa Kristo? Na huoni kuwa, hata kama tutaendelea kutenda dhambi, hakuna shida yoyote maana Kristo alishabeba dhambi zetu? Huu ni ufedhuli na uasi uliovuka mipaka Sungura. Kama una mawazo potovu ya namna hii, katubu mapema rafiki yangu. Huna asubuhi kabisaaa!! Kwako ni giza tu!! Isaya 5 inaposema hivyo, huzungumzia wale tu wanaomkubali na kumpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Wale wasiomwamini, barabara yao ni ileile –uangamivu wa milele.
  Ukiendelea na imani potovu ya namna hiyo, hatima yake utapotea tu. Mungu alishatupa chaguzi mbili za kufanya –uzima wa milele kwa njia ya imani kumwamini Kristo (kumchagua Yesu) na mauti ya milele kwa njia ya kuendelea na maisha yenye asili ya dhambi. Kama humchagui Kristo, hakuna ondoleo la dhambi. Yesu anasema, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi” –Mathayo 11:20-30.

  Uchaguzi ni lazima. Toka kwa ibilisi uende kwa Kristo!

  Neema ya Bwana ikufunike.

  Siyi

 82. Siyi,

  Kuhusu maana ya kuwa rohoni hiyo ni mada nyingine, kuijibu hapa ni kuanzisha kitu kingine kabisa. Nenda tu kajifunze rohoni ni wapi, kuwa rohoni ni kupi, na mambo kama hayo utapata majibu.

  Kuhusu dhambi zangu mimi huwa nambebesha nani:

  Nilikwambia kuwa kusema kwamba Kristo, yeye anabebeshwa dhambi na kila mtu anayeamini leo- hii siyo sawa.

  Nilikwambia si sawa kwa sababu dhambi za watu wote Yesu alishazichukua miaka 2000 iliyopita akapanda nazo msalabani, akamaliza hiyo kazi. Hakuja duniani kukusanya dhambi za watu ili akae nazo mkono wa kuume wa Mungu.

  Inasema hivi biblia; Isaiah- 5 But he was pierced for our sins,

  crushed for our iniquity.

  He bore the punishment that makes us whole,

  by his wounds we were healed.e

  6 We had all gone astray like sheep,

  all following our own way;

  But the LORD laid upon him the guilt of us all.

  Ndo hapo sasa nikakuuliza kama unaelewa maana ya imani.

  Yesu alishatusamehe siku nyingi, alishabeba dhambi zetu siku nyingi, maana ilikuwa ni lazima dhambi zako na zangu apande nazo msalabani ndipo ziondolewe.

  Utaniuliza ‘kwa hiyo tusitubu kama ni hivyo? nami nitakuuliza kwa hiyo tusiombe maana kabla hatujaomba keshajibu? – Hiyo ndo maana ya Imani!

 83. Siyi,
  Kabla sijajikita kukujibu kwenye mada, ngoja kwanza nijibu haya makandokando.

  Upumbavu, ujinga, siyo matusi bali ni sifa stahiki ya mtu fulani kutokana na uelewa wake ulivyo.

  Umeniambia nina akili ndogo, hilo laweza kuwa ni kweli, lakini inategemeana na umenilinganisha na nani. Lakini kwa jambo kama hili ambalo hata halihitaji akili kubwa lazima nishughulike nalo kwa kutumia akili ndogo tu.

  Mwisho, usichanganyikiwe mpaka ukasahau kuweka paragrafu kwenye makala zako, kama ulivyofanya hapo chini.
  ………………………………………………………
  Narudi kwenye mada:

  Sehemu iliyokufanya uone kuwa nina akili ndogo ni pale nilipokukatalia vigezo ulivyosimamia kutofautisha mbuzi wa azazeli na Kristo, na kumfananisha mbuzi wa Bwana na Kristo(mwanakondoo wa Mungu), nikakwambia kuwa wewe unajaribu kutumia tafsiri sisisi, kwa kule kusema kwako kwamba mbuzi wa azazeli alifanyiwa kitu fulani lakini Kristo hakufanyiwa.

  eg; Ulisema mbuzi wa azazeli, baada ya kupelekwa nyikani, hakurudi tena. Mwanakondoo wa Mungu baada ya kufa, alifufuka!! Damu ya mbuzi wa azazeli, haikutumika kwenye upatanisho wa mdhambi, n.k.

  Ukiendelea kusoma paragrafu zangu nimekwambia kuwa kuna mambo mengi tu ambayo Kristo alifanyiwa lakini mbuzi wa Bwana hakufanyiwa. Eg, Kristo aliwekwa msalabani lakini mbuzi wa Bwana hakuwekwa msalabani.

  Kwa hiyo mfananisho na mtofautisho uliotumia haukizi vigezo, unabaki kuwa kitu cha kusadikika tu.

  Kwenye hili swali ulikuwa unauliza nini sasa? hebu ona lilivyo: ‘Au unafikiri Yesu alishakufa mara moja, safari nyingine atakuja afe tena?’
  Siyi umechanganyikiwa!

  Lakini kituko kikubwa kuzidi ni hiki, nakunukuu ”Nikakwambia pia kuwa, hata shetani naye alikuwa na kivuli vilevile hadi atakapouliwa siku ya kiyama!’ Ati kwamba siku ya kuyama shetani atauliwa? aise, hii ni kali ya mwezi.
  Nikiijumlisha na ile ya shetani kuja kubebeshwa furushi lake la dhambi, ambayo in fact hujaijibu mpaka sasa, najiuliza sana kuwa unapata wapi ujasir wa kumwita Mungu wangu ‘mungu’ na wa kwako ‘Mungu’. Lazima huu ni ujasiri ulifichama kwenye ujinga.

  On serious note, sasa niambie wapi biblia inakwambia kuwa shetani atakuja kubebeshwa furushi la dhambi, na wapi pia inakwambia kuwa siku ya kiyama shetani atauliwa!

 84. Sungura,
  Mimi sina shida na wewe kuniita mbumbumbu, mjinga, mpuuzi n.k. Sina shida kabisa. Na wala usiwe na shida kwa matusi uliyootoa kwangu. Uwe na amani tu, maana najua ninajibizana na mtu wa namna gani!! Hilo halinipi shida kabisa ndugu yangu.
  Umeniambia kuwa maswali yako sikuyaelewa na hivyo nimeenda chaka na ulivyotaka nijibu!! Sawa!! Lakini hata kama utakataa wewe kukutolea mfano, unadhani unachokiamini wewe, ni sawa na ninachokiamini mimi????? mungu unayemwamini wewe unafikiri ni Mungu yuleyule anayeabudiwa na Siyi?? Nikwambie hasha!! So, kusema in refrence of you wala sikuona shida au tatizo. Sema wewe ndiyo mwenye matatizo makubwa rafiki yangu!! Kichaa huwa hajijui kama yeye ni kichaa, isipokuwa wenye akili timamu!!
  Na swali lako la pili, nililitendea haki kabisaa!! Ila kwa vile hutaki kuelewa, utabaki hivyohivyo tu!! Nilikwambia kuwa, katika Agano la Kale, Yesu alikuwa na kivuli kuanzia jina lake hadi umauti. Nikakwambia pia kuwa, hata shetani naye alikuwa na kivuli vilevile hadi atakapouliwa siku ya kiyama!! Na baadhi ya majina/sifa zao hawa mafahari wawili (Yesu na ibilisi), nilikutajia. Lakini nakuona unabisha tu. Kama unataka tafsiri sisisi ya vivuli hivyo, utakesha!!
  Swali la tatu unabisha sijalijibu. Ona unavyolalamika “Umesema kuwa mbuzi wa azazeli alibebeshwa dhambi za Israel na kuhani mkuu- ni sawa, lakini ukasema tofauti na mwanakondoo wa Mungu, yaani Kristo, yeye anabebeshwa dhambi na kila mtu anayeamini leo- hii siyo sawa.”
  Kimsingi una akili ndogo sana sana sana Sungura (samahani kama utaliona hili ni tusi). Sasa kama unafikiri mbuzi wa azazeli alimwakilisha Kristo, ina maana Kristo alikufa mara mbili pale msalabani? Kumbuka mbuzi wa Bwana na mbuzi wa azazeli wote hawa walibebeshwa dhambi za waisrael!! Na hii ilikuwa ni siku kuu ya upatanisho!!! Au unafikiri Yesu alishakufa mara moja, safari nyingine atakuja afe tena? Au hiyo kwako wewe ilimaanisha nini? Hivi unakielewa kweli kile kilichokuwa kikifanyika siku ya yom kippur in relation to the coming judgement day? Na kama unakataa kuwa Yesu leo habebeshwi dhambi na kila mtu, wewe dhambi zako huwa unazipeleka wapi? Au huwa unaanzia kwa kasisi ndiyo kasisi naye anazipeleka kwa Yesu au ikoje hiyo?? Biblia inasema, “…ninyi ni mzao mteule, UKUHANI WA KIFALME, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” 1 Petro 2:9, wewe Sungura unaukataa ukuhani huu!!?? Unataka upi sasa? Mpaka hapa unafikiri unachoamini wewe na kile ninachokiamini mimi ni sawa? Fyutu!! Wewe unaamini Kristo aliingia patakatifu pa patakatifu once for all, na akatoka. Haingiiingii tena hapo kwa kila mtu anayemwamini!! Mimi naamini hivi, Kristo alipoingia patakatifu pa patakatifu, muda kitambo uliopita, bado hadi leo yuko hapo patakatifu pa patakatifu akiendelea kuupatanisha ulimwengu huu na Baba yake.Siku akitoka tu hapo(ambayo siyo mbali sana), itakuwa ni mwisho wa rehema!! Ndiyo maana mimi na wewe hatuwezi kwenda sawa kiimani. Wewe unavuta kuelekea kusini mimi naeleka Kaskazini, wapi na wapi sasa!
  Mwisho (kwa leo), hebu nisaidie maana ya kuwa rohoni/mambo ya rohoni na jinsi yalivyo tofauti na mambo ya mwilini!! Kwa uelewa wako wewe roho ni nini? Na kuwa rohoni maana yake ni nini?? Huenda tunaweza kusaidiana kuanzia hapo!!
  Siyi

 85. Siyi,

  Nikuombe radhi kwanza kwa hiki ambacho nataka kusema, in case kama utakiona kuwa ni kitu kizuri kukwambia.

  Siyi, nasema hivi; Kumbe wewe ni mbumbumbu kabisa wa mijadala, hata hujui kuona kona za kusimama kujibu hoja za mpinzani wako. Lakini pia wewe ni mjinga wa vitu vingi hata vya kawaida, na nina wasiwasi kuwa katika maisha yako ya shule ulikuwa/huwa unakisa maswali mengi kwa kushindwa kuelewa swali.

  Swali langu la kwanza hujalijibu, lakini kwa ujinga tu na kutokujua kusoma vema katikati ya mistari umelazimisha kuwa huyo mtu niliyekwambia ni mimi, hivyo ukajikuta unatoa maelezo ya tofauti ya imani kati ya mimi na wewe. Soma tena hilo swali na useme kama anachoamini huyo mtu ni tofauti na unachoamini wewe, siyo kutoa maelezo ya tofauti kati ya mimi na wewe.

  Swali langu la pili hujajibu; katika mikeka yako hakuna mahali ambapo umenipa mstari unaosema kuwa Azazeli ni shetani au kwamba alikuwa ni kivuli cha shetani. Ulichokisema hapo ni vile wewe unavyofikiri, lakini hajanionesha statement ya biblia inayosema kuwa azazeli ni shetani au kuwa kilikuwa ni kivuli cha shetani.

  Swali la tatu umejibu, lakini kijinga sana bila kuangalia mahali unaposimamia kama pako imara au la.
  Umesema kuwa mbuzi wa azazeli alibebeshwa dhambi za Israel na kuhani mkuu- ni sawa, lakini ukasema tofauti na mwanakondoo wa Mungu, yaani Kristo, yeye anabebeshwa dhambi na kila mtu anayeamini leo- hii siyo sawa.

  Ni kwamba, ukitaka kwenda kwa hiyo ambayo mimi naiita tafsiri sisisi utakwama tu lazima. Tukiamua tu kuchukua kuwa mbuzi wa Bwana wakati ule ndo Kristo leo lazima tukwame. Kwa sababu mbuzi wa Bwana wakati ule alitolewa kafara na kuhani mkuu, lakini Yesu hakutolewa kafara na kuhani mkuu, bali alijitoa kafara yeye mwenyewe akiwa kuhani mkuu yeye mwenyewe.
  Mbuzi wa Bwana hakuangikwa msalabani, lakini Kristo aliangikwa msalabani, hakupigwa mijeredi mbuzi wa Bwana, lakini kristo alipigwa sana

  Mbuzi wa Bwana alipotolewa kafara na yeye hakufufuka kama ambavyo mbuzi wa kafara hakurudi, lakini kristo alipojitoa kafara alifufuka, Hakuna kuhani mkuu aliyeingia patakatifu pa patakatifu akiwa na damu ya Kristo kama mbuzi wa Bwana, bali Krsito aliingia mwenyewe mahali hapo akiwa na damu ya kwake mwenyewe.

  Kwa hiyo kutorudi kwa mbuzi wa azazeli, kutupwa kwake jangwani si kigezo cha kukana kuwa mbuzi huyo hakuwa kivuli cha Kristo kama mwanakondoo azichukuaye dhambi za ulimwengu, maana hata mbuzi wa Bwana ambaye ndo wamkubali kuwa alikuwa mfano/kivuli cha kristo nae hakufufuka, na hakufanyiwa mengi sana ambayo Kristo alifanyiwa.

  Mtu anayetubu leo siyo kwamba ndo anambebesha dhambi zake Kristo, kuwaza hivyo ni kuonesha kwa kiasi gani hujui maana ya imani. Maana kama ni hivyo ingempasa kristo kuingia patakatifu pa patakatifu mara nyingi mno, na kufa na kufufuka tena mara nyingi mno.

  Lakini Kristo alifanya hivyo mara moja tu kwa sababu yeye alitoa damu ambayo ina nguvu kuliko ya damu ya wanyama hivyo hapaswi kufanya hivyo tena na tena, it’s just once for all!

  Swali la nne kuhusu shetani kubebeshwa furushi la dhambi siku moja ulichojibu ni kichekesho sana. Msabato weye hata aibu huna.
  Katika hayo yote uliyoyasema liko wapi linaloonesha kuwa shetani atabebeshwa furushi la dhambi siku moja?

  Naona ulichokiongea ni ndoto za alinacha tu,hapapo mahala ambapo shetani atabebeshwa mizigo. Kama hujui ni hivi, dhambi kwa shetani siyo mzigo, kama ambavyo inzi kwa uchafu siyo shida hata kidogo. Utakatifu ndio mzigo mzito kwa shetani!

  Fikiri vema nilichokwambia, kuwa ng’ombe wa kuhani ni kivuli cha Kristo, mbuzi wa bwana ni kivuli cha Kristo, mbuzi wa azazeli ni kivuli cha Krsto, kondoo wa kafara ni kivuli cha Kristo

  Wasabato mmepigwa chenga kubwa sana ya mambo haya, pale yanapotoka mwilini kuja kuwa mambo ya rohoni, na ninyi kubaki mwilini mkitaka kuyatafsiri yaliyo rohoni.

  Si shule nyepesi kwenu hii!

 86. Sungura,
  Nianze kujibu maswali tu.
  1. Unadhani unachokiamini wewe kiko sahihi kuliko anachoanini yule?

  Jibu
  Unachosema ni kweli kuwa, watu hatufanani katika kuamini. Ninachoamini mimi, sicho unachokiamini wewe! Hiyo iko dhahiri kabisa na hakuna anayepinga! La msingi ni hili; pamoja na tofauti zetu kiimani, Mungu hatatuonea haya endapo mmoja wetu atakuwa anaamini sicho!! Kumbuka, Mungu ni mmoja tu, imani yake nayo ni moja tu, ubatizo wake ni mmoja vilevile. Sasa mimi na wewe tunapokuwa na imani mbili tofauti, ni dhahiri kuwa, ni lazima mmoja wetu atakuwa chaka na mwingine atakuwa sahihi!! Ndiyo sababu ya kuwa na mijadala hii, kusaidiana wale tunaoamini vibwengo tukidhani ni Mungu, tujichunguze na kuzichunguza imani zetu kama ziko sahihi kwa mujibu wa maandiko. Maana hakuna kingine cha kutusaidia kuwa sahihi kiimani, isipokuwa maandiko –Biblia tu. Sharti tuache mitazamo yetu, hisia zetu, na fikra zetu binafsi ili tumsikilize Mungu anasema nini ndipo tutasalimika! Badala ya kuwa na negavity na Siyi au Sungura, chunguza kwanza kile anachokisema kama kinawiana na Biblia. Tofauti na hapo rafiki yangu, hakuna asubuhi!!
  2. Siyi mbona mimi sijaona mahali biblia inasema kuwa Azazeli ni shetani,na ndo alikuwa kivuli cha shetani agano la kale, unaweza kunionyesha tafadhali?

  Jibu
  Kuna aya nyingi sana za maandiko nimekuonyesha. Sina uhakika kama uliisoma mikeka yangu ya nyuma kwa umakini maana ulikuwa unalalamika tueti mirefu sana. Nikusihi uipitie tena polepole. Kuna aya nyingi nilizitoa humo zinazoonesha ushabihiano uliopo kuhusu swali lako hili. Reje huko tafadhali.

  3. Mbuzi wa Azazeli ndiye aliyebebeshwa dhambi zote za Israel katika agano la kale, kuna uhusiano wowote wa hilo suala na hili la mwanakondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu, katika agano jipya?

  Jibu
  Hakuna uhusiano wowote uliopo baina ya mbuzi wa azazeli katika agano la kale, na mwanakondoo aichukaye dhambi ya ulimwengu katika agano jipya. Mbuzi wa azazeli alibebeshwa dhambi za taifa zima na kuhani mkuu, mwanakondoo wa Mungu, anabebeshwa dhambi na kila mtu anapomwamini Kristo leo. Mbuzi wa azazeli, baada ya kupelekwa nyikani, hakurudi tena. Mwanakondoo wa Mungu baada ya kufa, alifufuka!! Damu ya mbuzi wa azazeli, haikutumika kwenye upatanisho wa mdhambi. Damu ya mwanakondoo wa Mungu, ndiyo iliyokuwa ikizifunika dhambi za waovu na kuondoka wakiwa huru kabisa! Na mengine mengi. Sina muda ningekutondolea mambo lukuki rafiki yangu.

  4. Sijawahi kusoma ktk Agano jipya mahali popote panaposema kuwa shetani kuna siku atabebeshwa furushi la dhambi za ulimwengu, hivyo naona hilo ni wazo la kusadikika zaidi. Ila kama papo nioneshe tu rafiki yangu, Biblia ni kitabu kikubwa sana!

  Jibu
  “Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele” –Ufunuo 20:7-10.

  Mstari wa 7-9, unzungumzia habari za ibilisi akiwa ruupango!! Moto ukashuka ukawala (wanadamu waovu) na Ibilisi, akatupwa kwenye ziwa la moto. Kwa nini anatupwa humo?? Dhambi ya udanganyifu hakuianza tu baada ya kutoka ruupango ya miaka ya elfu moja, bali aliianza tangu zamani. Anatupwa humo kwa sababu “aliwadanganya” waliounguzwa tayari na wale waliotubu dhambi zao, wakasafishwa kwa damu ya mwanakondoo. Neno kuwadanganya hapo, linarejelea kwa wote. Biblia inasema kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe!! Ni kweli kabisa. Waovu wataangamia kwa uovu wao wenyewe. Shetani ataadhibiwa kwa kuwadanganya hao waovu, na ataadhibiwa kwa makosa/maovu ya wale watakaosamehewa. Mshahara wa dhambi ni mauti, sharti mwanzilishi wa dhambi afe kwa uovu huo!! Hii ndiyo maana ya ibilisi kupokea mshahara wa shida (dhambi) aliyoianzisha mwenyewe!!Na baada ya hapo, ibilisi hatarudi tena. Hatatokea tena kama alivyoenda mbuzi wa azazeli!!

  Hiyo ndiyo dhana sahihi kati ya mbuzi wa azazeli na mbuzi wa Bwana/mwanakondoo wa Mungu. Mwisho tafakuri aya hizi kuhusu mbuzi hawa;

  Mbuzi wa Bwana (Mwanakondoo wa Mungu)
  “Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya kwa damu ya ng’ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao” – Lawi 16:15-16. Huu ulikuwa ni mchakato wa ukombozi wa mwanadamu.

  Hebu linganisha na huyu….

  Mbuzi wa Azazeli
  “Naye akiisha (Kuhani) kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai. Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani” –Lawi 16:20-22. Huu ulikuwa ni uteketezaji wa dhambi na mwasisi wa dhambi.

  Neema ya Bwana ikufunike.

  Siyi

 87. Siyi,

  Kuna mtu yeye anaamini kuwa Yesu yuko na dhambi zetu mpaka sasa patakatifu pa patakatifu, mwingine anaamini kama wewe unavyosema kuwa Mungu hana ushirika na shetani- yaani dhambi, kwa hiyo yeye na dhambi ni kama mashari na Magharibi.

  Unadhani unachokiamini wewe kiko sahihi kuliko anachoanini yule?

  Siyi mbona mimi sijaona mahali biblia inasema kuwa Azazeli ni shetani,na ndo alikuwa kivuli cha shetani agano la kale, unaweza kunionyesha tafadhali?

  Mbuzi wa Azazeli ndiye aliyebebeshwa dhambi zote za Israel katika agano la kale, kuna uhusiano wowote wa hilo suala na hili la mwanakondoo wa Mungu azichukuae dhambi za ulimwengu, katika agano jipya?

  Sijawahi kusoma ktk Agano jipya mahali popote panaposema kuwa shetani kuna siku atabebeshwa furushi la dhambi za ulimwengu, hivyo naona hilo ni wazo la kusadikika zaidi. Ila kama papo nioneshe tu rafiki yangu, Biblia ni kitabu kikubwa sana!
  Ni hayo tu kwa leo!

 88. @ Sungura,
  Ninakuelewa vizuri ulipopigwa changa la macho!! Najua mantiki ya hoja zangu za kimaandiko unaziona kabisa mbashala, ndiyo maana unaanza kupindisha na kuanza kumtetea shetani. Shetani ana kivuli chake halisi katika Agano la Kale bro. Tangu Eden Shetani alitambulika kama uzao wa nyoka…., Kristo uzao wa mwanamke…. Enzi za Israel alitambulika kama mbuzi wa azazeli (aliyepelekwa porini not kilimani kama unavyofikiri wewe). Kilima cha Kristo, kilikuwa ni madhababu –sehemu ya kuchinjia wanyama wa kafara. Hii iilkuwa ikijengwa kwa mawe tangu enzi za akina Habili, Ibrahimu na kuendelea. Kipindi cha Waisrael, kilitengenezwa kichanja cha mawe nje ya hekalu –sehemu ya kuchinjia kafara. Na hiki kijiwe, kilichokuwa nje ya kanisa, ndicho kilichowakilisha mlima wa Kalvari. Mbuzi, kondoo n.k. wa Bwana, hawaakuchinjiwa ndani ya hekalu, acha kuchanganya madesa kijana. Mambo ya vivuli yako bayana sana, ila kwa wavivu wa maandiko, wataishia kama hapo unapoishia wewe. Kama Kristo alivyokuwa na kivuli, na shetani naye ana kivuli!! Tena kiko kibayana kabisa –mbuzi wa azazeli. Siku ile nikakwambia yaani hata watu wasiomjua Mungu, wewe Sungura wanakuzidi kufahamu baadhi ya mambo. Nilikwambia kuwa, licha ya kuangalia kwenye Biblia tu, angalia pia hata kwenye makamusi ya watu baki tu, utajifunza kitu. Mbuzi, kondoo, ng’ombe n.k. wa Bwana walichinjiwa nje ya hekalu bro, tena juu ya kilima kilichokuwa kimejengwa kwa mawe. Mbuzi wa Azazeli alipelekwa mbali kuashiria kuwa, Mungu hana shirika na Ibilisi –dhambi. Na wala hakuna suala la tafsiri sisisi hapa. Mambo yako bayana sana.
  shakira
  Siyi

  @ Pandael
  Ha ha ha ha haaa!!
  Umefufuka tena kaka!! Mimi huwa nakwambia wewe huna hoja ndugu yangu kabisaaa!! Sijui akina Ellen G. White na William Miller walikukosea nini!! Sijui!! Na hapa mimi, sijawanukuu kunisaidia kujenga hoja!! Nimenukuu Biblia rafiki. Hata hivyo, siku ile nikakwambia kuwa, akina William Miller na Ellen G. White wake, hawana uhusiano wowote na wokovu na mwanaadamu. Kuna mambo ambayo Mungu ametufunulia tuyajue na yale ambayo ameyafanya kuwa siri kwetu –hatuna haja ya kuendelea kuyahangaikia. Barabara ya kwenda mbinguni, ina alama na ishara njia nzima. Usipojitahidi kuzielewa alama na ishara hizo, utapotea tu maana utafikiri unasafiri kwenye barabara yenyewe kumbe umepotea. Jitahidi bro. Mbingu siyo lelemama rafiki yangu.
  Shakira too!!
  Siyi

 89. Pandael
  Ha ha ha ha haaa!!
  Umefufuka tena kaka!! Mimi huwa nakwambia wewe huna hoja ndugu yangu kabisaaa!! Sijui akina Ellen G. White na William Miller walikukosea nini!! Sijui!! Na hapa mimi, sijawanukuu kunisaidia kujenga hoja!! Nimenukuu Biblia rafiki. Hata hivyo, siku ile nikakwambia kuwa, akina William Miller na Ellen G. White wake, hawana uhusiano wowote na wokovu na mwanaadamu. Kuna mambo ambayo Mungu ametufunulia tuyajue na yale ambayo ameyafanya kuwa siri kwetu –hatuna haja ya kuendelea kuyahangaikia. Barabara ya kwenda mbinguni, ina alama na ishara njia nzima. Usipojitahidi kuzielewa alama na ishara hizo, utapotea tu maana utafikiri unasafiri kwenye barabara yenyewe kumbe umepotea. Jitahidi bro. Mbingu siyo lelemama rafiki yangu.
  Shakira too!!
  Siyi

 90. Sungura,
  Ninakuelewa vizuri ulipopigwa changa la macho!! Najua mantiki ya hoja zangu za kimaandiko unaziona kabisa mbashala, ndiyo maana unaanza kupindisha na kuanza kumtetea shetani. Shetani ana kivuli chake halisi katika Agano la Kale bro. Tangu Eden Shetani alitambulika kama uzao wa nyoka…., Kristo uzao wa mwanamke…. Enzi za Israel alitambulika kama mbuzi wa azazeli (aliyepelekwa porini not kilimani kama unavyofikiri wewe). Kilima cha Kristo, kilikuwa ni madhababu –sehemu ya kuchinjia wanyama wa kafara. Hii iilkuwa ikijengwa kwa mawe tangu enzi za akina Habili, Ibrahimu na kuendelea. Kipindi cha Waisrael, kilitengenezwa kichanja cha mawe nje ya hekalu –sehemu ya kuchinjia kafara. Na hiki kijiwe, kilichokuwa nje ya kanisa, ndicho kilichowakilisha mlima wa Kalvari. Mbuzi, kondoo n.k. wa Bwana, hawaakuchinjiwa ndani ya hekalu, acha kuchanganya madesa kijana. Mambo ya vivuli yako bayana sana, ila kwa wavivu wa maandiko, wataishia kama hapo unapoishia wewe. Kama Kristo alivyokuwa na kivuli, na shetani naye ana kivuli!! Tena kiko kibayana kabisa –mbuzi wa azazeli. Siku ile nikakwambia yaani hata watu wasiomjua Mungu, wewe Sungura wanakuzidi kufahamu baadhi ya mambo. Nilikwambia kuwa, licha ya kuangalia kwenye Biblia tu, angalia pia hata kwenye makamusi ya watu baki tu, utajifunza kitu. Mbuzi, kondoo, ng’ombe n.k. wa Bwana walichinjiwa nje ya hekalu bro, tena juu ya kilima kilichokuwa kimejengwa kwa mawe. Mbuzi wa Azazeli alipelekwa mbali kuashiria kuwa, Mungu hana shirika na Ibilisi –dhambi. Na wala hakuna suala la tafsiri sisisi hapa. Mambo yako bayana sana.
  shakira
  Siyi

 91. Siyi,

  Unaningoja kivipi sasa wakati nineshakwambia nini maana ya mbuzi wa Bwana na wa azazeli?

  Ujinga mkubwa zaidi ni kule kupiga panda kuwa jambo fulani unalijua wakati matamshi yako yanaonesha kuwa hujui kabisa.

  Wewe ni muongo wa kawaida tu ambaye hulazimisha uongo uwe kweli.

  Umemwambia Lwembe kuwa mbuzi wa Bwana alikuwa kwa ajili ya dhambi za Israel, wakati alikuwa kwa ajili ya kutakasa madhabahu, na dhambi za Israel ziliwekwa kwa mbuzi wa azazeli.

  Tukakwambia ndiye kristo aitwae mwanakondoo wa Bwana azichukuae dhambi za ulimwengu.

  Mabaki ya kafara iliyotolewa madhabahuni hayakuwekwa kwa mbuzi wa azazeli, bali yalipelekwa nje ya mji.

  Halafu, Roho mt alianza kuwaongoza lini wasabato Siyi? Maana miaka si mingi wasabato mlikuwa mnapinga sana suala la ujazo wa Roho mt.

  Unatengeneza logic zako nje ya neno la Mungu kwa kutumia fikra na fundisho la kidini tu, be independent!

 92. @ Lwembe,
  Litugia ni kwenu tu na si kwetu sisi wasabato. Tuko makini mno na Roho wa Mungu anatuongoza vilivyo kuyabaini mambo ya Mungu yaliyofunuliwa kwetu.
  Unachokosa kukiona, ni kitu kidogo sana; kwamba, mbuzi wa Bwana, alipozifunika dhambi za watu (Israel) kwa damu yake mle madhabahuni, damu za mbuzi huyo ziliendelea kubaki. Kumbuka, dhambi zilifunikwa tu, not deleted at all!! Kwa maneno mengine, ziliondolewa tu kwa mdhambi zikahamishiwa kwenye damu ya yule mbuzi wa Bwana. Kwa mantiki hiyo, dhambi ziliendelea kuwepo madhabahuni zikiwa zimefunikwa tu kwa damu ya mbuzi wa Bwana. Na ili madhabahu itakaswe, harufu ya damu na alama za damu hizo ziondolewe kwa ajili ya mwaka mpya unaokuja, uchafu wooote huo ulikusanywa na kuwekwa kwenye kichwa cha mbuzi wa azazeli aliyemwakilisha shetani ili abebe matokeo ya kile alichokifanya kwa wazazi wetu wa kwanza na vizazi vyao, ambao walikuwa wametubu/wameondolewa dhambi. Ndiyo maana hapo awali nilitangulia kusema kuwa, shetani angeadhibiwa kwa dhambi zake tu, asingekuwa na haja leo ya kuhangaika kuudanganya ulimwengu ili upotee dhambini!! Kwa nini? Kwa sababu, dhambi na makosa ya watu waliotubu, yasingemhusu!! Lakini sasa kwa vile anajua yanamhusu vilivyo, ndiyo maana kuna “…Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu” Ufunuo wa Yohana 12:12.
  Ukiwa mbumbumbu wa maandiko, utaendelea kuchanganya mambo haya hadi kesho. Na mimi ninachokiona hapa, unajaribu kupinga na kupindishapindisha tu kisa jambo hili, limesemwa na Siyi –msabato!! Ukweli unaujua kabisa ila hutaki tu kukiri kama ilivyo kawaida yako!! Shauri yako fursa kama hii itakapoondolewa!!
  Siyi

  @ Sungura,
  Mimi nakusubiri. Ukiwa na jibu la maana wewe leta tu. Lakini ukweli wa mambo ndio huo kaka. Wala huna haja ya kuendelea kuzungukazunguka. Mambo yako bayana kiasi kile.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 93. Siyi,

  Ati , ‘ooh what a joy”!
  What a joy wakati unaongea kitu usichokijua!

  Kuna mambo huwa naona ni kawaida tukitofautiana, maana hayana negative impact katika kuujua ikweli wa msingi wa Mungu. Lakini kwa jambo kama hili kwa mujibu wa barua yako ndefu, nachelea kukwambia kuwa wewe ni mjinga kabisa wa mambo haya. Na kama unachosema hapa ndo msingi wa wasabato wote, basi mnatia huruma.

  Siyi siyo hivyo ulivyosema, bali ni kama hivi ifuatavyo:

  Kwanza jifunze jinsi ya kujenga mantiki za maandiko. Katika hiyo Lawi 16 kuna vitu vitatu vimetajwa. Kuna ng’ombe mmoja, mbuzi wawili, na mwanakondoo mmoja.

  Kati ya hivyo vyote, hakuna hata kimoja kinachohusiana shetani, bali vyote vinamhusu kristo.

  Ng’ombe ni kwa ajili ya kuhani(Yesu kuhanani mkuu aliingia na damu yake- ng’ombe), mbuzi wa Bwana kwa ajili ya kutakasa hekalu, wala si kwa ajili ya kutakasa waisrael(ndo huko kupasuka kwa hekalu Yesu alipokata roho), mbuzi wa azazeli kwa ajili ya kuzibeba dhambi na uovu wa Israel, ndio huyo Yesu mwenye kuchukua dhambi ya ulimwengu, ndo huyo Yesu mwenye kuchukua madhaifu yetu, mwenye kubeba fadhaa zetu, na magonjwa yetu.

  Kondoo alikuwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, ndo huyo Yesu aliyetoa mwili wake uwe hiyo sadaka

  Huyo ndo Yesu tunaemtwika fadhaa zetu, aliyekwenda na dhambi zetu Kalvari(nje ya mji).

  Hilo wazo kuwa Yesu atakuja kumbebesha shetani furushi la dhambi haipo kwenye maandiko. Ni ya kwenu mmetunga kutokana na kushindwa kumtafsiri mbuzi wa azazeli, mkadhani kwa kuwa mbuzi mmoja ni Bwana, basi huyo mwingine ni wa shetani.

  Walimu vipufu ninyi, msioweza kuelewa maandiko lakini mwajiona mnajua kweli.

  Nimekuona una shida nyingine ya tafasi ya neno ‘kivuli’. Unataka mifano sisisi ya kilichofanyika agano la kale kifanyike na agano jipya. Pole sana, maana hautapata hicho kitu.

  Mbuzi wa Bwana alichinjwa, lakini Yesu hakuchinjwa. Yesu aliuawa nje ya mji lakini mbuzi wa Bwana aliuawa hekaluni. Hakuna mfanano sisisi hapo, bali kilichopo ni mantiki ya kifo.

  Yesu aliangikwa msalabani, mbuzi wa Bwana hakuangikwa. Kwa hiyo ukitaka kujua kuwa azazeli alimwakilisha kristo mwenye kuibeba dhambi ya ulimwengu kwa kutafuta huo mfanano sisisi hautakuja kuelewa.

  Isome vizuri comment ya Lwembe itakusaidia sana.

  Naweka koma tena!

 94. Siyi,
  Mafundisho ya Elen G. White na William Miller yamekutoboa macho na umekuwa KIPOFU.
  Wasabato wenzako wamenyamaza kimya kwa sababu wanajua Kwa hayo MAFUNDISHO MFU kuchemsha ni lazima.
  Kama nilivyotangulia kukuambia HUJATAKASIKA , haya mafundisho unayotoa kwa “wapumbavu” yanathibisha kauli yangu.
  Wewe na WASABATO wenzako HAMUAMINI kuna KUOKOKA DUNIANI. Mna tofauti gani na ndugu zenu WAKATOLIKI? Ni kweli Bwana Yesu HAKUWAFILIA na hata HAMNA UHUSIANO WOWOTE naye.
  MARKO 16:15-16 ” Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. ”
  Kama ninyi si WAPINGA KRISTO ni akina nani?
  Naelewa kuwa wewe ni Mgonjwa NAFSINI na MILINI na umebembelezewa sana TIBA (NENO LA MUNGU/INJILI HALISI) na NDG LWEMBE lakini UMEKATAA.
  Basi, kilichobaki kwako na kwa WASABATO wenzako mnaong’ang’ania MAPOKEO,KANUNI ZA IMANI na MAFUDISHO YA SHARTI ya ELEN G. WHITE na WILLIAM MILLER ni Kukataliwa na LAANA.
  WAGALATIA 1:8-9 ” Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe. ”
  POLE SANA!!

 95. Siyi,
  Mafundisho ya Elen G. White na William Miller yamekutoboa macho na umekuwa KIPOFU.
  Wasabato wenzako wamenyamaza kimya kwa sababu wanajua Kwa hayo MAFUNDISHO MFU kuchemsha ni lazima.
  Kama nilivyotangulia kukuambia HUJATAKASIKA , haya mafundisho unayotoa kwa “wapumbavu” yanathibisha kauli yangu.
  Wewe na WASABATO wenzako HAMUAMINI kuna KUOKOKA DUNIANI. Mna tofauti gani na ndugu zenu WAKATOLIKI? Ni kweli Bwana Yesu HAKUWAFILIA na hata HAMNA UHUSIANO WOWOTE naye.
  MARKO 16:15-16 ” Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. ”
  Kama ninyi si WAPINGA KRISTO ni akina nani?
  Naelewa kuwa wewe ni Mgonjwa NAFSINI na MILINI na umebembelezewa sana TIBA (NENO LA MUNGU/INJILI HALISI) na NDG LWEMBE lakini UMEKATAA.
  Basi, kilichobaki kwako na kwa WASABATO wenzako mnaong’ang’ania MAPOKEO,KANUNI ZA IMANI na MAFUDISHO YA SHARTI ya ELEN G. WHITE na WILLIAM MILLER ni Kukataliwa na LAANA.
  WAGALATIA 1:8-9 ” Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote”
  POLE SANA!!

 96. Siyi,

  Naona leo umetuletea Litugia ya Kisabato!
  Inapendeza saaana ktk masikio ya mjinga; kabla haijamkomaza ktk ujinga na kumfanya mpumbavu!

  Kuhusu Liturgia yenu kwa kifupi, huyo mtunzi yaonesha aliikosa maana nzima ya Mbuzi wa Azazeli na huyo wa Bwana!

  Mbuzi wa Bwana hakuichukua dhambi ya Israeli, bali alikuwa ni pazia ya iliyomficha mdhambi machoni pa Mungu, ndio huo upatanisho. Ndiyo hiyo Damu ya Mwana Kondoo.

  Mbuzi wa Azazeli ndiye aliyezibeba dhambi zoote za Israeli, yaani mapepo yote, mpaka ya dini, yalibebwa na Mbuzi huyo aliyekuwa msafi. Ndiye huyo Mwana Kondoo aichukuaye Dhambi ya ulimwengu!

  Lile jambo ulilolisema, kwamba lilipofanyika humo hekaluni na ktk Hekalu la Mbinguni lilifanyika pia; nilitegemea hilo likuthibitishie jambo la Mbuzi wa Bwana ktk milki ya kiroho pale pazia la hekalu liliporaruka licha ya Yeye kusulubiwa huko Calvari, ktk utimilifu wa jambo la Mbuzi wa Azazeli kwamba sasa mbuzi huyo Damu yake imeilipia Dhambi aliyoibeba; Isa 43:25 “… wala sitazikumbuka dhambi zako.”!

  Na pia unapaswa uelewe ni kwanini hao waliompleka hawakujiosha? Ni kwa sababu ya mapepo ya dini yaliyowapagawa hata wakajitangazia Hukumu wao wenyewe; lakini fursa ya kujiosha haikuishia hapo, siku ya Pentekoste Rehema ya Mungu iliwarudia tena; ndio yale mahubiri ya Petro yanayoendelea mpaka leo hii kwa watu walipoagawa mapepo ya dini wanaoikataa Damu ya Kristo, hapo wanapoungana na Israeli waliomtoa na sasa wao pia wakipewa fursa ya kujiosha ndio hilo Ondoleo la Dhambi! Mdo 2:36-38

  Mtunzi wenu alichoshindwa kukielewa ni kivipi Mbuzi wa Azazeli alikuwa tena ni Mbuzi wa Bwana? Na ktk kukosa kwake ufahamu ndio anawadanganya kwamba ktk kafara hizo kulikuwa na Ondoleo la Dhambi nanyi kwa upumbavu mnameza tu huku mkija na lundo la nukuu, halafu kumbe hata Maandiko yenyewe hamyajui!!!

  Dogo, moto upo!!

 97. Siyi,

  U are preaching too much unnecessarily!

  Huwa ukiongea kitu ambacho unadhani kuwa unakifahamu, huongea sana vitu vingi ambavyo si vya msingi.

  Nimeshangaa ulichokisema kuhusu mwaka 1840, huko ndo tunasema kulishwa matango mwitu.

  Huo ni muhutasari, nitakujibu!

 98. inaendelea….

  Sungura na wengine, haya ni miongoni mwa maswali machache tu ambayo wakristo wengi wa kij2, huwa nayo kuhusu jambo hili. Nami sina budi kuwaonesha njia tena kwa njia rahisi na yenye kueleweka kwa haraka.
  Kwa ufupi kabisa pasi kuwachosha wasomaji, napenda kusema kuwa, mbuzi KWA AJILI YA BWANA (JEHOVA) ambaye alichinjwa kwa ajili ya dhambi za mkutano mzima, alimwakilisha Kristo. Huyu ndiye aliyebeba dhambi za Waisrael wooote. Na ndiye anayebeba dhambi za wale wooote wanaofanyika wana wa Ibrahimu leo kwa njia ya imani katika Kristo. Ondoleo la dhambi za wanadamu hawa ni kwa NJIA YA MBUZI WA YEHOVA PEKE YAKE. Hakuna mbuzi mwingine au yeyote awezaye kubeba na kuondoa dhambi za watu, isipokuwa yule wa Bwana tu. Biblia inasema, “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa” 1 Petro 2:24. Mbuzi wa azazeli hakupigwa, wala huko porini haikujulikana alikokwenda. Kama ni kuliwa na wanyama wakali au kuwa mbuzi mwitu, yote yalimstahili. Hii ni tofauti na mbuzi wa Jehova. Uondoaji wa dhambi wapendwa, ulihusisha mauti (damu). Upatanisho katika agano la kale, ulihusisha damu za wanyama. Hakukuwa na maungamo na maondoleo yoyote ya dhambi za watu yasiyohusisha damu kumwagika na damu hiyo kunyunyizwa ndani hemani!! Hakuna aliyewahi kuiona au kuisikia damu ya mbuzi wa azazeli!! Na dhambi zetu, hazisafishwi kwa hiyo isipokuwa damu ya mbuzi kwa ajili ya Bwana – damu ya thamani sana, iliyosonda kafara ya Kristo mwenyewe.
  Yesu alifanyika laana kwa ajili yetu. Sote tunalijua hilo!! Yesu alikufa (temporal death) ili kutuokoa sisi kwenye eternal death. Nadhani kwa hili, huna ubishi Sungura!!
  Sikia ndugu yangu Sungura, “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu” -1 Timotheo 2:5. Kazi ya upatanishi anayoifanya Kristo kwa sasa mbinguni, ni ileile iliyokuwa ikifanywa na makuhani wa agano la kale. Tofauti ni ndogo sana ambayo ni kwanza, badala ya Yesu kutumia damu za wanyama kufunika dhambi za watu, anatumia damu yake mwenyewe ili kuwafavour hata masikini wa kutupwa nao wapte ondoleo la dhambi. Pili, hema alipo Kristo kama Kuhani wetu mkuu (mpatanishi), ni mfano wa ileile iliyojengwa na wanadamu hapa nyakati za agano la kale, tofauti ni kwamba ile ya mbinguni haikujengwa na wanadamu. Maana “kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake; kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake” –Ebrania 9:24:26. Na kumbuka, tangu mwanzo wa agano la kale, kile kilichokuwa kikifanyika duniani kwenye hema za kutolea kafara za wanyama, mbinguni nako mchakato huo ulikuwa ukifanyika japo kwa zana tofauti. Kwa maneno mengine, usafishaji wa dhambi kwa mdhambi, na damu zilizokuwa zikifunika dhambi ndani ya hema, kulifanyika kwa kumwaga damu. Kilichokuwa kinafanyika duniani, kilikuwa ni kielelezo tu cha kile ambacho kilikuja kufanyika baada ya kifo cha Kristo –damu ya Kristo iliyo bora zaidi ya damu za mafahali. Biblia inasema, “Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo”-Ebrania 9:22-23. Yesu aliyatekeleza hayo, kama kuhani tu. Baadaye angekuja kuwa kuhani mkuu –kuingia patakatifu pa patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wa mara ya mwisho –upatanisho wa siku kuu (yom kippur). Paulo anasema, “Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema YATAKAYOKUWAPO, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu”- Waebrania 9:11. Yesu alipopaa mbinguni, alienda kuhudumu katika hema ya mbinguni sehemu ya patakatifu kwa muda huo hadi miaka 1840’s AD, unabii unasema hivyo. Na katika kipindi hichohicho cha miaka 1840’s AD, Yesu aliingia patakatifu pa patakatifu kama kuhani mkuuu –rejea Waebrania 9:11. Kumbuka wakati Paulo anasema mambo hayo mema (YATAKAYOKUWAPO), ilikuwa ni kabla ya 1840’s. Kazi ya ukuhani mkuu anayoifanya Kristo, ambayo haina tofauti na ile iliyokuwa ikifanywa na kuhani mkuu hapa duniani enzi za agano la kale, alikuwa hajaianza. Hata baada ya kuianza kwa kipindi tajwa hapo juu, taratibu za upatanishi bado zilikuwa ni zilezile, tofauti ni hiyo damu, mandhari na huyo mpatanishi mwenyewe (Kristo) lakini mambo mengine yako vilevile.

  Siku Yesu akitoka patakatifu pa patakatifu, atafanya kama alivyokuwa akifanya kuhani wa agano la kale. Mbuzi wawili watakaopelekwa kwa ajili ya kupigiwa kura watakuwa ni Kristo mwenyewe (mbuzi/mwanakondoo wa Mungu) na mbuzi wa azazeli (ibilisi). Kwa vile Kristo alishapigiwa kura tangu mbinguni na akaonekana yuko upande wa Mungu, akachinjwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi za wanadamu waliotubu. Na kwa sababu Yesu amezifunika dhambi hizo kwa damu yake, zoezi la upatanisho litakapoisha, Kristo akitoka the Holy of Holies atasikika akisema, “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa”- Ufunuo 22:11. Kazi ya upatanisho itakuwa imefikia mwisho. Hakuna ungamo wala toba itakayopokelewa na Mungu tena!! Kazi itakayofuatia ni Kristo kuliijia kanisa lake –kulitenga mbali na ibilisi na malaika zake. Na ili Mungu asikumbuke dhambi za hawa waliokombolewa, patakatifu pa mbinguni patasafishwa. Dhambi za wateule zilizokuwa zimefunikwa na damu ya Kristo zitakusanywa zooote na kuwekwa juu ya ibilisi ili asikilizie maumivu ya dhambi ya uasi wake na matokeo ya dhambi za uasi wake kwa wanadamu waliokombolewa. Hii ndiyo maana ya mbuzi wa azazeli kubebeshwa dhambi za wanadamu waliotubu. Kwa maneno mengine, mbuzi wa azazeli, atafanywa dampo la dhambi za wote waliotakaswa. Uchafu wooote ambao Kristo anaukusanya sasa hivi (huko mbinguni) kutoka kwa wateule wake, mwishoni ataupeleka kwenye dampo –shetani kwa ajili ya kuuchoma moto. Hivyo, mbuzi wa azazeli pamoja na kuwekewa mikono na kuhani mkuu, huo haukuwa ni upatanisho, bali lilikuwa ni zoezi la utakasaji wa patakatifu!!

  Kubebeshwa kwa dhambi na makosa ya waisrel kwa mbuzi wa azazeli, haukuwa upatanisho, bali ulikuwa ni utakasaji tu wa hema ya Bwana mwishoni mwa mwaka kwa ajili ya mwaka mwingine mpya!! Kwa muda wa mwaka mzima, hema ya Bwana ilikuwa imetapakaa damu (hasa pazia) sehemu nyingi. Harufu za damu za wanyama za mwaka mzima zilijaa ndani!! Harufu za mafuta ya wanyama na nyama zilizokuwa zikichomwa ndani ya hema hiyo, zilijaa kwelikweli!! Ili kuitakasa hema hiyo, zoezi hilo lilifanyika siku kuu ya upatanisho, ambapo baada ya toba, maungamo na msamaha wa dhambi za mwaka mzima kwa taifa zima, hema ilipaswa isafishwe kwa ajili ya mwaka unaokuja tena. Kuhani hakuwa na budi kuzichukua dhambi zooote za mkutano mzima zilizokuwa zimefunikwa na damu za wanyama (waliowakilisha kifo cha Kristo), kuzibeba na kuzidampo juu ya kichwa cha mbuzi wa azazeli na kisha kupelekwa porini.
  Hivyo basi, azazeli hakuwa Kristo, bali alimwakilisha Shetani atakayebebshwa dhambi za wanadamu wote waliotubu ili aangamizwe nazo na wadhambi wengine wote. Hata yule mtu alipewa jukumu la kumpeleka huyo mbuzi wa azazeli porini, alipaswa kuoga na kujitakasa sana kabla ya kuchangamana na wengine. Biblia inasema, “Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika marago” Lawi 16:26. Je, kweli waliompeleka Yesu kalvari walifanya haya pia?? Hasha!! Mchakato huo ulifanyika kuonesha ukamilifu wa historia ya ukombozi wa mwanadamu kwa njia ya Kristo na uangamivu wa mwanadumu kwa njia ya Ibilisi.
  Baada ya kukamilika kwa kazi/zoezi la ukombozi, -yaani baada ya shetani kuwa alishaangamizwa na jeshi lake lote, ndipo Biblia inasema, “(Kristo) Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita” Ufunuo 21:4. Kwa maana “…waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti…” –Ufunuo 21:8. “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo” –Ufunuo 21:27. Watu hawatakumbuka wala kutamani uovu tena. Kwa maana Mungu anasema, “…agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu” Yeremia 31:33. Paulo anaiongezea kauli ile kwa kuirudia akisema, “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu”- Waebrania 8:10.

  Ooh, what a joy!!

  Neema ya Bwana ikufunike.

  Siyi

 99. Sungura,
  Yaani sitoi macho kukushangaa kwa vile unadhani unaongea mambo muhimu!! Hasha!! Nakushangaa sana kwa kuwa unajidai kulijua jambo hilo ilhali hulijui kabisa. Miongoni mwa mambo ambayo waj2 wengi mko nyuma zaidi ya hata mkia wa mbuzi, ni uelewa wa historia ya ukombozi katika agano la kale na utimilifu wake katika agano jipya!! Na kwa vile mmepingwa chenga kulielewa jambo hilo (msemo wa Lwembe), hata wokovu wenyewe ndani ya agano jipya, hamuujui!! Mmebaki kutaja jina Yesu, Yesu, Yesu tu bila ya kumjua hata Yesu kiundani –historia yake kamilifu. Wengi watanifikiria kama nawakejeli vile, lakini nawaambia ukweli ndugu zangu waj2 ukiwemo Sungura, Lwembe, Seleli(mwana mpotevu), Mhina, Pandael, Msella, Anthony, Tumaini, Marry, Deo, (na wengine wengi ambao siwezi kuyataja majina yenu yote), msipoamka na kuijifunza Biblia vizuri, mtaishia kuitwa wakristo tu. Kama mmeamua kuwa wakristo, iweni wakristo kwelikweli!! Baada ya wito huo, sasa niende moja kwa moja kwenye swali la Sungura…
  “Tufanye hivi; Nipe tu maandiko yanayosema hivi vitu vifuatavyo:
  ”wakristo wengi leo, wanaamini kuwa, damu ya Yesu inaondoa dhambi za watu -kuzidelete zisionekane popote kabla hata ya kuanganmizwa ulimwengu!! Wanaamini kuwa, mtu anapompokea Kristo, dhambi zake zooote zinaondolewa kwake (jambo ambalo ni sahihi kabisa), na kufutwa zisiletwe tena kwenye kumbukumbu kabla ya dunia hii kuchomwa moto. Dhana hii siyo sahihi kabisa. Dhambi za wanaotubu, zinawakilishwa na alama za damu ya Kristo katika hema ya mbinguni. Baada ya kazi ya upatanishi, sharti alama hizo (za damu zilizofunika dhambi) ziondolewe” – Hiyo imeandikwa wapi Siyi?”
  Jibu
  Kwanza, nikuombe uisome sura nzima ya Walawi 16 polepole na kwa umakini mkubwa kabla ya kusoma majibu yangu. Ukikiuka maelekezo haya, unaweza kunirudia tena ukidai hujaelewa. Tafadhali, fuata maelekezo na usome between lines. Mimi nitadonoa tu baadhi ya aya, maana najua utasoma sura nzima ili upate dhana nzima.
  Tuanze na mstari wa 8, Biblia inasema, “Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya Bwana; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli”. Mbuzi walioletwa, walikuwa wa pande mbili tu, -upande wa JEHOVA na upande wa Azazeli!! Kumbuka, Mungu ni wa upande mmoja tu!! Hata sisi ametuambia kuwa na Bwana mmoja tu na si wawili. Kitu kilicho upande wa Mungu, hakiwezi kuwa upande tena wa azazeli na kinyume chake!! Twende polepole kijana…
  Mstari wa 9 Biblia inasema, “Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana, na kumtoa awe sadaka ya dhambi”. Sasa chunguza utaratibu wa kutoa sadaka za kafara za wanyama ulikuwaje!!

  Kafara kwa ajili ya toba/ungamo la mdhambi

  “Na mtu awaye yote katika watu wa nchi akifanya dhambi pasipo kukusudia, kwa kufanya neno lo lote katika hayo ambayo Bwana alizuilia yasifanywe, naye akapata hatia; akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ndipo atakapoleta mbuzi mke mkamilifu, awe matoleo yake kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya. Naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi, na kumchinja sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa. Kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu yake kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya kuteketeza na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu” –Lawi 4:27-30.

  Tulichoona ni nini hapa??
  Kwanza, tumeona kuwa, mdhambi alipaswa kupeleka mbuzi (na pengine kondoo, njiwa n.k) kwa ajili kafara. Pili, mdhambi mwenyewe alipaswa kutubu dhambi zake zooote alizozitenda huku akiweka mikono yake juu ya kichwa cha mnyama huyo wa kafara. Na tatu, mdhambi mwenyewe, alipaswa kumchinja huyo mnyama wa kafara na ndipo kuhani alichukua nafasi yake. Zoezi hili lilikuwa likifanyika kila siku kwa muda wa mwaka mzima na kuhitimishwa na siku kuu ya upatanisho.nk.

  Siku Kuu ya Upatanisho mambo yalikuwaje??

  Biblia inasema, “Na Haruni atamsongeza ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake; naye atamchinja yule ng’ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake. Kisha atatwaa chetezo kilichojaa makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za Bwana, na konzi mbili za uvumba mzuri uliopondwa sana, mikononi mwake, naye atauleta ndani ya pazia. Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za Bwana, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa. Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba. Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya kwa damu ya ng’ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao. Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israeli. Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za Bwana na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote. Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke”-Lawi 16:11-19.

  Tumeona nini hapa?
  Kwanza, kuhani mkuu mwenyewe, alipaswa kujitakasa kwanza kwa kupeleka ng’ombe wa kafara kwa ajili yake na familia yake. Pili, taratibu zote za toba/maungamo kwa kumwekea ng’ombe huyo mikono kichwani mwake, alizifanya yeye mweyewe kuhani mkuu. Tatu, hata mbuzi aliyekuwa KWA AJILI YA BWANA, ambaye alipaswa kuchinjwa kwa ajili ya mkutano mzima wa Israel, alimwekea yeye mwenyewe mikono wakati wa kuungama na hatimaye kumchinja mwenyewe. Nne, taratibu zote za utoaji wa kafara, zilikuwa bayana kwa kila mtu. n.k.

  Zingatia:
  a. Kuhani Mkuu –aliyekuwa akimwakilisha Kristo, yeye alipeleka ng’ombe kabisa (wa kafara) kwa ajili ya ondoleo/funiko la dhambi zake yeye mwenyewe na familia yake.
  b. Taifa/mkutano wote wa Israel, sadaka yao ilikuwa ni yule mbuzi wa YEHOVA, -rejea aya ya 11!!
  c. Kumbuka, siku ya upatanisho ilikuwa ikifanyika mara moja tu kwa mwaka, tena mwishoni mwa mwaka.

  Sasa tuangalie mzizi wa hoja yako!! Tukirudi hapo juu kidogo aya ya 10, Biblia inasema, “Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili KUMFANYIA UPATANISHO, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli”. Aya nyingine inayofanana na hii ni ile ya 20-22. Biblia inasema “Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai. Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na KUUNGAMA JUU YAKE UOVU WOTE WA WANA WA ISRAELI, NA MAKOSA YAO, NAAM, DHAMBI ZAO ZOTE; NAYE ATAZIWEKA JUU YA KICHWA CHAKE YULE MBUZI, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani”-Lawi 16:2022 (msisitizo wangu).

  Maneno yenye msisitizo (herufi kubwa), ndiyo yanayowachanganya wakristo wengi leo, Siyo Sungura peke yake. Wapo wengi sana wanaosoma aya hizi na kudhani kuwa, mbuzi kwa ajili ya azazeli, alimwakilisha Kristo, jambo ambalo siyo kweli!! Kwa nini nasema hivyo? Miongoni mwa maswali ya kujiuliza ni haya…
  a. Je, inawezekana kweli kuwe na mbuzi KWA AJILI YA BWANA na papo hapo akawepo mbuzi KWA AJILI YA AZAZELI (tena waliopigiwa kura) halafu wote wakawakilisha kitu kilekile –yaani Kristo???
  b. Kama kweli wote mbuzi hawa walimwakilisha Kristo, je mbona mbuzi KWA AJILI YA AZAZELI hata hakuuwawa kama alivyouwawa mbuzi KWA AJILI YA BWANA, kama unabii unavyoonesha ndani ya Biblia tangu agano la kale kuhusu uhalisia wa mauti ya Kristo??
  c. Lakini kwa upande mwingine, kama akina Siyi wanadai kuwa mbuzi wa azazeli alimwakilisha shetani, je, inakuwaje kuhani mkuu aungame dhambi zake yeye mwenyewe na za waisrael kwa shetani?? Inawezekana kweli?? Au hii ina maana gani?
  d. Kwa mujibu wa sifa za wanyama wa kafara, ilikuwa ni ukamilifu –yaani asiye na waa lolote. Mbuzi hawa wawili (mbuzi kwa ajili ya Bwana na kwa ajili ya azazeli, nao walikuwa na sifa hizo), je, inawezekana mbuzi wa azazeli anayetafsiriwa kuwa ni shetani naye alikuwa ni mkamilifu? Sifa zake za uuaji na uongo wa tangu mwanzo, zinaweza kumpa sifa ya ukamilifu kweli?? Au hii ina maana gani??? n.k.

  Inaendelea……

 100. Siyi,

  Kweli tunatofautiana sana kuziona mantiki za maandiko. Umenikatalia kuwa Yesu hakufanyika mbuzi wa kafara (azazeli).
  Hebu acha tu-reason kwa akili ya kawaida tu ya kuyaelewa maandiko:
  Unadhani kwa nini Mungu alimwacha Yesu alipokuwa pale msalabani, mpaka Yesu akasema ”Mungu wangu Mungu mbona umeniacha?

  Kazi ya mbuzi wa kafara ilikuwa ni kutwishwa dhambi zote za watu na hivyo yeye(mbuzi) kufanyika dhambi, na kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti ndio maana ilimbidi akafe, tena porini.
  Ambapo hata kristo alibebeshwa dhambi zote za ulimwengu, akawa mdhambi na mshahara wa dhambi ni mauti, hivyo ilimbidi naye afe, tena kifo cha laana, na mbali na mji.

  Halafu leo nikikwambia kuwa Yesu alifanyika mbuzi wa kafara(scapegoat – azazeli) unatoa macho kunishangaa.

  Neno azazeli kwa maana ya mbuzi wa kafara lilitumika ironically kuonesha kwamba kitu kinachobeba uovu hakikustahili kukaa katikati ya jamii, hivyo kilitakiwa kutengwa kwa mfano wa shetani alivyotupwa toka juu (fallen angel).
  Ambapo kimira za mashariki ya kati azazel alisadikika kuwa ni pepo akaae jangwani huko mbali na watu.

  Hivyo mbuzi aliyebebeshwa hizo dhambi alifananishwa na hilo pepo (azazel), kwa maana ilimbidi naye akatupwe mbali jagwani.

  Nafikiri umejua sasa mantiki ya Yesu kuwa mbuzi wa kafara azazeli.

  Then prove me wrong on this point I cemented ”Katika agano jipya mwenye kufanyika azazeli si shetani bali ni Yesu mwenyewe, na tayari alishafanyika hivyo”

  Tufanye hivi; Nipe tu maandiko yanayosema hivi vitu vifuatavyo:

  ”wakristo wengi leo, wanaamini kuwa, damu ya Yesu inaondoa dhambi za watu -kuzidelete zisionekane popote kabla hata ya kuanganmizwa ulimwengu!! Wanaamini kuwa, mtu anapompokea Kristo, dhambi zake zooote zinaondolewa kwake (jambo ambalo ni sahihi kabisa), na kufutwa zisiletwe tena kwenye kumbukumbu kabla ya dunia hii kuchomwa moto. Dhana hii siyo sahihi kabisa. Dhambi za wanaotubu, zinawakilishwa na alama za damu ya Kristo katika hema ya mbinguni. Baada ya kazi ya upatanishi, sharti alama hizo (za damu zilizofunika dhambi) ziondolewe” – Hiyo imeandikwa wapi Siyi?

  Hayo mambo ya kwa imani katika agano la kale tutayajadili kwa upana, tumalize kwanza haya!

 101. Siyi,
  Mimi nimefurahi kwamba nawe umeliona hilo la Mhina kutetea Dhambi, yaani angekuwepo hapa Ziragora, nadhani angemwuliza kisa cha kujitoa mhanga? Maana amelowa Dhambi!!!

  Kuhusu maswali uliyoniuliza, ngoja niwe muungwana nikujibu japo maswali yenyewe ni ya kifedhuli!
  1. Umesema kuwa, “Ndio huo Ubatizo kwa Jina la Yesu Kristo unaokamilisha kuziondoa hizo dhambi unaousoma ktk Mdo 2:38!” Kama dhambi zinaondolewa kwa njia ya ubatizo tu, unafikiri watu ambao hawakuwahi kubatizwa (ubatizo wa maji mengi), nao wataenda mbingunji? Kama ni ndiyo, wataendaje kama dhambi zao hazikuondolewa kikamilifu?
  JIBU:
  Mungu ni mwaminifu hao waliohubiriwa Injili pungufu na wakaiamini hiyo, huwezi kuwahukumu kwa jambo wasilolijua; watahukumiwa kwa matendo yao lakini si kwa kulikana neno la Mungu kama wewe na Mhina! Ila waliowahubiria Injili pungufu hao hawatakwenda mbinguni.

  2. Umesema kuwa, “Sijui kama umeelewa kwamba Damu ya Yesu ni Neno lake? Hilo ndilo linalotakasa.” Nakuomba uthibitishe hili kibiblia!! Kuna kipindi ulisema kuwa, Neno la Mungu SHERIA, jambo ambalo nakubaliana na wewe kabisa. Je, kwa dhana hii mpya ya DAMU ya YESU, tunaweza kuiita nayo kuwa ni SHERIA?? Au kwa maneno mengine, DAMU YA YESU = SHERIA ZA MUNGU??? Hebu thibitisha rafiki!!
  JIBU:
  Damu ya Yesu ni Neno lake na ndilo linalo takasa: Yn 17:17 “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Nilikuambia swali lako ni la kifedhuli ni kutokana na wewe kuyashikilia mafundisho ya kifedhuli ambayo kwa hayo umeshindwa hata kuwa na ufahamu wa kawaida kwamba mambo baada ya kusulubiwa yanaongelewa ktk symbols ni mafumbo ambayo mafedhuli hawaambulii kitu! Wanasemaga “kalaga baho” usubiri kuiona Damu ya Yesu utashangaa uko ziwani!

  DAMU YA YESU = SHERIA ZA MUNGU??? hili hata silijui, labda ungeniuliza hivi: DAMU YA YESU = SHERIA YA MUNGU??? Yesu ndiye Sheria ya Mungu maana Yeye ni Mungu naye “Mungu ni Upendo” (1Yn 4:8); Ndiye huyo anayekaandani ya wanae aliowazaa kwa Roho ambao HAWATENDI DHAMBI, kwa sababu ndani yao wamejaa Neno lake ambalo ndio ile Damu mnayodhania inachuruzika huko mbinguni kwenye Kiti cha Rehema kwa jinsi mlivyopigwa chenga na Maandiko, kumbe inachuruzikia ndani ya Lwembe!

  Gbu!

 102. Ndg yangu Mhina,

  Sijui hata nikujibu nini, maana maelezo yako yoooote ni ya kuitukuza dhambi, hata Siyi amekuona hivyo, na anafurahia kwamba ziwani mtakuwa wengi!!!

  Mapema nilikuonesha Njia ya kupita ya Mdo 2:38 ili mambo magumu ya Mungu, yale mafumbo, kama Kuondolewa Dhambi, uyaelewe, ila naona umerudishiwa moyo wa jiwe, huna tena unyofu wa kuisikiliza Injili, bali unaisikilizaga akili yako tu na mambo yake ya Zambi!!!

  Hizo ngonjera za dini hazitakusaidia kitu ndg yangu kama hujaondolewa dhambi zako, utaishia kunukuu Maandiko usiyoyajua na mwishoni, si lazima upotee hapana, labda ukizidi ktk upumbavu wa kuyabehua Maandiko, vinginevyo utapita ktk Dhiki Kuu pamoja na swaiba wako Siyi aliyeukataa Wokovu, mtakuwa na wasaa mzuri wa kuyarejea ninayowaasa leo hii!

  Nakutakia tafakari yenye busara!

 103. Ndg lwembe, namaliza mjadala wetu kwa kukueleza kwamba, Sisi ni Watakatifu wa Mungu, tunaoendelea kukamilishwa siku hadi siku kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake kristo, kwa njia ya imani, mpaka utimilifu wote utimie!!!….ndiyo maana biblia inataka “TUSILEGEE” kwa kuwa kama tutalegea na kumsingizia kila kitu roho mtakatifu, basi hakika tutaanguka ijapokuwa tuliokoka na kuzaliwa mara ya pili, Soma(2Wakorintho 4:16). Mahalafulani katika biblia, mtume Paulo alisema” nautesa mwili wangu na kuutumikisha isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa!!. Sisi ni lazima tujitumikishe wenyewe kwa bidii yote, ili zile ahadi na nguvu za neno la kristo, ziweze kutenda kazi yake ndani yetu sawasawa na mapenzi ya Mungu, na hali hii ndiyo haswa maana ya kumtii Mungu na kuzaliwa mara ya pili, maana mtu huzaliwa haswa mara ya pili kwa neno la Mungu. Sasa, kwa sababu bado tunaendelea kukamilishwa siku hadi siku, hatutakiwi kujikweza kwa kusema kwamba, tayari tumefika au tumekwishakuwa wakamilifu kabisa, isipokuwa tunakwenda ngazi kwa ngazi, hatua kwa hatua, ndipo hali hiyo mtume Paul akaiita ” KUKAZA MWENDO” au kuchuchumilia yaliyombele ili tufikie ile mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Yesu kristo.Soma(wafilipi 3:12-14). Sasa, nikweli kabisa kama unavyoamini ndugu lwembe kwamba, sisi ni watakatifu kwa sababu tulikufa na kufufuka pamoja na kristo, tukazaliwa kwa mara ya pili, tukafanywa wapya, lakini tatizo ndugu lwembe unashindwa kujua kwamba, jambo hilo sio kile kitu halisi kabisa, ila huo ni mfano au ishara tu, ya imani yetu, inayotufananisha na kufa na kufufuka pamoja na kristo.Tazama, biblia inatuambia hivi” Kwa maana kama mlivyounganika naye katika “MFANO WA MAUTI YAKE” kadhalika mtaunganika kwa “MFANO WA KUFUFUKA KWAKE!!!. Soma(Warumi 6:5). Tazama, mtume Paul pia anasema” ….NIKIFANANISHWA NA KUFA KWAKE ILI NIPATE KWA NJIA YOYOTE KUFIKIA “KIYAMA YA WAFU” Soma(wafilipi 3:10-11). Kwa hiyo, lile jambo halisi linakuja mbeleni mwetu, ndiyo hiyo inayoitwa “KIYAMA YA WAFU” au ufufuo wa mwisho, ndiyo maana Paul akasema, hajidhanii kwamba, amekwishafika, au amekwishakuwa mkamilifu, hapana, ila “anakaza mwendo”. Kwa hiyo, kwa kielelezo hiki cha Mtume Paul, Hata sisi wakristo wa leo, tunakwenda ngazi kwa ngazi, hatua kwa hatua, tena hatulegei isipokuwa twakaza mwendo, na kama tungekuwa tumekwishakuwa wakamilifu kabisa kama malaika, basi kusingekuwa na haja leo hii ya kwenda makanisani ili kufundishwa na kujengwa!!. Mimi nimalizie kusema kwamba, utakatifu wa Mungu kwa watoto wake, bado ni wa juu mno!, kuliko upeo na mawazo ya wanadamu wote, ndiyo maana bado tunatakiwa tuendelee kumtumikia BWANA katika utumishi wetu. Alichokifanya Mungu kwa watoto wake, mpaka akawaita watakatifu sio kuwakamilisha kabisa hapa duniani ili wawe kama malaika, hapana, ila yeye alichokifanya ni kutupa ile chapa ya tabia yake takatifu kutoka kwenye ile sheria yake takatifu, ndipo kwa chapa ya tabia yake hiyo, tukaitwa wateule au watakatifu wa Mungu. Sisi ni watakatifu au wateule wa Mungu kwa njia ya imani yetu katika jina la Yesu, ndio maana biblia inasema” walioitwa ni wengi lakini wateule ni wachache, tena mteule hata akianguka mara saba, lakini bado ataamka!!!. Mimi naishia hapa kabisa, mbarikiwe wote, bw.lwembe, Siyi na wengineo wote. NIA YETU WOTE, NAAMINI SIO KUSHINDANA BALI KUJIFUNZA, WOTE TUNAFAA MBELE ZA MUNGU NAE MUNGU ANATUPENDA SANA.

 104. Lwembe,
  Naona bado unacheza sindimba. Mapachiko ya ndugu Mhina, yangekuwa yameandikwa na Siyi, ungesema kuwa ninatetea dhambi!! Sasa sijui kama na Mhina naye anatetea dhambi ama la!! Lakini jambo la msingi ni kwamba, Mhina ameeleza uhalisia wa maisha ya Kikristo kwa kizazi chetu hiki cha nyoka!! Nadhani utaokoteza pointi kama alivyokushauri, maana unaoenkana huna kitu chenye maana kiimani na kimafundisho ndugu yangu. Umejaa mafundisho ya kifedhuli tupu!! Ni udanganyifu mkubwa sana ulionao japo hutaki kuelewa hivyo!! Naomba nikuongezee vimaswali kabla sijakujibu.
  1. Umesema kuwa, “Ndio huo Ubatizo kwa Jina la Yesu Kristo unaokamilisha kuziondoa hizo dhambi unaousoma ktk Mdo 2:38!” Kama dhambi zinaondolewa kwa njia ya ubatizo tu, unafikiri watu ambao hawakuwahi kubatizwa (ubatizo wa maji mengi), nao wataenda mbingunji? Kama ni ndiyo, wataendaje kama dhambi zao hazikuondolewa kikamilifu?
  2. Umesema kuwa, “Sijui kama umeelewa kwamba Damu ya Yesu ni Neno lake? Hilo ndilo linalotakasa.” Nakuomba uthibitishe hili kibiblia!! Kuna kipindi ulisema kuwa, Neno la Mungu SHERIA, jambo ambalo nakubaliana na wewe kabisa. Je, kwa dhana hii mpya ya DAMU ya YESU, tunaweza kuiita nayo kuwa ni SHERIA?? Au kwa maneno mengine, DAMU YA YESU = SHERIA ZA MUNGU??? Hebu thibitisha rafiki!!
  Nakungoja sana.
  Siyi

 105. Siyi,

  Sio kwamba eti sitaki kukuambia, hapana, ila nilipoona imani zenu zinakaribiana sana ndio nikawajibu kwa pamoja!

  Swali unaloniuliza ni la msingi sana ili kupata kujua umeingia mlango gani ktk maze ya wokovu, maana kwa kadiri ya maelezo yako ni dhahiri kwamba umeingia mlango wa mauti, umeukosa ule wa Uzima!

  Unaniuliza:
  “”Kwa uelewa wako Lwembe, kinachotusafisha/kutuosha/kututakasa na dhambi ni DAMU ya Yesu au UBATIZO kwa jina la Yesu??””

  Kwanza, ni vizuri ukaiachilia akili yako kutoka ktk vifungo vya dini, iwe huru ili upate ufahamu wa mambo haya.

  Ili ufike ktk hatua ya kusafishwa/kuoshwa/kutakaswa dhambi zako, ni lazima kwanza uipokee Injili, hiyo ndio inayokujengea imani ukiisha kupewa kuisikia, ambako huja kwa neno la Kristo!

  Imani ndiyo inayokuongoza kuamini kwamba Kristo asiye na hatia alikufa badala yangu mimi mwenye dhambi, ili niachiwe kutoka ktk vifungo vya Ibilisi. Ndipo ktk hatua hiyo ya imani kuna sharti la Ubatizo ili kulikamilisha jambo hilo la kusafishwa dhambi zangu kwa Damu ya Yesu ambayo ni Neno lake; Ndio huo Ubatizo kwa Jina la Yesu Kristo unaokamilisha kuziondoa hizo dhambi unaousoma ktk Mdo 2:38! Naye Mungu akiisha kuziondoa dhambi hizo huzitupa ktk kilindi cha usahaulifu asizikumbuke tena!

  Pia, 1Pet 3:20-21 inakufunulia umuhimu wa jambo hilo kwa kadiri ya maangamizo yajayo ikikupa jinsi yake, ” … watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi…” Unaona Siyi, ingia safinani sasa wakati ungalipo, saa inakuja lango litafungwa!

  Sijui kama umeelewa kwamba Damu ya Yesu ni Neno lake? Hilo ndilo linalotakasa. Ule uzima wa mafahari au kondoo au mbuzi usingeweza kukurudia wewe, ndio maana kila mwaka kulikuwa na kumbukumbu la dhambi.

  Ili kukukomboa wewe, kulingana na Sheria ya Ukombozi, fahamu kwamba, haiwezekani wewe uzini halafu eti mbuzi afe badala yako, ndio mambo yaishe, hayaishi kwa uzima wa mbuzi! Hivi wewe unafikiri yule Magdalena wenu angewapelekea kondoo wale washitaki wake wangemwachia? Inahitajika damu yake imwagike, au ya nduguye aliye safi, ndipo uzima wa yule ndgye umrudie yeye; na kama ulivyowaona wale washitaki, hakuna hata mmoja aliyekuwa safi, wote tumetenda dhambi kama Maandiko yanavyosema, ndio maana ilimlazimu Mungu mwenyewe ktk Upendo, achukue mwili aje apambane na Hukumu yake mwenyewe ili wanae wawe huru! Kwahiyo kama Damu ya Mungu HAIONDOI Dhambi, basi ndugu yangu jua ya kwamba wewe mwenyewe ndiye DHAMBI; na ukiwa ndiyo hiyo Dhambi basi kwako iko Injili moja tu inayoweza kukusafisha, ZIWA LA MOTO!!!

  Gbu!

 106. Ndugu ck lwembe, Unajitahidi sana kupindisha ukweli, Mimi nia yangu sio mbaya kwako, ila lengo langu ni kutaka kuendelea kukuonyesha jinsi unavyoandika injili za uongo ambazo, hazina ule upendo wa kweli wa Mungu. Kwahiyo, itabakia kwa wewe kuamua kusuka ama kunyoa. Kwanza nimegundua kwamba hata maana ya kutubu wewe hujui!!, bwana Siyi alikuuliza swali zuri sana, kuhusu maana ya kutubu, sijui kama utamjibu. Kitu cha Muhimu wewe kutakiwa kujua ni kwamba, kutubu sio lesseni ya sisi kufanya dhambi kwa makusudi na kwa uhuru, isipokuwa lengo la kutubu ni la kumrudia Baba yetu pale tunapomkosea. Tazama, ni jambo la ajabu sana kwa Mkristo kama wewe, usiujue upendo wa Mungu na huruma yake, kwa kuwa, sisi kurudiwa na Baba yetu ni sehemu ya upendo wa baba na huruda yake anayotuonyesha ili asituhukumu kirahisi, ndio maana Mungu mwenyewe anasema” WOTE NIWAPENDAO MIMI NAWAKEMEA NA KUWARUDI !!. Soma(Ufunuo 3:19), Tena, katika Waebrania, neno la Mungu kwa kutaka kuthibitisha hilo, linatuambia hivi” Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili, Mungu awatendea kama wana, maana” NI MWANA YUPI ASIYERUDIWA NA BABAYE?, BASI KAMA MKIWA HAMNA KURUDIWA, AMBAKO NI “FUNGU LA WOTE” NDIPO MTAKUWA WANA WA HARAMU NINYI, WALA SI WANA WA HALALI. Soma(Waebrania 12:6-8). Kwa hiyo, kwa Mujibu wa neno la Mungu, ndugu lwembe ni mwana wa haramu, maana yeye anapinga tendo la sisi watoto wa Mungu, kurudiwa na Baba yetu pale tunapomkosea!!!!!. Tazama, wewe unashangaa lile andiko nililolinukuu la (warumi 3:23-26) ukisema kwamba halina tofauti na lile la kwako la (warumi 5:12), hayo ni kweli kabisa kwamba, ni maandiko yanayoelezea kitu kimoja ambacho ni sisi kusitiriwa na haki ya yule mmoja ambaye ni Yesu kristo (sio kwa haki yetu wenyewe na ukamilifu wetu wenyewe wa kimwili kama wewe unavyohubiri!!!). Biblia yenyewe iwazi kabisa, inasema hivi” Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele za zake kwa matendo ya sheria, Soma(warumi 3:20). Hii maana yake ni kwamba, sisi kwa ukamilifu wetu wenyewe, tukifika mbele za Mungu huko mbinguni, tutahukumiwa wote kwa sababu ya kutokukamilika kwetu katika mwili, lakini kwa sababu ya kukamilika kwa kristo na ile haki yake aliyokuwa nayo, ndipo sisi Mungu nae atatukubali kwa ile imani yetu kwa njia ya mwanae, ndio maana biblia inasema” Mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye, ninyi mmepata kuwa katika kristo yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, NA HAKI, NA UTAKATIFU NA UKOMBOZI > Kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana!!!. Soma(1Wakorintho1:29-31). Hapa sasa, ndipo panapoonyesha kwamba, sisi tunasitiriwa na haki ya kristo, sio haki yetu wenyewe, lakini jambo la ajabu, ndugu lwembe yeye anahubiri injili za kuzimu au pengine ni kwa kutokujua kwake, eti anasema kuwa yeye ni mkamilifu kama malaika, tena anajisifu kwamba, yeye hakosei wala hanashida ya kurudiwa na Mungu, kwa kuwa eti yeye hatendi dhambi!!!. Hizi ndizo hizo injili za kuzimu zilizojificha hapa duniani, Yaani badala ya kumuinua kristo, kumuamini na kumtegemea yeye pekee, wewe unafanya kazi ya kujitukuza kwa mwili wako huo wa kibinadamu huku ukijihesabia haki mwenyewe kwamba, hutendi dhambi wala ukosei. Wewe kwa ufahamu wako wa kuzimu huo, andiko linalokufaa ni hili pekee, soma(1Yohana1:10). Hebu nimalizie na swala la kutubu: Kutubu ni zawadi kutoka kwa Baba yetu. Hakuna aliye mwema kabisa ila mwema ni Baba pekee.Yeye mwenyewe wala hatutambui wema wetu na ukamilifu wetu, ila anatutambua kwa wema wa mwanae pekee, pale tunapotubu na kumpokea kama tutakuwa tumemkosea kwa bahati mbaya. Tazama Biblia inatuambi” AU WAUDHARAU WINGI WA WEMA WAKE NA USTAHIMILI WAKE NA UVUMILIVU WAKE USIJUE YA KUWA WEMA WA MUNGU UNAKUVUTA UPATE KUTUBU?, Soma(Warumi 2:4). Kwa hiyo ndugu lwembe, kutubu na kumrudia Mungu wetu, ni sehemu kabisa ya zawadi za wokovu wa Mungu, pale tu, tutakapomkosea kwa bahati mbaya na kutaka kumrudia kwa roho wa kweli na unyenyekevu kama mfano wa yule mwana mpotevu, ndio maana, neno la Mungu linasema” KWA MAANA NITAUNGAMA UOVU WANGU, NA KUSIKITIKA KWA DHAMBI ZANGU!!!!!. Soma(Zaburi 38:18). Ndugu lwembe, usipende kuwadanganya watu kwa maneno mazuri na ya kiufundi, au kama ni kweli ulikuwa hujui vizuri biblia, basi haya, hebu okota point hapo. Thax

 107. Sungura,
  Nilijua tu kwa wewe usiyejua kiundani kile kilichoanzishwa na Mungu pale bustanini baada ya anguko la Adamu na mkewe, ungesema kuwa mimi ni muongo, mzushi n.k. Hata sishangai, ila nakupa pole tu, maana hata unadiriki kabisa kusema kuwa Azazeli si Shetani bali ni Yesu mwenyewe!! Kama si ufedhuli ni nini rafiki yangu?? Kubali kufunguka Sungura, maana unazidiwa hata na watu wasiomjua Mungu!!! Angalia hata Kamusi yoyote ya Kiingereza itakwambia kuwa, azazel ina maana ya demon au a fallen angel!! Sasa wewe hiyo ya kwamba azazeli ni Yesu mwenyewe umeipata wapi?? Ukiwa masikini wa maarifa, ni vyema ukawa unajifunza kimyakimya tu, kuliko kujidai u tajiri kumbe huna!!
  Hata mimi sikusema kuwa Yesu aliingia patakatifu pa patakatifu mjini Yerusalemi na wala sikusema kuwa aliingia kule kwenye hema ya mbingumi akiwa na damu za wanyama. Nisome vizuri kaka. Na kama umekubali kuwa Kristo yuko patakatifu pa patakatifu mbinguni, na Musa aliambiwa na Mungu atengeneze mfano wa ile hema aliyooneshwa huko mbinguni. Akatengeneza ambayo ndiyo tunaijua kuwa pazia lake lilipasuka wakati wa kifo cha Kristo, je, unafikiri na lile la mbinguni nalo (lile alilooneshwa Msa), nalo lilipasuka?? Ajabu sana. Ndiyo maana unaipinga hata Neema ya Agano la Kale. Kuna aya zaidi ya 38 zizazotaja neno NEEMA katika Agano la Kale. Ukianza na Mwanzo 6:8, inaseama- “Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana”…..n.k., mbona haisemi alipata kibali kwa kutimiza sheria za kafara? Wewe vipi??
  Yaani unaonekana una shida kubwa sana ya kiuelewa rafiki. HAta suala la kafara tu linakupa shida. Kama mnyama aliyemchinja Mungu hakuchinjwa kwa ajili ya kufunikwa kwa dhambi za Adamu na mkewe, wewe unafikiri watoto wa Adamu walifundishwa na nani utoaji wa kafara za wanyama? Au Adamu mwenyewe umewahi kusoma popote kuwa Mungu alimfundisha utaratibu wa kutoa kafara za wanyama baada ya huyo wa bustanini?? Je, kama unadhani kafara za wanyama zilianzia kwa akina Musa, akina Ibrahimu na wanae wao walitoa kafara za watu? Kwani mshahara wa dhambi ni nini? Siyo mauti? Kama watu walitenda dhambi, na badala ya kufa waliua kondoo, mbuzi, fahari n.k., japo kwa kuzigharimia wenyewe, unafikiri hiyo haikuwa NEEMA?? Pole sana, inabidi ujifunze vizuri maana ya NEEMA!!
  Wuuuu!! Ona unavyosema, “Kitendo cha wa agano la kale kuchinja mnyama ndipo wahesabiwe haki siyo kitendo cha imani, imani ni sisi leo kuamini tumesamehewa kwa damu ambayo hata hatukuiona ikimwagwa hapo patakatifu pa patakatifu, wala hatukumwona kristo akipaingia, ispokuwa tunamwona akiwambwa msalabani, lakini tunauhakika kuwa alifanya hivyo kwa kuamini maandiko yanavyosema. – Hiyo ndiyo imani”
  Nakwambia leo umezungumza kama mtoto mdogo rafiki yangu. Sina uhakika kama ulikuwa sawa kifikra. Ulishawahi kunishauri kipindi fulani nijitathimini kama si kutulia kidogo kuhusu majibu yangu kwa watu. Leo na mimi nakupa ushauri huohuo!! Na kukuongezea wa ziada ya kwamba, ni bora ukawa unasoma michango yako kwanza kabla hujairusha hewani!! Watu wa agano la kale, kilichowaponya ni IMANI kama ilivyo kwetu leo. Soma (walawi kuaznia sura ya 3….) habari za kuweka mikono juu ya vichwa vya wanyama waliokuwa wakichinjwa kama kafara, uone kama haikuwa ni imani hiyo. Soma Waebrania inasema Kwa imani, Musa….., Kwa Imani Ibrahimu…….., Kwa imani… n.k., n.k.. Watu wa maagano yote, kilichowaokoa, na kitakachowaokoa ni IMANI tu!! Hiyo iko bayana kiasi hicho!!
  Aidha, mimi sikusema kuwa Yesu ataingia the Most Holy Place. Nilichokisema mimi ni kwamba, yuko kule tayari!! Kwa sasa anaifanya hiyo kazi!! Mojawapo ya kazi kuu ya kuhani kwa mujibu wa Biblia ilikuwa ni kuwaombea watu –kuwapatanisha na Mungu. Na ndiyo kazi kuu Yesu anaifanya kwa sasa. Biblia inasema, “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote”- 1 Yohana 2:1-2. Kipindi cha kutoka HAPO (the Most Holy Place ) KIKIFIKA, atatamka maneno haya, “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa” Ufunuo 22:11, maana hakutakuwa na maombezi tena. Hakutakuwa na toba tena!! Mlango wa rehema utakuwa umefungwa bro!!

  Huu ndio ukweli wa Maandiko, jitahidi kuufahamu!!

  Siyi

 108. C.k lwembe, Mimi naona unakosea sana katika misingi ya imani uliyojijengea. Tazama: Biblia inapokuambia kwamba, umezaliwa mara ya pili, huwezi kutenda dhambi, inatarajia kwamba, wewe ukiwa ni mtoto wa Mungu, ni lazima utasimama imara na kuhakikisha kwamba, utajilinda na yule mwovu shetani ili asikuguse akakupoteza. Sisi tunatakiwa tusimpe ibilisi nafasi ili ule uzao wa Mungu uweze kuendelea kukaa ndani yetu, ndio maana waraka huo huo wa Yohana uliounukuu, uliendelea kusema hivi” Twajua ya kuwa, kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi bali yeye aliyezaliwa na Mungu “HUJILINDA” wala yule mwovu hamgusi, Soma(1Yohana 5:18). Kwa hiyo, katika kuzaliwa kwetu mara ya pili, ni lazima pia tufahamu kwamba, anguko linaweza kabisa kutokea kama hatutalizingatia neno la Mungu na kusimama imara. Pia kama haitoshi, Paulo nae alituasa wakristo hivi” Anaejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Soma(1Wakor 10:12). Kwa hiyo, mitume wote wa Mungu, walitambua kwamba, ijapokuwa sisi tumeokoka na kuzaliwa mara ya pili kwa roho wa Mungu, Pia liko la kufanya zaidi, ili lile neno la Mungu litende kazi sawa sawa na ile ahadi yake, ndio maana bwana Yesu alisema” Basi kila asikiaye hayo maneno yangu na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili,,,,, Soma( Mathayo 7:24). Kwa hiyo, tusidanganye watu kwamba, ukishazaliwa kwa mara ya pili huwezi kupata anguko, isipokuwa uimara wa Mwana wa Mungu yeyote ni neno la Mungu pekee ambalo ndilo silaha yake ya pekee. Nilazima mmoja wetu akipungukiwa na silaha hii ataanguka, ndio maana biblia inasema” msimpe nafasi ibilisi”. Sasa, hebu niendelee kuitetea ile hoja yangu. Jambo linalo nisikitisha kwako ndugu lwembe, ni wewe kuikataa toba kabisa na wakati kunandugu zako wengi ambao waliokoka lakini wakampa nafasi shetani kwa njia ya kutolizingatia neno la kristo kuwa ndiyo silaha yao ya pekee. Lakini wanapoyagundua makosa yao na kutaka kutubu na kurudi kundini, Baba yetu anawapokea kwa sababu yeye anatupenda kwa upendo wa nguvu mno, kuliko hata haya mauti tunayoyaongelea sisi!!. Kwanza msamaha wa Mungu sio lazima ukutazame wewe jinsi ulivyo mwema kupita wengine, bali katika pendo na rehema zake Mungu mwenyewe, ndio maana bwana yesu alisema “hakuna mwema ila mwema ni baba pekee”. Nakuandikia maelezo haya kwa sababu wewe unaonyesha ni mtu unaependa kujitukuza mwenyewe na kujihesabia haki badala ya kupenda kuwa na unyenyekevu. Hebu tazama ule mfano wa Mwana mpotevu katika tafsiri ya kiroho iliyokusudiwa haswa ili ituonyeshe jinsi Baba yetu wa mbinguni alivyokuwa na upendo wa ajabu mno. Yule mwana mpotevu alipogundua kwamba alimkosea Baba yake alisema hivi” NITAONDOKA, NITAKWENDA KWA BABA YANGU NA KUMWAMBIA, BABA NIMEKOSA JUU YA MBINGU NA MBELE YAKO. Soma(Luka 15:18) linganisha na (Luka15:31-32). Istoshe, hata Petro ambaye alikuwa mwanafunzi wa yesu aliyeokoka, yeye alifahamu kuwa yeye hakuwa mkamilifu kwa asilimia zote, ndio maana alipomsaliti kristo, pia akatambua umuhimu wa kutubu kwa kweli na kumrudia baba yake. Sasa, ndugu yangu lwembe nikikwambia kwamba unahubiri injili za kuzimu zisizokuwa na kumrudia Baba yetu pale tunapokosea, wewe unaona nakusema vibaya jambo ambalo sio kweli!!. Hebu jitazame ndugu yangu jinsi unavyoshindana kuliko kuwa mkweli, umeshindwa hata kujua kwamba, wokovu wetu unahitaji vitu viwili ambavyo ni kumkiri kristo na kujinyenyekeza kwake kwa njia ya imani pekee!!!!. Soma( warumi 10:10). Wewe neno la Mungu linasema” Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote, soma(1Yoh 1:9), pia soma(Ufunuo 2:4-5), lakini kinyume chake wewe unatuhubiria ile injili yenye roho wa yuda mwenye ibilisi ambaye badala ya kwenda kutubu na kumrudia baba yake, yeye anaamua kwenda kujitundika na kujiuwa maana yeye alifikiri kwa Mungu hakuna msamaha wa kutubu kwa kweli na kurudi kundini!!!. Pole sana ndugu yangu. Asante kwa mawazo yako, lakini mimi nakuomba ukague hiyo misingi ya kanisani kwako vizuri…lakini ningeomba unipe tofauti kati ya petro aliyefanya dhambi na kutubu na kukubalika, na wewe unayepinga tendo la kutubu kama rafiki yako yuda.

 109. Siyi,
  WEWE NI MUONGO!!
  Robo tatu ya jibu lako kwa swali langu na la Mabinza ni uongo ulio na hila ya mafundisho potofu yasiyo na substance katika Injili ya kristo.

  Ona ulichosema;
  ”Baada ya kukamilika kwa kazi ya ukombozi –Kristo (aliye kuhani wetu mkuu) akikamilisha kazi ya upatanishi, atafanya vilevile kama alivyoasisi mwenyewe huko nyuma. Shetani atabebeshwa dhambi za wooote waliochomoka kutoka kwake –watakatifu waliokolewa. Kile alichokisema Mungu, sharti kitimie wapendwa”

  Hiki kitu unachokisema hapa Siyi ni uongo, hakuna andiko linalokwambia hivyo, ispokuwa ni hisia zako za kujaribu kufanya mfananisho wa kilichofanyikia agano la kale ukadhani kinafanana na agano jipya kwa mantiki hiyo.
  Katika agano jipya mwenye kufanyika azazeli si shetani bali ni Yesu mwenyewe, na tayari alishafanyika hivyo.
  Kule kusulubiwa kwake nje ya mji ( Golgotha) ni sawa na kule kupelekwa nje ya mji(porini) kwa yule mbuzi ktk agano la kale na ile mizoga ya wanyama ambao damu zao zimenyunyizwa madhabahuni. (Hebr 13:12 – And so Jesus also suffered outside the city gate to make the people holy through his own blood.

  Yule mbuzi hakuwa ametenda dhambi yoyote, kama ambavyo Kristo hakusulubiwa kwa kutenda dhambi yoyote, ispokuwa ni kule kubebeshwa hatia yeye asiye na hatia.

  Lakini pia elewa, tofauti na kuhani wa agano la kale ambaye aliingia patakatifu pa patakatifu siyo na damu yake bali ya wanyama, Yesu aliingia patakatifu pa patakatifu akiwa na damu ya kwake mwenyewe, na hakuingia patakatifu pa kibinadamu (hekaluni Yerusalem), japokuwa alisulubiwa kibinadamu kabisa.

  Kingine hiki hapa umesema:

  ”Dhambi za wanaotubu, zinawakilishwa na alama za damu ya Kristo katika hema ya mbinguni. Baada ya kazi ya upatanishi, sharti alama hizo (za damu zilizofunika dhambi) ziondolewe!! (Sijui kama ninaeleweka vizuri kwenu)!! Ninachosema ni kwamba, dhambi za Siyi baada ya kuondolewa kwake (na anazoendelea kuondolewa maana Kristo bado yuko patakatifu pa patakatifu akiendelea na kazi ya kuupatanisha ulimwengu), dhambi za Siyi bado zimeacha alama za damu ya Kristo, kwenye mapazia/kuta za hema ya patakatifu pa patakatifu mbinguni”

  Hili nalo ni fundisho potofu, amabalo linatoka katika wazo la kusadikika. Hakuna mahali injili inatuambia hivyo. Siyi huu nao ni uongo ambayo nyuma yake kuna dhana ileile yenu(wasabato) ya siku zote inayopingana na maandiko kuwa hakuna kuokoka tukiwa duniani.
  Dhambi zako zinaachaje alama za damu ya kristo kwenye mapazia ya hema za kukutania, ikiwa pazia la hema ya duniani lilipasuka la mbinguni analosema lenyewe bado linafanya nini?

  Na hiki hapa:

  ”watu wengi (hawa waj2) wanaamini kuwa, zamani za agano la kale, watu waliokolewa/hesabiwa haki kwa sheria. Wanaamini kuwa, katika agano jipya, watu wanaokolewa kwa neema tofauti na ilivyokuwa kwenye agano la kale. Jambo ambalo SIYO KWEL Neema imekuwepo tangu zamani, tangu anguko la Adamu. Kitendo cha kumchinja kondoo, mbuzi au fahari kwa niaba ya mdhambi, ilikuwa ni NEEMA tu hiyo”

  Ivi unaelewa hata maana ya Neema? Biblia ndiyo inayosema hivyo kuwa katika agano la kale watu walihesabiwa haki kwa sheria, na katika jipya kwa Neema. Wewe umeyatoa wapi maneno yanayosema kuwa hata katika agano la kale watu walihesabiwa haki kwa Neema, kama siyo mawazo yako tu vile ambavyo wewe unadhani (kusadikika). Huna hata aibu!!

  Mungu hakuchinja mwanakondoo kwa ajili ya kuondoa dhambi za Adamu on first place, alimchinja kwa ajili ya kuchukua ngozi ya kumvika Adam. Kondoo/wanyama waliochinjwa chini ya Torati ya Musa kwa ajili ya dhambi damu zao zilinyunyizwa tofauti kabisa na huyo kondoo wa Adam na Eva.

  Ili ujue mantiki ya neema katika hili, jiulize tu kwamba huyo mnyama ambaye mtu (mdhambi)alimtoa ilikuwa inamgahrimu nani? Kila mtu ilimlazimu atoe myama ambaye amemgharimu yeye mwenyewe (merited favour), lakini kristo alipokufa kwa ajili yetu ilikuwa ni gharama ambayo haijatugharimu sisi, bali ilimgharimu Mungu ambayo kwetu hiyo ni ‘unmerited favour – GRACE.

  Kitendo cha wa agano la kale kuchinja mnyama ndipo wahesabiwe haki siyo kitendo cha imani, imani ni sisi leo kuamini tumesamehewa kwa damu ambayo hata hatukuiona ikimwagwa hapo patakatifu pa patakatifu, wala hatukumwona kristo akipaingia, ispokuwa tunamwona akiwambwa msalabani, lakini tunauhakika kuwa alifanya hivyo kwa kuamini maandiko yanavyosema. – Hiyo ndiyo imani.

  Jambo la msingi sana sana ambalo nataka ulijue vizuri ni hili, kwamba; Yesu tofauti kabisa na makuhani wa torati (Agano la kale) hataingia tena patakatifu pa patakatifu ka ajili ya kutoa damu yake, alishamaliza hiyo kazi mara moja tu, na wala maandiko hayatuambii kuwa atapaingia tena kama wewe unavyodai. Na hapo ndipo ujue kwamba damu yake ina nguvu kuliko ya wanyama.
  ( HEBREWS 9:12 – He did not enter by means of the blood of goats and calves; but he entered the Most Holy Place once for all by his own blood, thus obtaining eternal redemption).

  Unatakiwa kuelewa maandiko, siyo kushika dhana za kusadikika!!

 110. Lwembe,
  Nakuona hutaki kuniambia moja kwa moja na badala yake unasemea kwa jirani habari za Siyi!! Si useme tu hapa moja kwa moja kaka?? Shida ni nini?? Tangu mwanzo, nimekwambia una safari ndefu sana ya kwenda!! Umeshikilia saaaaana creeds za dini yenu badala ya mafundisho ya Biblia. Na usipokubali kufunguka, ukajifunza, ukakubali kukaa chini ukalinganisha aya kwa aya na sura kwa sura, utapotea tu!! Kabla sijakusaidia katika hili ulilokuja nalo sasa dhidi ya Siyi (na mafundisho ya Biblia), naomba nikuulize swali dogo tu kwanza, halafu nitajaribu tena kwa mara nyingine kukusaidia. Usijidai hulioni kama ulivyofanya kwa baadhi ya maswali yangu ya huko nyuma.
  Swali.
  Kwa uelewa wako Lwembe, kinachotusafisha/kutuosha/kututakasa na dhambi ni DAMU ya Yesu au UBATIZO kwa jina la Yesu??
  Ninakusubiri!!!
  Siyi

 111. Kuhusu Kristo kuondoka ktk Kiti cha Rehema, kama yalivyo mawazo yako, ndivyo na ya swaiba wako Siyi yalivyo!

  Nyote dini zimewapumbaza mkaelekezwa kwamba Kristo yuko sehemu fulani huko mbinguni amekaa akiyapokea maombi na maungamo yenu akimrundikia Shetani mizigo ya dhambi zenu hizo mnazoendelea nazo!

  Mwenzako mapepo ya dini yamempeleka kuzimu kabisa, huko chini shimoni, yamemfunza kuikataa Damu ya Kristo kwa ajili ya Ondoleo la Dhambi, yaani kwishaa!!! Ninavyokuona nawe hauko mbali sana, maana hatua ni zile zile, huyo alianza kwa kuliita Neno la Mungu “ufedhuli”, nawe unaliita “mafundisho ya mashetani”!

  Kuipokea Neema ni kukipokea Kiti cha Rehema; ndio kumpokea Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, ndiko kuwa ndani yake na Yeye ndani yako, yeye ndiye arehemuye, yeye ndiye Rehema! Anapokuwa ndani yako maana yake Kiti cha Rehema kimo ndani yako, kaka! Ndio maana kwa upumbavu wenu mnapandishwa milimani kwenda kuomba Rehema, kwa kule kulikataa kwenu neno ambalo lingewaondolea dhambi zenu na Maandiko yakafunuliwa kwenu, mmeukataa Ubatizo unaoleta Ondoleo la dhambi Mdo 2:38, kwahiyo shina la dhambi lingalimo ndani yenu mtazunguka nalo maisha yenu yote kwa hasara ya kuupoteza Wokovu wenu!

  Ukisikia kwamba hakuna dhabihu kwa ajili ya kosa ulilolifanya basi jua ya kwamba Kiti cha Rehema kimeondoka ktk maisha yako, labda utabaki na uongo wa dini!! Akiondoka kaka, hapo panabaki panafuka moshi, badala ya Rehema kinakuwa Kiti cha Hukumu!!!

  Patakatifu pa Patakatifu kwa leo pako ktk mioyo ya hao walioondolewa dhambi zao na sasa kuwa wasiotenda dhambi, Mungu hushuka akae humo, miili yao ni Hekalu lake!!!

  Ukuhani ulipobadilika ninyi mlipigwa chenga, na kama Mungu ameyafunga haya msiyaelewe kadiri tunavyoendelea nanyi tukirudia rudia yale yale mnayoyakataa ni dalili tosha kwamba nasi twaweza kuishia ktk upumbavu wenu, tukalikataa Neno litutakasalo, ukilikataa Neno lolote lile, unakuwa umeikataa Damu kama Siyi kwahiyo unarudishwa na mapepo ya dini huko kwenye Torati, upende usipende haijalishi unaimba ngonjera gani ya wokovu, unapaswa uitimize Sheria yote au uangukie ktk laana ya Sheria kwa kuikataa Neema!!

  Gbu!

 112. Mhina,
  Unasema nikipewa “wanafunzi wapumbavu” ishirini!!! Bali sijawahi kuona darasa la wanafunzi wapumbavu, labda la wajinga, maana hakuna mpumbavu anayeweza kuelimika, pia nafahamu kwamba ni dini pekee zinazozalisha wapumbavu, kwahiyo hata wazo la kupewa wanafunzi wapumbavu, lazima liwe limetokana na upumbavu wa dini!!!

  Ktk ujinga uliamini kwamba dhambi haiepukiki kwa 100%, ndio ukaja na nukuu ya Muh 7:20 ukijihalalishia hali yako hiyo ktk “wokovu” ulionao. Nikakuambia kwamba hayo maelezo ya Muh yanazungumzia hali ilivyokuwa kabla ya Kristo. Tena nikakuambia maelezo hayo ndiyo haya hapa yanarejewa tena ktk Rum 5:12 ili kuyaleta hayo kipenzi chako ya Muh 7:20 ktk ukomo kwa hao wanaompokea Kristo; lakini kwa Giza la dini umeshindwa hata kuyaona hayo na badala yake unarudia tena kunukuu Muh 7:20 ukizidi kuing’ang’ania, huo kama si zaidi ya ujinga ni nini?!!
  Hivi unaijua kweli hata maana ya wokovu au mnajiimbia tu ngonjera za wokovu?

  Maandiko yanakuambia wazi kabisa kwamba:-
  “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.” 1 Yoh ‭3‬:‭9‬
  Angalia tafsiri yako ya Andiko hilo:
  “”Wokovu wetu unahitaji vitu viwili muhimu sana, kumkiri kristo na kujinyenyekeza kwake, kwa njia ya imani pekee. Wala mimi sikatai, nikweli kabisa kwamba, Mkristo aliyeokoka na kuzaliwa kwa mara ya Pili, hawezi kutenda dhambi kwa makusudi, …. Lakini pamoja na hayo yote, ni Muhimu kufahamu kuwa huyu mkristo bado ni Mwanadamu kama wanadamu wengine, hata pengine kwa kuteleza kwake, yeye huweza kuwa na chuki au hasira wakatifulani maana yeye bado hajawa mkamilifu kabisa kwa 100%. … Pasipo kutetea kwa udhehebu, ni lazima hata sisi wenyewe tunaojifanya kuwa tumeokoka, tena ni malaika ni lazima wakatifulani tunajikuta katika matatizo hayo au yafananayo na hayo, kwa kiasi hata ni kidogo sana cha kibinadamu, Soma (Mhubiri 7:20) , ndio maana pia, sio kwamba tayari tumekamilika kabisa ila twakaza mwendo huku tukisitiriwa na haki ya kristo (sio haki yetu), Soma( warumi 3:23-26).””

  Unaiona hiyo ngonjera yako isiyo na mbele wala nyuma!
  1: Ni wapi uliposoma kwamba “”wokovu unahitaji vitu viwili, kumkiri Kristo na kujinyenyekeza kwake, kwa Njia ya imani pekee”? Mnajisemea tu maneno ya dini bila ufahamu wowote ule kuhusu mnachokisema!
  Kristo ni Neno la Mungu, ambalo ndilo hilo ktk 1Yoh ‭3‬:‭9 ambalo wewe kuhusu hilo unasema, “”Lakini pamoja na hayo yote, ni Muhimu kufahamu kuwa huyu mkristo bado ni Mwanadamu kama wanadamu wengine, hata pengine kwa kuteleza kwake, yeye huweza kuwa na chuki au hasira wakati fulani maana yeye bado hajawa mkamilifu kabisa kwa 100%.””‬
  Kama unalikataa neno hilo la 1Yoh 3:9, ambalo ndiye Kristo, basi huyo unayemkiri na kujinyenyekeza kwake ni nani kama si mapepo ya dini yanayokutia upako wa kulitilia shaka neno la Mungu nawe hujui!!! Mungu anasema huyo aliyezaliwa kwake hatendi dhambi, wewe unatia “lakini” kama alivyofanya nyoka kule Edeni, halafu bila ufahamu unasema eti unayafanya haya kwa njia ya imani!!! Ukisikia Upumbavu wa dini, ndio kama huu!

  2: Ni wapi uliposoma kwamba, “”Mkristo aliyeokoka na kuzaliwa kwa mara ya Pili, hawezi kutenda dhambi kwa makusudi, …””
  Eti “hawezi kutenda dhambi kwa makusudi”; kazi yenu kuongeza ongeza maneno yenu juu ya neno la Mungu; umeambiwa hatendi dhambi wewe ili kuipotosha maana iliyokusudiwa unaongeza ‘kwa makusudi’; unaona mnavyoendeshwa na mapepo ya dini? Mnalisulubisha Neno la Mungu kwa mara ya pili kwa upumbavu wa kujitakia; umeambiwa ukiongeza juu ya Neno la Mungu jina lako LINAFUTWA ktk Kitabu cha Uzima!!

  3: Hata hiyo Rum 3:21-26 unayoniambia nisome, ina tofauti gani na Rum 5:12-17 uliyoshindwa kuielewa? Mnajibandikia tu vifungu! ndio maana unaendelea tu kufundisha jinsi ya kuendelea na dhambi ukijiokotea tu vifungu usivyovijua hata maana yake! Tazama unachokikazania: “…ni lazima hata sisi wenyewe tunaojifanya kuwa tumeokoka, tena ni malaika ni lazima wakatifulani tunajikuta katika matatizo hayo au yafananayo na hayo, kwa kiasi hata ni kidogo sana cha kibinadamu, Soma (Mhubiri 7:20) , ndio maana pia, sio kwamba tayari tumekamilika kabisa ila twakaza mwendo huku tukisitiriwa na haki ya kristo (sio haki yetu), Soma( warumi 3:23-26.””
  Wewe ni kweli hujakamilika, aliyekamilika hawezi kuja na maelezo yasiyoeleweka kama yako, bora hata ulivyokiri kwamba ‘unajifanya mmeokoka, tena ni malaika’, ila chunga, Paulo anasema akija hata malaika kutoka mbinguni akafundisha tofauti na Injili tuliyoifundisha sisi, kwamba “Aliyezaliwa na Mungu hatendi Dhambi…” yeye akasema hatujakamilika kwahiyo ni lazima tutende dhambi hata kidogo tu, huyo alaaniwe!!! Sasa wewe sijui ni malaika wa kutoka wapi, kama ni wa kuzimu huyo hana laana bali yeye mwenyewe ni laana!!! ndg yangu Mhina neno la Mungu usilirahisi, ni Upanga ukatao kuwili, lipokee kama lilivyo upone usitie akili mingi kama Siyi!!!
  …………………………

 113. @ Shalom Mhina.
  Nakupongeza kwa jinsi unavyojitahidi kuandika/kusema uhalisia wa maisha ya mkristo anayeukulia wokovu kila siku. Mkristo anayekufa kila siku katika ulimwengu wa mwili!! Mungu akubariki. Umenifurahisha sana. Nimeona nisinyamze kukushukuru. Bado jambo moja kwako, – Ikumbuke siku ya Sabato uitakase!!
  Neema ya Bwana ikufunike sana.
  Siyi

  @ Shalom Mabinza na Sungura!!
  Awali ya yote, mniwie radhi kwa kuchelwa kujibu maswali yenu. Hii iilitiokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu. Mnisamehe sana wapenzi!!
  Aidha, nimefurahishwa sana na maswali yenu marafiki zangu. Naomba kutumia fursa hii kuwajibu nyote kwa pamoja maana maswali au hoja zenu, zinaafanana kwa kiasi kikubwa!! Twendeni pamoja sasa….
  Kwanza, nipende kuwaondoa wasiwasi kuwa, hata Siyi anaamini kuwa Damu ya Yesu pekee ndiyo inayotusafisha na dhambi zetu zote!! Yenyewe hututakasa na kutuosha kabisa tukabaki safi bila ya waa lolote. Siyi na yeye anaamini hivyohivyo, wala msichanganyikiwe marafiki zangu.
  Pili, mpango wa wokovu kwa mwanadamu uliwekwa tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Tangu mwanzo, Yesu alipangwa na mbingu kwa kazi ya kuukomboa ulimwengu. Yohana anasema, “… Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”. Na ni kwa njia ya Kristo pekee wanadamu wote wataokolewa na mwanakondoo “…aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia” -Ufunuo wa Yohana 13:8. Kwa hiyo mchakato wa ukombozi tangu mwanzo ulivyokuwa, ndivyo utakavyohitimishwa. Ulianzishwa na Mungu (Kristo) mwenyewe, atahutimisha Kristo huyohuyo!! Jinsi alivyouanzisha, ndivyo atakavyouhitimisha!!

  Tatu, Sungura ameuliza kuwa mambo haya, nimeyatoa wapi kwenye Biblia?? Nipende kusema tu kuwa, hayo yote niliyoayasema, niliyatoa kwenye Biblia –soma Walawi 16-23. Ukisoma habari za ukuhani ulionzishwa na Kristo mwenyewe pale bustanini baada ya anguko la Adamu, ukaendelea hadi kipindi cha wana Israel hadi kufa kwa Yesu msalabani, utauona mchakato ni uleule tofauti ni settings tu!! Hata kwa ukuhani anaoendelea nao Kristo sasa mbinguni kama mpatanishi wetu, mchakato wa ukuhani ni uleule tofauti na settings na nani anayefanya kazi hiyo kwa sasa (Yesu) tofauti na ilivyokuwa hapo kabla ambapo ilifanywa na wanadamu (makuhani). Baada ya kukamilisha kazi ya ukombozi, Kristo atapasafisha patakatifu pa patakatifu (kama alivyokuwa akifanya kuhani mkuu enzi za agano la kale –Lawi 23 na ndipo atamkabidhi mwenye kuhusika (ibilisi) mizigo yooote ya dhambi ya akina Siyi, Sungura, Mabinza, Mhina, Lwembe n.k. wengine wote waliotubu akawapatanisha kwa Baba yake!! Hii ndiyo ilikuwa kazi ya kuhani mkuu siku kuu ya upatanisho.

  Nne, ukisoma sura za vitabu alivyovileta Mabinza, viko bayana sana; kwamba, badala ya kuendelea kuwa na machinjio ya wanyama kila sehemu palipo na hekalu/kanisa. Yesu alichinjwa (akamwaga damu yake ya thamani) kwa ajili ya ondoleo/pumzisho la mizigo ya dhambi kwa kila amwaminiye na kutubu!! Akina Adamu, Ibrahimu, Isaka, Musa, Haruni, Yoshua, n.k., walihesabiwa haki kwa imani ya kumwaga damu za wanyama (kafara za wanyama). Na hili lilidhihirika (lilionesha kukubaliwa) pale Mungu aliposhusha moto na kuteketeza sadaka zao!! Sisi leo tunahesabiwa haki kwa imani kupitia damu ya Kristo tu!! Maana wengine hata hatujaiona hiyo damu yenyewe ila kwa imani tu, tunapata ondoleo la dhambi. Tukianguka dhambini kwa kuteleza/makusudi, hatuna budi kurejea kwa imani na tumaini lilelile la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani tu katika damu ya Kristo. Katika Agano la kale, pamoja na Mungu kuonesha ukubali wa toba za watu (kwa njia ya sadaka za wanyama), bado dhambi hizo zilizotubiwa, zilimgonja mbuzi alimaarufu kwa jina la “mbuzi wa azazeli”. Azazeli -pori lisilokaliwa na watu, lenye wanyama mwitu wakali. Kila mwaka mbuzi huyo alibebeshwa zigo hilo!! Baada ya kukamilika kwa kazi ya ukombozi –Kristo (aliye kuhani wetu mkuu) akikamilisha kazi ya upatanishi, atafanya vilevile kama alivyoasisi mwenyewe huko nyuma. Shetani atabebeshwa dhambi za wooote waliochomoka kutoka kwake –watakatifu waliokolewa. Kile alichokisema Mungu, sharti kitimie wapendwa.

  Tano, wakristo wengi leo, wanaamini kuwa, damu ya Yesu inaondoa dhambi za watu -kuzidelete zisionekane popote kabla hata ya kuanganmizwa ulimwengu!! Wanaamini kuwa, mtu anapompokea Kristo, dhambi zake zooote zinaondolewa kwake (jambo ambalo ni sahihi kabisa), na kufutwa zisiletwe tena kwenye kumbukumbu kabla ya dunia hii kuchomwa moto. Dhana hii siyo sahihi kabisa. Dhambi za wanaotubu, zinawakilishwa na alama za damu ya Kristo katika hema ya mbinguni. Baada ya kazi ya upatanishi, sharti alama hizo (za damu zilizofunika dhambi) ziondolewe!! (Sijui kama ninaeleweka vizuri kwenu)!! Ninachosema ni kwamba, dhambi za Siyi baada ya kuondolewa kwake (na anazoendelea kuondolewa maana Kristo bado yuko patakatifu pa patakatifu akiendelea na kazi ya kuupatanisha ulimwengu), dhambi za Siyi bado zimeacha alama za damu ya Kristo, kwenye mapazia/kuta za hema ya patakatifu pa patakatifu mbinguni. Kutakaswa kwa patakatifu pa patakatifu (kwa mara ya pili), kutakuwa ni baada ya watakatifu kuokolewa. Baada ya hapo, shetani atapokea malipo yake na ndipo utimilifu wa kauli ya Mabinza “Dhambi zao na kutokutii kwao sitakumbuka tena”. Utimilifu wa kauli hii, unakuja baada ya kuwa Lucifer ameshaangamizwa tayari. Watu wanaishi bila dhambi!! Hakuna wa kuwadanganya tena!!

  Sita, watu wengi (hawa waj2) wanaamini kuwa, zamani za agano la kale, watu waliokolewa/hesabiwa haki kwa sheria. Wanaamini kuwa, katika agano jipya, watu wanaokolewa kwa neema tofauti na ilivyokuwa kwenye agano la kale. Jambo ambalo SIYO KWELI. Maana hata katika Agano la kale, watu waliookolewa kwa NEEMA tu. Neema imekuwepo tangu zamani, tangu anguko la Adamu. Kitendo cha kumchinja kondoo, mbuzi au fahari kwa niaba ya mdhambi, ilikuwa ni NEEMA tu hiyo!! Kuokolewa kwa akina Nuhu, kulitokana na NEEMA za Mungu. Kama ingekuwa sheria, Mungu angemuua Adamu palepale baada ya dhambi!! Ili kuelewa vizuri kazi ya Kristo kwa sasa, kama kuhani wetu mkuu, wakristo wengi hawana budi kusoma kazi ya kuhani na kuhani mkuu katika agano la kale ili wafunguliwe kwanza!! – Lawi 16-23.
  Saba, Mungu hakuumba kiumbe yeyote kwa ajili ya kumchoma moto au kumuua. Mungu atakachoua/kuchoma moto ni dhambi. Na kwa vile dhambi zinakaa kwa wadhambi, wakati Mungu akizichoma moto, na wadhambi nao wataungua. Ibilisi anajua kuwa kuna dhambi za watakatifu zitakazochomwa moto. Kwa vile yeye ndiye mwanzilishi wa dhambi, wakati wa kuzichoma moto, na yeye ataunguzwa kwa vile zigo litabebswa kwake. Huwezi kulielewa agano jipya, bila ya kulielewa vizuri agano la kale. Agano la kale, ndio msingi wa agano jipya, sharti lifahamike bayana kwa kila ajiitaye Mkristo, vinginevyo watu watabaki kuchanganyikiwa.

  Niwasihi kujisomea habari za kazi ya ukuhani. Siyi anaamini kuwa damu ya Yesu Kristo iko kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake na za wengine. Dhambi za Siyi, zinapoondolewa kwake, hazideletiwi, isipokuwa zinafunikwa kwa damu ya Yesu kwenye mapazia/kuta za hema ya mbinguni. Siku ya mwisho baada ya miaka elfu, shetani akishakufunguliwa, atababeshwa ile mizigo ya dhambi zooote za Siyi na wengine (watakaokolewa kama yeye). Jambo hili liko wazi sana wapendwa kimaandiko. Someni tu, wala hakuna ubishi wowote hapo!! Neema ya Bwana iwafunike.
  Siyi

 114. Siyi,
  Mimi si kwamba nakushangaa tu bali pia sijakuelewa kabisa! Siku ya tarehe 24/4/2015 kunako saa 10:44PM, pamoja na mambo mengine, ulimjibu Mhina hivi, “….Kuna kitu hujakiona hapa. Sikia, kaka!! Ni kweli kabisa damu za wanyama hazikuondoa dhambi. Zilifunika tu. Hata Damu ya Yesu mwenye, haiondoi dhambi, bali inafunika tu!! Huuuh!!! Usinishangae!!………” Je, ulikuwa timamu kweli Siyi? Hivi, mtu anaweza akawa mtakatifu kisha bado akawa na dhambi? Na ikiwa Agano la Kale lilikuwa kivuri cha uhalisi wa leo katika Kristo, iweje tena kitendo kilichotendwa na Mungu kama kivuri cha Sadaka ya ondoleo la Dhambi, kiwe tena mwendelezo katika Agano jipya kwa kifo cha Kristo? Maana ya kuja na kufa yesu malabani inafaida na maana yake nini Siyi? Unatuchanganya unajua?! Kwa maelezo yak ohayo sasa tunapataje ujasiri wa kusema kuwa Yesu alikuja kuitimiliza Torati? Au tunaposema, “Kwakupigwa kwake sisi tumepona” tumepona nini, ikiwa ‘DUDE’ bado kumbe limefunikwa tu, kama wakati wa akina mzee Haruni?! Tufafanulie bhana!

  Kwangu hujaeleweka, hebu soma Ebrania ile sura ya 10 kisha uelezee ulichokuwa ukikimaanisha uliposema, “……Hata Damu ya Yesu mwenye, haiondoi dhambi, bali inafunika tu!!……” !!!!!!!

  Ebrania 10:1-18 ambayo inasema hivi, “10 Kwa kuwa Torati ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka, kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu. 2Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena, kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. 3Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, 4kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.
  5Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani alisema,
  “Dhabihu na sadaka hukuzitaka,
  bali mwili uliniandalia,
  6sadaka za kuteketezwa na za dhambi
  hukupendezwa nazo.
  7Ndipo niliposema, ‘Tazama niko hapa, kama
  nilivyoandikiwa katika kitabu,
  Nimekuja kufanya mapenzi Yako,
  Ee Mungu.’ ”
  8Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe). 9Kisha akasema “Tazama niko hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi Yako.” Aondoa lile
  agano la kwanza ili kuimarisha la pili. 10Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.
  11Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi. 12Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu. 13Tangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake, 14kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.
  15Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema,
  16“Hili ndilo agano nitakalofanya nao
  baada ya siku hizo, asema Bwana.
  Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao,
  na kuziandika katika nia zao.”
  17Kisha aongeza kusema:
  “Dhambi zao na kutokutii kwao
  sitakumbuka tena.”
  18Basi haya yakiisha kusamehewa, hakuna tena dhabihu yo yote inayotolewa kwa ajili ya dhambi. Umeona Siyi, una la kusema hapo? Au uongezee na ile Lk 24:46-47 na ile Mdo. 10:43, kisha utuambie Jina hilo la Yesu huondoaondoaje dhambi, au utukufu wa jina hilo ulitokana na nini?

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 115. ,…zaidi ya yote, hili ninalolinukuu, lilikuwa ni jambo la ajabu sana kwenye hoja ya ndugu yangu lwembe. Ndio maana nilikwambia kwamba, wewe ukipewa wanafunzi ishiri wapumbavu ili uwahubirie injili, basi wanaweza wote wakaelekea kuzimu kama hawatayachambua vizuri hayo mafundisho yako ya kuzimu. Sina lengo la kukusema vibaya lakini ukiuona uongo wako, labda utaweza kunielewa kile ninachokishangaa kwako. Mimi sio mwalimu wala nabii, lakini huwa ninapenda kuusimamia ukweli kadiri niwezavyo. Tazama sasa nikunukuu ulivyokuwa unaniuliza swali la kuzimu lililojaa uongo mtupu! ” SASA UTAMUUNGAMIA NANI DHAMBI ZAKO HIZO, WAKATI HUYO MWENYE KUYAPOKEA MAUNGAMO YAKO AMEKWISHA ONDOKA KATIKA KITI HICHO YANAPOPOKELEWA MAUNGAMO HAYO?!!!!!…..Jamani nirudie tena kusema, hebu tuwe wa kweli. Hivi bwana yesu hatunae kabisa kwa sababu hata kwenye kile kiti chake cha rehema amekwisha ondoka kabisa? Amekwenda wapi tena? Inamaana sisi hatuna tena mwombezi wetu na kuhani wetu mbele za Mungu? Biblia si inasema kuwa yeye yuko patakatifu pa mungu akituombea na kutupatanisha na Baba akiwa ni kuhani wetu mkuu adumuye milele?, biblia si inasema hivi” BALI YEYE , KWA KUWA AKAA MILELE, ANAO UKUHANI WAKE USIOONDOKA. NAYE, KWA SABABU HII, AWEZA KUWAOKOA KABISA WAO WAMJIAO MUNGU KWA YEYE MAANA YU HAI SIKU ZOTE ILI AWAOMBEE!!!!. Soma(Waebrania 7:24-25) + (Warumi 8:34). Ukweli ndio huo, kristo ni mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ili kurudisha uhusiano wetu na Baba uliopotea. Bwana yesu anaitwa “kuhani mkuu wa Maungamo yetu”. Yeye tukikosea na kuwa tayari kutubu, huwasilisha maombezi yetu tunayoungama kwenye kwenye kile kiti cha enzi cha Baba. Na kwa sababu Mungu ni mwenye haki na upendo, hawezi kamwe kutukataa tena, ili tumrudie, haswa pale anapoiona haki ya mwanae na jinsi alivyojitoa kwa ajili yetu. Haijalishi ni dhambi kubwa au mbaya kiasi gani, ila anachokifuraia kwetu ni kutuona tunatubu kwa kweli na kumrudia yeye. Asante

 116. Wokovu wetu unahitaji vitu viwili muhimu sana, kumkiri kristo na kujinyenyekeza kwake, kwa njia ya imani pekee. Wala mimi sikatai, nikweli kabisa kwamba, Mkristo aliyeokoka na kuzaliwa kwa mara ya Pili, hawezi kutenda dhambi kwa makusudi, kwa kuwa yeye amefanywa mpya kwa roho, huku akiongozwa na sheria mpya ile ya uzima wa roho yenye uhuru, sio sheria ya dhambi na mauti. Lakini pamoja na hayo yote, ni Muhimu kufahamu kuwa huyu mkristo bado ni Mwanadamu kama wanadamu wengine, hata pengine kwa kuteleza kwake, yeye huweza kuwa na chuki au hasira wakatifulani maana yeye bado hajawa mkamilifu kabisa kwa 100%. Makosa hayo Pia ni dhambi ingawa tunaweza kuyaona kama ni makosa madogo madogo tu. Pasipo kutetea kwa udhehebu, ni lazima hata sisi wenyewe tunaojifanya kuwa tumeokoka, tena ni malaika ni lazima wakatifulani tunajikuta katika matatizo hayo au yafananayo na hayo, kwa kiasi hata ni kidogo sana cha kibinadamu, Soma(Mhubiri 7:20) , ndio maana pia, sio kwamba tayari tumekamilika kabisa ila twakaza mwendo huku tukisitiriwa na haki ya kristo (sio haki yetu), Soma( warumi 3:23-26). Ukweli ndio unaofaa kwa Mungu, sio unafki!!. Hata kama sio mimi ninaeteleza kidogo kiasi hicho kwa bahati mbaya, basi wako ndugu zangu ambao ijapokuwa waliokoka, lakini waliteleza hivyo, ufahamu huu, ndio niliokuwa nikiutetea na ndipo ukazaa lile swali ambalo ndugu lwembe amejifanya kama hakuliona. Swali lenyewe ni hili: je, kwa watu walioteleza katika huo wokovu wao na kutaka kutubu na kurudi kundini, nikweli hawana nafasi tena, kwa kuwa kutubu ni kwa wapagani peke yao, sio kwa ajili ya watu waliookoka maana hao hawawezi kutenda dhambi kwa hali yeyote ile kwa kuwa wao ni malaika, kama anavyotaka kutumaanisha ndugu lwembe?!. Huu ni uongo kabisa. Ukweli ni kwamba, likitokea lisilopaswa kutokea kwa mtu aliyeokoka na kumpokea kristo, bado atakuwa na nafasi ya kutubu na kurudi kundini, haijalishi kuwa ni mzee, kijana wala mtoto katika imani, sisi wote ni watoto wa Mungu katika imani, ni wamoja tunaozipeleka shida zetu na matatizo yetu kwa yuleyule mmoja. Ila tutakapo kosea na kumkataa kristo kabisa, huku tukimuacha kumtii roho wa Mungu na kuambatana na dunia hii kwa kuifuata vile iendavyo huku tumekuwa ni wasaliti wa wokovu wetu bila ya kutaka kutubu kwa kweli na kumrudia kristo, hapo ndipo kunakokuwa na kule kutarajia hukumu ya Mungu, maana hakutakuwa na dhabihu nyingine ya msamaha kwa kuwa tumemkanyaga mwana wa Mungu kimakusudi na kuifanya damu yake ya thamani ya agano kama kitu kisichofaa tena kwetu. Soma(ebrania 10:26-29). Kwa hiyo, mimi naona kuwa huo mtazamo wako ndugu lwembe ni potofu kwa sababu ni wa kujiinua kupita uhalisia wenyewe, na kwa njia hiyo, unaihubiri injili kwa mitazamo yako zaidi kuliko vile neno linavyomaanisha. Tazama, mara unasema kuwa kutubu ni kwa wapagani pekee wanaotaka kumpokea kristo, mara tena sijui kutubu ni kwa watoto wadogo waliokwisha mpokea kristo isipokuwa bado hawajakomaa kama wewe nk nk. Hebu jitahidi kuwa mkweli ndugu yangu, asante sana.

 117. Siyi,

  Unaweza kunithibitishia hili jambo kwenye maandiko tafadhali!?:

  ”Halikadhalika, damu ya Kristo, haiondoi dhambi zetu, bali inazifunika tu. Kwa maneno mengine, Kristo aliye hai, hutupumzisha dhambi zetu zooote tunazozitenda kwa mawazo/fikra/akili na matendo na sisi kujiona kama tumesamehewa, na kimsingi ndivyo ilivyo. Lakini ikumbukwe kwamba, Yesu hana bega la kubeba dhambi za Siyi na wengine miaka yooote. Na wala hana sehemu pa kuhifadhia dhambi za watu miaka yooote, pamoja na kwamba kwa sasa zigo la dhambi huwekwa patakatifu pa patakatifu pa mbinguni kusubiri mbuzi mwingine wa Azazeli (ibilisi) ili kuja kutwishwa zigo hilo siku ya mwisho na kuunguzwa nalo kwa moto!!”

  1. Wapi umepata maneno haya kamba damu ya Kristo haiondoi dhambi zetu bali inafunika tu?
  1a. Nini tofauti ya kuondoa na kufunika katika haya maudhui?
  2. Unaposema kuwa Yesu hana mabega ya kubeba dhambi zetu miaka yooote, una maana gani, na umelipata wapi jambo hilo?
  3. Ni andiko gani linakupa kujua kuwa zigo la dhambi huwekwa patakatifu pa patakatifu?

  Thank u!

 118. ……………………………………………
  Mhina,
  Mtazame swaiba wako Siyi anavyojikoroga kuhusu kauli yangu ya ‘Kutokutenda dhambi’ inayotokana na Maandiko hapo nilipoyanukuu, “Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi” (1Yn 3:5-6). Kisha nikasema, “”Huu ndio ukweli wa Injili kwa mkristo anayekua kiroho!””; Jibu lake kwa kauli hiyo ndio hili hapa:
  “””“ Huu ni ufedhuli mkubwa sasa!! Sasa tunapokuwa ndani ya Kristo ndiyo sheria inaondoka kwa vile hatutendi dhambi?? Leo kama wewe hauibi, je sheria ya nchi dhidi ya wizi imeondolewa kwako?? Na kama ni kweli, nenda kaibe sasa maana uko huru kuiba tu!!

  Yale maroho ya dini yanamleta mpaka Mlangoni, kisha yanamuacha mwenyewe akatae kuingia ili siku ya Hukumu yakae pembeni yakimcheka kwa upumbavu wake, kwamba Mlango aliuona lakini hakuingia! Msikilize hiki anachokisema, “”Sasa tunapokuwa ndani ya Kristo ndiyo sheria inaondoka kwa vile hatutendi dhambi??”” Jibu ni NDIYO! Hata ukiziondoa hizo alama zake za kuuliza, anakuwa yuko sahihi, kwamba anauliza jambo analoliona kuwa ni sahihi kiMaandiko, ila kwa jeuri ya yale maroho ndio anabeza! Anaendelea, “”Leo kama wewe hauibi, je sheria ya nchi dhidi ya wizi imeondolewa kwako??”” Jibu ni NDIYO! Mimi si mwizi basi Sheria ya wezi itanihusu nini? Mimi niko juu ya Sheria hiyo hainihusu! Angalia anavyomalizia kwa mkorogo akiwa ameyajua majibu yangu hayo ya NDIO, “”Na kama ni kweli, nenda kaibe sasa maana uko huru kuiba tu!!”” Jamani mtu ambaye HATENDI dhambi kwa asili yake, utamwambiaje aende akaibe, huyo ambaye si mwizi? Lazima uwe umechanganyikiwa, na hili huwapata watu ambao hufika ktk Mlango wa Kweli, wakajizubaisha kuingia kwa kuwauliza wakufunzi wao, ndipo Mlango hutoweka mbele yao!!!!

  Kama ilivyokuwa kwa Israeli walipojizubaisha kuingia Kaanani, maana yake ni kwamba hawakuliamini Neno la Mungu lililoshuhudiwa na akina Joshua na Kaleb kwamba ni kweli alilolisema Mungu litatimia kama mnavyoyaona haya mazao tuliyoyatoa huko yalivyo halisi!

  Lakini wao kwa jinsi walivyoizoelea dhambi inayowapa na nafasi ya kutubu, nayo kuwa ni sehemu ya maisha yao, wakakataa kulipokea Neno la Mungu linalowapa ushindi juu ya dhambi, wakasema Dhambi ina nguvu sana, sisi ni kama panzi mbele yake!!

  Mungu hukupatia sawasawa na unachokikiri, kuanzia hapo wakawa panzi, kutoka kuwa tai! Wakazunguka jangwani miaka arobaini wakafia humo wote waliokataa; kwani panzi ana uwezo wa kuruka umbali gani, hawana mbawa za kuwarusha huko juu hata walipokee Neno la kinabii, wao wanaruka huku chini umbali wa mafundisho ya makanisa yao tu, ndio hiyo mana wanayodondoshewa kutoka mbinguni hiyo inayowapa kuishi hiyo miaka arobaini huko jangwani kusiko na Ufufuo! Wao ni Zambi, zambi, zambi… mwanzo mwisho!!!

  Neno la Mungu linakupandisha huku juu alipo, huku ambako huwezi kutenda dhambi, wewe unaniambia, unanibembeleza eti nijishushe huko shimoni mliko nije nijifunze jinsi ya kutenda dhambi na kuungama; huo kama si upumbavu ni nini? Unajua afadhali ya mjinga anaweza kuelimika ili akiuzoelea ujinga basi ujinga huo humuingiza ktk Upumbavu amabao haunaga dawa! Hebu jifikirie, badala ya kukazana uifikie hiyo nchi ya wasio tenda dhambi wewe umekazana kujibakisha ktk nchi ya watenda dhambi na kuungama; sasa utamuungamia nani dhambi zako hizo wakati huyo Mwenye kuyapokea maungamo yako amekwisha kuondoka ktk kiti hicho yanapopokelewa maungamo hayo? Haujasoma kwamba kwa waliovionja vipawa, wakirudi nyuma wakaendelea na uzinzi wa kiroho, hizo ibada za sanamu mnazoendelea nazo zinazowakatalisha kulipokea Neno la Mungu, si mmeambiwa kuwa hakuna tena dhabihu juu yenu isipokuwa Hukumu!!! Ukikataa kwenda mbele Kiti cha Rehema kinaondoka, moyoni mwako, maana hicho Kiti ndilo hilo Neno unalolikataa!!!

  Tafakari, chukua Hatua ndg yangu, mambo ya Mungu yanataka utii kwanza ndipo utukuzwe!

  Gbu!!

 119. Mhina,

  Mengi ya maelezo yako mengine ktk post yako ya mwisho, kama ningeyatafakari kidogo, nisingekuuliza hata hilo swali nililokuuliza; maana kusema kweli yanaonesha kwamba wewe na Siyi hamko hata ktk makundi hayo, maana hayo makundi ni endelevu ktk kuukulia wokovu wakati ninyi mmedumaa!!!

  Ili kulibaini kundi lenu hilo ndiyo nikawatafuta ktk Maandiko, maana nafahamu hakuna kitu kipya duniani bali vyote vimo ktk Maandiko. Huko nikawakuta Israeli, hao waliotolewa Misri, ambao ktk ulinganisha na Kanisa, ndio hao watoto wadogo ktk imani unaowasoma ktk 1Yn 2:1-2 uliyoinukuu, huo ujumbe kwa watu wote kama ulivyosema, ambayo ndio msingi wa wewe kuyakataa Maandiko yanayokusogeza mbele yakikuondoa ktk Sheria hapo unapokamilishwa na kuwa mungu!

  Israeli walipotolewa Misri walikuwa ni watoto wadogo ktk imani. Huko jangwani ndiko walikoingizwa ktk ujana. Wakapewa Sheria huko, na Mungu akajifunua kwao kwa kiwango kikubwa sana ktk kuwapigania vita, kuwaponya magonjwa yao, kuwalisha na mambo mengine mengi sana. Hao ni sawa na Kanisa lililopewa moyo mpya wa nyama, kisha likapewa roho mpya, likivionja vipawa vya kimbinguni kwa kuingizwa ktk mabadiliko hayo kutoka ktk hali ya upagani, watu wasio na Mungu; na sasa wanapotakiwa kuvuka kuingia Utukufuni, huko Rohoni aliko Mungu, wanagoma; wanasema Dhambi haishindiki, huwezi kuenenda kwa Roho tu bila kutenda Dhambi, hayo ni mafundisho ya mashetani, wanajipa nguvu kwa kutafutiza Maandiko wanayoyalazimisha yauvuke wakati wake!

  Mhu 7:20 wanayoivusha kwa hila kuja huku iliko Neema inazungumzia hali ya mwanadamu kabla ya ujio wa Kristo, “Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi” haya ndiyo haya hapa yanayorejewa na Roho huyo huyo aliyeyaandika hayo huko nyuma na sasa akiyahuisha ili kuyaleta ktk ukomo, Rum 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi” basi mbele kidogo anatuonesha jambo hilo linapokomea, “17Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.” Mnaona mnavyojirudisha huko kwenye Sheria???

  ……………………………………..

 120. @ Mhina
  Kwanza, nakushukuru kwa majibu yako. Kimsingi, umejibu maswali yangu. Lililobaki ni mimi kukupatia sifuri au 1, 2, 3, ..100%. Nipende kutoa muhtasari wa majibu ili na wewe uone kama ulipatia ama la. Ninavyofahamu mimi, kuishi kwa kuufuata mwili, ni kuishi kwa kuyatafakari maovu, jambo ambalo matokeo yake huonekana kwa matendo –matendo maovu! Kuishi kiroho, ni kuishi kwa kuyatafakari mambo ya Mungu, jambo ambalo matokeo yake ni kutoonekana ukitenda ovu lolote!! Kwa ufupi, dhambi huanzia akilini/mawazoni/moyoni hata kabla haijaonekana ikitendwa!! Ikiwa hukohuko mawazoni/akilini/moyoni, Mungu huihesabu kama ni dhambi tayari, hata kama utaahirisha kuitenda!! Usipoitubu, itakupeleka motoni tu!!
  Pili, Kuenenda katika roho, ni kuishi kwa kuyatafakari mambo ya Mungu, Neno la Mungu na kuhakikisha kuwa, yale Mungu aliyoyaagiza yafanyike katika ibada, maisha, n.k., yanatendeka kama alivyoagiza. Ukitenda kinyume, utaangamia tu maana ibada yako ni bure mbele za Mungu. Si kila mtu anayemwabudu Mungu bure, huwa anajua kuwa ibada yake ni bure!! Wengine wanajua, ila wengine (tena walio wengi zaidi), huwa huwajui!! Tangu mwanzo historia inaonesha hivyo. Wakati wa maangamizi ulipowadia, Mungu aliwaangamiza tu bila kujali sincerity yao ya ibada ya bure!! Kwa hiyo unapaswa kuwa makini/kuwa rohoni zaidi unaposikiliza, au kusoma neno la Mungu na kuangalia kama yanayonenwa au unayoyasikia ndivyo yalivyo, na siyo kuruhusu misisimko tu ikutawale!! Huko ndiko kuwa rohoni, -kuruhusu akili/fikra/moyo(roho) zikuongoze kumjua Mungu na si misisimko/hisia (mwili).
  Jitahidi kujua kama hayo unayoyaamini, ni ya kiroho zaidi au ni kihisia zaidi!! Watu wengi huwa katika hisia za mwili, wakijidanganya kuwa eti wako rohoni!! Cha kuchekesha zaidi, utawaona waimbaji, wahubiri n.k., inafikia saa wanatoa machozi!!! Machozi kabisa!!! Ukimwuliza kwa nini unalia?? Atakwambia ana roho mtakatifu, kumbe ni hisia tu!! Ni ufedhuli uliopindukia!! Shetani tangu bustanini, dili lake kubwa, limekuwa ni kucheza na mioyo/akili/fikira na mawazo yetu tu!!! Haendi nje ya hapo!! Kwa hiyo, ndugu yangu Mhina, unapouaga mjadala huu, tambua kuwa, idadi kubwa ya watu, huendeshwa na hisia katika mambo ya kiimani, wakidhani ni RM wa Mungu, kumbe sivyo. Wamedanganyikaje???!!! Ni mada ndefu!! Bwana akuongoze kujitathimini wewe binafsi kwanza!! Mbingu si mchezo kaka!! Kazana aise!!
  Siyi

  @ Lwembe
  Kwanza, unaonekana una safari ndefu sana ya kwenda rafiki yangu. Ndefu sana. Ila huwa hutaki kuamini umbali mrefu wa safari yako uliyo nayo!! Hutaki kabisa!!! Mtu mwenye uelewa wa neno la Mungu, hawezi kusema haya huku akicheka kifedhuli. Ona ““Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Hahahaha…, nilidhani na UTII wa Sheria au Injili nao ni tunda la roho!!!! “”
  Kama unashangaa kutoliona neno UTII, ujue kuwa una macho ila huoni!! Neno utii lipo kwenye kwenye hiyo nukuu yako, tena ni la kwanza – pendo ndilo utimilifu wa sheria!!! Huwezi kuuzungumzia UPENDO, halafu UTII ukauweka pembeni, utakuwa unaumwa sana!! Sasa halipo kivipi!!?? Unaona unavyodanganyika wewe?? Rafiki, kuna pacha wawili tu wa kitu kinachoitwa UPENDO (yyani utmilifu wa SHERIA), nao ni – UTII (unaoleta uzima), na UASI (unaoleta mauti). Hakuna zaidi ya hivi vitu viwili!! Chagua kimojawapo!!
  Pili, umesema kuwa, “Chukua Biblia yako kisha tafuta mahali panapofundisha kwamba ONDOLEO la Dhambi linapatikana kwa kafara za wanyama; HAKUNA!!! Hakuna aliyewahi kuondolewa dhambi zake kwa kafara za wanyama ktk Biblia; Ondoleo la Dhambi limeanza kupatikana ktk Ubatizo wa Yohana kwa mara ya kwanza, na sasa linapatikana kupitia Ubatizo wa Jina la Bwana Yesu Kristo, Mdo 2:38!!!”
  Kuna kitu hujakiona hapa. Sikia, kaka!! Ni kweli kabisa damu za wanyama hazikuondoa dhambi. Zilifunika tu. Hata Damu ya Yesu mwenye, haiondoi dhambi, bali inafunika tu!! Huuuh!!! Usinishangae!! Sikiliza ndugu yangu!! Ukisoma historia ya utoaji wa kafara za wanyama, kulikuwa na siku moja maalumu kwa mwaka, ambayo ulipatanisho wa taifa/nchi nzima ulifanyika. Swali kwa nini ufanyike ilhali kila siku watu walienda kutubu dhambi hekaluni kwa makuhani?? Soma Biblia yako utapata majawabu tosha. Kwa ufupi tu nidokeze kuwa, siku kuu hiyo ya upatanisho, mbuzi wawili walipelekwa kwa ajili ya shughuli hiyo ya upatanisho. Mmoja alichinjwa kwa ajili ya toba ya dhambi za taifa zima. Na mwingine alibebeshwa dhambi zooooooote zilizotubiwa na taifa zima kwa muda wa mwaka mzima kichwani mwake, na kisha kupelekwa na kutelekezwa porini asirudi tena maana aliliwa na wanyama wakali -alikufa!! Habari hizi unaweza kuzipata kwenye Biblia tu, – Soma.
  Halikadhalika, damu ya Kristo, haiondoi dhambi zetu, bali inazifunika tu. Kwa maneno mengine, Kristo aliye hai, hutupumzisha dhambi zetu zooote tunazozitenda kwa mawazo/fikra/akili na matendo na sisi kujiona kama tumesamehewa, na kimsingi ndivyo ilivyo. Lakini ikumbukwe kwamba, Yesu hana bega la kubeba dhambi za Siyi na wengine miaka yooote. Na wala hana sehemu pa kuhifadhia dhambi za watu miaka yooote, pamoja na kwamba kwa sasa zigo la dhambi huwekwa patakatifu pa patakatifu pa mbinguni kusubiri mbuzi mwingine wa Azazeli (ibilisi) ili kuja kutwishwa zigo hilo siku ya mwisho na kuunguzwa nalo kwa moto!! Kwa hiyo dhambi tunazotubu kila siku, huwa hazifutwi na badala yake, huhamishiwa sehemu nyingine kumsubiri mhusika(mbuzi wa Azazeli –Ibilisi) kubebeshwa zigo lake siku ya hukumu. Ndiyo maana kama hujui, kwa nini Ibilisi anapambana ili aje afe na wengi?? Sababu kuu iko moja tu!! Anaufahamu uzito wa furushi lenyewe la dhambi za wanadamu, hivyo akicheza watu wakamjua Mungu sawasawa, ataachiwa zigo lote la watakatifu hao na hivyo kumfanya apate maumivu mengi zaidi ya kuunguzwa na moto siku ya mwisho. Ili aepuke hilo, anafanya kila njia kuhakikisha kuwa anamkamata Lwembe na wengine ili wampunguzie zigo maana wakibeba mizigo yao wenyewe, yeye (ibilisi) hatakuwa na mzigo mkubwa, na hivyo hataungua kwa maumivu makali sana japo atakaufa tu!!
  Kwa hiyo ndugu yangu Lwembe, kile kilichotendeka katika Agano la Kale, kilikuwa ni kivuli tu cha kile kitakachotendeka siku ya mwisho. Kazi ya damu za mafahari na ile ya Kristo, mimi huwa naiona bado ni ileile, tofauti ni kwamba, zile za mafahari, zilimwagika kila siku hekaluni (na kwa wenye uwezo) lakini hii ya Kristo, imemwagika mara moja tu kwa ajili ya wote – matajiri na masikini!! Mambo yako bayana kiasi hicho. Ila kwa wavivu wa kusoma Biblia, haya yooote watayaona ni mambo mageni, mapya, na pengine wasiyatilie maanani!! Kazi kwao, mimi nimemaliza!!
  Tatu, nakunukuu tena, umesema, “Niliwaambieni kwamba Andiko ktk 1Yn 1:8-10 linalosema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu, tukiziungama dhambi, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba, hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu”, nikasema hii ni Injili anayohubiriwa mpagani, hii ndio Injili inayomuongoza mpagani kuziungama dhambi zake na kubatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili apate Ondoleo la Dhambi zake; akiisha kuifikia hatua hiyo Andiko hili HALINA tena kazi kwake, haliwezi kumshitaki kwani amelitimiza hilo!!! Au nyie huwaga mnabatizwa ktk kila ibada, mkiisha kuhubiriwa Injili kanisani kwenu mnabatizwa kulingana na Mk 16:15-16, kwamba kila mkitubu dhambi mnabatizwa??? Yaani hamkui wala kuongezeka ktk kimo, kila siku mko darasa la kwanza?”
  Hili nalo bado ni shida kwako ndugu yangu. Hakuna neno la Mungu lililopitwa na wakati kwa yeyote ama aliye ndani ya kanisa au la!! Hakuna!! Maisha ya uongofu ni kujiona unazidi kupungua kila siku kadri unavyozidi kumsogelea/kumkaribia Kristo. Kwa mtu anayekua kiroho, hakuna hata siku moja atajiona kuwa amekua sasa!! Hakuna. Kadri unavyomsogelea Mungu, ndivyo unavyozidi kutambua madhaifu yako mengine na kuomba msaada wake wa kuyashinda!! Kila siku, mkristo yuko safarini kuelekea ushindi!! Kila siku tunakua!! Kwa wewe binafsi, huwa ni ngumu sana kujitambua kuwa umekua, ila watu wengine, wataona maisha yako na wala wewe hutajua kuwa umeshakua, ni mpaka Mungu akwambie!! Mbingu siyo lelemama, kazana bro!!
  Neema ya Bwana iukfunike
  Siyi

 121. Mhina,

  Nipo ndg yangu, sekta ya “Jua kali” hainaga likizo! Sema wkt mwingine nafasi inaruhusu kusoma tu! Nilipokuona unaaga ndio nikaamua nikuandikie, ili usije ukaondoka umeshikilia mambo yanayozidi kukudumaza, hata usiukulie wokovu!!

  Tazama ile roho ya dini ilivyokuzuia kuupata ujumbe kamili wa vifungu ulivyovinukuu, imekufanya uvikariri vifungu hivyo ktk ujumla usiokusudiwa, wakati ujumbe huo uko specific kwa makundi specific!

  Labda tukianzia hapa tunaweza kufika mahali tukaelewana:
  Kundi la kwanza ni la watoto wadogo, hao waliozaliwa kwa Injili, hao walioipokea Injili na wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo, wakaondolewa Dhambi zao; hao waliookoka, hao waliohesabiwa Haki kwa imani na sasa wanaketishwa chini kulishwa Neno la Mungu. Hawa ktk uchanga wao wanaweza kutenda dhambi, ujumbe wao ndio huu hapa:
  1Yn 2:1 “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.”

  Kundi la pili ni la Vijana, hao wenye nguvu. mtoto anayelishwa chakula chenye lishe nzuri huwa ni mwenye afya na nguvu, ndio haoa waliolishwa Neno la Mungu lisilogoshiwa, linajaa ndani yao likiuondoa uchafu na udhaifu wote na tamaa za dunia. Hilo humuongeza ktk kimo yule mkristo aliyezaliwa mara ya pili kwa Neno aliloliamini, likimbadilisha ktk kila hatua ya maisha yake, likimsogeza ktk kumfananinia Kristo, huyo ambaye ni Neno, na hivyo kwa kadiri hilo Neno linavyoongezeka ndani yake, dunia na mambo yake hutupwa huko nje, huyo huyawazia yaliyo juu, moyo wake huyapenda hayo, dunia na mambo yake hugeuka takataka, tena sumu! Ujumbe unaolihusu kundi hili ndio huu hapa:
  1Yn 2:14 “”…Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”
  Hili ndilo kundi la wale watoto wadogo walioongezeka ktk kimo kufikia kuwa vijana (morani!), ndio hao waliotakaswa!

  Vijana wakiisha kumshinda yule mwovu kwa Neno, ndipo huvishwa taji, hutukuzwa; ndiko kule kujazwa RM, huko kuzaliwa kwa Roho “1Yn 5:18 “Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.” hawa ndio akina baba, ujumbe wao ndio huu:
  2:14 “Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo…”
  Hawa wanamjua Mungu, yeyote mwenye kumjua Mungu HAWEZI kutenda dhambi, kwa sababu amezaliwa na Mungu!

  Basi kufikia hapa, kabla hatujaendelea, napenda nikuulize swali moja:
  Ktk haya makundi matatu, wewe uko kundi lipi?

  Gbu

 122. Lwembe, nimalizie kwa kusema kwamba: ” Sisi bado hatujawa watakatifu kabisa, isipokuwa tunaendelea kufanywa watakatifu siku hadi siku. Baba yetu ndiye anayetupa uwezo wa kuwa watakatifu kwa njia ya ile asili mpya na kutuongoza siku hadi siku kadiri ya shauku yetu ya kufanya ushirikiano na yeye katika kutii kwetu neno lake. Kwa hiyo, hatutakiwi kujiinua sana wala kulegea bali biblia inasema ” ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini ule utu wetu wa ndani ” UNAFANYWA UPYA SIKU HADI SIKU”. Soma(2 Wakorintho 4:16). Swali: Je, ni ushirikiano upi huo wa kiimani tunaotakiwa tuuonyeshe kwa Baba?, Ona, nikweli kabisa kwamba tumeokolewa kwa imani pekee, lakini sisi ni watoto wa Mungu ambao bado tunaishi hapa duniani. Dunia hii bado inachangamoto zake nyingi mno!, na kama nilivyosema huko juu kwamba, sisi sio kama malaika bali sisi ni wanadamu, ndio maana bado tumebakizwa na asili yetu ya “MWILI”. Dunia hii ambayo tunaishi, inatujaribu tusipendane, tuwe na chuki baina yetu, tutamani, tusiwe waaminifu nk. Naye Mungu ametuachia changamoto hizo zote zitupate kwa sababu, imani ya kweli inaweza kupimwa wakati kunauwezekano wa kutopendana, chuki, tamaa nk. Sasa, Yule tunaemtumikia na kumtii, hutoa njia ambayo ijapokuwa inamajaribu mengi na maumivu hata ya kimwili wakatifulani, lakini pia imani yetu huthibitika kwa njia hiyo kuwa ni ya kweli siku hadi siku mpaka kufikia utimilifu wake. Huu wote ni wajibu wetu sisi tuliookoka, sio kila kitu tusingizie kuenenda kwa roho, hapana!. Mungu alitaka kwa njia hiyo, tuwe ni washindanaji wa huo utakatifu wake kupitia hiyo imani yetu, yaani kwa njia ya imani yetu, tuthibitike katika haki yake, ndio maana biblia inasema hivi” NA MUNGU WA NEEMA YOTE, ALIYEWATIA KUINGIA KATIKA UTUKUFU WAKE WA MILELE KATIKA KRISTO, MKIISHA KUTESWA KWA MUDA KIDOGO , YEYE MWENYEWE ATAWATENGENEZEA, NA KUWATHIBITISHA NA KUWATIA NGUVU. Soma( 1Petro 5:10) + (1Petro1:6-7) + (2 Wakorintho 4:17). Nimalizie kwa kusema kwamba, hakuna haki isiyo na wajibu kabisa!!. Kama haki ya kisheria na zile amri zake zilikuwa na wajibu wake wa hukumu,basi hata neema ya Mungu na wokovu wake una wajibu wa utiifu na uvumilivu kwa yote.

 123. YaYayaaaa!!. Ndugu lwembe, hivi ulikwenda likizo?, ndio maana mimi niliaga na kuondoka, sioni sababu ya msingi ya kurudi tena kuchangia mawazo yangu, lakini kwa sababu mtazamo wako umenilenga na mimi, basi nimeona ni bora nijinasue kutoka kwenye huo uongo wako uliouandika. Sasa, ukiisoma biblia, ni vizuri kuielewa vile ilivyotaka kumaanisha kwa ujumla wake. Tazama ukisoma ile (1Yohana 2:1-2), utaona inasema hivi” Na kama mtu akitenda dhambi, tunaye mwokozi kwa Baba, Yesu kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu (yaani sisi tuliyeokoka), wala si kwa dhambi zetu tu(sisi tuliookoka)…… Bali na kwa dhambi za ulimwengu wote(na hao wapagani pia wanaotaka kumpokea yesu). Yohana aliandika waraka huu kwa watu wote ulimwenguni, ndio maana alitenganisha kati ya watoto wa Mungu na watu wa mataifa ulimwenguni kote. Tazama, Yule aliyesema kwamba akitenda dhambi, anaye mwokozi kwa Baba, ambaye ni yesu kristo mkombozi wake, kamwe hawezi kuwa ni mpagani, bali huyu ni mtoto wa Mungu ambaye tayari alishaokoka, lakini baada ya kuteleza bahati mbaya na kumkosea Mungu wake, ndipo akaamua kutubu kwa njia ya kristo ili arudi kundini. Kukosea kwa bahati mbaya na kutokwenda sawa sawa na mapenzi ya Mungu hutokeaga wakatifulani kutokana na udhaifu wetu wa kibinadamu, ndio maana nilinukuu andiko la (Mhubiri 7:20), linaloweka wazi kabisa kwamba “bila shaka hakuna mwanadamu hapa duniani ambaye afanya mema asifanye mabaya. Sisi kama alivyosema mtume Paulo kwamba” hatujawa wakamilifu kabisa, isipokuwa tunashika lile la kristo, twakaza mwendo ili tukubalike na Mungu, sawasawa na neema yake. Sisi wala Mtu yeyote hawezi akawa juu au sawa na kristo, ndio maana pia bado tunaitwa “WANAFUNZI WA KRISTO”. Ndugu yangu lwembe, tatizo lake ni kutaka kujiinua zaidi ya hata yale maandiko ya biblia na kujifananisha na malaika, jambo ambalo sio vile biblia inavyotaka tujiinue ila inataka tujishushe na kumpandisha kristo pekee. Labda ndugu lwembe nikuulize hivi” wewe ni mwanadamu unayemkosea Mungu wakatifulani hata kwa bahati mbaya au kwa kutokujua kwako, sasa unatubu kwa njia gani, na wakati wewe unasema kwamba, huwezi kufanya dhambi ila njia ya kutubu ni ya wapagani na watu wanaotaka kumpokea yesu pekee? Wewe unarudi vipi tena katika huo utakatifu wako baada ya kumkosea Mungu, hata kwa kosa dogo tu?!!, hebu kaka unisaidie vizuri hapo ili na mimi nikuelewe. Pia ukaendelea tena kuwadanganya watu, eti kuzini, kuiba, na kuua sio dhambi bali hayo ni matunda ya dhambi. Hivi kunatofauti gani kati ya dhambi na matunda yake yasiyo haki?!!, Biblia si inasema kwamba” kila lisilo haki ni dhambi?, kuiba, kuua, kuzini, haya si ni matendo yasiyo haki ambayo kibiblia ni dhambi?, iweje wewe unayejiita, mchungaji, mtume, mwalimu, nabii, malaika nk, usijue hata maana ya dhambi na matendo ambayo ni dhambi?!!!!……Yaani ndugu lwembe wewe, ukipewa wanafunzi ishirini wapumbavu ili uwahubirie neno la Mungu, utawapeleka wote kuzimu kwa sababu ya upumbavu wao wa kutoyatafakari yale yote unayowafundisha. Hivyo ndugu yangu, kuzini, kuiba, kuua, yote hayo ni dhambi kabisa, kwa sababu, hayo yote ni matendo yasiyo haki kabisa kabisa. Usiikariri biblia ila jaribu kuielewa ndugu yangu. Mimi sio mchungaji wala mwalimu, lakini nawashangaa ninyi waalimu wa siku hizi mnatuangusha sana!, na tatizo lenu kubwa ni kupenda kujiinua na kuwa wakubwa msiokosea, jambo ambalo si tabia ya kibiblia. Unatakiwa ujishushe wakatifulani ili ujifunze mengine kutoka kwa wengine. Asante.

 124. …………..
  Mhina, Siyi & Mjema,

  Niliwaambieni kwamba Andiko ktk 1Yn 1:8-10 linalosema, “Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu, tukiziungama dhambi, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba, hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu”, nikasema hii ni Injili anayohubiriwa mpagani, hii ndio Injili inayomuongoza mpagani kuziungama dhambi zake na kubatizwa kwa Jina la Bwana Yesu Kristo ili apate Ondoleo la Dhambi zake; akiisha kuifikia hatua hiyo Andiko hili HALINA tena kazi kwake, haliwezi kumshitaki kwani amelitimiza hilo!!! Au nyie huwaga mnabatizwa ktk kila ibada, mkiisha kuhubiriwa Injili kanisani kwenu mnabatizwa kulingana na Mk 16:15-16, kwamba kila mkitubu dhambi mnabatizwa??? Yaani hamkui wala kuongezeka ktk kimo, kila siku mko darasa la kwanza?

  Kwahiyo kukiri kwenu kutenda dhambi ni dalili ya kwamba kuna jambo la msingi mmelikataa, ndio huo ushuhuda wenu wa kugubikwa na Dhambi! Hakuna mafundisho ya dini yanayoweza kuliondoa Shina la Dhambi ktk mioyo yetu, ndio maana kwenu ni rahisi kukiri kutenda Dhambi kuliko Utakatifu, kwa sababu Dhambi haijaondolewa mioyoni mwenu! Uongo wa dini kama huu wa Siyi, unakushusha zaidi huko Shimoni kuliko kukupandisha: “””…Mwanzo 3:21. Huu ulikuwa ni utaratibu wa kuchinja wanyama wa kafara alioanzisha Mungu kwa Adamu na mkewe na vizazi vyao vyote. Utaratibu huo, tunauona unaendelea hadi kwa waisrael wakiwa na Musa jangwani, mpaka enzi za Kristo kabla hajabambwa msalabani. Uchinjaji huu wa kondoo, mbuzi, ng’ombe nk kwa ajili ya kufunika/kuondoa dhambi, ulikuwa ni kielezo cha kafara ya Kristo pale kalvarii!!Na haya siyo mawazo yangu ndugu yangu, ni maneno ya Mungu mwenyewe.””” Unaona! Ni maelezo mazuri yaliyoambatana na nukuu za Maandiko, lakini ni UONGO mtupu unaokuua kiroho ukiupokea!

  Kama unaweza ukaaminishwa kwamba “” Uchinjaji huu wa kondoo, mbuzi, ng’ombe nk kwa ajili ya kufunika/kuondoa dhambi,”” ni dhahiri kabisa kwamba hutaelewa chochote kuhusu Utakatifu, na hivyo kujibakiza ktk Uchafu wa dini, na Mungu huwa hakai pachafu! Chukua Biblia yako kisha tafuta mahali panapofundisha kwamba ONDOLEO la Dhambi linapatikana kwa kafara za wanyama; HAKUNA!!! Hakuna aliyewahi kuondolewa dhambi zake kwa kafara za wanyama ktk Biblia; Ondoleo la Dhambi limeanza kupatikana ktk Ubatizo wa Yohana kwa mara ya kwanza, na sasa linapatikana kupitia Ubatizo wa Jina la Bwana Yesu Kristo, Mdo 2:38!!!

  Pia naona dini imewaondolea kabisa ufahamu, naona kila mnapokutana na neno Amri au Sheria, akili yenu imepindishiwa kuelekea Amri Kumi! Bali Neno la Mungu lote ni SHERIA na AMRI!!! Mungu alipotamka kuwepo kwa jua, basi hilo tamko ndilo Sheria inayolitawala jua kuwa kama tunavyoliona, kila siku huchomoza na kuzama hakuna hata siku moja lilipofeli!!!

  Kwahiyo neno likisema hatutendi dhambi, hilo ndio sheria inayo kuongoza kutokutenda dhambi kwetu, hakuna nguvu wala mamlaka inayoweza kulizuia hilo! Neno linaposema, “Tubuni mkabatizwe kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi…”, hili ndilo Amri na Sheria ya Wokovu; likisema, “Mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria” basi twafahamu kwamba kwa Neno hilo, hao wanaoongozwa kwa Roho wameumbwa tayari kulidhihirisha Neno hilo, ninyi mkisema huo ni ufedhuli au kwamba, “”” Inaonekana wewe, unaongozwa na majini/mashetani, maana hayo, hayana sheria wala kanuni, madude hayo ni kwa roho tuuuu kama wewe!!”” Ni heri muwe mmeyasema hayo ktk Ujinga wa dini!!! ” Na matunda ya hao wanaoongozwa kwa Roho ndio haya: “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Hahahaha…, nilidhani na UTII wa Sheria au Injili nao ni tunda la roho!!!!

  Kuzini, kuua, chuki, uongo, nk haya si Dhambi bali ni matunda ya Dhambi; Dhambi ni Kutokuliamini Neno la Mungu!!! YN. ‭8‬:‭24‬ ” … msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu. Basi unapokosa kuliamini Neno la Mungu, hata neno moja tu, kama ilivyokuwa kwa Hawa, ndipo dhambi iliyopiga kambi hapo mlangoni pa moyo wako hupata fursa ya kuingia ndani na kujiimarisha! Inajiimarisha kwa kukuingiza ktk mafundisho mazuri yenye mfano wa utauwa lakini yakilikana neno la Mungu

  Mnasema sisi ni uzao wa ibrahim! Lakini Ibrahim alimwamini Mungu ninyi mnayaamini zaidi mafundisho yenu, hayo mchanganyiko kuliko Neno la Mungu! Wayahudi walisema wao ni uzao wa Ibrahim na wakamkataa Masihi wao wakiyashikilia mafundisho yao; ndio hao waliokufa ktk dhambi zao kwa kutokuamini kwao, kama ambavyo nanyi mtakufa ktk dhambi zenu kwa kutokuamini kwenu!!! Kulitilia shaka neno la Mungu hukuondoa ktk Njia Yake.

  Neno linapoagiza chochote kile, usiingize akili yako, inuka ulifuate, litakugeuza likuumbe upya, uwe kiumbe kipya, upewe asili mpya ya kimbinguni, uyafurahie na maisha yasiyo na kumbukumbu la dhambi!! Kwa maana hakuna mwenye kudumu ktk kumbukumbu la dhambi, yaani huyo aliye ktk sheria, awezaye kuyafurahia maisha ya wokovu. Hata hiiyo amri mpya wanayopewa, hakuna asiyejazwa RM anayeweza kuitimiza, huo ndio upya wake, vinginevyo jambo hilo liko ktk Torati, huko ambako liliongozwa kwa hukumu!

  Upendo wangu haujajengeka juu ya hiyo Sheria, ninachokifahamu mimi hiyo Sheria ndiyo challenge ya maisha yako ya kikristo ktk hatua hiyo uliyomo ndio maana unajitahidi ktk jambo hilo, hilo ni jema sana, hata wanafiki wanafanya kama wewe; bali ukweli ni kwamba Mungu ndiye Upendo, ndiposa huwezi kuudhihirisha upendo huo bila ya kuzaliwa kwa Roho! Sharti Yeye aliye Upendo ajidhihirishe mwenyewe anapokikalia kiti cha udereva ktk maisha yako, nawe kuwa chombo cha udhihirisho huo, hapo unapojiachilia mikononi mwake!

  Basi kama unazungumzia Utii, basi Yeye akiwamo ndani yako, ndiye ambaye huitikia “Amina” kwa kila neno aliloliandika ktk Biblia, maana hilo ni neno lake asingeweza kusema kwamba ah hilo haliwezekani, na ufedhuli mwingineo wa dini!!!

  Gbu!

 125. Mhina, Siyi & Mjema (kama kajificha, Siyi utampa ujumbe!),

  Nawaona mngali mnalizunguka Neno la Mungu la wakati, mkishindwa kabisa kulifikia au kuingia humo, ‘mkijifunza siku zote, ila msiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli’!!!

  Niliwaambia mjihadhari sana na maroho ya dini (Yane na Yambre); nikawaambia, hayo maroho ni majasiri sana, ndiyo yaliyomsulubisha Kristo, basi mkijilegeza kwa hiari yenu yakawashikilia, kujitoa ni ndoto! Kazi ya maroho hayo ni kukutia upako ili usiliamini Neno la Mungu ktk ukamilifu wake, yakikuongoza kuipokea sehemu na sehemu uikatae, na mwisho wa siku kubakia unazunguka kama pia, kama wale walioizunguka nyumba kule Sodoma wasiuone mlango, na leo hii Mlango ni Kristo, ambaye ndiye Neno la Mungu!

  Hebu jitazameni hapa jinsi mnavyojifungia nje ya ‘RAHA’!
  MHINA:
  “”””Biblia inasema” Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe wala “KWELI” haimo ndani yetu, tukiziungama dhambi, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba, hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu!!. Soma(1Yoh1:8-10). Kwa hiyo, ndugu lwembe unaejifanya huna dhambi, huna sheria, huwezi kufanya dhambi….hiyo ni injili ya uongo na yakupotosha, kwa Mujibu wa neno la Mungu …. Wewe ukienenda kwa roho yako tu, bila ya kujitiisha katika mafundisho ya kristo na kuyatii, basi ndugu yangu kuna hatari ya kuyatumikia maroho ya mashetani.”””

  Na SIYI naye akininukuu na kuhitimisha ono lake:
  “”””Kwanza, ”Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” nawe ukalipokea neno hilo, basi maana yake ni kwamba “ujinga haujakutoka”, ndipo huyo muhubiri kwa hiyari yako, amekurudisha dhambini upya kwa kutokuamini kwako!”
  Yaani ninyi mna dini ya mashetani rafiki zangu. Hicho ulichokinukuu ni andiko la Biblia!! Ni Biblia yenyewe!! Ni sauti ya Mungu hiyo!! Halafu wewe unasema kuwa tukiiamini hiyo sauti ujinga haujatutoka!!! Aaaah, kweli mna cults zisizoelezeka kaka!! Poleni sana!! Yaani poleni kwa kweli!! Ona unavyoenda mzimamzima, “Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi” (1Yn 3:5-6). Huu ndio ukweli wa Injili kwa mkristo anayekua kiroho!” Huu ni ufedhuli mkubwa sasa!! Sasa tunapokuwa ndani ya Kristo ndiyo sheria inaondoka kwa vile hatutendi dhambi?? Leo kama wewe hauibi, je sheria ya nchi dhidi ya wizi imeondolewa kwako?? Na kama ni kweli, nenda kaibe sasa maana uko huru kuiba tu!! Mna mafundisho ya mashetani kaka!! … Mafundisho yako ni ya kuzimu kaka! “””

  Kwa maelezo yenu haya mnajishuhudia jinsi ambavyo kweli “Ujinga” haujawatoka! Mnaimba wimbo msioujua, tena kwa ujinga, mnaona eti kuliamini na kulipokea Neno la Mungu ktk kile lisemacho ni “”… kuyatumikia maroho ya mashetani””! Tena kama asemavyo Siyi, kwamba ni “” mafundisho ya mashetani kaka!! … Mafundisho yako ni ya kuzimu kaka!””!!!! Sasa kama mnaweza mkajifikisha ktk kukiri mambo ya namna hii yenye kuwaua kiroho, bila ya hofu yoyote, mkiyasoma Maandiko na kuyakataa kwamba hilo haliwezekani, tena mkilifedhulisha Neno, kweli nyie mnaelewa mnachokifanya???

  Kuna jambo moja ambalo ninaamini hamlijui sawa sawa, “Nguvu ya kukiri”! Kama unaweza kukiri na ukapata wokovu, vivyo hivyo unaweza kukiri “kutokuwezekana kwa mkristo Kutotenda Dhambi” na ukapokea sawasawa na kukiri kwako, na ukafia dhambini!!! Hii ndiyo tabu tuliyonayo leo hii, wengi wetu hatukijui hata tunachokiamini, hata Mungu mwenyewe hatumjui, zaidi ya uongo wa dini tuliomezeshwa!!!

  Angalia dini zinakowapeleka, zimewafikisha ktk kukiri udhaifu, mkiukataa Utakatifu, “””…sisi bado hatujawa wakamilifu kabisa, Sisi ni kama wagonjwa tuliotibiwa, lakini matibabu yetu bado yanamhitaji dactari kwa ajili ya kukamilishwa zaidi.!!!””” Huu ndio mzunguko kamili wa mauti mnaojiingiza kwa ujinga, maana kwa kukiri kwenu hamtaufikia ukamilifu kamwe, kutokana na kukataa kuliamini Neno linalowakamilisha; dalili ya kwamba makusanyiko yenu HAYANA zile Huduma Tano zinazowakamilisha watakatifu, ndio maana kwenu ninyi jambo hilo ni la ajabu sana!! Tazama hapa Neno linachoamuru ktk Efe 4:11-12 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe”; Basi Neno la Mungu halijawahi kurudi bure, ni lazima likitimize lilichokinena kwa hao waliokusudiwa; kulikataa kwenu ni dalili tosha kwamba mna matatizo makubwa sana!

  …………

 126. Siyi, swali lako bado ni marudio!!!. Kuenenda kwa mwili ni kutii tamaa za miili yetu kwa kuzivunja sheria za Mungu na hatimaye tunajikuta tunahukumiwa na sheria hizo(andiko), lakini kuenenda kwa roho ni kuwekwa mbali na sheria ili tuwe mali ya kristo, ambapo kwa njia ya injili, anatufundisha jinsi ya kumtii Mungu kwa njia ya sheria ya uzima wa roho yenye uhuru na upendo, tunakuwa, ni watu tuliokubaliwa kwa neema huku tukiithibitisha haki ya Mungu kwa hiyo imani yetu, kupitia utii wa Mafundisho ya Bwana Yesu. Soma(Warumi 7:4-6). & (Warumi 3:31).

  au kwa ufupi: kuenenda kwa mwili ni kuishi kwa kufuata mambo ya mwili na tamaa zake, wakati kuenenda kwa roho ni kuishi kwa kuongozwa na roho wa Kristo na injili yake.MIMI NAISHIA HAPA. NAWASHUKURU WACHANGIAJI WOTE KWA USHIRIKIANO MWEMA.

 127. Mhina,
  Naomba uniambie maana ya mambo ya rohoni nay ale ya kimwili. Tunapolitii neno rohoni, huwa tunaliije tofauti na kulitii kimwili? Hebu tusaidiane kwanza hapa!! Halafu malizia kwa kutupa maelezo/ufafanuzi wa kuwa rohoni!! Hii itatusaidia kujua na kuelewa vyema maana ya kushika sheria rohoni na mwilini!!

 128. Lwembe, Siyi, tuendeleeni. Nimekwisha ielewa hii blog inavyokwenda kinyumenyume. Ndugu Siyi, hayo maswali yako ni marudio, ungekuwa ni kweli uliyazingatia majibu yangu, basi usingeniuliza hivyo ulivyoniuliza. Tazama: Tunapoandika katiba mpya, inatubidi tuifute ile katiba yote ya zamani. Lakini tunapoandika upya hiyo katiba mpya, hivi kutakuwa na ubaya gani kuyarudia baadhi ya mambo ya ile katiba ya zamani, endapo labda tunaona ni mambo mazuri ambayo bado yangetufaa pia katika hii katiba yetu mpya ya sasa?. Mimi ninaefuata na kutii yale ambayo kwenye hii katiba mpya yamekatazwa, kama hayo mambo ya kuzini, kuiba, kuabudu masanamu nk, mnawezaje tena kuniambia bado natii ile katiba ya zamani, hebu tazameni ninyi wenyewe jinsi hii katiba mpya ya bwana yesu nayo, inavyotaka mimi nitii na kutofanya mambo machafu kama hayo, soma(1Wakorintho 6:9-10). Ndugu Siyi, ukitaka tuelewane hapo, wewe na ndugu lwembe mnapaswa mniambie neno moja pekee, nalo ni hili” NDUGU MHINA USITII INJILI YA BWANA YESU, KWAKUWA NAYO PIA IMEKUFUNDISHA MAFUNDISHO KAMA YALE YA TORATI!!!. Mkishindwa kusema hivyo, basi ninyi wote mtakuwa ni waongo na wapotoshaji. Yale mambo yote ya agano la kale ya kufuata kimwili, katika agano jipya, mengi yanakuwa ya rohoni kwa njia ya agano jipya. Hayawi yaleyale kwa sheria zake zile zile, isipokuwa yanakuwa yametimizwa kwa asili yake ya rohoni, baada ya kusafishwa na damu ya yesu, ndio maana, ingawa Mungu ametujaza kwa roho wake na kutupa asili mpya na kuzivunja nguvu zote za dhambi juu yetu, yeye pia bado ameruhusu mabaki ya asili yetu ya kale ya dhambi kubaki ndani yetu, yaani “MWILI”. Kwa hiyo, hatuwezi kujifanya kama malaika kabisa hapa duniani, ndiyo maana pamoja na kuokolewa kwetu kwa neema, bado Mungu anataka tuwe ni watiifu wa neno lake.

 129. @ Mhina
  Ubarikiwe kwa ufafanuzi mzuri kiasi fulani ulioutoa kwa Lwembe. Mimi naona shida iliyopo ni watu/wewe kukiri tu utunzaji wa Sabato basi!! Hilo tu!! Maana mtu akikuuliza kuwa, hivi uzinzi, wizi, uongo, ibada za sanamu n.k., unazitiije kwa sasa tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo -Agano la Kale?? Nafahamu miongoni mwa jibu utakalonipa ni kwamba, watu wa agano la kale, walizitii sheria kutoka ndani ya mioyo yao. Mf. akina Yusufu, walikataa kuzini si kwa sababu sheria ya usizini iliandikwa popote, la hasha; bali ilikuwa ndani ya moyo wake –kutomuudhi Mungu!! Ukitaka kuniongezea jibu, utaniambia kuwa, baada ya dhambi kuingia, kushamiri na taifa teule(uzao wa Ibrahimu) la Mungu kupelekwa utumwani Misri, watu walimsahau Mungu kwa asilimia 100, utii wa sheria za Mungu (Amri 10), ulifanywa kuwa ni wa lazima kwa kuwekewa sheria ndogondogo zenye hukumu ndani yake. Kwa hiyo katika akili yako ndugu Mhina, tafsiri ya Sabato unaanza kuipotosha kuanzia hapo!! Unashindwa kutambua kuwa, jinsi unaavyozitii Amri 9 zingine, na Sabato unapaswa kuitii hivyohivyo. Ukijichagulia siku yako nyingine ya ibada, huna tofauti na kile alichokifanya Kaini –kutoa sadaka ya maembe, maparachichi, ndizi n.k. badala ya mwanakondoo/mwanambuzi, akidhani zote ni sadaka tu!! Nadhani matokeo ya Kaini unayafahamu!! Mwisho nikwambie kuwa, Mungu huwa hataki hoja na mawazo yetu mazuri!! Anachotaka kutoka kutoka kwetu ni UTII tu kwa kile alichosema. Hiyo ndiyo salama yetu.
  Neema ya Bwana ikufunikeni.
  Siyi

  @ Lwembe
  Najua kuwa unaujua ukweli mpaka sasa, ila kwa sababu ya dini, aibu na pengine woga fulani, ndio maana unaendelea kujifaragua hapa!! Ila siri ya mtungi unaijua kabisaaa!! Kipindi cha hapo nyuma, niliwahi kukuuliza kama mtu akiwa mkamilifu, sheria inakuwa haina nguvu kwake, hana dhambi, n.k., je, kwani akina Adamu baada ya kuumbwa, hawakuwa wakamilifu zaidi yako wewe? Mbona Mungu aliwapa sheria pamoja na ukamilifu wao? Kwani Mungu hakujua kuwa nimeumba viumbe wakamilifu hivyo hawana shida ya kuwa na sheria?!! Enhee, Malaika wa mbinguni wanafuata sheria, kwani wao si wakamilifu kaka?? Je, ukamilifu wa kuishi bila sheria, wewe unaupata wapi??
  Mimi naona unapinda tu kwa nguvu japo Mhina, Siyi, n.k. wanataka kukusaidia sana kukuonyosha!! Dini inayotaka uhuru dhidi ya sheria ya Mungu, hiyo ni dini ya Lucifer –maana ndiye mwasisi wa kupiga vita sheria za Mungu!! Yeye ni muasi wa sheria za Mungu; na ameteka watu maelfu kwa udanganyifu huohuo wa kutozitii Amri za Mungu ili apate wa kufa nao!! Na kuna mamilioni ya watu watakaufa pamoja na ibilisi kwa kuukumbatia udanganyifu wake huo. Mungu akusaidieni kuwafunulia hili.
  Neema ya Bwana ikufunikeni.
  Siyi

 130. Lwembe: Ipo sheria ya uzima wa roho kupitia imani ya bwana Yesu, ambayo ni tofauti kabisa na ile sheria ya dhambi na mauti (sheria ya Musa) aliyokuwa anaizungumzia bwana Siyi kwamba, bado inaendelea kwa maana haijatimizwa. Soma(warumi 8:2). Sheria hiyo ya uzima wa roho, ndiyo inayoitwa sheria ya kristo ya upendo, ambayo ndiyo inayotufundisha na kututiisha neno la kristo sawasawa na mapenzi ya Mungu. Lakini pamoja na hayo, sisi bado hatujawa wakamilifu kabisa, Sisi ni kama wagonjwa tuliotibiwa, lakini matibabu yetu bado yanamhitaji dactari kwa ajili ya kukamilishwa zaidi.Nimakosa wewe kusema kwamba, eti huna dhambi wala sheria ya kutii!!!. Biblia iko wazi sana kuhusu wanadamu inasema” BILA SHAKA HAKUNA MWANADAMU MWENYE HAKI HAPA DUNIANI AMBAYE AFANYA MEMA ASIFANYE MABAYA. Soma(Mhubiri 7:20). Istoshe, Paulo mtume wa Mungu pamoja na umaarufu wake wote katika injili, yeye anakiri hivi” Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu, la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na kristo yesu. Soma(wafilipi 3:12). Ndio maana sasa, kukawa na kutubu kwa njia ya kristo yesu ili atupatanishe na Mungu tena pale tunapoanguka. Tazama: neno ” Samehe” linamaanisha ” Kusafisha nia” au kufutilia mbali deni. Tunapomkosea Mungu kwa sababu ya udhaifu wetu wa kibinadamu, tunatakiwa tutubu kwa jina la yesu ili ” tusafishe nia” na kumrudia Mungu wetu kwa kufuata njia ya haki inayompendeza yeye. Biblia inasema” Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe wala “KWELI” haimo ndani yetu, tukiziungama dhambi, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. Tukisema kwamba, hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu!!. Soma(1Yoh1:8-10). Kwa hiyo, ndugu lwembe unaejifanya huna dhambi, huna sheria, huwezi kufanya dhambi….hiyo ni injili ya uongo na yakupotosha, kwa Mujibu wa neno la Mungu, kama nilivyokuonyesha. Lakini, hebu usikate tamaa, tubu sasa kwa jina la yesu ili upokee wokovu wa kweli na uzima wa milele. Lakini usisahau tena, ukaacha kulizingatia neno la Mungu na kujifanya unaenenda kwa roho pekee. Asante sana kaka,mimi niishie hapa, lakini ukiwa na tatizo basi niko tayari kulijadili tatizo ilo pamoja na wewe. Ubarikiwe.

 131. Mhina,

  Nakushukuru kwa majibu yako na pia kwa kuniaga! Basi tunapoagana napenda kuyarejea majibu yako na machache uliyoyaandika ili tuyatafakari zaidi, si lazima unijibu, maana naona unalalamikia kupinduliwa kwa comments juu chini; ila usichokijua ni kwamba hata Injili yenyewe nawe umeipindua kichwa chini!

  Kuhusu suala la Sheria, kama unakumbuka, nilikuambia huko nyuma kwamba wewe na Siyi imani yenu ni moja, tofauti yenu ni tafsiri tu ya hiyo Amri ya Nne.

  SIYI (akikusifia):
  “”Ulivyoyaweka ni sahihi kabisa!! Tutahesabiwa haki kwa kumwamini Kristo. Tukishaamini kuwa ametuweka huru, hatuna budi sasa kuishi sawasawa na Amri zake 10 kwa msaada wake, maana kwa nguvu zetu tu, hatuwezi kuzitii isipokuwa kwa nguvu zake!! Na nguvu zake, zimejificha kwenye zile amri kuu mbili –mpende Bwana Mungu wako…na mpende jirani yako…. Maana katika “… pendo ndilo utimilifu wa sheria” – Warumi 13:10. Huwezi kumpenda Kristo, halafu ukaasi sheria zake –amri 10, hata kama ni moja!! Huko ni kudanganyana kweupe rafiki!!””

  MHINA:
  “”…kumbe kule kusema: usiibe, usizini, usiseme uongo nk, ndiko kulikozaa hili neno ” upendo wa Mungu, tunawezaje tena kusema “HATUTII SHERIA”!!!. Sheria hazifuatwi kwa mahitaji yake ya mwilini kama israel, maana tayari kristo alikwisha zifia katika mwili wake, lakini imebaki kwa sisi kuzitii hizo sheria kwa asili yake ya rohoni ili tudhihilishe upendo wetu kwa Mungu na kuhesabiwa haki kwa imani ya yesu kristo.”

  Kwa kadiri ya maelezo yenu haya, hizo tenzi nzuri za kidini, kwa ujumla nyote mnazitii hizo Amri Kumi kwa msaada wa Kristo ingawa wewe unajikanyaga kanyaga lakini ukweli ndio huo, tofauti yenu ni ndogo sana, ni hiyo Amri ya Nne ambayo wewe unasema hiyo ilitimilizwa na Kristo, kwa hiyo hulazimiki kuitii ila unazitii hizo nyingine, ingawa hizo pia unakiri kwamba zimetimilizwa, ndiko huko kujikanyaga kanyaga

  Kuhusu swali langu la Yn 6:55-56, naona umeshindwa kulijibu, huenda ni kwa vile liko nje ya uwezo wako kiufahamu; swali lilihusu siku ile Kristo alipoyanena hayo, wewe unanipa jibu ktk ufahamu wa yalipofunuliwa huku kwenye Injili! Siyi alinielewa ktk urahisi na akanijibu kulingana na swali!

  Bali jibu sahihi ni kwamba Sheria ktk ujumla wake pamoja na hizo Amri Kumi “mnazozitii kiroho”, haikuwa na nguvu juu yao, ndio sababu walibakia hapo ili wamle nyama na kuinywa Damu yake ktk jinsi ya ule utoto unaoufikiria; wao wanajua jambo moja tu, kulipokea neno lake kama watoto wadogo!!!

  Jibu hili ndio udhihirisho wa dhahiri wa Rum 10:4 “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria” neno hili likiwatimilia wahusika.

  Kuna kundi kubwa waliondoka miongoni mwa wanafunzi wake wasiandamane naye tena kutokana na kauli hiyo kuhitilafiana na Sheria ktk ujumla wake, basi unapozungumzia kuzitii hizo Amri, ni dhahiri kwamba nawe umeungana na kundi hili kiroho.

  Nasi leo hii ktk ujumla wetu tukiifikia tena hiyo kauli ya Kristo iliyolitenganisha kundi la wanafunzi wake huko nyuma, na kwa siku yetu ya leo ndio hii hapa ktk Rum 10:4 ikitugawa tena!

  Ndipo kwa Mungu kuziandika hizo AMRI KUMI ktk mioyo yenu, basi ni dhahiri kwamba hamuwezi kuwa na maisha yaliyo tofauti na hayo maelezo yenu ktk kumlingania Mungu. Ndio kusema maisha yenu yote yatabaki ktk kiwango hicho, kumbukumbu ya dhambi ikidumu milele kwa kuhuishwa na hizo Amri huko mioyoni mwenu zilikoandikwa, ili kukabiliana na tamaa za mwili zinazowazunguka ktk ulimwengu mnaouishi, ndio sababu kauli za uzinzi, uasherati, wizi, uongo nk haziwaishi, dalili ya kwamba hamjafikia kufanywa kuwa viumbe vipya!!

  Kumbuka, you can’t jump higher than the life that you are living!

  Gbu!

 132. Mhina,
  Kwanza, nashukuru kwa jibu zuri. Umesema vyema kwa kiasi fulani. Ni kweli tangu zamani, Mungu amekuwa akiwaita watu wake wamwabudu katika ROHO (fikra/akili/mawazo) na KWELI (Kristo Mwenyewe au Biblia). Ukiangalia dhana hizi tu kwa ufupi, utagundua kuwa, Tunapomwabudu Mungu katika ROHO, hatupaswi kumwabudu kipumbavu –yaani bila ya kutumia akili/fikra/mawazo pevu. Tunapokuwa kwenye ibada, akili, fikra au mawazo sharti viwe katika hali ya kufanya kazi ipasavyo –kutambua/kujua kama mambo ya ibada unayoyafanya, ndivyo yanavyopaswa kufanywa mbele za Mungu. Kama ni kujifunza Biblia, jifunze kwa werevu mkubwa. Kama ni kuimba, imba kwa akili pia. Na kama ni kuomba/kusali, sali akili yako ikiwa timamu na yenye utambuzi wa kila neno unaloomba kwa Muumba wako!! Ukifanya mambo haya uko nje ya self control, hujitambui, huelewi hata unachoimba au kuomba huku ukisingizia kuwa umejazwa RM, huko ni kupagawa na mapepo. Ndani ya Biblia, hakuna hata mfano mmoja wa mtu aliyesali/kumwabudu Mungu akiwa nje ya self control. Mifano iliyopo, ni uchawi, usihiri, kupunga pepo n.k., mambo ambayo ni machukizo mbele za Mungu.
  Pili, kumwabudu Mungu katika KWELI, ni kumwabudu kwa kumfuata Kristo kama kielelezo chetu. Lakini zaidi ya yote, Neno lake (Biblia), ndiyo kweli inayotutakasa, hivyo ni sharti tumwabudu Mungu kwa kufuata Neno lake. Kristo anapokaa ndani yetu haina maana kuwa tunaenenda kinyume na sheria/amri zake -Biblia. Hiyo siyo sahihi. Kristo anapokaa ndani yetu, maana yake ni kwamba, tutapata nguvu na msukumo wa ndani kuishi sawasawa na neno lake. Hii ina maana kwamba, hatutajilazimisha kwa nguvu zetu kulitii neno lake. Hasha!! Badala yake, atatupatia nguvu ya ushindi dhidi ya dhambi na tutaishi automatically sawasawa na Biblia!! Tutashika amri zake automatically bila ya external force but through internal one!!
  Kwa hiyo, kumwabudu Mungu katika ROHO na KWELI, ni kumfanyia Mungu ibada ukitumia akili/fikra/mawazo thabiti –ukiepuka kudanganywa na wakati unamwabudu, hakikisha unazingatia taratibu zoooote zilizowekwa ndani ya Biblia, Kristo akiwa kielelezo chako!! Amri 10 za Mungu, hazijapitwa na wakati. Zilikuwepo kabla ya dhambi, zikaendelea kuwepo hata baada ya dhambi, Yesu na mitume wake wakaziishi bila shida yoyote, na zitaendelea kuwepo hata mbingu mpya na nchi mpya!! Ubarikiwe sana.
  Siyi

 133. ” NAOMBA UNIAMBIE MAANA YA KUMUABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI : “Ni ile hali ya sisi kumruhusu Roho mtakatifu atuongoze rohoni mwetu au mioyoni mwetu ili tumuabudu Mungu, tumsifu Mungu na kumuinua yeye pekee, “ni ile hali ya wewe kuamini ndani ya moyo wako, na Pia, kuwaambia wengine kwamba, kazi za Mungu zinapendeza ndani ya watu wote, lakini haswa kwa wale waliompokea kristo kuwa ni bwana na mwokozi wao awaleteaye neema, kweli ya Mungu na mwisho ule uzima wa milele, “ni ile hali ya kuyaona mambo yote ya kidunia ni kama hasara kwako, bali kuwa na Mungu ndani yako, ndilo jambo pekee la thamani sana, soma(wafilipi 3:8), Pia “ni ile hali ya kutengeneza mazingira ya kuonyesha kwamba, Mungu anakubalika kwa uzuri wa matendo yake ya ajabu…hebu tazama ndugu Siyi: Watu wa kale walianza kuliita jina la BWANA, wakalitii na kulitukuza, Soma(Mwanzo 4:26), nae ibrahimu alipokuwa akielekea nchi ile ya ahadi, jambo la kwanza alilolifanya ni kujenga Madhabahu kwa ajili ya ibada, Soma(Mwanzo 12:7), Siku zikaendelea, Wakaja wakina Nabii Musa na Mfalme Suleman ambapo wao, walijenga na kufanya ibada zao kwenye mahekalu na masinagogi yao.Lakini mwisho ni sisi wa siku hizi ambapo, miili yetu ndilo hekalu la Mungu, Soma(1Korintho 3:16). Hii maana yake sio kutokwenda makanisani, isipokuwa, maana yake ni kwamba, tunaweza pia kuabudu mahali popote katika mazingira ye yote, yawe Magumu au mepesi, mabaya au mazuri, kwa sababu, Mungu anakaa ndani yetu, hatuna haja tena ya kutii siku fulani pekee au mahalifulani Pekee, ndio maana hata Paulo na Sila, walifanya ibada gerezani!!!!, Soma(Matendo 16:25). Ndugu Siyi, unaweza kupewa majibu mbalimbali ya swali hili, lakini mimi ninaamini kuwa, hata hili jibu nililokupa ni sehemu ya jibu la kibiblia. ASANTE SANA.

 134. @ Mhina,
  Naomba uniambie maana kumwabudu Mungu katika ROHO na KWELI!!

  @ LWembe,
  Naomba unioneshe kwa kiasi/kiwangogani Sheria za Mungu (amri 10), zilifungamanishwa pamoja na sheria zake za kafara?? Hebu nisaidie tafadhali.

  Siyi

 135. ndg. Lwembe, Mimi nikujibu maswali yako ya Mwisho then naomba niishie hapo kwa sababu, hii blog naona imebadili mwelekeo wa juu chini na chini juu, jambo ambalo linanipa tabu kutumia kwa njia ya simu yangu ndogo mno. Qn1. “WAPI BWANA YESU ALIPOSEMA AMETIMIZA SABATO KWA AJILI YETU?……JIBU: “Mimi nilikujibu swali hili vizuri sana. Biblia haisemi kwamba, bwana Yesu ametimiza sheria moja moja kwa kuzitaja kama unavyotaka wewe utajiwe, isipokuwa, biblia inasema”kristo ni mwisho wa sheria ili kila amuaminie ahesabiwe haki” fullstop. Kwa hiyo ndugu yangu, wewe si unajua kwamba sabato ni sehemu ya sheria ile?, kwanini kuniuliza swali ambalo limeshajibika kwa ujumla wake!!. Tena biblia inaongeza hivi” MTU ASIWAHUKUMU KWA…..”SABATO” Mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo bali mwili ni wa kristo!!. Sasa kwanini mimi ambaye nimemvaa kristo, unaniuliza mambo ya kutii sabato, na wakati”sio mimi tena, ila ni yule kristo akaaye ndani yangu!!…au wewe huelewi maana ya “Mwili ni wa kristo”!!. Yaani bwana yesu anasema kuwa ameitimiza sheria yote kwa ajili yangu ili nimtii yeye(amri zote 10), halafu wewe eti unaniambia “mbona ile moja bwana yesu hajasema kwamba kaitimiza!!!!. Hili ni swali la ajabu sana. Qn2. Katika hayo uliyoyafafanua kutoka (Yohana 6:55-56), ni mafafanuzi ya kitoto yasiyokufaa mtu kama wewe unaeijua injili. Lakini mimi nitakujibu vyema kabisa kama ni kweli wewe huelewi maneno ya injili na fafanuzi zake kiasi hicho. JIBU: Katika andiko hilo, kamwe bwana yesu hakumaanisha sisi wanadamu eti tuule mwili wake wa kibinadamu na kuinywa damu yake ya kibinadamu kama unavyoelezea wewe!!, isipokuwa kitendo kile ni ishara tu, ya kiimani inayofundisha kristo kuwa ndani yetu na sisi kuwa ndani yake. Twasoma ufafanuzi wake hivi” KAENI NDANI YANGU, NA MI NDANI YENU. KAMA VILE TAWI LISIVYOWEZA KUZAA PEKE YAKE, LISIPOKAA NDANI YA MZABIBU, KADHALIKA NANYI, MSIPOKAA NDANI YANGU. Soma(Yoh15:4-7). Kamwe hapo hakuna mambo ya amri kumi au ile amri ya kuua inayoingiliana na mambo hayo, hili ni swali la kitoto mno mno!!. Qn3. WAPI PALIPOANDIKWA AMRI ZA MUNGU ZIMEANDIKWA NDANI YA MIOYO YETU?…….JIBU: “Mungu ametia sheria yake mioyoni mwetu kwa njia ya kristo, Soma(ebrania 8:10), ndiyo maana wewe unajitapa kwa kusema kwamba, ukiwa na huo upendo wa kristo ndani yako, basi pia huwezi kuzivunja zile amri kumi za Mungu kwa maana unaongozwa na roho wa kristo anayekukataza usitende dhambi yeyote. Lakini watu wa mataifa wasio ujua upendo wa kweli wa Kristo, wanaupendo nao, lakini upendo wao hauwazuii kuzivunja zile amri za Mungu. Wao tofauti na wewe, kwa huo upendo wao, huzini, huiba, hutamani, husema uongo nk. Je, mpaka hapo wewe hujajua thamani ya huo upendo wako kwamba, umejengwa juu ya sheria adilifu ya Mungu?. Sasa tazama: Sheria mpya ya kristo inayotuongoza, ni ya upendo. Lakini kuhusu huo upendo wa kristo, biblia inasema” maana kule kusema usizini, usiue, usiibe, usitamani na ikiwepo amri nyingine yo yote” INAJUMLISHWA KATIKA NENO HILI UPENDO!!. Kwa hiyo, hiyo sheria mpya ya upendo aliotupa bwana yesu, imetiishwa katika yale mapenzi yote ya Mungu, ndio maana pia, biblia inasema” pendo hilo ni utimilifu wa sheria yote”.Hatuwezi eti kusema kuwa tunashika pendo la bwana yesu la kumpenda Mungu na jirani zetu, halafu upande mwingine, tunazini, tunaiba, tunasema uongo nk, huo hauwe kuwa ni upendo wa kristo, ila utakuwa ni ule upendo wa watu wa mataifa wasioijua sheria ya Kristo ya upendo wa kweli. Lakini pia, kama nilivyomjibu ndugu Siyi kwamba, Zile amri kumi zilizoandikwa katika mawe na Musa, ndizo amri hizo hizo zilizoandikwa katika vibao ambavyo ni mioyo yetu, Soma(2Kor 3:3). Kwa andiko hilo pekee, linatosha kabisa kutuonyesha kwamba, ni kweli Mungu aliandika sheria yake(amri kumi), ndani yetu kwa njia ya kristo. Labda kama unabisha sana, utakuwa unayabishia maandiko, lakini sasa, itakubidi na wewe unijibu kwamba, hiyo sheria ya Mungu iliyoandikwa ndani yetu, wewe unafikiri ni sheria gani?,….si neno la kristo lenye haki na kweli?…..na sheria ya Mungu (amri kumi) si haki na kweli?. Nikweli kwamba tunaenenda kwa roho wa imani, lakini sisi situmetiishwa sawasawa na mapenzi ya Mungu?, haya bana KAZI KWAKO. Pia, kuhusu lile swala la Fungu la kumi mimi kutoa, labda kwa kuwa wewe ni mkristo safi usietakiwa kumpachikia mtu maneno ya uongo ambayo hajayasema, nakuomba sasa unionyeshe mahali katika blog hii, ambayo mimi nimesema” NATOA FUNGU LA KUMI”. Usipende kutia masingizio katika mambo ya Mungu tafadhali. Istoshe hata kama mtu ni kweli anatoa fungu la kumi, hakuna sababu ya kumhukumu mtu huyo kwa sheria yeyote kwa kuwa, biblia inasema heri kutoa kuliko kupokea, hebu usiwahukumu watu hao, ila waache wapokee heri zao kwa kuwa wametoa kwa ajili ya kuwapenda wengine. Qn4. KWANINI BWANA YESU AMEZITIMIZA AMRI ALAFU AKAZIANDIKA TENA MIOYONI MWETU?…….JIBU: ” ili tutii kwa asili yake ya rohoni, bila ya sheria yeyote ya dhambi na mauti kutushtaki, kutii kwa nia ya rohoni yenye asili ya Mungu mwenyewe au tuseme, ili tuenende kwa roho pekee. Tazama: asili ya torati ni ya rohoni, lakini dhambi ndiyo iliyotutenganisha na Mungu wetu kwa sababu sisi ni watu wa mwili. Biblia inasema” nia ya mwili ni mauti lakini nia ya roho ni uzima na amani. Soma(Warumi 8:7). Sasa, alichokifanya bwana Yesu sio kuondoa sheria ya Mungu ila kutimiza, yaani yeye alitufia sisi kupitia mwili wake ili yale maagizo ya sheria ya Mungu yaandikwe ndani ya mioyo yetu, Soma(warumi 8:2-5), ndio maana kuhusu matendo ya mwili ya kisheria, israel wakaambiwa” KWA SABABU HAWAKUFUATA KWA NJIA YA IMANI (sheria ya Mungu) , BALI KANA KWAMBA KWA NJIA YA “MATENDO”!!!!. Soma(Warumi 9:32). Mwisho, ndugu yangu wewe, ulitaka mimi nikufundishe jinsi ya kutii amri kumi za Mungu kwa njia ya rohoni, sasa, injili yote ya bwana yesu imefundisha jambo hilo, na mimi nilikwisha onyesha huko chini, tena niliweka amri ya Mungu na andiko la injili jinsi lilivyothibitisha sisi tunavyoweza kutii amri zote za Mungu kwa njia ya mafundisho ya bwana yesu ya rohoni, hali hiyo pia ilionyesha jinsi tunavyoweza kuithibitisha sheria ya Mungu kwa njia ya imani yetu, soma( warumi 3:31). Wewe ukienenda kwa roho yako tu, bila ya kujitiisha katika mafundisho ya kristo na kuyatii, basi ndugu yangu kuna hatari ya kuyatumikia maroho ya mashetani. Hebu jitiishe vyema katika injili ya kristo, utakuwa na wewe umekamilika katika mambo yote ya Mungu. ASANTE.

 136. Mhina,

  Asante kwa majibu ya kutosha yasiyojitosheleza!

  Jaribu kulisoma swali ulielewe kwanza, kisha ndio ulijibu kutoka uelewa huo ki Biblia, na si kuflow masomo yenu!

  Swali nililokuuliza ni jepesi sana, na linatokana na maelezo yako haya:
  “” …lakini kuna amri moja kati ya hizo, ambayo inahusu kutii siku ya sabato, hapo utiifu wetu upo katika kumtii bwana yesu, maana yeye ndiye “BWANA WA SABATO”. Kristo aliitimiza sabato ya Mungu ili sisi wafuasi wake, tumfuate yeye…kama alivyozitimiza na zile sheria nyingine. Hakuna kilichobaki cha kutushtaki katika torati, maana yote yalitimizwa na kristo.””

  Swali langu ni hili hapa, nalirudia tena ili unisaidie ktk hili: Ni wapi Kristo aliposema kwamba Sabato ameitimiliza hivyo haitupasi kuitii Amri hiyo kwa sababu yeye ni Bwana wa Sabato??

  Pia nilikuuliza huko nyuma kuhusu Yn 6:55-56 iliyowataka watu waule mwili wake na kuinywa damu yake, ni mitume tu ndio waliobaki walitimize hilo; ndipo ninakuuliza tena, Je, kwa hawa, hiyo Sheria au hizo Amri Kumi mnazozitii ninyi, zina nguvu tena kwao kwa jinsi ya rohoni na mwilini au la? Maana ktk hizo, iko Amri inayokataza kuua, na Torati inakataza kula nyama za watu na kunywa damu; naye Kristo hakulifafanua jambo hilo!!!

  Nikirudi ktk maelezo yako, licha ya kwamba hukunijibu swali langu, lakini yamezalisha maswali mengine pale nilposhindwa kukufuata nyuma. Basi uniwie radhi ninapoendelea kukuliza maswali kutoka hayo maelezo ili twende sambamba usiniache nyuma.

  Kuna mahali umesema hivi:
  “”””Roho mtakatifu, huwasaidia watu watiifu wenye dhamira na nia ya kumuishia Mungu katika matendo ya haki, ndiyo maana zile amri kumi za Mungu zikaandikwa ndani ya vibao vya mioyo yetu, ili kwa njia ya imani ya Yesu kristo, tuithibitishe ile sheria ya Mungu, Soma (ufunuo 14:12) +( 2Wakorintho 3:3).””

  Kwanza, kutoka maelezo haya napenda nikuulize jambo hili: Ni wapi ilipoandikwa kwamba Mungu ameziandika Amri Kumi ktk mioyo yetu?

  Pili, kama nimekuulewa vizuri, unafundisha kwamba kwa Amri hizo kuandikwa ktk mioyo yetu, tunapozitii ndipo RM hutusaidia ktk dhamira zetu za matendo ya haki, ili kwa njia ya imani ya Kristo, tuithibitishe ile Sheria ya Mungu.
  Kulingana na maelezo yako hayo, ni kwamba Imani msingi wake ni kuzitii hizo Amri Kumi ambazo zimeandikwa mioyoni mwetu, na ndizo zinazoiamsha dhamira na nia ndani yetu ya kumuishia Mungu. Nimejaribu kulitafuta fundisho hili ktk Maandiko uliyoyanukuu lakini nimeshindwa kulioanisha: 2Kor 3:3 inasema, “… mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.” SIJAZIONA hapa hizo Amri Kumi wala utenzi wako mzuri kuhusu RM kutusaidia ktk jinsi ya hayo uliyoyasema, naona unalazimisha kuyasimika mafundisho yenu yaliyo kinyume na kile Biblia inachokifundisha!!

  Pia unasema, “”Watu wa Mataifa, hatutakiwi kutii sheria ya Musa, isipokuwa tunatakiwa tutii injili ya kristo””

  Umesema Amri kumi zimeandikwa ktk mioyo yetu halafu tena unatuambia hatutakiwi kutii sheria za Musa, hivi kuna Amri Kumi za Musa na Amri Kumi za Kristo? Kati ya hizo ni zipi zilizoandikwa ktk mioyo yetu? Na kama zilitimilizwa ktk maana yako ya kwamba Kristo alizitimiza, basi ameziandika tena mioyoni mwetu ili tuzifanyie nini? Na kama hatupaswi kutii Sheria za Musa, Fungu la Kumi unalotoa, ni wapi Injili ilipokuagiza jambo hilo?

  Umeniambia kwamba, “”Kiujumla ndugu yangu, amri zote kumi, zimekuwa za utiifu wa rohoni, baada ya zote hizo, kutimizwa na bwana”
  Hebu nifundishe nami jinsi mnavyozitii ki”rohoni” hizo Amri Kumi zilizotimilizwa?

  Ninakushukuru kwa ushirikiano, maana kujibu maswali unayoulizwa kama ulivyoulizwa ni udhihirisho wa “matendo mema”!!!

  Gbu!

 137. Siyi,

  Shalom, “Myahudi”!!!

  Kuhusu kisa cha tajiri aliyekuwa Jehanamu, mimi nafahamu kwamba wewe hauliamini jambo hilo! Na si hilo tu, yako mengi sana ambayo hauyaamini!

  Tukirudi ktk mada, ngoja tuyatazame na haya mengine usiyoyaamini!

  Kuhusu Torati, mimi ninafahamu kwamba ninyi mmeigawa viapande vipande kukidhi mahitaji ya mafundisho yenu. Kwahiyo wewe kunitegemea mimi kuyarejea mafundisho yenu hapo ninapoirejea Kweli ya Maandiko, ndiko kule kukosa akili nilikokuambia!

  Lakini kwa habari ya Torati, kwa kadiri ya ufahamu nilionao, unaotokana na Maandiko, najua iko moja tu aliyopewa Musa, Mal 4:4 “Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.” Na pia nafahamu kwamba hii ndio iliyotimilizwa, kwahiyo unapozungumzia Torati leo hii hiyo inayotuleta kwa Kristo, ndiyo hii ktk ujumla wake na ukamilifu wake kama Torati. Kristo alipokuja mambo yote yalikamilika, kama ambavyo mvua hulinyeshea gugu na ngano pia, gugu likikamilishwa kwa ajili ya moto na ngano kwa ajili ya utukufu!

  Ukitaka kuichambua kiteolojia, utapata vipengele vingi sana ndani yake na unaweza kuigawa unavyopenda ilimradi huvibandiki tafsiri yako, maana Torati ni unabii, naye Mungu anatukataza kulitafsiri Neno lake! Kwahiyo kama nilivyokueleza, Neno la Mungu ni Sheria wakati wote, hata ikiwa ni maagizo ya vyakula au kafara au jinsi ya uchinjaji wa wanyama nk.

  Pia fahamu kwamba kila chenye Mwanzo kina Mwisho. Mungu anapoiunganisha Torati na Musa, hilo lilipaswa likuoneshe jambo fulani, kwamba hiyo imeasisiwa kukidhi mapungufu yaliyojitokeza kulingana na wakati. Kwahiyo jambo lolote linalohusiana na ‘wakati’ hufikia ukomo pale linapokuwa limekidhi haja. Mpango wa Mungu wa utumishi wa Musa ulikuwa ni huo tunaousoma ktk Biblia, tangu kuzaliwa kwake mpaka alipoambiwa apande mlimani; na Torati yake inakoma ktk ujio wa Kristo kwa wote watakao mpokea na kufanyika wana. Hawa ndio wanaopewa Imani, wakirudishwa kule Mwanzo, nayo Imani haina mwisho. Neno la Mungu lote kama lilivyo ktk Biblia, linakoma linapotimia; na ktk ujumla wake limegawanyika ktk sehemu mbili, kuna sehemu ya neno hilo inayolihusu Kanisa na nyingine inalihusu taifa la Israeli. Kwahiyo mimi ninazungumzia sehemu ya Kanisa. Ndio maana imeandikwa kwamba, 1Kor 13:10 “Ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika”; basi Torati iliyo kivuli, inabatilika ajapo Kristo aliye ukamilifu.

  Ulipokibeza kile kifungu cha Yn 6:55-6 kuhusu kuula mwili wa Kristo na kuinywa damu yake, ndio nikajua ya kwamba ni kweli unazitii hizo Amri 10 kama zilivyo ktk Torati, kiasi gani unafanikiwa, sijui; bali kuhusu jambo la kwamba Neno la Mungu ni Amri na unapaswa ulitii, uliposema unakubaliana nami ktk hilo, utakuwa umelisema nje ya ufahamu wako, kulingana na jibu lako kwa kifungu hicho cha Yn 6:56-7; ndio maana nikasema utakuwa na matatizo makubwa sana kiakili, maana huo ni mtazamo wa “a drunk sober man!” jambo ambalo halipo, na pia huwezi kuwa na “Imani” kwa hali hiyo uliyonayo, ukiisha kujiondoa ktk kulipokea neno la Kristo, hilo likupalo kusikia kunakoileta imani; na badala yake ukajirudisha huko kwenye Torati ukiyatimiza maagizo yake kwa ukamilifu, ndio kusema umehesabiwa pamoja na hao waliomsulubisha!

  Dogo, hebu rudi tena huko juu kwa mtoa mada, yasome hayo aliyoyaandika kwa kituo, unaweza kuangaziwa huko gizani uliko, ukauona na mlango wa kutorokea, vinginevyo saa yoyote ile moto unaweza kushuka!

  Kuhusu yale makundi manne yaliyobainishwa ktk Biblia nitarejea niyafafanue, upate na fursa ya kujipima joho!

  Gbu!

 138. Sasa hebu tazama ukweli huu ambao Pia, nilikwishauelezea huko juu, lakini kwa sababu ninyi ni vichwa ngumu, basi ngoja nirudie tena. TAZAMA: Kuhusu ibada za sabato, waumini hutoka majumbani mwao kwenda kwenye mahekalu kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Lakini Yule Mama alipokuwa akiongelea mambo ya Babu zao jinsi siku ya sabato walivyokuwa wakiabudu katika mahekalu yao siku ya sabato, bwana yesu akamwambia hivi” MAMA UNISADIKI , SAA INAKUJA AMBAYO HAMTAMWABUDU BABA KATIKA MLIMA HUU WALA KULE YERUSALEMU (hekaluni), NINYI MNAABUDU MSICHOKIJUA, SISI TUNAABUDU TUKIJUACHO KWA KUWA WOKOVU WATOKA KWA WAYAHUDI. LAKINI SAA IPO NA SAA INAKUJA AMBAYO WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU BABA KATIKA ROHO NA KWELI. Huu sasa ndio wakati wa kumuabudu Mungu katika roho na kweli katika siku zetu zote, sio tena kutafuta siku za sabato maana kristo ndiye sabato wetu wa kweli ndio maana anakaa ndani yetu kwa njia ya Mungu.

 139. Sasa hebu nimalizie kulijibu lile swali la ndugu lwembe aliloniuliza, ananiuliza ” NIONYESHE NI WAPI KRISTO ALIPOSEMA KWAMBA SABATO AMEITIMIZA HIVYO HAITUPASI KUITII KWA SABABU YEYE NI BWANA WA SABATO?…..Ndugu lwembe, kwanza katika swali lako hili, umenishangaza sana, kwa kuwa unaonekana kuwa na mashaka kama yale ya ndugu yako Siyi, ya kwamba bwana yesu alitimiza baadhi tu, ya sheria halafu nyingine akaziacha tuzifuate, lakini jambo hilo ndugu zangu sio la kweli, bwana yesu alitimiza matakwa yote ya sheria ili sisi tumtii yeye pekee. Biblia iwazi inasema” Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, AMEZALIWA CHINI YA SHERIA KUSUDI AWAKOMBOE HAO WALIOKUWA CHINI YA SHERIA” ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Soma(galatia4:4-5). Kwa hiyo ndg lwembe, Sisi tumekombolewa kutoka kwenye torati yoooote, hupaswi kumhukumu mkristo kwa kumtaka atimize kipande chochote cha sheria kwa sababu, sheria yote ilikwisha timizwa na bwana yesu, kwa hiyo, sisi kazi yetu ni kumtii yeye pekee katika injili yake. Labda kwa maelezo hayo niliyokupa, na mimi nikuulize hivi” ni mahala gani katika injili ya bwana yesu panapotufundisha kwamba tutii sabato ya Mungu kila jumamosi, zaidi ya yeye kutuambia tumtii yeye kwa kuwa yeye ndiye sabato mwenyewe?, Pia huoni kuwa hata hizo amri nyingine hatuzitii kama sheria ila tunazitii kwa kuwa zimo kwenye mafundisho ya injili ya bwana yesu kama nilivyonyesha huko juu?, tafakari haya ili ujiokoe na udhehebu wako ndugu yangu. Asante

 140. nawewe bwana Siyi, mimi nafikiri ulikwisha jimaliza mwenyewe hapo juu, kwa kuwa ulikubali wewe mwenyewe kwamba, zile amri kumi, tayari zimetimizwa na bwana Yesu kwa asili yake ya rohoni(jisome hapo juu), na kwa kukubali kwako huko, wasabato mnafanya makosa kusema kwamba, zile amri kumi bado hazijatimizwa na bwana yesu kwa asili yake ya rohoni, mnasema eti ziko vile vile!!!. Lakini hapo juu, umeonekana kukubali kwamba, haziko vile vile, isipokuwa kwa njia ya kristo, tunazitii sasa, katika roho pekee. Sasa mimi sijui kwanini msabato wewe, huko juu kabisa, ulikuwa unanipinga nini!!. Tazama ndugu Siyi, ukikataa na kusema kwamba, zile amri kumi hazijatimizwa na bwana yesu, basi pia ni lazima ukubali na zile hukumu zake pia zinakuhusu wewe, lakini ukikubali kwamba bwana yesu alizifia na kuzitimiza amri zote kumi kwa ajili yako, basi inakuwa pia, hukumu zake na mashtaka yake hayakuhusu wewe.Soma(kolosai 2:14-15).

 141. Roho mtakatifu, huwasaidia watu watiifu wenye dhamira na nia ya kumuishia Mungu katika matendo ya haki, ndiyo maana zile amri kumi za Mungu zikaandikwa ndani ya vibao vya mioyo yetu, ili kwa njia ya imani ya Yesu kristo, tuithibitishe ile sheria ya Mungu, Soma(ufunuo 14:12) +( 2Wakorintho 3:3). ndugu lwembe, wewe unasema kuwa huna sheria yoyote ya kutii, wakati Mungu mwenyewe anasema kuwa, ameiandika sheria yake katika kibao cha moyo wako, je, hujitambui kuwa kwa hali hiyo huna Mungu wala kristo ndani yako!!. Inaonekana wewe, unaongozwa na majini/mashetani, maana hayo, hayana sheria wala kanuni, madude hayo ni kwa roho tuuuu kama wewe!!. lakini sisi, tunaongozwa na sheria mpya ya kristo ya upendo, na kwa njia yake hiyo, basi tunajikuta tunamtii yeye pekee, na kwa njia hiyo, tunajikuta pia tunatii zile amri kumi za Mungu ndani yake, kwa kuwa yeye hakufuta wala kuondoa sheria za Mungu, isipokuwa alizitimiza kwa njia yake ya asili ya rohoni. (rumi 7:14).

 142. Huwa napitaga tena kwenye blog hizi, ili nijifunze na mawazo ya wengine. Lakini kwakua, ndg Lwembe bado unanihoji, nimeona nitoe ufafanuzi wa kile unachohoji. Kiujumla ndugu yangu, amri zote kumi, zimekuwa za utiifu wa rohoni, baada ya zote hizo, kutimizwa na bwana yesu. Hiyo amri moja ya sabato, niliipa ufafanuzi wa ziada ili ieleweke zaidi, sikumaanisha kwamba iliachwa au kuwa tofauti na zile nyingine, hapana. Watu wa Mataifa, hatutakiwi kutii sheria ya Musa, isipokuwa tunatakiwa tutii injili ya kristo “HAKI NA KWELI” ili tuithibitishe ile sheria ya Mungu kupitia imani ya Mwanae, tazama biblia inasema” kwa maana HAKI ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani, kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani. Soma(Warumi 1:7). Sabato na amri zote kiuhalisia havikuwa kwa ajili yetu, ila zilikuwa ni sheria kwa ajili ya kristo, ili akiishatimiza yote, na sisi tujitiishe chini yake, ndiyo maana hakuna hata mwanadamu mmoja, anayeweza kuhesabiwa haki kwa kutii sheria.Biblia inasema” Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, “WALA MFANYA SHERIA KATI YA MIGUU YAKE” hata atakapokuja yeye, Mwenye milki, ambaye Mataifa “WATAMTII”. Soma(Mwanzo 49:10). Hata kama unaishi kwa sheria ya kristo yenye uhuru na upendo, siyo kosa kabisa kusema wewe unachukia kuzini, kuiba, kusema uongo nk, kwa sababu ile dhamira na ile nia yetu, ndivyo vinavyozaa hali ya kumkataa shetani na kazi zake, mimi nakushangaa wewe kutopenda jambo hilo, kwa sababu kama nilivyosema hapo juu kuwa, tatizo lako wewe ukisikia kutii au mtu kukataa jambo baya, basi wewe huwa unawaza mambo ya kutii torati pekee, utafikiri katika hiyo imani yako huna mwili wala akili za kujishughulisha nazo, wewe ni roho tuuuu, jambo ambalo ni la uongo!!. Ubarikiwe

 143. Mhina (na Siyi),

  Religious wishful thinking ni very catastrophic!
  Watu wanapenda sana kuota ndoto za mchana kuhusu kufika kwao mbinguni; ukiwatikisa ukawarudisha duniani, halafu ukawaonesha na Mlango halisi wa kuingilia huko, wanakugomea mpaka wanashangaza, maskini, wao wanataka waendelee ktk ndoto zao tu!!!

  Siyi ni mfano mzuri sana wa jambo hili. Moyoni mwake anajisikia Utii wa hali ya juu sana wa Sheria; tena hizo zilizotimilizwa, na bado yu mbali saaana na Injili!

  Mnakiri kwamba kazi za Shetani zimevunjwa, halafu mbele kidogo mnaendelea kuzitukuza tena, mnaanza kuyakumbuka mambo yenu ya uzinzi, uasherati, chuki, uongo na mambo mengine yahusuyo mwili; halafu mkiisha kuyakumbuka hayo na hukumu zake, ndipo mnazitii sheria kwa majigambo mengi, mkijizuia nafsi zenu ktk mambo hayo na kumtukuza RM, mkiamini kabisa kwamba hiyo ndiyo sheria ya Kifalme, kumbe mnaogopa moto tu bila ya Maarifa!! Kutii Sheria ni kujizuia kutenda Dhambi!

  Jambo msilolijua ni kwamba tokea siku mlipoijua dhambi, huwa haitembei peke tena, sasa inaambatana na Torati iliyotimilizwa; ndio maana mnazungumzia “Utii wa Amri” mwanzo mwisho hamkui ktk kimo; haya hapa maelezo yako:
  “”Sasa, hebu tazameni jinsi tunavyoweza kutii amri zote za Mungu, kwa njia ya sheria mpya ya kristo yenye uhuru na upendo. AMRI YA KWANZA YA BWANA YESU, TUMPENDE MUNGU: ” Tukimpenda Mungu, ni lazima pia, tutazitii zile amri nne za kwanza, zinazofafanua uhusiano wetu na Mungu!!!. AMRI YA PILI YA BWANA YESU, TUWAPENDE MAJIRANI ZETU: Tukiwapenda majirani zetu, basi pia tutazitii zile amri sita zilizobaki, ambazo pia nazo, zinatufundisha, jinsi ya kuwa na uhusiano mzuri na watu wote…lakini kuna amri moja kati ya hizo, ambayo inahusu kutii siku ya sabato, hapo utiifu wetu upo katika kumtii bwana yesu, maana yeye ndiye “BWANA WA SABATO”. Kristo aliitimiza sabato ya Mungu ili sisi wafuasi wake, tumfuate yeye…kama alivyozitimiza na zile sheria nyingine. Hakuna kilichobaki cha kutushtaki katika torati, maana yote yalitimizwa na kristo.””

  Hivi unakielewa hicho unachokisema kweli? Unakataa kuwa huzitii Amri 9 lakini maelezo yako ndiyo hapo yanayozirejea kwa umahiri wa hila Amri hizo ukiikana hiyo moja kwamba unamtii Kristo, basi, hebu nioneshe ni wapi Kristo aliposema kwamba Sabato ameitimiliza hivyo haitupasi kuitii kwa sababu yeye ni Bwana wa Sabato??

  Nitashukuru ukinipa jibu la swali langu hili ili tuendelee kufundishana,

  Asante, &

  Gbu!

 144. Mhina
  Ha ha ha ha haa!! Unatangazaaa!!! Ha ha ha a!!
  Kah!! Haya bwana!! Mimi siwezi kukuzuia kutangaza rafiki yangu!! Una uhuru mkubwa sana wa kufanya hivyo!! Na kwa vile wewe ni mwalimu, una uhuru wa kusema nimepatia au nimekosea kwa majibu yangu yooote niliyoyaandika kwako!! Yaani ungekuwa Lecturer, ningehesabu sapu tu hadi mwisho wa kozi.. Ha ha ha sijui kama kweli ningeimaliza shule!! Mmmhh!!
  Kwanza, naomba nivunje amri yako ya kutonitaka kujibu tena!! Hata hivyo, sitajibu kwa kweli ila niseme tu kidogo halafu nijue moja, kujiandaa na sapu au keriova kabisa!! Tatizo moja ulilonalo, ni kusoma michango yangu yooote, ukiwa na wrong pre-conceived ideas kwa wasabato!! Na hili, haunalo wewe tu!! Wako wasomaji wengi, wenye mawazo ya namna hiyo!! Na kwa sabau ya mawazo hayo, wanajikuta ni wagumu sana kuelewa hata kama unachowaambia kinafundishwa makanisani kwao!! Lakini kwa vile umekisema wewe msabato, inakuwa ni shida kubwa sana kwao kulipokea neno hilo!! Udini, ndio unaowasumbua wengi!!
  Pili, tangu mwanzo na kila mara nimekuwa nikisema wazi kuwa, mimi sina dini wala dhehebu kwa majina yetu!! Naitwa msabato tu kwa vile nasali Jumamosi kama siku yangu ya ibada kwa mujibu wa Biblia!! Lakini ukinikuta anga zangu, mimi huwa ni mtu wa Biblia tu. Kila kisemwacho iwe ni ndani ya kanisa langu au kama kutoka kwa akina Lwembe, Seleli, Sungura, Mhina, Pandael na wengine wengi, kama kina mashiko kwa mujibu wa Biblia, mimi huwa nakipokea tu!! Nilishaamua kuacha mitazamo hasi kwa watu wa imani nyingine!! Tofauti na kukengeuka kwao kwenye usabato na vyakula, wana mambo mengine mazuri tu ya kujenga!! Na nimejifunza mengi sana, baada ya kujifunza kusikiliza, kuhoji, kudadisi n.k. kwa kuyalinganisha na Biblia. Na nikwambie ndugu Mhina, kwa njia ya majadiliano haya, kumenipa kusoma sana Biblia na kuomba mno, kiasi kwamba kuna baadhi ya mambo, mimi nayajua ukimuuliza msabato wa kawaida (asiyejishughulisha), hayaelewi!! Yaani hadi utashangaa!!
  Tatu, kwa hiyo, nikutie moyo ndugu yangu Mhina pamoja na kutangaza kwako, bado una fursa ya wewe kama wewe, kuweka mezani misingi ya mafundisho yenu kwa kuyalinganisha na Biblia mstari kwa mstari!! Ukiendelea kuyameza kama yalivyo, unaweza kuwa umemeza ndoano bila kujua!! Mimi nimeligundua hilo!!
  Nne, ukitaka kufahamu habari za adhabu za kuvunja amri 10, jifunze kwa Adamu!! Adamu aliambiwa kuwa, penalt ya uasi ilikuwa enternal death –total seperation from God!! Pendo la Mungu ndilo lililopunguza makali ya adhabu hiyo kwa kumpa mwanadamu fursa nyingine ya kutubu, fursa ambayo ilizaa torati(masharti) ya pili. Na mashrti ya fursa hiyo, Mungu akayaanzisha mwenyewe pale bustanini –kafara za wanyama, ambazo zilikoma baada ya kifo cha Kristo. Ukisoma Biblia yako vizuri, mfumo wa utoaji kafara, ulikuwa well calculated, kuanzia sehemu ya kutolea kafara hadi steps zenyewe. Ukisoma habari za akina Ibrahimu, kila walipohamia, walijenga madhabahu ya kutolea kafara za wanyama!! Hadi kipindi cha kutolewa utumwani kwa kizazi cha Ibrahimu, utaratibu uleule ulikuwa ukifanyika, tena kwa kiasi fulani, ulikuwa advanced kidogo. Badala ya kujenga madhabahu tu, Mungu alimuonesha Musa madhabahu ya mbinguni na kumwambia ajenge na duniani kwa kufuata mjengo/mchoro uleule!! Kama sikosei, kila kambi waliyopiga waisrael jangwani, walijenga madhabahu yenye sehemu tatu. Sehemu ya kwanza na ya pili, zilikuwa ni sehemu za huduma za makuhani (any kuhani) wa kawaida wa kila siku!! Sehemu ya tatu, hiyo ilikuwa maalumu. Kuhani Mkuu tu ndiye aliyepaswa kuingia huko tena mara moja tu kwa mwaka mzima kwa ajili ya toba ya taifa zima la Israel!! Taratibu zote hizi, zilikuwa ni kivuli cha mauti ya Kristo! Wale waliopuuzia hata kanuni moja, walikufa kwa kupondwa mawe (kama mauti ya kwanza), na watakufa eternal death (mauti ya pili), siku Kristo atakaporudi!! Leo hatuna masharti hayo ya kafara pale tunapovunja amri 10. Adhabu iliyopo ni kifo kama matokeo ya dhambi husika(mauti ya kwanza), na hatimaye tutakufa eternal death, endapo hatutatubu mapema. Kwa hiyo, hadi leo, matokeo ya uasi wa amri 10, ni eternal death bro!! Msingi huu wa maelezo, ndio ulionifanya nikupatie aya za Kuhani Mkuu wa Agano Jipya – Kristo pamoja na habari za upatanisho!! Lakini nimeona hukunielewa!! Mambo haya yako bayana tu kwenye Biblia rafiki yangu. Ila ukiwa mvivu wa kusoma, utakuwa unaona malengelenge tu, halafu unaendelea kujidai kuwa wewe ni mtu wa rohoni kumbe sivyo!! Tatizo ni kwamba, huelewi tu!
  Tano, Torati asili yake ni ya rohoni. Ukisoma Biblia kuanzia mwanzo 1 hadi kutoka 19, hutaona sehemu yoyote inayoorodhesha amri 10. Badala yake, utaona watu wakiziishi tena kwa kuzidhihirisha tu!! Sasa jiulize, walizijuaje!!?? Ni swali ambalo kwa watu makini hujiuliza na kuamua kupoteza muda wao mwingi kufuatilia uhalisia wa jambo hilo!! Siko hapa tena kurudia habari za amri 10 vs sheria ndogo2 na hukumu zake!! Hasha!! Nimeziweka bayana sana kwa huko nyuma. Mimi nikushauri, hata kama hukubaliani na uelewa wangu kuhusu jambo hili, jitahidi kujifunza zaidi, tena ukimhusisha Mungu kwa maombi mengi ili ulijue tu hata kama utaendelea na imani yako hiyo!! Matukio yooote ya sheria ndogo2 na hukumu zake, vilimlenga Kristo!! Hiyo ndiyo torati iliyotimilizwa!! Amri 10, bado zipo!! Hata wewe mwenyewe, unakiri kuwa baadhi yake unaziishi kama walivyoziishi watu wa zamani pasina na kuonekana zimeandikwa wapi!! Swali la kujiuliza, utaziishije sheria zilizotimilizwa Mhina? Anyway kama hizo unaziishi kiroho zaidi kama ilivyokuwa hapo mwanzo, je, hizi ndogo2 na hukumu zake, zenyewe ziko kwenye kona ipi ya moyo wako? Kama torati ilitimilizwa, huku sehemu ya torati hiyo ukiishi, mbona nyingine huiishi? Huoni kuwa unavunja torati nzima kwa kutoziishi sheria zingine za kafara, ambazo nazo ni shemu ya torati unayoiishi rohoni?? Hii ni changamoto kwako!!
  Mwaisho, jitahidi tu kusoma sana Biblia Mhina!! Omba sana rafiki yangu!! Ni hasara sana siku moja ukija kukataliwa na Kristo, huku ulipoteza muda na rasilimali zako nyingi kufanya mambo ambayo ulidhani yanampendeza Mungu kumbe sivyo!! Maana nakuona kuna mambo mengine unayakana kwa kutokujua tu!! Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 145. Siyi….natangaza kwamba, umeshindwa kunipa majibu ya biblia, badala yake umenipa maelezo yenye misingi ya kanisa la wasabato Tanzania. Maandiko yote uliyoyatumia kama(2 wakor 5:18) sijui na(1Timotheo 2:15), nimeyafuatilia lakini hayahusiani kabisa na kile nilichouliza. Mimi sijauliza mambo ya damu ya upatanisho hatakidogo!!, oky usijibu tena. Pili, torati yote imetimizwa na bwana yesu, nawewe ulilikubali jambo hili, maana torati ikiwa yote inamaanisha ni yote kama ulivyojieleza, lakini torati ikitimizwa vijisheria vyake vidogo vidogo pekee, kamwe haiwezi kuwa imetimizwa yote, kwa kuwa msingi mkubwa wa torati ni zile amri kumi za Mungu. Pia swali hili oky, usinijibu tena. Tatu: nakuomba unionyeshe adhabu iliyokua ikimpasa mzinifu, mwizi, na mvunja sabato ya Mungu katika zile amri zake kumi. Naomba unionyeshe adhabu za watu hao waliovunja amri za Mungu kwamba, walipaswa adhabu gani?, ukishazitaja, ujue wazi kwamba, zitawapasa ninyi wasabato wa leo kwa kuwa, wewe umekazania sana kwamba, bwana yesu alitimiza kafara ya vile vijisheria vidogo vidogo lakini amri kumi ziko vile vile.(inamaana na adhabu zake zitakuwa vilevile)…kwa kuwa hazijatimizwa na bwana yesu. Jambo jingine, wewe na ndugu lwembe,Mmeshindwa kabisa kunielewa ndio maana mnaniambia nafuata mri tisa huku nikiiacha ile moja ya sabato!!!. Nimeonyesha tangu huko juu waziwazi kwamba, kwanza mimi sifuati amri kama sheria ya muongozo inavyotaka katika sheria ya Musa, isipokuwa, kwa sababu amri zote kumi zimetimizwa na bwana yesu kwa njia ya sheria yake mpya ya upendo, na kwa kuwa mimi ninaitii injili ya kristo, basi kwa njia ya injili pia, ninazitii amri zote kumi, kama nilivyoonyesha Pale juu. Huko ndiko kuithibitisha sheria ya Mungu kwa hiyo imani yetu(kutii kwa roho). Ndio maana Mungu akasema” NITATIA SHERIA YANGU KATIKA MIOYO YAO NA KATIKA NIA ZAO NITAIANDIKA. Hili ndilo agano la rohoni lililotimiza lile la kwanza kwa njia ya kristo. Ndugu Siyi, mimi nikupongeze katika jibu lako la Mwisho, ni kweli kabisa jinsi ulivyoelezea, lakini mimi na wewe tunapishana pale wewe unapotaka kuishikilia vilevile kama ilivyo, ile torati ya Musa, halafu hapohapo unataka uwe kwenye injili jambo ambalo biblia haifundishi hivyo kabisa, kwa kuwa yesu ni mhudumu wa agano jipya kwa wale wanaomuamini katika injili, Yeye sio mhudumu wa torati ya Musa hata kidogo, ili uokolewe na kupata utakaso wa dhambi zako, ni lazima kuyaacha yale mafundisho ya awali na kujitegemeza kwa yesu kwa njia ya imani na upendo anaotupa katika mafundisho yake.

 146. BASI MUNGU ATUBARIKI WOTE KWA UPAMOJA WETU NA KUTUOKOA KWA NEEMA YAKE YA SISI KUMPOKEA KWETU MWANAE. Mbarikiwe wote.

 147. Hongera bwana Lwembe, kumbe wewe ni malaika, ndio maana mitazamo yetu bado inatafautiana. Wewe ni kwa roho tuuuu, bila hata kutii mafundisho ya injili ya kristo. Sasa, kama hali ni hiyo, mimi huwa najiuliza kuwa, hivi hii injili tumeandikiwa ya nini?, kwa dhumuni gani?, si ili tujitiishe katika mafundisho yake ili tuthibitike katika hiyo!!. Tazama sasa ndugu lwembe, unasema” tunda la roho ni Upendo nk, lakini huo upendo ulionao, umejengwa katika misingi ya ile sheria ya Mungu = torati yote na manabii ” Maana kule kusema, usiibe, usiseme uongo, usizini, usitamani nk, kumejumlishwa katika huo upendo, ndiyo maana bwana yesu anasema” Mkinipenda = MTAZISHIKA AMRI ZANGU!!!, Wewe nilichogundua ambacho hukijui ni kushindwa kutofautisha kati ya utiifu wa torati na utiifu wa injili, ndio maana ukisikia neno kutii basi unakuwa unawaza mambo ya torati ya Musa Pekee!!. Lakini ukweli upo palepale kwamba, tumeokolewa kwa neema lakini utiifu wetu kwa bwana Yesu ni lazima lazima ndugu yangu. Huko kuenda kwako kwa roho, kama hakutakua na utiifu wa sheria ya kristo ya kuitii moyoni mwako, utapotea kabisa ndugu lwembe.Mungu hakusema kwamba, watu wake katika injili wataenda kama roho au kama malaika, hapana, ila Mungu alisema hivi” NITAIANDIKA SHERIA YANGU KATIKA MIOYO YAO.,.. Tazama ndugu lwembe, Mungu alitaka, Pamoja kwamba anatuokoa kwa neema yake, lakini pia kwa nia zetu, tumtii yeye, ndiyo maana kukaja mafundisho mbalimbali ya injili ya kututiisha. Huyo Mtume Paulo, unaetaka kuitafsiri injili yake, sio tu kwamba, anataka tutii sheria za kriso, ila anataka pia tuzitii mpaka mamlaka!!!. Huku ndiko kukamilishwa kuwa nikweli wewe ni mwanafunzi wa Yesu kwa kua, pamoja na kwamba, unaenenda kwa roho, lakini pia unatii injili ya huyo anaekuokoa. Sasa ndugu yangu, wewe ukitaka upuuze mafundisho ya mitume na wanafunzi wa yesu, basi ni lazima utatoka nje ya mstari wa injili na kudanganywa na roho za mashetani badala ya kua na roho wa kristo wa kweli. Imani yako bila ya kutii kila lililoandikwa ktk injili, ni kazi ya bure kabisa!!. Ubarikiwe

 148. Hongera mpendwa wangu Mhina. Umeifikisha maada mahali pa kuamua. Kuna sababu nyingi sana za wanaoamini kwamba Yesu hakuitimiza torati yote, ambazo siyo za kibiblia, zinazowafunga katika imani yao. Niliona mahali mtu mmoja aliorozesha sababu mia moja. Lakini biblia imejaa ushahidi kwamba Yesu aliitimiza torati yote. Nawe umenena vema katika maelezo yako yote nilivyoyapitia.

  Kama kuna mapungufu naona ni katklika hali ya kuendelea kupata ufunuo zaidi wa Neno la Mungu.

  Pendael Simon
  Kwa mtazamo wangu, jinsi nilivyotafakari; tofauti ya dhambi na maovu; dhambi inajitegemea yenyewe; ilikuwepo kivyakevyake, iliingia kwa Adam na hatimaye uzao wake (kwenye mbegu) baada ya Adam kuacha kumwamini Mungu. Hivyo dhambi ni uharibifu unaotokea kwenye utu aliouumba Mungu in contrast to wanaozaliwa upya wanazaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyoharibika, the incorruptible seed. (1Peter 1:23)

  Kwa hiyo kwa jinsi nilivyotafakari, nimeona kwamba dhambi iko inajitegemea, huu uharibifu huwa ni matokeo ya ile dhambi. Ndiyo maana ili kutatua tatizo la dhambi uumbaji mpya ulihitajika; na ule utu ulioharibika unaondolewa (Rumi 6:6)

  Lakini, maovu ni yale yanayoonekana kwa yule mtu ambaye dhambi iko ndani yake. Kwa nje anajidhihirisha kwa matendo yake maovu na hali yake ya mwili na nafsi. Mfano wa matendo maovu yanayoashiria kuwa mtu ni mdhambi ni list ya makatazo katika torati. Mfano kuabudu miungu, Kuua, kuzini, kuiba n.k, hayo ni maovu.

 149. Lwembe,
  Kwanza, “”Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” nawe ukalipokea neno hilo, basi maana yake ni kwamba “ujinga haujakutoka”, ndipo huyo muhubiri kwa hiyari yako, amekurudisha dhambini upya kwa kutokuamini kwako!”
  Yaani ninyi mna dini ya mashetani rafiki zangu. Hicho ulichokinukuu ni andiko la Biblia!! Ni Biblia yenyewe!! Ni sauti ya Mungu hiyo!! Halafu wewe unasema kuwa tukiiamini hiyo sauti ujinga haujatutoka!!! Aaaah, kweli mna cults zisizoelezeka kaka!! Poleni sana!! Yaani poleni kwa kweli!! Ona unavyoenda mzimamzima, “Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi” (1Yn 3:5-6). Huu ndio ukweli wa Injili kwa mkristo anayekua kiroho!” Huu ni ufedhuli mkubwa sasa!! Sasa tunapokuwa ndani ya Kristo ndiyo sheria inaondoka kwa vile hatutendi dhambi?? Leo kama wewe hauibi, je sheria ya nchi dhidi ya wizi imeondolewa kwako?? Na kama ni kweli, nenda kaibe sasa maana uko huru kuiba tu!! Mna mafundisho ya mashetani kaka!! Ila ni nguvu sana na ninyi kuja kuligundua hilo maana na ninyi mnaamini kuwa ni neno la Mungu hilo!! Poleni tu!! Tunapozaliwa na Mungu, ni kweli tunakuwa viumbe vya Mungu visivyo na dhambi, lakini haina maana kwamba sheria hiyo imeondoewa kwetu!! Sheria iko palepale!! Adamu na Hawa walipoumbwa, waliumbwa wakiwa wakamilifu kuliko Lwembe na waumini wenzake, lakini walipewa sheria!! Kwa nini Mungu asingewaacha tu kwa vile walikuwa ni wakamilifu??? Mafundisho yako ni ya kuzimu kaka! Ila itakuchukua muda mrefu sana kuja kuligundua hilo. Acha itoshe sisi kukwambia hivyo tu!!! Huenda siku moja Mungu atakufungua macho zaidi uone ufedhuli huo mnaoukumbatia na kutaka kuwabambikizia na wengine!! Hadanganyiki mtu ndugu yangu!!
  Pil, wewe fedhuli kwelikweli rafiki yangu!! Fedhuli kwelikweli!! Unachokifundsha hapa ni total perfection ambayo haipo kwa wakristo walio wengi!! Tangu Adamu baada ya dhambi, maisha ya mwandamu yamekuwa ni ya kuanguka na kusimama. Mpaka enzi za Kristo, mitume wake walikuwa ni watu wa kuanguka na kusimama. Kuna vipindi walimkataa hadi Bwana wao, lakini walitubu wakendelea na imani yao!! Kwa kusema haya, nisieleweke kuwa natetea dhambi!! Na wala usiibuke na hoja fedhuli ya namna hiyo!! Ninachosema ni kwamba, ukamilifu upo, lakini haundoi sheria!! Hata mitume walipofikia ukamilifu, sheria hazikuondoka kwao!! Mungu anatii sheria bro!! Asingekuwa anatii sheria, asingetoa sheria kwa viumbe vyake!! Asingekuwa anatii sheria, asingeumba vitu vikiwa kwenye mfumo wa kutii sheria ya asili!! Mungu anapendezwa sana anapoona viumbe vyake tukitii sheria zake, kama matokeo ya kwetu kumpenda YEYE.
  Tatu, habari za Sabato nimerudia kuzisema mara kadhaa hapa!! Kama wewe Lwembe una dini nyingine ndani ya Biblia tofauti na ile waliyoenda kuabudu siku za Sabato, ilete hapa!! Lakini kama huna, acha tuendelee kuwa washamba wa kufuata Neno la Mungu kuliko kuwa werevu wa kipumbavu!! Wewe kama unafuata imani ambayo haiko kwenye Biblia eti kwa kufanya hivyo unakuwa mwerevu, songa mbele. Sisi akina Siyi, tumeamua kubaki na ujinga wa kufuata kila isemacho Biblia.Sabato ndiyo dini ya Biblia –mwanzo hadi ufunuo!! Hakuna dini wala dhehebu lingine humo – ni usabato tu!! Kama ninyi mnafikiri kuna heri kwingineko kokote mbali na kumwabudu Mungu siku ya Sabato, endeleeni na ufedhuli huo!! “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana” – Yoshua 24:15. Kile anachosema Mungu ndicho nitakifuata mimi!! Na hiyo ndiyo hekima kwangu!! Mengine ni ufedhuli mtupu!!
  Siyi

 150. Mhina,
  Kwanza, aya ndani ya Biblia ni nyingi sana zinazosema kuwa sheria za maagizo ziliishia msalabani. Mojawapo ni
  2 Wakorintho 5:18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
  Kiungo cha upatanisho kilikuwa ni damu za wanyama kaka. Bila damu hakukuwa na upatanisho isipokuwa kwa wale waliopeleka unga mwanana!! Sharti kuu la kuondolewa/ kufunikwa dhambi, lilikuwa ni damu. Kristo ndiye aliyefanyika kafara kwa wanadamu wote na hapohapo akawa kuhani mkuu (mpatanishaji)!! Waebrania 9:11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, Waebrania 8:1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni.
  Kwa hiyo Kristo alifanyika kuwa mambo mawili. 1. Kafara ya wadhambi 2. Mwombezi wa wadhambi (kuhani). Zote hizi, zilikuwa ni sheria za maagizo a.k.a torati ya maagizo!

  Wagalatia 3:24 Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.
  Sheria za maagizo ndizo zilizotuleta kwa Kristo – kitu halisi!! Damu ya Kristo ndiyo inayotusafisha sasa na uovu wote. Kwa sasa hakuna haja ya kwenda kwa mchungaji eti ukaombewe!! Omba wewe mwenyewe kwa Mungu kupitia kuhani mkuu (mmoja tu) Yesu Kristo. “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu”- 1 Timotheo 2:5.

  Pili, Mhina siku ile nilisema neno TORATI ni jumuishi!! Nikasema kuwa, linabeba hata maana ya zile sheria zilizokuja kabla ya dhambi, walizopewa akina Adamu na mkewe Bustanini!! Lakini pia, linabeba dhana ya sheria zote zilizokuja baada ya dhambi. Sheria zote hizi za aina mbili, zinajulikana kama TORATI kwa sababu zimeandikwa ndani ya vitabu vya TORATI (vile vitano vya Musa)!! Sasa hapa naona ulitoka patupu bila kunielewa!! Ni vizuri tu ukaelewa ni torati ipi –ile iliyokuwepo kabla ya dhambi au ile iliyokuja baada ya dhambi iliyoishia msalabani?? Jitahidi tu kukagua hapo!! Na haina maana kwamba, vitabu vyote 5 vya mwanzo wa Biblia, leo havina kazi tena!! Hasha!! Hebu tulia, na tafakuri kwanza habari ya torati kabla ya kufkia hitimisho la kuniita mlaghai!! Tafadhali ndugu yangu, dhana ya Torati niliyoisema, wewe ikague hata kwenye lugha yake ya asili ya Kiebrania, utaikuta hii maana ninayokwambia kaka. Sikuongpei hata kidogo!!

  Tatu, naona pia hatujaelewana kwenye suala la TORATI!! Bado wewe unazijumuisha pamoja!! Ngoja twende polepole Mhina!! Katika Agano la Kale, sadaka za dhabihu, zilizingatia sheria ipi? Amri 10 au sheria za maagizo -kafara?? Jibu ni jepesi zililenga sheria za kafara, sheria ambazo mtu akishindwa kuzitimiza, zilikuwa na hukumu yake pembeni!! Pamoja na kwamba sheria za maagizo zilitegemea uvunjaji wa Amri 10, hali kadhalika, hukumu za sheria za maagizo, zilitegemea sheria za maagizo zenyewe!! Amri 10 zimekuwepo tangu mwanzo, kabla ya dhambi. Na ndizo zilizovunjwa na akina Adamu na Hawa, Mungu akawaanzia sheria za maagizo zenye hukumu ndani yake. Kile alichokuja kukitimiliza Kristo, ni zile sheria pamoja na hukumu zake zilizokuja baada ya uvunjaji wa amri 10!! Hata leo, tunaposamehewa bure na kupewa hukumu ya kuwa huru, hakutufanyi kurudi tena kwenye uvunjaji wa amri 10. Ikitokea tukaanguka, cha kwanza kabisa ni kumililia Kristo atusamehe kwanza na kutuweka huru, kisha huturejesha kwenye utii wa amri 10 zilizokuwepo tangu mwanzo!! Kwa hiyo amri 10 hazitikisiki wala haziondolewi na chochote!! Zenyewe zipo na wakristo wote waliosamhehewa kwa damu ya Kristo, wakawekwa huru, hawana budi kuishi sawasawa (kutii) na amri 10, ili wasiendelee kumsulubisha Mwana wa Mungu!! Kwa hiyo, dhabihu za wanyama, ziliwakilishwa na Kristo ndiyo maana leo wasabato hatuhangaiki na dhabihu za namna hiyo!! Damu ya Kristo yatosha!! Tunachotakiwa sasa baada ya kuwekwa huru, ni kuishi tu sawasawa na Amri zake 10 basi!! Tena anasema, tunaweza tu kuzitii amri zake kwa sisi kukaa ndani yake. “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” – Yohana 15:5 .
  Nne, napenda kurudia tena kusema kuwa, amri 10 hazikutimizwa pale msalabani!! Maana ya ayah ii, “MNADHIHILISHWA KWAMBA MMEKUWA BARUA YA KRISTO TULIYOIKATIBU, ILIYOANDIKWA SI KWA WINO, BALI KWA ROHO WA MUNGU ALIYE HAI, SI KATIKA ” VIBAO VYA MAWE” ILA KATIKA VIBAO AMBAVYO NI MIOYO YA NYAMA!!!!!. Soma( 2Wakorintho 3:3).” Ni kwamba, kwa sasa hizo amri 10 hazipo tena kwenye upeo wa macho yetu zikiwa juu ya mbao za mawe!! Ziko mbinguni!! Paulo anachokifundisha hapa ni kwamba, baada ya kuwa tumeshasamehewa kwa dhabihu ya Kristo, utiifu wa amri kumi unapaswa kuanzia mioyoni kama ilivyokuwa kwa watu wa zamani agh. kabla ya kudhirihiswa mlimani Sinai!! Amri 10 ziiliandikwa ndani ya mioyo ya watu. Baada ya kifo cha Kristo, hali ile imerudishwa tena –kuishi kwa msukumo wa ndani wa kutii amri 10. Dhambi sharti zikome kuanzia mawazoni halafu kwa mwili iwe ni matokeo tu!! Na hiki ndicho kiini cha injili ya mitume. “Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika” Waebrania 10:16

  Kwa hiyo sheria za dhabihu zilitegemea uvunjaji wa amri 10. Halikadhalika, hukumu zake pia zilitegemea utekelezaji wa sheria za maagizo!! Yule aliyetekeleza vyema, aliwekwa huru. Na yule aliyezembea, walimponda mawe!! Kwa hiyo Yesu alikuja kukomesha sheria za dhabihu na hukumu zake tu!! Amri 10 bado ziko palepale!! Kama na amri 10 zingeishia msalabi, leo kusingekuwa na dhambi, maana dhambi huja kwa sababu ya uwepo wa sheria!! Na wakristo tungekuwa tunafanya kila aina ya ufisadi maana amri 10 zimegongomelewa msalabani!! Je, ni kweli tuko huru kutendeka tupendavyo kisa tunamwamini Kristo?? Hasha!! Amri 10 bado zipo na kazi yake ni endelevu!! Nimekuona jinsi ulivyomjibu Lwembe kwenye amri 10. Sehemu niliyotia umakini mkubwa ni kwenye amri ya 4. Umeslide ile mbaya rafiki!! Hebu iangalie hiyo tafsiri yako upya, maana haisaidii chochote kama unashika amri 9 huku moja ukiiacha bila sababu za msingi!! Mungu akusaidie kuliona hilo!!
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 151. Sungura,
  Kwanza, mimi nakuona kama na wewe ni walewale akina Pandael!! Nimekuwa na wewe kwenye mijadala kadhaa hivi!! Habari za sheria za Musa, nilishaanza kuziongelea zamani sana hapa mtandaoni! Nikasema, zinaitwa ni sheria za Musa kwa sababu umaarufu wake(kwa jina hilo) unaonekana zaidi kwa kizazi cha Israel kilichokuwa kimetoka kwenye uasi –Misri!! Kabla ya hapo, sheria hizo zilikuwepo na wala hazikujulikana kama ni za Musa. Zaidi ya hapo, nikakurahisishia kuwa, sheria za Musa, ni sheria zilizokuja baada ya dhambi!! Kwa akili yako ndogo, wewe ukakonkludi kuwa hizo zilikuwa ni sheria za Musa!! Kwani Musa alikuwepo baada tu ya dhambi?? Wewe vipi ndugu??!! Mbona huwa unapenda kurudisha mambo nyuma tu kila wakati?? Au unafikiri hizi ndizo logic/sense zako za kuhoji sasa!!!!?? Hivi kweli watu wanaohoji huwa wanahoji hivi kama wewe unavyofanya?? Mimi nakuona hauko hapa kwa ajili ya kujifunza, isipokuwa, uko kifalisayo zaidi!! Unatafuta tu kosa au sehemu ya kumbania mtu!! Na nilishakusoma muda mrefu sana!! Kwangu utachemka tu maana kila nilisemalo, ni Biblical!! Kamata cha Biblia ili upone wewe!!
  Pili, Biblia nzima ni SHERIA!! Kama huelewi, waulize hata marafiki zako akina Lwembe watakwambia!! Walishalithibitisha hilo kwa uelewa wao wenyewe!! Kwa hiyo nikisema kuwa amri ya Sabato kabla ya dhambi iko Mwanzo 2:1-3, ndivyo Biblia isemavyo!!!! Na kama unafikiri hiyo siyo amri, amri yenyewe ya kuishika Sabato iko wapi sasa?? Maana kwenye kutoka 20:8-11, inasema IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE…!! Hoja, kwani ilisemwa lini (kama amri kwa uelewa wa Sungura) hadi tukaisahamu na sasa Mungu anataka tuikumbuke?? Acha ufedhuli rafiki yangu!! Kama huna hoja kama nduguyo Pandael, ni vyema tu ukakaa kimya kusoma michango ya wengine. Si kila mara uchangie kama huna cha kusema!!
  Tatu, nazidi kukushangaa kama siyo kuwashangaa nyote mnaouliza kuwa ni wapi watu wa zamani waliitwa wasabato!! Yaani mnatia huruma!! Kama dini iliyotajwa ndani ya Biblia ni Sabato, waumini waliitwaje? Wanafunzi wa Kristo walijulikana kama Wakristo kwa ufuasi wao kwake tu. Je, waliokuwa waumini wa dini ya Sabato, mnafikiri ninyi waliitwaje? Au mnafikiri waliitwa wajumapili?? Yaani maswali haya kabisa watu wazima na akili zenu ndo mnauliza ili kupoteza muda wa mtu!! Hii ni ishara tosha kabisa ya kuishiwa hoja!! Hivyo mnataka kila neno ni mpaka lionekane lenyewe!! Mtakesha na mtapotea tu kwa kuukataa wokovu!! Shauri yenu ndugu zangu!!
  Neema ya Bwana iwafunike

 152. Siyi,

  Jambo unalolifanya si la kiungwana!
  Kumbuka kwamba kuna madhehebu ya dini ya kikristo zaidi ya laki moja diniani kote ambayo yanawakilisha idadi hiyo iyo ya mafundisho tofauti tofauti.

  Kwahiyo unapolazimisha mafundisho yenu ya Kisabato kuwa ndilo Neno la Mungu, huo si uungwana, na wala jambo hilo halimsaidii yeyote yule zaidi ya kuwapofusheni Wasabato wote ili msilitoroke kundi lenu, huenda huo ndio wajibu mliopewa!

  Lakini uungwana ni kudumu ktk spirit ya majadiliano, tukiyakagua hayo mafundisho tofauti tofauti tuliyonayo ili kuyabaini kama yanalilingania Neno la Mungu au la. Maarifa ya Neno la Mungu huongezeka ktk jinsi hii, kwahiyo jitahidi usilivuruge jambo hili zuri kwa kupandikiza uongo wa dini yenu kisha kuulazimisha kuwa ndio ukweli huku ukijua fika kwamba wapendwa wamezifungua Biblia zao wayatazame hayo ya Adamu kuitunza Sabato kabla ya Anguko, jambo ambalo halipo; hauoni kwamba hilo litaletelea wewe kupuuzwa??

  Unapopuuzwa kutokana na kulikosea adabu Neno la Mungu, ni ishara kwamba Mungu alikwisha kukupuuza zamaaaani huko kabla ya misingi ya dunia kuwekwa!!

  Hebu prove me wrong kwa kubakia ndani ya wigo wa Neno la Mungu, kwamba hilo ktk purity yake ndilo Yakini yetu!

  Baada ya kukuambia hayo, sasa naweza kuyaendea maswali uliyoniuliza na pia kuyatazama maelezo yako mengine ktk kioo cha Maandiko ili yenye kufaa tuyachukue tujiongeze ktk Maarifa, na ambayo si sawa tukujuze ili uyabwage kabla hayajakuua!

  Gbu!

 153. Inaendelea….

  Mhina,

  Yaani mtu akikujia na kukuambia kuwa, “”Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” nawe ukalipokea neno hilo, basi maana yake ni kwamba “ujinga haujakutoka”, ndipo huyo muhubiri kwa hiyari yako, amekurudisha dhambini upya kwa kutokuamini kwako! Injili hupofua pia macho ya wasioamini! Maji yale yale yaliyombeba Nuhu safinani, ndiyo yaliyokiangamiza kizazi cha wasioamini, vivyo sheria; wengine imewapeleka kwa Kristo wakaivuka Hukumu; na wengine imewasomba ktk mafuriko yake ikiwapeleka Hukumuni, maana hakuna sheria bila hukumu!

  Tofauti na jambo hilo, iwapo uliitii Injili, Utii huo hukuingiza ktk hatua mpya hapo unapozaliwa kwa Roho wa Mungu. Maana Kristo “Alidhihirishwa ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi” (1Yn 3:5-6). Huu ndio ukweli wa Injili kwa mkristo anayekua kiroho! Tazama fungu la 9 linachokisimika mioyoni mwetu, akiipandikiza ile shauku ya kumfanania, “Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.”

  Ndipo kwa mawazo yako Mhina, unategemea mambo haya yakutokee huko mbinguni utakapokuwa unaishi kama hao malaika unaowasema??? Ktk Gal 5:16 Mungu anatuasa, “Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza KAMWE tamaa za mwili.” (msisitizo ni wangu), kinyume na hili, wewe unanifundisha kwamba ni lazima niendelee kufanya Dhambi: “”Ya kwamba eti uwezi kufanya dhambi tena, huna sheria au taratibu zozote za makatazo ya kukutiisha nk, hapana, ila unatakiwa, ukishaokolewa kwa neema ya kristo, uanze kulisikiliza neno la kristo, kulifanya na kuliishi sawasawa na Mapenzi yake”” Mapenzi ya Mungu ndiyo hayo anayonitaka nienende kwa Roho, huyo aliyenizaa, ndipo ananihakikishia kwamba, “”Nikiongozwa na Roho, sipo chini ya sheria””; Sasa nimuamini nani kati yenu, wewe unayeniambia Sheria ni lazima au Mungu anayeniambia siko chini ya Sheria??

  Jambo jingine unalopaswa kufahamu ni kwamba Sheria ni kamilifu, Torati inapotimilizwa ndipo inapoufikia ukamilifu wake kama Sheria. Kwahiyo Kristo anapoitimiliza Sheria maana yake anaifikisha ktk ukamilifu wake kwa wote watakaoendelea ktk Sheria. Wigo wa Dhambi ndio uliopanuliwa, kwamba sasa si ktk mwili tu bali hata ktk kuwaza kwetu; Nazo Adhabu za hukumu zake, HAKUNA zilizopunguzwa kama anavyokudanganya Siyi, kwamba mkristo unaweza ukazini halafu uende ukatubu, eti kwa ile Neema ya Kristo utasamehewa, maana yeye alizibeba dhambi zetu zote, ndio maana hatupigwi mawe siku hizi za Neema! Ukisikia ufedhuli, basi hakuna unaoipita injili kama hii!!

  Kama Torati ilikamilika ilipotimilizwa, unashangaa nini inapokomeshwa? Tena haikukomeshwa kwa wote, bali kwa hao waliompokea Kristo ambao wamepewa Sheria ya Kifalme ambayo pia ni KAMILIFU kama ilivyo Torati iliyotimilizwa; Sheria zote zinajitegemea, kwahiyo unapotaka Torati iliyotimilizwa iiongoze Sheria ya Kifalme, hayo ni mawazo yako kama alivyowaza Petro alipotaka kujenga vibanda vitatu, huo si mpango wa Mungu! Toka lini ulisikia kwamba Mungu huwaga anatii Sheria?

  Sheria ya Kifalme ni ya Roho na si mwili, nalo tunda la Roho ndilo hili hapa, Gal 5:22-23 “Upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo HAKUNA SHERIA.” Torati iliyotimilizwa haiwezi kuzaa tunda la Roho. Hivi ukijizuia kumtazama mwanamke kwa kumtamani, au ukijizuia kumchukia nduguyo nk, ndio tunda la Roho?? Tunda la Roho linapatikana kwahawa tu; “Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.” Hakuna aliyesulibishwa halafu akawa mzima, unakufa kwanza, na ndipo unapofufuliwa ktk Kristo ukiwa ni kiumbe kipya ndipo mambo hayo yanawezekana kwako. Vinginevyo ndio inaonekana akina Lwembe wanaleta hadithi za kufikirika!!!

  Gbu!

 154. Mhina,

  Hahahahahahaha…..! Kutokuamini ni zigo la misumari kwenye gunia!

  Kwa taarifa yako ndg yangu, wako hao malaika wanaoishi mbinguni, na pia wako malaika wanaoishi hapa duniani, Ufu 2:1 “Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso…”!

  Nilikuuliza maswali mawili kulingana na jambo tunalolijadili, badala ya kunijibu, naona kwa hila ya kutonijibu, ndio unanilalamikia, “”…hao wengine wanao kunywa damu ya Yesu na kutii injili ya kristo, nao wanamakosa gani?”” Ni wapi hapo nilipowasema hao wanaokunywa damu ya Yesu na kutii injili ya Kristo?? Jibu swali kulingana na context lilivyoulizwa, usiniwekee kauli zako mdomoni, jinsi hii ni sehemu ya kuwa “muongo”; basi huo utii wako unaoupigia debe uko wapi?

  Ktk maelezo yako, nimesikitishwa sana nilipoiona jinsi yako ya kuithibitisha Sheria ya Mungu, zile Amri Kumi ukizitii kama ulivyoziorodhesha, kichekesho kiko kwenye ile ya Nne!!! Pia nilichokigundua kwako ni kwamba hujajua kwamba mtume Paulo aliyewekwa kuwa mwalimu kwa Mataifa, ameifundisha Torati iliyofafanuliwa vizuri saana, akiiunganisha na Injili!!! Tazama, umeirejea vizuri sana Torati iliyofafanuliwa ila umeshindwa kuvuka uingie ktk Neema, umeshindwa kumfuata nyuma Paulo akuingize huko kwa Kristo; wewe katikati ya safari umeanzisha mambo yako hayo, ndio maana umebaki njia panda ukiikosa ile kona ya Injili, na sasa akina Siyi wanakupeleka huko kwao, makaburini!!!

  Tatizo kubwa ninaloliona kwako ni ule “utapi mlo wa Injili” unaotokana na mafundisho ya dini unayolishwa; na matokeo yake ndio haya, kwako wewe kila Andiko linadumu milele, jambo ambalo si sahihi, ndio maana hukui ktk kimo, miaka yote uko darasa la pili tu, kama akina Siyi! Kwa taarifa yako, Maandiko mengi sana yanatimilizwa kadiri unavyokua ktk kimo kulingana na unavyoendelea ktk uanafunzi wako. Maandiko hayako kiholela, ni shule kamili; “Enendeni mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu…!

  Labda nikupe mfano ulio hai, ngoja tukuangalie Mhina (nimesema mfano tu, usije ukanirarua!):
  Haya, Mhina ni mpagani aliye ktk ibada za miungu ya huko kwao. Ndipo siku moja anakuta na mtume Petro, huyo aliyetumwa kuihubiri Injili kwa kila kiumbe, [Mk 16:15-16 ” Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.”]

  Basi, hapo anapoifunua dhambi kwako, ndipo sehemu ya mahubiri yake ingekuwa hivi:
  Rum 5:12 “Kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”
  Kisha akaendelea,
  1Yn 3:4 “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi”
  Rum 6:23 “Mshahara wa dhambi ni mauti”
  Mal 4:1 “Angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.”
  1Yn 1:8-10 “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”

  Ukiisha kufikishwa mahali kwa Injili ukajiona u mwenye dhambi, hata ukachomwa moyo wako, hiyo ni dalili nzuri, ndipo lingekujia lile swali maarufu, Mdo 2:37, “Tutendeje, ndugu zetu?” Swali hili haliwezi kumjia mtu ambaye hajahubiriwa Injili, Swali hili ndilo kipimo cha kwanza kuhusu Imani, kwamba Neno la Kristo umehubiriwa, likakupa kusikia, ukaiona na Hukumu unayoiendea, ndipo kwa Imani ukaitafuta Neema, maana hakuna unaloweza kulifanya wewe kama wewe hata ujiokoe na Hukumu hiyo; ndipo out of desperation ungemuuliza Petro swali hilo, “Nitendeje ndg yangu?” Injili imeweka Mlango mmoja tu wa kuitorokea Hukumu, Yesu Kristo; nao Ufunguo wa Mlango huo alikabidhiwa Petro, Mt 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za Ufalme wa mbinguni.”; Tazama hapa anavyolifungua hilo LANGO la Ufalme: Mdo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu”; ndio hili neno tunalosisitiziwa, “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”!!!

  Sasa ulipoisikia hiyo Injili, ikakushitaki ktk dhamira yako, ukauliza, ufanyeje? Ukapewa jibu, UKATII, ukabatizwa kwa jina la Bwana Yesu Kristo, Ukaondolewa Dhambi zako zooote, ukasafishwa na udhalimu wote wa ‘matendo ya mwili hayo ambayo ni dhahiri, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo’; Basi ukiisha kupita ktk hatua hii muhimu, maana yake ni kwamba Maandiko yote hayo niliyokunukulia, kwako yanakuwa YAMETIMILIZWA, hayakuhusu tena, ukiona yanakuhusu, hiyo ni dalili mbaya, kwamba hukuelewa chochote!!

  Inaendelea….

 155. Mhina,Kuna tofauti gani kati ya Dhambi na Makosa?Swali hili nilishauliza bila Mafanikio kutokana na jinsi MNAVYOCHANGANYA hizi dhana mbili.Naona unawakanganya sana Wasomaji na Wachangiaji wa Mada kwa maelezo yako.

 156. Siyi kaka: Mimi nilihitaji andiko la injili lenye kuonyesha kuwa, Bwana Yesu alitimiza sheria za Adamu na mkewe Pamoja na vijisheria vidogovidogo pekee. Mimi sikuhitaji maelezo ambayo hayajibu swali langu moja kwa moja, hebu twende kimaandiko na kiuhalisia zaidi. Kama hakuna andiko hilo katika injili, basi nakuomba usirudie tena kupotosha watu. Jambo la Pili, tazama sasa, uongo unakuzidi mpaka unajijibu wewe mwenyewe!!, eti unasema hivi” TORATI NI NENO LA JUMLA, NA MAANA YAKE NI “VITABU 5 VYA SHERIA, YAANI KUANZIA MWANZO HADI KUMBUKUMBU LA TORATI”. Umeona hapo?, Bwana Yesu naye alivyokuja akasema” NIMEKUJA KUTIMIZA TORATI YOTE….., Na kwa mujibu wa maelezo yako ,torati yote ni vile vitabu vyote vitano vya Musa, sasa sijui utauficha wapi tena uso wako wa uongo, unaokataa kwamba, zile mri kumi katika hivyo vitabu vya Musa hazijatimizwa!!!!!!!!. Jambo la tatu, ambalo hukulijibu, Mimi nilitaka kujua jambo hili kwa upande wa wasabato: Musa alitakasa dhambi kwa dhabihu za damu za wanyama katika torati, Lakini bwana Yesu katika injili, anatakasa dhambi zetu kwa damu yake mwenyewe, yaani kwa kumwaga damu yake isiyo na hatia, alifuta kabisa yale madai ya haki kwa kila dhambi na uvunjaji wa torati (amri kumi na vijisheria vidogovidogo vyote), ndipo akawa dhabihu ya wale wanaomuamini katika injili yake. Hii maana yake ni kwamba, zile dhabihu za damu za wanyama, zilitumika katika torati Pekee, na Pia, hii dhabihu ya damu ya kristo, imekuja kwa ajili ya injili yake pekee. Swali langu kwa ndugu Siyi ni hili: iweje wasabato mshike torati ya Musa, halafu mtumie dhabihu ya damu ya kristo katika utakaso wenu badala ya kutumia dhabihu za wanyama kama torati ilivyoagiza?, ninyi si mnasema kua, bwana yesu hajazifia wala kuzitimiza hizo amri kumi….sasa mbona hamfuati ule utaratibu wa hiyo torati, badala yake mnataka haki ya yule ambaye hamumuamini kua alizifia na kuzitimiza hizo amri kumi kwa ajili ya haki na utakaso wenu, limewezekana vipi hilo?!!!. Mwisho, kwakeli ninyi wasabato mnadanganyana sana kwa kua, nikweli kabisa kwamba, bwana Yesu alizitimiza hata hizo amri kumi kwa ajili yenu, ijapokua ninyi mnakataa: Sasa hebu ona ndugu Siyi, kama kweli una jicho la kuona ukweli wa biblia: Sheria zilizochongwa katika mawe ni zile amri kumi. Wana wa israel, walishindwa kabisa kuuangalia uso wa Musa, uliokuwa na utaji wa utukufu wa Mungu, Soma(kutoka 34:1). Sasa, katika injili kuhusu sheria hizo zilizotimizwa na bwana Yesu, twasoma hivi” MNADHIHILISHWA KWAMBA MMEKUWA BARUA YA KRISTO TULIYOIKATIBU, ILIYOANDIKWA SI KWA WINO, BALI KWA ROHO WA MUNGU ALIYE HAI, SI KATIKA ” VIBAO VYA MAWE” ILA KATIKA VIBAO AMBAVYO NI MIOYO YA NYAMA!!!!!. Soma( 2Wakorintho 3:3). Pia ukiendelea kulisoma zaidi mpaka chini kabisa andiko hilo, basi, utapata picha ya wazi zaidi kuhusu Musa katika zile amri kumi pale sinai, mpaka jinsi bwana Yesu alivyozitimiza hizo amri kumi ambazo Musa, alizipokea pale sinai. Lakini pia, katika ile( Warumi 7:7-8) , amri ya kutamani ni ile amri ya kumi katika zile amri kumi za sheria. Sasa, kama bwana Yesu alitimiza vile vijisheria vidogovidogo pekee, hiyo amri ya kumi ya kutamani, mbona Mtume Paul anaifafanua kua ni amri ya sheria iliyokua ni kioo cha kutuleta kwa kristo?!!! Ushahidi wa kimaandiko, upo mwingi mno kwamba, torati yote iliishia kwa kristo. Yatosha, kwaheri ndugu Siyi, usikasirike maana tunaelimishana tu, Mengine nimekusamehe kukuuliza… BARIKIWA.

 157. Ndugu lwembe, Asante kwa mawazo yako. Sasa hebu sikia: Ukiokolewa kwa neema ya kristo ndugu yangu, haimaanishi kwamba, wewe uishi hapa duniani kama vile malaika wa mbinguni, Ya kwamba eti uwezi kufanya dhambi tena, huna sheria au taratibu zozote za makatazo ya kukutiisha nk, hapana, ila unatakiwa, ukishaokolewa kwa neema ya kristo, uanze kulisikiliza neno la kristo, kulifanya na kuliishi sawasawa na Mapenzi yake, ndio maana Yeye mwenyewe akasema hivi” MAMA YANGU NA NDUGU ZANGU NDIO HAO WALISIKIAO NENO LA MUNGU NA KULIFANYA!!. Soma(Luka 8:21). Sasa tazama: Sheria ya dhambi na Mauti ni ile torati ya Musa yenye makatazo ya hukumu, lakini sheria mpya ya kristo yenye uhuru, ndio ninayoiongelea mimi kwamba, pamoja na kuokolewa kwetu kwa neema ya Mungu, ni lazima tutii injili ya bwana yesu, ili tuithibitishe haki ya Mungu(ile kweli) ,ndio maana hata bwana yesu alisema” sikuja kuitangua sheria ila nimekuja “KUITIMIZA”. Sasa, Sisi wakristo, tunaithibitisha sheria ya Mungu (amri kumi) katika injili ya bwana yesu, tukitii kwa njia ifuatayo:- ” (1)MPENDE MUNGU NA JIRANI YAKO: katika injili ya Yesu” Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote, Hii ndiyo amri iliyo kuu tena ni ya kwanza, na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii Mpende jirani yako kama nafsi yako.Soma(Mathayo 22:37-39). (2)USIABUDU SANAMU: Katika injili” Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu ikimbieni ibada ya sanamu, Soma(1Wakorintho 10:14)(1Yoh 5:21). (3)USILITAJE BURE JINA LA MUNGU: Katika injili” Yaani “Jina la Mungu ni lazima litukuzwe” Soma(Mathayo 13:16). (4) IKUMBUKE SIKU YA SABATO: Katika injili” Bwana Yesu akauliza hivi”Na huyu Mwanamke aliye wa ” UZAO WA IBRAHIMU” ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikumpasa “AFUNGULIWE KIFUNGO HIKI SIKU YA SABATO?, Soma(Luka 13:16), ukweli katika injili: Sisi ni “UZAO WA IBRAHIMU” Kwa hiyo, tunapokea ile ahadi ya Mungu kwa njia ya imani kupitia Yesu kristo, Mwokozi aliye ahidiwa, yaani bwana wa Pumziko la kweli, akitutoa katika mizigo ya magonjwa, umasikini, dhambi nk. Soma(Mathayo 11:28-30). (5) WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO: Katika injili: ” Waheshimu Baba yako na Mama yako, amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. Soma(waefeso 6:2-3). (6) USIUE: Katika injili” kila amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mnajua ya kua” KILA MUUAJI HANA UZIMA WA MILELE UKIKAA NDANI YAKE. Soma(1Yohana 3:15). (7-10) USISEME UONGO, USIZINI, USIIBE, USITAMANI: Katika injili” Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake, kwa maana tu viungo kila mmoja kiungo cha wenzake, Soma( Waefeso 4:25), na katika ile (1Wakorintho 6:9-10), Inasema hivi: ” Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu?, msidanganyike, washerati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala WAZINZI, wala wafiraji, wala walawiti, wala WEVI, wala WATAMANIO, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi!!!. Kwa hiyo ndugu lwembe, umekua ukinisingizia sana kwamba, mimi ninafanya makosa kutii amri ambazo bwana yesu amezitimiza katika injili yake, kosa langu hapo ni nini?, hao wengine wanao kunywa damu ya Yesu na kutii injili ya kristo, nao wanamakosa gani?, huoni kuwa, wewe usietii mafundisho ya bwana yesu, ndiye unaepotea, wewe unataka uishi kama malaika, kwa kisingizio kwamba wokovu ni kuishi burebure bila ya utiifu wa amri zozote za kufuata na kujitiisha katika maisha yetu…kwakweli hakuna maisha ya aina hiyo katika ukristo, labda wewe huwa uendagi kanisani kufundishwa jinsi ya kuishi maisha ya wokovu, ndio maana unataka kujiona kama mfarisayo asiye na kosa lolote, ambaye anaishi kama malaika. Kila jambo ni lazima liwe na utaratibu wake wa kikanuni ili tuweze kuwafundisha na kuwarithisha na watoto wetu, sasa wewe ukidai kua huna sheria za kristo, huna dhambi, tena umeokolewa bure na unaishi bure bila ya kanuni yoyote ya Kukutiisha na kukuongoza, basi wewe utakuwa ni malaika ndugu lwembe. Kuhusu mambo ya Yuda, kwakweli mimi nimeyasahau huko juu, tuwaachie wasomaji watayapima hayo tuliyo yaandika huko juu wao wenyewe. Ubarikiwe, ndugu yangu.

 158. Mhina,
  Kwanza, sheria zilizotimizwa na Kristo, ni zile ambazo Mungu alizianzisha baada ya Adamu kuanguka dhambini; “Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika” – mwanzo 3:21. Huu ulikuwa ni utaratibu wa kuchinja wanyama wa kafara alioanzisha Mungu kwa Adamu na mkewe na vizazi vyao vyote. Utaratibu huu, ulipaswa kufuatwa na kila mtu aliyeamini dini ya Adamu aliyoipokea kutoka kwa Muumbaji!! Wale waliokwenda kinyume na utaratibu huu, Mungu alizikataa ibada zao mbashala!! Watoto wa Adamu walifundishwa utaratibu huo vizuri japo mmoja aliuasi na matokeo yake sote tunayajua. “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde” Mwanzo 4:3-7. Utaratibu huo, tunauona unaendelea hadi kwa waisrael wakiwa na Musa jangwani, mpaka enzi za Kristo kabla hajabambwa msalabani. Uchinjaji huu wa kondoo, mbuzi, ng’ombe nk kwa ajili ya kufunika/kuondoa dhambi, ulikuwa ni kielezo cha kafara ya Kristo pale kalvarii!!Na haya siyo mawazo yangu ndugu yangu, ni maneno ya Mungu mwenyewe.

  Pili, TORATI ni NENO la JUMLA!! Na maana yake, ni vitabu 5 vya sheria yaani kuanzia Mwanzo hadi Kumbukumbu la TORATI lenyewe; vitabu vilivyoandikwa na Musa. Ndani ya vitabu hivi, kuna Amri 10 za Mungu; msingi wa maelekezo yote waliyopewa Adamu na mkewe kabla hawajaasi. Na kuna sheria za maagizo, taratibu mpya zilizokuja baada ya kuanguka kwao dhambini kama tulivyoona hapo juu!! Vyote hivi, kwa ujumla wake, vinajulikana kama TORATI maana viliandikwa kwenye vitabu hivyo vitano vya Musa. TORATI iliyokuwepo kabla ya dhambi (Amri 10), hizo ni za milele. Hata Yohana alipooneshwa hekalu la mbinguni(Kristo akiwa alishakufa tayari), aliliona Sanduku lililokuwa likitumika kubebea Amri 10 za Mungu enzi za Waisrael “Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana” – ufunuo 11:19. Hakuziona zile sheria ndogondogo za kafara zilizokuwa zikiwekwa pembezoni mwa Sanduku hilo, maana zenyewe, ziliishia msalabani tu. Kwa hiyo ndugu yangu Mhina, unapolitumia neno hili TORATI, ni vyema ukaliewa mipaka, mapana na urefu wake!! Biblia inaposema kuwa MTAZISHIKA AMRI ZANGU NA HUKUMU ZANGU”, ina maana kwamba, mtazitii Amri 10. Na mtu akivunja mojawapo, hukumu yake iko bayana, mwambieni atekeleze(alete mnyama wa kafara) au akishindwa kmleta, tekelezeni kwake(mpondeni mawe) mara moja!! Hayo ndiyo yalikuwa ni maisha ya wenzetu wa agano la kale. Kwetu mambo yamekuwa ni tofauti kidogo. Hukumu yetu ilishalipwa tayari. Hatudaiwi sisi!! Hakuna haja ya kwenda kutafuta mbuzi, kondoo n.k. wa kuchinja au hakuna hukumu ya kupondwa mawe, pale unapobainika umevunja amri za Mungu!! Kilichopo ni kumwangalia na kumwamini tu huyo aliyetulipia hilo deni la hukumu na kisha YEYE huturejesha kwenye UTII wa AMRI 10 za MUNGU. Tunaposamehewa bure, haturuhusiwi kutenda dhambi tena!! Hii ndiyo maana ya kuokolewa kwa Neema rafiki yangu (vitu vitu viwili tu muhimu) – imani na utiifu wa amri 10 za Mungu. Ukiwa na imani tu huku unavunja amri za Mungu, imani yako imekufa!! Ukiwa na utiifu tu wa sheria kimabavu bila ya kuwa na imani kwa Yesu, utiifu wako ni bure vilevile. Sharti vitu hivi viende pamoja, imani ikitangulia na utii wa sheria ukifuata kama matokeo ya imani na upendo wetu kwa YULE tunayemwamini -Kristo. Na hiki ndicho alichokidemonstrate Kristo wakati akishughulika na wadhambi, “… Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena”- Yohana 8:11. Unapoupokea msamaha wa Kristo bure, sharti uishi sawasawa na Neno lake!!
  Tatu, kama unaona kuna Wasabato huwa wanawasha mioto huko makwenu, jua kuwa hao ni wasabato ambao bado wanakua kiimani!! Ni wachanga!! Siku moja tu watakapoongoka, wataacha kupika au kuwasha mioto siku za Sabato. Kama ni majirani zako, endelea kuwakumbusha kuwa siku za Sabato, hawapaswi kuwasha moto!!

  Kwa hiyo, ndugu Mhina, huwezi ukavichanganya vitu vyote hivi viwili – Amri 10 za Mungu na Sheria za maagizo (zilizotuleta kwa Kristo), kwa kigezo cha kutumia neno TORATI. Watu watakucheka rafiki yangu!!
  Ubarikiwe sana.
  Sabato njema.
  Siyi

 159. Siyi,
  Unalalama bure, unaanza kuogopa mpaka kivuli chako mwenyewe.

  Ni wewe uliyeziita kuwa zile sheria ndogondogo kuwa ni za Musa. Ulisema hicyo ukiwa unamjibu Mhina.

  Nami nikakwambia kuwa Mungu aliyesema wana wa Israel watunze sabato ( ktk amri kumi) ndiye aliyesema mvunja sabato apigwe mawe.

  Ndo nikasema sasa inakuwaje hizo ndogo ziwe za Musa¿

  Ona hapa chini nakunukuu;

  “Torati yenye nguvu ya mauti –kifo cha kupondwa mawe, ilikuwa ni sheria ndogondogo za Musa zilizokuja baada ya dhambi!!”

  Watu wengi hapa tumekutaka uthibitishe au utupe andiko linalosema kuwa Yesu alikomesha tu sheria ndogondogo za kafara. Hujafanya hivyo badala yake unaongea tu tafsiri zako.

  Hebu imagine, kwa mfano mtu anapokwambia umpe andiko lenye kuagiza watu watunze sabato kabla ya dhambi, unampa Mwa 2:1-3, atakuona u mtu wa namna gani kama si mpuuzi?

  Hiyo mistari inasema kuwa Mungu alipumzika siku hiyo, akaibariki na kuifanya takatifu.

  Hakuna amri yoyote katika hizo tungo za mistari hiyo. Na wala hatu mahali popote Adam anapumzika siku hiyo, wala Ibrahim, wala Isaka, wala Yakobo, ispokuwa wajukuu wa Yakobo baada ya kutoka Misri, baada ya amri kumi kuwa zimetoka.

  Kwa hiyo Siyi unapojibu maswali kwa namna huo kwangu upuuzi na kupotezeana muda.

  Tunapokuuliza utuonyeshe ni wapi biblia inaonesha kuwa waliomwamini kristo waliitwa wasabato, halafu wewe unaanza kuleta ngonjera, huo kwangu naona ni upumbavu au wa makusudi au wa kutokujua.

  Kitu kingine, kuna mahala fulani umesema Yesu alitimiliza yaani alikomesha zile torati za kafara.

  Point yangu hapa ni kwamba umeelewa vema kuwa kutimiliza ni kokomesha kitu.

  Nitakushangaa sana kesho na keshokutwa ukianza tena kuniletea maana za ajabuajabu za neno kutimiliza.

  Siyi, mimi katika kujadili huwa nauangalia mwelekeo wa mtu kiufahamu kisha najadili nae accordingly.
  Eg; kwenye mjadala wetu wa kuokoka duniani nisingeweza kuleta mstari unaosema kuokoka in future, halafu nokausimamia kama mstari wa kuthibitisha kuwa tunaokoka tukiwa duniani. Hiyo ni kwa sababu nilishajua kuwa wewe unaamini kuokoka in future.

  Sasa wewe kwenye mijadala akili ya namna hiyo huna, ndio maana unaweza kuleta Mwa 2:1-3 kuthibitisha kuwa Mungu aliamuru watu wake sabato kabla ya dhambi.
  (Ukielewa nilichosema hapo kitakusaidia).

  Kama unadhani kristo kuwa Bwana wa sabato maana yake ni hiyo, hebu niambie, Bwana wa siku ya Jumatano ni nani.

  Kuna point hufika mimi hukuona hauko-independent kabisa kiufahamu. Bali huwa unaamua tu kusema vitu ambavyo ni msimamo wa dini yako na walimu wako.

  Angalia, kila mtu unayejàdili nae aghalabu hukulaumu kwa jambo lilelile, hata kama ni kwa maneno tofauti.

  Angalia Mhina anavyokulaumu, Angalia Pendael anavyokulaumu, Angalia Lwembe anavyokulaumu, juu ya style yako ya kudadavua mambo.

  Mwisho, siku ya sabato kidunia huwa haihusishi dunia nzima at once. Kwa hiyo kukiwa na tukio linalotakiwa kufanyika siku ya sabato kidunia, kuna watakaotangulia kulifanya na wengine watafuatia the next day.

  Lakini pumziko hilo likiwa la rohoni(of course kama ilivyo sasa hivi) wamwaminio kristo wote duniani hulishiriki simultaneously!

  Siyi, talk sense usilalame tu!

 160. Mhina ndg yangu,

  Naona unazunguka saaana na Maandiko, kisa? Nawe, kama akina Siyi tu, unashindwa kuyaamini Maandiko; Sheria unazitaka (ila ziwe 9 tu!), na Neema nayo unaitaka! Isome mwenyewe kauli yako hii:
  “”Sisi hatupo tena chini ya sheria ya dhambi na mauti, sisi tupo katika sheria mpya ya kristo ya upendo yenye uhuru LAKINI, tukiishi sawasawa na mapenzi Ya mungu, yaani sawasawa na makatazo yake.”” (Unaiona hiyo ‘lakini’ yako?)
  Hayo makatazo ya Mungu unayapata kutoka wapi kama si Sheria? Kwanza Uhuru wenye makatazo ndio kitu gani?? Makatazo ni hizo Dhambi ambazo ndg yake ni Hukumu, hiyo ndio inaitwa Sheria, na inawahusu watu wasio na haki!!!

  Mfano wa Yuda umeupindua sana mpaka inashangaza! Nilichokisema ni kwamba Yuda alikuwa na vipawa hata akaombea wagonjwa, lakini alikuwa mwizi wa sadaka Kanisani; nikidhani kwamba unajua kuwa mpaka Yuda anajinyonga, alikuwa hajazaliwa kwa Roho! Ujumbe niliokuwa nakufikishia, ni kwamba kama hautajisogeza kwa kuyaamini Maandiko, basi utakwamia hapo ulipo, na unaweza ukaishia kuiba sadaka kama Yuda au akina Anania na Safira, kwa sababu jambo la Utii wa Sheria linahusiana zaidi na kuogopa ukali wa Hukumu kuliko upendo, na wengi wanazitii Sheria kwa kuogopa kuchomwa moto na si kwamba eti wanampenda Mungu!!!

  Pia naona umeshindwa kabisa kuielewa maana halisi ya ‘Uhuru’ unaoutangazwa ktk Injili, kwani kila unapotajwa uhuru huo, mawazo yako hukimbilia kudhani kwamba mambo ya Utumwa wa Dhambi, huko kuwa mzinzi au mwizi au muongo ndio uhuru wenyewe, ndio maana lazima uuambatanishe na utii wa sheria kuuongoza; dalili kwamba ungali unapambana na dhambi, ishara ya kuwa bado u chini ya Torati, nawe hujui!

  Pia elewa kwamba, ktk mwendo wa ukristo, hufikia hatua ambayo Dhambi huondelewa, si kusamehewa, hapana huondolewa; basi Dhambi inapoondelewa, Sheria haiwezi kubakia; itabaki imshitaki nani, na kuhusu nini hata hukumu iwepo, ilhali Dhambi haipo?!! Sheria ikiisha kuondoka, utatii nini? Huo uzito ulionao moyoni mwako, unaokuzuia kulipokea Neno zuri la Mungu, ni dalili ya kwamba hujapata Ondoleo la Dhambi, hujaipokea kikamilifu Dhabihu iliyotolewa kwa ajili yako ili upate hilo Ondoleo la Dhambi, shina lake ling’olewe kutoka moyoni mwako; ndio maana bado unashitakiwa na mambo hayo ya uzinzi, uongo, uasherati, wizi wa fungu la kumi nk, mambo yanayoidhihirisha hali uliyonayo, roho inataka lakini mwili ni dhaifu!!

  Nikuulize jambo, iwapo jiji la Dar es Salaam lingekuwa ni kambi ya Watakatifu, je, kungejengwa vituo vya polisi, mahakama na magereza yake?

  Ktk Amri 9 unazozitii, iko moja inayosema “Usiue”; sasa hebu nawe niambie, utaitii vipi Amri hii na wakati huo huo moyoni mwako uwe umeridhia kuula mwili na kuinywa Damu ya Kristo (Yn 6:55-56)?? Pia niambie, kwa hao ambao walikubali kuula huo mwili na kuinywa hiyo Damu yake, Je, Sheria au hiyo Amri, ingali ina nguvu kwao?

  Gbu!

 161. Ndugu Siyi, asante kwa majibu. Kwanza, nakuomba unionyeshe maandiko katika biblia, yanayosema kua, Bwana Yesu alitimiza, sheria za Adamu na Mkewe Pamoja na vijisheria vidogovido na vijikafara vyake. NAOMBA HILO ANDIKO TAFADHALI. Pili, Wewe unayapotosha sana maandiko kwa kua, unatafsiri kwa mawazo yako. Tazama, mimi huko juu nilikwambia ukweli huu: AMRI KUMI + SHERIA ZOTE NDOGONDOGO + HUKUMU ZAKE = TORATI YOTE ALIYOITIMIZA BWANA YESU. Kwa hiyo, bwana Yesu aliitimiza torati yote, kama alivyosema, lakini ni kwanini wewe, zile amri kumi unazifanya kua sio sehemu ya torati, hivi umefundishwa na nani biblia wewe?!!!!!!!. Lakini hata hivyo, ukiamini kua, bwana yesu hakutimiza zile amri kumi, basi lazima uelewe kua, wewe bado unaishi na kushika torati ya Musa na hukumu zake kama Mungu alivyoamuru, ndio maana mimi kwa sababu ninajua utaratibu wa kuishi chini ya torati, nilikuuliza kwamba, mbona wasabato mnazivunja amri za Mungu bila ya kua na utaratibu wa kuadhibiana sawasawa na torati inavyoagiza?….lakini kwa sababu wewe hujui maagizo ya torati, ukaona kama ninautumia ukristo wangu vibaya kwa kutowashauri wasabato wenzio vizuri!!!. Hapa kazi yetu ni kuchimbua ukweli unavyotakiwa sawasawa na maagizo ya Mungu, sio sawasawa na ushauri wa Mhina. Mungu anaposema” MTAZISHIKA AMRI ZANGU NA HUKUMU ZANGU” anakua amemaanisha kisawasawa, kamwe hamaanishi eti mpaka Mhina na ukristo wake akushauri, mimi sio mwokozi wa wasabato. Ukweli upo palepale kwamba, watu wote wanaoishi chini ya torati, wanakua pia chini ya hukumu na laana za Mungu mwenyewe(sio hukumu za Mhina), hebu soma andiko hili ndugu Siyi. (Galatia 3:10). Kama Mwenyezi Mungu alitoa maagizo yake katika amri kumi kwamba: Mzinifu auwawe, Mwizi akatwe mkono, anaefanya kazi siku ya sabato auliwe, Soma(kutoka3:14) nk, hapo wasabato mtapataje kupona, wakati ninyi mnatii torati ya Musa badala ya injili ya bwana yesu?, kushika amri kumi kama alivyozipokea nabii Musa, hakuwezi hata siku moja, kukufanya uwe ni Mwanafunzi wa bwana yesu, Soma(Yohana1:17) + (luka 16:16). Wasabato mnadanganyana sana kwa kua, huwezi kupata haki ya kristo na kutumia kafara yake kwa jambo ambalo, bwana yesu hajalifia wala kulitimiza, hebu ndugu siyi fafanua, huo uhuru wenu na haki yenu, vilizaliwa kwa njia gani kwa kriso?….haki ilipatikana kwa njia ya msalaba pekee, pale bwana yesu alivyoifia torati yote, na kusema” imekwisha”. Tazama, biblia inasema” YEYE MWENYEWE ALIZICHUKUA DHAMBI ZETU KATIKA MWILI WAKE JUU YA MTI, TUKIWA WAFU KWA MAMBO YA DHAMBI, TUWE HAI KWA MAMBO YA HAKI, NA KWA KUPIGWA KWAKE MLIPONYWA!!!. Soma(1Petro2:24). Usipoamini kua, bwana yesu alitimiza torati yote kwa ajili yako, basi inakubidi kile asichokitimiza kama ni hizo amri kumi inakubidi uzitafutie haki yako na kafara yako wewe mwenyewe, ndio maana wana wa israel walitumia dhabihu ya wanyama kwa sababu mwokozi bado alikua hajaja!!. Tazama: Wana wa israel katika sabato, waliagizwa na Mungu wasitoke mahali pao, Soma(kutoka 16:29), Wao walitakiwa kutotembea mwendo mrefu siku hiyo, walitembea umbali mfupi sana na hatimaye urefu ule ukaitwa “MWENDO WA SABATO” Soma(Matendo 1:12), lakini wasabato wa leo, siku za j,mosi mnatembea mwendo wa zaidi ya kilometa moja kwenda makanisani, je, hiyo ndiyo sabato ya kweli?, wakinadada huku kwetu kila j,mosi wanawasha moto ili wapike pure!!…je, hiyo mnayoitekeleza ndiyo sabato ya kweli ndugu zangu?!!, Soma(kutoka 20:10,35:2,3). Jambo jingine, kusema kua, umeokolewa kwa kushika vitu viwili ambavyo ni kuamini na kushika sheria, ni makosa makubwa mno, tena, hilo sio fundisho la biblia kabisa, maana unaonekana kujaribu kujihesabia haki wewe mwenyewe kwa matendo ya kushika sheria!. Ndugu siyi, ni wapi biblia inaposema, tumeokolema kwa vitu viwili, yaani kushika sheria na imani?, hili andiko pia nitakuomba unionyeshe kwenye biblia…ni mahali gani?, biblia inasema kua, tumeokolewa kwa neema pekee, Mambo ya kutii sheria ya kristo, yanafuata baadae kama njia sahihi ya kumuishia Mungu sawasawa na neno lake, ili tuthibitishe ile imani na upendo wake aliotupa. Lakini kwa wasabato inawezekana jambo ulilonielezea likawa ni sawa kwa sababu ninyi bado ni wale wagalatia wanaoshika injili na sheria ya Musa kwa wakati mmoja!!!, ndio maana pia usema kua, haiwezekani kutenganisha torati ya Musa na injili ya bwana yesu, na wakati biblia inasema” torati ilikuja kwa mkono wa Musa ila neema na kweli zimekuja kwa njia ya kristo!!!. Pia, biblia inasema kua, nguvu za torati ni dhambi na nguvu ya dhambi ni mauti, maana yake ni kwamba, ukivunja zile amri kumi kwa kuiba,kuzini,kuvunja sabato unayoitumaini mwenyewe kwa juhudi zako nk, mwisho wa Mambo hayo ni Mauti, kama Mungu mwenyewe alivyoagiza, Pia soma( Warumi 7:7-8), lakini jambo la ajabu, ndugu Siyi anabadilisha neno la Mungu kwa kusema, eti nguvu za torati ni vile vikafara vidogovidogo na vipengele vyake!!!!!!. Mwisho, Sisi wote ni lazima tuwe wahudumu wa agano jipya, tulimpokea bwana yesu ili tuwe wahudumu wa agano jipya, sio wahudumu wa torati!!. Soma(2 Wakorintho 3:6)….ukibaki kua, mhudumu wa torati, itakubidi pia, ujitafutie kafara yako na haki yako, kwa kua, bwana yesu hakua haki na kafara ili watu waendelee kushika torati, ila alitukomboa kutoka kwenye laana za torati(amri kumi) ili atuweke mbali na dhambi na Mauti…haya ndugu siyi, jana sikuwepo, nilishinda kazini, lakini leo nitakuwepo, twende kazi…

 162. Sungura,
  Kwanza, hayo si maneno yangu.Ni maneno niliyoyanyambua kutoka kwenye Biblia!! Si maneno ya kufikirika wala propaganda!! Ni ukweli wenyewe, ambao hata malaika akishuka kutoka mbinguni, hawezi kuukanusha!! Wewe kama unafikiri ni maneno ya kufikirika tu, endelea na fikra hizo. Hatari na usalama wa maisha yako, uko mikononi mwako mwenyewe!!
  Pili, amri ya kushika Sabato kabla ya dhambi, ni mwanzo 2:1-3. Soma!! Kuhusu la kukuonesha kuwa Kristo alikomesha tu amri ndogondogo na si Amri 10, hilo nilishalifanya tena nikakuleta hadi tofauti zake hivi majuzi tu kwenye maada hii https://strictlygospel.wordpress.com/2012/06/23/sababu-za-wakristo-kuabudu-jumapili/#comment-38328, mchango wangu wa tarehe 04/03/2015, nikijibu maswali ya namna hiihii!! Tena nilikutahadhalisha, usome between lines!! Kama husomi mapachiko ya miitiko ya maswali unayouliza kila mara, nakushuri urejee hapo juu kwenye link tajwa. Kwa sasa sirudii kusema jambo ambalo nilishalisema mara nyingi tu tena nikalirudia majuzi tu!! Sifanyi hiyo biashara!!
  Tatu, ni kweli hakuna amri ya musa, zote zilikuwa ni za Mungu na mwanzilishi wake ni Mungu. Hayo yote nimeyesema huko kwenye hiyo link. Kwa vile husomi, ndiyo maana unaendelea kuibuka kila siku na maswali yaleyale!! Nenda kasome hapo juu kwenye link husika!!
  Nne, kama utatanguliza fikra na mawazo potofu kuwa kila linalosemwa na wenzako walio kinyume chako kimtazamo ni UJINGA na UPUUZi, nachelea sana kusema kama wewe kuna siku utayaamini hayo wayasemayo licha ya kuyathibitisha kwa kila hali kwenye maandiko!! Utaendelea kuwa mkavu tu!! Na kimsingi, nikushauri pia kuwa, ukiwa na kauli za namna hiyo, utavunja watu mioyo ya kuwa wanajibu hoja zako!! Ni mbaya sana kumdharau mtu kabla hajatenda!! Na sidhani kama huo ndiyo ukristo unaojifunza kanisani kwako bro!! Kimsingi unahitaji mabadiliko. Sote tuna madhaifu na tunahitaji mabadiliko, lakini ni jambo jema kushauriana japo sote ni wadhaifu!!
  Tano, Biblia inasema kuwa Yesu aljiita mwenyewe kuwa ni Bwana wa Sabato, siyo mimi. Hakujiita kuwa ni Bwana wa jumapili!! Kama ni mawazo ya kijinga, basi yalikuwa ni ya Yesu!! Kama ni kutotumia hiyo cooommmooooosenseeeesss unayosema, basi Yesu alianguka kwa hilo!! Kama kufikiri kinyume na kauli ya Yesu, ndio akili, wewe songa mbele!! Tangu mwanzo, YEYe aliitunza, Sabato, Akaviagiza viumbe vyake vyote kuitunza Sabato, na katika agano jipya, kajitambulisha kwa title hiyohiyo!! Na wakati akijitambulisha kwa title hiyo, hakuwa anaenda kusali jumapili sinagogini!! Wewe leo unamuita mjinga!! Wafusi wake pia nao wajinga!! Poa!! Wewe endelea na hizo logic zako tu!! Sisi tunasikiliza UJINGA na kufuata UTAHIRA wa Kristo ulionenwa ndani ya Maandiko matakatifu!! Tumeamua kuwa washamba pamoja na Yesu, kuliko kuitwa wenye akili wa ibilisi!!
  Sita, ukiwa na akili yenye shingo ngumu kama ya kwako, usitarajie hata siku moja kuja kuielewa Biblia!! Maana wewe ni too much know!! Hufundishiki!! Sasa lini utakuja kuielewa Sabato. Acha sisi tulioamua kushuka na kuwa kama watoto, maana kwa kufanya hivyo, ndipo kuna ahadi ya kuurithi ufalme wake!! Na utakuwa unaona watu wanajichanganya kumbe unayejichanganya ni wewe mwenyewe!!
  Saba, kama umeamua kweli kujifunza na kujadiliana na watu hapa mtandaoni, ni vyema ukawa a good listener!! Ukajibu hoja za watu bila ya kuzipindisha!! Ukikosa jawabu, kukaa kimya nayo ni sehemu ya hekima kaka!! Ukweli wa Maandiko, utabaki kuwa palepale hata kama sisi wanadamu tutakuwa na logic zetu pinzani!! Kamwe hatutambadilisha Mungu!!
  “Jitahidi(soma) kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” – 2timothy 2:15.
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 163. Mmhh Siyi,

  Haya ni maneno yako;-

  Kwa maelezo mengine, enzi za akina Musa, kulikuwa na sheria ndogndogo shurutishi za kukufanya uishi kwa mujibu wa sheria za nchi-katiba!! Yesu alipokuja, aliondoa tu zile sheria ndogondogo shurutishi na kuacha ile sheria kuu ya nchi ikiendelea palepale kama ilivyokuwa mwanzo!!

  Haya ni maneno ya kufikirika Siyi, unafikiri hicho ndo alichokifanya Yesu, huna uhakika wowote.
  Unaongea tu propaganda zako.

  Hebu thibitisha pasi na kuacha punje ya shaka haya yafuatayo:-

  Siyi, hebu nioneshe mahali ambapo kuna amri ya kushika siku ya sabato kabla ya dhambi!

  Nioneshe pia mahali panaposema kuwa kristo alikomesha tu amri ndogondogo shurutishi.

  Huwa sioni kama kuna amri za Mungu za Musa, zote zilikuwa amri za Mungu. Musa hakufanya jambo bila kuagizwa na Mungu.

  Eg; Amri ya kukumbuka siku ya sabato ilitolewa na Mungu, lakini pia sheria ya afanywe nini aliyeivunja hiyo amri ilitolewa na Mungu, siyo Musa. Sasa hapo wapi kuba amri ya Mungu na ya Musa?

  Na hizo ndogndogo maana yake nini, ni zile nje ya amri kumi? Amriumi ndo zinaendelea kushika hatamu?

  Lakini kuna maulizo na fikra zingine sina jinsi ya kuziita badala ya kuziita za kijinga.

  Unapouliza swali kuwa ni wapi Yesu alijiita ni Bwana wa J’pili kwangu hilo ni ulizo la kijinga ambalo mtu kauliza bila kutumia common sense.

  Kwanza alisema yeye ni Bwana wa sabato coz the topic on table ilikuwa ni sabato. Sasa unategemea vipi angesema tu kuwa yeye ni Bwana wa J’pili kutoka hewani? Common sense.

  Lakini inaonekana hata maana ya yeye kuwa Bwana wa sabato hujaielewa.

  Kuwa bwana wa:- maana yake ni kuwa mtu huyo ni mkuu kuliko hicho ambacho anafanyika kuwa bwana juu yake. Hivyo kristo ni mkuu juu ya siku zote za wiki. Haikusemwa J’2 wala J’3 hapo coz mjadala haukuhusu siku hizo.

  Kitu kingine, tofautisha kati ya sabato na siku ya sabato. Hivi ni vitu tofauti.
  Sabato is all about rest/pumziko, na siku ya sabato ni siku ya kupumzika.

  Unapoongelea pumziko unapaswa kukumbuka maneno ya Yesu aitapo kuwa njoni kwangu msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nitawapumzisha.

  Halafu jiulize kama hapo alikuwa anaongelea siku ya kupumzika au pumziko lenyewe. Ambalo pumziko hilo kinsibgi ni la milele na ni la rohoni.

  Nilishawahi kukwambia Siyi, kuwa hakutakuwa na usiku wala mchana, hivyo utajuaje kuwa leo ni siku ya sabato imefika ili upumzike?

  Agano jipya halijaleta siku ya kupumzika, limeleta pumziko lenyewe. Tulioitikia huo mwito wa Yesu tumepata hilo pumziko.

  Kwenye hii mada, nyi ambao mmekuwa wachangiaji wakuu kuna vitu wote mnajichanganya na vingine of course mnapatia.

  Tatizo mnaandika mno, until u mnajikuta mnajichanganya wenyewe!

 164. Mhina,
  Nakushukuru kw amaswali yako ndugu yangu.
  Naomba nikujibu haraka na bila ya kupoteza muda
  Maswali
  1. Hivi wasabato mnatarajia kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa haki ipatikanayo kwa njia ya kumuamini bwana yesu pekee au kwa haki ipatikanayo kwa kutii kikamilifu mahitaji yote ya amri kumi za Mungu (sheria za Mungu?

  Jibu
  Ulivyoyaweka ni sahihi kabisa!! Tutahesabiwa haki kwa kumwamini Kristo. Tukishaamini kuwa ametuweka huru, hatuna budi sasa kuishi sawasawa na Amri zake 10 kwa msaada wake, maana kwa nguvu zetu tu, hatuwezi kuzitii isipokuwa kwa nguvu zake!! Na nguvu zake, zimejificha kwenye zile amri kuu mbili –mpende Bwana Mungu wako…..na mpende jirani yako…. Maana katika “… pendo ndilo utimilifu wa sheria” – Warumi 13:10. Huwezi kumpenda Kristo, halafu ukaasi sheria zake –amri 10, hata kama ni moja!! Huko ni kudanganyana kweupe rafiki!!

  a. kama ni kwa haki ipatikanayo kwa neema ya Mungu katika yesu kristo, kwanini wewe unakataa sasa kua, bwana yesu aliitimiza haki yote katika zile amri kumi ili akuokoe wewe na kukupa hiyo haki yake itakayo kuletea ile neema ya Mungu?

  Jibu
  Neema maana yake, ni upendeleo kwa mtu asiyestahili!! Kile alichokifanya Kristo kwetu, ni kutulipia lile deni la dhambi ambalo hatukuwa na uwezo nalo kulilipa wenyewe!! Alipolipa hilo deni, hakutuambia sasa eti tuko huru kuendelea kutenda dhambi zingine!! Hasha!! Alituasa tuishi sawasawa na sheria zake zote –Amri 10. Kwa hiyo, hatutaokolewa kwa kumwamini Yesu tu, huku sheria tukiziweka pembeni!! Tutaokolewa kwa kumwamini Kristo –kuikubali kafara yake pale msalabani na kisha kuishi sawasawa na amri zake!! Aidha, hatutaokolewa kwa kushika Amri 10 tu!! Hilo halipo!! Tutaokolewa kwa vitu viwili – a. kumwamini Yesu na b. kuzishika Amri zake 10. Nje ya hivi vitu viwili, hakuna wokovu Mhina!!

  (b) kama mnahesabiwa haki kwa kutimiza mahitaji yote ya Amri kumi za Mungu, bwana Yesu anahusika vipi tena, kuwa ni kafara yenu, na wakati yeye hakutimiza zile amri kumi ili awe kafara ya hizo amri?

  Jibu
  Yesu hakuja kutimiliza/kukomesha Amri 10. Yesu alikuja kutimiza sheria zilizokuja baada ya Adamu na mkewe kuasi pale bustanini!! Amri 10, zilikuwepo hata kabla ya uasi wa Adamu na mkewe!! Kwa hiyo, ni vyema ukaelewa kabisa kuwa, Yesu hakuja kukomesha Amri 10!! Kilichokomeshwa ni sheria za maagizo alizozianzisha Mungu mwenyewe baada ya mwanadamu kuasi!! Torati ya Amri 10 haina uhusiano wowote na torati ya kafara!!

  (c) iweje pia, wasabato wa leo mnaivunja sabato yenu waziwazi kwa kutembea umbali mkubwa siku ya sabato, kuzini, kuiba, kusema uongo nk, bila ya kua na utaratibu wa kuadhibiana, wakati mnasema sheria zile hazijatimizwa na bwana Yesu, isipokua ziko vilevile tangu nyakati za Musa, bwana Yesu katika hali hiyo, anakuaje tena ni mkombozi wenu, wakati yeye hajazifia hizo amri kumi ili awe kafara yenu.

  Jibu
  Kutembea umbali siku ya sabato, siyo dhambi!! Kama una aya yoyote inayosema hivyo, nisaidie na mimi nitafurahi kujifunza. Pili wale wasabato wazinzi, wezi, waongo n.k., unaowasema, nafiki ni vyema kama ungewaona, ukawasaidia kwanza, kabla ya kuwashuhudia hapa kwa mabaya!! Sina uhakika kama dini yako inakufundisha kuwa ukiona jirani yako, anaanguka, umcheke na kumshuhudia kwa ubaya badala ya kumsaidia kama mkristo mwenzake!! Saidia unaowaona wanaanguka rafiki badala ya kuwaponda!! Hata hivyo, uzinzi, wizi n.k., huo ni udhaifu wa mtu mmoja mmoja!! Ndani ya mkungu wa nazi, unaweza kukuta ndizi zingine zimewiva na zingine bado ilhali ziko kwenye mkungu huohuo mmoja!! Hata Yesu, alikua na mitume wengine wezi, wauaji, na wengine walikuwa ni waaminifu!! Miisho yao wote, tunaifahamu!! So usishangae kuona bado kuna wafedhuli ndani ya kanisa!! Hao wataendelea kuwepo tu hadi Yesu arudi, na nina imani hata kwenu, watu wa namna hiyo wapo ndani ya kanisa. Taratibu za kushughulika na watu kama hao ndani ya kanisa, tunazo tena nzuri sana!! Ukiona mtu hajashughulikiwa, jua kuwa hajajulikana kwenye kanisa!! Hivyo, msaidie wewe unayemuona kwa sasa kabla ya kanisa kumuona na kumchukulia hatua kwa mujibu wa mathayo 18.

  (d) biblia inasema” ikiwa kwa neema, haiwi tena kwa sheria. Sasa, mbona wasabato wanataka kupokea neema na kutimiza haki ya amri kumi kwa wakati huohuo.

  Jibu
  Huwezi kuitengenisha NEEMA na AMRI 10!! Ni pande mbili za shilingi moja!! Sheria iliyotimilizwa ni ile ya kafara na vipengele vyake vyote, ndio maana leo hatuchinji tena wanyama wa kafara wala kufanya sabato za miezi, miaka n.k. Hizo ndizo sheria zilizotimilizwa/komeshwa!! Na ndizo zilizotuleta kwa Kristo!! Amri 10, hazikutuleta kwa Kristo, maana zenyewe zilikuwepo hata kabla huyo Kristo (muumbaji), hajakorofishana na wanadamu!!

  d. Nb: nimegundua kua, wasabato hawaelewi maana ya kafara. Kafara ya kristo ni kutufungua katika vifungo vya sheria za Mungu (amri kumi). Hata wale wanyama wa dhabihu, walitolewa kwa ajili ya kufunika ile nguvu ya torati (amri kumi). kwa kua, nguvu ya torati ni dhambi. Sasa, swali la mwisho: kwanini wasabato wanamtaja bwana yesu kua ni kafara yao na wakati hakuzifia wala kuzitimiza hizo amri kumi ili kuvunja ile nguvu ya torati?.

  Jibu
  Nguvu ya torati hapo, ni nguvu ya torati za kafara na vipengele vyake!! Siyo torati ya amri 10 kaka!! Hapa ndipo tunawaacha mlio wengi!! Mnadhani kuwa, torati yenye nguvu ya mauti, ilikuwa ni amri 10. Hasha!! Torati yenye nguvu ya mauti –kifo cha kupondwa mawe, ilikuwa ni sheria ndogondogo za Musa zilizokuja baada ya dhambi!! Kabla Adamu hajaasi, sheria hizo ndogondogo, hazikuwepo, vinginevyo, Adamu angepondwa mawe!! Nguvu ya amri 10, ilikuwa ni kumtenganisha mwanadamu na Mungu MILELE (kwa kifo cha siku zooote), jambo ambalo Mungu hakulipenda!! Leo ukiwa muasi, utakufa, lakini kuna kifo kile cha pili cha kukutenga na Mungu milele zote. Kwa hiyo, Amri 10, zina nguvu ya kifo kwenye mauti ya pili. Sheria za kafara, zilikuwa na nguvu kwenye mauti ya kwanza – ya kupondwa mawe!!

  Ngoja nikuachie hapa huenda nitakuwa nimetoa mwanga kwa kiasi fulani ili uingie mwenyewe kuchimba na kujua uhalia wa mambo haya!! Karibu sana rafiki.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 165. ndugu siyi, Mimi najiona ninaandika mambo mengi ya maana kwako lakini kamwe hayakusaidii. Basi naomba tuyaache kama yalivyo hayo mambo ya huko juu, isipokua mimi ninakuomba unisaidie kunijibu swali langu kama lifuatavyo: Hivi wasabato mnatarajia kuhesabiwa haki mbele za Mungu kwa haki ipatikanayo kwa njia ya kumuamini bwana yesu pekee au kwa haki ipatikanayo kwa kutii kikamilifu mahitaji yote ya amri kumi za Mungu (sheria za Mungu? (a) kama ni kwa haki ipatikanayo kwa neema ya Mungu katika yesu kristo, kwanini wewe unakataa sasa kua, bwana yesu aliitimiza haki yote katika zile amri kumi ili akuokoe wewe na kukupa hiyo haki yake itakayo kuletea ile neema ya Mungu? (b) kama mnahesabiwa haki kwa kutimiza mahitaji yote ya Amri kumi za Mungu, bwana Yesu anahusika vipi tena, kuwa ni kafara yenu, na wakati yeye hakutimiza zile amri kumi ili awe kafara ya hizo amri? Hapa ninamaana kua, bwana Yesu hawezi kua kafara ya sheria ambazo hajazitimiza wala kuzifia kwa ajili yake, ndio maana biblia inasema kua, ikiwa kwa neema haiwi tena kwa sheria. Kua kafara maana yake ni kukifia kitu ili kiwe huru. Soma kwa makini sana ( Warumi 7:1-4). (c) iweje pia, wasabato wa leo mnaivunja sabato yenu waziwazi kwa kutembea umbali mkubwa siku ya sabato, kuzini, kuiba, kusema uongo nk, bila ya kua na utaratibu wa kuadhibiana, wakati mnasema sheria zile hazijatimizwa na bwana Yesu, isipokua ziko vilevile tangu nyakati za Musa, bwana Yesu katika hali hiyo, anakuaje tena ni mkombozi wenu, wakati yeye hajazifia hizo amri kumi ili awe kafara yenu. (d) biblia inasema” ikiwa kwa neema, haiwi tena kwa sheria. Sasa, mbona wasabato wanataka kupokea neema na kutimiza haki ya amri kumi kwa wakati huohuo. Nb: nimegundua kua, wasabato hawaelewi maana ya kafara. Kafara ya kristo ni kutufungua katika vifungo vya sheria za Mungu (amri kumi). Hata wale wanyama wa dhabihu, walitolewa kwa ajili ya kufunika ile nguvu ya torati (amri kumi). kwa kua, nguvu ya torati ni dhambi. Sasa, swali la mwisho: kwanini wasabato wanamtaja bwana yesu kua ni kafara yao na wakati hakuzifia wala kuzitimiza hizo amri kumi ili kuvunja ile nguvu ya torati?. Mimi nikuache unijibu viswali hivi bwana siyi, halafu tuendelee, lakini kwa mfumo huu wa maswali na majibu ili tusipoteze muda kwa mambo ambayo sio maada yetu. Nisaidie kunijibu ndugu yangu, labda na mimi naweza nikakuelewa na kua msabato mwezio, uwezi jua bana!!!. Ubarikiwe.

 166. @ Mhina,
  Kwanza, Duuu, nimeshtuka kuniambia kuwa nimeandika mambo mengi ya uongo!! Lakini nakuona umenichomekea kaswali kwa ndani ukasema, “Je, ndugu Siyi, sheria hiyo ya kutoa talaka alioiandika Musa ilikuhusu na wewe?” mmh, kama ningezaliwa enzi za Musa, zingenihusu, maana ningekuwa na hali ileile ya uasi ambao Israel walitoka nayo Misri!!
  Pili, hebu nisaidie na mimi dhana nzima ya sheria ya dhambi na ile sheria ya mauti!! Hivi ni vitu viwili tofauti?? How? Au vina ufanano?? How?
  Tatu, umesema kuwa “Sisi hatupo tena chini ya sheria ya dhambi na mauti, sisi tupo katika sheria mpya ya kristo ya upendo yenye uhuru lakini, tukiishi sawasawa na mapenzi Ya mungu, yaani sawasawa na makatazo yake. Huko ndiko kuithibitisha sheria ya Mungu kwa hiyo imani yetu, tazama (warumi 8:4) (warumi 3:31)”
  Maelezo yako haya, ni sawa na mtanzania yeyote anayeishi kwa kufuata sheria na taratibu zoote (bila shruti), hatimaye huonekana kana kwamba, kwa mtu huyo, sheria ya nchi, haina nguvu kwake!! Umesema kuwa tuko huru, lakini hapohapo, ukasema tena kuwa tunafuata makkatazo (sheria) yake ili tudhihirishe upendo wetu kwake!! Kimsingi huna tofauti na huyo Mtz!! Kushindwa kutambua kuwa, Neema aipatayo ya kutii sheria bila shuruti, haimpi fursa hata chembe ya kuzivunja sheria zilizopo!!! Kwa maelezo mengine, enzi za akina Musa, kulikuwa na sheria ndogndogo shurutishi za kukufanya uishi kwa mujibu wa sheria za nchi-katiba!! Yesu alipokuja, aliondoa tu zile sheria ndogondogo shurutishi na kuacha ile sheria kuu ya nchi ikiendelea palepale kama ilivyokuwa mwanzo!! Mtu akishindwa kutofautisha hivi vitu viwili, ataendelea kwenye dimbwi la upofu miaka yake yote na atafia dhambini bila ya kuwa na tumaini lolote!! Nikushuri ndugu yangu Mhina, kwanza jenga dhamira ya kujifunza huku ukitaka kuthibitisha kila kitu kilichosemwa na wenzio kama ni cha kibiblia ama la mbali na kuwahukumu kuwa ni waongo!! Jitahidi!! Mhina, kilichoondolewa na Yesu, ni sheria ndogndogo shurutishi ndugu yangu, siyo sheri kuu ya nchi/utawala wa mbinguni. Na kwa vile katika mkitadha wa Biblia sheria zote hizi ziliitwa kwa jina la TORATI, wengi tumeingia mkenge kuzifanya kama ni kitu kimoja kumbe sivyo!! Na tutapotea tu kwa ushupavu wetu wa kutotaka kusikia ukweli wake!!
  Nne, kama bila sheria hakuna dhambi, huku unasema kuwa sheria ilianza rasmi utendaji wake baada ya kuandikwa na Musa, na wakati huo, ukisema kuwa watu wa zamani kabla ya Musa, waliishi kwa sheria na direct maagizo kutoka kwa Mungu, Je, bado unakataa kuwa sheria za Mungu zimekuwepo tangu mwanzo kabla ya dhambi??? Elewa tafadhali, nasema kuwa, unakubalina nami kuwa sheria za Mungu zilikuwepo kabla ya dhambi?? Na unakubaliana nami, wakati wa Musa, ulikuwa ni wakati wa kukidhihirisha tu ile sheria iliyokuwepo tangu mwanzo?? Kama utabisha, njoo na maelezo ukifafanua, kile alichokivunja Adamu na mkewe, kilikuwa ni nini? Na usisahau kueleza ni wakati gani Mungu alikuwa akiwapa watu wa zamani maagizo tu bila sheria hadi wakafikia kipindi cha sheria cha Musa?
  Tano, umeuliza maswali nadhani ambayo hayakuhitaji kujibiwa na mimi. Naomba kuivunja hiyo kanuni ya kutokukujibu ili nisahihishe kile ulichosema baada ya kuuliza hayo maswali.
  a. ….je, nikweli kua, ile sabato katika ” wakolosai 2:16″ iliyokomeshwa, sio ile sabato ya amri ya nne inayohusu Pumziko la wasabato?
  Jibu
  Ndiyo ni kweli kabisa. Kwa wanafunzi wazuri wa Biblia, chukua muda kujifunzaq habari hizo!! Sabato ya Amri ya Nne, ni Sabato iliyoanzishwa na Mungu mwenyewe kwa ajili ya wanadamu ili wamwabudu YEYE. Kwa hiyo, kwa vile Sabato ilifanyika kwa ajili yetu kumwabudu Mungu muumbaji, tusipoizingatia, kimsingi tunamkosea Mungu makusudi tu tena mbashala!! Sabato ya wakolosai 2:16-17, ilikuwa ni aina mojawapo ya sabato zilizoambatana na sheria zingine za maagizo ya kafara ambazo zilikuwa ni kivuli cha kifo cha Kristo pale msalabani. Leo sheria hizo, hazipo tena!! Sabato na Amri zingine 9, zipo bado.

  b. Je, nikweli kua, bwana yesu aliitimiza torati yote bila ya kutimiza ile amri ya nne ya sabato?
  Jibu
  TORATI YOTE iliyokuja baada ya DHAMBI, Yesu aliikomesha msalabani!! TORATI YOTE iliyokuwepo kabla ya dhambi, hiyo ni ya milele zote!! Kwa hiyo kwa vile Amri ya Nne(Sabato) ni mojawapo ya TORATI iliyokuwepo kabla ya dhambi, Yesu hakuikomesha hiyo!! Bado ipo hadi mbinguni!!

  c. je, nikweli sabato inaendelea?
  Jibu
  Ndiyo. Ilikuwepo, imekuwepo, ipo, itaendelea kuwepo hadi Yesu atakaporudi na mbinguni, Sabato hadi Sabato, tutaenda kumwabudu Mungu milele!! Kristo ndiye muumbaji na ndiye aliyeifanya na Sabato. Kama hata ndani ya agano jipya amejitambulisha kuwa YEYE ndiye Bwana wa Sabato, akionesha mfano mzuri kwa siku za Sabato kwenda mahekaluni kusali na mitume wake, leo akina Mhina mmepata wapi ujasiri wa kujiita wakristo (wafusi wa Kristo) ilhali hamtunzi Sabato yake? Kwani mnasoma kuna sehemu yoyote ndani ya Biblia kuwa Yesu kuna kipindi alijitambulisha kuwa YEYE ni Bwana wa jumapili? Mnanitia huzuni kweli rafiki zangu!!

  Mwisho (but not least) nakungoja kwa maelezo yakinifu kuhusu hoja na maswali yangu. Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 167. @ Lwembe,
  Kwanza, bado unaamini kuna tajiri alikuwa jehanamu akitaka kurudi duniani? Mmmh, jamani!! Nakushauri ujisomee tena upya ukielewe hicho kisa!!
  Pili, suala la TORATI na ukomo wake, kimsingi ni tatizo kwako!! Shida iliyo kubwa zaidi kwako ni KUIUNGANISHA TORATI PAMOJA na kuifanya kama ni kitu kimoja kwa mantiki yake!! Ukiulizwa swali la kuhusiana na hiyo torati unayong’ang’ana kuijua ndugu yangu, haujibu chochote, badala yake unatuambia hatujui kilichotendeka msalabani!! Kweli!! Nikushauri kwa mara nyingine tena, ujifunze habari za torati. Hata kama hutaki kusikia na kuamini sana habari za TORATI, jitahidi tu uijue itakusaidia sana.
  Tatu, nakubaliana nawe kuwa Neno la Mungu ni Sheria kwa maana ya COMMANDMENT!! Sijui kama sheria za maagizo, vyakula, kafara n.k. na zenyewe ni COMMANDMENT!! Sielewi!! Ila ninachokushangaa rafiki yangu, wewe unaniambia akili yangu haina akili!! Sasa, nami nikuulize, kama Neno la Mungu ni Sheria kwa maana ya Commandment, je, ni 10 commandments tu ndizo zilifikia mwisho? AU ni Neno la Mungu lote limekuwa mwisho wa Sheria baada ya kifo cha Kristo? Tafadhali, ulete jibu hapa!!
  Nne, naomba unibainishie hayo makundi manne ya watu walioandikiwa Biblia ukithiyathibitisha kibiblia, asili zao, na hatima zake!!! Maana sikujakuelewa. Unaonekana kama unasema kuwa, watu watakaokolewa, sharti wapitie madhehebu kadhaa hivi ndipo waupate wokovu!! Au una maana gani??? Hebu leta utondoti tafadhali!!
  Tano, nakungoja kwa majibu. Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 168. ….je, nikweli kua, ile sabato katika ” wakolosai 2:16″ iliyokomeshwa, sio ile sabato ya amri ya nne inayohusu Pumziko la wasabato? Je, nikweli kua, bwana yesu aliitimiza torati yote bila ya kutimiza ile amri ya nne ya sabato?,je, nikweli sabato inaendelea?….ndugu Siyi, mimi nafikiri haya ndiyo mambo haswa ya kujadili ili tufikie muafaka mzuri. Sasa hebu ona: Neno la Mungu linasema hivi kuhusu amri zote za Mungu na kile alichokitimiza bwana yesu” Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake, ndiyo ” SHERIA YA AMRI ZILIZO KATIKA MAAGIZO” ili afanye hao wawili (mataifa na wayahudi waliotii sabato), Kuwa mtu mpya mmoja ndani ya “NAFSI YAKE” Soma(waefeso 2:15). Mimi ndugu Siyi, nilikueleza vizuri huko juu kua, bwana yesu anatupa Pumziko la kweli la rohoni nafsini mwetu, kwa njia mpya ya kutupatanisha na Mungu. Soma(2Wakorintho 5:17-19). Biblia iwazi sana kuhusu jambo hili, inasema” Maana kuna kubatiliwa kwa ile ” AMRI ILIYOTANGULIWA” Kwa sababu ya udhaifu wake, na kutofaa kwake, kwa maana ” ile sheria” haikukamilisha “NENO”……Soma(Waebrania 7:18:19). Sasa ndugu Siyi, Kristo ndiye “NENO LA MUNGU” Yeye ndiye kuhani wetu wa Milele, tazama biblia inasema kua” vitu vyote vilifanyika kwa yeye (neno la kweli) na Pasipo huyo, wala hakikufanyika chochote kilichofanyika!!!. Soma(Yohana1:3). Yeye ndani yake ndimo mlimojaa kila kitu, hata hiyo sabato, ilifanyika kwa ajili yake, ndio maana akasema “mimi ndimi bwana wa sabato”….istoshe Pia, Yeye ndiye “HEKALU LA MUNGU LA KWELI”. Hebu tazama, anawaambia wayahudi hivi, kuhusu mambo ya mahekalu na kutii sabato ” LAKINI NAWAAMBIA KWAMBA HAPA YUPO ALIYE MKUU KULIKO HEKALU!!!. Soma(Mathayo12:6). Pia hebu tazama yule mama alimuuliza bwana yesu hivi ” Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko yerusalemu (hekaluni) ni mahali Patupasapo kuabudia. Bwana Yesu akamwambia hivi” MAMA UNISADIKI, SAA INAKUJA AMBAYO HAMTAMWABUDU BABA KATIKA MLIMA HUU, WALA KULE YERUSALEMU (hekaluni) ….Ninyi mnaabudu msichokijua, sisi tunaabudu tukijuacho, kwa kua, wokovu watoka kwa wayahudi. Lakini saa inakuja nayo saa ipo, ambayo waabuduo halisi watamuabudu Baba katika “ROHO NA KWELI”!!!!. (Yoh4:24-25).

 169. Ndugu siyi: mbona umeandika mambo mengi lakini ya uongo ndugu yangu!!. Kwanza mimi nilisema, torati ni moja tu, ambayo, Mungu mwenyewe, alimuongoza Musa katika chuo, aandike hukumu ya hiyo sheria yake, Pamoja na vijisheria vidogo vidogo zaidi ya 500 vilivyowahusu israel, ili kudhibiti mazingira yao, kwa lengo la kujilinda na maadui. Ushahidi wa vijisheria hivi, uko mwingi sana katika agano la kale, lakini hata katika agano jipya, ipo sheria ya kutoa talaka ambayo Musa aliwaandikia israel kutokana na ugumu wa mioyo yao…Je, ndugu Siyi, sheria hiyo ya kutoa talaka alioiandika Musa ilikuhusu na wewe?, Soma(Mathayo 19:7). Lakini mimi sikutaka tujadili jambo ambalo, sio maada yetu isipokua wewe umechomekea. Jambo la Muhimu ni lile lile ya kwamba, bwana Yesu alitimiza torati yote na manabii, ili atuweke mbali na sheria ya dhambi na mauti. Sisi hatupo tena chini ya sheria ya dhambi na mauti, sisi tupo katika sheria mpya ya kristo ya upendo yenye uhuru lakini, tukiishi sawasawa na mapenzi Ya mungu, yaani sawasawa na makatazo yake. Huko ndiko kuithibitisha sheria ya Mungu kwa hiyo imani yetu, tazama (warumi 8:4) (warumi 3:31). Mimi bado sijajua mnachokikataa ndugu zangu, lakini hicho mnachokihubiri, kinamakosa!!!. Labda atokee mwalimu kutusaidia kwa ujumla wetu ili tujifunze vyema. Tazama: ndugu Siyi, anataka kushika torati kama ilivyo, ili aipate ile sabato yake, huku hapohapo anataka na neema ya bwana yesu kwa wakati huohuo, wakati biblia inasema, sheria ilikuja kupitia mkono wa Musa, lakini neema na kweli zimekuja kupitia bwana yesu. Kamwe huwezi kuishi kwa kutimiza sheria halafu hapohapo upokee neema, hilo haliwezekani kwa sababu neema imekuja ili iiondoe sheria ili iwe kwa neema na utiifu wa rohoni, tena ulio huru kwa ajili ya kudhihirisha ule upendo wa Mungu. Lwembe nae anataka uhuru kabisa usio na wajibu wa utiifu wowote, ndio maana alimpongeza Yuda huko juu kua, ijapokua alikua ni muizi wa sadaka, lakini bado alitembea na bwana kikamilifu, huku akitoa watu mapepo!!!. Sasa ni uhuru gani wa kibiblia wa namna hiyo?!!. Ndugu siyi….kuhusu mwanzo wa sheria kuwepo rasmi, ni Pale nabii Musa, alipozipokea katika mlima sinai, ili ziwe ni amri kamilifu kwa wanadamu. Tazama, biblia inasema hivi” maana kabla ya sheria dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria, lakini mauti ilitawala tangu “ADAMU MPAKA “MUSA”. Soma( warumi 5:13-14). Kwanini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa? Kwa sababu hapo pa Musa, ndipo sheria ilipoandikwa rasmi kwa ajili ya watu wote, hii maana yake ni kua, wale watu wa mwanzo kabla ya Musa, walitawaliwa na sheria na kanuni hizohizo, lakini waliongozwa na maagizo ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu ili watii. Ndugu siyi, jibu langu hili, nimeliandika huku nimesimama kazini ili lianze kukutangulia….lakini ngoja baadae, nitaandika jibu la mambo yanayohusu sabato pekee, ili uone mwenyewe ulivyowadanganya na kuwapotosha watu. Mimi natumia kajisimu ka mfukoni, ndio maana inakua shida kwangu, kupangilia vizuri. Asante ndugu siyi….usikasirike ila tuendelee tu, kuelimishana. Ubarikiwe sana ndugu yangu.

 170. huko juu, nilimwambia siyi ” hebu nisaidie na wewe kunijibu….” . Nikimaanisha kua, tunasaidiana kuchangia mawazo kwa pamoja. Hapo juu nimemwambia lwembe “uweke hoja zako ili nikusaidie, inawezekana kwa ufahamu wa kawaida, nilieleweka vibaya….lakini mimi, ninaamini kua, tunasaidiana katika mawazo yetu (sikua na maana ya kibabe iliyoeleweka). Basi, poleni kwa kutoeleweka kwangu, kwa maana hata mimi nikitafsiri hivyo mlivyonielewa, kwakweli naona haviji, maana mimi sio mwalimu wala mchungaji, mimi ni mkristo wa kawaida…tena kwa 100% nawahakikishieni kua,mtakua mnaijua injili au mliijua injili mapema kuliko mimi. Asante bwana sungura kwa ushauri wako mzuri.

 171. Siyi,

  Kwanza nakupongeza saaaana kwa kuwa mkweli ktk jibu ulilonipa kwa swali langu; kwa jibu lako, ni dhahiri kwamba umeungana na hili kundi, “60Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia?… Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.”!!!

  Basi yanapokuja masuala ya IMANI, wewe huwezi kuwa na Imani, kwani Imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo ambalo ndilo hili hapa unalilolikana, hapo ulipoambiwa: Yn 6:55-56 “Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.” Jibu lako kwa AGIZO hili ni hili hapa:
  1.Kuhusu kuula mwili wa Yesu na kuinywa damu yake unaniambia:
  “”Wewe unafikiri, amri ya USIUE, ilimaanisha nini? Ilikataza kuua watu au wanyama?””
  Basi kama jibu lako hili kwa hili Agizo ulilopewa ndio huo unaouita UTII, inakubidi ukapimwe akili zako, utakuwa una matatizo makubwa saaana!!!!

  Agizo lolote la Mungu ni Amri na ni Sheria, ktk maana ya Commandment. Kwahiyo Neno la Mungu ktk ujumla wake ni Sheria kila ambapo Shetani yupo; akiwapo ktk mwili Torati ndiyo Sheria inayouongoza mwili, na kwa aliyeingia ktk kiwango cha Roho, huko hupewa Sheria ya Kifalme imuongoze ktk kumshinda Ibilisi, 1Yn 5:4 “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.” Bila ya Imani HAIWEZEKANI kumpendeza Mungu!

  Kwa vile uko ktk kundi lisiloweza kumpendeza Mungu, ni dhahiri kwamba hata Maandiko yake si rahisi ukuyaelewa ipasavyvo, ndio maana unajinukulia tu vifungu nje ya ufahamu!

  Kwa taarifa yako Biblia ina jumbe za aina nne kwa watu wa aina nne; ya kwanza ni kwa hao wanaoujia ukristo, wakiingizwa ktk Kuhesabiwa Haki; aina ya pili, ni kwa hao waliohesabiwa haki na sasa wakilishwa neno linaloWATAKASA, wakiwekwa tayari kwa utumishi hapo watakapotukuzwa. Aina ya tatu ni kwa hao waliozaliwa kwa Roho, hao wenye kuubeba Utukufu wa Mungu. Na aina ya nne ni kwa roho zilizoko kifungoni leo hii ambazo hazina fursa ya kuokolewa, hivyo zinahubiriwa kwa ushuhuda tu kuhusu hilo walilolikataa ule Wokovu, kabla ya misingi ya ulimwengu kuwekwa, huko alikochinjwa Mwana Kondoo; ndio hao ambao majina yao HAYAKUANDIKWA ktk Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo!

  Kwahiyo unapokuja na mlolongo wa nukuu kama uliouleta, hili ndilo linaloonesha umekwamia wapi! Labda ninukuu Andiko mojawapo kati ya hayo yenye mwelekeo mmoja ktk mantiki, ili ujionee mwenyewe hicho nilichokiona kwako:
  “”1 Yohana 2:3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.””

  Ktk maelezo yangu nimekuambia kuwa Torati inaendelea kwa wote walio ktk Sheria, ambao kimsingi ndio hao walio ktk ile hatua ya kwanza na ya pili; na haya ndiyo mahubiri wanayopaswa kuhubiriwa ili wayajue mambo haya. Yaani unapofikia ktk hatua ya kuzishika Amri zake kwa uaminifu, kwa jambo hilo unakuwa umemjua Mungu; ni hatua nzuri kwamba sasa unamjua Mungu! Hakuna anayelikataa neno hili!!!

  Yako Maandiko mengi sana yanayourejea Msingi huo, pamoja na hayo uliyoyanukuu, yote yanaliasa Kanisa kuendelea ktk Imani kulingana na mafundisho hayo ya msingi, ndio lile Fundisho la Mitume, na kwa hilo, sasa wanamjua Mungu. Kwa kundi hili Kristo kwao hajawa Mwisho wa Sheria bado; hata wewe mwenyewe ni shahidi, hiyo Lk 18:20 uliyoinukuu inayarejea yaliyojiri kati ya Kristo na yule kijana tajiri, akikiri kwa kinywa chake kwamba Sheria yote anaitimiza, lakini Amani au lile Pumziko hanalo moyoni mwake, ndio maana anamuuliza Mungu afanyeje? akaambiwa aibwage Sheria, ule utajiri wake, amfuate, naye kama nawe uliye tajiri wa mafundisho ya Kisabato alikataa!!!

  Unajua, Maandiko yako wazi saaana, ni kwa vile bado unatembea ktk nuru hafifu, huko kivulini, vinginevyo kwa nukuu niliyokuleteeni ulipaswa ujue huo ujumbe ni wa nani nilipokuambia:
  “”” Wenye kutenda Dhambi ndio wanaoihitaji Sheria ili iwafunulie hizo dhambi zao, Rum 3:19-20 “Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.””””

  Tazama, ujumbe huo kimafundisho, haumhusu aliye ktk Ufalme, huyo ambaye amezaliwa kwa Roho, ndio maana unaanza hivi, ” Basi twajua…” hii ni open declaration kuhusu hali ya hao waliong’ang’ana na Torati wakiikataa Neema; yaani hao waliozaliwa kwa Roho wanayajua hayo kuhusu hao!!!

  Na ujumbe huu, ile aina ya nne, unawahusu hao walio kifungoni kwamba ile Neema waliyoikataa, imewapa hao walioikubali fursa ya kuwa wana wa Mungu, ndio hawa hapa, upende usipende, mambo ndio yako hivi: 1Yn 3:9 ” Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu” ndio nikakuambia kuwa hawa hawaihitaji Torati!!!

  Najua ni vigumu kuyaelewa hayo, lakini ndivyo Injili ilivyokuja, ina chakula kwa makundi yote, unajua hata wa kuhukumiwa ni lazima wapewe chakula ili waifikie Hukumu!!!

  Gbu!

 172. @ Mhina,

  Asante kwa ushauri,
  Lakini ingependeza zaidi iwapo huo msaada unaopenda unipe, ungetanguliwa na jambo la wewe kuwajibika ktk kauli unazozitoa ili uoneshe ukomavu ulionao hata huyo unayetaka kumsaidia awe na imani na huo msaada; vinginevyo inakuwa ni “tambo” tu zisizo na tija!

  Maelezo yangu yote niliyoyaandika yanatoka ktk Msingi wa Maandiko, kwahiyo unaponiambia nitumie mafundisho ya kwenye Biblia, nakuona ni sawa na yule tajiri aliyetaka aruhusiwe kurudi duniani ili akawaambie ndugu zake hali aliyoikuta huko jehanamu! Bali maelezo yangu yamejengeka ktk Maandiko yafuatayo, kama hayaeleweki kwako, ndio hivyo tena ndg yangu, sina namna ya kuyafafanua zaidi kulingana na nilivyojaaliwa kuyaelewa:

  1: SHERIA/TORATI KUENDELEA KUONGOZA –
  Mt 5:17-18
  “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
  Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.”

  2: SHERIA/TORATI KUTULETA KWA KRISTO –
  Gal 3:24 “Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.”

  3: UKOMO WA SHERIA/TORATI –
  Rum 10:4
  “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.”

  *Kristo anakuwa ni ‘Mwisho wa Sheria’ kwa huyo aaminiye hivyo; ndio maana Paulo anasema mtu asiwahukumu kwa jambo lililokwisha kupita- DONE AWAY WITH! Kwa asiyeamini, huyo anaendelea na Sheria, hiyo iliyotimilizwa mpaka hapo mbingu na nchi zitakapoondoka!

  Pia Hukumu za Torati leo hii zinatimizwa kulingana na Sheria ilivyotimilizwa, kwahiyo kuzitegemea Hukumu za mwilini kama kupigwa mawe mpaka ufe, ni ishara ya kukosa Maarifa, wengi wa walio ktk Sheria leo hii watashangaa sana huko mwisho watakapokusanywa na wazinzi wa kipagani ktk kuadhibiwa, licha ya utauwa wao, Ufu 16:21 “Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu” unayaona mawe hayo, amesema mpaka yote yatimie hakuna kinachoondolewa!!!!

  Maswali aliyokuuliza Siyi yanahusu Sabato na utunzwaji wake, katika mantiki ya Amri Kumi, kulingana na tafsiri yao. Nawe majibu uliyompa yanalingana na tafsiri yako ya jambo hilo; kwamba unazitii Amri 9 kati ya hizo na hiyo ya Sabato maelezo yake ndio kama ulivyoyatoa; Kwahiyo kati ya wewe na Siyi mimi sioni tofauti yoyote kati yenu, isipokuwa Siyi anafikiri anazitunza Amri zote 10 kama zilivyo ktk Torati, nawe 9; na linapokuja jambo la kutimilizwa kwa hizo Amri, ndipo kila mmoja wenu anaizungumzia Neema!!!!

  Huo ndio Uhuru mliojitwalia, kuabudu jinsi mnavyopenda ninyi; jambo linalofanana na ibada ya Kaini, huyu ndiye mwanzilishi wa kumtaka Mungu amkubalie matakwa yake ktk jinsi ya kumuabudu!!!

  Ktk kumalizia, bado napenda tuliangalie lile jambo la “Imani bila matendo imekufa”; hili ni fundisho la msingi sana kwetu, na ninaamini ni Mapenzi makamilfu ya Mungu kwamba tulifikie jambo hili ktk maisha yetu ya kawaida ili tuipate faida ya wito wetu ktk Kristo.

  Gbu!

 173. Tatizo lenu mnaandika mambo mengi kwa wakati mmoja, utadhani ndio mnachangia kwa mara ya mwisho.

  Andikeni mambo machache yenye kulenga hoja ya msingi, ili hata mwenye kujibu ajibu kwa mwelekeo thabiti.

  Mnapoandika mambo mengi kwa mara moja mnatengeneza matatizo mengi zaidi.

  Ndugu Mhina, kuna lugha fulani kwa uwanja kama huu huwa sioni kama ni ya kiungwana sana kuitumia, ni huku kumwambia mwingine kuwa ‘Umsaidie’. Kama ulivyomwambia Lwembe hapo kua “labda kama una hoja ya maana iandike ili nikusaidie”

  Hii ina maana gani, kwamba wewe unajua zaidi kuliko yeye? La hasha, wote tuko darasani.

  Ila pia nakusihi uandikage kwa paragrafu(…nimeongea Kiswahili cha Kihehe hapo, hahaaa)

  Ukifanya hivyo utakuwa unaandika makala zilizochambuka vizuri zaidi.

  Ila nakupongeza kuna mahali fulani umekuja vizuri sana, hasa ktk kujibu maswali ya ndg. Siyi!

  Big up!

 174. Lwembe,
  Umeongea vizuuuuuri sehemu ya mwanzo katika pachiko la kwanza ila mwishoni ukachepuka. Mchuko huo, ndio umeukumbatia sana kwenye pachiko lako la pili. Katika habari za Torati, kuna shida nyingi zinazokusumbua!! Zinakuondoa kabisa kabisa kwenye mstari. Kwa mtu anayekufuatilia vizuri, nina imani huwa nakushangaa sana rafiki yangu. Mimi nitaongelea shida moja tu na siku nyingine, huenda nitazungumzia hizo shida zako zingine za kiuelewa katika suala la torati!! Twende pamoja sasa…
  Kwanza, umesema kuwa,
  ““…KRISTO NI MWISHO WA SHERIA…” (Rum 10:4)
  Kuhusu hili la pili, kwamba “Kristo ni Mwisho wa Sheria”, hili pia ni halisi kama linavyojishuhudia. Andiko hili linatangaza Ukomo wa Sheria yote na si sehemu tu ya Sheria hiyo, kwani Sheria ni Kamilifu, hivyo huwezi ukaigawa vipande vipande, ukakitupa hiki na kukibakiza kile, utakuwa umeitangua”
  Sasa hebu jiulize ndugu yangu, kama Sheria ni kamalifu kama ulivyosema, kitu kikamilifu kinawezaje kukoma au kuondolewa tena?? Na je, kama hakuna sheria iliyoondoka, mbona wewe leo hupeleki ng’ombe, mbuzi, njiwa nk wa kafara kwa viongozi wako wa dini? Au wewe mwenzetu unayafanya hayo?
  Mahali Fulani nimekusoma unasema hivi, -Mungu alitushauri kumsikiliza mwanaye Yesu Kristo. Na ukasema kuwa, Kristo ni kinywa cha Mungu –sauti ya Mungu. Sasa sikiliza kinywa cha Mungu kinavyosema;
  Yohana 14:15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
  Yohana 15:10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

  Amri zipi hizo Mungu anatuagiza kuzitii??
  Jibu
  Marko 10:19 …… Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.

  Luka 18:20 …… Usizini, Usiue, Usiibe, Usishuhudie uongo, Waheshimu baba yako na mama yako.

  Unaona hiyo sauti ya Mungu ndugu Lwembe?? Wewe ukitunukulia paragrafu ya Paulo inayosema kuwa “Yesu ni mwisho wa sheria” na tafsiri yako hiyo potofu, kwa upendo wote, sisi tutakunukulia maandishi ya mtu aliyeishi na Kristo, aliyemsikia kwa masikio yake na kumuona kwa macho yake –Yohana.
  Yohana anasema, “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo” -1Yohana 1:1-3.

  Fundisho la Yohana ni lipi sasa??
  1 Yohana 2:3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.
  1 Yohana 2:4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake.
  1 Yohana 2:7 Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.
  1 Yohana 2:8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung’aa.
  1 Yohana 3:22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.
  1 Yohana 3:23 Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.
  1 Yohana 3:24 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
  1 Yohana 4:21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
  1 Yohana 5:2 Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.
  1 Yohana 5:3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
  2 Yohana 1:4 Nalifurahi mno kwa kuwa nimewaona baadhi ya watoto wako wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.
  2 Yohana 1:5 Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tangu mwanzo, kwamba tupendane.
  2 Yohana 1:6 Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.

  Unatuambia sikilizeni sauti ya Mungu kwa njia ya maneno ya Mwanaye, wewe unatunukulia maneno ya mitume tena kwa kuyapotosha tafsiri yake!! Oooh, pole sana bwana!! Sisi hatudanganyiki kirahisi hivyo ndugu yangu. Kauli zako licha ya kuwa ni za uongo, pia zinakinzana sana ndugu yangu. Sijui kama ni kweli sisi ndiyo hatujui kilichotendeka msalabani!!…
  Mf hebu angalia hii:
  “Kuhusu huyo aliyezaliwa kwa Roho wa Mungu, Maandiko yanasema kwamba huyu HATENDI DHAMBI! Basi asiye tenda Dhambi atakuwaje chini ya Sheria?”

  Mara nyingine unasema kuwa Yesu ni mwisho wa sheria!! Yesu ni mwisho wa sheria kwa akina nani sasa? Je, muumini akitenda kosa, sheria iliyokomeshwa na Kristo, kwake muumini huyo itamrudia? Au kama sheria yote ilikomeshwa na Kristo pale msalabani, ina maana wale wasiomjua Mungu sasa hivi, hawatendi dhambi??? Acha mafundisho ya kifedhuli ndugu yangu!! Wewe kama hutaki kuisikia sauti ya Mungu, endelea tu na imani zako za kuamini kuwa Hawa alizini na nyoka busatanini, badala ya kudanganywa, isingekuwa ujanja wa shetani, sisi leo tusingezaliwa, maana Adamu asingejua kulala na mkewe asingefundishwa na nyoka ….n.k. Na mengine mengi ya kiheretic!!!
  Naamini saa inakuja utakayoamua kumtafuta Mungu, lakini angalia usije ukajikuta umechelewa!! Bwana akusaidie sana.
  Sabato njema.
  Siyi

 175. Mhina
  Nikushukuru kwa mapachiko yako rafiki yangu. Binafsi sitakuwa na maelezo mengi sana. Pale ambapo sitaeleweka, karibu kwa kuniuliza tena. Twendeni pamoja sasa….
  Kwanza, ifahamike kuwa, tangu, mwanzo Amri 10 za Mungu zimekuwepo. Katika kitabu cha mwanzo hadi cha kutoka 19, Amri zote 10 zimeonekana. Zaidi ya hapo, kuna amri(sheria) zingine nje ya zile amri 10, ambazo pia zimeonekana kwenye sehemu hiyohiyo ya mwanzo wa Biblia. Takribani sheria zote (torati nzima), zimeonekana ndani ya Biblia kabla ya kitabu cha kutoka 20. Ushahidi upo mwingi tu ukitaka nitakupatia!! Hivyo, kwa maneno mafupi, hakuna torati ya Mungu wala ya Musa iliyoandikwa na Mungu au Musa kuanzia sura ya kutoka 20 (na vitabu vilivyofuata), ambayo haipo nyuma ya sura hizo na kitabu cha mwanzo!! Yote aliyoyaandika Mungu kwa kidole chake, akamwambia na Musa naye kuandika sheria ndogndogo, yalikuwepo zamani tu hata kabla ya hapo. Kwa hiyo, hakuna sheria ya Mungu au Musa iliyotolewa kwa watu fulani kutokana na mazingira yao. Mungu hana sheria za mazingira wala makabila!! Neno la Mungu ni kwa watu wote!! Wakati tukuiendelea na mjadala wetu, hili nimeona niliweke wazi kwanza!!
  Pili, kwa mantiki ile ya kwanza hapo juu, ni vyema tukawa makini rafiki yangu Mhina, tunaposema kuwa, Torati yote na manabii, vimetimilizwa na imani yetu katika Kristo bila ya kuifahamu vyema asili (chanzo) ya torati!! Huwezi kuthibitisha kitu kilichoondolewa!! Kama TORATI yote na manabii havipo, unasemaje tena kuwa kwa upendo wetu ndani ya Kristo, tunavithibitisha??!! Kwa maelezo mafupi tena, napenda kusema kuwa, ni vyema ukaifahamu asili ya Torati, kabla ya kuhitimisha ulivyohitimisha hapo!!
  Tatu, msingi wa TORATI tangu mwanzo, ulikuwa ni kudumisha uhusiano kati yetu na Mungu, – yaani kwa sisi kuyatii maagizo yake aliyotupa baada tu ya kutuumba!! Torati hii, ilikuwa ni Torati ya milele kwa Mungu na kwa wanadamu!! Tulipoasi tu, tulivunja Agano la TORATI ya mwanzo!! Kuivunja huko, hakukuifanya TORATI hiyo iondoke, maana ilikuwa ni ya milele!! Adhabu ya kifo ilitukabili!! Kwa vile makusudi ya Mungu kutuumba hayakuwa kutuangamiza, bado alitoa nafasi ya pili ya sisi kufanya uamuzi tena wa kumsikiliza ama la!! Akaongeza Torati nyingine ya kushughulika na wadhambi, -torati ya kafara (na sheria ndogondogo) ili ziturejeshe kwenye utii wa Torati ya kwanza!! Torati hii ya pili, ndiyo (sheria) iliyotuleta kwa Kristo!! Tungekuwa agano la kale, tungelazimika kutafuta wanyama wa kafara kwa ajili ya kuondoa/kufunika madhambi yetu!! Lakini kwa vile tuko agano jipya ndani ya Kristo (aliye mwisho wa torati pekee ya kafara na tanzu zake), tunamwendea YEYE tu kwa imani na kupata ondoleo la dhambi –kumtwisha YEYE madhambi yetu yote!! Kwa hiyo, Kristo, amekuwa akiturejesha kwenye ule utii wa TORATI ya mwanzo kabla ya dhambi kwa njia ya kumwamini!! Kwa maneno mengine, utii wa torati ya mwanzo kabla ya dhambi, upo palepale na wala hautakuja kubadilika kwa wale wanaompokea Kristo leo!!
  Nne, umeomba nikusaidie kujibu swali la aina za Sabato ndani ya Biblia. Kwa ufupi sana rafiki yangu Mhina, ndani ya Biblia, kuna aina kadhaa za sabato. Mbali na Sabato ya Amri ya nne katika (mwanzo 2:1-3, Kutoka 20:8-11, 31:13-17, Walawi 19:3, Ezekiel 20:12 n.k.), kulikuwa na sabato zingine nyingi ambazo zilikuja kwa Waisrael kama sheria ndogondogo zilizolenga kuwakumbusha Waisrael kwenye Torati ya mwanzo (iliyohusisha AMRI 10, vyakula n.k.). Na miongoni mwa torati zile ndogondogo (sheria) za sabato, kulikuwa na sabato za miandamo ya miezi (1 Nyakati 23:31, 2 Nyakati 2:4, 2 Nyakati 31:3, Nehemia 10:33, Ezekieli 46:4-6), sabato za matarumbeta (Walawi 23:24, 39,), sabato za kufunga miganda (Walawi 23:15,16, torati 16:9,10), sabato za miaka (ya kupumzisha ardhi) (Walawi 25:8,10), Sabato za siku za upatanisho Walawi 23:27-32, Walawi 16:29-31) na kadhalika. Nikushauri uyasome mafungu hayo polepole. Mwisho utaona kwamba, aina zote hizi za sabato, zilienda sambamba na utoaji wa kafara za wanyama, ndege na hadi unga, jambo ambalo lilikuwa ni kivuli cha Kristo!!! Waumini wa sabato hizi, walikuwa ni Waisrael wote (japo waasi pia walikuwepo ambao waliuawa). Kwa ufupi, kafara za wanyama na unga ndani ya sabato hizo, zililenga kuwakumbusha Waisarel mara kwa mara na kwa kila jambo kuwa, kuna Sabato ya Amri ya nne ndani ya torati ya mwanzo, ambayo, Mungu aliitangaza kwao kama ISHARA kati ya YEYE na watu wake Israel!! Kwa matukio mengi yaliyofanyika katika agano la kale, kama sehemu ya sheria za maagizo, kimsingi yalilenga kuifunua tabia ya Mungu -Amri zake 10, ikiwemo Sabato ya siku ya Saba ya kila wiki!! .Hizi ndizo aina za sabato ambazo zilikuwa ni miongoni mwa torati ile ya pili-torati iliyokuja baada ya dhambi. Kwa sababu aina zingine hizi za sabato zilikuwa ni sehemu ya sheria ambayo ilikuwa ni kivuli cha Kristo, ndani ya agano jipya, msisitizo umewekwa kwenye Torati ya kwanza ya kabla ya dhambi ikiwemo na Sabato ya amri ya nne. Kwa nini? Kwa sababu, aina zingine zote za sabato(kwa vile zilikuwa ni sehemu ya torati ya kafara), zilikomeshwa na kafara ya Kristo!! Ndiyo maana mtume Paulo katika Wakolo. 2;16-17, anafundisha na kuwaonya kizazi kile kisichoamini juu ya ujio wa Kristo ya kwamba, mtu asiwahukumu kwa sabato za miandamo ya miezi ambazo zilikuwa ni sehemu ya sheria za kafara. Inasikitisha sana leo kuwaona watu wanaodai wamepumzishwa bure mazigo yao ya dhambi, wakiisahau na wengine kuipuuza kabisa torati ya mwanzo!! Inasikitisha sana!!

  Tano, pumziko tulilobaki nalo leo, ni pumziko la Sabato ya amri ya nne ndani ya Kristo aliye kafara yetu sote. Watu wa agano la kale, walitua mizigo yao ya dhambi kwa mafahari ya kondoo, mbuzi, ng’ombe, njiwa n.k, ambayo kimsingi wengine yaliwagharimu fedha nyingi kuyatafuta. Pumziko lao, lilithibitika pale moto uliposhuka ukateketeza sadaka zao hizo!! Walipopumzishwa, walipaswa wakaishi sawasawa na TORATI ya mwanzo. Na walipoivunja tena torati ya mwanzo, walirudi tena kutoa kafara!! Leo sisi, wa kumtwisha mizigo hiyo ni Kristo mwenyewe kama anavyosema, “njooni kwangu, ninyi msumbukao…. nami nitawapumzisha..” bila ya gharama yoyote. Hata sisi leo, tunapopumzishwa kwa imani tu, sharti tuishi sawasawa na TORATI ya mwanzo!! Ikitokea tumeanguka, hatuna budi kumletea mizigo hiyo tena Kristo, bila ya gharama yoyote!! YEYE hachoki!! Na hii ndiyo maana ya ile Neema katika agano jipya!!
  Niishie hapa kwa sasa. Naamini huenda ukawa na maswali zaidi ya kuniuliza. Karibu sana ndugu yangu tunaposonga mbele kuelimishana mambo haya yanayohusu wokovu wetu. Neema ya Bwana ikufunike.
  Uwe na Sabato njema
  Siyi

 176. Mhina, Hujaona Mistari ya Maandiko katika Maelezo ya Lwembe!! Ukishajenga dhana ya KUBISHANA hutaelewa Chochote kamwe.Tatizo la kunga’ng’ania Mafundisho Ya Dhehebu lako ni jambo hatari na hatimaye LITAKUZUIA USIINGIE MBINGUNI.

 177. ndugu lwembe. Unapoandika au kufundisha jambo, ni vizuri, ukatumia mafundisho mengi ya biblia kuliko kutumia maelezo mengi ya midomoni mwako, istoshe, maswali ya ndugu siyi, mimi nimekwisha yajibu hapo juu. Labda kama una hoja ya maana uiandike ili nikusaidie ndugu yangu…Mungu akubariki tusifanye mashindano, isipokua tuelimishane. Asante.

 178. …….ninaendelea,

  “…KRISTO NI MWISHO WA SHERIA…” (Rum 10:4)
  Kuhusu hili la pili, kwamba “Kristo ni Mwisho wa Sheria”, hili pia ni halisi kama linavyojishuhudia. Andiko hili linatangaza Ukomo wa Sheria yote na si sehemu tu ya Sheria hiyo, kwani Sheria ni Kamilifu, hivyo huwezi ukaigawa vipande vipande, ukakitupa hiki na kukibakiza kile, utakuwa umeitangua!

  Jambo hili, linaanza kutimia ktk ujio wa Kristo, tangu kutungwa kwa mimba yake, mengi ya Maandiko yanayomhusu yanaanza kutimia, “Bikira atachukua mimba”, nk, mpaka kusulubiwa na kufufuka kwake, Lk 24:44 “… ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi.” Jambo lililotimia linaondoka ktk mlolongo wa kusubiriwa au kutegemewa, kiasi kwamba hawa wanaoambiwa hayo, hatuwategemei tena wajirudishe ktk sintofahamu ya hayo wanayofunuliwa! Yanapotimia yote aliyoandikiwa; kutimia kwa hayo ndiko kunakoifikisha Torati katika UKOMO, ambao ni zao la huko kutimia kwa hayo aliyoandikiwa!

  Vinginevyo, basi unapaswa ujiulize, iwapo Torati ilitosha kutufikisha uweponi mwa Mungu, basi kulikuwa na haja gani ya kumleta Masihi? Lakini haja hiyo ilikuwepo, sababu Mungu aliwapa Ahadi itayoitimiza haja hiyo, Kum 18:15, “Bwana Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye”; ndio maana Israeli walikuwa ktk kusubiri kutimia kwa Ahadi hiyo, “Wewe u nabii yule?”; walikuwa ktk shauku hiyo ili wayapate hayo ambayo yangewaingiza ktk hatua nyingine hapo watakapomsikiliza huyo; na asiyemsikiliza angekatiliwa mbali; na yote yaliwatimilia, waliomsikiliza wakavushwa kuingizwa ktk Agano Jipya, na wliomkataa wakakatiliwa mbali!!!

  Basi unapojenga tabia ya kuwa msikivu wa maelekezo, hilo litakusaidia kuuepuka uharibifu unaokuja. Punguza kihelehele, acha Mungu aongee, usipende kumchomekea liturgia na katekesimu zenu, na wengine mafundisho yao ya akina Miller, mama White na sijui akina Jesuit Ri…, na makorokoro mengine; kama Petro alivyojaribu kumchomekea Kristo mambo ya dini yao, naye kama wewe akaona eti ‘Neema pekee’ haitoshi kumuokoa, akataka na Sheria iendelee, na Hukumu ya Mungu iwashukie; “Bwana ni vizuri sisi kuwapo hapa; ukitaka, nitafanya vibanda vitatu, kimoja chako wewe (Neema), na kimoja cha Musa (Sheria) na kimoja cha Eliya (Hukumu ya Mungu)”, unaona jinsi ujinga wa dini unavyoweza kukupofusha?! Wewe ulikwisha ambiwa kwamba akija “nabii yule” Msikilizeni yeye; nawe umemtambua tayari, kwanini hutulii umsikilize kama ulivyoaswa? Kama alivyoonywa Petro, “Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye”; ndivyo nasi tunavyoonywa tuyasikilize Maandiko; unapoambiwa “Kristo ni Mwisho wa Sheria”, sema ‘AMINA!’, usitafute kuleta mambo yako ya dini, hilo pekee latosha kumfanya Mungu apendezwe nawe pia!!

  “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Yn 6:63 Mwili usio na uzima haufai kitu, nao uzima tunaambiwa umo ktk Roho, nalo Neno la Mungu tumeambiwa ndilo ‘roho, tena ni uzima’. Basi ili tuwe hai ktk Kristo ni lazima tulishwe hilo Neno lake lote, na si mchanganyiko unaoishia kutudumaza, kwani imeandikwa, “mtu hataishi kwa mkate pekee, bali kwa kila neno litokalo ktk kinywa cha Mungu”!

  Nasi twafahamu kwamba kinywa cha Mungu ni Kristo ktk siku zetu hizi. Pia twafahamu kwamba mitume ndio mwili wa Kristo uliodhihirishwa, ndipo Injili waliyoihubiri, kwa uhakika ndilo hilo Neno litokalo ktk kinywa cha Mungu ambalo twapaswa kuishi kwalo lote na si kulikata vipande, hiki ukile na hiki useme hakikuhusu, utaishia nje ya kambi ya watakatifu!

  Sheria inafikishwa ktk ukomo kwa yule aliyefikishwa kwa Kristo kwa Sheria. Huyu ndiye aliyeipokea Injili iliyohubiriwa na mitume ktk ukamilifu wake, ikampitisha ktk zile hatua tatu, Kuhesabiwa Haki, Utakaso, na mwisho Mungu Akamtukuza kwa kumjaza Roho wake, ule Uzima wake, naye kufanyika “kiumbe kipya” pale alipozaliwa kwa Roho wa Mungu. Huyu ni sehemu ya Mungu ktk ukamilifu wake, ndio wale “miungu” maana wana uzima wa Mungu ndani yao, hao waliofanyika wana!! Naye aliye mwana hupewa mamlaka ya kutawala hapo anapofikia kufanana na baba yake ndiko huko KUTUKUZWA! Neno lake huwa ni neno la baba yake, moyo wa baba yake ndio wake; “Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu” (Yn 14:20); [Jamani, Mungu ndani yako, halafu ukaibe sadaka kanisani, au ukazini na mke wa jirani yako, ama kweli hiyo ni injili ya kipuuzi sijawahi kuisikia, ndio kwanza naisikia kutoka kwenu wapendwa, ndio maana niliwaambia kuwa HAMKIJUI kilichotendeka ktk ujio wa Kristo!!!!]

  Kuhusu huyo aliyezaliwa kwa Roho wa Mungu, Maandiko yanasema kwamba huyu HATENDI DHAMBI! Basi asiye tenda Dhambi atakuwaje chini ya Sheria? Ndio maana nilikuomba unioneshe mahali popote ktk Maandiko ambapo Kristo, au Petro au Paulo au mtume yeyote yule unayemjua, kwamba alijizuia kuzini au kuiba, nk, akiitii Sheria; na kama hujapaona hapo, basi hilo latosha kuufungua ufahamu wako na kukupa kiu ya kukifikia kiwango hicho ili haki yako iweze kuizidi ile ya Wafarisayo wanafiki wa leo, hao wanaohangaika na Sheria wasizoziweza wala kuzijua, wanaimba tu mapambio ya UTII wa Sheria!!!

  Wenye kutenda Dhambi ndio wanaoihitaji Sheria ili iwafunulie hizo dhambi zao, Rum 3:19-20 “Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” Hawa ndio hao walio ktk Sheria/Amri na Utii; walioipokea sehemu ya Injili iliyohubiriwa na mitume, sehemu nyingine ya Neno hilo wakaikataa, na hivyo kulipungukia na kushindwa kuzivuka zile Hatua, wakakwamia ktk Kuhesabiwa Haki, na wengine ktk Utakaso, na wengine ndio kabisaaa, wameondoka ktk imani, wamechukuliwa na mafundisho ya mashetani wako huko maporini, hawajui chochote kuhusu Injili, wana mfano tu wa utauwa, bali wakiikana Injili – hawa hata kuwahubiri ni kazi bure, maana Mungu anasema tuachane nao!

  Ninayo mengi ya kuyasema, kulingana na Maandiko, bali ngoja nikomee hapa kwa leo ili muifungue hazina iliyomo mioyoni mwenu, tupate kufahamiana zaidi!

  Gbu!

 179. Ndg Mhina,

  Kwanza kabisa, napenda kuliweka sawa jambo moja ambalo naona unalipotosha kwa makusudi; Ni wapi katika maelezo yangu niliposema kwamba UHURU ktk Kristo au Neema vinatupa fursa ya kuzini, kuongopa, kuiba sadaka kanisani kama Yuda na mambo mengine ya kipuuzi ya jinsi hii, na kwamba hatutahukumiwa kwa hayo?

  Usipandikize KUTOKUAMINI ktk mioyo ya watu kwa hila ya kuligeuza jambo jema na kulifanya chafu!!! Kama wewe HAUAMINI kwamba tumeokolewa kwa “Neema pekee”, unaona kwamba na Kutii kwako Sheria kulihusika pia ktk kuokolewa kwako, hili ndilo zao la ‘Ujinga wa dini’ unaopandikizwa ktk mioyo ya wakristo na kuwadumaza; kuhusu hao, Biblia inasema, “Wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli”; ni hasara kiasi gani kukaa ktk mafundisho yatakayo kufanya “usiweze kabisa” kuufikia ujuzi wa kweli!

  Kuhusu Sheria/Torati, ni vizuri ukafahamu kwamba hiyo iko MOJA tu, ndani yake ndimo mna vipengele vingi, pamoja na hizo Amri Kumi. Hivyo, Maandiko yanapolirejea neno “Sheria” au “the Law” ktk maelezo yake, ni ktk maana ya hiyo Sheria inayokutawala Kuzaliwa kwetu mara ya pili, huko kunakotufanya TUUONE Ufalme wa Mungu. Maana Dhambi haifunuliwi kwa Sheria ya Kifo iliyotutawala hapo tulipozaliwa ktk mwili, tulipokuwa tusio na Mungu! Ndipo tunapaswa kufahamu kwamba Torati ndiyo inayotutoa ktk Sheria ya Kifo hapo inapotuingiza ktk Uanafunzi, tumjifunze Mungu, Maandiko yanatuambia hiyo ni “mwalimu”; na tukiisha kufuzu ndipo ituachilie pale inapotukabidhi kwa Kristo anayetuingiza ktk Ufalme wa Mungu unaoongozwa kwa Sheria ya Kifalme baada ya kuwa tumezaliwa kwa Roho wa Mungu.

  Kwahiyo Sheria zote tatu ni kamilifu, tena ni halisi, na hakuna inayotumika nusu nusu! Sheria ya Kifo ndiyo inayokuongoza kuzaliwa kwetu kwa mara ya kwanza ktk mwili. Hii ndiyo inayotuzamisha ktk Dhambi mpaka tunageuka kuwa Kifo, lile GIZA! Basi Sheria hii haiwezi kukuongoza kuzaliwa kwetu mara ya pili maana huu ni wakati wa Nuru kuchomoza ikilifukuza hilo Giza, ndiyo hiyo Torati, kile kivuli. Vivyo Torati haiwezi kukuongoza kuzaliwa kwetu kwa Roho maana hiyo ilikuwa ni kivuli tu cha hiyo NURU, ndiyo hiyo Sheria ya Kifalme, hiyo inayowabadilisha wafuasi wake kuwa hiyo nuru; ndio maana huwezi kuzisikia hadithi za Giza mahali panapotawaliwa na Nuru, labda huko kwenye utawala wa kivuli cha hiyo Nuru, ambako wengi wameharibika macho yao baada ya kupandikiziwa nuru bandia za vikoroboi vinavyofuka moshi!!!

  Kutoka ufahamu huu, sasa tunaweza tukayatazama matamko mawili muhimu sana yanayoihusu Sheria/Torati ktk wakati wetu. Kristo anaposema, “Sikuja kuitangua, bali kutimiliza”, na pia hapo inapotangazwa kwamba “Kristo ni Mwisho wa Sheria”, haya ni mambo mawili yaliyo halisi tena yanayojitosheleza ktk maana iliyokusudiwa hapo yaliponenwa.

  “…SIKUJA KUITANGUA, BALI KUTIMILIZA…” (Mt 5:17-18)
  Bila ya kuyawekea tafsiri yoyote ile ya kimafundisho, anaposema, “Sikuja kuitangua, bali kutimiliza”, hili linatudhihirishia kwamba Sheria yooote inaendelea, tena si tu kama ilivyopokelewa huko nyuma, bali sasa inaingizwa ktk utimilifu, yaani ukamilifu. Ndio hayo unayoyaona yanayotokana na Sheria hiyo hiyo, bali sasa yakipandishwa kutoka ktk kiwango cha mwilini na kuingizwa ktk kiwango cha rohoni: “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, …” nk. Basi huku ndiko kuitimiliza Sheria, hao watu wa kale, wengine waliua ili waibe tu, lakini sasa, Hasira tu juu ya ndg yako inakuingiza ktk Hukumu ya Kifo sawa sawa na aliyeua ktk mwili! Hakuna unaloweza kuliongeza wala kulipunguza ktk Sheria baada ya kutimilizwa kwake, maana hiyo sasa ni KAMILI!.

  Pia anaendelea kusema, “…Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Hili linatuhakikishia zaidi kwamba Sheria itaendelea mpaka huko mbingu na nchi vitakapoondolewa! Kwahiyo jambo la kuitimiza sehemu ya Sheria na kuiacha nyingine, kwa kisingizio chochote kile, ni kinyume cha Maandiko kama yanavyojishuhudia, Sheria inapaswa itimizwe yote. ‘Guilty in one, guilty in all’!

  Ndio maana Siyi, licha ya kukusifia, mwisho amekushangaa, “”Kama sheria zingine zote 9 mnazikubali na kuzitii kiasi hicho, iweje mshindwe kwa ile moja tu ya Sabato?? Au hamuoni kuwa utii wenu kwa amri 9 ni bure kama ile moja mnaiacha??””; huu ni mshangao wa haki kulingana na kukiri kwako kuzitii hizo Amri 9, isipokuwa hii moja tu ya Sabato, ambayo sijaona mahali popote pale ilipoondolewa, hata Paulo hakusema “Msihukumiwe kwa kuvunja Sabato” ktk maana ya kutokuitii Amri ya Nne; Amri ziko Kumi ndg yangu, na unapaswa uzitii zote, tena ktk jinsi zilivyotimilizwa, na ieleweke kwako pia kwamba HAKUNA Neema inayoweza kukunasua kutoka ktk mtego wa Sheria uliojiingiza!

  Kwahiyo ndg zangu tusijidanganye kwamba kuna Sheria zilizoondolewa, hiyo ni hila ya Ibilisi, akijaribu kuwapumbaza kwa kuzigawa, sijui za kafara, nyingine za Maadili, na uongo mwingine wa dini; Dhambi ni dhambi tu, nayo Sheria twafahamu ilishughulika na Dhambi na Hukumu yake! Kwahiyo Sheria haiwi Sheria hapo unapoiondoa sehemu yoyote ya hiyo Sheria; Sheria ni kamilifu, ndio maana inapaswa itimizwe yote! Kristo kuwa Bwana wa Sabato hakuiondoi Amri ya Nne, bali kwatudhihirishia kwamba hiyo Sabato ni yake, nao Israeli walipewa tu na wakaambiwa waitunze, Sabato si yao bali ni ya Kristo!

  Nitaendelea tulitazame lile Andiko la pili…

  Gbu!

 180. Asanteni sana, Ndugu Lwembe na Ndugu Siyi kwa Pamoja. Kwanza Kwa Ndugu Lwembe, Mimi nimekuelewa, hakuna tabu ndugu yangu, tofauti zetu za kimitazamo, ndizo zinazotuimarisha zaidi katika imani, tuendelee tu, kuelimishana. Sasa nije kwa ndugu Siyi na maswali yako, lakini nitakujibu kwa maelezo yanayojitosheleza : Tazama, zile “AMRI 10″ ndiyo hiyo torati yenyewe (sheria za Mungu), na yale maagizo yake yote, aliyoyaandika na kuyaamrisha nabii Musa, ndiyo hukumu ya hiyo sheria,(hukumu ya amri za Mungu). Mwenyezi Mungu, aliandika sheria zake kwa mkono wake mwenyewe, halafu akamuagiza nabii Musa katika chuo, aandike hukumu za hiyo sheria pamoja na vijisheria vidogovidogo, vilivyo wahusu israel kutokana na mazingira yao. Tazama biblia inasema hivi” Musa akawaita israel wote, akawaambia, enyi israel “ZISHIKENI AMRI NA HUKUMU” Ninenazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuangalia “KUZITENDA”.Soma(Kumbuk 5:1-2). Ndiyo maana Mungu akawaambia israel hivi” Kwa ajili ya hayo mtazishika ” AMRI ZANGU NA HUKUMU ZANGU” ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo, Mimi ndimi BWANA. Soma(walawi 18:5). Sasa, Biblia inaposema ” torati yote na manabii” inamaana kuwa, ni agano la kale lote, linakuwa halina tena sheria yeyote ya kutushtaki mbile za Mungu, isipokua, tunafaidika na zile simulizi nyingi za kinabii zinazotuonyesha mambo muhimu ya kuyahahamu na kuyazingatia katika imani yetu. Bwana yesu ametimiza agano la kale, ambapo, kwa njia ya sheria yake mpya ya upendo, ametufundisha kuithibitisha ile sheria kwa hiyo imani yetu, kwa njia ya rohoni na kuzaa matunda ya haki yanayompendeza Mungu, ndiyo maana akatuambia hivi” Basi yeyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni hivyo hivyo, maana hiyo ndiyo ” TORATI NA MANABII!!!. Soma(Mathayo 7:12). Sasa ndugu Siyi, nakuomba hebu swali lako (b) unisaidie wewe ndugu yangu, unifahamishe: hivi kuna aina ngapi za sabato? Na hiyo sabato unayoiamini wewe ni ya amri ya ngapi katika zile amri kumi? Na hizo sabato nyingine, hao waumini wake, wanapumzika siku gani?, kwakweli ndugu siyi, ukinisaidia hayo maswali ambayo uliniuliza mimi, utakua umenisaidia sana, maana, mimi ninavyojua ni ile sabato moja pekee iliyohusu PUMZIKO LA SIKU YA BWANA, katika amri zake ambapo siku hiyo, hata ukiwasha moto ili uchemshe chai, unaweza kuuwawa!!!. Kristo ndiye bwana wa sabato, maana yake ni kuwa yeye ndiye hilo “PUMZIKO LA KWELI LA ROHONI”. Kivipi?….Mwenyewe alitukaribisha kwake, kwa kusema hivi” Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo, nami “NITAWAPUMZISHA” .Bwana yesu alikua anaongelea Pumziko au raha ya kweli ya rohoni, kwenye hizo “NAFSI ZETU” Sio mwilini mwetu kama torati ilivyoagiza, ndiyo maana akasisitiza kwa kusema ” nira yake ni “laini” na mzigo wake ni “Mwepesi” soma(Mathayo 11:28)….hiyo ndugu siyi, ndiyo maana ya bwana yesu kuwa “bwana wa sabato” ikimaanisha yeye ndiye” pumziko la kweli la rohoni”. Ukweli ni kwamba, ni Mungu mwenyewe ambaye, baada ya kutuona hatuwezi kutimiza torati yake kwa ukamilifu wote, ili kukidhi mahitaji yake ya haki, ndipo akaamua kutulinda yeye mwenyewe kwa huruma wake, kupitia imani na mwili wa mwanae….yaani: Mungu alikuwa ndani ya kristo, akiupatanisha ulimwengu na “NAFSI YAKE”, ili asituhesabie makosa, tena akatutia “NENO LA UPATANISHO” ndiyo maana, Mtume Petro, akasema hivi” NANYI MNALINDWA NA NGUVU ZA MUNGU KWA NJIA YA IMANI, HATA MPATE WOKOVU ULIYOTAYARI KUFUNULIWA WAKATI WA MWISHO. Soma(1Petro1:5) + (2Wakorintho 5:19). Ndugu Siyi, mimi kwanza, nisiendelee zaidi ya hapo, ili ndugu yangu nawewe upate nafasi ya kuchangia na kujibu vile vijiswali. Asante, nakusubiri ili tuendelee kuelimishana ktika bwana.

 181. Hahahaaaaa…..

  Siyiiiiiiiii!!!

  Umeyaona majibu ya Mhina?
  Pole, maana najua hujamwelewa kabisa wala kukubaliana nae.

  Umemuuliza maswali ya sheria ya torati kama farisayo vile!

  Hukutegemea kama majibu ya Mhina yatakuwa hivyo.

  Pole!

 182. Ndg Mhina,

  Ninakushukuru kwa mafundisho unayoyaleta, yanasaidia sana kupata mitazamo tuliyonayo kuhusu Maandiko na jinsi mitazamo hiyo inavyotuongoza ktk maisha yetu ya kila siku, ule ushuhuda utokanao na mitazamo hiyo!

  Jambo la kwamba nimeandika ili “kuficha aibu” yangu, si la kweli, na hata wewe mwenyewe unafahamu hivyo; la si hivyo, basi ulikuwa na wajibu wa kuliweka wazi hilo uliloliona kwamba ni la aibu ktk hayo niliyoyaandika ili iwasaidie hao wanaojifunza wapate kuifikia Kweli ya Injili!

  Labda aibu niliyonayo ni ile kwamba HUJAYAELEWA niliyoyaandika, kwahiyo inanilazimu niongeze bidii ktk kuyaweka wazi zaidi ili ushawishike kuyatazama upya Maandiko (najua unayo bidii ktk hili), kisha uyalinganishe na hayo mafundisho ya Katekesimu/Liturgia yanayokuongoza unapoisoma Biblia yako!

  Pia umeniambia kwamba mimi ni mvivu wa kuisoma, kuielewa na kuiamini Biblia yangu, tena ni mwenye kuhukumu ovyo wengine; hilo lawezekana kwa sehemu, bali kuhusu kuiamini Biblia, hiyo ni changamoto kwetu sote, na ndio inayoleta majadiliano haya, tukiitafuta ile “Kweli” kuhusu Sheria, ili kusoma na kuielewa kwetu Biblia kuwe kwa faida ya kutujengea Imani hapo tunapofikia KUYAAMINI hayo tunayoyasoma na kuyaelewa kama yalivyo kusudiwa, na hivyo kuwekwa HURU na vifungo vya dini tulivyovizoelea, tukiibwaga na Mitazamo yetu yenye makengeza hapo tunapoipokea IMANI!!

  Ngoja nijaribu tena!!!

  Gbu!

 183. Mhina,
  Nakushukuru kwa andiko zuri. Naomba unijibu swali langu lenye vipengele vinne tu kwa sasa, kabla hatujaendelea mbele zaidi katika majifunzo yetu.
  Naomba upitie kwanza pachiko langu hapo juu nililolitoa mwezi januari – M. Siyi says: 06/01/2015 at 3:46 PM kisha useme,
  1. Kwenye mchango wako huu umezungumzia torati, sheria au amri?
  a. Na kama ni torati, ni torati ipi hasa iliyokomeshwa na Kristo?
  b. Unajua aina ngapi za ssabato ndani ya Biblia?
  c. Sabato ya amri ya Nne, ni torati/sheria, au amri?
  d. Ni nini maana ya Bwana wa Sabato?

  Ninakungoja kwa majibu ili tuendelee kwa hicho ulichokiandika.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 184. JIBU LANGU KWA SIYI: Kwanza ndugu yangu, naomba uelewe kuwa, Bwana yesu aliitimiza torati yote, hakuacha yodi wala nucta ya torati, kwa ushahidi wa Maneno yake mwenyewe. Soma(Mathayo 5:18) + (Luka 24:44). Sisi tu mwili mmoja ndani ya Yesu kristo, Yaani sisi tunamuishia Mungu kwa njia ya yesu kristo bwana na mwokozi wetu. Hapo inakuwa, sio sisi tena, ila ni yule kristo akaaye ndani yetu. Hivyo ndugu, tutakapojaribu kutimiza torati, haswa ile amri ya sabato uliyoitaja wewe, basi inamaanisha waziwazi kuwa, wewe bado hujaamini kwamba, bwana yesu aliitimiza torati yote na manabii kwa ajili yako!!….Maana, biblia iko wazi kabisa, inasema” KRISTO NI MWISHO WA SHERIA ILI KILA AMUAMINIYE AHESABIWE HAKI. Soma(rumi 10:4). Tazama ndugu siyi, biblia inasema”TUMEFUNGULIWA KATIKA TORATI” Yaani “tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika ” HALI MPYA YA ROHO” Si katika hali ya zamani ya “ANDIKO” = (Torati). Umeona ndugu siyi hapo?, soma(warumi 7:6). Kwa hiyo ndugu siyi, ukiamini kuwa amri tisa katika torati zilitimizwa na bwana yesu, kasoro ile moja ya sabato, basi utakuwa bado umejifunga katika lile kongwa la wagalatia kwa hiyohiyo mri yako moja ya sabato!!. Soma(wagalatia 3:1-4). Sisi tupo katika sheria mpya ya kristo, itupayo hali mpya ya roho, sio sheria ya Musa, yenye kufuata na kutimiza amri kwa ajili ya haki, hapana. Soma(galatia 6:2). Sisi ni Taifa jipya la kristo, tazama bwana yesu anawaambia wayahudi hivi” kwa sababu hiyo nawaambia, ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa Taifa lingine lenye kuzaa matunda yake!!. Soma(Mathayo 21:43). Tazama katika Taifa hili la wateule wa Mungu, Mambo yanakua yamekomazwa zaidi, kwa maana “YAMETIMIZWA NA BWANA YESU KWA UHALISIA WAKE”…Ndiyo maana biblia inasema” Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi au “SABATO” Mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo, bali mwili ni wa kristo!!!!. Soma(wakolosai 2:16-17). je, ndugu siyi, kwa andiko hilo, unafikiri itanipasa kuhukumiwa kwa hiyo amri ya sabato kama ulivyofikiri? , hapana, mimi naamini sinto hukumiwa kwa maana, bwana yesu hakutimiza amri tisa au kumi pekee, ila alitimiza torati yote na manabii kwa ajili yetu wote…tukiwa ni wenye dhambi, ili tupokee ile neema ya Mungu kupitia yeye, ndiyo maana yeye mwenyewe akasema” NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA KWA MAANA SIKUJA KUWAITA WENYE HAKI, BALI WENYE DHAMBI. Soma( Mathayo 9:13). Sisi, kristo ametuita, tumuamini na kutenda mapenzi yake, ili ” TUENENDE KATIKA UPYA WA UZIMA WAKE. Sasa, ijapokuwa sheria mpya ya Yesu, bado inataja yale maagizo yote ya amri kumi katika torati, lakini kwakeli mambo na majukumu yake ni tofauti kabisa!!…na hali hiyo ndiyo inayoleta maana ya “KUTIMIZA SHERIA KWA BWANA YESU” Sio kuondoa, Pia “TUIDHIBITISHE SHERIA” Sio tuidharau…ndiyo maana bwana yesu anaitwa “dhihilisho la upendo wa Mungu kwetu, (kwa tafsiri ndefu ya biblia…. Soma(Yohana 3:16). Ile sheria pya ya upendo ya bwana yesu, kwaujumla wake, imeongelea ile “HAKI na KWELI” ya Mungu ktika sheria zake(torati yote na manabii)….ndiyo maana biblia inasema” maana kule kusema, usizini, usiue, usiibe, usitamani na ikiwepo amri nyingine yo yote, “INAJUMLISHWA” Katika neno hili, ya kwamba mpende jirani yako kama nafsi yako. Soma( Warumi 13:9-10). Sasa, hilo pendo la bwana yesu ni la vipi? Pia, limewezaje kutimiza torati yote na manabii, mpaka likawa ni mwisho wa sheria?…..jibu, ni kwa njia ya injili yake kupitia imani yake na upendo aliyotuachia kama ifuatavyo: MPENDE MUNGU NA JIRANI YAKO: “Huu ndio msingi wa torati yote na manabii, na pia, ndio hiyo sheria mpya ya bwana yesu ya upendo!!. Soma(Mathayo 22:36-40). USILITAJE BURE JINA LA BWANA MUNGU WAKO: “Yaani jina la Mwenyezi Mungu “LITUKUZWE”!!. Soma(Mathayo 6:9). USIABUDU MASANAMU: ” Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu ikimbieni ibada ya sanamu!!. Soma(1Wakorintho 10:4). WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO: ” Waheshimu baba yako na Mama yako, amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia, Soma(waefeso 6:2-3)….sijui niendelee kiasi gani tena, ila nilichotaka kukionyesha hapo, ni jinsi injili ya bwana yesu, ilivyotimiza zile amri zote za Mungu kwa njia ya sheria yake mpya ya upendo!!!. Hakuna pa kutokea hapo kwa wale wazinifu, walevi, waizi, nk…waliokuwa wanajaribu kukwepa amri za Mungu, sasa je, amri za kristo katika injili yake, ambazo kimsingi zimezingatia kukataza yale yale, je, pia mtazipinga?!!!!!. Namalizia na wewe ndugu siyi, ili tuelimishane vema ndugu yangu. IKUMBUKE SIKU YA SABATO: ” Kristo ndiye bwana wa sabato, maana biblia inasema hivi” kabla ya kuja ile imani, tulikuwa “TUMEWEKWA CHINI YA SHERIA” Tumefungwa mpaka ije ile “IMANI ITAKAYOFUNULIWA” Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani (sio kuhesabiwa haki kwa kutimiza torati na amri zake kama ile ya sabato, hapana.) Soma(galatia 3:23-25). Ndugu Siyi, nimalizie kwa kusema: sisi wakristo kwa ujumla wake, tunatakiwa tumuabudu Mungu kila siku, tujifunze neno lake kila siku, ili tusimpe ibilisi nafasi. Lakini sio kosa, sisi kujiamulia jambo hili siku tuliyoipanga na kuona inatufaa, iwe j, pili iwe j, mosi, wote hatuna makosa, isipokua mwenye makosa atakuwa ni yule anaetafuta siku hiyo ili atimize torati ya Musa, jambo ambalo halipo kabisa katika injili ya bwana yesu. Soma(warumi14:5). Basi, tuendelee kuelimishana ndugu yangu. Ubarikiwe.

 185. Mhina,
  Mungu akubariki sana kwa jibu zuri na lenye ujumbe mzito. Nafikiri Sungura na Milinga watakuwa wamesuuzika mioyo kabisa ha ha ha ha!! Najua walichokuwa wanakihoji kwako, sasa umekiweka wazi!!
  Kimsingi umesema mambo makubwa sana ambayo waj2 wengi huwa hawayasemi mbashala kama ulivyofanya wewe na somebody Msella!! Mimi nakiona kilichobaki kwenu ni Sabato tu basi!! Uelewa wa siku ya Sabato na Kristo aliye wa Bwana wa hiyo Sabato, bado unawapinga chenga kubwa sana!! Kama sheria zingine zote 9 mnazikubali na kuzitii kiasi hicho, iweje mshindwe kwa ile moja tu ya Sabato?? Au hamuoni kuwa utii wenu kwa amri 9 ni bure kama ile moja mnaiacha?? Kimsingi, kwa mara nyingine nitawaomba (Mhina, Msella na wengine kama wapo) mnipe uelewa wenu kuhusu Sabato na Bwana wa Sabato -Kristo!! Au mnasoma wapi kuwa Yesu alipokufa msalabani na Sabato iliishia hapo kama amri zingine 9 zinaendelea hadi leo? Nawasihi mrudi kujisomea upya sehemu hiyo. Ni aibu sana kama mtapotea mkiwa na nuru asilimia 99 kiasi hiki!!
  Nitawachungulia baadaye kidogo. But all in all, mmenibariki sana.
  Neema ya Bwana iwafunike.
  Siyi

 186. JIBU LANGU KWA WOTE: Ndugu wachangiaji wote, kwa kuwa, hii blog iko taratibu sana, kuweka michango yangu hewani, basi kwa ujumla wenu, nimeona niwajibu kwa upamoja, kulingana na mitazamo na mawazo yenu, niliyoyasoma huko juu. Kwakweli mimi nilikwisha waambia huko juu ya kuwa, huo upendo wa bwana yesu, siyo sawa kabisa na huu upendo wenu, mnaoufundisha hapa wa kuwapa uhuru kabisa wa kutenda hata matendo mabaya bila ya kuwa na hatia za kiroho, eti kwa kisingizio kuwa, mmeokolewa kwa neema pekee!!. Mimi nakubali kuwa, nikweli kuwa, tumeokolewa kwa neema pekee bila ya matendo yoyote, lakini ndugu zangu, ni lazima tuishi maisha ya ki kristo, yenye misingi ya uadilifu, ili tusimtende dhambi Mwenyezi Mungu, kwa kisingizio cha kuwekwa huru mbali na sheria. Tazameni biblia inatuambia hivi” MAANA NINYI, NDUGU, MLIITWA MPATE UHURU, LAKINI UHURU WENU USIWE SABABU YA KUUFUATA MWILI, BALI TUMIKIANENI KWA UPENDO. Someni( galatia 5:13). Mwenyezi Mungu alitaka hivi, kupitia huo upendo wa Mwanae, sisi tuithibitishe haki yake kwa kutenda matendo mema ambayo, tuliumbwa nayo kwa asili yetu ya rohoni tangu awali, ndiyo maana, Mtume Paulo akasisitiza ” MAANA TU KAZI YAKE, TULIUMBWA KATIKA KRISTO YESU, TUTENDE MATENDO MEMA, AMBAYO TOKEA AWALI MUNGU ALIYATENGENEZA ILI TUENENDE NAYO!!!!!. Someni(Waefeso 2:10). Kwa hiyo ndugu zangu, msiogope kusikia, neno ” kutii sheria” mkafikiri kuwa, neno hilo linaondoa ile neema yetu, tulioipokea kwa bwana yesu, kwa ajili ya kutupatia haki, hapana, isipokuwa neno kutii, ni matokeo ya ule upendo wetu, Soma(Yohana 14:15). Ndiyo maana pia biblia inasema hivi” KWA MAANA HUKO NDIKO KUMPENDA MUNGU, KWAMBA TUZISHIKE (TUZITII) AMRI ZAKE, WALA AMRI ZAKE SI NZITO, Someni(1Yohana 5:3). Hii maana yake ni kwamba, tukimpenda Mungu, basi Pia tutazitii amri zake zote, kupitia sheria mpya ya kristo ya upendo (siyo kuzitii kupitia torati kama ilivyoagiza…naomba nieleweke vizuri hapa, kwa maana, sisi kwa uwezo wetu wenyewe, kamwe hatuwezi kutimiza sheria ya Mungu kwa haki yetu, isipokuwa, baada ya kristo kutimiza haki yote, ndipo anatuongoza katika sheria yake mpya ya uhuru na upendo, kutii kwa njia ya imani na upendo wake anaotupa. Sasa, hebu tazameni jinsi tunavyoweza kutii amri zote za Mungu, kwa njia ya sheria mpya ya kristo yenye uhuru na upendo. AMRI YA KWANZA YA BWANA YESU, TUMPENDE MUNGU: ” Tukimpenda Mungu, ni lazima pia, tutazitii zile amri nne za kwanza, zinazofafanua uhusiano wetu na Mungu!!!. AMRI YA PILI YA BWANA YESU, TUWAPENDE MAJIRANI ZETU: Tukiwapenda majirani zetu, basi pia tutazitii zile amri sita zilizobaki, ambazo pia nazo, zinatufundisha, jinsi ya kuwa na uhusiano mzuri na watu wote…lakini kuna amri moja kati ya hizo, ambayo inahusu kutii siku ya sabato, hapo utiifu wetu upo katika kumtii bwana yesu, maana yeye ndiye “BWANA WA SABATO”. Kristo aliitimiza sabato ya Mungu ili sisi wafuasi wake, tumfuate yeye…kama alivyozitimiza na zile sheria nyingine. Hakuna kilichobaki cha kutushtaki katika torati, maana yote yalitimizwa na kristo. Someni (1Wakorintho 15:56). Lakini, ni lazima tufahamu kuwa, bwana yesu hakuitangua torati na manabii, eti ili sisi tuwe huru kutenda dhambi, isipokua yeye aliitimiza ili wafuasi wake wote wanaomuamini, waithibitishe hiyo sheria kwa njia ya rohoni katika hiyo imani yake, Someni(warumi 8:4) (warumi 3:31). Ule uhuru na upendo uliomwagwa ndani ya roho zetu, ndiyo haswa tumaini letu la kweli, kwa kuwa, ile nia yetu ni lazima itasukumwa na huo upendo unaozaa yale maisha ya utii, utokanao na huo upendo. Soma(Yohana 14:21). Sasa hebu tutazame, nini umuhimu wa matendo mema kwa sisi tunaojifanya tunamwanini bwana yesu, halafu eti tunaona kuwa hayana maana kabisa kwa kisingizio kuwa umeokolewa kwa neema pekee. Ndugu zangu wote, nilikwishasema huko juu kuwa, mwenyezi Mungu ni mtakatifu asiyepaswa kudhihakiwa kwa uovu wowote, tazama, yako matendo mabaya, yanayoitwa kibiblia “MATENDO YA GIZA” ambayo kazi yake ni kuwawakilisha wafuasi wa shetani, halafu yako matendo mema ambayo kibiblia yanaitwa ” MATENDO YA NURU” ambayo nayo kazi yake ni kuwawakilisha wateule wa Mungu. Nikweli iliyowazi kuwa, tunaokolewa kwa neema pekee, kama Baba yetu ibrahimu alivyopata haki kwa njia ya imani pekee…lakini ndugu zangu, kipimo haswa cha imani ya kweli ni kuzaliwa kwa matendo mema ya “NURU” Kama pia Baba yetu ibrahimu alivyothibitika kwa Mungu !!. MNALIJUA HILO?, Ni kwamba, imani ya kweli, huwa inatabia ya kuzaa matendo mema, kwa kuwa tabia ya Mungu ni “HAKI” NA “KWELI”…. Ndivyo pia, alivyotuagiza kristo kwa kusema hivi”MAANA KILA MTU ATENDAYE MABAYA HUICHUKIA NURU, WALA HAJI KWENYE NURU, MATENDO YAKE YASIJE YAKAKEMEWA, BALI YEYE AITENDAYE KWELI HUJA KWENYE NURU, ILI MATENDO YAKE YAONEKANE WAZI YA KUWA YAMETENDWA KATIKA MUNGU, Someni(Yohana3:20-21). Jamani, hebu niwaambie ukweli kuwa, Matendo mema katika imani yetu, ndiyo yanayotufanya sisi tuwe WAKRISTO ili tuwe chumvi kwa wengine katika kuitangaza, ile kweli ya injili ya kristo, kwa ndugu zetu wengine wasioamini ipasavyo, ili nao waanze kumuamini bwana yesu na kumtukuza Mungu wetu wa kweli aliye mbinguni, ndiyo maana bwana yesu akatusisitiza kwa kutuambia ” VIVYO HIVYO NURU YENU NA IANGAZE MBELE YA WATU, WAPATE KUYAONA MATENDO YENU MEMA, WAMTUKUZE BABA YENU ALIYEMBINGUNI!!!!!!. Someni (Mathayo 5:16). Ndugu zangu wote katika bwana, ijapokuwa sisi tutanyakuliwa kwa neema ya kristo, lakini ili tuthibitishe kuwa sisi ni watoto wa nuru, basi amini usiamini ni lazima hiyo nuru yetu ithibitike hapa duniani ili idhihirishe ya kuwa nikweli tulimjua huyo Mungu aliyetuokoa na tunaishi maisha yanayompendeza yeye, ndiyo maana, Yohana mtume wa Yesu, kwa unyenyekevu mkubwa wa kiroho, akatushauri kwa kusema” MPENZI USIUIGE UBAYA, BALI UIGE WEMA. YEYE ATENDAYE MEMA NI WA MUNGU BALI YEYE ATENDAYE MABAYA HAKUMUONA MUNGU (hamjui Mungu)!!!!!!!. Someni(3Yohana1:11). JIBU LANGU KWA WACHANGIAJI WOTE NI HILO, AMANI YA BWANA IWE JUU YENU. Mbarikiwe sana.

 187. @Milinga
  Pole sana kama unataka kuwa msabato kwa kuwaangalia wasabato!! Ukifanya hivyo, hutafika popote!! Wapo wasabato waaminifu kabisa. Na wapo wasabato wafedhuli pia –wasabato jina tu!! Kama wewe unafikiri kuwa msabato peke yake ndiyo tiketi ya kuokolewa hapo baadaye, umedanganyika!! Kuna mambo/vigezo vingi vitakavyokufanya uende mbinguni, japo kimojapo ni kuwa msabato halisi. Sabato (zikiwepo na amri zingine) ni mandatory kwa watu wote walio hai isipokuwa kwa mtu anayetubu dakika ya mwisho wa uhai wake. Nikushauri utake sana kufanana na Kristo aliye Bwana wa Sabato na siyo kufanana na watu. Hatumwamini Kristo ili tufanane na watu, bali tufanane na Kristo mwenyewe!!
  Majibu ya maswali yako;
  Swali la 1
  “Je, HII NDIYO SABATO aliyoikusudia MUNGU wanadamu wawe nayo? Mbona mnakuwa bize sana kanisani badala ya KUSTAREHE?”

  Jibu
  Jifunze usabato ulivyo. Wale wanaoivunja sabato kwa maana ya kufanya usafi, kunyosha nguo, kununua au kupika chakula n.k. siku ya sabato, hao wanatenda dhambi. Wale wanaofanya majukumu ya kikanisa, kama vile kuhubiri, kusaidia watu kama vile wagonjwa n.k. hao hawatendi dhambi. Jifunze kwanza usabato kabla ya kuuzungumzia usabato.

  Swali 2
  “Hivi mwimbaji wa Kisabato awapo kanisani akiimba nyimbo tangu asubuhi mpaka jioni anaporudi home anakuwa hajachoka? Au kuchoka ukitoa huduma za kanisa ni KUSTAREHE?”

  Jibu
  Uimbaji ulikuwepo siku za sabato hata tangu zamani za OT. Kazi ya kuhubiri/kufundisha Biblia kanisani ni luksa. Hiyo si dhambi!! Ushauri wangu, jitahidi kuufahamu kwanza usabato, maana unaandika vichekesho kaka!!

  Swali la 3
  “Mbona tunawaona wasabato wengi wakienda kusali umbali mrefu sana kutoka majumbani mwao hadi kanisani tofauti na kanuni za SABATO kuwa huruhusiwi kutembea umbali wa zaidi ya mita 200 hadi 500 yaani umbali wa kutupa jiwe?”

  Jibu
  Hili la kutembea umbali wa kurusha jiwe siku ya sabato, linawatafuna watu wengi hasa wasio wasabato. Milinga, na wengine, naomba mnioneshe aya ndani ya Biblia inayosema kuwa, wasabato wanapaswa kwenda mwendo wa kurusha jiwe tu siku ya sabato!! Naomba aya!! Nitafurahi kujifunza kwenu pia!!

  Swali la 4
  “Kama Mungu ALISTAREHE SIKU YA SABA BAADA YA KAZI, Mbona wasabato hawafanyi STAREHE? Au hili Neno KUSTAREHE lina maana gani kwenu wasabato wenzetu?”

  Jibu
  Neno starehe maana yake ni pumziko, hali ya kutofanya kazi yoyote yenye lengo la kujiongezea kipato au chakula!! Kibiblia, neno starehe katika muktadha wa Sabato, ina maana ya pumziko takatifu la siku ya saba ya juma(jumamosi ya leo) la kujifunza ukuu na upendo wa Mungu kwa wanadamu. Siku maalumu ya kumwabudu Mungu kama ishara yake ya uumbaji.

  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 188. @ Sungura
  Maswali yangu kwako
  1. Naomba unifafanulie maana ya imani isiyo na matendo na yenye matendo kwa mujibu wa amri ya 1-4, na kisha amri 5-10 katika Biblia.
  2. Ni nini maana ya imani bila matendo na imani bila matendo ya sheria? Hebu fafanua Biblically!!

  Majibu ya maswali yako
  Swali 3.
  1. “Ivi ni wapi biblia imesema kuwa kifo cha Yesu kilikomesha tu mambo ya kafara na mambo mengine ya torati na sheria zake yalibaki kama yalivyo?”

  Jibu
  Kama unafikiri kifo cha Kristo kilikomesha na mambo mengine ya torati na sheria zake, nenda kaibe kama hawatakupiga na kukufunga jela!! Nenda kazini uone kama hutashughulikiwa. Kwa ujumla, vunja amri za Mungu ili uone kama utasalimika mbele za Mungu. Mungu anakuita wewe binafsi kama Sungura ili uishi kwa kufuata maagizo yake. Kamwe usitake kufanana na watu. Taka kufanana na Kristo, aliye tumaini la wokovu wako.
  Amri(sheria) za Kristo ni kweli siyo nzito. Maana hizo ni amri za Mungu mwenyewe. Hujidhirisha kwetu tu pale tunapompenda Mungu kwa dhati. Ni amri zinazotokana na upendo –matunda ya upendo a.k.a matunda ya roho. Amri za Musa ndizo zilizokuwa nzito kwa kweli maana kwa masikini ilikuwa ishu kubwa sana. Adhabu ya kupondwa mawe kwa mdhambi, ilikuwa balaa mno!! Na Mungu alizotoa kama kivuli tu, kwa ajili ya kifo cha mwanaye. Kristo alipobambwa msalabani alizikomesha. Na hazikuwa sheria za kafara peke yake. Sheria nzito za namna hiyo(mbali na amri 10), zilikuwa nyingi.
  Na ukitaka kujua maana ya kifo cha Kristo na kazi yake, angalia maana za mnyama, njiwa au unga uliotolewa kama sadaka ya kuteketezwa kwa mdhambi enzi za OT. Angalia kwa umakini maana ya kafara hizo, na kile walichokuwa wakikifanya makuhani sehemu ya nje ya hema, sehemu ya patakatifu na sehemu ya patakatifu pa oatakatifu sana, huenda utag’hamua kitu chochote. Just do a self study!! Jifunze maana ya vitu vyote vilivyokuwemo ndani ya hema ya kukutania au hekalu, kuwa vilimaanisha nini!! Ni mambo marefu sana nikianza kukueleza hapa kwa sasa.
  Kwa msaada zaidi, ukijifunza mambo hayo, utakuja kubaini kuwa, kuna sheria za maagizo na amri kumi. Amri 10 hizo ni za Mungu. Zilikuwepo hata kabla ya dhambi na kabla ya mlimani Sinai. Hizo ni za milele. Kuna sheria za maagizo, hizo ni pamoja na sheria za vyakula, uraia, sikukuu za vibanda, pamoja na sheria za kafara!! Kifo cha Kristo, kilikuja kukomesha tu mfumo mzima wa kafara za wanyama tu na siyo sheria zingine wala amri 10.
  Kwa habari za wasukuma wasabato wa bariadi na magovi yao, mimi sijui!! Huenda ungeenda ukawauliza kama wanatahiri ama la!! Hapo ungekuwa na jibu sahihi!! Ukimuuliza Siyi au ukimtaka awachunguze wanaume wenzake wa kisabato kama wana magovi, utamuonea tu!! Nijuavyo mimi, suala la tohara ni zaidi ya jambo la kiroho, ni la kiafya pia. Wewe leta hoja kama unayo!! Acha kupiga porojo kijana!!

  2. Swali la 4.
  “Halafu kweli, mbona Morning star radio huwa haizimwi ifikapo saa Ijumaa saa kumi na mbili jioni ili kuwafanya wafanyakazi wake wapumzike a.k.a wastarehe kama sheria inavyotaka?”

  Jibu
  Nami napenda zaidi ya hapo, kwani makuhani wa zamani hawakufanya kazi ndani ya mahekalu/mahema siku ya sabato na wasihesabiwe dhambi? Wafanyakazi wa redio wanaposimamia kazi ya injili iwafikie watu maeneo ya mbali, wana tofauti gani na makuhani hao?!!

  Wewe kama utaendelea na ubishi wa kung’ang’ania uasi, endelea lakini tambua kuwa, hatima yake, ni upotevu na uangamivu wa milele. Zipo sheria zilizokomeshwa na kifo cha Kristo. Na zipo sheria ambazo, bado zipo hali leo na zitaendelea kuwepo hadi Kristo takaporudi. Uhuru tulio nao mbele za Kristo, siyo uhuru wa kuendelea kuzivunja amri zake (kutenda dhambi), hasha!! Uhuru tulio nao ndani ya Mwokozi wetu, ni utii wa amri zake kama matokeo ya upendo wetu kwake. Na hiyo ndiyo maana ya wepesi wa nira yake na amri zake pia.

  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 189. bw. Lwembe, maelezo yako mengi ni ya mtu asiejua vizuri jambo ila anajaribu kulitetea kwa kuficha ile aibu yake, kwa hiyo hebu tuwaachie wanaojifunza wayatafakari wao wenyewe.

 190. mr. Sungura, umenisababisha nirudi tena ili unijibu maswali yangu mawili. Ni wapi mimi nimesema kuwa torati bado inashika hatamu? Ni wapi mimi nilipotetea mambo ya kushika sabato!.

 191. Siyi,

  Hebu twende ndani zaidi na kwa detail zaidi.

  Ivi ni wapi biblia imesema kuwa kifo cha Yesu kilikomesha tu mambo ya kafara na mambo mengine ya torati na sheria zake yalibaki kama yalivyo?

  Nimekuona hili umelisema mara nyingi sana.

  Lakini naona kama ni wazo la kufikirika zaidi kuliko kuwa halisia katika maandiko. Na mawazo haya hutokana na mtu kushindwa kuelewa nini ilikuwa maana ya kifo cha kristo katika kuhusiana na torati na hivyo anaishia kuchanganyikiwa.

  Miaka yote ambayo torati ya Musa imekuwepo Israel hawakuweza kuishika, pamoja na kufa bila huruma pale waliposhindwa kuishika, lakini bado hawakuachaga kuivunja.

  Ati leo out of those penalties mataifa akina Sungura na akina Siyi na akina Lwembe, akina Muhina, kina Milinga, n.k, ambao hapo kwanza hawakuwahi hata kuwa na habari ya Yehova,waje watakiwe kuishika torati na kuiweza!

  God is not that crazy.

  Yeye mwenyewe alichoka na wana wa Israel ambao waliona matendo yake ya kutisha, sembuse na mataifa hawa ambao hawakuwahi hata kuwa na hint ya habari zake aje awalazimishe kuishika torati.

  Kama Yesu na kifo chake alichokiondoa ni zile kafara tu, uko wapi sasa wepesi wa sheria yake, maana kusema kwake kuwa amri zake ni nyepesi alimaanisha sheria ya torati/ sheria ya Musa ilikuwa nzito.

  Ku wapi sasa kusema kwake kuwa nira yake ni laini na mzigo wake ni mwepesi, ulaini wa nira yake tofauti na wa nira ya torati uko wapi, uwepesi wa mzigo wake u wapi, kama bado hawa mataifa wanapaswa kuubeba mzigo mzito wa sheria ya Musa?

  Au unadhani kilichokuwa kizito ni wale wanyama wa kafara za kila mwaka? Unatakiwa kujua logic za mandiko.

  Tena ni kongwa gani ambalo Petro alisema kuwa liliwashinda baba zao na wso wenyewe, hivyo halitakiwi wawatwishe mataifa, ni hao wanyama wa kafara au?

  Nionyeshe basi maandiko yanayoonyesha kuwa hii Yesu aliiondoa kwa kifo chake, na ile hakuiondoa, maana naona unaongea kikusadikika tu!

  Kama naweza kuhesabiwa haki kwa kutunza sabato, baso imani yenye kunifanya nihesabiwe haki nafasi yake hapo ni nini basi? Maana ktk kuhesabiwa haki au ni kwa njia ya matendo ya sheria, au ni kwa njia ya imani. Yaani moja ikifanya kazi moja haifanyi.

  Ivi ninyi wasabato mnashika torati ipi hasa, je ni zile amri kumi, lakini mbona kutokula nguruwe hakuko kwenye amri kumi, au ni pamoja na zile nyingine zilizp nje ya amri kumi, lakini mbona ninyi hamtahiri siku ya nane kama alivyofanya Yesu.

  Halafu, ivi wasabato wote wanaume hakuna wenye magovi kweli, wasukuma wale wa bariadi walitahiriwa lini, ninavyowajua hawapendi kabisa kukatwa?

  Jaribuni kuchunguzana ninyi wanaume wa kisabato, maana naamini kuna wenye magovi, hivyo wamevunja torati.

  Au na kutahiriwa nako ilikuwa ni sadaka ya kafara, hivyo kifo cha Yesu kimekukomesha?

  Halafu kweli, mbona Morning star radio huwa haizimwi ifikapo saa Ijumaa saa kumi na mbili jioni ili kuwafanya wafanyakazi wake wapumzike a.k.a wastarehe kama sheria inavyotaka? Maana mtangazaji, fundi mitambo, n.k kuendelea kuwa ofisini siku ya sabato ni kufanya kazi.

  Kwa kifupi, hamwezi kuishika torati leo, ni kelele tu za uongo wa dini.

 192. Wapendwa,

  Katika yote hii ya Mr. Siyi imeninyanyua kutoka kwenye kiti changu mpaka nikaamua niandike angalau kidogo tu kuchangia mada hii.

  Siyi amenifurahisha sana aliposema wao wasabato wanaiheshimu siku ya sabato kama Mungu alivyofanya siku ya saba akapumzika na kustarehe. Nanukuu kutoka kwa Mr. Siyi, …………………”“Ikumbuke Siku ya Sabato uitakase…”
  Mwanzo 2: 2-3 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; AKASTAREHE SIKU YA SABA, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Kutoka 16: 23 Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana KESHO NI STAREHE TAKATIFU, SABATO TAKATIFU KWA BWANA; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi. 30 Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba. Ndiyo maana sisi wasabato tunaamini kuwa kupika chakula/ au kununu chakula/kitu chochote siku ya sabato kwa makusudi ni dhambi ya kuvunja Sabato””

  Ukweli ni kwamba Wasabato hawafuati SABATO YA BWANA kama yanenavyo maandiko hayo kwani tunaishi nao na tunaona matendo yao kila siku mitaani kama wao pia wanavyotufahamu na kuona matendo yetu mitaani sisi ambao hatufuati Amri za Kale.

  Zifuatazo ni sababu zangu zinazodhihirisha kuwa hakuna Mtu anayeifuata SHERIA YA SABATO katika zama za leo. Sababu hizo ni:

  1. MUNGU ALIPUMZIKA NA KUSTAREHE SIKU YA SABA AKAACHA KAZI ZOTE.

  Wasabato hawapumziki wala kustarehe siku ya Saba kama Mungu alivyofanya na kuamuru Wanawaisraeli wafanye. Siku ya Sabato tunawaona wakiwa bize kanisani. Huyu yuko bize kuhubiri, yule yuko bize kuimba, mwingine yuko bize kupika chakula cha waliofika kanisani, wengine wako bize na kuandaa ukumbi wa kanisa, wengine wako bize za Studi za Redio zao, Wengine wako bize kuendesha magari kwenda kanisani, wengine wako bize kunyoosha nguo za kuvaa ili waende wamependeza kanisani, wengine wanaendesha baiskeli kwenda kanisani kusali.

  Maswali kwa Siyi na Muhina:

  Je, HII NDIYO SABATO aliyoikusudia MUNGU wanadamu wawe nayo? Mbona mnakuwa bize sana kanisani badala ya KUSTAREHE?

  Hivi mwimbaji wa Kisabato awapo kanisani akiimba nyimbo tangu asubuhi mpaka jioni anaporudi home anakuwa hajachoka? Au kuchoka ukitoa huduma za kanisa ni KUSTAREHE?

  Mbona tunawaona wasabato wengi wakienda kusali umbali mrefu sana kutoka majumbani mwao hadi kanisani tofauti na kanuni za SABATO kuwa huruhusiwi kutembea umbali wa zaidi ya mita 200 hadi 500 yaani umbali wa kutupa jiwe?

  Kama Mungu ALISTAREHE SIKU YA SABA BAADA YA KAZI, Mbona wasabato hawafanyi STAREHE? Au hili Neno KUSTAREHE lina maana gani kwenu wasabato wenzetu?

  Naomba leo niishie hapa kwanza ili nipatiwe majibu ya maswali yangu.

 193. Mhina inaendelea…
  Kuna vijimakosa vya kiandishi, niko taiti nakosa muda wa kuedit, so ucjali sana)

  Kwa hiyo usipoangalia kwa makini unaweza ukafikiri kuwa Yakobo anasema kuwa tunahesabiwa haki kwa matendo, la hasha hamaanishi hicho.
  Kuna tofauti kati ya Imani bila matendo na imani bila matendo ya sheria.

  Ibrahim hakuhesabiwa haki kwa sababu ya kile kitendo cha kusafiri na Isaka mpaka kumweka juu ya kuni ili amchinje. Bali alihesabiwa haki kwa kule kukubali moyoni mwake kufanya ambacho Mungu kamwambia.(kukubaliana na Mungu)

  Hata kama yangetokea mafuriko ya maji asiweze kusafiri kwenda kwenye ule mlima, au hata kama angeugua akashindwa kusafiri kufanya hilo tendo la kumweka kijana juu ya kuni, angehesabiwa tu hiyo haki.

  Rum 4:3- inasema kuwa kama Ibrahim alihesabiwa haki kwa sheria basi ana sababu ya kujigamba, lakini si mbele za Mungu.
  Lakini sasa hivi Ibra alihesabiwa haki kwa kile kitendo cha kumwamini Mungu kuwa alichosema kitakuwa.

  Ukitaka uhesabiwe haki kwa kazi uliyofanya, maana yake ni kwamba hiyo haki yako siyo neema tena, lakini ni stahili yako ya lazima.

  Lakini yeye ambaye hakufanya kazi yoyote ya kumpa hiyo haki lakini kamwamini mwenye kuwahesabia haki wasiostahili pia, basi kwa huyo hiyo haki ni kwa njia ya imani.

  Mhina, mnaotaka kuhesabiwa haki kwa kuwa hamkuiba, hamkula nguruwe, mnasali siku ya J’mosi, ni sawa na kuwa na bidii ya bure maana haiko ktk mtiririko wa kweli ya Mungu.

  Haki inayotokana na kushika hayo, inaitwa haki kwa njia ya sheria. Kwamba mtu anaishi kwa kushika hayo, ikitokea amekosa kuyashika basi tena hana haki.

  Ivi ulishawahi kujiuliza kuhusu kosa la uzinzi la Ibrahim, kwa nini Mungu alipotezea, kwa nini hakumwadhibu Ibrahimu?

  Haya, nasubiri maswali, maana najua kuna vitu nimeongea vitaibua maswali.

  Thank u!

 194. Mhina,

  Mara kadhaa umeonesha mashaka kama naweza kukuelewa maana unadhani sijui sawasawa.

  Sikia bro, ni kweli sijui yote, lakini haya ambayo wewe ubaongea ni ya kiwango cha kawaida sana kama si cha chini.

  Sasa, ni vigumu sana kuongelea imani bila kuijua hiyo inani ni nini na ikoje.

  Nilitunia neno Faithna Belief ili tu nijaribu kukukunbusha kuwa imani ni kitu kipana, japo wewe unakiangalia kwa angle moja tu.

  Kuna kitu kinaitwa Common faith(imani tu ya kawaida). Kama hii ya ” ujimkiri Yesu kwa kibywa chako ya kuwa ni Bwana…. Rum 10: 5-13.

  Na kuna imani ambayo ni karama eg: imani kama punje ya haradali, ambayo ndo inayosemwa ktk 1Wakor 12:9 – to another (it is given) faith by the same spirit.

  Common faith ndo hasa tunayoongelea hapa kwa habari ya kuhesabiwa haki kwetu.

  Lakini imani kama karama ndo hasa anayoongelea yakobo, kwamba unasema namwamini Mungu kwa ajili ya jambo fulani halafu hufanyi yale ambayo ni wajibu wako.

  Aliyeambiwa na Yesu ajitwike godoro aondoke asingejitwisha asingepona. Ilikuwa ni wajibu wake kujitwisha godoro, kuonesha kwamba ameukubali uwezo wa anayemwambia kufanya hivyo(Yesu)

  Ndo hiyo imani inayosemwa ktk Mark 11:24 …yoyote myaombayo …aminini mnayapokea…

  Ndiyo hiyo bila matendo imekufa. Kwamba bila tendo la kujitwika godoro, bila tendo la kwenda kunawa baada ya kupakwa tope machoni, bila tendo la kumfuata Yesu ili mwanao awe mzima( biti Yairo), bila tendo la kutoka kwenye mtubwi na kutembea majini, bila tendo la kujipenyeza mpaka uguse upindo wa vazi la Yesu( mama aliyetokwa na damu, imani hiyo imekufa!

  Na wala haimaanishi bila tendo la kusali siku ya sabato, bila tendo la kutokuzini, bila tendo la kutotoa zaka, bila tendo la kutokutamani mali ya mwingi, bila tendo la kutomchukia nduguo, n.k, sentensi ya %imani bila matendo imekufa” haiongelei matendo ya sheria.

  Nitaendelea….

 195. Mhina,

  Ivi kama torati bafo inashika hatamu, kwa nini Yesu anatupa amri mpya ya kupendana, kwani torati haikuwa imeagiza kupendana?
  Kwa nini hii ya Yesu iitwe amri mpya, kuukuu yake ni ipi, maana hakuna kitu kipya bila kuwepo kikuukuu!

 196. Lwembe,
  Kwanza, nilikwambia tangu siku ile kuwa, ufedhuli kaka siyo mzuri. Mtu mzima na akili yako kabisa huwezi kusema “Maandiko yana kona nyingi saaaana ndg yangu, tena za makusudi ya kuwapoteza watu wa dini!”. Haya ni maneno ambayo hayafai kusemwa na Mkristo anayemwamini Kristo kiuhalisia. Maana ukisema hivyo, utakuwa unamaanisha kuwa Mungu amenena nasi kwa njia ya mafumbo tu kiasi kwamba hatuwezi kumwelewa!! Na wewe peke yako tu, ndiye mwenye ujuzi wa hayo mafumbo ya Mungu na unataka tukuamini hivyo!! Huuni ufedhuli wa kutosha kabisa!! Maana Biblia inasema, “Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake” Isaya 48:16.
  Pili, Huwezi kusema kuwa Mhina hazijui sheria!! Umeingia kichwani mwake ukaona jamaa ni mbumbumbu wa sheria??? Huenda wewe ndiye huzijui!! Ndiyo akili yako inaishia tu kwenye sheria za kafara peke yake!! Huendi beyond kama anavyoenda Mhina. Kama hata na amri 10 zingeishia msalabani, baada ya kifo cha Kristo, kusingekuwa na dhambi tena, maana hakuna sheria/amri. Kama hakuna sheria/amri, hakuna kosa!! Je, ni kweli leo hakuna makosa/dhambi? Kama mambo hayo yapo, ina maana baadhi ya sheria alimaarufu AMRI, zipo na ndizo kioo chetu cha kutusogeza karibu na Kristo ili atutakase kwa damu yake by faith only!! Wewe, Sungura na wengine, ndio mnaoishia kwenye sheria za kafara, jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama wenu wa baadaye kwa wakristo kama mnavyojiita!! Kupitia kinywa cha Kristo mwenyewe, tunaambiwa kuwa, Tukimpenda Kristo, sharti tuzishike amri zake (Yohana 14:15. Na wala hakusema kuwa, nikifa tu, mtaachana na amri hizo!! Hakusema!! Na zaidi ya hapo anasisitiza kuwa, “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito” -1 Yohana 5:3. Ishara aliyotupa Mungu ya kuonesha kuwa tunampenda na kumcha YEYE, ni kuzishika Amri zake kama matokeo ya UPENDO wetu kwake na kwa wanadamu wenzetu, na siyo kujiita umeokoka!! Na kama wewe ni mwanafunzi mzuri wa Biblia, huwezi kusema kuwa upendo na utii haviendani!! Huko ni kutudanganya kabisa. Huwezi ukampenda baba yako mzazi, halafu usifuate maagizo yake!! Haiwezekani; ndiyo maana ya “Mkinipenda, mtazishika amri zangu” Yohana 14:15. Kama utampenda Mungu, utendaji wa matendo mema alimaarufu matendo ya sheria/amri, utatokea kiotomati tu, kama matokeo ya upendo. Na hili ndilo fundisho la Biblia tangu Agano la Kale hadi Agano Jipya!!

  Neema ya Bwana ikufunike
  siyi

 197. Mhina,
  …. ninaendelea

  Tatizo kubwa la Dini ni kule kujaribu kuyatangulia Maandiko, ndipo kwa kutumia kwenu akili mnaishia ktk ujinga, mkijitwisha mizigo isiyowahusu! Hakuna anayeweza kuyaelewa Maandiko bila UFUNUO; Mungu ameyaseti ktk jinsi hiyo! Nayo Imani ni Ufunuo na si “Kutii Sheria”; na wala Kutii Sheria si udhihirisho wa Imani bali ni udhihirisho wa kuiepuka Hukumu yake! Ni Sheria au Amri ipi aliyoitii Habili ambayo nduguye Kaini aliivunja, hata Mungu akamtakabali yeye tu na dhabihu yake? Mwa 4:3-5 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake.”

  Hao hapo ndg wawili wakimtolea Mungu sadaka kulingana na shughuli zao wanazozifanya. Mkubwa akakataliwa, yeye na sadaka yake!!! Hakuna maelezo ktk Agano la Kale yanayotuambia kwanini Kaini alikataliwa, na wala yanayotuambia kwanini Habili alikubaliwa. Wengi wa waliojirudisha huko kwenye Sheria, wametunga Uongo wa kwamba sadaka ya Kaini ilikuwa ni ya “mazao mabovu” ndio sababu Mungu hakuipokea; huu ni Uongo! Na kulingana na Sheria, yeyote anayeongeza juu ya Neno la Mungu anastahili kifo, na ndio maana wengi leo hii wamekufa licha ya kwamba wanatembea, lakini kwa ujinga wataukosa Uzima wa Milele!!!

  Lakini Maandiko huku Ng’ambo yanalifunua jambo hilo kwamba, “Kwa Imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini.” Kama Imani ilihusiana na Kutii Sheria unakokufundisha, tungaliliona jambo hilo hapo Sheria hiyo ilipotolewa kwa Kaini na Habili, lakini halipo! Basi kutoka Andiko hili ndio tunafahamu kwamba Imani ni Ufunuo, Habili alifunuliwa sadaka inayopaswa kutolewa, na Kaini HAKUFUNULIWA, yeye alitumia akili zake tu, na akategemea Mungu amkubalie ktk mambo yake ya dini, labda aliipamba madhabahu yake kama zinavyopambwa leo hii kwa maua nk, kinyume na madhabahu ya Habili iliyotapakaa damu!!!

  Basi Imani ndio mlango wa kwanza unaofungua mawasiliano kati ya Mungu na watoto wake na si jitihada za mwili!!! Mungu amelificha jambo hilo kwa makusudi, ametuacha tuendelee ktk akili zetu! Yaani hilo Andiko na mengineyo unayoyaona ktk hiyo Ebr 11, yanasomeka hivi: “”Kwa Ufunuo Habili alimtolea…””; yeye alifunuliwa kuhusu ibada hiyo, maana Mungu ndiye anayejua tufanye nini ili atukubali kama wanae tena, ndio hayo maelekezo aliyopewa Habili naye AKAYAPOKEA, na si kuyatii; Kutii kunahusiana na Sheria na Utumwa, bali ktk Upendo sisi hupokea mambo mazuri ya Mungu anayotukirimia, kwa NEEMA, ndio huo Ufunuo!

  Nilikupeni kisa cha Yn 6:55-56, jaribu kukirejea kisa hicho ili kikusaidie kujifunza kuhusu Imani. Wengi misimamo ya dini zenu mnaichukulia kuwa ndio Imani. Matokeo ya jambo hilo ndio mmekaririshwa ngonjera za kwamba mnapoambiwa kwamba mnao Uhuru ktk Kristo, basi kwa kutumia kwenu akili, upesi mnauona Uhuru huo kwamba ni kujihusisha na Uzinzi, wizi, ufisadi nk; huku ndiko kuchanganyikiwa ninakokusema! Uhuru ktk Kristo ni UPENDO!!!

  Tazama dini inachoweza kukufanyia ni kukuleta mpaka hapo ulipo na kisha kukufungia hapo usiendelee mbele! Dini inakufikisha mpaka ktk kiwango cha kuzaliwa mara ya pili, ndiko huko kuhesabiwa haki kwa Imani unakokirimiwa baada ya kuamini kwamba Mungu yupo, ktk Kristo, na ukatakaswa, tayari kwa kutumika. Hatua hii inakufanya UUONE Ufalme wa Mungu, Yn‬ ‭3‬:‭3‬‬‬‬ “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Sasa, kuliona jambo na kuhusika nalo ni mambo mawili tofauti. Maelezo yako mengi ni ya mtu aliyeuona Ufalme wa Mungu kupitia dini, kisha akafungiwa hapo asiendelee mbele apate KUINGIA humo ili yale aliyoyaona kwa huko mbali sasa aweze kuyashika kwa mikono yake ktk uhalisi wake.

  Dini zinakupiga locki ktk sehemu hii kwa kukupa mafundisho yanayopingana na Neno la Mungu, ili kukuzuia USIUINGIE Ufalme wa Mungu ukawaacha wao huko nje peke yao!!! Yn.‬ ‭3‬:‭5‬ “Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Dini inakufikisha kiwango cha kupewa roho mpya, ambaye wengi wetu twadhania kwamba ndiye RM, ndipo tungetulia hapo kama kuku wa kizungu na kuendelea kunenepeana tukingojea kuchinjwa! Umuhimu wa kujazwa RM wa kweli unaonekana tunapofikia Hatua ya KUINGIA ktk Ufalme, ndiko huko Kuzaliwa kwa Roho ukiisha kuwa umezaliwa kwa maji (Mdo 2:38), hapo ndipo utayaelewa na ya huyo tasa anayenunua vinguo vya mtoto asiyenaye; na jambo la “Imani bila matendo imekufa” utalielewa hili pia ktk urahisi wa lilivyo tamkwa na si ktk jitihada za dini ulizosetiwa ili utoe sadaka nyiiiingi mpaka uweke viraka suruali yako!

  Nitarudi tumtazame huyo tasa na Ibrahimu ktk ujumla wa suala la Imani!!!

  Gbu!

 198. Mhina,
  …. ninaendelea

  Labda tuiangalie tena IMANI ili tujiridhishe kuhusu hiyo ili tupate kujua kwa uhakika hiyo ni nini tunapoyatazama hayo matendo “mema”. Maandiko kuhusu IMANI, yanatuambia kama Sungura, nawe pia ulivyoyanukuu, kwamba, “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Sasa ukilichukua Andiko hili kiakili utaishia kudai magari na majumba ya fahari uliyoyaona ktk ndoto zako za “Alinacha”; hata wengine nimewahi kuwaona wakiamrishwa kuyaendesha magari ya ndoto zao mpaka nikajisikia aibu. Mtu mzima anaambiwa “Haya, kwa imani washa gari na uliendeshe!” Ndipo ungemsikia, “Te-nyenyenyee, vruuuum…….!” Kama si wendawazimu ni nini? Wengine bila ya aibu hujipachika utakatifu kwa kutii Amri moja tu inayohusu Sabato, kwamba hicho ndio kipimo cha imani; nao hawajui kwamba kwa jambo hilo wamejiingiza ktk Laana ya kutoitimiza Sheria yote!

  Lakini, ukilitafakari Andiko hilo ktk Nuru ya Injili, utasogezwa mbele zaidi ktk ufahamu, maana kama Imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo, basi ni lazima uwe na hilo Tarajio kwanza ndipo uhakika wa tarajio hilo utafsirike kama Imani; pia ubayana wa hayo yasiyoonekana ni lazima utanguliwe na KUYAONA hayo (Matarajio) yasiyoonekana, ndipo tendo hilo liwe bayana ktk ukamilifu wa Imani! Hivyo basi, hayo yasingewezekana Kutarajiwa au kuwa Bayana mpaka Ahadi au Maelekezo yanayoyatambulisha mambo hayo yawe yametolewa kwanza, vinginevyo huwezi kutarajia jambo usilolijua na wala ubayana wake hauwezi kuwapo pia, “”fullstop!””!!

  Tena, Maandiko kuhusu hiyo Imani, ule msingi wake unaokupelekea kuwa na hiyo hakika ya mambo yatarajiwayo, hata yakawa bayana hayo yasiyoonekana, yanatufundisha kwamba, “Imani” huja kwa kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Sasa, iwapo kusikia kwetu huja kwa neno la Kristo, hivyo tukiisha kupewa huko kusikia ndipo Imani yaweza kuja; Basi kutii kwako Sheria, hiyo ambayo haikuwaletea hao “kusikia” hata wapate “Imani”, hauoni kwamba kujishughulisha kwako na jambo hilo ni kujipoteza Njia? Tazama hapa kinachoongelewa ktk Ebr 4:2: “Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao (WALIOIPOKEA TORATI). Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.” (Msisitizo ni wangu).

  Unaona, hiyo Habari Njema waliyohubiriwa, ile Torati au Sheria haikuwafaa kitu kama ambavyo nawe haijakufaa, kwa kule kutochanganyika na Imani! Imani ni jambo jipya linalokuja ktk package ya Injili ya Yesu Kristo kama ilivyohubiriwa na mitume; Sheria inaambatana na Hukumu, ndio ile Laana mliyojiingiza kwa kutokuitimiza Sheria yote, na ndio maana mngali mnahangaika na dunia, mkijitahidi ktk hili na lile ili kujiweka ktk “utakatifu” mliojitungia, hamjui hata kwamba Utakatifu ni wa Mungu, yeye ndiye hutupa sisi Utakatifu wake!

  Bado naendelea….

 199. Mhina, (na Siyi nawe),

  Maandiko yana kona nyingi saaaana ndg yangu, tena za makusudi ya kuwapoteza watu wa dini! Maelezo yako mengi, naweza kusema ni ya mtu aliyeihifadhi Liturgia au Katekesimu kwa wingi moyoni mwake kuliko Neno la Mungu; nilipokuona umekazana na ” Imani bila matendo ‘mema’ imekufa” ndipo nikakuona na katekesimu yako; umefanya vema kumshukuru Sungura!!

  Maswali aliyokuuliza Sungura, kama ungechukua wasaa kuyatafakari ktk UHURU wa Injili, yangekusogeza angalau hatua moja kuelekea kufunguliwa akili ili uyaelewe na Maandiko!

  Unapozungumzia “Imani bila matendo imekufa”; halafu ukalipeleka Neno hilo kumaanisha ni “Utii wa Sheria” (usizozijiua), unakuwa ni sawa na mtu aliyejipoteza porini, yaani umeikosa ile kona ya Injili, ukapitiliza na Torati! Mungu anatangaza ktk Rum 10:4 kwamba, “Kristo ni Mwisho wa Sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki”, basi huwezi ukaigeuza kauli hii kwa namna yoyote ile na ukabaki salama!

  Agano la Kale ndg yangu, pamoja na Sheria zake zilizoandamana na Hukumu zake, linakamilika ktk ujio wa Kristo, ndio maana mahali fulani Mungu anasema kwamba ameongea nasi kupitia manabii na hiyo Torati, mpaka kipindi cha Yohana Mbatizaji; baada ya hapo anaongea nasi kupitia Mwanae! Ni muhimu sana utafute kujua maana ya kauli hii kwanza ili uweze kuendelea mbele ktk usahihi, vinginevyo ndio unaishia ktk mkanganyiko kama huu uliomo; kwamba ungali unataka Mungu aseme nawe kupitia Sheria, na pia aseme nawe kupitia Mwanae ambaye ndiye ile “Imani” inayoikomesha Sheria; basi utamrejeshaje Mungu ktk jambo alilolikomesha, kwamba alikosea kulifikisha ktk ukomo? Kama huko si kujichanganya ni nini? Ndio maana unaulizwa kuhusu jambo hilo la Sheria, kwamba, iwapo Kristo aliitimiza Sheria yote, basi ni nini alichokisaza kuhusu Sheria ambacho wewe na jamaa zako akina Siyi ndo mnakitimiza??? Jambo lililotimizwa kaka, maana yake limekwisha au limekamilika, kujaribu kufanya chochote kulihusu maana yake ni kwamba HUJAELEWA kilichofanyika, ndio kule kuabudu usichokijua, kama ninavyokuona, ishara ya ukosefu wa Imani!

  Unapovuka kuingia ktk Agano Jipya bila ya ufahamu kamili wa kilichofanyika, utayakosa mambo mengi sana matamu aliyokutayarishia Mungu! Hatari ya kwanza unayojiingiza ni pale zile Sheria zinaporejewa tena upande huu, pale unapokutana na Maandiko kama “Amri mpya nawapa…”, au anaposema, “Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, …” nk; kisha ukayachukua hayo na kuanza kujitahidi kuwapenda nduguzo, ukijitahidi kuikimbia hasira, ukiongeza jitihada za kujizuia uzinzi, nk, huku ukiimba mwimbo wa “imani” kwa bidii kuiongoza nafsi yako ktk kuyatimiza hayo; ukweli ni kwamba umejirudisha ktk Sheria, si ile ya Agano la Kale hapana, bali hii iliyoboreshwa huku ktk Agano Jipya, hilo la rohoni, nayo Sheria hii mpya Hukumu zake ni za Rohoni, yaani hakuna anayekupiga mawe ktk mwili, bali roho yako imekwisha kupigwa mawe!!!!

  inaendelea….

 200. KUTIMIZA TORATI NA SHERIA MPYA YA KRISTO: Basi, nimalizie kwa kusema kua, katika maisha yetu ya imani, ni lazima kufanya matendo mema yanayompendeza Mungu, ili ile imani yetu, ithibitike na kutuletea nguvu zaidi, kwa kua, hata hiyo sheria mpya ya kristo ya upendo, inatufundisha na kututaka sisi, tuithibitishe haki, kwa kufuata kile kielelezo cha maisha yake ya upendo….tena ” tuenende kwa adabu, si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu, bali mvaeni bwana yesu kristo, wala msiuangalie mwili hata kuwasha tamaa zake. Huku ndiko kutimiza torati na manabii kwa bwana yesu kristo, katika sheria yake mpya ya upendo…kwamba, sio tu, tuseme tunaimani, ila yeye alitaka hao walioamini wenye imani, wathibitike zaidi katika maisha yao ya kila siku, mbele za watu wote, yaani pia inawapasa wawe na matendo mema ya kuwatofautisha na kuwathibitisha, hiyo imani yao mbele za watu wote, ndio maana, biblia inatuambia hivi” ili tukihesabiwa haki kwa neema yake (KRISTO) , tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu, Ni neno la kuaminiwa, na mambo haya nataka “uyanene kwa nguvu” ili wale walioamini Mungu, wakumbuke kudumu katika ” MATENDO MEMA. Hayo ni “MAZURI, TENA YANAFAIDA KWA WANADAMU, !!!!!!!!. Soma(Tito 3:7-9). Ndio maana Pia, Mtume Paul aIisema” YAVUENI MATENDO YA GIZA NA KUVAA SILAHA ZA NURU”….Sasa, ni nini kuyavua matendo ya giza kwa mkristo?, si kuyaacha matendo mabaya ili utende matendo mema ya nuru?. Basi hii ndio haswa maana ya imani yenye matokeo ya kutupa nguvu ya kutarajia chochote tunachomuomba mungu, na kutufikisha katika uzima wa milele. Na hii pia, ndio ukamilifu wa torati yote na manabii, yaani kujifunza huu upendo wa kristo, wenye sheria mpya ya uhuru na upendo. Ndugu sungura na wafuatiliaji wote, mimi naishia hapa, mbarikiwe sana.

 201. Pandael,
  Unachosema ni kweli. Sasa wewe sema ulichotaka kusema hapa ili tuendelee na mjadala badala ya kuendelea kuuliza rhetoric qns!! Sawa mzee??? Karibu sana
  siyi

 202. ndugu sungura, nilisahau kukujibu na swala la yule tasa. Lakini ukweli unaendelea vilevile kwa kua, hata huyo tasa alipokua na imani ya kutarajia kuzaa, wewe mwenyewe uliona matendo yake ya imani yalivyomsaidia, maana alichukua hatua ya” KUANZA KUNUNUA NGUO ZA MTOTO KABLA YA KUA NA UJAMZITO!!!!!!!!!!!

 203. ….wala usiwe na wasiwasi ndugu Sungura, utanielewa tu. Mimi sasa ninaondoa maelezo mengi ili nikujibu vile unavyotaka. SWALI: Unataka tofauti kati ya imani na kuamini…si ndivyo ndugu yangu?…Sasa bahati mbaya, mimi sijawahi kuona fundisho la namna hiyo katika biblia, labda unionyeshe, usitumie mawazo ya akili zako, utapotea..tumia elimu na mawazo ya biblia peke yake, sawa?. Biblia inafundisha maana ya imani na jinsi ya kuishi kwa hiyo imani, kama nilivyoeleza hapo juu, fullstop!!. Kamwe hakuna tofauti ya imani na kuamini kwa kuwa, huyo huyo mwenye hiyo imani, ndiye anaeamini. Tazama vizuri: katika maana ya imani, tunatarajia mambo mengi kwa hiyo imani, bila ya matendo yoyote, yaani, kwa imani tu, Mungu atatusaidia yeye mwenyewe, mfano: Kumuomba Mungu atulinde wakati wa usiku, wezi wasiweze kutuibia, ni sawa tu, hiyo ni maana ya imani, maana umekua na hakika ya mambo unayoyatarajia. Lakini sasa pia, kuna jinsi ya kuishi kwa hiyo imani yako, katika maisha yako ya kila siku, ambapo pia kwa hii, biblia inasema kua “WAZEE WETU WALISHUHUDIWA”…Kama nilivyoonyesha mfano wa Nuhu hapo juu. Je, wewe ukimuomba Mungu akulinde usiku kwenye nyumba yako, huchukui hatua ya kufunga milango yako, eti kwa sababu ni kwa imani pekee!!!!. Tazama, ibrahimu pamoja na imani yake iliyompatia haki, alichukua hatua pia ya kumtoa mwanae isaka, awe sadaka kwa Mungu. Hili ndilo haswa, Mtume yakobo alilotufundisha, sio matendo ya kutafuta haki ila ni matendo ya utiifu wa hiyo imani yake, iliyompatia hiyo haki. Je, wewe unafikiri matendo haya hayana maana kabisa? Unafikiri ni matendo yasiyo ya maana kabisa juu ya imani yako?…haya, kama ni hivyo, lala milango wazi kwa makusudi kabisa, bila ya kuchukua hatua ya kuifunga hiyo milango ya nyumba yako, halafu umwambie Mungu akulinde kwa imani pekee, uone kama Mungu atakulinda. Bado nasisitiza kua, imani bila ya matendo yake mema ” IMEKUFA. Sasa, yakobo alizungumzia haswa jinsi ya kuishi kwa hiyo imani unayoitumaini kwamba, ni lazima tuzingatie matendo mema, akimaanisha haswa kwa wale wote ambao wamekwisha amini, ili awakomaze ile imani walioipokea, iambatane na matendo mema pia, hivyo pia, ndivyo kristo, alivyotuamuru “ZINGATIENI HAKI ILI MKATENDE MEMA”. Mimi bado sijaelewa linalokupa tabu ni lipi!!. Wewe unaongelea maana tu, ya imani, lakini bado hujajua jinsi ya kuishi kwa hiyo imani yako. Mtume Paul, alizungumzia haswa, maana ya imani, halafu kule mbeleni, akafundisha jinsi ya kuishi maisha ya imani yanayompendeza Mungu, hebu jifunze biblia vizuri ndugu yangu. Yakobo nae, akafundisha jinsi ya kuishi kwa imani katika maisha yetu. Bwana yesu na mitume wengine waliobaki walizungumzia mambo yote kwa wakati mmoja, yaani maana ya imani na jinsi ya kuishi kwa hiyo imani, ndio maana wewe unachanganyikiwa kwa kua, bwana yesu anafundisha kua, katika imani aliotupa, tuwapende majirani zetu kama tunavyojipenda sisi wenyewe, lakini jambo la ajabu wewe unaniuliza “IMANI KUA NA HAKIKA YA MAMBO YATARAJIWAYO, INAUHUSIANO WOWOTE NA MIMI KUMPENDA JIRANI YANGU !!!!!!. Vipi wewe ndugu yangu?. Usilazimishe biblia ifuate elimu yako, usije ukamkosea Mungu….sawa ndugu yangu?. JIBU LA SWALI LAKO JINGINE: Matendo ya imani yanayozaliwa na utiifu wa sheria, ni kama ile sheria ya kristo, inayotuambia hivi” Mmesikia kwamba, imenenwa, umpende jirani yako, na umchukie adui yako, lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi ili mpate kua wana wa Baba yenu aliye mbinguni, soma( Mathayo 5:43). Huu ni mfano mmojawapo tu, ndugu yangu, lakini yapo matendo mema mengi sana, aliyotufundisha bwana yesu, yaliyozaliwa na sisi kuwa watiifu wa sheria yake mpya ya upendo, na utiifu mbele za Mungu. Lakini utaona kua, ile sheria ya amri(andiko au torati ya Musa), haikua na msamaha, isipokua ilikua, uruma wake unajitukuza ndani ya hukumu. Biblia inasema kua, mtu aliyeidharau sheria ya Musa “HUFA PASIPO HURUMA” Maana, ile na matendo yake yote ya kutii sheria, ilikua ikisimamia haki ya Mungu, ambaye yeye HAKI YAKE NI KAMILIFU TUSIYOWEZA KUITII KWA ,100%. Mambo mengine ninayoandika, sijui kama unanielewa vizuri…unatakiwa ujue mambo ya sheria kisawasawa, ndio uweze kunielewa. Pia ufahamu wako wa biblia uwe wa kuridhisha, ndio utanielewa, mimi naamini bwana sungura unanielewa vizuri, hakuna tabu.Pia soma(embrania 10:28). JIBU JINGINE LA SWALI: Sasa ndugu yangu wewe, unachukua tu, maana ya imani ili ujenge hoja ya maisha yetu yote ya imani, si utatupoteza wewe!!!. Biblia haisomwi mstari mmoja ndugu yangu…lazima uelewe hivyo, ziko habari na matukio mengi yanayotufundisha maana halisi ya jambo katika uhalisia wake. Hivi mimi nimalizie hapa kwa kukuuliza hivi: ukiwa unaishi kwa hiyo maana ya imani uliyotuonyesha, haitakupasa wewe kumpenda jirani yako??, kwanini usimpende jirani yako!!!, wewe unafikiri imani ni kukaa tu, kama rohoti au jindege fulani?, hujui kuwa hiyo imani yako, inakupasa uidhihirishe kwa ndugu zako kwa njia ya upendo na kuwatendea watu mambo mema?, bado hujajua kua, wewe ni chumvi ya dunia kwa ndugu zako!!, bwana yesu alivyosema, tuwapende jirani zetu na kuwatendea matendo mema, tukilinganisha na hii imani yako, unayouliza kua ” KUNAHAJA GANI YA IMANI ITARAJIWAYO NA KUMPENDA JIRANI YANGU” Hivi hapo tujifunze imani yako isiyokamilika au ile ya uhakika ya bwana yesu, aliyetutaka sisi tuwapende jirani zetu?!!!!. Ndio tatizo la kutumia elimu nyingi za shule, badala ya kujifunza neno la kristo, HAYA SASA NA WEWE HEBU NISAIDIE HAPO NA UNIONYESHE HASWA, TUNAPOTOFAUTIANA NDUGU YANGU. Mwisho, Yakobo alikua akiongelea ” MATENDO MEMA KATIKA IMANI”…NIkweli kabisa kua ni ” imani bila matendo” sio bila matendo mema” neno mema haliondoshi ukweli ule….lakini nakiri kua, sikutenda vyema kunukuu biblia kwa msisitizo ule, basi nakuomba tusameheane, maana sio kweli kua, nilitaka nipotoshe. Oky, kazi kwako.

 204. Siyi,
  Si kila mchangiaji kwenye “Blog” hii anajua kila kitu ambacho miliwahi kuchangia.Mimi ni mchangiaji mpya kwenye “Blog” hii, hivyo ungenieleza tu mwanzoni kuwa mlishachangia kuhusu jambo nililowauliza.
  Ahsante.

 205. @ Mhina,
  Unazidi kuwa mtaaaamu!! Kah!! Songa mbele, mimi nakufuatilia tu kwa nyuma!! Ubarikiwe sana mtumishi.

  @ Pandaeli
  Najua unafahamu. Zaidi ya hayo, maswali yako hayo tulishawahi kuyajadili hapa mtandaoni. Tena nakumbuka nilitoa fasili ya dhambi, makosa na maovu au uovu!! Wewe kama una jambo la kusema, sema!! Acha kupiga chengaaa na kuzungukazunguka!! Be straight!!!
  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 206. Mhina,

  Umeongea saana, lakini nasikitika kuwa kuna maswali ya msingi hujanijibu.

  Mimi siyo mjinga na siandiki kwa pupa, kwa hiyo ninapokuuliza kitu usinichukulie poa kama ulivyofanya.

  Nilikuuliza tofauti ya Belief na Faith juu ya kile Yakobo amesema.
  Lakini hukunielewa kabisa, wewe ukadhani ninaongelea aina za imani(belief)

  Na maswali kadha wa kadha yako hapo nilikuuliza.

  Mimi imani yangu ni ile yenye msingi wake kwa mitume na manabii, sina imani tofauti. Simply hukunielewa.

  Kitu kingine unapotosha ni kule kusema kuwa Yakobo amesema imani bila matendo mema imekufa.
  Hakusema imani bila matendo mema, bali imani bila matendo, full stop!

  Mhina matendo ya imani yanayozaliwa na utiifu wa sheria ni yapi na yapi no matendo yanayozaliwa na amri?

  Imani (faith) ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

  Hebu niambie, kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo kuna uhusiano wowote na kumpenda jirani yangu?

  Na kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo kuna uhusiano wowote na tasa kuanza kununua nguo za mtoto bila kuwa na ujauzito?

  Haya maswali yaangalie kwa makini, kuna kitu ambacho nataka ugundue maana ya imani bila matendo imekufa.

 207. Siyi,
  Nimekuuliza ili nipate jibu kutoka kwako, kama hujui tofauti kati ya DHAMBI na MAKOSA, basi ni vema ukasema hujui.

 208. Asante sana “SUNGURA”!!. Sijui hili jina unatania, au ni lakwako kweli, maana ni jina la mnyama hili !!…oky, hakuna tabu ndugu yangu. Maswali yako ni ya msingi. Naandika kwa ujasiri kwa maana injili sio ya kwangu ila ni ya kristo,(tumepewa ujasiri na sio woga.). Hata hivyo, sijidhanii kua nimekamilika katika kila jambo, isipokua, mimi nakamilishwa na viungo vyengine kama wewe na wengineo. Hivyo, nivizuri tukikosea tusahihishane, sio kwa mashindano ila kwa haki yote….na mimi nikotayari kabisa, ndio maana niko hapa. BWANA SUNGURA: Usichanganye jambo la aina moja katika kulielewa. Kuna maana ya imani, na jinsi ya kuishi kwa hiyo imani, katika maisha yetu ya kila siku. Hakuna imani tofauti, zilizofundishwa na mitume katika vitabu vyote vya injili, tazama unavyosema” hebu tazama maana ya imani halafu uangalie kama iko sawa na ile imani aliyoifundisha yakobo!!!, si kwa tafsiri sahihi ulitaka utuonyeshe tafauti za imani katika injili kwa kigezo hicho?!!, basi ndugu yangu, imani ni ileile isipokua wewe huelewi. Ukweli ni kuwa, hakuna imani ya namna nyingine nyingine kwenye biblia, imani iliyofundishwa na mitume wote, ni ya aina moja inayomhusu yesu kristo pekee. Biblia inasema” MSICHUKULIWE NA MAFUNDISHO YA NAMNA NYINGINE NYINGINE, Ikimaanisha kua, imani ya injili ya kristo, na mitume wake wote, ni ya namna moja. Wewe kama unaiamini biblia, basi nakuomba uamini na yale ninayokuandikia.Tazama nikusaidie sasa: Kuna maana ya imani, na jinsi ya kuishi kwa imani katika maisha yetu ya kila siku. Nikweli kua, imani ni “BAYANA YA MAMBO YASIYOONEKANA” Lakini, tazama Nuhu kwa imani, akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasioonekana bado, Yeye kwa jinsi alivyomcha Mungu vizuri kwa imani na matendo yake mema ya utiifu, biblia inasema” ALIUNDA SAFINA, APATE KUOKOA NYUMBA YAKE!!!. Soma( Waebrania 11:7). Hii ndio ileile maana ya ” IMANI PASIPO MATENDO MEMA IMEKUFA. Sasa ndugu sungura, hiyo tofauti ya imani unayoiona wewe iko wapi!!. Ibrahimu vile vile, matendo yake mema ya utiifu yalimsaidia katika imani yake, soma(Yakobo 2:21-23). Tatizo ninyi mnachanganya kati ya matendo haya ya utiifu yanayozaliwa na hiyo imani, na yale matendo ya sheria yanayozaliwa na amri(sheria), ndio maana pia, mtu wa namna hii ni shida kumuelewa Paulo, bwana yesu na mtume yakobo kwa wakati mmoja. Imani ya kweli, huwa inatabia ya kuzaa matendo mema, ili ithibitishe ile haki ya Mungu. Sasa tazama kuiba, kuzini nk, ni sehemu ya mambo maovu ambayo kamwe hayawezi kuithibitisha haki ya Mungu…na ndivyo injili yote ya bwana yesu na mitume wake kwa pamoja walihubiri injili ya namna hii. Tazama Yakobo mtumwa wa Mungu, na wa bwana yesu kristo, akatuambia hivi” lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikilizaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikilizaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo, maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo!!!. Soma(Yakobo 1:22-25). Vivyo hivyo, bwana yesu alikuja mwenye haki, ili atufundishe na sisi maisha ya haki, tuyazingatie, ili “TUKANDENDE MATENDO MEMA MBELE ZA WATU WOTE” ndio maana, hata yeye mwenyewe, hakutufundisha maisha ya kusikiliza neno na kuliamini pekee, ila Pia alitaka tuwe watendaji wa hilo neno lake, akisema hivi” NA KILA ASIKIAYE HAYO MANENO YANGU ASIYAFANYE, ATAFANANISHWA NA MTU MPUMBAVU…..,Soma( Mathayo 7:26). Swali lako jingine, ni kweli kabisa kua, bwana yesu aliitimiza sheria yote, ndio maana hapo juu nilisema kua, tatizo, ninyi, mnachanganya matendo ya sheria na matendo ya imani, ni lazima mfahamu kua, paulo alifafanua matendo ya sheria jinsi yalivyokoma katika mwili wa kristo, na Yakobo yeye anazungumzia matendo yazaliwayo na hiyo imani jinsi itupasavyo kuyaishi. Hivi ni vitu viwili tofauti, lakini katika ileile imani mmoja. What next….kristo hakutaka tena sisi tuwe chini ya matendo ya sheria takatifu ya Mungu, yeye ametuacha huru, lakini lengo la kuachwa huru sio kuvunja tena na kutotii yale yanayomchukiza Mungu, isipokua, lengo ni ili sisi tuthibitike kwa uhuru na unyenyekevu katika kutii bila ya kuongozwa kwa nguvu na lile andiko takatifu la Bwana, liletalo mauti yake kwa wale wote wasiotii kikamilifu. Tunathibitika kwa sheria ya uhuru na ya kifalme katika haki yake yeye aliyetupa hiyo haki yake na kutuacha huru, yaani KRISTO!!. Au ndugu sungura, wewe kama ndugu lwembe, unafikiri huo uhuru wetu ni wa kutenda mambo yaleyale maovu aliyoyakataza Mungu katika amri zake?, hapana, ndio maana hata Mungu mwenyewe alisema”IWENI WATAKATIFU KWA MAANA MIMI NI MTAKATIFU”. Nikweli hatuwezi kua watakatifu kama Mungu wetu, hapa duniani….lakini tukimfuata kristo katika mafundisho yake, kama kielelezo chetu, basi, na Mungu wetu nae atatukubali na kututakasa sawasawa na mapenzi yake. Sisi uhuru wetu maana yake ni kua, chumvi ya Dunia, ili bila sheria, bila adhabu, watu wote watuone kua, tunakwenda sawasawa na sheria ya Mungu katika maisha yetu yote hapa Duniani…maana biblia inasema kua, sheria ni kwa ajili ya wakorofi, ikiwa kama kioo chao iwaonyeshe dhambi zao bila ya kuwasaidia. Lakini sisi, hatuitangui sheria ila tunaithibitisha sheria kwa hiyo imani yetu. Mwisho kuhusu ibrahimu: Yeye aliitwa na Mungu kwa imani ili amuamini Mungu, kama wewe leo hii unavyoitwa na kristo ili umuamini kristo, ibrahimu alimuamini Mungu na kumtii katika matendo yake, kama wewe leo hii, unavyotakiwa kumuamini bwana yesu na kumtii katika matendo yako….uende kanisani, utoe sadaka nk. Hayo nawewe kwa sasa ndio baadhi tu, ya matendo yako mema mbele za kristo, ubarikiwe.

 209. @Mhina,
  Naona unaelekea kuzuri!! Unaelekea kupona ugonjwa mkubwa sana uliokuwa nao rafiki yangu!! Umeanza kuelewa jambo ambalo waj2 wengi, hawaliewi!! Na ukiwaambia, unaonekana mtu wa agano la kale, mtu wa sheria!! Farisayo!! Wanafikiri, Neema (Kristo), na Amri zake, wanapingana!! Endelea hivyovhivyo!! Na nikushauri, usichoke kuendelea kujibizana na watu tafadhali. Wewe endelea tu!! Mungu anaona jitihada zako!! Don’t givu up bro!!

  @Pandael
  Wewe unaelewaje dhambi na makosa? Kuna tofauti kweli? Ipi hiyo? Au kuna ufanano vilevile? Upi huo?? Nataka kujua kwanza, wewe unafahamu nini kwenye dhana hizi mbili halafu tuanzie hapo… Karibu sana!! Nakungoja

  @ Sungura,
  Unaonekana uko butu sana katika uelewa wa neno!! Naona unambishia Mhina tu bila sababu yoyote ya msingi. Usikasirike brother!! Wewe ni ndugu yangu, tumetoka mbali katika mijadala hii ya majifunzo. Nikudonolee kidogo tu kwamba, kile anachokizungumzia Yakobo, ndicho alichokiishi Ibrahimu. Amri za Mungu zimekuwepo tangu zamani sana, naam baada ya uumbaji tu!! Zamani za kabla ya kudhihirishwa mlimani Sinai kwa mara nyingine kwa kizazi kiteule kilichokuwa kimeasi huko utumwani. Na huu hapa ni ushaidi kuwa, Amri za Mungu ambazo kwa hizo watu wote wa zamani waliziishi wakahesabiwa haki, zilikuwepo… Twende pamoja…. Ni hizi hapa
  Amri 10 za Mungu kabla ya Mlima Sinai
  1.
  “Usiwe na miungu mingine ila MIMI”
  Mwanzo 2: 16 “BWANA MUNGU AKAMWAGIZA huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. Mwanzo 15: 7 Kisha akamwambia, MIMI NI BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi. Mwanzo 17: 1 “…. Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, MIMI NI MUNGU MWENYEZI, UENDE MBELE YANGU, UKAWE MKAMILIFU”. Kutoka 3: 6 Tena akasema, MIMI NI MUNGU WA BABA YAKO, MUNGU WA IBRAHIMU, MUNGU WA ISAKA, NA MUNGU WA YAKOBO. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu”. Mungu alitaka kuheshimiwa YEYE tu na si miungu wengine!!
  2.
  “Usijifanyie sanamu za kuchonga-ibada za sanamu…”
  Mwanzo 35: 2 Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, ONDOENI MIUNGU MIGENI ILIYOKO KWENU, MJISAFISHE MKABADILI NGUO ZENU. 3 Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea. 4 NAO WAKAMPA YAKOBO MIUNGU MIGENI YOTE ILIYOKUWA MIKONONI MWAO, NA PETE ZILIZOKUWA MASIKIONI MWAO, NAYE YAKOBO AKAZIFICHA CHINI YA MWALONI ULIOKO SHEKEMU. Mungu aliwataka watu wamwabudu YEYE tu na siyo miungu migeni (sanamu).

  3.
  “Usilitaje (katika ibada na kauli za kiimani) Bure jina la Bwana Mungu wako,- YEHOVA”
  Mwanzo 4:26 Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza KULIITIA JINA LA BWANA. Mwanzo 12:8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea Bwana madhabahu huko, AKALIITIA JINA LA BWANA. Mwanzo 16:13 Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye?. Mwanzo 21:33 Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele.
  Zingatia, Mungu hakutaka jina lake kutajwa ovyoovyo na watu walioshiba maharage!! Alitaka litajwe kwenye ibada za kumwabudu na kumsifu YEYE.
  4.
  “Ikumbuke Siku ya Sabato uitakase…”
  Mwanzo 2: 2-3 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; AKASTAREHE SIKU YA SABA, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya. Kutoka 16: 23 Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana KESHO NI STAREHE TAKATIFU, SABATO TAKATIFU KWA BWANA; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi. 30 Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba. Ndiyo maana sisi wasabato tunaamini kuwa kupika chakula/ au kununu chakula/kitu chochote siku ya sabato kwa makusudi ni dhambi ya kuvunja Sabato.
  5.
  “Waheshimu Baba yako na Mama yako…”
  Kwanza elewa kuwa “Adamu ni mwana wa Mungu” (luka 3:38). Mwanzo 3:17 AKAMWAMBIA ADAMU, KWA KUWA UMEISIKILIZA SAUTI YA MKE WAKO, UKALA MATUNDA YA MTI AMBAO NALIKUAGIZA, NIKISEMA, USIYALE; ARDHI IMELAANIWA KWA AJILI YAKO; KWA UCHUNGU UTAKULA MAZAO YAKE SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO. Adamu alipoipuuza sauti ya mzazi wake –Mungu, yaliyompata tunayafahamu sote. Hata leo usipomtii mzazi ndg yangu, tarajia laana na masaibu maishani.
  6.
  “ Usiue”
  “SAUTI YA DAMU YA NDUGU YAKO INANILILIA KUTOKA KATIKA ARDHI. BASI SASA, UMELAANIWA WEWE KATIKA ARDHI, ILIYOFUMBUA KINYWA CHAKE IPOKEE DAMU YA NDUGU YAKO KWA MKONO WAKO” Mwanzo 4:8,10.
  7.
  “Usizini”
  Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. NIFANYEJE UBAYA HUU MKUBWA NIKAMKOSE MUNGU?(mwz 39:7-9).
  8.
  “ Usiibe”
  Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! UMEKULA WEWE MATUNDA YA MTI NILIYOKUAGIZA USIYALE? (Mwanzo 3:11) Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.(Mwanzo 30:33) Awaye yote utakayemwona kuwa nayo miungu yako, yeye asiishi. Mbele ya ndugu zetu ukitambue kilicho chako kwangu, ukakichukue. Maana Yakobo hakujua ya kwamba Raheli ameiiba.( Mwanzo 31:32). Hasha! Watumwa wako wasifanye hivi; tazama, hizo fedha mlizoziona kinywani mwa magunia yetu, tumekuletea tena kutoka nchi ya Kanaani. Tuwezeje sisi kuiba nyumbani mwa bwana wako fedha au dhahabu? Atakayeonekana kuwa nacho miongoni mwa watumwa wako, na afe, na sisi nasi tutakuwa watumwa wa bwana wangu.(Mwanzo 44:8-9). Wapenzi, tangu mwanzo wizi ilikuwa ni ishu kubwa. Kubwa sana iliyowapeleka watu/wakosaji kwenye umauti tu.
  9.
  “Usimshuhudie jirani yako Uongo”
  Katika Agano Jipya Yesu anamtaja shetani kama muongo na baba wa huo uongo tangu mwanzo. Why?? Kwa sabau alimshuhudia Mungu uongo kwa Hawa….. “lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.(Mwanzo 3:3-5). Angalia, Hawa naye alimshuhudia Mungu uongo…. anasema “Msiyale wala msiyaguse….” Kwani Mungu alimkataza hata kuyagusa kweli??
  10..
  “Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako”. – Mwanzo 39:7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala name. Mwanzo 31:30 Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu? nk

  Sungura, jitahidi ufunguke… Mungu anakupenda sana rafiki yangu. Acha ubishi wa akili tuambao hauna maana yoyote.
  Neema ya Bwana ikufunike.

  Siyi

 210. Mhina,

  Ni nani unayempa hiyo tahadhari yako hapa, wewe unadhani ndo umeongea kitu sahih sana ktk hoja zako?

  Unatakiwa uchangie tu halafu uache wasomaji waamue.

  Kama unaielewa vema imani aliyokuwa anasema Yakobo mtume, hebu niambie ina uhusiano gani na kuiba?

  Hebu rudi kidogo ujikumbushe definition ya imani kisha uchunguze kama yakobo alikuwa anaongelea imani unayosema wewe.

  Au chunguza kati ya Belief na Faith ni kipi Yakobo anaongelea na uone kama kina uhusiano na kuiba au kuzini.

  Lakini pia suala la Yesu kutimiza torati kila wakati mwalisema bila hata kujua undani wake, japo tumeusema sana huo undani lakini hata hamjifunzi.

  Yes, umesema Yesu alikuja kuitimiza torati, then baada ya kuitimiza what next?
  Maana imesema hakuna hata yodi ya torati itakomeshwa hata kama mbingu na nchi zitakoma, ispokuwa mpaka pale yote yatakapotimia, na kumbe Yesu aliyatimiza. Ndipo nikakuuliza sasa hapo juu, what next.
  Mwisho, unaweza kuniambia Ibrahim aliwezaje kutokuiba bila kuwepo sheria inayomwambia asiibe?

 211. Imani pasipo matendo mema “IMEKUFA”. Haya sio maneno ya Mhina, ila hilo ni fundisho halisi la biblia. Sehemu yote ya amri za Mungu, imo ndani ya hayo “MATENDO MEMA”. Kinyume cha kukataa ukweli huo ni kuwa mtenda dhambi usietii matendo mema, na watu wa aina hii, paulo anawaita “WAABUDU SANAMU” au wafuasi wa shetani!. Jambo la muhimu sana kukazia hapa ni kwamba, hatufanyi hayo matendo mema kwa lengo la kutimiza sheria na kupata haki, HAPANA, HAPANA, HAPANA!!…Maana biblia inasema kua, haki inapatikana kwa njia ya kumuamini bwana yesu pekee, isipokua tunafanya matendo mema, kwa kua sisi ni watoto wa Mungu, tunaotakiwa kuishi maisha ya kumpendeza Mungu na kumkataa shetani na kazi zake zooote, hiyo ndiyo kazi ya roho mtakatifu kutuongoza maisha ya upendo na amani hapa duniani, bila kufanya dhambi ijapokua hatuongozwi na sheria…. ndio maana Paulo akauliza hivi” TUFANYE DHAMBI KWA SABABU HATUWI CHINI YA SHERIA BALI CHINI YA NEEMA?!!!!!……Ukiendelea kuusoma mstari ule, Paulo anatoa jibu la msisitizo kwa kusema “HASHA! HAMJUI YA KUWA KWAKE YEYE AMBAYE MNAJITOA NAFSI ZENU KUWA WATUMWA WAKE KATIKA KUMTII, MMEKUWA WATUMWA WAKE YULE MNAYEMTII, Soma(warumi 6:15-16). Ukweli ni kwamba, tunamtii mungu katika matendo mema, kwa sababu ni utumishi wa dhambi ndio uletao MAUTI, na ni utumishi wa huo utii ndio uletao HAKI, ndio maana biblia inawaita wakristo” WATUMWA WA HAKI”!!!!. Sasa, wewe kama huna huo utii wa kuithibitisha hiyo haki ya Mungu, katika matendo yako mema hapa duniani, usifikiri Mungu nae atakupenda na kukupa haki ya kristo kule mbinguni ili uepuke jehanamu ya moto!!. Kwaherini, naamini mchango wangu kwenye hii hoja umetosha. AKUNA KAMA YESU – LAKINI TUNAWAJIBIKA KUMFUATA HUYO YESU KWA KUISHI NA KUFANYA MATENDO YANAYOMPENDEZA YEYE.

 212. Lwembe,
  Unaweza kudhani unajua kumbe huelewi!! Sasa hivi unadhani unatuelewesha kumbe unatupotosha tena mbashala!! Sikiliza kaka, huwezi kuwa mfuasi wa CHADEMA, CCM, CUF n.k. kama hufuati katiba, na ilani za chama husika!! Huwezi kuwa mwanachama!! Huwezi kuwa mfuasi wa Kristo, ilhali huyafanyi ya Kristo! Huwezi kuwa!! Na tunakushauri tu, usiendelee kutudanganya kama huna jema la kutuambia, ni vyema ukatulia kujifunza!! Kwa. Mfano, Kristo hakusema, kumbuka kupumzika (siku yoyote), hasha!! Alisema, Ikumbuke siku ya Sabato uitakase!! Hiyo ya siku yoyote, ndani ya katiba ya Kristo, umeipata wapi? Ni kifungu kipi hicho?? Acha ufedhuli kaka!! Nakushauri ukae chini kwanza, ujifunze kwa utulivu!! Ukifuata mapokeo ya dini yenu, utapotea tu maana hakuna wokovu huko!!
  Majibu ya maswali yako.
  Swali 1
  Je, TORATI iliruhusu jambo hili la kula nyama za watu na kunywa damu????

  Jibu
  Wewe unafikiri, amri ya USIUE, ilimaanisha nini? Ilikataza kuua watu au wanyama?

  Swali 2
  Siyi, Sheria za Maadili ziliruhusu jambo hili?????

  Jibu
  Mwitiko wako kwa swali la kwanza, ndilo jibu la swali ya pili.

  Swali la 3
  Wenye kuijua Sheria walijiondoa kundini baada ya kuambiwa jambo hilo, hebu niambieni, ninyi mngechukua uamuzi gani kama mngalikuwepo ktk siku hiyo ambayo hata sasa leo hii mko ktk siku hiyo????

  Jibu
  Akina nani hao wenye kuijua sheria? Hebu wataje binafsi nione kama nafanana nao hata chembe!!

  Mwisho (but not least), nikuombe uthibitishe kama kweli katika Agano la Kale, hakukuwa na imani isipokuwa sheria tu ndizo zilitawala!! Thibitisha hilo haraka tafadhali!! Ukiona unashindwa, tangua kauli yako haraka sana hapahapa mtandaoni!!
  Nakuongoja!!
  Neema ya Bwana ikutangulie.
  Siyi

 213. ndugu zangu wote katika bwana. Myapime mafundisho yote, mnayojifunza humu, msije mkakaririshwa vitu ambavyo haviko sawasawa. Waalimu wengi wa injili, sio lazima wawe wanania mbaya ya kuwapotosha, lakini wakati mwingine mwalimu huyo inawezekana hajajifunza jambo kwa usahihi wake wa kutosha, akajikuta anakuambukiza sehemu mbaya ya ule ufahamu wake. Msidanganyike ndugu zangu, Mwenyezi Mungu kamwe hadhihakiwi kwa mambo maovu. Huwezi wewe eti uibe, uzini, uwe muongo, UIBE SADAKA KANISANI KAMA YUDA,….Halafu eti ujipe moyo kua utaokolewa kwa neema pekee!!!!!!…..sasa kama ingekua ni rahisi kiasi hicho, kungekua na haja gani ya kuyakataa na kuyapinga maovu hapa duniani, kungekua na haja gani ya kujazana makanisani kufanya ibada nk, kumbe mambo ni bwereeeeee!!!!. Huyo yuda anaechukuliwa kama mfano mzuri wa mabaya yake aliyoyafanya, ya kuiba sadaka za kanisani, aliishia waaaapiiiii, Mimi sijawahi kuisikia injili ya kipuuzi kama ya namna hii aliyoifundisha ndugu lwembe!!. Inasikitisha siku hizi, kuona baadhi ya makanisa yakifungua mabaa, yakiuza sigara na hata baadhi ya wachungaji wanavuta sigara kwa kisingizio kua, tumeokolewa kwa neema pekee!!. Sinto koma kukemea mafundisho hayo mpaka yesu atakapo rudi kuchukua kanisa lake. Wanaigeuza injili ya kristo kua ni upuuzi, ili wahalalishe yale maovu yao, ambayo, baba wa dunia hii, amewanasa. Yaani mtu akisikia kutii sheria tu, anaona ni jambo baya, pasipokujua kutii huko ni kwa namna gani, yeye anataka uhuru wa kufanya mambo yote mabaya…ili amsingizie bwana yesu kua eti amemuokoa na kumuacha huru kabisa!!, mtu hajui matendo ya sheria yaliyofutwa wala matendo ya imani ambayo inampasa ayaishi.

 214. bwana lwembe. Nikweli kua, sheria haiwezi kuithibitisha imani, lakini tazama, imani inaweza kuithibitisha sheria, unalijua hilo?!!. Hili ndilo alilolifanya bwana yesu….sio kufuta sheria ila “KUTIMIZA”….ili sheria hiyo, ithibitike mioyoni mwa wale wanaomuamini, kwa njia ya imani yake. Haya sio maneno yangu au ya thebebu langu, isipokua ni maneno ya Mungu kwenye biblia ambayo hata wewe mwenyewe unayo, na umeishika, lakini umvivu wa kuiamini, tazama(warumi 3:31). Tunaithibitisha sheria katika imani, sio kwa ajili ya kutafuta haki, hapana…maana hata mimi mhina ninajua kua, siwezi kupata haki mbele za Mungu kwa matendo yangu ya kufuata sheria, ila haki ya Mungu, inapatikana kwa njia ya imani katika yesu kristo….lakini utiifu huu wa matendo mema unatusaidia kuonyesha upendo kwa mungu na jirani zetu. Nikweli kua,Kristo ametutoa katika matendo ya sheria na kutuleta katika njia ya imani, lakini imani yetu hiyo, itakwendaje bila ya matendo mema!!!!…hakika haiwezekani, ndio maana Yakobo akaandika hivi” IMANI BILA MATENDO MEMA IMEKUFA!!!. Mahala pengine Yakobo akasema hivi”MAANA KAMA VILE MWILI PASIPO ROHO UMEKUFA, VIVYOHIVYO NA IMANI PASIPO MATENDO MEMA IMEKUFA!!!!!. Soma(Yakobo 2:26). Haya matendo mema yazaliwayo na ile imani ya roho wa Mungu akaaye ndani yetu ni pamoja na mijumlisho ya yale mambo yote mabaya aliyoyakataza Mungu kama vile: kutoiba, kutozini, kutosema uongo nk, ndio maana, biblia inatuambia hivi” HAMJUI YA KUWA NINYI MMEKUWA HEKALU LA MUNGU, NA YA KUWA ROHO WA MUNGU ANAKAA NDANI YENU? KAMA MTU AKILIHARIBU HEKALU LA MUNGU, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO….KWA MAANA HEKALU LA MUNGU NI TAKATIFU AMBALO NDILO NINYI. Soma(1Wakorintho 3:16). Kwa hiyo ndugu lwembe, sheria au amri za Mungu unazozikataa, tayari ziko katika hiyo imani yako, kwa kua, kama wewe utajiita ni mkristo, halafu unazini, unaabudu masanamu, unapenda kudanganya watu nk, kwa kisingizio kua, bwana yesu amekukomboa, basi ujue ndugu, umepotea hakika. Neema ya kristo haikuja ili ikupe uhuru wa kufanya dhambi isipokua imekuja ili ikuimarishe zaidi na zaidi. Wewe umvivu wa kuisoma biblia na kuielewa, ndio maana umejaa udini wa kuhukumu ovyo wengine, ukidhani safari ya mbinguni ni ya kanisani kwenu pekee. Kama ukotayari mimi nitakufundisha hapa, somo la maisha ya mkristo, labda linaweza kukusaidia zaidi, au vipi ndugu yangu? Ijapokua hapa si mahala pake…haya, tuendelee kuelimishana kwa upendo na amani, bwana akubariki.

 215. r.m,
  (na pia Siyi & Mhina, kama itawasaidia kuinua ufahamu wenu!)

  Kwanza napenda niwaeleweshe kwamba kuwa mkristo si jambo la dini ktk maana ya udhehebu au kuwa ktk kundi fulani maarufu, mnaojitukuza ktk hili na lile; mkristo ni yule ambaye amemuamini Kristo kupitia Injili kama ilivyohubiriwa na mitume, na si hadithi uchwara za “kuongozwa na RM” usiyemjua, ndi maana wengi wetu tunaishia kuongozwa na mapepo ya dini huku tukijidhanisha kwa bidii kwamba ndiye RM!!!

  r.m. nimekuuliza swali jepesi lililo wazi sana kiasi kwamba hata vipofu wa dini wanaliona, inashangaza kwamba wewe na jamaa zako mmelikosa jambo hili muhimu ambalo lingewainua ufahamu wenu na kuwatoa ktk jitihada suicidal mnazoendelea nazo ktk ulimwengu wa dini!

  Narudia tena:
  Yn 6:55-56 “Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.”

  Je, TORATI iliruhusu jambo hili la kula nyama za watu na kunywa damu????

  Siyi, Sheria za Maadili ziliruhusu jambo hili?????

  Wenye kuijua Sheria walijiondoa kundini baada ya kuambiwa jambo hilo, hebu niambieni, ninyi mngechukua uamuzi gani kama mngalikuwepo ktk siku hiyo ambayo hata sasa leo hii mko ktk siku hiyo????

  Mkinipa jibu ktk urahisi wa swali nililowauliza, itarahisisha kuendelea na mjadala ktk Nuru ya Maandiko badala ya mafundisho ya dini yaliyopindishwa!

  @Mhina,
  Suala la kwamba “HATUTII SHERIA” sio somo la kusoma darasani na kujikaririsha usichokijua. Inakulazimu kwanza ujue ni kwa vipi kwamba Sheria HAIKUWA na IMANI ndani yake, ndipo unaweza ukafika ktk uelewa unaoweza kukupa ufahamu ukaijua Sheria ni nini na Imani ni nini! Hauwezi ukawa na vyote viwili, Sheria na Imani, ukijiona unatii Sheria basi jua fika kwamba HUNA Imani!!!!

  Imani imekuja ktk Injili, na ndiyo inayoikomesha Torati ktk ukamilifu wake, maana Sheria hizo mnazoendelea nazo ni kivuli cha mema ambayo hamjayafikia, hiyo Imani! Nayo Imani ndiyo inayopelekea Kuzaliwa mara pili, kule kubadilishwa nia, kuwa kiumbe kipya! Yaani hapo zamani ulikuwa na Asili ya Dhambi ambayo ungali unaendelea nayo, nayo Sheria haina nguvu ya kukufanya uache Dhambi, ndio maana HAKUNA aliyehesabiwa Haki kwa kuzitii Sheria.

  Basi ukiisha kubadilishwa nia, ile asili kutoka kuwa kunguru mla mizoga hadi kuwa hua mla nafaka, je, utajizuia kula mizoga? Hua hali mizoga kwa asili, kwanza hana nyongo, kiasi kwamba akila mzoga ni lazima umuue! Au nikuulize ndg Mhina, kuna mahali popote pale uliposoma kwamba Yesu alijizuia kuzini au kuiba? Je, haujasoma kwamba Yuda aliombea wagonjwa na wakapona, na bado alikuwa mwizi wa sadaka? Kuzaliwa mara ya pili ni HALISI ndg yangu!!!

  Mungu anaposema kwamba unakuwa “kiumbe kipya”, cha kimbinguni, kwa kule kuzaliwa kwako kwa Roho wa Mungu, usidhani anakuletea ngonjera za kukariri kwa ajili ya mashindano ya dini, hapana, HIVYO NDIVYO UNAVYOKUWA UKIZALIWA MARA YA PILI; ndani yako anakaa Kristo, ndiye anayekuongoza, kulingana na Asili yake; Ukijiona unajizuia kuzini au kuiba au una hasira za hovyo nk basi jua wewe bado ni KUNGURU, mla mizoga na nafaka, a HYPOCRITE, ndio hao wenye kuzitii Sheria huku wakidai kwamba wana Imani!!!

  Wameyaamini mapokeo ya dini yao kuliko Maandiko, na mwisho Maandiko kwao yamefungwa, ndio hao wanaojitahidi kujiokoa kwa Sheria!!!!

  Gbu all!

 216. ,…kumbe kule kusema: usiibe, usizini, usiseme uongo nk, ndiko kulikozaa hili neno ” upendo wa Mungu, tunawezaje tena kusema “HATUTII SHERIA”!!!. Sheria hazifuatwi kwa mahitaji yake ya mwilini kama israel, maana tayari kristo alikwisha zifia katika mwili wake, lakini imebaki kwa sisi kuzitii hizo sheria kwa asili yake ya rohoni ili tudhihilishe upendo wetu kwa Mungu na kuhesabiwa haki kwa imani ya yesu kristo.

 217. @ r.m.
  Usipate taabu ya kujitambulisha kwangu mtu wa Baba!! Wewe songa mbele kutiririsha mazuri hapa!! Nakuona Bwana anazidi kukukirimia mambo makubwa na mazito!! Na hili unalolifanya ni la msingi zaidi kuliko kujitambulisha kwa siyi tu!! Who is siyi by the way??!! Tandika injili mtu wa Mungu!! Mambo mengine baadaye. Bwana akutangulie zaidi unapotoa mambo makubwa ambayo yatawafungua macho akina Lwembe, Sungura na wengine wa aina hiyo.
  Tuko pamoja mno mtumishi.
  siyi

  @ Sungura,
  Yote uliyouliza, tulishawahi kuyajadili hapa mtandaoni kwa siku za nyuma. Kwa sasa, naomba nisikujibu kabisa ili nisivuruge mtiririko huu mzuri wanaouendesha ndugu r.m. na Lwembe. Habari za amri kumi kuwepo kabla ya mlimani sinai nilishazileta hapahapa mtandaonni!! Zipo!! Wewe fuatilia tu.
  Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 218. wana wa Mungu, tupo katika sheria ya roho yenye uzima na uhuru ulio katika yesu kristo, tumeachwa mbali (tumefunguliwa) toka kwenye sheria ya dhambi na mauti….hii maana yake haiondoi sheria ya Mungu ila inaihibitisha hio sheria na kuiadhimisha kwa njia ya rohoni. Mtume Paulo alitoa jibu hili kwa watu wote wanaofikiri kua sheria zimebatilishwa (zimefutwa) na bwana yesu kwa kuuliza na kujibu hivi” BASI, JE….TWAIBATILISHA SHERIA KWA IMANI HIYO? HASHA !! KINYUME CHA HAYO TWAITHIBITISHA SHERIA !!!!! Soma(rumi 3:31). kuithibitisha sheria sio kuiondoa au kuipuuza bali ni jinsi ya kuitii kwa nia ya rohoni bila shuruti au kulazimishwa kwa amri na adhabu, lakini ni lazima kutii ili kuonyesha upendo kwa Mungu, biblia inasema hivi” HUKO NDIKO KUMPENDA MUNGU KUZITII AMRI ZAKE. Amri ya yesu ni upendo, lakini upendo huo tafsiri yake na maana yake ni kutoka kwenye zilezile amri kumi za Mungu, kwa sababu upendo huo umejengwa katika ileile misingi ya torati na manabii…yaani kama bwana yesu mwenyewe alivyosema kua ‘MPENDE BWANA MUNGU WAKO, MPENDE JIRANI YAKO > lakini anasisitiza watu wajue kua “KATIKA AMRI KUU HIZI HUTEGEMEA TORATI YOTE NA MANABII” Soma( Mathayo 22:40), Paulo nae afafanua vyema kwa kusema” MAANA KULE KUSEMA, USIZINI USIUE USIIBE NK……..INAJUMLISHWA KATIKA NENO HILI YA KWAMBA MPENDE JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO…….BASI PENDO NDILO MWISHO WA SHERIA. Soma(rumi 13:9-10) …..Kwa hali hio, umeona kua, upendo wa yesu umefungwa katika misingi ya torati na manabii (amri kumi za Mungu), Biblia katika waefeso 2:20, inatuambia” MMEJENGWA JUU YA MISINGI YA MITUME NA MANABII”…..KATIKA KRISTO, MNAUNGANISHWA HATA MUE HEKALU LA MUNGU.(tafsiri nyepesi). Kwa hiyo jamani, Tusidharau sheria, kwa kua, sheria ndio msingi wa injili, Hatupaswi kufwata mahitaji ya sheria lakini inatupasa kuzitii si kwa ajili ya kutafuta haki ila kwa ajili ya kuudhihirisha upendo wetu kwa Mungu, ili nae atukubali na kutupa ile haki yake iliyo katika njia ya yesu kristo pekee. lakini utakapo ihubiri injili yenye kutoa uhuru wa kuiba kuzini nk, huku ukiwaambia watu wasitii sheria,kwakweli, hiyo itakua sio injili ya yesu ila ni injili ya mapokeo ya kanisa lako…huku mwenyewe maskini ukijiona ni mjanja kuliko watu wote!!!!!!. Mungu akusaidie uongeze ufahamu wako hapa kwa njia hii. Asante

 219. Siyi,

  Bado u mjinga kiasi hiki juu ya mambo haya brother?

  Kwamba kabla ya dhambi amri kumi zilikuwepo, dah!!

  Ivi Adam aliwahi kuambiwa kuwa asizini, asiibe?
  Au Ibrahim, au Yakobo waliwahi kuambiwa usizini?

  Na sikukuu za makambi na vibanda nazo zingalipo kwamba kanisa la kristo lapaswa kuzishika!!

  Nani kati ya mitume aliwahi kuagiza au kulifanya hilo, au ni katika kanisa la wapi kwa kanisa la kwanza waliwahi kushika hizo sikukuu?

 220. Mmmh
  Lwembe….
  Mbona unakuwa kama huelewi habari hizi rafiki?? Mbona tulishakueleza siku nyingi sana habari za uhusiano wa NEEMA na AMRI 10? Tena Siku ile, nikawaletea tofauti bainifu kabisa kati ya neno Sheria/torati na amri kumi. Mbona kama ungekuwa na hoja, kwa nini usingeleta/usingeyapangua hayo niliyoyaleta siku lie??
  Nakukumbusha kidogo, ni kweli kuna sheria/torati zilizoishia msalabani. Kabisa leo hazipo!! Ila kuna sheria chache bado zingalipo tunaziendeleza kwa mf. makambi, sikuukuu za pasaka, n.k. Hizi nazo zilikuwa ni sheria/torati zilizokuwepo tangu zamani. Na hadi leo zipo.
  Amri kumi, nikasema hizo, hazikukoma mpaka kesho. Hivyo kuna tofauti kubwa kati ya sheria/torati vs amri kumi. Rejea mchango wangu wa huko nyuma. Nimeweka vizuri japo kwa ufupi sana. Acha kutulisha mambo yenu ya dini kaka. Wasabato tuko makini kiasi hicho!! Hatubahatishi!! Watakaoamua kupotea, waliamua kupotea tu!!
  Kabla ya dhambi, mbingu zilikuwa na utaratibu wa sheria. Baada ya dhambi, sheria ziliendelea kuwepo, naam na zingine kuongezwa kabisa!! Baada ya kifo cha Kristo, sheria zilizokuwepo kabla ya dhambi, zinaendelea kuwepo siku zote. Na baadhi ya zile zilizoletwa baada ya dhambi, nazo zimeendelea kuwepo. Usitudanganye kwamba kwa Mungu ni uhuru tuuuuu, uhuru tuuu usio na taratibu, sheria wala kanuni!! Wanaoamini hayo, hiyo ni dini ya ibili!!
  Kusingekuwa na sheria(amri 10) kabla ya dhambi, Adamu asingeanguka dhambini!! Kama hakutakuwa na ssheria (amri 10) kwa leo, basi kusingekuwa na dhambi vilevile. Nakushauri uache ufedhuli wa kudanganya watu kijana.
  “Jitahidi(soma) kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” -2timothy 2:15.
  Changamka!!
  Neema ya Bwana ikutangulie
  Siyi

 221. bwana siyi…asante, unataka kujua kirefu cha r.m,oky …..subiri nikimalizana na huyo jamaa yako hapo juu, nitafafanua maana ya jina hilo. barikiwa ndugu

 222. Hivi ndugu lwembe, unaposema: HATUTII SHERIA ZA MUNGU” unafahamu kua unamaanisha, wewe unaona sio makosa wakristo, kuzini, kuiba, kusema uongo, nk ?!!. kama umaanishi hivyo, tatizo lako liko wapi ndugu yangu ili nikusaidie? unalonipinga likowapi??!!….unapupa ya kuandika sana wewe, lakini usijali, mimi nitakusaidia. ndugu yangu, bwana yesu kama alivyosema yeye mwenyewe ya kua, hakuja KUONDOA SHERIA BALI AMEKUJA KUZITIMIZA. Neno “KUTIMIZA” halimaanishi kuondoa isipokua neno hilo linamaana “KUKAMILISHA”. Swali lako: ni vipi mtume Paulo aandike “kristo ni mwisho wa sheria ili kila amuaminie ahesabiwe HAKI ??!!….hapo Paulo alikua anaelezea ile hali ya watu, kufunguliwa katika ile hali ya torati katika mwili(andiko) au kuenenda katika mwili na adhabu. ili watu waenende katika hali mpya ya roho, na sio kufuta kabisa sheria za Mungu kama wewe unavyofikiri ili walevi walewe, wazinifu wazini, waizi waibe nk…halafu wote waende mbinguni, hapana…ukristo hauko hivyo ndugu yangu!!!!..Mtume Paul afafanua hili kwa kuseme hivi” BASI SASA TUMEFUNGULIWA KATIKA TORATI, TUMEIFIA HALI ILE ILIYOTUPINGA (ya kufuata sheria kwa mwili) , ILI SISI TUPATE KUTUMIKA(kufuata sheria) , KATIKA HALI MPYA YA ROHO, NA SI KATIKA HALI YA ZAMANI YA ANDIKO ( ya mwili na adhabu).Soma(rumi 7:6). Hii ndio maana ya kuenenda kwa roho, yaani sio kutotii sheria kabisa ila yale maagizo ya torati, yaani sheria, zifuatwe kwa njia ya rohoni ,si kwa ajili ya kutafuta haki kama zamani isipokua ni kwa ajili ya asili ya hiyo torati kwamba, Mungu mwenyewe alisema kua asili ya hiyo ni huko rohoni kwa ajili ya kujitiisha kwetu vyema kabisa mbele zake, ndio maana mtume Paul kwa sababu yeye alielewa vyema, alifafanua tena katika (warumi 8:3-4), akasema hivi” MAANA YALE YASIYO WEZEKANA KWA SHERIA KWA VILE ILIVYOKUA DHAIFU KWA SABABU YA MWILI (udhaifu wetu wa kufuata sheria kwa mwili), MUNGU KWA KUMTUMA MWANAE MWENYEWE KATIKA MFANO WA MWILI ULIO WA DHAMBI NA KWA SABABU YA DHAMBI, ALIIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI (adhabu za torati ziliishia katika mwili wa kristo) …. > ILI MAAGIZO YA TORATI YATIMIZWE NDANI YETU (kufuata sheria kwa roho sio kuzipuuza kabisa) SISI TUSIOENENDA KWA KUFUATA MAMBO YA MWILI BALI MAMBO YA ROHO. Soma ( rumi 8:3-5). Huku ndiko kumuabudu Mungu katika roho na kweli, ambako Mungu mwenyewe alikuahidi tangu zamani kupitia kinywa cha nabii yeremia, akisema hivi kuhusu watoto wake ambao ni mimi na wewe bw. lwembe ” NITATIA SHERIA YANGU NDANI YAO NA KATIKA MIOYO YAO NITAIANDIKA, NAMI NITAKUA MUNGU WAO NAO WATAKUA WATU WANGU!!!!!!!!!! Soma( yeremia 31:33-34). Bw.lwembe umeona hapo, Mungu hakusema sheria zake kupuuzwa kabisa isipokua amesema” ataiandika mioyoni mwetu > kwa njia ya msalaba wa yesu kristo, ndio maana hata yule bwana katika biblia aliemuuliza bwana yesu kua, afanye nini ili aurithi uzima wa milele, bwana yesu alimwambia, kama anazijua amri kumi za Mungu basi azifuate, alipojifanya amezishika zote….bwana yesu akamwambia, umebakiza jambo moja, uza mali zako zote ili unifuate (ushike imani yangu na hizo amri za Mungu)….jamaa alikua na mali nyingi akaona ni bora aingie mitini, ndipo twapata ile maana ya ule ufunuo, unaoonyesha siku ya mwisho kwa watakatifu wa Mungu utakavyokua ” HAPO NDIPO PENYE SUBIRA YA HAO WATAKATIFU WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU NA IMANI YA YESU KRISTO!!! Soma (ufunuo 14:12). Mimi naona nimthibitishie bw. lwembe kua, kujinyenyekeza kwetu mbele za yesu kristo, kamwe hakutakua na maana, kama tutakua wavunjaji wa amri za Mungu kama kuiba, kuzini, kusema uongo nk….na kama unakubaliana na mimi, tatizo lako, lilikua ni nini mpaka uniandikie mibarua yako mirefu namna hiyo hapo juu!!!!!!!…..nasisitiza tena na tena, nikweli tumeokolewa kwa neema ya kristo ili kuhesabiwa haki katika yeye, lakini neema hiyo,Mwennyezi Mungu ameifunga kwa misingi ya torati na mamabii, ili tuwe bora kuliko wale babu zetu wa zamani, na kamwe sio eti kuwafundisha watu kua, wakristo hawafuati sheria, vipi wewe ndugu yangu!!!!, hivi kama walevi na wazinifu wanapata nafasi ya kuisoma hiyo injili yako unayotufundisha, si watakuja wote kwenye ukristo wakifikiri mambo ni bwerereeeee!!!!!!!!. Mwisho ni kwamba, wewe ulikataa kua, amri za Mungu, sio zile sheria zake, hebu tusaidie, hivi katika biblia amri za Mungu nyingine unazozijua wewe ni zipi utuonyeshe. barikiwa.

 223. r.m.
  (sijui wewe ni roho mtakatifu) au maana ya r.m. ni nini??
  haha ha ha ha!!
  Umeongea maneno mazito sana mtumishi. Hadi nayarudiarudia kuyasoma. menibariki sana kwa ushauri mzuri na ujumbe mzuri na mzito ulioundika hapa. Mtiririko wako wa mawazo naufananisha na jamaa yangu hivi kipenzi jina lake naye linaanza na r. Nikiri tu kuwa kwangu umekuwa mmbaraka sana. Endelea kuchangia rafiki.
  Big up man/woman 4 a wonderful text!!
  Praying for u!
  siyi

 224. ….. mwisho katika kumalizia,

  Hebu lifikirie jambo hili; kwamba unaambiwa ili uendelee ktk safari yako ya kuuendea Wokovu, Mungu anakwambia ni lazima UONDOLEWE Dhambi zako, ili Yeye aje akae ndani yako; na njia ya kuziondoa Dhambi hizo amekuwekea hapo wazi kabisa ktk Mdo 2:38, Ubatizo kwa jina la Bwana Yesu Kristo, uzamishwe ktk maji mengi na si vibakuli vya maji, badala ya kuitii AMRI hiyo, unajipangia kutii Amri ya Nne inayohusu Sabato usiyoijua, na kujiridhisha na Ubatizo wa jina la Baba na la Mwana na RM ambao hata maana yake huijui, achilia mbali faida yake; halafu unaikuza mbegu ya hitilafu ilipandikizwa ndani yako na dini, kwa kujiamini kabisa unauliza, “Tumfuate nani, Yesu Mwalimu au Petro/Paul mwanafunzi?” na kuongeza, “Mwanafunzi anaweza kumpita mwalimu wake?” Hizi ndizo kauli zinazokubakiza kwa uhakika ktk “Kusanyiko la wafu” wanaotembea!

  Hawa hapa mfano ulio hai wa kusanyiko la waaminio waliolitilia shaka Neno la Mungu, kama ambavyo nasi tulivyo kulingana na mafundisho yetu:
  Yn 6:55-56 “Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.”

  Kuhusu hayo anayowaambia Kristo, Torati yao, ile Sheria na Amri na Hukumu inawaambia hivi:
  Kum 5:17 “Usiue.”
  Sasa, ili upate kuula mwili wake si ni lazima auawe, vinginevyo mtamlaje naye abaki kuwa mzima? Kwanza suala la kula nyama ya mtu pekee ni wendawazimu; tena itapaswa achinjwe ili Damu yake imwagwe! Lakini yeye kawaambia wainywe na hiyo damu yake, nayo Torati inawatahadharisha kuhusu damu, Kum 12:23 -25 “Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama. Usiile; imwage juu ya nchi kama maji. Usiile; ili upate kufanikiwa, na watoto wako baada yako utakapofanya yaliyoelekea machoni pa BWANA.”

  Hili kama si balaa ni nini? “60Basi watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia, walisema, Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia?… Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma, wasiandamane naye tena.”

  Umewaona hao waliodhania wamemwamini? Hao hapo wamekwama, mambo yamekuwa magumu, yamewashinda, wakajirudisha hekaluni kwao wakayatubia makosa yao ya kumfuata yule Kristo, wakapeleka na kondoo wa kuchinja, wakaendelea ktk Sheria! Safari yao ya Wokovu ikaishia hapo, licha ya vipawa walivyovionja, bali hawakumuamini Kristo kutoka ktk vilindi vya mioyo yao, ilikuwa ni “imani” iliyojengeka akilini tu, isiyo na mizizi moyoni, ndiyo ile intellectual faith!

  Lakini kwa wale mitume halisi mambo yalikuwa ni tofauti, kumbuka pia kwamba Kristo hakuyafafanua maneno yake hayo, yalikuwa ni makavu kama yalivyo, hata hivyo tazama yaliyojiri: “67Basi Yesu akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.”

  Haya, hao akina Petro waliobakia hapo ili wainywe hiyo Damu na kumla Nyama yake, je, kwa hawa nguvu ya Torati ingalimo ndani yao ktk ukamilifu wake? Endelea nao mbele mpaka ktk nyumba ya Kornelio, je, hawajaivunja Torati kwa kuingia humo??? Wao walikwisha yavunja madaraja ya kurudia ktk Sheria siku walipomtambua Kristo ni nani, yaani walikuwa “sold; lock, stock and barrel!” Sheria ya Kifo kwao ilikoma walipoipokea Sheria ya Uzima, ule Wokovu ambao ndio Sheria ya Kifalme, kwa hao wenye kuzaliwa mara pili; hawa ndio hao ambao HAWATENDI dhambi, nayo Dhambi ni KUTOKUAMINI!!!

  Kutembea njia mbili kwa wakati mmoja ni UNAFIKI, hayo ni maisha ya kunguru anayekula mizoga na nafaka; ndiko huko kutafuta kutembea ktk Neema na wakati huo huo utembee ktk Sheria!!!

  Acheni kushikilia mapokeo ya dini zenu huku mmebeba Biblia zenu, mtahukumiwa kwa hilo, kwamba mlitembea na kweli mikononi mwenu, lakini HAMKUIAMINI, badala yake mkapokea ya wanadamu mkiiacha Kweli mliyoibeba!

  Gbu!

 225. Ninaendelea…..

  r.m.

  Tukiyarejea unayoyakana, kwanza ni vizuri ujiachie ktk uhuru unapoyasoma Maandiko. Maandiko ndiyo yanayokuambia kwamba Kristo ndiye mwisho wa Sheria, na tena ndiyo hayo hayo yanayokuambia kwamba uzishike Amri zake, hizo ambazo ndizo Sheria; basi iweje uzishike Sheria ambazo zimeishia kwa Kristo? Lakini kuna Andiko pia linalotuambia kwamba Torati kazi yake ni kutuleta kwa Kristo, huko inakoishia Sheria, unaona! Yaani kwa maneno mengine, Wokovu ndio mwisho wa Sheria, yeyote aliyeukataa Wokovu, au asiyefikiwa na Wokovu, huyo bado yuko chini ya Sheria, haijalishi amemkiri Kristo kwa maneno matamu kiasi gani, huyo yungali chini ya Sheria na anapaswa kulipa Zaka yake katika ukamilifu wa Sheria na mambo yote yanayohusika na Sheria ayatimize mpaka hapo atakapofikishwa kwa Kristo, maana imeandikwa, “Amelaaniwa asiye itimiza Sheria yote”; nayo LAANA inaondoka unapoupokea Wokovu hapa duniani ulipko laaniwa, hakuna laana inayoondolewa mbinguni!!!

  Huo ndio ukweli wa jambo hilo, si la elimu ya dini au shule, bali ni experience halisi inayomtimilia mwaminio ktk maisha yake ya kawaida ya kila siku, Amani ya Bwana ipitayo fahamu zote itokanayo na Wokovu, kwa aliye ktk Wokovu, na Hukumu ya Mungu itokanayo na Sheria kwa aliye ktk Sheria!!!

  Labda tujirudishe ktk Maandiko ili tuyaone hayo ktk uhalisi wake jinsi yalivyo. Kwanza tulione jambo la Kuhesabiwa Haki kwa Imani. Mfano wake utatupa ufahamu mzuri kulihusu jambo hilo ktk kipimo cha Sheria ili tuone jinsi ambavyo Sheria ISIVYOHUSIKA na kuhesabiwa Haki kwetu.

  Kristo alipokuwa tayari kuanza Huduma, aliwaita mitume, akiwachagua kama alivyowaita. Sijaona mahali popote pale kilipotumika kigezo cha Utii wao wa Sheria kilichowafanya wastahili kuitwa. Kama ni kwa kigezo cha Utii wa Sheria, hizo Amri kumi nk, kuhani mkuu na baraza lake walistahili kuwa mitume kuliko hao wavuvi wasio na elimu!

  Lakini Neno la Mungu ndio Sheria na Amri, basi alipowaita waliutii wito wake, wakajinyenyekeza kwake na kuwa Wafuasi wake wa Kwanza hapa duniani! Basi, kama tunavyowaona, hao hawakuitwa kwa kuzitii Sheria bali kwa NEEMA. Neema ndiyo iliyowaita na ndani yake ndimo kuna Kuhesabiwa Haki kwa Imani pale walipouitikia wito huo! Ndipo juu ya jambo hilo AKAWATAKASA kwa Neno lake, na Neno lake hilo lenye KUTAKASA akaliweka kwa hao kwa ajili yetu, Yn17:19-20 “Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli. Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.”

  Sasa Shida ya kwanza kulipata kanisa linapoliendea jambo hili ni yale mafundisho yaliyo ktk mpindo! Fundisho la kwanza ni kuikana Mamlaka waliyopewa mitume kuhusu Neno la Mungu. Watu wamefundishwa kuuamini Uongo wa dini ulio wazi kabisa badala ya kweli wanayoiona ktk Maandiko. Injili yooooote imeletwa na mitume, hizo habari za Yesu tunazozisoma hakuna hata moja aliyoiandika Kristo kwa mkono wake bali aliwaongoza hao walioziandika kwa Roho wake kupitia mitume wake kulingana na Ahadi yake. Basi mkristo anapofikia kuwatilia shaka mitume, ukomo wa safari yake ya kwenda kwa Kristo humfika ktk hatua hiyo, naye hubakia kuwa mshirika mwaminifu wa kusanyiko lake na HUFIA hapo njiani kama Israeli walivyofia jangwani, ndiko huko kujirudisha ktk Sheria kunavyowatimilia walioupungukia wokovu!

  ………… inaendelea

 226. r.m…,

  Kwanza nikushukuru kwa maelezo yako mazuri na yenye nia njema kabisa kulingana na nilivyoyaona binafsi.

  Lakini ni lazima tufahamu pia kwamba kuwa na nia njema peke yake hakutoshi kutufanya tumlinganie Bwana, yaani unaweza ukawa “sincerely wrong” kwa kuendekeza hisia za dini yako, badala ya kulitafakari jambo ktk uhalisi wake kulingana na Neno linachokitangaza!

  Pia ni vizuri ukafahamu kwamba HAKUNA mtu yeyote anayeweza KUMHUKUMU mwingine; ni Neno la Mungu pekee linalohukumu, maana hilo ni Upanga, tena ulio na makali kuliko upanga ukatao kuwili, basi ni vizuri ukalikaribia kwa uangalifu, ukiwa ktk usikivu na si unyenyekevu wa dini ambao mara nyingi hukosa adabu na hivyo kuwasababishia wafuasi wake vilio vya kuhukumiwa!

  Mungu ndiye aliyesema “Kristo ni mwisho wa Sheria”, je, amekosea? Kwamba tunalazimika kuendelea ktk Sheria licha ya Kuhesabiwa Haki kwetu kwa imani? Ni lazima uliweke sawa unalotuambia, usituzungushe ktk hisia za dini zisizo na ufahamu, ngoja nikunukuu:
  “”kamwe kamwe msidanganyike, hakuna kumpenda Mungu bila ya kumtii huyo Mungu katika sheria zake, huo ni uongo uliodhahili kabisa. alichokifanya bwana yesu sio kuondoa sheria za Mungu bali “kutimiza”. kwa hiyo, kwa sisi tunaomuamini, nikweli hatuhesabiwi haki kwa hizo sheria, ila ni lazima tuzitii ,ili tuweze kudhihirisha huo upendo wetu kwa Mungu na hiyo imani yetu kwa mwokozi wetu yesu kristo, ndio maana biblia inasema: KWA MAANA HUKO NDIKO KUMPENDA MUNGU KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE (sheria zake).””

  Sasa kama ni kweli kwamba hatuhesabiwi haki kwa hizo sheria, basi huo ULAZIMA wa kuzitii sheria una faida gani ya kiUngu ilhali kuzitii huko hakutuzalishii haki? Pia ingetufaa zaidi kama ungetuonesha mfano hata wa mtu mmoja ktk Biblia aliyefaulu kuwa na Upendo kwa kuzitii Sheria, itasaidia sana kuliko hii ngonjera ya upendo unayotushawishi kwayo tuiache Neema tuliyokirimiwa, tujirejeshe ktk kongwa la Sheria tulikotolewa, ambavyo Mungu hawajibiki tena kuturejesha ktk Neema baada ya sisi kuiona si kitu!

  Mungu anaposema tuzishike Amri zake, nawaona kwa makusudi ya kusimamisha mafundisho ya dini zenu mmelipotosha neno hilo ili liwe ni zile Amri Kumi, mkililazimisha kwa hila jambo hilo la Sheria kulitawala upya Kanisa ambalo HALIHUSIKI na mambo hayo!

  Kwa ushauri, ukiwa ni ndg yangu; jambo la kwanza elewa kwamba wanyapara wako wa dini hawakuoni huku kwenye blog, basi kaa ktk mkao wa kujifunza, UTAFUNGULIWA kutoka vifungo vya dini vinavyowanyang’anya wafuasi wao ufahamu!

  Nitaendelea…..

 227. Mmoja hapo juu kwa kujiamini kabisa ameandika hivi…”neema tunayokirimiwa ya kuhesabiwa haki kwa imani “NA SI KWA KUZITII SHERIA” !!!!!!!!!. Hili nalo ni jambo. kwa nini wana wa Mungu mnapenda kushindana na kuhukumiana kwa maneno mazitomazito, badala ya kujifunza kwa kunyenyekeana??….hivi ninyi kwa akili zenu mnafikiri neno la Mngu lina mshindi zaidi ya Yesu kristo?. wote sisi tunajua kwa sehemu tu, kwa hiyo michango yetu mbalimbali inawasaidia wengine kujifunza kwa kulinganisha na mafundisho ya biblia kwa uthibitisho zaidi….kwa hiyo ni vizuri kua makini na mambo tunayo andika au kuyakosoa, isije ikawa wewe unaekosoa kumbe ndio mwenye matatizo. kamwe kamwe msidanganyike, hakuna kumpenda Mungu bila ya kumtii huyo Mungu katika sheria zake, huo ni uongo uliodhahili kabisa. alichokifanya bwana yesu sio kuondoa sheria za Mungu bali “kutimiza”. kwa hiyo, kwa sisi tunaomuamini, nikweli hatuhesabiwi haki kwa hizo sheria, ila ni lazima tuzitii ,ili tuweze kudhihirisha huo upendo wetu kwa Mungu na hiyo imani yetu kwa mwokozi wetu yesu kristo, ndio maana biblia inasema: KWA MAANA HUKO NDIKO KUMPENDA MUNGU KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE (sheria zake). Ndugu zangu, nawaandikia haya kwa unyenyekevu kabisa ya kwamba, ile neema ya mwokozi wetu yesu kristo, imefungwa ndani ya zile amri kumi za Mungu na huyu bwana wa sabato, ambapo tukizitii amri zile kwa njia ya rohoni na kumuamini Mungu kupitia imani yetu kwa yesu kristo….TUTASHINDA HAKIKA, Kwa sababu tutakua tumempenda Mungu kwa kutii kwetu sheria zake (UPENDO WETU KWA MUNGU UTAKAMILIKA) na kua na imani kwa yesu kristo, kwa ajili ya kuhesabiwa kwetu HAKI katika mwanae….ndio maana kule mwisho wa biblia yaani kwenye ufunuo, kwa wale walioshinda, biblia inasema: Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU NA IMANI YA YESU. Soma(ufunuo 14:12). nikweli kabisa kua ni kwa neema tu, lakini kitendo cha kutojua msingi au chanzo cha hiyo neema, kinaweza kuwafanya watu waone ni sawa tu, kuishi maisha ya dhambi wakifikiri kua wataokolewa burebure tu, jambo ambalo sio sahihi….nilazima sisi tukiwa ni watoto wa Mungu tuache dhambi kwa bidii yote kwa dhamira yetu yote, halafu baada ya hapo ndipo ule utakatifu wa kustahili kwa haki iliyondani ya mwokozi wetu ndipo >BWANA MUNGU WETU ATATUPA. nawaomba ndugu mue makini sana mnapoandika injili zenu humu kwa kua ni watu wengi sana hujifunza kwa njia hii, pia acheni tabia ya kuhukumiana kwa maneno makali ya kukatisha wengine tamaa kwani hamjui ya kua mawazo yenu tafauti ni ya maana sana kwa watu wanaojifunza!!!!. amani ya bwana iwe juu yenu, asanteni.

 228. @ Lani,
  Hebu tutulie tujifunze kwao pia!!
  Neema ya Bwana ikufunike pia

  @ Sungura na Lwembe
  Ha ha ha ha haa!!
  Shalom wajoli wa Bwana ! Mimi napendekeza twende polepole. Somo hili la sisi ni miungu, linahitaji great attention!! Si mchezo wapendwa!! Naomba, twende polepole kabisa. Nitawauliza maswali tu ambayo nitahiji majibu.
  1. Mnafikiri Mungu aliumba miungu (wanadamu) mienzake mnamo siku ya 6?
  2. Kama ni ndiyo, je, miungu iliyoumbwa kwa mfano wa Mungu/YEHOVA(kwa kila kitu), inaweza kutenda dhambi?
  3. Kama ni hapana, mnafikiri udanganyifu wa shetani ulileta faida kwetu sisi wanadamu ya kuitwa miungu ambapo hapo kabla ya kuwa na sifa ya kujua mema na mabaya, hatukuwa nayo?
  4. Uhusiano wetu kati yetu na Mungu kabla ya dhambi, hamuoni kuwa ulikuwa ni wa kiukandamizaji –Mungu alitukandamiza kwa kutufanya tusiitwe miungu? Alitaka kutuficha nini hasa?
  5. Uhusiano wetu na Mungu baada ya dhambi, hamuoni kuwa umeongezeka sana hadi leo tunaitwa miungu? Kwa maneno mengine, hamuoni kuwa shetani/dhambi imeleta faida kwetu ya kuitwa miungu??
  6. Biblia inaposema Ee Israel Bwana Mungu wako ni mmoja –YEHOVA, huku na sisi tena kumbe ni miungu, hamuoni kuwa Biblia hii inajichanganya? Tufuate nini sasa?
  Naomba niishie hapa kwa leo. Karibuni kwa majibu yenu ya moja kwa moja na mafupimafupi kama itawezekana. Wasalaam.
  Neema ya Bwana iwafunike.
  Siyi

 229. Sungura,
  Umeisema Kweli inayotawala! Wengi kupitia dini zao wamepumbazika sana kuhusu Shetani; walipoambiwa kuwa ni “baba” wa Uongo, basi wao humchukulia kwamba uongo wake ni 100%, jambo linaloonesha kuwa hata uongo wenyewe hawaujui ni nini!

  Na kwasababu hawajui uongo ni nini, ndipo wakiisha kuwa wamekamatwa ktk hila ya kutokuujua uongo ni nini, dini zao huwakaririsha uongo mwingi sana, ambao wao huupokea kwa furaha sana wakiamini kutoka vilindi vya mioyo yao kuwa hiyo ndio Kweli ya Mungu, licha ya kuwa na Biblia zao kwapani!

  Bali Uongo ni Kweli iliyopindishwa; na kwamba siku zote, Kweli ndiyo inayotangulia, naye Shetani hulichukua hilo Neno la kweli na kulipindisha ndipo huwalisha “”maziwa yaliyogishiwa”” nje ya ufahamu wao, ndio hao wenye kuikataa Neema halisi, kwahila hiyo hurudishwa ktk Sheria wasiyoijua na kuishia upotevuni!!

 230. MUNGU NI MWEMA KWA KILA MMOJA TATIZO NI SISI.TUJIFUNZE NA TUSIWE WAJUAJI MAANA BADO HATUJAJUA.MBARIKIWA

 231. Lani,

  Kitu kingine ambacho watu wengi huwa hamkioni na hamkitambui ni hiki, kwamba shetani is a cunning spirit.

  Hakuna mtu muongp au tapeli ambaye maneno yake kwa 100% huwa ni ya uongo. Lazima achanganye uongo na ukweli.

  Hilo suala la kwamba shetani alisema uongo akimwambia Eva kuwa siku mkila mtafumbuliwa macho na kufanana na Mungu kwa kujua mema na mabaya (Mwa 3: 5) hata halikuwa na uongo ndani yake.

  Uongo ulikuwa kwenye mstari wa 4 kuwa hakika hamtakufa. Mungu alikuwa amesema “Hakika mtakufa”.

  Ili ujue kuwa haikuwa uongo ila ni ukweli wenye hila ona baadae Mungu anachosema: Mwa 3: 22- sasa mwanadamu amekuwa kama mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya!

  Hata kwa Yesu, shetani alisema ukweli wenye hila “jitupe chini maana imeandikwa atakuagizia malaika….., na ni kweli imeandikwa hivyo.

  Usipojua hilo utaendelea kuukana ukweli wa Mungu just kwa sabavu umetumiwa na shetani kwa hila!

 232. Lani,

  Nafikiri majibu ya angalizo ulilompa Siyi kuhusu sisi kuwa miungu umeyapata kwa Lwembe.

  Sihitaji kuongeza mambo mengi sana, hilo jibu linakutosha kabisa.

  Kuna mtindo wa uandishi huwa naupenda sana, wa kusema kitu fulani ambacho kiko kwenye maandiko bila bila kuyataja hayo maandiko.

  Mtindo huu naupenda maana husaidia sana kuwatambua wasiojua maandiko ila wamejaa fundisho na fikra ya dini zao.

 233. YESU ANAITIMILIZA TORATI NDANI YETU, MAANA YEYE NDIO MTENDAJI, HAPO AWALI BABU ZETU WALICHUKUWA NAFASI YA WAO KUWA WATENDAJI, NDIO MAANA AGANO JIPYA LIKAWA MUHIMU KWETU.

  MPENI MIILI YENU NDIYO DHABIHU YA KUMPENDEZA.

  1 WAKORINTHO 7:19
  “KUTAHIRIWA SI KITU, NA KUTOKUTAHIRIWA SI KITU BALI KUZIHIFADHI AMRI ZA MUNGU.”

 234. 1 YOHANA 5:3
  “KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE; WALA AMRI ZAKE SI NZITO”

 235. Mwisho, napenda niyarudie machache kuhusu kukoma kwa Torati.

  Kimsingi, jambo la kwanza tunalopaswa tuelewe ni kwamba Mungu tumnajua kutoka ktk Maandiko, naye hujidhihirisha kupitia hayo. Kama kuna elimu yoyote inayomhusu Mungu iliyo nje ya Maandiko, au yenye kupingana na Maandiko, hiyo ni elimu inayokuingiza ktk umauti.

  Biblia ktk Gal 3:24 kuhusu Torati inasema, ” Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.” Basi ili yeyote yule aweze kufika kwa Kristo, ni lazima awe ameongozwa na hiyo torati, hapo inapoifunua dhambi na kuiweka wazi mbele yake kisha yeye kufikia kujitambua kwamba ni mwenye dhambi anayehitaji Rehema ya Mungu ili aepuke adhabu ya mauti. Nayo Rehema hiyo ndiyo inayotafsirika ktk Neema tunayokirimiwa ya KUHESABIWA HAKI kwa imani na si kwa kuzitii Sheria.

  Hivyo basi torati na mauti ni mapacha wasioachana, maana Maandiko yanasema HAKUNA aliyehesabiwa haki kwa sheria, nasi twatambua wasio na Haki wanastahili Hukumu!

  Yeyote aliyefikishwa kwa Kristo, kama alivyoongozwa na Torati, huyo huzaliwa mara ya pili kwa Roho na kuingizwa ktk Sheria ya Kifalme ambayo walio ktk torati hawajui chochote kuihusu. Ni mambo yaliyo nje ya ufahamu wao mdogo, ndio maana wanashangaa mkristo kuwa mungu leo hii, kwao ni hadithi za kale!

  Hakuna anayewaongoza watu kwa Sheria mbili, Sheria inakuwaga moja tu; kwa ambao bado wako mafunzoni, hao walio safarini wakiongozwa na Torati ikiwapeleka kwa Kristo, hawa unapowasikiliza unaweza ukadhania kwamba wamekwishafika kwa Kristo kwa hadithi zao, lakini wajaribu kwa Neno la Kristo, labda uwaulize, “Hivi yule mwivi siku ile pale msalabani, alikwenda peponi siku ile?” Ndipo utawaona wasivyoelewa, mara watakurudisha huko kwa Muhubiri wakwambie kuwa wafu wamelala makaburini, – Maandiko bado yamefungwa kwao, HAWANA RM, mwenye kuyafumbua mafumbo ya Mungu, bado wako mafunzoni, ni watoto wadogo!

  Siku wakikua, wataingizwa ktk Sheria ya Kifalme, watayaelewa na Maandiko,

  until then,

  Gbu!!!!

 236. Siyi & Lani,

  Kwanza niwapongezeni kwa mikanganyiko!

  Mtu akiwasikiliza juu juu ni LAZIMA ataamini kwamba ninyi ni Wakristo, lakini kumbe ni wale “waliojitenga na Imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”! 1Tim 4:1

  Unajua Shetani huwatia watu upako ili wasiliamini Neno la Mungu; nao upako huo huja ktk vifurushi vya dini; ndiyo hayo mafundisho yanayotokana na roho zidanganyazo!

  Mnaweza kuwa msioelewa kutokana na ‘upako’ huo kuwafunga ufahamu wenu, kama ulivyowafunga Wayahudi, lakini ninaamini tukiwatazamisha Neno la Mungu, kwa Nguvu iliyomo humo, mtaponyoshwa kutoka mikono ya uharibifu inayozishikilia fahamu zenu na hivyo kuwakosesha Maarifa mnapolisoma Neno la Mungu mkifanywa kuwa watumwa wa mambo ya kijinga mliyoaminishwa kwamba ndio Kweli!

  Tazama jinsi mlivyotolewa ktk Ukristo na kutumbukizwa ktk dimbwi la mafundisho ya mashetani bila ufahamu: Kuhusu “Wakristo kuwa miungu” bila ya aibu mnasema na kuamini kwamba,
  “””HILI NI FUNDISHO LA MAPINDUZI, FUNDISHO LA KIZAZI KIPYA/NEW AGE NA OCCULTISM. FUNDISHO PIA LA WAMARMONS. AMELIFUNDISHA SHETANI PALE EDENI””
  Masikini hamuijui hasara inayowakabili kwa kufundisha jambo kinyume na Injili; ni bora mngejipa nafasi ya kujifunza kutoka kwa wapendwa, mkayakagua na Maandiko kuliko mlivyolikurupukia Neno hilo na kumwaga sumu ya ’nyoka’ ili kuwapofua wachanga macho yao ya kiroho, walipungukie Neno la Mungu kama mlivyo ninyi!

  Neno linaloshughulika na watu wa jinsi yenu lilikwisha kutoka, na huwa halirudi tupu bali hutimiza kile lilichosema, Gal 1:8 “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.” Basi hebu niambieni mtaikimbiaje hiyo LAANA ilhali Neno ndilo hilo hapo, nanyi mnasema alichokifundisha RM ni OCCULT?

  Zab 82:6 “Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.”
  Msiwe wajinga, Mungu hana utani na mtu awaye yeyote yule, Yeye analiangalia Neno lake tu! Na amesema ajapo RM, kumpinga huyo ni Jehanum moja kwa moja!

  Roho za dini huwa hazifi, ziliwapagaa Wafarisayo huko nyuma, wakatoka wakilipinga Neno la Mungu, nanyi pia mnatembea njia hiyo hiyo:
  “Wa…. (Wasabato?) wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.”Unawaona! Ni watu wa dini, tena ni wasafi sana, hawali chochote kilicho najisi, hata kama aliyewaambia kuwa hiki ni najisi, kisha baadaye akawaambia amekisafisha, wao hupendelea makatazo zaidi kuliko uhuru; wanaishika sana sabato, wanaweza kukuua kwa kuivunja ila wanaendelea na uzinzi wa kiroho hapo wanapolitukana Neno la Mungu wakiliita OCCULT ktk furaha ya kuyashikilia madude yao waliyojitungia!
  Yn 10:34-35 “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka) …”

  Masikini hawajui chochote kuhusu Mungu, wapo hapo wanaigiza wasiyoyajua; kwao Biblia imefungwa, Dan 12:4 “Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu…” ndio maana kwa jambo hili wanakuambia wewe kuwa mungu ni kufuru!!!!!!!

  Bwana na awaondelee KUTOKUAMINI kwenu!

 237. SIYI
  MCHANGIAJI UNAYEITWA SIYI JILINDE SANA NA FUNDISHO, ALILOKWAMBIA MCHANGIAJI MMOJA HAPO,

  AMESEMA: “Ivi wewe hujui kwamba sisi ni miungu,”

  HILI NI FUNDISHO LA MAPINDUZI, FUNDISHO LA KIZAZI KIPYA/NEW AGE NA OCCULTISM. FUNDISHO PIA LA WAMARMONS.

  AMELIFUNDISHA SHETANI PALE EDENI

  MWANZO 3:5
  “KWA MAANA MUNGU ANAJUA YA KWAMBA SIKU MTAKAYOKULA MATUNDA YA MTI HUO, MTAFUMBULIWA MACHO, NANYI MTAKUWA KAMA MUNGU, MKIJUA MEMA NA MABAYA.”

  KUFANANA NA MUNGU NI KATIKA UTUKUFU, YAANI HAPO ADAMU NA HAWA WALIPOUMBWA WALIKUWA NA UTUKUFU AMBAO BAADA YA DHAMBI WALIUPOTEZA.

  HIKI NDICHO TUNACHOPASWA KUKITAFUTA,NA TUNAPEWA NA ROHO MTAKATIFU. PAULO ATUSHUHUDIA HAPA CHINI;

  2 WAKORINTHO 3:17,18
  “BASI ‘BWANA’ NDIYE ROHO; WALAKINI ALIPO ROHO WA BWANA, HAPO NDIPO PENYE UHURU, LAKINI SISI SOTE, KWA USO USIOTIWA UTAJI, TUKIURUDISHA UTUKUFU WA BWANA, KAMA VILE KATIKA KIOO, TUNABADILISHWA TUFANANE NA MFANO UO HUO, TOKA UTUKUFU HATA UTUKUFU, KAMA VILE KWA UTUKUFU UTOKAO KWA BWANA, ALIYE ROHO.”

  PAULO ANASEMA KUURUDISHA UTUKUFU.

  MUNGU NI MMOJA:

  ISAYA 46:9

  “KUMBUKENI MAMBO YA ZAMANI ZA KALE; MAANA MIMI NI MUNGU, WALA HAPANA MWINGINE; MIMI NI MUNGU WALA HAPANA KAMA MIMI;”

  TUJILINDE MAFUNDISHO MATATU YA SHETANI PALE EDENI YANAWACHUKUA WENGI TUSIWE HUKO.

 238. Siyi,

  Kwa habari ya unachomwambia Chemo, mini naona umekosa la kusema. Unanifanya nikushangae kwa kweli.

  Ivi wewe hujui kwamba sisi ni miungu, ivi hujui kuwa sisi ni roho wanaoishi mwilini? Siyi umekuwaje bhana?

  Kwani unaposoma inasema Mungu alisema na tufanya mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu, wewe huwa unaona inamaanisha nini hapo zaidi ya vile ambavyo inaeleweka?

  Chemo kasema na kuonesha maandiko ya kila anachokisema, wewe hukubali unaona anajiinua. Hebu basi wewe tuambie hayo maandiko yanamaanosha nini?

  Kumbuka msemo wangu kuwa Kiburi ni pale unapojiinua bila Mungu kukuinua, lakini pia kujishusha wakati Mungu kakuinua si unyenyekevu huo, bali ni kiburi pia.

 239. @ Tunkuh
  Mungu akubariki sana kama ulinielekezea mimi hizo Baraka. Mpango wa mbingu ni kwamba, mtu akikuombea, Baraka, mwombee Baraka maradufu. Nami sina budi kufanya hivyo. Ubarikiwe sana rafiki. Nafikiri ushauri wako wachangiaji tunaopenda kuandika kiingereza, tutabadilika. Mungu atusaidie sote.

  @ Chemo,
  Asante kwa maelezo yako rafiki. Bado nakuona una taabu nyingi imefunika. Ila kukwambia hivyo hapa mtandaoni, inaonekana kama Siyi anakughasi na kukujeli! La hasha rafiki!! Ninachosema, ni kile ninachokisoma hapa baada ya wewe kuandika. Naona una shida kubwa. Na hili hutalikubali kwa sasa, ni mpaka hapo utakapojinyenyekeza kujifunza kwanza. Kwa nini? Hebu angalia uelewa wako ulivyo mashakani…
  1. Umesema wewe ni Roho, kwa sababu umezaliwa kwa Roho. Sasa, naomba nikuulize, kuwa, Mungu ni Roho, na wewe umezaliwa na huyo Roho, je, wewe ni mungu? Au Mungu ni Roho, Kristo ni mwana wa Roho, hivyo na YEYE ni ROHO, na sisi Kristo ni kaka yetu kwa njia ya imani, je sisi nasi ni miungu/mikristo? Na kwa vile Kristo hututakasa na kuturejesha kwenye hali ya usafi aliyokuwa nayo Adamu na mkewe kabla ya anguko, je, Adamu na Hawa kabla ya dhambi, walikuwa ni roho/miungu? Kama jibu ni ndiyo, ina maana Mungu aliumba miungu au roho wenzake wadogo?
  2. Umesema kuwa, “Mungu amenitoa kutoka kiwango cha mwilini ( Mwanzo 6:1-3, na chakuwa mavumvi tu Mwanzo 3, na kuniweka katika LEVEL yake mwenyewe. For I am sitted with Christ, NOW, IN THE SPIRIT…” Kwa maelezo mengine, umesema kuwa, hapo kabla ya dhambi, Mungu alikosea kumuumba mwanadamu na kumuweka katika ngazi ambayo hakufanana na Mungu. Ila baada ya dhambi, Kristo akaja kutukomboa, sasa hivi Mungu amebadilisha mfumo wake na kutufananisha na YEYE mwenyewe kabisa kuliko hapo awali kabla ya dhambi!! Kwa maana nyingine, unasema kuwa, shetani alileta faida kubwa kwetu ya kufananishwa na Mungu katika roho!! Au siyo kaka?? Una una maana gani hapa??
  Kama sivyo, nakushauri ukae chini kuyajifunza hayo mafungu polepole. Mungu anahuzunika sana anapoona kuwa watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa!! Pole sana. Ila mimi nitaendelea tu kukuombea hata kama wewe hupendi mimi kukufanyia hivyo. Neema ya Bwana ikufunike.
  Siyi

 240. 1 WAKORINTHO 14:32
  “NA ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII”

  MANABII NA WATU WENGI SIKU HIZI WANAOJIITA MITUME HUPINGANA NA MITUME KATIKA BIBLIA, MITUME WANAPOKAZIA AMRI WAO WANATENGUA..

  MFANO:

  WAEFESO 6:2,3
  “WAHESHIMU BABA YAKO NA MAMA YAKO; AMRI HII NDIYO AMRI YA KWANZA YENYE AHADI, IPATE HERI, UKAE SIKU NYINGI KATIKA DUNIA. NANYI,

  KWA MANENO HAYA YA PAULO NANI ANASEMA HATUITAJI TORATI.

  UKIONA MTU ANASEMA KINYUME NA MANABII NA MITUME KUWA NAE MAKINI.

 241. Hivyo basi, siyo mimi ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu (Galatia 2:20), anaishije? kwa maana yeye ndiye mwanzilishaji na mkamilishaji wa imani yangu, na moyo wangu haunihukumu, ndiyo maana ninao ujasiri wa kuukiri ukweli wa Kristo, na kumkiri yeye.

 242. Wote, tuwe na amani! Niseme machache kuthibitisha maelezo yangu hapo juu. Na ninapenda kuwa huru kuelezea kwa lugha zote mbili, ya kiswahili, na ya kiingereza.

  1 Mimii, ni roho.
  Aliyezaliwa kwa mwili ni mwili, na aliyezaliwa kwa Roho ni roho (Yohana 3:6). Na kuzaliwa na Roho ndiyo kuokoka. Kwa hiyo, mimi nimezaliwa na Rohi, hivyo mimi ni roho.

  2. Nimezaliwa kwa Mungu (Yohana 1:11-13)
  Bali wotw waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika kuwa watoto wa Mungu, ndio wale WALIAMINIO jina lake, waliozaliwa si kwa damu, wali si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, BALI KWA MUNGU

  na, 1 Yohana 5:1
  Kila mtu aaminiye ya kwamba Yesu ni Kristo AMEZALIWA NA MUNGU, na pia (1 Petro 1:23) nilizaliwa mara ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyiharibika, KWA NENO LA MUNGU ambalo li hai ña ladumu milele.

  3. Mimi ni wa asili ya Mungu (2Petro 1:4)
  Tena kwa hayo, ametukirimia ahadi kubwa mno na za thamani, ili kwamba, ili kwamba mpate kuwa washirika wa ASILI (soma: tabia) ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu, ulioko duniani kwasababu ya tamaa. I am no longer a natural being.

  4. Ninao uzaima/uhai wa Mungu (uzima wa milele)
  1 Yohana 12
  Yeye aliye naye Mwana anao huo uzima (uzima wa milele, anao SASA); asiye naye Mwana wa MUngu, hana huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo haya ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mlioliamini Jina la Mwana wa Mungu

  5. Mimi (roho) ni mmoja naye (1 Corinthians 6:17)
  Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.

  6. Utambulisho wangu, (my identity) ULIBADILISHWA, haukuboreshwa. Roho iliyokuwepo hapo kabla sijazaliwa mara ya pili, na mambo yake yote iliondoshwa. (2Corinthians 5:17)
  Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya.

  7 Hii roho iliyozaliwa ni Roho ya Kristo (Rumi 8:9)
  Lakini ikiwa Roho wa Mungy anakaa ndani yenu, ninyi hamuufuati mwili, bali mnaifuata Roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

  8. Jinsi yeye alivyo, ndivyo na mimi nilivyo hapa duniani, WAKATI ULIOPO. (1Yohana 4:17)
  Katika hili, pendo limekamilishwa kwetu, ILI TUWE NA UJASIRI SIKU YA HUKUMU, KWAKUWA KAMA YEYE ALIVYO NDIVYO TULIVYO NA SISI ULIMWENGUNI HUMU.

  9. I am the righteousness of God. Mimi ni haki ya Mungu. (2 Corinthians 5:21)
  Yeye asiyeijua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwaajili yetu, ili sisi TUPATE KUWA HAKI YA MUNGU katika yeye.

  10. Haiwezekani kunihusisha na mwili. Haiwezekani kukubaliana na mambo ya mwilini ya Galatia 5:19-21. Nimetafakali, nikakubali, baada ya kushawishiwa juu ya utambulisho wangu kikamilifu. (I am fully persuaded) Rumi 8:38

  Mungu amenitoa kutoka kiwango cha mwilini ( Mwanzo 6:1-3, na chakuwa mavumvi tu Mwanzo 3, na kuniweka katika LEVEL yake mwenyewe. For I am sitted with Christ, NOW, IN THE SPIRIT, na mengine mengi yameandikwa ili tupate kujua kusudi timilifu la Mungu. Na yeyote apendaye kujifunza, atabarikiwa, maana sikusema maneno yauhusuo mwili pekee, bali roho.

  Na kuamini, ni kule kukubaliana na Mungu, kwa yote aliyoyasema.

 243. Asante saaana mtumishi, kuna vitu nimejfunza hapo umenibariki kwa kweli. Halafu mimi napata shida kwakweli hv inakuwaje unasoma mada kwa kiswahili unachangia kwa lugha nyingine? Je unahakka hicho ulichochangia kitaeleweka kwa walengwa? Tujitahidi kusoma mazingira hiyo nayo ni hekima.

 244. Siyi,
  Swali langu liko wazi sana. Kwamba Yesu ni dini?

  Kwa nini hujalielewa sasa?!!

  Just nijibu.

  lakini pia sioni wapi Chemo kajiinua katika yale aliyosema. Kusema kinyume chake ni kujaribu kujinyenyekesha kusiko na maana.

  Kujiinua wakati hujainuliwa ni kiburi, lakini pia kujishusha wakati Mungu amekuinua nacho ni kiburi vilevile!

  Anyway, tuendelee na swali langu!

 245. Sungura,
  Nashukuru sana kwa ushauri wako. Kimsingi ni ushauri mzuri. Nimeupokea rafiki yangu. Nilitumia maneno magumu na makavu kwa chemo ili kumrejesha kwenye hali ya utu. Maana yeye alijiona kama amekuwa daraja moja na Mungu, ana akili ya Mungu, chata ya Mungu na anaweza kusoma mioyo ya watu wengine, mambo ambayo kimsingi binadamu tunaoukulia wokovu kila siku, hatujafikia huko.
  Ajabu zaidi, anaamini kuwa anajua kumbe hajui baadhi ya vitu vingine muhimu sana kwa ajili ya wokovu wake. Nilitumia maneno makali na magumu ili arejee na kukaa kwenye jukwaa la mijadala kwa lengo la kujifunza na si kupayuka “mimi nina muhuri wa Mungu, chata ya Mungu, connected na Mungu nk, ilhali ni mtu aliye gizani anayehitaji msaada.
  Kuhusu habari za dini kuwa ni njia sijui sijaeleweka wapi. Nina imani nilieleweka vizuri. Kama wewe hujaelewa, uliza ni wapi usaidiwe tu.
  Tuko pamoja jukwani
  Siyi

 246. Siyi,

  Hebu sema tena, kwamba Yesu ni dini?

  Halafu maneno unayomkosoa nayo Chemo siyo ya kusemwa na mtu mzima kama wewe. Tumekuwa wote SG hapa kwa muda ni vizuri kubadilika pia katka kauli zetu.

  Siyo haki kumwambia Chemo kuwa ni mtu asiyejua chochote, huko ni kukosa uungwana. Mtu akisoma anachosema Chemo atakwambia kuwa si mtu wa kumwambia kuwa hajui chochote!

  Ni vema kujua kutenda haki kwa wengine ili ili wenye hekima wasikuone kuwa ni mtu mwenye maneno ya juujuu ya kishabiki!

  Tumia maneno yako kwa mtu kwa haki!

 247. @ Mhina,
  Mungu akubariki ndugu yangu kwa ufafanuzi mfupi lakini ulioshiba. Kimsingi nilivutiwa na maelezo yako yooote ya siku ile, isipokuwa hapo mwishoni ndyo sikukuelewa ndiyo maana nikakuomba maelezo/ufafanuzi kabla ya kukutafisri visivyo!! Kusema wazi, pachiko hili la Msella, sikuelewa kwamba kuna waj2 wenye uelewa sahihi namna hii kwa baadhi ya ufafanuzi wa sheria za Mungu. Katika hili, kuna sehemu ndogo sana tunayotofautina. Ndogo sana. Nasikitika akina Msella, Magreth na wengine wote waliochangia mwanzoni kabisa, hawakujibu maswali yangu. Nakushukuru sana wewe Mhina, John Paul na kipenzi changu Chemo anayejitahidi kuvumilia licha ya makavu anayoyapokea. Neema ya Bwana iwafunike sana kwa ujumla wenu. Tuzidi kuombeana sana ili Bwana atufunulie sehemu tusiyoiona, tuione kwa uhalisia wake.

  @ Chemo
  Ha ha ha ha ha!!
  Kwanza, unafurahisha sana rafiki rangu wa rohoni. Umenena vyema, nami sikupingi wala kukubishia. Utambulisho wako, unaujua wewe mwenyewe na Mungu wako. Lakini angalia usije ukajihesabia haki ndugu yangu!! Ukajiona mwenye haki zaidi ya wengine, kazi ambayo ni Mungu peke yake ndiye anaweza kuifanya!! Utambulisho wako huo, uangalie vizuri. Ni ushauri tu wangu kwako.
  Pili, umesema wewe huna dini. Na neno dini, ni neno la Kiarabu lenye maana ya NJIA. Na njia kwa mujibu wa Biblia, ni Kristo mwenyewe. Maana yeye ndiye NJIA na uzima… Sasa ukisema kuwa wewe siyo mtu wa dini, huna dini, n.k. tukueleweje tunapouangalia utambulisho wako hapo juu na kauli hii?? Je, hujui kuwa kwa kusema huna dini, siyo mtu wa dini, unamkana YEYE aliye DINI yaani NJIA na uzima..-Kristo?? Kimsingi, nimekuelewa kuwa wewe huna Yesu rafiki yangu. Huna Yesu, japo huelewi kama huna kweli!!
  Mimi nikushauri uendelee kubaki hapa mtandaoni ujifunze hata kama si kwa kujibizana na Siyi, huenda utaambulia cha kukusaidia. Maana unafikiri unajua mambo kumbe masikini wa Mungu huna hata chembe!! Unapapasapapasa tu. Pole sana rafiki yangu Chemo

  @ Lani
  Ha ha ha ha ha !!
  Ubarikiwe sana Lani. Daah!! Umefunua kitu kikubwa sana hapa ndugu yangu. Mwenye akili ni nani basi? Ni nani atakayeishi kwa mujibu wa Biblia inavyowatambua wenye akili?? Lani, tusaidiane kuwaelimisha hawa ndugu zetu. Maana wengine wanaamini kuwa ni wana Mungu, wana alama ya Mungu, kitabulisho cha Mungu n.k. huku wamkina mbashala YEYE aliywaita kutoka gizani kuingia katika nuru yake ya ajabu… Tuwasaidie hawa na kuwaombea pia.
  Ubarikiwe sana Lani.
  Siyi

 248. NDUGU CHEMO NA SIYI KUNA NDUGU MUWASAIDIE KATIKA HUU MJADALA ILI
  WAACHE KUJISIFU, MUNGU ANAWAJUA WATU WENYE AKILI

  BIBLIA IMETAMBULISHA WATU WENYE AKILI KAMA IFUATAVYO;

  MOJA:IMEMTAJA MWENYE AKILI KUWA ANAYESHIKA AMRI ZKE NA KUZITENDA

  KUMBUKUMBU 4:6
  “ZISHIKENI BASI ,MKAZITENDE, MAANA HII NDIYO HEKIMA YENU NA AKILI ZENU,MACHONI PA MATAIFA WATAKAOZISIKIA AMRI HIZI ZOTE,NAO WATASEMA HAKIKA TAIFA HILI KUBWA NI WATU WENYE HEKIMA NA AKILI”

  MBILI:UKIWEZA KUPAMBANUA ALAMA YA MNYAMA

  UFUNUO 13:18
  “HAPA NDIPO PENYE HEKIMA. YEYE ALIYE NA AKILI NA AIHESABU HESABU YA MNYAMA HUYO; MAANA NI HESABU YA KIBINADAMU. NA HESABU YAKE NI MIA SITA SITINI NA SITA.”

  TATU: UKIWEZA KUMTAMBUA YULE MFALME ANAYELETA UHARIBIFU/MNYAMA
  UFUNUO 17:9
  “HAPA NDIPO PENYE AKILI ZENYE HEKIMA.VILE VICHWA SABA NI MILIMA SABA ANAYOKALIA MWANAMKE HUYO”

  MAANA KUNA WATU WANAJIITA WENYE AKILI HALAFU WASIJUE BILA KUWA NA AMRI ZIMEANDIKWA MOYONI ALAMA YA MNYAMA,HUTAITAMBUA,WALA MNYAMA/MFALME WA SABA WALA WA NANE HUWEZI MTAMBUA.

 249. Siyi, tazama vizuri hapa, siku moja utakuja kuelewa.

  1 Corinthians 2: 6-16

  Walakini, iko hekima tuisemayo kati ya wakamilifu; ila si hekima ya dunia hii, wala ya hao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilika, bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu, AMBAYO WENYE KUITAWALA DUNIA HII HAWAIJUI HATA MMOJA, maana kama wangaliijua wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu, lakini kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu) mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao; LAKINI MUNGU AMETUFUNULIA SISI KWA ROHO, MAANA ROHO, HUCHUNGUZA YOTE, HATA MAFUMBO YA MUNGU. Nayo, twayanena si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, TUKIYAFASIRI MAMBO YA ROHONI KWA MANENO YA ROHONI. Basi, mwanadamu wa tabia ya asili, hayapokei mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake huyo, ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. LAKINI, MTU WA ROHONI, HUYATAMBUA YOTE, WALA YEYE HATAMBULIWI NA MTU. Maana, ni nani aliyeifahamu AKILI (soma NIA) ya Bwana amfundishe (soma amwelimishe)? Lakini sisi tunayo AKILI (soma NIA) ya Kristo (Msisitizo ni wangu)

  Na je, nikikwambia, kwamba mwili wangu ni hekalu la Roho Mtakatifu, (1Cor 3:16, 2Cor 6:19), na kwamba my body is the temple of the living God… UTAELEWA?

  Hayo yote, ndiyo yaliyonipa kuufahamu moyo wako, kiasi I identified you, and put you on your rightful place, sishangai ukighadhabika, ndio kawaida ya watu wa tabia ya mwilini.

  Asante

 250. Haya Siyi. We songa mbele tu. Ila nikusaidie kidogo kunielewa, Mimi ni mmoja na Mungu (2Corithians 5:17). Nimebarikiwa na Baraka Zote Za rohoni (Ef 1:3) Nimekubalika katika mpendwa Kristo Yesu (Ef 1:6). Ninayo akili ya Kristo (1Cor 1:16), I have the unction from the Holy One, and I know all things (1John 2:20). I have the anointing in me that teaches me ALL THINGS (2 John 2:27) I am the righteousness of God (2Corinthians 5:21). HUO NDIO UTAMBULISHO WANGU; NIMEUKUBALI, HAKUNA HAJA YA KUHITAJI PROOF KWA NGURUMBILI ASIYEFAHAMU MAMBO YA ROHO WA MUNGU (For I am FULLY PERSUADED of my identity in Christ), SIO HAYO MENGI AMBAYO UMEYAWEKA KWENYE MAELEZO YAKO HAPO JUU.

  Sina hata haja ya kuyachambua maana nitakuwa napoteza muda; ukiisha ujua moyo wa mtu, ya nini kuendelea kushindana naye? Wewe mambo niliyoyaweka hapo juu hayakufai, haujafika huko, moyo wako uko chini, kwa sababu wewe ni wa ulimwengu huu (you are from below not from above); kazi yako ni kutetea dini. Mimi SINA DINI, Ukristo sio dini, ni kule kuzaliwa na Mungu. Ndiyo maana nasema mimi sina dini. Katika kiwango hiki cha uelewa wa Mungu, maombi n.k, n.k, yana mtazamo tofauti sana. Mtu wa asili ya mwili, hawezi kuyatambua mambo ya Roho wa Mungu, kwa maana huyo kwake, NI UPUUZI; si ajabu kwamba haya yoote ninayoyaandika ni upuuzi kwako Siyi.

  Mimi sikuombei, kwa sababu maombi hayawezi kukusaidia. Ningekushauri, ujifunze NENO la KRISTO, maana dini imekuleta hapo ulipo, NENO la KRISTO litakufunulia yaliyo mengi katika ROHO. Unafikiri wale waliokupuuzia wamekuogopa, au wamekasirika? I dont think so, waliona haina tija kuendelea kumpigia nguruwe gitaa, na kumtupia nguruwe lulu, eti ili akaoge, apige pamba safi awe pet cat. Ndo maana wakakuacha katika makandiko yako ya DINI.

  Nimemaliza Siyi

 251. UFAFANUZI….. ” Ndio maana watu wengi (sio siyi) wasioujua upendo wa Yesu na utimilifu wake katika sheria, hawaelewi wala hawaoni tofauti kati ya upendo wa Mungu na ule upendo wao wa kibinadamu waliouzoea kwenye maisha yao na dini zao mbalimbali. Wao kwa kutoelewa kwao, wanaona kama ni yaleyale…ndio maana wengine husema “dini zote ni sawa, jambo ambalo sio la kweli. Nilikutaja wewe kimakosa, basi nisamehe na ubarikiwe. Kwaheri.

 252. Mhina,
  Kimsingi nimebarikiwa sana na maelezo yako ya mwanzo kwenye pachiko lako hili la sasa. Bwana akubariki sana. Sehemu uliyoniacha ni hii, “Pia wao hufikiri kua, ule upendo wao wa kibinadamu ni sawa tu, na upendo wa Mungu tulioupokea ndani ya Yesu kristo, ndio maana kama bwana siyi huko juu, anaona kua, kama swala ni upendo basi kila mtu anao, Pia kama swala ni imani tu, basi kila mtu anayo…jambo ambalo sio kweli, tena ni vitu tofauti kabisa”.
  Kama utaweza, naomba ufafanuzi. Sijakuelewa hapo kabisa.
  Nitashukuru sana

  @ Chemo
  Asante kwa kuujua moyo wangu, japo kimsingi huo ni uongo wa wazi Chemo. Wewe mwanadamu, unawezaje kuusoma moyo wa mtu mwingine??? Wewe Mungu siku hizi rafiki yangu!!?? Hujui kuwa hiyo nayo ni kufuru tosha?? Wewe sema kuwa, huna hoja tu za kujadiliana na Siyi, basi!! Yaani wewe ni masikini wa neno kiasi hicho!! You cannot biblically defend what you believe!!?? Haina haja ya kuwa na dini ambayo huwezi kuitetea kwa misingi ya maandiko. Hakuna haja rafiki!! Najua kwa maneno haya yanakukera na kukuudhi sana, lakini ukweli ndio huo. Na mimi nimekuwa mtu wa makavumakavu tu siku hizi. Mwenye kuchukia shauri yake!! Lakini ni lazima aambiwe ukweli, maana neno la Mungu ni upanga!.Usitarajie upanga ukikupitia utabaki unacheka!! Hasha!! Kilio, maumivu na hasira zitakuandama! Huna budi kuwa makini, maana ukiona hivyo, tambua kuwa, you are absolutely under the carnal mind control!! Hatari iliyoje!!
  Hata hizo baraka huna!! Ungekuwa nazo, usingekuwa hapa!! Wewe ni masikini tu tena unayehitaji Neema na Baraka za Bwana. Na kwa taarifa yako, dini ya Kristo ni kuombea wanaowaudhi. Sasa kama wewe unakerwa na Siyi, na hutaki hata akuombee, je wewe unaweza kumwombea kweli? Acha unafiki rafiki yangu!! Wewe ni ndugu yangu katika Kristo lazima nikwambie ukweli. Ukikasirika, shauri yako. Ukinuna, yote mema kwangu!! Wako wengi walioishiwa hoja kama wewe wakang’ang’ania baadhi ya aya za Biblia zilizofyatuliwa kwa mabomu ya Kweli. Hata wewe, nakuona unashikilia kilekile ambacho kimeshapinduliwa tayari. Sasa, la kukusaidia sina ila kukuombea tu japo hutaki. Na kwa vile hutanifunga mdomo, mimi nitaendelea tu kukuombea kwa sababu ninakupenda!! Ningekuchukia, nisingekwambia!!
  Kama una sikio la kufa, utakufa tu milele. Lakini kama una sikio la kuokolewa, Kristo alikufa kwa ajili yako pia. “Jitahidi (soma) kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli” 2 Timotheo 2:15.

  Kwa upendo wote.
  Siyi

 253. Rumi 8:1-4

  1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

  2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

  3 MAANA YALE YASIYOWEZEKANA KWA SHERIA, KWA VILE ILIVYOKUWA DHAIFU KWA SABABU YA MWILI, MUNGU, KUWA KUMTUMA MWANAWE MWENYEWE KATIKA MFANO WA MWILI ULIO WA DHAMBI, NA KWA SABABU YA DHAMBI ALIIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI; (Nimesisitizia kwa herufi kubwa)

  4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.

  Na Rumi 8:31-37

  31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?

  32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?

  33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.

  34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.

  35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?

  36Kama ilivyoandikwa, ya kwamba,Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa,
  Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.

  37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.

  38 KWA MAANA NIMEKWISHA KUJUA HAKIKA YA KWAMBA, WALA MAUTI, WALA UZIMA, WALA MALAIKA, WALA WENYE MAMLAKA, WALA YALIYOP, WALA YATAKAYOKUWAPO, WALA WENYE UWEZO,

  39 WA;A YALIYO JUU, WALA YALIYO CHINI, WALA KIUMBE KINGINECHO CHOTE HAKITAWEZA KUTUTENGA NA UPENDO WA MUNGU ULIO KATIKA KRISTO YESY BWANA WETU. (Nimesisitiza kwa herufi kubwa)

 254. Siyi, mimi siiuchukii, ila kwa kule kuujua moyo wako nimeona nisizidi kukinzana nawe kwa maneno. Na hapa unakuja kujionyesha kwamba yote unayoyasema yanatoka kwa Mungu.

  Ni sawa tu, sina haja ya kujadiliana zaidi na wewe. Nakutakia safari njema tu huko uendako, kama ulivyodai kuwa ni kule walikoenda Yesu na Mitume, maana waliipita njia unayoipita.

  Mengine juu ya kuniombea na kunitakia baraka, kiukweli ni kwamba mimi nimeokwishabarikiwa na baraka zoooote ninazozihitaji kwakuwa ninayo Roho wa Kristo (Ef 1:3, 2 Peter 1:1-3) sihitaji baraka wala maombi ya Siyi, na tena, sikuchukii wala sikutengi, wala sikusengenyi; kwa kauli zako nimepata tu kujua wewe ni mtu wa namna gani na nimeujua moyo wako.

  Ninaendelea kukupenda tu, maana hiyo ndiyo kitu ya maana kwangu. Ni Yesu aliyekufia msalabani, mimi sitafikia kiwango cha concern cha Yesu juu ya hali ya mtu yeyote. Ila imenipasa, na nimechagua kukupenda katika tendo na katika kweli. Sitakudharau wala kukupuuza. Nitakujali wewe na utu wako; ni msingi wa heshima na uwana wa Mungu

  Mhina.
  Hongera sana my enlightened brother. Mambo unayoyaeleza yako wazi mno, lakini bado yanahitaji enlightenment, kwasababu mioyo mingi imejawa na aina nyingine ya mafundisho.

  Aina hizi za mafundisho ni kikwazo cha ufahamu kufunguka ILI MTU AWEKWE HURU APATE KUFELLOWSHIP NA MUNGU. Ni walio huru pekee wanaoweza ku-fellowship na Mungu.

  Endelea tu ndugu MHINA kutupia kweli hapa, maana wengi wanapokea kimyakimya na kuwa huru zaidi na zaidi. You are blessed and you are being a blessing to us.

  Asante Mhina.

  Asante SG, asanteni wote.

 255. * UPENDO WA MUNGU WA KUTIMIZA SHERIA….SIO ULE UPENDO WA WANADAMU. Watu wengi hufikiri kua, ule upendo wa kawaida wa kibinadamu, ndio ule upendo wa Mungu, uliokamilishwa ndani yetu ili kutupa ujasiri katika siku ya hukumu, lakini hilo sio kweli. Ule upendo wa Mungu, ulio ndani ya Yesu kristo, unaotukamilisha, ni tofauti kabisa na ule upendo wa kibinadamu tunaoujua sisi. Upendo wa Yesu, (yale mafundisho yake) watoka kwa Mungu, kwa kua, Mungu ndiye aliyetupenda sisi na kutupa “HUO UPENDO WAKE”…ndio maana pia unakamilisha sheria zake zote. Tazama Biblia inasema hivi” KWA KUA, KATIKA HILI PENDO LIMEKAMILISHWA KWETU ILI ” TUWE NA UJASIRI KATIKA SIKU YA HUKUMU KWA KUA, KAMA YEYE ALIVYO, NDIVYO TULIVYO NA SISI ULIMWENGUNI HUMU. Soma(1Yoh 4:17). Tukiwa na upendo huu wa Mungu ulio ndani ya Yesu kristo pekee mioyoni mwetu, basi itakua hata yale maneno yetu na matendo yetu, vitalingana na kile “TUNACHOKIAMINI”….Ndio maana bwana Yesu akasema “Mdomo hunena yale yaujazayo moyo. Soma(Mathayo 12:34). Katika upendo huu, haiwezekani tena kwa mtu kuvunja zile sheria (amri) za Mungu ndani ya huyu Bwana wa sabato kama: kuiba, kuzini, kusema uongo, kuabudu sanamu nk. Kwanini?….KWA MAANA HUKO NDIKO KUMPENDA MUNGU, YAANI TUZISHIKE AMRI ZAKE. Soma(1Yoh5:3)….na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwokozi kwa Baba, > Yesu kristo mwenye “HAKI”….naye ndiye “KIPATANISHO” Kwa dhambi zetu, wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. Na katika hili twajua ya kua tumemjua yeye, ikiwa “TUTASHIKA AMRI ZAKE”. Soma(1Yoh2:1-3). Lakini tunaona kwa upande mwingine, ule upendo wa kawaida wa kibinadamu, unatoka haswa kwenye mawazo ya hao wanadamu wenyewe na shetani. Kwanini?…kwa sababu wao, hawakiri kua Yesu ni Mwana wa Mungu aliyekuja katika mwili, pia hawashiki amri za Mungu za kweli, wala ile “KWELI” haimo ndani yao. Wao hua, wanafanya usawazo wa sawa kati ya sheria za Mungu jinsi ya kuzifuata na ile neema ya Mungu jinsi ya kuipokea, na wakati ikiwa kwa neema haiwezi tena kua kwa sheria, au basi neema isingepaswa kuitwa “NEEMA”!!!!. (Rumi 11:6). Pia wao hufikiri kua, ule upendo wao wa kibinadamu ni sawa tu, na upendo wa Mungu tulioupokea ndani ya Yesu kristo, ndio maana kama bwana siyi huko juu, anaona kua, kama swala ni upendo basi kila mtu anao, Pia kama swala ni imani tu, basi kila mtu anayo…jambo ambalo sio kweli, tena ni vitu tofauti kabisa.

 256. Wapendwa, nawasalimu nyote katika Kristo. Nawashukuru sana kwa michango yenu
  @ Chemo
  Pole sana rafiki yangu. Kuna kipindi Yesu alinena maneno ambayo baadhi ya wanafunzi wake nje ya wale 12, waliondoka na hawakurudi tena. Kuna walimu wa dini ambao na wao hawakumwelewa Kristo. Walimkasirikia!! Wakamwita ana pepo!! Walimsusa!! Kimsingi, walifanya yote ambayo yangeonekana kuipinga kazi yake na hata kuchafua CV ya Masihi. Alikuwa ni Ibilisi aliyekuwa akifanya kazi ndani yao!! Yesu aliwafahamu vyema, akawaambia “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”- Yohana 8:44. Lakini walionekana kulalamika sana kuwa na wao walikuwa ni wacha Mungu. Walidai kuwa, na wao ni watoto wa Mungu. “Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu, mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, nami nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma” Yohana 8:42.
  Si rahisi kuyavumulia maneno ya KWELI ndugu yangu Chemo. Maneno yanayotoka kwa Mungu, huwa ni machungu sana. Yanaudhi, yanakera, yanatia kichefuchefu na kimsingi, huwa hayapendwi na wana wa yule adui isipokuwa wa NURU tu. Muda fulani ulipofika, Yesu alibaki mwenyewe, mitume nao walibaki walibaki wenyewe. Siyi sioni ajabu kususwa na watu kama wewe. Na siyo wewe tu. Wapo wengi sana waliofanya hivyo. Haya ni baadhi tu ya alama zinazonionesha kuwa, niko kwenye barabara sahihi. Barabara aliyoipitia Kristo na mitume wake. Nami kwa imani na ujasiri mkubwa, nasonga mbele. Maana hii siyo kazi yangu, bali ni kazi ya YEYE aliyenituma –Kristo. Kwa kuusema ukweli wa Biblia, najua kuwa kuna watu ninaowakera na kuwaudhi sana. La kuwafanyia sina. Ninawaombea tu kwa Mungu watubu kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema. Hata wewe nakuombea pia!! Ubarikiwe sana.

  @Mhina
  Mimi ni mkristo. Nampenda Kristo kwa mujibu wa Yohana 15:14. Naiamini sana Biblia maana ndiyo msingi wa imani yangu. Nakifundisha kile choote kinachofundishwa na Biblia. Shida iliyopo rafiki yangu Mhina, ni mapokeo yaliyoshamiri miongoni mwa wapendwa wetu. Tatizo ndilo hilo. Jaribu kufunguka zaidi ujifunze kwa taratibu lakini kwa uhakika, utagundua mambo mengi. Mtafute Mungu maadamu anapatikana!! Mwite maadamu yu karibu… Kama kweli umeamua kuwa mkristo, kuwa mkristo kwelikweli rafiki yangu. Ni hasara kubwa sana kama utaikosa mbingu na huku ulijinyima baadhi ya anasa za dunia kwa kujiita mkristo!! Ni hasara iliyoje!! Ukiamua kuwa mpagani, kuwa mpagani hasa ili uifaidi dunia. Ukiamua kuwa mkristo, kuwa mkristo haswaa!! Na kila upande una hasara na faida zake. Nakupendekezea upande wa kuwa mkristo haswaa, maana huko kunalipa sana. Hautajuta endapo utadhamiria kuwa mkristo haswaa!
  Ubarikiwe

  @ Wengine wanaSG
  Habari za Sheria/Torati na Amri Kumi nilizitofautisha vizuri-rejeeni kwenye mchango wa tarehe 06. Januari mwaka huu (M. Siyi says: 06/01/2015 at 3:46 PM) . Niliatarajia watu wangetoa mchango kinzani kwa kukipinga kile nilichokisema kuwa hakiko sahihi badala ya kulalamika tu. Shida ninayoiona kwa wengi wetu, ni kung’ang’ania matakwa yetu ambayo kimsingi Mungu hakubaliani nayo. Hakuna atakayeuona ufalme wa Mungu kwa kuimbiana liturujia isipokuwa kwa kuyasoma Maandiko!! Na niwatie moyo kuwa, siku hizi hakuna cha teolojia wala ukasisi. Kila kitu kiko wazi. Hata wewe unawea kusoma lugha yoyote ya asili ya Biblia kwenye Agano la Kale na Jipya, ukaelewa maana halisi ya kile kilichokuwa kimekusudiwa na aya husika. Hakuna kudanganyana eti mimi ni mchungaji nakijua zaidi kiebrania na kigiriki kuliko niyi wengine. Walimu wengi wa uongo, wanatumia sana hii njia kuwahadaa watu. Ukiwa mjanja (mfuatiliaji wa mambo), hutadanganyika kabisa. Lakini ukiwa mvivu, utaendelea kulishwa unga wa ndele na hatima yake, ni uangamivu tu.
  Nawaombea nyote.
  Siyi

 257. SIRI YA WOKOVU NA TORATI NI HII
  WARUMI 8:3-4
  “MAANA YALE YASIYOWEZEKANA KWA SHERIA, KWA VILE ILIVYOKUWA DHAIFU KWA SABABU YA MWILI, MUNGU KWA KUMTUMA MWANAWE MWENYEWE KATIKA MFANO WA MWILI ULIO WA DHAMBI, NA KWA SABABU YA DHAMBI ALIIHUKUMU DHAMBI KATIKA MWILI; ILI MAAGIZO YA TORATI YATIMIZWE NDANI YETU SISI,TUSIOENENDA KWA KUFUATA MAMBO YA MWILI, BALI MAMBO YA ROHO.”

 258. .1 YOHANA 5:3
  “KWA MAANA HUKU NDIKO KUMPENDA MUNGU KWAMBA TUZISHIKE AMRI ZAKE; WALA AMRI ZAKE SI NZITO”

 259. Tumsifu yesu kristo, bwn siyi, nimekufuatilia sana ktk michango yako mingi, tatizo lako ndugu yangu wewe, uamini kile biblia inachofundisha….sidhani kama wewe ni kweli ni mkristo, napata wasiwasi sana kuamini hivyo, lakini usijali…isipokua unatakiwa uwe ni mtu wa kujifunza na kupiga hatua, usikubali kubaki sehemu moja bila ya kupata muafaka wa rohoni mwako. Mimi sina ya kuchangia maana mengi yamekwisha fafanuliwa kwa njia moja au nyingine. Ubarikiwe.

 260. Asante sana ndugu Siyi. Ninasalia tu na mtazamo wangu, mara tu baada ya kuufahamu moyo wako.
  Endelea kwa huru wote!

  Kwa wengine
  Biblia imesema wazi kwamba yodi moja ya Torati haitaondoshwa hata itimie, tena mbingu na nchi vitaondoka, lakini Torati yote ni sharti itimizwe ili mtu aweze kuhesabiwa haki na Mungu.

  Kwa wale wanaoiamini biblia nzima, Rumi 10:4 Kristo ndiye mwisho wa sheria kwa ajili ya kuhesabiwa haki kwa kila aaminiye.

  Kwahiyo, Torati ikibidi kutimizwa ni lazima itimizwe yote, yeye asiyeitimiza ni mdeni, na amelaaniwa. Nafikiri ndiyo msingi wa maada.

  Kwahiyo kwa hao wasioitumainia sheria kuhesabiwa haki, bali wanaamini kule kuhesibiwa haki ya Mungu, kulikokamilishwa na Kristo, kwao hao Torati imetimizwa na Yesu. Maana alipofufuka alisema mwenyewe kwamba ilimpasa yampate yote ambayo aliandikiwa katika Torati, Manabii na Zaburi; alipokuwa akibatizwa alimwambia Yohana kwamba imetupasa kuitimiza haki yote.

  Tuendelee kutafakali!

 261. Ndugu Chemo,
  Pole sana rafiki yangu.
  Kwanza, ninaamini kuwa vicheko vipo vinavyotokana na kufurahishwa na vile vinavyotokana na vituko avifanyavyo mtu!! Ukiona mtu anakucheka, ni vyema ukajiuliza, ‘anacheka juu ya hicho nilichosema, au ananicheka mimi mwenyewe’? Hata kama ukiwa jukwaani, usifikiri kuwa watu wengine watacheka kwa sababu umeongea mazuri ya kufurahisha, hapana, wengine watakucheka tu kwa sababu ya mambo ya ajabu unayoyafanya ambayo kimsingi hawakutarajia!! Hivyo kuna uwezekanano wa watu kulaugh at you au kulaugh with you!! Inabidi uwe makini na hizo dhana mbili rafiki yangu!!
  Pili, kama kuna sehemu nilionekana kujiinua sana, nisamehe bure. Ni udhaifu tu wa kibinadamu. Hata mimi sikujua kama hilo nalo la kujiinua, lipo kwangu!! Siyi sina uelewa mkubwa kiviiile!! Bado ni mwanafunzi wa Biblia tu. Nisamehe tu rafiki yangu kama nimekukwaza!! Sipendi sana kukwaza watu, japo walio wengi, ukimwambia madhaifu yake, maovu yake, upotovu wake, n.k. huishia kukasirika!! Tuombeane sana!!
  Tatu, ukisema kuwa hutajibizana na mimi tena, bado ni jambo jema tu. Maana kila mtu yuko huru!! Ila ninachokiona mimi, ni kuishiwa hoja. Ukikosa cha kusema, sababu ya kunyamaza huwa haikosekani!! Pole kwa kuishiwa ya kusema hapa SG. Kimsingi, inabidi ujifunze vizuri habari za sheria, torati na amri. Unachanganya sana mambo rafiki yangu. Unaweza kuwa na uelewa mkubwa wa mambo mengine, lakini hili la sheria, amri na torati, bado una safari ndefu ya kwenda.
  Nne, nimekuona unajaribu sana kutofautisha AKILI na ROHO!! Na kwamba kuna mambo ya kutumia akili na mengine ya kutumia roho tu. Nakupa changamoto nyingine, nenda kajifunze habari za AKILI na ROHO with an open mind. Pls, don’t learn with pre-conceived ideas za mafundisho yenu ya dini!! Nenda kama hujawahi kusikia habari za roho na akili kwa mujibu wa Biblia.
  Tano, uwe makini katika maisha yako ya imani. Shetani hachezi na nafsi za watu. Bali anacheza na akili (mind) zao!! Kwa maneno mengine, dini siyo maluweluwe rafiki yangu. Dini/imani ni kuwa na true & clear understanding ya hicho unachokiamini!! Zaidi ya hapo, ni spiritualism!
  Sita, mimi Siyi sitakuchunia ukiamua kuniuliza lolote kama ninalifahamu. Nitakwambia tu. Kwa hiyo ukiwa na lolote la kuniuliza, wewe lete tu. Sina kinyongo na mtu. Sina uadui na mtu. Ninawapenda watu wote isipokuwa kuwaamini tu. Ninayemwamini ni mmoja tu –Kristo aliye Bwana! Nakutakia maisha mema ya kumtafuta Mungu!
  Neema ya bwana ikufunike
  Siyi

 262. Chemo & Lwembe,
  Siku ile nimejibu kimakosa badala ya kumwelekezea Lwembe, nikamwelekezea Chemo!!! Duuu hiyo nayo kali ya mwaka 2015!! Mniwie radhi wajoli. Nashukuru meseji ilifika.
  Sasa, naomba niwajumuishe nyote kwenye pachiko hili. Nimesoma majibu yenu nyote wawili. Kwa njisi nilivyowaelewa (kwa vile mmezungumza kitu kilekile), ni kwamba, Sheria/Torati yote iliyobaki kwa sasa, ni upendo kwa jirani; jambo ambalo ni kweli kabisa. Amri ya kwanza na ya pili ya kumpenda Mungu na jirani (amri ya 1-10) siku hizi katika Agano Jipya, hazipo!! Maana ni torati ile, japo hata hiyo torati yenyewe, hamuielewi!! Na under ignorance, mnaifanya Amri ya pili iwe Torati/Sheria!! Mnapiga sebene tu!! Ndiyo maana baadhi yenu wamekimbia hata hawataki kujibu maswali yangu licha ya kuwauliza sana. Walijua walipokuwa wamechichanganya!! Nashangaa ninyi ndugu zangu, mmekomaa na ng’hinda huku mkidhani hamsikiki kumbe inapiga kelele kila mtaa mnaopita kuwa ninyi ni mafedhuli “ …watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo” –Yuda 4!! Mmekomaa kudanganya watu hapa mtandaoni!! Msikasirike!! Ngoja niwaambie marafiki zangu!!
  Naomba niwape homework. Sitaki muwe na kazi kubwa sana. Nendeni katika Agano Jipya tu. Lugha ya Agano Jipya, imetumia neno lilelile moja (japo kwa maumbo tofauti kidogo) kwa maneno –TORATI na SHERIA -nomos/nomou/nomon) likiwa na maana ya sheria/torati za kafara, maadili ya jamii za kiisrael, afya, n.k.!! Sheria au torati ambazo kimsingi zilikuwa msaidizi wa mkurugenzi mkuu wa katiba ya Mungu –Ten Commandments. Ilikuwa hivi, mtu akitaka kuishi bila ya kuvunja sheria/torati hizo, ilikuwa ni kumpenda jirani yake kwanza kama anavyojipenda yeye. Kutomtendea mabaya ndugu yake. Hali kadhalika, ukiangalia kwenye Agano Jipya hilohilo, neno lililotumika kwenye Commandments -amri kumi za Mungu ni entolas. Kwa hili ilikuwa hivi, ukitaka kuishi bila kumkosea Mungu, mtu alipaswa kuishi sawasawa na torati/sheria na amri. Kimsingi alipaswa kuishi kwa kuzifuata zote. Na vyote hivi, vilijengwa kwenye msingi mmoja tu –UPENDO kwa Mungu na mwanadamu mwenzio. Sasa, fuatilieni muone wenyewe kama kuna uhusiano wa hicho mnachong’ang’ania kati ya nomos na entolas kuhusu utimilifu wa torati/sheria vs utimilifu wa Amri. Ni kipi kilichotuleta kwa Kristo? Ni nomos au entolas?? Jaribuni kuangalia kama kuna uhusiano wowote ama la!! Nisiwatafunie kila kitu!! Otherwise, acheni kuwa wabishi ndugu zangu. Wenzenu huenda walilitambua hilo mapema ndiyo maana wakakaa kimya licha ya kuulizwa maswali mengi na Siyi!
  Someni Biblia kwa kutulia. Acheni kudanganyika vijana!! Acheni kufuata dini ya mwili. Fuateni dini ya rohoni!! Maana daima na siku zote, mwili na roho huvutana/hupingana!! Na walio wengi, wameitii miili (matakwa ya miili yao) na kuyafanya dini!! Kuna mambo ambayo miili yao under the influence of the devil, inayatamani na wao wamekosa hali ya kujimudu!! Hisia ndizo zinazotawala miili yao badala ya akili!! Mmepotea sana ila hamjui tu!!
  Nawaombea sana!!
  siyi

 263. Ndugu Siyi,

  Kumbe kicheko chako kilikuwa cha hila? Ndiyo maana C.K. Lwembe alikigundua mapema, nafikiri ni kwasababu anauzoefu nawe wa muda mrefu.

  Mimi, sina tena haja ya kuendelea na mabishano na wewe. Nilichokionyesha hapo kimeambatana na maandiko kabisa. Kama ulivyoamua kudharau na kujiona kwamba wewe ndiye ujuaye sana, usidhani mimi leo naweza kukubadilisha mtazamo wako. Itakuwa ni kuupoteza wakati tu.

  Na hata hauna haja ya kuijibu hiyo response yangu ya tarehe mbili, kwasababu mimi nia yangu ni kuzungumza na moyo, siyo akili; wewe akili zako ziko juu sana, ndo maana unatuonea huruma sisi/mimi nisiyezitumainia akili zangu mwenyewe, nimeamua kukubaliana na Mungu anavyosema tena waziwazi. Kwa hekima yako uliyoionyesha, hakuna namna ya kuendelea kujibu hoja zako. Ila kama yupo mwingine anayetamani kupokea moyoni; heart to heart, nitakuwa tayari kuendelea na mazungumzo naye. SG ni platform ya watu wengi zaidi ya Chemo na Siyi.

  Kuna namna nne ambazo mtu yeyote anafundisha anazitumia:

  1 Corinthians14:6

  But now, brethren, if I come to you speaking with tongues, what shall I profit you unless I speak to you either by revelation, by knowledge, by prophesying, or by doctrine

  1. Kwa mafundisho ya sheria
  2. Kwa kutoa Unabii
  3. Kwa kutoa ufahamu
  4. Kwa kufunuliwa (Kuwa na nuru ya neno binafsi kwa uwezo wa RM)

  Hiyo namna ya mafundisho ya sheria ndiyo namna ya chini kabisa. Wayahudi hawakuwa tayari kufunuliwa MUNGU na njia zake, na mawazo yake na asili yake, ndiyo maana wakapewa sheria. Sheria haimonyeshi kabisa kabisa asili ya Mungu. Mungu siyo slave master. Ila wanaotaka kuendelea kuwa chini ya utumwa, hawalazimishwi kuwa enlightened!

  Hiyo aina ya pili, ndio hao wengi wanaokimbilia kwa Mitume na Manabii ili waelezwe mambo yanayohusu maisha yao. Wamejaa kwenye makanisa mengi ya kiroho

  Hiyo ya tatu, ni wale wenye kujibidiisha katika kusoma; hususan, mambo yanayomhusu Mungu. Wakapata ufahamu kwa kusaidiwa na hayo mambo waliyoyasoma kutoka vyanzo mbalimbali kama vitabu vinavyoandikwa na waalimu wa neno na kutoka kwenye biblia.

  Lakini hiyo ya mwisho inatokana na hiyo ya tatu hapo, hawa ndio waliokuwa-enlightened, kwa kufahamu role ya RM katika kufundisha; wamachunguza, wametathmini, wametafakari, wamemuuliza maswali na kusubiri awajibu (maana Mungu anaongea, na kondoo wake huisikia sauti yake) na kupata moja kwa moja ndani ya mioyo yao ufunuo juu ya mambo ya Mungu. Ufunuo huu sio ndoto, maono na njozi bali ni moja kwa moja mtu ANAJUA kwamba; mfano kwa kupigwa kwake niliponywa, inanihusu mimi, na ni kweli, bila shaka yeyote, siku zote na katika mazingira yote.

  Kwa hiyo, hii level ya enlightenment, hailazimishiwi. You can not argue someone into a revelation. He/she must get it him/herself.

  Mtu yeyote anaweza kuamua kutoka katika level moja, kwenda level nyingine, na pia anaweza kuamua kubaki level ile ile aliyofikia tu, akaona inamtosha.

  Halafu, wewe shambulia tu maada, ukiona mtu anatia huruma kwa kushindwa kwake kushusha nondo, wewe mshushie uone kama atakataa. Mimi kama unayoyafundisha yata-bear witness in my heart, siko tayari kujiinua kwa kiburi cha yale ninayoyajua tu. Niko tayari ku-apprecieate dignity yako, na kupokea kabisa yale unayoyanena moyoni mwangu. Ila kama unatupia mambo ya akilini, sitakuwa tayari kuendelea na hayo.

  LETS GROW UP AND COMMUNICATE USING OUR HEARTS, HEART TO HEART. Tutumie akili kwa kazi yake ya kupokea mambo kutoka kwenye milango ya fahamu na kuyatafsiri, lakini mambo haya ya rohoni, ukitumia tu akili yako yanageuka kuwa upuuzi.

  Uwe na siku njema.

 264. Chemo,
  Inabidi ubadili mtazamo wako. Si kila wakati mtu anapocheka, huwa amefurahishwa na kitu/jambo. Mara nyingine hucheka tu baada ya kuona jambo Fulani likamshangaza na kustaajabu hasa akimwangalia huyo anayelifanya, analifanya kwa kujiamini kabisa!! Mshangao huo pia humfanya mtu acheke!! Sasa, wewe inabidi utumie akili, kama uliona nimecheka sana, halafu nikauliza maswali yaliyokutatiza, take your turn!! Sawa mzee??

  Suala la kumwabudu Mungu huenda sambasamba na matendo ya ibada!! Mf. Mtu anayetambikia, hufanya ibada za matambiko (matendo) kwa mizimu/wazee wake. Sasa unapomwabudu Mungu, unafanya nini kwa ajili ya kuonesha kuwa unamwabudu YEYE?? Ni kuwatendea wanadamu wengine mazuri tu au??? Mimi naona hapa ndipo mlipoachwa solemba!! Mwanadamu mmemfanya na yeye kuwa Mungu kiasi kwamba, lolote mmfanyialo mwanadamu, ndiyo ibada yenu kwa Mungu!! Mungu mmemuweka pembeni kabisa, Paulo John alisema haya!! Mimi niwashauri tu kama mna ibada zenye mitazamo ya namna hii, zitafakarini njia zenu kungali mapema. Mnaabudu msichokujua huku mkidai mwakijua!! Na hili ndilo tatizo maana kwa vile mwaamini kuwa mwakijua, huku hamkijui, itakuwa kazi kubwa sana kuwaelimisheni!! Ni gharama ya ujinga!!
  Nakuona pia una tatizo la siku za wiki. Na hili ndilo linalowasumbua sana ninyi watu wa j2. Mnafundishwa kabisa kuwa, Biblia na hata vitabu vya Historia, havijaweka bayana mfumo wa siku za wiki, saa, mwezi na hata mwaka wa tangu zamani!! Mmechanganyikiwa sana marafiki zangu!! Wasabato hatubahatishi niliwaambia tangu mwanzo!! Tuna utondoti wa kutosha kuhusu saa, siku, wiki, mwezi na hadi mwaka tangu zama za kale!! Tunayafahamu hayo kwa kina na marefu. Kama wewe/ninyi hamjui, hilo ni tatizo lenu!! Jitahidini kuyajua, vinginevyo, mtakufa kibudu kwa kukosa maarifa ya Mungu!! Wewe Chemo kama huyajui mambo ya saa, siku, wiki nk, kwa mwaka tangu zamani kiasi cha kukufanya ubweteke kiasi, hicho, jifunze kwetu!! Usijidai kujua wakati hujui!!
  Jambo lingine linalowafanya mpotee kirahisi, mnaamini kuwa, dini/imani ni MALUWELUWE tu!! Mtu akijazwa RM, anakuwa kwenye maluweluwe!! Akili ya kawaida inapotea!! Anakuwa hajielewi!! Ufahamu wa kutambua na kuchanganua mambo unapotea!! Hii ndiyo mnayoamini kuwa ni kazi ya RM. Hata huyo RM hammfahamu hata punje!! Mmeng’ang’ana RM, RM, RM, hadi mnatia huruma tu!! Hata sielewi niazie wapi kuwaelewesheni na kwa akili yenu ilivyo sasa, kwa kweli mnahitaji maombi!! Maombi mengi sana!! Yapo mengi tulishajadili hapa mtandaoni. Nikiyaleta kwenye mada kama hizi, itaonekana kama natoka nje ya mada!! Wewe chukua hatua binafsi. Nina mambo mengi ya kukupeni ili ufunguke!! Nitafute kwa siyimnn@yahoo.com tuzungumze huko!!
  Ngoja nikomee kwa sasa. Nitakuja kwenye mchango wako wa tarehe 2/01/2015.
  Hosea 4:6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

  Nakuombeeni sana.
  Siyi

 265. Nikushukuru sana ndugu Siyi kwa mwitikio wako. Naona umefurahi. Name nimefurahi kwa kufurahi kwako. Na kwa kunitakia nifunikwe sana na neema ya Kristo. Ninaihitaji sana, sana neema hiyo katika maisha yote. Mungu azidi kufunua neno lake ndani ya moyo wako ndugu yangu.

  Halafu nikushukuru sana ndugu C.K Lwembe kwa majumuisho yako. Nakubaliana na mtazamo wako kwa asilimia mia. Umejibu maswali yoote aliyouliza ndugu yangu Siyi, tena kwa kuonyesha kwamba maswali yake yalikwishajibiwa na maelezo ya pale juu. Mungu akubariki sana Lwembe.

  Lakini pia nipitie humohumo alimopita kaka Lwembe, kukazia zaidi.

  Maswali
  1. Je, leo tunaweza tusimwabudu Mungu na tukaabudu kitu kingine, ila tukawapenda sana wanadamu wenzetu, na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunampenda Mungu??? Zingatia; “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao” kutoka 20:4-5.
  2. Je, inawezekana tukawa na mungu mwingine, ila tukawapenda tu wanadamu wenzetu, na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunampenda Mungu??? Zingatia: “Usiwe na miungu mingine ila mimi” Kutoka 20:3

  Jibu
  Ukiupata huo upendo wa Mungu, mwitikio wako itakuwa ni kumsifu, kumtukuza na kumwinua kwa jinsi anavyostahili. Kwakuwa Mungu ni Roho, wale wamwabudua imewapasa kumwabudu katika Roho na Kweli. Kwahiyo upendo wa Mungu hauwezi kukufundisha kuabudu miungu mingine. Je, kumwabudu Mungu maana yake nini?

  Swali
  3. Je, tunaweza kukataa ishara/alama ya Mungu, ila tukawapenda wanadamu wenzetu, bado tutakuwa tunampenda Mungu?? Zingatia: “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase”. Kutoka 20;8

  Jibu
  Mungu NI PENDO; sit u kwamba anatupenda kwa kuona haya/aibu tu; bali kwasababu yeye mwenyewe ni pendo. Ukifunuliwa upendo wa Mungu, ukamwabudu yeye katika Roho na Kweli, unakuwa umekubaliana na kila hitaji la Mungu. Mtu asiye mwana, hawezi kumwabudu Mungu katika Roho na kweli. Hivyo, ni lazima kuzaliwa na Mungu kwanza, ndipo unaweza kumwabudu. Yesu ndiye Bwana wa Sabato. Yesu, ndiye utakaso, hekima ndiye haki, ndiye ukombozi (1Corinthians 1:30). Hivyo, kutakaswa kwa sabato amekwishakufanya mwenye nayo, yaani, huyo Bwana wa Sabato, YESU NI KILA KITU.

  Swali
  4. Je, tunaweza kuwa tunalitaja bure jina la Mungu, pengine kwa kumshukuru kwa sababu ya kupata ka-escrow, ila tukawapenda sana wanadamu wenzetu, bado tutakuwa tunampenda Mungu?? Zingatia; “Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure” Kutoka 20:7.

  Jibu
  Hahaha, you have a sense of humor! Kutaja bure jine la Mungu ni kutozaa matunda. Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, …(Galatia 5:22-23) na ndio linalihitajika kuzaliwa kwa mtu. Sasa ukiwa na upendo wa Mungu, tunda la Roho, litadhihirika. Utamanifest si upendo peke yake, bali na furaha na amani …
  Ukifunuliwa huu upendo wa Mungu, moyo wako utaendeshwa na upendo (your heart, and subsequently all your life will be driven by the live of God). Hautakuwa na capability nyingine nje ya huo upendo. Hata imani yako inatenda kazi kwa upendo. (Faith works by love).
  Nimalizie na mfano wa mwana mpotevu. (in points form) Luke 15:11-32
  • Mwana alidai kilichokuwa kinamwangukia katika mali ya baba yake, baba akampa akamruhusu kuondoka, kuwa huru
  • Mwana anatapanya mali kwa starehe
  • Dhiki inaikumba nchi, mwana anapata taabu, kazi hakuna, anapata kazi duni, anatamani kula chakula ambacho ni mabaki ya chakula cha nguruwe (imagine!)
  • Mwana anazingatia moyoni mwake, anakumbuka utambulisho wake. Anatengeneza formula ya kurudi kwa baba yake
  • Lakini baba, tangu siku ile alipomruhusu alikuwa na tabia ya kutazama njia ile aliyoiendea mwanaye, akisubiri kwa matarajio kwamba atarudi, akanunua kanzu na pete ya thamani
  • Mara, siku moja, kwa mbali, anamwona mtu aliyekondeana kwa taabu nyingi, amechoka, hatambuliki, ulimwengu umempiga kwelikweli.
  • Baba alimkimbilia, akamrukia shingoni, akambusubusu shingoni
  • Akawaagiza watumwa walete vile vitu alivyoviandaa kwa muda mrefu. Na kusherehekea kurejea kwa mwana aliyekuwa amepotea, aliyekuwa amekufa.
  Hii si habari ya mwana aliyepotea tu, ni habari ya baba mwema, mwenye unconditional love. Mwana aliporudi, hatumwoni baba akimtaka a account for the money he gave him. Hata sermon ya mwana ya kumtaka baba amfanye mmoja kati ya watumwa wake, baba hakuisikiliza. HAKUMTAKA AFANYE KITU CHOCHOTE ILI KUMWONYESHA BABA KWAMBA ANAMPENDA. Unauonaje upendo wa namna hii? Ni pendo la namna gani alilotupenda baba?

  Nahitimisha kwa kusema, kazi ya msalaba ni love story ya Mungu kwangu. Mungu hayuko busy na kunihesabia makosa na kuset moto wa jehanamu; MUNGU YUKO BUSY KUNIPENDA. Hiyo ndiyo jumla ya habari ya upendo wa Mungu.
  Mungu awabariki wote.

 266. Siyi,

  Acha uongo, mtu aliyeyafurahia maelezo mazuri na yaliyo wazi kama hayo ya Chemo, hawezi kuwa na kicheko wala maswali kama uliyoyauliza!

  Maswali unayoyauliza ndiyo yanayoudhihirisha uongo wako, hiyo furaha uliyonayo inayoambatana na kicheko, haiendani na maswali yako, maana hayo yanaonesha HUJAELEWA CHOCHOTE ktk hayo yote aliyoyaleta Chemo, sasa ni kipi kilichokufurahisha?!!!

  CHEMO:
  “”Nitoe mtazamo wangu juu ya kumpenda Mungu, hiyo amri ya kwanza. Tunampenda Mungu kwa sababu yeye ndiye anayetupenda kwanza. Hatufanyi bidii ya kumpenda Mungu kwa kutumia akili zetu. Iko namna ya kumpenda Mungu inayotokana na ufahamu kwamba yeye ndiye aliyenipenda kwanza. Kwahiyo, kwa upendo wake ule alionipendea, na mimi najifunza na hatimaye nautumia huo upendo wake kumpenda yeye (1 John 4:19). Ukitaka kutumia upendo wa kwako kumpendea Mungu utakuwa worn out. … Hata upendo nao unatoka kwake, siyo wa kwetu.””

  SIYI:
  “” 1. Je, leo tunaweza tusimwabudu Mungu na tukaabudu kitu kingine, ila tukawapenda sana wanadamu wenzetu, na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunampenda Mungu??? Zingatia; “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao” kutoka 20:4-5.””

  Kama Upendo, huo umbao tunawapenda sana wanadamu wenzetu, si wetu bali unatoka kwa Mungu, sasa utapata wapi huo upendo wa kuwapendea hao wanadamu wenzako iwapo haumuabudu Mungu bali hivyo vitu vingine? Ndio maana nasema wewe hujaelewa chochote ktk hayo aliyoyaleta Chemo!

  Halafu ktk na. 2, unauliza tena eti uwe unaabudu miungu, halafu kwa kuabudu kwako hiyo miungu ukawapenda wanadamu wenzako, ndio uwe unampenda Mungu???!!! Maswali kama haya ni ya mtu aliyechanganyikiwa; umeambiwa upendo unatoka kwa Mungu na si miungu lakini kwa kukosa ufahamu, UNAFIKI unauita Upendo!!!!

  Sikiliza Siyi, RM ndiye utu wa ndani wa mtu, naye RM ni Neno la Mungu ktk Ukamilifu wake na si doctrines uchwala zinazojiwakilisha kama Neno la Mungu! Bila RM hao unaosema wanadamu wenzako, wanaishia kuwa beasts tu, hao Hayawani!!! Tazama, hayo majeshi yaliyoko huko Kongo na kwingineko ni ya wapagani watupu? Wakristo wamo wengi sana tu, na ktk ujumla wao ndio hao wanaowabaka wanawake na vibinti na uchafu mwingine; mama anaye nyonyesha ananyang’anywa mtoto na kutupwa huko kando ili wanajeshi hao wajifurahishe, ni chini zaidi hata ya hao hayawani!!! Hiyo ndio kazi ya dini!

  Pia umeuliza swali lako kipenzi, yaani ni kama yule kipofu aliyefumbuliwa macho kwa sekunde akamuona tembo; ndipo watu wanaposimulia kuhusu shingo nyembamba ya twiga, yeye kwa furaha kabisa huuliza, “Nyembamba kama ya tembo?” Nakuona nawe ulipofumbuliwa macho uliiona hiyo Amri ktk Kut 20:8 ihusuyo sabato!

  Sabato kaka hakuna anayeivunja! Kuivunja sabato ni kufanya kazi siku saba!!!! Sabato ya Kiyahudi ni kwa taifa lao kulingana na walivyozihesabu siku kwa kadiri ya ufahamu wa siku waliotoka nao huko Misri walikozaliwa na kukulia maisha yao yooote! Kuyalazimisha Maandiko yaseme jambo ambalo Mungu hajataka kulisema ni UONGO wa hali ya juu, tena wenye Hasara ya juu sana!

  Nimewahi kukuambia kuwa usijisumbue na mambo ambayo Mungu ameyaficha, lakini naona huna unalolielewa! Hebu niambie siku ya kwanza mpaka ya tatu zilikuwa ni siku za masaa mangapi? Maana ni ktk siku ya nne ndipo majira tuliyonayo yameanza, kwahiyo kama umetengeneza hesabu za siku kutoka hizo siku saba za Mwanzo ukadhania zinafanana na hizi za leo, huo ndio uongo wenyewe, unaotokana na kuvamia mambo!!!

  Pia hiyo Amri yako kipenzi ni sehemu ya Torati, hiyo Sheria, inayokomea kwa Kristo. Basi unapovuka kuingia ktk Nchi Mpya ya Agano Jipya, hilo la Damu ya Bwana wa Sabato, tambua kwamba siku HAIWEZI kuwa juu ya Mwenye siku! Mwenye siku ndiye siku yenyewe kaka; basi ukisikia “Siku ya Bwana”, Rev 1:10 ” I was in the Spirit on the Lord’s day, …” jua ndio hivyo beat limebadilika, Amka wewe usinziaye uyaone mambo mapya; unataka kununua vitu kwa shilingi mia ya mmasai, utaitiwa “mwiiiiiiizi!” Na jinsi watu walivyo na usongo wa kuzikosa pesa za escrow, basi watakupiga mawe mpaka ufe, maana wote walio nje ya Kristo, Sheria inaendelea nao, watake wasitake!!!!

  Kwa kifupi maswali yako yote ni ya mtu asiyejazwa RM; na kwa vile Maandiko yote ni INSPIRED, basi hata kuyaelewa yanasema nini ni lazima nawe uwe INSPIRED, ndiko huko kujazwa RM, nje ya hapo, ndio kama hivi, tunatwanga maji ndani ya kinu! Ngoja nikunukulie tena alichokuonesha Chemo:
  “” Galatia 5:14 “Maana torati YOTE imekamilika neno moja, nalo ni hili, “Umpende jirani yako, kama nafsi yako” (Msisitizo ni wangu)””
  UNAAMBIWA umpende jirani yako na si siku ya sabato, nenda kautafute Upendo wa Mungu ulipo kwanza ndipo mambo hayo yanayoikamilisha Torati yatakuwa Halisi kwako, vinginevyo utaendelea kutembea gizani!!!!!!

  Basi ukitaka kupona jiondoe ktk ule ukaidi wa “Tumfuate nani, Yesu Mwalimu au mitume wanafunzi?” maana kutoka ukaidi huo ndio Mungu ameifunga milango ya ufahamu, kiasi kwamba mtu niliyekuona hapa kwenye blog kwa zaidi ya miaka…, halafu leo unauliza maswali ya jinsi ya mpagani asiye zijua hata Sheria, inashangaza na kusikitisha saaana; utaabuduje miungu halafu uwe na upendo??????

  Siyi, aibu hii! Au ndiko kule kunyang’anywa mpaka kidogo ulicho nacho kumekutimilia?????

  Duh! Inabidi ukarudishiwe nyota huko kwa wenye kuzirudisha, maana huku kwenye Wokovu HAUPO kabisa, basi ni bora ujiendee hata huko kwa warudisha nyota kwani it doesn’t make one bit of a difference!!!!

  Gbu my brother!!

 267. Chemo,
  Nashukuru sana kwanza kwa kuyaelewa maswali yangu na majibu yako pia. Kimsingi umenifurahisha sana. Nimecheka sana. Ila hatimaye nikawa na vimaswali vidogo vichache hivi, ambavyo nitakuomba uvijibu, ndipo nitoe mwitiko wangu wa jumla. Je, unaweza kuvijibu pia licha ya wengine kukaa kimya!! Maana naona kama wamesusa maswali yangu. Viswali vyenywe vinavyohitaji ufafanuzi, ni hivi hapa;
  1. Je, leo tunaweza tusimwabudu Mungu na tukaabudu kitu kingine, ila tukawapenda sana wanadamu wenzetu, na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunampenda Mungu??? Zingatia; “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao” kutoka 20:4-5.

  2. Je, inawezekana tukawa na mungu mwingine, ila tukawapenda tu wanadamu wenzetu, na kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunampenda Mungu??? Zingatia: “Usiwe na miungu mingine ila mimi” Kutoka 20:3.

  3. Je, tunaweza kukataa ishara/alama ya Mungu, ila tukawapenda wanadamu wenzetu, bado tutakuwa tunampenda Mungu?? Zingatia: “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase”. Kutoka 20;8

  4. Je, tunaweza kuwa tunalitaja bure jina la Mungu, pengine kwa kumshukuru kwa sababu ya kupata ka-escrow, ila tukawapenda sana wanadamu wenzetu, bado tutakuwa tunampenda Mungu?? Zingatia; “Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure” Kutoka 20:7.

  Neema ya Bwana ikufunike Chemo.
  Nakungoja sana.
  Siyi

 268. Naomba kuongezea kidogo;

  Galatia 5:14
  Maana torati YOTE imekamilika neno moja, nalo ni hili, “Umpende jirani yako, kama nafsi yako” (Msisitizo ni wangu)

  Hapa mwandishi anasema torati Yote imekamilika katika neno moja la kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Ili ku-support zaidi maelezo kwamba zile sheria mbili (kama anavyoziita Siyi) zimejumuishwa na zinakamilika katika hii moja.

  Asanteni

 269. Ahaa, nimeelewa sasa swali lako Ndugu Siyi. Unauliza, ili kudhihirisha upendo wetu kwa Mungu inatupasa kufanya nini? What works should we do?

  Jibu
  Yonana 14:15-16
  Mkinipenda, mtazishika amri zangu, nami nitamwomba Baba, naye atawapa mfariji mwingine ambaye ata kaa kwenu daima.

  Lakini, amri zake ni zipi?

  Yohana 13:34
  Amri mpya nawapa, ya kwamba mpendane, KAMA VILE MIMI NILIVYOWAPENDA NINYI, NANYI PIA MPENDANE, Hivyo watu wote watatambua kuwa mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. (msisitizo ni wangu). Na
  Yohana 15:12
  Amri yangu NDIYO HII, mpendana KAMA NILIVYOWAPENDA NINYI…. HAKUNA ALIYE NA UPENDO MWINGI KAMA HUU, WA MTU KUUTOA UHAI WAKE KWAAJILI YA RAFIKI ZAKE. (msisitizo ni wangu)

  Yesu alitupendaje? Aliutoa uhai wake kwaajili ya wenye dhambi. Yaani, vibaka, wanyang’anyi, wevi, wasengenyaji na hata waliomuuwa. Sisi hatuhitaji kufa msalabani kama yeye alivyokufa msalabani, bali imetupasa kuwachukulia wengine kuwa bora kuliko sisi wenyewe.
  Mfano, Yesu alipowaosha wanafunzi wake miguu alikuwa anadhihirisha jinsi inavyotupasa kuwachukulia wengine. Aliwaambia wanafunzi wake sababu ya yeye kuwaosha miguu. Lakini kule kuwaosha miguu ilikuwa ni mfano tu wa kuonyesha wengine upendo.
  Hizi amri zilizokuwa mbili hapo kale, sasa zimefanywa moja; maana alisisitiza kwamba “greater love than this has any man”. Hivyo kumbe, hakuna upendo mkuu kuliko huo wa Mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya rafiki zake. Apendaye kwa jinsi hiyo amekamilisha neno la Mungu.

  Pia unaweza kusoma zaidi 2 Yohana 1:5-6
  Na sasa mama, nakuomba, si kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tokea mwanzo, kwampa tupendane. Na huu ndio upendo: tuenende kwa kuzifuata amri zake. Hii ndiyo ile amri, kama mlivyosikia tangu mwanzo kwamba mwenende katika hiyo.
  Kwa hiyo kumpenda kwetu Mungu kunapitia kuwapenda wengine kama Yesu alivyotupenda sisi. Yesu alituonyesha mfano. Kwa namna ya mfano wake, inawezekana kuwapenda wengine.
  Upendo wa Yesu hauna masharti (unconditional love), aliupenda ulimwengu wote, bila kujali kama wao wataurudisha upendo huo. Alitupenda upeo, lakini lazima uweze kulitafakari sana neno la Mungu, linalohusu jinsi alivyotupenda yeye, hata utakapopata kujua ndani ya moyo wako (yaani kupata ufunuo wa upendo huo) ndipo utakapou-appreciate, na kuutumia huo upendo ulioupokea moyoni mwako kuwapenda wengine.
  Ili kudhihirisha kwamba sisi ni wana wa Mungu imetupasa pia kuwapenda wengine bila kuzingatia vigezo na masharti yeyote.
  Kwa kuwa twawezaje kumpenda Mungu tusiyemuona endapo hatuwapendi jiriani zetu tunaowaona? Ni kupitia hawa tunaowaona ndipo tunampenda Mungu kwa mioyo, kwa nguvu, kwa akili, na kwa nafsi zetu zote.
  Na tunakuwa tumelishika neno lake hilo, la kupendana, na pendo la Mungu linakuwa limekamilika kwetu kweli kweli. Hakuna namna nyingine ya kuudhihirisha upendo wetu kwa Mungu.

  Karibuni na wengine mchangie, ili tujifunze toka kwenu.

  Asanteni sana; mbarikiwe.

 270. Ndugu Chemo,
  Nashukuru sana kwa maelezo yako. Kimsingi umeeleza vizuri kuwa Mungu ndiye aliyetupenda sisi kwanza. Na kwa kutambua pendo lake kwetu, ndio maana na sisi tunajikuta tunampenda tu. Sheria ya pili wachangiaji hasa mtoa somo, wameieleza vizuri sana sana. Hata kama kuna madhaifu, basi ni machache. Pengine kwa Wasabato, usishangae fundisho hilo ukalikuta linafundishwa vilevile kwenye hiyo amri ya pili ya mpende jirani kama nafsi yako. Hivyo basi, sina shida saaaana na maelezo/ufafanuzi wenu wa sheria/torati ya pili.
  Shida yangu ambayo mpaka sasa naona bado mnaikwepa kuijibu ni ile ya torati/sheria ya kwanza ya mpende Mungu wako kwa nguvu, akili n…… Bado naomba sana, sana na sijui hatuelewani wapi!! Tafadhali, unaweza kutumia ufafanuzi wenu wa sheria ya pili kufafanua sheria ya kwanza?? Tunaishikaje amri ya kwanza kama matokeo ya msukumo wa moyoni?? Hebu leta ufafanuzi kwa mukitadha wa ufafanuzi wenu wa amri ya pili. Kuna kitu mnakikwepa hapo!! Msella, Magreth, Sungura, John Paulo, Chemo, Lwembe, Seleli (mwana mpotevu), Padael, Mwikabe, Orbi na wengine wengi, tafadhali, leteni maelezo yenye kukidhi haja. Nina imani maswali yangu yanaeleweka!! Mbona hamyajibu sawasawa??
  Ninawangoja sana!!
  Siyi

 271. Haleluya Orbi. Mungu akubariki sana kwa kuelezea vizuri sana juu ya nani mwenye haki kwa Mungu. Ni Kristo tu; aliyeishika sheria yote kikamilifu kabisa mpaka mwisho. Mimi, na wewe Orbi, tunapokea tu kwa imani ile haki ya Kristo. Na kwaajili hiyo tu Mungu anatukubali kama anavyomkubali Kristo, na anaridhishwa (pleased) nasi. Kama ilivyoandikwa, mwenye haki wangu ataishi kwa imani (Waebrania 10:38)…. na kwamba pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6)

  Matendo yanayofuata kusikia neno la Kristo ndiyo yanayokamilisha imani, maana yapo matendo ya sheria, ambayo unashurutishwa kuyafanya kupitia hilo agizo, na yapo matendo ya imani, ambayo unayafanya baada ya kukubaliana na lile neno ulilolisikia lililojaa moyoni mwako, unayafanya hayo kwa kupenda.

  Ndugu Siyi, 1 Timothy 1:8-10 KJV
  8. But we know that the law is good, if a man use it lawfully;
  9. Knowing this, that the law is not made for a RIGHTEOUS MAN, but for the LAWLESS and DISOBEDIENT, , for the UNGODLY and SINNERS, for UNHOLY AND PROFANE, for MURDERERS OF FATHERS AND MURDERERS OF MOTHERS, for MANSLAYERS,
  10. For WHOREMONGERS, for THEM THAT DEFILE THEMSELVES WITH MANKIND, for MENSTEALERS, for LIARS, for PERJURED PERSONS, and if there be any other thing that is contrary to sound doctrine. (Emphasis is mine)

  Kwahiyo, kwa mtu ambaye amezaliwa na Mungu, ana ROHO YA KRISTO NDANI YAKE, ambayo haitendi dhambi tena, inayo haki ya KRISTO, ninao ujasiri wa kusema kwamba torati ya Musa haina kazi kwake.

  Hauwezi kuwa na haki ya Mungu kama haujazaliwa na Mungu. Kazi ya torati ni kumhesabia mtu makosa, siyo kumhesabia mtu haki.

  Nitoe mtazamo wangu juu ya kumpenda Mungu, hiyo amri ya kwanza. Tunampenda Mungu kwa sababu yeye ndiye anayetupenda kwanza. Hatufanyi bidii ya kumpenda Mungu kwa kutumia akili zetu. Iko namna ya kumpenda Mungu inayotokana na ufahamu kwamba yeye ndiye aliyenipenda kwanza. Kwahiyo, kwa upendo wake ule alionipendea, na mimi najifunza na hatimaye nautumia huo upendo wake kumpenda yeye (1 John 4:19). Ukitaka kutumia upendo wa kwako kumpendea Mungu utakuwa worn out.

  Kwasababu ya uharibifu, kizazi cha wanadamu hakikuwa na kitu chochote cha kumfanyia Mungu, kinachompendeza. Hata upendo nao unatoka kwake, siyo wa kwetu.

  Asante

 272. Ndugu Orbi,
  Shalom. Sijui kama ulikuwa unajibu maswali yangu niliyoulizeni hapo juu. Lakini hata kama hukuwa unajibu, ngoja nikuelekezee wewe mwenyewe kuna sehemu umeniacha kwenye mchango wako. Nainukuu, “Matendo mema kwa sisi tuliokolewa ni kui hakikisha ile Imani hai iliyoko ndani mwetu…..Tunaionyesha Imani iliyotuokoa kwa wengine (Sio Mungu) kwamba Tumeokolewa!”
  Swali
  1. Je, unaamini kuwa mtu anapomkiri Kristo kuna hatua baada ya hapo –yaani mchakato wa kuukulia wokovu?
  2. Jibu lako kama ni ndiyo, je, tunaukulia huo wokovu kwa kuzitimiza zile amri mbili kuu au amri moja tu –ya mpende ndugu yako kama nafsi yako? Tunamuwekaje Mungu pembeni katika mchakato wa sisi kuukulia wokovu???
  3. Na kama jibu lako ni hapana (hakuna machakato wa kuukulia wokovu), ni sahihi tangu sasa tukaamini juu ya dhana ya ‘Once Saved Always Saved’??. Kwa maneno mengine, sisi tuliokolewa (kama msemavyo), hatuna haja tena ya kumpendeza Mungu (tunaweza kuishi tupendavyo), isipokuwa wanadamu wenzetu tu?

  Naomba sana, sana, sana, uje na majibu ya maswali haya. Nakungoja.
  Siyi

 273. John Paul,

  Nimeshukuru mno kwa maneno yako…. Nanukuu…”.Matendo mema tunayoyatenda ni matunda ya mabadiliko yanayotokana na utendaji au uhai wa ile imani katika Kristo Yesu iliyo ndani yetu.”

  Kwa kifupi hivyo ndivyo Injili (Habari Njema) Zinazoletwa na Injli ya Kristo zinavyosema. Hatukubaliki mbele za Mungu kwa matendo Mema yoyote yale….! Hata Agano la Kale Haikuwa hivyo……ni kutolifahamu Agano hilo….! Au kulisoma kwa macho ya kengeza….! Hakuna alilolifanya Abraham…..Daudi na wengineo wengi ili Mungu awakubali….behind the scene unaiona Neema ya Mungu juu ya watu aliowatumia….!

  Matendo mema kwa sisi tuliokolewa ni kui hakikisha ile Imani hai iliyoko ndani mwetu…..Tunaionyesha Imani iliyotuokoa kwa wengine (Sio Mungu) kwamba Tumeokolewa!

  Kama tutaingia mbinguni kwa ajili ya Matendo mema, basi mbinguni patakua mahali pa majigambo……maana nikikutana na watakatifu walioingia huko nina haki ya kuwauliza, Je ulifanyaje mwenzangu mpaka ukaingia huku? Jibu litakuwa mwenzako nilifunga sana….! Nilitoa sadaka sana…! Nilisaidia maskini…..! Niliacha kazi na kwenda kumtumikia Mungu…..! Neema na kazi ya Yesu msalabani itakuwa ni bure…! nGUVU NA ROHO MTAKATIFU ITAKUWA NI BURE…..

  NITAKAPOINGIA MBINGU ITAKUWA NI KWA NEEMA TU……NI KWA KAZI YA MSABALANI………NAPOWEZA KUISHINDA DHAMBI KATIKA MAISHA HAYA NI KWA NGUVU ZAKE….NA KWA NENO LAKE ALILONIPATIA……

  Mfano mzuri ni Kornelio….alifunga sana…..alitoa sadaka sana…..alitenda mema mengi mbele za wanadamu….na hata Mbingu ilitambua hivyo….LAKINI ILIBIDI APELEKEWE WOKOVU…….! ILIBIDI MBINGU ITUME MTU (PETRO) KUMSAIDIA MTENDA MEMA HUYU…..!

  Kwa kifupi matendo mema kwa Mkristo ni LAZIMA KABISA…..SI KWA AJILI YA KUOKOLEWA BALI KUUONYESHA WOKOVU WAKO…..!

  Tutasimama mbele za Mungu kwa HAKI ya Kristo ambayo ametupatia………tunamsogelea Mungu Kwa Haki ya Kristo………Upendo wa Kristo ndani yetu kama uko hai…..Utawapenda wasiostahili kupendeka…..Utawasemehe wasiostahili kusamehewa…Utachukuliana na watu wasiostahili kuchukuliana nao…..Utatawezesha kuvumilia magumu yasiyoweza kuvumilika….nk…NI KRISTO MWANZONI MWA WOKOVU……NI KRISTO NAPOTEMBEA KATIKA WOKOVU LEO……NI KRISTO NITAKAPOSIMAMA MBELE ZA MUNGU MWISHONI MWA MAISHA YANGU…….

 274. @ Magreth,
  Asante sana kwa pachiko lako refu la Kiingereza lenye ufafanuzi wa faiwa ya “kuitimiliza torati”. Nimekufuatilia vyema. Kimsingi umehitimisha vyema kuwa, kuwapenda wenzetu, ndio ukamilifu wa sheria. Na sheria katika Agano Jipya, ziko mbili tu. 1. Mpende Mungu wako… na 2. Mpende Jirani yako… Sijaona msimamo wa maelezo yako ya amri ya kwanza –mpende Mungu wako… Hiyo nayo unasemaje?? Au wamatifa hatuna haja ya kumpenda Mungu kama Wayahudi, isipokuwa kupendana sisi kwa sisi tu? Sitarajii unipachulie na kunipachikia tena maandishi ya mtu. Nitafurahi kukuona wewe mwenyewe kwa maneno yako. Nakungoja.
  @ Sungura,
  Kabla sijachangia chochote, hebu msaidie Msella kujibu maswali yangu hayo!!
  @. Chemo.
  Umesema kuwa, sheria ipo “4. Kwaajili ya wasiomjua Mungu (1 Timothy 1:8-10)”. Je, wanaomfahamu Mungu wao sheria haina kazi kwao?? Hebu tondoa tafadhari!!
  @ John Paul
  Nafikiri nisipokushukuru sana, sitakutendea haki rafiki yangu. Kongole kwakweli. Sasa niende kwenye hicho ulichokijibu. Hoja ya kwanza, umeijibu hivi, “Baada ya sheria kuondolewa kwenye vibao vya mawe (Agano la Kale) na kuandikwa katika mioyo (Agano jipya) Nielewavyo mimi sasa ni kwamba Matendo ya mwili HAYAKAMILISHI uchaji Mungu bali huwa ni MATOKEO YA MTU anayemcha Mungu. Mtu HAAGIZWI (Sheria) KUTENDA MEMA ndiyo awe amekamilisha imani yake bali Badiliko la Moyoni alilolipata (Wokovu) ndilo litazaa matendo mema”
  Kwa mshadidio wa maelezo ya Msela, nilivyokuelewa ni hivi;
  a. Ni kweli sheria katika Agano Jipya, imeandikwa ndani ya mioyo yetu. Nakubaliana na wewe kabisa.
  b. Ulipoanza kuniacha ni hapa, “Nielewavyo mimi sasa ni kwamba Matendo ya mwili HAYAKAMILISHI uchaji Mungu bali huwa ni MATOKEO YA MTU anayemcha Mungu”.
  Swali, kama matendo hayakamilishi imani ya mtu kwa Mungu wake, ni nini sasa kinachomfanya muumini aonekane amekamilika kwa Mungu wake? Au ni ile imani tu ya ndani ya moyo wake? Kumbuka Yakobo anasema imani isiyokuwa na matendo imekufa!! Hebu nisaidietafadhari!!
  c. Aidha umeendeea kusema kuwa, “Mtu HAAGIZWI (Sheria) KUTENDA MEMA ndiyo awe amekamilisha imani yake bali Badiliko la Moyoni alilolipata (Wokovu) ndilo litazaa matendo mema”

  Mwitiko
  Ni kweli kabisa. Swali unalopaswa kulijibu, ni hili; Kama imani inaweza isiwe na matokeo(matendo mema) yenye kuonesha ukamilifu wa imani ya mtu, bado imani hiyo yaweza kuendelea kuwa na sifa kweli ya kuwa hai? Kama sivyo, huoni kuwa imani na matendo ni pande mbili (head and tail) za shilingi moja??

  @ Kwa ujumla wenu (mliochangia)
  Kimsingi Msella alileta fundisho zuri sana la haki kwa imani. Na amefundisha vizuri sana kwa mujibu wa sheria ya pili katika Agano Jipya- sheria ya kumpenda jirani kama nafsi yako. Sheria ya kwanza, -ya mpende Mungu wako…. Hajaizungumzia kabisa. Na Paulo John ameiita kuwa ni torati ya Agano la Kale. Haipaswi kufuatwa. Kwa maneno mengine, amri ya 1-4 zilizokuwa kwenye mbao mbili za mawe, katika Agano Jipya, hazipo tena!! Au sivyo John?? Na kama sheria hizi mbili ni ufupisho wa ten commandments, ambazo kwa leo utimilifu wake unapaswa kuongozwa na upendo; Je, mbona hamjaeleza upendo wetu kwa Mungu katika Agano Jipya unapaswa kudhihirishwaje. Namuomba Msela na yeyote atakayechangia, agusie na sehemu hii ya amri ya kwanza ndani ya Agano Jipya!!
  Karibuni sana
  Siyi

 275. Mpendwa ktk Kristo Yesu mwenyewe ktk mathayo 22:29 anatamka kwamba”mwapotea kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.Pia Paulo ktk 2timotheo 3:15 anasema”na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa njia ya imani iliyo ktk Kristo Yesu.Hivyo jitahidi kuyajua maandiko kwa sababu yatakupa hekima hatimaye wokovu.MUHIMU SANA NI HILI=NIA YA MWILI NI UADUI JUU YA MUNGU KWA MAANA HAITII SHERIA YA MUNGU WALA HAIWEZI KUITII(warumi 8:7).Paulo anaendelea kusema”KAMA MTU AKIJIONA KUWA NI NABII AU MTU WA ROHONI NA AYATAMBUE HAYO NINAYOWAANDIKIA KWAMBA NI MAAGIZO YA BWANA(1wakorintho 14:37).Inakuwaje ujiite mtu wa rohoni walakini huyatambui maagizo ya Bwana.Yohana anatafusiri dhambi kuwa ni UVUNJAJI WA SHERIA(1YOHANA 3:4).Mungu alitoa SHERIA kwa njia yaMusa,pia neema na kweli kwa njia ya Yesu Kristo(YOHANA MTAKATIFU 1:17).Sheria ambayo haikupitia kwa Musa ni ya uongo.Yesu anawaita watu WANAFIKI kwa sababu wameacha MAMBO MAKUU YA SHERIA(adili,rehema na imani)

 276. Mr. Siyi

  Wakati tunamsubiri Joel Msella ajibu uliyomuuliza mimi pia nimesoma maswali yako na nimeona niweke mchango wangu kutokana na nilivyokuelewa.

  Umeandika hivi:

  “1. Kama Mungu ametutaka kuishi sawasawa na alivyoagiza, na Mwanaye akasisitiza kuishi huko sharti kuongozwe na moyo na matendo ya mwili, yathibitishe kile kilichomo moyoni ambacho Mungu amekisema kwetu. Je, kama kweli una uelewa huu, kwa nini baadhi ya matendo mema kama vile kutunza Sabato ya siku ya saba, huyafanyi? Au hayo hayaongozwi na moyo? Kama yanayoongozwa na moyo, mbona moyo huohuo unakuongoza kufanya mambo tofauti na yale aliyoyasema Mungu ndani ya neno lake?”

  Baada ya sheria kuondolewa kwenye vibao vya mawe (Agano la Kale) na kuandikwa katika mioyo (Agano jipya) Nielewavyo mimi sasa ni kwamba Matendo ya mwili HAYAKAMILISHI uchaji Mungu bali huwa ni MATOKEO YA MTU anayemcha Mungu. Mtu HAAGIZWI (Sheria) KUTENDA MEMA ndiyo awe amekamilisha imani yake bali Badiliko la Moyoni alilolipata (Wokovu) ndilo litazaa matendo mema.

  Nadhani pia ndivyo Joel Msella kaandika hivi”

  “Kama wana wa Mungu, tunatarajiwa kufanya yaliyo mema (soma pia Mathayo 5:16, 1 Timotheo 2:8-10, Tito 2:7-14; 3:14), lakini SI MATENDO HAYO yanayotufanya tuhesabiwe haki mbele za Mungu (angalia Warumi 3:23-24, Waefeso 2:8-9, Warumi 11:6, Wagalatia 2:21, ). Tukitarajia au kutafuta kuhesabiwa haki kwa sababu ya matendo yetu mema tunarudi kule kwenye torati na kuachana na neema.

  Matendo mema tunayoyatenda ni matunda ya mabadiliko yanayotokana na utendaji au uhai wa ile imani katika Kristo Yesu iliyo ndani yetu.”

  Suala la KUTUNZA SABATO ni sheria na wala siyo moja ya matendo mema tunayotakiwa kuwafanyia wengine.

 277. Sheria ni nzuri, ya rohoni, imetoka kwa Mungu kwaajili ya kutimiza kusudi fulani.

  (Warumi 7:12) Kwahiyo, sheria ni takatifu, na amri ni takatifu, na ya haki, na njema.

  1 Timothy 1:8 Na tunafahamu kwamba sheria ni njema ikitukiwa vizuri (mahali pake).

  MSTARI WA 14Kwakuwa tunafahamunkwamba Sheria ni ya rohoni, lakini mimi ni wa mwilini, nimeuzwa katika dhambi.

  Kwahiyo, sheria sio mbaya, inafaaa kwa kazi yake, inapotumika mahali pake. Ni takatifu, ni ya rohoni, ni ya Mungu.

  Kazi ya Sheria
  1. Ni kwaajili ya walio chininyansheria. (Warumi 3:19)
  2. Kufunga vinywa vya ulimwengu wote na kuidhirisha hatia yake kwa Mungu. (Rumi 3:19) au kuhukumu (Warumi 7:7)(Wagalatia 3:22)
  3. Kuipa nguvu dhambi (1 Wakorintho 1:15-56)
  4. Kwaajili ya wasiomjua Mungu (1 Timothy 1:8-10)
  5. Iliongezwa kwasababu ya makosa (Wagalatia 3:19)
  6. Kutuangalia/kututiisha/kutulea, kutuleta kwa Kristo (Galatia 3:23-24)

  TUMEWEKWA HURU TOKA KWA SHERIA
  Rumi 7:6 Lakini sasa tumefunguoiwantoka kwenye sheria…

  HATUKO CHINI YA SHERIA
  Rumi 6:14 Dhambi haitawatawal tena kwakuwa HAMPO CHININYA SHERIA BALINCHINI YA NEEMA

  Galatia 3:25 Baada ya imani kuja imani hatupo tena chini ya mwangalizi.

  Mwisho, sheria alikuwa ni mwangalizi au msimamizi, (kama msimamizi wa mirathi vile) ambaye usimamizi wake umekoma baada ya wana kufikia umri wa kumwamini Mungu, na kurithi ahadi zake wao wenyewe.

  Mwarobaini wa dhambi siyo Torati, maana ingekuwapo sheria iwezayo kuhuisha basi kuhesabiwa haki kungekuwa kwa sheria. Mwarobaini wa dhambi ni kuzaliwa mara ya pili, kuzaliwa na Mungu,bunakuwa na utambulisho mwingine. hauitwi tena mdhambi,

 278. Well stated Msella!

  Umechambua vema na kuwasilisha hoja kwa ukamilifu wake!

  Big up!

  Siyi, nilipoona kwenye highlights kwamba umechangia nilijua tu kuwa lazima utatengeneza mpindo wa kuileta mada kwenye sabato. Na ndicho ulichofanya, na ninavyokujua lazima utalazimisha kwa sehemu kubwa sana kuielekeza mada kwenye kujadili sabato.

  Please soma vizuri alichokichambua Joel ili ukipate vizuri zaidi kabla hatujaendelea sana, maana najua kwenye hii mada utachangia sana kwa kuwa inagusa mambo ya torati, hahahaaa!

  Take care!

 279. What Does It Mean to “Fulfill the Law”?

  by Lois Tverberg

  Do not think that I came to abolish the Law or the Prophets; I did not come to abolish but to fulfill. Matthew 5:17 (NASB)

  A difficult passage for many Christians is Jesus’ saying in Matthew 5:17 that he “came not to abolish the law but to fulfill it.” A traditional way of interpreting it is to say that when Jesus “fulfilled the Law” he brought it to an end, even though in the next several verses, Jesus says quite forcefully that this isn’t true. The key is that the phrase “fulfill the Law” is an idiom, and found several other places in the New Testament and in Jewish sayings from Jesus’ time. By studying these passages we can understand the saying more fully. Moreover, we can read Paul’s important writings about “fulfilling the law,” and see what they mean for us.
  “Fulfill the Law” as a Rabbinic Idiom

  It will help us greatly to know that the phrase “fulfill the Torah” is a rabbinic idiom that is still in use even today. The word we read as “law” is torah in Hebrew, and its main sense is teaching, guidance and instruction, rather than legal regulation. It is God’s instructions for living, and because of God’s great authority, it demands obedience and therefore takes on the sense of “law.” The Torah is often understood to mean the first five books of the Bible, but also refers to the Scriptures in general. In Jesus’ time, and among Jews today, this is a very positive thing – that the God who made us would give us instructions for how to live.1 The rabbis made it their goal to understand these instructions fully and teach people how to live by it.

  The translation of “to fulfill” is lekayem in Hebrew (le-KAI-yem), which means to uphold or establish, as well as to fulfill, complete or accomplish.2 David Bivin has pointed out that the phrase “fulfill the Law” is often used as an idiom to mean to properly interpret the Torah so that people can obey it as God really intends. The word “abolish” was likely either levatel, to nullify, or la’akor, to uproot, which meant to undermine the Torah by misinterpreting it. For example, the law against adultery could be interpreted as specifically against cheating on one’s spouse, but not about pornography. When Jesus declared that lust also was a violation of the commandment, he was clarifying the true intent of that law, so in rabbinic parlance he was “fulfilling the Law.” In contrast, if a pastor told his congregation that watching x-rated videos was fine, he would be “abolishing the Law” – causing them to not live as God wants them to live. Here are a couple examples of this usage from around Jesus’ time:

  If the Sanhedrin gives a decision to abolish (uproot, la’akor) a law, by saying for instance, that the Torah does not include the laws of Sabbath or idolatry, the members of the court are free from a sin offering if they obey them; but if the Sanhedrin abolishes (la’akor) only one part of a law but fulfills (lekayem) the other part, they are liable. 3

  Go away to a place of study of the Torah, and do not suppose that it will come to you. For your fellow disciples will fulfill it (lekayem) in your hand. And on your own understanding do not rely. 4 (Here “fulfill” means to explain and interpret the Scripture.)

  Fulfilling the Law as Obedience

  There is another sense of the phrase “fulfill the Law”, and it is to carry out a law – to actually do what it says. In Jewish sayings from near Jesus’ time, we see many examples of this second usage as well, including the following:

  If this is how you act, you have never in your whole life fulfilled the requirement of dwelling in a sukkah! 5 (One rabbi is criticizing another’s interpretation of the Torah, which caused him not to do what it really intends.)

  Whoever fulfills the Torah when poor will in the end fulfill it in wealth. And whoever treats the Torah as nothing when he is wealthy in the end will treat it as nothing in poverty. 6 (Here it means “to obey” – definitely the opposite of “fulfill in order to do away with.”)

  Interestingly, these two usages of “fulfill” seem to be key to understanding Jesus’ words in the passage in Matthew 5 that begins with him speaking about “fulfilling the law.”

  …Anyone who breaks one of the least of these commandments and teaches others to do the same will be called least in the kingdom of heaven, but whoever practices and teaches these commands will be called great in the kingdom of heaven. (Matt. 5:19)

  Here the two actions of “practicing” and “teaching others to do the same” are an exact parallel to the two idiomatic senses of “fulfill,” while the words “break” and “teach others to break” are the idiomatic senses of “abolish.” So, Jesus’ statement about fulfilling and abolishing the Torah is a parallel to this sentence. Parallelism was a very common way of emphasizing an idea in the Bible, and especially for Jesus.7 By understanding the idiom we see that Jesus was emphatically stating his intention, which was to explain God’s word and live by it, and not to undermine it.
  What does this mean for us?

  In the past, the idea that “Christ brought the Law to an end by fulfilling it” has been the traditional rationale of why Christians are not obligated to keep the laws of the Old Testament. We overlook the fact that in Acts 15, the early church declared that Gentiles were not obligated to convert to Judaism by being circumcised and taking on the covenant of Torah that was given to Israel. They are told instead that they must simply observe the three most basic laws against idolatry, sexual immorality and murder, the minimal observance required of Gentile God-fearers.8 The reason Christians have not been required to observe the Torah was not because it has ended, but because we are Gentiles.

  Paul, of course was zealous in saying that Gentiles were not required to observe the Torah, when some were insisting that they become circumcised and take on other observances. He himself still observed the Torah, and proved it to James when asked to do so in Acts 21:24-26, but he still maintained that Gentiles were saved apart from observing it. He supported this by pointing out that they were filled with the Holy Spirit when they first believed in Christ, not after they had become more observant of the Torah (Gal. 3:2-5). He also used the example of Abraham, who also was a Gentile who never observed the laws of the Torah that were given 400 years later, but was justified because of his faith. (Gal. 3:6-9) 9

  Paul’s use of “Fulfill the Law”

  The question then becomes, if the Torah is God’s instructions for how to live, then are Gentiles entirely excluded from its wonderful truths? Surprisingly, in both Romans and Galatians, after Paul has spent a lot of time arguing against their need to observe the Torah, he actually answers this question by speaking about how they can “fulfill the Law.” He says:

  Let no debt remain outstanding, except the continuing debt to love one another, for he who loves his fellowman has fulfilled the law. The commandments, “Do not commit adultery,” “Do not murder,” “Do not steal,” “Do not covet,” and whatever other commandment there may be, are summed up in this one rule: “Love your neighbor as yourself.” Love does no harm to its neighbor. Therefore love is the fulfillment of the law. (Rom. 13:8-10)

  For the whole law is fulfilled in one word, “You shall love your neighbor as yourself.” (Gal. 5:14; NASB)

  If Paul is using first idiomatic sense of “fulfill the Torah” discussed above, he is saying that love is the supreme interpretation of the Torah – the ultimate summation of everything that God has taught in the Scriptures. He is reiterating Jesus’ key teaching about loving God and neighbor that says “All the Law and the Prophets hang on these two commandments” (Matt. 22:40). The two laws about love are not just more important than the rest, they are actually the grand summation of it all. A later rabbi put it this way: “Love your neighbor as yourself – this is the very essence (klal gadol) of the Torah.” 8 Love is the overriding principle that shapes how all laws should be obeyed.
  Love as Fulfilling the Torah

  Paul also seems to be using the second idiomatic sense of “fulfill the Torah” to say that loving your neighbor is actually the living out of the Torah. When we love our neighbor, it is as if we have done everything God has asked of us. A Jewish saying from near that time has a similar style:

  If one is honest in his business dealings and people esteem him, it is accounted to him as though he had fulfilled the whole Torah. 9

  The point of the saying above is that a person who is honest and praiseworthy in all his dealings with others has truly hit God’s goal for how he should live. He didn’t cancel the Law, he did it to the utmost! Similarly, Paul is saying that when we love our neighbor, we have truly achieved the goal of all the commandments. So instead of saying that the Gentiles are without the law altogether, he says that they are doing everything it requires when they obey the “Law of Christ,” which is to love one another. For him, the command to love is the great equalizer between the Jew who observes the Torah, and Gentile who does not, but who both believe in Christ. Paul says,

  “For in Christ Jesus neither circumcision nor uncircumcision has any value. The only thing that counts is faith expressing itself through love.” (Gal. 5:6)

  Other New Testament writers also highlight it the commandment to love as the central law that all must follow. James says, If you really keep the royal law found in Scripture, “Love your neighbor as yourself,” you are doing right (James 2:8). And finally, John sums up everything in terms of love:

  This is love: not that we loved God, but that he loved us and sent his Son as an atoning sacrifice for our sins. Dear friends, since God so loved us, we also ought to love one another. No one has ever seen God; but if we love one another, God lives in us and his love is made complete in us. 1 John 4:7-12

 280. Shalom.
  Sifa na Utukufu ni kwa BWANA YESU ailiyedharau aibu na kutufilia Msalabani.
  TORATI ilikuwa ni mfano wa NEEMA, lakini TORATI haikuwa na Nguvu za KUOKOA ndani yake. TORATI ilikuwa ni polisi wa kuwatia watu jela,bali ilihitaji NEEMA kuwatoa watu gerezani.
  DAMU YA YESU KRISTO ,INJILI,HUTUKOMBOA NA DHAMBI.
  WAEBRANIA 10:1-29 ” 1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
  2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?
  3 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
  4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.
  5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari;
  6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo;
  7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu.
  8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati),
  9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.
  10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.
  11 Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.
  12 Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu;
  13 tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.
  14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
  15 Na Roho Mtakatifu naye amshuhudia; kwa maana, baada ya kusema,
  16 Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo,
  17 Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
  18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
  19 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,
  20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;
  21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu;
  22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.
  23 Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu;
  24 tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri;
  25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
  26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
  27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
  28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
  29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
  Pia WAEBRANIA 2:1-4 ” 1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa.
  2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki,
  3 sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;
  4 Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.”
  Ni kweli Kabisa tunapaswa KUAMINI KAZI ALIZOMALIZA BWANA WETU YESU KRISTO.
  Bwana Yesu Awabariki.

 281. Ndugu Msella na wengine, shalom…
  Kwanza, Ubarikiwe sana kwa ufafanuzi wa maandiko. Nitumie msemo wako wa kuimba ukiwa nje ya key. Key imewekwa na umeonekana kuimba vizuri sana rafiki yangu, ila kuna sehemu sauti yako inaparuza sana kiasi cha kumkosesha raha mwalimu. Niombe nipate muda nije na sehemu hiyo ndogo sana unayoonekana kuparuza kidogo tu!!
  Pili, umesema vyema kuwa, ni kweli haki zetu sharti zizidi zile za mafarisayo. Mwishoni ukakasisitiza kuwa, imani yetu, haiwezi kukosa matendo mema halafu ikaendelea kuitwa imani safi/hai!! Hasha!! Kwa maneno mengine, matendo mema ni yale matendo yanayoonesha upendo kwa Mungu na wanadamu wenzetu. Kwa hiyo matendo mema, YANAPASWA YATENDWE NA MTU KUTOKANA NA MSUKUMO WA NDANI MOYONI MWAKE –UPENDO. Kimsingi, umeeleza mambo mengi mazuri rafiki yangu. Nilichoondoka bila kukuelewa ni hiki;
  1. Kama Mungu ametutaka kuishi sawasawa na alivyoagiza, na Mwanaye akasisitiza kuishi huko sharti kuongozwe na moyo na matendo ya mwili, yathibitishe kile kilichomo moyoni ambacho Mungu amekisema kwetu. Je, kama kweli una uelewa huu, kwa nini baadhi ya matendo mema kama vile kutunza Sabato ya siku ya saba, huyafanyi? Au hayo hayaongozwi na moyo? Kama yanayoongozwa na moyo, mbona moyo huohuo unakuongoza kufanya mambo tofauti na yale aliyoyasema Mungu ndani ya neno lake?
  2. Hivi dhambi/tendo jema huanzia moyoni au akilini/mawazoni? Au akili na mawazo ni vitu viwili tofauti au ni kitu kilekile??
  3. Na kama torati yote (matendo ya sheria) ilitimizwa na Kristo pale msalabani; je haya matendo mema yanayopaswa kudhirisha uhai wa imani zetu, ni matendo ya Torati/sheria? Kama ni hapana, ni kwa namna gani? Na kama ni ndiyo, huoni kuwa sheria/torati haijaisha?
  Nakungoja kwa ajili ya kupewa ufafanuzi wa hoja hizo tatu hapo, wakati naangalia kama nitapata muda wa kuleta chochote kuhusiana na wasilisho lako zuri. Vinginevyo, Neema ya Bwana ikufunike mpendwa!!
  Siyi

 282. Bwana Yesu Asifiwe saana.

  Barikiwa sana mtoa maada. Umedadavua vema ndugu; Kristo aliitimiza Torati kwa kutenda yoooote, ambayo torati ilihitaji mtu ayatende ili kuhesabiwa haki. Lakini pia, Kristo alitimiza hata yale ambayo Torati ilihitaji kwa mtu asiyeitimiza Torati, yaani alilaaniwa kwa kuangikwa mtini, kama mbadala wa kizazi chote cha wenye mwili, ambacho hakiwezi kuitimiza Torati. Lakini pia, alishinda mauti, kama vile manabii walivyotabiri. Hivyo haimpasi mtu kuhesabiwa haki kwa kutimiza Torati tena, wala haimpendezi Mungu kutimiza kwake mtu huyo Torati, bali kule kuamini kazi ambayo Mungu mwenyewe, ndani ya Kristo Yesu aliifanya pale msalabani.

  Tunahitaji ukweli huu ndugu katika Kristo

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s