Ni Mwaka Mpya wa 2015!

Happy New Year 2015 Hot Colors On Black Backgrounds

Mpendwa Msomaji wa SG,

Tunamshukuru Mungu kwa ajili yako kwa vile umekuwa pamoja nasi kwa mwaka mzima wa 2014. Mungu wa mbinguni na akubariki na akujalie kuyazingatia yale mema yote uliyojifunza katika familia hii kubwa ya Strictly Gospel. Vile vile tunamuomba Mungu akupe neema ya kukuwezesha kusahau iwapo kwa namna moja au nyingine ulikwazika katika jambo lolote hapa!

Wale wenye mahitaji ambao bado hawajapata majibu yake bado Mungu ni muweza; Ni Mungu anayejibu maombi. Ni Mungu ajibuye kwa wakati wake ulio sahihi. Tarehe zinabadilika lakini Mungu habadiliki na wala Ahadi zake hazibadiliki. Tuzidi kumuomba yeye kwa kuwa hatuna Mungu mwingine zaidi yake! Tunaendelea kuomba Mungu pamoja na wewe. Amina!

Kwa wale ambao wamekuwa na mambo dhahiri ya kumshukuru Mungu kwamba amewatendea; Tunamshukuru na kumtukuza Mungu pamoja nawe!

Sasa, Mwaka mpya unaingia. Yawezekana mwaka mpya ukaja na mambo mapya kwako au yanaweza kubakia yale yale. Jambo la msingi hapa ni kwamba Usiweke moyoni mambo yaliyopita, iwe ni mazuri au mabaya; kwa maana maisha hayarudi nyuma bali yanasonga mbele. Kama ulikutana na mambo mabaya usiyakumbuke na kuanza kuhuzunika tena, usije ukanung’unika na mkosea Mungu. Wala usije ukakumbuka mafanikio yako ya mwaka 2014 na kuyaweka moyoni, yasije yakakupa kiburi na Bwana Mungu akakukasirikia!

Mtangulize Mungu kwa mwaka huu ukiwa mpya na hata utakapokuwa mkuukuu usije ukabadili mpangilio ukaitanguliza Dunia na Mungu ukamuweka nyuma!

Heri ya Mwaka Mpya 2015!

Advertisements

16 thoughts on “Ni Mwaka Mpya wa 2015!

 1. M.Siyi,
  Shalom.
  Naomba unisaidie, WANAOABUDU siku ya JUMAMOSI wanatumia KALENDA IPI?
  Ahsante.

 2. Sungura,

  Unaijua kalenda iliyokuwepo kabla ya dhambi?

  Unayaamini maneno ya Yesu kwamba, “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo” -Yohana 14:1-3???????
  Siyi

 3. Heri ya mwaka mpya,CK LWEMBE na wengine!

  MWAKA 2015 NI MWAKA AMBAO MIZIZI YA UKOMBOZI
  WA WATEULE WA TANZANIA ITAONEKANA KUIMARIKA ZAIDI!
  (ZABURI 89:19).

  Mungu alishaandaa watu ambao sasa anawatumia KUDHIBITISHA
  UTUKUFU WAKE.Kanisa la Tanzania linakwenda kuikomboa Tanzania!
  Mungu amesikia kilio cha wateule wanaoishi Tanzania ili kutimiza
  kusudi la Tanzania kuumbwa!

  Huu ni mwaka ambao yatatokea mambo ambayo yatawawasha
  masikio watu wote wenye nia mbaya na TANZANIA.Ni mwaka ambao
  kazi nyingi za manabii wa uongo(mashetani) zitaharibika kwa viwango
  vya kutisha mno.Hawataamini kile kitakachotokea katika huduma zao
  na maisha yao ya kila siku!Bwana anakwenda kuwatukuza wateule
  waliokubali kuvaa unyenyekevu wa Yesu na utukufu huo utaonekana
  wazi sana hata kwa wale vipofu na viziwi wa maisha ya kiroho.

  Mwaka huu wateule wajiandae kuona jinsi Mungu anavyowaaibisha
  MAFISADI na kuwatumikisha jinsi apendavyo yeye!Misingi ya kusiasa,
  kiuchumi,kielimu,afya na kijamii ITAONEKANA WAZI JINSI INAVYOJEGWA
  NA MUNGU MWENYEWE!Mungu ataendelea kupeleka misiba kwa
  manabii wa uongo waliojikita katika sekta zote hapa nchini.Huu ni mwaka ambao hata watu wasioamini wataanza kujitambua na kuiona
  hatima nzuri ya taifa la Tanzania.Hatima ambayo Mungu aliikusudia
  sasa itaanza kuonekana kwa macho ya nyama.Hebu tusome kwa undani kile ambacho Mungu anasema katika ZABURI 89:19.

  Huu mwaka ni mtamu sana kwa wateule wanaojitambua kiroho
  ambao walikuwa WAKISUBIRI MPENYO WA KITAIFA KWA UVUMILIVU
  MKUBWA.Ni mpenyo katika ulimwengu wa roho ambao unakwenda
  kuthibitika katika ulimwengu wa mwili.Mwaka 2015 Mungu amelichagua
  taifa la Tanzania ili ajithibitishe kwa WATESI WOTE WANAOTAMANI
  KULIANGAMIZA HILI TAIFA USIKU NA MCHANA.Uganga na uchawi
  wa manabii wa uongo unakwenda kuteketezwa na moto ulao!Utateketea kama vile moto unavyoteketeza mabua makavu.Na kama
  unadhani natania soma ISAYA 47:8-15.

  Serikali ya Tanzania inaongozwa na wateule wa Mungu aliye hai….
  Hakuna mjinga wala mpumbavu yeyote anayeweza kubatilisha
  kusudi la Mungu ndani ya Tanzania.Wakati Tanzania inapovikwa vazi
  la unyenyekevu ndipo na mashetani waliojikita katika kila sekta
  wanavyovuliwa mavazi yao mekundu na kuachwa wakiwa uchi wa
  mnyama!Mbwamwitu naomba msinikasirikie bali muulizeni mungu
  wenu amekosea wapi.

  HUU NI MWANZO TU…………….

 4. Mh, Siyi,

  Kalenda ya mji ule, upi huo rafiki yangu?

  Halafu, ivi kuna siku itatokea wewe utakuwa raia wa mbinguni eh?

 5. Lwembe,

  “Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu”- 1 Wakorintho 1:25. “Maana hekima ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasaye wenye hekima katika hila yao” -1 Wakorintho 3:19. “Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii”- Torati 29:29.

  Sitaki kubadili mada hii kuwa mjadala wa mwaka una siku ngapi!! Huko nyuma tulishajadili sana jambo hili na wewe ukachangia positively!! Nina imani hata michango yako leo bado ipo kwenye maktaba yangu. Suala ya siku ndani ya mwaka kwa mujibu wa Biblia, liko bayana sana!! Siku inaanza muda gani na kuisha muda upi; limewekwa wazi saaana!! Haina maana leo watu/walimwengu watakapoamua kusherehekea mwanzo mpya wa mwaka kuanzia saa sita usiku eti na Mungu naye atabadili neno/msimamo wake!! Hasha!! Haina maana kwamba sisi walimwengu tukiwa na miezi ya siku 29 au 31 na Mungu naye atabadili idadi ya siku za mwezi ndani ya Neno lake! Hasha!! Neno la Mungu halitabadilika milele na hakuna mwenye hekima yeyote chini ya jua atakayelibadilisha!!

  Kwa vile Siyi niko duniani, nikisafiri kuelekea kwenye makao ya amani, furaha na shangwe siku zote, sina budi kuanza leo kujifunza habari za kalenda ya mji ule. Kwa maana “… mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu” – Kolosai 3:1-4.

  Ukitaka kuwa raia mwema wa mbinguni, duniani hautaeleweka kwa wenye hekima zao, maana utakuwa na hekima ya Mungu. Na hekima ya Mungu vs hekima ya dunia, vinapingana sana.

  Neema ya Bwana ikufunike
  Siyi

 6. Siyi,

  Hahahahaha………!
  Unahangaika sana na mazingira bila ya Maarifa! Kuna mambo ambayo Mungu hayamsumbui wala watu wake; mojawapo ya hayo ni Uongo wa dini unaojaribu “kuziiba” siku! Siku zote ni za Mungu na HAKUNA anayeweza kuzibadilisha zaidi ya kujibadilisha ufahamu wake yeye mwenyewe na kuishia kuuamini upuuzi wake kwamba ndiyo kweli, na hivyo kuishia kuufanania upuuzi wake hata kujitambulisha kwa huo upuuzi!

  Hesabu ya siku 30 za mwezi ni sawa, hiyo ya kinabii, lakini hatuwezi kujirudisha ktk hesabu hiyo, maana hakuna mahali hesabu hiyo ilipoambatanishwa kuwa shart la Wokovu! Tofauti na jambo hilo, hesabu ya miaka tuliyonayo leo hii, imejengeka katika msingi wa Wokovu, nayo dunia nzima inalikiri jambo hilo, whether Chinese or Isis, wote wanalitambua hilo hivyo kwamba huu ni mwaka wa 2015 tangu Kuzaliwa kwa Mwokozi!

  Kwahiyo unapolikataa jambo hili ndiko kule kupumbazwa na dini tunakokusema; yaani unalikana jambo la kuzaliwa kwa Mwokozi, kama ambavyo Katoliki wanavyolikataa jambo la “kula mwili wa Kristo na kuinywa damu yake” ktk ile siku ya Ijumaa aliyosulubiwa, wakiwazuia waumini wao kula nyama ktk siku hiyo, wakiungana na wale 70 waliojitenga na Kristo baada ya kuambiwa jambo hilo!

  Kiroho ndio wameukana Wokovu!!!

  Maarifa Siyi ni muhimu sana ktk maisha yetu ya kila siku. Ni kupitia hayo ndio Mungu anatuhakikishia Uhuru wetu kupitia Ufahamu anaotupatia ili kutuongoza ktk nyendo zetu akitutoa ktk kutumikishwa na dini kama mazezeta!

  Hebu nikurudishe tena ktk jambo la siku ili uone how smart God is!
  Israeli walipotoka Misri Mungu akawapa Mwongozo wake wa maisha ili waufuate. Sasa si kwamba hakujua watafanyanao nini huo Mwongozo, aliyajua yote mpaka mtakayoyafanya ninyi akina Siyi kwa kadiri mtakavyoyabadili mambo na kuanza kuabudu siku badala ya Mwenye siku!

  Tena nyie wavamiaji ndio huwa na mambo mengi kuhusu msiyoyajua kuliko wenye chao! Haya, mmejing’ang’aniza kwamba sabato ilitunzwa kuanzia kwa Adamu, na kwamba siku aliyopumzika Mungu ni Jumamosi na hiyo ndio Ishara na muhuri wa Mungu; kuibadilisha ni kuivunja na hivyo kustahili Jehanum!

  Vizuri, hebu mtazame Joshua alichokifanya hapa, ameihamisha siku ya Sabato kutoka Jumamosi mnayoijua na kuipeleka Jumapili, kama utayaamini Maandiko!

  “Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni. Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. Hayo, je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha Yashari? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima. Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizoandama baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.” (‭YOS.‬ ‭10‬:‭12-14‬ SUV)

  Dogo, chezea Mungu wewe! Anasema MNAABUDU MSICHOKIJUA! Leo ndio siku anayoyafunua aliyoyaficha ili tuishangilie “Siku ya Bwana” wetu sisi tulio watumwa na rafiki zake, Yeye aliye Baba yetu, hata Siku yake imekuwa ni Siku yetu kulingana na urithi aliotupatia hapo tulipofanywa kuwa wanawe, ndio maana tunaweza kurejea mpaka huko ktk siku za Joshua na kuyaona hayo aliyoyaficha kwa ajili yetu!!!

  Siyi, nakutakia Mwaka Mpya utakaokuingiza nawe ktk Upya wa kuzaliwa kwa Roho wa Mungu ili uione na kuila manna iliyofichwa kwa ajili ya wanaozaliwa mara ya pili, hao wanaopewa ukuhani na hivyo ni lazima wapewe fundo la manna hiyo, kulingana na Sheria ya ukuhani!

  Karibu sana!!!

 7. Heri ya Mwaka Mpya kwenu nyote wana SG!

  Ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba ametupa tena fursa ya kuwepo hapa duniani ili kulitimiza kusudi lake Kuu, kuhakikisha kwamba tumeupokea Wokovu wake aliotukirimia kwa Neema!

  Wakati umesonga saaaana, huenda hivi sasa Bwana amesimama Mlangoni tayari kulifunga Lango la Neema, yaani ktk hizi siku za mwaka huu mpya, huenda anatusubiri sisi wawili tu, mimi na wewe ndio tuliobakia huko nje tukihangaika na dunia ya dini, hiyo yenye kupumbaza. Ombi langu ni Bwana na atushike mkono atuvutie ndani kama wale malaika walivyomvutia ndani Lutu na kuufunga Mlango kule Sodoma!

  Ninawatakia nyote wakati uliojaa furaha inayotokana na kusogea Uweponi mwa Bwana, na hivyo magumu na makavu yote ya maisha, yawachipukie kama fimbo ya Haruni, ili furaha yenu iwe kamili!!!

  Gbu all!

 8. Asanteni SGs
  Mungu awabariki kwa kazi njema. Kimsingi mimi huwa sihesabu mwaka kama wanavyofanya walimwengu. Naamini kuwa, tunapotangaza miisho na mianzo ya miaka kama hii tuliyo nayo kwa sasa, kimsingi tunaunga mkono kazi za ibilisi. Kwa mujibu wa biblia, siku ina saa 24, wiki ina siku 7, mwezi una siku 30 na mwaka una siku 360 tu. Sasa, hili la mwaka una siku 365/365¼ tunalipata wapi?
  Mungu awabariki sana.
  Tuko pamoja tu katika injili.
  Siyi

 9. Bwana mungu alyetupatia uzima huu na awe pamoja nasi na kuutafakari upendo wake kwetu sisi hasa kwa 2015. Tumtegemee Kristo aliezaliwa kwetu na kuwa wake daima naye akae ndani ya roho zetu ili tutende yale yote yaliyomema daima. Amen

 10. MUNGU AWABALIKI SANA KWANI IMEANDIKWA TUPIGE KELELE TUWAHUBILI WATU MAKOSA YAO NANYI MUNGU AWABALIKI KWA KUTIMIZA KUSUDI HILO LA MUNGU (ISAYA 58:-1)HERI YA MWAKA 2015

 11. AMINA Nami ninawatakia Heri ya mwaka mpya 2015 Familia ya SG  Siaka S. Nyanchiwa    Internet cafe and College Controller        P.o Box  70 Serengeti, Mara, Tanzania.           P.o Box 417 Tarime,Mara, Tanzania.    Contacts: sianchwa@yahoo.com/sianchwa@gmail.com. Mobile:            +255755527476.

 12. Amen wapendwa tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kutuweka hadi leo hii. Mungu ana kusudi lake maalumu kukutunza na kukuweka hadi leo hii, tusimama imara kila mmoja ktk kusudi uliloitiwa ndipo Mungu atapoonekana kwa kina kwetu, Zaburi 90:14-17.
  Niwatakie heri ya mwaka mpya kwenu nyote!

 13. SG,
  Shalom.
  Mungu wa Mbinguni awabariki kwa HUDUMA NZURI YA KUMTANGAZA KRISTO.
  Heri ya Mwaka Mpya 2015, NENO LA MUNGU likiwa TAA ya kumulika NJIA ZETU.
  YOHANA 4:24 ” Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
  Mwaka Mpya 2015, Mungu ametuacha tufikie Lengo la KUMJIA KRISTO kwa njia hii;
  MATENDO 2:37-39 ” Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
  ****UTUKUFU NI KWA BWANA YESU KRISTO****
  Watu wote na waseme AMINA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s