Kuwaombea Watu Bila Kuwapa Nafasi ya Kutubu Dhambi zao

crusade in Katuna

Kuanzia Mwaka 2000 kurudi nyuma ilikuwa kila panapofanyika kusanyiko la Neno Mungu; iwe Semina, Mkutano wa Injili au nk ilikuwa ni jambo la muhimu sana watu kupewa nafasi ya Kutubu dhambi zao na kumpokea Yesu ili waanze maisha Mapya kama Wafuasi wa Yesu Kristo!

Siku hizi ni tofauti. Yapo majengo mengi na kumbi mbali mbali panapotolewa huduma ya Neno la Mungu lakini hawatoi nafasi ya kuwaruhusu watu kutubu dhambi zao ili waanze maisha mapya. Wanawaombea watu matatizo yao na kuwaacha warudi kama walivyokuja. Aliyekuja ni mpagani anarudi hivyo hivyo. Aliyekuja ni Muislam anarudi hivyo hivyo akiwa muislam. nk

Kwa nini watumishi wa nyakati hizo walikuwa wanalichukulia kwa uzito mkubwa suala la kumpa mtu nafasi ya kumpokea Yesu lakini siku hizi, mahali pengi, linaonekana kama siyo jambo muhimu?

Advertisements

9 thoughts on “Kuwaombea Watu Bila Kuwapa Nafasi ya Kutubu Dhambi zao

 1. hao watumishi wa hivyo hawajaitwa bali wamejiita ni majambazi katika shamba la Bwana

 2. Tiba kubwa kwa watu toba ni muhimu nafasi itolewe.

  Strictly Gospel wrote:

  > a:hover { color: red; } a { text-decoration: none; color: #0088cc; } a.primaryactionlink:link, a.primaryactionlink:visited { background-color: #2585B2; color: #fff; } a.primaryactionlink:hover, a.primaryactionlink:active { background-color: #11729E !important; color: #fff !important; } /* @media only screen and (max-device-width: 480px) { .post { min-width: 700px !important; } } */ WordPress.com Strictly Gospel posted: ” Kuanzia Mwaka 2000 kurudi nyuma ilikuwa kila panapofanyika kusanyiko la Neno Mungu; iwe Semina, Mkutano wa Injili au nk ilikuwa ni jambo la muhimu sana watu kupewa nafasi ya Kutubu dhambi zao na kumpokea Yesu ili waanze maisha Mapya kama Wafuasi wa Ye”

 3. ndg, asante kwa kutambua hayo. I want to tell you this; the world is now changing, even faith is changing-not on the positive way but in a bad way as we are making it to be very simple as life is now going on to be very simple.
  Note; remain in your faith dont allow any body/thing to change you; receive the gospel but measure it before if its true or not.1John 4:1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
  Angalia makanisa ya sasa yanavyohubiri utajiri, mafanikio na kusahau habari za kuacha dhambi na toba ya kweli; wanaacha kuhubiria watu waache dhambi, wanahubiri habari za kutoa n.k. TAFUTA IBADA YA KWELI NA HIYO IBAKI NDANI MWAKO.
  Mungu akubariki sana.

 4. Shalom wapendwa hii ni mbaya sana, tusiwaseme hao watumishi tu hata majumbani mwetu ni muhimu sana kuwahubiria lakini kuwaongoza kwenye wokovu wanafamilia maana hawa ndo hutumika na ibilisi kutuangusha. Agizo la Pentecost …. Waanzie Jerusalem, nasi tuanzie manyumbani mwetu. Mikutano na makanisa imejaa hao watu tumetoka nao kwetu unakuta watoto, ndugu, rafiki, wafanyakazi tunawabeba huko hata watoe nafasi hatuwakumbushi tumekauka. Hata waliompokea na kurudi nyuma hatuwaonyi au kuripoti wasaidiwe. Hii kupiga kimya ilitaka kuniua mara mbili na kijana aliyezoea kuja kwangu na baadae kuunga urafiki na msichana wa kazi. Mwanzo alitubu akawa moto kisha akapoa akaanza kukwepa ibada za jioni pamoja ila jumapili kanisani anakuja baadae aliiba na kuua na pia kutaka kuniua mimi, kifupi tuliponea Yesu tu, ni muujiza! Ilikuja gundulika ni jambazi sugu na hii nilionywa na Roho Mt na kutamka wazi anatembea na roho ya mauti nijazembea au kutomruhusu kabisa kwangu au kuhakiki wokovu wake. Mungu atusaidie

 5. watu wengi nyakati zaleo wanapenda uponyaji na kumkataa’mponyajimwenyewe
  ( kupenda sabato-kumkataa
  BWANA wa sabato mwenyewe)

 6. SHALOM.
  Watumishi wa siku hizi ni WATUMISHI WA TUMBO.Wanajali zaidi pesa kuliko nafsi ya mtu.
  Injili ya SIKU HIZI ni ya ‘ISHARA na MAAJABU’ ili kutimiza MATHAYO 24:24 ” Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule.”
  Sehemu kubwa ya INJILI YA LEO inahubiriwa na MAKRISTO (Si WAKRISTO) WA UONGO na MANABII WA UONGO na ‘slogan’ yao ni; NJOO UONE ISHARA $ MAAJABU!
  Hakuna MAFUNDISHO sahihi ya NENO LA MUNGU.Mafundisho sahihi ya NENO LA MUNGU ndiyo yanayomfanya mtu ahukumike na kutubu Dhambi.
  Mfano wa INJILI YA KWELI ni Kwenye MATENDO 2:37-39 ” 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
  Pia kuna namna ambayo SI YA KIBIBLIA katika Kuwaongoza watu kwa KRISTO. Kwa mfano: KUWAONGOZA WATU SALA YA TOBA NI FUNDISHO LA KIAKILI KABISA ambalo HALIMAANISHI KUWA MWENYE DHAMBI KATUBU.
  BIBLIA inasema kwenye MATENDO 2:38-39 ” 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
  ***KUWAONGOZA watu SALA YA TOBA ni FUNDISHO LA IBILISI.***

 7. Mi nafikiri wana mazingaombwe wamekuwa wengi maana nyakati za mwisho hizi shetani anafanya kazi kwa viwango visivyo vya kawaida ( UFUNUO WA YOHANA 12:12,17)

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s