Kalenda/Calendar Ipi ni Sahihi?

2015-calendar

Duniani kuna kalenda nyingi ambazo hutumiwa na jamii, dini au kikundi fulani cha watu, zote zikiwa na mpangilio tofauti wa siku katika Mwaka. Kwa mfano ziko zinazoonyesha mwaka una siku 365, zingine una mwaka 360. Kalenda inayotambulika zaidi inaonyesha mwaka huu ni wa 2015 AD/BKK wakati nyingine zinataja ni mwaka tofauti kutokana na Kile walichoweka msingi wao juu yake!

Je, Kalenda ipi ni sahihi kufuatana na Biblia?

Advertisements

19 thoughts on “Kalenda/Calendar Ipi ni Sahihi?

 1. @ Milinga,
  Nashukuru kama umepitia makala hiyo. Mungu akubariki sana. Naomba nijibu maswali yako kwa kifupi sana. Swali la
  1. Nikitaka kalenda ya Mungu yenye siku 360 ili niiweke ukutani au mezani au kwenye Simu yangu naipata wapi?

  Jibu
  Kama utaihitaji, tengeneza ya kwako kwa mujibu wa Biblia. Acha kufuata za walimwengu. Sisi wakristo tumeshazidiwa na waislamu kabisa. Wao wana kalenda na miaka yao kabisa, pamoja na mikanganyiko ya miaka hii tuliyo nayo sasa kuwepo, wao wanayo ya kwao. Tengeneza ya kwako, utakuwa nayo hivyo utakuwa na uwezo wa kuiweka kwenye ukuta au simu.
  2. Je, kwa kutumia kalenda hiyo unayoiita ya Mungu ninaweza kuweka mipango yangu ya maendeleo kwa miaka mitano au kumi ijayo na kila siku nikapanga jambo la kufanya kwa kutumia hiyo kalenda (kama ipo)?

  Jibu
  Ndiyo, inawezekana kabisa japo itakuwa ni kalenda ya kwako tu na hao waumini wenzio. Wengine watawashangaa na kuwaona kama wenda wa zimu. Lakini heri watu wawaite wenda wa zimu huku Mungu akiwaita kuwa ni wenye busara na hekima kubwa. Unaogopa kuwa tofauti na mifumo ya kiulimwengu?? Kama unaona aibu, Mungu naye atakuonea aibu tu na wala usihangaike sana!! Kama unataka kufanana na dunia fanana nayo tu. Lakini kama unataka kufanana na Mungu, lazima uhesabu gharama!!
  3. Je, kuna nchi hata moja wanayo hiyo kalenda na ukienda maofisini au majumbani mwao unakutana na kalenda hizo zikiwa zimebandikwa ukutani kwa matumizi ya kujua siku na tarehe za matukio ya kila siku au ni kalenda tu inakuwa kichwani mwa mtu? (Can you show a written calendar that follows God’s days?)

  Jibu
  Huenda zipo, ila sina uhakika. Na huenda zisiwepo, napo sina uhakika. Nilicho nacho uhakika ni hiki, Mungu ana kalenda yake. Hata kama watu wote duniani kote hawataifuata, hicho hakitabadilisha mawazo wala mpango wa Mungu!! Kalenda ya Mungu itaendelea kubaki palepale. Watakaofundishwa wakailewa, wakakaidi wao wenyewe, hukumu inawaongoja. Ingekuwa heri kama wasingejua japo nayo isingewasaidia kitu. Siku zote ni za Mungu, na mpangilio wa siku hizo, nao ni wa Mungu. Wewe ukikubali shetani akakuibia hata kitu kimoja tu, -mpangilio wa siku za Mungu, utakuwa umekwenda na maji hakika. Hakuna usalama wowote rafiki. Mimi sina hiyo kalenda, ila nikiwa kwenye mambo yangu ya dini, huwa sipendi kabisa hata mtu kumsikia akimwinua ibilisi ndani ya kanisa akisema heri ya mwaka mpya kwa maana ya miaka hii ya siku 365!! Huo ni ufedhuli mkubwa sana kwangu!! Natambua kalenda ya dunia. Lakini pia, naitambua kalenda ya YEHOVA ambayo ndiyo napaswa kuizingatia zaidi hata kama nitasalia mwenyewe tu.
  Ubarikiwe sana. Kama utakuwa hujaridhika na majibu yangu, karibu sana tena.
  Neema ya Bwana ikufunike.

  @ Pandael
  NAshukuru sana kwa swali lako. Huenda kweli swali lako hili sikuliona kipindi kile. Maana sikumbuki kama nililijibu/nilishawahi kujibu swali la namna hii. Hata hivyo, naomba nilijifu kama ifuatavyo;
  Swali
  “Wanaoabudu Siku ya Jumamosi Wanatumia KALENDA ipi?”

  Jibu
  Wanatumia kalenda ya Mungu.
  Nadhani jibu langu linaeleweka kwako na hata kwa wengine. Kama una tashwishwi nyingine, karibu pia.
  Neema ya Bwana ikufunike rafiki
  Siyi

 2. Siyi, Shalom. Swali hili nilishakuuliza kwenye ile Mada/Heri ya 2015 labda hukuliona.Swali langu ni “Wanaoabudu Siku ya Jumamosi Wanatumia KALENDA ipi?”. Ahsante

 3. Siyi!!!

  Asante kwa darasa zuri lenye uchambuzi wa kina. Sina haja ya kukataa uchambuzi wako kwa sababu umejikita kwenye history facts.

  Nina maswali machache tu naomba unisaidie:

  1. Nikitaka kalenda ya Mungu yenye siku 360 ili niiweke ukutani au mezani au
  kwenye Simu yangu naipata wapi?

  2. Je, kwa kutumia kalenda hiyo unayoiita ya Mungu ninaweza kuweka mipango yangu ya maendeleo kwa miaka mitano au kumi ijayo na kila siku nikapanga jambo la kufanya kwa kutumia hiyo kalenda (kama ipo)?

  3. Je, kuna nchi hata moja wanayo hiyo kalenda na ukienda maofisini au majumbani mwao unakutana na kalenda hizo zikiwa zimebandikwa ukutani kwa matumizi ya kujua siku na tarehe za matukio ya kila siku au ni kalenda tu inakuwa kichwani mwa mtu? (Can you show a written calendar that follows God’s days?)

  Asante na samahani kwa maswali yangu mengi?

 4. Inaendelea…

  Kalenda ya Wiki ya Wayahudi
  Kalenda ya siku ya Wayahudi ilikuwa ikianzia machweo na kuishia machweo ya siku inayofuata. Mfumo huu wa majira ya siku ulikuwa na historia ndefu ya utamaduni wa jamii za kale za Mesopotamia, ambayo hapo zamani, ilijulikana kama Uru ya Ukalidayo. Kalenda ya Wayahudi ni kalenda yenye historia iliyokuwa ikitumiwa na taifa la Wayahudi, kwa kufuata taratibu na misingi ya Myahudi wa kwanza – mzee Ibrahimu. Kalenda hiyo ilikuwa ni kalenda ya siku saba za wiki. Kwa vile ilikuwa ni mwendelezo wa kalenda ya jamii za Mesopotamia, katika kalenda ya Wayahudi, siku za wiki hazikuwa na majina isipokuwa siku moja -Shabbath. Siku zingine, ziliitwa majina kwa kuanzia na neno “yom” (wingi yamim) lenye maana ya “siku” likufuatiwa na namba kadinali za Kiebrania Rishon (~ kwanza), ~ Sheni (-a pili) hadi siku ya sita. Siku ya saba iliitwa ‘shabbat’ (Sabato) kwa Kiebrania’ lenye maana ya mapumziko. (Totten, 1890). Hivyo, kalenda ya siku za wiki kwa Kiyahudi ilikuwa ikisomeka kama ifuatavyo;
  Kiebrania Fasili(maana)
  Yom Reeshone(Rishon) – (Sunday) Siku ya kwanza ya wiki
  Yom Shaynee (Sheni) – (Monday) Siku ya pili ya wiki
  Yom Shlee´shee (Shelishi) – (Tuesday) Siku ya tatu ya wiki
  Yom Revee´ee (Revi’i) – (Wednesdy) Siku ya nne ya wiki
  Yom Khah´mee´shee (Chamishi) – (Thursday) Siku ya tano ya wiki
  Yom Ha´shee´shee (Shishi) – (Friday) Siku ya sita ya wiki
  Shabbat – (Saturday) Mapumziko (Sabato)
  Siku ya kwanza ya wiki ilikuwa ni Yom Reeshone (Sunday), ambayo kwa leo inaitwa Jumapili katika Kalenda ya Kiswahili. Hali kadhalika, siku iliyofuata iliitwa siku ya pili na kuendelea hadi siku ya sita Yom Ha´shee´shee (Friday) ambayo kwa leo ni siku ya Ijumaa. Siku ilikuwa ikianza jioni hadi jioni ya siku inayofuata. Kutokana na mabadiliko ya majira, baadhi ya siku, hazikuwa na saa sawa na siku zingine ndani ya wiki na hivyo kuleta tofauti ya urefu kati ya mwaka mmoja na mwingine (Online Jewish Encyclopedia).

  Kalenda ya Kiarabu
  Kalenda ya Kiarabu ilianza wakati wa Hija. Kalenda hii, ilianzishwa kwa kufuata kalenda ya mzunguko wa mwezi (lunar calendar) kuanzia mwishoni mwa mwezi kuelekea mwanzoni mwa mwezi wa Hija. Ilikuwa ni Kalenda iliyoanza siku ya kwanza ya mwezi wa MuHarram, katika mwaka wa Hijrah; kipindi cha tarehe za Hija – Anno Hegirae, ambayo ilianzia tarehe 16, Julai, 622 B.K. (1 A.H). Hiki kilikuwa ni kipindi alichohamia mtume Mohamed (s.w.s.) kutoka Makka kwenda Madina, (Waleed, 1992).

  Aidha katika lugha ya Kiarabu, utamkaji wa majina ya siku, ulifuata mfumo huohuo wa lugha za kale za kimesopotamia ambao ulikuwa na misingi ya nasaba za lugha ya Kiebrania. Utamkaji wa jina la siku ulitanguliwa na neno la Kiebrania ‘yom’ kwa Kiarabu “yawm” (wingi ayyām) lililokuwa likimaanisha ‘siku’. (Online Encyclopaedia of Islam). Imegundulika kwamba, katika kalenda ya Kiarabu, majina yote ya siku za wiki, yaliandikwa kwa kutumia namba za kadinali zikitanguliwa na neno “yawm”. Mfumo na mpangilio wa majina ya siku ulikuwa sawa na ule uliokuwa ukitumiwa na Wayahudi. Mpangailio na maana za majina ya siku ya wiki kwa Kiarabu vilionekana kama ifuatavyo;

  Kiarabu Fasili Kiswahili
  Yawm Al-Aḥad – الأحَد (Sunday) Siku ya kwanza Jumapili
  Yawm Al-Ithnayn- الإثْنَين (Monday) Siku ya pili Jumatatu
  Yawm Ath-Thulaathaaʼ – الثَلاثاء (Tuesday) Siku ya tatu Jumanne
  Yawm Al-Arba’aa’ – الأربَعاء (Wednesday) Siku ya nne Jumatano
  Yawm Al-Khamīs – الخَميس (Thursday) Siku ya tano Alhamisi
  Yawm Al-Jumu’ah – الجُمُعة (Friday) Siku ya sita Ijumaa
  Yawm As-Sabt – السَبْت (Saturday) Siku ya Sabato Jumamosi
  (mapumziko)
  Chanzo: http://www.patheos.com/Resources/Additional-Resources/Islam-Days-of-the-Week, https://cmes.uchicago.edu/sites/cmes.uchicago.edu/files/uploads/ Middle%20Eastern%20Calendars.pdf, http://forums.watchuseek.com/f21/translation-days-week%3Barabic-english-day-date-wheel-259659.html
  Inaonekana kuwa, kalenda ya Kiarabu, ilitumia mfumo na mpangilio wa majina ya siku sawa na ule wa Wababeli na Wayahudi. Online Encyclopaedia of Islam). Aidha, ikumbukwe kwamba, hadi kufikia mwaka 1582 B.K., kalenda ya siku saba za wiki kwa Warumi (chini ya utawala wa Gregori I) ilikuwa ikitumiwa na mataifa mengi sana duniani. Mpaka sasa, mataifa mengi, yamekuwa na mfumo wa siku saba za wiki, sawa na ilivyokuwa hapo zamani kabla na baada ya kugunduliwa kwa maandishi (Introduction to Calendar; USNO na ISO retrived on 6th Januari 2015).

  Kalenda ya Wiki ya Waswahili
  Katika utamaduni wa Waswahili, majina ya siku yamekuwa na changamoto kubwa sana. Ikumbukwe kwamba, asili ya lugha ya Kiswahili ni lugha za kibantu; pamoja na kwamba kuna maneno kutoka lugha zingine za kigeni kama vile Kiingereza, Kijerumani, Kihindi, Kireno, Kiajemi, Kiarabu n.k. Lugha hizi pia zimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuongeza idadi ya misamiati katika lugha ya Kiswahili kama ilivyo kaida ya lugha zingine duniani.

  Mpangilio na majina ya siku za wiki katika kalenda ya Waswahili, kwa mara ya kwanza uliasisiwa na wanaleksikografia wazungu mnamo miaka ya 1930. Wanaleksikografia hawa walikuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kusanifu lugha ya Kiswahili katika kamati ya lugha ya Afrika ya Mashariki enzi za ukoloni (Johnson, 1939:ix).
  Katika utafiti wa majina ya siku kwa lugha ya Kiswahili, maandishi awali yanaonesha kuwa, majina ya siku za wiki kwa Kiswahili hayaoneshi usuli wala chanzo halisi cha majina hayo. Kamusi awali zilionekana kuorodhesha majina hayo bila ya kutoa maelezo ya kutosha ya kumsaidia msomaji. “Siku za wiki ni Jumamosi – Saturday, Jumapili – Sunday, Jumatatu – Monday, Jumanne – Tuesday, Jumatano – Wednesday, Alhamisi – Thursday – Ijumaa- Friday” – (Johnson 1939;160). Baadhi ya majina haya, hayana maana bainifu na wala hayaoneshi usuli wake kiasi cha kuingizwa kwenye usanifu wa lugha ya maandishi.
  Aidha, taarifa za msingi za mtunga kamusi yeyote, daima hufanyiwa utafiti kutoka katika lugha ya maandishi kwa kiasi kikubwa, (Kipfer 1984:55) pamoja na kwamba, lugha ya mazungumzo nayo huwa na sehemu fulani kama vile katika masimulizi ya aina ya makala, hotuba na taarifa zilizokwishaandikwa kwa ufasaha na usanifu wa lugha yenyewe. Lugha andishi hupewa kipaumbele zaidi kwa sababu, lugha hiyo huwa sanifu na kwa kiasi kikubwa, hufuata kanuni zote za kisarufi kuliko lugha ya mazungumzo. Misamiati mingi inayotumika katika lugha andishi, mara nyingi huandikwa kwa kuzingatia taratibu za usanifu wa lugha husika, Mdee 1985:69.
  Kwa kufuata kanuni za uingizaji wa vidahizo katika kumusi, kuna maswali mengi yanayohitaji majibu kuhusu majina ya siku za wiki katika lugha ya Kiswahili, mpangilio wake pamoja na maana za majina hayo. Kwa mfano, chanzo cha neno ‘juma’ kwa majina hayo, linatokana na lugha ya Kiarabu “gum’ah” au “jum’ah” lenye maana ya jamaa/jamii au kusanyiko la watu wengi kwa ajili ya ibada. Aidha, neno juma katika utamaduni wa Mswahili, humaanisha jina la mtu aghalabu mwanaume (Online Encyclopaedia of Islam). Inaonekana kuwa, neno juma kupewa maana ya wiki (siku saba), liliwekwa bila kuzingatia misingi ya uandishi wa kamusi; kwa maana kwamba, msingi na maana ya neno hilo ni la mkopo, hivyo neno lolote linapokopwa kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine, halipaswi kubadilishiwa maana yake ya msingi. Hii ni kwa sababu, neno hilo huandikwa kwa kuzingatia umbo na utamkaji wake wa asili japo hufanyiwa marekebisho kidogo ya umbo na matamshi katika lugha lengwa bila ya kuharibu maana yake ya asili (P.C.K. Mtesigwa 2004, Cannon, G. 1999, Fromkin et al 2003:512).
  Hivyo basi, imethibitika kuwa, hakuna uhusiano wowote wa jina la siku kuambikwa neno au kiambishi awali ‘juma’ likifuatiwa na namba kadinali kama yalivyo baadhi ya majina ya siku katika lugha ya Kiswahili kwa sasa; Jumamosi, Jumapili, Jumatatu, Jumanne na Jumatano.
  Tukirejea kuangalia maana ya neno ‘juma’, lenye maana ya -jamaa, jamii au kusanyiko la watu wengi; na kisha kuliambika neno -namba kadinali ili kuwa jina la siku, maana itakayopatikana kwa jina hilo la siku ni dhana tofauti na maana halisi ya jina la siku. Kwa mfano neno ‘mosi’ likiambikwa ‘juma’ kama kiambishi awali, neno tutakalopata ni jumamosi, ambalo litakuwa na maana ya mwanaume mmoja anayeitwa Juma (mosi =moja na juma =jina la mtu mwanaume), Jamaa/jamii moja au kusanyiko moja la watu*. Jumapili, litakuwa na maana ya wanaume wawili wanaoitwa Juma, jamaa au jamii mbili au makusanyiko mawili ya watu*. Jumanne, Jumatano na kadhalika. Maana hizo, hazipo kikamusi. Ni ukweli usiopingika kwamba, maana halisi na za msingi kwa maneno Jumamosi, Jumapili, Jumatatu, Jumanne na Jumatano, hazipo kabisa katika muktadha sahihi wa matumizi yake kikamusi na hivyo kubakia kwenye matumizi yasiyo sahihi ya misamiati yenye maana tofauti na inavyotumika.
  Changamoto nyingine kubwa ni kuhusu mpangilio wa siku za wiki katika lugha ya Kiswahili, ambao unaonekana kuwa na mkanganyiko kwa kiasi fulani.
  Jina la siku kwa Kiswahili Mpangilio wake
  Jumamosi Siku ya 1 ya wiki
  Jumapili Siku ya 2 ya wiki
  Jumatatu Siku ya 3 ya wiki
  Jumanne Siku ya 4 ya wiki
  Jumatano Siku ya 5 ya wiki
  Alhamis Siku ya 6 ya wiki*
  Ijumaa Siku ya 7 ya wiki
  Chanzo: Johnson 1939:160, Kamusi Teule ya Kiswahili, 2014, TUKI, 2013, BAKIZA, 2010.
  Huu ndiyo mpangilio wa siku za wiki katika kalenda ya Waswahili. Siku ya kwanza ya wiki, huanzia na Jumamosi na kuishia na Ijumaa. Mpangilio huu wa siku una changamoto nyingi. Miongoni mwa changamoto hizi ni pamoja na hizi zifuatazo;
  Kwanza, mapumziko ya mwishoni mwa wiki katika kalenda ya Waswahili, yako mwanzoni mwa wiki tofauti na kalenda zingine za mataifa mengine duniani kama tulivyoona huko nyuma. Mpangilio huu uko tofauti sana na wanaleksikografia wengi duniani wanaounga mkono hoja ya kuwa na mapumziko baada ya kazi mwishoni mwa wiki tofauti na ilivyo katika kalenda ya wiki katika lugha ya Kiswahili, (Concise Oxford English Dictionary 2004, Sinclair et al, 1979, TUKI 2013).
  Aidha, mtiririko huu, bado unawapa changamoto wataalamu na watumiaji wa kamusi za Kiswahili wanapokuwa na mitazamo kinzani ya mtiririko wa siku za wiki –siku ya kwanza hadi ya saba. Ni ipi siku ya kwanza, pili, tatu na hadi ya saba ya wiki katika utamaduni wa Mswahili? Mpaka sasa, kuna mvutano wa kimtiririko wa siku za wiki, japo majina na maana zenye ukakasi zikiendelea kubaki zilezile (J. S. Mdee et al (2011, TUKI 2013, BAKIZA 2010).
  Pili, siku ya sita katika kalenda ya Waswahili ni Alhamisi. Neno alhamisi, linatokana na neno la Kiarabu, Al khamsah lenye maana ya ‘-a tano’, (Darussalam Research Division, 2003, Rahman I., 2013). Swali la kujiuliza, mtu anawezaje kutoka siku ya tano – Jumatano na halafu akaenda siku hiyohiyo ya tano (Alhamisi) japo kwa jina tofauti? Hii inaonesha kuwa, kalenda ya Waswahili ya siku za wiki, ina siku mbili zenye jina moja lenye maana ileile japo linatamkwa na kuandikwa tofauti -Jumatano na Alhamisi. Yote haya, yana maana ya –a tano (siku). Hii ni changamoto ambayo inapaswa kutafutiwa ufumbuzi maalumu.
  Tatu, ndani ya kalenda hii, hakuna siku ya sita ya wiki kama ilivyo kwa kalenda za mataifa mengine. Waswahili tuna siku ya kwanza hadi ya nne. Siku ya tano kimaana, ziko mbili na halafu baada ya hapo, tuna siku ya saba tu. Kimaandishi, inaonekana kama kuna siku ya sita (Alhamisi), lakini kimaana ni siku ya tano, na hivyo kutokuwa na siku ya sita kwa maana ya jina.
  Nne, siku ya Ijumaa inayoonekana kuwa ni siku ya Saba katika kalenda ya Waswahili, nayo ina mkanganyiko mkubwa wa kimaana. Ijumaa ni neno lenye, asili ya neno-kitenzi katika lugha ya Kiarabu – (jamaʿa), likiwa na maana ya “kukusanyika, kukutana au kujumuika pamoja”. Waswahili walilitohoa neno “Al-Jumu’ah” na kuliandika kama Ijumaa – (Friday) –siku ya kukusanyika, kukutana au kujumuika pamoja na aghalabu katika ibada ili kuifanya siku hiyo iwe ni siku ya mwisho wa wiki. Pamoja na kuifanya siku ya Ijumaa kuwa ni siku ya Saba kwa kufuata kalenda ya Waswahili, bado kuna mkanganyiko mkubwa kimtiririko na kimaana katika majina ya siku za wiki katika kalenda hii.
  Tano, pamoja na siku za Alhamisi na Ijumaa kuwa ni siku za mapumziko katika siku za nyuma kwa mataifa mengi ya Kiislamu, hadi kufikia karne ya 21 kuna mataifa mawili tu –Irani na Afughanistani yanayoiadhimisha Alhamisi kama nusu siku ya mapumziko na Ijumaa kama siku nzima ya mapumziko. Mataifa mengi yenye itikadi za namna hizo, yameshafuata mfumo na utaratibu wa mapumziko ya siku za mwisho wa wiki –Jumapili na Jumamosi pamoja na kwamba, Ijumaa ni siku ya makutano ya ibada kwa mataifa hayo.

  Mwisho
  Ukweli uko bayana, licha ya kung’ang’ania udini wetu. History does not cheat!! Biblia inasema kuwa siku ya kwanza ya wiki ni jumapili na siku ya saba(sabato) ni jumamosi. Historia nayo iko bayana kiasi kile. Hakuna haja ya watu kuhangaika na kalenda za kizushi za leo. Wanapaswa kurejea kwenye kalenda ya Mungu mwenyewe. Kalenda ya siku saba, kila siku ikiwa na saa 24 tu. Ni vizuri tukaelewa kuwa, mwezi una siku 30 na mwaka una siku 360 tu na si vinginevyo. Hii ndiyo kalenda ya Mungu. Tofauti na kufanya hivyo, kufuata mafundisho ya wanadamu na kuiacha amri (neno) ya Mungu, jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha yetu ya baadaye.
  Neema ya Bwana iwafunike
  Siyi

 5. Utangulizi
  Kuna makundi makuu mawili ya nadharia zinazoelezea chimbuko la dunia. Kundi la kwanza ni lile la wayakinifu (materialists) –linaloamini kuwa, dunia na vyote vilivyomo, vilitokea kutokana na migusano au mimeguko ya mada, mabadiliko ya viumbe n.k. Kundi hili hujumuisha wanasayansi na wanafalisafa mbalimbali. Ni kundi la wanauhalisia. Kundi la pili ni lile la wadhanifu (idealists) –linaloamini kuwa, dunia na vyote vilivyomo, ni matokeo ya kazi ya Mwenyezi Mungu. Wakristo, Waislamu na Wayahudi wote duniani, wanaunga mkono nadharia hii kwa kuamini kuwa, dunia na vyote vilivyomo, viliumbwa na Mwenyezi Mungu kwa muda wa wiki moja -siku sita za kazi na moja ya mapumziko. Nadharia zote hizi (udhanifu na uyakinifu), hutumika katika kufanyia tafiti mbalimbali. Katika makala hii, tutatumia kundi la pili la nadharia –ya udhanifu kuchunguza mada yetu husika. Tutachunguza kwa ufupi historia ya kalenda ya siku za wiki kama inavyooneshwa na kundi hili la nadharia tangu uumbaji hadi sasa.

  Mwanzo wa Kalenda ya Siku za Wiki.
  Kwa mujibu wa nadharia ya uumbaji, dini kubwa duniani kama vile Ukristo, Uislamu, Ahmadiyya, na Uyahudi kwa asilimia kubwa, zinaamini kuwa, dunia na vyote visivyoonekana na vinavyoonekana juu ya uso wa dunia, vilitokana na uumbaji wa Mungu (Biblia-Mwanzo sura ya 1 na ya 2; Kur’an 11:7). Kwa upande wa dini ya Ubudha na Uhindu wao baadhi ya madhehebu yao, wanaamini uibukaji na baadhi wanaamini uumbaji. Kwa kufuata nadharia hii ya uumbaji, historia inaonesha kwamba, mfumo wa kalenda ya siku saba za wiki, uliasisiwa na Mwenyezi Mungu baada ya kuiumba dunia na kuwapa wanadamu wa kale walioishi ili wauendeleze. Haukuwa mfumo wa kalenda kama ulivyo kwa siku za leo, bali ulikuwa ni utaratibu ambao jamii za kale zikiwa kwenye makazi yake –zilikuwa na utaratibu huo wa kusoma majira ya siku. Siku za wiki hazikuwa na majina rasmi isipokuwa siku moja kama tutakavyoona huko mbele. Kabla ya maandishi kugunduliwa, inaaminika kwamba, watu hao wa kale, walitumia jua, mwezi na nyota katika kusoma majira ya siku. Utaratibu huo uliendelea kwa kipindi kirefu na katika jamii nyingi za wanadamu, hadi maandishi yalipogunduliwa, (Samuel, 1963, Encyclopedia Britannica Online; Retrieved on Januari 2015).

  Kalenda ya Wasuma na Waakadi
  Imegundulika kuwa, jamii za mwanzo kutumia kalenda ya siku za wiki, zilikuwa ni jamii za watu wa Mesopotamia waitwao Wasuma na Waakadi. Watu hawa waliishi kaskazini na kusini mwa mito ya Tigrisi/Hidekeli na Frati katika nchi ijulikanayo kwa leo Iraki mnamo miaka ya 4000 K.K., baada ya gharika ya Nuhu. Jamii hizi za Wasuma naWaakadi zilijulikana kwa jina maarafu la mji wa sehemu waliyokuwa wanaishi – Babeli na hivyo jamii hizo kujulikana kama Wababeli. Wababeli waliishi kwenye nyumba zao za udongo zilizokuwa zimejengwa karibu na mahekalu chini ya utawala wa makuhani (viongozi wa dini). Wababeli walikuwa wakitumia kalenda ya Biblia ambayo ni kalenda ya siku saba za wiki ikianzia siku ya kwanza ya wiki, (Samuel, 1963, Meyer, P. 2005).
  Hadi kufikia karne ya 6 K.K. mpaka karne ya 4 B.K. mataifa mengi yaliyofuata baada ya Wababeli, (isipokuwa machache kama vile Ugiriki, Uturuki, Ashuru, Misri n.k.), yalikuwa na mifumo na kalenda ya siku za wiki tofauti na ilivyokuwa kwa Wababeli. Kwa mfano, mataifa mengine kama vile Wamaya walikuwa na wiki za siku 13 hadi 20, Wamisiri walikuwa na siku za wiki 10, Wajapani na Wakorea walikuwa na siku za wiki 10, Waakani (Nigeria) walikuwa na siku 6 za wiki, Wayaveni (Indonesia) walikuwa na siku 5 za wiki n.k. (Bartle, P. 1978). Mkanganyiko huo wa kalenda tofautitofauti za siku za wiki kwa mataifa hayo, ulikuja kufanyiwa marekebisho na dola ya Rumi ilipoitawala dunia kuanzia mwaka 68 K.K hadi mwaka 538 B.K. Ndani ya kipindi hicho mnamo mwaka 321 B.K. chini ya utawala wa Mfalme Constantino I, mfumo wa siku 7 za wiki kama ulivyokuwa kwa Wababeli, ulirejeshwa tena, (Meyer, P. 2005).

  Kalenda ya Wiki ya Warumi
  Rumi ilipoitawala dunia, mifumo na taratibu za kalenda za siku za wiki za Babeli vilirejeshwa. Idadi ya siku za wiki ilikuwa ni ileile ya zamani, japo kwa kipindi hicho, siku zilipewa majina ya mkopo. Pamoja na mvuto wa Rumi kwa mataifa mengi yaliyokuwa chini yake kufuata utaratibu huo wa kalenda ya siku saba za wiki, baadhi ya mataifa mengine yaliendelea na kalenda zao hadi mwanzoni mwa karine 20 B.K. Mfano, Umoja (wa zamani) wa nchi za Kisovieti ulikuwa na kalenda tofauti ya siku za wiki. China na Japani zilikuwa na siku 10 za wiki, n.k. (Efstratios T. et al, 2011). Na ilipofika mwishoni mwa karne ya 20, mataifa karibu yote duniani, yalikuwa yakitumia utaratibu wa siku 7 za wiki, ambao uliokuwa ni matokeo ya jitihada zaidi za wafalme wengine wa Kirumi waliofuata baada ya Constantino I (Flavius Valerius Aurelius Constantinus Augustus; (272 – 337)).
  Urejeshaji wa kalenda ya siku 7 za wiki uliofanywa na mfalme Costantino I, haukuwa tofauti na kalenda ile ya Wagiriki. Wagiriki waliziita siku za wiki kwa kutumia majina ya sayari, ambazo kwa Wagiriki, ilikuwa ni miungu iliyoabudiwa, japo ilipewa hadhi tofauti. Kwa Wagiriki siku za wiki zilijulikana kama ‘siku za miungu’ (theon hemerai -days of the gods). Majina ya siku za wiki yalitolewa kwa kufuata hadhi za miungu yao –kuanzia mungu mkuu kuelekea mungu mdogo. Siku ya kwanza ya wiki, ilipewa hadhi ya jina la mungu mkuu wa Kigiriki. Siku ya mwisho wa wiki, ilipewa jina la mungu wao mdogo. Mungu mkuu wa Wagiriki alikuwa ni sayari jua ambaye alipewa hadhi ya siku ya kwanza ya wiki: hemera heli(o)u: siku ya jua. Siku ya pili ya wiki waliita kwa jina la mungu wao anayefuata baada ya jua –sayari mwezi hemera selenes – day of the moon: siku ya mwezi. Siku ya tatu ya wiki iliitwa hemera Areos/ Tiw/Tyr – day of Ares: siku ya mungu wa vita. Siku ya nne iliitwa hemera Hermu – day of Hermes: siku ya mungu hermes, mungu wa biashara. Siku ya tano iliitwa, hemera Dios – day of Zeus: siku ya mungu wa anga au mbingu (ngurumo). Siku ya sita iliitwa hemera Aphrodites – day of Aphrodite: siku ya mungu wa mapenzi na urembo. Na siku ya saba iliitwa, hemera Khronu – day of Cronus: siku ya mungu wa kilimo na aliyekuwa mtawala wa ulimwengu wote kabla ya kuondolewa na mungu zeus. (Webster’s Dictionary;1989; William M., 1975; Morris, W. 1976).
  Kwa upande wa Warumi, wao walizitafsiri maana za majina ya siku za wiki kutoka kwa Wagiriki. Majina yaliyotafsiriwa kutoka lugha ya Kigiriki kwenda Kilatini yalianza kwa mpangilio na mtiririko uleule wa lugha chanzi – Kigiriki. Siku ya kwanza ya wiki kwa Kilatini ilitafsiriwa kwa jina la sayari jua – dies solis ( > Sunday). Siku ya pili ya wiki ilitafsiriwa kwa jina la sayari mwezi dies lunae (> Monday). Siku ya tatu iliitwa siku ya sayari Mirihi – dies Martis: (> Tuesday). Siku ya nne iliitwa siku ya sayari Utaridi – dies Mercurii (> Wednesday). Siku ya tano iliitwa kwa jina la sayari Mshtarii – dies Jovis (>(Thursday). Siku ya sita iliitwa kwa jina la sayari Zuhura – dies Veneris (>Friday), na siku ya saba iliitwa kwa jina la sayari Zohali – dies Saturni- (> Sartuday). (Online Encyclopædia Britannica; Webster’s Dictionary;1989).
  Aidha, lugha zenye uhusiano na lugha ya Waingereza (Anglo-Saxon languages) nao waliiga mfumo wa uandishi wa majina ya siku za wiki kutoka kwa Warumi kama walivyofanya Warumi kutoka kwa Wagiriki. Waingereza na lugha zingine zenye uhusiano na Kiingereza, nao walichukua majina ya siku za wiki kama yalivyo na kuyatafsiri yote kuanzia siku ya kwanza ya wiki hadi siku ya saba. Maana za majina ya siku za wiki kwa Kiingereza zilikuwa sawa kabisa na zile maana za majina hayo kwenye lugha ya Kigiriki na Kilatini. Bila ya kupoteza maana za msingi, Waingereza waliyatafsiri majina ya siku za wiki. Kuanzia kwa Wagiriki, mtiririko ulikuwa kama ifuatavyo;
  Mpangilio na Maana za Majina ya Siku Saba za wiki Kigiriki – Kiingereza
  Kigiriki Kilatini Kiingereza Fasili yake
  1. hemera heli(o)u dies solis Sunday(sun+day) siku ya mungu jua
  2. hemera selenes dies lunae Monday (moon+day) siku ya mungu mwezi
  3. hemera Areos dies Martis Tuesday (Tiu or Tīw+day) siku ya mungu wa vita
  4. hemera Hermu dies Mercurii Wednesday (Woden+day) siku ya mungu mlinzi/kiongozi
  5. hemera Dios dies Jovis Thursday (Thor+day) siku ya mungu wa ngurumo
  6. hemera Aphrodites dies Veneris Friday(Freia/frigus..+day) siku ya mungu frigga (mahaba)
  7. hemera Khronu dies Saturni Sartuday(saturn+day) siku ya mungu mtawala/kilimo
  Hivyo basi, pamoja na majina ya siku kubadilika kutoka kwa Wagiriki hadi kufikia kundi la lugha zenye uhusiano na Kiingereza (Anglo-Saxon languages), maana za majina hayo hazikubadilika mpaka leo. Aidha, katika kamusi na insaiklopidia (agh. za zamani) za Kiingereza bado mpangilio na maana za majina ya siku za wiki havijabadilishwa. Bado siku ya kwanza ya wiki ni Sunday (Jumapili ya leo) na siku ya saba ni Sartuday (kwa leo Jumamosi) (J. M. Sinclair et al, 1979, Online Encyclopadia Britanica).

  Itaendelea…

 6. MCHANA WAPENDWA MCHANA HUWA NA SAA KUMI NA MBILI NA USIKU KUMI NA MBILI

  YOHANA 11:9
  “YESU AKAJIBU, JE! SAA ZA MCHANA SI KUMI NA MBILI? MTU AKIENDA MCHANA HAJIKWAI; KWA SABABU AIONA NURU YA ULIMWENGU HUU.”

 7. KAMA MKRISTO ATAWEZA KUHESABU SIKU TATU ZA USIKU NA MCHANA NI ZIPI ALIZOKAA YESU KABURINI,BASI ATAKUWA AMEWEZA KUTAJA MAJIRA YA SIKU YA BIBLIA.

  MATHAYO 12:40
  “KWANI KAMA VILE YONA ALIVYOKUWA SIKU TATU MCHANA NA USIKU KATIKA TUMBO LA NYANGUMI, HIVYO NDIVYO MWANA WA ADAMU ATAKAVYOKUWA SIKU TATU MCHANA NA USIKU KATIKA MOYO WA NCHI”

  SIKUTATU ZAUSIKU ZIPI? NA
  SIKU TATU ZA MCHANA ZIPI?

 8. MATUNDA 9 ELIYA.
  Naona roho ya MUNUO imekung’ang’ania sana mpaka hujitambui.Hiyo kalenda uliyotuonesha ni KALENDA YA Munuo mchaga!! Hebu niambie Mlichoshinda SILOAM ni nini. Munuo ALIWADANGANYA alimuua SHETANI 2008 na ninyi kuonesha MMEPOFUSHWA MACHO mkaamini huo UKENGEUFU wa kutisha.Badaye Munuo akawadanganya kuwa yeye ni Adamu wa Pili Mkaamini….nk. HAYO NDIYO SILOAM MMESHINDA? Leo unataka Kutupumbaza na sisi kuwa ETI HIYO Kalenda uliyoitaja ni ya MUNUO.
  Shame on you!!

 9. Matunda 9 Eliya,

  Umenukuu vifungu vya Biblia vinavyoyataja majina ya miezi, lakini nilikutegemea utuoneshe pia hiyo miezi, kwa mfano Adari, umejifikishaje ktk ufahamu kwamba huo ndio mwezi wa 12, kwa kigezo kipi?

  Na kwamba mwezi una siku 28, mmetumia kigezo gani kujua hilo?

  Pia siku, ya 3 ni ipi kwa leo na unajuaje kwamba ndiyo hiyo?

  Halafu siku zenu zinaanza saa ngapi, jioni kama wenzenu Wasabato au saa ngapi haswa?

  Gbu!

 10. NAUNGANA NA SHILO SILOAM YA KWAMBA KALENDA SAHIHI NI KALENDA YA MTUME ELIYA YA KANISA LA SILOAM YA KWENYE KITABU CHA NENO{BIBILIA] . NITATOA UFAFANUZI MRAISI TU ILI WASOMAJI MPATE KUELEWA.
  1. KWANZA NI WAZI KUWA WIKI MOJA INA SIKU 7 TU
  2. MWEZI MMOJA UNA WIKI 4 TU.
  Hivyo mwezi mmoja una siku 7×4 = 28. Kwa maana hiyo mwaka mzima wenye miezi 12 una siku 336 tu. Hii ndiyo calendar sahihi ya Mungu iliyoandikwa kwenye kitabu cha NENO (BIBILIA). Pia calendar ya Mungu ina majina ya siku zilizotamkwa na Mungu mwenyewe ambazo ni siku ya 1,2,3,4,5,6 na 7 na sio siku ya jumatatu- jumapili (Mwanzo 1:1-31 na Mwanzo 2: 2-3). Pia kalenda ya Mungu ina miezi yenye majina yaliyotamkwa na Mungu mwenyewe ambayo ni:- MWEZI WA 1- ABIBU / NISANI ( Kutoka 12:2, 23:15, Nehemia 2:1), MWEZI WA 2- ZIVU (Mwanzo 8:14, 1Falme 6:1), MWEZI WA 3 – SIWANI ( Kutoka 19:1, Esta 8:9), MWEZI WA 4- TAMMUZI ( 2Falme 25:3-7), MWEZI WA 5- ABU ( Hesabu 33:38), MWEZI WA 6 – ELULI (Neh 6:15), MWEZI WA 7 – ETHANIM ( Mwanzo 8:4, 1Falme 8:2), MWEZI WA 8 – BULI (Zakaria 1:1, 1Falme 6:38), MWEZI WA 9- KISLEU (Ezra 10:9, Nehemia 1:1), MWEZI WA 10- TEBETH (Esta 2:16), MWEZI WA 11- SHEBATI ( Zekaria 1:7), MWEZI WA 12 – ADARI (Esta 3:7, Ezra 6:15) na sio mwezi January- December. Siku za Jumatatu- Jumapili na Miezi ya January – Desemba sio majira ya Mungu bali ni majira ya dunia na ulimwengu yaliyoanzishwa na papa Gregory wa 12 na aliitangaza kalenda hiyo mwaka 1582 na ni kalenda ya FREE- MASON bila kuficha. Na ukweli ndio huo. KANISA LA SILOAM TUMESHINDA NA ZAIDI ya kushinda kwakuwa tumeijua kalenda sahihi ya MUNGU WA KWELI KUPITIA UFUNUO WA MJUMBE WA MAPENZI YA MUNGU ELIYA ADAMU WA PILI MUNGU WA MAJESHI. KWAKWELI TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUWA SASA TUNAISHI KWA KUIFUATA KALENDA YA MUNGU. LEO HII WAKATI DUNIA WANASEMA NI TAREHE 14/1/2015 SISI KANISA LA SILOAMU TUKO TAREHE 15, ZIVU MWAKA WA 4 WA UKAMILIFU, YAANI TUKO JUU YA YOTE, VYOTE NA WOTE.

 11. Lani,
  Ni wapi ktk Maandiko ilipofundishwa kwamba siku huwa inaanza saa 12 jioni na kumalizika saa 12 jioni inayofuata?

  Gbu!

 12. BIBLIA NDIYO INA KALENDA YA KWELI
  YAANI;
  -KILA MWEZI HUWA NA SIKU 30
  -MWAKA UNA SIKU 360
  -JUMA HUANZA JUMAPILI NA KUISHA JUMAMOSI
  -SIKU HUANZA SAA 12 JIONI NA KUISHA SAA KUMI NA MBILI JIONI KESHO YAKE.

 13. KALENDA SAHIHI NI YA BIBLIA

  -YAANI KILA MWEZI KATIKA MWAKA UNA SIKU 30
  -MWAKA MZIMA UNA SIKU 360
  -SIKU YA KWANZA YA JUMA IKIWA NI JUMAPILI NA YA SABA JUMAMOSI

  LAKINI TUKUMBUKE KUWA MAJIRA YALIBADILISHWA NA UTAWALA WA KIRUMI

  “NAYE ATAAZIMU KUBADILI MAJIRA NA SHERIA” DANIELI 7:25

 14. Bwana yesu asifiwe kalenda ya 2015 tunayotumia iko sawa kwani alipozaliwa huyu mwanaume YESU kalenda iliyokuwa inatumika ikafutwa na kuanza upya hawa wanaotaka kushinda na kalenda ya kumkumbuka YESU hawawezi kwani YESU jina lake linapita majina yote jina lake li hai likitajwa hata leo shetani anatetemeka hivyo waasisi walioona ni mhimu wakanza upya kalenda hawakuwa wajinga bali hekima ya MUNGU iliwaongoza amina

 15. Nimefatilia kwa makini majira (calendar) ya mtume Eliya nimeona iko sahihi na biblia Hakuna calendar nyingine iliyo sahihi. Ahsante

 16. hii ya!2015 ikosawa
  ndg zetu watoto wa
  kijakazi hupenda ligi.
  ( mashindano )&watoto
  wa mungwana. wana wa
  AHADI.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s