Je, Hivyo Siyo Kuwaombea Waliokufa?

PrayerSiku hizi kwenye mitandao kumeibuka tabia, ambayo hata wakristo wanaifanya,  ya kuweka picha ya mtu aliyekufa zamani mfano Mzazi, Kaka, Dada au rafiki wa karibu. Halafu akishaweka picha hiyo anaandika kuonyesha mtu huyo alikufa ni mwezi umepita, mwaka au miaka kadhaa.. Maneno ya wasoma wanaochangia kwenye picha hiyo mengi huwa ni R.I.P na baadhi ni maneno ya kuonyesha wanavyomkumbuka au jinsi pengo lake lisivyozibika.

Kitendo hiki cha kuweka picha ya mtu ambaye ameshakufa kisha anaombewa RIP kwa upya kinaweza kufananishwa na IBADA YA KUOMBEA WAFU ambako kufanywa na baadhi ya Imani za dini mbali mbali duniani huku Neno la Mungu likisema kuwa “Baada ya Kufa ni Hukumu” (Ebr 9:27).

Una maoni gani kuhusu tabia hii?

Advertisements

61 thoughts on “Je, Hivyo Siyo Kuwaombea Waliokufa?

 1. CK !?
  Mie mzima sana bro,
  Kwa kweli hapa sijakuelewa kabisa nini umekusudia kunifundisha, unajua elimu yako iko juu sana hivyo unapoongea na mtu unaejua kuwa ni ‘mpumbavu’ na ni mjinga basi shuka chini kidogo ili unipate kwaajiri ya Kristo, bro!!

  Kweli gani unayoizungumzia ambayo ninaikataa? Nimesema tujifunze Pendo, kwa urefu upana na wimo wake ili tuweze mjua Mungu wetu kwa usahini, wewe unasema Pendo ni “Porojo” Bro nnaomba ufafanuzi ktk hilo! Kama huwezi kuelewa na kuamini kuwa Jehovah yumo ktk Utatu basi sina la kukushawishi kwani Yesu Bwana ndie aliefundisha hayo kwa upana sana. Nimesema Roho mtakatifu ni ile Pumzi aliyopuliziwa Adam toka kwa Yesu, na m-Adam anapokosa kumtii Yesu, huyo Roho huondoka na huyu m-Adam huwa maity anaeishi sawasawa na wale wengine wanaongojea R.I.P (Ndivyo Adam alivyokuwa! Alipokula tunda yaani alipokaidi “NENO, usile” Roho akamuacha hivyo akawa maity mbaka siku alipokamilisha kama wale wengine akawekewa R.I.P! fahamu kwamba Mungu alimwambia ‘siku utakapokula utakufa ‘hakika’ na ibilisi akamwambia hiyo sio KWELI !! Je wewe CK unaona kati ya Mungu na ibilisi ni nani aliesema KWELI!?? Kwa akili zako ni ibilisi! maana Adam hakufa alipokula tunda aliendelea kuishi, hivyo kwa mtazamo wako, Mungu ni Muongo na ibilisi ni mkweli !! si ndio kweli hiyo unayoisema bro ??? )

  Nnaomba unielimishe kwa kifupi/kirefu, nikubali nini ili nisiwe mjinga tena!!?? Mimi nnaamini ktk kujifunza NENO sana tu, ila nnaamini NENO la Yesu lina Madarasa, kuna La kwanza hadi University Ebrahia5:12-14 endelea 6:1-3, na kwa mujibu wa NENO, PENDO ndio Chuo Kikuu Cha Elimu Warumi13:8 -11 (tukiujua wakati!) !! Sasa sikatai kuwa huenda ktk macho yako mie ni mpumbavu na mjinga wa mwisho maana nnaamini ktk ‘Porojo’ (vile mnavyoliita PENDO!) je haiyumkiniki kwamba hesabu moja ukiwapa darasa la kwanza na hesabu hiyohiyo ukiwapa wa Chuo Kikuu watakupa majibu sahihi ambayo ni tofauty!? Haikuiingii akilini kuwa wale wa Chuo Kikuu wanayajua majibu ya darasa la kwanza ila wa darasa la kwanza huona wale wa Chuo wamekosea !?? CK, ndivyo elimu ya PENDO ilivyo.

  Hebu tujadiliane kama ndugu, mbona mnatanguliza vifua vyenu mbele!? Wa mbele yetu ni Yesu peke yake, nasie wote na kina Paulo, na kina Petro tuko back low, mabishano yasiona maana hayatufai sisi tunaopaswa ‘kuutambua wakati’

  CK bro, hebu tuulizane maswali kama watu wazima wenye kumtafuta Mungu kwa dhati na wala sio usungura sungura!

  Asalaam aleikum.
  Jackson.

 2. Mulele,

  Hujambo kaka?

  “Ujinga” ni hali anayokuwanayo mtu yeyote yule asiyeijua “Kweli” ya jambo fulani, hata jambo hilo likiwa ni Injili!

  Nao “Ujinga” hukoma pale unapoikubali “Kweli” ya jambo hilo. “Porojo” ni “Ujinga” uliokubalika kwamba ndio “Kweli” kabla ya kuijua hiyo “Kweli”. Lakini unapokutana na hiyo “Kweli”, kisha ukaikataa kwa kuipenda hiyo “Porojo” na misisimko yake, jambo hilo hukuingiza ktk hatua ya mbele zaidi isiyo na tiba, ndio huo “Upumbavu”; hapa ndipo wengi wetu tunapopigwa “Chapa ya Mnyama”!!!

  “Pendo” unalolisoma ktk Injili linahusiana na Mungu, yeye ndiye hilo Pendo. Kwahiyo sharti yeye awe ndani yako, ndipo atajidhihirisha yeye mwenyewe kwa hilo Pendo alilo! Ndio maana ninakushangaa unaponiambia “”Lakini fahamu bro, hakuna sehemu yoyote ktk majadiliano haya nilipo tamka kwamba mimi nnalo PENDO au mimi ni Mkiristo”; kwahiyo unakiri kwamba unazungumzia jambo usilolijua kana kwamba unalijua – hii ndio inaitwa “Porojo”, ndio ule ujinga!!!

  Vinginevyo basi chukua hiyo “Kweli” uibadili na hiyo porojo ili umjue Mungu ktk uhalisi wake na si hizo porojo za, “””Na Jehovah ni holy Trinity :1: God Father :2: God Son :3: Holy Spirit hii ya tatu ndio tuna share with HIM””” Haya ni mambo ya kufikirika, hayakuondelei “Ujinga” bali yanauimarisha ili ukomalie ktk upumbavu maana ni mambo yanayotokana na UONGO, nao uongo twafahamu unatokana na Ibilisi, Maandiko yanasema kwamba huyo ndiye “baba wa uongo”, hata ukiwa ni wa kidini!

  Kuhusu “Uongo”, hebu utazame huu usemi unaweza kukusogeza ktk ufahamu:
  “Lies are created by the Envious, repeated by the Stupids, and believed by the Idiots”

  Gbu!

 3. Inasemekana mungu wao si Mungu wetu kwahiyo hata amani inaweza kuwa siyo amani ile ya Kristo,lakini twendeni hivyohivyo tutafika

 4. Msanjila eh!?
  Ni kama kukuita jina lako Christmas au Jul au Weihnachten au Navidad au Krismas badala ya Noel !! Yoooote hayo ni jina lako moja yaani Noel ila ni ktk lugha tofauty!! Asalaam aleikum ni salaam ambayo Bwana Yesu pekee ndie aliekuwa na maana halisi anapoitamka!! Shalom ni Amani ni Salaam!! Wazungu wametunyunyuzia chuki ktk elimu zao juu yetu !! Ndio maana nikikutakia Amani kwa ki-Arabu unahisi ‘ukakasi’, unakheri wewe Msanjila kwa sababu umetamka KWELI yako, wengine wanaogopa wenzao ila wamo tuu, utawasikia wakijibu hivyo hivyo ki-UKKAKASI-kakasi 🙂 🙂

  Ukisoma maelezo na majibu yangu ktk mada tofauty hapa SG, utaona msisitizo wangu ktk Pendo na elimu yake kama NENO linavyo tutaka tujifunze na kisha tuwe nalo tele, lakini inatisha sana pale uonapo wakufunzi wanajibu kwamba Pendo ni ‘porojo’ na tena zinawafaa ‘wajinga’ dah!

  Nnakwambia na wewe Msanjila, kwa Mungu hakuna Njia ya ‘wengi’ hivyo usijiunge ktk ‘hatujakufahamu’!! niulize ni nini hujanifahamu kama wewe??

  Tuwe na elimu ya kujua kuwa elimu ya Yesu pekee ktk falsafa ya kumtafuta Mungu kuwa inayo madarasa!! Darasa la Kwanza, la Pili, la Tatu hadi la Saba! unafanya mtihani alafu unaingia kidato cha Kwanza, cha Pili cha Nne unafanya mtihani! Unaingia cha Tano cha Sita! Unafanya mtihani wa kuingia Rumi 12:10 ambayo ilitokana na Ebrania5:11 hadi Ebrania6:1-3 na hayo ya Mizimu tutayafanya Mungu ‘akitujalia’ sio ‘Msingi’ brother Noah !!

  Kama hujanielewa niulize bila kupitia kwa ‘Mulele, sisi tunakutaka……..’ Nikawaambia miongoni mwa ‘sisi’ yumo ibilisi, ‘WA’kaniuliza ibilisi ni mwanamke au ni mwanaume? ‘Wa’kanishinda 🙂 🙂
  Usiwe miongoni mwao bro! Kwani Injiri ni Habari Njema kwa sikio moja moja !!

  Kama Navidad ina ukakasi, basi Shalom brother Emmanuel (Krisimasi, Noel) 🙂 Rumi14:14

  Nduguyo
  Jakisoni.

 5. Aleikum wa asalaam Bro. Lwembe, (=Amani iwe juu yako pia!)
  Oh, ahsante sana kwa elimu, na samahani sana kwa ujinga wangu wa kutofahamu, lakini si ndivyo tunavyopaswa kujifunza bro ? Lakini fahamu bro, hakuna sehemu yoyote ktk majadiliano haya nilipo tamka kwamba mimi nnalo PENDO au mimi ni Mkiristo, ila msisitizo wangu mara zooooote ni TUJIFUNZE PENDO ili tupate kumjua Mungu wetu kwa USAHIHI bila ya kuudai UKRISTO wa kuzaliwa au wa kurithi! Kumbe maskioni mwenu ni ‘porojo za pendo’!? dah!? Samahani sana bro, ‘nnawakwaza’ !! Mie nnaona nnatoa hoja nzito za kuigeuza ‘dunia’ kumbe ‘kwenu’ ni porojo za kijiweni !? Hoii !!

  Nimejitahidi kushawishi hili, ili kwamba tuwe WAMOJA lakini nnaona nnaeleweka na kutafsirika vibaya ‘kwenu’. Nnaomba mnisamehe ndugu yenu, sana kwa tabia yangu ya ubishi na kung’ang’ania jambo.
  Ahsante sana bro kwa kunisamehe kwa niaba ya ‘wenzio’.

  Asalaam aleikum!

 6. Mulele, waleikum salaam! (??)

  Pendo ni tabia ya Mungu; Mungu ni Pendo. Kwahiyo porojo za “Upendo” ni nzuri na zenye kupendeza ktk vijiwe vya dini, lakini yeyote anayesema anao Upendo, huyo ni dhahiri anatuambia kwamba anaye Roho wa Mungu ndani yake.

  Naye Roho wa Mungu ndiye aliyeiandika Biblia, basi inashangaza sana unapokutana na mkristo anayedai kuwa na Pendo, yaani yule Roho wa Mungu, halafu anatiririsha mafundisho ya ajabu kama haya:
  “””Mjema!!?? Kwa taarifa yako maana ya Holy Spirit ni ile Pumzi aliyopuliziwa babaako!! Na Jehovah ni holy Trinity :1: God Father :2: God Son :3: Holy Spirit hii ya tatu ndio tuna share with HIM”””
  Mambo haya kimsingi yanaashiria kwamba mkristo huyo ni mwanajumuia wa mojawapo ya Cults za “kikristo”, kwahiyo ni mtu anayepaswa kuombewa ili akombolewa kutoka mikono ya uharibifu kabla hajakubuhu ktk hayo mafundisho yenye kufisha na hivyo Mungu kumhesabia pamoja na wenye kufuru kwa kumsingizia RM mafundisho yaliyojaa kifo kama haya!!!

  Mulele, unaweza kuwa kwa ujinga umechagua kifo bila kujua; maana Paulo anasema kwa uhakika kwamba, ukifundisha injili tofauti na waliyoifundisha wao, basi na ULAANIWE; ndipo kwa mambo haya ya ajabu unayoendelea nayo, inaweza kukugharimu sana huko mbele; jiepushe nayo!

  Kuhusu Sungura, kwa kadiri ninavyoisikia sauti yake, ile authority, sijawahi kufikiria kuwa ni mwanamke! Hebu recharge your receptors, inaonesha ziko chini saaaana, almost street corner type, mpaka unapoteza maana ya majadiliano yenye kuujenga mwili wa Kristo!

  Asalaam aleikum!

 7. Sungura,
  Kwanza naomba samahani kwa matusi yooote uliyonitukana, unisamehe dadaangu mdogo, na pili, jifunze kwamba ktk kumuendea Mungu usihusishe ‘sisi’, ktk wengi yumo shetani !!
  Sasa ukiwa kama Sungura, naomba uniulize swali dada :p
  Asalaam aleikum. (ina maana: Amani iwe juu yenu)

 8. Mulele,

  Nafikiri kuna jambo la msingi unatakiwa kututhibitishia.

  Tuambie ni kwa jinsi gani Mungu aliumba wañadamu mara mbili, yaani wa-mataifa na kisha Adamu.

  Maana mimi naamini umekosa tu kuelewa pale Mungu alipokifanya kwanza kila kitu ktk ulimwengu wa roho na kisha baadae akaja kuvidhihirisha ktk mwili.

  Haya uwanja ni wako.

 9. Mulele,

  Naomba tusizoene na kukoseana heshima kipumbavu, hii ni public platform.

  Kama unachangia hoja changia hoja, sio kila ukichangia unanitajataja kipuuzi kwa mambo yasiyo na tija.

  Kumbuka rules and conditions za matumizi ya uhuru wako wa kuchangia kwenye mtandao zina-apply.

  Kama kuna kitu kinachohusiana na mada nimechangia ukaona hakiko sawa, nipinge kwa mujibu wa utaratibu unaokubalika.

  Kama wewe unadhani unamwelewa Mungu kuliko akina sisi, ungetuambia habari ya umebatiza waislam wangapi huko Zanzibar, siyo maneno yenye dhihaka.

  Ufalme wa Mungu siyo manenomaneno tu, ni nguvu, na kazi yenye matokeo.

  Unataka kila wakati tuongee kama tuko kwenye kijiwe cha bao, wakati unajua hapa tunapaswa kusema mambo yatakayosaidia maisha watu?

  Hebu sema katika sehemu hizo mbili ulizonitaja hapo juu, kuna neema gani ya kumsadia asomaye hayo maneno uliyonitaja kwayo?

  Please naomba ukue ktk ufahamu wako!

  Asante!

 10. Lani kakaangu!
  Wacha kudanganyika na kuwadanganya wenzio kaka!
  Hebu jiulize ktk hiyo mistari yote uliyoianisha je wewe uko sehemu gani wakati UNAPOSOMA SASA HIVI!? UMEKUFA au UMZIMA !!? Sasa mbona unachagua KUFA!!? We vipi bro !!?? Ingawa uchaguzi ni wa mmoja binafsi, lakini Bwana anatushauri “CHAGUA UZIMA ILI……” au usharogwa kama kina Sungura waliokatika fyuzi (Mwanamke gani ajiite Mkiristo anaeweza kukosa adabu kuliko huyo asie Mkiristo!? Mathayo 5:17 🙂 🙂 ?? Hey bro, huu ni uamuzi wa mtu binafsi na wala siwezi kuwalazimisheni kujifunza ! Lakini mfahamu kitu kimoja kuwa: Kama we ni mmoja wa viongozi wa familia, basi UCHAGUZI wako unao uwezo wa kuwa- influence familia yako kwa BARAKA zako, au kwa laana.

  Bro Msanjila,
  Ahsante sana, lakini amini usiamini kakaangu, tukilijua NENO ki usahini hata huko “kuombeana ndani ya Kanisa kutakoma”!!! Watu watajifunza kuwa WAZIMA na wala sio kuja ‘kununua kuombewa’ nao watakuwa WAZIMA na UTAJIRI wa halali kabisa kwa maana hiyo ndio HAKI ya WATEULE!! Kaa na indhari kuwa mambo ya HUKUMU hayalihusu Kanisa la Yesu (labda la kina Sungura) !!! “Sisi tunajua kwamba tumepita kutoka mautini kuingia UZIMANI kwa maana twa WAPENDA ndugu” Kumbe PENDO ndilo daraja la kutuvusha kuingia UZIMANI, “yeye asie PENDA akaa ktk mauti” 1John3:14 Kumbe mauti ni kinyume cha PENDO.

  Ingawa UFALME WA MUNGU umo ‘ndani yetu’ lakini ni lazima itumike NGUVU ktk kuuteka na wala sio kwa ‘porojo’ zilizo jaa humo mitaani.

  Tukijifunza PENDO na kulielewa tutakuwa na ELIMU juu ya kila kitu!
  “Lakini sasa inadumu IMANI, TUMAINI, na UPENDO, hayo matatu”

  Asalaam aleikum! (Amani iwe kwenu!)

  Jackson Mulele

 11. jackson zebedayo mulele nakuunga mkono A to Z ,hata kanisani unakuta familia nzima ukristo wao ni wakuzaliwa toka babu na bibi na vizazi na vizazi,hii ni hatari,hata kina petro,paulo nk walivuliwa na Yesu kutoka ktk dini zao na hata Yesu sababu ya kufa ni kuonekana analeta elimu ambayo haikuwepo duniani.Tena afadhali ya sasa angalau wokovu umeanza kupokelewa,watu wanaombewa badala ya kudhani kuwa uponyaji ktk biblia ni hadithi,kumbe ni kitu halisi.Kwahiyo mi nasema twendeni nao polepole watakubaliana nasi tu.Wasiwasi wangu na swali langu,endapo kama kuna imani ya dini au madhehebu fulani walikoseaga kumwabudu Mungu ktk taratibu za ubatizo,kuombea maiti nk,je MUNGU SIJUI ATAWAHUKUMU VIPI,je atahukumu vizazi na vizazi ,kama ni hivyo basi ndo maana Yesu alisema wateule ni WACHACHE

 12. JAPO BINADAMU HULALA YESU AMETULETEA UZIMA NA ATATUFUFUA SIKU YA MWISHO.

  AYUBU 14:12
  “NI VIVYO HIVYO MWANADAMU HULALA CHINI ,ASIINUKE; HATA WAKATI WA MBINGU KUTOKUWAPO TENA HAWATAAMKA.”

  1 WATHESALONIKE 4:16,17
  “KWA SABABU BWANA MWENYEWE ATASHUKA KUTOKA MBINGUNI, PAMOJA NA MWALIKO, NA SAUTI YA MALAIKA MKUU, NA PARAPANDA YA MUNGU; NAO WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA, KISHA SI TULIO HAI, TULIOSALIA, TUTANYAKULIWA PAMOJA NAO KATIKA MAWINGU , ILI TUMLAKI BWANA HEWANI; NA HIVYO TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE.”

  1 WAKORINTHO 15:52
  “KWA DAKIKA MOJA, KUFUMBA NA KUFUMBUA, WAKATI WA PARAPANDA YA MWISHO; MAANA PARAPANDA ITALIA, NA WAFU WATAFUFULIWA, WASIWE NA UHARIBIFU, NASI TUTABADILIKA”

  TUUHIFADHI UHAI WETU UBAVUNI PA YESU,NAYE ATATUFUFUA SIKU YA MWISHO.

 13. Brother Chriss, Suala la kujadili kama shetani ni mwanamke au ni mwanamme halitatusaidia lolote ktk kumjua Mungu wetu nami kwakweli sivutiwi na mazungumzo hayo ya ki-Sungura (samahanini!) Kwanini tusiulizane mambo ambayo yatainua elimu na Imani yetu ktk kumjua Mungu wetu!? 2Timothy2:19 “Lakini NENO la Mungu lasimama ktk muhuri hii ya kwamba, Bwana awajua walio wake” Kwanini tusitafute “kujulikana na Bwana”!?? Kwanini tujadili mambo ya Shetani!? Anatuhusu na nini? Bwana anasema Mathew11:29 “tujifunze kwake” na John14:15 Bwana anasema ‘Tukimpenda tutazishika AMRI zake’ na kwa mafundisho yake hajawahi kutufundisha kwamba ktk Yeye tutakufa!! Kumbukeni na mjue hili ndugu zangu siku zote kuwa Shetani hana neno lake mwenyewe, bali hutumia NENO lilo hilo la Bwana ili KUTUTEGA, nami nnasema tena kuwa: Kuna ushawishi wa Shetani (Ibilisi) ktk kila msatari unaotaja Kifo ktk biblia.

  Brother Chriss, wengi wetu tunafuata mkumbo ktk NENO la Mungu, wengi hudhani kuwa Bwana Yesu alileta na ni muanzilishi wa DINI ya KIKIRISTO !! Hili jambo Ibilisi amelishika kwa mkono wake wenye nguvu sana brother, sio kweli hata kidogo U-KRISTO SIO DINI BALI NI NJIA YA KUUENDEA UZIMA WA ‘MILELE’! Kama wewe umezaliwa ‘mkiristo’ babaako nae ‘mkiristo’ babu yako pia ‘mkiristo’ basi jiangalie sana ktk Bwana! Watu wa jinsi hii hudhania kwamba ‘wamepata neema kuzaliwa ktk DINI ya Mungu’ na wanabweteka wakijua kuwa wao wanaijua NJIA!! Huu ni mtego wa Ibilisi! 1Corrinthias10:11 NENO linasema ‘kama unadhani umesimama basi ujiangalie usianguke’ Mathew11:12 “Ufalme wa mbinguni hupatikana kwa NGUVU, nao wenye NGUVU watauteka” Hebu tujiulize swali jepesi tu, Kwanini watu walio ‘makanisani’ hu ubiriwa NENO la Mungu hilo hilo kila siku!? Je ni kweli NENO lina wabadilisha?

  Kuna watu wengi wasio ‘Wakiristo’ kwa aslili ambao wanaisoma sana biblia na kugundua kuwa HAKIKA YESU KRISTO NI BWANA maana hata vitabu vyao vinawadhibitishia hilo! Hao ni WENYE NGUVU!!!!! Mimi na wewe tumebakia kuulizana ety shetani ni mwanamke au mwanamume na kuambiana ‘shut up’ 🙂 maana kila mmoja anajua sana! 🙂 🙂

  Christoph kakaangu, bila kujitafity na kujua kama wewe ni wa Adam au ni mMataifa, safari ya kuuendea Ufalme ni ngumu kwa YEYOTE!!, hatupaswi kuifuata ‘dunia’ bali NENO! Na NENO hatuwezi kulimaliza kujifunza kabla ya ule MWISHO! (Ndivyo lisemavyo!) na hili NENO linaitwa NENO LA UZIMA!! mjadala wa mauty unatoka wapi!? (Nadhani jibu unalijua sasa!:-)

  Sijui kama umenielewa kakaangu, ‘Waache wafu wawazike wafu wao, lakini wewe nifuate’. kumbe ‘tumfuate’ ili tufanye nini!?? Tujifunze NENO LA UZIMA ili tuwe wazima na tuibadili dunia ktk Yeye.

  Asalaam aleikum (Amani iwe juu yenu)

  Jackson

 14. Mulele,
  Huwa sipendi kujadili nje ya mjadala, lakini ngoja leo nimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake kwa ajili ya faida yake.

  Tunachojadili ktk hii mada hakina uhusiano kabisa na mambo ya jinsia, lakini nimekuwa nakupuuza kwa muda mrefu sana kwa kutaka kwako kujua jinsia yangu, kwa sababu haihusiani kabisa na mada.

  Nilikutaka uthibitishe kibiblia kuwa Mungu aliumba mtu mara mbili, lakini badala ya kufanya hiyo homework unauliza maswali ya kimaamuma.

  Unalazimisha fundisho ambalo ni potofu kwa sababu ya kukosa weledi wa kuyajifunza maandiko na kujua Mungu alivyofanya uumbaji.

  Whether una umri kama wa baba yangu, I don’t care, ukiongea upumbavu nitakwambia tu.

  Kuna logical question umeelezwa hapo, kuwa shetani ni “baba” wa uongo, na wewe umesema shetani hajulikani kama ni mwanamke au mwanaume.
  Hebu jibu na hilo kuliko kuendelea kupoteza muda wako kutaka kujua kama Sungura ni mwanamke au mwanaume.
  (Asante Christowello kwa hoja nzuri)

  Mulele, hebu sasa jibu maswali hayo ya msingi badala ya kung’ang’ani mambo yasiyo na tija ya kujua jinsia ya Sungura. Japo, kama ungekuwa mtu makini psychology iliyo kwenye maandishi yangu ingetosha kukupa jibu.

 15. Sungura!?
  Ama wewe mbona unawaaibisha wazazi wako na waliokulea!? Je NENO linasemaje kuhusu wajibu wa WANAWAKE ktk Kanisa!? Dear, Kama ukiisoma vizuri biblia utagundua kuwa Malaika wana form ya uanaume, kwa Ibrahim, kwa Lot, kwa Mariamu (sio muhimu sana) lakini Ibilisi yeye hana form. Kuwa na staha kwa wenzio hasa kama we ni Mwanamke basi unapaswa uwe na namna ya kuzungumza mbele yao! Hao ‘waislam’ kama wako hivyo unavyowasemea basi wao wako ki-biblia zaidi kuliko we unaeweza kumwambia mwananamume saiz ya babaako ‘shut up’ mbele za watu! je? Je sio mataifa huo?Unatamaa ya kuoa au kuolewa weye!?? Lau kama umeolewa basi pole yake huyo ‘baba wa nyumba’! na ni aibu kwake na kwa Kanisa lako, hii si tabia ya Mwanamke wa ki-Kristo hata kidogo kwa viwango vya ki-biblia. Ktk hii mitandao mnautukanisha Ukristo Sungura!!

  Kuwa mpole Mamaangu (kumbe ni mwanamke), unisamehe usije taka kunipiga bure! lakini je!? unaweza ona tofauty ya Mwanamke wa Adam na m-Mataifa!? Mmataifa aliumbwa sawasawa na Mwanamume ila kila mmoja kwa jinsi zake na hata ktk ngumi anaweza mpiga mumewe bila wasiwasi, lakini wa Adam, alitoka ubavuni mwake, ni mwili mmoja!! Hawezi kutamka ‘shut up’ wala Pumbavu kamwe, maana kwake Mwanamume ni Kichwa.

  Bila kujijua kama we ni wa Adam au we ni mMataifa, unakazi kubwa sana kuuingia Ufalme dada. Hapo kuna njia mbili za tofauty.

  Asalaam aleikum! (Aliianzisha Bwana Yesu!)
  Jackson Mulele

 16. Mulele,

  Kuniuliza kama mimi ni mwanamke au mwanaume ni swali la kipumbavu sana, hasa ukijumlisha na zile sababu unazoulizia hilo swali.

  Mtazamo wako wa kutaka mtu anaposema kitu lazima ijulikane kama ni mwanaume au mwanamke ni wa kiislam.

  Nahisi umeathirika na fikra ya kiislam ndio maana umejaza heresy kichwani mwako. Nafikiri una tabia za wanaume za kizanzibari, maana kwa hiyo elimu unayojaribu kutoa hapa inaonyesha wewe hujawa-influence waislam na ukristo ila wewe umekuwa influenced na uislam.

  Ukisema shetani ndiye ambaye si mwanamke au mwanaume, kwani malaika wanajulikana kama ni wanaume au wanawake?

  Huielewi biblia wala utendaji wa Mungu. Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kuwa mjinga kiasi hicho cha kushindwa kuelewa kuwa Mungu aliumba mtu mara moja tu.

  Msamiati wa “wamataifa” umekuja pale Mungu alipoamua kumtenga Ibrahim na kumfanya taifa. Sasa wewe unapolazimishi kuwa alianza akaumba wamataifa ndo akaja kumuumba adamu, ni upofu mkubwa sana wa kuyaelewa maandiko.

  If u can’t talk sense u better shut up!!!!

 17. twendeni nao polepole,hata hao ambao bado wanaamini ktk kuombea maiti watabadilika tu.tumetoka nao mbali,watu walienda sana kwa waganga wakienyeji,sasa hivi wanaombewa kwa jina la Yesumimi naamini watabadilika tu,hata ktk kubatiza watoto.hata wokovu upingaji wake sasa hivi si kama zamani,hata hao ambao bado wanaombea maiti nafikiri watakuja kukubali tu vkwamba baada ya kifo ni hukumu hakuna cha RIP.Maana ijnili inavohubiriwa watu wanafunguliwa,so watafunguliwa tu.

 18. SHIDA KUBWA NI UONGO ULIOSAMBAZWA NA VITABU SABA VYA BIBLIA ZENYE VITABU 46 VYA AGANO LA KALE.

  WAANDISHI WA KANISA LA RUMI BAADA YA KUPEA BIBLIA YA KIEBRANIA KUFASIRI WALIONGEZA VITABU SABA AMBAVYO BAADA YA KUVIANDIKA BIBLIA ILIONEKANA KUJIPINGA, HIVYO VITABU HIVI HAVINA UVUVIO WA ROHO.

  MFANO WAMAKABAYO HUSHABIKIA KUWAOMBEA WAFU

  2 WAMAKABAYO 12:44-46

  “KWA MAANA, KAMA HANGALITUMAINI KWAMBA ASKARI WALIOKUFA VITANI WATAFUFUKA SIKU MOJA, INGEKUWA UJINGA USIO NA MAANA KUWAOMBEA WAFU. ALIONA HAKIKA KWAMBA……..

  WAYAHUDI WAMEZIKATAA HISTORIA ZILIZOMO KATIKA VITABU HIVYO,NA WAPROTESTANTI PIA.

 19. Ndugu,
  Tukijifunza NENO, nalo likikaa Kwa wingi ndani yetu, kwa usahihi (Kolosai 3:16) tutaoanisha mambo mengi yanayoendelea ktk dunia na NENO na tutakuwa wenye Amani tukimjua sana.Mungu wetu kwa Usahini. Mfano Qur’an inamuelezea Bwana Yesu kwamba, alipokuwa na miaka 10 alikuwa akicheza na wenzie nae alikuwa akichukua udongo na tutengeneza vitoys vya ndege kisha AKAVIPULIZIA PUMZI YAKE vikaruka vikiwa hai !! Sishangai kwani maneno hayo nnayaambatanisha na NENO Alipo muumba Adam alifanya hivyo.Kitabu hichohicho kinamuelezea Bwana Yesu kuwa alikutana na wenye ukoma na akawaponya kwa NENO lake, sishangai kuwa hivyo ndivo alivyo waumba wa-Mataifa, kwa NENO! Ndivyo kitabu hicho kinavyo muelezea Bwana kuwa yeye ni NENO la Mungu (moja ya Majina yake ktk Qur’an ), sishangai kwani Yesu NDIE Bwana 🙂

  Kwahivyo si ngumu kwangu kuona kuwa vingine aliviumba kwa NENO na Adam alimfinyanga na kumpulizia Pumzi yake.
  Je, hivyo sio Kuwaombea wafu!? (ndilo swali letu)
  Whether mtakubali au mtakataa, kuwaombea wafu ni sahini kabisa kwa Mataifa kwani Bwana aliruhusu hilo (Lakini wewe enenda zako ukautangaze Ufalme wa Mungu), lakini ktk Ufalme wa Mungu kifo sio kitu cha kujadili kwa maana imeandikwa kuwa Yesu alikuja kutukomboa na mauti, na mauty ziko za namna mbili, na zote hizo Yesu alitukomboa 1Corinthians 15:25-26

  Pia, kubalini au kataeni ndugu zangu, mistari inayozungumzia kifo inasauti ya ‘kubembeleza’ ya Ibilisi ndani yake, (Yohana8:44) ikielezea ushahidi wa kidunia kwamba “ni mtakatifu gani ambae hajafa asiekuwa na dhambi!?” Mbona hata “watakatifu” pia wamekufa!? Nawauliza, Je MSHAHARA WA DHAMBI SIO MAUTI !? Je mnataka sasa kusema kuwa NENO linasemaga uwongo !!? Hao tunaowaita “Watakatifu” je unajua Bwana aliwaitaje!!? Yohana 10:7-14, wakati Bwana anatuonya kusema kuwa YEYE pekee ndie MLANGO, mbona sie tunakaidi na kutaka tuwafuate ‘wao’ na wala sio kupita ktk MLANGO!? Aminini lau msiamini, mauti imeandikwa sehemu chache sana katika NENO (biblia) kuliko PENDO! Hivyo tukijifunza PENDO basi tutamjua Bwana kwa sana tuuu na hatutamaliza kabla hajarudi !!Waefeso3:17-

  He! Wengine mnachukia kwasababu “maneno yangu mengi hayana tija” na pia kwanini sipendi ‘kujifunza kuhusu kufa’.

  Tubarikiwe na Bwana na Amani yake itawale Kanisa lake.

  Amina.

  Bro Mjema: Uumbaji vs Uibukaji ndio kitu gani hicho!?

 20. Asante Sungura; umefunua vema. Naona imekaa wazi zaidi; viumbe wote walioumbwa kwa neno katika Mw 1, walikuja kufanywa kwa mavumbi ya nchi katika Mw 2:19. Nimejufunza kitu kipya pia. Nilikuwa naimiss hiyo sehemu;

  Asante sana!

 21. Hivi ni ngumu safari yetu itakuwa ktk kujifunza. Huyu jamaa (Sungura) kaniuliza swali tena zuri sana:
  “Kuna hili umelisema, nakunukuu “Romans 5;12-14 Inatufundisha yale yaliyotekea pale Eden kwamba baba yetu alichagua kufa na kuwa kama M-mataifa (wale aliotumwa kwao!) Unaweza kuthibitisha kuwa kuna wa- mataifa ambao Adam alipoumbwa alitumwa kwao?
  Yaani super swali !!! Sasa, soma jibu la swali hili na ufafanuzi wake ili uweze ona kuwa huyu muuliza swali ni Farisayo’s/Sadukayo’s tuu na wala sio m-Kristo! (Mafarisayo wakikuuliza swali ujue jibu wanalo, na jibu lako hata kama ndio u-KWELI, hawana haja nalo, Sadukayos 😦 Sasa kama unayajua hayo, kwanini uliuliza swali!? Nnaamini kabisa (100%), kabla hawaja kupaste kwa hayo, mie nilishadanganywaga ‘pumba’ hizo kitambo sana (tena sio hapa TZ, kwaoo ktk vyuo vyao!!)!! Lakini NENO la Nabii Isaya/Daniel lipate kutimia, hizi ndio nyakati zetu za KUAMKA, Bwana yu karibu kurudi! Niliomba tangia kwanza kuwa TUSIZODOANE bali tujifunze tukiwa na adabu ktk Yesu Bwana! SG ni mahali pa kufundishana na kuElimishana (Nimegundua hilo!) nilikiri hapa kuwa lile swali la Petro alijuaje kuwa yule ni Elia na Moses!? Oh, nilipata kitu kipya pale. Ahsante sana SG
  Wa-Asalaam aleikum.
  Jackson Mulele.
  NB: SUngura naomba usinisemeshe bila ya kujitambulisha kwanza.

 22. Sungura!?
  Katika majadiliano (hasa yanayomuhusu Jehovah ) ni muhimu sana Mwanamke kusimama kama Mwanamke na Mwanaume nae pia, kujuana kama huyu anaesema hivi ni Mwanamke au Mwanamume ni muhimu sana ktk Kanisa. Hivi wewe Sungura ni Mwanamke au Mwanamume !?? Basi utakuwa na silka za ki-Ibilisi waziwazi maana Ibilisi si mwanamke wala si mwanamme. (inafika mara ya 8 nnauliza swali hili hili moja maana nnahisi we ni Mwanamke lakini wajifanya Mwanamume!) Hebu nnaomba jibu lako ili nikuelezee kitu kwa faida yako ktk Kristo Yesu.

  Ahsante sana Bro. Yona Kayuni kwa hoja yako ambayo ndio inayotusumbua hata sasa bila kujitambua.
  Jackson Mulele.

 23. mulele,

  Kwanza nimekujua hufundishiki.

  Pili,unatutoa kwenye mada husika. (kuwaombea wafu >>> uumbaji vs uibukaji)

  Sitakikubishana nawe. Ombi langu ‘..tufunguliwe akili zetu,tupate kuelewa na maandiko’ Luka 24:45.

  Ubarikiwe mjoli.

 24. Tatizo la kizaz hk neno “Wakristo” linatumika vibaya sana tofauti na asili yake ktk Kanisa la kwanza, mafarisayo na masadukayo leo wanajiita Wakristo, walevi, wachawi, wazinzi wanajiita wakristo lakn mfuasi wa Kristo hawez fanya ibada za wafu na sanamu kama hzo na Mungu anachukizwa sana sana.

 25. Mulele,

  Kaa chi ujifunze, punguza maneno mengi yasiyo na substance. Unaongea manenomaneno mengi mno rafiki, lakini mengi hayana tija.

  Kitu kinachokusumbua ni kidogo sana, hujui kuwa Uumbaji unaoonekana katika Mwanzo sura ya 1 ilikuwa ni kazi ya Mungu katika ulimwenguvwa roho.

  Hata mtu aliumbwa kwanza ktk ulimwengu wa roho kabka Mungu hajachukua mavumbi ya nchi kuyafanya mtu halisi ktk mwili.

  Unachokuja kukiona katika sura ya pili ya Mwanzo ni ule udhihirisho sasa ktk mwili wa hivyo vitu ambavyo Mungu aliviona kuwa ni vyema kwanza ktk ulimwengu roho.

  Unayemwona ktk sura ya pili anaumbwa toka ktk mavumbi ndio huyo ambaye Mungu alishamfanya katika ulimwengu wa roho ktk sura ya kwanza.

  Kungekuwa na watu walishaumbwa ktk sura ya kwanza, tusingeona tena ktk sura ya pili kuanzia mstari wa tano kuwa ardhi haikuwa na mtu wa kuilima.

  Aliyeanza kuilima ardhi ni huyo ambaye alifanywa toka mavumbini ktk sura ya pili.

  Sasa hao mataifa walioumbwa kwa neno pamoja na viumbe wengine katika sura ya kwanza walikuwa wapi kuilima ardhi mpaka ije ianze kulimwa na huyo aliyefanywa toka mavumbini?

  In fact, hata viumbe waliokuwa wameamriwa watokeze kwa namna zao katika sura ya kwanza walikuja kufanyizwa baadae katika sura ya 2:19- Bwana Mungu akafanyiza toka katika ardhi kila mnyama na kila ndege wa angani.

  Kwa hiyo hata wanyama na ndege walifinyangwa toka mavumbini.

  Soma vizuri biblia!

 26. Mjema!?
  Ama we unafuata ‘mkumbo’ !!
  Niombe radhi kwa kuniita Muongo kakah! Unajua NENO linasema muongo ni Ibilisi na pia ni mwenye chuki, sasa mie sina hata kuwakaribia hao! Nia yangu ni mimi na wewe tuwe na Elimu ya Mungu wetu ili tuweze kumuabudu ktk Kweli na Roho (Kwa maana YEYE anawatafuta watu kama hao ili wamuabudu)

  Angalia Mjema,
  Katika kutafuta NENO, ili uweze kuupata mwanga inakupasa kwanza uondoke ktk ‘sisi’ na uingie ktk ‘mimi’ (jifunze kwa brother Chemo!) NENO la Mungu linamlenga mtu mmoja mmoja (Mwenye masikio na asikie!) sasa ukifuata Mkumbo (sisi tunachokutaka ni utudhibitishie………) sisi wewe na nani!? Je unawajua hao kina sisi!? Kuwa makini sana na ‘sisi’ ktk NENO la Mungu kwasababu humo ndimo anamokaa Ibilisi shetani!

  Sasa bro, we unadhani kuwa Jehovah angeishi miaka millioni 66 angekuwa kesha zeeka vya kutosha, si ndio unavyo waza? Hebu igawe hiyo miaka 66 millioni kwa 2Petro3: 8 je unapata ngapi!?? Hebu soma tena kuhusu UUMBAJI ukiihusisha hiyo 2Petro3:8 utapata kapicha kadogo ka hizo siku 6 za UUMBAJI bro 🙂
  Soma NENO bila ya kuingiza stories (bible school) utaona kuwa hizo ‘hadithi’ zinamnyanyapaa Hawa! Kwani kumbe waliumbwa SIKU MOJA, ndio au hapana!!???? Au baada ya kuumbwa Mke na Mume ni vipi tena huyu aingie ktk Ubavu!? Wacheni UJINGA wa kijinga!!!!!! (Wazungu wanajua kuwa Africans are not human beings which have spiritual experience but Africans are SPIRITUAL beings which have a human experience, YES WE ARE, the Adams !!!!.
  Mjema!!?? Kwa taarifa yako maana ya Holy Spirit ni ile Pumzi aliyopuliziwa babaako!! Na Jehovah ni holy Trinity :1: God Father :2: God Son :3: Holy Spirit hii ya tatu ndio tuna share with HIM 🙂

  Tujifunze NENO ili tuweze kuziona fikra za wanasayansi na kuwafahamu (Kimsingu, kwa akili zao wagundue fones watupe tutumie, wagundue madege watupe tuyapande, wao ni WATUMWA kwetu!)! Amini usiamini bro, bila kujua kwamba asili yako ni Adam au Mataifa huna safari ktk kuutafuta Ufalme wa Mungu. Utajikuta unahamasika kuzitumia ‘Akili’ na kwa hizo huwezi hata kugundua ‘baskeli’ . NENO linatutaka kwamba hizo Akili zetu lazima zizoeshwe (zilowekwe) NENO 1Corinth 14:20

  Mjema eh!? Ukiona sayansi inasema kitu na wewe wa Rohoni ukielewi basi ujue na wewe ni sayantist (mjinga) 🙂 Hakika NENO ndio UTIMILIFU wa Elimu zoooooooooooooooooooooooooooooteeee!!!
  (Niulize nikwambie kuhusu Qur’an ! Hanidanganyi mtu kuhusu hiyo hata kidogo, kwanini!? Nnalijua NENO!)

  Brother, hatupaswi kuzodoana (ety we ni Muongo! mbona Sungura kawa so smart!? we vipi bro?) bali tuhojiana kama wenye Hekima tukiwa na lengo moja, kuuingia UFALME ambao YEYE kasema UMO NDANI YETU !!

  Wa-Asalaam aleikum.
  Jackson Mulele.

 27. WAKRISTO WA SASA TUSIPOANGALIA TUTAFANYA MAMBO YA JABU KULIKO ZAMA ZA GIZA.

  MOJA:

  1343 PAPA WAKANISA KATOLIKI ALISHABIKIA MAWAZO KUWA JUMUIA YA WAAKRISTO, HUUNGANISHA WATAKATIFU MBINGUNI,KANISA DUNIANI NA WAFU .
  AKIDAI NI KAZI YA KRISTO,WAKRISTO,WATAKATIFU MBINGUNI DUNIANI KUWAOMBEA WAFU NA KUWATOA KATIKA VIFUNGO VYAO MAHALI ALIPODHANI WANATUMIKIA ADHABU

  MBILI:
  MARCH,15,1517 PAPA WAKATOLIKI AITWAYE LEO X, ALISEMA ANAHITAJI KUJENGA UFALME KUPITIA UJENZI WA KANISA KUBWA LIITWALO ST PETER.CATHEDRAL.

  LEO ALITANGAZA YEYOTE ATAKAYETOA PESA KWAAJILI YA UJENZI WA JENGO HILO, MARA SARAFU YAKE ITAKAPODONDOKA KATIKA KIKAPU NDUGU YAKE ANAYETUMIKIA ADHABU SEHEMU ALIYOIITA PURGATORY ATATOKA KWENDA MBINGUNI.

  PIA ALIUZA VIPANDE VYA MSAMAHA WA DHAMBI KWA WA MIAKA ZAIDI YA MIA MBILI KWA WAUMINI. HIVYO UKITENDA DHAMBI KAMA ULINUNUA KIPANDE HIKO UMEKWISHASAMEHEWA.

  HIKI NDICHO KINAPELEKEA KANISA HILI KUWA NA IBADA ZA MAREHEMU AMBAZO NI KWAJILI YA KUWAKUMBUKA NA KUWAOMBEA, NAKUTOA SADAKA KATIKA IBADA HIZO.

  KUMBUKA IBADA HIZI NDUGU WAWEZA KUZIFANYA MUDA MREFU BILA KUJUA HATIMA YA NDUGU ZAO.IBADA HIZI HUFANYIKA KILA SIKU ASUBUHI KATIKA MAKANISA HAYO.

  WAPENDWA NDUGU ZANGU, ALIYEKWISHALALA, KITABU CHAKE CHA MATENDO KIMEFUNGWA. TUPONE SASA WAPENDWA

 28. Ndugu Mulele,

  Naona kama mafundisho yako ni extrabiblical. Yana ka ukweli ka baadhi ya statements kwaajili ya kumvutia unsuspecting passerby. Ukweli ni kwamba Adam ALIUMBWA (created) Mwanzo 1:26-27, hapa alikuwa mtu, maana Mungu alikwisha sema, “Natuumbe mtu kwa sura na mfano wetu”

  Kisha Mwanzo 2:7, Mungu ALIMFANYA (made) yule mtu kwa mavumbi ya nchi; ili huyu mtu aweze kuwa in contact na mazingira ya dunia hii. Huo ndio uelewa wangu kwa jinsi biblia inavyoeleza kiurahisi kabisa. Linganisha hapo Mwanzo na pale Yohana 6:63, …Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu chochote… MANENO HAYA niyanenayo ndiyo roho na ndiyo uzima. Ni halali kusema, huyo mtu (roho) alikuwa ameumbwa kwa yale maneno ya Mw 1:26-27.

  Account ya wazungu na sisi weusi kutofautiana ngozi, inatokana na wale wazao wa Nuhu, ambao walikuwa ndo mbegu ya ulimwengu mpya baada ya ule wa kwanza kuteketezwa kwa ile gharika; yaana Yafeti, Hamu na Shemu. Ukifuatilia tu ile geneology ya Hamu; yaani huyo baba wa Kaanani, utakuta hata sisi weusi tunatokana na hiyo geneology yake, kwa jinsi ya mwili. (Mw 9:18-28) Ambapo tunasoma kwamba uzao wa Hamu, yaani Kaanani ulilaaniwa na Nuhu, lakini Yafeti na Shemu walibarikiwa. Mimi ninavyosoma naona hiyo laana matokeo yake katika mwili yalikuwa sisi weusi (Waafrika, Wahindi n.k)

  Lakini kwa sasa, hata hao waliokuwa wamelaaniwa zamani wana asili mpya, yaani, asili ya Mungu, kupitia Yesu Kristo. Hivyo laana za mwilini haziapply tena, maana huyo aliye ndani ya miili yao myeusi n.k ni Mbarikiwa wa Bwana, na anatubariki kwa baraka zote za rohoni (Ef 1:3); tonatofautiana kuziachilia hizo baraka kwa jinsi tunavyobadilisha akili zetu….basi!….Kwa habari hii, wacha niishie hapa

  Asanteni

 29. mulele,

  Wewe muongo. Ushaidi wa kisayansi unaousema haupo sanjari na NENO la Uzima unalodai kuliamini!

  Ikiwa umeamini kuwa wanadam wamekuwepo kwa zaidi ya miaka mamilioni amini basi kuwa hakuna MUNGU na hatujaumbwa bali tumekuwepo tulivyo wanadamu kwa bahati mbaya uibukaji (evolution) maana haya mawili ni kichwa na mkia wa shilingi ile ile.!

  Mulele,tunachokutaka ni kututhibitishia ndani ya Bible hayo mamilioni ya miaka na sio nadharia za wanasayansi ambazo hata zenyewe ni maksio tu! Usichanganye ” ..Imeandikwa..” na “. Wanasayansi wanasema..” haya mawili hayawezi kubebeka kwenye kapu moja bro.

  Ubarikiwe.

  ¤¤¤akawafungua akili zao,wakaelewa na maandiko¤¤¤

 30. Sungura,
  Theologian wanayo historia sahini kabisa inayo thibitisha kuwa Adam hazidi miaka elfu sita (6,000 years) Mathayo 1:1-17. Wana-Sayansi (walioPEWA kula Tunda la ujuzi wa Mema na Mabaya) wanao ushahidi sahini kabisa wa fossils and mifupas inayo thibitisha kuwa binadamu amekuwa katika dunia kwa zaidi ya miaka Millioni sitini na sita (66,000,000 years) Sungura, utaifahamu Science yao vema kabisa na usahini zaidi kuliko Wao ukilijua NENO.

  Ahsante sana kwa swali lako na Kwa mtindo huu, tunaweza kuelimishana na kuijua KWELI ndugu yangu! Matarajio yetu ni Kurudi kwa Bwana na kumpokea mawinguni na wala sio R.I.P, tumetumwa kuwapoza, kuwaponya na kuwafufua R.I.P
  🙂 🙂 🙂
  Asalaam aleikum, dada !! (we ni m’mama, si ndio !?! 🙂

 31. Soma Mwanzo 1 yoote! Utaona chapter hiyo inaelezea kuhusu Uumbaji na wakazi wake na watawala wake! Mwanzo 2 inaanza kwa ku-confirm kwamba Mwanzo 1 ndio Uumbaji, Mwanzo 2:1-2 “Basi mbingu na nchi zikamalizika na jeshi lake lote :2: Na siku ya saba Mungu ALIMALIZA KAZI YAKE YOTE ALIOIFANYA, akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yote alioifanya.

  Je mbaka hapo hujafahamu tu kwamba Adam aliumbwa nje ya ‘Uumbaji’?? Ni wazungu ndio wametufundisha hiyo theory ingawa NENO liko wazi kabisa. Ktk Uumbaji, Bwana aliposema ‘Kwa jinsi zake’ inamaana kama ni Samaki basi walitokea Papa, Nyangumi, Perege, Sangara, Kambare, maDagaa, Sato’s, na ‘jinsi zake Samaki’s’ zote tunazoziona leo! Bwana aliposema ndege wa angani, ‘kwa jinsi zake’ basi wakawepo; Njiwa, Kunguru, Tai, Visiesie, Kuku, Mabata, Vijore, na ndege wote tunaowaona ‘leo’, je haikuingii akilini kuwa hata Mwanzo 1;27 Yesu aliwaumba Mwanamke na Mwanaume kwa jinsi zake!? Wazungu, waChina, waHindy, waEskimo, ‘kwa jinsi zake’!?

  Adam hakuumbwa kwa NENO kama the rest of creation !!! Hebu we Sungura angalia rangi ya ngozi yako alafu angalia rangi ya undongo, je unaona tofauty ?? je rangi ya mzungu inafanana na ya udongo!? Wazungu wao walipewa kula tunda la Ujuzi wa mema na mabaya lakini wewe babaako alikatazwa asile hilo sababu yeye alipaswa abaki na Imani ktk yale aliyo vuviwa na Yesu (ile pumzi ya Mungu ina ujuzi kuliko Akili) na hata ukisoma vizuri NENO utagundua kuwa hata dhambi zinatofautiana sana, au waitafsiri vipi Warumi 14;23??

  Ni ngumu ndugu yangu kuiona na kuiendea NJIA kama hatuwezi kufahamu asili yetu kwamba twatokana na nani. 1Yohana 4:4 unadhania hao wengine wanatokana na nani!? Lakini bado ni ile hiyari ambayo iko ndani ya Wateule na ni hiyohiyo iliyoko ndani ya Mataifa.

  Mtume Paul yeye alijijua kuwa alitumwa direct kwa waMataifa na wala sio kwa Wateule, hata Bwana aliwaambia wale11 kuwa “Afadhali mshike njia kuwaendea Kondoo waliopotea wa .. …. na kwa Mataifa msiende kwanza”

  Lakini Sungura!? we ni baba kweli !!? 🙂

  Asalaam aleikum = Shalom = Amani YANGU iwe juu yenu!
  (Hiyo ilikuwa ni Salaam ya Bwana lakini kwa kukosa kwetu elimu, sijui kama haiwakwazi 🙂

 32. Mulele,

  Kuna hili umelisema, nakunukuu
  “Romans 5;12-14 Inatufundisha yale yaliyotekea pale Eden kwamba baba yetu alichagua kufa na kuwa kama M-mataifa (wale aliotumwa kwao!)”

  Unaweza kuthibitisha kuwa kuna wa- mataifa ambao Adam alipoumbwa alitumwa kwao?

  Ni hilo tu!

 33. Wapendwa,
  R.I.P Mbona hiyo iko sawa ktk-NENO!??? Hoja hii aliulizwa Bwana Yesu na ‘mlokole mmoja’ Luka 9:59, je Bwana alimjibu nini!? Mbona nyie mnaendeleza unafiki na kutiana moyo ktk kufa!? Mnadhani pindi ukifa (ktk njia hii) hao wataozika hawatakutolea R.I.P!?? Je utainuka weye na kusema mie niliokoka hivyo usiniwekee hiyo!!?? Kwani Bwana alimjibu nini yule aliejiita ‘Mlokole’ kama tunavyojiita!? WAACHE WAFU WAWAZIKE WAFU WAO, BALI WEWE ENENDA UKAUTANGAZE UFALME WA MUNGU. Je!? Nikisema kwamba hoja ya RIP inawahusu WAFU na wanaoijadili ni miongoni mwao sitakuwa sahini !!?? Hivi hatuwezi ona kuwa katika Ufalme wa Mungu hakuna hoja wala mazungumzo ya WAFU!?

  Sisi tunapaswa kulijua NENO ili Shetani aweze kutuheshimu! Kama hulijui NENO wewe ni maiti unaengojea kufa, Ndugu Lami, Ibilisi akikuletea Muhubiri 9:5 nawe mpe ile Yohana 11;26 na swali lake juu!! PM Dittu, wacha kufarijiana na Sungura ambae ni vigumu kueleza kama ni mke au mume. Lwitiko? Kama mama kaondoka? ni vema sisi tusiondoke ila Tumngojee Bwana Isaya 40:29-31, Sungura eh? wana wa Mungu hawafarijiani ktk kufa, hasha !! Pst. Frank Divine- Grace, si wote ‘wafao’ kwamba wanalala, brother unaposoma NENO kuwa makini na sauti ya Ibilisi katika NENO la Mungu, soma vizuri Kujaribiwa kwa Bwana utagundua kuwa Shetani alilitumia vema NENO lakini kwa bahati mbaya Bwana ndie NENO! Lakini sisi (mimi na wewe) sio NENO hivyo tuitambue sauti ya Ibilisi ktk NENO hiyo mistari inayo himiza kufa ni sauti ya Ibilisi. Brother Frank Wawi, Bro Eliphace, Mutani, da’Mage, Kaka Mjema, Tumaini eh? Nijifunze nini sasa, Kufa? Katika Ufalme wa Mungu somo hili halipo kaka 🙂

  Naomba tena samahani kama ntakuwa nimemkwaza yeyote ktk hoja hizi

  Asalaam aleikum = Amani iwe kwenu nyote.
  Jackson.

 34. Asante Mulele, umenipa kutafakari zaidi, wacha nitafakari kwa kimya, maana nimejifunza kitu kizuri toka kwako; kumbe uongo ni jambo lolote atakalokuambia ibilisi. Kwa hili nakubaliana nalo moja kwa moja bila hata kutafakari. Wacha niyatafakari hayo mengine. Nakushukuru Mulele

 35. Naungana na wewe Lani kwa asilimia 100, hatuna ijara na waliokufa. mimi nadhani ile kumbukumbu wanaweza kuweka picha, lakini maneno yanayoandikwa hapo basi yawahusu watu wanaoishi. kwa mfano unaweza kusema maneno tu ya shukurani kwa mungu kuendelea kuwapigania tangu walipoondokewa labda na mzazi, kuomba ulinzi wa mungu na kumshukuru mungu tu kwa namna kama hiyo. Lakini jinsi wanavyoielezea hiyo picha, unakumbukwa na watoto wako, mkeo n.k ni zaidi ya kuchanganyikiwa, maana hata wao wanaelewa hiyo picha haina uhai wowote wa kuona wala kusikia au kusoma hayo maneno, na picha hiyo haina connection yoyote na yule mtu kule kaburini. Jamani tubadilike, tusifanye mambo kwa copy and paste.

  asanteni wengine kwa michango yenu.

 36. Lwitiko,

  Pole rafiki sikujua uliondokewa na mzazi. Ingependeza kama nasi kanisa la GG tuwe tunajulishana mambo kama hayo ili tuweze kufarijiana.

  Lane,

  Umegusia jambo ambalo nataka kusema, hivyo ngoja niongeze tu kidpgo.

  Hii tabia ya kuongelesha wafu naoona sana hata kwa wapendwa. Utakuta mtu ànasema “ni mwaka mmoja tangu ututoke, tunakukumbuka sana”.
  Au mtu anapatwa na tatizo fulani halafu anaamua kuandika maneno “baba ungekuwepo haya yote yasongenipata”.

  Na kuna kipindi fulani TBC1 huwa nashindwa kuelewa mantiki yake. Wanaweka picha za wafu halafu wanaandika maneno kama niliyosema hapo juu, na mengine mengi.

  Na huwa hasa nashindwa kuelewa lengo la wenye hao ndugu wanaopeleka hizo picha. Sijui hasa huwa wanamtangazia nani, au basi ni kule kujionesha kwa watu. Maana zile picha za kumbukumbu za kuzaliwa hiyo inaeleweka kuwa mtu anapongezwa, sasa hii ya picha ya marehemu yenyewe sijui huwa na maana gani!

  Nafikiri wana wa Mungu ni muhimu kuwa makini na mambo haya.

 37. Salaam Mutani,
  Ninafurahia sana kuona kuwa unataka kuijadili Mada hii ktk kina chake na wala sio kujadili matawi.

  (Ni wa-Mataifa ndio wanaokufa mara moja na baada ya kufa ni hukumu!?)
  Ndio, kwasababu wa Adam wao hawako tena chini ya Sheria, wao ni wa Imani (Imani haina hukumu ila Sheria inayo) 1John3;14 ‘Sisi’ tunajua kwamba tumepita kutoka Mautini kuingia Uzimani kwasababu TWAWAPENDA NDUGU (Pendo ni Imani)

  Romans 5;12-14 Inatufundisha yale yaliyotekea pale Eden kwamba baba yetu alichagua kufa na kuwa kama M-mataifa (wale aliotumwa kwao!). Adam ndie baba wa kizazi chake kwani yeye ndie ‘mzaliwa wa kwanza’ mwenye Pumzi ya Mungu, hivyo baada ya kuasi alifukuzwa kutoka uwepo na ulinzi wa Yahwe na akaingia ‘Duniani’ (angalia, Mungu akawavika mavazi ya NGOZI za wanyama, tambua kuwa NGOZI inatokana na wanyama walio’KUFA’ pia lile toto lake korofi Bwana alilitia alama ili hao Mataifa wasimlipize kisasi kwa sababu alikuwa kajiunga na ‘genge lao’ kwasababu tu yeye alikuwa ni wa ukoo wa ki-Mungu, wala sio wa ki-dunia)

  (Je Adam aliumbwa na hali ya KUFA au alijichagulia KUFA?)
  Mwanzo 2;17 Walakini matunda ya mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya………….. Hii mbona haiitaji torch Mutani!? Inamaana kama hutokula (ndilo agizo USILE!!) hutokufa kabisa hata milele, Je wayasadiki hayo!? Hivi sie tunamuelewa Mungu anapotukataza au anapotutaka kufanya jambo!? Yahwe alimwambia Adam usile, ibilisi akamwambia Hawa, Mungu ni muongo kwani anajua siku mtakapokula MTAFUMBULIWA MACHO NA KUWA KAMA YEYE! (Unajua Chemo? Jambo lolote atakalo kwambia ibilisi hilo ndio UONGO ! Lakini kwa akili za kawaida utagundua kuwa ibilisi ALISEMA UKWELI KABISA !! Lakini Mungu anatutaka tujifunze kuwa jambo lolote analolisema (Yahwe) ndilo KWELI na ni kinyume kwa ibilisi. Kwa Adam tunakufa: Kwa Kristo tunaishi. RIP haiusiani na Kristo ktk hali yoyote na wala KUFA SIO MPANGO WA MUNGU na kufa kuko namna 2 na hizo zote 2 Kristo ametukomboa !!!!!!!!!!!!!!!! Lau kama hamtaki basi !!

  NB: Tunapaswa kujihadhari na Maandiko haya haya !! Kwa sababu ki-msingi Shetani huwa hana NENO lakini hulitumia NENO lilo hilo la Yesu ili kuwapotosha WATEULE !! Sasa jihadhari na mafundisho maana hakuna binadamu anaemjua Yahwe, Jehovah Mungu akamzidi Ibilisi !! Maana nae pia ni Mungu wake 🙂

  Mie nimejaribu kuijibu hoja kutoka SHINANI lakini walio wengi hawataki, hawajazoea wanataka porojo za juujuu tu ety ‘umetoka nje’ 🙂 🙂

  Asalaam aleikum = Amani iwe juu yenu

 38. MATANGAZO HAYO YAMEKUWA NA SHIDA MOJA , NENO “TUNAKUKUMBUKA” AMBALO HUONYESHA KUWA MFU HUYO AWEZA KUSIKIA HAYO MANENO ANAPOAMBIWA TUNAKUKUMBUKA KUMBE WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE,WALA HAWATASIKIA HAYO MANENO TUNAYOWAANDIKIA KATIKA MAGAZETI AU KATIKA TV.

  MHUBIRI 9:5
  “KWA SABABU WALIO HAI WANAJUA YA KWAMBA WATAKUFA; LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE, WALA HAWANA IJARA TENA; MAANA KUMBUKUMBU LAO LIMESAHAULIWA”

 39. Nakumbuka mnamo mwaka 2013 mama yangu alipofariki baada tu ya mazishi siku kama ya pili nikaamua kupitia kadi ambazo marafiki, ndugu na jamaa walizileta. zilikuwa ni card zile tunaita” condolence ” . au sympathy. Nilikuwa nataka tu nijue na kusoma faraja ambazo marafiki walizileta. Katika kupitia card moja baada ya nyingine na kuangalia daftari la rambirambi nikakuta idadi kuwa ya watu wametumia neno “RIP” na wachache wametumia salamu za kawaida na maneno ya faraja kama vile ” Mungu awafariji kwa kuondokewa na mama yenu” . Na mama yangu aliondoka akiwa ameokoka. Nilifahamu fika amelala katika Bwana. Katika mambo ambayo kwa kweli nilijizuia ni hilo neno ” RIP” kama wengine walilitumia ni wao walifanya hivyo lakini Mimi sikulitumia neno wala siku tengeneza nafasi ya hilo neno kutumika. Wengine huwa wanaenda Facebook wanaweka picha ya marehemu au tangazo la kufiwa si vibaya kuwataarifu marafiki lakini marafiki wakiandika RIP wewe hujafanya ibada ya wafu. Ila wewe mwenyewe ukiwachanzo cha kuanzisha hizo ibada kwa kujua au kutojua hapo sasa kuna wa lakini
  Mwezi wa 12, tarehe 26 mwaka 2014 shemeji yangu akaniambia inabidi tutembelee lile kaburi lipo hapa hapa morogoro. Na Mimi kwa kweli nilikuwa na hamu ya kutembelea walau niangalie tu, hiyo siyo vibaya. Hata akina mariamu walitembelea kaburi LA Yesu baada ya kufa na kuzikwa japo hawakumkuta, alishafufuka. Lakini shemeji yangu akaniambia inabidi twende na mishumaa na maji. Niliposikia hivyo nikajua sasa huyu anaelekea katika “rituals” nilikataa waziwazi huku akisikia. Nikamwambia kama tunakwenda kutizama tu Hamna shida ila hivyo vitu vingine Mimi sishiriki. Nataka kusema Mimi binafsi sikubaliani na neno “RIP” kama MTU aliyeokoka. Hata kama namfahamu MTU ambaye ameokoka amekufa huwa situmii neno hili. Na wala sina shida na wale waliolitumia mama yangu alipofariki kwasababu wamelitumia hawajalitumia haibadilishi jambo lolote. Nachojua mama yangu amelala katika kristo si kwasababu ya neno ” RIP” ila kwasababu ameondoka akiwa ndani ya kristo. Neno rip ni faraja tu za kidunia. Lakini halina nguvu yoyote kubadilisha destiny ya MTU. Wanao s tarehe baada ya kufa ni wale tu waliokufa katika kristo au ndani ya kristo ambao kuishi kwao ni kristo na kufa ni faida. Ni wale waliokoka na kutembea pamoja na Mungu vizuri katika maisha yao hapa duniani. Harafu nafikiri ibada ya wafu inaenda ndani zaidi kuliko matumizi ya neno Rip. Huko utakuta matambiko na kuwasiliana na roho za watu waliokufa na mambo wengine. Japo matumizi ya neno rip si sahihi kwa watu wanaofahamu Mungu ipasavyo.

 40. Brother Frank Divine,

  Kuna mambo umesema sawa, lakini hili la R.I.P sijakubaliana na wewe. Iwe kwa kujua au kwa kutokujua hiyo ni kuombea mfu.

  Wewe itoe kwenye Kiingereza kuja kwenye ile ya Kiswahili ( Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi).

  Hatupaswi kufarijiana kwa maneno ambayo siyo biblical. Yako maneno mazuri ya kibiblia kama ” Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe”

  Tufarijiane kwa hayo!

 41. Wapendwa,

  Awali ya yote uhai tulonao niwa mhimu sana kuweka mambo yetu ya umilele sawa! Na pia umilele wetu upo chini ya uamuzi wetu wenyewe tungalipo hai. ndugu waweza kuwa msaada kwetu kupata uzima wa milele tungali hai na sio tulalapo mauti.

  Pia napenda tusome, Mhubiri 9:5-6, 10 ” kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 9.6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; WALA HAWANA SEHEMU TENA KATIKA JAMBO LOLOTE LILILOFANYIKA CHINI YA JUA.9.10Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa HAKUNA kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.”

  Aya hapo juu inajieleza vyema. Tafakari maneno yenye herufi kubwa.utapata jibu!

  Kuwaombea au kuwaomba wafu ni matendo ya kipagani yaliyoingizwa kwny baadhi ya iman za kidini, jambo ambalo halisapotiwi na neno la Mungu. Hatuwezi kubadili historia za ndugu zetu waliolala mauti. Watahukumiwa kwa jinsi walivyoishi wakiwa hai na sio jitihada tuwezazo kufanya kwa niaba yao wafapo.

  Hii ni desturi inayotufanya tuishi kizembe (bila kumtii kristo) tukitegemea kuombewa “tulazwe mahali pema peponi”. Jambo lisilowezekana.

  Mbarikiwe.

 42. Mimi nafikiri kuweka hiyo R.I.P ni sehemu ya kuwafariji wale waliyofiwa.
  ★ Lakini sikubaliani na huyo wa kiingereza anayesema eti “at the point of death is determined weather the person is in heaven or dambation.” Haya mambo ya damnation au heaven sio kwa sasa. Wote wafao kwa sasa hulala mpaka Bwana Yesu atakaporudi kuhukumu waliyohai na wafu ili atenge kondoo na mbuzi, ni akina nani waingie mbinguni na nani waende jehanamu! (Yohanna 5:28-29, 1 korintho 15:51, Ufunuo 20:12-13)
  ★Mpaka atakaporudi bado wpte waliohai na wafu Yeye Kristo ni Bwana wa wote (Rumi 8-9)
  ★ Hiyo R.I.P wengi wanaifahamu kikawaida kumaanisha REST IN PEACE lakini pia ina masna ya RETURN IF POSSIBLE. Hivi vyoote si maombi ila ni maneno yanayoonyesha matamanio ya mtu ingewezekana, yaani, ni wishes to sio prayer at all.
  Mungu awabariki.
  ★ Kiukweli Biblia inasema wotevwafao wanalala (sleep/rest) kama ilivyo katika 1 Thesalonike 4:13-16 japo inatoa tumaini kwa wanao lala katika Bwana.
  Kwa hiyo hatuwaombei wafu bali tunawafariji waliofiwa. Na tunawapa tumaini wale wanaomwamini Bwana Yesu kuwa wafu wao watafufuliwa Bwana atakapokuja na mawimbi. HALELUYAH.
  Pst. Frank Divine-Grace.
  Arusha.

 43. Hahaa, Mulele,

  Sungura kaingiaje tena hapa?

  We changia mada bwana watu tujifunze inatosha.

  Ukituletea matango mwitu lazima tushugulike nawe. Potelea mbali kama utaona kuwa hiyo ni mipasho, hata hivyo, kupashana ukweli ni ya ki biblia.

  Na mada ni rahisi kweli.

  R.I.P siyo ya kimaandiko hilo liko wazi. Na tatizo lake siyo uzungu wala undengereko, bali ni ujinga au kuchukulia mambo poa.

  Kiswahili hii husemwa ” Mungu ailaze pema roho ya marehemu( sijui kama ina kifupi chake).

  Hii imetokana na ibada za wafu za Catholic. Kwa vile ndo dini kubwa, basi dunia imefuata.

  L.I.P (Live in peace) Mulele!

 44. Mulele, Duh…Nafurahi kuelezea hisia zako ila Bila shaka hukuelewa mada ya kuchangia…. Ni kweli wengi tumejikuta tukiyafanya hayo ila bila shaka kupitia mafundisho haya tumeelewa… Suala la Watu kuchanga mawazo hasa kwa kuandi RIP nakubali kabisa kuwa ni Ibada ya Wafu ila Biblia Takatifu imeweka bayana kuwa matendo yao hufuatana nao..Whether umefanya vibaya ama vizuri…

 45. Mtu akishakufa na lake hakuna ktk ulimwengu huu hivyo kinachofanyika ni ibada ya mizimu, haifai Tumwabudu Mungu Baba peke yake

 46. mulele,

  Umetoka nje ya mada.ukiönyesha uwezo wako juu ya uumbaji,lakini ht ivyo unaöne kana kuwa kataa wazungu aliokuletea biblia ila una wakubali kwny uibukaji-evolution.

  Wala hakuna yeyote aliyekuogopa popote kwny mada hapa SG km unavyodai.

  Pole rafiki. hata admin. Ameona ulivyotoka nje,ingawa hajakutaja moja kwa moja.mada hapa ni Ibada kwa wafu wala sio Uumbaji ambao hata wenyewe umeupotosha kweli.

  Nakushauri rafiki, kubali kujifunza kwa wengne.usidhani wewe daima upo sawa.

  Karibu sana

  Wasalimu Zanzibar.

 47. Binafsi sijakuelewa ndugu Jackson Mulele.

  1. Unasema Adam hakuumbwa kwa neno, hebu nifundishe John 1:1-3 inasema nini juu ya neno na uumbaji; ukilinganisha na tofauti kati ya Mwanzo 1:26-27 na Mwanzo 2:7 ili unipe mtazamo utakaonisaidia kukuelewa na kukupambanua

  2 Unasema ni wamataifa ndio wanaokufa, hebu nifundishe vizuri hapo kupitia Rumi 5:12-14

  3. Unasema Adam alichagua kufa, naomba nieleze vizuri maana ya neno hili katika Mwanzo 2:17… “maana siku utakapokula katika huo utakufa hakika”.

 48. Ni ujinga wa kiroho na ni mbinu za shetani kuwafanya watu kumuinamia bila kujua unakuta mtu anacoment rip hajui hata mana ke .

 49. Bwana yesu asifiwe wapendwa wote.mimi nimeelewa maada naomba nichangie kama ifuatavyo.kuweka picha za marehemu na kuwakumbuka mimi nasema ni dhambi na hao wanaofanya hivyo ni watu hawajui neno la Mungu kwani mtu anapokufa kumbu kumbu lake linatoweka kufanya hivyo ni ibada ya sanamu Mungu anasema sanamu zina macho hazioni,zina masikio hazisikii,zina midomo hazineni,nk sasa nyinyi? mnao weka picha na kuziombea,kuwakumbuka,na kuwatakia walale pema peponi.mnafanya kitu msicho kijua kama wasomaji wengi walivyo changia kupitia andiko la waebrania 9:27 biblia inasema kama vile wanadamu walivyo wekewa kufa mara moja baada ya kufa ni hukumu.anayejua kuwa huyu yupo motoni,au uzimani(peponi kama wengi wanavyopenda kusema ni Mungu tu.mimi huwa siwaelewi hata viongozi wa dini wanao wadanganya wafiwa mtu amekufa hosipitali kisha anahifadhiwa kwenye vyumba vya maiti kwa siku kadhaa wanandugu wanajipanga kufanya mazishi imepita siku moja,mbili,tatu,au wiki anakuja kiongozi wa dini anomba mungu amlaze pema peponi nasema sala za viongozi wa dini haziwezi kubadi hukumu ya MUNGU mtu anapokufa saa ileile anahukumiwa kuna sehemu mbili tu mtu akiwa ameokoka na kuishi maisha matakatifu anapokufa yeye analala tu kwa mjibu wa neno la Mungu anapewa mwili wa mbinguni usio na uhalibifu na kwenda kwenye makao ambayo Yesu ameenda kuwaandalia watakatifu.na wale wanaoishi maisha machafu ya ufisadi,uovu wa kila aina na kusema huwezi kuokoka duniani wanapokufa moja kwa moja wanaenda Jehanamu sehemu ya mateso ya milele mimi nawapenda wachungaji wa kilokole hata kama amekufa asikofu wanasema Bwana alitoa Bwana ametwaa Jina lake libalikwe wasomaji wote wa mahali hapa niwakumbushe kazi ya YESU alikuja kutafuta na kumwokoa mwanadamu aliyepotea katika dhambi soma yohana 3:16..21,warumi 10:9..10,1wakolinto 3:18,zaburi 3:16
  kwa leo naomba nishie hapo nasema Mungu awabaliki ni mimi mjoli wa kristo
  stephen ngulloh

 50. Tatizo ni uelewa na mapokeo kwa wanadamu namengine bila hata kuyachunguza wanayaangukia na wanayafuata ili kuogopa wanadamu watawaona wa ajabu. wakati Mungu anawaona wa ajabu. baada ya kifo ni hukumu hiyo R.I.P utaipata wapi wakati Mungu ameishafunga jarada lako, ni sawa na kumwambia mfungwa gerezani pumzika kwa amani jela kuna amani jela.  Tusipotoshwe na mapokeo yasiyo na maanaMbarikiwe  Siaka S. Nyanchiwa    Internet cafe and College Controller        P.o Box  70 Serengeti, Mara, Tanzania.           P.o Box 417 Tarime,Mara, Tanzania.    Contacts: sianchwa@yahoo.com/sianchwa@gmail.com. Mobile:            +255755527476.

 51. Mpendwa Msomaji tunakuomba USOME POST VIZURI KAMA ILIVYOANDIKWA. Maana inaonekana mada haijaeleweka au kuna watu wanasoma haraka haraka pasipo kuangalia kinachotakiwa kujadiliwa hapo ni nini hasa!

  Karibu kwa maoni kutokana na mada hii. Asante

 52. Ebrania 9:27 “Na kama vile ‘watu’ wanavyowekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu”. Mbona huo mstari uko wazi kwamba unawazungumzia wa-Mataifa!? Hao ndio ‘wamewekewa kufa mara moja’ lakini wewe soma Warumi sura ya 8  ili upate kupambanua tofauty kati ya Adhabu na Neema na kwamba WEWE unaweza kufufuka ungali hai (Pumzi ya Mungu kwa Adam ikimtoka uhesabiwa kuwa amekufa angali anaishi, anafanyika ni m-Mataifa asie jua kuzaliwa mara ya pili kama Askofu, Kadinari, Papa, Mchungaji, Padre, Doctor of Divinity, Nicodemus John 3:1-13  !!) Kwani nyie SG mnaogopa!? Mbona hamhoji !? Basi na nyie ni wa-Mataifa mnaongojea kufa ‘mara moja’  🙂 Wala sio Straight to the Gospel kama mnavyo jidai !!  Au SG ni Ndugu Sungura (wa-Mipasho) !?

   FYI: ‘Wakristo’ ni = Banil Adam = wa-Milele = Wa-Mungu. Lau kama hamyataki hayo basi !!

  Jackson Z. Mulele.

  ************************

  JACKSON Z. MULELE

  OPERATION MANAGER

  P.O BOX 1477 JAWS CORNER

  STONE TOWN ZANZIBAR, TANZANIA

  MOBILE FONE: +255777415192

  LAND LINE: +255242239630

  jackson@wonderfulzanzibar.com [1]

   

 53.  Hello, Salaam, Kwa kweli neno kufa kwa ujumla wake haliusiana na Bwana Yesu hata kidogo. Yeye alikuja ‘kutu’komboa kutokana na huko ‘kufa’. Niliwahi kuandika hapa kuwa wazungu hawajawahi kutuletea Injili bali walikuja kututapeli na kutuletea dini ZAO na mila na desturi zao wakimtanguliza yesu wao ambae ni Blondy na blue eyes. Nimegundua kuwa ktk website yenu mnadai kuwa ni Strictly Gospel lakini kwa kweli nimegundua kuwa sio kweli kwamba Straight to Gospel. Mbona mengi niliyoandika kuhusu NENO hata kuya publish mmeogopa??? Ntawaambia vile NENO (Yesu Bwana) anavyosema kuhusu KUFA na nitarudia baadhi ya yale mnayoyaogopa!.

  Bwana Mungu, ktk uumbaji wake alitumia NENO kuumba KILA KITU hadi uumbaji ulipo kamilishwa kwa kuumbwa Watu, Mwanamke na Mwanamume (kwa jinsi zao) nao wakapewa Mamlaka ya kutiisha kila kilichopo chini ya jua.

  Baada ya kupita mamilioni ya miaka, Bwana Mungu akaamua kujitambulisha kwa watu wake, ili watu wake waweze kumuabudu, akamtengeneza Adam kama ‘Mjumbe’ kwa watu wake (Adam hajaumbwa kwa NENO kama viumbe wengine na alipuliziwa Roho Mtakatifu ambayo ni; SEHEMU YA 3 YA MUNGU, hivyo Adam alikuwa ni Mtawala ktk Ufalme wa Mungu.)

  Viumbe vyote viliumbwa ‘kwa jinsi zake.’ Adam aliumbwa kwa jinsi ya Mungu. Viumbe vyote viliumbwa wake kwa waume, majike na madume kwa wakati mmoja, Adam aliumbwa kwanza kabla ya Hawa, akapewa Elimu yote kuhusu ‘kila kitu’ kabla ya Hawa ambae alitoka ktk yeye.   Kifo kilikuwepo tangu Ibilisi alipotupwa huku ‘duniani’ na kila kiumbe (hata watu pia) kilikuwa na jinsi ya kifo kwa sababu ya Ibilisi. Adam aliumbwa kuishi milele na kifo kilikuwa ni chaguo lake binafsi, nae alipaswa kuwafundisha ‘Mataifa’ kuhusu kumuabudu Mungu peke yake na hivyo kumuepuka Ibilisi ambae kifo ni silaha na ni vazi lake.

  Adam, aliumbwa na uweza kuliko kiumbe chochote hata kuliko malaika hata kuliko ibilisi mwenyewe, na ibilisi alijua kwamba uwezo wa Adam ulikuwa ktkt kumtii Mungu tu. Hawa, hakuwahi kumuona wala kuzungumza na Mungu wakati wowote bali kwake Mungu alikuwa ni Adam, alichokisema Adam kwake ndicho alichokisema Mungu. Ibilisi alifanikiwa kuingiza Kifo kwa Adam kwa kupitia Ubavu wake, ndio maana alisema Adam, “ni huyu Mwanamke ulienipa”  Elimu ya NDOA !!

  Mungu alimkasirikia Adam ingawa kosa alilifanya Mwanamke kwa sababu Mwanamke pia ni Adam, kwamba walikuwa ni mwili mmoja kwa maneno yake Adam mwenyewe!! Lakini Bwana aliweka ahadi ya kuzaliwa Bwana Yesu ktk Mwanzo 3;15 na hivyo ktk uzao huo Ibilisi ATASHINDWA, na hizi tuishizo, ndizo zama za ushindi ktk Yesu Kristo Bwana wetu !!

  Hebu tuyaangalie Maandiko bila ya kuchanganya na maneno ya wazungu, tuone ahadi zetu ni zipi na tuzisimamie bila uoga! Danieli, Ayubu na manabii wengi walitabili kuhusu zama hizi zetu !! Inatupasa tuyaSOME Maandiko kwa usahihi na wala sio kufuata mkumbo !!

  Kifo sio mpango wa Mungu kwa wa-Adam wala wa-Mataifa !! Kuna mauti namna 1 kwa wa-Mataifa, kufa ni kufa tu, yaani kufariki, kuaga dunia, kudedi,  !! Lakini kuna mauti namna 2 kwa wa-Adam, kule kuipoteza Pumzi ya Mungu (aliyopuliziwa baba yetu Adam ambayo ni Takatifu na ni sehemu ya 3 ya Mungu) ambayo hiyo humpelekea wa-Adam kuishi kama m-Mataifa anaengojea kukamilisha mauti !!

  Ukiona mtu anakufa, NENO linasema anapokea mshahara wake !!! Labda mlete hadithi lakini ndivyo linavyosema!! Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni ………………!!!!

  Tujifunze, tuulizane  na wala tusibishane, basi tunaona mwangaza mbele yetu !!

  Ndimi Jackson.

   

  ************************

  JACKSON Z. MULELE

  OPERATION MANAGER

  P.O BOX 1477 JAWS CORNER

  STONE TOWN ZANZIBAR, TANZANIA

  MOBILE FONE: +255777415192

  LAND LINE: +255242239630

  jackson@wonderfulzanzibar.com [1]

   

 54. Hivi maana yake nini? Mada imetolewa kwa lugha ya kiswahili harafu mtu anachangia kwa lugha ya kiiengereza. Si wote tunajua hiyo lugha jamani.

 55. Question: “What does the Bible say about praying for the dead?”

  Answer: Praying for the dead is not a biblical concept. Our prayers have no bearing on someone once he or she has died. The reality is that, at the point of death, one’s eternal destiny is confirmed. Either he is saved through faith in Christ and is in heaven where he is experiencing rest and joy in God’s presence, or he is in torment in hell. The story of the rich man and Lazarus the beggar provides us with a vivid illustration of this truth. Jesus plainly used this story to teach that after death the unrighteous are eternally separated from God, that they remember their rejection of the gospel, that they are in torment, and that their condition cannot be remedied (Luke 16:19-31).

  Often, people who have lost a loved one are encouraged to pray for those who have passed away and for their families. Of course, we should pray for those grieving, but for the dead, no. No one should ever believe that someone may be able to pray for him, thereby effecting some kind of favorable outcome, after he has died. The Bible teaches that the eternal state of mankind is determined by our actions during our lives on earth. “The soul who sins is the one who will die. . . . The righteousness of the righteous man will be credited to him, and the wickedness of the wicked will be charged against him” (Ezekiel 18:20).

  The writer to the Hebrews tells us, “Just as man is destined to die once, and after that to face judgment” (Hebrews 9:27). Here we understand that no change in one’s spiritual condition can be made following his death—either by himself or through the efforts of others. If it is useless to pray for the living, who are committing “a sin that leads to death” (1 John 5:16), i.e., continual sin without seeking God’s forgiveness, how could prayer for those who are already dead benefit them, since there is no post-mortem plan of salvation?

  The point is that each of us has but one life, and we are responsible for how we live that life. Others may influence our choices, but ultimately we must give an account for the choices we make. Once life is over, there are no more choices to be made; we have no choice but to face judgment. The prayers of others may express their desires, but they won’t change the outcome. The time to pray for a person is while he or she lives and there is still the possibility of his or her heart, attitudes, and behavior being changed (Romans 2:3-9).

  It is natural to have a desire to pray in times of pain, suffering, and loss of loved ones and friends, but we know the boundaries of valid prayer as revealed in the Bible. The Bible is the only official prayer manual, and it teaches that prayers for the dead are futile. Yet we find the practice of praying for the dead observed in certain areas of “Christendom.” Roman Catholic theology, for example, allows for prayers both to the dead and on behalf of them. But even Catholic authorities admit that there is no explicit authorization for prayers on behalf of the dead in the sixty-six books of canonical Scripture. Instead, they appeal to the Apocrypha (2 Maccabees 12:46), church tradition, the decree of the Council of Trent, etc., to defend the practice.

  The Bible teaches that those who have yielded to the Savior’s will (Hebrews 5:8-9) enter directly and immediately into the presence of the Lord after death (Luke 23:43; Philippians 1:23; 2 Corinthians 5:6, 8). What need, then, do they have for the prayers of people on the earth? While we sympathize with those who have lost dear ones, we must bear in mind that “now is the time of God’s favor, now is the day of salvation” (2 Corinthians 6:2). While the context refers to the gospel age as a whole, the verse is fitting for any individual who is unprepared to face the inevitable—death and the judgment that follows (Romans 5:12; 1 Corinthians 15:26; Hebrews 9:27). Death is final, and after that, no amount of praying will avail a person of the salvation he has rejected in life.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s