Kuona miti kwenye ndoto ina maana gani?

Shaloom wapendwa!

Naitwa Fina, naombeni ufafanuzi juu ya ndoto hii.

Kwanza kabisa na mapito makubwa sana. Siku moja nikiwa ofisini nikiwa namuuliza Mungu ni kwanini yote hayo, ghafla nilipata kausingizi kazito kama dakika 2 hivi nikaota napita msituni miti imekatwa na inaendelea kukatwa. Ghafla mti mkubwa ukawa unaniangukia lakini cha kushangaza ule mti niliuona umeshaanguka mimi nimepita salama. Lakini baada ya kuvuka pale nikashangaa wakati naendelea kutembea kamti kengine kadogo kakaanguka mbele yangu kakaniblock.

Naombeni msaada watumishi wa Mungu.

Asante

Advertisements

27 thoughts on “Kuona miti kwenye ndoto ina maana gani?

 1. Mrs. Christina,

  Kuna mbegu gani ambayo Roho mtakatifu ameipanda kuhusu utofauti wa maono na ndoto unayosema kuwa hakuna mtu atakaeiharibu?

  Please, hebu jaribu kuongea mambo kwa ‘usiriaz’ zaidi ya hapo ndugu. Mrs. anapaswa kuonesha weledi na umakini wenye hekima kuliko unavyojaribu kuji-present.

  Kwanza unaongea kinafiki, ukijaribu kuwa ‘ neutral’ lakini ndani ya mistari unayoandika vimelea vya huo unafiki vinaonekana.

  Huwi wazi sana unaandika kitu fulani ukiitikia mchango wa nani, bali unaandika kama vile hakuna mtu fulani una-respond kwenye comment yake.

  Ongeza uungwana tafadhali!

 2. Mtumishi FINA

  Asante sana kwa mada uliotuwekea mezani.
  Katika hili utafiti wa shetani na wa Yesu UMEENDA VIZURI

 3. TABASAMU LA YESU LINAENDELEA KUCHANUA ZAIDI!!!(WAFILIPI 1:15-18).
  Tunajifunza mengi hapa na kwa wale wanaojitambua kiroho
  wanaendelea KUUONA UTUPU WA WAPOTOSHAJI.Mtumishi
  Pandaeli wakati fulani alieleza habari ya watu kujionyesha
  RANGI ZAO.Kwa muongozo wa Roho Mtakatifu unaweza
  kuona namna ambavyo watu katika mada hii inayohusu
  ulimwengu wa roho TULIVYO ONYESHA RANGI ZETU.

  KILA MMOJA AMESHABARIKIWA NA MUNGU WAKE.
  Wale wanaotembea na roho ya hekima na mafunuo
  wameshaelewa kile ambacho kinamfanya Yesu atabasamu
  hapa.Hakuna atakayeweza kuiharibu mbegu ambayo Roho
  Mtakatifu ameipanda kuhusu uhusiano ulipo kati ya maono,
  ndoto na kazi za mbwamwitu.

  Watumishi Sungura,Pandaeli, Servant,Millinga na wengine wote
  ushiriki wenu NI MUHIMU SANA.Tuendelee KUZIANIKA SIRI ZA
  SHETANI.

 4. Mrs CHRISTINA K.
  Majibu yako yamenishangaza kweli.Mbona husomi hata kile unachoandikiwa vizuri?
  Hebu ona ulichoandika “Tunafahamu tofauti
  ya maono na ndoto na hakuna aliyesema dada fina aliota ndoto”
  Tazama jinsi ulivyokwenda KINYUME NA NILICHOANDIKA “……Hivyo hicho kilichompata Dada Fina kulingana na Maelezo yake ni NDOTO wala si MAONO.”
  Mrs CHRISTINA K, mara nyingi unajibu vitu ambavyo HUJAULIZWA na kuacha vile ULIVYOULIZWA. Mara nyingi hutulia KWENYE MADA na unajikuta upo ” OP”
  Pia Ujue kuwa MWENYE ROHO MTAKATIFU hajitangazi Kama unavyofanya wewe hata Wale MITUME wa YESU hawakujitangaza au Kujinadi Bali watu wenyewe WALIKIRI kuwa wapo pamoja na YESU yaani ROHO MTAKATIFU YUPO NDANI YAO,Pia watu ndio WALIOWAITA WAKRISTO baada ya kuwaona wanamfanania KRISTO( MATENDO 11;26 “…..Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.”).
  Vile vile Watu WALIWAJUA kuwa WALIOPINDUA ULIMWENGU,
  Hata PETRO alipokuwa akimkana YESU WALIMJUA kuwa ni Mwanafunzi wake kwa jinsi alivyokuwa.
  Kwa hiyo, huyu roho uliye naye wa MATANGAZO nina mashaka naye.Ungekuwa na Roho Mtakatifu usingejitetea kwa jambo ulilolifanya la KUMKOSOA na Kumuita Majina Mabaya Mr Milinga wakati alipoandika kitu sahihi.
  Kumbuka VITISHO VYAKO unavyotumia havisaidii bali ni mazingira tu uliyojiwekea ya KUJILINDA au KUJIHAMI( Diffensive Mechanism)
  Pia nashawishika kusema Vitu vingi alivyoandika UMETUMIA AKILI nyingi na wala USIMSINGIZIE Roho Mtakatifu.
  Pia MTEULE huwezi kumjua kwa akili zako.
  ****EPUKA KUJIHESABIA HAKI BURE.****

 5. “Siku moja nikiwa ofisini nikiwa namuuliza Mungu ni kwanini yote hayo, ghafla nilipata kausingizi kazito kama dakika 2 hivi nikaota napita msituni miti imekatwa na inaendelea kukatwa”……Pigania Imani…tazama ni namna gani basi maombi yako ulivyokuwa unayawasilisha hapo ofisini…..muda mwingine tunajisahau namna tunavyoongea na mungu inaweza badala ya kuomba (1)tunatamka maneno magumu (2)tumenung’unika….wakati wa mapito makubwa kama unavyosema ndio wakati wa kuishindania imani sifu shukuru mungu…..misamiati ya kwanini mara nyingi sana haipeleki destiny nzuri….YUDA 1

 6. Mrs. Christina ( japo sina hakika kama kweli wewe ni mrs.)

  Sikuwa na mpango wa kuchangia hii mada, lakini kwa sababu mbili tatu hivi inabidi nachangie kidogo, hasa kuhusu uandikaji wako.

  Kwanza, unafanya mada nyepesi iwe tata for no reason, kwa sababu huna tabia ya kutulia sawia kwenye mada husika.
  Hebu fikiria hapa mada ni ndg Fina kutaka tafsiri ya hiyo miti aliyoota, lakini wewe umejaza mjadala na mambo ya mbwamwitu, wana wa shetani, manabii wa uongo,aghalabu kuliko ulisema tafsiri ya alichkiota Fina.

  Pili, unajaribu kutuonesha kuwa kila kitu ambacho wewe unaandika hapa kimetoka kwa Roho mtakatifu, kitu ambacho si kweli. Ni kujaribu tu kutisha wale walio na mawazo tofauti na ya kwako.

  Tatu, unapenda sana kumwita mbwamwitu au mjumbe wa shetani kila yule ambaye yuko na wazo tofauti na wewe. Mimi hili naliona kama ni uchanga ktk ujuzi wa kweli ya kristo na kiuandishi.

  Na bila shaka hicho ndo kimemfanya hata Pendael akuambie hicho alichokwambia hapo juu.

  Kiukweli Milinga alipojaribu kuja na mawazo tofauti kidogo na ya kwako, ulimjibu na kumwita hayo majina kiujanja tu wa kifasihi.

  Labda nikunukuu ili kuthibitisha hilo:
  “Wajumbe wa shetani (mbwamwitu) mara nyingi wakiona umekaribia
  kupata ufahamu wa jambo fulani kuhusu maisha yako UTAWASIKIA
  WAKISEMA HIYO NI NDOTO YA SHETANI AU NI KWA SABABU YA
  UCHOVU NA SHUGHULI NYINGI KWAHIYO USIWE NA WASI WASI !!”

  Haya maneno kimsingi ulikuwa unamwambia Milinga indirectly.

  Na hii tabia inakufanya uandike makala ndeeefu, lakini pia zisizokaa sawawa kwenye mada husika.

  Inachosha kusoma, na pia inasababisha mtu mwingine aione michango yako kama si ya mtu aliyejifunza.

  Manabii wa uongo wapo tu tangu kale na kale, na hawatalifanya chochote kanisa la kristo.

  ( si ajabu nami nikaitwa mjumbe wa shetani kwa kusema hayo, hahahaaaaa)

 7. Mtumishi PANDAELI
  Mambo ambayo Roho Mtakatifu ananiongoza kuandika hayapingani
  na hoja ya mtu yeyote, yanajitosheleza yenyewe.Tunafahamu tofauti
  ya maono na ndoto na hakuna aliyesema dada fina aliota ndoto.
  Mimi siandiki kwa sababu ya maoni ya wanadamu naandika kile
  ambacho Mungu ananiongoza kuandika.NAFICHUA PALE NINAPOONGOZA KUFANYA HIVYO.WALE WALIO ROHONI WANAELEWA
  KILE AMBACHO ROHO ANAONGEA NAO.

  HAKUNA ANAYEWEZA KUMKOSOA ROHO MTAKATIFU.Katika mjadala
  huu wapo watu ambao wana karama ya kutafsiri ndoto na maono.Na
  hii ni mada nyeti sana katika siku hizi za mwisho lazima wateule waijue
  KWELI.Kama wewe ni mteule tena mnyenyekevu fuatilia MAFUNDISHO
  YA ROHO MTAKATIFU.

  KILA MMOJA ASIMAME KATIKA NAFASI YAKE NA ASEME KILE
  AMBACHO MUNGU WAKE ANAMUONGOZA MAANA SI WOTE
  WANAOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.Hata mimi nikiandika kitu
  kwa mapenzi yangu mwenyewe aliye na ROHO WA KRISTO ATAJUA
  NA ATATUMIA HEKIMA KUNISAHIHISHA.NAWAJUA WATU AMBAO
  WANAONGOZWA NA ROHO YA SHETANI NA UWEPO WAO UNAWAPA
  WATEULE WANAOJITAMBUA ZAIDI YA USHINDI.

 8. Mrs Christina K. Ni vizuri kwa NEEMA ya MUNGU kutafakari kwa kina kuhusu Michango inayotolewa na Wachangiaji wa MADA.Kwa Mfano Mr.Milinga amechangia jambo ambalo limebeba ukweli.Sisi ni binadamu na Wala si MALAIKA na wala tusijiweke kundi la MALAIKA.Tukiwa tunaongozwa na Roho Mtakatifu tunaitwa WANA WA MUNGU (WARUMI 8:14).Hivyo kwa Kuwa Sisi si MALAIKA kuna wakati Tunaota NDOTO zinazotokana na Shughuli nzito au jambo tuliloliwazia sana.Ndio Maana kila NDOTO au MAONO yoyote hupimwa Kwa NENO LA MUNGU.Kutafsiri NDOTO au MAONO ni Kazi ya Mungu.Ndio maana si kila mtu anaweza Kutafsiri NDOTO au MAONO.

 9. Wapendwa. Shalom. Kuna Tofauti Kati ya NDOTO na MAONO.Ndoto hutokea unapokuwa UMELALA na MAONO hutokea ukiwa MACHO.Hivyo hicho kilichompata Dada Fina kulingana na Maelezo yake ni NDOTO wala si MAONO.Tuepuke kuchanganya NDOTO na MAONO.

 10. Mtumishi FINA
  Mtu yeyote anayeongozwa na roho Mtakatifu hupewa ufahamu
  ndani ya moyo wake kuhusu ndoto au maono anayoonyeshwa.
  Elimu kuhusu ndoto na maono(ulimwengu wa roho) ni pana mno
  na inahitaji umakini wa Roho Mtakatifu.Hakuna mtu yeyote duniani
  anayeweza kufundisha mambo ya ndoto na maono KWA USAHIHI
  mpaka ROHO MTAKATIFU ampe MUONGOZO.

  Ulimwengu wa roho umejaa lugha za mafumbo ambayo hakuna
  mtu anayeweza kuyafumbua bila muongozo wa Roho Mtakatifu.
  Hebu jaribu kupiga picha ya maono ambayo Mtume Petro alionyeshwa
  kuhusu KUTOWABAGUA WATU WA MATAIFA.Wakati ule kina Petro
  yaani wayahudi walikuwa wanajihesabia haki kwamba wao pekee
  ndiyo wanaostahili WOKOVU na watu wa mataifa mengine kama
  kina Kornelio hawakustahili!! Kwahiyo Mungu akaamua amtume
  Petro akahuburi habari za wokovu nyumbani kwa Kornelio na
  alipoona kuwa moyo wa Petro utaweka ukuta kuhusu jambo
  hilo AKAAMUA KUZUNGUMZA NAE KWA NJIA YA MAONO.

  Mtume Petro alikuwa anawaona watu wa mataifa KUWA NAJISI
  yaani kwamba akichangamana nao WATAMNAJISI!!Mungu akamvizia
  Petro mchana wa saa sita wakati ameshikwa na njaa sana akamletea
  MAONO ili kuiponya roho yake.Maono aliyoonyeshwa yalihitaji hekima
  ya Roho Mtakatifu na ufahamu wa rohoni ili kujua kile ambacho
  Mungu alikuwa ana maanisha.Ndani ya maono Petro alionyeshwa
  aina zote za wanyama wenye miguu minne na hao watambaao na ndege wa angani.Kisha sauti ikamjia ikasema ondoka Petro uchinje
  ule.Lakini Petro akasema Hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe
  kitu kilicho kichafu au najisi.Sauti ikamjia mara pili ikamwambia Vilivyo
  takaswa na Mungu usiviite wewe najisi(MATENDO 10:9-15)

  Jambo ambalo tunatakiwa kujifunza hapa ni kwamba ingekuwa
  rahisi kwa Petro kwa sababu ya njaa kali kuyatafsiri yale maono
  kuwa Mungu anamuonya kuhusu kutokataa chakula chochote
  ambacho angepewa na wenyeji wake pale alipofikia kwa bwana
  mmoja aliyekuwa anaitwa Simoni.Ingekuwa ni rahisi kwa Petro
  kudhani kwamba Mungu anamwabia ale chochote atakacho
  pewa kwa sababu VIMESHATAKASWA.Pia hapa kulingana na majibu
  aliyotoa Petro tunagundua kwamba alikuwa na changamoto
  ya kuchagua vyakula yaani kuna vyakula ambavyo kwake vilikuwa
  ni najisi.Hata hivyo kwenye maono Mungu alikuwa haongelei habari
  ya vyalula au wanyama kama alivyomuonyesha bali alikuwa anazungumzia WATU WA MATAIFA NA KABILA mbali mbali kwamba
  na wao wanastahili wokovu kwa kuchangamana na wayahudi!!

  Katika maisha ya kawaida kama wewe ni mshauri wa kiroho
  mtu akikusimulia maono kama haya na akaomba tafsiri ni lazima
  uombe hekima na ufahamu wa Roho Mtakatifu ili uweze kumsaidia
  vinginevyo unaweza ukampoteza.Maandiko yanasema katika
  MATENDO 10:17-23 Kwamba baada ya Petro kuonyeshwa yale
  maono hakuyaelewa na alikuwa na shaka ndani ya nafsi yake
  lakini wakati huohuo Mungu alikuwa ametuma watu kutoka nyumbani
  kwa Kornelio ili kutegua kitendawili cha Petro na aliposita kufuatana
  nao ROHO MTAKATIFU akamwambia usisite kwa sababu mimi ndiye
  niliye watuma.Walipomuambia wametumwa na nani na kwa sababu
  gani ndipo Petro akapata ufahamu juu ya kile alichoonyeshwa
  kwenye yale maono.Ndiyo maana walipofika kwa Kornelio jambo
  lililowashangaza wenyeji ni pale Petro alipotamka kwa sauti kuu
  na kusema kuwa ” ……Hakika natambua ya kuwa Mungu HANA UPENDELEO bali katika kila Taifa mtu amchaye na kutenda haki
  hukubaliwa na yeye “-MATENDO 10:34. Ujumbe huu unaonyesha
  wazi kwamba hatimaye Petro alielewa maana ya yale maono
  kwa MUONGOZO WA ROHO MTAKATIFU.Na kuanzia siku hiyo Petro
  aliacha kuwabagua watu wa mataifa mengine wasio wayahudi. KATI
  YA WATU WA MATAIFA NA KABILA ZOTE DUNIANI KUNA WATEULE
  LAKINI SI WATU WOTE DINIANI NI UZAO WA YESU WENGINE NI
  UZAO WA NYOKA(MWANZO 3:15).TUSIPOLIJUA HILI BADO HATUJAWA
  HURU KWELI KWELI(soma na utafakari YOHANA 17:6-17).Yesu hakuja
  duniani kwa ajili ya uzao wa shetani bali kwa ajili ya wateule.Kuna watu mpaka mfumo huu wa dunia utakapoisha HAWATAPATA NEEMA
  YA WOKOVU.

  KUHUSU NDOTO AU MAONO YANAYOTOKA NA UCHOVU,MAWAZO
  AU SHUGHULI TULIZOFANYA MCHANA KUTWA.
  Hizi ni ndoto au maono AMBAYO MARA NYINGI huwapata watu
  WAPUMBAVU(wasio mjua Mungu).Hii haina maana kwamba watu
  ambao hawajaokoa Mungu hasemi nao kwa njia ya ndoto na maono.
  Ukweli ni kwamba huwa anasema nao sana na wakati mwingine
  kuliko watu walio ndani ya wokovu!

  Mungu huwafuatilia wateule wake ambao aliwajua hata kabla
  HAJAWAUMBA(YEREMIA 1:4-5).Unaweza ukawa hujaokoka lakini
  ni mteule wa Mungu na ndiyo maana Mungu anasema na wewe
  kwa njia ya maono na ndoto ingawa mara nyingi humuelewi na
  umekuwa ukipuuzia yale anayokuonyesha au labda umefika
  mahali unadhani ni upuuzi tu usio na maana yoyote.SIKILIZA KWA
  MAKINI duniani kuna watu wabaya na wazuri(MITHALI 16:4 , ZABURI
  58:3).Namaanisha duniani kuna uzao wa Mungu na uzao wa shetani
  na kila mmoja hupewa ndoto na maono na mungu wake.Ndiyo maana
  kwa watu waliookoka huongozwa na Roho Mtakatifu kupambanua
  yale wanayoyaona katika ndoto au maono.YAWEZEKANA KABLA
  YA KUOKOKA ULIWAHI KUOTA NDOTO ZA KIPUMBAVU ZILE ZINAZOELEZEWA KATIKA KITABU CHA MUHUBIRI.
  LAKINI NATAKA NIKUAMBIE NDANI YA WOKOVU HATUNA NDOTO
  ZA NAMNA HIYO, KILA NDOTO UNAYOOTA IWE NI NZURI AU MBAYA
  IMEBEBA UJUMBE AU TAARIFA MUHIMU KUHUSU MAISHA YAKO.
  HEKIMA YA ROHO MTAKATIFU ITAKUWEZESHA KUTAMBUA HILA
  NA MBINU ZINAZOTUMIWA NA SHETANI KWENYE NDOTO NA MAONO.
  HATA UKILETEWA SURA YA MTU AMBAYE HAUSIKI NA HICHO
  UNACHOONYESHWA ILA NI KWA HILA UTAJUA TU.

  Wajumbe wa shetani (mbwamwitu) mara nyingi wakiona umekaribia
  kupata ufahamu wa jambo fulani kuhusu maisha yako UTAWASIKIA
  WAKISEMA HIYO NI NDOTO YA SHETANI AU NI KWA SABABU YA
  UCHOVU NA SHUGHULI NYINGI KWAHIYO USIWE NA WASI WASI !!
  SIKILIZA MPENDWA HAIJALISHI UNAOTA NDOTO AU KUONA MAONO
  YA NAMNA GANI, MUULIZE MUNGU MAANA YAKE.NI LAZIMA UJUE
  KWASABABU GANI AU NI JAMBO GANI LINAENDELEA KATIKA
  ULIMWENGU WA ROHO ambao ni halisi zaidi kuliko huu wa damu
  na nyama.SIRI NA TAARIFA ZA MAISHA YA WATEULE ZIKO KATIKA
  ULIMWENGU WA ROHO AMBAKO NDIPO VITA KATI YA UZAO WA YESU NA UZAO WA NYOKA INAPOANZIA.NA HII NDIYO VITA KALI
  KULIKO ZOTE CHINI YA JUA(Soma na utafakari MWANZO 3:15).

  MTEULE NI WAKATI WETU WA KUANZA KUJITAMBUA KIROHO
  NDANI YA NENO LA KRISTO.

  KWA YEYOTE ANAYETAKA KUWASILIANA NA MIMI BILA YA KUJALISHA KWAMBA NI MBWAMWITU AU MTEULE WA YESU
  TUWASILIANE KWENYE upendouliohai@gmail.com

  MWAKA 2015 NI MTAMU SANA KAMA TUTAISHI NDANI
  YA NENO LA KRISTO NA KUYATAMBUA MAFUNDISHO YA
  MASHETANI.

  KARIBUNI ILI YESU ATUPE CHANGAMOTO HALISI.

 11. Dada Fina,

  Siyo kila ndoto hutoka kwa Mungu. Ndoto nyingi humuijia mtu kwa sababu za uchovu, mawazo mengi, msongo wa mawazo, akili kulemewa, ubongo kuchoka.

  Mara nyingi ndoto itokayo kwa Mungu humuijia mtu akiwa katika hali ya utulivu na bila msongo wa mawazo ya mapito magumu.

  Kama ulikuwa katika hali ngumu ya kuwaza na kutafakari sana, huenda ndoto ikawa ni taswira tu ya mchoko inayotokana na mambo yanayokusonga.

  Ushauri wowote utakaoupata jaribu kuutazama na kuuoanisha na hali halisi kisha Mungu akupe faraja

 12. Mrs. Christina please naomba mawasiliano yako kama hutojali. Nahitaji msaada wa kunasuliwa mahali.

 13. Mjoli Haule
  Barikiwa sana.
  Kuna kanisa ambalo linamtangaza Mungu aliye hai lakini
  limekalia KITI CHA SHETANI!!Mchungaji anadhani amekalia KITI
  cha Yesu kumbe ni cha shetani!Matokeo yake mchungaji anaruhusu
  mafundisho ya mashetani ndani ya kanisa na waumini wanapoyapokea
  wanajikuta wanazini na sadaka zinazotolewa na sanamu.Kila kukicha
  watu wanaendelea kuongozwa na mafundisho ya Baalamu na kwa
  sababu hii Mungu amekasirika na kuyazuia mafundisho aliyolikusudia
  kanisa(mana iliyofichwa).

  Ndani ya mfumo kama huu ambao shetani ameweka kiti chake
  kwenye madhabahu ni vigumu kwa huduma za watu kukua na
  kujulikana ndani ya kanisa.Si tu kwamba kanisa linadumaa kiroho
  lakini pia linakufa kabisa kiroho.Mchungaji anapewa muongozo
  na kiti cha shetani alichokalia.Wanamaombi wanapoona mambo
  hayaendi wanakazana kuvunja nguvu za giza bila ya kutafuta
  maarifa ya jinsi ya kutubu.Ni toba ya kukiri kwamba kuna mlango
  ulifunguliwa mpaka shetani akaingia kanisani na kuweka kiti chake.
  Ndani ya kanisa wale wanaosimamia kweli wanategwa na kuuwawa
  kwa sababu ya uaminifu wao.Mchungaji anashirikia na mbwamwitu
  bila ya kujua.Matokeo yake madhabahu imenajisika kwa kutiwa giza.
  Watu wanakazana kufunga na kuomba na kufanya mikesha kila
  ijumaa LAKINI WANAENDELEA KUTESEKA KIROHO NA KIMWILI!!!
  Vijana hawaoi wala kuolewa, wamekazana na majungu,uzushi,unafiki
  magomvi,wivu,Manung’uniko,tamaa,kiburi na uasherati.Watu wenye fedha na cheo ndiyo wanaopewa upendeleo!Macho na masikio ya rohoni ya kanisa
  yamekufa na wale wanaoona wanamuona shetani aliyejivalisha
  vazi la utakatifu!Pia kama kuna ndoa zinafungwa ni BATILI
  yaani si zile za mpango wa Mungu.

  Mambo haya yameandikwa WAZI KABISA katika UFUNUO 2:12-17
  na ndiyo mambo ambayo yanaendelea sasa ndani ya makanisa
  mengi.Huu ni wakati ambao shetani analipepeta kanisa kwa
  kututenga na IMANI YA KRISTO.Kwa staili hii UMOJA WA KANISA
  unaendelea kuvurugwa.Makanisa hayashirikiani bali yanaumana
  na hii ni vita ya wenyewe kwa wenyewe.Madhabahu nyingi
  zimetiwa giza huku watu wakiendelea kuruka na kushangilia.
  Mbwamwitu(waliokwisha kataliwa) wamejipenyeza kwa siri sana
  ndani ya makanisa yetu nasi tumewapa nafasi za uongozi,
  uimbaji na kuhubiri na tumewaamini sana kuliko tunavyomuamini
  Yesu!!Na wao bila kufanya makosa WAMEVURUGA KABISA KARAMU
  ZETU ZA UPENDO(Soma kwa kutafakari YUDA 1:3,4,12,13).

  MUNGU ANATUTAKA TUFANYE NINI?
  Mungu anasema kama tumegundua tuko ndani ya kanisa
  kama hili dawa ni TOBA.Tunatakiwa kutubu kwa sababu ya
  kufungulia mlango ambao umewafanya mbwamwitu waingie
  na kutuzidi nguvu.Unajua mbwamwitu wanaweza wakaingia
  ndani ya kanisa lakini mkiwajua na kuwazidi nguvu katika ulimwengu
  wa roho wataanza kuondoka mmoja baada ya mwingine.Tunapoingia
  katika maombi ya rehema, Mungu anarejesha macho na masikio
  ya rohoni ya kanisa na roho ya hekima na mafunuo inaanza
  kutawala.Kwahiyo tunapopata huu ufahamu, kanisa zima kuanzia
  mchungaji tunatakiwa kuvaa magunia na kuomba rehema.Mungu
  anatutaka tutubu na tusipotubu NENO LAKE LITAFANYA VITA NA SISI!
  Hapa maana yake tunapata KIPIGO MARA MBILI.Tumeshapigwa na shetani alafu na Mungu anatushughulikia!Ni zaidi ya mateso!Hapa
  watakaopona ni wale tu WENYE MASIKO YA KUSIKIA kile ambacho
  Roho Mtakatifu anatuambia.Roho Mtakatifu anaeleza haya
  katika UFUNUO 2:16-17 “Basi tubu na usipotubu,naja kwako upesi
  nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.Yeye
  aliye na sikio na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa…”

  Mungu anasema atafanya vita na wateule wote wanaojihusisha
  na mafundisho ya mashetani.kuna watu ambao bado wameshikilia
  mafundisho ya Baalamu na mafundisho ya wanikolai(Soma UFUNUO 2:14-15).

  KITAKACHOTOKEA BAADA YA KUKUBALI KUFANYA TOBA
  Ufunuo 2:17 unatoa jibu ” ………Yeye ashindae nitampa baadhi ya ile
  MANA ILIYOFICHWA , nami nitampa JIWE JIPYA na juu ya jiwe hilo
  limeandikwa jina jipya ASILOLIJUA mtu ila yeye aliyelipokea”
  Maana yake kuna kiwango fulani cha mafundisho(mana) ambayo
  yalikuwa yamezuiwa mpaka TUTUBU.Kwa sababu ya kiti cha shetani
  kuna vipawa ndani ya kanisa VIMEFUNIKWA na HAVIJULIKANI.
  Tunapotubu vile vipawa vitafunuliwa nasi tutajulikana kwa majina
  mapya.KANISA LITAKUA KIROHO NA KIMWILI.Upendo na mshikamano
  utatawala ndani ya kanisa.

  Mtumishi christowellu
  Roho Mtakatifu amejibu maelezo yako ya tarehe 22/01/2015 at 10:19 AM.

  Mtumishi Humphrey gutte Onyinge
  Barikiwa na endelea kutega MASIKIO YAKO YA ROHONI.Yesu
  anataka amalize kabisa hii BIASHARA YA MBWAMWITU.

 14. Mrs CHRISTINA K….

  Namshukuru Baba, Bwana wa Mbingu na Nchi kwa kukufunulia hayo maana ndivyo ilivyopendeza mbele zake.

  AMEN …..Kama ilivyoishia 2014 ……Mwaka 2015…….. Pia mashauri yote ya wasio haki………Mbwa mwitu……Mungu wa Mbingu na Nchi anakwenda kuyabadili na kuwa ubatili,

  Mashauri yao…. Yanakwenda kukataliwa nao waenda kujisonga na kufa….(2Fal 17:23)

  ‘Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.

  Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.

  Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku. ” Ayu 5:12-14

  Mjoli Haule

 15. nampenda sana Yesu alikula nao, alikunywa nao lakini hiyo haikumbadilisha kutoka kuwa mwana wa Mungu na kumfanya msukule anayeonekana au asiyeonekana, alibaki kuwa mwana wa Mungu milele na atabaki kuwa hivyo milele. wana wa Israeli kuishi Misri miaka 430 hakikuwabadilisha kuwa wamisri walibaki kuwa waisraeli. mkenya akiishi Tanzania hatogeuka awe mtz atabaki kuwa mkeii. . mchaga yupo kila kona ya tz lakini sijawahi kusikia amebadilika na kuwa kabila jingine analoishimo.
  sauli akizidi kulitesa kanisa akamwendea kuhani mkuu ampe barua akawaue zaidi akiwa njiani kwenda kulitekeleza hilo Yesu akamjia kwa ukali lakini kwa upendo wenye upole “mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. lakini simama uingie mjini nawe utaambiwa yakupasayo kutenda”. sauli hakuwa na tofauti na nabii wa uongo maana hata nabii wa uongo anamuudhi Yesu na siku moja isiyo na jina Yesu atamzuia atamwambia fulani inatosha usiniudhi tena, toa unabii wa kweli naye atamtii maana hakuna anayeagizwa na mfalme moja kwa moja halafu akiuke maagizo yake, halafu hata kama amebadilishwa bado wapo ambao hawataamini watamuona mtu yule kuwa bado ni nabii wa uongo kama kwenye matendo 9:20-21, 26-30.
  katika safari zake mtume Paulo alienda Asia akakaa huko miaka 7 unadhani alikua akifanya nini huko? alikua akizichunguza roho za kule, ni yeye pekee aliyezunguka sehemu nyingi akihubiri lakini pia alikua akijifunza mila na tamaduni zao ili aweze kuzifananisha au kuzitofautisha na Mungu wake yeye ndipo akafikia kutuambia tuzichunguze kila roho, Mrs christina utamtambuaje mtu kama hujamsikiliza au kuangalia matendo yake? Yesu alimtambuaje petro kwamba atamkana? ni dhahiri ni kutokana na tabia yake, alimjuaje Yuda kwamba atamsaliti? ni tabia yake. Mrs christina hakuna aliyekamilika soma danieli 2 na ufunuo 2 na 3 na usipoelewa tafuta kitabu changu kinaitwa udhaifu wako ndiyo adui yako mbaya zaidi usipokipata bado ninazo kopi utapata kitu.
  wakati Yesu anakamatwa petro akamkata mtu sikio na Yesu akamwambia rudisha upanga wako alani mwake, maana hamjui ni roho ya namna gani mliyonayo, petro hakujua kwamba ndani yake kulikua na roho ya msamaha “usiposamehe hausamehewi na Mungu wa mbinguni” na roho ya upendo “waombeeni wanaowaudhi adui zenu” petro alihukumu lakini alisahau kwamba muda mchache unaofata nayeye atakua kama wale atamkana Yesu. siku moja katika kugoogle nikakuta mtu ametoa sala ya kuwaombea wachawi nilipoisoma sikumuelewa hata kidogo ETI akavunja nguvu za giza ukiwemo uchawi halafu akaanza kuwaombea wachawi rehema, ilinipa shida sana maana mentality yangu ilikua si walipenda wenyewe kumtumikia shetani sasa nawaombea nini!? wakati huo nami nilikua kwenye vita kubwa na wachawi wa mtaani kwetu kwahiyo ilikua inaniwia vigumu sana kuelewa lengo la mtoa sala maana nikiangalia mashambulizi waliokuwa wananitupia napambana nao live katika roho wala sijalala kwakweli sikuelewa somo. siku moja roho mtakatifu akaniuliza ” christowellu kwanini wewe ni mtanzania na sio muhindi?” nikamjibu ni kwa sababu nimezaliwa Tanzania. akaniuliza tena kwanini umeokoka? nikasita kujibu nikitafakari swali lile kisha nikamjibu sababu umeniokoa, Akaniuliza tena kwanini unanitumikia? nikamwambia coz umeniita nikutumikie. akaniambia mimi ndiye nilipenda uwe hivyo si wewe NI KWA NEEMA TU, angeruhusu niwe muislamu ningekua labda ningezaliwa ndani ya familia ya mzee juma au al farooq. angependa niwe mzungu, mwarabu, mchina hakuna ambaye angezuia bali ilimpendeza nizaliwe tanzania tena niwe mnyiramba maana hata angependa niwe mndengereko au mkurya ningekuwa, kama ilivyo upande wa nuruni watumishi huitwa na gizani pia huitwa vivyo hivyo, na hawana ubishi maana shetani anao ushawishi mkubwa na wanapoingia huko hata wakitaka kutoka hushindwa maana wametegwa kwa maneno ya midomo yao mikataba waliyoingia, ndiyo sababu unapaswa uwaombee ili wapewe rehema.
  Simoni akamwalika Yesu aje ale kwake, alipokuja mwanamke kahaba Simon akasema moyoni mwake kama Yesu angekuwa nabii angemtambua huyu kahaba yaani Simoni alitaka Yesu asogeze miguu pembeni asiguswe na kahaba how foolish was he!!!!?

  siku moja nikamwambia Mungu kamwe sitakaa nikuelewe ingawa nakujua maana nikimfikiria Yuda alibatizwa ubatizo wa maji mengi, alitumika kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, alitoa MAPEPO aliombea wagonjwa wakapona lakini anaisubiri jehanamu, Musa ilifikia mahali Mungu alimsifia mbele ya wengine kwamba ni rafiki yake na ataongea nae wazi wazi lakini cha kushangaza hata yeye aliyetegemewa kuingia kaanani hakuingia lol huruma na aibu iliyoje kisa nini? alipiga mwamba utoe maji. eliya pamoja na kujitamba kote mbele ya mabaali na kumnadi Mungu wake mbele ya miungu yao bado alifika sehemu akampunguza nguvu, uwezo na mamlaka Mungu wake kwa utisho mdogo tu wa yezebeli. akamweka Mungu pembeni akamkimbia mwanamke ndipo sa Yesu anatuambia ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke. hakuna kanisa lisilo na mapungufu liwe la baba paroko na mama Maria. liwe la kunena kwa lugha. liwe la kizazi cha kwanza au channe. liwe la sadaka ya bahashani au sirini. liwe la nabii wa kweli au wa uongo, la mchungaji wa mshahara au mchungaji wa wito. kikubwa ni Mungu anataka kila mmoja aangalie mapungufu yake kisha atengeneze na Mungu, kwanini anataka hivyo? kwakuwa IPO saa baba anatusubiri tumuabudu katika roho na kweli tu sio samaria- rc. Lutheran, anglikana. wala sio yerusalemu-pentekoste. kati ya farisayo na mtoza ushuru unadhani farisayo tungemwitaje kwasasa kama sio mbea? mbali ya kutuonyesha unyenyekevu wa kila mmoja anapoenda kwa Mungu na mtazamo wa kila mmoja Yesu alitaka pia kutufundisha tuangalie yanayotuhusu zaidi na si kufuatilia ya wengine ooh fulani kafanya hivi au vile kwani Mungu hawaoni? mwenyewe anasema wameumbwa wabaya kwa siku ya ubaya acha Mungu mwenyewe awahukumu you know what? at last its between me or you and God not between us and God. Mimi nimechagua kuabudu katika roho na kweli tu ili anilishe mwenyewe kama alivyoahidi kwenye ezekieli 34:14-16.wakati huo huo nikiogopa kunyooshea wengine kidole maana kwanza naweza kuhukumu mtu fulani mwizi kumbe ngozi aliyokamatwa nayo kaiokota na vidole vinavyobaki vinarudi kwangu, acha nikazane kuondoa boriti langu mie. SHALOM.

 16. WAKATI WENGINE WANAFURAHISHWA NA UWEPO WA MANABII
  WA UONGO WENGINE WANAHUZUNIKA,WANALIA NA KUOMBOLEZA!!!

  Yesu alishajua kuwa manabii wa uongo watakuwepo na watawapotosha YAMKINI hata wateule lakini hakuacha KUTUONYA
  kwamba tuwatambue na kuwaupuka manabii wa uongo.Katika MATHAYO 24:24,25 Yesu anatoa onyo kali na kujiondoa kwenye
  lawama kwa kusema “…..Tazama, nimekwisha waonya mbele”.Yesu
  anasema kwa kuwa nimeshawaambia kuwa manabii wa uongo
  watakuja msije mkanilaumu na katika MATHAYO 7:15 Yesu anaweka
  msisitiza kwamba JIATHARINI NA MANABII WA UONGO(MBWAMWITU).
  Mtume Paulo baadae anaeleza kwa undani kwa nini tunapaswa
  kujiepusha na manabii wa uongo.

  Mtume Paulo alipojulishwa kwamba baada ya kuondoka kwake
  duniani manabii wa uongo(mbwamwitu) wataanzisha mafundisho
  ya uongo ili wawateke na kuwatenga wateule na IMANI YA YESU,
  Paulo alishindwa kujizuia na ikabidi alie na kuomboleza kwa miaka 3
  usiku na mchana!!( soma na utafakari MATENDO 20:28-31).Katika
  Maandiko haya Paulo anatuambia kwamba kazi ya mbwamwitu
  ni kupotosha neno la Mungu ili KUZITEKA NAFSI ZA WATEULE.Unaweza
  usiwe ndani ya huduma ya nabii wa uongo lakini NAFSI YAKO
  IKAWA IMETEKWA na mafundisho yake ambayo unayafuatilia bila kujua.
  Katika ISAYA 42:18-22, Roho Mtakatifu anaeleza kwa undani namna
  ambavyo manabii wa uongo WAMETEKA NAFSI, MACHO NA MASIKIO
  YA ROHONI YA WATEULE na kuwafanya kuwa misukule inayoonekana
  na isiyoonekana!!Kazi nyingine ya manabii wa uongo ni kuzuia ZAKA
  na sadaka zote ambazo wateule walitakiwa kumtolea Yesu.Ni zaidi ya
  hasara kuwa ndani ya wokovu na huku unaujenga ufalme wa ibilisi.

  christowellu asante sana kwa mchango wako.

  KAMA KUNA MTU ANAWEZA KUMFUTA YESU MACHOZI BASI
  NA AFANYE HIVYO.NI RAHISI SANA KUJICHEKA KULIKO KUWACHEKA
  WENGINE!!

 17. Shalom. teh teh dada Christina huwa unanifurahisha sana juu ya manabii wa uongo lol nabaki nacheka sana huwezi kufafanua kitu bila kuwachomeka, kama ndipo ulipoitiwa hapo mwili wako na ukawe dhabihu njema katika kukomboa roho za wateule wanaodanganywa lakini pia ukumbuke kwamba ni lazima wawepo watu kama hao ili neno litimie kama lilivyo tabiriwa. na tena usiache kuwaombea Yesu alituagiza tuwaombee wanaotuudhi yamkini kwa maombi yako ukaokoa roho ya angalau mmoja wao na kumpatanisha na Mungu, kumbuka heri wapatanishi…..

 18. Ubarikiwe sana Mtumishi christowellu!
  umeongozwa kutoa somo na ushauri ambao utatusaidia sana
  hasa katika nyakati hizi ambazo elimu kuhusu ndoto na maono(ULIMWENGU WA ROHO) imepotoshwa na wengi WANAANGAMIZWA
  kwa kukosa HEKIMA na MAARIFA ya Roho Mtakatifu kuhusu yale
  wanayoonyeshwa na kuyasikia kwenye ulimwengu wa roho.Ni neema
  iliyoje kukutana na USHAURI NA MAFUNDISHO YA ROHO MTAKATIFU.
  Manabii wa uongo ambao wengine sasa wanajiita wachungaji na mitume
  ili kuficha uhalisia wao WAMEKAZANA KUFUNDISHA MAFUNDISHO
  NA KUTOA USHAURI ULIO KUFA kuhusu ndoto na maono.Hata hivyo
  pamoja na kuwapotosha waumini wao, vitabu wanavyoandika
  kuhusu maono na ndoto VINAWAFICHUA WAO WENYEWE NA KAZI
  ZAO!!!ISAYA 42:18-20 inaeleza changamoto kubwa tuliyonayo wateule
  katika KUELEWA KILE TUNACHO KIONA NA KUKISIKIA kwenye ulimwengu wa roho.

  Kila mtu aliyezaliwa mara ya pili ana haki ya kutembea na ROHO
  YA UNABII ambayo ni ROHO MTAKATIFU(UFUNUO 19:10).Hii ndiyo
  Roho ambayo hututafsiria ndoto na maono ya aina zote.Kuna watu
  ambao sasa hivi wamejiweka kwenye nafasi ya Roho Mtakatifu
  ya kuwatafsiria watu ndoto na maono na hii ni zaidi ya hatari.Kazi
  kubwa ya manabii wa uongo ni kupotosha na kuzambaza elimu
  ya uongo kuhusu ndoto na maono.Tunatakiwa kueleza habari
  zetu za ndoto KWA KADIRI TUNAVYOONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU
  NA NI HATARI SANA KUWAELEZA WATU MAMBO AMBAYO HATUJARU
  HUSIWA KUYASEMA.KUNA SIRI NYINGI AMBAZO MUNGU HUTUONYESHA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO na ni lazima
  tuombe hekima ya Roho Mtakatifu ili tusiwafaidishe watesi na kumkasirisha Mungu.Na wakati mwingine Mungu anaweza akatoa
  kibali uweke wazi kile ulichoonyeshwa ili WALIOKUSUDIWA WAPONE.

  USHUHUDA
  Mteule fulani ambaye alikuwa akiabudu katika huduma fulani
  ya nabii wa uongo jijini Dar-es-salaam aliwahi kuota ndoto(siyo maono)
  kwamba mmoja wa wasaidizi wa huyo nabii ANAKATA MITI alafu yeye
  akawa anasikitika kwanini huyu mtumishi anafanya hivyo na katika ndoto alitamani sana kama angeweza kumzuia asiendelee kukata hiyo
  miti lakini alishindwa akabaki anamuangalia tu!Baada ya kutoka kwenye
  ndoto alimuomba Mungu amfichulie sawa na YEREMIA 33:3 na LUKA 12:2.

  Hii ndoto ilimnyima amani huyu ndugu lakini hakuelewa nini hasa
  maana yake.Akaota ndoto nyingine kwamba anapigana na nabii wa
  hiyo huduma na kufanikiwa kumpiga na kumshinda na baadae akaota
  tena yule nabii anamshambulia kwa kumrushia nyoka napo pia akamshinda!Akamuota tena msaidizi wa huyu nabii anamzuia asipande
  ngazi zilizokuwa zinaelekea juu kwenye mafanikio fulani.MWISHO WA
  SIKU IKABIDI HUYU MTEULE AKAE CHINI NA KUTAFAKARI KWA KINA
  TENA KWA KUJUMLISHA NA KUTOA ILI APATE MAANA HALISI YA
  YOTE ALIYOONYESHWA.Kabla ya kuwashirikisha watu wengine
  ilibidi kwanza amshirikishe Roho Mtakatifu na hekima ya Yesu ikaanza
  kumpa jibu moja badala ya jingine.

  Kwahiyo kumbe ndoto moja inaweza ikatafsiriwa na ndoto nyingine
  lakini pia si lazima upewe maana ya ndoto yako kwa haraka inategemea Mungu amekusudia nini ingawa ishara huwa zinaonekana
  mapema na kuja kuthibitishwa baadae.Wakati Roho Mtakatifu anaanza
  operation ya kumtafsiria kile alichoonyeshwa, huyu ndugu alianza
  kujiuliza kwanini ALIKOSA AMANI KUMUONA YULE MTUMISHI ANAKATA MITI na kwanini alitamani sana kumzuia?Akapata jibu kwamba kile kitendo cha kukata miti kilikuwa siyo KIZURI na hakina
  wema ndani yake.Roho Mtakatifu akamuambia kwamba ana kitu ndani
  yake ambacho kinapingana na hiyo huduma na Mungu anamuonyesha
  maangamizi yanayoendelea ndani ya hiyo huduma.Hii ilikuwa ni baada
  ya yeye kusoma kitabu fulani ambacho kilikuwa kinaeleza kwamba
  miti tafsiri yake ni watu na hivyo yule msaidizi wa nabii alikuwa
  anaangamiza watu ndani ya ile huduma na yeye akapewa kibali
  cha kutamani kwenda kinyume na hayo maangamizi.

  Roho Mtakatifu akaendelea kumuambia kuwa WENYE HUDUMA
  WAMEMKASIRIKIA kwa sababu anatoa siri zao kwa kuwatafsiria
  watu ndoto na maono wanayoonyeshwa na ndiyo maana sasa
  anaonyeshwa wazi wazi jinsi NABII NA MSAIDIZI WAKE WANAVYO
  MSHAMBULIA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.Na ni kweli kwamba
  huyu mteule alikuwa anaongozwa mara nyingi kuwaeleza watu
  tafsiri ya ndoto na maono wanayoonyeshwa na akakumbuka kuna
  mtu aliwahi kumweleza kuwa tangu amefika katika hiyo huduma
  aliota KWAMBA YEYE NA WENZAKE WAMEINGIA KAMBI YA MAADUI
  KIMAKOSA NA HAO MAADUI WANABUNDUKI NA MBWA WAKALI SANA.Hata hivyo alipomueleza akuelewa kwa haraka mpaka alipokuja
  kuota kuhusu yule msaidizi wa nabii ANAVYOKATA MITI.

  FINA ameonyeshwa INAKATWA NA MWINGINE unadondoka na kumzuia.Maana ya miti ni ile ile lakini kwa yule mtumishi wa kwanza
  ili maanisha WATEULE WALIKUWA WANAANGAMIZWA NDANI YA ILE
  HUDUMA YA NABII WA UONGO NA HUKU KWA FINA WATESI WAKE
  WANAANGAMIZWA INGAWA VITA SI NYEPESI.MAONO YA FINA
  YANAFAFANULIWA KWA UNDANI ZAIDI NA EZEKIELI 2:6.

  MWAKA 2015 ROHO MTAKATIFU ANAKWENDA KUFUNDISHA KWA
  UNDANI SANA ELIMU KUHUSU NDOTO NA MAONO ILI KUWEKA
  WAZI UPOTOSHAJI WA MANABII WA UONGO NA KUZIKOMBOA
  NAFSI ZA WATEULE ZINAZOANGAMIZWA KATIKA HILI ENEO.WATEULE
  WENGI WANAKWENDA KURUDISHIWA MACHO NA MASIKIO YAO
  YA ROHONI KAMA MUNGU ALIVYOKUWA AMEKUSUDIA KATIKA
  YOELI 2:28-32.

  HUU NI MWAKA MTAMU SANA KWA WALE WALIODHAMIRIA
  KUJITAMBUA KIROHO.KIZUIZI CHA MPENYO KATIKA MAISHA
  YA WOKOVU NI DHAMBI NA MARA NYINGI TUMEJIKUTA TUNAJIHESABIA HAKI KATIKA MAMBO MENGI SANA.MUNGU
  ATUREHEMU ILI AKAPOKEE SADAKA ZETU ZA MAOMBI
  NA SADAKA NYINGINE IKIWEMO ZAKA(SOMA ZABURI 51:16-19).

 19. hiyo miti inayokatwa maana yake katika hali ya kawaida miti ikikatwa moja kwa moja inasababisha njia kutokea na mtu kuona mbele kwa urahisi. ulimuuliza Mungu kwanini yote haya yanakupata? amekupa jibu nalo ni sababu ya watu waliokuzunguka kila upande hawakupi nafasi ya kupumua. lakini pamoja na kusongwa huko kunakokatisha tamaa lakini lione tumaini alilokuonyesha kazi kubwa imeshafanyika maadui wengi wameshasambaratishwa. sasa adui zako wako wawili wa kwanza ni huo mti mkubwa unaotaka kukuangukia ukumalize kabisa tafuta unamuwakilisha nani na wa pili mti mdogo uliokuzuia usipite nao ni adui mwingine. sasa huyu anayezuia njia unafanyaje. kwanza lazima uelewe kwamba katika hali ya kawaida umekuta kigogo kidogo ni dhahiri ungekiruka na kuendelea na safari ndio nikakuambia hapo juu kwamba ni Kitu unachokiona ni kidogo sana huoni madhara yake kwa urahisi. kazana kuomba dada maana njia mbele i wazi Yesu alisema namna hii haitoki ila kwa kuomba na mahali pengine tukashauriwa na Paulo tusichoke kumuomba Mungu.

 20. Shalom. dada FINA kwanza kabisa nikuulize swali baada ya kuonyeshwa hayo maono ( si ndoto) ulirudi kumuuliza roho mtakatifu maana yake? maana mwanzo kabisa ulimuuliza swali wakati anakupa jibu ulimuuliza anamaanisha nini? pili nikupe ushauri ni vizuri kabla hujamuuliza mwingine awaye yeyote uwe unamswalika kwanza Roho Mtakatifu- kwanini nasema hivi? kwa sababu kama unataka kujua vya rohoni na umjue sana Mungu unapaswa utafute mwenyewe usipende mteremko wa kutafuniwa kila siku hautaweza kukua hata kidogo. pili wakati mwingine mtu anaweza kukupa tafsiri sawa na alivyoelewa yeye au kutokana na experience yake juu ya kile umemuuliza labda yeye alipewa tafsiri nyingine tofauti kutokana na hali aliyokuwa nayo au lilivyokuwa kusudio la Mungu kwake na kumbe Roho Mtakatifu kwako anamaana nyingine tofauti. mfano imezoeleka mbuzi ni roho za mizimu lakini mbuzi huyo huyo anaweza akawa anakuwakilisha wewe sasa wewe kwa haraka unaweza ukaona amefungwa kamba ukaanza kushangilia kumbe mbuzi huyo anakuwakilisha wewe, ulimwengu wa giza (wachawi, waganga na watumishi wengine wa shetani) wamekufunga miguu sasa niambie hapo hautaomba maombi ya kinyume kweli? maana ulipaswa uvunje matokeo yake umeshukuru. Mungu alimwambia Ezekieli asimame kwa miguu yake ili aseme nae Ezekiel 2:1. tatu ni haki yako akupe akili katika mambo yote kama alivyo ahidi katika 2 timotheo 2:7 amesema katika mambo yote sio darasani tu. sasa nije kwenye tafsiri. kawaida msitu ni kuwa katika confusion inayochangiwa na vitu vingi tofauti tofauti. mti humuwakilisha mkuu hasa katika ulimwengu wa giza yaani mkuu wa anga ambalo wewe uko unakaa maana wakuu wa anga hutofautiana kati ya anga na anga, miti huwakilisha watu wasio wema kwako, wanaokutakia mabaya. miti uliyoiona imekatwa ni maadui waliowekwa pembeni ili upite inaweza kuwa ulifanya maombi ya vita sana au wapo waliosimama kukuombea na maombi yanaendelea na maadui wanazidi kusambaratishwa. hako kamti kadogo kalikoanguka mbele yako kakakublock muulize Roho Mtakatifu ni nani? yupo mtu amekua kikwazo cha wewe kuvuka nawewe huoni kwamba yeye ni tatizo kwako. labda ana kuinfluence tabia zinazomzuia Mungu asijibu haja ya moyo wako. huo mti mkubwa uliouona mwanzo umekatwa halafu ghafla ukaona unakuja kukuangukia yaweza kuwa kuna hali ulidhani umeishinda au kuna jaribu ulidhani umelivuka kumbe bado hujavuka. natumai Kristo atazidi kukufundisha na kukuongoza katika njia unayopaswa kuiendea Zaburi 32:8. Barikiwa.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s