Hakuna kitu kinaitwa Mizimu!!

Wakristo wengi tunashabikia filamu nyingi ambazo zimejaa mitaani zenye majina ya Zombie zikionesha kuwa watu wanaweza kutembea baada ya kufa.

Lakini pia filamu nyingi nchini Tanzania huonesha ndugu wa marehemu wakiwatokea wakiwa na mavazi meupe, kama wafu walio hai, huita mizimu na mahoka

Imani hizi ni mafundisho ya uongo yanayoandaa uongo mkubwa utakaohadaa ulimwengu, wachungaji wengine huwaambia waumini wapya kuwa wanasumbuliwa na roho za ndugu zao waliokufa na kuombewa.

ANGALIZO:
Mungu anasema

Mwanzo 2:17
โ€œWalakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo, utakufa hakika.โ€

Nyoka anasema

Mwanzo 3:4
โ€œNyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa”

HIZO KAULI MBILI NDIO PAMBANO KUBWA, LAKINI MUNGU ALITUONYESHA NAMNA YA KRISTO ALIVYOWEZA KUUCHUKUA UHAI WAKE TENA BAADA YA KUFA. NI KWA KUMMWAMINI MUNGU.

Lena

Advertisements

36 thoughts on “Hakuna kitu kinaitwa Mizimu!!

 1. Mulele,

  Tuendelee tu, mpaka utakua na kupata ufaham wa mtu mzima.

  Unajenga hoja kwa pupa sana. Nilivyoutoa ule mfano wa kilichojiri Yesu alipotembea juu ya maji, mtu akiwa na akili sawasawa hawezi hata kudhani kuwa nilimaanisha Yesu ni mzimu.

  Ni mtu mwenye akili nyepesi tu ktk kuyadadisi mambo ndo anaweza kufikiri nilimaanisha kuwa Yesu ni mzimu.

  Jiongeze ili upate uwezo wa kusoma katikati ya mistari!

 2. We bibi vipi? Ni wapi niliposema ‘Hakuna mizimu’? Sasa kama wanafunzi walisema Bwana Yesu ni ghost hivyo Bwana Yesu ni ghost !? Wengine walimuita Beelzebub na mkuu wa mapepo, je kwa sababu ‘wao’ mmesema hivyo, je ndio yuko hivyo!? Okay uko sawa sister, Bwana Yesu pia ni mzimu !!

  Sungura!? Nimemuomba samahani brother Lwembe nae ‘amenisamehe’ kwa niaba ‘yenu’ hivyo inatosha sister! Mimi nimeshajifunza kutokana na ile ‘deep knowledge’ nnafahamu sasa!

  Amani iwe juu yenu (Asalaam aleikum!)
  Jackson Mulele.

 3. AYUBU 6:9

  “KAMA VILE WINGU LIKOMAVYO NA KUTOWEKA, NI VIVYO HUYO ASHUKAYE KUZIMUNI HATAZUKA TENA KABISA. HATARUDI TENA NYUMBANI KWAKE, WALA MAHALI PAKE HAPATAMJUA TENA”

  YESU AMETUPA UFUFUO SIKU YA MWISHO.

  YOHANA 6:44

  “HAKUNA MTU AWEZAYE KUJA KWANGU, ASIPOVUTWA NA BABA ALIYENIPELEKA; NAMI NITAMFUFUA SIKU YA MWISHO.”

  HAYO MNAYOYAONA MAJUMBANI MWENU NI MAPEPO SIO WAFU.

 4. Lwembe,

  Ilikuwa kidogo tu nikwambie kuwa shule uliyoitoa ktk kumjibu r.m na Mulele iko deep kiasi kwamba nilijawa na mashaka kama wataelewa. Lakini nikasema ngoja nisubiri wajibu.

  Huyo hapo Mulele kajibu, na majibu yake yanaonesha jinsi gani hiyo shule iko mbali mno na ufahamu wake.

  Mulele,

  Umesema huna interest na kujadili mambo ya mizimu.
  Hiyo imenionyesha jinsi gani hujasoma mada inataka nini.

  Kama huna interest ya kujadili mambo ya mizimu hukutakiwa kuchangia katika hii mada, maana inahusu mambo ya mizimu.

  Umejikita sana kujadili suala la kifo,
  na umenukuu mahali ukasema “KISHA TULIO HAI TUTABADILISHWA”!

  Lakini nakushangaa umeshindwa kuona mistari ya nyuma ya happo uliponukuu, panapokwambia kuwa hatutawatangulia ‘waliolala mauti’.

  Sidhani kama unaielewa mantika iliyo katika maneno yanayosema kuwa sisi hatutakufa.

  Kumbuka aliyesema kuwa hatutakufa ndo kasema kuwa Tujapokufa tutakuwa tunaishi. Lazima ujue hapo vinaongelewa vifo viwili.

  Ivi ulishawahi kusoma vizuri lile tukio la Yesu kutembea juu ya maji, biblia inasema wanafunzi walipomwona walidhani ni nani?

  Biblia ya Kiswahili imesema “kivuli” ya Kiingereza imesema “ghost”!

  Halafu wewe unasema hakuna mizimu, au huelewi maana ya mizimu tukueleweshe?

  Huwezi kujadili habari za ufalme wa Mungu, halafu kwenye huo mjadala ukaacha au ukapuuza kumsema shetani.

  Unless umejifunza na kuzijua mbinu za adui yako, huwezi kushinda vita!

 5. Lwembe bro !?
  Umehoji, “Ninasema kwamba ufahamu wako ni wa chini saana, kutokana na wewe kusema kuwa, mambo ya mizimu ni ya kitoto.”
  Hivi bro? Ebrania 5:12 hadi 6:1-3 haisemi waziwazi kuwa “Kufufuliwa wafu na hukumu ya milele” ni mambo ya kitoto!? Ebr5:14 “LAKINI CHAKULA KIGUMU NI CHA WATU WAZIMA, AMBAO AKILI ZAO KWA KUTUMIWA, ZIMEZOEZWA KUPAMBANUA MEMA NA MABAYA” Kwani akili yako haijazoezwa!? Basi sio ajabu !! Bro, mbona Yohana 1; 1-3 inaonyesha wazi wazi wazi kuwa Mungu ni UTATU !? Au akili yako haijazoezwa KUTUMIWA kupambanua!?

  Unazionaje sentesi hizi!? (1) PENDO lina nguvu kubwa saana kupita Mauti!? (2) Tukijifunza PENDO, tutaufahamu udogo na udhaifu wa Mauti na maajenti wake (magonjwa, ajali, udhaifu na UMASIKINI.) (3) Tukijifunza PENDO tutamjua Mungu kuliko kupitia Elimu yoyote chini ya Jua (4) Ili tulijue PENDO ni lazima tuanze kwa Kusameheana na KUPENDANA sisi kwa sisi SG’s

  Nnaomba maoni yenu ndugu zangu

  Asalaam aleikum (Maana yake: Amani iwe kwenu)

  Jackson Mulele.

 6. Lwembe ๐Ÿ™‚
  Umepanic kakah! Hebu tuliza jazba alafu nitafutie mstari unaokuahidi kwamba ukimwamini Yesu utakufa na utaenda ‘mbinguni’. Hilo swali lako samahani kwani sina interest na mambo hayo ya mizimu! Kwani kwa Imani yangu ya kijinga (kama unavyoiita) nnasimama kwamba Bwana aliposema “Waache Wafu wawazike Wafu wao” alikuwa na maana kwamba mambo ya Wafu tuwaachie Wafu, lakini wewe nenda kautangaze Ufalme wa Mungu, akili yangu inanituma kwamba ktk Ufalme hakuna majadiliano ya Kifo! Basi sasa inadumu IMANI, TUMAINI na UPENDO, hayo MATATU.

  Bro, Ukiupata mstari huo, je wewe ni maiti au ni mzima!? (ni lazima ujijue!) kama ni maity ni okay ‘atakufufua’, lakini kama ni mzima mbona unachagua kufa!? Usharogwa!? Ety “Kama HAKUNA KIFO, basi iweje UPEWE Uzima wa Milele?” na ” iwapo hakuna kifo basi na Injili nayo HAIPO” Ama!? hizo ni akili zako Lwembe!? Hujasoma kuwa “Nasi TULIO HAI TUTABADILISHWA!?? Sasa !? Lwembe!? Tangu aliposulubiwa Yesu, kufa ni hiyari yetu! Mitume na Manabii wao ni tofauty na sisi ! Hebu msome Paul ktk 1Korintho 4:9-10 akiwasemea Mitume wenzake! “Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za mungu. Nafikiri Mungu ametufanya sisi mitume tuwe watu wa mwisho kabisa, kama watu waliohukumiwa kuuawa, maana tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu” Je yanakuingia hayo Lwembe!? Je wewe unaengojea kufa alafu ndio upate uzima wa milele unapata wapi hiyo ‘elimu’? Au nawewe ni Mtume!?? Hebu msome tena na tena Paul upate kumuelewa! Unajua ktk Mitume na maNabii Paul ni Mtume ‘wetu’ !! Hebu soma hiyo na usinijibu!

  Asalaam aleikum (Amani iwe juu yenu!)
  Jackson Mulele.

 7. Ndg Jackson,

  Kama HAKUNA KIFO, basi iweje UPEWE Uzima wa Milele? Jambo la kwamba unapewa Uzima wa Milele ni ishara kwamba ulikuwa umekufa, kiroho kwanza halafu kimwili!! Injili ni Habari Njema kwa walio kifoni, mbinguni hakuna Injili inayohubiriwa! Injili ndiyo inayowafufua wafu, Injili ni Ufufuo; iwapo hakuna kifo basi na Injili nayo HAIPO!!!

  Unasema,
  “”Ni lazima sana tujihadhari na tabia zetu na majadiliano yetu ktk BWANA. PENDO ni MUNGU na MUNGU ni PENDO tukianza jifunza habari zake, hatutakuwa na time ya mambo hayo ya โ€˜kitotoโ€™ kuingia akilini mwetu!””

  Maelezo yako haya yanapendeza sana ktk masikio ya wajinga, bali unapoyaleta ktk Maandiko, utaona kwa hakika kwamba ni maelezo ya mtu aliyejichanganya! Biblia ndiyo inayotufundisha kuhusu kifo, na pia kuhusu miungu na mizimu yake; si umesoma kwamba Shetani, pamoja na watumishi wake hujigeuza wafanane na malaika wa nuru; basi ukisema kwamba hakuna mizimu au kwamba mambo ya mizimu ni ya “kitoto”; hauoni kwamba hiyo ni kauli ya mkristo aliye ktk ufahamu wa chini sana?

  Ninasema kwamba ufahamu wako ni chini saaana, kutokana na wewe kusema kwamba “mambo ya mizimu ni ya kitoto” huku wewe mwenyewe ukiwa ktk ibada ya mizimu, nawe hujui!!! Ngoja niyanukuu maelezo yako yanayolithibitisha jambo hili:
  “”” Mungu yupo ktk UTATU Mtakatifu (Trinity)(1) Mungu Baba Luka 18:19 (Yahweh, Jehovah) (2) Mungu Mwana NENO: Yohana 1:1 (Yesu Kristo) (3)Mungu Roho Mtakatifu (Rhoho, ambae ktk Adam, tumepewa Ushirika na Mungu kupitia yeye ambae ndie Pumzi ya Mungu) Mwanzo 1:2b”””

  Haya ni maelezo ya dini ambayo hujiwakilisha kama Neno la Mungu, ndio maana nikasema ni maelezo matamu ktk masikio ya wajinga! Na matokeo ya kuamini tenzi tamu za kuzimu kama hii ni kifo kama cha mtu aliyekuwa blindfolded kwa mafundisho ya dini, kisha kuongozwa Shimoni huku akiimbishwa mapambio ya kwamba HAKUNA kifo, naye akienda KUFA!

  Ulipoambiwa kwamba Shetani hujigeuza afanane na malaika wa nuru, naona mawazo yako yalikupeleka ktk taswira za malaika wanaong’ara, hao wenye mbawa unaowaona ktk sinema; bali Ibilisi ni roho naye hucheza na Maandiko kupitia watumishi wake, ndipo kutoka ktk Maandiko, angekuzalishia tenzi nzuri kama hiyo ya “Utatu” uliyoileta, akiisha kukutekenya na kukuingiza ktk msisimko wa kidini wa kuzaliwa mara ya pili nje ya utaratibu aliouweka Mungu, naye akijua fika kwamba kwa jambo hilo utaishia naye Shimoni!!!

  Usimtengenezee Shetani himaya nje ya Neno la Mungu. Hakuna anayemjua Shetani zaidi ya Mungu, hizi hadithi za “kwamba, Zama za TORATI zilianzia kwa Adam na zilikwishia aliposulubiwa Bwana Yesu” zinakufanya uzidi kudidimia maana ni uongo ulioaminishwa kwamba ndio kweli. Achana na mafundisho hayo mfuate Mungu akufundishe ili uzijue na hila za Shetani maana yeye ndiye mwenye kuyajua mpaka mawazo ya Ibilisi; Isa 45:7 “Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.” (“I form the light, and create darkness: I make peace, and create evil: I the Lord do all these things.” KJV) Umeeelewa?

  Jackson, usizitegemee hisia zako za “utakatifu” wa dini kukuvusha ukiepuke kifo, yafuate Maagizo ya Mungu ili upone, hakuna aliye ktk ibada ya mizimu ambaye HATAKUFA. Wasiokufa ni hao ambao wamefufuliwa kwa Injili nao wakatoka kutoka katika makaburi ya kidini yaliyokuwa yakizishikilia nafsi zao, wakilishwa pumba kama hizo unazotuletea tule! Hebu niambie, utazaliwaje mara ya pili ilhali yule Jackson wa zamani yungali hai? Maandiko yanatuambia kwamba tunashiriki kifo cha Kristo. Je, kuna kati yetu aliyewahi kusulubiwa?

  Haya ni mambo ya rohoni, yanayomzungumzia Adamu wa Mwa 1:26, huyo ambaye aliingia kifoni akiwa ktk mwili, huyu ndiye anayefufuliwa kwa Injili akiipokea ndani yake na ile nguvu iliyomfufua Kristo kwa ajili ya ule mwili wake katika ile siku ya mwisho, ambayo umeisema kwa usahihi kabisa, kwamba ni siku ya mwisho ya kifo! Ndiyo hiyo siku ambayo Kristo atarudi na hao akina Adamu waliofufuliwa huko nyuma kwa Injili, bali miili yao ili lala makaburini, na sasa wakirudi kuja kuichukua kwa ile Nguvu ya ufufuo iliyomo ndani yao waliyoipokea kutoka kwa Kristo kupitia Injili waliyoletewa na mitume! 1Thes 4:14 “Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye”; hawa ni hao ambao walilala mauti wakiwa wameitwa na Mungu kupitia Injili ya mitume, (2Thes 2:14 “Whereunto he called you by our gospel, to the obtaining of the glory of our Lord Jesus Christ”)!!

  Haya Jackson, kuna swali nililomuuliza Lani kuhusu tukio tunalolisoma ktk 1Sam 28:11-19, naona jibu limemtatiza kidogo, amepatwa na kigugumizi cha Injili, basi labda nikusikie nawe unaesmaje kuhusu jambo hili: “Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. 14Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.”

  Huyo muhubiri ktk video hapo juu anasema huyo tunayemsoma hapo juu hakuwa Samweli bali ni mzimu/pepo; nawe unasemaje???

  Gbu!

 8. TUNAPOINGIA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO……
  Ndipo tunapokutana kweli yote tunayotakiwa kuiishi.
  Tujenge tabia ya kutafuta uthibitisho kwenye ulimwengu
  wa roho ambao taarifa zake ni halisi zaidi.Kulielewa neno
  siyo rahisi kama tunavyoweza kudhani, tunahitaji muongozo
  wa rohoni katika mambo mengi.Mtume Paulo alipopelekwa
  kwenye ulimwengu wa roho alipata ufahamu na Maarifa ya kweli.

  Mungu atusaidie sana.

 9. Mrs Christina,
  Ahsante sana kwa changanuo zako zinazoonyesha hamu yako ya kusimama ktk Kristo Yesu.
  Mama!? Ngoja nirudie tena ile kauli ya Bwana alipo mwambia yule mtu alieomba rukhsa kwenda kumzika babaake ambayo kwa maana nyingine alikuwa akimuomba hata rafiki yake Yesu ili nae akashiriki maziko ya babaake! (si ndio kawaida ya ‘urafiki’?) lakini huyu ‘rafiki’ alimjibu nini!?? WAACHE WAFU WAWAZIKE WAFU WAO, BALI ENENDA UKAUTANGAZE UFALME WA MUNGU.

  Kwa kauli hii peke yake, inatujulisha kuwa UFALME WA MUNGU HAUUSIANI NA KIFO !! Sasa hii kujadili Mizimu kwa kweli haihusiani na INJILI !!

  Nilijaribu kuifafanua ile Ebrania 5:11, “Tunayo Mengi ya kusema juu ya jambo hili, lakini ni vigumu kuwaelezeni, kwa sababu ninyi si wepesi wa kuelewa. 12 Sasa mngalipaswa kuwa tayari walimu, lakini mnahitaji bado mtu wa kuwafundisheni mafundisho ya mwanzo ya ujumbe wa Mungu. Badala ya kula chakula kigumu, mnapaswa bado kunywa maziwa. 13 Kila anayepaswa kunywa maziwa huyo ni mtoto bado, hajui uadilifu ni nini. 14 Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu waliokomaa, ambao wanaweza kubainisha mema na mabaya”

  Kumbe kuna “MAFUNDISHO YA MWANZO YA UJUMBE WA MUNGU” Hiyo inaweka wazi kuwa kama yapo ya “KWANZA” basi yapo ya “PILI” na ya “TATU” na kuendelea hadi “UNIVERSITY” sawa sawa na madarasa yetu ya ki-dunia! Mama, kama unamuona Mchungaji anazunguka nchi yote akifundisha watu kuhusu MIZIMU huyo ni mwalimu wa labda la “PILI” ๐Ÿ™‚ Maana NENO linasemaje!? Endelea hiyo Ebrania6:1-3 Basi, tusonge mbele kwa yale yaliyokomaa na kuyaacha nyuma yale mafundisho ya mwanzo ya Kikristo. Hatuhitaji kuweka msingi tena kwa kurudia yale mafundisho ya mwanzo kama vile kuachana na matendo ya kifo, kumwamini Mungu; 2 mafundisho juu ya ubatizo na kuwekewa mikono; ufufuo wa wafu na hukumu ya milele. 3 tusonge mbele! Hayo tutayafanya, Mungu akitujalia” Unaona vile NENO lilivyo tamu!? Je unaona huyo mzee ni Mwl wa darasa gani!? Ukweli ni kwamba hatuna muda wa kujadili ety maadui zetu ni nani, au ety kuna roho zinakaa kuzimu au mambo kama hayo “yasiyo na UHAI” yanatuhusu nini!? ‘Waache wafu wawazike wafu wao, lakini wewe………….’

  Ni lazima sana tujihadhari na tabia zetu na majadiliano yetu ktk BWANA. PENDO ni MUNGU na MUNGU ni PENDO tukianza jifunza habari zake, hatutakuwa na time ya mambo hayo ya ‘kitoto’ kuingia akilini mwetu! Mambo ya kuzimu waache wa kuzimu wayajadili lakini hata NENO lina hoji 2Korintho6:14 -17 “Tena panaulinganifu gani kati ya Kristo na Beriali? Bali wewe nenda “Kautangaze Ufalme wa Mungu” (Mbona mnataka kufa?? Yeremia 27:13, Ezekiel33)

  Nnachelea kuona kuwa “Kanisa limefundishwa kuto kukua” na hiyo inapelekea watu kuuogopa UKWELI ndio maana inakuwa ngumu kupanda ‘darasa’ maana inatakiwa watu ‘wachache’ tu ktk kumjua Kristo Bwana wetu kwa usahini ili KULICHACHUSHA KAPU ZIMA!

  MUNGU ni PENDO na PENDO ni MUNGU, mamaangu! UFALME wa MUNGU tutaujua kwa usahini iwapo tutajifunza IMANI ktk PENDO!
  “Sasa inadumu IMANI, TUMAINI, na UPENDO, hayo matatu na ktk hayo matatu, lililo kuu ni MIZIMU ! ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ˜ฆ ๐Ÿ˜ฆ

  Wa assalaam aleikum! (Amani iwe juu yenu! )
  NB: Wenye ‘elimu ndogo’ hii salaam pia inawakwaza! ๐Ÿ˜ฆ Asie kinyume chetu, yuko upande wetu huyo!

  Jackson Mulele.

 10. Wapendwa mtu akifa amekufa, hakuna suala la mzimu wala wafu kuja kutembelea waliohai. Hizo ni hila la shetani na malaika zake kujenga hofu kwa watu iliwakatambike na kumkosea Mungu. HAKUNA MZIMU WALA MIZIMU, ILA KUNASHETANI ANAYESUMBUA WATU AKIJIFANYA NI ROHO ZA WALIOKUUFA.

 11. Mrs chr.
  Jaribu basi kuweka maelezo mafupi maana Unaendaga flat harafu unaandika vitu vingi yaani nikisoma coment zako kama vile zinafuta kitu ambacho ninakua nimapata kwenye fahamu zangu.

 12. MHUBIRI 9:5
  โ€œKWA SABABU WALIO HAI WANAJUA YA KWAMBA WATAKUFA; LAKINI WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE,โ€

 13. WACHANGIAJI WAMEZUNGUMZA MANENO YANAYOCHOKONOA
  SANA NA WAMEIFANYA MADA KUWA TAMU MNO!!!

  Mulele umetulisha chakula kigumu na kwa wale ambao bado
  wanakunywa maziwa tuwaombee neema ya Yesu ili waoteshwe
  meno ya kutafuna chakula kigumu.NDANI YA KRISTO HAKUNA KUFA
  BALI KUNA KUISHI MILELE LAKINI TUSIPOTII TUTAKUFA NA KUPOTEA
  MILELE.NINI MAANA YA HII SENTESI, “YEYE ANIAMINYE MIMI AJAPOKUFA ATAKUWA ANAISHI”-YOHANA 11:25 na katika mstari wa
  26 Yesu anakazia zaidi pale anaposema “NAYE KILA AISHIYE NA KUNIAMINI HATAKUFA KABISA HATA MILELE. JE! UNAYASADIKI HAYO?”.Ni lazima kumruhusu Roho Mtakatifu atufafanulie neno
  la Kristo kinyume na hapo tutaangamizwa huku NENO LIKITUSIKITIKIA!

  Ni kweli kabisa tulio ndani ya Kristo HATUNA KITU kinaitwa MAUTI!
  Mauti inahusiana na wafu ambao wamefungwa sehemu inayoitwa
  KUZIMU.Kwahiyo kuzimu kuna mizimu ambayo inaitwa mapepo,majini,
  mashetani na majina mengine mengi pamoja na roho za watu waliokufa katika dhambi.Kwa ujumla mizimu ni roho za malaika WAASI
  akiwemo na shetani mwenyewe.Pamoja na kwamba kuzimu ni sehemu
  ya kifungoni lakini roho za malaika waasi zimeruhusiwa kuja duniani
  na kuudanganya ulimwengu wote(Tafakari YUDA 1:6, UFUNUO 12:7-9).
  Hizi roho zinapokuja duniani zitambulika kama ROHO ZIDANGANYAZO(I TIMOTHEO 4:1)
  ndiyo maana zinajivalisha uhalisia wa watu waliokufa ili tuamini kwamba
  hao ni ndugu zetu waliokufa!!Ndugu Servant ameeleza haya kwa upana na undani.Wala hatuhitaji tena kujiuliza mizimu ni nini na inafanya
  kazi gani.Wafu walio kuzimu kule kifungoni hawawezi kuja tena duniani.
  Wapo katika majuto ya milele wakingoja kutupwa kwenye ziwa la moto.MIZIMU IMESABABISHA UMASIKINI NA MATESO MAKALI
  KATIKA MAISHA YA WAKRISTO WENGI.

  Ni nadra sana kukuta ELIMU KUHUSU MATHARA YA MIZIMU
  ikifundishwa katika makanisa ya KIPENTEKOSTE.Ndiyo maana Yesu
  anasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa MAARIFA.Kujua
  mizimu ni nini na inafanyaje kazi ya KUIBA,KUCHINJA NA KUHARIBU
  yaani kuleta LAANA,HAYA NI MAARIFA YA UKOMBOZI.Ndani ya madhehebu ya manabii wa uongo wanafundisha sana elimu ya jinsi
  ya kujikwamua na mizimu lakini uliwahi kuona wapi shetani akimuaibisha shetani mwenzake!?Kwahiyo kama unataka kujua kwa
  undani kuhusu SIRI YA MIZIMU NA JINSI INAVYOFANYA UHARIBIFU
  FUATILIA KWA HEKIMA YA ROHONI YALE YANAYOFUNDISHWA NA
  MANABII WA UONGO TENA IWE NI KWA MUONGOZO WA ROHO
  MTAKATIFU.Ndiyo! Kama wao wanatuma wajumbe wao kuja katika
  makanisa yetu kutupeleleza na Yesu anatuma watu wake kwenda
  KUUANGALIA UCHI WAO.Kimsingi kuna maarifa ambayo wanayo
  yalipaswa kuwa maarifa yetu kwa sababu sio yao bali WANATUMIA
  MAARIFA YETU KUTUANGAMIZA!!!

  Hata hivyo kwa msaada wa Mungu aliye hai na kwa sababu ya
  MAARIFA YA YESU YALIYOMWAGWA DUNIANI KOTE kama ilivyotabiriwa katika HABAKUKI 2:14,NIMEONA SASA KUNA MWAMKO
  MKUBWA WA WATEULE KUELEWA DHANA YA MIZIMU NA NAMNA
  YA KUIKABILI.MWAKA 2014 MWALIMU NA NABII MWAKASEGE
  ALIFUNDISHA MADHARA YA MIZIMU KWA UNDANI SANA NA MBEGU
  HIYO ILIPANDWA NCHI NZIMA.UNAPOFUNDISHA SUALA LA MIZIMU
  NI LAZIMA PIA UWAELEZE WATEULE MADHARA YA KUTOA SADAKA
  KWA MIUNGU MINGINE WAKIWEMO MANABII WA UONGO.UNAWEZA
  UKAPATA MAARIFA YA NAMNA YA KUKABILINA NA MIZIMU LAKINI
  KAMA BADO UNATOA SADAKA ZAKO KATIKA MADHABAHU YA SHETANI UTAENDELEA KUWA MATEKA SAWA NA ISAYA 42:22.
  KWANINI? KWASABABU MIZIMU NI VITENDEA KAZI VYA MANABII
  WA UONGO AMBAO KIMSINGI HAWAKUTENGANISHI NA MIZIMU
  BALI WANAKUUNGANISHA NAYO!!!NA KWA KUWA UNAABUDU KATIKA
  MADHABAHU ZA MIZIMU BILA KUJUA UNAFANYWA KUWA MASIKINI
  KWA SIRI.

  WATEULE TUAMKE NA KUJITAMBUA KIROHO.MAPUNGUFU TULIYO
  NAYO KAMA KANISA TUSIKUBALI YAWE FAIDA NA SABABU ZA
  MANABII WA UONGO KUTUANGAMIZA.

 14. Lani brother,
  Hebu tujadiliane NENO hili ktk Yohana 11.
  Kwa mujibu wa NENO, siku ya ‘mwisho’ ina maana SIKU YA MWISHO WA KIFO (la sihivyo NENO milele litapoteza maana yake!) !! Kwahiyo ‘Kiama’ ni neno lenye maana ya Hatma, Kusanyiko, Hitma au kwa maana rahisi kabisa, KIAMA ni YESU ambae ndie PENDO au UHAI, yaani Yahweh, Jehovah yaani, MUNGU.

  Mungu yupo ktk UTATU Mtakatifu (Trinity)(1) Mungu Baba Luka 18:19 (Yahweh, Jehovah) (2) Mungu Mwana NENO: Yohana 1:1 (Yesu Kristo) (3)Mungu Roho Mtakatifu (Rhoho, ambae ktk Adam, tumepewa Ushirika na Mungu kupitia yeye ambae ndie Pumzi ya Mungu) Mwanzo 1:2b

  Yohana 11:23 Bwana akamwambia Ndugu yako ATAFUFUKA (kwasababu Yesu nipo hapa tayari!)
  Yohana11:24 Najua kuwa ATAFUFUKA ktk UFUFUO SIKU YA MWISHO (Kama wewe Lani na ‘Kanisa’ mnavyo waza)
  Yohana11:25 Yesu akamwambia: Mimi ndimi huo UFUFUO, na UZIMA, yeye aniaminie MIMI ajapokufa atakuwa anaishi. (Yaani, Kanisa eh!? Mkisema ‘UFUFUO” basi ndio MIMI, Mkisema UZIMA basi mjue ndio MIMI !! Adam, Ibrahim, kina Elisha, Daniel, Daudi, na Manabii na ‘Watakatifu’ woote na walioisikia SAUTI YANGU kama huyu kakaenu Razaro, watalala hadi hapo NITAKAPO MPOKONYA SHETANI FUNGUO NDANI YA HIZO ‘SIKU 3’ NITAKAPO SHUKA HADI HUKO HUKO KWAO, KUZIMU NA “KUMFANYIA” Mathayo 27:52-53.
  Yohana 11:26 Nae kila AISHIE NA KUNIAMINI, HATAKUFA KABISA HATA MILELE, je unayasadiki hayo!? (Mstari huu, unatutenganisha na ule wa 25, unamaanisha kuwa 25 unawazungumzia WAKALE kwa waziwazi, na 26 unatuzungumzia SISI TULIO HAI na kutukandamiza na swali ambalo daima tunamtia hofu sana BWANA, IMANI Luka18:8 …..’ataikuta Imani duniani!?! )

  Bwana Yesu, yeye ni JABALI ni MWAMMBA, tukijifunza ktk tabia zake za ubinadamu utakuta alikuwa hashangazwi na kitu chochote kwa maana YEYE ndie alieviumba. Lakini kuna kitu kimoja tu ambacho hicho pekee ndicho chenye uwezo wa kumShangaza Bwana Yesu, sio mara moja wala mara mbili ‘alishangaa’ sana alipokiona! Hebu tujiulize yeye ndie alieumba ‘vitu vyote’ je ni jambo gani hilo linaloweza kum MSHANGAZA Bwana!? Luka7: 9 Yesu aliposikia hayo ALISHANGAA:,

  IMANI ndio vita yetu, Efeso 6:12 ingawa watu wengi tunatumia AKILI lakini IMANI inashindana na AKILI nayo IMANI haina AKILI kama ilivyo kwa AKILI haiwezi kamwe kuwa na IMANI !! Wagalatia 3: 7 Baraka zimeamriwa kumshukia Ibrahim na wanawe nao wenye IMANI hao ndio watoto wa Ibrahim.

  IMANI ndio kitu gani hasa!?

  Naomba tujifunze: IMANI hasa ni kidude, au kitu, au kifaa gani !? Je inaonekana? Inashikika? Ni kitu yabisi au ni kitu cha kufikirika tu!? Je IMANI ni kitu kinaweza kuvaliwa na kuvuliwa na mwenye nacho? Je IMANI inaweza kumshangaza alienayo!? Je IMANI inaambukiza? Je matendo kama kuwaombea watu nao wakapona MANI inahitajika hapo? IMANI pekee ndio iliyomshangaza Bwana alipoiona miongoni mwa watu (hasa wa-Mataifa), ina maana IMANI ni kitu adimu sana ktk binadam. 1Wakorinttho 13:13 Lakini sasa inadumu IMANI, TUMAINI, UPENDO haya matatu, na katika hayo, lililo kuu ni UPENDO!
  Ndugu zangu, haya MATATU ni MOJA! Tunapaswa kujifunza IMANI katika UPENDO ili tuwe na TUMAINI ktk Kristo Yesu
  Asalaam aleikum..

 15. Kaka!?
  Si kweli kwamba sikio la kufa halisikii dawa!! Ni kweli kwamba Ezekiel: 33, Yeremia:27 sikio LIMECHAGUA !!
  NENO linasema na liko wazi wazi kabisaa! “Kisha SISI tulio hai…………” Sasa hebu jiulize, wewe ni maiti au ulio hai!?? Sasa mbona UNACHAGUA mauty!?? Kumbukumbu la Torati 30:19 Lani, unao ‘ufahamu’ wako weye mwenyewe au ni mwngine ndie anakuchagulia!? (sorry bro!) Je sasa ushamjua ni nani anaetuchagulia ๐Ÿ™‚ ?? ni sir IBILISI !!

  Nilikwambia, tujifunze na tujiulize kupitia Yohana 11:21-26. kwamba, Zama za TORATI zilianzia kwa Adam na zilikwishia aliposulubiwa Bwana Yesu (najua hamjafundishwa hivyo, ingawa NENO liko wazi kabisa kwetu ๐Ÿ™‚ ), TORATI (Sheria) iliambatana na kifo ‘ Heri na siku nyingi duniani’ kwamba Ilikuwa hata ukiishika 100% hatimae utakufa tu, lakini ukiwa na ‘tamaa’ ya KUFUFULIWA pindi Yesu (Mwokozi) atakapokuja yaani SIKU YA MWISHO WA MAUTI ! Je unajua kwanini Yohana Mbatizaji ndie kiumbe bora kuliko ‘binadamu’ yeyote alie/atae zaliwa na mwanamke Mathayo 11;11!? Nikwasababu yeye ndie alie MUONA Yesu na KUMTANGAZA, lakini kumtambua kwamba NDIYE, hata Mzee Simeoni alimtambua! Luka2:29, maana Yohana alitumwa kuitengeneza NJIA ya NJIA!!!

  Lani kaka yangu, Bwana Yesu hausiani na kifo!! Wala MAANDIKO hayapingani wakati wowote! Lakini na tujifunze kwa YOHANA, huyu Yesu hasa ni naniiiii!!!?? Hata yeye Yohana na wanafunzi wake liliwachanganya sana pale Yohana alipokatwa kichwa!! Maana walijua kuwa PINDI AJAPO YESU ATATUOKOA NA KIFUNGO CHA MAUTI Ayoub 14;14. lakini mbona Yohana kaafaa?!?!?? (tujifunze!)

  Brother, hili sio somo rahisi ! Ni lazima tutambue kuwa ni ktk Yesu Kristo pekee ndio kuna ‘Madarasa’ ktk kumjua Mungu wetu Ebrania 5:12-14 endelea Ebrania 6:1-3 “Na hayo tutayafanya Mungu akitujalia” Je unaona brother kama hapa tunajadili mambo ya Chekechea!? Je mambo ya CHUO KIKUU ya kuyajadili, ya Uzima wa milele, UFALMENI, Kuishi ktk Utajiri halisia, Kukimbiwa na magonjwa na baba yao kifo, Kuwashangaza na kuwavuta wa-Mataifa kwa Yesu kwa style ya maisha yetu ni Kupi!? Romans13:8 -10, he? UTIMILIFU !? Ina maana PENDO ndio UNIVERSITY OF ALL EDUCATIONS AND CLASSES!!? Ephesians 3:17-19 (ktk vyuo vyenu kuna watu mnawaita ma’Professors, maGwiji, yaani wao ndio walioandika hiyo ‘mitaala’, sasa ktk Pendo NENO anasema “Pendo ni Elimu ipitayo ufahamu wa maGwiji !”) Lakini we blaza kwa vi akilivyo vidogo unanishawishi ety ‘Pindisha’ Maandiko!! ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ Brother mie siwezi labda mtafute Askofu au kadinari au Papa ama ‘Changu’ yeyote akupindishie !!

  INJIRI ya Yesu, haina nafasi ya kujadili kifo!!! Maana ya INJIRI ni “Habari NJEMA kwa watu wooooote!” Kifo sio ‘njema’, RIP sio ‘njema’ !! talaka sio ‘NJEMA’ umaskini sio ‘NJEMA’ magonjwa sio ‘NJEMA’ au we unaonaje bro, R.I.P ni habari NJEMA !?

  Brother Lani, nimeipenda hoja yako yakutaka ‘Kupindisha Maandiko’ ingawa imenishinda, lakini nnakuona we jasiri sana, yaani unamtaka ‘mtu’ alipinde NENO !! ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ we Jeshi nini!?

  Nduguyo
  Jackson Mulele.

  NB: Mathayo 11:11 Yesu ndie Bwana Mathayo :23-25 Yohana ni miongoni mwetu, mie nawe, kumbe ubora wetu ni ktk KUMJUA !
  (tujifunze kaka!)

 16. 1 WATHESALONIKE 4:16-17
  “KWA SABABU BWANA MWENYEWE ATASHUKA KUTOKA MBINGUNI PAMOJA NA MWALIKO, NA SAUTI YA MALAIKA MKUU, NA PARAPANDA YA MUNGU, NAO WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA. KISHA SISI TULIO HAI, TULIOSALIA, TUTANYAKULIWA PAMOJA NAO KATIKA MAWINGU, ILI TUMLAKI BWANA HEWANI; HIVYO TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE.”

  HILO FUNGU LABDA LINATUAMBIA NI LINI WAFU WATAKAPOFUFUKA NDUGU MULELE.
  MAKUNDI MANGAPI JE SIO WALIOKUTWA HAI NA WAFU? AU TUNAPINDISHAJE HILO FUNGU LILETE MAANA KAMA UNAVYOPENDELEA. AU HALIJIELEZI. HEBU ONGEZA NENO ULIPINDE KAMA NI VEMA KUYAPINDA MANENO YA BWANA.

 17. ASANTE NDUGU MULELE NIMEPENDA UNAPOTUMIA MAANDIKO
  INANIPA URAHISI KUJIFUNZA KWAKO.

  NIMESOMA ASSIGNMENT ZAKO ALIZONITUMA. UNANIFANYA NISOME BIBLIA, NAKUSHUKURU.

  LABDA NISAIDIE ANDIKO HILI ULISHUHUDIE KWA ANDIKO YESU ALIMAANISHA SIKU YA MWISHO IPI.

  YOHANA 6:40
  “NA MAPENZI YEKE ALIYENIPELEKA NI HAYA, YA KWAMBA WOTE ALIONIPA NISIMPOTEZE HATA MMOJA, BALI NIMFUFUE SIKU YA MWISHO.”

  LIMEJIELEZA WAZI.
  HEBU LIPINDISHE MPENDWA.

 18. Brother Lani,
  Una’tiririka’ vizuuuri alafu huyo! unatumbukia shimoni!! Atakufufuaje siku ya mwisho ungali hai!? Kuna :1: Waliokufa ktk Kristo :2: WALIOHAI. Je ktk makundi hayo mawili, sisi tuko kundi lipi!? Sasa kwanini mg’ang’anie kufa!? Je hamuisikii sauti ya Shetani humo!? Hamuamini au hamuelewi!? Yesu ni UZIMA, kufa kuko namna 2 na namna zote TUMESHAKOMBOLEWA NA YESU. Aliwaambia dada zake Razaro (Walokole!) Ndugu yenu atafufuka! Akasema ndio najua kuwa atafufuka siku ya mwisho (kama mnavyosema nyinyi!) Bwana akajibu: Hiyo siku ya mwisho ndio MIMI na huo ufufuo ni MIMI na huo UZIMA NDIO MIMI!! Sasa mkisema kuwa siku ya mwisho kakaenu atafufuka ina maana HAMNIJUI !!(kama mnavyo sema nyinnyi SG !!)

  Jamani Yesu hausiani na Kifo!!!!!! kwa maana nyinginee Yesu ni opposite ya Kifo. Hebu study ile Yohana 11:21-26 Kwanza mjiulize swali la msingi je ninyi mmelala MAUTI kama kina Musa, Elia, Elisha, Adam, na Manabii (25?) au nyinyi ni AISHIE yaani MLIO HAI? Mimi, Lani, Dotto, Lwembe, Sungura, John Paul, Wellu, Mchungaji…, Askofu…. da’Mage, Kanisa, Mataifa, Makafiri, ….. (26??) Wote wana subiri INJIRI, hivi ni KWELI kwamba INJIRI ina kifo ndani yake!!?? (Naomba mtu anijibu, NDIO!!)

  KILA UONAPO NENO ‘mauti’ KTK NENO (biblia) UJUE KUNA SAUTI YA shetani INAKUVIZIA !!! KAMA VILE UKIONA ‘PENDO’ BASI KUNA NGUVU NDANI YAKE! au na nyie msharogeka kama Hawa!? Msiogope jamani, NJIA ni Yesu peke yake Nae ni UZIMA ! Nae anatuita sie RAFIKI zake Mbona hamtaki kujadili jambo hili?

  Ni mie
  Jackson.

  NB: Kuna mauti mara2 kwanza ni kupoteza Pumzi ya Mungu (kama Adam !) Alafu ni ile ya kuandikiwa RIP ! Zote hizo zimelipwa kwa DAMU YA YULE ‘MSHKAJI’ !!

 19. Lani,
  Hiyo Biblia niliyoinukuu ni ile ya vitabu 39; basi hebu nipe jibu la swali langu, Je, huyo aliyepandishwa na huyo mwanamke mchawi, alikuwa ni Samweli au mzimu???

 20. YESU KATUFUNULIA YOTE,KUNA WAFU WALIOLALA, MAPEPO PIA YAPO LAKINI MAREHEMU HAWATEMBEI WAMELALA.

  JAPO BINADAMU HULALA YESU AMETULETEA UZIMA NA ATATUFUFUA SIKU YA MWISHO.

  AYUBU 14:12
  โ€œNI VIVYO HIVYO MWANADAMU HULALA CHINI ,ASIINUKE; HATA WAKATI WA MBINGU KUTOKUWAPO TENA HAWATAAMKA.โ€

  1 WATHESALONIKE 4:16,17
  โ€œKWA SABABU BWANA MWENYEWE ATASHUKA KUTOKA MBINGUNI, PAMOJA NA MWALIKO, NA SAUTI YA MALAIKA MKUU, NA PARAPANDA YA MUNGU; NAO WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA, KISHA SI TULIO HAI, TULIOSALIA, TUTANYAKULIWA PAMOJA NAO KATIKA MAWINGU , ILI TUMLAKI BWANA HEWANI; NA HIVYO TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE.โ€

  1 WAKORINTHO 15:52
  โ€œKWA DAKIKA MOJA, KUFUMBA NA KUFUMBUA, WAKATI WA PARAPANDA YA MWISHO; MAANA PARAPANDA ITALIA, NA WAFU WATAFUFULIWA, WASIWE NA UHARIBIFU, NASI TUTABADILIKAโ€

  TUUHIFADHI UHAI WETU UBAVUNI PA YESU,NAYE ATATUFUFUA SIKU YA MWISHO.

 21. NDUGU WAPENDWA

  BIBLIA YENYE VITABU 39 AGANO LA KALE,

  INASOMEKA HIVI;

  KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10-11

  ASIONEKANE KWAKO MTU AMPITISHAYE MWANAWE AU BINTI YAKE KATI YA MOTO, WALA ASIONEKANE MTU ATAZAMAYE BAO, WALA MTU ATAZAMAYE NYAKATI MBAYA, WALA MWENYE KUBASHIRI, WALA MSIHIRI, WALA MTU ALOGAYE KWA KUPIGA MAFUNDO, WALA MTU APANDISHAYE PEPO, WALA, MCHAWI, WALA MTU AWAOMBAYE WAFU.”

  BIBLIA YENYE VITABU 46 VYA AGANO LA KALE

  INASOMEKA HIVYO;

  KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10-11

  ASIPATIKANE KWAKO MTU AMCHOMAYE MWANAWE AU BINTI YAKE KATIKA MOTO, APIGAYE BAAO, AAGUAYE,ANAYEBASHIRI,MLOZI,AFUNGAYE VIFUNDO, AVAAYE HIRIZI, AULIZAYE PEPO AMA MIZUKA, AIOMBAYE MIZIMU AU MAHOKA.”

  BIBLIA YA 1 INATUMIA NENO 1.WAFU 2.WAFU
  BIBLIA YA 2 INA MANENO1.MIZUKA.2. MAHOKA3.MIZIMU

  NAAMINI KWA KUWA WANA IMANI YA PURGATORY AMBAYO HUAMINI WAFU WAPO MAHALI FULANI NA WANAWEZA KURUDI MAJUMBANI KWAO NA KUWATOKEA NDUGU. NDIO MAANA WANAAMINI UMIZIMU NA KUBADILI HAYO MAFUNGU
  BADALA YA NENO WAFU WAKAWEKA MIZIMU NA MAHOKA.

  TUJICHUNGE:

 22. 1Sam 28:11-19
  “Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. 12Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. 13Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. 14Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.

  15Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje. 16Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa BWANA amekuacha, naye amekuwa adui yako? 17Yeye BWANA amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; BWANA amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. 18Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya BWANA, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii BWANA amekutendea hili leo. 19Tena pamoja na wewe BWANA atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena BWANA atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti. ”

  Haya Lani, huyo muhubiri ktk video hapo juu anasema huyo tunayemsoma hapo juu hakuwa Samweli bali ni mzimu/pepo; nawe unasemaje???

  Gbu!

 23. Ndugu yangu Wellu, mi pia ni mmoja wa watu wanapinga hoja ya umizimu.

  Nini je ninachoamini?

  Naamini kuwa mapepo huigiza watu waliokufa.. ili kuwaaminisha watu uongo.

  siamini pia watu wanaokopi mafundisho kwenye mikutano ya injili, bila kutuletea vigezo vya mizimu katika maandiko.
  yaani kuwa wafu wanaishi.

  siamini wafu wanaweza kuturudia kama mizimu au mahoka, naamini kuna mapepo

 24. -Je, ni kweli kwamba mtu akifa roho yake huwa inarudi katika ulimwengu wa walio hai na kuanza kuongoza maisha yao?

  Kama mtu akifa roho yake inahifadhiwa na Mungu mahali fulani basi hicho kinachoishi kama MIZIMU ni mapepo yenye KUIGIZA kama roho ya mtu aliyekufa.

 25. Kwani MIZIMU ni nini? Bila kufahamu maana yake ni vigumu kuamua uwepo au kutowepo kwake.

 26. Hi Da’Margrethe,
  I’m responding after the video which you post, “What does the bible says about ghosts?”. I thought I were the first to answer this topic “Hakuna kitu kinaitwa Mizimu” but surprisingly to see my comment came after your video, which sound like I’m acknowledging with your video, while to me is absolutely erroneous and kindergartens one.

  I’m saying this again to you my sister, Devil has never had his own word when talk to God’s people, but he uses the same WORD OF GOD to misleading us, to prove this study Genesis3:1-1, Mathew4:3,6, Luke4:10- Always the Devil must refer to the ‘Word of God’ . We have to get into our spirit that, Devil is the ONLY enemy to Adam’s children,(Not the Nations!) and you have also to put into your spirit that even Jesus our Lord called Himself as SON OF ADAM for same purpose or rescuing us

  Dear, Jesus came to rescue us from the sin which Adam our father committed through his Rib and received death on his own will. There’s two deaths!!! Spiritually and Physically, and both of them WE ARE REDEEMED BY JESUS OUR LORD, FREEEEEEEEELY!!!!

  Wherever you read ‘any’ scripture in WORD OF GOD which mentioning death, the Devil is there around to trap you with It! (Remember, the Devil has given to ‘Promote or Trap you’ through the scriptures!!!) Remember, there’s two deaths and in both of them, we are freed! The man in the video doesn’t know exactly what he’s talking about but used by the Enemy to implant same fear, Death, all deaths discussions is related to our Enemy. We have to discuss LOVE which is contrary to Death! There’s so much POWER in studying LOVE than discussing death in its weakness. LOVE has more POWER than Death ever obtain. 1John4:7-8; BELOVED, LET US LOVES ONE ANOTHER, FOR LOVE IS GOD, AND EVERYONE THAT LOVETH IS BORN OF GOD AND KNOWETH GOD. HE THAT LOVETH NOT KNOWETH NOT GOD, FOR GOD IS LOVE.
  How about this verses !?

  Please Da’Magreth, let us discuss in Kiswahili, this Kiswahili, will be spoken in heaven ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ (kidding)

  Asalaam Aleikum. (may peace be upon you)

 27. JAMANI TUONYESHANE MIZIMU NA MAHOKA KATIKA BIBLIA, MI NAONA WAFU, MAPEPO NA MKUU WAO IBILISI/ SHETANI.

 28. Shalom Wandugu,

  Ukisema mizimu haipo, ni sawa na kusema shetani/mapepo/vinyamkera/majini/ nakadhalika hayupo, cha kujadili labda ni kujiuliza mizimu (gods)nini.

  Barikiwa
  Anthony M.

 29. Amani iwepo !
  Ni lazima wapendwa kujitambua, either sisi ni wa Adam or sisi ni mMataifa!? (Kuna nguvu ya ziada ktk kulijua hili!)
  Katika wa-Mataifa, Mizimu ilikuwepo kabla ya kuumbwa Adam, na Mungu aliipa uwezo wa kutenda kwa hizo nguvu walizopewa na Yeye Mwenyewe Jehovah 1Samuel 28:7-25. Alipokuja Adam, yeye alikuja na ile ‘Pumzi ya Mungu’ ambayo ilikuwa (ina) na elimu kamili ya Mungu na UWEZA, hata yule mwanamke mchawi alitambua hilo! (mbona nyinyi hamtambui!?)

  Sio rahisi kumshawishi m-Mataifa (wao hawakukatazwa kula tunda la ujuzi yaani kutumia Akili) kuwa “Yesu anaokoa” 1Korintho 18 -19, lakini NENO linasema hata sisi kwa asili ni waMataifa lakini kwa NEEMA tumekombolewa kwa Damu yake Yesu (wala mtu asijisifu……) Na ktk Matendo 17:30, Mungu anatutaka kuelewa kwamba tunaishi ktk zama gani.

  Ndugu zangu, MIZIMU IPO, NA BADO INA NGUVU SANA!! Walakini haikuhusu wewe!!! Mathayo 8:22- Lakini Yesu akamwambia, NIFUATE, waache wafu wawazike wafu wao (mbona hamuelewi??)

  Wa-Asalaam aleikum.
  Mulele.

 30. Kuhusiana na mizimu
  mzimu1 nm mi- [u-/i-] spirit worship place. 2 ancestral spirit, dead personโ€™s spirit….Mizimu ni roho ambazo huchukua uhusika wa watu waliofariki. huwa zina sifa (character) zinapenda kutambikiwa na kuabudiwa kama Mungu…wakati mwanadamu anafariki huwa na hatima mbili tu yaani kwenda mbinguni(Kumkubali YEsu kristo ) au Kuzimu (Kumkataa)…ingawa zipo nadharia ambazo zinajaribu kueleza kwamba hipo sehemu inaitwa limbo sehemu ambazo hukaa roho zilizokufa katika dhambi za asili
  (In the theology of the Catholic Church, Limbo is a speculative idea about the afterlife condition of those who die in original sin without being assigned to the Hell of the Damned)
  Kifupi ni mojawapo ya makundi ya roho zilizoanguka (fallen angel) na mara nyingi sana zinachukua nafasi za kupinga wokovu inapotokea mpendwa katika familia iliyokuwa ipo connected na roho hizo anapookoka. zinahusika na kufunga na kutesa vizazi vya wale walioweka maagano kwa njia ya wanyama, hata kutoa kafara wanadamu kwa lengo la kuzisihi ulinzi, mafanikio, nk.. kazi ya hizi roho kubwa imebainishwa…yohana10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu”…(Laana)
  Lakini mimi binafsi sikuwahi sikia mchungaji yoyote tangia nakuwa akisema mtu anasumbuliwa na mizimu ya nduguze waliofariki(ila kwa waganga washirikina icho kitu kipo)…
  Kifupi roho hizi zipo na zinakuwa zinapenda kujiingiza na kufunga maagano na ndugu waliobakia hai mara nyingi sana katika misiba kutokana na shughuli za mila na desturi za koo au mbali husika, vilevile tamaduni za kurithishana majina na mambop mengi ambayo hayampi mungu utukufu….wakati mwingine unaweza kuwa umeokoka lakini inapotokea msibani kuumia sana kuwa na uchungu wa muda mrefu kupitiliza kuhusiana na ndugu huyo aliyekufa huwa inatokea katika Ulimwengu wa roho unaunganishwa na roho hizo…
  Dalili ya roho hizi….kufungwa kielimu, magonjwa ya urithi, tabia zisizompa mungu utukufu zinazofanana katika ukoo, umasikini, wokovu kuwa na vita kwa mhusika, ndoto zakuongea na wahenga mara kwa mara..
  ……..Kifupi roho hizo zipo na zinapigana usiku na mchana kuleta mabalaa kwa watu wanaojiunganisha nazo waliounganishwa nazo kwa kujua au kutokujua..na kuleta hujuma kwa waliookoka kutoka koo zilizowatambikia wasisonge mbele na kuwakatisha tamaa….ashukuliwe MUNGU anatupa kushinda na kusonga mbele

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s