Kuvamiwa kwa Taifa la Israel!!

Mungu awabariki sana, mimi ninaomba mnisaidie kujua kuhusu kuvamiwa kwa Taifa la Israel je kutatokea baada ya unyakuo au kutatokea kabla ya unyakuo? na ni mataifa gani yatakayoungana kuivamia Israel kama anavyosema Zaburi 83 yote vita ambayo itakomeshwa na Kristo baada ya kuja na kusimama katika mlima wa mizeituni?

–Jovianus

Advertisements

27 thoughts on “Kuvamiwa kwa Taifa la Israel!!

 1. BWANA WETU YESU KRISTO ASIFIWE.wapendwa wakristo wanzangu,mungu awabariki kwa michango yenu.nimebarikawa sana,lakini kumbukeni kuwa mtu mmoja hawezi pewa ujuzi wa mambo yote,kwa sehemu mtu anafahumu na tena mwengine anafahumu kwa sehemu,tukiunganisha yaliyo ya kweli toka kila sehumu tutafanya vyema.kitu muhimu sana ni kumjua YESU KRISTO KWA USAHIHI ZAIDI ILI TUE NA UZIMA WA MILELE,vile inavyo sema maandiko,UZIMA WA MILELE NDIO HUU,WAKUJUE WEWE MUNGU WA KWELI NA WA PEKEE NA YESU KRISTO ULIYE MTUMA,JOHN 17:3.si vibaya kujua wakati na nyakati na matukio lakini atanisopozijua lakini ninao wokovu wa kweli,kwa kutubu na kubatizwa kwa jina la yesu kristo na kujazwa roho mtakatifu na kuishi maisha yanayo mpendeza mungu,sitakosa uzima wa milele kwa kuwa sijui nyakati na matukio.tuendeleeni kuchangia lakini tujue haya mambo ni mazito mno,kwaivyo tusimdharau mtu kwasababu tu amekosa ufahamu,na kila mtu ajifunze kwa mwenzake akiona angalau pana ukweli.

 2. Bwana yesu asifiwe wapendwa mimi nimpongeze ndugu sungura kwa mchango nami nongezee maelezo kidogo hapo Biblia inasema mungu anasema hapendi kuona hata mtu moja anapotea anataka kuona wote wanaokolewa pamaoja na hayo watu bado wanapenda giza kuliko kuipendanuru sasa nije kwenye mada taifa la israel litavamiwa baada ya unyakuo kwa nini
  1.baada ya kanisa kunyakuliwa mpinga kristo ataanza kutawala kwa kipindi cha miaka saba kipindi ambacho kitagawanywa kwa vipindi viwili na kila kipindi miaka mitatu na nusu(ufunuo 11:-2..3miezi arobani na miwili(42)/ufunuo 13:5) kipindi hicho biblia inasema itakuwepo dhiki ambayo hajawahi kutokea tangu ulimwengu uumbwe soma mathayo 24:21) wakati huo kutakuwa hakuna kuuza wala kununua mpaka uwe una chapa ya mpinga kristo yaani namba sita sita 666 sasa kipindi cha kwanza mpinga kristo ataelekeza mateso makali kwa mataifa mengine kwa israeli kutakuwa na ahahueni lakini kipindi cha pili yaani miaka ile mitatu na nusu mpinga kristo ataigeukia taifa la israel mateso yakayo ipata israel yatafanya watambue kuwa yule hakuwa masihii wa kweli na kufanya upinzani naye watapata mateso mpaka watakimbilia katika bonde la halima gedoni na kumulilia bwana kutokana na maagano ambayo bwana alisha jifunga na yakobo,israel itamfanya yesu aje kuwaokoa israel kwa kila kabila watu kumi na mbili elfu
  2.leo utakuta mtu anakataa kuokoka anasema ataoka siku za mwisho hutakuwa na nafasi wakati huo unatakiwa kuokoka sasa ndio wakati uliokubalika ambao ni sasa
  kipindi cha dhiki kuu au dhiki kubwa ndipo taifa la israel litavamiwa na kuzidiwa kulingana na kumkataa mpinga kristo ambaye atakuwa anatawala wakati huo na lazima ujue israel taifa kubwa lenye nguvu kubwa za kijeshi
  kwa leo nishie hapo

 3. Lani, Usiwe na hofu kwani Wewe na Wasabato wenzako pamoja na Wale Waliokataa Injili Iliyohubiriwa na Mitume MTAPITIA KWENYE DHIKI KUU. *** MITHALI 27:22 ” Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano;Upumbavu wake hautamtoka***

 4. Mungu alimwokoa Nuhu from gharika. Mungu alimuokoa Lutu from moto wa Sodoma na Gomora.Kadhalika Yesu atalinyakua kanisa lake litoke duniani kabla ya dhiki kuu.

  Revelation 3:10.
  Because thou hast kept the word of my patience, I also will keep thee from the hour of temptation, which shall come upon all the world, to try them that dwell upon the earth.

  TOFAUTISHA UNYAKUO NA KURUDI YESU MARA YA PILI. UNYAKUO NI KABLA YA DHIKI KUU NA KUJA KWA YESU MARA YA PILI NI BAADA YA DHIKI KUU.

 5. Mungu alimwokoa Nuhu from gharika. Mungu alimuokoa Lutu from moto wa Sodoma na Gomora.Kadhalika Yesu atalinyakua kanisa lake lito duniani kabla ya dhiki kuu.

  Revelation 3:10.
  Because thou hast kept the word of my patience, I also will keep thee from the hour of temptation, which shall come upon all the world, to try them that dwell upon the earth.

  TOFAUTISHA UNYAKUO NA KURUDI YESU MARA YA PILI. UNYAKUO NI KABLA YA DHIKI KUU NA KUJA KWA YESUS MARA YA PILI NI BAADA YA DHIKI KUU.

 6. YESU ATAKUJA BAADA YA DHIKI KUU,

  SHUHUDA HII HAPA CHINI NI YESU MWENYE ANAZUNGUMZA:

  MATHAYO 24:29-31

  “LAKINI MARA BAADA YA DHIKI SIKU ZILE, JUA LITATIWA GIZA, NA MWEZI HAUTATOA MWANGA WAKE, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA; NDIPO ITAKAPOONEKANA ISHARA YA KE MWANA WA ADAMU MBINGUNI; NDIPO; MATAIFA YOTE YA ULIMWENGU WATAOMBOLEZA, NAO WATAMWONA MWANA WA ADAMU AKIJA JUU YA MAWINGU YA MBINGUNI PAMOJA NA NGUVU NA UTUKUFU MWINGI. NAYE ATAWATUMA MALAIKA ZAKE PAMOJA NA SAUTI YA PARAPANDA, NAO WATAWAKUSANYA WATEULE WAKE TOKA PEPO NNE,TOKA MWISHO HUU WA MBINGU MPAKA MWISHO HUU.”

 7. Yesu atakuja kabla ya dhiki kuu. Pia Yesu atakuja kabla ya kuvamiwa Isael. kUJA KWA YESU NA KUVAMIWA KWA ISRAEL YATATOKEA KWA MFULIZO YAANI KWA MUDA MFUPI, YAKIKARIBIANA. Mataifa yatakayoivamia Israel yatakuwa Iran, Urusi na China na mengineyo. Soma Ezekiel 36,37,38 na 39.

  HEMBIU SOMENI PIA HII HABARI NZURI HAPA CHINI KWA KIMOMBO:

  Astonishing 1968 Prophecy by 90-Year-Old Woman
  8:00AM EST 2/10/2015 Bert Farias

  An old woman of 90 from Valdres in Norway had a vision from God in 1968. The evangelist Emanuel Minos had meetings (services) where she lived. He had the opportunity to meet her, and she told him what she had seen. He wrote it down, but thought it to be so unintelligible that he put it in a drawer. Now, almost 30 years later, he understands he has to share the vision with others.
  The woman from Valdres was a very alert, reliable, awake and credible Christian, with a good reputation among all who knew her. This is what she saw:
  “I saw the time just before the coming of Jesus and the outbreak of the Third World War. I saw the events with my natural eyes. I saw the world like a kind of a globe and saw Europe, land by land. I saw Scandinavia. I saw Norway. I saw certain things that would take place just before the return of Jesus, and just before the last calamity happens, a calamity the likes of which we have never before experienced.
  She mentioned four waves:
  1. “First before Jesus comes and before the Third World War breaks out, there will be a ‘détente’ like we have never had before. There will be peace between the super powers in the east and the west, and there will be a long peace. (Remember, that this was in 1968 when the cold war was at its highest. —E. Minos) In this period of peace there will be disarmament in many countries, also in Norway and we are not prepared when it (the war) comes. The Third World War will begin in a way no one would have anticipated—and from an unexpected place.
  2. “A lukewarmness without parallel will take hold of the Christians, a falling away from true, living Christianity. Christians will not be open for penetrating preaching. They will not, like in earlier times, want to hear of sin and grace, law and gospel, repentance and restoration. There will come a substitute instead: prosperity (happiness) Christianity.
  “The important thing will be to have success, to be something; to have material things, things that God never promised us in this way. Churches and prayer houses will be emptier and emptier. Instead of the preaching we have been used to for generations—like, to take your cross up and follow Jesus—entertainment, art and culture will invade the churches where there should have been gatherings for repentance and revival. This will increase markedly just before the return of Jesus.
  3. “There will be a moral disintegration that old Norway has never experienced the likes of. People will live together like married without being married. (I do not believe the concept ‘co-habitor’? existed in 1968. —E. Minos.) Much uncleanness before marriage, and much infidelity in marriage will become the natural (the common), and it will be justified from every angle. It will even enter Christian circles and we pet it—even sin against nature. Just before Jesus’ return there will be TV programs like we have never experienced. (TV had just arrived in Norway in 1968. —E. Minos)
  “TV will be filled with such horrible violence that it teaches people to murder and destroy each other, and it will be unsafe in our streets. People will copy what they see. There will not be only one ‘station’ on TV, it will be filled with ‘stations.’ (She did not know the word ‘channel’ which we use today. Therefore she called them stations. —E. Minos.) TV will be just like the radio where we have many ‘stations,’ and it will be filled with violence. People will use it for entertainment. We will see terrible scenes of murder and destruction one of the other, and this will spread in society. Sex scenes will also be shown on the screen, the most intimate things that takes place in a marriage.” (I protested and said, “We have a paragraph that forbids this kind of thing.” —E. Minos.) It will happen, and you will see it. All we have had before will be broken down, and the most indecent things will pass before our eyes.
  4. “People from poor countries will stream to Europe. (In 1968 there was no such thing as immigration. —E. Minos.) They will also come to Scandinavia and Norway. There will be so many of them that people will begin to dislike them and become hard with them. They will be treated like the Jews before the Second World War. Then the full measure of our sins will have been reached (I protested at the issue of immigration. I did not understand it at the time. —E. Minos.)
  The tears streamed from the old woman’s eyes down her cheeks. “I will not see it, but you will. Then suddenly, Jesus will come and the Third World War breaks out. It will be a short war.” (She saw it in the vision.)
  “All that I have seen of war before is only child’s play compared to this one, and it will be ended with a nuclear atom bomb. The air will be so polluted that one cannot draw one’s breath. It will cover several continents, America, Japan, Australia and the wealthy nations. The water will be ruined (contaminated?). We can no longer till the soil. The result will be that only a remnant will remain. The remnant in the wealthy countries will try to flee to the poor countries, but they will be as hard on us as we were on them.
  “I am so glad that I will not see it, but when the time draws near, you must take courage and tell this. I have received it from God, and nothing of it goes against what the Bible tells.
  “The one who has his sin forgiven and has Jesus as Savior and Lord, is safe.”
  Bert M. Farias, revivalist and founder of Holy Fire Ministries, is the author of several books including the newly released My Son, My Son—a beautiful father-son journey co-written with his son Daniel for the purpose of enriching and empowering parents to train their children in God’s ways. He is also the co-host of the New England Holy Ghost Forum, a school of the Spirit. Follow him at Bert Farias and Holy Fire Ministries on Facebook or @Bertfarias1 on Twitter.
  Unless otherwise specified, the opinions expressed are solely the author’s and do not necessarily reflect the views of Charisma Media.
  Did you enjoy this blog? Click here to receive it by email.

 8. Hali ya Taifa la Israeli imefungwa ktk unabii uliotolewa ktk kitabu cha Daniel, yale “Majuma Sabini”, Dan 9:24 ” Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu…”

  Basi ukijua Israeli leo hii wako ktk juma la ngapi, utaijua na hali ya Kanisa, maana Mungu aliahidi kuwarudia Israeli baada ya kuwatia upofu ili Injili ije kwetu. Hivyo umuhimu wa Israeli ktk kujua hali yetu si jambo la kupuuzwa, maana wakati wetu wa kuokolewa unakoma hapo Mungu anapowarejea Israeli akiisha kuliondoa Kanisa lake ktk lile tukio maarufu linalosubiriwa nasi sote kwa hamu kubwa sana bila ya Maarifa!!!!

  Ndio kusema Kanisa linaweza liakawa limeondolewa tayari nasi HATUJUI tumekazana tu na mafundisho yasiyo na tija, yanayotutia upofu na ujinga wa kuyaondoa macho ktk kutazama panapostahili, Neno la Mungu, ile Injili ya mitume, badala yake tumepewa kutazama mafundisho ya dini yanayoelea hapa duniani yakingojea kuangamizwa pamoja nasi tuliyoyashikilia!

  Wengine baada ya Israeli kutoweka ktk ramani ya dunia, wakajizalishia mafundishao kwamba HAKUTAKUWEPO tena na Taifa la Israeli, Mungu amelifuta na nafasi yake kupewa Kanisa; yale majuma sabini wakayamalizia kwa Titus alipoibomoa Yerusalemu; Ghafla Israeli imewaibukia, kama mtu aliyeufungua mlango wa bafuni wakati unaoga; ndio hao wameyashikilia mafundisho yao (kile kitaulo), wanashindwa kwenda kuchukua Kweli ya Injili iwafunike aibu yao, ndio hao wanaokuambia HAKUNA UNYAKUO ule wa Siri!

  Jambo zuri ni kwamba wanategemea kupita ktk Dhiki Kuu kwa kukiri kwao wenyewe, Mungu awarehemu ktk ujinga wao!

  Gbu all!

 9. Endelea kubarikiwa sana mtumishi Israeli
  maelezo yako ni muhimu sana.Ni vyema mtu kukosolewa
  kuliko kupambwa wakati wote.NAENDELEA KUJIFUNZA.

 10. Wapendwa; MSIDANGANYWE au MSIPOTOSHWE na Mafundisho yasiyoendana na BIBLIA .Kanisa la Mungu Aliye Hai (Bibi Arusi Wa Kristo) HALITAPITIA KWENYE DHIKI KUU.Wale Wanaosema hakuna KUOKOKA sasa ndio watakopitia Dhiki pamoja na WANAWALI Wapumbavu ambaye hakuwa na Mafuta (ROHO MTAKATIFU).Hawa WANAWALI wapumbavu Wameamini NENO HALISI LA MUNGU na Hawapo kwenye Madhehebu,Wapo nje ya Madhehebu.

 11. Duh mi mnanichanya tu maana kila mtu ni mtaalamu kutetea hoja yake Ananikela mtu mmoja Tu anayejifunika Roho Mtakatifu bila Yesu Ili asingwe maelezo anayotoa mi nadhani mtu kutoa maelezo yanayotofautiana na idea zako haimfanyi kua Umbwamwitu Huwenda we ndo ubwamwitu wa ukweli Yesu anasema unatowaje kibanzi jicho la jilani yako wakati una bonge jiti jichoni mwako mi nimsomaji tu wa mada na coment sina la kusema juu ya mada maana nachanganyikiwa tu pia nayitowa kelo yangu hio Mchangiaji filani ananikela si mada hii tu mada zote anazochangia anajifunika Roho Mtakatifu bila Yesu na kuvaa macho ya Ubwamwitu ndio maana anaona wenzie kama ubwa mwitu haishangazi hata mlevi somtime anaona watu kama miti inatembea.
  Asanteni nawapendeni nyote najifunza vingi kutoka kwenu na Mungu aibariki Blog hii na utukufu ni kwake Kristo.

 12. MAKUNDI YALIYOAMUA KUPOTEZA UKWELI JUU YA KUWA
  ROHO YA MPINGA KRISTO INATENDA KAZI HATA SASA. NDIO WANAOTAKA IONEKANE KUWA TAIFA FULANI LA NCHI ZA MASHARIKI NDIZO ZITAKUWA NA MKUU AMBAYE ATAIBUKA KAMA MPINGA KRISTO KWA KUVAMIA ISRAELI.

  NA KUPOTEZA WATU WAJUE KUWA MPINGA KRISTO HATOKI NDANI YA UKRISTO. BALI NI MKUU WA MATAIFA YA MASHARIKI ATAKAYEONGOZA MATAIFA FULANI KUIVAMIA ISRAELI YA KIMWILI.

  1 YOHANA 4:3
  “..NA HII NDIYO ROHO YA MPINGA KRISTO AMBAYO MMESIKIA KWAMBA YAJA; NA SASA IMEKWISHA KUWAKO DUNIANI.”

  MFUMO WA
  Praeterist:
  ULISEMA MPINGA KRISTO ALIKUWA NERO, UKAWA UMETABIRI MAPEMA SANA KINYUME NA BIBLIA.

  Futurist :
  ULIZUNGUMZA HABARI YA BAADAE SANA JUU YA UVAMIZI WA TAIFA LA ISRAELI YA KIMWILI NA MPINGA KRISTO,BAADA YA UNYAKUO IKAWA MBELE SANA JUU YA TUKIO.
  WAKIDHANI PIA ISRAELI ITAVAMIWA BAADA YA UNYAKUO. MFUMO HUU UMECHUKUA MADHEHEBU YETU MENGI YA KIKRISTO.

 13. WAKRISTO WALIOIAMINI DAMU YA YESU HAWAHITAJI TENA DAMU YA WANYAMA. HIVYO

  DHIKI KUU ITAANZA NDIO KUNYAKULIWA KUMLAKI BWANA MAWINGUNI KUTAFUATA.

  WATAKATIFU WATAKAVYOINGIA MBINGUNI WALIOKUWA MBINGUNI WATAZUNGUMZA HIVI?

  UFUNUO 7:14
  “NIKAMWAMBIA , BWANA WANGU, WAJUA WEWE. AKANIAMBIA, HAO NDIO WANATOKA KATIKA DHIKI ILE ILIYO KUU, NAO WAMEFUA MAVAZI YAO, NA KUYAFANYA MEUPE KATIKA DAMU YA MWANAKONDOO.”

 14. HONGERA MTUMISHI LWITIKO

  Maelezo yako yanaendelea kutimiza UNABII WA YESU katika
  LUKA 12:1-2 ambayo inasema
  “………Jilindeni na CHACHU(MAFUNDISHO) ya Mafarisayo,ambayo ni
  UNAFIKI.LAKINI HAKUNA NENO LILILOSITIRIKA AMBALO HALITAFUNULIWA , WALA LILILOFICHWA AMBALO HALITAJULIKANA”

  UHUSIANO WA TAIFA TEULE NA MATAIFA MENGINE DUNIANI
  PAMOJA NA NCHI ADUI WA TAIFA HILI NA NINI KINACHOENDELEA
  NI MAMBO AMBAYO YALIKUWA YAMEFUNIKWA KWA MUDA MREFU
  HASA KWA WATEULE WALIO WENGI LAKINI KWA SASA MAMBO
  HAYA MTUMISHI LWITIKO AMEYAWEKA WAZI MNO KULIKO VAZI
  LA KAHABA MZOEFU!!!

  NAENDELEA KUJIFUNZA MENGI HAPA KWA JINSI YA ROHONI.

 15. Katika ile zaburi ya 83: 6-8 anayataja hayo mataifa. Yalikuwa ni mataifa ya zamani sana kipindi cha agano la kale. Lakini mpaka yao haijafutika hata sasa kama Israel ilivyokaa katika nchi waliyopewa miaka 3000 iliyopita hata sasa. Mipaka haijafutika hata kama haionekani kuwa ipo kwa sasa lakini ipo. Hema za edomu na waishmaeli ni palestinians Arabs pamoja na wajordani wa kusini, moabu na wahagari ni waarabu wa Palestine pamoja na wajordani wa kati. Gebali, amoni na waameleki ni Hezbollah, Lebanon ya kaskazini na waarabu wa Sinai.
  Filisti, tiro na ashuru ni Hama’s walioko Gaza, hezbollah, Lebanon ya kusini. Ashuru ni Syria na kaskazini ya Iraq. Kumbuka hata maeneo yanawakilisha mipaka isiyofutika na nani anakaa katika mipaka hiyo kwa sasa

 16. Asante kaka sungura kwa kulielezea jambo hili. Michango wako umegusia vitu muhimu na Dada Christina pia. Hivi nani anajua ugomvi unaondelea mashariki ya kati kati ya Israel na waarabu wa Palestine ni ugomvi wa kugombea kitu gani hasa? Kwa nini mataifa ya kiislamu ya kiarabu kila wakati yanafikiria kupigana na kuiondoa Israel mahali ilipo! Mataifa hayohayo pia yanawatesa wakristo mashariki ya kati. Huu mkakati wa mataifa ya kiarabu ya kumsimika Mungu wao ” Allah”,na kufanya uislamu uenee na kutawala dunia kama maono yao yanavyowaonyesha wako tayari kufanya vita. Watafanya vita na wa kristo wanaomjua Yesu watafanya vita na Israel. Watafanya vita na kanisa watafanya vita na Jerusalem. Ila Mungu wetu atajifunua na kujijulisha yeye ndiye Mungu mkuu na wala sio yule wafuasi wake wanaosema ” Allah Akbar” yaani Allah is the greatest . katika zaburi ya 83:1-8 unaona mataifa ambayo yalikuwa ni maadui wa Israel kipindi hicho cha zamani wakipanga hila namna ya kutengeneza umoja wa kijeshi wakiwa na lengo moja la kulifuta na kuliangamiza taifa la Israel. Angalia Mstari wa 4 ” wamesema njoni tuwakatilie mbali wasiwe taifa na jina la Israel halitakumbukwa tena” . Ama kweli biblia imethibitika na kuhakikishwa na Mungu mwenyewe. Biblia inachosema ndiyo jambo lilivyo usijaribu kuhisasahisha biblia. Kile kinachozumgumzwa mstari ile wa nne ndio kitu hicho hicho ambacho mataifa ya kiislamu ya kiarabu inakihimiza kwa sasa. Iran inaeleza waziwazi namna itakavyo liangamiza taifa la Israel na imetoa sababu 10 na njia ya kutekeleza kampeni hiyo, mayo ni kupata silaha za nucleur ambapo itaweza kuangusha hilo Bomu katika mji wa tel Aviv Israel na kulifuta taifa la Israel katika ramani ya dunia. Hicho ndicho mtunga zaburi ya 83 wana wa asafu wanachotueleza. Hezbollah na Hama’s pia wako katika huo mpango wa kufanya vita na Israel. Kama vile ilivyokuwa katika ile vita ya mwaka 1967 ambapo mataifa ya kiarabu yaliungana na kufanya vita na Israel kwa lengo LA kulifuta taifa la Israel lakini walishindwa, utawezaje kufuta taifa ambalo Mungu mwenyewe amelipanda. Siku zinakuja ambapo mataifa ya kiarabu yatatengeneza umoja wa kijeshi nao watakuja kama mchanga wa bahari kwa lengo la kuliangamiza taifa la Israel. Lakini watashindwa. Mtunga zaburi ya 83 alikwisha liona hili na katika ule mstari wa 18 zaburi ile ya 83 ameeleza ni nini yatakuwa matokeo ya hiyo vita.

 17. Wandugu,

  Kuvamiwa kwa Israel kutatokea baada ya kanisa kunyakuliwa.

  Kama tujuavyo kuwa Israel walimkataa Kristo na mpaka sasa hawaamini kuwa ndiye Masihi. Wanaamini ni jamaa fulani tu aliyekuwa na uwezo fulani na ujanjaujanja wa kushawishi watu.

  Na hii ni kwa sababu alitokea kwa namna ambayo ilitofautiana kabisa na mitazamo yao.

  Kwa mfano; hawakuwahi kugundua kuwa Yesu alitokea kwenye mji wa Daudi, bali walijua Yesu alitokea Galilaya- Nazareth ambako hapakuwa pamenenwa popote kuwa Masihi angetokea huko.

  Na kiukweli kabisa Yesu hakutokea Galilaya wala Nazareth, bali alitokea Bethlehem ya Daudi kama ambavyo Mafarisayo walikuwa wakidai.

  kwa hiyo Israel wa mwilini bado wanajua kuwa Masihi hajaja. Na huyo ambaye biblia inamwita mpinga Kristo ni mpinga Kristo kwetu, lakini kwa Israel wa mwilini huyo jamaa akitokea watajua ndiye kristo.

  Na kumkubali kwa kutasukumwa na yule aitwae nabii wa uongo (lakini kwetu). Wao wataamini kuwa jamaa ni nabii wa kweli.

  Baadae nabii wa uongo na mpinga Kristo watafanya chukizo la uharibifu na kuwafanya sasa Israel washituke kuwa huyo jamaa siyo Masihi, maana Masihi asingefanya hilo atakalolifanya.

  Kushtuka kwao kutawafanya wamkatae, na hapo ndipo watakapovamiwa na mataifa, maana mpinga Kristo atakuja kwa jina la kutatuo mgogoro wa kiuchumi wa dunia, kwa hiyo Israel kumkataa itakuwa ni kusababisha mgogoro mkubwa zaidi wa kiuchumi, hivyo karibu dunia nzima itakuwa kinyume nao.

  Hapo ndipo watajikuta wako kwenye dhiki kubwa sana pamoja na dunia nzima pia. Maana vita vitakuwa vikali mno.

  Na mateso yatakapozidi ndipo Yesu Kristo (Masihi wa kweli) atakaposhuka kuwaokoa Israel.

  Ngoja nikomee hapa kwanza!

 18. ROHO MTAKATIFU ANASEMA NINI KUHUSU TAIFA LA ISRAELI?

  Ningependa kurudia tena KAULI HII kwa uzito wake.Si kila anayepotosha neno la Mungu ni MBWAMWITU, wengine ni
  wateule wasiojitambua yaani ambao hawana uelewa na jambo
  husika ingawa wanadhani wanalijua sana.Watu wengi hatujui kwa
  undani kuhusu taifa la Israeli kwahiyo ni lazima tukubali Roho
  Mtakatifu atuongoze katika kweli yote kuhusu TAIFA TEULE
  LA ISRAELI.Kinachonifanya nizidi kupata raha kwa ndani ni ile hali
  ya Roho Mtakatifu kumtumia mtu yeyote bila kujalisha yuko upande
  wa Yesu au wa shetani kunene lililo KWELI.Mbwamwitu hulazimishwa
  na Roho Mtakatifu kusema lililo Kweli bila ya kujijua au kudhani
  kwamba wanatekeleza hila fulani!!!

  Mtumishi LWITIKO amewahi kutueleza kwa undani sana kuhusu
  taifa la Israeli na kwa wale ambao walifuatilia hakika walifumbuliwa
  macho na masikio.1 YOHANA 2:20,27 iko wazi sana kuhusu namna
  ambavyo Roho Mtakatifu anatutia katika KWELI YOTE katika mambo
  yote ambayo tunahitaji kuyafahamu.Lakini tunapoanza kuzungumza
  suala la kuongozwa na ROHO MTAKATIFU wengine wanakereka kwa
  ndani na mwaka huu watakereka zaidi .Kama unadhani natania
  hebu tumsikilize Roho wa Kristo anasema nini kuhusu maelezo
  ya watumishi LANI na PANDAELI;

  Mtumishi LANI unapaswa kuangalia na kutafakari maelezo yako
  kwa upya kwa sababu yamepita pembeni mwa ile kweli kuhusu
  swali lililoulizwa na ndugu JOVIANUS.

  Mtumishi PANDAELI hongera kwa kutoa muongozo ambao
  utawaweka wateule katika nafasi ya kuijua kweli kuhusu taifa
  la Israeli na kile kinachoongelewa katika ZABURI YA 83.

  MUHIMU TUKALIJUA HILI
  Taifa la Israeli ni mboni ya jicho la Mungu na lango la uchumi
  na dira ya kiroho kwa mataifa yote duniani( SOMA ISAYA 60 yote).
  Siri zote za muelekeo na hatima ya mataifa ya Israeli zimefichwa
  ndani ya taifa teule la Israeli.KWAHIYO MADA YOYOTE INAYOLIHUSU
  TAIFA LA ISRAELI NI NYETI MNO NA NI MWIBA MCHUNGU SANA
  KWA MBWAMWITU.Tunahitaji kunyenyekea sana ili kujua mengi
  ya muhimu kuhusu taifa teule la Israeli.

  Taifa la Israeli limekuwa na mataifa adui hata kabla ya kutangazwa
  rasmi kuwa taifa katika ramani ya dunia ili kutambuliwa na umoja
  wa mataifa.VITA inayoelezewa katika zaburi ya 83 IPO NA ITAKUWA
  KABLA YA UNYAKUWA.Huko nyuma mataifa kadhaa ya kiarabu
  yakishirikiana na URUSI yaliwahi kuungana kwa nia ya kuifuta Israeli
  katika uso wa dunia na yakashindwa vibaya na ndivyo itakavyokuwa
  katika vita hiyo anayokuja.

 19. Si vibaya mtumishi wa mungu ukatuelewesha kwa mapana kuhusiana na huo mchakato wa Israel kumkili yesu tupate ufahamu
  Niliwahi kusoma katika encyclopedia ya historia na nikiunganisha na mstari huo
  LUKA 19:41
  41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.
  Wanaisrael walikuwa na schema masihi atakaekuja atakuwa ana sifa za Shujaa wa kivita ambaye atawaongoza katika kupambana na mapinduzi dhidi ya dola la Warumi…Hivyo waliona Bwana Yesu hakuwa wa namna hiyo walivyofikili hivyo wakamkataa….hivyo baada ya kifo chake yesu waliibuka masihi wengi hawa baadhi yao John of Giscala, Bar Kokhba ambao uasi wao ukasababisha kubomolewa kwa jerusalem kuchomwa kwa hekalu na baada ya kipindi icho ndipo ardhi ikabadilishwa ikaitwa syria palaestina proviance na hawakuwai kurudi tena mpaka 1947 au 48
  Hivyo nafahamu tu historia nilioandika kwa ufupi kweli nipe maarifa mapya juu ya mchakato huo

 20. Wapendwa wasomaji , yako mambo mawili hapa .when you think of Destiny take it into two perspectives : spritual destiny and physical destiny. maandiko yanapo eleza habari za kuja kwa Yesu kwa mara ya pili ,Inagusa makundi mawili ya watu wataokutwa katika Dunia . Bila kujali umekutwa wapi .watu wenye mioyo safi na wenye mioyo chafu.waisraeli kama wameendelea kudumu katika vita mpaka wakati huo wa kuja kwa Yesu siamini saana kwamba watapata kibali kwa sababu tu Waisraeli miongoni mwao huenda yakawepo makundi hayo kama sehemu nyingine za Dunia . Mie kwa uelewa wangu Kuvamiwa kwa taifa la Israel, kwa sababu kila jambo lina mwisho wake; Taifa la Israel litavamiwa kwa maana ya Israel Dunia na Taifa la Israel kwa maana watakatifu wa Mungu Duniani watavamiwa .Jambo hili linahiji makundi yote kujipanga kwa ajili ya nyakti kama hizo.

 21. Lani, Huna mawanda mapana Kuhusu Taifa la Israel .Pia Unachanganya Habari za Israel kama Taifa na Habari za Wakristo wa Mataifa mengine. Padre Ribera (japo hata simjui) anahusika vipi na kuvamiwa kwa taifa Israel?Israeli Kuvamiwa Si habari za Siasa bali ni habari za Kiroho.Nilikuandikia kuwa Ungekuwa unaujua Mchakato mzima wa Israel kuja Kumkiri YESU kuwa ni MASIHI ungejibu hilo swali vizuri.Umezungumzia SANA habari za Israeli baada ya kumkataa Masihi mbona huoneshi jinsi watakavyokuja kumkubali kuwa ni Masihi wao? Hebu soma tena hilo Swali kwa makini ili uweze kung’amua jambo? AMANI IKAE NA ISRAEL

 22. LUKA 19:41
  “ALIPOFIKA KARIBU ALIUONA MJI AKAULILIA, AKISEMA, LAITI UNGALIJUA, HATA WEWE KATIKA SIKU HII, YAPASAYO AMANI! LAKINI SASA YAMEFICHWA MACHONI PAKO.”

  YESU ATASHUKA NA YERUSALEMU MPYA KWA KUWA ILE YERUSALEMU YA KWANZA ILI MKATAA MWENYE MJI.

  YERUSALEMU=MAANA YAKE MJI WA AMANI
  YESU NI MFALME WA AMANI.

  WAEBRANIA 6:20
  “ALIMOINGIA YESU KWA AJILI YETU, MTANGULIZI WETU, AMEKUWA KUHANI MKUU HATA MILELE KWA MFANO WA MELKISEDEKI.”

  WABRANIA 7:1
  “KWA MAANA MELKISEDEKI HUYO MFALME WA SALEMU, KUHANI ALIYE JUU,..”

  YESU ATASHUKA NA YERUSALEMU MPYA.

  ANAETEGEMEA AMANI JUU YA ISRAELI YA KIMWILI..KWA SASA HAKUJUA YAPASAYO AMANI YA YERUSALEMU.

  VITA JUU YA YERUSALEM NA ISRAELI NI ENDELEVU MPAKA
  MFALME WA AMANI, ATAKAPOSHUSHA MJI MPYA AMBAO WOTE/WATAKATIFU WATAKAOKUWA NDANI YAKE WANAMKUBALI.

  HUU WA SASA TUSIUTAZAME TUKALETA USHABIKI WA NIDHAMU YA UOGA.

  WAEBRANIA 13:12
  “KWA AJILI HII YESU NAYE, ILI AWATAKASE WATU KWA DAMU YAKE MWENYEWE, ALITESWA NJE YA LANGO.BASI NA TUTOKE TUMWENDEE NJE YA KAMBI, TUKICHUKUA SHUTUMU LAKE. MAANA HAPA HATUNA MJI UDUMUO, BALI TWAUTAFUTA ULE UJAO”

  TUNAPOFIKILIA AMANI YA ISRAELI TUKUMBUKE PIA;

  LUKA 19:41
  “ALIPOFIKA KARIBU ALIUONA MJI AKAULILIA, AKISEMA, LAITI UNGALIJUA, HATA WEWE KATIKA SIKU HII, YAPASAYO AMANI! LAKINI SASA YAMEFICHWA MACHONI PAKO.”

  TUACHE USHABIKI WA SIASA ZA MASHARIKI, TUCHUNGULIE MAANDIKO YANATUAMBIAJE.

 23. WARUMI 9:6
  ” SI KANA KWAMBA NENO LA MUNGU LIMETANGUKA. MAANA HAWAWI WOTE WAISRAELI WALIO WA UZAO WA ISRAELI.

  YESU ANAPOZUNGUMZIA DHIKI KUU ANAZUNGUMZIA DHIKI KWA WAKRISTO WALE WATAKAOKUWA HAI SIKU ZA DHIKI KUU.

  TUTAMBUE BAADA YA KUFUFULIWA NA KUPAA MBINGUNI NI UFUFUO WA PILI NDIO UTAKUWA UNASUBIRIWA. WENGINE WAKIWA WAFU NA SHETANI AKIWA AMEFUNGWA MIAKA ELFU MOJA. HIVYO TUTAMBUE KUWA BAADA YA KUPAA MBINGUNI NA YESU HAKUNA HABARI YA ISRAELI KUVAMIWA HUKO NYUMA.

  UFUNUO 20:2
  “AKAMSHIKA YULE JOKA, YULE NYOKA WA ZAMANI, AMBAYE NI IBILISI NA SHETANI, AKAMFUNGA MIAKA ELFU;”

  UFUNUO 20:5,6
  “HAO WAFU WALIOSALIA HAWAKUWA HAI HATA ITIMIE ILE MIAKA ELFU.HUO NDIO UFUFUO WA KWANZA, HERI NA MTAKATIFU, NI YEYE ALIYE KATIKA UFUFUO WA KWANZA.”

  NDUGU JOVIANUS: HIVYO HAKUNA ISRAELI WA MUNGU/MKRISTO ALIYEKUBALIKA ATAKAYEBAKI DUNIANI BAADA YA UFUFUO WA KWANZA.

  HIVYO WALE WANAOTUMIA THEORY ZA PADRE JESUIT, RIBERA HAWANA JAMBO LA KUTHIBITISHA MADA YAO KATIKA MAANDIKO KUWA WATU WENGINE WATABAKIA KWA AJILI YA MATESO MAALUMU IKIWA PAMOJA NA ISRAELI KUVAMIWA BAADA YA WATU KUPAA.

  MATHAYO 24:21
  “KWA KUWA WAKATI HUO KUTAKUWAPO DHIKI KUBWA, AMBAYO HAIJATOKEA NAMNA YAKE TANGU MWANZO WA ULIMWENGU HATA SASA. WALA HAITAKUWAPO KAMWE. NA KAMA SIKU HIZO ZISINGALIFUPIZWA, ASINGEOKOKA MTU YEYOTE; LAKINI KWA JILI YA WATEULE ZITAFUPIZWA SIKU HIZO.”

 24. LANI, Maelezo yako yanajikanganya mno!Kwa kweli hujajibu hilo Swali kama lilivyoulizwa.Unaujua Mchakato mzima (the whole process) Wa WAISRAELI kumkubali Y ESU kama MASIHI wao?Nafikiri ungeujua huo MCHAKATO ungeweza kujibu hilo swali vizuri.Hiyo CHAPA Uliyozungumzia ni ipi?Je,Unaamini Mungu Ahadi yake na ISRAELI (taifa) ni ya Milele?Je,unajua kuwa Mungu alisema ATAKAYELAANI Israeli (taifa) AMELAANIWA?Pia kauli yako ya Kusema AGENDA ya Taifa la ISRAEL Kuvamiwa imetungwa ka WELEDI na KUWASHAWISHI Wakristo Kuhusu Vita vya Mashariki ya Kati SI SAHIHI.Taifa la Israel kuvamiwa IMEANDIKWA katika NENO LA MUNGU wala si Kauli ya kutunga. AMANI IKAE NA ISRAEL.

 25. Jesus is coming soon.
  “kisha nikajikuta kwenye uwanja wa stadium katikati, nikiwa najibishana na mtu, akiniuliza , wewe mama unatuambia na kukiri kuwa Jesus Christ is coming?
  nikajibu mbele ya umati uliojaa uwanjani kuwa YES. -nikaongeza sema soon ili ukamilishe hiyo sentensi.
  Akaniambia tuanze mapambano tuone kama ni kweli au la. nikapewa mchuano wa mchezo unaoitwa dats wa kurusha mishale kulenga targets. sijawahi ucheza, lakini nilipewa vile vimishale mkono tele, nikavirusha vyote kimoja kimoja, na vyote vikalenga ndio( Yes). watu wote umati ukashangilia sana.
  sijui wewe unasema nini? kubali au ukatae ukweli uko palepale, kuwa Jesus is coming soon.

 26. PILI: TUSIDANGANYIKE NA AGENDA YA ISRAELI YA KIMWILI YA SASA, TUNA TAIFA JIPYA LA ISRAELI AMBALO LIMEPEWA UFALME, LINAWAHUSISHA WAISRAELI WALE WA KIMWILI WANAOMKUBALI YESU NA WATU WA MATAIFA WANAOMKUBALI YESU HAWA NDIO ISRAELI WA KIROHO, HILI NDIO TAIFA JIPYA LA ISRAELI.

  YESU ALISEMA HIVI:

  MATHAYO 21:43

  “KWA SABABU HIYO NAWAAMBIA, UFALME WA MUNGU UTAONDOLEWA KWENU, NAO WATAPEWA TAIFA LINGINE LENYE KUZAA MATUNDA YAKE.”…….45. WAKUU WA MAKUHANI NA MAFARISAYO, WALIPOSIKIA MIFANO YAKE, WALITAMBUA YA KUWA ANAWANENEA WAO.”

  WATU WANAOITWA RAPTURIST WANAWAFUNDISHA WATU
  1. KUWA WATAKATIFU WATAKUWA MBINGUNI WAKATI WA AMAGEDON
  2.KUNA MUDA WA ZIADA BAADA YA WATAKATIFU KUPAA MBINGUNI KUTAKUWA NA VITA YA KIMWILI NA KUTIWA CHAPA
  3.TAIFA LA ISRAELI YA KIMWILI KUVAMIWA.

  HAYA YOTE YANA AGENDA ILIYOTUNGWA KWA WELEDI, NA KUWASHAWISHI WAKRISTO WA SASA KUSHABIKIA VITA YA MASHARIKI YA KATI, KUWAPOTEZA KATIKA RAMANI HALISI YA VITA HALISI, WAKIJIKANA UTAIFA WAO NA KUWARUDISHIA WAISRAELI WA KIMWILI.

  TUKUMBUKE HAPA:
  MATHAYO 21:43

  “KWA SABABU HIYO NAWAAMBIA, UFALME WA MUNGU UTAONDOLEWA KWENU, NAO WATAPEWA TAIFA LINGINE LENYE KUZAA MATUNDA YAKE.”…….45. WAKUU WA MAKUHANI NA MAFARISAYO, WALIPOSIKIA MIFANO YAKE, WALITAMBUA YA KUWA ANAWANENEA WAO.”

 27. MOJA: TUTAMBUE KUWA YESU AKIJA MARA YA PILI HATAKANYAGA CHINI, TUTAMLAKI MAWINGUNI.

  MARKO 13:27
  “NDIPO ATAKAPOWATUMA MALAIKA NA KUWAKUSANYA WATEULE WAKE TOKA PEPO NNE, TOKA UPANDE WA MWISHO WA NCHI HATA UPANDE WA MWISHO WA MBINGU.”

  1 WATHESALONIKE 4:16,17
  “KWA SABABU BWANA MWENYEWE ATASHUKA KUTOKA MBINGUNI, PAMOJA NA MWALIKO, NA SAUTI YA MALAIKA MKUU, NA PARAPANDA YA MUNGU; NAO WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA, KISHA SI TULIO HAI, TULIOSALIA, TUTANYAKULIWA PAMOJA NAO KATIKA MAWINGU , ILI TUMLAKI BWANA HEWANI; NA HIVYO TUTAKUWA PAMOJA NA BWANA MILELE.”

  WALA TUSIDANGANYIKE NA AGENDA YA UNYAKUO WA SIRI,

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s