Masuala ya mahusiano sipati picha kamili!

Bwana Yesu asifiwe wapendwa.

Mimi ni mgeni kwenye blog hii ila naamini nimekutana nayo kwa makusudi muhimu.. kwenye pita pita nimekutana na maoni na shauri nyingi kutoka sehemu mbali mbali hivyo na mimi ningependa msaada toka kwenu..

Nina jambo ambalo kiufupi linanitatiza na bado sina majibu yake hivyo kwa michango yenu tofauti labda mwaweza nisaidia, kipindi cha nyuma naweza sema nilisumbuka sana katika maswala ya mahusiano yaani kila kijana alie nifuata alikua muisilamu au mkristo jina maana hata mlango wa kanisa haujui.

Nilimlilia Mungu juu ya hili akawa mwaminifu na kuniletea mtu.. kuna kaka nilimwona mara moja nikiwa na rafiki zangu kiukweli moyo ukagongana nae sikujua ni nani wala anaishu gani.. ikapita miezi miwili nakumbuka ndio siku nimetoka lia sana na Mungu kunipa kijana kwa imani, next day nakuta missed call hamuwezi amini sijui how ila ndani yangu nilihisi ni yule kijana nilomwona miezi miwili iliyopita.. basi akaomba tuonane nae akaonesha interest kwangu kiukweli tulikua na chemistry sijui niwaelezeje kama nilimjua maisha yangu yote.

Kabla sijajikita kwenye urafiki nilimwomba kwanza Mungu aniambie kama ni yeye au sie yeye.. katika ishara nilizo omba ZOTE zilitimia kama nilivyo omba Mungu.. Si mtu wa kanisani sana ila ana hofu ya Mungu na wazazi wake ni watumishi wa dhehebu fulani.. alionesha dalili zote za mtu anaetaka kuoa.. ila ni kama alikua anapatwa na wasiwasi leo anataka kesho ni mtu mwingine kabisa na baadae kesi za kujamiiana zikawa nyingi japokuwa alikua muelewa ukisha mtajia dhambi anatulia hasumbui… lakini nikachoka nikamwambia tuachane.

Ajabu wiki kabla sijamwacha niliota ndoto ya kwao wakiniambia niachane na mtoto wao kwani hawanitaki na mimi nikapatwa na kitu ghafla nikamwambia tuachane bila kujielewa na wala sikuomba juu ya ile ndoto..

Basi nikawa naumwa sana.. siku nikiomba na kikundi kanisani kuwa kama ni yeye tunampa siku kadhaa awasiliane na mimi kweli kabla ya zile siku kwisha akanitafuta kuwa ananijulia hali… nikiacha kuomba anapotea hanitafuti siku nyingine tena nikamwomba Mungu na kuna dada wa kanisani alidai ameona maono kua ni mume wangu ila anahitaji kuombewa sana maana kwao wana nguvu za giza.

Siku nyingine ndoto ikaja nasafisha nyumbani kwao na kupaweka safi, ndoto nyingine kua amekuja kanisani kujitambulisha.. basi kuachana kwetu kukawa miezi kadhaa anapotea baadae anaibuka hili ni jambo linalonisumbua sana. Na alisha jitambulisha kwa wazazi  wangu japo kwao hakunitambulisha.

Kila tulicho omba juu yake kinatookea ila yeye moyo wake bado mgumu, nakumbuka mwezi uliopita nilimtafuta na kumwambia achague either awe nami au aache kunichosha mara anaibuka mara anapotea.. akasema yeye mwenyewe anapitia wakati mgumu na haelewi kwanini maana anajaribu kweli kweli kutonitafuta au kuwasiliana ila anajikuta kuna kitu kina msukuma na haelewi kwanini na ana feel kama tutarudiana… nikamwambia uamuzi ni kwake mimi sitaki kupoteza nguvu akajibu si vyema tuwasiliane kwa simu vyema tuonane kuliongelea ila ajabu hadi leo hii kakaa kimyaa..

Sasa mimi naelewaje juu ya hili wana wa Mungu hili swala la mwenza limekua mzigo kwangu na la kuusumbua moyo wangu..mengi sijayasema ila kiufupi ni hayo.. ishara nilipewa ndoto zimeonwa na mimi mwenyewe nimeota pia japo sio ndio ndie au ndie sie ila yale nilomwomba Mungu afungue kwa wakati huo Alijibu ila kwa sasa naona amechoshwa na mimi maana kakaa kimyaaaa juu ya ombi hili yaani kila niombapo Mungu yuko kimyaaa.. japo kuna mama wa maombi kanisani anadai yeye bado ana msukumo wakuombea yule kijana na bado anaona uso wake mara kwa mara..

Kuna siku nilifanyiwa delivarance mtu tena wa kwao alidai tumuache na hawanitaki maana nimempeleka kwa Yesu..naombeni ushauri.. mnapata nini juu ya hili.. maana me nahisi niko too emotional hata kusikia Mungu atapo sema na mimi juu ya hili..

–YJ

————————-

Bwana Yesu asifiwe wana SG, tumejaribu ku edit baadhi ya maneno na kupangilia naamini itasomeka vyema, karibu yule mwenye msaada kiroho anaweza kumpa ushauri japo nasi tunawasiliana naye kwa mwongozo zaidi. Mbarikiwe

–SG

Advertisements

29 thoughts on “Masuala ya mahusiano sipati picha kamili!

 1. kwa Mungu hakuna lisilowezekana dada usikate tamaa uwe tu mvulilivu na kudumu katika maombi

 2. Hekima,Naona umelewa kwa mvinyo wa Uasherati wa Mafundisho ya Munuo.Aliyekuambia kuandika neno SILOAM kwa herufi kubwa inamaanisha namheshimu huyo MPINGA KRISTO WENU (MUNUO) na nakubaliana na huo uasi wenu ni nani?SILOAM ni jina la nani?Sikulaumu kwa sababu najua kuwa WAUMINI WOTE WA MUNUO WA MUNUO MMEPAGAWA MAPEPO.Mungu airehemu nafsi yako yenye dhambi.

 3. namshukuru Mungu kwa kuwa Neno SILOAM umeliandika kwa herufi kubwa kuonesha jinsi unavyomuheshimu Eliya Ad2 Mungu wa majeshi, aliyetumwa (yoh 9:7). at pendael.kwa kuwa hata kitabu cha Neno kimesisitiza jina lake liandikwe kwa herufi kubwa. Si mimi bali ni wewe mwenyewe ukiongozwa na Roho ya Eliya umeweza kuandika hayo Mungu wa Eliya lazima akuinue kwa kazi hii nzuri, kwani hata mimi mwenyewe nilitakiwa kuandika kwa herufi kubwa lakini sijafanya hivyo Mungu wa Eliya anisamehe, ubarikiwe mfuasi.

 4. ye hata kwa ndoto alikuwa mumeo na anazuia mume mwingine asije zinaa zingine ulifanya hata kabla hujamjua Mungu ukiwa mtoto ule ni uovu wa baba zako uliopatilizwa nao lazima ukutane na aliyetumwa ili kutoka kwenye vifungo vyote hivyo la sivyo utaomba ushauri kila eneo nakujikuta uko uchi wakati Mungu katanda pindo la vazi lake ili kukusitiri na aibu(ezekiel 16:8), kuna ndoa za dini na madhehebu ambazo hakuna msingi wa Neno, unakuta mchungaji, askofu au cheo chochote atakachojiita anasema ‘M’ umekubali kumuoa ‘J’ na kuishi naye katika shida na raha, uzima na maradhi, hata kifo kiwatenganishe na wanaofungishwa wanasema ndio, kwa kuwa (mithali 6:2) iko wazi hivyo baba zetu waliokiri ujinga huo wakati Mungu hajawahi kutamka hivyo mahali popote waliturithisha matatizo na laana badala ya baraka. Mungu tangu mwanzo hakuwahi kutamka hayo mfano mwanz 1:28, mwanz 9:1-17, mwanz 17:1-8, mwanz 24:60, kumb 28:1-14,ezekil 16:62-63, ebran 8:10-12, kwa hiyo ili utoke hapo lazima utolewe kutoka kwa asiyetumwa. SHIKA NENO……

 5. vile vile wengi hatujajua kuwa kuna tofauti kati ya ndoa na agano. Ndoa ni makubalia kate watu wawili mke na mme na shahidi si Mungu ndani ya ndoa bali ni watu(ebrania 13:4) na agano ni mapatano kati yako wewe/mwenza wako na Mungu ndie shahidi wa agano (malaki 2:14-16) mfano wa ndoa kuna ndoa za mizimu, ulipokuwa mdogo babu yako alikuwa anasema wewe ni mke wake na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa kuwa mlipatan hata wewe hukukataa hata kama hukukubali lakini kwa sababu hukutoka kwenye mila za kwenu tangu ulipozaliwa (ezekiel 16:1-5), kuna ndoa za mkeka, ndoa za bomani ambazo hizi ni sheria za dunia na dini zinazohalalisha watu waendi wakazini (kumbu 22:28-29), kuna ndoa za majini na mapepo kwa wale waota ndoto na tulidanganywa shuleni kuwa ukiota uko na m/ke au m/me halafu ukaamka amejichafua ujue umkuwa lakini si kweli zile zilikuwa ni ndoa zilizofunga maisha yetu kwa siri, ndoa za kimila ambazo huambatana na laana(kumb 25:9-10), ndoa za mke na waume wengi au mume wake wengi (1kori 6:16) yeyote uliyewahi kuzini na

 6. Hekima,Naona umetangaza Sera za Nabii wenu wa Uongo (MUNUO).Unawakaribisha watu SILOAM kwa Munuo aliyejiita ‘bwana wa majeshi,adam wa pili halafu 2008 alimuua Shetani?’.Kama ni SILOAM ya Munuo ni Shimo la kwenda kuzimu na unamwalika huyu dada ili mkamvike ‘roho ya Upinga Kristo’ maana ndiyo inayopatikana SILOAM kwa Munuo.Hekima yako si ya Kiungu.

 7. wengi hawajatoka kwenye misingi hiyo mibaya ndio maana wanakutana na wanyama wakali kwa kuwa njia wanayopitia siyo ya utakatifu (isay 35:8-10) hata ungekuwa na haki kupita yesu lakini kama ndani yako kuna misingi mibaya haki yako hakusaidii (zab 11:3),(ezekil 33:12-13) haki yako unapata kwa kuvunja misingi ndani yako na mwenzako. Karibu siloam ubomoe misingi mibaya

 8. Mungu anasema kwenye mwanzo 2:24 uweze kupata mwenza lazima utoke kwa baba, na mwanzo 12:1-3 inafafanua zaidi ya kwamba ili ubarikiwe baada ya kutoka kwa baba na jamaa zako na kwenye nchi yako lazima uende kwenye nchi ya Mungu. Maana yake wewe na huyo mwenzako lazima mtoke kwenye tabia za ubinti, uvulana, mila, desturi, kabila, utaifa, elimu ya dunia, tabia za asili, matendo ya mwili(gal 5:19-21), halafu mpate tabia ya Mungu ndipo hayo unayoomba yatokee. Bila kusahau (2nyak 15:3-8) bila kuhani wa kweli (yoh 9:7), Neno la kweli, Mungu wa kweli, madhabahu ya kweli (kumb 12:1-6), chochote unachoomba hakitatokea, hata kama wanaokuombea na kukushauri ni wazoefu na unawaamini lakini Mungu haangalii uzefu akitaka kumuua goliti anayekusumbua(1sam 17:32-37)

 9. Pole dada Yolanda kwa yaliyokupata, usikate tamaa kwa maana hakuna jambo linalomchukiza Mungu wetu kama hilo, na ndo maana anasema kila amwendeae lazima aamini yupo tena huwapa thawabu wamtafutao. maombi yako si bure ktk Bwana, ila nikushauri hivi, omba ktk tafakari ya yale yote ambayo ulikwisha omba na Mungu akakupa ili uongeze imani yako then mweleze Mungu kuwa unaamini hata hilo ni jambo dogo sana kwake. focus pia kwenye mambo mengine ambayo Mungu amekupa mfn kazi na huduma, relax, usifungwe na wakati, kumbuka kibiblia jinsi Mungu hakufungwa na wakati kumpa mtoto Sara na mwanamke mshunemu. Amini majibu yako yanakuja tena mazuri, kiri hivyo kila wakati, usikubali shetani akukirishe tofauti, naamin baada ya Muda Mungu atakujib na kuzidi, tena atakupeleka ktk ndoa na familia uitakayo

 10. Bwana Yesu asifiwe dada Yolanda asante kwa taalifa mimi nilikuwa nadhania huenda umeingia kwenye ndoa kinyume na mapenzi ya Mungu sasa uko kwenye jalibu ndio unashilikisha kuomba ili Mungu ahusike
  pia napenda kuwashauri dada zangu wengine ambao wakishawishiwa ama kuchumbiwa kinyume na mapenzi ya Mungu huwa hawataki kushauliwa kwa lolote mimi nimeshuduia dada moja tulikuwa tunasali naye akachumbiwa na mtu wa imani tofauti naye akijifaliji atamwombea Mungu atambadilisha kinyume chake yule dada yuko kwenye jalibu mpaka anakalibia kukakata tamaa
  ukingia kwa makusudi huku unajua kuwa ni vibaya ukajifaliji kuwa Mungu atamwokoa ukakubali kufungwa na mtu asiye amini hutapata mlango wa kutokea
  Dada zangu msijidhanie kuwa mmechelewa kwani Mungu anasema si vema uwe peke yako yuko mwenzi ambaye Mungu amekuandalia kwa Mungu hakuna kuchelewa wala kuwahi
  balikiwa nyote Amina

 11. Bwana @Stephen asante kwa ushauri ila AM SORRY TO SAY sijaolewa na wala sina mchumba.. hio nisimulizi ya yalionikuta kwa kijana ambe baada ya kuomba ndipo alikuja katika maisha yangu.. but nashukuru Mungu sijaingia kwa agano la ndoa kama udhanivyo kwaani ninge lipa gharama mara 2.. ila asante

 12. mimi nichangie kwa kusema vijana wengi hawataki kushauliwa wala kuskia na biblia inasema mtu akijifanya anajua neno hajui kiti (1wakolinto 8:-2) sasa wewe Dada mimi nataka ni kwambie kweli watu hawataki kukuambia kweli wanakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa hata hayo maombi unayo omba Mungu hayasikii kwani Mungu huwa hasikii wenye dhambi sasa wewe umeingia kwenye Ndo bila kufuta mpango wa MUNGU halafu shida imeanza mafarakano yako katikati yenu ndio uanze kuomba Mungu hawezi kusikia huko ni kupoteza mda wako kwanza anza kuomba rehema kwa kosa ulilo fanya kuingia kwenye Ndoa bila kufuta Mpango wake.
  Mpango wa Mungu ni huu Biblia iasema katika (2wakolinto 6:-14) kwamba usifungiwe nira na watu wasio amini kwa njinsi isivyo sawasawa sasa wewe unalazimisha ukaingia kwa tamaa zako za mwili
  mabinti wengi wanaacha mpango wa Mungu kwa sababu ya tamaa zao kwa mfano kama wewe ni mpendekosite chumbiwa na mpendekosinte mwenzako lakini usifungiwe nira na mtu ambaye hamko imani moja kwa kufikiri utambadilisha huko ni kupoteza mda wako chumbiwa na mtu wa imani moja kama ni mkristo anayeamini pata mkristo mwingine anayeamini
  sasa kwa kifupi maombi ya wenye dhambi Mungu huwa haskii soma Yohana 9:-31,isaya 59:-1..3,isaya 1:-15) dada kwanza omba rehema kwa Mungu kwa kosa ulilo fanya kuingia kwenye ndoa bila kufuta mpango wa Mungu mpango wa Mungu kwanza uchumbiwe bado ukiwa nyumbani makubaliano ya pande mbili yafanyike kwa maana ya kukubaliana
  Moja kijana wa kiume na kijana wa kike wakubaliane kisha wazazi wote wa pande zote hapo ndipo zinafuata baraka za ndoa makanisani hivyo ndio mtoto wa ibrahimu alifuta soma mwanzo sura ya 24 yote
  kwa leo niishie hapo balikiwa nyote amina

 13. BWANA Yesu asifiwe.
  mwanzilishi wa Ndoa ni Mungu. tuendelee kuomba Mungu atatuonesha mahali kokote tulipokwama ambako panazuia ndoa kufanyika. Mungu ni mwaminifu sana. me nilianza kuomba masuala ya ndoa Mungu akasema na mmi kuhusu maagano yaliyofanywa kwenye familia yangu amabayo yalikuwa yanampa shetani uhalali wa kuvuruga aliyokusudia Mungu. asante kwa damu ya Yesu amabayo ni agano la milele linalofuta maagano yote yaliyotangulia.

  Ushauri
  1: Endelea kuomba na kuongea na Mungu. pia Omba kutakaswa nafsi yako na kujitenga na family ties na chochote Roho atakachokuongoza
  2: Yaani endelea kumtumikia Mungu….the battle is not yours. kama kuna kitu kinamsumbua shetani ni pale unapomtumikia Mungu kwa uaminifu wakati uko kwenye majaribu makubwa.
  3: ni Roho Mtakatifu atakayewakutanisha. Isaya 34:14

  Isaya 34:16
  16 Look in the scroll of the Lord and read:
  None of these will be missing,
  not one will lack her mate.
  For it is his mouth that has given the order,
  and his Spirit will gather them together.

  Endelea kumtumikia Mungu na Neno la Mungu litatimia tuu Isaya 55:9-11

  Annie

 14. Mmh jamani,

  Mbona kuna vitu vya ajabu vinaendelea kwa watu juu ya suala la kuoa na kuolewa!!

  Yolanda unasali wapi?
  Na T.H pia, unasali wapi?

  Things are not that complivated aise. Mlishawahi kusoma lwenye biblia mtu mmoja aliwahi kupata mke/ mume kwa maombi tofauti na ishu ya Isaka?

  Hofu na vitisho ambavyo vimejengeka kuhusu ndoa kutokana na masimulizi ya walio katika ndoa zilizoshindwa kumefanya kuoa kuonekane ni dude lililo tata ile mbaya, kitu ambacho siyo kweli.

  Msingi wa kupata mwenzi siyo maombi, mafunuo, maono, ndoto, wala ishara.

  Kuna msingi ambao tumeupuuza tukidhani ni wa kimwili sana, lakini kumbe ndo msingi ambao watu wa biblia waliutumia.

  Chunguzeni, Ibrahim alomuoa nani kimahusiano, Isaka alimuoa nani kimahusiano, Yakobo alimuoa nani kimahusiano, hata Yusuf baba wa kambo wa Yesu alimuoa nani kimahusiano.

  Angalieni pia mchakato wa Ruth kuolewa na Obed ulikuwaje kimahusiano.

  Kwa nini tunataka kupata wenzi kwa mafunuo na maono kana kwamba kwamba maisha ya ndoa tunaenda kuyaishi kiroho, wakati haya bibloa ometutaka wanaume tukae na wake zetu KWA AKILI, wala haojasema tukae nao kwa kuongozwa na Roho mt?

  Misingi ikiharibika, matokeo yake ndio haya sasa.

  Yusuf hakusubiri kufunuliwa alipotaka kumwacha Mariam,ila ilimbidi kufunuliwa katika kulijibu swali la kwa nini asimwache. Na mimi naamini hata Yusuf kumpata Mariam haikuwa kwa maombi wala maono.

  Ninyi dada zangu, msipoteze muda kuomba waume, kuweni busy kumtumikia Mungu na kufanya shuguli zenu. Kisha jishugulisheni kujifunza jinsi ya kukaa na mume na kutunza familia. Mungu hajawahi kuwapa homework ya kuomba wenzi wa maisha, mnafanya kazi isiyo yenu.

  Nitakuja tena!

 15. Dada yangu kwa kifupi ni kwamba hapo hapo alipokwama yeye na wewe umekwama. Ni wote mmekwama sehemu moja. Na pia ni shida wewe kujinasua na umekwama kwasababu yake. Sio kwamba you are too emotional japo hiyo inaweza kuwa ni sababu kwasababu wasichana wengi mnapokuwa katika mahusiano mnakuwa emotional sana. Angalia namna unavyotakiwa kutoka hapo. Rudi tena mbele za Mungu umuulize tatizo ni nini?

 16. SHALOM,
  POLE SANA WOTE MNAOPITIA CHANGAMOTO ZA MAHUSIANO. TUNAWAOMBEA MUNGU AWAFUNGULIE MLANGO.TUNASHAURI PIA MTAFUTE KITABU KIPYA (KIMETOKA MWAKA JANA) CHA ” MWENZI WA MAISHA” (THE LIFEMATE).

  KITABU HIKI KINA MAJIBU MENGI YA MASWALI YALIULIZWA KATIKA MJADALA HUU. KIPO EFATHA BOOKSHOP (DAR), VICTORIA BOOKSHOP (MWANZA), KIMAHAMA BOOKSHOP (ARUSHA NA TABORA) AU PIGA 0767 681078

  MUNGU AWABARIKI SANA!!!!!

 17. asante servant..

  na T.H pole sana mama… ila Mungu wetu sio mdhalimu na wala hasemi uongo.. nacho amini kama shauki iko ndani mwetu kama vijana ya kuoa/kuolewa basi wakati umefika wa kufanya hivyo maana jiulize kwanini hukua nashauku hii 5yrs back.. hivyo basi tunacho takiwa kufanya nikuomba kwa bidii bila kukata tamaa kama mtumishi elia na wengineo wengu…

 18. dada umefunguka sasa walau tunazidi pata nafasi ya kukushauri
  1)Nadhiri ya mama ya kutaka kuolewa na mzungu
  2)Ndugu wa karibu na jamaa zako kuzaa nje ya ndoa
  Niamini nachokuambia na kitakusaidia sasa hivi mpendwa wewe unakuwa kama unatafuta kuotesha Mti juu ya mti ambao una mizizi mikubwa sana (Family tree)
  Nakushauri tafuta masomo haya usiyapuuzie
  1)Uponyaji wa mti wa familia by John Paul katika bookshops ingawa kilikuwa adimu kipindi fulani sijajua kwa sasa
  2)Maombi ya Mzaliwa wa kwanza kama LANGO by Christopher Mwakasege
  3)mBINU ZA KUMUOMBEA mzaliwa wa kwanza kama Lango by Christopher Mwakasege
  ….wengi sana wanaona ni kama nadharia tu kufuatilia misingi ya wahenga wao wapi walipoanzia kutokana kuwa swala linaonekana la kiimani….lakini mungu ameachilia neema kusoma shahada saikolojia ambapo wapo wahasisi wengi wanamkataa mungu lakini wanakubaliana na swala ya family tree…..inafikia wengi sana wanakata tamaa hata kumn’gunikia lakini naamini vitakupa hatua vitabu hivyo

 19. Pole sana Yolanda, napata maumivu ya unachopitia mana hakina tofauti sana na nilichopitia kuna vitu viwili vyafanana kabisa mamangu aliombaga sana baby girl for 7 years na alifanikiwa kunipata mimi pia kuna kaka alionesha nia ya kua nami ila kila nikiomba sikupata majibu ya kua ndo mume wangu.Alikua na imani na hofu ya Mungu mno lakini sikuwahpata maono kua ndo mume nikabadili maombi kumuombea apate mwenzi kwakua mimi siye nikaoneshwa kwenye ndoto mdada ambaye alikua anamuaproachi lakini hakua bint mwenye nyendo nzuri nikamwambia nilichoota akasema ni kweli kuna binti ameona amfuatilie. wkt anarudi kwao akiwa anasubiri Pantoni huyo dada nae alikua humohumo sa kuna wamama wakaanza kumzungumzia tabia zake walikaa karibu na yule kaka. Alipofika nyumani akaniambia amepata tabia za huyo dada na hawezi kuendelea kumfuatlia ni kweli hafai. Akasafirigi lakini kabla ya safari alinunua kiwanja na gari kama ni vitu vya kunishawishi ili akirudi anipatie ili nikikubali tufunge ndoa fasta akiwa huko safarini mkoani alifariki ghafla na suti alizoandaa kwa harusi ndo aliyovishwa maiti. Cha tatu tunachofanana ni kuomba wenzi kabla hatujafanya uamuzi. NINACHOAMINI KUNA TATIZO KATIKA WAKAKA WA SASA SIO WOTE MANA UKIFUATILIA WENGI WANAPENDA MAHUSIANO NA WADADA WA KIDUNIA NA MATOKEO YAKE WANAANGUKIA PABAYA WANAPORUDI KWA TULIOSIMAMA WANAKUTA HAWANA NAFASI TENA. TUNAWEZA KUJILAUMU KUA SISI NDO TUNAKOSEA KUMBE NI WAO NA TAMAA ZAO ZA KIDUNIA. tuombeane nduguyangu. NAWAOMBA SANA MLIOFIKIA NDOA MTUPE CHANGAMOTO MLIZOPITIA WAKATI WA KUSAKA HAO WENZI NA JINSI MLIVYOWEZA KUPITA. MBARIKIWE SANA NA BWANA MUNGU WA MBINGUNI.

 20. Pole sana Dada yangu,ni wengi wanaopitia wakati mgumu kama wako.Hata hivyo,Mungu yu karibu kuwasaidia.Nashauri utafute kitabu cha ‘Mwenzi was maisha’ utapata majibu ya kutosha.DSM kipo pale efatha Bookshop.Barikiwa!

 21. christowelu.. ubarikiwe na Mungu mtumishi wa Bwana.. KUJIBU MASWALI YAKO:

  1. nina amini asilimia100% Yesu pekee ndie anaweza kunitoa kwanye shida yoyote na ndio maana nina mkimbilia yeye katika hila licha ya kuonekana mjinga kwa nifanyayo sababu yake.

  2.ninacho taka kwa Mungu ni amani ya moyo na kuto mkosea sababu ya jambo liwalo lolote lile. na kwa sasa sina amani maana ibirisi amekua wakushuhudia sana akili yangu mpaka kupelekea kuhisi fahamu zina ruka.. so nina taka niwe na amani awe yeye asiwe yeye.

  3.hapo ndipo nina changanyikiwa maana i was so sure ndiye aliye toka kwa Mungu. juu alikuja pale nilipo omba kwa kumaanisha na kushirikisha hata watu wa Mungu juu yetu.. ila vita ilipo anza ndipo na akili ika vurugika nikawa siamini mara na amini.. ila mwanzo niliamini 100%

  4.niliomba mume na babo naombea mume.

  5.niliomba tokana na vigezo vyangu na niliandika na barua kwa Mungu ya ninae mtaka na kwakumalizia na LET HIS WILL BE DONE.. maana naweza taka mkate kumbe yeye anataka kunipa cake.

  6. nilisha muuliza na sababu ninaijua.. nilisha wahi kaa na mama na anasemakatika watoto mm alisikia sauti ya Mungu kabisa ikimwambia mimi atapata mtoto wa kike maana aliomba sana wa kike bila mafanikio na alifikiakukata tamaa ndipo Mungu akasema nae juu ya hilo. alipo pata ujauzito akaweka mkono kua nitakua mtumishi na nitaolewa na mzungu maana yeye alipenda niolewe na mzungu japo mm sija wahi penda hivyo… tangu mdogo nikweli nilikua mtumishi mzuri naniliweka nadhili kadhaa na Mungu ambazo am sorry to say nini vunja baadhi na ilini kosti kuomba rehema mpaka kua hapa nilipo
  nashukuru kanirudishia karama ya utumishi ninaweza hubiri na bado ni muhubiri.

  nahisi maombi ya mama yangu yame ni funga kwa hilo japo nae aliomba juu ya yule kaka akajibiwa mind you huyo kaka sio mtanzania japo ni wale wana danganya ni wa tanzania (kipizi)

  nilisha pata kaka mlokole kabisa na wazazi wake wachungaji ila moyo ulikataa kabisa na alileta ugomvi mkubwa kati ya baba na kaka zangu kwani kaka walikataa kabisa niwe nae. ila wazazi walilazimisha. ya Mungu mengi kaka yule alifariki.

  umetaja habari ya ester nakumbuka katika maombi yangu flani niliambiwa nisome habaro ya moldekai ndugu ya ester..

  short history katika koo pande zote mbili ni familia yetu tu imeokoka..

  na mara nyingi nilipo fanyia deliverance iligundulika kaka kafugwa kwao na mzazi wake na mm nimefugwa na ma bibi wote wa wili mashangazi zangu aliolewa mmoja ndoa ilidumu 11months.. wengine hawajui mlango wa chumba cha ndo ni wameishia kuzaa njee na ni watu wazima.. kuna laana naweza sema ya kuzaa nje ya ndoa pande zote mbili kwani hata kaka zangu wame patwa na janga hilo kuzaa nje hadi kupelekea kuoa..

  kwa kijana nimeona tu madhabau tofauti na me nikifanya usafi kwa na mama yangu iwe tuna piga deki au tunaosha vyombo..

  naweza sema kama kuomba sijui tena nianzie wapi na ndio maana nimeleta hoja hii kwenye uwazi atae GUSWA/WIWA kunibeba kwenye maombi maana hata Yesu msalaba ulipo mzidia alisaidiwa kuubea..

  maana nimefunga nakuomba kama sio yeye apotee kabisa kwenye maisha yangu nisi wasiliane nae na wala asinitafute na Mungu aweke chachu wakosane hadi na dadangu. ila wapiii anakazana. chakushangaza ni aina ya maombi nimeomba kwa wanaume wengi sana wanao nisumbua Mungu adili nao watoke kwenye maisha yangu na nikafaulu ila kwa huyu shetani siju Mungu kashika bango.

  naombeni msaada katika hili..
  POLENI SANA KWA MAANDISHI MENGI

 22. Mungu ni halisi je ukimwomba mkate akupe jiwe au samaki akupe nyoka Hapana jichunguze acha kuchanganya maombi na hisia dada ninachojua Mungu si mwanadam hata aseme uongo bado hujampa nafasi asilimia zote nyingine ziko kwa huyo kijana badilika utamwona Mungualie hai

 23. YJ
  Shalom,
  pole kwa yale unayopitia.
  naomba nianze na maswali,
  1. je, unaamini kwamba Yesu anaweza kukutoa kwenye shida uliyomo?
  2. unataka nini?
  3. unaamini kwamba huyo ndiye aliyetoka kwenye moyo wa Mungu?
  4. uliomba upewe mume au mchumba?
  5. kama uliomba upewe mume, wakati unaomba upewe mume uliomba upewe mume wa aina gani?
  6. ulishamuuliza roho mtakatifu kwanini ulifululiza kufatwa na wale wa mama mdogo na wale wakristo jina?
  usikurupuke kujibu tafakari na uelewe msingi wa haya maswali kuhusiana na tatizo lako ndipo ujibu. lakini pale huna amani kujibu kuwa huru your privacy matters too.
  nikupe jibu la kuzunguka ili uzungushe akili na ndipo utakapoweza kuelewa zaidi.

  dada mmoja alifatwa na wakaka wawili, aliyemkubali kumbe hakuwa chaguo la Mungu, lakini kwa neema roho mtakatifu akamwambia kwamba huyu mwingine ndiye akamwonyesha na ubaadae wa jinsi itakavyokua kwa kila mmoja. akamwambia huyo uliyemchagua wewe utakua hivi na hivi na huyu ninayekuletea mimi utakua hivi na hivi. kifupi yule aliyemchagua yeye angempa mateso na huzuni baadae na huyu anayechaguliwa ndiye atakayempa furaha maana anafanana na hitaji la moyo wake, hapa ndipo tulipoambiwa kwamba Mungu hutupatia mwenzi wa kufanana naye. dada yule alimuomba kama ndiye basi anionyeshe na mimi ndipo ataamini na atakubali chaguo la Mungu,wakati huo tulikua hatujazoeana na yule dada kiasi cha kunieleza mambo yake, siku moja nikiwa kwenye maombi nikaletewa sura ya mtu nisiyemfahamu roho mtakatifu alipoona nimenasa feature zote za kumtambulisha picha ile ikaondolewa nilimuuliza huyu ni nani? akaniletea picha ya huyo dada na huyo kaka pamoja kisha akaniambia mume wake. sikumwambia mara nilisubiri wakati wake, wakati ulipofika nikamweleza kuwa kuna mtu anamfatilia lakini yeye ana wasiwasi yuko hivi na hivi akasema ndiyo nikamwambia ndiye mume wake, dada yule wakati namwambia alikua mtulivu wala hakushituka Tulifanya maombi tuliyotakiwa kufanya maisha yakaendelea, baada ya miezi sita ndipo aliponiambia kwanini nilimuona mume wake kumbe ni sababu alitaka uthibitisho, haikuishia hapo baada ya muda yule kaka alianza kubadilika akawa mwiba kwa yule dada, alipokuja kunieleza nilirudi kupiga goti nikauliza Yesu kwani wewe umekua muongo? kwanini kuniletea mtu ambaye kumbe sie? nini tatizo? majibu aliyoleta ni kwamba dada yule hakuwa na kibali kwa yule kaka alitakiwa aombe kibali kama esta, pili kawaida ya wazazi ivunjwe, hapa ikabidi nimhoji dada kuhusu wazazi wake na wazazi wa kaka, kumbe kawaida yao ilikua kwamba baba wote walizaa nje ya ndoa, hivyo ilibidi tufanye maombi ya kuondoa kawaida ya wazazi isije ikaathiri uhusiano wa vijana hawa kumbuka Mungu hupatiliza wana maovu ya baba zao. baada ya maombi yale haikuchukua muda kaka akaanza kumjali dada, akaanza na utambulisho kwa pande zote, wanakaribia kusema yes I do. hapa tunapata nini? hata kama ni chaguo la Mungu bado ana tabia za asili, bado ana tabia alizorithi toka kwa wazazi, alizoadopt kwenye mazingira aliyokulia nk nk nk. unapaswa kujua nini kipo nyuma ya pazia lasivyo utaomba na kuomba bila kujua unaomba nini. barikiwa na uonyeshwe njia ya kuyafikia majibu yako, maana wengine kama sauli walipoona Mungu hajibu wakaenda kwa waganga na kumbe Isaya anauliza je haiwapasi watu kuuliza habari kwa Mungu wao? nitakaporudi nitakuletea kisa cha dada mwingine naamini kupitia shuhuda hizi utajengwa na kujua jinsi ya kujinasua.

 24. Pole dada YJ kwa kipindi ulichonacho. Nami nimepitia magumu na bado sijapata mwelekeo hadi sasa na nimeanza kuombea maswala ya mahusiano yangu tangu mwaka 2002. Nashauri upitie ushauri nilioshauriwa kwenye post yangu ya JE NI ULIMWENGU WA SASA? PAMOJA NA USHAURI UNAOTOLEWA KUTAKUA NA KITU CHA ZAIDI. NAOMBA WANA SG WAKE KWA WAUME MTUSAIDIE SISI TULIOAMUA KUMTUMIKIA MUNGU TUMEKUA NA WAKATI MGUMU SANA. MBARIKIWE

 25. na hapana wana wa Mungu sija wahi mlazimu aokoke. sana tu nime mshuhudia neno la Mungu kama nishuhudiavyo wengine na kumuuliza ni nini kina mfanya asimpe Mungu maisha yake kama hajampa akasema alisha okoka kiruthelan basi nikamwacha sna niku mkaribisha kanisani au semina au mikutano kama wa mwakasege alihidhulia mpaka mwisho na hakatai..

  nashukuru Mungu kanipa neema na uwezo wakushinda tamaa ya mwili napia nikaweza achana nae hata japo nilimpenda…(nini kitanitenga na upendo wa kristo right?)

  ananiumiza tu pale anapo kufa na kufufuka ki mawasiliano na shindwa ku MOVE ON..

 26. @SEVERNT kwanza kabisa hili swala niliandika kwa haraka na kunamambomengi sana sana nimeacha, ila natumai aliyo taka Mungu yaonekane ndio yaliyo onekana.

  kujibu maswali yako hakua analazimisha uasherati ila lilikua ni swala linajitokeza na pia naweza sema hajaokoka ila ni ruthelan na kama nilivyo sema katika historia ya wanaume wanifwatao yeye pekee ndio naweza sema swala la Mungu na kanisa hana kuhimizwa ni uamuzi wake mwenyewe.
  nina shaka na kwao kua na nguvu za giza maana si mara moja wala mbili nimeota niki fanya usafi kwao then ndio nina ingia napia niliona babake aki pigia madhabau ambayo sio ya kutatanisha.. just because ni mtumishi haimaanishi ni halali.

  kwenye swala lakusema naomba kwa ku beep naweza kukubali nina weza chukua week ya kupiga na kufunga na kumlilia Mungu ndio utaona yule kaka anafufuka na kunitafuta hata kwa msg nadhani likitokea hivo napunguza kasi na ku relax

  ILA KIUKWELI WATU WA MUNG, NAJUA UFALME UTA TEKWA NA WENYE NGUVU NA PIA VITA VYETU SIO KATIKA MWILI. ILA KWAKWELI NIMECHOKA KUOMBEA JAMBO HILI HILI TANGIA 2012

  nimelia naMungu amtoe katika maisha yangu asinitafute wala ila ajabu atakaa mwezi ataibuka kua anasikia kusukumwa kunitafuta. nimesha tafuta hadi mmama akaongee nae kua mimi sipendi usumbufu na aniache niendelee na maisha yangu atafute wamataifa since ndicho atakacho labda ila nimegonga mwamba..

  msg haachi kutuma na simu japo nime mmblock kwangu anatafuta wanizungukao ila kunitamkia analotaka hatamki..

  kama nimzigo nimeshindwa ubeba jamani niwekeni tu kwenye maombi yenu.

 27. BWANA YESU ASIFIWE,

  Kabla sijachangia sana nikupe bole dada yetu, lakini hongera kwa changamoto hiyo ambayo wengi huwakuta. kama sijaelewa vizuri inaonyesha huyo kijana wa kiume hajaamini mambo ya Kristo kwa level yako au hajaokoka.

  kwa haraka haraka nikushauri, endelea kuomba Mungu amuokoe kama ndio yeye maana kwake yeye yote ya yawezekana, na kama ni kweli Mungu atamwokoe na kumweka vile wewe unataka, take a note, ila usimwambie aokoke, bali Mungu mwenyewe Amwokoe kwani yaonyesha wewe umemhusisha Mungu na kama ni kweli Atafanya, maana ukimwambia wewe aokoke basi yumkini akakupoteza wewe na yeye akapotea jumla maana baada ya kuoana ndiyo kila kitu hudhihilika mbivu na Mbichi.
  Amen, ni maoni yangu. nasubiri wengine

 28. NDOTO
  Kweli ningependa kidogo kuzungumzia hasa hapo kuhusiana na swala la Ndoto ni kweli mungu huwa anatumia Ndoto kuwasiliana na watu wake lakini kifupi mungu afungwi katika box la mazoea yetu tunapokuwa tunahitaji ajibu maombi yetu. kama ni kusudi la MUNGU usipatwe na mashaka litatimia kwa wakati wake. Usiombe kwa kubipu kama maelezo yako yanavyoeleza. Inapotokea kweli mahali hapo MUNGU alikusudia kuwaweka kama Mwili mmoja. Na lipo kusudi la Mungu katika eneo hilo .huwa MUNGU anafanya Divine intervention katika mahusiano hayo mfano
  -Mathayo 1:19
  “19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
  mfano wa pili
  -Mwanzo 24:7
  . 7 Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke tokea huko; 8 na yule mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi, utafunguliwa kiapo changu hiki; lakini usimrudishe mwanangu huko.
  TAHADHARI
  Shetani anafahamu kabisa ulimwengu wa leo vijana wengi wanapenda sana kuoteshwa ndoto nae atapitia humohumo tena anatoa ndoto za kufurahisha furahisha…ieleweke tu kwenye kusudi la mungu huwa si mara zote lakufurahisha wakati mwingine hubeba kweli maumivu na uchungu.
  MASWALI
  1)Hivi kweli mtu wa kutoka kwa MUNGU aanze kulazimisha kuingia kwenye Uasherati?
  2)Halafu si kazi ya Mwanadamu kumbadilisha mtu. Wokovu huwa unatoka kwa Yesu kristo tu.
  3)Wazazi wake ni watumishi wa mungu dhehebu fulani yeye hajaokoka ila ana hofu na mungu. lakini anakuambia muingie katka uasherati. mara hiyo tena kuna nguvu za giza zinatoka kwao zinakupinga. Hapo umeniacha sijakuelewa kabisa
  LA MWISHO NI KWANGU NI HILI……dada YJ kuwa makini Mungu anaposema nasi kupitia mungu roho mtakatifu kumbuka kuwa roho mtakatifu ni mtendaji katika UTATU MTAKATIFU neno lake huwa lina nguvu ya uumbaji linakuja na nguvu…shetani ni mbembelezaji sana jikumbushe kwa samsoni.delilah akukasirika akasusa (kama leo tunavyosema)au akamkatia tamaa samson ijapokuwa samson hakumueleza ukweli mara moja kuhusiana siri yake ya nguvu. lakini alibembeleza sana na mwishoni akafikia lengo lake. Dada onesha msimamo wako wewe ni wa kristo ukitamka kitu umetamka. Kama kweli wa kutoka kwa MUNGU atakuwa wako tu
  Ayubu42:2 “Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika”

 29. Bwana Yesu asifiwe.
  Pole sana dada maana kwa sasa ni %kubwa sana watu wanalalamikia swala la mahusiano na ndoa,kwa hili Mungu atusaidie sana.
  Mimi kwa ufahamu wangu mdogo naamini ni ulimwengu/anga mbili zinapigana kwenye ulimwengu wa roho. Cha muhimu ni kusimama kwenye maombi na kuvunja hizo roho pamoja na kujipatanisha/kuomba kibali kwa ndugu zake pamoja na kuendelea kumfungua.
  Mungu akupe ushindi mkubwa dada yangu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s