Kukosa maono ni sababu ya kushindwa kwako – II

maono

Inaendelea kutoka https://strictlygospel.wordpress.com/2015/01/27/kukosa-maono-ni-sababu-ya-kushindwa-kwako-i/

Kutokuwa na vipaumbele katika maisha.

Kukosa maono kunapelekea mtu kushindwa kujizuia na huku kushindwa kujizuia ndikokutokuwa na vipaumbele. Mtu yeyote mwenye maono ni lazima atakuwa na vipaumbele vyamsingi  katika maisha yake na vipaumbele  hivyo umpelekea kufikia utimilifu wa maonoaliyonayo.

Vipaumbele ni vitu ambavyo upewa umuhimu wa hali ya juu na upewa umakini mkubwazaidi ya vitu vingine vyote. Na vitu hivi uweza chukua muda mwingi wa mtu kuliko vituvingine  vyote  na  mtu  uwa  makini  sana  kutoruhusu  vitu  vingine  ambavyo  vitaharibuutaratibu uliopo. Vipaumbele upelekea utimilifu wa maono aliyonayo mtu na umfanya mtukuzingatia kuwa sehemu sahihi, wakati sahihi na watu  sahihi.

Kwa mfano mwanafunzi  awapo shuleni  ni  lazima awe na vipaumbele  vya msingi  kamakumtumikia Mungu kama balozi wa Yesu katika eneo asomalo na kusoma kwa bidii zotekwa kuwa ni jukumu la msingi pia lililompa kuwepo mahali hapo. Na si kwa wanafunzi tubali  hata  aliyepo  kazini  ni  lazima  awe  na  vipaumbele  vya  msingi  vitakavyompelekeakufanikiwa katika kufikia hatima yake iliyo njema.

Hasiye  na  vipaumbele  ufanya  mambo  yake  pasipo  mpangilio  na  uwa  ni  mtu  asiye  namisimamo juu ya yale ayafanyayo na ukosa kujitoa kikamilifu katika mambo ayafanyayo.

Katika vipaumbele ni vyema kuzingatia kuwa kila jambo katika ulimwengu huu lina majirayake, na nyakati zake na utambuzi huu utamfanya mtu kufanya kitu sahihi katika wakatisahihi na kuepuka kufanya jambo ambalo lipo nje ya wakati.

MAMBO YA MSINGI KATIKA KUFANIKISHA VIPAUMBELE VYAKO.

– Chagua marafiki sahihi.

– Kuwa mahali sahihi, sehemu sahihi na ukifanya jambo sahihi.

– Kila  jambo ulifanyalo zingatia  wakati  kwa kuwa kila  jambo lina  wakati  wake namajira yake/ukomboe wakati.

– Ishi kwa malengo, timiza malengo yako.

– Usiishi maisha ya kuigiza, ishi maisha yako.

– Tumia vyema fedha uzipatazo hata kuweka akiba ya kukusaidia baadae.

– Kuwa hodari na moyo wa ushujaa/ usiogope kwa kuwa yapo mengi yaogopeshayo ilasababu ya kutoogopa ni kuu zaidi ya hayo yote.

– Mwamini Mungu.

– Jiamini wewe mwenyewe kuwa unaweza.

Matumizi mabaya ya muda.

Kukosa maono pia kunamsababisha mtu kutotumia muda wake vizuri hii ni kwa sababuhana  kitu  kinachomchochea  kutumia  vizuri  muda  wake  kwa  kuwa  maono  ni  kamamuongozo  unaomchochea  mtu  kufanya  kazi.  Kuna  msemo  unasema,  ‘Time  wasted,  lifewasted’ kwa kumaanisha kuwa kupoteza muda ni kupoteza maisha, hii ni kwa sababu mudakamwe hauwezi  kujirudia yaani  ukienda umeenda.  Kila saa tulipatalo hapa chini  ya juatwapaswa kulitumia vyema kwa kuwa halitokuja kurudi tena na haliwezi kukusubiri wewekutokana na uzembe au kutojitambua kwako.

Matumizi  mabaya  ya  muda  ni  pamoja  na  kujishughulisha  na  kufanya  mambo  ambayohayatakusaidia  kufikia  malengo  yako,  kwa  mfano  kutumia  muda  mwingi  kuangaliatamthilia,  filamu  na  kufanya  michezo  mingi  isiyo  na  mchango  wowote  wa  kukufanyaufanikiwe katika maisha yako.

Hii  utokea  kwa  vijana  wengi  sana  kuwa  na  matumizi  mabaya  ya  muda  kwa  kutazamamifululizo ya matamthilia kwa muda mwingi na wengine utumia hata muda wa kusoma au kazi na muda wa kumfanyia Mungu ibada, wengine pia umaliza muda wao mwingi kuchezamagemu ambayo uchukua muda mwingi pia sana, na wengine utumia muda mwingi katikamitandao ya kijamii. Vitu vyote hivi uwa na uzuri wake na ubaya wake na uweza msaidiamtu au kumuharibu kabisa;  ila ni  vyema kuzingatia sana muda kwa kufanya mambo yamsingi zaidi  ambayo usaidia katika kufikia mambo ya msingi na hata kugundua mambomakubwa. Wengine wamekuwa wakiamini kuwa hawawezi kugundua mambo makubwa ilatatizo moja wapo ni matumizi mabaya ya muda.

“ukitaka  kufanya  mambo  makubwa  na  yakatokea  na  kuushangaza  ulimwengu,hata  kuweka  historia  ya  kuishi  kwako  kwa  kugundua  na  kufanya  mambomakubwa ambayo wengine hawayafanyi ni lazima uwe makini katika matumizi yamuda wako kwa faida na kwa busara kwa kukwepa kila kitu kisicho na faida”

Kwa Waafrika suala la matumizi mabaya ya muda kwao limekuwa ni kawaida sana na watuwengi  wamekuwa  na  tatizo  la  kutoheshimu  muda.  Kuna  msemo  ambao  umekuwa  nikichocheo kikubwa cha watu kushindwa kutumia muda wao vizuri, na kichocheo hiko nineno ambalo upendwa sana kutumiwa haswa nchini Tanzania lisemalo, “muda wa kizungu,na muda wa Kiswahili/Kiafrika,”  maneno haya yamesababisha watu wengi kuendelea natabia ya matumizi mabaya ya muda katika miadi/mapatano yao na mambo mengine mengitu.  Katika matumizi  ya muda waswahili  wakitaka kuanza shughuli  saa 3:00 utoa taarifakuwa tukio litaanza saa 3:00 ya kizungu na uamini kuwa saa 3:00 ya Kiswahili katika miadini sawa na saa 4:00 ya Kiswahili au utoa taarifa kuwa tukio linaanza saa 2:00 wakijua kuwawatu watachelewa mpaka saa 3:00 ndo waanze. Tiba ya tabia hii ni kuanza katika muda wamapatano hata kama watu wamechelewa kwa kufanya hivyo siku nyingine itafanya wawahizaidi. Matumizi mabaya ya muda umfanya mtu kutofikia mambo mengi na kuyafanya kwausahihi. Si kweli kuwa kuna muda wa kizungu na muda wa Kiswahili, ni vyema kwa kilammoja kuzingatia matumizi ya muda na kuheshimu matumizi hayo.

Mungu Anaona Ambayo Wengine hawaoni juu yako.

Ikiwa Mungu aliona taifa kubwa ndani ya Yakobo mchunga mifugo wa Labani, akaonaWaziri Mkuu ndani ya Yusufu mfanya kazi wa ndani na mfungwa kule Misri, akaonamkombozi wa Israeli kwa Musa mchunga mifugo kule Midihani kwa Kuhani Yethro,Akamwona  Mwamuzi  wa  Israeli  Gideoni  yeye  Ambaye  alikuwa  dhaifu  na  kutokakatika familia ya hali ya chini sana, Akamwona Yefta aliyekataliwa na ndugu zake nakumfanya kuwa mwamuzi wa wana wa Israeli, Akaona Mfalme wa Israeli ndani yaDaudi Mchunga mifugo na hakutazamiwa hata na baba yake, Akaona Mwokozi waulimwengu na Mfalme wa mataifa katika Zizi la Ng’ombe (Yesu), Leo hazuiwi na haliuliyonayo  wewe  kukufanya  mtu mkubwa,  usiache  kumtumaini  ni  lazima atafanyaalichokusudia kwako.

–Na: Mwl. Kelvin Kitaso

Advertisements

3 thoughts on “Kukosa maono ni sababu ya kushindwa kwako – II

  1. Ni kweli sisi waafrika Mungu atusaidie sana sisi hatuwezi hasa kwa swala la kutunza ibada utaona kibao kinaelekeza ibada itaanza saa 9:00am lakini ibada itaanza saa nne au saa tatu na nusu na hii ili tubadilike kama umesema tukio fulani litaanza mda frani ni kuanza bila kusubili mtu yeyote napenda kuungana na mtoa mada kweli mda ni mali ukisha potea hauwezi kuludi
    pia sisi ni wazembe hata kwenye kazi ziwe zetu au za mwingine utakuta mtu ana biashara,au anamiliki ofisi mojawapo atafungua kwa kupenda hataheshimu mwisho wateja wakihama utaanza kuomba na kufunga kuombea hiyo kazi nasema hapo hakuna pepo au shetani ebu tubadilike jamani tuheshimu kazi zetu na za wengine
    kwa maana Mungu anasema ukiwa mwaminifu kwa machache Mungu anasema atakuweka juu ya mengi
    balikiwa nyote

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s