Sababu saba zitakazokufanya kuwa mshindi…

Glory to GOD watu wa MUNGU, leo ninataka nizungumze na wewe Sababu saba zitakazokufanya kuwa Mshindi Duniani…Zifuatazo ni Sababu hizo..

1.NENO LA MUNGU LIWE KWA WINGI NDANI YAKO..
Neno la MUNGU likiwa kwa wingi ndani yako ni Dhahili utakuwa Mshindi lakini ndani yako kukiwa na Maneno mengine kinyume na Neno la MUNGU unaweza ukatikiswa na adui na kujikuta umeanguka, ndio Maana Mfalme Daudi akasema “Moyoni Mwangu nimeliweka Nno lako nisikutende dhambi” Zaburi 119:11,Je moyoni mwako wewe umeweka Neno la namna gani??

2.MAOMBI/KUOMBA….
Daniel,Eliya,Mussa,Bwana YESU,nk Hawa wote walihakikisha wanaishi katika Maombi,Wakati Mwingine kwa kufunga,Bwana Yesu kuna sehemu aliwaambia wanafunzi wake hamkuweza kukesha name hata saa moja

Mathayo 26:40 “Akawaendea wale wanafunzi, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, Ndiyo kusema hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni na kusali ili msije mkaingia katika majaribu. Roho i tayari lakini mwili ni dhaifu.”

3.MAONO..
Hakikisha katika maisha yako Duniani unakuwa na maono, (Yaani mtazamo wa Mbeleni) hata kama wenzako hawajafika wewe unasema nitafika, usiishi bila maono, ukiwa na maono mipango yako inakuwa inaenda vizuri pasipo na shida.

Bila ya kuwa na maono ya wapi unaelekea ni rahisi kuchukuliwa na upepo na kupelekwa usikokutazamia. Maono yatakufanya ujue ni nini ufanye kwa ajili ya Mungu na maisha yako kwa ujumla.

Mithali 29: 18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

4.KUTOKUWA NA TAMAA YA VITU VISIVYOFAA
Kuna watu wanatamani vitu visivyofaa ambavyo ni kinyume na agizo la MUNGU, Ndiyo maana MUNGU akasema usitamani mke wa jirani yako,wengine wanatamani mali za wengine bila kujua chanzo chake na wengi wamepotea kwa namna hiyo

Zaburi 119:37 Unigeuze macho yangu nisitazame yasiyofaa, unihuishe katika njia yako.

5.AMBATANA NA MARAFIKI WEMA..
(Mithali 27:17) Chuma hunoa chuma. ni dhahili chuma hakiwezi kunoa embe angalia marafiki zako wanakunoa au?? angalia mtazamo wao, kuwaza kwao,nk..Wao waliokutana na Marafiki wabaya, ambao wamesababisha mpaka maono yao kufa na kurudi nyuma kwa kumuacha BWANA YESU KRISTO..Wapo waliokutana na marafiki wabaya waliokuwa na lugha chafu na kusabadilisha..Je una marafiki wa aina gani??

6.KUTOMWEKEA MUNGU MIPAKA

Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na hili hawezi…kitendo hiki Mungu anakiita kuwa ni ‘DHARAU’ kwake… Zaburi 78:41 inasema, “Wakarudi nyuma wakamjaribu MUNGU; Wakamwekea MPAKA Mtakatifu wa Israel” Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani toka Misri kwenda nchi ya Maziwa na Asali-Kanaani. Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi waone kama kama kweli ni nchi ya ‘Maziwa na Asali’…10 kati yao Waliporudi walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila inakaliwa na Wanefili-wana wa Anaki…majitu na ya kwamba wao ni kama panzi tu na hawawezi kwenda na kuimiliki. Joshua na Kalebu walileta habari njema…waliona kwa macho lakini wakazungumza kile ambacho ni ‘UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO’ wakamwamini Mungu kuwa aweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim (Hesabu sura ya 13 na ya 14) na wote waliomwekea Mungu mpaka walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya ahadi…WALIFUPISHA MAISHA YAO KWA KUTOKUAMINI KWAO…Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85( soma Joshua 14:6-14) na inaeleza pia ya kuwa Joshua alikuwa MZEE SANA, alikufa akiwa na miaka 110 lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale BWANA alipompumzisha(Joshua24:1-29)Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako…ishi maisha ya IMANI…Usimwekee Mungu mipaka, kumbuka, “Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia” Isaya 55:8-11

7.KUACHA DHAMBI

Dhambi ni mbaya…inakutenga mbali na Mungu (Isaya 59:1-2) lakini kibaya zaidi inapunguza maisha yako…inakufanya ufe kabla ya muda wako…Unafurahia kuishi maisha ya dhambi? ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe,mwenye kinyongo, kisasi nk? Unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako…unafanya kazi ambayo mshahara uitwao ‘MAUTI’ utaupata.Katika Warumi 6:23 Biblia inasema, “Kwa maana mshahara wa DHAMBI ni MAUTI(KIFO), bali karama ya Mungu ni uzima wa Milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” pia Biblia inasema, “Roho itendayo DHAMBI ndiyo itakayokufa”Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu wa kuishi…Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI kwa kutoikwepa dhambi ya Uzinzi? au ni Wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba?Dhambi ni adui mkubwa kwangu na kwako!

–Mwl.Conrad..

Advertisements

11 thoughts on “Sababu saba zitakazokufanya kuwa mshindi…

 1. AMEN,AMEN,AMEEEEEN!!!! WATUMISHI WA MUNGU MBARIKIWE NA BWANA.MUNGU AZIDI KUWAINUA NA KUWATETEA KWENYE HILA ZA mwovu shetani.

 2. ninawasalimu nyote kupitia jina linalo pita majina yoteyani jina la BWANAWETU YESU KRISTO kwanza nimpongeze ngugu yangu MABINZA LS kwa mchango wake mzuri mimi amenibaliki sana kwa ufafanuzi wake ebu tuwe watu wa kujifunza sio wa kubisha tu bila kuwa na hoja za msingi
  biblia inasema neno la kristo na likae kwa wingi ndani yetu neno kweli ni yesu mwenyewe ni sawa na kusema biblia nzima ni Yesu mwenyewe sasa biblia inaposema neno likae kwa wingi ndani yetu inaa maana ebu tuishi kwa kulitendea kazi neno la Mungu shida kubwa hata wale waolaumu wapendekoste kuwa ni waongo,wachawi.nk wanasahau kuwa nao wanawajibu
  1.wewe kabla ya kulaumu wewe ukoje je unamwabudu Mungu ktk Roho na kweli au ndio wale mnaongalia kibanzi kwa wengine wakati wewe una boliti ndani ya jicho lako. yesu anakuta kwanza tuondoe matatizo yetu kwanza ndio tuanze kuwasaidia wengine
  2.pia hata nyinyi mnaolaumu manabii wa uongo,walokole nk mnakosea mnaonekana hamjui neno biblia inasema ukiona ndugu yako anapotea ukamuacha bila kumsaidia damu yake itatakwa kwako ina maana ukiona mtu anakosea yani ni mchawi,mwongo,nk ili usiwe mnafiki mbele Mungu mwendee mweleze kuwa unacho fanya ni makosa kwa mujibu wa neno la mungu unampa na maandiko nani jasili hata kama mnasali naye kanisa moja kazi ni kusema pembeni ebu tuache kuwa wanafiki
  3.tuwasaidie watu waishi sawa na neno la mungu linavyo elekeza hakuna dhehebu lisilo na wabaya kote kuna magugu,ngano.ila yesu anataka ngano ukibaki kuwa magugu jiandae kutuwa motoni

  mubalikiwe nyote

 3. Chicharito, na wapendwa wengine,
  Swala si UPENTEKOSITE, kuwa Mpentekosite si kuwa “Mcha Mungu”! Kila kusanyiko linalokwenda pamoja kuabudu Mungu pahali fulani, huwa limebeba waumini wa aina tatu kuu, Kundi la kwanza na ndilo kubwa, ni wale waamini, wasiyo amini Neno lolote la Mungu ndani ya kusanyiko husika, kundi la pili ambalo nalo lina fuatia kwa ukubwa ni wale wapo waamini wanaoamini sehemu ya Neno la Mungu lakini hawaamini kila Neno la Mungu,lakini si Neno ndani ya kusanyiko, na kundi la tatu ni waamini wenye imani ya “Watoto wadogo”, Imani isiyo na shaka na Neno la Mungu hata kipengele kimoja, Imani ya kundi hilo la tatu ni Imani isiyotikisika, na pahali pao pa kuabudia wanapajua, yaani ni katika Roho na kweli!

  Aitha yakupasa pia kuelewa kuwa Upentekosite ama pahali wanapokwenda kukusanyikia watu ili kumwabudu Mungu, hapo si pahali pa kuabudia, pahali pa kuabudia palipo halisi ni pale pawapasapo watoto wa kweli wa Mungu kuabudia, ni pale ambapo Bwana Yesu Kristo alipopaelezea wakati akimwambia yule mama Msamaria, wakati wa mazungumzo yao pale kisimani. Ukiisoma kwa makini ile Yohana 4:23-24 inasema, “23Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. 24Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.’’

  Unaona? Kumbe, sasa unaweza kuona kwamba, swala si mtu kuwa mpentekosite, maana ni rahisi tu kumkuta mpentekosite muuongo, mwizi, nabii wa uongo, kahaba na kadhalika au mchawi kama ulivyosema, kinachotakiwa ni “Mwabudu Mungu” aabuduye katika Roho na kweli, kumbe pahali pa kuabudia ukipajua na ukapaendea ili kumwabudu Mungu, ndipo Mungu “atakutaka”!

  Usishangazwe na Wapentekosite Waliookoka lakini ni ‘Wachawi’ watu kama hao naweza kuwaita ni “Wasamalia”. Utakubaliana nami ukimsikiliza yule mama Msamaria katika ile Yohana 4:20, alipokuwa akizungumza na Bwana Yesu, katika mazungumzo hayo aligusia aina ya ibada aliyokuwa akiitumia ili kumwabudu Mungu, na hata kuainisha pahali pafaapo pa kuabudia, mama huyo alimwambia Yesu Kristo kuwa, “20Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.’’
  21Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 22Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi.

  Kwa mjibu wa Bwana Yesu utaona kuwa, Kumwabudu Mungu si kwakuwa watu wanaitikadi na imani ya Dhehebu fulani, bali Ibada ni ile inayotokana na ule “uoho na ukweli” katika kuabudu. Kwa hiyo, uwe mpentekosite lakini kama humwabudu Mungu katika Roho na kweli, mpentekosite kama huyo, ana kuwa anaabudu asichokijua na hata kama amebahatika kuwa “Myahudi” yaani mtu asiye na ira yoyote katika roho yake, lakini akawa bado anashikilia mira na desturi za “Upentekosete” wake huyo bado atakuwa anakwenda kuabudia katika “Yerusalem” ya duniani apapo amepafanya kuwa ni pahali pake pa kuabudia. Kwa mjibu wa Bwana Yesu Kristo ni kwamba, Mungu hayupo katika “Upentekosite” Kwa hiyo nidhahili kuwa Mungu hawataki wanaoabudu katika upentekosite, bali wanao abudu katika Roho na kweli!

  Kumbuka kwamba,
  “Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.’’

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 4. Mbona kuna Wapentekonaste wapo Makanisa ya Kiroho na wachawi wakubwa kwanini tusiwaweke kwenye Fact ya 7….ndio maana tunaambiwa waache Dhambi, Mithali 1:10

 5. Miss Christina K,
  Umezidi kunipeleka mbali na kunipotezea uelewa! Unataka kuniambiaje? Hiyo Factor Namba 7 ndiyo inayotakiwa kukaa kwa wingi ndani ya Mwamini ili aishi maisha ya ushindi?

  Tazama ulivyosema, “Factor namba 7(KUACHA DHAMBI) ndiyo iliyoficha hizo factor
  nyingine.INJILI zinazohubiriwa sasa hasa katika huduma za manabii
  wa uongo na makanisa ya kiroho yaliyokengeuka HAZITUWEZESHI
  KUPATA MAARIFA YA JINSI YA KUACHA DHAMBI bali zinatuwezesha
  KUELEMEWA NA MIUJIZA YA MIZIGO YA DHAMBI!!………..” mwisho wa nukuu.

  Mh! yawezekanaje mtu aliyeokoka na akiendelea katika wokovu, akawa tena ndani ya maisha ya dhambi? Neno la Mungu linasema katika Yohana 1:12 inasema kuwa “12Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina Lake.”

  Sasa Miss Christina K, ni manabii wa Uongo wapi na ni makanisa ya kiroho ya namna gani yaliyokengeuka, ambayo upo tofauti nayo, wakati nawe unaongea na kutufundisha hapa kama wao?

  Wapendwa, Aliyeokoka ni mtoto wa Mngu, huyo hawi na dhambi na hawezi kutenda dhambi, msisikilize mafundisho ya uongo, kama huamini hebu soma hii, ona hii 1Yhn. 3:7-8, inasema, “7Watoto wadogo, mtu ye yote na asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama Yeye alivyo na haki. 8Yeye atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa sababu Ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziangamize kazi za Ibilisi.

  Na Kwa waongo, wanao wadanganya watu kuwa, waweza kuwa umeokoka kisha ukatenda dhambi, kasha ukatubishwa tena! Kwa makusudi, kukinzana na Neno la Mungu! Hivyo kuwa kinyume na mstari huu wa 9 sura ya 3 ya 1Yohana hiyohiyo, inasema, “9Ye yote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.”

  Manabii wa uongo hawawapendi hata hao washirika wao, ambao pia ni ndugu zao, bila huruma huwanyonya mali na pesa, kwa uongo na unafiki huwadanganyishia miujiza, ambayo pia siyo yao, na huwapotosha kwa kuwaita mbele na kuwatubisha dhambi, badala ya kuwalisha Neno la Mungu ambalo hilo ndilo hutakasa makosa ya watu!

  Kwa maana hiyo, msishangae nikisema hivyo, kwa sababu nguvu ya kusema hivyo inatokana na huu mstari wa 10, katika hiyo 1Yhn.3, AMBAPO INASEMA “10Kwa jinsi hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na watoto wa Ibilisi nao. Ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.”

  Esther_mushi kwa mchango wako wa tarehe 18/02/2015 mida ya 12:08 PM sijakuelewa kila nikiusoma, pengine nitakuelewa ukiufafanua vizuri, usikwazike tupo kujifunz tafadhali.

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai”

 6. Ubarikiwe mtumishi

  Sent from my Huawei Mobile

  Strictly Gospel wrote:

  > a:hover { color: red; } a { text-decoration: none; color: #0088cc; } a.primaryactionlink:link, a.primaryactionlink:visited { background-color: #2585B2; color: #fff; } a.primaryactionlink:hover, a.primaryactionlink:active { background-color: #11729E !important; color: #fff !important; } /* @media only screen and (max-device-width: 480px) { .post { min-width: 700px !important; } } */ WordPress.com Strictly Gospel posted: ” Glory to GOD watu wa MUNGU, leo ninataka nizungumze na wewe Sababu saba zitakazokufanya kuwa Mshindi Duniani…Zifuatazo ni Sababu hizo.. 1.NENO LA MUNGU LIWE KWA WINGI NDANI YAKO.. Neno la MUNGU likiwa kwa wingi ndani yako ni Dhahili utakuwa Mshindi “

 7. Barikiwa sana Mtumishi.
  Hizo factor ni nzito zinaweza kuandikiwa zaidi ya vitabu milioni moja!
  Kwa kweli tukifanikiwa KUACHA KUISHI MAISHA YA DHAMBI(1 YOHANA 3:1-4) ndipo tunapoyapata na hayo mengine.

  Factor namba 7(KUACHA DHAMBI) ndiyo iliyoficha hizo factor
  nyingine.INJILI zinazohubiriwa sasa hasa katika huduma za manabii
  wa uongo na makanisa ya kiroho yaliyokengeuka HAZITUWEZESHI
  KUPATA MAARIFA YA JINSI YA KUACHA DHAMBI bali zinatuwezesha
  KUELEMEWA NA MIUJIZA YA MIZIGO YA DHAMBI!!Sasa usinikasirikie
  kwa sababu nimewataja tena mbwamwitu,mimi niko bize naendelea
  kutafakari SABABU SABA ZITAKAZOWAFANYA WATEULE WAWE
  ZAIDI YA WASHINDI!

 8. Asante sana mwalimu kwa ujumbe mzuri, nimebarikiwa moyoni na nimetiwa udadisi mwingi na hivyo kutaka kujua zaidi kama ifuatavyo:-

  1. Nikisoma katika Yohana 1:1 inasema “hapo mwanzo alikuwako “Neno” naye “Neno”, alikuwa Mungu….” , katika hiyohiyo Yohana 1:14 inasema, Neno akafanyika mwili akakaa mwetu…” (kwa maana hiyo Neno ndiye Yesu mwenyewe). Na nikiendelea kuiangalia hiyohiyo Yohana sura 15:5, Bwana wetu Yesu kristo anatuambia kuwa, “…..bila mimi ninyi hamuwezi kufanya Neno lolote”! Sasa, wewe
  umetufundisha hivi:-

  1.NENO LA MUNGU LIWE KWA WINGI NDANI YAKO..
  Neno la MUNGU likiwa kwa wingi ndani yako ni Dhahili utakuwa Mshindi lakini ndani yako kukiwa na Maneno mengine kinyume na Neno la MUNGU unaweza ukatikiswa na adui na kujikuta umeanguka, ndio Maana Mfalme Daudi akasema “Moyoni Mwangu nimeliweka Nno lako nisikutende dhambi” Zaburi 119:11,Je moyoni mwako wewe umeweka Neno la namna gani??

  “Neno” la Mungu linalopaswa kukaa kwa wingi ndani ya mwamini, ambalo ni tofauti na hayo mambo mengine sita uliyoyaainisha, ili akiyapata mtu awe mshindi, (ambayo nayo nayaona kuwa umenukuu “Neno” hilohilo la Mungu), Je, “Neno” la Mungu unalomaanisha ni kitu gani au ni lipi, lipaswalo kukaa kwa wingi ndani ya Mwamini ili ajumlishe na hayo mengine sita kufanya yawe mambo saba ya ushindi?

  “Ufahamu ni chembe ya uhai!”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s