Mambo yanapoharibika unafanyaje?

Watu wengi wamekwenda kwa hisia kuhusu kuingia kwenye suala la ndoa. Kuna wengi walidhani Mungu aliwaambia kwamba wenzi wao ni kutoka kwake na walipoingia kwenye ndoa wanatamani kuondoka baada ya mambo kuwa magumu wanagundua hawakuwa sahihi. Je wafanyeje? ni hatua gani wachukue?

Advertisements

4 thoughts on “Mambo yanapoharibika unafanyaje?

 1. kama misingi imeharibika mwenye haki atafanya nini?
  toka kitabu cha mwanzo mpaka ufunuo sijaona aliewahi kuishi na mwanamke bila tashwishi?
  adam alikipata kwa sababu ya hawa mkewe na kusababisha anguko kuu,
  ibrahim na sara ndoa yao pia ilikuwa na changamoto nzito.
  musa na miliam wasomi wanakumbuka….
  daudi ndo mchepukaji mzuri
  mwanae suleimani ndo mwisho wa reli….
  samsoni mzee wa totoz….

  endelea kuorodhesha mpendwa,

  nachotaka uone waseja kama akina daniel, jesus. paulo, atleast wanamaliza riadha yao wakiwa na ushuuda mkuu.

  nachotaka kusema ishi na mwanamke ujue mapungufu ya mwandamu.
  hao wanaojita walimu wa ndoa huwe na uhakika wanafundisha mapokeo na theory tuuuuuuu

  bado najifunza

 2. Mr. Mulele wasalaam,
  Nimeona mchango wako hapo juu ni kweli uliyoyasema ila nadhani kulingana na swali lilivyojielekeza sioni kama muulza swali utakuwa umemjibu.
  Nadhani ungejibu kuwa
  1.Je! ni nn hasa kipimo cha kumpata mchumba/mke mwema.
  2. Je waliowapata wake wema kwa maombi huku wakidhani Mungu aliwaambia kwamba wenzi wao ni kutoka kwake na walipoingia kwenye ndoa wanatamani kuondoka baada ya mambo kuwa magumu wanagundua hawakuwa sahihi. Je wafanyeje?
  3. Na ni hatua gani wachukue?

  Katika majibu yako umetoa maelezo mengi kama mahubiri ya jumla vile, mimi nilitegemea kuwa kwa sababu umesema kuwa wewe ni msomi basi ungejibu kwa kufuata swali linavyotaka na kwa mtiririrko unaoeleweka.

 3. Ndugu zangu,
  Nnatamani kupata changamoto kutoka kwenu ili nami nipate jua ni nini sababu ya kuvunjika kwa NDOA na watu kuwa disappointed baadae.

  Ndugu zangu,
  Tambueni kuwa, Mungu ametuletea elimu ya NDOA kupitia kwa Adam, kwamba Adam alikuwa “Mkamilifu” lakini kwa kule kutolewa ‘Ubavu’ akawa sio mkamilifu tena hadi Ubavu urudi mahali pake ndipo Ukamilifu wa Adam utakapo kuwa nae! (kumbuka NENO, hakuna mtu ataemuona Mungu asipokuwa na huo Utakatifu yaani Ukamilifu!!)

  Hebu angalia Uumbaji, hakuna tofauty baina ya wanyama na watu ila ni ktk Akili tu. Humu duniani kuna watu ambao ni wanyama kuliko wanyama hata nasi kwa kutolielewa NENO tunashiriki ktk unyama hasa ktk NDOA zetu. Hebu angalia wanyama wanapoingia ktk ‘ndoa’, je ni yupi anaelea watoto ‘peke yake’ !? je sivyo inavyo kuwa pindi migogoro ktk hizo NDOA inapoanza!? Kuku, Mbwa, Mabata, Mapaka na wote hao ni Mke ndie hubakia na kuhangaika na watoto na baba akilazimishwa ku’saidia’ je tofauty iko wapi!? Wanyama 😦 !

  Ktk NDOA halisi ya ki-Adam, hilo halipo kabisa! Namna pekee ya Mama kuwapenda watoto wake ktk KWELI ni KUMTII Mumewe (ndio Kumpenda Mumewe) na namna pekee ya Mume kuwapenda watoto wake ktk KWELI ni KUMPENDA Mkewe. Utajiri ulio utajiri halisi umo ndani ya NDOA, Uzima ulio halisi wa milele umo ndani ya NDOA, Baraka zooote kutoka kwa Mungu hushukia ktk NDOA. Ukamilifu wa Mwanamke ni Mwanamume, na ukamilifu wa Mwanamume ni MUNGU. (Hivyo ndivyo NENO la Mungu linavyosema)

  Waalimu wetu mara nyingi wanatifundisha mambo ambayo hayahusiani na NDOA wakiyaita “Mafundisho ya NDOA” ambayo kwa kweli ni uzoefu wao ktk kuwajua Watu wakipingana na NENO ki- waziwazi.
  Ndugu zangu, Bila ya kujua na kujifunza kuwa wa Bin-Adam, basi NDOA zetu hazina tofauty na za wanyama (labda tofauty ndogo sana) Kuvumiliana, kuchukuliana, ‘kusameheana’ kujifunza ‘kumzoea’ na mambo kama hayo hayaleti uhalisia wa NDOA ya ki-Mungu. Tusome ili tuwafundishe vijana wetu KWELI kwasababu KWELI ndio itakayo ‘tutoa’ ktk giza !
  Ndugu, Kumbuka kuwa kuna Watu ambao ni tofauty na Bin-Adamu !! Mithali ya Kiswahili: “Kwenye watu kumi, Bin-Adam mmoja” ina uhalisia sana ktk somo hili.
  NB: Watu waliumbwa kwa NENO
  Bin-Adam aliumbwa handmaiden 🙂 Huyu ni Mjumbe/Balozi wa Mungu duniani kwaajili ya Watu !!

  Ndugu yenu
  Jackson Mulele

  Salaams.

 4. Ndugu zangu,
  Kumekuwa na natharia nyingi zinazo husu NDOA na mafundisho ya ‘kimapokeo’ ya namna ya kuishi ktk NDOA.
  Mimi ni mzaliwa ktk familia ya ki-lokole na kupitishwa na kupitia ktk vyuo kadhaa vya biblia hapa Tanzania Ulaya na America. Mimi, leo ninaliangalia NENO la Mungu kwa namna ya tofauty na hizo jumuia zote inapozungumziwa NDOA.

  Ninaposoma NENO, ninaliona lipo wazi kuwa Mungu aliwaumba Watu kwa sura na mfano wake kwa NENO, Mwanamke na Mwanamume kwa wakati mmoja ‘kwa jinsi zake sawasawa na viumbe vingine’ na Bwana akawabarikia na kuwaambia “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuitiisha yaani hawa walikuwa tofauty na wengine wote kwamba hawa walipewa AKILI ili wawaongoze wale wengine” Hivyo nnapata ufahamu kuwa Mwanamke na Mwanamume waliumbwa siku moja tena wako na uwezo unaolingana ila kila mmoja ni kwa “jinsi yake” (yaani mwanamume ana’jinsia’ ya kiume na Mwanamke ana ‘jinsia’ ya kike! na hivyo wakikutana kimwili kwa jinsi ya taratibu ya AKILI zao yaani MILA zao, basi watakuwa Mke na Mume) Hivyo ndivyo NENO linavyoonyesha ktk ufahamu wangu jinsi Mungu alivyo umba, nae akasema “Natazama, kila kitu ni chema”

  Muulize mwana theologian yeyote akuambie uumbaji wa kila kitu uko ktk kitabu gani!? Atakuambia ni Mwanzo sura ya kwanza, ambayo ni sahihi kabisa. Maana hata hiyo sura ya pili inaanza kwa kuthibitisha kuwa sura ya kwanza ndio UUMBAJI KAMILI, yaani “Basi, mbingu na nchi zikamalizika na jeshi lake lote.”

  Adam
  Adam ni NABII wa kwanza kutoka kwa Mungu (soma ukoo wa ki-nabii ktk Mathayo1: nawe utapata picha kuwa walikuwapo Manabii na watu waliotumwa kwao ktk nyakati zote yaani Mataifa)

  Maana halisi ya NDOA tunaipata kutoka kwa NABII wa kwanza yaani Adam. Yeye hakuumbwa kwa NENO, Mke wake alimtegemea yeye ili apate NENO, Adam alikuwa ni muwakilishi wa Mungu kwa Mkewe ndio maana Hawa alisema direct kuwa “Mungu ametukataza tusile” wakati utafahamu kuwa yeye hakuwahi kupewa agizo lolote na Mungu ila Mumewe maana yeye hakuwapo ! Kwahiyo NDOA za sasa ni za ki-Mataifa tu sababu Mke na Mume wana uwezo sawa! Lakini kama Mke akifahamu kuwa yeye ni sehemu ya Mumewe na ametoka Ubavuni mwake, kamwe hawawezi kubishana na ndio UFALME wa MUNGU na watoto watakao zaliwa na hao ni Warithi kamili wa Ufalme wa Mungu.

  Katika NDOA halisi, Mke ndie anaemkamilisha Mumewe na kuwa WAMOJA, Mume ndie anaetoa Mahari na kutuma washenga na kuiandaa NYUMBA yaani YEYE MWENYEWE. Mke ndie anaeweza kuibomoa au kuijenga nyumba ‘yake’ yaani Mbavu zinakaa ndani ya Mwili hivyo ‘nyumbani kwa Mbavu’ ni Mwili wa Mwanamume Mithali14:1

  Sasa, Ili tuweze kuwa na NDOA halisi, ni lazima NENO la Mungu likae kwa wingi ndani yetu ktk hekima yote, Mume akijua wajibu wake ktk NDOA na Mke nae akijua wajibu wake. NDOA ni Baraka tupu na wala sio KWELI hata kidogo kwamba ‘tunapaswa kuvumiliana ktk NDOA’

  PENDO lina majukumu tofauty kabisa kutoka ktk kila upande, tofauty na tunavyofundishwa “kupendana” kwa mfano, ni upungufu wa ufahamu kudai kuwa unampenda Mungu wakati hutii AMRI yake, ni uongo, ujinga, na kujilisha upepo na kutoa sadaka za bure! PENDO ktk NDOA ni vivyo hivyo, kuna majukumu ya baba kwa Mkewe na watoto wake na kuna majukumu tofauty kabisa ambayo kwayo ndio Mama na watoto watasema tunaMPENDA baba yetu, wala sio kuishia kusema kama tulivyo ktk NDOA zetu zenye mabishano na ngumi na matusi na kununniana kwa mara kwa mara! Ni NDOA za ki-kafiri ambazo tunaita Maaskofu na watumishi ‘wazithibitishe’ 🙂

  Inafikia wakati nnapotafakari ELIMU YA NDOA nnatia shaka kwamba bila kuifahamu NDOA hatuwezi kuingia ktk UFALME wa Mungu ambo YEYE mwenyewe alisema umo ndani yetu! NDOA ndio UKAMILIFU wa mwanadamu Mathayo5:48 na ktk NDOA ndio kwenye Furaha na Uzima wa milele. NENO ukamilifu linatokana na kuunganisha vitu ili viwe KIMOJA

  Vijana wanatakiwa kusimama ktk Elimu ya Mungu ili waelewe kuwa wao kama wazazi watarajiwa wanatakiwa kuandaa mazingira ya uungu ktk mahusiano yao badala ya kutazama kama ‘walimwengu’ wanavyo tazama na kuwakiana tamaa ya mali au uzuri wa sura au mambo mengi mafu.

  Shaloom!
  Jackson Mulele

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s