‘Maaskofu hatuna mamlaka ya kuwaamulia waumini kuhusu katiba mpya’ – PENGO

UFUATAO ni ujumbe mfupi wa Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alioutoa jana katika Kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam kuhusiana na waraka wa maaskofu uliotolewa hivi karibuni kwa Wakristo nchini kujiandikishakikamilifu na kisha kuikataa Katiba Inayopendekezwa wakati wa kura ya maoni kwa vile haikujadiliwa kiuadilifu.

“Maaskofu hatuna mamlaka ya kuwaamulia/kuwalazimisha waumini wetu wafanye uamuzi gani kuhusu katiba, kuwaamulia ni kuwadharau kuwa hawawezi kufanya uamuzi sahihi wao wenyewe na kuingilia uhuru wao.

Waraka huu unaleta utengano katika taifa kuwa Wakristo, tumechukua uamuzi dhidi ya serikali na wengine….

Tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa tafakari yao binafsi bila shinikizo letu…..

Wakati hili linajadiliwa nilikuwa Italy katika kusimikwa makardinali na baadaye India, wengine wakavumisha nimelazwa,..wengine nimefariki, lakini namshukuru Mungu hizo ni dua za kuniongezea maisha marefu na afya (makofi).

Nililetewa waraka nikausoma, umepitishwa baada ya tafakari kubwa nauheshimu. Lakini nadhani tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa uhuru baada ya kutafakari….

Si sahihi tukaenda katika katiba kama Wakristo kwa shinikizo la kupinga katiba…

Wawe huru anayepinga kwa hiari yake anayekubali kwa dhamiri yake….
Sidhani kama viongozi wa dini sasa tuna amri ya kulazimisha uamuzi juu ya katiba….

Magazetini

Advertisements

11 thoughts on “‘Maaskofu hatuna mamlaka ya kuwaamulia waumini kuhusu katiba mpya’ – PENGO

 1. Bwana Yesu Asifiwe!Heri ya mwaka mpya, na hongereni kwa kazi njema mnayoifanya! Ninawaletea clip ya ujumbe wa Gwajima kwa askofu Pengo, ili ikiwa itafaa, basi na wapendwa wapate kuyasikia hayo yanayoendelea ktk ulimwengu wa Kikristo! Bwana awazidishe ktk yote yenye kumpa utukufu! Ck

 2. Hahahaha…!
  Maandalizi yamekamilika, foleni ya kupiga kura ya maoni ni ndefu saaana, tena jua ni kali saana, wapendwa wamejiwahi kwa kuja na miamvuli ili waitimize “Amri” waliyopewa na maaskofu wao.

  Ilipofika zamu yao, wakasema mioyoni mwao, “Kwa Jina la Yesu, napiga kura ya HAPANA!!” wakapiga kura hiyo ya HAPANA, wakayakataa mapendekezo hayo ya Katiba!

  Nilipokutana na mmoja wao, nikamuuliza sababu haswa zilizompelekea kupiga kura hiyo ya ‘Hapana’. Akajaribu kujieleza, lakini akagundua kuwa alikuwa anajaribu kuyarejea aliyoyakariri kutoka “Tamko la maaskofu”, ndipo mwisho akaniambia kuwa, ukweli ni kwamba, yeye ameuitikia tu wito wa viongozi wake, mambo mengine yeye hajui lolote; hii ndiyo aibu anayoisema askofu Pengo!

  Labda niwaulizeni wapendwa, baada ya “Amri” hiyo kutolewa, waumini wana haja gani ya kuisoma katiba pendekezi hiyo ilhali uamuzi umekwisha kufikiwa? Hata ikatokea wakapewa nafasi ya kuchangia hoja ktk katiba hiyo, watachangia nini wakati ufahamu wao ulikwisha fungwa na maaskofu wao?

  Maaskofu, timizeni wajibu wenu wa kuwafikisha waumini wenu ktk kiwango cha wao “Kupakwa Mafuta”, hapo ndipo mtaiona na Raha ya Injili, maana wakiisha kupakwa hayo mafuta, hawatahitaji tena miongozo yenu yenye kulidharaulisha Kanisa lililonunuliwa kwa thamani kuu sana, huyo aliyelinunua ndiye atakayeliongoza ktk mambo yote, hata ktk kura ya katiba!

  1 Yohana 2:27
  “Nanyi mafuta yale mliyopata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha, lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.”

  Na mwisho, usia wangu kwa maaskofu, ni kwamba mkiutimiza wajibu wenu huo, basi hao waumini wenu kwa kuwa wao wapakwa mafuta, wanaweza kuwasaidia sana ktk maamuzi yanayolihusu Kanisa, ukichukulia kwamba nafasi zenu za uaskofu si za kuteuliwa na Mungu bali ni za kisiasa zaidi, kwani ninyi mliitamani nafasi hiyo ndipo mkagombea kwa kampeni!!!

  Gbu all!

 3. Amani ya Kristo iwe kwenu katika utimilifu wake!

  Ndugu wapendwa, hakuna mahali katika maagizo ya Mungu (Neno lake kwetu) panapoagiza wachungaji, maaskofu n.k. kutowaelimisha waumini wao masuala ya uraia au kwa lugha nyepesi masuala ya kisiasa.

  Kwanza watu wengi hawajui kama Mungu ndiye Muanzilishi wa uongozi, utawala na taratibu zake zote. Mungu ndiye aliyeweka wafalme, waamuzi na watawala tangu mwanzo; tena ndiye aliyewapa maelekezo, wakati mwingine aliwateua, aliwaonya na kuwahukumu kupitia manabii (yaani watumishi wake) ambao tunawakataa leo wasifanye hiyo kazi.

  Kama tunaelewa kuwa viongozi wetu wa kiroho ni watumishi wa Mungu, kwanini tusielewe kuwa wanaufahamu fulani juu ya jambo linalotuzunguka?

 4. Pengo huwa hapendi kutanguliwa na baadae kuonekana anafuata mkumbo, lakini katika hili mbona hakusema waislamu waliposema wasipopata mahakama wataikataa katiba. Mtazamo wangu maaskofu hawakukosea, nyie mnaotaka kuspiritualize kila kitu mbona kwenye kura mnaenda kupiga. Maaskofu ni watanzania kama walivyo wanasiasa, wao kusemea wanachoona kwani ni kosa. Hata mheshimiwa mwenyewe mbona alisema msimamo wake mbao of course ndio ulikuwa msimamo wa chama chake wakati wa ufunguzi wa bunge la katiba, na hakutakiwa kufanya hivyo kwa position yake kama rais.

  Binafsi siungi mkono hoja ya pengo hata kidogo.

 5. Kwa hiyo,

  Mtu/mtumishi wa Mungu kuwaambia watu( hasa waumini) kitu kizuri cha kuchagua kinachohusu mstakabali wao kama sehemu ya taifa ni kuacha utumishi wa injili?

  Kwani kumwambia mtu uchaguzi mzuri wa kufanya kati ya vitu viwili vilivyo mbele yake, hiyo siyo habari njema ni nini?

  Kwa nini watumishi wanapowahimiza watu kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hakuna kiongozi wa serikali wala askofu wala shekhe aliyesema kuwa kufanya hivyo ni kuwaamulia watu kitu cha kufanya na ni kuingilia kazi za siasa?

  Kama mlikuwa hamjui, basi jueni sasa kuwa kuwaambia waumi juu ya mambo hayo nfo kumpa Kaisari kilicho chake. Na ni sisi tusiokuwa wa Kaisari tunaoambiwa kumpa Kaisari kilicho chake, na hiyo ni kwa sababu bado tunafungiwa nira na Kaisari kwa jinsi ilivyo sawasawa!

  Lazima tujue kuwa kuna sehemu siasa na Injili zinaungana na kuna mahali zinaachana. Hizo angle tunapaswa kuzitambua ili tufanye lililosahihi kwa wakati sahihi.

  Ndo hivyo!

 6. nimegundua vitu vingi katika hii inchi,wengine cjui wanasoma bibilia kama gazeti la udaku au mungu wa dunia hii amewapofusha fikra.kwani kanisani tunaenda kujifunza au kutoa sadaka 2 kama ni kujifunza basi hili wanatufundisha,na kama tunaisikia sauti ya mungu kupitia watumishi wake na hii ni sauti ya mungu,mbona hatupingi maelekezo mengine yanayotolewa kanisani kuhusu waumini mbona hatusemi tunawaingilia waumini mbona munasema mungu amesema,kama amesema amesema kupitia nani kama sio viongozi au watumishi wa mungu,nini maana ya kwenda kanisani ?ni kitu gani kinachotokea duniani hakipo kwenye bibilia mpaka unasema viongozi wa dini hawatakiwai kuwaamulia wananchi,mimi nadhani tusipotoshane chamsingi neno la mungu linasema nini basi?mfano soma ezekieli 18;20-32.mungu ana sema roho itendayo dhambi ndio itakayokufa,endelea kusoma mungu aongee na roho yako na upone kwa jina la yesu,pia mungu ameagiza watumishi wa mungu waonye,wakaripie na kufundisha sasa wewe sijui unasoma bibilia gani?mambo mengine yanakela kweli kwel?mungu gusa masihi wako kwa mkono wako maana wewe ndiwe mwenye haki?labda niongezee kwa kusema dini na siasa haviwezi kutengana vyote vinategemeana kimojawapo kama hakipo dunia haiwezi kwenda popote,lazima tuelewe kuna huduma na uongozi haviwezi kutengana,siasa si mchezo mchafu bali walioko ndani ya siasa ndio wachafu sasa kama siasa ni chafu basi wasafi wanahitajika watatoka wapi kama sio wenye hofu ya mungu?sasa watu wamelogwa kwa kudai viongozi wa dini wasiingie kwenye siasa tutawaliwa na mawakala wa kuzimu mpaka lini mungu mwenyewe anatushangaaa?ametupa kila kitu lakini tumeibiwa.ni sawa na kuwa silaha harafu hujui jinsi ya kuitumia itakua tu.mwanzo 1:28.tuache ushabiki tufanye yale tuliyoagizwa na mungu si kupinga kwa akili zetu bali ktk neno la BWANA,daniel,yusufu n.k tanzania fufuka mungu atawale kwa jina la YESU.namshukuru mungu kukutana na changamoto hizi zinanifanfa nijifunze mengi ila upende usipende mwanakondoo anaenda kutawala tanzania aneenda kufanya mapinduzi kwa jina la YESU watanzania wameamka yesu anawahitaji

 7. MADHEHEBU ni VYAMA VYA SIASA, ndio maana Madhehebu si Makanisa.KANISA halijishughulishi na siasa bali Kuhubiri Injili ya Yesu Kristo (MARKO 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.”Viongozi wote wa MADHEHEBU ni Wanasiasa.

 8. MADHEHEBU na VYAMA VYA SIASA, ndio maana Madhehebu si Makanisa.KANISA halijishughulishi na siasa bali Kuhubiri Injili ya Yesu Kristo (MARKO 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.”Viongozi wote wa MADHEHEBU ni Wanasiasa.

 9. Binafsi na unga mkono waraka wa Askofu Pengo, Maskofu wanatoa mamla hiyo wapi, na jee hiyo ndio shuguli tulioitiwa kufanya kama watumishi wa Mungu? Sana tunachochea chuki ambazo azina msingi wowote wala faida yoyote. Tusiingizi siasi kanisani, ambaye ameshindwa na kazi ya kanisa ajiunge na wanasiasi tu, kuliko kujificha kwenye mgongo wakanisa. Nafikiri maskofu walifanya hivyo awajatumia vizuri vyazifa zao ambazo Mungu aliwapa za kuujenga ufalme wake. Biblia inasema here wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Naona ipo haja ya maskofu kujitathini upya katika kauli zao, wakuwa kama Mungu watu, yaani unasikitisha sana, tunazidi kuwachanganya washirika na kuwagawa kwa maslai binafsi. Mungu atuurumie sana kwa koso hilo, wajirudi kwa kauli hiyo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s