Askofu Kakobe awakemea watumishi wa Mungu!

Askofu mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakaria Kakobe hivi karibuni aliongea maneno makali kwa watumishi wa Mungu yaliyopelekea baadhi ya watu (kanisa) kujihoji kuhusu maisha yao na wakati huo huo wengi ikiwemo watumishi wa Mungu kukemea hali ya Askofu huyo kuhukumu bila kuwajua wahusika maisha yao binafsi na Mungu.

Askofu Kakobe alimwakia Rose Muhando kwa wazi  na kusema “Leo sikwepeshi…wanaume wanatikisa viuno Rose Muhando, hiyo ni team ya kwenda motoni, hakuna Mungu humo ndani….watu wanaoenda mbinguni hawako hivyo Rose Muhando rudi msalabani kama hujazaliwa mara ya pili zaliwa leo.Unatikisa viuno…..viuno unaleta kanisani,viuno peleka bar Rose Muhando kila mahali stage show, stage show, vitu hivi havikuwepo assemblies, vitu hivi havikuwepo kwa wapentekoste, nani atainuka mchungaji kukemea, kila mtu anajifanya ameokoka lakini huoni wokovu ule

Aliendelea kuwashukia wanasiasa maarufu kama Nape Nnauye, Mh. Mwakyembe, Mh. Lazaro Nyarandu na Paul Makonda na kuwataka  wajipime, warudi msalabani na kuzaliwa mara ya pili. Aliendelea zaidi na kusema “Mimi hapa sihitaji mtu, Waziri ukija hapa, Raisi ukija hapa utanisaidia nini, Raisi huwezi kunipa hela mimi.. mimi ndio nitakupa, mimi sihitaji hela ya mtu, Mungu aliyeniita ana fedha na dhahabu vyote ni mali yake, sihitaji hela ya mwanasiasa, sihitaji hela ya waziri…wakija kuleta harambee zao hapa watajisifu, tutashindwa kuwapiga kama hivi ninavyowapiga, lakini sasahivi ninakupiga Nape, nakupiga Makonda, Nakupiga Mangula, siangalii sura ya mtu hapa….Injili iko pale pale.

Hakuishia hapo alimshukia mtumishi wa Mungu TB Joshua na kusema “Na tunaona mlolongo wa watu sasahivi wanajifichaficha wanaenda kwa TB Joshua, kwenye mchanganyo, TB Joshua hata haubiri kuhusu kuzaliwa mara ya pili, anazungumza vitu vya ajabu ajabu na miujiza feki, watu wanajazana hapo kama Mwigulu Nchemba

Mpaka sasa hakuna Mchungaji aliyemjibu Askofu Zakaria Kakobe.

Advertisements

42 thoughts on “Askofu Kakobe awakemea watumishi wa Mungu!

 1. Tu viungo katika mwili wa Kristo ILA HUWEZI UKAWA KIUNGO CHA KILA MAHALI KATIKA MWILI ndio maana tunatofautiana katika utendaji.
  Ukikuta unao umahiri mkubwa wa kukosoa viungo vingine katika mwili wa kristo ujue kipawa hicho cha kukosoa Mungu alikileta kikusaidie kujikosoa mwenyewe na badala yake kimetumika isivyokusudiwa.

 2. Ni kweli Pendael,

  Na alaaniwe kabisa.

  Lakini hebu sema sasa na wewe, mtu aliyenizaa katika Bwana kwa nini asiwe baba yangu ktk kristo?

  Hebu tuongeeni sasa ktika namna ya kutoa majibu!

 3. WAGALATIA 1:8-9
  “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe”.

 4. Wapendwa,
  Kuna vitu vingine kuvipotezea muda mimi huona kama ni upotevu mkubwa sana, wakati viko wazi sana kwenye maandiko.
  Kwanza naomba tukumbuke kuwa kila kitu kwa asili ni chema ila huja kuharibiwa na matumizi.

  Yesu aliwaambia wasimwite mtu Rabbi, ambayo kwa tafsiri ilikuwa ni Title anayopewa mwalimu wa kiyahudi kama heshima kwake (Mt 23:8)

  Lakini katika Waefeso 4:11- Biblia inasema Yesu alitoa wengine kuwa….. ..walimu! Ndio maana kwa mjinga wa maandiko ni rahisi sana kujichanganya hapa!

  Na kinachotofautisha ulimaanisha baba ipi au mwalimu ipi, siyo herufi kubwa na ndogo (hiyo miundo ya lugha tu za uandishi), bali ni ile mantiki halisi uliyoibeba ndani yako au niiite Context.

  Lwembe aliniambia Paul hakumaanisha kuwa wale watu wamwite baba, lakini sasa yeye mwenyewe hakuniambia Paul alimaanisha nini!

  Hebu tuone hilo andiko:

  ”14 I am writing this not to shame you but to warn you as my dear children. 15 Even if you had ten thousand guardians in Christ, you do not have many fathers, for in Christ Jesus I became your father through the gospel” 1Cor 4;

  Ivi andiko kama hili lilivyowazi, kama halimaanishi kuwa Paul anawaambia hao waefeso kuwa yeye ndiye baba yao-katika injili, lina maana gani nyingine katika muktadha wa tunachojadili hapa?

  Kuna neno Children- watoto
  Kuna neno father – baba

  Unapokuta kuna baba na mtoto mahali, unadhani kuwa suala la mmoja kuitwa baba na mwingine kuitwa mtoto ni la kuambiwa tena kati ya hao wawili, ivi unahitaji kumwambia mtoto wako akuite baba, ambaye tayari ameshajua kuwa wewe ni baba yake?

  Lazima kutafuta kujua na kujifunza nini context ya ”msimwite mtu baba duniani…., kuliko kubishana kwa maneno ya pupa tu!
  ………………………………………………………………..
  Na wewe ndugu Pendael, punguza zomeazomea yenye maneno matupu tu yasiyo na neema ndani yake, na bila wewe mwenyewe kutoa majibu sahihi.

  Mwisho wa siku tunataka watu waijue kweli wamwelekee Kristo, siyo kuwazodoa tu na kuwafukuzia mbali.

  No one knows everything,keep learning!!

 5. CHRISANT SAGARA;
  Kama ulifikiri unaweza kuhalalisha huo ‘uharamu’ kwa kujidai kuna neno la asili la ‘baba’ umegonga mwamba.
  Nimekutaka utuoneshe wazi hiyo asili ya neno ‘baba’ matokeo yake umeleta NGONJERA za Dhehebuni kwako.
  Pia, hujanikwaza kwani hivyo ndivyo ulivyo.Hayo mafundisho ndiyo yaliyokujaza moyo.
  POLE sana kwa kuwa na ‘baba’ FEKI kama huyo anayekulisha MATANGO MWITU au MAFUNDISHO POTOFU.
  Kwa kuwa umeamua KUAGA kwa kuishiwa na kuogopa ‘kutumbuliwa’ zaidi, kawapashe habari wenzako kuwa KAULI MBIU ya SG BLOG ni ” INJILI HALISI NA THABITI”.
  Hivyo kama unafanya majaribio ya kuingiza HILA za SHETANI kwenye NENO LA MUNGU, hapa umechemka.

 6. KWAKO PENDAELI SIMON.

  Kama nitakuwa nimekukwaza ndugu yangu Pendael Simon au nimeeleweka vibaya haitakuwa ndio mtazamo wangu au makusudio yangu kueleweka hivyo kwa Mungu. kwako haitakuwa na namna ya kufanya nieleweke vingine kwa hiyo msg niliyoitanguliza. kikubwa siko kwenye malumbano au mdahalo nikijua matunda ya kufanya hivyo mara nyingi huwa si kwa utukufu wa Mungu.

  Na kwakusema hivyo sijisikii kuongeza au kuendelea na maada hii kwa maana wa kuelewa ameelewa na wa kuchagua vyovyote vile atakavyo bado anahiyari tumepewa na Mungu kuchagua. Ili kuepusha kuingiliwa na kazi za mpinga Kristo na kujikuta mnakula sahani moja kikombe cha Mungu na kikombe cha Mashetani. Makusudi yangu hasa ni kueleweka vyema. Mungu anisaidie kuelewesha hapo patakapokuwa pamepungua.

  Kipekee ninawashukuru waasisi wa Blog hii, washiriki wote wenye mapenzi mema, bila kumsahau Baba yangu wa kiroho ambaye amekuwa mwaminifu kwa Mungu sana hata kutufundisha kweli yote na kutufanya kuwa na hofu zaidi kutoka Kwa Mungu.
  Paulo mtume aliwataja wale ambao aliwafundisha kuwa ni wafuasi wao na wa Bwana iThesalo 1:6. Alitambua umuhimu wa wazazi wa Kiroho kwao tena wamehesabiwa kutoa hesabu yetu kwa Bwana Waebrania13:17. nisipotambua haitakuwa haki.

  Ninathubutu tena na tena kusema
  Ninampenda Baba yangu wa Kiroho yeye anayeingia gharama kubwa kwa ajili yangu nipone.
  MUNGU AWABARIKI WASOMAJI WOTE

 7. Ninajua ninaweza kutumia muda mwingi sana kutumia maandiko mengi na mwisho hakuna ambacho kitaongezeka kwako . ili mtu aelewe somo lolote hata kama ni hesabu au history yapo mambo ya msingi yamhusuyo kuwanayo vinginevyo mwalimu atalaumiwa tu kwa jinsi ambavyo mwanafunzi hataambua kitu.

  kiufupi sitaangaika sana kufungua maandiko mengi kwa kulinganisha na lugha ya asili kwa neno hilo sababu hata hii ya kiswahili bado yapo maeneo ambayo neno baba limetumika kwa maana tofauti tofauti pia .
  Mfano Mwanzo 4:20, 21 utaona kwa maandiko hayo mawili limetumika kama mwanzilishi. mtu ambaye ndiye aliyeanzisha jambo fulani wote ambao watafuatia nyuma yake yeye ataitwa baba yao . aliyekuwa wakwanza kutumia vyombo vya muziki au kujenga nyumba . wanamuziki wote na wajenzi wote imeandikwa huyo ndiye baba yao . siyo hilo tu hata shetani ambaye ni wakwanza ktk kufanya dhambi na kusema uongo naye aliitwa baba wa uongo Yohana 8:45. hivyo mwanzilishi hata wa familia naye ni baba Mwanzo 9:18 – 23, Mwanzo10:21 na maandiko mengine mengi. Ibrahimu anatajwa kama baba wa mataifa mengi Mwanzo17:4-5. Biblia anatambua binti waliozaa na baba yao kama mzazi , Mwanzo19:31-38. Mathayo 2:22 inamtaja mtu ambaye ni baba (Helode) ili sisi tunapomtaja tumtamkeje ikiwa neno baba duniani ni kwa Mungu pekeyake si huyo tu watatajwa kina Yohana kwa baba yao Zebedayo Mathay4:21-22.

  Yesu mwenyewe anatambua kuwa tuna mababa hapa duniani aliposema nimekuja kumfitini mtu na babaye hakumaanisha kutufitini na Mungu Mathayo1o:35-37 na alitumia neno baba kama lilivyo, ampendaye baba kuliko Yesu hamstahili , hakumaanisha Mungu. ningeenda kwenye lugha ya asili pengine ingekuwa lahisi kutofautisha baba inayotajwa hapo na ile ya Mungu. mfano Yohana 5:17-18 ambapo ilimtaja Mungu na wale waliielewa ile lugha vizuri ndio maana ukiangalia tafsiri ya kiswahili inaweza kukusumbua kwamba Yesu kusema baba yangu tu wao hawakumaanisha yusuph ambaye alijulikana kama mzazi wa Yesu lakini walielewa mbali zaidi kwa neno alilotamka moja tu . lilitosha kutambulisha Yesu ni Mungu. kwa maneno yao wakakiri kuwa anajifanya kuwa sawa na Mungu kumwita Mungu baba yake. na Baba ile pia kwenye lugha ya asili inatofautiana na ile ya Mathayo 6:9 tunaposema Baba yetu uliye mbinguni. hii inamtaja Mungu lakini haitupi sisi sehemu katika Mungu huyo zaidi ya viumbe wake kwa muumbaji. ile ya Yohana 5 inampa mtamkaji kuwa sehemu ya huyo Mungu. Yesu aliwaambia wayahudi kumwambia baba yenu au mama yenu akijua kabisa tunao hao Mathayo15:5 na kama hataki tumwite mtu baba angeanza yeye kuacha kulitumia neno hilo kwanza ndipo tujifunze kwake angalia anavyolitumia hapa Marko10 :5-7. kwamba imetupasa kumwacha baba na mamayetu ili tuambatane na mke. hapo ukiichukua utakavyo unaingia dhambini. baba anayetajwa hapo ambaye tutamwacha ili tuambatane na mke ni baba yupi. na tunapowafundisha wengine tutawaeleza vipi kama wazazi hatupaswi kuwaita baba ikiwa Yesu mwenyewe ameitumia hivyo. kanisa la kwanza wao walielewa vizuri na waliitumia ipasavyo sijui wao na wewe yupi mwenye uelewa zaidi wa kile Yesu alisema nao uso kwa uso na wewe ambaye umeibuka na andiko moja tu. Waebrania12:9 inataja baba wa kimwili na baba wa kiroho ambao tunapaswa kujitia chini yao na kimsingi hawakumaanisha Mungu. angalia pia Waefeso6:1-4. waheshimu baba na mama katika bwana.

  Mungu aliposema katika mwanzo 2:24 kuwa mtu atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe hakumaanisha kumwacha Mungu. japo kwa lugha ya asili neno baba lililotajwa hapo na lile ambalo Yesu alilitumia kusema msimwite mtu baba linatofautiana hii ni kutokana na mapungufu tu ya lugha yetu pamoja na zingine. ila kwasababu umehitaji kulitumia kama linavyotambulikana kwa lugha hii. basi kwa andiko hilo unapooa tu basi unatakiwa kuachana na Mungu wako na kuambatana na mkeo. hapo sijui kama tutaelewana kama ni mchungaji akufungishe ndoa na akuambie uachane na Mungu kwa sababu umeoa.
  yapo maandiko mengi kama nilivyosema hata nikitumia biblia nzima hapa sitaweza kubadili chochote kwenye ufahamu wako. ninamsihi Mungu anisaidie maarifa ya kuwasaidia watu wa namna yako.

  Inawezekana ukajifanya unauchungu sana na neno Baba kuitwa kwa yeyote huku mwenye nyumba wako tu ulikopanga unamwita hivyo, na kama ktk ufahamu wako umesimamia kila baba ni Mungu na ukaamini hivyo basi utakuwa na miungu mingi pengine kuliko ya india.

  MUNGU AWABARIKI WOTE AMBAO WAKO TAYARI KUMPENDEZA.

 8. Chrisant Sagara,
  Hebu tueleze ASILI ya neno Baba.
  Pia ni vyema ukajifunza matumizi sahihi ya maneno kulingana na mazingira.
  WAEFESO 4:11″Naye alitoa wengine kuwa Mitume; na wengine kuwa Manabii; na wengine kuwa Waiinjilist; na wengine kuwa Wachungaji na Waalimu;”
  Baba Mchungaji au baba Mwiinjilisti katajwa?
  Pia huyu mchungaji au mtume au mmojawapo hawa wahudumu wakirudi nyumbani watoto wao huwaita Baba.
  Kanisani kuna Baba mmoja tu, naye ni BWANA YESU KRISTO.
  Madhehebuni kuna baba mchungaji,mama mchungaji, na majina mengine ya watumishi wa tumbo.
  Hivyo kabla ya kuongea kwa sababu tu kiongozi wa dhehebu lako ‘ameshushwa cheo’, hebu FIKIRI KWANZA.

 9. ni gharama sana kumfundisha mtu masomo yanayomhusu aliyezaliwa mara ya pili na kumpa ambaye hata kuzaliwa mara ya pili hajui ni nini kama Nikodemu alivyokuwa. leo neno baba eti watu wanajifanya limekuwa geni masikioni mwao kwa mwanadamu kuitwa hivyo na wakati huo huo majumbani mwao si kwa wazazi tu hata wenye nyumba ambazo wamepanga tena wengine ni wapagani kabisa lakini wanawaita baba mwenyenyumba . Biblia inaposema msimwite mtu baba duniani inamaana gani. hilo ndio la msingi watu wangepaswa kujiuliza kutokana na maandiko ili wapewe majibu. na pale ambapo unakutana na jambo ambalo linakupa utata flani ki biblia , usiwe mwepesi wa kuingiza tafsiri zako maana unaweza ukatafsiri uongo si kwamakusudi ila kwa kutokuwa na ufahamu sahihi, pamoja na hayo uongo huo utatosha kukupeleka motoni. tena unakuwa umemsingizia Mungu ndio amesema kwa hicho unachoeleza tofauti. kumbuka Yesu anajua pia kwamba kuna mababa ambao watakuwepo duniani . ili kupata tafsiri nzuri tungeweza kutafuta neno hilo toka kwenye lugha ya asili na lilivyokuwa likitumika . na baada ya hapo tuangalie kile kilichotajwa kuhusiana na wazazi wa kiroho kwetu na ilivyokuwa ikiwataja . ki ukweli ingekuwa nzito zaidi kuliko hicho mnachofikilia kwa huyo aliyemwita mchungaji wake baba yake. Baba mchungaji ni sahihi kabisa kuitwa hivyo na haichukui nafasi ya Mungu kwetu kabisa. kama wachungaji wenu sio baba wa kiroho kwenu siwalazimishi maana siku hizi ndani ya kanisa hakuna kondoo. wote wanajichunga wenyewe haipo tofauti mchungaji na mchungwaji.

  Itatusaidia nini kama tukipewa ushindi katika mambo ambayo hayana faida yoyote katika roho zaidi ya kutupelekea kumtukana Mungu tu. ninajua hata kama nitatoa muda mwingi sana kuelimisha matokeo nimeyaona hapo juu kwa waelimishaji wengi na wametumia hekima sana haikusaidia.

  ninampenda sana baba yangu wa Kiroho kama wakiri wa Mungu Tito 2:7 na nimeona anavyotoa uwakiri wake katika kukemea dhambi. ninawatamani sana wale ambao wanamtazama na kumsikiliza kila siku Mungu anisaidie na nina hakika nikikaa chini ya mtumishi kama huyu anayesisitiza utakatifu bila kuangalia uso wa Mtu ninanafasi kubwa sana ya kuingia mbinguni. Huyu ni baba yangu Askofu Zacharia Kakobe.

 10. Sungura,

  ”Msimwite mtu baba duniani”
  Mtume Paul kwa kusema, 1Cor 4:15 “Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.”
  Kauli hii haimainishi kwamba mt. Paulo anawaambia hao “wamwite baba”!!!

  Ni rahisi sana kutoka Andiko hilo kudhania kwamba amesema wamwite baba au mtu aliyekuzaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili, basi huyo wapaswa kumwita baba, ni ujinga wa kiroho kumwita mtu baba au kukubali kuitwa “baba”!!!

  Gbu!

 11. Sungura, kama nilivyosema, sina cha kujibizana na wewe kuhusu hoja zako za kipuuzi.Endelea kuropoka kwani umekunywa mvinyo wa Uasherati wa mafundisho toka kuzimu.Najua wewe ni MTOTO WA KAINI” Muuaji wa Neno” unayejitahidi kuungamiza KWELI YA NENO LA MUNGU kwa kutumia Werevu ulionao.Kwa kuwa umejitoa mhanga kupambana na KWELI YA NENO LA MUNGU,endelea kwani ASUBUHI MOJA UTAJIKUTA JEHANAMU.

 12. Sungura, kama nilivyosema, sina cha kujibizana na wewe kuhusu hoja zako za kipuuzi.Endelea kuropoka kwani umekunywa mvinyo wa Uasherati wa mafundisho toka kuzimu.

 13. Mhh, Pendael,

  U are axaggerating something out of nothing and for nothing”

  Wewe mwenyewe unaonesha uko na chuki na Kakobe, sasa sijui anayechukia ccm na anayaemchukia anayechukia ccm nani ana chuki zaidi!

  Kila ukitaka kuongea kitu dhidi ya Kakobe huwa unaongea vitu vilevile kwa jazba ilele na kwa maneno makali yaleyale.

  ”Msimwite mtu baba duniani” ina maana yake pana ambayo bila shaka watu wengi huwa hawaipati sawasawa.

  Kama ilikuwa na maana hiyohiyo sisisi ya kutomwita mtu ‘baba’, basi hata wazazi wetu tunapowaita baba tunatenda dhambi.

  Ni vizuri sana kulitazama jambo kwa upana katika context yake. Biblia iko wazi kuwa mtu akikuhubiria injili katika kristo nawe ukamfuata kristo huyo anakuwa baba yako. Sasa kwa kulijua hilo mtu unapaswa kurudi kuangalia kwa makini Yesu anaposema msiwe na baba duniani alikuwa anamaanisha nini, au vinginevyo Paul alipingana na Yesu kule kwa wakorintho.

  (1Cor 4:15 – Even if you had ten thousand guardians in Christ, you do not have many fathers, for in Christ Jesus I became your father through the gospel).

  Nilitegemea pia tungeangalia zaidi usahihi wa kile alichosema mtu badala ya kumwangalia mtu aliyesema, ili kujadili kwetu kujikite kwenye kilichosemwa na si aliyesema. Hapa naona mkazo wa comment unawekwa zaidi kwa Kakobe kuliko kuwekwa kwa alichosema Kakobe.

  Hufika wakati mtu ukaamua kufanya juu ya mtu kama Yesu alivyosema kwa habari ya mafarisayo kuhusu wanachosema na wanachotenda.
  (Mt 23:3 – So you must be careful to do everything they tell you. But do not do what they do, for they do not practice what they preach).
  usashihi wa alichosema Kakobe, hicho ni cha muhimu zaidi kuliko Kakobe

  Kama mtu unadhani kuwa Kakobe hana biblical moral command inayotosha kumfanya kuwa mfano wa kuigwa, basi angalia kama alichosema kiko sahihi ukifuate hicho.

  Huo ndio wito wangu kwa wachangiaji!

 14. CK LWEMBE na MABINZA LS, mmenena ndugu zangu, na BWANA YESU AWABARIKI kwa jinsi mnavyomtetea mbele za watu na na Mbele ya kizazi hiki KIKAIDI kisichopenda KWELI YA NENO LA MUNGU. Huyu David Carol ni Kipofu aliyekwishalewa mvinyo wa mafundisho potofu.Leo hii anamwita Kakobe Baba kesho atamwita nani kama si MUNGU?Kakobe huyu anayesifiwa na Waabudu kivuli, katika mafundisho yake amekuwa mstari wa mbele KUPINGA UBATIZO KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO pamoja na kusema MITUME WA BWANA YESU WALIKUWA NA MAFUNDISHO TOFAUTI!! Kama si UPINGA NENO (KRISTO) nini? Wanaoitwa Wapentekoste wa madhehebu leo wameyarudia matapishi ,mfano; huyu David Carol anayemwita Askofu wake “Baba”, ukweli ni kwamba ameshindwa tu kumwita ‘Baba mtakatifu’ kama wafanyavyo ndugu zake. MABINZA LS, umesema vyema kuwa Kakobe ana chuki na CCM ndio maana ametumia mimbara yake kama Jukwaa la siasa kwani yeye ni UKAWA, kwa hiyo, hivi ni vita vya kisiasa Mimbarani na si mahubiri. Mwaka 1995 Kakobe alimpigia Mrema kampeni ya kwenda Ikulu huku akiahidi Mrema akishindwa ataacha Uaskofu matokeo yake Mrema hakuwa Rais na hakuacha Uaskofu.Sasa hii anayohubiri ndiyo FULL GOSPEL au ni HYBRID GOSPEL? Kwa hakika MATHAYO 24:24 ,IMETIMIA. ***MUNGU HAANGALII SURA YA MTU BALI HULIANGALIA NENO LAKE APATE KULITIMIZA***. Amani ikae na WAAMINIO.

 15. David Carol,
  Unasema kwa furaha kabisa, “Mungu azidi kukutumia Baba yetu.”
  Bali Mungu anasema, MT.‬ ‭23‬:‭9 “Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.”!

  Tafakari, chukua hatua!

  Gbu!

 16. Mpendwa DAVID CAROL,
  Kutoa maoni ama kumkosoa mtu si kwa sababu anachukiwa, msimamo wa mtu hauwezi kuwa ndiyo kigezo cha utakatifu, lazima kila jambo lipimwe kwa Neno la Mungu! Aidha ieleweke kwamba kukosoa maoni ama mafundisho ya Askofu Zachary Kakobe siyo ndiyo watu wana “sapoti” ubaya na tabia zinazochochea ama kuzalisha ubaya. Vilevile ‘kumsapoti’ Kakobe hakuna maana ya moja kwa moja kuwa una ienzi Pentecostal Assembles ya zamani au ya leo, unaweza ukawa unafiki tu pia! Upentekoste ulifika na kuishia pale ulipo sasa. Kipindi hiki ni cha ubayana, uwazi na ukweli katika Neno, ambalo ndiyo ile ‘KWELI’ ambayo watu wenye kuifuata wanawekwa huru na kuwa huru kwelikweli!
  Unaweza kusema kwa mtazamo na upenzi, na kuuacha ule ukweli. Askofu Kakobe amekuwa haeleweki kwa kipindi hiki cha mwishomwisho, hasa kwangu Binafsi kwa kuwa mara nyingi nimemuona na kumsikia akifanya mazungumzo na mafundisho ya kimtizamo badala ya kusimamia Neno kama kigezo cha Injili halisi ya Mungu. Hebu tazama maelezo yake kama yalivyoletwa na mleta habarii hii hapa, imeelezwa kuwa Kakobe huku akizingatia zaidi maisha ya watu binafsi, alimcharukia Rose kwa ukali na dharau na kuwasakama kwa bidii bila staa makada na viongozi waandamizi wa chama cha kisiasa cha CCM na kusema, nanukuu,
  “…………“Leo sikwepeshi…wanaume wanatikisa viuno Rose Muhando, hiyo ni team ya kwenda motoni, hakuna Mungu humo ndani….watu wanaoenda mbinguni hawako hivyo Rose Muhando rudi msalabani kama hujazaliwa mara ya pili zaliwa leo.Unatikisa viuno…..viuno unaleta kanisani,viuno peleka bar Rose Muhando kila mahali stage show, stage show, vitu hivi havikuwepo assemblies, vitu hivi havikuwepo kwa wapentekoste, nani atainuka mchungaji kukemea, kila mtu anajifanya ameokoka lakini huoni wokovu ule ”
  ………Aliendelea kuwashukia wanasiasa maarufu kama Nape Nnauye, Mh. Mwakyembe, Mh. Lazaro Nyarandu na Paul Makonda na kuwataka wajipime, warudi msalabani na kuzaliwa mara ya pili. Aliendelea zaidi na kusema “Mimi hapa sihitaji mtu, Waziri ukija hapa, Raisi ukija hapa utanisaidia nini, Raisi huwezi kunipa hela mimi.. mimi ndio nitakupa, mimi sihitaji hela ya mtu, Mungu aliyeniita ana fedha na dhahabu vyote ni mali yake, sihitaji hela ya mwanasiasa, sihitaji hela ya waziri…wakija kuleta harambee zao hapa watajisifu, tutashindwa kuwapiga kama hivi ninavyowapiga, lakini sasahivi ninakupiga Nape, nakupiga Makonda, Nakupiga Mangula, siangalii sura ya mtu hapa….Injili iko pale pale.
  Hakuishia hapo alimshukia………. TB Joshua na kusema “Na tunaona mlolongo wa watu sasahivi wanajifichaficha wanaenda kwa TB Joshua, kwenye mchanganyo, TB Joshua hata haubiri kuhusu kuzaliwa mara ya pili, anazungumza vitu vya ajabu ajabu na miujiza feki, watu wanajazana hapo kama Mwigulu Nchemba“ mwisho wa kunukuu.
  Alikuwa akimaanisha nini, na je katika hilo kuna utakatifu gani unaoweza kupatikana iwapo mwamini atayafuata mafundisho hayo? Je, huo si mtazamo na upenzi wake binafsi anaotaka kuufanya kuwa ni Neno la Mungu? Kwani kuna Upentekoste wa zamani na wa sasa katika Neno la Mungu? Kinachowaharibia watu na kuwanyang’anya ile sifa nzuri ya ucha Mungu ni ule ubinafsi na uchoyo! Kakobe yote hayo ni kwa sababu ya kwanini watu mashuhuri wasiende kwake wakati yeye na TB Josua wapo katika renk moja! Kwani, kipindi kile Mh. Mrema alipoenda kwa Kakobe, mbona Kakobe hakumpa pesa Mrema na kumfukuza, au kwa vile Mrema alikuwa tayari mpinzani wa CCM? Acheni uongo! Tatizo la Askofu Kakobe ninaloliona kwake ni aitha haipendi CCM au amemezwa na tabia za siasa ya Dunia, ndiyo maana analazimisha mitazamo, hisia na matakwa yake binafsi kuwa yawe ndiyo Neno la Mungu! Ndugu yangu DAVID CAROL nimekuona hapa ukimwita Askofu Kakobe baba!
  Elewa kuwa, hatutaishi na wala hatutakuja kuishi kwa Jambo lolote litokanalo na watu ama maraika, ila tu kwa Neno la Mungu, kwa vile hatuna MWANADAMU tunayepaswa kumwita Baba!
  (Ufahamu ni chembe ya Uhai!)

 17. Mungu amzidishie neema Askofu Zachary Kakobe. Wasiopenda kweli watasema mengi lakini ukweli utabaki pale pale. Askofu Kakobe ameitwa na Mungu, hakujiingiza katika huduma ili kutafuta pesa. Waumini wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, hasa wale wa Dar es salaam wanajua ni kwa jinsi gani Mtumishi huyo amejitenga na Ulimwengu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu. Mahubiri kama hayo ya kukemea na kukalipia, hayajaanza leo, tangu mwanzo wa huduma yake amekuwa akihubiri kwa viwango hivyo hivyo hata sasa anazidi kukaza nati. Hapa tunapaswa kujiuliza, kwa nini aliitaja Assemblies na Pentekoste? Askofu Kakobe alikuwa ni mshirika wa Assemblies huko nyuma kabla ya kuanzisha FGBF mwaka 1989 kwa uongozi wa Mungu. Anaijua vizuri Assemblies na Pentekoste ya zamani ilivyokuwa. Watumishi wengi wa kipentekoste wameuacha upendo wa kwanza. Kweli ya Mungu wanazidi kuichuja na kufundisha kwa viwango vya watu walivyo. Nani atasimama nyakati hizi na kukemea kama Kakobe? Mungu azidi kukutumia Baba yetu. http://WWW.bishopzacharykakobe.org

 18. Hahahahahaaaa, kweli, Dunia imekwisha, hata maasikofu wanafikiria “Ukwale” mtupu?!! Inachekesha kama si kusikitisha sana, mimi nadhani mjueni kwanza Askofu Kakobe kama si kumwelewa. Hata hivyo zipo pia chuki binafsi ndani ya mtu ambazo mtu anaweza kuzigeuzageuza zikawa ni “KAMA” Neno la mungu, si nia yangu kuunga mkono ushetani hapa, ninachotaka walau mjue tu kwamba, mtu anaweza kuchukia jambo na kwa sababu zake akaliita dhambi kama ambavyo anawaona akina Nappe na wengineo kuwa wapo nje ya Msalaba, hayo ni mawazo ya chuki binafsi za kakobe na siyo Neno la Mungu! Kiukweli chuki ama utofauti wa kuwaza na kutazama (Siyo kwa mjibu wa Neno la Mungu) ndiko kulikozalisha mifumuko na utitiri wa madhehebu yanayojiita ya ki Kristo leo, kwa kifupi huyo ndiye shetani na kazi zake!

  Ni kweli Biblia inasema watu waenende kwa tofauti ya umataifa yaani si kama kwa desturi za wasio amini na pia wafanye mambo kwa kiasi, kwa hekima, kwa heshima na kwa utaratibu. Lakini tunapozungumzia “Kucheza Mziki” kwa kifupi ni “Kutikisatikisa mwili kwa kuufuatisha mziki!” Kutikisika huko kwa mwili ambapo hapa namaanisha ‘kucheza mziki’ kunategemea utamaduni, mira na desturi za wachezaji wenyewe! Ambapo kwa Wakerewe kukata Viuno ni ndiyo hasa ‘ufundi’ katika kucheza mziki, wasukuma hutikisa mabega wanapocheza ngoma ya ‘Wighasha ama ile ya Bucheye’ lakini Wasukuma haohao wanapocheza Bughoboghobo huruka ruka na kukimbia kimbia huku na kule, wakati huo huo wakitumia zana za kilimo na siraha za asili (Mikuki na au Fimbo). Lakini wasukuma haohao pia, wanapocheza Bhunungure huruka kwa mtindo wa wacheza Sarakasi! Sasa ukienda kasi, utakuta kwamba ukiruka kama Mmasai wakati unacheza ngoma ya kisukuma ya ‘Wighasha’, au hata ukiwa Msukuma ukaruka ‘Kinungure’ wakati kinachochezwa hapo ni ‘Wighasha’ Wasukuma wataona kuwa unafanya fujo, na kwakweli itabidi uamliwe kukaa chini, na ukikaidi utalambishwa bakora, hata kama ngoma imekukolea namna gani!

  Kwa maana hiyohiyo, Daudi inaposemwa alicheza hadi nguo zikamvuka, hakucheza nyimbo ama mziki tofauti na uliokuwa ukichezwa pale, ila kilichoonekana kwa aliyeshangazwa na uchezaji ule, NDIKO KUKABAKI KUNAMSHANGAZA YEYE PEKE YAKE, NA WALA SI YULE MUNGU AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA AKICHEZEWA MZIKI ULE! Ninachotaka ukijue hapa ni kwamba, unafanya vile ama unacheza vile UKINIA nini? “JAMBO LOLOTE LISILO LA IMANI NI DHAMBI, Biblia inasema!”

  Cha kuzingatia katika kutenda ni ‘Neno’ la Mungu, ambalo hilo huchambua na kuiweka wazi ‘NIA’ ya mtendaji. Kufikilia ki mtazamo, ama kiupenzi hizo ni ‘Akili’ binafsi. Unapozungumzia jambo Fulani na kuliita ni dhambi, ni lazima Biblia iwe imesema hivyo. Lakini mahali ambapo Biblia inapopaacha kimya, wewe kwa nini uingize story zako za kimtazamo na hisia zako za kidini na kuzifanya eti ni Neno la Mungu?! Unataka kusema mtu akicheza kwa kunengua, kwani adhabu ya “dhambi” hiyo ni nini?

  Ukiwa katika mwili, lazima usumbuliwe na mambo ya mwili, huwezi kamwe kuwa huru. Biblia inasema Mwana (ambaye ndiye Neno) akikuweka huru unakuwa huru kwelikweli, na pahali pengine inasema watu wakiijua ile kweli, watakuwa huru; kweli ni nini? Kweli ni NENO la Mungu! Unaposema ama kuita “kukata Viuno” ni vibaya kwa Rose mhando na wanakwaya wengine, ni lazima utuonyeshe ni kwa mjibu wa nini, kwa mtazamo ama kwa Neno?! Ni kweli ukiwa Mtu wa Mungu, hekima maarifa, busara na ufunuo wa Roho mtakatifu ni mhimu katika utendaji wetu wa kila siku. Wakati mwingine inashauriwa na Neno la Mungu kwamba, “mambo mengine yaache ikiwa kunawaamini wachanga, na pengine panasema unapaswa kutofanya mambo Fulani ama kutokula chakula Fulani ili usiwakwaze wengine”. Lakini usilazimishe watu wasifanye mambo kwa uhuru kwa maelezo kuwa unakwazika, acha kuangalia kama vipi!

  Biblia inasema, dhambi hutokana na tamaa zilizomo ndani ya mtu. Lazima ujiulize kwanini wewe, ukiona tu watu wanakata viuno unajisikia hivyo unavyojisikia? Na hatimaye kufikia mkataa kuwa hicho ukionacho mbele yako ni ukataji viuono wa kidhambi! Kuweni huru, Neno liwaweke huru jamani. Mbona wale waisraeli walioingia nyumbani kwa ‘Kahaba’ Rahabu, hawakufikilia au kumuona kuwa huyu ni kahaba, leo ninyi mnapokwenda ama kuona tu Rose anaimba mnatelemsha macho yenu kiunono mwake, mnamtaka nini? Biblia, inasema ukimtazama mwanamke kwa matamanio, tayari umekwisha zini naye. Sasa Kakobe anaposema Rose ananengua sana, huwa anafananisha na kunenguaje? Wanaume wengi, kama akina Kakobe wanatuambia tu juu ya kukata viuno kwa akina Rose, lakini hawatuambii, ni wangapi wanaowavua nguo ki mawazo na kuwabakiza uchi wa mnyama, mwanapokuwa wakiingia kanisa hadi wanapokwenda kuketi! Maana kwa mawazo mtu hutenda dhambi! Mbona mnafikiria sana kuwa kukata kiuno kwa Rose ni tendo la kimahaba?! Ikiwa si Neno la Mungu ni nani kawaambia ananengua kimahaba? Siyo tamaa iliyondani mwenu inayowapeleka huko?! Mwacheni anayeimbiwa na Rose aseme yeye, ninyi msimsemee, maana hakuna katika Biblia panapoelekeza namna ya kukata kiuno kufaako mtu akiwa akicheza mbele za Mungu, kila mtu na athibitike mwenyewe kwa kadri ya maelekezo ya Roho mtakatifu!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

 19. Sungura
  Hivi kwani kukata mauno na kukata mabega inaweza kuwa sawa ? nmekujibu kwamba hipo hali ya tamaa yataamshwa na hali ya asili ya mwili wa binadamu…..nimekuelezea zipo ibada ambazo zilikuwa zikiishia katika vitendo vya ngono ambazo ni za miungu na ndio nikamkuambia makuhani wa miungu hiyo kazi zao ilikuwa kuwaunganisha watu wao na miungu baada ya kupokea maagizo na hayo yalikuwa baadhi ya matendo
  Sasa hiyo miungu ikiwa asili yake ni kuzimu sasa matendo hayo yatakuwa yameletwa kwao kutoka wapi? na hayo maelekezo ya vitendo kama hivyo?
  Kama itakuwa bado hujaelewa itakusaidia hii makala The Histoly channel episode 1 lust

 20. Servant,

  Hata sijaelewa umejibu nini sasa. Maelezo yako siyaelewi yanalenga kusema nini hasa. Labda unifafanulie.

 21. Hahaaa, Lwembeee!

  Sawa, huyo dada sauti yake iko hivyohivyo almost katika nyimbo zake zote za kuabudu!

  Bless u!!

 22. “”Ukapigwa wimbo wa dada mmoja ambaye alikuwa ameuimba huo wimbo kwa hisia kali sana ikiwemo kutoa sauti ya kulia.””

  Huyu dada, Sungura, kila anapoimba hulia hivyo au hisia kali hizo zilimjia mara hiyo tu ndo akalia?!

 23. Sungura
  kukata mauno kwani inaweza kuwa sawa na mabega?……. napomaanisha mtazamo wa kibaiolojia tu nazungumzia mwili wa binadamu tu pasipo nafsi yapo mambo yanaamshwa na hali ya asili ya mwilini na ndio maana vitu kama hivyo wanenguaji kwa asili isingekuwa rahisi kuwaona katika kanisa…wangepatikana katika kumbi za starehe leo kakobe kakemea kuwaona wakaka lakini rahisi tu yangenyamaziwa kesho jinsia tofauti wangebeba………usijali kukudhibitishia Mungu tunayemuamini yeye yupo Mbinguni(mathayo 6:9) sasa miungu mingine ambayo ni roho kamili wanaweza kuwa wanatokea wapi?…..

 24. Servant,

  Hujanijibu nilichokuuliza. Mimi nimetaka unithibitishie kuwa kukata mauno asili yake ni kuzimu. Na kisha nikakutaka uniambie kuhusu kukata mabega kama na kwenyewe ni dhambi.

  Mimi huwa sipendi mtu anayeongea tu vitu kwa mazoea kwa sababu vimekuwa vikiongewa hivyo na watu wengi, bila hata kujua undani wa vitu hivyo..

  Elewa jambo moja kuwa hakuna kitu najisi kwa asili yake, bali vitu huja kuwa najisi(dhambi) kutokana na matumizi.
  Na kinacholeta unajisi kwenye matumizi huwa ni nia. Nia ikiwa njema matumizi yatakuwa mema, na kitu kitakuwa chema.

  Huo mtazamo wako unaouita wa kibailojia, ndo hapo udhaifu wako ulipojificha. Kwanza ni mtazamo upi huo wa kibaioljia ambao unakwambia kuwa kukata kiuno ni dhambi?

  Kwa mfano, dunia leo umejawa na unajisi wa ngono, na ndio dhambi inayoitesa sana dunia. Lakini kwa mjinga ni rahisi sana kuona au kuwaza kuwa ngono imetoka kuzimu, just kwa sababu amefocus sana kwenye matumizi najisi ya ngono.

  Lakini ngono imeumbwa na Mungu, na akatoa matumizi yake sahihi, ila watu kwa kusukumwa na ‘cunning spirit’ ya shetani, wamebadili matumizi mazuri ya ngono.

  Nilikuuliza hayo maswali ili nikufikirishe ujaribu kuona nini hasa tatizo.

  Hatuongozwi na opinion za kuzimu wala za dunia katika kufanya kwetu mambo, bali tunaongozwa na kweli katika neno la Mungu.

 25. Sungura
  Kuzimu nyumba ya Shetani na mapepo ambaye kulingana na maandiko ndiye alieanzisha dhambi sasa kuna jema kweli linaweza toka huko la kumfaa mwanadamu?

 26. Sungura
  si kwa kutazama kibiblia tu hata mtazamo wa kibaiolojia rahisi rahisi hamna haja ya kuendelea kuzungumzia
  …….Barikiwa

 27. Landelinus,

  Nani hasa unaemwambia hayo maneno?

  Wewe ulishajifunza ukaufikia ujuzi wa kweli siyo, hebu tuambie basi ukweli ulionao juu ya hilo. Sidhani kama kuna mtu amesimamia suala la Daudi kucheza katika hii mada. Na hata kama angekuwepo, tungemwambia kuwa Daudi hatuambiwi kama alikata mauno ila alicheza mpaka nguo kuanguka.

  Tuambie wewe uliyekwisha kuufikia ujuzi wa kweli, je, kucheza kwa kukata mauno biblia imesema kuwa ni dhambi? Zingatia neno kucheza, ulitofautishe na neno kukata mauno, maana kuna kukata mauno ambako hakutokani na kucheza muziki.

  Kuna kitu bila shaka niliwahi kukisema hapa pia kwenye mada fulani:

  Usiku zilikuwa zikipigwa nyimbo za kuabudu kwenye radio fulani ya kikristo. Ukapigwa wimbo wa dada mmoja ambaye alikuwa ameuimba huo wimbo kwa hisia kali sana ikiwemo kutoa sauti ya kulia.

  Gafla mpendwa mmoja akapiga simu analalamika kuhusu uimbaji wa huyo dada kuwa unampeleka kwingine. Nilishangaa sana, maana huko kwingine alikokusema ni kwenye suala la chumbani la wanandoa.

  Unaona, wengine tunaposikia sauti nyororo yenye kutuingiza uweponi mwa Bwana, yeye anasikia sauti ya mahaba yenye kumtoa uweponi na kumzamisha mahabani.

  Je, watu waache kulia mbele za Mungu kwa sababu Landelinus ataamshiwa hisia za mahaba, au Landelinus asaidiwe kubadili nia yake?

  Nia ya ndani matters a lot!

 28. 2Timotheo3:7 wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
  WAPENDWA endeleeni kujifunza lakini hilo la kunengua viuno sijui kama itafika wakati mtakapo lielewa maana mnalipenda sana .na mlivyo mabingwa wa kutafsri maandiko kama mpendavyo utasikia Daudli alicheza MUNGU AWASAIDIE MFIKE WAKATI MUWE KAMA WATOTO WADOGO

 29. Servant,

  Kwamba kukata mauno ni dhambi, yes inawezekana kabisa. Lakini vipi kuhusu kukata mabega au kunengua mabega, nayo ni dhambi?.

  Halafu, hebu twende ndani zaidi; ivi udhambi wa jambo hilo uko kwenye nini hasa, je ni kwa sababu limetokea kuzimu kama ulivyosema, au ni kwa sababu husababisha wanaume waingie kwenye tamaa zinaa, au ni nini hasa?

  Karibu sana.

 30. ukizungumzia namna ya uchezaji huo “ukataji viuono” asili yake si kanisani haya masuala yamwekwa katika kundi la lust (lechery) kama ni mfuatiliaji mzuri wa masomo mbalimbali yaliyotokana na mafunuo na watumishi mbalimbali na makala za kanisa la awali mfano mwa karne nyingi zilizopita alizoandika pope gregory 1 na orodha za aina za dhambi za mauti 7, dante alighieri katika kitabu cha ushairi “dante inferno”. na unapo mrejea mtume paulo…..utagundua asili yake ni kuzimu na dini za miungu ya wahindi na wakaanani wa kale miungu kama “rati” “qeteshi” ndiyo utakuta masuala ya kukata viuno tangia dunia ya kale….Hamna kupaka rangi hayafai na wala hayakubariki asili yake na historia yake tangia misingi ya kanisa yalikataliwa hivyo lazima yakemewe tu…hamna namna ya kumpa ibilisi shetani kuingiza mguu wake kanisa la leo kwa mlango wa usasa….

 31. Wandugu,

  Ivi hapa tunamjadili Kakobe au tunajadili alichosema Kakobe, mbona tunachanganya madesa?

  Nelson, kabla hujawa mkristo kama ilivyoshauriwa hap juu ( sina hakika kama wewe si mkristo), kukata mauno siyo dhambi. Maana hakuna andiko ambalo limesema kuwa ni dhambi.

  Hilo ni suala ambalo liko kwenye fungu la dhambi za hali( conditional transgression).
  Hizi ni dhambi ambazo hutokea kutokana na matumizi ya kitu au jambo. Ambapo mara nyingi tatizo huwa liko kwenye nia.

  Ukienda Kongo ukaingia kwenye kanisa ukakuta wanamsifu Mungu jwa jinsi sisi hapa Tz tulivyo, lazima utadhani hao watu hawajaokoka, maana kwao kucheza ni kukata mauno, na haiwapi tabu.

  Sisi hapo kukata mauno n = na kuhamasisha mambo ya chumbani, mambo ya mahaba, mambo ya ngono.
  Yaani sisi kukata mauno jirani yake ni mambo ya mapenzi.

  Na hiyo inatokana na matumizi mabaya ya kukata mauno ambao watu wanatoka nao huko misri. Walizoe hivyo kwamba wakiona tu kwenye dansi mwanadada anakata mauno wanaanza kuwakwa tamaa/ kusisimka.

  Hawajawahi kupona huo mtazamo mpaka leo, kwa hiyo kwao kukata mauno kanisani ni najisi mno. Nami siwalaumu.

  Mwingine hula mboga tu na nwingine hula vyote, biblia inasema.

  Ispokuwa sasa hufika sehemu tukaangalia nini yaweza kuwa nia ya mkata mauno. Kila kitu na kiasi.

  Kuna ukataji mauno unaweza kabisa ukaona mazingira yake na nia ya mkataji haiko sawa. Unakuta imelenga si kumtukuza kristo bali kujisismua na kuwasisimua waonao, just kama nia aliyokuwa nayo wakati yuko misri.

  Juzi nimeona clip fulani ya Rose akimsifia H.baba( msanii wa bongo fleva) kwa show nzuri aliyofanya walipokuwa wote kwa mh. Nyarandu.

  Binafsi ilinionesha nia ambayo si salama ndani ya mtumishi huyu. Kwamba amezama sana pia katika kuushabikia mziki huo wa bongo fleva.

  Sijui show ya jamaa huyo ilikuwaje, lakini nnamjua hyo jamaa anakata sana mauno, maana alikuwa mcheza kadogori tangu siku nyingi.

  Sasa jinsi Rose alivyompa saluti kwenye ile clip, mimi niliogopa na kuona kuwa kwa utamaduni wetu kama kanisa hapa Tz., haikuwa sawa.

  It’s just too much!

 32. ndio askofu umesema kweli 2pu lazma injili yakweli ikemewe bila kuangalia uso wa mtu. dah UBARIKIWE SANA KWA KUTOBOA UKWELI UO,WATU HATUWEZ KUPONA PASIPO KUJUA KWELI UBARIKIWE BABA

 33. Bwana Mlinga nadhani badala ya kurudi kuanza kumhukumu Askofu Kakobe ni vyema tuka-appriciate yale aliyoyanena Askofu kuwa yana Ukweli au Laa…!!
  Nafikiri ukianza kubadilisha mwelekeo wa discussion kuwa et na Kakobe nae ana makosa nadhani utakuwa una-disolve hoja kuu bila sababu ya msingi maan swala hapa si kuangalia nani ni msafi zaidi bali kuangalia yasemwayo ni sawa au laa..

  Kwa ufupi naungana na wachangiaji wengi kuwa aliyonena Askofu ni amin na kweli. Ingawaje ukikutana na walokole wa kisasa wata-dilute hii hoja kwa evidence nyepesi ili washinde katika kutetea maovu yao.

  Nashauri tujaribu kuenenda katika mwenendo ulio sawa na wa haki kama biblia inavotaka na sio kwa tafsiri nyepesi tulizonazo kwa kuzibuni buni.

 34. YOTE YATASEMWA LAKINI UKWELI UTABAKI KUWA UKWELI TU HUSUSANI PALE WATU WANAPOAMBIWA UKWELI HUGEUKA NA KUWA WAKALI BINADAMU TULIO WENGI TUNAPENDA KUDANGANYWA NA KUBEMBELEZWA TU! MAOVU SIKU HIZI YANAFANYIKA WATU HATUTAKI KUAMBIWA UKWELI KILA MMOJA AJITATHIMINI NI WAPI ANAELEKEA “MTUMISHI WA MUNGU BISHOP KAKOBE ZIDI KUSONGA MBELE USIANGALIE SURA YA MTU WALA UMBILE LA MTU”

 35. Isaya 30:9
  ” 9 Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana; 10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo; 11 tokeni katika njia, geukeni mtoke katika mapito; mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele yetu”

 36. All that has been said by him is absolute facts…anyone having a spirit of God should agree with what he confidently outspoken..
  its 100% pure what God needs his men to tell others who misbehave according to the need of gospel.

  Lazima tukubali mbingu si rahisi as we think,,mbingu inahitaji kujikana kwelikweli na kuwa mbali na immitation zozote za udunia ktk maisha ya wokovu..

  Mungu akubariki sana Bishop Kakobe and its my prayer that he may strengthen you more and more.

 37. Hahahahaaaaa inachekesha sana siku hizi. Ukitaka kupata sifa na kuwa maarufu wewe chambua madhaifu ya watu wengine tu. Bhaaasi. Utakuwa maarufu kuliko Zito Zuberi Kabwe, kuliko Dr. Slaa, Kuliko David Kafulila, Kuliko Rose Mhando, nk. Yaani wewe chambua tu wengine kwenye jamii. Chambua maovu yao hasa hiyo ya kutikisa viuono au kupokea harambee, basi unakuwa maarufu.

  Angalizo tu ni kwamba uwe makini saana unapokemea wengine na wewe uhakikishe uko sawa sawa siyo mbele ya jamii tu bali hata mbele za Mungu.

  Kila mtumishi anayekemea wengine iwe wanasiasa au watumishi wa Mungu au waimbaji asijisifu kuwa yeye ndiye mwenye Injili isiyoghoshiwa bali anyenyekee kwani dunia hii imezidiwa na watu wasiokuwa wa kweli.

 38. nyakati za leo mimi namfananisha askofu kakobe na nabii mikaya aliyesimama katika kweli alisema kweli bila kuangalia huyu ni mfalme au ni mtu wa heshima au na fedha leo wachungaji mtu akiwa na pesa hata kama anaenda kinyume hawawezi kumkemea lile andiko la kemea kalipia wameliondoa halitumiki tena leo leo waimbaji wengi sio nuru ya ulimwengu wanafanyia biashara neno la Mungu kama huyo dada aliyetajwa mtu anaendenda kwenye shindano la pombe kuimba,waimbaji wengi wanavaa nusu uchi makanisani,mavazi ya kidunia yameingia kanisani wachungaji wako kimya eti hiyo ni hekima si jui wanafata injili gani ikiwa yesu aliona mabaya aliyakemea alipoona watu wanafanya biashara ndani ya hekalu alikemea akawambia imeandikwa nyumba hii itakuwa ni nyumba ya sara leo injili ya wokovu imeachwa si wachungaji,wainjilsti,mitume,wote ni kutafuta fedha kupitia neno la mungu roho ya gehazi aliyefuta fedha ya namani ndio inatenda kazi
  mimi ninampongeza sana kakobe kukemea hata watumishi wenzake leo tuna vingozi mafisadi nchi inaenda mrama lakini hao vingozi wanapokuja katika nyumba za sara kwa ajili ya kutoa michango,ufadhili wa namna yoyote viongozi wanafumbwa midomo mimi nasema mpone kwa jina la Yesu
  KAKOBE MUNGU AKUPE AFYA NA MAISHA MAREFU ENDEREA KUKEMEA DHAMBI UMEBAKI NABII WA KWELI PEKE YAKO

 39. Kakobe mwenyewe kwa hakika anahitaji KUZALIWA MARA YA PILI kutokana na MAFUNDISHO YAKE MENGI YANAYOPINGANA NA BIBLIA.
  Kuzaliwa MARA YA PILI ni KUZALIWA KUTOKA JUU wala si kujiunga na Dhehebu fulani.
  Mtu ALIYEZALIWA MARA YA PILI HAWEZI KAMWE KUKANA MAANDIKO MATAKATIFU (BIBLIA).

 40. Ni vigumu sana kueleweka kwa ulimwengu wa dini uliojiuza kwa dunia na kuyazoelea mambo hayo kuwa ni sehemu ya maisha isiyoathiri utakatifu wetu, na hivyo kuendelea ktk sifa na utukufu wake, tukiamini kwamba hizo ni baraka za Mungu, kama ambavyo Hawa aliuamini kabisa ulaghai wa nyoka!

  Lakini ukweli ni kwamba, aliyoyasema ni Kweli tupu inayopaswa kutazamwa ktk uhalisi wake, kulingana na nafasi zao, hao viongozi walio ktk utumishi, hao walioiruhusu dunia kuingia makanisani, nayo imeingia na miungu lukuki!

  Dunia ilipoingia Kanisani, iliingia na utukufu wa yule mungu wa fahari, Hybris; ikaimwaga fahari ya dunia kanisani, yakazaliwa majivuno, kujikweza, kiburi; vyombo vya muziki wa dansi na beat zake vikahamia kanisani, kwaya za usharika zikawa ni vitu vya ajabu; yakazaliwa “mashindano” ya kwaya yaliyolazimisha kutafutwa kwa attire zenye utukufu, kitani safi kwa wachungaji na mambo mengine mengi ya kifahari; pole pole waumini wakaanza kupendezwa na kujitambulisha na mambo hayo! Kabla hawajaelewa kilicho wafika, kusanyiko lote wakamsujudia yule mungu wa utajiri, mammon, na shauku ya maisha ya kifahari ikazaliwa mioyoni mwao; sasa wanataka kanisa kubwa la kisasa, vyombo vya muziki vya kisasa, wanataka kuwa na redio, tv, mchungaji naye anataka fahari yake, nyumba ya kueleweka na usafiri uliotukuka, yeye ni mtume na nabii nk, nk….!

  Ni nani anayeibeba fahari yote hiyo ya watumishi wote hao? Ni muumini wa kawaida; anaibebaje? Kwa kukamuliwa sadaka!! Tamaa ikiisha kupandikizwa moyoni mwako, inamwagiwa petroli kwa injili za utajirisho, ukiwa mgumu, unachanganyiwa na injili za kupambana na wachawi wanaoiroga kazi yako na biashara yako nk! Ndipo unarudishwa huko Agano la Kale kuoneshwa dhabihu zinazomfanya Mungu akutazame, unatoleshwa hizo ili ziambatane na maombi yako, ndipo mihemuko huchukua nafasi yake na kukuongoza kutoa sadaka za kumwaga!!

  Ili kukupoza, viongozi huwaagiza waimbaji “maarufu” waliotukuka, hao wanaojitegemea, wanawalipa ujira wa ‘utumishi’ wao, ndipo wangeyaburudisha makusanyiko kwa nyimbo safi za injili zilizotungwa ktk beat “walizomnyang’anya” Shetani huko duniani, nao waumini ktk mihemuko waliyomo huzirejea hizo beat walizoziacha huko nyuma na sasa zikihuishwa kwao kama zilivyohuishwa kwa watunzi; ndio hivyo viuno na mastage show yanayoambatana na burudani hizo amabazo mara nyingi huishia na sadaka ya tukio hilo!!!!

  Kuhusu TB Joshua, ndio kama alivyosema, bali kwa kusema kwake kwamba hawahubiri watu “kuzaliwa mara ya pili”, sidhani kama yuko sahihi kimaandiko, kwani mahubiri yoyote yanayomhubiri Kristo humfanya mpagani au mtu wa dini azaliwe mara ya pili, ndiyo kule kuiamini Injili na kubatizwa kunakomfanya mtu huyo aokoke, Mk 16:15-16 ” Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.” Ndiko huko ‘Kuhesabiwa Haki kwa Imani’; huyu ktk hatua hii anakuwa amezaliwa mara ya pili, akiugeukia na Kuuona Ufalme wa Mungu, ndio maana wanaweza kuombewa na wakapokea uponyaji huo, na wakitaka mafanikio ya mali huombewa na wakayapata!

  Hii ndiyo hatua ambayo hata yeye askofu Kakobe anawafikisha waumini wake na kukwama nao hapo wasiweze Kuiingia ktk Ufalme wa Mungu kutokana na mafundisho hafifu wanayoendelea nayo, wakishindwa kuliamini Neno la Mungu kama lilivyowajia, wakiliongeza na hekima yao na hivyo kuifisha ile “Fire Power” iliyohifadhiwa ndani ya Neno hilo ambayo ingewarusha huko anga za juu zinazofikiwa na rocket tu, huko “heavenly places”; bali wao kwa uzito wa Kutokuamini, wanabakia hapo umbali wa ndege za kawaida ambazo huruka umbali wa mawingu juu kidogo tu, na siku ya mawingu na ngurumo na radi huwa haziruki kabisaaaa!

  Mwisho, tuseme kwamba hilo ndilo “Banzi” aliloliona askofu Kakobe, haya mtoeni “Boriti”!!!

  Gbu all!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s