MUZIKI wa KUSIFU na KUABUDU!!

kwaya1

“Sio kila sauti ya mdundo au maneno ni muziki wa kusifu au kuabudu. Muziki ni mjumuisho wa mambo matatu ambayo huwezi kuyatenga: hisia (feelings), maneno (lyrics) na mapigo (melody). Haya yote ni zao la moyo wa mwimbaji na wala sio akili yake.”- (Seth, 2015).

Ukiondoa HISIA kwenye MANENO, huna muziki!
Ukiondoa MANENO kwenye MAPIGO ya muziki, huna muziki!

Kinachofanya tofauti kati ya mziki na mziki ni namna haya mambo matatu yametumika katika wimbo, kisha ukafanyika muziki. Kumbuka, bubujiko la hisia moyoni mwa mwimbaji ndio MSINGI wa muziki wake. Mafanikio ya Mfalme Daudi katika muziki wake (uimbaji wa sifa za Mungu) ilikuwa ni hisia zake mbele za Mungu ambazo alijikuta yanakuja maneno na midundo (vinanda) ambavo hata sasa vinadumu japo ni miaka zaidi ya 2000 imepita.

Mfalme Yehoshefat aliagiza watu waimbe “maneno ya Daudi” na walete “vinanda vya Daudi”; na Daudi naye akasema “Sifa zawapasa wanyofu wa moyo”! Daudi alijua ubora wa sifa za Mungu sio ala za muziki wala maneno ila MOYO wa mwimbaji; na hii ndio inayotofautisha kati ya burudani (sanaa ya muziki wa kidunia) na kusifu na kuabudu.

Frank Philip.

 

Advertisements

3 thoughts on “MUZIKI wa KUSIFU na KUABUDU!!

 1. Nimesahau;

  Maneno/ mashairi bila melodia ya naneno au ya ala za muziki, lakini maneno gayo yakiwa kwenye mapigo huo nao ni muziki.

  Eg; Rap, yenyewe ni mapigo na mashairi/ maneno (lyrics) inakuwa imekamilika, melodia ya ala huja kuinogesha tu na kumwongezea hisia mgani!

 2. Mmh, Frank,

  Najisikia kusema hapana kwa kiasi fulani kikubwa.
  Naona kama kuna kitu zaidi ya hapo ulitaka kukisema, lakini hukukisena kwa hiyo mantika ya ulichosema imejikuta haiko kamili sana.

  Kwanza kuna muziki kwa maana ya sauti za ala, na kuna uimbaji kwa naana ya naneno yaliyo katika melodia.

  Kisha kuna muziki kwa maana ya muungano wa ala za muziki na maneno yaliyo katika melodi( yaani uimbaji)

  Melodia ya muziki bila maneno bado ni muziki, na melodia ya maneno bila muziki bado ni muziki vilevile.

  Kinubi cha Daudi kilimtoa pepo ndani ya sauli, hapo Daudi hata hakuimba.
  Kanisa leo halijui power ya muziki(ala za muziki), ndio maana hawawezi hata kuacha dakika kumi za muziki tu bila maneno. Lakini ala za muziki hutabiri mbele za Mungu.

  Hisia za mtu hazitengenezi muziki, bali zinaupa nguvu muziki wake ya kuweza kuleta matokeo( effects) , hasi au chanya kwake mwenyewe na kwa msikilizaji/ mppkeaji pia.

  Kwa mfano mziki wa Daudi tulichobaki nacho leo ni maneno yake tu(lyrics), hatujui kinubi chake kilitoa melodia gani, au hayo maneno aliyaimba kwa melodia gani. Kwa hiyo haya mapigo yake hatuyajui coz melodia ndiyo inayoamua mapigo yaweje!

  Unyofu wa moyo wa mwimbaji siyo ndio unaotengeneza muziki, bali unatengeneza au unafanya muziki wake imguse au umpendeze Mungu.

  Hata wasio wanyofu wa moyo tunaoba wanapoimba melodia nzuri na kuweka naneno mazuri miziki au nyimbo zao zinawagusa watu, japo zinaweza,au wao wenyewe wanaweza kuwa hawampendezi Mungu kwa mioyo yao.

  Bila hisia muziki/wimbo bado ni wimbo, ila unaweza usiwe wenye kuleta mguso wa ndani.Kwa hiyo hisia ni kitu kinachokupa nguvu wewe mwanamziki/ mwimbaji ya kuweza wewe mwenyewe au msikilizaji kugusika na muziki au wimbo wako.

  Hisia ndio kitu kinachofanya moyo wa mwanamziki au mwimbaji na msikilizaji uyeyushwe na kuguswa na muziki au wimbo huo, ambapo kwa sisi waabudu Mungu aliyehai, mguso au myeyuko huo wa moyo hutengeneza nafasi ya mioyo yetu kuwa tayari kuguswa na Roho mt.

  Na kwa mtu wa dunia myeyuko au mguso huo hupelekea kufanya kitu chochote kulingana na ujumbe ulio kwenye wimbo au vile hisia zake zitamtuma. Eg, kuna watu huvua nguo, kujiua, kuvuta bangi, n.k.

  Huo myeyuko au mguso wa moyo ndio burudani yenyewe. Nyimbo zote za Mungu na za dunia lazima ndani yake kuna burudani. Eg, kulia, kupiga kelele, kucheza, kucheka, n.k

  Burudani hiyo kwa mwamini humpelekea kummiminia mungu moyo wake.

  Ni kweli nia ya mwimbaji/mwanamziki ndicho cha msingi zaidi ktk wimbo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s