Pombe ni hatari katika safari ya kwenda mbinguni!

jesus-beer

1 Timotheo 5:23

Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo Mara kwa Mara.

QN …
A. Mvinyo uliotajwa hapo ni pombe?

B. Kwanini Paul alimwambia Timotheo atumie mvinyo ili apone kwanini hakumwombea kwa Mungu ili amponye?

KUNYWA POMBE NI DHAMBI KWA WATU MUNGU, HAKUNA UTETEZI WOWOTE WA KIBIBLIA. JAMBO LA KWANZA LUGHA YA KISWAHILI HAIKUWA NA MANENO YA KUTOSHA KUTAJA AINA ZOTE ZA DIVAI/MVINYO/VILEO. KTK ULIMWENGU ULE WA ZAMA ZA BIBLIA HUSUSANI UYAHUDI NA UYUNANI,WALIKUWA NA MANENO TOFAUTI KUTOFAUTISHA KINYWAJI HUSIKA TOKA KWENYE ZAO LA ZABIBU. NI KAMA AMBAVYO CRUDE OIL IKIPITIA REFINING PROCESS HUTOA PETROL,DIESEL,KEROSENE ETC VIVYO HIVYO ZAO LA ZABIBU HUTOA DIVAI KILEO,DIVAI PURE JUICE,DIVAI DAWA,ZABIBU KAVU ETC

HAYA NI MAJINA YANAYOTOFAUTISHA AINA HIZO KAMA YANAVYOONEKANA KWENYE HEBREW BIBLE(TANAKH) NA GREEK BIBLE(SEPTUAGINT)
(1)TYROSH PURE JUICE OF CANA (JOHN 2)
(2.) YAYIN THE MOST COMMON WINE IN THE BIBLE
(3)CHEKAR
(4.)MAMCHAK
(5.)GATH

KATIKA HIZI ZIPO AMBAZO NI DAWA ZA KUPAKA VIDONDA TUYATAZAME HAYA MAANDIKO FROM OJB
PROV 31:6
|6| Give strong drink unto him that is ready to perish, and yayin unto those that be of bitter nefesh.

JH 2:10
|10| And the Rosh HaMesibba says to him, Everyone sets out the yayin hatov first, and when they have become drunk, he sets out the inferior; you have kept the yayin hatov until now. |11| This was the reshit

1TIM 5:23
|23| No longer drink only mayim, but use a little yayin because of your stomach and your frequent illnesses.

DIVAI ILIYOKUWA NI JUICE PURE NA HALALI KUNYWEWA BILA SHARTI NI TYROSH,INGAWA YAYIN NDIYO ILIKUWA THE MOST COMMON DIVAI. SASA HATUNA BUDI KUJUI DIVAI WAS A CUSTOMARY ACCEPTED DRINK,INGAWA TUNAKUMBUKA MUNGU ALIWAKINGA WATU KADHAA WALE ALIOWATENGA KWA KUSUDI LAKE,MAKUHANI ETC,BILA SHAKA UNAKUMBUKA MKE WA MANOA AND ALL SUIT-STORIES.

SASA LET ME CLEAR A DOUBT ON TIMOTHY. HUYU MCHUNGAJI TIMOTHEO ALIISHI KTK MJI WA EFESO,THE WATER OF THE CITY YALIKUWA SALTY AND HARD.WENGI HAWAKUWA WANAPENDELEA KUNYWA MAJI AKIWEMO TIMOTHEO, SASA KWA KUWA WATU WALIKAA HATA JUMA ZIMA BILA KUNYWA MAJI,WENGI WALIPATA SHIDA YA MATUMBO KTK MMENG’ENYO (CONSTIPATION),TIMOTHEO SUFFERD THE SAME,SASA PAULO ALIKUWA ANASHAURI “WATER THERAPY” ,AMBAPO WATU WALICHUKUA MAJI NA KUYACHANGANYA NA YAYINI KIDOGO ILI YAWE NA TASTE UWEZE KUNYWA. THE REASON BEHIND WAS NOT ULEVI,INGAWA BADO MSIMAMO WA MWISHO KUHUSU KILEVI NI “USIGUSE,USISHIKE,USIONJE” KOLOSAI 2:21

TUTAKUWA WAJINGA KAMA TUTALAZIMISHA UKRISTO WETU TUUFANANISHE NA ULIMWENGU WA KALE WA UJINGA (MATENDO 17:30) AMBAPO MUNGU HAKUWA AMEJIFUNUA KWA UKAMILIFU,WE ARE LIVING AT THE MAXIMUM REVELATION ERA

Mwl.Conrad Conwell Matimba Komba

4 thoughts on “Pombe ni hatari katika safari ya kwenda mbinguni!

 1. Bwana Yesu asifiwe !

  Ahsante Ndugu David Kwa swali lako.
  Ahsante pia Ndugu Stephen na Akwili kwa mitazamo yenu.

  “Biblia inasema Hivi : Wakolosai 2: 20-21 :
  20 Nyinyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa katika nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti: 21“Msishike hiki,” “Msionje kile,” “Msiguse kile!” 22Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu. 23Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima kwa namna ya ibada wanayojishurutishia, unyenyekevu, na kuutendea mwili kwa ukali; lakini hayafai chochote kuzuia tamaa za mwili.”(BHN Version)

  Kufundisha Injili siyo kuogopesha watu, inaomba kutulia na kuyatafakari maqndiko ili ueleze mambo ya kiroho.

  Hebu fikirini, ni siku gani dhambi iliwai kuwa kitu kinachogusika, ao kinacholiwa, ao kinywaji?
  Dhambi siyo kitu bali ni tendo ao hali. Hence mvinyo, vyakula, wanawake, … siyo dhambi. Lakini ulevi, ulafi, uasherati(uzinzi), … ni dhambi kabisa.

  David, hatuna ruhusa ya kuhukumu kanisa linalotumia mvinyo kwani hiyo mvinyo ndiyo Yesu aliwapa wanafunzi wake. Wasiotumia mvinyo ina maana wanatumia kinywaji kingine. Sasa hapa kinachohitajika ni ile roho iliyo tayari kujiunga na Yesu Kristo katika hilo toleo.
  Mifano Zaidi: “ Dhambi ya Adam na Hawa siyo tunda lakini ni lile tendo la kula tunda lililokatazwa. Dhambi ya Kaini siyo matoleo bali namna alivyotoa. Dhambi ya Anania na Safira siyo hela bali tendo la kudanganya RM.” Ukitazama vizuri kinachoitwa dhambi siyo kitu bali ni tendo litokalo moyoni. Ina maana pompe haiko dhambi, hata Mungu alitolewa pombe. Kukosa kiasi ao kulewa ndo dhambi
  Pia kama pombe ni dhambi, kuna mahala ambapo dhambi inaweza ruhusiwa kawa dawa ? Ao tuseme ukiambiwa kama kupona kwako kunategemea uasherati na mwanamke fulani utakubali?
  Hakuna hata siku moja dhambi itageuka dawa ama mtu aombe ruhusa ndipo aitende. Dhambi ni machukizo, full stop.
  Nadhani kuwahubiri watu kama mvinyo ni dhambi ni kuwapa mafundisho ya kutisha tu bila msinji wowote, ni kutengeneza wakristo wasio na ufahamu, wasiojua dhambi ni nini na kwa nini iepukwe. Sasa ukiwa Mchungaji kwa mfano unao wakristo wenye hofu ya jambo wasilolifahamu, fahamu huna watu wenye akili, una wapumbavu. Inayotakiwa ni ukweli ya kwamba pombe siyo dhambi lakini ni lazma itumiwe kwa uangalifu na kiasi. Kwani kwa kunywa ao kula unaweza kwaza wengine ao unaanguka ndani ya dhambi ya ulafi na ulevi. Sikiliza dhambi ya ulevi na ulafi ni sawasawa kama jinsi pombe na chakula ni sawasawa.
  Mambo kama uongo, kutojizuiza, kasirani, fitina, kusengenya, kuua, kuzini, kuabudu sanamu, ulafi, ulevi ….ni matendo ao hali, wala huwezipata dhambi ambayo ni kitu kinacholiwa, kinywaji ao kinachogusika.
  Ndo maana Yesu akasema hivi:
  “Matayo 15: 16-19:
  16 Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
  17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
  18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
  19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;”

  Mambo mengine kama Samson ao Yoane, kumbukeni kama imeandikwa hata nywele zake Samson zibaki pasipo kunyolewa. Tukidaka hilo, tuseme basi kama kunyolewa ni dhambi?
  Kinachotakiwa ni kusoma Biblia jinsi inavyofaa. Mimi sinywe lakini sijihesabu haki kwa ile, wala siwezi hukumu anaekunywa pasipo kulewa. Lakini nikimuona ndani ya mabaraza ya waovu nitamuonya kwani ile ni dhambi. Hence mnaona kama vitu vingi sana vinazunguuka pombe, ndo maana unapofundisha weka msisitizo kwa kila neno ndipo mhusika ajihuzuru yeye mwenyewe. Kweli akiona kama hataweza kunywa kwa utaratibu yote inayozunguuka lile tendo hatakunywa.

  God bless you !

 2. Tukiangalia kuna tofauti katika mambo mengi na sio moja kati ya ukristu na dini ya uyahudi wao wako chini ya sheria ya torati na sisi tuko chini ya amri ya Kristu, wao wanaisikiliza sheria ya torati, sisi tunamsikiliza Roho mtakatifu, Bwana alisema kuwa, yeye Roho atakuwa akitufunulia mapenzi ya Kristu na Baba, kwa hivyo kile kilichoamriwa na kuhusiwa na mitume kupitia Roho mt. ndicho kilichokuwa mapenzi ya Kristu na Baba pia,
  A) Watu wanasema mtume Paulo aliruhusu pombe kwa kuwa alisema
  “Mtume Paulo alimwambia mtume timotheo: “Tokea sasa usinywe maji tu, lakini tumia mvinyo kidogo……”!?
  1) Alikuwa na maana kuwa mwanae timotheo alikuwa hatumii mvinyo ila alikuwa akinywa maji tu, Na ndio maana alimwambia “Tokea sasa”, ina maana hapo kabla alikuwa hana mazoea hayo, na iwapo angekuwa nayo basi angeambiwa
  “usiache kutumia mvinyo kama kawaida yako”
  2) Hiyo sentensi nzima inaonekana kama anatoa ruhusa, kwa hiyo iwapo tungefanikiwa kuiona barua ya timo kwa Paulo tungeweza kuona swali la Timo, inaelekea Timo alimuuliza mtume Paulo,
  “Je, Baba, ninaruhusiwa kunywa mvinyo kwa sababu nimeugua tumbo na dawa pekee ni mvinyo tu” na ninaamini kutokana na ukosefu wa teknolojia kipindi hicho dawa zilikuwa chache, kwa hivyo timo alikuwa akingojea ruhusa na ndio maana sentensi ile ikawa inaashiria kutoa ruhusa.
  3) Hata hivyo alimruhusu kuitumia kama dawa na sio kujiridhisha nafsi yake kama wafanyavyo walevi.
  4) Na pia vilevile ilikuwa barua ya Mtume Paulo kwa Timo na sio kwa Kanisa
  5) Hakuna asiyejua kuwa hospitalini hutumia baadhi ya madawa ya kulevya kama ganzi kabla ya mtu kufanyiwa operation? Je, wagonjwa wote wanaofanyiwa watakuwa mateja kwa sababu hiyo? Au, je Mungu atawahukumu watu waliofanyiwa operation kwa sababu vilevi ni dhambi? Basi hiyo ndio sawa na kusema Timo alikuwa mlevi au amehukumiwa kwa sababu ya kutumia mvinyo kama dawa ya tumbo.
  B) Watu wanasema mbona katika agano la kale watu walikuwa wakilewa na bado wlikuwa watu wa Mungu!?
  Lazima tutambue kuwa walikuwa chini ya agano la kale, agano la sheria, na wala haikuandikwa katika amri za torati kuwa ukinywa divai umetenda dhambi, japokuwa pia watakatifu wa kale hawakupendezwa nayo sana, ila kwakuwa walikuwa chini ya sheria, Mungu hakuona haja ya kuwafunulia yote mpaka hapo masihi alipokuja.
  C) Watu wanasema mbona Bwana alitenda muujiza wa divai!?
  Bwana aliishi kipindi cha agano la sheria kipindi kile kulikuwa hakuna la kushangaza kama mtu wa Mungu akitumia divai, lakini yeye baada ya kufunuliwa (yaani kutusafisha na damu na kutupa roho mt.) aliwafahamisha watu kweli yote ya kuwa wamepewa Roho mt, na wasimnajisi kwa kitu chochote hata kwa mvinyo, Kwa hivyo akatimilisha agano la kale kwa agano jipya
  Hekalu la Mungu lilipasuka hekaluni baada ya Bwana kufa msalabani hii ikimaanishia – Transition from the old testament to the new, sasa hekalu la Mumgu li ndani yetu, hivyo ni dhambi kuunajisi mwili kwa vile viingiavyo na haviishii katika kuingia tu bali huleta hasara hadi kwa vile vitokavyo yaani mawazo na matendo yaliyoathiriwa uingizwaji wa pombe au kilevi mwilini.
  Sidhani kama kuna sehemu kwenye agano jipya wanaongelea kuhusu kuruhusiwa kwa watumishi wa Mungu kanisani kutumia divai sembuse kuwa walevi labda ile sehemu ya Paulo na Timo na inaonekana kwa zile kauli alizozitumia za kutoa ruhusa, inaashiria haikuiruhusuwa kwenye kanisa.
  Na isitoshe ile ilikuwa barua ya Mtume Paulo kwa Timo na sio kwa Kanisa na wala hakuwaruhusu wapendwa wengine isipokuwa Timo aliyekuwa akiumwa tumbo, si ajabu alivyopona tumbo aliacha kutumia divai.
  Wapendwa si kila ugonjwa utatoka kwa miujiza ya Mungu mbona kuna watumishi wengi wa Mungu wanaugua? Kila kitu ni kwa mapenzi ya Mungu saa nyingine mtumishi huugua na kuacha kusafiri kisha ajali ikatokea huko mbele, je hatoacha kumshukuru Mungu kwa kuugua!?
  Sidhani kama kuna sehemu kwenye agano jipya wanaongelea kuhusu kuruhusiwa kwa watumishi wa Mungu kanisani kutumia kileo chochote isipokuwa ipo sehemu ambapo mtume Petro kupitia Roho analionya kanisa
  1PETRO 4:3
  Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ULEVI, na karamu za ulafi na VILEO, na ibada ya sanamu isiyo halali.
  Wapendwa kinywaji hakiwi pombe mpaka kichanganywe na kileo.(Alcohol)
  Mambo ya mataifa yaliyotajwa kwenye mstari huo yanachafua hekalu la Bwana ndani yetu yaani Kristu,
  Wapendwa hata tukinywa pombe kidogo bila kulewa, tumekunywa kileo, neno la Bwana litasimama kinyume kutushuhudia ukweli.
  Mungu atusaidie wapendwa, wengine wetu tunadhani kuwa Mungu atalinusuru dhehebu fulani kwa kutangua neno lake ndani ya biblia, yeye si kigeugeu.
  Wapendwa tusidhani neema ni njia pana neema ni njia NYEMBAMBA iyendayo uzimani.
  Soma sehemu ya biblia ukijisikia unakwazika basi ujue hilo ndilo linalo kuhusu, ukijisikia unakwazika mpendwa ndio njia yenyewe nyembamba hiyo.
  Wapendwa tunaotumia Pombe au Vileo tutubu Mungu atatusamehe
  Na wale walio katika madhehebu ya watumia vileo watubu na kubatizwa upya kwa maji mengi na kuomba wajazwe Roho wa Kristu. Kisha wote kwa pamoja tuiendee njia nyembamba kwa unyenyekevu.
  Upendo wa Bwana Yesu Kristu uwe nanyi siku zote
  Amen

 3. Bwana yesu asiwe nyote kwanza nisema nimpongeze mtoa mada nami napata nafasi ya kutoa elimu
  kwanza kileo ni dhambi biblia ianasema tusionje wala tusiguse kwanza mtoa madaametoa maandiko mengi nami nitakuongea kama ifutavyo:-
  soma habakuki 2;15 kama Mungu anamwambia anaye mpa mwingine kileo vipi kwa anaye kunywa itakuwaje biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kusosa maalifa kama mtoa mada alivyo sema zabibu ilikuwa inaweza kutoa aina nyingi za vinywaji sawa na zabibu zinazo limwa dodoma zinatengeza orange,pamaja na dodoma wine ambayo ni kilevi napenda kukuambia tangu mwanzo sio mpango wa mungu watu wapotee kwa kunywa kileo
  ndio maana alikuwa amewachagua kwa ajili ya utumishi aliwaelekeza wajiepushe na kileo kama mke wa manoa wakati wa kumzaa samsoni soma (waamuzi 13;-4) soma pia waefeso 5:18
  alicho sema paulo kumshauli timotheo ilikuwa ni kutumia dawa kwa ajili ya udhaifu wa tumbo ukitaka kujua divai ilitumika kama dawa ludi kwa mtu aliye angukia mikononi mwa wanyanganyi njisi ilivyo muhudumia yule msamalia kwa kumpaka divai katika majeleha yake soma (luka 10:34) sasa leo unakutana na watu wamekufa kiloho wakitetea kunywa pombe mnasoma bibli gani nyinyi biblia ina kataa chachu kwetu utakuta mtu anasema yesu alitengeneza pombe kwenye halusi ya kana pale kwenye halusi ya kana ile ilikuwa juice njema kwani Mungu si kigegeu wa kubadilika sasa nije kuhusu ushirika mtakatifu kwanza hairusiwi kushiriki chakura cha bwana kama hujazaliwa mara ya pili(kwa maana ya kuokoka maana biblia inasema fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu ile divai inayo paswa kutumika inatakiwa isiwe na chachu yoyote au kilevi kwani inafananishwa na damu ya yesu soma ( 1wakolinto 11:-25…30) ndugu kamahuja okoka okoka kwanitunaishi nyakati za mwisho Yesu yuko mlangoni tayali kuja kulichukua kanisa lake toka hapa wanapotumia kilevi kushiriki ushirika mtakatifu
  balikiwa nyote

 4. Bwana Yesu asifiwe.
  Kanisa ninaloasali mimi tunashiriki meza ya Bwana kwa Mvinyo ambao una kilevi asilimia kubwa tu sana,
  Je ; Hii ni sawa au sio sawa
  Na kama sio sawa kwa nini bado tunaendelea kunyweshwa pombe kanisini.
  Naomba majibu ya msingi yanayoambatana na maandiko kwa faida yangu na wakristo wengi ambao nao hushiriki meza ya Bwana kama hii

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s