Askofu Gwajima kufikishwa kwenye vyombo vya sheria!!

ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za  kashfa na matusi.

Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.
Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria. ichukue mkondo wake.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Video iliyoleta matatizo
Advertisements

42 thoughts on “Askofu Gwajima kufikishwa kwenye vyombo vya sheria!!

 1. Kazi kubwa ya wachungaji ni kuionya serikali inapoonekana kukosea na kama tukikaa na dhana ya eti kusema ni siasa basi biblia haijajamaza inasema katika ezekia kuwa ukiona mwenye dhambi akifanya dhambi na usipomuonya basi uovu wake utakuwa juu ya vicha vyao sisi wachungaji hatukubari uovu huo uwe juu yetu na ndio maana tunaionya serikali yetu na ndicho nalichofanya mchungaji gwajima

 2. Kamanda wa Yesu usiogope simama imara na yesu yupo mbele yako kado yako unalindwa na Yesu hakuna kitu cha thamani chochote kisichokuwa na gharama na wala hakuna vita isiyo na kamanda kamanda wetu mkuu ni Yesu wewe gwajima umesimama upande wa Yesu kwa niaba ya Tanzania

 3. Poor Pendael,

  You said ”SEED OF DISCREPANCY”, what is it?

  Watu kama wewe nawapenda mno; wakali, wenye jazba, wasiopenda kukosolewa, wenye kujifanya wanajua kila kitu, lakini ndani ya maandishi yao kuna mapungufu mengi ya kimantiki na kifikra. Hujui hata kuunganisha logic za mambo mengi unayoandika, unalipuka tu ukiwa umefura kwa jazba.

  Naona umejiapiza kutonijibu, hahaaa, You are just a simple coward Pendael!

  Kama wewe unajiamini kuwa una Roho wa Mungu kwa nini unamkimbia mtu mwenye roho unayoiita ya Ibilisi? Kwa mujibu wa maandiko wewe mwenye Roho wa Mungu hutakiwi kuwa kuwa na roho ya uoga.

  Well, hata ukiacha kujibu, huna majibu yoyote ya maana ya kunisaidia mimi na msomaji mwingine mwenye akili timamu. Na sikuandikii ili ujibu, ila naandika kupinga pumba ambazo unataka kutulisha.

  Kuna knowledge utakujaga kuipata zamani sana, na moyoni mwako utakiri kwamba nilichowahi kukwambia ni cha kweli.

  Ni kujidanganya sana kudhani kuwa Neno la Mngu = Biblia. Tafuta kwenye maandiko ni wapi utalipata hilo jambo. Kwenye biblia kuna mpaka anwani ya aliyeprint, kuna dibaji, kuna yaliyomo, na zingine zina kamusi n.k, kwako Pendael hayo yote ni maneno ya Mungu eh?!!

  Go back to school!

 4. SUNGURA, Pia umesema utabembea na mimi mpaka ujinga unitoke, kaa ukijua kuwa UNAVYOFIKIRI kwamba eti wewe unaweza Kuni fundisha, kwangu mimi hayo unayoita Mafundisho ni MATAPISHI na anayekula MATAPISHI ni MBWA.Hivyo, kuanzia sasa na kuendelea,wakati wowote na mahali popote iwe hapa SG ama kwingineko SITAJIBIZANA NA WEWE KAMWE, KWANI KWANGU MIMI KINACHOKUONGOZA NI roho INAYOPINGANA Na NENO LA MUNGU, na naelewa kwamba YOU ARE ORDAINED FOR THAT PURPOSE.Ndio Maana kuonesha HUNA HATA CHEMBE YA UKRISTO NDANI YAKO, bila woga Ulidiriki kusema katika Mada zilizopita eti BIBLIA INA MANENO YA MUNGU NA YA WANADAMU, na hii imesababishwa na Mbegu (SEED OF DISCREPANCY) iliyo ndani yako.Kama ulivyosema utaendelea kubembea na mimi, endelea wala usichoke kwani Umejiandaa kwa hilo na upo kwa ajili hiyo kwani Kulingana na MITHALI 27:22 “HATA UKITWANGA KWA MCHI KINUNI PAMOJA NA NGANO, UPUMBAVU WAKO HAUTAKUTOKA”.

 5. SUNGURA, Kuniita Mpumbavu hainitishi hata kidogo.Nilisema na ninaendelea kusema bila woga, wewe na rafiki yako Oguda YOU ARE JUST PRESSUMING TO BE CHRISTIANS, na kwa kuwa mnatetea UOVU bila kuogopa vitisho vyako hakika Mna ‘roho wa Ibilisi’.

 6. Pendael,

  Nimeshakwambia kuwa nitabembea na wewe mpaka ujinga utoke kwa kichwa chako. Maana unajiona uko smart sana kifikra lakini umejaa ukutokuelewa wa kutosha tu, na kwa sababu hasira hukaa kifuani pa mpumbavu, basi umekubali zikae kifuani mwako kiasi kwamba huoni hata kilichosemwa.

  Kabla ya kusema sana, jaribu tu kwa huo ufahamu wako ambao kwa kutaka kwako umeamua uwe butu, fikiri kama askofu Pengo angeambiwa kuwa amejaa mapepo ya usaliti kama lenyewe lingekuwa si tusi.

  Hakuna mahali ambapo Pengo kaambiwa kuwa amevaa pampers/ nepi, ni wewe tu Pendaele ambaye umeamua uwe na akili ndogo umesikia hayo maneno katika yale aliyosema Gwajima.

  Unaongea kwa opinion ipi, ulitaka Pengo achaguliwe maneno ya heshima ya kumkemea nayo siyo, vipi basi mfalme kuitwa mbweha lilikuwa neno la heshima? Au kwa sababu lilisemwa na Yesu na liko kwenye maandiko unakosa namna ya kuli- criticize, lakini lingekuwa limesemwa na Kakobe ungetokwa povu mdomoni ukilipinga.

  Ati unasema hayo ni maneno ya kumwambia baba au mamako!! Kwani Gwajima alikuwa na anamwambia baba au mama yake? Sidhani kama fikra yako wewe iko sawa.

  Mwisho, kama wewe ni mkristo na una ufahamu sahihi wa neno la Mungu, be very careful na maneno kama haya, nakunukuu; ”(na huyo mliye naye ni roho wa Ibilisi)”- HAPO ULIMAANISHA ROHO NILITONAYO MIMI NA OGUDA NI YA IBILISI.

  Nafikiri umenielewa maana ya kukwambia kwangu kuwa ‘be careful’!!

  Jitahidi kujibu hoja na si kunijibu mimi au yeyote unayejibu hoja zake.

 7. Lwembe naendelea..

  Najua wewe pia ni miongoni mwa waumini ambao wameambiwa na maasjofu wapige kura ya ‘hapana’ kwa katiba pendekezwa, vipi umeshamuuliza askofu wako kwa nini anakuamuru kufanya hivyo?

  Lakini pia, je, ikitokea mahakama ya kardhi imeanzishwa na ikaleta madhara kwa wakristo, kisha ikabidi ipigwe mbiu ya wakristo wote kufunga na kuomba kumlilia Mungu juu ya madhara hayo ya mahakam ya kardhi, vipi nawe utaitikia hiyo mbiu?

  Kuna na hili nalo umenishangaza kweli uwezo wa kufikiri Lwembe, nakunukuu;

  ”Kwa mfano labda kumetokea na chokochoko ambayo inailazimu nchi kuingia vitani, Amiri Jeshi ameyaamuru majeshi kupigana na adui. Lakini baraza la maaskofu halijaridhika na jambo hilo, ndipo nao wanatoa tamko la kuwaamuru askari wote walio wakristo waweke silaha chini, nao kwa utiifu kwa viongozi wao wa kiroho wakiamini kwamba hilo ni Agizo la Mungu, wanaweka silaha chini!!!”

  Lwembe kwa akili yako kabisa, unaona kuwa huu ni mfano anuai wa kuulinganisha na suala la mahakama ya kardhi, au unadhani kuwa maaskofu ni ‘bogus’ kabisa kiasi hicho, na wewe una akili nyingi sana kuliko wao kiasi hicho?!!!

  Ndio hapo mimi hufika nikau-question sana uwezo wako wa kufikiri hasa kwenye issue hizi zinazohitaji akili pana kuzichambua. Sijui kama wewe ni mzembe au ndio uwezo wako.

  Na umemalizia comment yako na swali la kitoto mno, huku likijichanganya na maelezo yako yaliyo ndani ya paragrafu hiyohiyo, kwa kushindwa kwako kuielewa formation ya utumishi wetu kwa Mungu leo( japo siamini kama kweli huiekewi au ni kukosa tu umakini), huku ukifikiri kama mtu wa agano la kale.

  Ona ulivyosema;
  “Hakuna mkristo anayekatazwa kugombea uongozi ktk siasa, hili liko wazi kabisa kuliko mnavyojitahidi kuliweka. Bali nafasi yoyote ya uongozi ina mipaka yake; ni mfalme yupi ambaye alikuwa kuhani?”

  Sasa unaponiuliza kuwa ni mfalme yupi ambaye alikuwa ni kuhani, lakini hapohapo umeshasema kuwa hakuna mkristo anayekatazwa kugombea uongozi ktk siasa, nakuona ni mtu uliyepotea njia na kufika usikokujua.

  Jibu ni jepesi sana Lwembe;

  Kila mkristo leo ni kuhani, maana pazia lilipasuka na hivyo kutufanya wote tuweze kupaingia patakatifu ambapo palikuwa panaingiwa na makuhani tu.Kwa hiyo unaposema kuwa wakristo wanaruhusiwa kugombea nafasi za uongozi ktk siasa, maana yake unasema kwamba makuhani wanaruhusiwa kuwa wafalme.

  Ndio maana niliwahi kukwambia kuwa hao wenye haki ambao biblia inasema wakitawala watu wote hufurahi, wanapatikana kanisani, ni wakristo – ni makuhani!

  Na hapo ndipo utakapoiona habari ya kanisa kuwa ndani ya serikali na serikali kuwa ndani ya kanisa.

  Ndo hivyo Lwembe!!

 8. Lwembe,

  Kuna jambo moja huwa siachi kukushangaa, labda mpaka siku nitakapojua sababu ya jambo hilo kuwa hivyo ndo nitaacha kukushangaa.
  Unavyojua kupangilia maneno, unavyojua matumizi ya lugha, na unavyoonekana kuwa afahamu wako uko vizuri, ni tofauti kabisa na uwezo wako wa kujengo hoja yenye mashiko kwenye mada ambazo ambazo huhitaji fikra ya kina
  .
  Je ni kwa sababu nimekuweka katika level ya juu sana kiufahamu hivyo nikatarajia matokeo makubwa sana, hivyo yakija tofauti najikuta napigwa butwaa? Bila shaka inawezekana ni hivyo, hasa kutokana na jinsi ulivyomzuri kwenye lugha.

  Umeanza kwa kusema kuwa shida yetu ni pale tunaposhindwa kuuona mstari mwembaba unaovigawa neno la Mungu na siasa, na hivyo tunaishia kuvichanganya. Nami najiuliza ni wapi nimechanganya neno la Mungu na siasa na kuviona kuwa ni kitu kimoja au vinafanana?

  Kuna mambo ya ajabu kwelikweli umeongea kwenye hiyo comment yako, nakunukuu tena:

  ”Mchanganyiko wa Neno la Mungu na Siasa unatengeneza “Nguvu” – a power block, ambayo ni negotiating tool. “Nguvu” hii hutumika ktk ‘KULINDA’ maslahi ya wakristo pale yeyote au serikali inapoonekana kuyakanyaga – ki Biblia nguvu hii hutafsirika kama “mnyama” (beast)!!!”
  Kwanza, wazo hili umelitoa kwenye hoja ya uongo ambayo mimi binafsi sijaisema (yaani kuchanganya neno la Mungu na siasa), lakini pia umekuja kutafsiri kutoa tafsiri ambayo siioni kwenye maandiko Lwembe. Yaani siona popote biblia inasema kuwa nguvu inayotokana na kuchanganya neno la Mungu na siasa inaitwa mnyama au ‘beast’ kama ulivyoiita. Labda nithibitishie hilo Lwembe.

  ”Mwisho wa siku wakristo wataishia kuutegemea ‘Umoja’ huo ktk ulinzi wa maslahi yao badala ya huyo aliyewakomboa kwa kuwafia”

  Unasema kuwa umoja wa wakristo unakuja kuwafanyawakristo wautegemee umoja huo kiulinzi badala ya aliyewafilia.
  Mimi huwa napenda kutumia maandiko kwa haki.
  Lwembe Kristo alisisitiza tuwe na umoja, je hakujua kuwa umoja huo utakuja kutusababisha tuutegemee kiulinzi badala ya kumtegemea yeye, kama mchungaji Lwembe anavyosema leo?

  Naendelea kukunukuu:
  “Ni ninyi tu akina Sungura msiofahamu kwamba askofu anahitaji msamaha; Mdo 23:5 “Paulo akasema, Sikujua, ndugu zangu, ya kuwa yeye ni Kuhani Mkuu; maana imeandikwa, Usimnenee mabaya mkuu wa watu wako.”!!!
  Kwa kutumia hili andiko unamaanisha kuwa unamkubali Pengo kuwa ni kuhani mkuu. Nashangaa leo unamuona hivyo Pengo, lakini huko nyuma hata wewe ulishawahi kumnena vibaya. Na wewe unahitaji msamaha. Lakini pia unasimamisha utetezi wa hivi wa kumtetea Pngo, just kwa sababu leo uko kinyume na Gwajima, hivyo ku unatafuta hoja ya kukuunga mkono. Lwembe huo ni unafiki.

  Lakini sijui kama hiyo habari ya Mdo 23:5 umeisoma vizuri ukaielewa, maana utagundua kuwa Paul naye kama alivyofanya Gwajima, alimtukana Anania ambaye alikuwa kuhani verse 4. Alimwita “ukuta uliopakwa chokaa”, Gwajima yeye kamwita Pengo kuwa yuko kama mtoto aliyefungwa nepi, sasa tofauti ni nini?

  Nitaendelea….

 9. Sungura,

  “Haki yenu isipoizidi ya Waswahili wa mitaani…!!!”

  Shida kubwa mliyonayo ni pale mnaposhindwa kuuona mstari mwembamba unaovigawa, Neno la Mungu na Siasa, na hivyo mnaishia kuvichanganya, mkidhani kwa Mchanganyiko huo you are doing yourselves a great favor; kumbe maskini, unknowingly, you are sealing your fate! Hilo Jukwaa la Kikristo, good as it looks, and the need for it, is the first step in the deviation from the Faith; ni sawa kabisa na askofu alipoagiza aletewe bastola yake ili ajilinde, trusting in a gun!

  Ibilisi kwa werevu mkubwa, pole pole analiondoa kanisa kutoka ktk kumtegemea Mungu, akilipa maarifa ya jinsi ya kuwa na nguvu za kujitegemea lenyewe; ndio huo Umoja! Mchanganyiko wa Neno la Mungu na Siasa unatengeneza “Nguvu” – a power block, ambayo ni negotiating tool. “Nguvu” hii hutumika ktk ‘KULINDA’ maslahi ya wakristo pale yeyote au serikali inapoonekana kuyakanyaga – ki Biblia nguvu hii hutafsirika kama “mnyama” (beast)!!!

  Mwisho wa siku wakristo wataishia kuutegemea ‘Umoja’ huo ktk ulinzi wa maslahi yao badala ya huyo aliyewakomboa kwa kuwafia; ni nani kati ya maaskofu hao anayeweza kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine? Huyo hapo Gwajima, mbona kabaki peke yake akipigana kuikoa nafsi yake, wako wapi hao aliokuwa akiwatetea? Nimewaona walala hoi tu waliokusanywa huko vituo vya polisi, wanalalama “Mbona askofu Pengo amemsamehe, kwa nini serikali iendelee kumshikilia?” Kumbe wanajua kwamba Pengo amemsamehe! Ni ninyi tu akina Sungura msiofahamu kwamba askofu anahitaji msamaha; Mdo 23:5 “Paulo akasema, Sikujua, ndugu zangu, ya kuwa yeye ni Kuhani Mkuu; maana imeandikwa, Usimnenee mabaya mkuu wa watu wako.”!!!

  Basi kanisa linapofikishwa ktk hali hiyo ya kuutegemea ‘Umoja’ wao, ndipo lile neno la “Amelaaniwa yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake, Na moyoni mwake amemwacha Bwana” ktk Yer 17:5 linapowatimilia!!!

  Hivyo, ni vizuri mkafahamu kwamba kitendo walichokifanya maaskofu kupitia Umoja huo ni cha hatari sana kwa usalama na umoja wa nchi kama taifa. Tafsiri na udhihirisho wa Umoja huo ndio hiyo “Nguvu” kupitia mamlaka waliyojitwalia ya kuzitawala nafsi za waumini wao ktk kificho cha Neno la Mungu, wakiwaagiza wakristo WOTE, from all walks of life – pamoja na Pinda, wakajiandishe, kisha wapige kura ya HAPANA!

  Iwapo maaskofu hao wataachwa wajitwalie mamlaka juu ya waumini wao, basi tafsiri rahisi ya jambo hilo ni kwamba mamlaka mpya itakuwa imezaliwa ktk utawala wa nchi

  Kwa mfano labda kumetokea na chokochoko ambayo inailazimu nchi kuingia vitani, Amiri Jeshi ameyaamuru majeshi kupigana na adui. Lakini baraza la maaskofu halijaridhika na jambo hilo, ndipo nao wanatoa tamko la kuwaamuru askari wote walio wakristo waweke silaha chini, nao kwa utiifu kwa viongozi wao wa kiroho wakiamini kwamba hilo ni Agizo la Mungu, wanaweka silaha chini!!!

  Kwahiyo Pengo being more spiritual kuliko hilo kundi la maaskofu, he became a Mikaya against the 400! Tazama, Pengo ameirejea nafasi ya uaskofu kulingana na Biblia kwamba, hao maaskofu hawana mamlaka hayo waliyojitwalia, na wote wanaompinga ktk kauli yake hiyo wana argue kutoka ktk udhaifu wa imani, maana tumaini lao wameliweka ktk Umoja wao, hiyo Beast Power!

  Jitahidini kuyapanua mawazo yenu kwa kuongozwa na Neno la Mungu, ile reflection, na si siasa za dini!! Hakuna mkristo anayekatazwa kugombea uongozi ktk siasa, hili liko wazi kabisa kuliko mnavyojitahidi kuliweka. Bali nafasi yoyote ya uongozi ina mipaka yake; ni mfalme yupi ambaye alikuwa kuhani?

  Gbu!

 10. Oguda,

  “Haki yenu isipoizidi ya Waswahili wa mitaani…!!!”

  Inashangaza saana jinsi mnavyojitahidi ku spiritualize a non-spiritual issue simply because muhusika, kwa standard yenu ni VERY SPIRITUAL!!! And in the course, mnaamini kwamba hiyo harangue was a great spiritual sermon!!!

  Hebu nipeni jibu kwa hili swali wanalouliza Waswahili: Wanasema, askofu ktk “mahubiri” yake alimtuma malaika aende akampige askofu Pengo; ila sasa wanashindwa kuelewa, what really got him so scared till he ordered a gun for his self defense, counting no more on his beloved angels??? Malaika walimkimbia???

  Na kuhusu utovu wa adabu, hata ndg za askofu wa kimwili wameliona hilo kosa alilolifanya; how can you be soooo blind!???

  Halafu kuhusu hilo jambo la kwamba sisi ni “wasengenyaji” mimi nadhani kwa wewe kusema kwamba you are sorry kutuambia hivyo, in itself is a high level of hypocrisy!! Look at it yourself, Kakobe anaongelea mwenendo wa mkristo in the sight of God – Wokovu; na Gwajima anaongelea makubaliano ya maaskofu ktk kikao chao cha kujadili katiba pendekezi, jambo ambalo halina uhusiano wowote ule na wokovu; kuyaleta kwako mambo haya mawili tofauti ktk ulinganishi ni hila ya kumuingiza na askofu Kakobe ktk hali potofu ya askofu Gwajima, ili umsafishe mchafu kwa kumchafua msafi; which is very low!

  Na ndilo jambo linalowafanya mulione neno “pampers” ktk mantiki ya jinsi lilivyotumika kwamba its a cool ‘Biblical word’ in its relevancy, which befittingly makes you part of that savage joke! Hebu wazia hili kwamba eti unatutaka tumfuate askofu tukamueleze haya tuliyoyaandika, mimi nilidhani wewe ndio ungemfuata askofu huyo na kumueleza kwamba asimsimange Pengo, kuliko kutuambia sisi ambao tumeyaweka wazi hayo tuliyoyasema hapa mtandaoni! Kwani huu mtandao unahitaji password, hata yaliyomo humu yawe ni masengenyo? Msitumie maneno kwa hila!!

  Gwajima ndiye aliyemsengenya Pengo huko kanisani kwake; otherwise SG iko wazi sana, kama maaskofu hawapiti huku, ni kutokana ya hofu yao ya kukutana na Kweli, hata hivyo, wako walio jasiri wengi tu huwa ninawasoma mafundisho yao!!! Ukimya wa hao wengine unasikitisha sana, maana nilitegemea wawatangazie waumini wao kuhusu mtandao huu, uwe sehemu ya kuwakomaza kwa changamoto zinazopatikana humu, kama hiyo ya kukalishwa juani huku “Yesu” akiruka na chopper, na si kujitahidi kuifumba midomo inayoyaweka wazi hayo ili ukandamizaji wa kiroho uendelee!

  Mimi ninaamini kwamba SG is not a back street thing kama unavyotaka kui potray. Ninaweza kukuhakikishia kwamba watu wanaotembelea SG kwa kule kutembelea kwao sight hii, they got wiser in spiritual matters 100 times over, kuliko hao wanaoshinda makanisani wakihubiriwa na kufundishwa na watumishi wasiotumwa na Mungu; nasema wasiotumwa kwa sababu Kanisa linaongozwa na Roho ya Kristo, na si kwa akili za mtu au hekima ya kibinadamu ambayo leo hii manifestation yake ndio hayo makubaliano ya maaskofu ambayo mnayalazimisha kuwa neno la Mungu out of ignorance!!

  Kwa bahati mbaya, unajichanganya sana pia, kwani kuwa na audience ya watu milioni 2 au zaidi, does that make you more spiritual kuliko mwenye watu wawili au watatu? (kwanza utadaiwa roho za watu milioni 2!); Au kuanzisha makanisa kama mradi wako, halafu ukawaambia hao uliowakusanya jinsi ulivyopata shida kwa “kazi hiyo ya Mungu”, nao wakakuona ktk jinsi hiyo; does that count in the sight of God? Usijidanganye, malipo yako ulikwisha kulipwa na hao uliowakusanya, Mungu alisema atawaambia “Ondokeni siwajui” impersonators!!!

  Kwahiyo ni vizuri ukafahamu kwamba kazi ya Mungu hufanywa na watu waliotumwa na Mungu mwenyewe, naye huwapa Roho yake iwaongoze kama alivyowafanyia mitume; Mungu hamtumi yeyote yule bila kumpa Roho wake, hivyo hatutegemei mafundisho tofauti tofauti juu ya jambo moja, a sign of confusion. Ndio maana nilikuambia kama si Injili kama ilivyohubiriwa na mitume, yeyote anayejishughulisha na hiyo ninaamini they are wasting their time, labda kama they do it for the money, then at least they got themselves a bargain!

  Pia jambo la kunitaka niende kwenye tv au niandike magazetini, fahamu kwamba kila jambo lina wakati wake, ukiyakurupukia hayo utaishia kurusha mambo ya hovyo kama hiyo clip mnayoisifia; which is a disgrace to the true Christian community kasoro wachache ninyi ambao vision yenu imekuwa blurred!

  Unajua, no matter how hard you try, how manipulative you can be, theres only one avenue where u will ever get to be: what u chose to identify with! And as long as u people have chosen to identify with that harangue, fitting it on Christ, and trying to get every one to believe so, I’m afraid, u are walking the fools’ alleyway, having followed an impersonating spirit!!

  Gbu my brother!

 11. Oguda, mimi ninajua wewe na Shabiki mwenzako Sungura mmejaa Mapepo ya Ushabiki.YOU ARE JUST PRESSUMING TO BE CHRISTIANS.Kuitana MAN of God ni kujipachika cheo ambacho Ibilisi mwenyewe hufanya hivyo. Liko wazi kwamba hata hamjafunzwa adabu,na huyo mliye naye ni roho wa Ibilisi.Hivi kama una Akili timamu unaweza kumwambia Baba/Mama yako kuwa ‘AMEVAA PAMPERS/NEPI?Wewe na Sungura mkiambiwa MMEVAA NEPI/PAMPERS mtajisikia murua?Hebu nendeni hapo Polisi alipopekekwa Gwajima, mkawaambie Polisi kuwa aliyoyasema Gwajima ni maneno mazuri kama HAMJAKIONA CHA MOTO.Umetumia neno Mbweha alilotumia YESU kuhalalisha Upagani.Unaposema ‘ninakasirikaga’ ni mtazamo wa fikra potofu ulionao mawazoni mwako na pia usifikiri kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kufurahia/kutetea Uchafu kama huu unaoitwa ‘mahubiri’ labda kichaa ndiye atakayetetea!

 12. Dear man of God Sungura , I really appreciate these. ” ukimkosoaga, huwa MTU was Mungu Pendaeli, aliyependwa sana na Mkombozi wa Roho na nafsi, hukasirikaga”. Anyway, mbele HP atuambie km neno , mbweha, je, kwa mtazamo wake huo, Leo si ndo Gwajima angeonekana ni shetani KBS?
  EJ O.

 13. Pendael,

  Seriously kabisa unataka uonyeshwe neno “pampers” kwenye biblia ili iwe vipi yaani?

  Ivi umejaribu kufikiria ni lini matumizi ya pampers yalianza, na huko nyuma kulikuwa na neno nepi, ambalo nalo kabla ya hapo bila shaka kulikuwa na maneno mengine yenye kumaanisha kila ambacho pampers humaanisha!

  Ni sawa na mtu kukwambia uonyeshe neno ‘simu’ kwenye biblia. Haliwezi kuwemo kwa sababu hicho kitu wakati biblia inakoma kuandikwa kilikuwa hakijavumbuliwa.

  Haya sasa, neno pampers kwenye biblia halimo,so what is the point there Pendael, unataka kusemaje kutokana na kutokuwemo neno hilo kwenye biblia?

  Au unataka tuwe tunaongea tu misamiati ambayo iko kwenye biblia ndugu? hebu anza wewe tuone kama utaweza.

  Vipi kama angeitwa mbweha au mbwa, yenyewe yangekuwa si matusi kwa sababu yanapatikana kwenye biblia eh?

  Ivi wewe hujui kuwa lugha huzaliwa, hukua na hufa, lakini mawasiliano huendelea kwa kutumia misamiati mingine lakini kilichokusudiwa kuwasilishwa hubaki kilekile?

  Kwa mfano, unataka tuendelee kuita bwawa kuwa ni birika just kwa kuwa neno birika linapatikana kwenye biblia, japo maana iliyokusudiwa kwenye maandiko ni tofauti kabisa na maana ya neno birika leo.

  Pendael, nikikukosoa unakasirika lakini, jaribu kuzingatia mantiki na usahihi wa vitu unavyovisema!

 14. “Dear Pendaeli, you are too combatant, very astonishing!! However, you seems to be sailing in the same quotes”. Acha hasira ndg mpendwa, nikisoma ninaona km povu zinakutoka”.

  Issue si Gwajima, hv been here at SG for many yrs, i think before you were in. Please, we hv been, and thats what i was aiming at, morality, once we are called christians we are obliged to.

  Come again with another lesson, a constructive one.
  Thanx, dear man of God.

  HEBU SOMA HII KAMA ITAKUSAIDIA;
  “3 Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
  4 amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya;5 na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
  ****YOU CAN’T CHANGE YOUR DESTINY.****

 15. Kinacho nitatiza na kujiuliza wapendwa! Kuweni macho, nimeshtuka sana kwa kujua hili. Aliyeenda kumshtaki mchungaji Gwajima polisi siyo kardinali pengo, ila ni muumini wa dini ya kiislamu anayeitwa Abdalah Aboubakar. Ameenda polisi na kufungua mashtaka dhidi ya Gwajima kwa kumtukana pengo. Nasikia nyuma yake huyu jamaa kuna kundi la waislamu. Hii imenifanya nianze kulitazama hili jambo lote kwa macho ya tofauti sana.

 16. edmund john oguda,
  Naona unajitahudi kuogelea kwenye MATOPE ya mafundisho yaliyoko kwenye uafahamu wako.
  Unasema
  ” Kwanza kbs, ni declare interest, mimi si mshirika wa Ufufuo na Uzima, na sijawahi kuwa, na kwamba, ht msingi wa huduma ile bado nipo kwenye utafiti wangu, maana, NENO ninalijua kwa sehemu, ninaomba kwa sehemu, ufahamu ninao, upambanuaji ninao pia, naam, hiki ni kipindi cha R/Mtakatifu.”
  POLE SANA KWA KUJISIFU na kujificha ndani ya kasha la UFUFO NA UZIMA!!
  Pia unaendelea kusema;
  ” Najua mtaendelea kukataa, lkn mufanyacho nyie ni masengenyo tu, you dare go public on the TV, or on the News papers, huku SG, ni family ndogo sana ya watu walewale siku zote, na hao kwakuwa, hawana uanachama humu, hawana muda wa kufuatilia haya majungu/masengenyo yetu humu SG, badala yake wanazunguka wakijitaabisha kwa ajili ya injili na maendeleo yenu km wakristo. Yaani, call a spade a spade, inashangaza bros!!,”
  Hakuna MKRISTO mahali popote anaweza kukubaliana na “filth” unayojaribu kuietetea kisa GWAJIMA ni mtumishi wa MUNGU.
  WAKRISTO hawali matapishi bali hula FRESH MEAL “NENO LISILOGOSHIWA”,
  ILA UKILIACHA NENO LA MUNGU MATAPISHI NI CHAKULA CHENYE AFYA KWAKO.
  Nafikiri hata hujui hata KUSUDI LA SG, ndio maana unapayuka kwa MAELEZO YASIYO NA MAANA. Tena UNAKIRI WEWE MWENYEWE NI MSENGENYAJI.Bila shaka wewe hufai kuwa hapa SG kwa sababu hapa si mahali pa wasengenyaji.
  Unatuambia tunafanya MASENGENYO kisa Kipenzi chako anakosolewa, hii inaonesha kuwa hata maaana ya MASENGENYO hujui.
  Pia kama umezoea Kuonekana kwenye TV, kuandika makala kwenye Magazeti au Kuhubiri Siasa mbele za watu, endelea kuifanya hivyo wala siwezi kufanyia kazi USHAURI wako uliojaa UPOTOFU.Kama unataka mijadala hii usomwe na watu wengi unaweza kwenda KUCHAPISHA KATIKA magazeti yanayosomwa na watu wengi.
  Vilevile umeendelea kujisifu kwa kusema ” ……lakn, ninapenda kukuambia ya kuwa, baada ya muda wa miezi kama MITATU hv, nilipata salaaam, indirectly kupitia shemasi mmoja, confidant wake, ya kuwa, akinukuliwa kung’amua ya kuwa, “Mr. Oguda ni mmoja wa wakristo ambao ni wajasiri mno, na wakweli, na ambao si km washirika wengine, huangalia tu Mch wao akizama, hawawezi kumwambia!!”.
  UKO SAHIHI KUJISIFU, ila hebu Jipime kwa NENO LA MUNGU si kwa Mchungaji,Mashemasi wa kwa Washarika kwani hao wanaweza kukupeleka JEHANAMU kwa hizo sifa.
  Kama ungekuwa na ROHO WA KRISTO angekupa ujasiri wa kukemea hicho alichofanya Gwajima.Lakini kwa kuwa una “roho” nyingine HUWEZI KUTETEA KWELI Kwa sababu haimo ndani yako.
  Pia umetoa ushauri kama wafanyavyo WALEVI, ukiwaambia TUBUNI MKABATIZWE KWA JINA LA YESU KRISTO MPATE ONDOLEO la sivyo mtaingia Jehanamu, wao Watakuambia USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA.Ni maneno ya MFA MAJI uliyoyatoa kwa kusema ;
  ” Ninyi, Pendaeli na Lwembe mnamponya nani? No, Lwembe/ Pendaeli, watu hawa ni wa kusaidiwa tu, MARKO; “hata tuufikie utimilifu wa dahari”, Bado hamjafika ninyi, msikaze hukumu kwa wenzenu hv sasa, punzi ingalipo, Bwn atawarehemu km ni wakosa kwa hesabu hizo nizionazo kM mlivyomjadili kwenye mijadala hii huyo Gwajima, lkn pia Paulo anawakumbusha ya kuwa, “AJIDHANIAYE AMESIMAMA na AANGALIE ASIANGUKE”.
  Umejaribu kutumia MAANDIKO kuhalalisha UOVU unaoukumbatia.NImekutaka unioneshe neno PAMPERS kwenye BIBLIA matokeo yake umaeufyata!Usijaribu kunishauri niamini huo UKAFIRI wala usijidanganye kuwa una ROHO WA KRISTO.
  Gwajima kwako ni mtu mzuri na alichokifanya ni kizuri, endelea kumpigia debe kwani roho zenu zinafanana!
  HEBU SOMA HII KAMA ITAKUSAIDIA;
  “3 Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa,
  4 amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya;5 na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
  ****YOU CAN’T CHANGE YOUR DESTINY.****

 17. I HAVE LIKED THESE DEAR MAN OF GOD, SUNGURA;;

  “Ndiposa tuelewe alichomaanisha Yesu kusema sisi ni chumvi na nuru ya ulimwengu.

  “Nuru haiwi nuru ndani ya nuru, bali huwa nuru ndani ya giza, na chumvi haiwi chumvi ispokuwa mahali ambapo itàzuia kitu kuoza, hapo ndipo uchumvi wake utadhihirika”.

  “.Lakini pia inawezekana sehemu ya kanisa iliyoko kwenye serikali ni ndogo sana kwa sababu ya hayo mafundisho ya uongo kuwa usichanganye sisa na injili, hivyo watu wakajua kuwa kwenye siasa si kumtumikia Mungu, au haijui wajibu wake au nuru yake inamezwa na giza”.

 18. Lwembe,

  Jambo ulilonitaka kulifafanua hata haliko tata, ni jambo jepesi tu.

  Serikali ni watu ambao wanawatumikia wananchi, na watu hao wanaweza kuwa ni mimi na wewe.

  Na mimi na wewe tumeokoka, kwa hiyo sisi ni kanisa, na pia ni serikali.

  Mimi na wewe kuwa miongoni mwa kundi linalounda serikali na wakati huohuo tu sehemu ya kanisa, kunamaanisha kuwa sisi ni serikali au sehemu ya serikali ndani ya kanisa.

  Lakini mimi na wewe kuwa sehemu ya kanisa na hapohapo tu sehemu ya serikali, kunamaanisha kuwa sisi ni sehemu au ni kanisa ndani ya serikali.

  Ndiposa tuelewe alichomaanisha Yesu kusema sisi ni chumvi na nuru ya ulimwengu.

  Nuru haiwi nuru ndani ya nuru, bali huwa nuru ndani ya giza, na chumvi haiwi chumvi ispokuwa mahali ambapo itàzuia kitu kuoza, hapo ndipo uchumvi wake utadhihirika..

  Mimi sijui kanisa lililoko ndani ya serikali wamekwenda huko wakiwa wamefundishwa nini, maana kwa kweli nuru yao na uchumvi wao unafanya kazi kidogo sana.

  Lakini pia inawezekana sehemu ya kanisa iliyoko kwenye serikali ni ndogo sana kwa sababu ya hayo mafundisho ya uongo kuwa usichanganye sisa na injili, hivyo watu wakajua kuwa kwenye siasa si kumtumikia Mungu, au haijui wajibu wake au nuru yake inamezwa na giza.

  Mwangalie kijakazi aliyejua wa kiebrania aliyejua wajibu wake japo alikuwa sehemu ndogo sana sana ya serikali ya akina Naamani mwenye ukoma.

  Lakini alitengeneza historia kwa kujua kwake wajibu wake. Alikuwa amefunzwa akajua wajibu wake, kama Esta vile.

  Lwembe nawajua watu ambao ni majaji, makatibu wakuu, wakurugenzi, naafisa wa Tis, n.k,ambao ni wazee wa makanisa na wachungaji wasaidizi na wengine wachungaji kabisa Na baadhi yao wamekuwa wakifichua maovu makubwa.

  Wakati mwingine wanazidiwa tu kwa sababu ya uchache wao na kukosa nguvu ya mafundisho sahihi juu ya hilo.

  Lwembe, Yusufu aliwezaje kukaa katikati ya giza nene kiasi hicho na nuru yake ikang’ara, na akaendelea kumcha Mungu.

  Hao akina Daniel waliwezaje, ndani systemi za upagani wa kutisha na nuru yao ikang’ara?

  Sisi tunakosaje akili ya kuweza kukaa katikati ya hilo giza na nuru yetu ikang’ara, badala yake tunahimizana kujitenga na hilo giza?

  Ngoja tu nikomee hapa kwanza.

 19. Kwanza kbs, ni declare interest, mimi si mshirika wa Ufufuo na Uzima, na sijawahi kuwa, na kwamba, ht msingi wa huduma ile bado nipo kwenye utafiti wangu, maana, NENO ninalijua kwa sehemu, ninaomba kwa sehemu, ufahamu ninao, upambanuaji ninao pia, naam, hiki ni kipindi cha R/Mtakatifu.

  Lwembe & Pendaeli, yoote mliyoyaanyooshea kidole ktk paras zenu, bado kwa maoni yangu, especially, msemapo kuwa, huyo na ministry yake si mtumishi wa Mungu, NI WASENGENYAJI, am sorry to honourably comment so before the dear holy servants, sababu, ni kwamba, mumemuona mwenzenu aliyeifanya kazi hiyo mnayoidai kuifanya kwa usahihi wake? Umesoma hii, “mtumishi wa Mungu ASK. Kakobe AWAKEMEA Watumishi wa Mungu”. Sasa angalia details zake ndani alivyowachambua, na ndivyo alivyofanya mtumishi Gwajima kwa ASK mwenzake.

  Najua mtaendelea kukataa, lkn mufanyacho nyie ni masengenyo tu, you dare go public on the TV, or on the News papers, huku SG, ni family ndogo sana ya watu walewale siku zote, na hao kwakuwa, hawana uanachama humu, hawana muda wa kufuatilia haya majungu/masengenyo yetu humu SG, badala yake wanazunguka wakijitaabisha kwa ajili ya injili na maendeleo yenu km wakristo. Yaani, call a spade a spade, inashangaza bros!!, Sungura ashawaambia yote hapo juu, kaorodhesha watumishi wote wa nchini hpa, hata marehemu, mwana injili nguli aliyefyeka pori la Tanganyika, mzee wenu Kulola, na bado mlimkosoa tu. Biblia inasema Lwembe ndg yangu, “kwa wenye hofu, hofu, kwa wenye heshma, heshma,……….”, labda, uzoefu wenu wa kutokuwa na makundi ya kuongoza watu waendao mbinguni, yamkini ni tatizo mojawapo.

  Niwashauri tu ya kuwa, know, and incur the costs, muanzishe makanisa sasa, hayo muyaonayo na kuya RIDICULE, hayakuja hivihivi, wamelipa gharama hao ndg, ht km wakiwa wanahubiri mvuani ama juani km ulivo mention, Jesus did the same, ingawaje usafiri siku hizo ulikuwa ni punda/Hammer ya nyakati za Biblia.

  Niliposema, LAWFULLY yupo right, ukataka tena ni weigh na maelezo ya Pengo, niliishakuyapima, kwani, yeye Pengo ni respondent kwenye hii kadhia, alikuwa attacked, sawa, ila hukusema Lwembe km ktk utetezi wake Pengo aliitwa km Ask mkuu wa jimbo Kuu la Dsm, na kushirikishwa kwenye baraza/ Christian Forum, ingawaje ni kweli alisafiri kwenda Italy, lkn, he was on the list, na alijua kwakuwa, kazi ya jukwaa ilkuwa waazi kwake, linafanya na kutaka nini kwa ajili ya wakristo nchini, na mwenyekiti wake akiwa ASK. TARCIOUS NGALALEMTWA (Mkatoliki mwenziye), naye AKAANGUKA SIGN kwa niaba ya jimbo kuu.

  Narudi palepale Lwembe msiyumbishe haki ya mtu, km Gwajima kampa direct, mkubali tu, msiangalie venue saana, ndo nika quote, nadhani hukunielewa, “Mwambieni huyo Mbweha, ……………..”. Yesu aliyatamka hayo akiwa wapi?
  Nilichokigundua kwenu kwa ujumla, Gwajima km ilivyokuwa kwa watumishi wengine kwenu km alivyowaorodhesha ndg yetu Sungura, hawezi kupata heshma kwenu, na alikuwa kwenye waiting list ya kushughulikiwa, sasa lilipokuja hili la Pengo, mkaona murua kbs.

  Nimalizie kwa ushuhuda huu mdogo, mimi binafsi nilikwishawahi kusimama ktk mjadala ambao uliletwa na mch. wangu ndani ya kanisa, na kwakuwa, ulikuwa, mjadala huru, yaani, ili mradi uwe tu na maandiko constructive, nilisimama na nikapata nafasi, constructively nikachangia, mchango wangu, uliheshimiwa na mch wangu, though ali feel kuwa dissapointed kwa sehemu, akakubali hoja zangu lkn baada ya kuzichambua na kuwa km anazitupa nje hivi, baadaye nili suggest ya kuwa, according to the word of God, ni heri Pastor uachane na mijadala ya namna hii, baada ya hapo, washirika wenzangu wengi, waliniona km vile ninashindana na mch, lakn, ninapenda kukuambia ya kuwa, baada ya muda wa miezi kama MITATU hv, nilipata salaaam, indirectly kupitia shemasi mmoja, confidant wake, ya kuwa, akinukuliwa kung’amua ya kuwa, “Mr. Oguda ni mmoja wa wakristo ambao ni wajasiri mno, na wakweli, na ambao si km washirika wengine, huangalia tu Mch wao akizama, hawawezi kumwambia!!”.

  Ninamfahamu mtumishi mmoja pia, naye aliwahi kumfuata mch mmoja, na kumwambia anayoyaona kwake ktk ulimwengu wa Roho, na mengine anayoyasikia, na kuyalinganisha na maandiko, na mch huyo aliona ni uponyaji mkuu kwake. Ninyi, Pendaeli na Lwembe mnamponya nani? No, Lwembe/ Pendaeli, watu hawa ni wa kusaidiwa tu, MARKO; “hata tuufikie utimilifu wa dahari”, Bado hamjafika ninyi, msikaze hukumu kwa wenzenu hv sasa, punzi ingalipo, Bwn atawarehemu km ni wakosa kwa hesabu hizo nizionazo kM mlivyomjadili kwenye mijadala hii huyo Gwajima, lkn pia Paulo anawakumbusha ya kuwa, “AJIDHANIAYE AMESIMAMA na AANGALIE ASIANGUKE”.

  Stay tuned.

  Mubarikiwe.
  OGUDA J.E.

 20. Kwa wale “wanaojiita wakristo” halafu kwa ujasiri kabisa wanasema Gwajima hakumtukana Pengo, naona mmezidiwa UFAHAMU na huyu mwanafamilia wa Gwajima ambaye bila kumpendelea ndugu yake alikiri kuwa Gwajima ALIMTUKANA PENGO.
  Soma hii sehemu ya habari kutoka mtandaoni ili ugundue mwenye hekima na ufahamu wa kutosha katika kupambanua mambo.

  “………….Wakati huohuo, Methusela Gwajima ambaye ni Mwanafamilia amekemea vikali kitendo cha kutukanwa kwa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na kwamba ni kinyume cha sheria.

  Alisema kitendo hicho ni cha fedheha, ni kinyume cha sheria ya nchi na kwamba, alitakiwa kumfuata na kumweleza na si kumtukana matusi makubwa na kumsababishia aibu kubwa.

  Aliongeza, Gwajima abebe msalaba wake mwenyewe kwa kwenda kuomba msamaha, kwani aliamua kumchafua kiongozi huyo wa kiroho, na kwamba itamsaidia kurudisha heshima ya mwanzo aliyokuwa nayo.”

  (Imeandaliwa na mtandao http://www.habari za jamii.com)

  Mnaosema Gwajima hakumtukana Pengo mnaweza kwenda KUBISHANA na huyo mwanafamilia kuliko kubishana na ndg CK LWEMBE ,Pendael,…nk.
  Hakika. mnaosema Gwajima hakutukana mnahitaji TIBA ya KIMWILI na KIROHO ili mpone.

 21. Lwembe,

  Kwani askofu wangu ametenda kama alivyotenda Pengo mpaka nimpe hivyo vivumishi?

  Angekuwa ametenda yanayostahili hizo sifa na nikawa na sababu ya kumwambia, ningefanya ulichonitaka kufanya.

  Kwa hiyo Lwembe kama ulikuwa unajibu swali langu la ni matusi gani Gwajima kaongea ambayo kwa viwango vya biblia yako kwenye kundi la matukano?, naomba uendelee kutoa majibu yako.

 22. Sungura,

  Kuna hili jambo jingine ulilolisema ambalo ni la msingi sana iwapo tutafika mahali tukajiridhisha kuhusu hilo kama unavyosema, nakunukuu:
  “”Jambo jingine ambalo niko radhi tubishane hapa mpaka tutoke na jibu sahihi ni huu uongo kuwa kanisa na siasa havichangamani, au siasa na injili havichangamani. Naona watu wengi tu akiwemo Lwembe, wanasema sana juu ya jinsi gani watumishi wa Mungu hawatakiwi kujihusisha na siasa.””

  Kutoka maelezo yako hayo, umeendelea kwa uhakika kabisa:
  “”Nataka tu niseme kuwa kanisa ni sehemu ya serikali na serikali ni sehemu ya kanisa.””

  Basi ukitufafanulia jambo hili la “kanisa kuwa sehemu ya serikali, na serikali kuwa sehemu ya kanisa”, itatusaidia wengi sana kuondoka ktk mtazamo tofauti tulio nao.

  Gbu!

 23. Sungura,

  Acha ushabiki!

  Yaani kweli hujui hata matusi ni nini? Acha mizaha!

  Haya, rudi kwenye hiyo clip halafu kila mahali alipotajwa Pengo, weka jina la askofu wako kisha mpelekee; mtakapomalizana naye, utayajua matusi ni nini!!

 24. Oguda,

  Tazama ndg yangu, call a spade a spade if at all unaijua spade!

  Suala la watu kunyeshewa mvua, nilianza kulisemea la kupigwa jua kwanza, kwamba how can a Godly man ever keep the people in that torment of a BLAZING sun and him flying a chopper?!! Nilirudi ktk Biblia kuitazama Huduma ya Kristo, sikuliona jambo hilo, na Roho apaswa kuwa mmoja; huko nimewaona watu wakilishwa vyakula mpaka wakamtaka awe mfalme wao!!! Hata kwa mitume, lile kanisa la kwanza waliuza possessions zao ili wakidhi haja zao kama familia moja! Usimtafute Mungu kwenye mambo makubwa makubwa, utamkosa; yuko ktk hayo madogo madogo unayoyaruka!!

  Pia, Biblia yako Oguda, isome kwa kituo, usitegemee kwamba kutakuweko na trumpet itakayopulizwa ili ku set in TRIBULATION! Zitazame roho zinazo hudumu, zinamdhihirisha Kristo au la, hakuna middle ground, na haijalishi wingi wa watu au sifa anayoipata mtumishi, ndio maana umeambiwa uzipime roho at your own expense, Mungu akiisha kukuwekea Neno lake hapo, una hiyari kulitumia au kuli compromise!

  Kwamba “Gwajima yuko lawfully right”, well, kulingana na kilichotokea, na kiwango chake, siwezi nikakupinga ktk hilo, maana inategemea uliyeamua kumuamini; kauli ya Pengo niliyoisikia ni kwamba yeye hakuwepo alikuwa Italy, hivyo nani anasema kweli kati ya watumishi wa Mungu hawa wawili, hilo nimewaachia wenyewe!

  Kuhusu Yn 17:15 ndg yangu ni kweli kabisa, huwa tunakosea ktk hili na lile, lakini ukumbuke pia kwamba tunawajibika ktk kuihubiri Injili na si kuigeuza mimbara kuwa sehemu ya vijiwe vya kisiasa! Kama Pengo aliigeuza kauli yake ya awali ili kumfadhili Pinda, basi Gwajima kuleta kejeli madhabahuni ili kumfadhili Lowasa, ndio huo MZAHA tunaousema ambao wewe unauona ni Neno la Mungu!!! Hata hivyo ndg yangu, unao uhuru wa kuliona tukio hilo ktk jinsi unavyoliona, mitazamo yetu inategemea sana mioyo yetu ilikolalia!

  Hii ya mwisho ni kali zaidi; unaniambia, “”…you have almost 0.00% of approval, locally or internationally of the servants of God.”” Hahahahaha….! Sikia ndg yangu, Biblia iko MOJA tu duniani, no matter how many versions of it there is! Kwahiyo, jambo ambalo nimejifunza kutoka humo ni kwamba kuna biashara ya “NAFSI” inayoendelea; na “Wachuuzi” ni weeengi sana, si umemsikia Paulo akisema anamposea sisi Kristo, sasa unadhani hao aliosema kwamba wakija kukuposa wakakuletea habari tofauti na ile waliyokuletea wao WALAANIWE; Je, unavyofikiri ukiposwa na hao utapelekwa wapi???
  Pia refresh you mind, hao watakao lia na kusaga meno huko mwisho ni hao walioposewa Ibilisi, huyo aliyejifanya Mtakatifu, yule mpanda farasi mweupe wa Ufu 6:2!!

  Kwahiyo sio u local au ukimataifa wa muhubiri, bali je, anahubiri sawa sawa na Injili waliyoihubiri mitume? Ikitoka nje hata IOTA moja, SIMPI nafsi yangu, ninamkataa yeye na injili yake, huo ndio msimamo wangu kuhusu nafsi yangu; it’s the best thing that God ever gave me, and He proved this to me when He left His Throne to come for me, ninakushauri nawe ndg yangu, Value it, it’s the best thing that you got!

  Finally niseme kwamba, jambo zima nililiona ni mzaha, a savage one for that matter, ndio nikalisemea ktk uchungu wake, kwamba by all standards hiyo sio Ministry of Christ, yeyote mwenye macho na ayaone hayo, walio vipofu ndio hivyo tena, wasubiri uponyaji kama bado upo!

  Kagua tena hiyo Malaki 3:3, utakuwa umekinukuu vibaya; u got so hot!?

  Easy does it brother,

  The Lord bless u!

 25. Edmund John Oguda,Naona umemezwa na ENTICING SPIRITS mpaka huitambui Biblia zaidi ya Mafundisho ya Mch.Gwajima.Kama Pengo hajaenda Polisi/Mahakamani usinilaumu bali laumu vyombo vya habari.Unashindwa kutumia ufahamu wako kuwa MATUMIZI YA MANENO KWENYE BIBLIA huchukui tu na kuyatumia unavyotaka.Kwa mfano, huwezi kwenda kushuhudia Machangudoa halafu ukawaambia “Ninyi mbwa mtaangamia”!Ingawa mzinzi anafanishwa na mbwa lakini hapo UMETUMIA AKILI?Hebu nioneshe PAMPERS kwenye Biblia!Nafikiri umejipanga kweli kweli kutetea huu ukafiri kisa Gwajima ni Askofu wako/mtumishi anayekulisha.Unaniambia “You are lost my dear Pendael”, haya ni maneno ya MFA MAJI.Kuhusu kupotea Usijali kwani ipo Siku tutakutana mimi, wewe pamoja na watu wote MBELE ZA MUNGU ndipo TUTAKAPOJUA NANI KAPOTEA.

 26. Sungura,Umetoa mawazo yako na uko sahihi kwa mtazamo wako.Kama ulivyosema kuwa tusibishane,nami siko tayari kubishana au kutetea Ukafiri.Mimi nitashikilia ninachoamini.

 27. Naendelea,

  Maadamu hapa tunajadili suala la Gwajima kumtukana Pengo, ningeomba tuwe maalum (specific); Gwajima alimtukana Pengo tusi gani, maana naona kila mtu anasema Gwajima kamtukana Pengo.
  Au ni matusi gani Gwajima kaongea ambayo kwa viwango vya biblia yako kwenye kundi la matukano? Pendael ni kipi ambacho unakiita kuwa ni uchafu na matusi ambacho Gwajima kasema?

  Jambo jingine ambalo niko radhi tubishane hapa mpaka tutoke na jibu sahihi ni huu uongo kuwa kanisa na siasa havichangamani, au siasa na injili havichangamani. Naona watu wengi tu akiwemo Lwembe, wanasema sana juu ya jinsi gani watumishi wa Mungu hawatakiwi kujihusisha na siasa.

  Nataka tu niseme kuwa kanisa ni sehemu ya serikali na serikali ni sehemu ya kanisa. Na hivi huwezi kuvitenganisha. Kinachokea sasa hivi katika hili taifa ni msuguano wa ukweli na uongo dhidi ya kauli ya siku nyingi ya kuwa ‘usichanganye siasa na dini’. Watu imefika sehemu wanakosa usahihi wa kauli hii, maana ki mantiki halisi huwezi kuvitenganisha.

  Labda kama wangesema kuwa usichanganye sera za chama fulani na injili au dini kidogo ingeleta maana.

  Nani hapa kati yetu ambaye si sehemu ya siasa za nchi hii na hapohapo yeye ni kanisa, je Lwembe ni wewe, au je Pendael ni wewe?

  Lazima tujiulize kwanza kanisa ni nini na Siasa ni nini kwa usahihi wake,kisha tujiulize kanisa linahusikaje na utawala, na siasa zinahusikaje na utawala wa nchi, kabla hatujaja kwenye mtazamo wa kwamba kuongea mambo ya utawala wa nchi au siasa kanisani siyo sawa.

  Na siyo sawa kwa kigezo au andiko gani?

  Biblia inaposema kuwa mwenye haki akitawala watu hurahi humaanisha wakitawala wapi, kanisani au?

 28. Again C.K Lwembe, bro wangu, ktk mjadala mzima, ht km ndivyo muonavyo ya kuwa, yamkini alikosea saana, kuyazungumzia hayo, yao na akina Pengo mimbarini kwake, mbele za watu wake, mmechukizwa tena ktk kile mkifanyiacho mzaha, kwamba alikuwa anawazungumza ‘ati, watu waliochooka, huku wakinyeshewa mvua’, lkn, tutambue ya kuwa, jambo hili lina sura mbili, moja ni hiyo, lkn pili ni ile baada ya polisi na matukio yaliyofuatia, ambayo, nami kwa upande wangu, niliguswa na hili la pili ndg zangu, ndiposa nikawaulizeni ya kuwa, lile TUNDA LA ROHO liko wapi nyakati hizi miongoni mwetu? Mmelitupilia mbali kbs nanyi, kwani, ht angalikuwa ni mshami kbs bado usingalipata rehema walau kidogo??

  Ndg yangu Pendaeli, anasema, yoote aliyoyatamka Mch. Gwajima kwenda kwa Askofu mwenziye Pengo ni uchafu kbs, hata kwenye Biblos, yaani, Biblia Takatifu hayapo kbs. Ninadhani, kwakuwa, hakutamka matusi ya asili ya nguom
  ni, nadhani, maneno km vile, mjing/ujinga, mpuuzi/upuuzi, mpumbavu/upumbavu, nilikuwa ninamheshimu, sasa basi, hafai kbs, n.k., Pendaeli, yatafute kwenye Biblia utayapata pia.

  However, lawfully, Gwajima is also right, km ameweza kutujulisha kuwa, mipango yoote ASK. Pengo alikuwa aware nayo, naye ukimsikia kwenye utetezi wake, anasema na kukiri kuwa, alikuwa anafahamu yoote, na kupewa nyaraka za makubaliano mbili na kuzisoma kiisha kuzisaini, NINI kilimfanya baada ya siku mbili tu kugeuka nyuma? Km si kushiba maharage ya akina Pinda, nduguye, school/classmate mwenziye?? Unataka nimtetee Pengo ktk sura hii? You are lost my dear Pendaeli.Pengo ni msaliti wa nafsi za Watanzania, Watanzania ni pmj na Kanisa, regardless ni Waliookoka, ama Wakristo dini. Therefore, wanapokutana au walipokuwa wanakutana kujadiliana, waliachilia shughuli zao mbalimbali, zikiwapo za kiinjili kulala, sasa inapotokea wewe nami hatulioni hili, baasi, ni tatizo kubwa ndg zangu.

  And for your information, Pengo hajaenda polisi km unavyotaka kutuaminisha, Kova, ameyasikia haya mitandaoni, na maelekezo toka juu yamechangia Gwajima kuitwa kituoni, na hv anaonekana ni team Lowassa, ndiyo wkt muafaka ukaonekana ili wammalize kbs.

  Ndg yangu C.K. LWEMMBE, tambua ya kuwa, Kristo Yesu kwa andiko hili anatuona ya kuwa, tuko mbinguni kwa ule usajili wa awali, lkn, kwa hbr ya miili hii, bado hatujahama; YOH.17:15.

  Lkn pia, kwa hbr ya wapi azungumzie hayo anayoyayataka ama aliyoyaona yanafaa kuzungumzwa dhidi ya Pengo, sikumbuki vzr, lkn unakumbuka ya kuwa, Bwm Yesu alimrarua waazi Mfalme Herode, akimwambia, ” Mwambieni huyo mbweha,……………..”.
  Ndg yangu, Lwembe, kwa hbr ya upambanuaji wa huyu siye na huyu ndiye mtumishi km inavyoelekezwa ktk para zako 4 kwangu kwenda chini, nasikitika kusema ya kuwa, mijadala mingi nimewahi kuipitia huko nyuma, mengine tumeshea ideas upande mmoja, lkn, you have almost 0.00% of approval, locally or internationally of the servants of God. Hili alinitishi sana, kwakuwa, yapo mambo ambayo, mimi humalizia kwa hili andiko; MALAKI 3: 13, ” Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua, …………………..”

  MUBARIKIWE.

 29. Ninyi watu,

  Hata sisi katika kujadili kwetu kwa viwango vya Mungu tuko na mapungufu mengi sana ya kimisimamo na mitazamo. Sijawahi kuona mtumishi ambaye tuliwahi kumjadili hapa wote tukamuunga mkono.

  Hiyo inajaribu kunifikirisha sana kama kwa viwango vyetu hapo SG kuna hata mtumishi mmoja wa kweli hasa hapa Tanzania, na hata duniani kote. Labda ambacho tunatakiwa kuelewa ni kwamba hata sisi kwa viwango vyetu vidogo vya utumishi tulivyonavyo tungefanya jambo na likaletwa hapa tungekosolewa na kuonekana kuwa tulifanya makosa katika jambo hilo hata kuliko kuliko hao watumishi, japo sisi wenyewe bila shaka tungekuwa tunaamini tumelifanya sahihi.

  Sasa ni muhimu sana kuogopa kuhukumu mambo kwa mtazamo wa jumla, na kujikuta unamuona mtumishi fulani wa Mungu hafai na hivyo ukajikuta umeingia kwenye suala la kumnenea vibaya au kumhukumu mpakwa mafuta wa Bwana bila ya wewe mwenyewe kuwa na nguvu ya mamlaka ya kufanya hivyo.

  Tangu zamani katika historia ya biblia suala la watumishi kumtumikia Mungu huku wakiwa na mapungufu fulani limekuwepo, lakini waliothubutu kunena au kutenda isivyo sawa juu yao hawakuhesabiwa kuwa walifanya sahihi.

  Ni mtumishi nani leo katika taifa hili ambaye tutamjadili hapa Lwembe, au Pendael, au mimi Sungura tusimtoe kasoro, je ni Mwingira, je ni Kilaini, je ni Malasusa, je ni Kakobe, je ni Gamanywa, je ni Mwanisongole, je ni Getruda Lwakatare, je ni Batenzi, je ni Lusekelo, je ni Ndegi, je ni Pengo,je ni Maboya au ni nani? Mbona hawa wote tulishawatoe kasoro! Ndio tuseme kuwa Tanzania hatuna watumishi wa Mungu ambao wamekamilika/ wanafanya mambo sawasawa na mapenzi ya Mungu? la hasha.

  Lakini ivi Lwembe au Pendael au Sungura leo tukiwa wachungaji wakubwa, je tutafanya kila kitu sawasawa na kabisa na biblia inavyosema na kila mtu akasema kuwa tumepatia, au sisi huko tunakochungwa, wachungaji wetu wanapatia kila kitu kulingana na mitazamo yetu?
  Ni mara ngapi basi tumewakosoa uso kwa uso kama tunavyofanya hapa mtandaoni kwa hawa watumishi ambao inatokea tukawajadili hapa, au hapa tunafanya unafiki zaidi?
  Mbona sisi kwa namna moja ama nyingine ni matunda ya hao hao tunaowakosoa kwa maneno makalimakali na kejeli nyingi tu leo!!

  Mpaka mzee Kulola ambaye mimi naweza sema ni miongoni mwa magwiji wa injili ya moto hapa Tanzania, bado alikuwa na kasoro au mapungufu yake, lakini haikuwahi kumwondolea heshima yake ya utumishi mbele za Mungu.

  Sikieni watu wa Mungu, mtumishi kufanya kosa hasa ambalo ni kosa kwa mujibu wa utamaduni wa jamii na kwa sheria ya nchi husika, au hata la kibiblia, si maana yake kuwa amekuwa si mtumishi wa Mungu. Tujitahidini sana kutumia maneno ya staha na adabu kufanya tunachokiita kuwakosoa kama alivyoagizwa Timotheo na Paul jinsi ya kuwakemea wazee, yasije yakatupata yaliyompata aliyekubali kumuua Saul mfalme kwa upanga wake, pamoja na kwamba Saul alikuwa ameshanyanywa ufalme ktk ulimwengu wa roho.

  Nitaendelea…

 30. Edmund John Oguda.Mimi sijali kejeli zako ulizotoa kwenye maelezo yako.Nimeamini katika watu wenye mizaha na wewe upo.Hivi, mbona haumtetei Pengo kama wewe ni MKRISTO KWELI, badala yake unaukumbatia UKAFIRI wa matusi?Unajua unaweza kufikiri Gwajima ameonewa, ndio maana UNAMTETEA HATA katika UJINGA.Unapotetea Ukafiri kama huu unazidi kujiweka mbali na Mungu.Maelezo yako yanamfanya asiyemjua Mungu afikiri BIBLIA inaunga mkono Uchafu kama huu, eti” Mchungaji akitukana aombewe na asiambiwe ukweli wala kuulizwa”.Nimekutaka utupe uthibitisho wa hayo maneno ya Mch.Gwajima kwamba ni ya Kwenye Biblia kama ulivyodai, matokeo yake unasema tunamsimanga.Hatupo hapa kutetea UOVU wa aina yoyote au wa mtu yeyote mwenye cheo au asiye na cheo.Kumwombea mtu si MATANGAZO vinginevyo utakuwa ni UFARISAYO.Hizo changamoto wala hazijakusaidia!Kumbuka,hapa ni mahali pa kujenga roho,nafsi na miili ya watu.Be gentle!

 31. Oguda,

  Shedding “Crocodile tears” don’t make saints!

  (Kwanza acha hila ya kuchanganya ugonjwa wa askofu na tukio tunalolijadili, ni mambo mawili tofauti, hapa hatuzungumzii ugonjwa!!)

  Unapozungumzia baraka kwa ” …enyi mulionalo jambo hili ktk roho kuliko mizaha”, mimi nadhani ungetuwekea wazi “ukiroho” wa jambo hili kwanza, ili nasi tuone jinsi ambavyo tumelikosa hilo kwa kuikosa hiyo Roho ya Kristo, ndipo kwa kuwa kwetu na “roho nyengine” tukaliona ni jambo la mzaha!

  Vinginevyo, utatufanya tuamini kwamba nawe u sehemu ya mzaha huo kwa kuliona jambo hilo kuwa ni la kiroho, na ukatafuta kuwaaminisha watu hivyo, kuliko jinsi ya mzaha lilivyoletwa!

  Leo ni siku tofauti saaana, Maandiko yako wazi sana. Hayo ndiyo yanayowasimika watumishi na kuwatofautisha na hao waliojisimika wenyewe kwa manufaa yao binafsi. Kama jambo hili hulijui, basi utaishia kumwita kila anayepanda mimbarani ni “mtumishi wa Mungu” hata wanao yafunga magugu; ndio lile jambo analolisema mtume Paulo kwamba “Mtu akiwa mjinga na awe mjinga” maana yote yako wazi!

  Nukuu ya mtume Paulo unayotaka kuitumia, haina uhusiano wowote ule na jambo hili! Hiyo clip ni ya kisiasa zaidi ingawa imerekodiwa kanisani, kwahiyo kwa vile huna uwezo wa kuyapambanua mambo haya, ndio umekuwa mwepesi wa kumhusisha Mungu ktk jambo la huko gizani, ukatafuta na watu waliombee, ukishindana na Mungu huyo huyo anayekuonesha peupe kwamba hapo mimi sipo!!!! Yaani Mungu anaposema “Tokeni katikati yao” wewe unasema kaeni tuwaombee!!!!

  Je, Kristo kwa kuwaita Wafarisayo, hao watu wa dini waliokuwa wakiishikilia Torati, “wana wa majoka”; unaonaje, hiyo nukuu ya mtume Paulo uliyoitumia itafaa hapo?! Mtumishi wa Mungu aliye ktk ukuhani hufanya kazi ya Mungu tu, na si kuchanganya na siasa, Mungu huwa hashiriki Utukufu wake na chochote kile, nao vipofu wa dini huwaga hawajui hata ni lini Mungu aliondoka; “mtumishi” akiwaambia “Bwana ameniambia…” wao huitikia “Amina!” mpaka siku nyumba itakapowaangukia na kuwaua wote!!!

  Usichanganye Neno la Mungu na siasa za dini, vinazalisha “kanisa vugu vugu” having a form…!!!

  Gbu my brother!

 32. Ninashukuru
  Kwa changamoto ndg yangu, kabla sijarejea km nilivyoahidi hapi awali. Niseme tu ya kuwa, Unaweza kuwa na maandiko lukuki tena ya msingi km nilivyoona, lkn, ktk hali iliyopo ss isiwe na tija kbs on the ground, ninikukubali, quotes nyingi za kimaandiko zimekutoka kichwani kwelikweli, lkn zina chembe ya huruma na upendo ndani yake?
  Unasema, mfano, ht Pauli alimkemea Petro, ni kweli, lkn ww hujafanya hivyo ndg yangu, ungelifanya hivyo, nsingeliandika, mumemsimanga mno, ndo tofauti ss.

 33. Edmund John Oguda.Maelezo yako yamejaa urasimu mwingi.Si MAOMBI tu bila KUAMBIWA UKWELI.Biblia inasema tunapaswa kuonyana,kukaripia,nk…Mbona Paulo alimkaripia Petro na Petro akashukuru?Hawa si Malaika bali binadamu.Kinachotakiwa hapa SG ni INJILI HALISI na THABITI na si huo Uchafu anaozungumza Gwajima.Mimi siko upande wa Gwajima wala Pengo(Soma mchango wangu kuhusu hili), niko upande wa NENO.Nafikiri hata wewe unamhitaji Mungu akusaidie sana.Maelezo yako yameegemea kutetea Uchafu (maelezo ya Gwajima dhidi ya Pengo),unataka kutuambia huu nao ni Ukristo wa Biblia ipi?Confidently,unasema ” Naam hakuna ambacho Mch.Gwajima amekisema nje ya biblos”.Hayo matusi ndio ‘biblos’ kwako, au umetumia neno ‘biblos’ ukifikiri watu hawalijui kuwa ni Biblia?Labda alichokisema Mch.Gwajima ipo kwenye ‘biblos’ ya UFUFUO na UZIMA!!Kama ulivyoahidi utarejea baadaye,hebu rejea ili ututhibitishie aliyoyasema Mch.Gwajima yapo kwenye ‘biblos’ ipi.

 34. Naam, mubarikiwe mno, enyi mulionalo jambo hili ktk roho kuliko mizaha, n.k., am sorry to say/ comment tumeacha kuwaombea Watu, especially Watu wa Mungu. Inawezekana humuelewi Gwajima na Huduma yake, lkn isifike kiwango cha kukosa ht huruma, ambayo ni moja ya Tunda la Roho kwa yaliyomkuta. Hayo au hiyo hali au Tabia, ni matunda ya shibe ndg zangu, ni aliyeshiba maharage tu ndo anaweza kuzungumza mzaha juu ya hilo jambo lililomkuta Mch. Gwajima. Ile hofu ya kiMungu miongoni mwetu iko wapi, ni lini Magoti yako uliyataabisha, na tumbo lako likaitikia njaa kuwaombea watumishi wa Mungu? Ht km kwa viwango vyako, si watumishi, lkn, tambua Paulo mtume,anahoji, “Hu nani wewe umsemaye mtumishi wa mwengine/ mwenzako”? Tambua, wako walio chini yao ambao wamenunuliwa kwa damu hiyohiyo iliyokununua wewe. Ndg zangu, tuwaombee Watu na si kuwacheka, hii si roho ya Kristo wandugu. “Iweni na roho ya Kristo ileile”. Nasisitiza ndg zangu, to ridicule the servants of God ni roho nyengine hiyo, haitoki juu, ht mkitumia nahau nyingi zenye semi rembwa za kiroho, lkn zitanuka tu harufu za kifedhuli zisizo na uungu ndani yake. Pima ukisemacho. Na ni km vile ulikuwa siku zote unamsubiria ajikwae tu. Naam, hakuna ambacho Mch. Gwajima amekisema nje ya biblos, ntarejea baadaye. Mubarikiwe.

 35. Sungura,

  Kwamba nimemezwa na roho ya mzaha, yawezekana ukawa sahihi; unajua, unapokuwa ktk dunia ya mizaha ni vigumu sana kufanya tofauti!

  Kulingana na maendeleo tuliyomo, tunaweza kuwa tumejipanua kuliko uwezo wetu, na hivyo ili kukidhi haja ya vyombo tulivyovianzisha, kama redio na tv, basi tukaamua kutengeneza na clips za mizaha kwa ajili ya watazamaji wetu ktk jinsi ambayo sisi wenyewe tumeshawishika kwamba clip hiyo italeta msisimuko!

  Mimi nilipoiona hiyo clip sikuyaamini masikio wala macho yangu, yaani huo msisimuko! Lakini kwamba imetayarishwa na “Rudisha Tv” inayomilikiwa na kanisa la Ufufuo na Uzima; na kwamba lilikuwa ni “Tamko” lililotayarishwa, basi jambo lote lapaswa kuchukuliwa kama lilivyotokea pamoja na msisimuko uliokusudiwa!

  Basi, mzaha wa matusi na kejeli unapotayarishwa na kuchezwa ktk viwanja vya kanisa, siku ya ibada, huku wahusika wakinyeshewa mvua, mchezaji kiongozi aliyezungukwa na walinzi wake wakiipamba scene hiyo, tena akiwaambia wanaotaka kulirekodi tukio hilo wajitayarishe, na camera man wa Tv yao akiyarekodi hayo kwa ajili ya programu zao, basi Sungura unanitaka niseme nini kuhusu jambo hilo??

  Ninachoweza kukuambia ni kwamba, hiyo clip inaweza ikawa best seller, yaani anaweza akawa trillionaire overnight, iwapo wataalamu wataweza wakayabadili matusi hayo na kuyawekea maneno ya staha, labda kama, “Okoka ewe mwenye dhambi, ikimbie Jehanamu ya moto; tubu dhambi zako ubatizwe kwa Jina la Bwana Yesu Kristo, upate Ondoleo la Dhambi zako, upokee na vipawa vya Roho Mtakatifu!!!” Jaribu kuondoa sauti kwenye video hiyo halafu utaniambia!!!

  Gbu!

 36. Lwembe,

  Nafikiri kuna kitu cha maana zaidi chakumfanya mtu ajifunze ulitakiwa kukiandika, kiwe hasi au chanya, kuliko hicho ulichoandika sasa kwenye comment yako!

  Au na wewe umemezwa na roho ya mzaha, hivyo ukajikuta unaandika mzaha kwa wingi?!

 37. “Mchungaji” Gwajima ni “Mpakwa Mafuta” wa Bwana; ni “mtumishi” anayemuwakilisha Kristo, ukimuona mchungaji huyo, ni sawa na kumuona Kristo! Kwahiyo, kama Nicholaus Pius Said anavyosema, “ALIKUA ANATETEA NA KULINDA NAFASI YA KUTANGAZA INJILI YA KWELI”; yaani huyo mchungaji hapo mnayemuona ktk hiyo video ni Kristo, yaani huyo ni Roho Mtakatifu anayehudumu na kunena hayo mnayoyasikia!!!!!

  Nalo kusanyiko lote la hao waliofufuliwa linashangilia jambo hilo!

  Huu ndio UTANI wa mwaka! Ni utani utakao wagharimu wengi wao Hukumu, maana kwa kila hali, roho anayehudumu ktk kusanyiko hilo Si Roho wa Kristo, ni yale maroho yaliyomwagwa ktk siku hizi za mwisho, yale maroho ya Mt 24:24!!!

  Tena maroho yenyewe ni very sadistic, na huwa hayavijali hata vyombo vyao vya utumishi, huviadhibu baada ya kuvistarehesha; si mnawaona hapo wanavyolowa mvua, hao hapo jua lao na mvua yao, ila mchungaji ana “edikopter”, na kila mtu unayemuona hapo akilowa chapwa, wana mategemeo makubwa sana ya mafanikio kama ya mchungaji wao!!!!

  Basi ndg zangu, hebu liwazieni jambo hili, kwamba mchungaji ndo huyo hapo, mvua ikimteremkia kisawasawa, hana namna ya kuikimbia kwa sababu yule roho hawezi kumruhusu aikimbie mvua, halafu ana donge la kupingwa na Pengo, akimuwazia Pengo aliko ktk muda huo, labda St Peters au St Joseph, kule mbele kwenye mazulia ya kueleweka, yeye ndio kwanza anaruka matope, akiiwazia ile hali tulivu ya ibada aliyomo Pengo, hasira ndo zinazidi kumpanda, na mwisho kale kauzi kembamba kalikokuwa kanaishikilia ile ‘sanity’ yake kakakatika, akawa si yeye tena, yale maroho yakamfikisha kileleni yakambwaga chini matopeni kama unavyomuona hapo, muita misukule akageuka msukule wa hayo maroho!!

  Katoliki, yaondoeni hayo mashtaka dhidi yake maana ninyi wenyewe mnapoiangalia hiyo video mnapaswa mjue kwamba huyo si mzima, amepagawa; waiteni wale wataalamu wenu wa ‘exorcism’ wamtibie!

  Chezea misukule weye!!!
  Pigeni “majeshi majeshi” mumrudishe mchungaji kabla “Hajaishia zake”!!!!

 38. WAPENDWA;
  Kuna tofauti kubwa kati ya KANISA na DHEHEBU.KANISA ni mali ya BWANA YESU na DHEHEBU ni mali ya SHETANI/IBILISI.
  Nimekwisha kuchangia katika “blog” hii kuwa MADHEHEBU YOTE ni ya IBILISI na watu wamefumbwa macho na MAPOKEO YAO na KANUNI ZA IMANI za MADHEHEBU YAO hata NENO LA MUNGU hawalioni.
  Haya ni Matunda ya MADHEHEBU,Gwajima ANAMTUKANA na KUMKASHIFU Pengo, Pengo naye kampeleka Polisi (kamshtaki).Kuna UKRISTO wa namna hii wa kutukanana na kupelekana POLISI/MAHAKAMANI?
  Hizi ni dalili tosha kuwa MADHEHEBU yameandikwa IKABODI “Utukufu umeondolewa”.Usishangae haya kwani bado mengine mazito yanakuja
  Wote (Pengo na Gwajima) wanahitaji kuachana na SIASA za MADHEHEBU yao na kukubali kuwa WAKRISTO (MATENDO 11:26 “…………..Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia.”)
  Ili uwe MKRISTO ni Lazima UTUBU na KUBATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO na SI VINGINEVYO (MATENDO 2 :37-38 ” 37Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
  38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
  39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.”
  Soma MATENDO 8;14 “14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;
  15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;
  16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. 17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. ”
  Pia, MATENDO 10:47-48 ” 47 Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?
  48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.”
  Vilevile,MATENDO 19:1-5 ” 1 Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.3 Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana.4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.5 Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”
  Gwajima,Pengo na wengine wanaotaka kwenda Mbinguni, bado NEEMA ipo msifanye mioyo migumu bali njooni kwenye KIJITO CHA UTAKASO/DAMU YA YESU mmpokee ROHO MTAKATIFU .

 39. TUNAITAJIKA KUOMBA JUU YA HILO HATA KAMA KAFANYA KOSA KISHERIA ILA ILIKUA KWAAJILI YA KUTETEA HAKI ZA WAKRISTO DHIDI ZA MAHAKAMA YA KADHI HEBU JARIBU KUMSIKILIZA KATIKA MAELEZO YAKE YA KWANZA ALIKUA ANATETEA NAKULINDA NAFASI YA KUTANGAZA INJILI YA KWELI.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s