Raisi Kikwete azungumzia mahakama ya Kadhi!

Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Freddy Maro).

Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa viongozi wa kamati ya Amani mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kitaifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam juzi

 

RAIS Jakaya Kikwete amefafanua msimamo wa Serikali katika mjadala unaoendelea wa Mahakama ya Kadhi, na kuweka wazi kuwa Serikali haina mpango wa kuianzisha, wala kuiendesha.

Mbali na hiyo, Rais Kikwete ambaye jana alizungumza na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Dar es Salaam, pia alielezea kusikitishwa kwake na tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, lililowaelekeza waumini wao kupigia Katiba Inayopendekezwa kura ya Hapana.

Akifafanua suala la Mahakama ya Kadhi, Rais Kikwete alisema Serikali ina msimamo wa mambo mawili katika mahakama hiyo.

Kwanza, alisema Serikali haina mpango wa kuianzisha na kuiweka katika Katiba na pili, haihusiki kuiendesha na badala yake, Waislamu wenyewe ndio watakaoiendesha.

Alisema kimsingi, mahakama hiyo ilikuwepo kabla ya Uhuru na kinachotakiwa kuzungumzwa ndani ya Bunge, ni Sheria ya Kutambua Uamuzi Unaofanywa na Kadhi.

Alifafanua zaidi kuwa Mahakama hiyo ya Kadhi, haihusiki na mambo ya jinai, isipokuwa mambo ya kijamii ikiwemo talaka, mirathi na mengine ya aina hiyo.

Alitoa mfano wa Sheria ya Kiislamu, iliyokuwepo tangu zamani, ambayo inatambua chombo hicho na kusisitiza kuwa kinazungumzwa, ni uamuzi unaofanywa na Kadhi utambulike tu.

Katika mfano huo, alisema Muislamu ukigombana na mke wake, kuna mabaraza ya usuluhishi ambayo huyo mwanamke atapaswa kwenda, ila wakishindwa na ataomba talaka ambayo inaidhinishwa na Kadhi, ambaye ndiye msajili wa vyeti vya ndoa kwa Waislmau.

Baada ya kutoa ufafanuzi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Shehe Alhad Musa, alimshukuru Rais Kikwete kwa ufafanuzi alioutoa na kusema Wakristo na Waislamu siku zote ni wamoja na wataendelea kuishi kwa amani, furaha na ushirikiano.

Katika hilo, Shehe Alhad alinukuu Biblia katika Kitabu cha Mathayo tano, mstari wa 25, ambao unasema; “Patana na mshitaki wako, mngali njiani, asije akakupeleka kwa Kadhi na Kadhi akakukabidhi kwa Polisi na Polisi akakutupa korokoroni.”

Katiba Pendekezwa

Akizungumzia Katiba Inayopendekezwa, ambayo inasubiri kupigiwa kura na wananchi, Rais Kikwete alisema Katiba hiyo imewakilisha vitu vingi kuliko Katiba iliyopo.

Alifafanua kwamba Katiba Inayopendekezwa, imeweka haki za makundi mbalimbali ya jamii, kuliko iliyopo na kuongeza kuwa yeye binafsi ameisoma na kurudia kuisoma, lakini hajaona mahali popote ambapo ina kasoro.

Alisema isingekuwa rahisi kuweka maoni ya kila mtu katika Katiba, na kufafanua kuwa yale ambayo hayajawekwa sasa hivi, utafika wakati wake na yatawekwa.

Alibainisha kuwa haikuwa rahisi kwa maoni ya kila mtu kuingia katika Katiba Inayopendekezwa, kwani hata CCM ilikuwa na mambo 60 waliyopendekeza, lakini kati ya hayo ni 12 tu yaliyoingia.

Rais Kikwete alisema Katiba sio Msahafu au Kurani, ambayo haiwezekani kubadilishwa hata nukta. Alitoa mfano wa Zanzibar, kwamba wakati kuunda Muungano, yapo mambo yalionekana ni muhimu kubakia katika Muungano, lakini kadri muda ulivyokwenda yameondoka.

Jukwaa la Wakristo

Akizungumzia tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania, Rais Kikwete alisema amehuzunishwa na kufadhaishwa na tamko hilo la viongozi wa dini la kutaka waumini wao wajiandikishe kwa wingi, lakini wapige kura ya Hapana kwa Katiba Inayopendekezwa.

Tamko hilo lilitolewa na jukwaa hilo linaloundwa na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT).

Rais Kikwete alisema, tamko hilo litakuwa pia limekwaza waumini, kwa kuwawekea mipaka ya kidemokrasia na kukwaza hata viongozi wenyewe.

Alitoa mfano kwamba kwa tamko hilo, muumini hataweza kusimama na kumwambia kiongozi wa dini asiwaingilie katika uamuzi, kwa kuwa kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila mtu, na ikitokea hivyo, hata kiongozi husika atakwazika.

Subira kwa NEC

Kuhusu uwezekano wa Kura ya Maoni kufanyika Aprili 30 kama ilivyotangazwa na Serikali, huku kazi ya kuandikisha wapigakura ikiendelea kusuasua, Rais Kikwete alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inayoratibu uandikishaji wa wapigakura, itazungumza kuhusu walipofikia wakati muafaka ukifika.

Amani Kuhusu amani ya nchi, Rais Kikwete alisema viongozi wa dini pia wa jukumu kubwa la kuimarisha amani ya nchi.

Katika utekelezaji wa jukumu hilo, Rais Kikwete aliwataka viongozi hao wajaribu kuepuka kutumiwa na watu wenye nia mbaya, kwa sababu wanafahamu kuwa viongozi wa dini wana ushawishi katika jamii na wana watu wengi nyuma yao.

Alisema machafuko yatakayotokana na mvurugano wa kidini, hakuna mtu atakayeweza kuyazuia, hivyo ni vyema viongozi hao waendeleze mshikamano.

Alitoa mwito kwa mikoa mingine nchini, kuunda kamati za amani kama ilivyo Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini mkoani Dar es Salaam.

Kadhi yuko Kibiblia

Akitoa neno la shukrani, Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Askofu Valentino Mokiwa wa Kanisa Anglikana Tanzania, alielezea kufurahishwa na maelezo ya kina yaliyotolewa na Rais Kikwete.

Alisema pia alifurahishwa na maneno aliyonukuu Shehe Alhad kutoka Mathayo 5:25 yaliyoonesha kwamba kumbe Mahakama ya Kadhi ni ya Wakristo, maana ipo katika Biblia, na kufanya ukumbi uvunjike kwa kicheko.

CHANZO: HABARI LEO

Advertisements

23 thoughts on “Raisi Kikwete azungumzia mahakama ya Kadhi!

 1. Servant, hakuna jipya kwa sababu umeshazoea KUOGELEA KWENYE MAJI MACHAFU (KUGAAGAA MATOPENI).
  Siku moja utajua hiyo WAGALATIA 1:8-9 ni laana isiyo na sababu, wala usipate shida,endelea kugaagaa matopeni.

 2. Hakuna jipya kutoka kwako…..”Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu”

 3. Servant, wakati unakuja utaposhindwa kukenua meno yako.Kama wewe ni ” Servant” wa Ibilisi huna budi kucheka kwa sababu NENO LA MUNGU kwako ni la kufanyia mzaha.
  Umenukuu andiko hili,2Timo 3:5 “…wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake..” ukijirelea wewe na WALUTHERI wenzako kuonesha jinsi mlivyo mbali na ufalme wa Mungu mkiyashika MAPOKEO YA WAZEE na KANUNI ZA IMANI zilizoasisiwa kwenye BARAZA LA NIKEA mwaka 325 A.D.
  Ni kweli mna mfano wa UTAUWA,mna MAASKOFU wakuuu, Wachungaji wenu Huvaa KOLA na MAJOHO meupe kuonesha “utakatifu bandia”,Kwaya zimevikwa MAJOHO kuonesha aina ya “malaika warukao”, Mnaimba liturugia na Kuongozwa na KALENDA YA DAYOSISI, mnabatiza watoto na kuwapa “kipa dhaifu” wakiwa watu wazima…….nk.
  Endelea kucheka, lakini tambua UMELAANIWA kwa mafundisho yako MFU.
  WAGALATIA 1:8-9 ” 8 Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.
  9 Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”

 4. hahaha…..Pendael kuna wakati unanifurahisha sana ndio mawazo yako na hivyo yapokelewa mwenye kuyachambua atagundua Ndugu unajichanganya mwenyewe…na ndio maana unakuwa ueleweki
  2Timo 3:5 “…wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake..”

 5. Ukimuuliza m-K.K.K.T, suala la ubatizo, labda muulize kuhusu kubatiza watoto.
  Lakini ukimhoji kuhusu suala la kubatiza kwa jina la Yesu au kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt. ni kujaribu kuukata mti ambao hata wewe umepanda juu yake.

  Pendael, naamini hata wewe mchungaji wako au wewe mwenyewe umebatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho mt., kama si kweli thibitisha hapa kuwa si kweli.

  Hili suala la ubatizo tulishalijadili hapa, lakini bila shaka hatukuhitimisha. Lakini yako mambo ya kijiuliza kwanza kabla ya mtu kuweka msimamo kuwa kuna mmoja kakosea.

  Swali la kwanza la kujiuliza ni je, Yesu alikuwa nabii, je alikuwa mtume? Kwa mimi nijuavyo, jibu ni ndiyo.

  Yeyote anayesema kuwa Petro na mitume walibatiza kwa jina la Yesu, kilichonyuma wa hoja yake ni kwamba, imani yetu imejengwa katika misingi ya mitume na manabii, hivyo kama wao walibatiza kwa jina la Yesu tu inabidi nasi tubatize hivyohivyo.

  Ok, lakini Yesu akiwa kama nabii mkuu, na mtume mkuu, ndiye aliyetoa agizo la kubatiza akisema: -Therefore go and make disciples of all nations, baptizing them in the name of the Father and of the Son and of the Holy Spirit,
  :- Mt 28:19)

  Lakini kwa habari ya kufukuza mapepo, na kuponya wagonjwa, Yesu alisema wazi pia, kuwa kwa jina langu watatoa pepo (Mark 16:17). Kwa nini hakusema kuwa kwa jina Baba, na Mwana, na la Roho mt.watafukuza pepo?

  Ukumbuke pia, kuna suala la kubatizwa kwa Roho na kwa moto

  Sasa ukirukia tu kusema kuwa anayebatiza kwa jina la Baba, Mwana , na Roho mt.anakosea, au aliyebatiza kwa jina la Yesu pekee alikosea, mimi nitakuuliza anakosea/alikosea nini wakati anachokifanya kimeagizwa kwenye maandiko, kama ambavyo anayebatiza kwa jina la Yesu anafanya ambacho pia kwenye maandiko kilifanyika?

  Baba ndani ya mwana, mwana ndani ya Roho mt, na Roho mt. ndani ya Baba,
  udhihirisho wake duniani ni YESU.

  Ukisema Baba, Mwana, Roho mt, sawasawa na umesema Yesu, ukisema Yesu sawasawa na umesema Baba, Mwana, Roho mt.
  Kwa sababu katika Mwana ndimo unamotimia u-Baba wote.

 6. Servant,Unazidi kujibainisha wewe ni ‘SERVANT’ wa nani.Uliongea kwa sababu ya Mhemko tu.Umesema nipo hapa SG kutafuta Wafuasi, hujafikiri vya kutosha kuhusu hilo la .K.K.K.T kupitia wewe ambaye ni WAKALA, imeshajitangaza kwa biashara ya washirika hapa SG na kwingineko.Ndio maana Ulipata shida ya kutambua ninapoabudu kwa sababu sitangazi biashara ya kutafuta Washirika (Wateja) kama wewe.Umese nimalizie na ‘kamsemo kangu’ japo haya ni madharau lakini Msemo huu ni kweli tupu na pengine siku moja utakutana nao hukumuni.Ikiwa Umebatizwa ukiwa MTOTO tena kwa VYEO vya BABA, MWANA na ROHO MTAKATIFU, nafsi yako ingali ina Dhambi kwani Biblia imesema hivyo. MATENDO 2:38 ” Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa Jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”.Haya, K.K.K.T wanabatiza kwa kufuata kanuni hii ya MATENDO 2:38? ‘Mungu ahiremu nafsi yako yenye dhambi ‘

 7. Pendael,
  Ngoja ñiseme na hiki, umesema kuwa sina mamlaka ya kukuaia ujitoe kwenye mijadala ya SG.

  Nafikiri hapo umelipuka tu rafiki; mamlaka ya kukwambia ujiondoe ninayo, na ndio maana nimekwambia tayari. Sasa utasemaje kuwa sina mamlaka ya kukwambia wakati tayari nshakwambia?

  Labda sema hivi, sina mamlaka ya kukutoa SG. Lakini hata ningekuwa nayo, kwa nini nikutoe wakati uko hapa kujifunza, na ninakuona kabisa unahitaji kujifunza?

  Lakini ukweli ni kwamba kama wewe hupendi kukosolewa, kuhojiwa, na kupingwa kutokana na unachokisema, basi jitoe, lakini ukiendelea kuwepo na ukasema kitu kisicho tutakukosoa tu na kukupinga.

  Ndo hivyo Pendael!

 8. “Kila mtu kwenye jukwaa hili akiwa anaeleza mtazamo ulio kinyume na wewe unavyotazama ni MPINGA KRISTO…..hapo ndipo unapofanya ni sikuelewi kabisa
  Yuda 1:10 Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama wanyama wasio na akili.”
  -Usitake shauri lako na mtazamo wako watu wote waufuate kwa kuwa ndicho unachoamini wewe
  -Nna wasiwasi hata hapa SG hupo kutafutatafuta wafuasi kama sikosei waumini wa mtazamo wako. sababu hata kama mada isingehusu lile unalosimamia pasipo kuwa na ufahamu nalo huwa unajaribu kupachikapachika mtazamo wako ili ujadiliwe
  -malizia kabisa na kale ka msemo wako wa kujiinua “Mungu airehemu nafsi yako yenye dhambi” sababu tu watu hawasimami na yale unayoamini wewe na wewe peke yako ndio unaenda mbinguni

 9. Sawa Pendael,

  Vyovyote utakavyoamua kuniita; mjinga, kibarua, mpinga kristo, no one who cares!.
  Ukweli utabaki palepale kuwa umesema uongo ambao huna namna ya kuukana.

  Lakini pia hujui kujadili ispokuwa unachokijua ni ku- opinionate, hasa wale ambao huwako imara sana kihoja.

  Mnaobanwa kwa hoja no kawaida yenu kuanza kuita wengine kuwa waounga kristo. Huo nao ni ujinga tu kama zilivyo tu aina zingine za ujinga wa kutoyaelewa maandiko sawasawa.

  Kwani wewe ndo kristo mpaka uniite mpinga kristo? Maana mimi ninekupinga wewe na mawazo yako mapesi lakini unalazimisha kuyapa uzito usiokuwepo.

  Pendael hujui kujenga hoja ambazo zitaendana na maandiko unayojaribu kuyatumia kuzithibitisha.

  Kunukuu andiko out of its essence ni udhaifu ambao watu wengi wenye kuchukulia mambo kirahisirahisi wanao.

  Siyo kule kunukuu andiko fulani kunakoleta maana ya wewe kujua maandiko, bali ni kule kutumia maandiko sahihi kiusahihi mahali sahihi ndiko huleta maana ya wewe kujua naandiko.

  Pendael, ukisema jambo ktk usahihi wake, nitakupongeza, lakini ukitudanganya na kuongea kiholelaholela nitakukatalia tu lazima, upende usipenda.

  Habari ndo hiyo pendael, wala usikasirike, mjadala unaendelea!

  Habari ndo hiyo Pendael.

  Asante .

 10. Sungura,Umenifanya nikuandikie yafuatayo; 1.Wewe huna MAMLAKA YOYOTE ya kuniambia nijitoe/nijiondoe SG kwa sababu ya kukataa kujibu hoja zako ZISIZO na maana, wewe ni kama Kibarua anayeishi kwa hasara.2 BIBLI inasema MPUMBAVU Umjibu kutokana na Upumbavu wake; hivyo kwa kuwa umeniambia “Una dhehebu” ,dumu ukijua ninalo lile ulilonipa.3.Kwenye ile Mada ya MAKUNDI NDANI YA WATU WALIOKOKA nilikuambia mambo mengi, na ni pamoja na kuwa wewe U KIPOFU,MNYONGE,UCHI NAWE HUJUI, hiyo ni kulingana UFUNUO 3:14-22.4 Kumbuka kuwa UBONGO wako ni kama Punje ya karanga, hivyo unapaswa kuongeo kwa TAHADHARI kwani Mimi SIWAOGOPI WAPINGA KRISTO.

 11. Pendael,

  Kama unataka kila mtu ajibu hoja zako kama wewe unatakavyo basi jukwaa hili halikufai. Ukiandika kisicho sahihi lazima tutukuhoji na tukwambie hakiko sahihi. Kubishana kwa maana ya kujadili kila mtu akitoa mawazo yake ambayo yanaweza kutofautiana na ya mwingine ndo msingi wa majadiliano yetu hapa.

  Sijakulazimisha kujibu hoja zangu kama huna majibu, unaweza tu ukachapa lapa ndugu yangu. Lakini msimgi wetu hapa ndio huo. Huwa tunajadili jambo hata mwaka mzima mpaka tupate jibu linalofaa au tukosejibu hivyo tuamue kutokukubaliana.

  Sasa wewe hulka yako kama ni kutotaka kuhojiwa na kukosolewa jukwaa hili halikufai. Tuache tuliozoea kuhoji na kuhojiwa na kutakiwa kutoa majibu ya tulichokisema.

  Kama wewe ulikuwa hujui kuwa huwezi kulitetea kanisa basi sasa unajua, maana hata ukitaka kulitetea hutaweza, kama ulikuwa hujui nafasi ya madhehebu katika hii nchi basi sasa unajua, na kwamba hata wewe uko kwenye moja ya madhehebu.

  Binafsi siwezi nikakuacha tu unaongea kitu ambacho si sahihi bila kukwambia kuwa hakiko sahihi au ukithibitishe. Hata kama hutajibu hoja zangu, acha, lakini kukwambia nitakwambia tu.

  Nimekwambia ututhibitishie kuwa wewe hauko kwenye dhehebu, unaanza kugwayagwaya na kulalamika,lakini maadamu umeamua kutoa hoja zako hapa jukwaani bila shaka ulijithibitisha kuwa una kitu unachokijua, na ndicho hicho ninakutaka ukithibitishe, vinginevyo ukubali kuwa umesema uongo Pendael!

  Do away with domineering spirit Pendael!!

 12. Servant
  Umeandika“Mwapotea sababu hamyafahamu maandiko”,hayo ni YESU aliyasema,ndipo ungekuwa unajua MAANA YAKE wala Usingekuwa MLUTHERI.

 13. Sungura, naona umeanza kuongea mambo yasiyo na maana kwangu.Hivi mtu kulitetea KANISA inamaanisha ni la Kwake?Sikulaumu kwa sababu ndivyo nafsi yako ilivyo na ndivyo ulivyo hasa. Jambo hili nishajibizana nawe sana kwenye Mada “MSIOGOPE VITISHO VYA WANATHEOLOJIA” na “MAKUNDI NDANI YA WALIOOOKOKA”. Ulishazoea kubishana/kushindana, hivyo SINA MUDA WA KUPOTEZA KUJIBIZANA NA WEWE.
  SHIKA SANA ULICHONACHO…..

 14. Sikia Pendael,

  Wewe huwezi akalitetea kanisa maana siyo la kwako, yuko mwenye kanisa ndiye anayelitetea. Au wewe ndiye kichwa cha kanisa mpaka ulitetee? Acha hayo maneno mepesi ya kusema vivi hivi.

  Usijaribu kuongea manene yasiyo na substance kwa ajili ya kushinda mjadala, aongea vitu ambavyo vina ithibati na uhalisia. Wewe tetea imani yako tu ili umalize mwendo salama, lakini kanisa huwezi kulitetea wewe.

  Na tena unapokaza kusema kuwa wewe hauna dhehebu, huko nako ni kuleta utoto usio na tija katika mambo ya msingi. Hebu thibitisha kuwa wewe hauna dhehebu just kwa kutuambia huwa unakusanyika wapi na mchungaji wako ni nani, hiyo itatosha kuthibitisha kuwa kweli wewe huna dhehebu.

  Ninyi ndo husema kuwa hamna dini, lakini mkiwa mnajaza documents sehemu ya dini mnasema ni wakristo. ….?????

  Kuna vitu vya msingi vya kuambizana hapa ambavyo hatupaswi kuwa navyo amabvyo ni udhehebu, udini, kama ambavyo hata wewe una kabilalakini hupaswi kuwa mkabila.
  Lakini hata neno ukristo sidhani kama liko sawa.
  Kwanza ni jina lilioitwa na watu, lakini pia inatosha mimi kuitwa ‘wa-kristo na wewe kuitwa hivyo hivyo ‘wa-kristo, kwa mujibu wa muundo wa ngeli yake.

  Kwa hiyo hata wewe kujivunia ukristo si kitu cha maana sana maana si Mungu aliyelitunga hilo jina bali ni watu kutokana na mtazamo wao. Kwa hiyo kuitwa wa-kristo hai-add value ya maana sana, maana naweza leo nikaamua kujiita ‘wa-yesu (myesu), ispokuwa cha msingi ni mimi/wewe kuwa mwanafunzi wa Yesu.

  Halafu unatuambia kuwa majina ya madhehebu ni majina ya makufuru, kwa kigezo gani Pendael, kama si kuandika tu vitu kwa sababu mtu una ufundi wa kupangilia sentensi? Ni andiko gani limesema kuwa majina ya madhebu ni majina ya makufuru, au unataka kutuambia kuwa maana ya kilichosemwa kwenye Ufunuo 17:3 yaani kwamba yale majina aliyojaa yule mwanamke ni madhehebu, kivipi kaka?

  Pendael, tuongee mambo kwa uhalisia!!

 15. Servant, kama ulivyosema mwanzoni unapata shida kunielewa hata sasa nimeamini bado hunielewi (hatuelewani lugha). Nilikuuliza swali kuwa;KANISA NA DHEHEBU ni kitu kimoja?Hukujibu hilo swali kwani lingefungua uelewa wako.Hiyo K.B.Y.K umeipata wapi?Ulishawahi kusikia Kanisa linaitwa K.B.Y.K au umetunga ili nifanane na wewe (K.K.K.T)? Msingi wa imani yetu ni BIBLIA,haya ni baadhi ya kile tunachoamini. 1.Ubatizo ni kwa Watu wazima( si watoto), na ni KWA JINA LA YESU KRISTO (MATENDO 2:38-39, 8:14-17, 10:48, 19:1-5, WAKOLOSAI 3:17) .2.Hatuamini kwamba Mungu ana NAFSI 3,bali tunamwamini Mungu mwenye nafsi 1 ( WAEBRANIA 6:13 ambaye Jina lake ni Bwana Yesu Kristo.3.Tunaamini kuwa Wanawake hapaswi kufundisha wala kutawala Wanaume wala haruhusiwi kushika huduma yoyote ndani ya Kanisa la Mungu, 1 TIMOTHEO 2:8-15, 1WAKORINTHO 14:34-36, 1TIMOTHEO 3:1-13). 4 Tunaamini kuwa Shetani ndiye aliyeanzisha Madhehebu ili kutenganisha WAKRISTO (kuvunja umoja wa Roho) 1WAKORINTHO 1:4-9, 1 WAKORINTHO 14:33). 5Tunaamini kuwa BIBLIA ni NENO LA MUNGU na ndani yake hakuna hata neno moja la mwanadamu UFUNUO 22:18-19).6Tunaamini kuwa Baraza la Makanisa Ulimwenguni ndio ALAMA YA MNYAMA.Hayo ni baadhi tu ya Mambo unayoweza kulinganisha na yaliyoko K.K.K.T.

 16. Pendael
  ok linaitwa kanisa la bwana yesu kristo K.b.y.k (kama ni kwa kifupi) hata mimi linaitwa kanisa la kiinjilisti la kirutheri Tanzania (K.k.k.t) lakini usharika wetu hupo mapipa sijajua wewe usharika au kusanyiko lenu kwa mkoa uliopo ni wapi au lilipo huko ulipo tu

 17. Servant, hebu tafakari KANISA na DHEHEBU ni kitu kimoja?Ni hali ya kawaida kumwelewa mtu fulani au kutomwelewa.Hata wewe, si kila mtu anakuelewa, hata mimi kuna mahali nashindwa kukuelewa.BWANA YESU KRISTO hakueleweka na kila mtu karibia kila NENO alilosema bali WATEULE tu ndio waliomwelewa. Kwa mfano BWANA YESU alisema ” Msipokula mwili wangu na kuinywa Damu yangu…”,jamaa walikimbia kwa kutoelewa alichomaanisha,nk..MITUME na MANABII hawakueleweka na kila mtu bali WATEULE tu ndio waliojaliwa kuwaelewa.Kama ukifuatilia kwa makini kuna kitu utaelewa tu hata kama hutaifuata.Kwa Kifupi Mimi ninamwabudu Mungu katika Kanisa la Bwana Yesu Kristo (si Dhehebu).Pia katika Biblia nzima hakuna Wanaitwa Walutheran,Waanglikana,Wapentekoste,Wabatisti,Wamethodisti,Wakataloki,Wapresibitarian..nk, haya majina yanaitwa Majina ya MAKUFURU kulingana na UFUNUO 17:3. Pia, Wanafunzi Wa Yesu Kristo Waliitwa WAKRISTO, MATENDO 11:26 “……..Na Wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia”.Sina Dhehebu kwa sababu YESU KRISTO na Wanafunzi wake hawakuwa nalo.

 18. Pendael
  huwA sIKUelewagi nini unachamaanisha mimi nikisema naabudu kanisa la kiinjilisti la kirutheri tanzania (kkkt) kwa hiyo wewe unaabudu kanisa la kanisa…

 19. Hapana Pendael,

  Unachokisema siyo kweli.

  Ni maandiko gani yaliyotimia ambayo unasema leo yametimia, yametimia kwa kigezo gani sasa?

  Wewe hauko kwenye dhehebu, huwa unakusanyika wapi, chini ya mti au nyumbani kwako?

  Tuongeeni mambo hapa kwa uhalisia, siyo kwa kujificha katika maandiko huku tukikosea kuyafasiri. Unapomwambia mtu atoke kwenye dhehebu halafu ukakomea tu hapo, akiwa mchanga lazima umchanganye na kumpoteza.Maana atajiuliza je, atoke Pentekoste aende Aglikana, au atoke anglikana aende Lutherani, n.k? Maana hayo ndio madhehebu.

  Lakini cha ajabu wewe mwenyewe unaemwambia hivyo uko kwenye dhehebu, na jana tu ulikuwa umekusanyika kwenye hilo dhehebu mkimwabudu Mungu,sasa hapo si ni kujichanganya!!

  Hakuna namna kwenye hili taifa utakusanyika publicly kusali bila kuwa katika mfumo wa dhehebu, na dhehebu halina tatizo lolote. Chenye matatizo ni vichwa (mindset) vya watu walio ndani ya hayo madhehebu.

  Ndio hivyo!

 20. Hii hatari, shehe anasema “Waislamu na Wakristo ni wamoja”!Nadhani sentensi sahihi ni “Madhehebu ya wanaojiita wakristo na Waislamu ni wamoja”.Askofu naye akasema “….kumbe mahakama ya kadhi n4 ya Wakristo….”.Hii ni ‘special’ kwa WAKRISTO TU, 2WAKORINTHO 6:14-18 ” Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza.15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari (ufisadi)?16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.17 Kwa hiyo,Tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.18 Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi” WAPENDWA yakimbieni maanguko ya kuta za Babeli (Madhehebu),ikimbieni ghadhabu ya Mungu.Hii ni dalili tosha ya kuja/kurudi kwa KRISTO kwa mara ya Pili,tubu ubatizwe Kwa JINA LA YESU KRISTO ili uwe Mkristo (MATENDO 2:38-39),toka katika hayo Madhehebu.Kwa kweli,LEO HII MAANDIKO HAYA YAMETIMIA.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s