Matukio ya kutisha yanayotokea duniani!!

Kumekuwa na matukio mengi yanayoendelea duniani, hakuna amani ya kweli na vifo vya ajabu hutokea, nchi nyingine wakristo wanauawa na pengine kutengwa!!. Je kuna haja ya wakristo kufundishwa kuhusu nyakati za mwisho? Mafundisho mengi hivi sasa ni kuhusu matumaini, mafanikio na hata mara nyingi watumishi kutosimamia kweli ya Kristo. Una mawazo gani? Je kanisa lifundishwe kuhusu Nyakati za Mwisho?

8 thoughts on “Matukio ya kutisha yanayotokea duniani!!

 1. Ndugu zangu,
  Tunasoma, tunatazama vyombo vya habari na pengine kushuhudia Wakristo wa kichinjwa na kuchukiwa potepote Duniani. Taasisi mbali mbali na juhudi za kimataifa zimefanywa ili kukomesha jambo hili, lakini uzoefu na uhalisia unatuambia na kutuonyesha wazi kwamba, mwanadamu ameshindwa kabisa kukomesha jambo hili. Na kwa msemo mzuri ni kwamba, mwanadamu ameshindwa kujilinda na badala yake anatengeneza mbinu “nzuri” zaidi ili aweze kujiangamiza mwenyewe!

  Si hivyo tu, watoto nao si watii tena na hawana heshima kwa wazee waoa, Watoto hawawapendi wazazi na wazazi upendo kwa watoto wao haupo tena, kusingiziana kati ya vijana na wazee, vijana kuona kwamba wao ndiyo bora na wanaufahamu zaidi ya wazee wao, hakuna yeyote anayejihusisha na kuwatunza ama kuwasaidia wazee na wasiojiweza, lakini Biblia inasema “Taifa lisilo na wazee halina ‘Baraka’!” Vijana wengi kupenda vurugu, kushabikia mabaya na kutopenda kazi, maandamano na tamaa za wanasiasa, wazazi kutelekeza familia, wakimbizi kuzikimbia nchi zao, njaa na kiu, ubinafsi na uchoyo, wizi na dhuruma, kupenda pesa kuliko kumpenda Mungu, watu wakali, watu kutojizuia na hawana kiasi, watu wasio na ‘tafadhali’ mioyoni mwao, kutokuwa na shukurani ama kuoneana huruma, wahubiri wa injili ya uongo, matetemeko ya nchi na mafuriko, vita na viongozi kung’ang’ania madaraka, watu kutojari mapatano. Tamaa za wanaojiita wachungaji za kutawara kisiasa,uongo wa waziwazi na ule wa kupitia simu na aina nyingine za mitandao, ulevi kila mahali, ukahaba wa kupindukia, kukosa aibu na woga wa kutenda ubaya, kupotea kwa amani, fitina n.k.

  Sambamba na mambo hapo juu; ipo habari ya kuuawa kwa Wakristo kwa pamoja vina lengo moja tu, yaani Dunia hii iishe!, Mambo haya yote ni sharti yatokee, ili Neno lote lililomo katika Biblia ambayo ni Neno la kweli la Mungu mwenyewe, litimie!

  Je, wakristo wafanye maombi ili mauji na ukiuwakwaji wa haki za kuabdu zikomeshwe? Ukweli ni kwamba, Mungu hatasikiliza maombi kama hayo! Kwa sababu, Mungu hulichunguza Neno lake apate kulitimiza; hivyo basi, maombi yajibiwayo ni lazima yawe ndani ya Neno la Mungu (mapenzi ya Mungu). Kwakuwa Neno la Mungu linasema wauaji na usaliti unaofanywa kwa wakristo ni tamko la Mungu mwenyewe kuwa ‘WATAWAUA WAKRISTO’ basi ni lazima iwe hivyo, mambo yote yatapita lakini si Neno la Mungu. Kwa hiyo, omba uombavyo, funga ufungavyo lakini wakristo watachukiwa na hata kuuawa na walimwengu, maana hilo ndilo elekezo la Neno la Mungu.

  Biblia imeeleza wazi kuwa, wakristo walio wafuasi wa kweli wa Yesu kristo ni lazima wengi wao wachukiwe na walimwengu na baadhi yao kuuawa! Ukisoma katika Mathayo 24:9-10 inasema, “Ndipo mtasalitiwa, ili mteswe na kuuawa, nanyi mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili yangu. Wakati huo, wengi wataacha imani yao, nao watasalitiana kila mmoja na mwenzake na kuchukiana. Kusalitiwa kwa wakristo na ukristo, kusalitiana wao kwa wao kiimani, kuuawa kwa wakristo na kuchukiana wao kwa wao, kunatokana na ukweli huo hapo!

  Ujue na uelewe kuwa ufahamu ni chembe ya Uhai! Biblia inazidi kusema kuwa, Yesu aliwajurisha wanafunzi wake mapema kuwa watapatwa mateso, ili wakristo wawe na taarifa, alisema, “Lakini nimewaambia ninyi mambo haya, ili saa hiyo ikiwadia mpate kumkumbuka ya kuwa nilikuwa nimewaambia.”
  Ikiwa taarifa tayari tunayo kuwa tutauawa kwa ajiri ya Kristo, basi, ni bora sana . Hofu haina nafasi kwa mkristo kwa sababu, kufa ni faida na kuishi ni Kristo! LAKINI KUMLILIA MUNGU ASITISHE JAMBO LILE, BADALA YA KUMUOMBA AKUMBUKE ULE MPANGO WAKE WA KUFUPISHA WAKATI WA MWENDELEZO WA TUKIO HILO, NI KUMPINGA KRISTO!” Kwa hiyo wakristo wanapaswa wajitie moyo na kusonga mbele kwa kuwa watakumbuka pia kwamba, hata kiongozi wao mkuu (YESU) alitendewa hivyo na watu wa dini za kilimwengu, hivyo nao wajue kuwa, kupitia kifo ama mateso kwa sababu ya ukristo si ajabu wala si mkosi au bahati mbaya, bali ni mpango na makusudi ya Mungu mwenyewe!

  Labda ni kwanini wakristo wanachukiwa na wanauawa? Wakristo wanachukiwa na hata kuuawa kwa sababu wao si wa ulimwengu huu, kama ambavyo Bwana wao Yesu kristo hakuwa wa ulimwengu huu.
  Biblia inasema kuwa kwa kupitia mateso hayo, watu wataikana imani, na kwakuwa Mungu anatafuta waamini wa Imani wa kweli na wenye kumuabudu katika Roho na kweli basi, kuuawa huko na kuteseka huko kutafanya mchujo ili wapatikane wakristo wa kweli!
  (Ufahamu ni chembe ya Uhai!)

 2. Amen Mjema mimi naungana na wewe kabisa. Mimi nimekuwa nikiabudu kwenye kanisa moja kubwa sana hapa Tanzania na huenda Africa mashariki lakini hakuna nguvu ya Mungu hata kidogo tumeishia kupamba kanisa tuu, wakati watu wanapaswa kuhubiriwa injili halisi kuwa hizi ni siku za mwisho lkn sivyo.

 3. ……mafundisho yawepo na watu wakumbushwe ili muda wote waishi maisha ya toba…..na pia ili imani zetu zisipungie kwa vitisho vya ulimwengu huu….sisi tuwe watu wa ulimwengu ujao ambao tumeandaliwa na Bwana Yesu….
  ….na haya tuone na tuzidi kuiamini biblia maana haya yote yametabiliwa……

 4. kuna umuhimu wa wakristo kufundishwa kutambua nyakati za mwisho badala ya matumaini,mafanikio na utajiri

 5. Nionavyo mimi,

  Kwanza, haya matukio si kwanza kutokea kwa wakristo duniani, hata kwa kanisa la kwanza.

  Lakini naomba kutofautiana kidogo na Sebastian(mleta mada), na niungane kwa sehemu kubwa na Mjema:

  Natofautiana kidogo na Seba katika suala la mkakati wa kimwili wa wakristo kujilinda. Hatuwezi kuwa na mkakati wowote wa kimwili wa kujilinda katika hivi vita, vinginevyo ndo tunataka sasa kupigwa zaidi. Islam ambayo inazaa huu ugaidi ni spirit ambayo iko kwenye operation, hatuwezi kama wakristo kupambana nayo kimwili tukaweza. Tunayoyafanya kimwili yanatakiwa kuwa maelekezo toka rohoni, ndipo tunaweza kushinda (vita vyetu kama kanisa si vya damu na nyama).

  Mwislam kama mwislam ni mtu mzuri tu, tatizo ni spirit iliyo ndani ya imani yake

  Naungana kwa sehemu kubwa na Mjema katika suala la maombi. Matokeo ya maombi(kazi ya ulimwengu wa roho), huleta madhara yake mpaka kwenye ulimwengu wa mwili. Yaani nguvu inayozaliwa na maombi ina uwezo wa kumstopisha gaidi kama inavyoweza kumstopisha mchawi.

  Na ninashawishika kuamini kuwa kanisa haliombi kama lilivyokuwa miaka ya nyuma. Mimi kuona kiwango cha uchawi Tanzania kinaongezeka, mauaji yenye kuhusishwa na ushirikina yanaongezeka ni ishara kuwa kanisa haliko sawa kwenye eneo la maombi.

  Islam ni roho ambayo inafanya kazi pamoja na majini na mapepo, hivyo kanisa litakapoamua kufocus kwenye maombi ya kusabaratisha hiyo roho, lazima spirit ya kujitoa muhanga itapungua kama si kwisha kabisa.

  Mimi naamini kuwa hakuna mwislam yeyote serious ambaye hana pepo au jini ndani yake, hayupo.

  Mimi naomba kama kuna mtu uko karibu na msikiti au familia ya mwislam kwelikweli, jiweke sawa kabisa, kisha fanya mkakati wa maombi yenye makusudi dhidi ya spirit zinazofanya kazi nyuma yao, halafu utatuambia hapa matokeo yatakayojiri.

  Kuna mwaka m fulani Bonke alikwenda kuhubiri Mombasa, wiki mbili kabla ya mkutano kuanza, usiku zilikuwa zinasikika sauti za majini zikisema ”aise jamaa amekaribia kuja, tuondokeni”

  Mimi leo siuoni utendaji wa kanisa ule wa kutisha na kuwasha masikio angalao kama hapo zamani kidogo, sioni ishara na maajabu vikitokea. Leo watu wanashangaa muujiza wa pepo kumtoka mtu, mtu kupona malaria, mtu kupa gari, n.k.

  Lakini naamni tukiharibu nguvu za majini, tukawaponya wagonjwa wao, tukawaponya viwete wao, wakayaona matendo makuu ya Mungu wetu, hakuna atakayepata nguvu ya kufanya ugaidi wa namna hii.

  Kwa kifupi, revival is on high demand!!

 6. Haitoshi kufundisha habari za nyakati za mwisho pekee naamini wakristo wengi wanauelewa kuhusu nyakati za mwisho, kwa maoni yangu wakristo tumefanikiwa sana katika maeneo mengi hasa katika ulimwengu wa Roho namna ya kupambana na hila za shetani na baada ya shetani kuona kuwa tumemshinda katika eneo hilo akagundua kuwa tunamapungufu katika eneo la ulimwengu halisi ‘physical world’hivyo wakristo lazima tuwe na mtazamo mwingine katika eneo hili yaani vita halisi katika ulimwengu huu wa mwili.
  Nadhani hawa wenzetu wanachofanya nikuweka vitisho kwa jamii ya Wakristo na wale wanaotamani kuwa wakisto waone kuwa ukristo si salama tena na kuwa katika dini hii ni kujitakia kifo na hivyo kuufuta ukristo duniani.
  Viongozi wa dini watafakari ni namna gani wakristo wawe katika hali ya amani wanapofanya ibada zao.Nguvu zinazotumika katika kupigana katika ulimwengu wa Roho pia zitumike katika ulimwengu wa mwili.Si maanishi wakristo wajitoe muhanga au waanzishe vikundi kama za Alshabab hapana bali tuwe na strategic thinking on security issues kwenye makusanyiko yetu.

 7. Kadri hofu ya Mungu inavyozidi kupungua mioyoni mwa wanadamu, ndivyo maovu yanavyoongezeka. Siku zinazokuja, yataongezeka zaidi ya haya tunayoyaona le!! Huu ni upepo tu, mvua bado!!

 8. Wapendwa Bwana Yesu apewe sifa,

  Pamoja na udhahiri wa matukio ya siku za mwisho.bado weng wetu ndani na nje ya kanisa wamelala usingizi fofofo! hawana macho ya utambuzi/ya kiroho kujua kuwa ni hv punde Yesu yuaja.

  Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Yesu,licha ya kuarifiwa mapema kuhusu kifo na ufufuo wa Bwana wao,bado hawakuwa tayari mara hayo yalipotokea.

  Wapendwa licha ya kujua ukweli wa matukio haya tusipokesha ktk kuomba na kudumisha ushirika wetu na Roho Mtakatifu,atatujia km vile mwivi kwa sindano ya ganzi tuliyochomwa na uyo adui ni masumbufu ya maisha haya-kutafuta mali utajiri na heshima-upumbaza sana haya.

  Ujumbe wa kizazi hiki wapaswa kuwa:

  1.Watumishi wa Mungu wafundishe Injili ya milele-watu waache dhambi na utauwa wa kweli maishani maana saa ya hukumu yake imekuja. Kama inavyopatikana ktk ufunuo 14:6-18- ujumbe wa malaika watatu.

  2.watu wasipewe injili nyepesi nyepesi tu-miujiza,uponyaji,utajirisho.kiini cha Injili kiwe- kuutafuta ufalme wake na hayo mengne yote watazidishiwa.

  Tudumuni ktk kuomba na kufuata ushauri wa ufunuo 3-tununue dawa ya macho-Roho Mtakatifu.

  Mbarikiwe.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s