Semina ya Mwl Mwakasege Dodoma


SOMO: FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA BARAKA ZA AGANO NA MUNGU

Neno kuu: Eph 1:3

SIKU YA KWANZA.

LENGO: Kukusaidia uzidi kufaidika na baraka zinazopatikana ndani ya imani uliyonayo katika Kristo Yesu.
🔹Kutokuwa na msukumo wa kuwashuhudia wengine habari za Yesu ni dalili ya kutokuridhika na wokovu.
🔹Usipoona faida ya kuwa ndani ya Yesu huwezi kupata msukumo ndani yako wa kushuhudia wengine.

MSISITIZO: BARAKA ZA AGANO. Msisitizo zaidi kwenye agano lenyewe.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA (MSINGI)

1. Mungu anaweza kumbariki mtu nje/ ndani ya agano naye. Mwanzo 17:15-21
🔹Ishmael alibarikiwa na Mungu nje ya agano.
🔹Isaka alibarikiwa na Mungu ndani ya agano.

2. Unaweza ukawa ndani ya agano na Mungu na usifaidike na baraka zilizomo ndani yake. Mwanzo 39:1-6
Mfano: Yakobo
🔹Yakobo alitakiwa afaidi baraka za agano, lakini kwa kuuzwa kwa Yusufu baraka zote zilikwenda misri.

3. Kufaidika na baraka zilizopo ndani ya agano ni uamuzi wako hata kama wewe ni mhusika wa agano hilo. Kumb 30:19-20
🔹Mungu ameweka uchaguzi ndani ya agano kuna baraka na laana, uzima na mauti. Ndani ya agano kuna mabadilishano.

4. Hali yako ya maisha inategemea kama unatembea na kuishi katika agano la Mungu. Mwanzo 49:1-2,28
🔹Kitu kilichobadilisha watoto kuwa kabila ni baraka walizoachiliwa na baba yao Yakobo.
🔹Kuna baraka zinazotengeneza na kubadilisha maisha ya watu. Mwanzo 28:1,6-7.

Jumatatu,13/04/2015
Mwl.Christopher Mwakasege :

1.Baraka zinazokuja kwa Kuwa umeomba ingawa zipo nje ya Baraka zako za kurithi zilizopo nje ya agano la Mungu.
Mwanzo 17:17-
Mwanzo 15:17-18
*Je Baraka nazoomba kwa Mungu zipo kwenye agano au hazipo?
Galatia 3:13,14,29

*Si kila mkristo ni mali ya kristo
Galatia 4:6-7
Warumi 8

***Usisome Biblia kama biblia BALI Soma Biblia kama Agano
Tunaomba sawasawa na Mapenzi ya Mungu.

2.Baraka za kujitafutia na zile zilizopo katika agano.
-Baraka za agano hutafuti yan zipo ila unazipata kutokana na maelekezo unayopewa.
Mwanzo 17:15-17

-Humuhitaji Ishmael kama Isaka hayupo.
-Baraka inakuja na baraka
Mwanzo 28:1-9

Agano lina msimamo wake.

*Agano ndani ya agano,yan hutafuti mume bali unapewa mume.
Makusudi maalumu ya ndoa yanayowekwa na Mungu yapo ndani ya agano.

Ukiingia kwenye ndoa na Ibrahim unakuwa umeingia kwenye agano la Mungu na Ibrahim.
Ni sawa na mdada anayetaka kuolewa na mchungaji lakini hataki kuwa mama mchungaji,Hahahahahahaha

*kuoana ni kusimama pamoja na kulitumikia kusudi pamoja siyo kukaa tu pamoja..Upate yule ambaye Mungu kamuweka kwa ajili yako..

3.Kutaka kubarikiwa kwa kufuata mkumbo badala ya kufuata maelekezo ya Mungu.
Mwanzo 49:28
Mwanzo 26:1-5

******Usijaribu kuishi kwa mkumbo kwa sababu wewe ni Mtu wa tofauti******NI GHARAMA KUBWA MNOO.

-Je kufanikiwa kwako unaiga kwa nani?
-Kila mmoja ana mbaraka wa kwake.

-Hakuna namna ambayo uzao wako ukaharibika kama upo kwenye agano na Mungu.
-Huwezi kuitwa kama huitajiki.

Mungu anakupa nafasi kwasababu kuna kitu umebeba ndani yako

–Mwl Conrad
Advertisements

6 thoughts on “Semina ya Mwl Mwakasege Dodoma

 1. Ndugu Mabinza,

  Nafikiri utakuwa umekurupuka ukisema umekosoa Mwalimu Mwakasege. Ni heri ungesema kama katika alilofundisha alisema kona moja, na wewe umelipitia lingine. Ndivyo lugha ya Biblia ilivyo. Hata naye Mwalimu angelikujibu nafikiri angesema kama somo moja analifundisha kitofauti kulingana na kusudi la RM.

  Asante.

 2. Bro Mabinza
  Hayo unayoyaelezea ni NIA ya Bwana

  Mwakasege yupo sawa ……
  Rejea ni nini! anachofundisha ….Kama nitakuwa nimemuelewa jinsi mimi nilivyopitia hayo maandiko ya Mwakasege kama yalivyoletwa kwetu na Bro Conrad.
  Kuwa unakwenda Mbinguni ndio….Lakini maisha ya safari yako uliopitia/unayopitia hapa duniani ni ya taabu kama Mzee Yakobo.

  Mw47.8 -9 Farao akamwuliza Yakobo, Je! Siku za miaka ya maisha yako ni ngapi?
  Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.

  Hiyo ndio tofauti yake Yakobo na baba zake,kumbuka wakati wa ujana wake,Alikimbilia ugenini kwa hofu(uhamishoni)kumkimbia Kaka yake Esau akamtumikia Labani miaka 20 kuchunga mbuzi,Kati ya miaka hiyo aliyotumika,Miaka 14 alikuwa anatafuta ndoa,Mara kumi Labani alimbadilishia mshahara wake.Najua unafahamu namba 10 ni namba kamilifu ilitakiwa Labani apate kibano toka kwa Bwana kwa mujibu ya wakati ule.

  Mjoli Haule

 3. Mwalimu Mwakasege ni mmoja wa waalimu mashuhuri, nampenda na kumheshimu sana Mwalimu huyu. Lakini nimelazimika kukosoa ama kuweka sawa ile hoja kama iliyopo mbele yetu, Kwa mjibu wa mleta habari, yenye kichwa cha habari “ Semina ya Mwl Mwakasege Dodoma” chapisho ambalo alilileta hapa tarehe15/04/2015, ndiyo hasa imenifanya nije hapa kutoa maoni yangu.
  Kwakifupi Mwalimu Mwakasege amenicha ‘peke yangu’ aliposema hivi, nanukuu,
  “ 2. Unaweza ukawa ndani ya agano na Mungu na usifaidike na baraka zilizomo ndani yake. Mwanzo 39:1-6
  Mfano: Yakobo, Yakobo alitakiwa afaidi baraka za agano, lakini kwa kuuzwa kwa Yusufu baraka zote zilikwenda misri.” Mwisho wa kunukuu.

  Sijui kama Mwalimu alipitiwa ama aliacha tu kuliweka vizuri jambo hili la Yusufu kuuzwa Misiri. Kuuzwa kwa Yusufu Misri ndiko kulikofanya Wana wa Ibrahim kuwepo Misiri, na kimsingi halikuwa jambo la bahati mbaya ama la kumkosesha Yakobo Baraka zake za msingi zilizokuwa ndani ya Ahadi ya Mungu, kwa Ibrahimu ambaye ndiye ‘Baba yao’!. Ieleweke kwamba, katika tukio la wana wa Yakobo kuwa utumwani Misri kulikuwa ni kwa mjibu wa sura mbili, moja ni kwa sababu ya Ibrahim mwenyewe na Mungu kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Mwanzo 15:10-13; ambayo inasema kuwa, “10Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili. 11Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza. 12Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake. 13Kisha BWANA akamwambia, ‘‘Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao wenyewe, nao watakuwa watumwa na watateswa kwa miaka mia nne”. Huo mstari wa 13 ndiyo unaothibitisha Yakobo kuwa utumani halikuwa jambo la kuihamishia baraka yake Misri, ilikuwa ni adhabu!

  Lakini la pili inaelezwa kuwa ni Mungu kwa njia ya ‘Kivuri’ kuionyesha safari ya wana wa Mungu ya kwenda Mbinguni! Tazama pia Matendo ya Mitume 7:1 na kuendelea……

  Kwa maana hiyo, Baraka za Yakobo hazikwenda Misri kama ambavyo Mwalimu alivyofundisha, kilichowekwa na Mungu Misri na kuonekana kuwa ni ‘baraka’ ilikuwa ni kuwatunza wana wa Israeli wapate kuishi ili kuutimiliza mpango wote wa Mungu kama ambavyo alikuwa amepanga. Kwa kuyaona hayo kuwa yalitukia, tunazidi kuiamini Biblia kuwa ni Neno la Mungu timilifu, na kwamba, halipingani au kuongopa.

  Kwa maana hiyo Ibrahim na Yakobo watabaki wabarikiwa na baraka yake Yakobo haikuhamia Misri. Ukisoma kwa utulivu Biblia yako, au hata hiyo Mwanzo 15:10 na kuendelea utaona kuwa, Bwana Mungu aliweka AGANO na Ibrahimu na kumbariki baraka zote za rohoni; na hata zile za mwilini alimthibitishia Ibrahimu kuwa, baada ya utumwa, atamtoa huko akiambatana na mali nyingi!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s