Chukua hatua baada ya kujifunza, Fanyia kazi – Cosmas Kisela

kisela

Watu wengi hufikia uamuzi wa kufanya mageuzi katika maisha yao, baada ya kuona maumivu ya kukataa mabadiliko yanakuwa makubwa zaidi kuliko yale ya kukubali mabadiliko (Myles Munroe). Hakuna mabadiliko yasiyokuwa na gharama au kiasi fulani cha maumivu! Usisubiri maumivu yawe makali zaidi ndio ukubali kubadilika na kurekebisha mwenendo wako! Unaweza kuchukua hatua za mabadiliko mapema zaidi ili pia uweze kukua, kuongezeka, kustawi, na kufanikiwa mapema zaidi. Ni mambo gani unaweza kuamua kyabadilisha sasa hivi katika maisha yako?

Tatizo letu kubwa siyo ujuzi wa mambo mengi saaana; tatizo letu kubwa ni uamuzi thabiti wa kuyaweka kwenye matendo yale machache tunayoyajua. Yesu alisema, mtu akipenda KUFANYA mapenzi ya Baba yangu ATAJUA kwa habari ya yale mafunzo….. (Yoh 7:17). Kuna kiwango cha ufahamu ambacho huwezi kukipata katika maisha kwa kusoma tu bila kuyafanyia kazi hayo unayoyasoma au unayofundishwa. Kuna watu wamelenga tu kuongeza ujuzi na si kufanyia kazi ujuzi walio nao; wanajua mambo mengi sana kiasi kwamba hata hawajui waanze na lipi, lipi wafanye, na lipi wasifanye. Dawa ni kuanza kuweka katika matendo kwa bidii kile kidogo unachokijua, bila kuacha kuendelea kujifunza kwa bidii: MATENDO => MATOKEO

Hatuwezi kujifunza kuogelea kwa kusoma tu vitabu na kuandika juu ya kuogelea. Kuna wakati lazima tuingie majini, tuanze kuogelea kwa vitendo, tukutane na mawimbi na upepo mkali, na wakati mwingine tufikie hatua ya kuzama, lakini tukiibuka baada ya hapo, tunaibuka na ujuzi halisi, uzoefu halisi, nidhamu halisi n.k. Huu ni ukweli wa maisha, usiukimbie, ukabili, uruhusu ukuguse na wakati mwingine ukuumize, baada ya hapo utakua, utaongezeka, utaendelea, na utakuwa mtu bora zaidi. Chukua hatua baada ya kujifunza, yaweke kwenye matendo yale uliyojifunza, lipa gharama inayotakiwa (kumbuka unaweza kukweka kulipa gharama lakini huwezi kukwepa majuto na matokea ya kukwepa kulipa gharama). Uwezo unao, sababu unayo, ukichanganya na nia thabiti matakeo bora ni kitu cha lazima.

–Mchungaji Cosmas Kisela

Advertisements

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s