Furaha imetoweka nani ya Nyumba!

maombi2

Wapendwa katika Kristo!

Tumsifu Yesu Kristu! Nimefaidika na kufarijika sana kwa mafunzo mbalimbali kwenye blog hii! Mubarikiwe. Nipo katika shida kubwa kimaisha! Pamoja na bidii nyingi uchumi kwangu kwa miaka 4 sasa umezidi kudidimia kiasi kwamba Hata kula imekufa shida! Ada za shule, mavazi ni duni! Madeni yamezidi hayalipiki. Watoto wangu wamekua kama yatima furaha imetoweka ndani ya Nyumba. Mifugo yangu na rasilimali zangu ziko mashakani, tayari moja ya mashamba yangu lipo kwenye hati hati ya kupokonywa. Mipango yangu haiendi nimetoka uza baadhi ya ardhi yangu ipi kujikwamua kiuchumi kwa mipaka kadhaa sasa sifanikiwi na sasa hali ndio mbaya! Naomba Msaada wenu wa mombi. Mungu awabariki! Amen.

–Lourance M

—————————-
Wapendwa naomba utamke kitu juu ya mama huyu furaha iliyotoweka kwenye nyumba yake irudi  Mungu afanyaye njia pasipo njia akaonekane na kufungua njia kwake kwa jina la Yesu Kristo. Omba kwa kadiri Roho wa Mungu atakavyokuongoza!
Advertisements

6 thoughts on “Furaha imetoweka nani ya Nyumba!

 1. mpendwa kama wewe ni mkristu na umefka katka hali hiyo
  mambo mawili ladhima roho yako itasema nawe,
  ikiwa iko hali ya hukumu plz usifanye moyo wako kuwa mgumu just surrender kwa Yesu alie Bwana wa wote wenye mwili nae atakuelekeza yakupasayo kutenda.
  dont strugle.
  ikiwa una amani na mungu wako tambua ni majira yale ya nyakati za kupoteza, kukosa na kuhitaji kama majarbu, huwe na uhakika kipindi hicho kitapita na nyakati za kuburudishwa zitafuata,

  kwa sasa endelea kujinyenyekeza chini ya mkono wake wenye nguvu nae atakukweza kwa wakati wake.
  linda moyo wako jinsi unavyosikia mwito wa Bwana ndani yako na wala usikaze kusikia hukum za yule mwovu akikuvunja moyo kuwa hukuitimiza kweli yote au wewe sio mwaminifu kwenye kikumi na mambo mengine km hayo.
  ukweli ni kuwa hakuna alie mkamirifu mbele za Bwana ila NEEMA YAKE INATUTOSHA,

  Mungu wangu akukumbuke.

 2. Barikiwa katika jina YESU!!! Uwe na amaini uone mkono Wa bwana..yote yanawezekana kwake Jesus Christ..

 3. Dada kama umeokoka na hayo yote yanakupata ujue ni jaribu lako. Ayubu alimwambia mkewe: Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake. Ayubu 2:-10b. Na kama hujaokoka mpe kwanza Yesu maisha yako awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako na hayo yote Mungu atafanya njia.

  Kukuombea sio shida, utaombewa lakini kama hujaokoka shetani atarudi maana ana uhalali. Barikiwa

 4. Bwana Yesu asifiwe mpendwa mimi nachangia kama ifuatavyo mimi sisemi nitakuombea ila nataka nikupe ushauri ambao utakukwamua kwani wakati mwingine tunaomba Biblia inasema tunaomba vibaya sasa tufanyaje
  Biblia inasema tukisikia neno la Mungu na kulitendea kazi Neno Kuna ahadi Mungu anasema atatubaliki mjini na mashambani na Mungu anazidi kutoa ahadi nyingi ansema ataamuru Baraka zituijie na kutufanya kuwa vichwa ebu soma (kumbukumbu la Tolati 28:1…..10) ndipo sasa mimi nasema watu wengi wanataka kuombewa wakati wanatembea kinyume na neno la mungu
  1kwa mfano wewe nimwaminifu kumtolea Mungu kwa sadaka mbalimbali kama Zaka,Dhabihu,Malimbuko. kwani ili Mungu akubariki habaliki patupu Ibrahimu alibalikiwa na Mungu baada ya kumtoa mwanawe Isaka soma mwanzo 22:15…19)
  2.Wakati uko kwenye jagwa,shida,au jalibu la kupungukiwa hapo ndipo kwenye mtihani ambao wengi wanashidwa kumbe ukishinda jalibu ndipo utamwona Bwana na kushudia mambo makubwa ebu angalia mfano huu wa mama mjane aliyejalibiwa kwa kutoa (1wafalume 17:10…..16)alijalibiwa kutoa wakati yeye ni mjane lakini alipo tii alimwona Mungu kwa kiwango kikubwa sana
  sasa wewe unauza mashamba nk utakuta wengi wakati kama huu wanashindwa hivyo kufalakana na huyu Mungu kama uko mwaminifu na umesimama kwenye Neno la Mungu ubalikiwe namkumbushe Mungu juu ya ahadi za mungu juu yako ila kama uko nje ya Neno la Mungu tubu na kejea kutendea kazi Neno la Mungu Mungu ni mwaminifu na atabaki wa kuaminiwa
  Balikiwa sana Bwana Yesu Amina

 5. YOTE NANAWEZEKANA KWAKE YEYE AAMINIE; OMBENI NANI MTAPEWA ;TAFUTENI NANI MTAONA ; UKIMWOMBA MKATE ATAKUPA MKATE SIO JIWE. Dada yangu magumu hayo na matatizo yanayokusonga ni ya muda tu. Usiku utapita asubuhi itakuja ya mabo mema ya kufanyikiwa na kugeuza utega wako kuwa furaha na baraka tele. hizo ni hila za yule mwovu. Yakupasa sasa umtumainie Bwana naye atatenda.Tunakuombea tu na baada ya muda mfupi utatoa ushuhuda kuwa mambo yote yamebadilika na ni baraka na mafanikio tu.

 6. Tutakuombea ila neno pia linasema “UKIPATWA NA MEMA UFURAHI NA UKIPATWA NA MABAYA UFIKIRI”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s