Mungu awabariki!

ej

Mtumishi wa Mungu EJ Oguda kushoto wakati wa maandalizi ya mkesha wa Strictly Gospel

Bwana Yesu asifiwe wapenzi Familia ya SG, naamini mnaendela vyema katika BWANA, ninawashukuru wote ambao bado mnaendelea kuchangia mada mbali mbali, kutuma email na kuomba ushauri na maombezi. Ninatambua mchango wa kila mmoja hata watembeleaji wa blog hii. Kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu group email yetu haifanyi kazi kwa sasa, tunatazamia kufungua group jipya, ikiwa ungependa kujumuika nasi tafadhali tujulishe na utaungana na wenzako kupata habari na mafundisho mbali mbali kuhusu ufalme wa Mungu. Kama umejaza form ya kushirikiana na Strictly Gospel unaweza kuacha tu hii na kwa wale ambao ni wageni au ambao wangependa kuwa kwenye group hilo na kufahamu zaidi kuhusu sisi. Tujulishe kwa kutuma email strictlygospel@yaho.co.uk

Kwa Tanzania tumekua kimya kwa muda kwa sababu tunashughulikia masuala muhimu kuhusu huduma na kuanza kazi ni pamoja na kuwafikia watu wengi kiurahisi. Wana maombi tuendelee kuomba hasa kwa viongozi wa huduma hii ili maono Mungu aliyoweka ndani yao yakatimie na Utukufu ukawe kwa Mungu, Tuendelee kufarijiana kuhusu Upendo Mkuu wa Bwana wetu Yesu Kristo na pia kuwaombea wenye mahitaji mbali mbali yanayoletwa kwenye blog hii.

Kwa USA na Canada huduma yetu na maombezi itaanza mwezi August ikiwa na watumishi kutoka sehemu mbali mbali watakaohudumu ukipenda kupata updates kwa njia ya simu au email tafadhali wasiliana nasi kwa email strictlygospel@yaho.co.uk

Na mwisho kabisa Ndugu yetu EJ Oguda amefiwa na mkewe na wameshazika wiki iliyopita, unaweza kuwasiliana naye moja kwa moja na kumfariji kwa simu no 0762-925-577. Mtumishi wa Mungu Oguda amekuwa nasi kwa shughuli mbali mbali za huduma. Itapendeza akipata simu kutoka kwako

Mungu awabariki wote, ninawapenda!

–MD

Advertisements

5 thoughts on “Mungu awabariki!

 1. Ndugu Ogudu,

  Yeye aliyeanzisha kazi ndani yako ataikamilisha. Yuko nawe kukufariji wala hauko peke yako. Ataziba hilo pengo ndani ya moyo wako na kuiondoa simanzi ya moyo ambayo imekupata kwa muda tu.

  Naomba ufarijike kwa maneno haya machache tunayokufariji nayo, huku mfariji mkuu Roho mt. akikuimarisha zaidi nafsi yako.

  Amen

 2. Brother Oguda,
  Pole sana ndg yangu!
  Bwana na akupe Nguvu zake ktk mapito haya magumu; aufariji moyo wako pamoja na familia yako yote!

 3. Amina Mtumishi wa Bwana tupo pamoja na pole kwa mtumishi wabwana kwa nyakati hizi ngumu kwake ila kumshukuru mungu maana ndio mapenzi yake  Siaka S. Nyanchiwa    Internet cafe and College Controller        P.o Box  70 Serengeti, Mara, Tanzania.           P.o Box 417 Tarime,Mara, Tanzania.    Contacts: sianchwa@yahoo.com/sianchwa@gmail.com. Mobile:            +255755527476.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s