Ndoto hii inajirudia rudia!

ndoto

Ndugu wapendwa mimi naitwa Faustin kutoka Songea Tanzania,  ninaomba ushauri juu ya ndoto hii, Nina miezi yapata tisa sasa ninaota ndoto za kukutana vitu vya ajabu sana, Mara watu walio kufa zamani, kuona maumbo tofauti ya kutisha na Mara nimelala naota navutwa na lijitu la ajabu naaza kupiga kelele “kwa jina la Yesu Mara linaniachia mpaka siku nyingine napiga kelele ambazo jiran yangu ambae nimelala nae anasikia sijawahi kuota ndoto nzuri na mpaka sasa ndoto hizo hazikati kabisa kwangu mpaka naweka biblia kichwan pindi nalala lakin wapi naomben msaada wenu jamani.

Advertisements

8 thoughts on “Ndoto hii inajirudia rudia!

 1. Tatizo hilo liko kwenye ubongo wako. Wala usilitafute sehemu nyingine. UBONGO wako umeingiliwa na mvurugiko unaosababishwa na mazingira mabaya.

 2. Hebu Hama eneo hilo uende mbali kidogo au mbali sana. ikiwezekana mji wa mbali kama vile Dodoma utafute nyumba ya kupanga upya, au uende Mwanza au uende Iringa Mjini hivi. Ukiona hali hiyo imejirudia unipigie simu. Ninaamini haitajirudia kamwe.

  Unakabiriwa na tatizo la mazingira machafu. Mazingira unayoishi huenda hayana hewa safi. Hayana utulivu wa kisaikolojia. Hayana utulivu saana kivile. Endapo utapata eneo au makazi yaliyo safi na salama vindoto hivyo vitakuwa historia.

 3. Hizo si ndoto njema,,tafuta kanisa la waliookoka wanaohubiri Wokovu uombewe!

 4. jibu la maisha yako ni YESU pekee, Mpokee leo awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.

 5. Bwana asifiwe watumishi wa Mungu pole sana ndg yangu ndoto Kama hizi zipo nikweli ndugu yangu Kama hujampokea YESU hasa kuishi maisha ya wokovu wako roho wakwenda njia za Giza atatawala maisha yako kwani hata mimi niliku naota ndoto Kama hizo tena zaidi kwani ilifika hatu ninakatwa kichwa kabisa tena mpaka ilibidi saa ingine sitamani hata kulala mapema au nakesha hasa mchana nilikua silali kabisa Kwani nilikua naota ndoto za ku tisha nili ishi Kwa hali hiyo Kwa mda mrefu nikiwa shuleni mpaka nika anza kazi hadi nikaoa na mshukuru Mungu Kwa alinipa mke ambaye alinisaidi hasa Kwa kumtafuta Mungu Kwa nguvu nyingi mno Kwani wote tu wakristo ila katoliki/sabato najua wengi mnajua ilivyo changamoto imani inahitajika elimu/mafundisho na kumwomba roho Mtakatifu juu ya hayo.
  Point yangu ndg yangu nikwamba kuombewa,kufunguliwa na vingi Kama hivyo nimhimusa lkn zaidi ni ww mwenyewe kuatayari na kuatayari kutembea na Mungu wa kweli Kwa kila jitihada Hilo tatizo Mungu atalitatua bila shida yoyote pia ni Maono ambayo utapata kujua thamani ya hayo pia mm mwenye ndoto ambazo nilikua naziona Sio zuri Kwangu kwembe Ilikua ninaonyeshwa jinsi ya maisha halisi ya Kwangu na familia yangu na jamii zima Kwa ujumla hivyo na mshukuru Mungu napia nina msihi Mungu aendelee kwani ndio naona imani nilio nayo inazidi kuimarika kwani Kwa kupitia hizo ndoto najua ni wapi Na kupambana napo hivyo ina nifanya kila wakati na mda wowote nikifanya kazi ninakua ktk sala Maombi ni muhimu sana nahaya ni kweli nili ya pata Kwa kupenda kusoma bibilia na mafundisho mengi kutoka Kwa watumishi wa Mungu tofauti tofauti na mababa wa kiroho hivyo nimejaribu kukupa Mwanga kidogo kwamba hayo yapo ila usipokua makini unapoteza Karama yako na kuacha njia ya Mungu na ukaelekeza nguvu zako za thamani Kwa shetani kupitia waganga #washirikina ili upate majibu ya haraka hayana manufaa yoyote kwahiyo kuatayari kutatua Hilo jambo kwanjia sahihi ya Mungu ktk roho na kweli ili usije ukapoteza kitu cha thamani ulicho nacho .
  Ubarikiwe Kwa jina la YESU KRISTO

 6. Je umeokoka? kama hujampokea Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako, mpokee sasa, sema maneno haya moyo ” BWANA YESU NAKUJA KWAKO NI MNYONGE NA MWENYE DHAMBI TELE, NISAMEHE DHAMBI ZANGU, ANDIKA JINA LANGU KWENYE KITABU CHA UZIMA NAUL UNIJAZE ROHO WAKO MTAKATIFU, WEKA ULINZI WAKO UKINIZINGIRA KWA UKUTA WAKO WA MOTO, VUNJA LAAANA ZOTE NA NIKOSI YA MABABU KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETH…. AMEN” KUANZIA SASA ANZA KUSOMA BIBLE YAKO KWABIDII NA KUHUDHURIA MAKANISA YANAYOHUBIRI WOKOVU… KAMA UMEOKOKA NA MAMBO HAYO YANAKUTOKEA NAKUDHAURI NENDA KWAWACHUNGAJI WENYE NGUVU ZA MUNGU WATAKUSAIDIA.

 7. Rafiki nakushauri kama unaweza uende SCOAN kwa Prophet T.B. Joshua ukafanyiwe deliverance! Hata kama hujaweza usife moyo Bwana YesuYu Hai naye ni Mtetezi wetu. Endelea kufunga na kuomba wewe mwenyewe.Soma Matt 17:14-21. Ubarikiwe

 8. Kuweka biblia kichwani ni sawa nakuwa na simu iliyo zimwa kinachotakiwa nikusoma yaliyo ndani ya biblia kikubwa ni masomo yapi yatakayokusaidoa. Ilotatizo lako nikwamba umeunganishwa na nguvu za giza bola wewe kuwa na habari.Dawa nenda kwa watumishi wa Mungu waliokoka waliyeko jirani yako. Wambie wakuombee na wakuongoze sala ya kuvunja mikataba ya mapepo yote yanayo kujia ndotoni. Utapokea muhijiza wako na hautaziota tena hizi ndoto.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s