Ubatizo kwa watoto wadogo ~ inaendelea

Mbarikiwe sana wana wa Mungu kwa michango yenu ya mawazo kuhusu mada ya. Mchango wangu kuhusu mada hii ni wa jumla kwa kusema kuwa, Ni vizuri kutenganisha namna Mungu alivyojifunua kwa watu katika nyakati tofauti ili kujua jinsi watu wa nyakati hizo walivyo mfuata Mungu. 1. wakati wa agano la kale 2. wakati wa agano jipya Grace period). 3.wakati wa kanisa la mwanzo (matendo ya mitume).4. wakati wa utawala wa kanisa la Roma. 5. wakati wa uamsho . 6. wakati wa uamsho wa kipentekoste kule azusa street USA. na 7. wakati wa sasa( naita wakati wakanisa huria). Ukidadisi vizuri kuhusu namna ubatizo ulivyofanyika katika nyakati utagundua wapi ubatizo ulipoteza mwelekeo na hasa jinsi Mungu alivyokusudia ubatizo uwe.

Nimeshitushwa sana na maelezo ya mch Malisa kwa kuharalisha ubatizo wa watoto wachanga kuwa ni sahihi. Inawezekana mchungaji ni miongoni mwa wachungaji ambao hawajasoma vyuo vya kichungaji na amejikuta ameitwa kuwa mchungaji bila kupata vyuo kama ilivyo kwa baadhi ya watumishi wa Mungu. Na ninahisi mch Malisa kwa makusudi kabisa umeweka fundisho hilo ili kuwavutia watu katika kujiunga na kanisa lako na iko siku utaruhusu na jambo lingine kwa kusudi hilo hilo.

Nawabariki sana wachangiaji wengine endeleeni kutafuta elimu ya Mungu kwa manufaa a kujenga wokovu wetu ili tuimalike na kufikia kimo cha utimilifu wa kristo jiepusheni na fundisho hili la mch Malisa kwa habari ya ubatizo wa watoto wachanga hilo sio sahihi nawaambia bila kusita sita. Amina.

Kennedy Simtowe

kusoma zaidi kuhusu ubatizo https://strictlygospel.wordpress.com/2008/07/16/swali-8/

Advertisements

20 thoughts on “Ubatizo kwa watoto wadogo ~ inaendelea

 1. Asante sana MILE kwa maoni yako katika mada mbali mbali hapa Strictly gospel.
  Jambo tunalopenda kukushauri ni kwamba jitahidi kuandika kwa herufi ndogo, utumie herufi kubwa pale panapotakiwa tuu!! Hii ni kwa ajili ya kumrahisishia msomaji asome bila kuumia macho!

  Endelea kushiriki na mjulishe mwingine kuhusu blog hii!

 2. UBATIZO NI TANGAZO LA VITA,MAJARIBU NI BAADA YA KUBATIZWA
  NDIO MAANA BAADA YA UBATIZO,KUNA WANAOKIMBIA, WANAOTEMBEA.WANAOTAMBAA,

  1 PETRO 3:21
  “AMBAYO YALIKUWA MFANO WA UBATIZO UNAOWAOKOA NINYI SASA. UBATIZO SI SHAURI LA KUONDOA UCHAFU MWILINI, BALI NI AHADI KWA MUNGU INAYOFANYIKA KATIKA DHAMIRI NJEMA. HUWAOKOENI KWA NJIA YA UFUFUO WA YESU KRISTO”

  “BWANA MMOJA, IMANI MOJA, UBATIZO MMOJA, MUNGU MMOJA, NAYE NI BABA WA WOTE, ALIYE JUU YA YOTE NA KATIKA YOTE NA NDANI YA YOTE.” WAEFESO 4:5-6

  SISI WAKRISTO KUWA NA UBATIZO WA AINA MMOJA NI MUHIMU;

  MATHAYO19:13-15
  “NDIPO AKALETEWA WATOTO WADOGO ILI AWEKE MIKONO YAKE JUU YAO NA KUWAOMBEA; WANAFUNZI WAKE WAKAWAKEMEA.
  LAKINI YESU AKASEMA, WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU; WALA MSIWAZUIE; KWA MAANA WALIO MFANO WA HAO, UFALME WA MBINGUNI NI WAO.
  AKAWEKA MIKONO YAKE JUU YAO, AKATOKA HUKO.”

  NIMEJIFUNZA KUWA YESU ALIWEKA MIKONO JUU YA WATOTO KUBARIKI
  SISI,SIKU HIZI TUNAFANYA UBARIKIO/KIPAIMARA KWA WATU WAZIMA.HALAFU WATOTO TUNAWABATIZA,WAKATI WA YESU WATOTO WALIWBARIKIWA WATU WAZIMA WALIBATIZWA.

  WANAOBATIZA WATOTO WADOGO HUJIKUTA WAKIVUNJA KANUNI MBILI ZA BIBLIA KWA WAKATI MMOJA

  1.KUBATIZA WATOTO
  2.KUBATIZA MAJI MACHACHE

 3. ahsanten sana kwa kufafanua zaidi,nashaur nanyi SG kuleta mada za ndoa,jinsia na mahusiano vijana wanapotea sana huko dhambi inayoumiza kila siku,sasa ubatizo una nini ikiwa mtu haishi kuzini?kuharibu ndoa? humu ndan mada zinazotawala ni sanamu, siku ya kuabudu(sabato) ubatizo na utakatifu, angalau hyo ya utakatifu kwan lengo la hayo mengne ni utakatifu,kwa mfano mtu abatize kuzamishwa baharini,yamfaa nini ikiwa hana MUNGU?au ninyi kuamini mnafikir ni kutamka? tena kuna hasara gan akibatizwa mtoto akakua vizur tena akaish kitakatifu,mnadhan atakosa kiti mbinguni eti kwa kuwa alibatizwa akiwa mtoto? kama ni hvyo pasingekuwapo na wa kwenda motoni kama kutamka ndio kuokoka, ni hayo tu.

 4. sdakayanda
  mungu akubariki kwa mchango wako,nimesoma kutoka kwenye anuani uliotupatia hapo chini,nimepata mambo mazuri sana kuhusu ubatizo,lakini hukutofautisha mambo haya katika ubatizo wa maji mengi,mtu yeyote aliye zamishwa majini amebatizwa,lakini kuzamisha tu bila kuliitia jina la BWANA YESU KRISTO ni bure.umeshambulia sana wakatoliki lakini labda wewe pia wafuata mafundisho yao kwa kubatiza kwa mafumbo,yaani kwa baba na mwana na roho mtakatifu.na wote waliobatizwa na mitume walibatizwa kwa jina lake YESU KRISTO.huu ni ufunuo wa fumbo katika mathayo 28:19,ambalo lilifunuliwa kwa mitume na roho mtakatifu.na huu ubatizo ni kwa ajili ya ondoleo dhambi pamoja na yale mengi ambayo ulikwishaelezea.
  ubarikiwe.

 5. pendael simon
  wewe ni ndugu yangu katika kristo yesu,atakama hatujuani uso kwa uso lakini mungu anatujua,nimesoma mchango wako wa 22-6-2015 na nimeona vile mungu amekufunulia kweli amboyo imefichwa kwa wengi.lakini uliposema kuwa {mimi ni MWANA WA TAI} ulimaanisha nini?

 6. Kiukweli ni mahekalu ya mashetani pekee ndiyo hubatiza watoto wachanga, tena kwa kunyunyizia nyunyizia maji

  Wakolosai 2:8 “Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.”

  *Matendo 8:36, 37, 38 “…yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu…naye akambatiza.”

  (NB: Katika biblia ya kikatoliki, kitabu cha Matendo sura ya 8, mstari wa 37 umetolewa, wameandika mstari wa 36, wakaruka mpaka mstari wa 38, mstari wa 37 haupo umefutwa. Sababu kuu ya kufuta mstari huo wa 37, ni kwa sababu mstari huu unathibitisha kwamba, mtu lazima aamini kwanza, kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu ndipo abatizwe. Mtoto mchanga hawezi kufanya hivyo.) Kujifunza zaidi kuhusu ubatizo tembelea anuani hii, https://sdakayanda.wordpress.com/je-ulibatizwa-katika-kristo/

 7. Ndugu Dauban,
  Ubarikiwe kwa maelezo yako,ila nikutaarifu tu ya kwamba mimi ni MWANA TAI.
  Pia, soma Mchango wangu wa tarehe 22-06-2015 kwenye mada hii.
  **MALAKI 4:5-6, IMETIMIA**

 8. Pendael simon,
  mimi niko upande wa mitume,vile mitume hawakubatiza watoto wadogo nami pia siungi mkono ubatizo wa watoto wadogo,vile mitume walibatiza kwa maji mengi{kuzamisha} nami pia,vile mitume walibatiza kwa kuliitia jina la YESU nami pia,vile mitume walihubiri MUNGU mmoja pekee aliye ndani ya YESU KRISTO nami pia, vile mitume walifundisha kuwa YESU KRISTO NDIYE MUNGU WA KWELI NA UZIMA WA MILELE (1John 5:20-21) nami pia,naweza kuendelea hata zaidi lakini najua ndugu yangu Pendael Simon amenielewa.

  Sasa unawze sema chenye ulikuwa wataka kusema,karibu. Lakini ujue aliye vuguvugu ni wewe ambaye ulishindwa kunielewa niko upande gani.

 9. DAUBAN, Biblia haitaki mtu VUGUVUGU.Kabla sijasema niliyotaka kusema naomba unijibu swali langu; WEWE UKO UPANDE GANI?

 10. Neno EBAPTISTHE {kiyunani} ambalo lina maanisha kunawa na neno BAPTIZO {pia kiyunani} ambalo linamaanisha KUZAMISHA au KUTUMBUKIZA ni maneno mawili yenye maana tofauti, mfano mtu akisema KUOGA na KUOGELEA,haya ni maneno mawili tofauti yenye maana mbili tofauti.so kama hili neno EBAPTISTHE ilitumika kwenye bibilia kumaanisha KUNAWA,haimaanishi BAPTIZO pia ni KUNAWA.siku hizi wandugu zangu wapendwa mambo yamebadiliswa kiasi kwamba atakamusi ya siku hizi hazitoi maana ya maneno sawasawa na vile zilikuwa mwanzo.shetani anajaribu kupotosha lugha ili watu wa mungu wasigundua uonga wake.neno BAPTIZO itabakia tu na maana hii KUZAMISHA AU KUTUMBUKIZA AU KUZIKA,na wote walio na ROHO WA KRISTO wanaielewa vyema sana kama vile mitume pia walilielewa,na kwa njia hiyo hawakuhusika na ubatizo ingeni zaidi ya kuzamisha,wengine wanasema yule askari alibatizwa na watoto wake,huu ni uongo,matendo 16:33 inasema YEYE NA NYUMBO YAKE AU JAMAA YAKE,maandiko hayasemi YEYE NA WATOTO WAKE WADOGO,{jihadharini na walimu wa uongo}.

 11. BWANA WETU YESU KRISTO alifundisha wanafunzi wake kumi na mmoja,akawambia ngojeeni jerusalemu mpaka mvikwe ngufu utokao juu,yaani ROHO MTAKATIFU ATOKAE KWA BABA.wanafunzi hawakuruhusiwa kuhubiri wala kufundisha kabla hawajapokea ROHO MTAKATIFU, kuenda chuo cha bibilia au chuo cha uchungaji haisaidii mtu kuhubiri au kufanya jambo lolote la kiroho kama huyo mtu au huyo mchungaji hajapokea ROHO MTAKATIFU,sikuhizi kanisa linakuwa bila ufunuo wa kweli wa neno la Mungu kwa sababu viongozi wanategemea sana masomo na elimu ya kibinadamu kuliko ujazo wa ROHO WA MUNGU na MAFUNUO YALETWAYO na huyo ROHO. Hawa viongozi hawana roho wa Mungu na ni vipofu,watu ambao walipewa kazi ya uongozi na wanadamu wenzao wala si Mungu,hawakuitwa na Mungu na atakama waliitwa na Mungu basi hawakungojea wajazwe nguvu itokayo kwa Baba na atakama walijazwa basi hawakutii sauti na mafunuo ya kweli ya huyo ROHO ATOKAE KWA BABA WA BWANA WETU YESU KRISTO ndiyo sababu wanaongoza watu katika njia iendayo kuzimu pasipokujua.

 12. Ndg Rich,

  Maelezo yako ni mazuri masikioni lakini kimsingi ni maelezo ya mtu anayeukimbia Uwepo wa Mungu, ambao ni Neno lake!

  Ubatizo wa ki Biblia ni wa kuzamisha, hiyo ndiyo tafsiri sahihi ya jambo hilo, hapo linapojitafsiri kimatendo hata nabii kufikia kupewa jina la huduma hiyo. Kwahiyo kama unaye mtoto mchanga na unataka kumbatiza, hebu fikiri mara mbili kabla hujamtumbikiza chini ya maji!!! Watoto ktk Biblia walipelekwa hekaluni wakawekewa mikono.

  Pia ahadi ya watoto unayoisoma ktk Matendo 2:38-40 umeielewa nje ya muktadha wake, hakuna mtoto mchanga anayeitwa na Mungu amjie, hao wamekabidhiwa wazazi wao wawalee mpaka watakapofikia umri wa kutambua kwamba “wote tumetenda dhambi na tunahitaji msamaha” ndipo watatubu au wataziungama dhambi zao na kisha kubatizwa kwa Jina Yesu Kristo kama ilivyoagizwa, ikiwa ni ishara ya UTII wa agizo hilo.

  Neno la Mungu linajitosheleza, usibadili Maandiko kwa faida binafsi. Wote wanao ongeza kwenye Neno la Mungu, majina yao yatafutwa ktk Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo; usiendekeze ulaghai wa dini; imeandikwa “Aaminiye na kubatizwa…”, hakuna mtoto mchanga anayeamini!!!

  Gbu!

 13. ndugu zangu ktk bwana: hebu atokee mmoja wenu halafu aseme kwamba, alilelewa na wazazi wake ktk maisha ya kikristo, lakini wakati wa kumkiri kristo na kubatizwa, yeye alimkiri nabii mwingine na kukataa kubatizwa. Hapo ndipo panapoonyesha kwamba, ile misingi ya wazazi wetu mara zote inakuwa ndio misingi yetu ya kuendeleza ile imani yetu. Tunapobatizwa tukiwa watu wazima, hatuanzi moja isipokuwa tunakiri kuendeleza ile imani yetu kutoka kwa wazazi wetu, ndio maana mtu akikiri kinyume na imani ya wazazi wake, anaonekana kuwa amepotea!!. Na huu ndio ukweli kwamba, imani haianzii ukubwani ila inaanzia tangu kuzaliwa kwako…ndio maana inakuwa ni shida kwa mtu kubadilika kirahisi. Watu wasiolelewa katika misingi ya imani au wale wasioamini ndio wanaobatizwa haswa ukubwani, wanakuwa ni kama watu waliokuwa wamepotea au hawakumjua mungu tangu mwanzo, ndio maana pia wakati wa mwanzo wa injili ni majitu mazima pekee ndiyo yaliyokuwa yanazamishwa kwenye mito ili yaokoke na kuwarithisha na watoto wao maana uwezi ukawabatiza watoto wakati wazazi wao bado ni wapagani!!. Kizazi cha leo kinawabatiza na kuwalea watoto ktk msingi wa kristo tangu wadogo kama ishara kamili ya kristo kukubalika kikamilifu na ile ahadi yake ya ubatizo kumfikia kila mmoja kutimia. Soma(Matendo 2:38-40). Nawaombeni msiwe na mitazamo ya kibinafsi maana kwa njia hiyo, hamtajenga ila mtabomoa na kuonekana mmepungukiwa na ule upendo wa Mungu. Kila mtu na athibitike mwenyewe ndani yake kuwa ameokoka na kumpokea kristo kuwa ni bwana na mwokozi wa maisha yake. Amen wadau

 14. Ubatizo ni mfano wa nje (ishara) unaoonesha mabadiliko ya ndani. Zile tabia na utu wako wa kale unakufa, kwa hiyo, Mungu anategemea kuona utu mpya ndani yako na hiyo ndio maana ya kuzaliwa kwa mara ya pili. Nikweli kabisa kwamba, kibiblia ubatizo unaofahamika ni wa watu wazima kuzamishwa na kuinuliwa mfano wa kufa na kufufuka Pamoja na kristo, Soma(warumi 6:5), lakini hata hivyo, tatizo tunayatazama mambo haya kimwili zaidi kuliko kiroho wakati biblia inatuambia tuenende katika roho. Neno la Mungu linasema “ajionavyo mtu ndivyo alivyo”. Mashaka yako ndiye adui wako, maana biblia inasema “wenye wasiwasi, waoga na wasioamini hawataurithi ufalme wa Mungu. Tumeokolewa kwa neema ya Mungu pekee na kamwe sio kwa matendo yetu yeyote….anachotaka Mungu kwa mwanadamu ni mabadiliko ya ndani ambayo kwa hayo, utakuwa ni mtiifu wa kila jambo analoliagiza Mungu kwenye neno lake. Sisi sio wakamilifu kabisa, hivyo hata kanisa haliwezi likawa kamilifu kabisa. Anachokitaka Mungu kwetu sio ukamilifu wetu ila anataka atuone tukiendelea kukaza mwendo siku hadi siku, tazama Mtume Paul anasema” Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba NIMEKWISHA KUSHIKA, ILA NATENDA NENO MOJA TU, NIKIYASAHAU YALIYO NYUMA, nikiyachuchumilia yaliyo mbele, NAKAZA MWENDO, niifikilie mede ya dhawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika kristo yesu. Soma(wafilipi 3:13-14). Sasa ndugu zangu katika Bwana, badala ya kutafutiana mapungufu yetu na kulaumiana, ni vizuri tukapendana na kutiana moyo, ili tuendele kuukulia wokovu wetu vizuri. Tukija swala la kuwabatiza watoto wadogo ambalo ndilo msingi wa mada hii, Biblia inasema, ahadi ya ubatizo haikuja kwa watu wazima pekee ila ni ahadi ya Mungu kwa watu wa rika zote….”Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu kristo mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho mtakatifu kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, NA KWA WATOTO WENU, na kwa watu wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. Soma(matendo 2:38-40). Mtoto akibatizwa, wazazi ndio wanawajibika kuwalea watoto hao sawa sawa na neno la Mugu. Watoto wakikua na kuwatii vizuri wazazi wao, wanakuwa wamemtii Kristo na Mungu, maana kichwa cha mwanamke ni mwanaume, kichwa cha mwanaume ni kristo na kichwa cha kristo ni Mungu!!. Kwa hiyo, watoto wanakua wameikiri imani ya kristo kwa njia ya kuwatii wazazi wao, ndio maana hata wale watu wazima wanaokiri ubatizo, hatujawahi kuwasikia wakikiri imani nyingine tafauti na ile waliotiishwa na wazazi wao!!. Kwa hiyo, kama ulibatizwa ukiwa mdogo, endelea na ukristo wako kwa imani thabiti bila woga au wasiwasi, kama ulibatizwa ukiwa mtu mzima nawewe kaza mwendo, kama hukubatizwa kabisa ni lazima ukabatizwe bila ubatizo haitawezekana…maana shetani anachukua cha kwake na Mungu anachukua cha kwake. Huo ndio mtazamo wangu, naomba kuwasilisha hoja

 15. Praise God..!
  Swali hili ni pana sana hasa utakapowauliza watu wa pande zote. Kwa mfano ukiwauliza wanaobatiza kwa maji machache watakupa majibu barabara , ukiwauliza wanaobatiza kwa maji mengi vilevile utapata majibu barabara. Wapo pia wengine wanaobatiza kwa moto, kwa jina la Yesu na hata kwa Roho Mtakatifu.
  KITU MI NINACHOKIONA HAPA NI KUWA KWA SISI WENGI WETU TUNAYAJADILI MAMBO KWA USHABIKI KUWA MM NIPO DHEHEBU FULANI BASI LAZIMA NITETEE MSIMAMO WA DHEHEBU LANGU. Mi nafikiri tujadili kwa kujifunza na sio kueleza msimamo wa dhehebu lako ambalo nalo pia limetokana na mapokeo ya Wazee/Wachungaji/Askofu/Mtume/Nabii wa kanisa lako. Unajua ukisema tuangalie Historia ya neno ubatizo na lilivotumika kwenye biblia kwa kipindi hicho utaona bado kuna mapana yake ambayo wengi hatuyaoni. Tuanze kwa kudadavua swala zima la ubatizo kama lilivotumika kwa lugha ya Kiyunani

  UBATIZO UNAWEZA KUTAFSIRIWA KWA MAANA 3 KAMA IFUATAVYO:-

  >>>>**Maana ya KWANZA [1]*** ni kuzamisha ( to dip/immerse), maana hii huko nyuma kabla ya kutumiwa na waandishi wa agano jipya ilimaanisha tendo la kutumbukiza nguo kwenye dawa iwezayo kubadilisha rangi na kuipa rangi nyingine, leo tunaita ‘tye and dye’. Tafsri hii ndio tunayoiona ikitumika mara kwa mara katika matumizi ya neno ubatizo kwenye Agano jipya.

  >>>>***Maana ya PILI [2]*** ilikuwa ni kusafisha kitu, au mtu kunawa kwa kutumia maji. (washing). Ili kuthibitisha hili, hebu tuangalie jinsi lilivyotumika katika agano jipya tunasoma: “Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula.” Luka 11:38. Neno kunawa hapa kwa kiyunani ni ‘ebaptisthe’ sawa na ‘baptizo’ kutegemea na matumizi. Unaona wazi hapa kuwa kunawa sio kuzamishwa, na kama maana ya ubatizo ni ile tu ya kuzamisha basi hapa tungesoma kuwa, ‘alistaajabu kwa sababu hakuzamisha mikono kabla ya chakula.’
  Katika Mk.7:4 tunasoma, “Tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali, na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.” Hapa pia tunaona matumizi ya neno batiza kwa maana ya kuosha kwa kiyunani.

  >>>>***Maana ya TATU [3]**** matumizi yake ni tofauti kabisa kwani aina hii ya ubatizo haihusu kutumia maji. Yohana Mbatizaji akizungumzia ubatizo huu anasema: “Kweli mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi ……yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.” Luka 3 :16. Na Marko 1:8 (Mimi nimewabatiza kwa maji lakini ajaye YESU atawabatiza kwa Roho Mtakatifu)

  Matumizi ya neno ubatizo kwa Roho Mtakatifu linamaanisha kumwaga au kumwagiwa.Tuangalie maandiko yanasemaje. Hapo juu tumesoma Yohana Mbatizaji akiwaambia watu kuwa kuna Yeye atakae kuja kuwa batiza watu kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. Tendo hilo lilikamilika siku ya Pentekoste. Mtume Petro akimnukuu Nabii Yoeli kuhusu ubatizo wa Roho anasema, “Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu….” Mdo.2:17. Hapa matumizi ya neno kubatizwa kwa Roho kuna maanisha kumwagiwa Roho Mtakatifu na sio kuzamishwa.

  Sasa tunaona hapa kwamba kumbe ubatizo unamaana zaidi ya ile moja tunayoijua ya kuzamisha. Mkazo huu unatokana na aidha kutokuijua vyema lugha ya kiyunani au mtazamo wa mafundisho ya kimadhehebu.

  HEMBU TUENDELEE KUJIFUNZA MAANA YA UBATIZO KAMA ALIVYOSEMA BWANA YESU
  >>>>***MAANA YA NNE [4] ****
  Bwana Yesu mwenyewe alituma neno ubatizo kwa maana tofauti na ile ya kubatiza kwa maji. Tunasoma, “Lakini nina ubatizo unipasao kubatizwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe.” Luk. 12:50. Ni wazi kuwa hapa Bwana Yesu anaita mateso yanayomsubiri pale msalabani kuwa ni ubatizo.
  Pia tunasoma katika Matthayo 20:22-23 (

  >>Baada ya maelezo hayo ni bayana kuwa UBATIZO ni wa lazima kwa muumuni Mkristo ili kuzaliwa mara ya pili yaan kuokoka. Swali linalobaki ni Je Ubatizo gani ni sahihi…?? (WA MAJI MENGI?, KIDOGO, MOTO, JNA LA YESU au ROHO MTAKATIFU)

  Ukifwatilia Biblia kwa Makini utabaini kwamba kutokana na Tafsiri ya maana ya Ubatizo ni bayana kuwa UBATIZO unaweza kufanyika kwa namna mbalimbal kama inavyojidhihirisha katika maandiko yafuatayo…

  – Ubatizo wa Roho Mtakatifu Tafadhali tusome Matendo 1:5 , Matendo 1:22 , Matendo 11:16 ,
  – Ubatizo wa Jina la Yesu, Matendo 2:38 , Matendo 10:48 , Warumi 6:3 ,
  – Ubatizo wa Nyumba nzima bila kujali mdogo au mkubwa, Matendo 16:33 , Matendo 18:8

  (Ipo pia mistari mingi inayoeleza ubatizo wa wingu juu ya wana wa israel walipokuwa jangwani upo pia ubatizo wa ndimi za moto n.k n.k )

  NA HATA YESU ALISEMA KTK Marko 16:16 …(aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa) Mathayo 28:19 (inasema nendeni ulimwenguni mwote mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho mtakatifu) hapa hakusema ubatizo uwe wa aina gani.

  MIMI NADHANI KUSEMA KUWA KWA SABABU YESU ALIBATIZWA NA MAJI MENGI BASI LAZIMA NA SISI WAFUASI WAKE TUBATIZWE KWA MAJI MENGI TUTAKUWA HATUJAYATAFAKARI MAANDIKO KWA KINA….MAANA HUYUHUYU YESU MWENYEWE ALINENEWA NA YOHANA MBATIZAJI KUWA “Kweli mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi ……yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.” Luka 3 :16.
  NA ISITOSHE PIA YESU MWENYEWE ALISEMA “Lakini nina ubatizo unipasao kubatizwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe.” Luk. 12:50. Ni wazi kuwa hapa Bwana Yesu anaita mateso yanayomsubiri pale msalabani kuwa ni ubatizo.

  Maana kama mtasema tutumie ubatizo alioutumia YESU basi mhakikishe tunamuiga na kumfwata Yesu kwa kila alichokifanya bila kuweka tafsiri zetu wala mafunuo yetu. Mfano tuhakikishe hata mavazi, ukaaji, na tamaduni nyingine nyingi zilizokuwepo kwa kipindi kile tunazifwata ili kuendana exactly na YESU. Maana kwa walokole tulio wengi ni wazuri kwa kumcopy Yesu kwa baadhi ya mambo yenye maslahi nayo na kuacha mengine ambayo hayana maslahi kwao. Huku tukitoa tafsiri mbadala kwa kusema kuwa ni mafunuo ya Roho Mtakatifu hata kama ni akili zetu wenyewe. (Na swali litabaki Je unavosema ni Roho Mtakatifu ndo kukufunulia, kwann kila Mlokole aseme amefunuliwa na Roho Mtakatifu huku kukiwa na tafsiri tofauti toka kwa huyo Roho Mtakatifu. Na huku kila mmoja wetu akijinadi kuwa Roho Mtakatifu aliye nae ndo wa kweli, sasa jiulize tuna jumla ya madhehebu na vikundi vya kipentekoste / walokole zaidi ya 3,000 na hapo kila mmoja anasema ana Roho Mtakatifu anaemuongoza kunena ayanenayo. Mwishowe utaona ni mchanganyiko usio na ukweli ndani mwake bali tunaongozwa na akili na tamaa zetu)

 16. Wapenzi,

  Mimi nina mawazo ya kichokozi tu na kufikirisha.

  Ivi Yesu aliwahi kubatiza mtu?

  Ivi ubatizo aliobatizwa Yesu ndo tunaobatizwa nao sisi?

  Kama utasema kuwa Yesu hakubatiza mtu kwenye maji, Yohana alimaanisha nini aliposema …. ajaye nyuma yangu yeye atawabatiza kwa Roho na kwa moto?

  Lakini tunaposema watoto ni vema tukawa more specifi, maana kuna hili swali pia kama je watoto wadogo wanaweza kujazwa na Roho mt?

 17. SHALOM.
  Ubatizo wa watoto wadogo ni Fundisho la kipagani liloanzishwa na dhehebu la Katoliki Baada ya kuanza kuwaua WAKRISTO WALIOAMINI INJILI YA MITUME.
  MARKO 10:13-16-YESU ALIWABARIKI WATOTO SI KUWABATIZA.
  Pia, kama BWANA YESU, mwanzilishi WA IMANI YA KIKRISTO ALIBATIZWA AKIWA MTU MZIMA WEWE NDIO AKUKUBALI KWA UBATIZO WA WATOTO WADOGO?
  Wakati mwingine Watu hutafuta Mistari ya Maandiko kutoroka Wajibu?MFANO, HABARI YA NYUMBA YA KORNELIO,MWIZI MSALABANI.HUJUI HATA UKITAFUTA ANDIKO LA KUTENDEA UOVU UTALIPATA?
  YESU ALISEMA NI MTU ANAYEAMINI (MARKO 16: 15-16) SI ANAYEAMINISHWA NA MDHAMINI AU NA DHEHEBU FULANI.
  UBATIZO ULIOPO KWENYE BIBLIA NI WA WATU WAZIMA TENA “KWA JINA LA YESU KRISTO” SI KWA VYEO,BABA, MWANA, ROHO MTAKATIFU BALI NI KWA “JINA”
  Hakuna mtu aitwaye Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu Duniani.Hilo lilikuwa fumbo (MATHAYO 13:34-35) Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni Bwana Yesu Kristo.Soma-MATENDO 2;36, 4;10-12,YOHANA MT,17;6,11-12,WAFILIPI 2;10-11.
  Mitume ndio walioachiwa Maagizo na wengine wote wanaotaka kwenda Mbinguni hujenga kwenye Msingi huo,soma-1KOR 3;10-15, LUKA 10;16,WAEFESO 2;20.Mitume Waliokuwa na Ufunuo Walibatiza KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO.Soma BIblia Yako vizuri-MATENDO 2;38, 8;12,16, 10;47-48, 19;4-5,WAKOLOSAI 3;17 ” Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”. Ubatizo ni TENDO, ndio maana WAKRISTO wa KWELI hubatiza Kwa JINA LA YESU KRISTO.
  Sasa kama HUJABTIZWA Kwa Jina La BWANA YESU KRISTO, UMELAANIWA ( SOMA KWA MAKINI-WAGALATIA 1:8-9).
  Ni ukweli usiopingika wanaowapinga Mitume wa Bwana Yesu ni wapinga Kristo.Kuwa Mpinga Kristo ni kuwa Mpinga Neno,na kuwa mpinga Neno ni kuwa mpinga YESU (Luka Mtakatifu 10:16)
  KAMA UNA ROHO MTAKATIFU HUTAPINGA NENO LA MUNGU KAMWE.
  HIVYO, MTU YEYOTE ANAYEDAI KUWA NI MKRISTO NA HAJABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU KRISTO (MATENDO 2:38-39, 8:14-16, 10:48, 19:1-5) BADO NI MPAGANI.
  ****NA WATU WOTE WASEME AMINA****

 18. Ninaendalea!chakujifunza hapa ni kwamba Kama ingekuwa mpango mzuri wa Uhuru wa makanisa ili kurekebisha kanisa la kwanza wema wa jambo hili tunge uona nilibatizwa utotoni pia nililelewa kumjua Mungu Kwa elimu nyingi kuhusu Neema/imani ya YESU KRISTO Kwa kupitia ishara tofauti tofauti ili kuimarisha imani hasa nikijua nini ninacho abubu na imani Hii ni juu ya nani na hivyo nili/nina endelea kila wakati kukiri imani Hii basi kinacho Shangaza nikwamba nimeona tulio wengi tuna amini kwamba vitu Kama hivyo vina tutenge na Mungu lkn viko ndani ya imani ya Mungu/YESU na Matendo yake ndio maana ubatizo wa watoto umekua nimoja ya elimu inayo tusumbua sana imani hii na Sio watoto tu pia wa maji ya kikombe tufundisheni tujuee kuimarisha imani/matendo ya Bwana wetu YESU KRISTO inaweza ikawa bora zaidi kuliko elimu za kubadilisha badilisha mafundisho na tukubaliane kwamba unapo jua mambo mengi ndio unapo pata maarifa ya kutaka marekebisho ambapo tunaona hasa Kwa furusa Hii ndio inayo leta Tafakari nyingi kwenye neno la Mungu yani bibilia na mengine mengi Kama mapoke ya kanisa nilifurahishwa sana na mafundisho ya kwamba hamna kitakachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu mkuu ila Kwa imani ya YESU yapo mengi yanayo wenza kututenganisha ya kiambatana na mafundisho mengi ya shetani na hili la mathehebu na mafundisho kuhusu matendo mema hasa ya YESU KRISTO lina yumbisha waamini Kwa sehemu kubwa sana na kuzidi kupoteza hofu ya Mungu hasa Kwa next generation Kwa sababu mpasuko au Uhuru wa makanisa unaendelea kila siku ya Mungu hasa Kwa Nchi za Africa ambao ndio tumepata mwamko mkubwa na tukijaribu kuacha Yale ya kale na kuanzisha mapya unasababisha kuona nimambo ya kawaida tu na hamna hofu ndani ya hili basi tuwe na nia moja Kwa wakristo ili tuweze kumwomba Mungu Kwa umoja tumfukuze shetani Bali ni machafuko Kati wakristo Kwa wakristo kwa hili ni shetani anafanya kazi naona nibora tu tafute elimu/mafundisho Kwa mashahidi halisi wa imani ya Bwana wetu YESU KRISTO kwetu sisi .jmapili njema

 19. Thanks Kwa hili mm Sio mchungaji ila ni mmoja hasa mwenye mwamko wa kutaka kujua mambo mengi yanayo mhusu Mungu mkuu Kwa hali yakwaida na hasa tunapo pitia mafundisho tofauti tofauti hasa Kwa hili janga kubwa la mathehebu kulingana na shida juu maisha tunapata elimu nyingi hasa kwa viongozi wetu ambao tayari hawaoni shida kufanya jambo lolote jema/baya ilimradi tu wapate umaarufu hili tokea zamani sana ktk historia tena kila mmoja akitumia bibilia kuhalalisha mafundisho yake na swali hapa nikwamba Kama kanisa la kwanza au wanalosema la Roma lilifanya mambo mengi kinyume na Mungu basi hapa jambo mhimu iliku nikutatua hayo matatizo Sio kuyakimbia ili ukee pembeni ukiamini ndio utaweza kulitatua tatizo hapana ndugu tatizo Sio kulikimbia ndio maana Leo Hii kila mmoja anapo pata furusa yoyote basi hutumia mda huo kujipatia wafuasi au waamini.Kubatiza watoto wadogo na vitu Kama Lozari amboyo iko kwenye hiyo picha ya mtoto hapo juu na vitu vingine vinavyo endana na hivyo ni vyakiimani zaidi na hili wachungaji au watumishi wa Mungu wanalijua kabisa ila chakujifunza ha

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s