Sitamani kuoa!!

mpweke

Bwana Yesu Asifiwe,
Kwanza namshukuru Mungu sana kwa kunijalia uhai na elimu hadi elimu ya juu na pia kunipa kazi. Naomba sana maombi yenu na ushauri kwani nina tatizo kubwa sana kwangu ambalo limenifanya nikate hata tamaa ya kuendelea kuishi. Nilipofikiria zaidi nikaona Mungu ana sababu ya mimi kuwa hai. Mimi ni kijana umri wa miaka 30! Sijawahi kufanya mapenzi au kuvutiwa na mwanamke yoyote maishani mwangu!!!

Ninapata msisimko wa mwili nikiwa mwenyewe tu ila nikiwa na msichana siwezi hata kuvutiwa kwa namna yoyote ya kutaka kufanya nae tendo la ndoa. Kwa uelewa wangu, nisipovutiwa na msichana na kusisimka hakuna maana ya kuwa na mchumba. Hivyo imenifanya nisitamani kuoa kabisa ila jamii itanionaje kama sitaoa kabisa? Najiuliza Married couples go old together!! As for me who will I go old with? Will I remain single forever?

Kuna wakati nikiwa na marafiki wakike, wanapoonyesha kunitaka kimapenzi huwa nawakimbia sana. Ukweli ni kuwa naogopa tendo la ndoa!! Wakati mwingine nikiona vijana wadogo zangu wakiwa wanaoa machozi yananitoka maana sijui mimi nitaanzia wapi ili niweze kuwa na mke. Sio tu mke niweze kumtimizia haja zake ikiwa ni pamoja na kufanya nae tendo la ndoa ambalo naamini ndilo la msingi zaidi kwenye ndoa. Kikristo kama waliooana hamkufanya tendo la ndoa maana yeke bado sio mke na mume, (marriage consummation)

Naomba sana niombewe niweze kujiona mwanaume halisi ili kukabiliana na ndoa au niweze kuishi maisha yenye amani moyoni kumtumikia Mungu maishani mwangu.

Ahsante sana na imani kuwa Mungu anasikia Maombi yetu ataniponya

–Brian

Advertisements

16 thoughts on “Sitamani kuoa!!

 1. Ahsanteni tena sana kwa ushauri wenu, na samahanini sana kwa kuchelewa kujibu.
  Kwa Mr Milinga, najijua kuwa sihitaji kupima uume wangu kwani niko vizuri nikiwa mwenyewe! Tena night dreams ni mara kwa mara sana tu ila tatizo nikuwa physically sivutiwi na mwanamke kimapenzi.
  Ndugu NM ninaomba nisiweke namba za simu hapa kwani naogopa kutafutwa kwenye simu mara nyingi na watu nisiowajua vyema. Email yangu ni brianimushi@gmail.com natumaini tutawasiliana kupitia email.
  Nimeanza maombi maalum naomba sana ushirikiano wenu Mungu aweze kunifungua na kuondoa hofu iliyopo ndani mwangu.
  Ahsanteni sana

 2. Ndugu kuwa mwaminifu tu na Mungu. mimi nakuona uko vizuri kwani ishara za uanaume unazo pale uume unaposimama kila ukiamka na unasema ukiwa peke yako unasisimuka.

  ushuhuda huu utakusaidia binafsi nimeokoka nikiwa na miaka 28 na nilikuwa nashiriki sana mambo ya mwili. siku ambayo Yesu alipoanza nifuatilia baada ya kujua kuwa dhambi iliyokuwa inanitesa ilikuwa uzizi. akashughulikia pepo liliokuwa ndani yangu lilokuwa linanisukuma kuzini mara kwa mara. sasa nini kilitokea na hali kama yako ilivyonisumbua hadi nikaanza kujihisi sina uwezo tena kama unavyojidhania nitafute 0752 450200 siwezi kujieleza sana huku maana huu ni ubao.

 3. Pole sana ndg ila ninachotaka kukushauri hapa ni kwamba ume fanya lamaana sana kutumia blog kwama Hii Kwa kutaka ushauri hvyo basi ushauri wowote hapa hautaenda kinyume na utukufu wa MUNGU MKUU/YESU KRISTO basi elekeza jitihada zako zote kwake yeye pia jambo jema zaidi umepataelemu ya kutosha Kwa haya maisha ya hapa duniani kwani shetani anajitahi kuteka fahamu za watu wengi wanaofanikiwa katika elimu Kama ww na kuhakikisha elimu Yao Sio jambo ambalo Mungu anahusika lkn ukweli ni kwamba yeye ndio anaye weza yote basi jambo hili nirahisi sana sana Kama utakua na washauri wa karibu sana na ww hasa wana saikolojia na watumishi wa Mungu na nguvu zako zote Kwa Mungu ili umruhusu apambane na kila magumu yaliyoko na pia ushauri mkubwa ambao ni wa mwisho ni msogelea Mungu na hasa kuelekeza maombi yako yote Kwa MUNGU MKUU/YESU KRISTO na umpe nafasi bila ya kujishauri mara mbili mbili.Ubarikiwe ktk jina la YESU KRISTO

 4. Nenda Hospitali ya Muhimbili kama uko Dar ukapimwe uanaume wako kama uko sawa.

  Watakupima male hormones kama zipo. Endpao hazipo watakupa ushauri kama uishi hivyo milele ama utafute mke kama gresha tu la kuridhisha ukoo wako na marafiki zako.

  Watakupima kama umezaliwa ukiwa HIVYO HIVYO, au watapima kama ni tatizo la UBONGO au watapia kujua kama ni TATIZO LA MISHIPA FULANI YA HISIA au watapima kujua kama UNAJIFANYA MWENYEWE ama la.

  Wahi ukapimwe. Kisayansi hakuna mtu anayeweza kufikia umri wa miaka 30 akiwa hajasikia msisimko wa kuvutiwa na mwanamke. Hata kama siyo kufanya mapenzi na mwanamke basi utavutiwa ukiwa kwenye NDOTO USIKU au MCHANA ukiwa usingizini. Kama hata NDOTO NYEVU HUPATI USIKU unatakiwa uwahi kupimwa kwenye IDARA za afya ya UZAZI HOSPITALINI.

  Poleni sana kwa kukosa amani. Mungu atakusaidia.

 5. Kama ungeenda kwa wanasaikolojia wangekuambia matatizo yako ni “Gamophobia” “Erotophobioa” yaani ni hofu ya kuoa na ya physical love…….lakini kwa uhakika zaidi procedure itakuwa raisi kama kwanza ukiwashirikisha watumishi wa mungu then ukaenda kupata Therapist au guidance and counselling service sababu matatizo kama hayoyanaweza sababishwa kibaiolojia au experience za utotoni

 6. Pole sana kaka Brian, mimi nakushauri utafute mtumishi wa Mungu, mwenye neno la Mungu ndani yake akufanyie maombi, yawezekana ukawa na pepo mahaba ndio maana hutamani mwanamke yeyote. Pia nakushauri uwe unafanya maombi hata ukiwa peke yako, Mungu ni mwaminifu kwetu tukimuomba kwa Imani. Muombe Mungu akupe mke mwema wa maisha yako na kusudio lake. Usijali hao wanaosema ndoa zao zinawasumbua, ni kwavile hawakumshirikisha Mungu kabla ya kuoa/kuolewa. Bali wewe bado unao muda mzuri, ukimuomba Mungu atakupa mke mzuri na ndoa yako itakuwa salama daima, maana Mungu wetu hatupi sisi vilivyo vibovu, kwake yeye kila kilicho kizuri hupatikana. Na huenda Mungu ana kusudi na wewe. Bali mimi naamini ukisimama kwa Mungu kikamilifu hayo yote yataisha na utaoa tu.

 7. Mimi wala sikupi pole bali hongera kwa kuwa muwazi hivi. Ugonjwa ukishajulikana ni rahisi kuutibu maana unajua ni dawa gani utumie!
  Tatizo lako limeshajulikana.

  Zingatia ushauri 2 uliotolewa hao juu:

  1. Hakikisha uko vizuri na Mungu. Ufanye/Ufanyiwe maombi ili kuondokana na hali ya uvamizi wa ngugu za giza iwapo ilitokea hivyo!

  2. Tafuta mshauri wa kisaikolojia ili uweze kuondokana na hofu ya KUOA. Usiendelee kuon a kama vile kuoa ni MZIGO mzito.

  Naamini kabisa msaada wako katika hayo mawili!

 8. Ingawa sijui unakoishi,ila tafuta kitabu cha MWENZI WA MAISHA pale efatha bookshop,kitakufaa sana.

 9. Tafuta mtumishi wa Mungu au mchungaji wako kwa counseling, usifiche chochote ili upate ushauri wa namna ya kuishi na kufunguliwa… Yawezekana Kuna maisha unayaishi au Ulikuwa ukiishi huko nyuma yamefungulia uvamizi wa kipepo yakaharibu mtazamo, viungo vya uzazi na psychology yako juu wa wanawake… Ushauri wangu 1.Toba, maombi ya nguvu na ushauri 2. Dumu ktk mafundisho halisi ya Neno la Mungu kila siku 3. Jitenge na mambo ambayo au dhambi zinazokuzinga kwa upesi, hasa marafiki, magazine, majarida, vitabu, porno contents like movie or video, magrup machafu mitandaoni, masturbation na kukaa pekee bila Sababu. 4. Tafuta kazi , kipawa au huduma yako na ichochee… Tumika kanisa unaloabudu. Ditrich

 10. pole kaka subiri wakat ukitafuta hisia kama bado wakat utajuta hisia za mapenzi ni kali sana tuliza akili pata ushauri kwa watumishi lakini si vijana

 11. Brian. Natumaini ukizingatia ushauri uliopewa utafanikiwa tu. Ila ni vema kuishi pamoja.

 12. Ahsanteni sana kwa kuchukua muda wenu kunishauri. Nakiri kuwa kuna ndugu zangu wa karibu sana, wanateseka kwenye ndoa zao, lakini binafsi sidhani kama ni sababu ya mimi kuwa hivi nilivyo (Blessed & Anthony)
  Pia nakiri (sikutaka kusema mwanzo) kuwa nilishawahi kujichua miaka ya 2012 na 2013 nikawa addicted sana ila namshukuru Mungu kwa sasa sina hiyo addiction tena.
  Nikiwa peke yangu ninapata hisia za kimapenzi na mwili unarespond ‘erection’ hasa usiku na asubuhi kinachonifanya nijione sina tatizo kimwili.(Anthony)
  Najiona kama kuishi na mwanamke ni kujibebesha mzigo ambao ni mzito sana kwangu, sijui nifanyeje niweze kuziamsha hisia za mapenzi nikiwa na mtu/mwanamke pembeni yangu bila kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. (Siyi)
  Nitajitahidi kufanyia kazi ushauri niliyoupewa naomba Mungu anisaidie.
  Ahsanteni tena sana.

 13. Kaka Brain, Pole sana.. ila mimi nina maswali kwako; Je kuna mtu au watu ambao ulikutana nao ambao wakikuambia ubaya waliokutana nao katika ndoa? kama ndio inawezekana kabisa hii ndio sababu ya yale unapitia leo.

 14. Pole sana Brian,Mungu ni mwema atakusaidia.Tafuta kitabu cha MWENZI WA MAISHA kwenye maduka ya vitabu vya kikristo,kuna mengi utajifunza likiwemo tatizo lako.Lakini pia tafuta mtumishi mzuri wa Mungu mweleze tatizo lako akushauri na kukuombea,naamini tatizo litaisha.

 15. Pole sana ndugu.
  Naomba nianze kwa kuchangia kama ifuatavyo.
  1. Upo mda wa Bwana unaokubalika wa wana wake kuingia. Katika. Mahusiano. Maana ukiomba kutamani mwanamke wakati mda haujatimia ni dhambi. Una heri kuwa hivyo.
  2. Yapo matatizo yanayohitaji maombi, hapo nadhani kama mshauri. Nahitaji kujua je ukiwa peke yako kama. Ulivyosema hujisikia hisia za kupenda ni za namna gani hizo? Maana yapo mambo mengi ya kijamii. Mfano zipo jamii nyingine huwafundisha watoto/washirika kujichua kama njia ya kuepuka magonjwa kwa kuhofia. Lakini njia hiyo ni dhambi na ina matokeo mabaya mojawapo likiwa ni kuingiwa na pepo ambalo litakuwa substitute ya mke na kukufanya usipende wanawake.
  3. Mshituko wa kijamii ambao unatokana na jamii uliyoishi labda kuna kitu ulikiona kwa mwanamke au habari uliisikia au ulihadithiwa au uliisoma au uliona picha za maungo ya kike yakakutisha hivyo yamekuingia kichwani mwako na yanaweza yakasababisha hayo yote.
  4. Hayo yote yataweza kwisha. Ni heri yako kwani umeona tatizo kabla ya mda haujaenda sana. Hivyo nashauri mtafute mtu aliye owa ambae moyo wako utamkubali halafu mueleze hayo. Ataweza kukujenga kisaikolojia na hata kukuombea pia atakupeleka hadi pale safari ilipobakia na ukamaliza vizuri. Vyema akawa ameoa na yupo safi kiroho . Anaweza asiwe dini moja ila atakye payahekima toka kwa Mungu.

  Naishia hapo nitarejea nimeandika kwa simu ya mkono.
  Anthony mwenda

 16. Brian,
  Pole sana. Lakini uamuzi unao wewe mwenyewe rafiki!! Mimi nakuona kama ni mtu uliye mzima kabisa kimaumbile na kihisia, ila hujayaamsha mapenzi tu ndiyo maana bado uko hivyo ulivyo. Siku ukiyachokoza, uangalie sana maana unaweza usiwe mwaminifu kwa mkeo tena!! Tafuta social psychologist umwelezee tu hiyo hali atakusahuri vizuri na sehemu pa kuanzia!! Uko vizuri, huna haja ya kulialia kijana.Mambo mengine hayahitaji maombi ni ya wewe mwenyewe tu kuyashughulikia huku ukimruhusu Mungu kuingilia kati. Chukua hatua. Changamka, umri wa kuoa ndio huo rafiki yangu.
  Ubarikiwe sana
  Siyi

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s