“Nina tatizo na mpenzi wangu!”

 

Dear All,

Bwana Yesu Asifiwe,  Poleni kwa Huduma. Mie ni Mdada naitwa JJ, nimeokoka tangu 2004 nampenda Yesu,ila ninashinda yangu ambayo ninaomba niwashirikishe katika maombi yenu, mie ninatatizo na  mwenzi wangu ambaye tuliaidiana kuoana, ila mpaka sasa kila nikimwambia naona haeleweki na mie nampenda sana, ni nami kila siku namwomba Mungu huyo ndo awe mwenzi wangu. sasa ninaomba msaada wenu, make nimefunga na kuomba mara nyingi na kuwashirikisha wachungaji mbalimbali na wana maombi wengi, na huyu kaka ana onyesha interest kweli kuwa ananipenda lakini tatizo afanyi maamuzi yoyote yale,

Nawatakia huduma njema.

-J

Advertisements

13 thoughts on ““Nina tatizo na mpenzi wangu!”

 1. Pole sana mpendwa,ushauri wangu ni kuwa mara nyingi sisi twamshauri Mungu afanye vile tunataka sisi badala ya kumwuomba Mungu afanye kulingana na mapenzi yake,tazama wana wa israeli waliomba Mungu awape mfalme,haikuwa mapenzi yake wawe na mfalme mwengine ila mungu.walipewa mfalme lakini kwa hasara.nakuomba unapomuomba Mungu kwa jambo hili mwache Mungu afanye mapenzi yake,labda si mapenzi ya Mungu mwuoane na huyo na ukilazimisha atakupa lakini kwa hasara kwako,na ukiwacha Mungu afanye mapenzi yake, utakupa kwa faida yako, ikawa ni huyo au ni mwengine.

  Mungu akubariki wakati unazingatia mambo haya.

 2. Pale ambapo urafiki kati ya watu wawili ni wa karibu mno na mmoja wao anasita kuelekea katika ndoa huwa ni changamoto sana kuambiana na hupelekea kusababisha maumivu zaidi. Pamoja na maumivu ya moyo ambayo mtu anaweza kuwa nayo nafikiri ni baraka kubwa kuishi na mtu anayekupenda kikamilifu. Mapenzi yasiyorejeshwa (unrequited love) ni maumivu ya kudumu na wala si mpango wa Mungu. Hivyo mimi ushauri wangu ni huu: chukua hatua za kurudi nyuma, punguza ukaribu na mtu huyo ikiwezekana hata kukata mawasiliano kwa muda ili upate fursa ya kuona mambo sawasawa, pengine hata kutoa fursa kwa vijana wengine kukukaribisha kwao (na hili ndio kusudi.) Ukiona vyema mwite mwenzako mzungumze kama watu wazima na umwambie nia ya moyo wako. Kama akikukubalia, vyema. Kama sivyo, rudi nyuma upone. Moyo hutaka kile inachokitaka na tamaa ya moyo si kiongozi cha kuaminika katika maamuzi magumu. Maumivu ya moyo huisha- hivyo maumivu yasiwe chanzo cha kuacha kutumia busara. Wengi huachwa kwenye mataa au kuingia kwenye ndoa zenye matatizo kwa kusisitiza uhusiano wenye walakini tokea mwanzo. Ninazungumza kutoka katika uzoefu wangu na pamoja na maumivu niliyoyapata na kuyasababisha, namshukuru Mungu kwamba haya yaliniwezesha kupambanua baina ya mambo ya msingi na yasiyo ya msingi. Narudia: ni baraka kubwa kupata mwenzi anayekupenda na kukuhitaji. Maisha yako yatakuwa na furaha.

 3. Nakupa pole kwa hilo.Naungana na Maoni na ushauri wa waliotangulia Nasaha zote nimezikubali naomba uzitendee kazi.Naongezea kwa kusema,Akili yako Isichoke Kufikiri MEMA/Kutenda MEMA.Kuna macho ya mwili ambayo mara nyingi huleta matokeo mabaya,Kuna macho ya rohoni ambayo hujificha sana lkn Itakuja kufahamika baadae.Usimlazimishe sana ila Jitahidi kufanya uchunguzi ujuwe Anania gani na wewe!!Kila la heri!!

 4. Pole ndugu kwa maumivu hayo ya moyo, kwamba hukipati ukipendacho.
  Nimesoma michango ya wasomaji na kwa kweli ni ya muhimu kuyazingatia.
  Napenda niseme kitofauti kuwa, mwenzako jayupo tayari kwa sasa kuingia katika hatua nyingine ya mahusiani, kwa sababu anazozijua yeye na hataki kukuambia ukweli kwa sababu anazozijua. Kweli ndiyo itakayokuweka huru, muo m be mungu uuujue ukweli.
  kama ukweli ni kwamba hapendi muishi pamoja ni jambo jema.t kuliko akabadilike wakati mmeshafunga ndoa takatifu. Kama msomaji mmoja alivyosema kuwa inawezekana kuwa huo sio mpango wa Mungu kwako.
  Joyce mayer huwa anadema wakati mwingine sisi wapendwa tunapanga mipango kisha ndio tinamshirikisha Mungu, kuwa huu ndio mpango wangu Mungu naomba nibariki na ufanikishie hili. Mungu kwa uaminifu wake anatufanikisha, lakini sio muda wote. Cha wewe unachotakiwa kuomba ni kuwa unahitaji kuolewa akupe mime mwema, atatoka wapi ? Mungu anajua. Ondoa holo la kusema huyu ndie nimpendaye au nimtakaye

 5. Mm:ni
  ELIFURAHA M MOLLEL
  Dada JJ ushauri wangu ni kwamba mtegemee Mungu baadam anapatikana, yy ni msaada wa karibtu wakati wa shida uwenda huyo mwezi wako mambo yake hayajakaa sawa na anakudhamini sana hataki uje ukae maisha ya shida cha msingi na sekondari muombee sana na ikiwezekana hata mfuate mwezi wako alipo umulize kulikoni, kwan may be ww unamwogopa mwezi wk na dunia ya sasa hv ni dunia ya ukweli na uwazi kama unamwogopa hutaweza kujua kuna shida gn, BIBILIA TAKATIFU inatafundisha kwamba mke Mwema mwenye busara hutoka kwa BWANA vilevile mme mwema mwema mwenye busara hutoka kwake mtegemee sana bwana mungu atakujibu sawa sawa na huhtaji kwko MUNGU WA MBINGU NA NCHI AKUBARIKI SANA BARIKIWA SANA

  AMEN

 6. Dada J.J.
  “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”- Mithali 14:12. “Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu” Mithali 16:2, “Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu; Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia”- Mithali 17:24, “Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huipima mioyo”- Mithali 21:2.

  Akili na macho hudanganya, mgonje Mungu na hupaswi kulalamika kwa hilo! Jifunze kumshangilia Bwana wakati wa shida!
  Neema ya Bwana ikufunike.

  Siyi

 7. Maombi ni zaidi ya kufunga na kunena kwa lugha na kukesha maombi ni kuomba katika kusudi la Mungu,
  Je niulize unadhani huyo ni kusudi la Mungu kwako?

 8. Bible says ” maandalio ya moyo n ya mwanadamu lakn jawabu la ulimi latoka kwa Bwana” kama umeamua kutumia akili basi maliza kwa akili, ila nakushauri mtumaini Mungu na majibu ya Mungu huwa n tofauti n mitazamo yetu dada, angalia ucje ukajuta milele ktk NDOA

 9. Bwana Yesu asifiwe mimi nakushauri endelea kumngoja Bwana Biblia katika mhubili inasema kila jambo kuna wakati wake .wakati wa kuolewa na wakati wa kutoolwa /wakati wa kufurahi na wakati wa kutokufulahi acha haraka tumia tunda la kuvumilia Mungu anayo sababu ya kuchelewesha kwa Mungu hakuna kuchelewa wala kuwahi amina

 10. Pole sana, kuna tatizo la msingi katika uhusiano wenu.Tafuta kitabu cha MWENZI WA MAISHA, efatha bookshop,DSM,Kimahama,arusha au BIble society,Dodoma.Ni kitabu kizuri,utapata majibu ya tatizo lako na hatua za kuchukua! Barikiwa sana

 11. Shalom dada JJ,
  Mimi ntakupa ushauri mdogo tu, wenye sehemu kuu mbili kama ifuatavyo. (1) Mosi, kabla hujaanza kufikiri kwamba may be kuna kitu hakiko sawa kwa mwenzako, fanya tathmini kwanza ya mahusiano kati yako na Mungu yalivyokuwa kabla ya kumpata huyo mtu na yalivyo sasa.
  Mungu alimwambia Ibrahimu amtoe sadaka mwanaye wa pekee. Hakuna kitu ambacho Mungu hakuwa anajua kuhusu moyo wa Ibrahimu, mpaka afanye jaribio (experiment) ili ajue. Lakini ukweli ni kwamba tathmini ya Mungu kuhusu moyo wa Ibrahimu ilionyesha kwamba Isaka ameanza kuchukua sehemu ya Mungu kwenye moyo wa Ibrahimu. Mungu aliona ameshapata mgombea mwenza kwny moyo wa Ibrahim, akamwambia mtoe awe sadaka. Ibrahimu alitii sauti ya Mungu, akawa tayari kumtoa awe sadaka. Mungu hakupenda mahusiano yake na Baba wa imani yaingiliwe na Isaka. Sasa yawezekana na wewe huyo (mtu) ndiye Isaka wako, na kama Mungu akiona nafasi yake kwenye moyo wako inaanza kuchukuliwa, Mungu haoni shida kumzuia.
  Pia soma habari za Musa. Hakufanya kosa kubwa sana kuliko wengine kiasi cha Mungu kumzuia kuingia Kanaani, lakini naamini wana wa Israel walimuamini kiasi cha kumwona Mungu kwao, ndo maana Musa alipokawia mlimani walishauriana watafute Mungu mwingine. Mungu alijua Musa angeingia Kanaani wangeenda kumuabudu. Mungu akamzuia asifike kanaani. Inawezekana huyo ni Musa kwako, na hana kosa, lakini Mungu akamzuia kwa usalama wa roho yako. Point yangu ni kuwa MAKINI NA NAFASI YA MUNGU KWENYE MOYO WAKO, MWANADAMU ASIICHUKUE.
  (2) Pili, Ukishamaliza tathmini na kutekeleza point ya kwanza hapo juu, amini kabisa kwamba kama hilo jambo limetoka kwa Mungu, ni ahadi ya Mungu kwako, basi itatimia tu, kwani Mungu si mtu hata ajute, au aseme uongo,,,, Hesabu 23:19. Ahadi yako ijapokawia ingojee dada yangu (ingoje ahadi huku ukiomba …. Habakuki 2:3). Ijapokawia, ingoje.

 12. Mpendwa katika Bwana,

  Kwanza nakupa pole kwa tatizo lako hilo, lakini ufumbuzi wa tatiozo hilo upo kwa YESU mwenyewe, ni wewe tu kubadilisha mbinu ya kuomba kwako ili uweze kupokea majibu yako kutoka kwa Bwana! Inawezekana ukawa unaomba na kufunga sana lakini usijibiwe maombi yako kwa kuwa ombi lako ni tofauti na mapenzi ya Mungu kwako (1 Yohana 5:14-15), lakini pia Mtume Yakobo anasema unaweza kuomba lakini hupati si kwamba huombi kwa bidii la hasha, bali unaomba vibaya kwaajili ya matakwa yako mwenyewe na sio mapenzi ya Mungu! Kuomba kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu ni kwa muhimu sana ili tuweze kupokea kutoka kwa Mungu kwa kuwa Mungu ndiye ajuaye mipango ya maisha yetu hapa duniani (Yeremia 29: 11). Unapoenda mbele za Mungu jitahidi kumwomba Roho Mtakatifu ili akuwezeshe kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu, na sio kwa kufuata hisia au akili zako mwenyewe, na wala usiwe na majibu yako kichwani na kumlazimisha Mungu akujibu kama vile unavyopenda wewe. Mimi pia nilipitia hali kama hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya mitano bila majibu yoyote yale hadi nilipobadili mbinu ya kuomba na kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie, sasa nimefanikiwa kwani Mungu amenijibu na kunipa kile nilichomwomba. Jambo lingine la muhimu hapa ni kuutafuta uso wa Mungu kwa bidii sana, halafu Mungu atashughulika na maisha yako kwa kuwa anajua tunachohitaji kabla ya sisi kuomba (Mathayo 6:32-33). Ukiutafuta uso wa Mungu na kuyajua mapenzi yake katika maisha yako Mungu hawezi kukuacha kamwe bali atashughulika na maisha yako kwa kuwa anajua mahitaji yako (Isaya 65:24). Nikutie moyo mpendwa wa Bwana, usikate tamaa bali endelea kumtafuta Mungu kwanza na kujitahidi kujua yapi ni mapenzi ya Mungu kwako (yaani kusudi la Mungu katika maisha yako) kwa kuwa Mungu hufanya kazi na wale wampendao wanaotembea katika kusudi lake katika kuwapatia mema (Warumi 8:28-30). Ukijua yapi ni mapenzi ya Mungu kwako ni rahisi sana kujua kipi niombe, kipi ni Mungu anataka na kipi ni machukizo kwake na hivyo sipaswi kuomba hicho, na Mungu Roho Mtakatifu atakuwezesha kuomba vile inavyompendeza Mungu (Warumi 8:26-27). Lakini pia jitahidi kusoma sana neno la Mungu litakusaidia kujua lipi kusudi la Mungu na ahadi ambazo Mungu amewaahidia wale awapendao, na hivyo uweze kuomba kwa kufuata ahadi za Mungu kwako. Mungu wangu akubariki sana na akutie nguvu ili uweze kusonga mbele bila kukata tamaa! AMINA.

 13. Amen,
  1. unamuomba Mungu kila siku ili huyo awe mwenzi wako lakini je, umeshasikiliza jibu toka kwake unayemuomba?? kawaida yeye huwa ana majibu matatu ndiyo, hapana, subiri, ndiyo kama unayempenda ndiye huyo aliyekuchagulia yeye, subiri kama anataka awatengeneze vilivyosalia ambavyo kama hajatengeneza kabla ya kuwaunganisha basi mnaweza kufarakana milele, Hapana kama anajua huyo si Adam wako na Adam wako yupo kwingine, sasa nikuulize ktk kuomba kwako miaka yote hiyo ulijibiwa nini??

  2. ukiona mambo hayaendi unapaswa uulize kwanini hayaendi, je ulishamuuliza roho mtakatifu kwanini??? alikupa jibu gani?? maana inawezekana wewe una shida au huyo unayempenda ana shida labda majini mahaba yanazuia au mizimu ya ukoo haijamkubali mmoja wenu, ni lazima uende rohoni uangalie kwanini mambo hayaendi.

  Kristo na akupe kilicho bora zaidi, siku njema.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s