RAIS ASIYE NA YESU NI MZIGO KWA TAIFA LAKE…..

Mgombea kuteuliwa Uraisi kwa ticket ya CCM, Mchungaji na Jaji Augustine Ramadhani akiongoza Ibada katika moja ya huduma yake!

Hili tumeliona  juzi siku ambayo TAIFA LA MAREKANI lilipitisha NDOA ZA JINSIA MOJA SASA MAJIMBO YOTE 50 YA MAREKANI, Jambo hili KUZIMU NI SHEREHE, Lakini MBINGUNI Hakuna hata mmoja ALIYEFURAHIA,SIYO MUNGU BABA,MUNGU MWANA,WALA ROHO MTAKATIFU,NA HILI HALIMAANISHI MUNGU AMEMSHINDWA SHETANI HAPANA SHETANI HAJAI KABISA KATIKA MKONO WA MUNGU,WALA UFALME WA MUNGU,NA KAMWE HAWEZI NA HILI Tunaliona PALE AMBAPO SHETANI ALIPOTAKA KUMPINDUA …MUNGU MBINGUNI WALIOTUMWA KUMSHUSHA SHETANI NI MALAIKA,KWANI UNAFIKIRI MUNGU ALIKUWA HAWEZI, NO! MUNGU ANAWEZA ILA HAWEZI KUPAMBANA NA KIUMBE ALIYEMUUMBA (MUNGU ALIWAACHIA MALAIKA KAZI HIYO,KWANINI?? LEVEL YA SHETANI HAILINGANI NA MUNGU HATA KIDOGO….

Leo hii SHETANI KAINGIZA NDOA YA JINSIA MOJA MAREKANI ASIDHANI MUNGU HAONI,LA HASHA! ILA MUNGU ANAZIDI KUTUFUNDISHA TUWE MACHO NA KUONA YALE YALIYOANDIKWA KATIKA BIBLIA NI KWELI NA HALISI,HAPA WATEULE TUJIFUNZE..

Mambo ya Walawi 18:22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”

Mithali 5:18 “Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako.”

19 Ni ayala apendaye na paa apendezaye; Maziwa yake yakutoshe sikuzote; Na kwa upendo wake ushangilie daima.

Warumi 1:23 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.

24 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.

25 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;

26 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.

1Wakorintho 6: 8 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 11 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.

SOMA na MWANZO 19:1-13…

Ufunuo 22:11-12 ” Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. ”

–Mwalimu Conrad

7 thoughts on “RAIS ASIYE NA YESU NI MZIGO KWA TAIFA LAKE…..

 1. Mr Milinga,
  Ni kweli, rais hawezi kwa nguvu zake akayazuwiye maovu. Lakini zambi ya rais inaweza angamiza taifa lake. Ndoa ya jinsia moja siyo kwamba ilikuwepo, no no no; kwani kabla rais ahalalishe lile tendo katika katiba, lile tendo lilikuwa ufiraji, ushoga tu. Lakini leo limeitwa ndoa kwani katiba inalikubali. Ina maana dhambi inahalalishwa at the point that makanisa wameanza “bariki hizo ndoa”. Rais hawezi zuwiya dhambi, ndio, lakini kuihalalisha inaweza angamiza zaidi.

  Ubarikiwe.

 2. WAPENDWA. Huu ni wakati wa Kila ANDIKO LA BIBLIA KUTIMIA.Kama MUNGU alisema katika Neno lake watatokea MASHOGA,WAPINGA KRISTO,MANABII na MAKRISTO,WAALIMU wa UONGO,MAFUNDISHO YA MASHETANI,WATU WAKAIDI WENYE MASKIO YA UTAFITI,…..nk haya yote na mengine aliyoyanena MUNGU ni LAZIMA YATOKEE/YATIMIE na HAKUNA Mkristo anayeweza kulizuia NENO LA MUNGU lisitimie.Chakufanya, ni kujisalimisha Bwana Yesu Kristo/Kumkabidhi YESU maisha yako.KANUNI ya kuwa Mkristo ni KUTUBU na KUBATIZWA katika JINA LA YESU KRISTO (MATENDO 2:38-39).Ikimbieni Ghadhabu ya Mungu inayokuja Duniani.

 3. MWALIMU CONRAD, Umesema Mbinguni kuna Mungu Baba,Mungu Mwana na Roho Mtakatifu.Hebu nifafanulie Kimaandiko.

 4. Kuna jambo watu wengi hawaelewi.

  Huwezi kulifanya taifa lote likawa ni Wakristo tena walokole. Haiwezekani.

  Kama kuna wapendwa wanafikiria hivyo watasubiri sana. Marekani siyo tu kwamba lina mchanganyiko wa wapagani na wakristo na waislam bali pia lina uhuru wa kuabudu.

  Swala la ndoa za jinsia moja hata kama likizuiliwa kisheria haina maana kwamba watu wenye tabia hizo hawatafanya uovu huo. Huwezi kuzuia uovu kwa kutunga sheria za kuwazuia watu wenye jinsi moja kulalana.

  Hata Mungu alipowakataza wana wa Israel alifanya hivyo baada ya kuona kuwa tabia hizo zilikuwepo.

  Kwa hiyo hata kama utampata Rais anayempenda Yesu, hataweza kuzuia sheria kutungwa ya kuwaruhusu watu wenye jinsi moja kuishi kama ndoa halali kwa sababu haendi Ikulu kuendesha Ibada.

  Mbona kuna sheria nyingi zipo Tanzania na duniani kote kama vile sheria za vilevi, sheria za sigara, sheria za vyombo vya habari, nk na zote zimeruhusu mambo yasiyofaa nchini.

  Mfano, Sheria ya Uvutaji Sigara inaruhusu watu kuvuta sigara ila isiwe hadharani.

  Sheria ya vilevi inaruhusu watu kunywa na kulewa ila kistaarabu. Hata bia kali sana kama vile Konyagi zimeruhusiwa ingawa hazina tofauti na gongo au bangi.

  Sheria ya vyomvo vya habari inazuia kurusha mambo yasiyofaa kimaadili kama vile picha za ngono na utamaduni usiofaa. Lakini utakuta vyombo vingi vya habari vinarusha miziki na picha ambazo mara nyingi hata hazifai.

  Kwa hiiyo kumpata Rais anayempenda Yesu haitasaidia kuondoa maovu nchini.

  Kitakachosaidia kuondoa maovu nchini ni Injili pekee ya Ufalme iokoayo mamia kwa maelfu lakini siyo Rais wa nchi.

 5. Obama no mzigo sana kwa taifa hili. Shetani uses many tools to brainwash masses and inherit them into his wicked kingdom.
  obama, is arguably the most dangerous and wicked president to ever rule America. As a Christians living here I am sad to see how time and again the masses fall for his lies….

  When a nation detours from the word of God what is left is confusion, fear and distraction as we see it now….

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s