Roho ya kukata tamaa!

rejection

BWANA YESU ASIFIWE, naomba msaada wa maombi, naitwa EVA, nasumbuliwa na presha na roho ya kukata tamaa. nina mtoto mdogo hajafikisha miaka miwili! Kila mmoja naomba aseme kitu juu yangu. Mungu awabariki

–E

Advertisements

4 thoughts on “Roho ya kukata tamaa!

 1. Pole sana dada Eva!

  Ila mimi naomba nikushauri kwamba INABIDI UPAMBANUE VIZURI ili ujue ADUI YAKO NANI. Maana huwa inasemwa ADUI NAMBA MOJA WA MTU NI MTU MWENYEWE!

  Hili hutokea kwa mtu KUTOJIKUBALI na kuanza kutafuta wa kumtupia Lawama. Mfano ni rahisi mtu kusema NINA ROHO YA KUKATA TAMAA badala ya kusema NIMEKATA TAMAA!

  Ninachosema hapa ni kwamba JITAMBUE NAFSINI, tambua pale uliosimama. Jione kwamba Unaweza kuamua juu ya nafsi yako. Jione jinsi ambavyo UNAWEZA KUKATAA MAWAZO HASI. Tambua NGUVU iliyomo katika Maamuzi yako. Ukishatambua hili utaona namna ambavyo unazo NGUVU bado ambazo unaweza kuzitumia kuchagua UJASIRI na Kukata tamaa kutaondoka.

  Kama ni suala la mtoto linakukatisha tamaa namna ya kumlea, washirikishe hata wazazi wako au mzazi mwenzio, kama yuko karibu nawe, ili mzigo huo uwe mwepesi kwako. Isije ikawa hilo ndilo linakukatisha tamaa.

  Mungu wa mbinguni akusaidie.

 2. Eva,
  Mungu yupo paoja nawe. Roho Mtakatifu akufariji. Usiogope. Nimeomba kwa ajili yako naamini Mungu atakusaidia.
  Damu ya Yesu inenayo mema, inene rehema kwa ajili yako pia, sawa sawa na ahadi za BWANA na kwa ajili ya Yesu Kristo uwe huru kweli kweli
  Neema

 3. E si maombi tu, unahitaji ushauri pia, tafuta mtu ambaye unaona kwamba ni muaminifu mwenye hofu ya Mungu ambaye unaweza ukambwagia moyo wako, aliyekata tamaa anahitaji maombi lakini si maombi tu bali ushauri pia faraja, kutiwa moyo nk nk, unapoongea na mtu anayekutia moyo ile sumu iliyoletwa na kukata tamaa inayosababisha mapigo ya moyo yatoke nje ya mstari hunyonywa na faraja zile ndipo unapojikuta unajua mzima mbali na magonjwa na hofu. presha ni matokeo ya msongo ulionao, inaweza kuwa pia kuna kutokusamehe ndani yako kwa waliokukosea, au labda kutopata kile ulichotarajia kukipata, jichunguze nini chanzo, nkutakie ufumbuzi mwema wa matatizo uliyonayo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s