Utasimama Wapi?

that_cry_behind_you

Hezekia alipougua ugonjwa ambao aliambiwa utamsababishia Kifo alilia mbele za Mungu, akamkumbusha jinsi alivyokwenda mbele zake kwa UKAMILIFU na Unyoofu wa Moyo na Mungu akamponya. (2Wafalme 20:1-7).

Mtu huyu wa Mungu alikuwa amejitengenezea Hazina na Ushahidi wa kumfanya akumbukwe na Mungu. Mungu alikubaliana kabisa na maisha ya Hezekia kwamba yalikuwa ni Mema!

Katika Kitabu cha Hosea 6:1 kuna maneno haya:

Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu.

Hapo tunaona jinsi watu wa Mungu walivyojikuta katika matatizo kwa kuwa Mungu mwenyewe ndiye aliyekuwa Amewararua. Hawa wakawa wanahimizana Kumrudia Mungu kwa kuwa ni mwenye Rehema. Hawakuwa na ujasiri wa kusema wamwambie Mungu angalau jema fulani walilofanya kwake.

Maandiko hayo mawili yanaonyesha namna mbili za kwenda mbele za Mungu. Aliyotumia Hezekia na hii inayoelekezwa katika Hosea.

Ni changamoto kwetu leo kwamba Ikitokea umepatwa na tatizo, utatumia njia gani wakati wa kumuomba Mungu akutoe katika shida hiyo?

Utamkumbusha mema uliyotenda au Utaomba rehema zake tuu ndiyo zikubebe? Je, tuna ujasiri wa kumwambia Mungu kwamba kuna mema kadhaa ambayo basi hata Mungu ayaangalie hayo ili aiondoe shida iliyopo mbele?

Ni jambo la kutafakari kwetu sote!

JP

Advertisements

5 thoughts on “Utasimama Wapi?

 1. Wapenzi,
  Michango yenu ina nguvu sana kwa pachiko la JP. Ila nilichoshindwa kuelewa ni baadhi yenu kuukataa utu wema wa Hezekia uliomfanya Mungu kusikia maombi yake (Hezekia). Ninavyoelewa mimi, pamoja na madhaifu yetu ya kila siku, tunaweza kuwa wema pale tunapotenda mema hasa utendaji huo unapotokana na msukumo wa rohoni. Kama wasafiri wa kwenda mbinguni, tunakufa kila siku katika ulimwengu wa mwili (ubinafsi, uchoyo, tamaa mbaya, wivu, chuki, hasira n.k.) na tunakuwa hai katika ulimwengu wa roho (kuwa na matunda ya roho kama alivyosema Sungura). Tunaweza tukawa tunajikwaa na kuanguka mara kwa mara kwa isivyo bahati, lakini hali hiyo, haituzuii kuwa wema.
  Yesu alisema, “Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake” Luka 6:43-45.

  Hii haina maana kwamba tunakuwa wema kabisa (bila doa). Hasha! Kadri tunavyoukulia wokovu, ndivyo tunavyozidi kuushinda ulimwengu na mambo yake kama Kristo alivyoushinda! Haya ni mapambano! Kupigana ni lazima. Sasa tunapopigana vizuri, tunakuwa ndani ya kauli ya Kristo katika Luka 6:43-45. Anyway, siandiki ili kubishana na mtu, ila nilikuwa natoa uellewa wangu wa neno kuhusu hoja nzuri iliyotolewa na JP ikifuatiwa na michango mizuri kutoka kwenu nyote.

  Neema ya Bwana iwafunike

  Siyi

 2. Ivi mtu kuwa mwema au mwenye haki kunatokana na nini?

  Nafikiri JP yuko sahihi kuwa maisha mema ya Hezekia ndo yalifanyika rejea mbele za Mungu, yakawa sababu ya Hezekia kulia machozi na kisha Mungu kuyaona hayo machozi yake.

  Maisha y mtu kutafsiriwa kuwa ni mema kunatoka na yeye kutenda matendo mema. Na mimi ninavyoelewa mtu kuwa mwema kunatokana na kutenda matendo mema, maana hayo ndo tumeumbwa tuyatende.

  Pia iko mifano mingine wenye kuonesha kuwa Mungu huguswa na matendo yetu zaidi; Tunazijua habari za Kornelio : Acts 10; 1- At Caesarea there was a man named Cornelius, a centurion in what was known as the Italian Regiment. 2 He and all his family were devout and God-fearing; he gave generously to those in need and prayed to God regularly. 3 One day at about three in the afternoon he had a vision. He distinctly saw an angel of God, who came to him and said, “Cornelius!”

  4 Cornelius stared at him in fear. “What is it, Lord?” he asked.

  The angel answered, “Your prayers and gifts to the poor have come up as a memorial offering before God.

  (MAOMBI YAKO NA SADAKA YAKO KWA MASIKINI)

  Tunazijua pia habari za mwanamke Dorcas: Acts 9: 36 In Joppa there was a disciple named Tabitha (in Greek her name is Dorcas); she was always doing good and helping the poor. 37 About that time she became sick and died, and her body was washed and placed in an upstairs room. 38 Lydda was near Joppa; so when the disciples heard that Peter was in Lydda, they sent two men to him and urged him, “Please come at once!”

  39 Peter went with them, and when he arrived he was taken upstairs to the room. All the widows stood around him, crying and showing him the robes and other clothing that Dorcas had made while she was still with them.

  40 Peter sent them all out of the room; then he got down on his knees and prayed. Turning toward the dead woman, he said, “Tabitha, get up.” She opened her eyes, and seeing Peter she sat up.

  (ALITENDA MEMA NA KUSAIDIA MASIKINI)

  Lakini jambo la mwisho naomba tukumbuke kuwa UTU WEMA ni tunda la roho, kwa hiyo tunatakiwa kuwa wema.

  Baada ya kusema hayo basi niseme kwamba tunatakiwa kufuatilia ili kujua Yesu aliposema kuwa hakuna mwema il Mungu alimaanisha nini!

 3. Rehema zake zitubebe sote Watanzania ndilo ombi coz sote tumetenda dhambi naam sote pia na kupungukiwa na uwepo wa Mungu

 4. Tukiwa ni watoto wa Mungu ni lazima tujitahidi kuonyesha kwamba, tumekubaliwa na Mungu mwenyezi, watenda kazi tusio na sababu ya kutahayari. Tukimwendea Mungu kwa shida, kwa shukurani ama kwa haja yoyote yatupasa tumwendee kwa ujasiri tu kwamba yeye ametukubali, kwa sababu ni kwa Neema yake ambayo ndiyo inatufanya tufike hapa tulipo ama kuwa kama tulivyo leo. Si kwa wema, si kwa uzuri wala si kwa juhudi yoyote Mungu hutusaidia soma Yhn 15:5, yeye hutusaidia kwa upendo tu, upendo wa AGAPE yaani pendo lisilo na sababu yeyote! Sikwamba watu wasiweke mbele matendo mema la, Neno linasema tutamuona Mungu katika maisha yetu tukiwa na huo UTAKATIFU, utakatifu hutokana na utakaso, na utakaso chanzo chake ni Neno la Mungu ambalo kwa ujumla wake ndiyo lililobeba matendo mema, mfano mmojawapo ni kule kufanya mapatano ya amani na watu wote hutusabibishia kuupata utakatifu ambao katika huo ndipo tunapo muona Mungu katika maisha yetu!

  Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na ndugu yangu JP kuwa inafaa kujikagua na kuona kama lipo jambo lolote jema ambalo tunaweza kuliegemeza katika utetezi kwa wakili wetu (Bwana Yesu) ili kwamba, kwakweli Mungu litamfanya aonekane katika shida zetu. Lakini kwa habari ile ya Hezekia, si kwamba Mungu alimponya kwa vile ni Mwema la, ila tu alitenda matendo mema, kwa hiyo watu wasijizanie kuwa ni kwa wema wa mtu Mungu hupokea na kusikia maombi!

  Mtu mmoja anaweza kushangaa kuwa, yawezekanaje mtu asiye mwema akafanya mambo mema?! Hapa sina muda wa kuelezea mifano iliyopo na au ni kwa jinsi gani inawezekana, ila elewa tu kwamba inawezekana! Katika ile 2wafalme 20:3, Hezekia anamuomba Mungu hivi “3“Ee BWANA, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote na kufanya yaliyo mema machoni pako.’’ Hezekia akalia sana sana.” Lakini Mungu kupitia Nabii wake Isaya, anajibu Hezekia kuomba kwake katika ile 2Waflme 20:5 hivi, “5“…………..: ‘Nimeyasikia maombi yako na kuona machozi yako, nitakuponya. Katika siku ya tatu kuanzia sasa utapanda kwenda hekaluni mwa BWANA.” Ukiuangalia kwa makini mstari huo utaona kwamba kilichoonwa kuwa ni “matendo mema” ya Hezekia kwa Mungu ni ‘Utumishi’ na wala si wema wake Hezekia; ndiyo maana anaponywa na kuambiwa kuwa atarudi kutumika Hekaruni baada ya siku tatu!

  Hatupaswi kusitasika ama kujaa hofu tunapotaka kupeleka maaombi yetu kwa Mungu ili kupata msaada wake katika eneo lolote katika maisha yetu, kwa kujihofia kuwa hatutakubaliwa kwa kuwa hatuna wema wa kutosha kumshawishi Mungu atuponye ama atusaidie haja zetu, kwa sababu Neno linasema “Mwema ni mmoja tu, ndiye Mungu”! Hezekia akiwa mfano kwa mjibu wa mleta maada hii, nami na mrejea Hezekia matendo yake ili kuonyesha wazi pia kuwa hakuwa mtenda mema yote ama mwenye kufikiri kwa Busara muda wote. Ukiendelea kuisoma hiyo 2Wafalme sura ya 21utaona ambavyo Hezekia alisababisha Taifa lake kuingia mikononi mwa wa Babeli, siwezi kusema Hezekia “hakumuelewa” Mungu, ama Hezekia “alimjaribu” Mungu, alipoambiwa kutakuwa na “Amani” katika kipindi chote cha uhai wake; kwa Neno hilo yeye Hezekia akawaruhusu maadui waione kila Siri ya nchi na hazina yote! 2Wafalme 21: 12-19 inasema hivi, “12Wakati ule Merodak-Baladani mwana wa Baladoni mfalme wa Babeli akamtumia Hezekia barua pamoja na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua kwa Hezekia. 13Hezekia akawapokea wale wajumbe na kuwaonyesha vitu vyote vile vilivyokuwa katika ghala zake, yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu cho chote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha. 14Kisha nabii Isaya akaenda kwa mfalme Hezekia na kumwuliza, “Hao watu wamesema nini na wametoka wapi?’’ Hezekia akajibu, “Wametoka nchi ya mbali, wametoka Babeli.’’ 15Nabii akauliza, “Wameona nini katika jumba lako la kifalme?’’ Hezekia akasema, “Wameona kila kitu katika jumba langu la kifalme, hakuna kitu katika hazina yangu ambacho sikuwaonyesha.’’ 16Kisha Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la BWANA: 17Hakika wakati utakuja ambao kila kitu katika jumba lako la kifalme na vyote: 17Hakika wakati utakuja ambao kila kitu katika jumba lako la kifalme na vyote vile ambavyo baba zako waliweka akiba mpaka siku hii ya leo, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna cho chote kitakachobaki, asema BWANA. 18Baadhi ya wazao wako, nyama yako mwenyewe na damu yako, ambao watazaliwa kwako, watachukuliwa, nao watakuwa matowashi ndani ya jumba la mfalme wa Babeli.’’ 19Hezekia akajibu, “Neno la BWANA ulilosema ni jema.’’ Mfalme alifikiri, “Lakini si patakuwa na amani na usalama wakati wa uhai wangu?’’”

  Kwahiyo Hezekia hakutenda Vema katika hilo, cha Msingi kila tunapotaka kumwendea Mungu ni lazima tutambue kuwa YUPO, na tumwendee kwa Ujasiri huku tukiamini kabisa kwamba yeye kwa pendo la ajabu ametupenda na hivyo ametukubali tu kuwa sisi ni watoto wake na hivyo tunazo haki za kitoto kwa baba yetu. Sisi ni watenda kazi ambao hatuna sababu ya kutahayari, na hatuna wema wakutosha kuondoa makosa yetu, na hivyo ati tupate kukubaliwa sala zetu, ila kwa NEEMA yake sisi tunapaswa kutosheka!

  “Ufahamu ni chembe ya Uhai!”

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s