Matumizi ya UPAKO

anointed

UPAKO, kwa tafsiri ya jumla, ni Nguvu ya Mungu inayoingia/inayokaa/inayotenda kazi  ya Mungu ndani ya mtu kutokana na Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu huyo!

Siku hizi kumeibuka MATUMIZI mengi ya Upako kama vile Kuondoa Chunusi Usoni, Kulainisha Ngozi ya mwili, Kufanikiwa Biashara, Kufaulu Mitihani, Kusafiri Nje ya Nchi, Kumiliki Mali nk.. Ambapo Watu mbali mbali wamekuwa wakitoa Matangazo na KUALIKA WATU kwa ajili ya KUWAOMBEA ILI KUPOKEA Upako kwa ajili ya kimojawapo ya au vyote vilivyotajwa hapo juu!!

Je, Hayo Nayo NI MATUMIZI SAHIHI YA UPAKO?

Advertisements

5 thoughts on “Matumizi ya UPAKO

 1. Wapendwa,
  Kuna sabau ya kujua maana ya sentensi ‘utafuteni kwanza ufalme wake…, na mengine yote mtazidishiwa

  Ukianza kutafuta maana ya ufalme utakutana na kuwepo kwa mfalme ndo kunatengeneza ufalme, utakutana na kuwepo kwa himaya, n.k.

  Lakini ukiendelea kunyambua jambo hili mwisho wa siku utakutana na mfumo wa ufanyaji mambo unaotoka kwa huyo mfalme, au kwa hiyo himaya. Watu wa himaya fulani utasikia wanasema kuwa ‘sisi kwetu huwa tunafanya kwa namna hii, au ile. Kufanya kwa namna hii au ile huo ndo ufalme(mfumo)

  Kwa hiyo muktadha mzima wa kuutafuta Ufalme wa Mungu, si kutafuta himaya ya Mungu, bali ni kutafuta kujua jinsi Mungu (Mfalme) anavyofanya na anavyotaka sisi tufanye. Ni kutafuta kujua kanuni za utendaji za Mungu, jinsi ambavyo anataka tutende ili tuwe sawa na alivyokusudia tuwe.

  Haki yake( Mungu):
  Kutafuta haki ya Mungu ni kutafuta kujua zile tabia za kimaadili ambazo zinakubalika mbele zake. Au kwa maneno mengine ni kwamba; Haki ya Mungu ni tabia za kimaadili za ki-Mungu.

  Hivyo, Yesu alikuwa anataka tujue kanuni za utendaji za Mungu ili tutende sawasawa na alivyotukusudia au anavyotaka, kisha tuzijue tabia za kimaadili za ki-Mungu.

  Ukisha kuwa na hivyo vitu matokeo yake ni kupata vitu ambavyo akili/mwili unavihitaji, e.g; Mavazi, malazi(nyumba), afya, chakula, na takataka zote ambazo huu mwili unataka.
  Kumbuka nia ya huu mwili na watu wasiomjua Mungu ni kuvipata hivyo vitu (mazidisho) kwanza, iwe kwa kufuata kanuni au kwa kutozifuata.

  Sasa, upako ni nguvu inayokuwezesha kutenda katika ufalme wa Mungu. Ukipata ufalme wa Mungu ila haki yake ukaikosa, lakini ukawa na upako, kitakachotokea ni matumizi mabaya (misuse) ya huo upako. Maana utakuwa umepungukiwa zile ‘Godly moral standards’.

  Mtu wa namna hii anaweza akawa anafurahia tu kuona akigusa watu wanaanguka chini bila sababu ya lazima kufanya hivyo, simply kwa sababu ndani yake kuna hiyo nguvu ya Mungu ya kumwezesha kutenda, lakini maadili ya kuitumia hiyo nguvu hana.

  Lakini tujiulize swali kuwa, huyu Mungu anayesema kuwa anajishugulisha hata na mambo yetu madogomadogo sana, angejisikia vibaya mimi kutumia hiyo nguvu(upako) kuondoa chunusi usoni, au kulainisha ngozi yangu, kufaulu mitihani?

  Kwa nini ajisikie vibaya, kwani anafurahia mimi kuwa na chunusi usoni au kuwa na ngozi yenye harara, au kufeli mitihani?

  Shida wengi tunadhani kazi ya Mungu ni kuhubiri, kuombea wagonjwa wenye magonjwa makubwa, kuwa wachungaji, kufanya maombezi tu. Siyo kweli!

  Mungu kukupaka mafuta ni wajibu wake,lakini matumizi ya hiyo nguvu ni wajibu wako, na utatoa hesabu!

 2. Stephen Ngullo,

  Unaelewa unachokisema, au unaongea tu kutoka kwenye kutokuelewa kwako bila kuwa na rejea yakinifu za ukisemacho?

  Unaposema biblia imesema tutaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya, lakini leo manabii wanapuliza, unaonekana kuwa mipaka yako ya ufahamu wa mambo ni mifupi sana.

  Unasemaje kwa habari ya kivuli cha Petro kuponya wagonjwa, au kivuli kwako ni sawasawa na mikono?

  Unasema kwa habari ya vitambaa kutoka kwenye mahema aliyokuwa anashona Paul kuponya wagonjwa, au kwako hivyo vitambaa ni sawa na mikono?

  Ulichotakiwa kufanya ni kuchambua unachokielewa kwa habari ya manabii wa uongo, maana hao tunajua kuwa wapo.

  Halafu unaposema ‘kutoa misukule’ unamaanisha nini?

  Unajua mtu unaweza ukawa mfinyu kwenye ufahamu wako kiasi cha kuona kila jambo usiloljua kuwa jambo hilo si sahihi!

  Unajua watu wengi mnataka muone tu mambo yaliyowahi kutokea katika maandiko, kama kufufua wafu, kuponya wagonjwa, kutakasa wakoma,viwete kutembea, vipofu kuona, n.k, nje ya hapo mnaona hayo siyo Mungu atendaye!

  Lakini jueni kuwa mambo mapya hayajawahi kuisha katika store ya Mungu. Wewe unaposhangaa suala la kupuliza wagonjwa wakapona, kuna watu ndege( aeroplane) zao zilipokuwa zingali angani tu, wagonjwa chini walianza kupona, kuna wagonjwa waliopita eneo mkutano ulipokuwa unafanyika wakapona japo mkutano ulishaisha!

  Mungu kufanya mambo mapya hajakoma ila biblia ndo imekoma kuandikwa!!

 3. Ameeen, somo zuri sana

  Sent from Yahoo Mail on Android

  From:”Strictly Gospel” Date:Tue, Jul 21, 2015 at 1:19 PM Subject:[New post] Matumizi ya UPAKO

  Strictly Gospel posted: ” UPAKO, kwa tafsiri ya jumla, ni Nguvu ya Mungu inayoingia/inayokaa/inayotenda kazi  ya Mungu ndani ya mtu kutokana na Uwepo wa Roho Mtakatifu ndani ya mtu huyo! Siku hizi kumeibuka MATUMIZI mengi ya Upako kama vile Kuondoa Chunusi Usoni, Kulainisha”

 4. Hapana si kazi maalumu, mi nadhani upako ni kutusaidia kumfuata na kumtumikia Mungu na ufalme zaidi hayo mengine Ni nyongeza tu au promotions zake yaani na hayo yote(mengine) mtazidishiwa!

 5. Leo kuna manabii wengi wa uongo.Biblia imeweka bayana namna ya kuwatambua manabii wa uongo. Tatizo la watu leo ni wavivu wa kutafuta kweli kwa kusoma wao wenyewe Biblia. Leo nitawapatia mifano michache namna ya kutambua manabii wa uongo;

  1.Biblia inasema kama nabii akisema neno kuwa itatokea jambo fulani nalo lisitokee hapo mnapaswa kujua huyo ni nabii wa uongo

  2.Jambo lingine ni kutotumia kwa usahihi neno la Mungu kama mtoa mada alivyo wasilisha. Upako ni nguvu ya Mungu inayokuwa ndani ya mtumishi au mtu na hii nguvu haina mahali pa kushindwa neno lolote kwani ni nguvu ya Mungu sasa leo unaona nabii anafanya mambo fulani fulani tu kama kutoa misukule bila kuwa na utukufu wowote wa kumtukuza Mungu. Miujiza yoyote katika biblia inafanyika kwa kumtukuza mungu soma Yohana 9:1…7/Yohana 11:4 sasa leo msukule alikuwa mchawi anafufuliwa kwa utukufu gani kweli Mungu anafufua wafu lakini kwa utukufu wa MUNGU kama akina Dolikasi nk

  3.Biblia inasema waaminio wataweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya leo tunashudia manabii wa uongo wanageuza neno wanapuliza wanasema upako/wanatumia vitu kama chumvi/maji/vitambaa kama wachawi au waganga wa kienyeji kweli wanaabisha Ukristo sina maana kuwa hivyo haviwezi kutumika vinaweza kutumika katika udhihilisho wa roho mtakatifu kama enzi za akina Paulo na Elisha si kama vinavyo tumika leo manabii wa uongo ni wapenda fedha. Biblia inasema mmepewa bure toeni bure lakini manabii wa uongo wanatumia karama za Mungu kujipatia fedha kwa kuuza vitambaa na chumvi nk

  Mwisho nikomee kwa hapo leo naomba tusome neno la Mungu nalo likae kwa wingi mioyoni mwetu ili tusidanganywe na hawa manabii wapenda fedha kama Gehazi.

  Ni mimi mtumishi wa Mungu katika nyakati za mwisho.
  Barikiwa

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s