UTABIRI kuhusu Viongozi wa Kisiasa

bible-sunset-2

Huku vuguvugu la Uchaguzi mkuu likiwa linaendelea, kuna jambo ambalo linafaa tukalitafakari na Kulijadili:

Wakati wa Utangazaji nia wa Wagombea nafasi ya Urais walisikika baadhi ya viongozi wa kiroho wakitaja majina, ya mtu ambaye kila mmoja aliona anafaa. Wengine walikwenda mbali hata kusema kuwa “Kaonyeshwa na Mungu” kwamba mtu fulani ndiye “Chaguo la Mungu”

Sambamba na viongozi kuyasema hayo, baadhi ya Waimbaji wa nyimbo za Injili nao Walitunga nyimbo za kusifia au Kutangaza kwamba huyo wanayeimba habari zake ” Ni chaguo la Mungu” na ndiye Rais ajaye!

Baada ya Chama Cha Mapinduzi kukamilisha taratibu za kumchagua atakayegombea nafasi hiyo ya Urais, Wote waliokuwa wakitajwa na kusifiwa na ama Viongozi wa Kikristo au Waimbaji wa Injili hawajachaguliwa!

Je, Nini maana ya Utabiri huo kutoka Viongozi na Wanamuziki wa Injili?

Je, Ni kwa kiasi gani NENO likitamkwa na mtu anayesema “Kaonyeshwa na Mungu” litapewa Uzito ikiwa ni kweli itakiwa kaonyeshwa na Mungu?

Je, Nini nafasi ya Mkristo katika kufanikisha upatikanaji wa Vingozi wa nchi wanaofaa?

Advertisements

11 thoughts on “UTABIRI kuhusu Viongozi wa Kisiasa

 1. Oguda, Sungura

  Ndoto inaweza kutafsirika kama ni maono kulingana na ushawishi ulionao juu ya jambo fulani.

  Kauli yako hii ndg Oguda, ndiyo inayouonesha uhalisia wa wazo la moyoni mwako wakati wote; kwamba wewe umekuwa ni mpenzi wa ENL!
  “”Ndg zangu, maono/ndoto hii wakati ninaletewa kuyashuhudia haya, mimi ni mmoja walioaminishwa na kelele za kisiasa za nchi hii ya kuwa, ENL ni fisadi, yaani, mwizi, asiye tuonea huruma kbs, kwa hiyo alistahili yote yaliyomkuta ktk siasa, lkn Mungu ni wa ajabu mno, kupitia ndoto/maono hayo, nilianza kufundishwa na kusadikishwa na R/Mtakatifu taratibu, na muelekeo wangu juu ya huyu mheshimiwa ukabatilishwa hata leo hii.””

  Kwamba “uliaminishwa na kelele za kisiasa za nchi hii ya kuwa, ENL ni fisadi” maana yake ni kwamba hata kujiuzulu kwake pia zilikuwa ni kelele za kisiasa, jambo ambalo haliendani na uhalisia, labda uwe bado uko ndotoni!

  Nachoweza kukuambia ni kwamba ENL is a great manipulator na ana annointing kali sana ambayo imewafanya watu wengi wawe besides themselves, kiasi kwamba wamekuwa kama chatu na mbwa! Kwa kuvutwa kwao na ule upako, hawana tena uwezo wa kufikiri sawa sawa, na badala yake wanaishi huko utopia ambako rais wao ni ENL!!!

  Kwahiyo maelezo ya hizo ndoto mbili uliyoyaleta, naweza kusema kwa uhakika ni ya fungu la pili kutokana na uhalisia wa mvuto alionao ENL ambao hauna rejea yoyote, ndio maana mvuto huo nimeuita ‘UPAKO”; na upako unaojumuisha matayarisho ya muda mrefu kufikia azma fulani, siamini kwamba unatokana na Mungu!!!

 2. Ndg, Oguda!

  Hiyo ndoto yako kama iko kama ulivyosema iko, imebeba uhalisia mkubwa sana wa kinachoendelea kwenye hili taifa!

  Mimi naona inaangukia kwenye namba tatu.

  Tuombe wanaotaka kushinda kwa hila wasifanikiwe kufanya hivyo
  Tuombe watakaoshindwa kihalali wasisababishe vurugu!

  Twendeni tukapige kura

  Mungu bariki taifa letu!

 3. TUOMBEE TANZANIA IWE AMANI,KIONGOZI ALIYETEULIWA NA MUNGU ATAKUWA KAMA DAUDI,GIDION,DEBORA NCHI ILIKUWA AMANI MIAKA 40,TUFUNGE NA KUOMBA KABLA YA UCHANGUZI 24-10-2015

 4. Samahani ndg watumishi, sikukusudia kuzungumzia siasa, ni ktk kuhitaji ufafanuzi au maelezo toka kwa mch Dan Seni, na mtumishi yeyote kanisani humu juu ya yale niliyoyaona.
  Je, nami ninaangukia ktk group lipi kati ya haya?? Sisemi kuwa, mimi ndiyo mimi, na ninadhani pia ya kuwa, na hao wanaosema wameambiwa mim sina kigezo cha kushindana nayo.

  Oguda J.E.

 5. Bwn apewe sifa watumishi wa Mungu!

  Rev. Dan John Seni, umenena mtumishi wa Mungu. Hoja namba Tatu (3) umeiweka vizuri sana ndg yangu.
  Sijui nianzie wapi, lkn ninaka ushuhuda kidogo, alafu nitaomba unisaidie ama wana jopo mnisaidie.

  Mwaka 2011, siukumbuki mwezi na tarehe, niliota, niliona maono ndotoni usiku kunako saa 9 hivi, ya kuwa, Nikamuona Mh.Edward Lowassa akiwa amesimama, hapo aliposimama alikuwa peke yake, anatazama mbele, kichwa akiwa amekiinua anaangalia juu akiwa amevaa suti nyeusi ya za mikono mifupi na miwani myeusi kiasi, akiangalia mbele yake, ambako kulikuwa na ukuta mwembamba mrefu sana wa matofali/blocks, yeye ktk kuuangalia ule ukuta yaani km mtu aliyekuwa anashangaa ya kuwa, atafikaje kule juu, huku akiwa amejishika kiuno chake kwa mikono yote miwili, ghafla nikamuona ameruka pale juu, na umbali wa ule ukuta, ulikuwa mrefu mno kiasi cha hakuna vipimo vya dunia hii, yaani, nikawa ktk ile ndoto/maono ninaona km vile mfano wa ukuta/mnara wa Babeli, kiisha, baada ya kuruka pale kileleni juu, nikaona tena mbele yake kuna ngazi mbili, tatu za ukuta mwengine, nao/napo nilipouangalia, ndg zangu, ni mrefu mno usiosimulika kuliko ule wa awali, na juu kbs kule anapotakiwa afike, kuna kama tower kubwa, na pale juu ya hiyo tower kuna kitu km gunia kubwa hivi, na ndani yake km kuna vitu ambavyo sikuvitambua vimejaa, na juu ya ile tower kuna ndege weengi sana na wakubwa mno, km vile labda kunguru mfano, wanarukaruka juu ya lile gunia.

  Wale ndege walipomuona ENL kwa chini kule, anajiandaa kuruka ili afike pale juu, wakachukua lile gunia, lkn ENL akawawahi akalidaka/kulinyakua miguuni mwao lile gunia, lkn likiwa limetoboka kidogo, na yale yaliyokuwamo ndani yake yakamwagika kidogo mno, wale ndege wakakimbia huku wakipiga kelele na kutawanyika, wakati akiwa ameshika lile gunia pale ktk tower ile nikaona mbele yake kuna njia kuelekea mbele yake, na kule mbele zaidi kuna mlima mkubwa mno, chini ya ule mlima kuna km njia ya pango hivi ndani yake, naam, kuelekea huko, nikaona wazee, yeye akiwa anapita katikati yao, pembezoni, kushotoni na kuumeni akiwa anapita katikati, wale wazee wamemuinamia, mbeleni mwake akatokea mzee mmoja ndani ya pango, ambaye alikuja haraka sana kumpokea ule mzigo,naam, yule aliyekuja kumpokea, alikuwa na ishara km vile, hili ndilo tulilokuwa tukilisubiri litimie, wazee wengine wakiwa ndani ya lile pango, mzee mmoja wapo akiwa amejaa mvi nyeupe sana hadi za nyusoni, pembeni yake nyuma ya wale wazee pangoni nikaona anachinjwa fahari kubwa la dume la ng’ombe ktk mafahari waliokuwamo pale, na wale wazee wakiwa ni wenye furaha sana.

  Ndg zangu, maono/ndoto hii wakati ninaletewa kuyashuhudia haya, mimi ni mmoja walioaminishwa na kelele za kisiasa za nchi hii ya kuwa, ENL ni fisadi, yaani, mwizi, asiye tuonea huruma kbs, kwa hiyo alistahili yote yaliyomkuta ktk siasa, lkn Mungu ni wa ajabu mno, kupitia ndoto/maono hayo, nilianza kufundishwa na kusadikishwa na R/Mtakatifu taratibu, na muelekeo wangu juu ya huyu mheshimiwa ukabatilishwa hata leo hii.

  Ktk hali hiyo hv karibuni nimekutana na mch. mmoja rafiki yangu, kwa miaka mingi, yaani, toka 2011 hv, alikuwa akiniambia siku zote, mwanangu Oguda, unapoteza muda na huyo mamvi wako, na alipokuja kukatwa kule Dom, ndipo akawa na uhakika zaidi, na wa kuniaminisha ya kuwa, huyo mtu wako mamvi amekatwa sasa, hawezi kuwa raisi wa nchi hii. Nikamwambia ya kuwa, mbona bado mapema!! Uchaguzi bado, napo sikujua km mamvi atatoroka aende huko aliko. Huyo mch siku moja akaingia ktk maombi ya kwake kwa ajili ya kanisa lake analoliongoza, lkn baada ya siku Tatu (3) hivi, naye akiwa amelala usiku mmoja, aliona ktk ndoto/maono ya kuwa, mashindano ya mbio ndefu, zile mbio akaonekana ENL/mamvi anakata utepe wa kumaliza zile mbio ndfu, Magufuli akifuatia kwa mbali sana, alipofika kwenye ile kamba/utepe, hakuendelea mbele tena, lkn kule mbele kuna kitu km trophy/kikombe cha mshindi, lkn mtoaji wa kombe lile akaanza kubabahisha kumkabidhi, lkn mwishowe akamkabidhi lile kombe. Hakuelewa vizuri, baada ya siku mbili hivi, wakati bado anajihoji juu ya ahayo aliyoyaona, akarejeshewa tena ileile ndoto/maono, toka hapo akaaanza kusikia moyoni mwake ya kuwa, huyo ndo raisi ajaye. Leo hii hana cha ubishi tena.

  Naam, ktk SG Group e-mail, 2011 niliandika kufahamisha juu ya hili, kwa e-mail adress yangu ya nyakati zile ogudaedmund@hotmail.com, lkn hii adress ilikuja baadaye kuwa corrupt hadi leo hii, na mods naye alinambia kuwa, ile adress yetu ya group ya siku zile pia ilikuja kuwa corrupt pia, hivyo, pakuipakua hakuna, lkn, niliyoyaona yanaishi.

  Rev. Dan John Seni, nimekuelewa, lkn ninahitaji fafanuzi, ninaangukia wapi ktk hili. Lkn pia, sina fahari juu ya hili hata hapo litakapotimia, km ni ndivyo ilivyo, Ni nadra mno hulizungumzia hili.

  Mungu awabariki kwa kuwachosha kwangu.
  Oguda J.E.

 6. Bwana Yesu Asifiwe sana. Nimerudi tena baada ya muda mrefu kutoonekana katika blog hii. Nashukuru kumkuta ndg John Paul akiendelea kufundisha watu katika blog hii. Nimemwona zamani sana. sasa nimerudi kwa namna ya uhakika.
  kwa kweli nimefurahi sana kuhusu mada iliyo mezani lakini pia mada yenyewe ina mkanganyiko kwani watu wanachanganya imani na uhalisia. siku hizi watumishi wengi wanatabiri kwa namna tatu-
  1. Kuna kitu ambacho unaweza kutabiri kwa imani tu lakini siyo kwamba Mungu amekufunulia bali ni kwa sababu una imani jambo hilo linaweza kutokea. sasa anapokuwa na imani hiyo badala ya kuwaambia watu kwamba nahisi kiongozi atakuwa huyu, basi anaamua kusema Mungu amemwambia hivyo.
  2. kuna wengine wanatabiri kwa kuangalia uhalisia wa jambo lenyewe. kwa mfano kuna baadhi ya wagombea ambao wana mvuto wa hali ya juu sana. yaani unamkuta mtu ameamua kumpenda mgombea fulani si kwa sababu amepewa fedha bali kwa sababu ndani ya huyo mgombea kuna ‘kinara’ ambacho kinang’arisha nyota yake.
  3. kuna wale ambao Mungu anaongea nao moja kwa moja juu ya kiongozi ambaye anaenda kuchaguliwa na watu wa Mungu. Huyu hatumii akili yake na wala hajaomba jambo hili aambiwe bali ni sauti ya Mungu inamwambia kwa ajili ya kuwaweka watu tayari kisaikolojia.
  Sasa tunapoangalia hapa nchini watumishi wengi wanatabiri kwa kutumia 1 & 2 badala ya 3. hili ndilo ambalo mimi naliona linaleta matatizo makubwa sana kwa ajili ya watumishi wengi na pengine kuleta migogoro kati yao na serikali.
  Kwa hiyo basi kama wewe ni mtumishi wa Mungu jaribu kuangalia unabii wako unatokana na chanzo kipi? imani? uhalisia au Mungu mwenyewe?
  Kuna mtu mmoja aliniuliza kwamba mimi ni team gani? nikamwambia kwamba mimi sina team. mtu hyu alikasirika sana kwa sababu alitarajia mimi nitakuwa team fulani.
  Natoa wito kwa wachungaji, mitume na manabiii! Ni wakati wa kunyamaza kimya ili kuacha Mungu afanye.
  Ahsante
  Pastor
  Daniel John Seni
  Shekinah Presbyterian Church
  Madale-Dar es salaam

 7. Kwani Raisi ameshapatikana jamani, si bado!

  Kama kuna watu wawili wamesemwa kuwa watakuwa wao, basi au wote hawatakuwa au mmoja tu ndiye atakayekuwa. Maana Raisi atakuwa mmoja tu! Kwa hiyo kati ya hao watoa unabii wawili mmoja lazima ni muongo au wote ni waongo.

  Lakini tusiseme kuwa ni waongo sasa hivi wakati Raisi hata bado hajapatikana.

  Kutoteuliwa na ccm siyo mwisho wa uhunzi, mtu anaweza akahamia chama kingine na akagombea akashinda. Lakini pia mgombea anaweza fariki wakati wa kampeni na uteuzi ukafanyika tena.

  Tujiandikishe kwenye daftari la mpiga kura ili siku ya kura tuweze kuchagua kiongozi wa taifa.
  Lakini pia tukumbuke kwa wanaofanya ushirika siku ya Jpili, tarehe ya kupiga kura ktk hili taifa ilipangwa hivyo( Jpili) kwa hila ili wakristo wengi wasipige kura.

  Naomba hiyo hila tuishinde, haya kama siku hiyo hatutakusanyika kufanya usharika tukakomea tu kupiga kura, tutakuwa tumemtumikia Mungu.

  Mwisho, kama watu wa Mungu, tuangalieni hali ya taifa letu, tutafakari kuhusu mstakabali wa watoto wetu, kisha tujiulize tumefikaje kwenye hii hali, baada ya hapo tufanye maamuzi yasiyo ya kiitikadi ya vyama vya siasa kuuondoa mfumo uliotufikisha hapa!

  Hali ya taifa ni tete kuliko itikadi zetu na njaa zetu!

  Bless us!

 8. Ndg Ngulo,
  Naona unajichanganya ktk mambo yaliyo rahisi! Mifano ya Maandiko uliyoileta haina uhusiano na mada kabisa; mtumishi anaposema Mungu kamwambia jambo fulani litakuwa hivi, lisipokuwa huyo anakuwa ni muongo, yaani roho aliye juu yake au anayemuongoza si Roho Mtakatifu; hakuna maelezo mengine yanayoweza kulibadili hilo, labda aseme kwamba “anatabiri” hilo linaeleweka.

  Soma vizuri mchango wa ndg John Paul utakusaidia sana ktk kulitafakari jambo hili, litakupa mwanga zaidi ili unapowafundisha watu Neno la Mungu iwasaidie kuzipambanua roho, kuliko hayo maelezo yako yanayoweza kuwafanya wameze kila uongo unaotoka madhabahuni!

 9. Ndg Stephen Ngullo,

  Mimi nadhani kumekuwa na matumizi yasiyo sahihi ya neno KUHUKUMU. Maana inapotokea kiongozi ametoa neno linaloleta mkanganyiko, kulijadili kwa ajili ya kujifunza ili kupata chenye kusaidia sidhani kama ni vibaya, na wala siyo kuhukumu huko.

  Kama inavyosema hapo juu mimi binafsi naona hapo kuna mambo ya kujifunza kama wakristo ili itusaidie kuenenda katika njia sahihi.

  Pia yale maandiko uliyonukuu mi naona hayo yako wazi kwa maana hii: Hezekia alipolia na kumuomba Mungu, Mungu ALIMTUMA TENA nabii ili akatangue yale maneno. Hakufanya kimya kimya. Yaani alitoa unabii wa kutekeleza jambo kisha akatoa na unabii wa kubatilisha.

  Kwa habari ya Ninawi, watu WALITUBU DHAMBI, haikuwa na namna Mungu ahukumu watu waliotubu.

  Kwa hiyo haya mawili yanaelezeka!

  Lakini haya ya kwetu, unakuta mwinjilist fulani anamtolea neno mgombea kisha mtumishi mwingine anamtolea neno mgombea mwingine, kisha wote wanakwama, natumaini hapo kuna mambo ya kujifunza!

 10. Bwana asifiwe wapendwa nami naomba kuchangia kama ifuatavvyo:-
  1.Biblia inasema kuwa Nabii akisema Neno nalo lisitokee atakuwa Nabii wa uongo
  2.pia Nabii anaweza kusema Neno nalo linaweza kutokea hayo yote yanatendeka kwa huruma za Mungu hapa naona nimewachanganya hasa kwa wale wasio soma biblia mimi kama mwalimu wa neno la Mungu ebu nikupe ushahidi kidogo juu ya neno la Mungu ili usiwanenee vibaya watumishi wa Mungu hata ukajipatia hatia
  1.Nabii Isaya wa kwenye Biblia alishawahi kusema Mfalme atengeneze mambo yake kwani ugonjwa ulio mpata atakufa(lakini baada ya maombi ya kumkumbusha Mungu Mungu hakutimiza ule unabii wa Nabii Isaya soma Isaya 38:1 /2wafalume 20:1..6)
  2Nabii Yona alisema kuwa mji wa Ninawi utaangamizwa baada ya siku arobaini. watu walimwamini Nabii Yona wakaamua kujinyekeza wakafunga kwa maombi ya kujinyekeza Mungu akaamua kutotimiza ule unabii wa Nabii Yona soma Yona 3:1..10)
  Baada ya kusema hivyo naomba tusiwahukumu watumishi walio kuwa wametamka tumwachie Mungu yeye ndiye anaye jua (soma kumbu kumbu la tolati 29:29)
  Mungu awabariki

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s