Kipimo Cha Wema wa Mungu Ni nini?

Good-Morning-Photos

1Nyakati 16:34 – Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

“Bwana Ni Mwema/God is good” ni maneno ambayo ni maarufu kati ya wakristo. Lakini, pengine, siyo kila mtu akiulizwa Ni kwa nini anasema Bwana ni mwema anaweza kuwa na jibu lililonyooka.

Je, ni nini KIPIMO cha Wema wa Mungu katika maisha yetu?

Ni kwa sababu ya afya njema? Au kwa sababu ya Mali na Elimu?

Yule mlemavu wa viungo vya mwilini au Masikini apataye mlo wake kwa shida, Naye Je, anayo sababu ya kuimba kwamba Bwana yu Mwema?

Wale watoto wa mitaani au Wahanga wa vita ambao viungo vya mwili vilipunguzwa kwa kulipukiwa na bomu, Je, wana sababu ya kusema Bwana ni Mwema?

Ni nini kipimo cha wema wa Mungu?

Advertisements

4 thoughts on “Kipimo Cha Wema wa Mungu Ni nini?

 1. nimependa logic ya swali hili, linatupa kufikiri vizuri.
  ukweli ni kuwa wema wa mungu ni dhahiri maishani mwetu hata kama hatna mahtaji yaliyo haja ya amioyo yetu.
  uwe tajiri au maskini
  mrefu au mfupi
  mweusi au mweupe
  mama wa watoto wengi au mgumba
  yatima au asiye yatima
  WEMA WA MUNGU ni pale wote tuna nafasi sawa ya kukubaliwa na yeye tunaporudi kwake kwa toba na kumaanisha.
  hii inamaanisha haki ya mungu juu ya maisha ya mwanadamu haitokani na sifa fulani fulani maishani mwetu, ispokuwa ni moyo wa uchaji.
  kutumia vigezo vya kuwa na! na kutokuwa na! ni confusion ambayo shetani huutumia kuondoa uhakika kwa wana wa Mungu kuwa Mungu ni mwema kwao.
  uthamani mkubwa ktk mambo ya mwanadamu ni yeye kumjua , na kujulikana na Mungu.(KUKUBALIWA NA MUNGU)

 2. Ni kweli wakati mwingine ugumu wa maisha unafanya tuone kama Mungu si mwema, lakini kiukweli hakuna mwema kama yeye maana hata katika dhĂ mbi na mabaya ambayo tumemtendea bado anatusamehe bure na anaendelea kutupa pumzi bure. Kwangu Mimi naona Wema wa Mungu bado ni mkuu sana nisiyestahili. Barikiwa kwa Mada nzuri sana.

 3. Mtumishi wa Mungu. Asante kwa majadiliano kama haya, unatufanya tukumbuke kushukuru kwa kila jambo. Rafiki yangu aliniletea kadi ya birthday inayonipa ushauri usemao.” Usisahau kupumua”. Kwangu mimi wema wa Mungu kwangu na kwa familia yangu ni uwezo wa kupumua. Unaonipa matumaini kuwa, as long as I still breathing, there is hope for future. naweza kuwa au kutokuwa na mahitaji leo Lakini isiwe Hivyo Kesho. Hivvyo vile ninaishi, namshukuru Mungu kwa hilo. Solomon anasena ni ubatili na kuna faida gani mtu kuhangaika kutafuta mali, na anapokufa wanawe wanayatawanya hovyo.
  ni siku mpya, tumshukuru Mungu kwa hilo.
  stay blessed

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s