Kwenye andiko hili WANA WA MUNGU ni watu gani??

 confronting_ev_ideas_wide1-300x248

“Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua” (Mwanzo 6:1-2)

Katika maandiko haya hapa juu, WANA WA MUNGU ambao waliwaona binti za wanadamu kuwa ni wazuri, wakawaoa na kisha kuzaa MAJITU, ni akina nani?

Je, walikuwa ni MALAIKA au walikuwa ni WANAADAMU tuu?

Advertisements

14 thoughts on “Kwenye andiko hili WANA WA MUNGU ni watu gani??

 1. Praise God, Bwana CK lwembe na Ndungu za In Jesus? Okay kama ni watoto wa Mungu according in Genesis 6:1-2 Ni wa sethi,sasa na hawa “ilikuwa siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA,shetani naye akaenda kati yao.” Ayubu 1:6

  Kama ni watoto wa Mungu ni uzao wa sethi Mpaka hapa after Noah ark uzao wa Kaini bado ilikuwa??? Please I need answer..thank you

 2. Praise God, Bwana CK lwembe na Ndungu za In Jesus? Okay kama ni watoto wa Mungu according in Genesis 6:1-2 Ni wa Sethi, sasa na hawa kwenye Ayubu 1:6 “Ilikuwa siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA,shetani naye akaenda kati yao”
  Kama ni watoto wa Mungu ni uzao wa sethi Mpaka hapa after Noah ark uzao wa Kaini bado ilikuwa??? Please I need an answer..thank you!

 3. Mengi Togwa,
  Mtoa mada anaandika ““Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua” (Mwanzo 6:1-2)
  Katika maandiko haya hapa juu, WANA WA MUNGU ambao waliwaona binti za wanadamu kuwa ni wazuri, wakawaoa na kisha kuzaa MAJITU, ni akina nani?
  Je, walikuwa ni MALAIKA au walikuwa ni WANAADAMU tuu?”

  SWALI ni ” Katika maandiko haya hapa juu (Mwanzo 6:1-2), WANA WA MUNGU ambao waliwaona binti za wanadamu kuwa ni wazuri, wakawaoa na kisha kuzaa MAJITU, ni akina nani?
  Je, walikuwa ni MALAIKA au walikuwa ni WANAADAMU tuu?”

  Hebu mjibu mtoa mada kuliko kuendelea na sentensi zenye utata.
  Katika maelezo yako ya 09/08/2015 at 7:44 PM, umesema katika Agano la Kale neno “wana wa Mungu” limetumiwa kama Malaika, na katika Agano Jipya neno “wana wa Mungu” lilimaanisha wale waliompokea Yesu.

  Je, kwa maelezo yako, umejibu swali lililoulizwa?
  Pia unapoulizwa swali, zingatia yale uliyoulizwa.

 4. Ck Lwembe,unapaswa kufahamu kuwa biblia iliandikwa kwa lugha ya kiebrania na baadae ikatafsiriwa kwa lugha ya kiyunani.Hivyo kunapotokea utata wowote ni lazima turejee ktk lugha ya asili ya biblia ili kupata tafsiri iliyo sahihi vinginevyo na wewe utakuwa mmojawapo wa wale wanaotafsiri masinagogi eti ni misikiti ya wayahudi.Anyway Yesu alisema hakuna anayekunywa divai ya kale akatamani mpya kwa kuwa asema ile ya kale ni njema hivyo na wewe tosheka tu na yale ambayo dini yako imekufundisha!

 5. Ck Lwembe,unapaswa kufahamu kuwa biblia iliandikwa kwa lugha ya kiebrania na baadae ikatafsiriwa kwa lugha ya kiyunani.Hivyo kunapotokea utata wowote ni lazima turejee ktk lugha ya asili ya biblia ili kupata tafsiri iliyo sahihi vinginevyo na wewe utakuwa mmojawapo wa wale wanaotafsiri masinagogi eti ni misikiti ya watahudi.Anyway Yesu alisema hakuna anayekunywa divai ya kale akatamani mpya kwa kuwa asema ile ya kale ni njema hivyo na wewe tosheka tu na yale ambayo dini yako imekufundisha!

 6. Ningependa kujifunza zaidi,kwa kweli ninashangazwa sana na vile wengi hujichanganya na kuchanganya maandiko

 7. Togwa,
  Ukianzisha mambo ya Kiebrania na Kiyunani ktk mambo rahisi yanayoeleweka, utaishia kujichanganya!

  Hakuna malaika aliye mwana wa Mungu. Malaika akikosea anatupwa jehanamu moja kwa moja, hakuna Injili ya kumuokoa! Adamu ndiye mwana wa Mungu wa kwanza, ndio maana Kristo anaitwa Adamu wa Pili.

  Tazama hapa Uzao wa wana wa Mungu, Lk 3:23-38:
  “Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli, wa Mathati, … 38wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.”
  Halafu tazama hapa tena, Mw 5:1-3:
  “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 2mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
  3Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.” Sethi ni wa sura na mfano wa Adamu ambaye naye ni wa sura na mfano wa Mungu!!!

  Wana wa wanadamu ndio hao waliozaliwa kwa Kaini, ambaye si wa Adamu; huyu ni mtoto wa yule mwovu, 1Yn 3:12 “… si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu,” ndio maana HAYUMO ktk ukoo wa Adamu!!!

  Kuhusu Ayu 1:6 hao wana wa Mungu ambao Shetani alijiwakilisha nao, hebu tazama hapa linavyojirudia jambo hilo hapo ambapo Mungu ktk Ukamilifu wake akiwa ndani ya Kristo, Yn 6:70
  “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara, na mmoja wenu ni shetani?”

  Amini unachokisoma ktk Biblia yako, Mungu atakupatia ufahamu kulingana na uaminifu wako unapoyasoma Maandiko yake!

  Gbu my brother in Christ!

 8. Wapendwa popote unapoona neno “wana wa Mungu”kwenye agano la kale tafsiri yake ni malaika au eloheem kwa lugha ya kiebrania,neno wana wa Mungu limetumika kumaanisha watoto wa Mungu ktk agano jipya tu likimaanisha wale waliompokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao.Linganisha AYUBU 1:6 na YOHANA 1:12

 9. WAPENDWA,
  Shalom.
  MARKO 12:25 ” 25 Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.”
  Ieleweke kuwa, MALAIKA HAWAOI kama Maandiko yasemavyo.Hakuna mahali popote kwenye BIBLIA inayosema Malaika wanaoa bali mitizamo na mafundisho ya wanadamu husema malaika wanaoa.
  MWANZO 6:1-2 ” Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.”
  WANA WA MUNGU.
  WANA WA MUNGU hapa,ni WANADAMU watoto wa SETHI. Soma maandiko;
  MWANZO 4:26 “Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Sethi naye akazaa mwana; akamwita jina lake Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana. .”
  TAFAKARI maneno haya;”….Hapo ndipo watu walipoanza kuliitia Jina la Bwana.”
  WARUMI 8:14 ” Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.”
  Mtu anapompokea au kumkubali Kristo anaitwa MWANA WA MUNGU, Soma
  YOHANA MTAKATIFU 1:12-13 ” Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. ”
  WANADAMU.
  WANADAMU ni wale ambao hawapo tayari kumpokea au kumkubali Kristo, hawa wamezaliwa kwa mapenzi ya mwili, damu na mapenzi.
  YOHANA MTAKATIFU 3:4-7 “Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.”
  ZINGATIA;
  Kilichozaliwa kwa MWILI ni MWILI na kilichozaliwa kwa ROHO ni roho.
  Amina.

 10. Magreth, ikiwa wale wana wa mungu wanotajwa kwenye mwanzo 6:1-2 ni ukoo wa Sethi na binti za wanadamu ni ukoo wa kaini kwa nini matokeo ya ndoa hiyo iwe ni kuzaliwa kwa majitu makubwa yaliyokuwa bora wakati huo?

 11. INTERPRETATION OF GENESIS 6:1-3
  Verses 1-2 For the glory of God’s justice, and for warning to a wicked world, before the history of the ruin of the old world, we have a full account of its degeneracy, its apostasy from God and rebellion against him. The destroying of it was an act, not of an absolute sovereignty, but of necessary justice, for the maintaining of the honour of God’s government. Now here we have an account of two things which occasioned the wickedness of the old world:-1. The increase of mankind: Men began to multiply upon the face of the earth. This was the effect of the blessing ch. 1:28 ), and yet man’s corruption so abused and perverted this blessing that it was turned into a curse. Thus sin takes occasion by the mercies of God to be the more exceedingly sinful. Prov. 29:16 , When the wicked are multiplied, transgression increaseth. The more sinners the more sin; and the multitude of offenders emboldens men. Infectious diseases are most destructive in populous cities; and sin is a spreading leprosy. Thus in the New-Testament church, when the number of the disciples was multiplied, there arose a murmuring (Acts. 6:1 ), and we read of a nation that was multiplied, not to the increase of their joy, Isa. 9:3 . Numerous families need to be well-governed, lest they become wicked families. Mixed marriages (v. 2): The sons of God (that is, the professors of religion, who were called by the name of the Lord, and called upon that name), married the daughters of men, that is, those that were profane, and strangers to God and godliness. The posterity of Seth did not keep by themselves, as they ought to have done, both for the preservation of their own purity and in detestation of the apostasy. They intermingled themselves with the excommunicated race of Cain: They took them wives of all that they chose. But what was amiss in these marriages? (1.) They chose only by the eye: They saw that they were fair, which was all they looked at. (2.) They followed the choice which their own corrupt affections made: they took all that they chose, without advice and consideration. But, (3.) That which proved of such bad consequence to them was that they married strange wives, were unequally yoked with unbelievers, 2 Co. 6:14 . This was forbidden to Israel, Deu. 7:3, Deu. 7:4 . It was the unhappy occasion of Solomon’s apostasy (1 Ki. 11:1-4 ), and was of bad consequence to the Jews after their return out of Babylon, Ezra. 9:1, Ezra. 9:2 . Note, Professors of religion, in marrying both themselves and their children, should make conscience of keeping within the bounds of profession. The bad will sooner debauch the good than the good reform the bad. Those that profess themselves the children of God must not marry without his consent, which they have not if they join in affinity with his enemies.

 12. Nalinganisha maandiko hayo na Ayubu 1:6 hivyo nami naona kuwa hao wana wa Mungu wanaotajwa hapo ni malaika. Pia huwa nahusianisha na Yuda 1:6

 13. Hapo nami nangonjea kujua but kwangu mi naweza sema ni Malaika..kwa sababu Mungu Alisema Roho yake haiwezi kuchanganyana na ya Wanadamu…

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s