Kuyahoji Majini wakati wa Maombezi.

 

 

The_Demons

Baadhi ya Watumishi wa Mungu wakati wa kufukuza Mapepo/Majini huwa wanahojiana nayo kwa muda mrefu. Anauliza; Anajibiwa na hata wengine huwaambia kusanyiko kuzingatia yanayozungumzwa na majini/mapepo hayo ili kama kuna la muhimu walichukue!!

– Je, ni sahihi kuhojiana na majini wakati wa kuyafukuza?

– Je, ni muhimu kuzingatia yale ambayo husemwa na majini/mapepo wakati huo?

Advertisements

22 thoughts on “Kuyahoji Majini wakati wa Maombezi.

 1. Mnaodhani kuwa kanisa siku hizi halina nguvu mnajidanganya sana, na sijui kwa nini mnasema hivyo.

  Je, chanzo cha nguvu ya kanisa kimeondoka mpaka mseme kanisa halina nguvu?

  Alisema mtapokea nguvu akisha kuwajilia juu yenu Roho mtakatifu.
  Ukisema kuwa kanisa halina nguvu unajaribu kusema kuwa Roho mtakatifu hayupo au hafanyi kazi ndani ya kanisa, kitu ambacho siyo kweli.

  Unayedhani kuwa kanisa halina nguvu, unatakiwa tu ujue kwamba wewe ndo hauna nguvu, maana aonavyo nafsini mwake mtu mdivyo alivyo.

  Wewe ukiona tu kanisa la nyumbani/kijijini kwenu limepoapoa unaanza kudhani kuwa kanisa halina nguvu. Provided Roho mt. yupo ndani ya kanisa, kanisa haliwezi kukosa nguvu.

  Tuacheni kuwa watu wa kulalamikalalamika, wewe kama unajua ni sehemu ya kanisa na unaona kuna kitu kimepungua ktk kanisa, chukua hatua ya kufanya lipasala ili kuondoa huo upungufu. Mungu hahitaji watu wengi ili kuleta uamsho, anahitaji mtu mmoja tu – wewe!

  Sasa unapokuwa mtu wa kulalamika unataka nani ajaze hilo pengo?

  Mnaokomaa kusema kuwa haitakiwi kuhoji mapepo hamna andiko la kusimamia, ni hisia zenu tu za uoga, mnaogopa kudanganywa na shetani. Lakini ukiona unadanganywa na shetani lazima ujue kuna upungufu ndani yako. Maana akiwa Roho mtakatifu amekaa ndani yako hawezi shetani/pepo kudanganya.

  Mungu mwenyewe alihojiana na shetani, Yesu aliyahoji mapepo, sasa ninyi hilo katazo mnalitoa wapi kwenye maandiko, au ni hisia zenu tu za uoga?

  Acheni uoga!

 2. Ndani ya kanisa kuna vipawa tofauti,ya kwanza ni mtume ya pili nabii ya tatu ni mwalimu,kufanya miujiza aina mbalimbali kama kuponya na ata kutoa mapepo,alafu kuna viongozi{wachungaji} na wenye kunena kwa lugha-1wakorintho 12:28.

  ninachotaka kusema ni hili,siku hizi kanisa halina nguvu. na kiu ya kufahamu neno la Mungu imepotea kwa sababu watu wamejiwekelea vipawa au karama ambao hawana. mtu ni mwalimu lakini hafundishi kweli kwa sababu hajapewa na Mungu,mwengine ana kipawa ya kutoa mapepo lakini kwa sababu hataki mafundisho ya kweli ili afanye kazi kulingana na mapenzi ya Mungu. hii ndo sababu kanisa halijui kama kuhoji mapepo ni sawa au si sawa. ushauri wangu ni kuwa kila mtu afanye kazi ya Mungu kulingani na kipawa alichopewa. ikiwa kuhoji pepo ni sawa au si sawa basi kuna mmoja tu wa kuhukumu naye ni MUNGU MWENYE ENZI YOTE NA MAMLAKA. dhamiri ndo inafanya kuhoji pepo iwe sawa au mbaya. ukihoji kwa nia mbaya atakudanganya na utadanganya wengi,jihadharini na wenye kufanya kazi ya Mungu kuwa biashara.

 3. Ipo hatari katika kuhojiana nayo hasa inapovuka hatua na kusema kuwa watu wavichkue vitu vzr visemwavyo na majini,maana shetan kwa uwakrishi wake ana uzoevu mkubwa katka kupotoa na kuondoa ukwel so kwa 7bu Yesu mwenyewe aliwashuhudia wanadam kua shetan ni mwongo na baba wa uongo sizan kama anaweza akaongea jambo jema ambalo laweza kua na faida kwa watu tena wa Mungu, yohana 8:44
  Afu tnapoutmia mfano wa Yesu kuhojiana na mapepo lazma tuwe makini sana maana yesu alikuwa na uwezo wa uungu ndani yake hvyo alifahamu fundsho la makusudi kwa watamaji kabla ya kutoa ruhusa a kuhojiana nayo na ndyo maana kwa kila hojiano kuna fndsho kwetu kuhusu ukuu wa Mungu na sehem zngne aliyambia yasimzihishe yalipo muita kua mwana wa Mungu, ingawaje ni kwel yesu alikuwa mwana wa Mungu lakn alikataa kwa sababu mapepo hayana ruhusa ya kuwadhihlsha watu wa Mungu lakn watu wa Mungu siku hzi wamekuwa wakipendzwa na mapepo kuwataja kuwa ni watmshi wa Mungu ila me binafsi hapa hua nakua na mashaka nao, maana shetan n mjanja sna.. Asanteni

 4. Samahani watumishi wa Mungu kwani nimechangia coments mbili ambazo zina wazo moja ila ni kwajinsi kila ninapo soma Hii mada napata msukumo kusema neno kwani ni mambo yanayo endalea katika jamii zinazotuzunguka na mbarikiwe Bwana wetu YESU KRISTO wote walio toa coments na pia wanao pata msukumo waendelee kuchangia kwani tunajifuzaj mengi ndani ya blog Hii pia abarikiwe aliyeweka maada Hii mbele yetu

 5. Bwana YESU asifiwe mtumishi Sio sahihi kuuliza majina au kufanya majadiliano na mapepo/majini na wachungaji wengine ni moja ya advatersement za huduma zao wakati wa kutafuta waumini ambao wa nahitaji kutafuta huduma za kutatua matatizo Yao binafsi Sio kujua neno la Mungu ndio maana ktk mikutano/semina mbali mbali hasa hapa kwetu Tanzania maada zina kosa muda na kufukuza mapepo,kuponya mara kufunguliwa ndio zina tawala mikutano/semina nyingi ambapo kuna ukweli kwamba yote hayo na mengine Kama hayo huondolewa au watu wengi hufunguliwa Kwa kulijua neno likifatana na kuliishi.

 6. Nafurahi kuona jinsi mafundisho na tafsiri potofu zinavyovuliwa nguo na kuachwa uchi na comments za watu waliobeba KWELI.

  kuna namna mbalimbali zinazotumiwa
  na wajumbe wa shetani ili kuwafanya watu WASIKILIZE ROHO ZIDANGANYAZO na mojawapo ni KUYAHOJI na KUHOJIANA na mapepo.Ufunuo tunaoupata katika 1 Timotheo 4:1-2, ni mzito , mpana na muhimu mno hasa katika nyakati hizi za mwisho ambazo zaidi ya asilimia 70 ya wateule wanatumikishwa kwenye MADHABAHU ZA WAJUMBE wa shetani.Unabii wa mtume Paulo unaendelea kututafuna.Tafakari Matendo 20:28-31.

  Mwenye masikio na asikie na mwenye macho atazame.

 7. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu Frank2jo,mchango wako umeniweka mahali pa zuri.
  Lazima watu waishi neno na si kulijua neno.

 8. Bwana YESU asifiwe watumishi ni mesoma coments tofautitofauti kulingana na uelewa wa kila mtu na kulingana neno bibilia ni kweli Kwa mtazamo wangu kuhoji mapepo/majini Sio lengo kamili na Kwa watumishi wengi wanatumia furusa hiyo Kwa ku advertise huduma zao Kwa mfano huuliza ninani aliye kutuma, kwanini unamtesa mtu huyu then unaendelea kuuliza maswali mengi mengi ukiwa unajua ni mapepo huku camera inaendelea kuchukua kila points baadaye inakuwa nimoja ya advertisement Kwa ajili ya huduma hiyo na mtumishi huyu anapata watu wengi kwajili ya matangazo hayo.

  Hiyo inawapelekea watumishi wengi kuhangaika kutafuta nguvu za kudili na mapepo na kweli hasa Tanzania watu wengi wana mapepo unaweza kwenda kwenye mkutano/semina kutoa mapepo ikawa imechukua robo tatu ya mda wamkutano/semina na dhumuni likawa halipo tena.

  Ndio mambo yanayo endelea kwenye makanisa ya kilokole baadaye watu wanabakia kulijua neno Sio kuliishi neno na lile fudisho la kujitenga na ambao hawaja sema nimeokoka ndio hapo linapofanya kazi kuna haja ya kumpokea YESU na hasa kuishi na jamii inayo kuzunguka hivyo Sio haja ya kujadiliana na mapepo Kwa sababu mapepo ndio yana fukuzwa Sio mtu aliingiwa na mapepo na uponyaji ni Kwa mtu Sio mapepo na kupitia mapepo au huduma inayo husu kuponya na kutoa mapepo ndio unasababisha watumishi wengi kupoteza imani yako Kwa waamini wao Kwa sababu kunapo Kua kuna waamini wengi wasomi au waliojitosheleza na mahitaji ya kimwili/kikawaida huwa hawawezi kuamini mambo hayo kwasababu mchungaji atatumia mda mwingi kutafuta wenye mapepo na kuhojiana nayo then anasau kuwa watu wengine wana Hitaji neno la Mungu.

  Ndio maana wachungaji wengi wanao fundisha neno huwa niwazuri sana Kwa jamii kwani ndio njia halisi ya kuponya roho za watu Kwa kulijua neno la Mungu na ndio uponyaji na unapo ruhusu majadiliano na mapepo ujue hitimisho ni lakutoka na kesho kurudi Kwa mtu huyo huyo unakua una mtoa mapepo mara Kwa mara,pia elimu ya mapepo Sio muhimu sana kwani ni elimu ya shetani na tunapo jua elimu sana kulingana na imani YESU hawezi ruhusu mda mwingi upate watumishi wake kujadiliana na mapepo kwasababu mchungaji ametumika tu ila anaye toa mapepo ni YESU mwenyewe na Hii nikarama ya roho Mtakatifu nasio jitihada za mtu mwenyewe. Kama kufoji vyeti ili upate kazi hapa kwahiyo hamna haja ya kuhoji ana na mapepo/majini na Sio swala la kusema imeandikwa wapi kwenye Bibilia.

  Jambo Kama hili nila kutafakari kulingana na mafundisho au uelewa wa neno la Mungu na mtu anapata jibu sahihi kwasababu shetani Yuko makini kutoa mafundisho mengi ili apoteze ukweli ndio maana hata mapepo yana tafuta majadiliano.
  Thanks

 9. Ni vema tukasema ukweli wa maandiko juu ya jambo kuliko kusema matokeo ya jambo, bila kuonyesha kama aliyepata hayo matokeo alilifanya jambo hilo kwa usshihi wake.

  Kuna tofauti kati ya kuhoji na kuhojiana. Hapa tunaongelea suala la kuyahoji majini, siyo kuhojiana na msjini.

  Yesu aliyahoji, wala hakuhojiana nayo( aliliuliza jina lake). Angalao tuna andiko linaloonesha mtu kuyahoji mspepo, lakini anfiko linalotukataza kuyahoji mimi sijalipata.

  Anfiko la 1Tim 4:1 wala haliongelei habari za kuhojiana na mashetani, linaongelea kujiingiza kwenye mafundisho ya kishetani. Kufuata mafundisho ya kishetani siyo kuhojiana na mashetani wakati unayakemea yamtoke mtu.

  Tujiulize, kwa nini Yesu alipoliuliza jina halikumdanganya lilisema ukweli pamoja na huo ukweli kwamba shetani ni muongo?

  Sasa kwa nini wewe unaogopa ukilihoji litakudanganya? Lazima kuna kitu hakiko sawa.

  Si lazima kuyahoji mapepo, lakini pia haukatazei kuyahoji unapotakiwa kufanya hivyo!

  Ukimhoji akakudanganya unatakiwa kujua kuwa amesema uongo, ukidanganyika basi wewe mwenyewe una tatizo.

 10. Mapepo ni maongo saaana!
  Watumishi wengi wanaofanya maombezi huutumia uongo wa mapepo hayo ktk kukuza umaarufu wao kwa jamii iliyojaa uoga na yenye uzoefu wa waganga wa kienyeji na sasa imehamia ktk wokovu kwa mintarafu ya kupambana na nguvu za giza!!!!

  Nazo sinema za kinijeria ndio zinapambisha moto kwa kuiharibu jamii kisaikolojia, pamoja na watumishi!!!

  Ondokeni ktk dini za wokovu muingie ktk wokovu wa kweli ambavyo mtajazwa Roho Mtakatifu wa kweli, ambavyo imeandikwa kwamba ikiwa hivyo hata yule mwovu hakugusi!!!

  Mbarikiwe!

 11. pole na maandalizi ya safari mtu wa Mungu! unyakuo na wengine ujio wa yesu mara ya pili! nimesoma maelezo yako,lakini niwe na neno kidogo! roho mt ndiye atiaye hekima namna ya kufanya isiwe sheria! rejea marko mt 4: 9.nikutakie safari njema!

 12. suala la kuhojiana na mapepo ni mbinu inayotumiwa sana na wajumbe wa shetani ili wateule wasikilize na kufuata maagizo ya roho zidanganyazo.

  Mchezo huu mchafu umewatenga wengi na imani ya Yesu Kristo.Mchezo huu ni muhimu mno ktk mafundisho ya mashetani.Tunahitaji roho saba za Yesu ili kupambanua na kuyaeleza mambo haya kwa usahihi.

  Werevu wa shetani umetumika sana kulieleza jambo hili tena kwa kutumia
  maandiko!Wasio na maarifa wanaendelea kuangamizwa.1 Timotheo 4:1 inaeleza jambo hili kwa undani mno.

  Mungu atuponye ufahamu.Atupe roho ya hekima na ufunuo ktk nyakati hizi za hatari.

 13. Hello,

  Naona kila mtu anasema haitakiwi kuyagoji mashetani.
  Lakini mimi nafikiri inategemea ni kuyahoji nini. Biblia haijasema kuwa tusiyahoji, wala kutuambia kuwa tuyahoji.

  Yesu alikuwa anayafumba kinywa si kwa sababu aliogopa yangemdanganya, bali kwa sababu yalitaka kumsema yeye ni nani, naye alikuwa hataki kudhihirishwa.

  Mbona aliyauliza jina yakamuomba jambo naye akayaruhusu!

  Ukiwa vizuri katika Roho mtakatifu pepo hawezi kukudanganya. Mbele ya Yesu lazima waseme ukweli kama wametakiwa kusema jambo.

 14. Si sahihi kuyahoji majini wakati wa maombezi, kutokana na sababu zifuatazo
  1. Si maagizo ya kibiblia kusikiliza mapepo. Kanisa limejengwa katika misingi ya mitume na manabii (Efe 2:20). Maana yake tuna haki ya kuiuliza Biblia, Mitume walifanyaje? Na Je! Yesu aliagizaje? Yesu alihojiana na mapepo au majini? Wakati fulani pepo lilitaka kuanza mahojiano na Yesu, akasema fumba kinywa mtoke.
  2. Shetani ndiye baba wa uongo. Pepo hawezi kuongea jambo kwa lengo la kuwanufaisha wana wa Mungu, anaweza kuwadanganya ili kuwafarakanisha. Taarifa ya shetani haiwezi kuaminiwa. Kama kuna kitu tunhitaji kujua Yesu anaweza kutufunulia

 15. hakuna haja ya kuhojiana na mapepo yalishindwa mbinguni yakatupwa ili ya udanganye ulimwengu soma ufunuo 12:7..9 mapepo ni maongo ukihojiana nayo yatakudanganya kwani biblia inasema shetani ni mwongo na baba wa huo.Yesu anasema ametupa mamlaka mbinguni na duniani kukanyaga nguvu zote za mwovu shetani sisi ni kukemea na kuyamuru kutoka kwa jina la Yesu kama Paulo alivyo kemea yule kijakazi aliyewapa faida bwana zake soma matendo 16:16..18
  balikiwa nyote

 16. je, ni sahihi kuhojiana na majini wakati wa kuyafukuza??

  Nina maswali yaliyotokana na hili swali
  1. sahihi ni nini??
  2. kuhojiana ni kufanya nini?
  3. majini ni nini?
  4. majini yanafukuzwa?
  5. kwanini majini yafukuzwe?
  5. usahihi wa jambo anatudhihirishia nani?

  je ni muhimu kuzingatia yale ambayo husemwa na majini/mapepo wakati huo?

  hapa napo nina maswali
  1. muhimu ni nini?
  2.kuzingatia ni nini?
  3.majini na mapepo ni Kitu kimoja au vitu viwili tofauti
  4. kama ni muhimu kuyazingatia umuhimu wake ni nini??

 17. Don’t Talk with Demons

  A second fact about Jesus and demons is this: He never held conversations with demons. He said, “Be quiet! Come out of him!”

  It is true that on one occasion Jesus asked a demon his name, but this was because the demon refused to go. I suppose you may ask a demon its name if they refuse to depart, but it’s not wise to hold a conversation with them. Ordinarily, Jesus shut the mouths of demons. This is the normal way of deliverance

 18. Nafikiri kuyahoji majini si tatizo sababu hata Yesu alikuwa akiyahoji;tatizo ni kushilikilia bahazi ya maneno yasemwayo.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s