Sala ya Bwana

 beautiful-theme-with-the-lords-pray
Bwana Yesu asifiwe!
Napenda niwashirikishe kuhusu SALA YA BWANA ambayo watu wengi tunaijua. Tutakwenda  kuona ufafanuzi ambao unaweza kutusaidia ili kuweza kujua namna sahihi ya kutumia.

Sala hii ya Bwana inapatikana katika kile kitabu cha Mathayo 6:9-13:

9: Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10:Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11:Utupe leo riziki yetu.
12:Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13:Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]Sala ya Bwana ni fupi sana lakini ina mapana yake kwa kuzingatia vipengere mbalimbali.
Katika sala ya Bwana kuna  vingere SABA (7) vya muhimu;
1. BABA YETU ULIYE MBINGUNI JINA LAKO LITUKUZWE.
Katika kipengele hiki mwombaji anapaswa kuwa na kipindi cha kumsifu na kumuabudu Mungu kwa majina yake, kabla ya kupeleka mahitaji yake, tambua kuwa Mungu anakaa Katika sifa
Jizoeze kumsifu na kumwabudu Mungu kwa majina Yake maana kila Jina Linabeba sifa za Mungu2. UFALME WAKO UJE HAPA DUNIANI
Katika kipengere hiki Yesu anatufundisha kufanya vita vya kiroho, kuvunja kazi za shetani na kuharibu nguvu za giza na kuzipinga hila za shetani ili kuruhusu ufalme wa Mungu uchukue nafasi.
Kumbuka kuwa shetani alitupwa dunia na amejenga ufalme wake, hivyo kuomba ufalme wa Mungu uje duniani ni kutangaza vita na mapambano dhidi ya ibilisi shetani. YAKOBO 4:7; 1PETRO 5:8-93. MAPENZI YAKO YATIMIZWE DUNIANI KAMA MBINGUNI
Katika kuomba kwetu ni muhimu sana kutafuta kuyajua mapenzi ya Mungu kwa watu wake duniani ambayo anataka yatimizwe.
Ukiisha yajua mapenzi hayo ya Mungu ni muhimu kukaa Katika kuyaombea ili yatimizwe Katika maisha yako.
Mapenzi ya Mungu hujulikana kwa kusoma na kusikiliza Neno la Mungu.
Mfano ni mapenzi ya Mungu watu wote waishi kwa Amani na utulivu (1TIMOTHEO 2:1-2),  ni mapenzi  ya Mungu watu waponywe magonjwa yao na kudumu Katika afya njema (3YOHANA 1:2)
NB: kuwa msomaji na msikilizaji mzuri wa Neno la Mungu kutakuwezesha kuyajua na kuyatambua mapenzi ya Mungu kwa watu wake walioko duniani.

4. UTUPE LEO RIZIKI YETU
Hiki ndiyo kipengere ambacho, mara nyingi, lengo la mwombaji yeyote hulenga.
Hiki ni kipengere ambacho mwombaji anatakiwa kupeleka mahitaji yake mbalimbali mbele za Mungu sawa sawa na haja za moyo zilivyo. Yawezekana ni mahitaji yanayotuhusu moja kwa moja sisi, lakini yaweza kuwa ni ndugu,  marafiki, majirani, nchi au taifa.
Na hapa Yesu alisema tunaweza kuomba lolote Katika Jina lake na Baba wa mbinguni atatenda
Soma YOHANA 14:13; MATHAYO  7:7-14, ISAYA 43:26.

5.UTUSAMEHE MAKOSA YETU
Katika muda wako wote wa maombi unatakiwa kupata muda wa kwenda mbele za Mungu kwa Toba ili kuungama na kutubu juu ya makosa mbalimbali ambayo huwa tumetenda kwa uovu mbele za Mungu.
Kumbuka neno linasema tukisema hatuna dhambi twajidanganya wenyewe na kweli haimo ndani mwetu, lakini tukiziungama dhambi zetu Mungu ni Mungu mwenye haki na rehema atatusamehe maovu yetu na kutusafisha dhambi zetu…1YOHANA 1:7-9
Pia hapa tunapata wakati mzuri wa kuomba Toba kwa ajili ya wengine, jamii yetu, kanisa lako, ukoo wako, kabila lako na taifa lako. Kama alivyofanya Daniel (DANIEL 9:1-19).

6.USITUTIE MAJARIBUNI BALI UTUOKOE NA YULE MWOVU (Shetani na hila zake na kazi zake)
Katika muda wako wote wa kuomba ni muhimu kupata nafasi ya kukiri na kuombea maeneo yako ya udhaifu ambayo yanaweza kukutia katika majaribu (YAKOBO 1:13-14).
Kukiri udhaifu mbele za Mungu na kumkabidhi Mungu udhaifu huo; husaidia sana ili shetani asije tumia udhaifu huo na mtu wa Mungu ukaingia Katika kumkosea Mungu na kuishi kinyume cha mapenzi ya Mungu.
Kila mmoja ana udhaifu wake kwa mfano:-hasira za haraka, masuala ya pesa, tamaa za mwili (zinaa na uasherati), matumizi ya ulimi (uongo,usengenyaji) na udhaifu wowote unaoujua mwenyewe.
Ni vema tena ni muhimu kupata muda na nafasi yakukiri  na kuombea maeneo yako ya udhaifu ambayo yanaweza kukutia Katika majaribu  mbele za Mungu.
7.KWA KUWA UFALME NI WAKO NA NGUVU NI ZAKO NA UTUKUFU NI WAKO TANGU SASA NA HATA MILELE
Kama mwanzo unapotaka kuanza maombi lazima kuanza kwa kumsifu na kumwabudu Mungu, vivyo hivyo mwombaji unatakiwa kumaliza maombi yako kwa kumsifu na kumtukuza Mungu. Mungu wetu hupenda sana kusifiwa na anatakiwa kusifiwa na kutukuzwa kila wakati (ZABURI 113)

Katika kipengere hiki cha saba tunaona Bwana Yesu anatufundisha sisi kama watu wake kufungua maombi yetu kwa kumsifu Mungu na kumtukuza pia anatufundisha kumaliza maombi yetu kwa kumsifu na kumwabudu Mungu. Jizoeze kila wakati uwapo Katika maombi Kumsifu na Kumwabudu Mungu pindi uanzapo na umalizapo (ZABURI150:6; ZABURI 33:1-5)

Kwa kuzingatia ufafanuzi huu tunaweza kuona kuwa kumbe  SALA YA BWANA siyo kitu cha kukiimba kwa kukariri kama tulivyozoea kufanya bali Sala ya Bwana ni muhutasari tu wa mambo muhimu yaliyopo katika kipindi cha maombi . Sala ya Bwana ni vipengele muhimu vya kuombea, pale tupatapo muda wa sala na maombi.

Asante na Mungu awabariki!!

Samwel Mmasa

7 thoughts on “Sala ya Bwana

 1. Nachukua nafasi hii kwa kumshukuru kila mmoja aliye changia Katika somo la Sala ya Bwana
  Katika YOHANA 17
  Hii ilikuwa ni sala ya Bwana Yesu mwenyewe aliomba
  Lakini hii nyingine ndiyo aliotuachia sisi ili tujue ni namna gani ya kuomba
  Hivyo nilicho kuwa naeleza Katika somo hili ni vile kupata ufahamu zaidi Katika Sala ya Bwana
  Na hii inaweza kuwa msingi mzuri wa maombi kwa Yule ambaye ni mchanga Katika kuomba akupata somo hili atajua ni namna gani anaweza kuomba!
  Pia Sala hii inatuwezesha kuwa na maombi ya muda mrefu maana tumebiwa ombeni bila kukoma

 2. Dada Gladys,
  “Sala ya Bwana” ni ile sala aliyoisali yeye km tunavyoiona hapo ktk Yn 17; hii nyingine ni jinsi alivyotufundisha kumwomba Baba yetu aliye mbinguni kwa maneno machache yanayojitosheleza, badala ya kuremba sana mpaka unasahau hata ulikoanzia!

 3. vyema sana mpendwa kwa somo zuri maana tusiwe tunapenda kupokea upako kwa mch.kakobe,gwajima, mwakasege au kaldinali pengo wakati hata sala ya BWANA hatuielewi,tunasali kwa mazoea,mimi naendelea kujifunza, mbarikiwe

 4. Asante ndugu Samwel kwa ufafanuzi huo mzuri juu ya sala ya BWANA.
  Mimi naomba tu Nisaidiwe kutofautiana fundisho na sala.
  Kwa ufahamu wangu hii sala ya Baba Yetu ilikuwa ni mafundisho ya Yesu kwa wanafunzi wake jinsi gani waombe. Lakini tukiangalia ktk Yohana sura 17 yote pale utaona kuwa Yesu alikuwa akiomba kwa ajili yake mwenyewe, na wanafunzi wa wkt ule na sisi wa zamani hizi. Je sala ya BWANA ktk hizi mbili ni ipi?

 5. Bwana asifiwe watumishi Asante sana Timu nzima ya Strictly Gospel Kwa kukubali na kuihariri pamoja na kuwashiriki watu wote somo fupi kuhusu Sala ya Bwana Baba wa mbinguni awabariki kwa kazi njema.

  Samwel Mmasa

  Ndugu, Mungu wa mbinguni akubariki!
  Fuatilia maoni ya wasomaji ili kujibu kama kuna swali litakalojitokeza kutokana na ufafanuzi wako. – SG

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s