Matumizi ya VITU badala ya JINA LA YESU.

20120425060612953

Kadri siku zinavyokwenda Matumizi ya vitu kama Vitambaa, Maji nk yanazidi kuongezeka ambapo watu wanaojulikana kama Watumishi wa Mungu HUVIOMBEA vitu hivyo kisha kuwagawia/Kuwauzia watu. Mtu akipatwa na tatizo anachotakiwa kufanya ni KUBANDIKA, KUPAKA, KUMIMINIA, KUNYWA au KUNUSA/KUVUTA kitu alicho alichonunua, kutegemeana na maelekezo ya matumizi ya kitu hicho.

Je, Jambo hili ni Sahihi katika Ukristo?

38 thoughts on “Matumizi ya VITU badala ya JINA LA YESU.

 1. Ezekieli 13:17-23 imeelezea juu ya matumizi yasiyofaa ya vitambaa hivyo. Wengi wanavitumia ili kwanza wapate manufaa ya kifedha kwa kuviuza. Pili wanavinuizia mapepo huku wakiwaamisha waumini kuwa ni miujiza ya Yesu itendayo kazi ndani yake, kumbe ni Shetani. Tatu wanavitumia ili kuwinda roho za watu kwa utabiri na maono yao wenyewe. Tusimame kwenye Neno, Shetani asituchezee.

 2. Ndugu Sungura,

  Tangu nilipoingia ndani ya hii mada nilisema kama matumizi mazuri ya vitu ni halali. Uhalali wake siyo ndani ya vitu lakini ndani ya namna vinavyotumika na matunda vinavyotoa. Hata Jina la Yesu , wewe mwenyewe ukilitumia kwa mzaa ao kwa lengo lako mwenyewe, ao kwa faida ya Ibilisi, … siyo halali.

  Yote inategemea hali ya mtu anaetumia vitu ao Jina la Yesu. Akiwa yeye mwanyewe hastahili, anavyofanya vyote si halali.
  Pia ulikuibaliana nami kama vitu vikiuzwa kwa mfano siyo halali. Hence I think tuko pamoja lakini nataka tu nisisitize kama siyo vitu tu vinatumiwa vibaya; hata Jina la Yesu watu wa lengo mbaya wanalitumia vibaya.

  Asante.

 3. Ndugu Dauban,

  Nafikiri hujasema tofauti na kauli yangu. Pengine ni jambo la upana na urefu ambalo hukuchunguza. Pia inatakiwa ufahamu kama hilo Jina la Yesu hutumiwa pia vibaya na watu wengi, hao wa Ibilisi. Alimradi, Jina la Yesu linapaswa pia tumiwa vizuri. Hapa sasa imetupasa kuchunguza yule mtu anaelitumia. Dauban, kama nimekuelewa, unahakikisha kama namna hivyo vitu vinavyotumika imekwisha pindishwa. Mim nakubaliana na hiyo kauli yako. Lakini nikupashe kama kupindisha matumizi ya Jina la Yesu ni hasara kubwa sana. Hence, hii unayoongea ni ok, lakini uitie ndani ya urefu na upana wake ndipo utagundua kama tukiacha hayo mabaya tutatambua kama kulitumia Jina la Yesu na kuvitumia vitu kama jinsi vilivyotumiwa na mitume yote ni halali lakini kila moja na lengo lake kwani:
  -Wakati wa mitume waliyotumia vitu hawakuwa na lengo ya okovu licha ya kuwa okovu ingeliweza fika baadaye.
  -Bali Jina la Yesu linaleta okovu, miujiza, rehema

  Sasa imekupasa kugundua hayo matumizi mabaya ya Jina la Yesu, ndipo uconnect na matumizi mabaya ya hivyo vitu. Ukifanya hivyo utatoa shauri kamilifu lanalolingana na neno kama “ategemeae mwanaadamu alaaniwe”.

  Mim kama mukristo sina haja ya kuwekewa mikono kwa Jina la Yesu na mtu ambae simfahamu, pia sina haja ya kuuza vitu ili ndivyo viniletee miuujiza. Ni kulitumia hilo neno la Yeremia 33:3.

  Hivi lengo langu hapa ni kusaidia watu kufungulikana macho, wafahamu kama kwa sasa, pamoja na kwamba vitu vinatumiwa vibaya pia Jina la Yesu nalo limetumiwa na watu wa Ibilisi. Nafikiri kama hii ndo inaweka angalisho zaidi kwa mukristo. Ndo maana Ndugu Dauban uliniona nikikuambia kama vyote ni halali (katika matumizi halali), yale ya msinji. Lakini pia kwa upande mwengine matumizi ya jina la Yesu na hivyo vitu yote siyo halali ( kama ni ya Ibilisi).

  Asante.

 4. ndugu Dauban
  comment yako ya mwisho imemrudishia Yesu utukufu.Udanganyifu na hila zimekuwa nyingi
  ni vema ktk nyakati hizi za hatari mashujaa wa Yesu wakategemea imani
  iliyo ndani ya jina la Yesu ambayo haipitii kwenye biashara ya maji, mafuta, vitambaa, sabuni, stika nk

 5. ndugu ziragora,
  umeongea sawa, lakini mimi nimejibu kulingana na swali lililoulizwa.{je matumizi ya hivi vitu ni sahihi katika ukristo?} yaani vile vinavyotumika siku hizi nisawa katika ukristo?.na nimejaribu kuelezea tofauti ya matumizi ya hivi vitu wakati wa mitume na siku hizi,ndo nikasema kwa kuwa njinzi vinatumika siku hizi nitofuati basi si halali katika ukristo.si halali pia mtu kuenda kwa kristo kwa nia ya kudaka tu miuza wala si wokovu,ijapokuwa wengi wanafanya hivyo lakini si halali.haifai tumfuate yesu kwa ajili ya mkate,yesu alikuja duniani akateswa,akasulubiwa si kwa ajili ya miujiza tu bali ni kwa ajili ya wokofu,miujiza halali katika ukristo ni ile iletayo wokofu.vitambaa na mafuta na maji yakileta miujiza baada ya kuombewa na kuuzwa hivileti wokovu wala utukufu wa mungu bali ni ajenti ya yule muongo,ambaye siku zote anabadilisha kweli kuwa uongo na kuwapotosha wale wasioweza kutambua ujanja wake.basi watu wa mungu wafuate jina la yesu kristo,jina lililetayo miujiza na wokovu kwa pamoja.
  asante

 6. Ndugu Ziragora,

  Sijui kama nilisema kitu kigumu, lakini ni vema tukakumbuka kuwa kiini cha mada ni kama ni sawa kutumia vitu kama vitambaa kwa ajili ya kuwahudumia watu, eg, kuwatoa mapepo, kuwaponya, nk.

  Mimi nasema ni sawa, labda tatizo liwe kwenye namna suala hilo linafanyika, eg; kuviuza, na kuwaaminisha watu kuwa bila hivyo vitu hawawezi kufunguliwa shida zao, hiyo si sawa.

  Kuhusu miujiza na wokovu nikasema kuwa wokovu ni mkuu kuliko muujiza, maana muujiza uko ndani ya wokovu. Lakini pia nikasema kuwa muujiza eg; uponyaji, kutolewa pepo, n.k, mara nyingi hutangulia kabla hata ya mtu kukamilisha mchakato wa wokovu, na nikatoa mifano iliyo kwenye maaandiko.

  Tena nikakumbusha kuwa miujizsa mingi ni sehemu ya wokovu. Kwa mfano kuponywa, kufunguliwa frm mapepo, n.k ni sehemu ya package ya wokovu (sozo).

  Na kama kuna mtuambaye anashabiia miujiza na kuiona ni ya muhimu kuliko wokovu, basi hajielewi.

  Asante.

 7. Dauban,

  Hauwezi ukasema miujiza inayotokana na matumizi ya hivyo vitu ni ya kishetani just kwa sababu mitume wala Yesu hawakutuambia tuvitumie. Hiyo reaction yako inanipa kuamini kuwa hufikirii mambo sawasawa.

  Ulitakiwa tu useme kuwa shida yako iko kwenye namna hivyo vitu vinatumika, siyo kwenye kama ni halali vitu hivyo kutumika, maana tayari kwenye maandiko vilishawahi kutumika.

  Kwamba tunatakiwa kujenga katika msingi wa mitume na manabii, hiyo ni kweli kabisa, lakini hili pia watu wengi hamlielewi sawia,ila mwapenda tu kulinukuu kwa vile limeandikwa.

  Ukiuchanganua huo msemo ktk msingi wake utaelewa kuwa kinachopigiwa picha ni nyumba. Sasa nyumba siyo msingi tu, siyo mchanga tu, siyo kokoto tu, bali inajengwa na kukamilishwa na vitu vingi.

  Kama mitume walijenga msingi wa mawe, renta huwa siyo mawe bali ni kokoto na cement nyingi, paa huwa siyo la mawe, bali ni vitu vingine kama mabati, etc, madirisha huwa siyo ya mawe pia.

  Maana yake ni kwamba hatulazimiki kufanya tu yale ambayo mitume walifanya. Mfano, walisafiri kwa boti, basi nasi leo tungesafiri kwa boti tu, maana hawakutuwekea msingi wa kupanda ndege.

  Si kila jambo tunalofanya lazima liwe lineabdikwa kwenye maandiko, ingekuwa hivyo, basi kuna mambo mengi sana tusingeyafanya leo, maana mitume hawakuyafanya. Mf. Hawakuwa kujenga kanisa(jengo), bt sisi tunajenga.

  Roho mt.hakomei tu walipokomea mitume, na kama tungefanya yale tu mitume walifanya tukakomea hapo, basi tungekuwa bado tunajenga msingi tu wala gatujaanza hata kuweka tofali.

  Nilikuambia kuwa ni kweli matumizi ya hivyo vitu yanaweza kuwa yanakosewa na watu wengi. Mambo ya kuviuza kwa pesa hivyo vitu yanaweza kweli yakawa makosa,lakini kwamba si halali kuwaambia watu wachukue hivyo vitu, au wawapelekee wagonjwa wao, ati kwa vile mitume hawakuwahi kuwaambia watu watumie hivyo vitu, bali watu wenyewe ndo waliamua kuvitumia, huo ni ufinyu wa kumjua Mungu Dauban.

  Asante

 8. Ndugu dauban,

  Nafikiri umereact kama mtu anaesoma kipande kidogo sana cha shairi na kuanza kuweka comments.
  Uhalali wa hivyo vitu ni kwamba vinatumika tu wala sikusema ni njia inayonyooka kila mara, kitofauti na kwamba ningesema havitumike. Leso ikiibwa kutoka kanzu ya Paulo kama ikileta muujiza wa uponyaji, ni hizo nguvu za Yesu zilizomo zinazotumika. Kwani kwa nini Yesu asizuize huo muujiza kutendeka? Lakini nafikiri kama umedaka kama miujiza kama hiyo mara nyingi siyo ya wokovu.
  Hence, vitu kutumika vinafaa tu kwa miujiza, ndo maana makusudi ufahamu uhalali wa kitu zungumzia kwanza lengo. Sasa hatutasema kama siyo halali kwa dauban kupata muujiza!!!! Kinachobaki ni kufahamu umetoka kwa nani. Maadam dauban shida yake ni kuupata ule muujiza na mwishoe ameupata, hiyo ni halali. Lakini kama dauban ameokoka na hashabikie miujiza kama mulokole anaekamilika ndipo ataanza chunguza sana.

  Jaribu kutochanganya muujiza na wokovu ndipo utaelewa.

 9. ndugu ziragora,
  wewe pia unataka kuingia katika upotovu wa hawa watu,hapo uliposema kuwa hivo vitu ni halali kutumika,umesahau kuwa jinsi vinatumika siku hizi ni tofauti na jinsi vilitumika wakati wa YESU na mitume pia,yule mwanamke aliamua mwenyewe kuguza pindo la vazi ya YESU KRISTO,YESU hakumwambia afanye hivyo,tena watu wenyewe waliamua kuweka wagonjwa wao barabarani ili angalao kivuli cha petro iwaguze anapopita,petro hakuwaambia wafanye hivyo,paulo naye hakuwaambia watu watumie vitambaa na leso bali watu wenyewe waliamua,na hata baada ya hapo hawakutoa agizo vitu hivyo vitumike,siku hizi waubiri wenyewe ndo huambia watu wavitumie baada ya wao kuziombea,huoni kunatofauti kubwa sana,matumizi ya hivi vitu kwa njia hi si halali tena ni ya kishetani,walokole halisi wajiepushe na hi ibada ya sanamu.wanafunzi halali wa YESU wataendelea kujenga juu ya msingi ya mitume na manabii,YESU KRISTO akiwa jiwe kuu la pembeni
  asante.

 10. Ndugu Sungura,
  Tafazali twende kwenye connection moja! Ukisoma tangu mwanzo wa mada tofauti ni ndogo sana na hakuna upinzani. Acha nijaribu hivi: Ukiangalia kwa makini mifano uliyotoa, utatambua kama hiyo miujiza haikuombwa wala kuuwza. Na hapo ndipo hupatikana kiini cha hizo tofauti.

  Hawa wandugu hawakuokolewa kwa miujiza lakini mokovu wao ndio muujiza mwenyewe iliyotoka kwa Yesu Kristo. Muujiza huokoe bali Jina la Yesu Kristo ndilo liokoalo.

  Kuombea mtu apone au kumtoa pepo siyo kumuokoa kiroho kwani kuna wengi wanaoponywa baadae wanabaki wapagani. Hence siyo muujiza iokoayo bali Yesu Kristo mwenyewe. Ndio maana kama muujiza unao lengo la wokuvu inatakiwa Jina la Yesu litajwe. Lakini muujiza kama muujiza tu, huwezi fahamu malango yake. Kwa mfano kama ni mtumishi wa Ibilisi anaeleta muujiza hiyo muujiza , itakuwa ya upotevu licha ya kuwa inafanana miujiza ya Yesu.

  Kwa mwisho nilidhani katika makala yako uliwaza juu ya possibilities mbili: miujiza kama miujiza tu ambayo hata vitu vyaweza tumiwa na miujiza ya wokovu itokayo kwa Yesu Kristo kwa mapenzi yake na ambayo walokole wanapashwa shabikia. Ndo maana nikakubaliana na wewe kama yote ni halali kiroho lakini matukio siyo sawa kila mara.

  Asante mpendwa.

 11. Ziragora,

  Nimekupata vizuri, lakini nina jambo la kusema kwenye dondoo yako ya nne, inayosema wokovu kwanza, kisha muujiza uombwe kwa uongozi wa Roho mtakatifu.

  Ni kweli wokovu ni wa muhimu kuliko muujiza, na mtazamo huu watu wengi sana wamekuwa nao pale wanapojaribu kuwashambulia wale ambao wanaonekana kushabikia miujiza.
  Lakini kwa mtu anayehitaji muujiza na wokovu kwa pamoja, mara nyingi tu huwa unatangulia muujiza kwanza ndo wokovu unafuatia.

  Mwangalie mlinzi wa gereza waliomofungwa Paul na Sila, anauliza linalompasa kufanya ili aokoke, baada ya muujiza wa kumfanya asijiue kutokea- mdo 16:27-29

  Paul mwenyewe anaanza mchakato wa wokovu (kubatizwa) baada ya kupata muujiza wa kuona – Mdo 9:18

  Watu wengi tu kwenye maandiko waliponywa matatizo yao kwanza ndipo likafuata suala la wokovu.

  Ni vigumu sana kumhubiria suala la wokovu mtu ambaye yuko matatizo kama ya magonjwa, njaa, n.k, bila kwanza kuwa umeyatatua hayo mambo. Na kuyatatua hayo huhitaji kitu kinachoitwa muujiza.

  Tukumbuke kuna mambo ambayo yanatokea kama muujiza ambayo ni sehemu ya kifurushi cha wokovu. Mfano; muujiza a uponya, kutolewa mapepo, nk. Kwa hiyo miujiza mingi ni part and parcel ya wokovu.

  Barikiwa

 12. mtimishi Ziragora
  Hongera, INPUTS zako zimebeba uzima.Zinaonyesha njia ambayo wana
  wa Mungu wanatakiwa kupita.

 13. Wapendwa Sungura na Dauban,
  Mniruhusu nije tena na hoja ndogo kuliko huko chini. Kwa kitu kidogo sana watu huweza ona wako tofauti bila kuonyesha huo utofauti. Nadhani Sungura na Dauban mnafahamu kam hivyo vitu vinaweza tumika kabisa. Lakini swali ni kujua kama ni halali kiroho, pia kiroho vinafalia nani kwa nini.
  Jibu: 1) Ni halali kiroho kwani vinatumika kiroho
  2) Vina tatizo kwani kutofautisha malango yavyo ni vigumu. Nguvu hizo hizo Ibilisi anazo. Ina maana wanaovitumia wokovu hawana, wanataka tu miujiza.
  3) Lakini pia Ibilisi analitumia jina hilo la Yesu. Hence matumizi ya hilo jina hayatoshe kwa kuthibitisha malango ya miujiza.
  4) Ndio maana wokovu kwanza, then miujiza au msaada wa Mungu uombwe kwa uongozi wa RM. Na anayeleta wokovu siyo vitu bali Yesu Kristo.
  5) Ndio maana imeandikwa “ategemeae mwanaadamu alaaniwe”. Kwa maana tumefanywa makuhani, tuna neema ya kufika kwa Yesu Kristo bila kuvitumia vitu ambavyo vimetoka kwa wanadamu.
  6) Hence hizo nguvu ziko kabisa lakini kuzitumainia siyo halali kwa mtu aliyeokoka.

  Asante

 14. Dauban, naendelea.

  Umesema kuwa kumpokea Yesu ndio kumpokea Roho mtakatifu.

  Hebu soma hii case study; Acts 19: 1 And it came to pass, that, while Apollos was at Corinth, Paul having passed through the upper coasts came to Ephesus: and finding certain disciples,

  2 He said unto them, Have ye received the Holy Ghost since ye believed? And they said unto him, We have not so much as heard whether there be any Holy Ghost.
  -Verse 6, And when Paul had laid his hands upon them, the Holy Ghost came on them; and they spake with tongues, and prophesied.”

  Hao wanaoitwa wanafunzi(deisciples) walikuwa ni watu ambao wamempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wao, lakini walikuwa hawajapokea Roho mt.

  Baadae katika mstari wa sita ndipo tunaona wanakuja kumopkea Roho mtakatifu.

  Kama haya matendo mawaili ni ‘interchangeable’ basi kutoke kwa moja kungekuwa kumemaanisha kutokea kw lingine, kwa hiyo kusingekuwa na sababu ya jingine kuja kutokea baadae.

  Lakini ni kweli Yesu ndiye Roho ndiye Baba (hiyo nayo ni shule nyingine)

  Asante.

 15. Dauban,

  Jatika kunijibu umesema maneno haya; ”JINA la YESU halikutoka kwa paulo likaingia kwa leso bali ni UPAKO au NGUVU ya ROHO MTAKATIFU aliye ndani yako na tena imekuzingira ndo hufanya kazi zake,hii ndo sababu pepo anaweza kutoka kwa kukuona tu bila wewe kumkemea,anapokutazama hakuoni wewe mdhaifu bali yuamwona YESU MWENYE NGUVU NA MAMLAKA,kwa kuwa umemvaa,wagalatia 3:27.unaweza kutoa pepo pasipokutaja jina la YESU,ukijua unaye YESU ndani yako na wewe ndani yake unaweza kuamrisha tu toka na hapohapo anatoka.kitu unafaa ujeu ni kuwa si wewe bali ni YESU KRISTO aliye ndani yako kwa njia ya ROHO MTAKATIFU ndiye anafanya kazi hizo zote”

  Sasa kama unajua kuwa jina la Yesu halikutoka kwa Paul likaingia kwenye leso, bali kilichoingia kwenye leso ni upako wa Roho uliokuwa ndani ya Paul, kinachokushangaza leo vitambaa na vitu mbalimbali vikitumika kupomya watu ni nini?

  Kama unajua kuwa naweza/waweza kutoa pepo bila kutaja jina la Yesu, kinachokushangaza nini leo nikitoa pepo kwa kutumia kitambaa?

  Ukiniambia kuwa natakiwa nijue kuwa si mimi mwenye kutenda hayo bali ni Yesu aliye ndani yangu, nakushangaa sana. Kabisa unajaribu kufikiri kuwa mimi sijui anayefanya hayo si mimi?
  Labda tu nikuongezee kitu katika kiwango cha juu kidogo hapo, anayefanya hiyo kazi ni mimi kwa mamlaka niliyopewa na Yesu. Alisema nimewapa mamlaka ya kukanyaga nge na nyoka,…., toeni pepo, takaseni wakoma, fufueni wafu, nk.

  Ntaendelea!

 16. ZIRAGORA,
  MUNGU BABA WA BWANA WETU YESU KRISTO AKUBARIKI KWA MCHANGO WAKO SAFI.

 17. kwa habari ya matumizi ya maji, mafuta, vitambaa nk ambayo ndiyo injili ya msingi ktk madhabahu za mitume na manabii wengi wa leo, Mungu anatoa ANGALIZO kwa wateule wote ktk ISAYA 42:18-22

  Katika maandiko haya Yesu anaeleza wazi kwamba tatizo la watu wake ni vipofu na pia ni viziwi.Anatuonyesha mambo mengi lakini HATUELEWI yaani
  hatuyatii moyoni.Mambo mengi wanayofanya hawa wanaoitwa mitume
  na manabii wakati mwingine hayahitaji
  hata ufahamu wa rohoni kutambua kwamba ni wizi na uuaji mkubwa.Wanafanya biashara ya kuuza maji, mafuta , vitambaa na stika mchana
  kweupe!

  ktk mstari wa 22, Yesu anatoa wito
  kwa wateule wenye macho na masiko ya rohoni kuwasaidia wenzao waliotekwa na mambo ambayo Hayatoki kwake.

  Hatuhitaji kusikiliza mafundisho au mahubiri ya mtu kuhusu UHALALI wa matumizi ya vitu hivi bali TUNAPASWA KUMSIKILIZA ROHO MTAKATIFU.Kuyatambua mafundisho potofu na mambo yote yanayofanyika kwa HILA
  Inahitaji MAARIFA YA ROHO WA KRISTO.

 18. sungura
  niruhusu niendelee kukujibu.
  kufanya kazi kwa hivyo vitu vitategemea,vyaweza kufanya kazi kwa ajili ya imani ya mwenye kuitumia kupitia kwa huruma{neema}YAKE BWANA YESU,siyo kwa sababu yule muombezi amafanya jambo jema kwa kuuza au kuombea hivyo vitu.JINA la YESU halikutoka kwa paulo likaingia kwa leso bali ni UPAKO au NGUVU ya ROHO MTAKATIFU aliye ndani yako na tena imekuzingira ndo hufanya kazi zake,hii ndo sababu pepo anaweza kutoka kwa kukuona tu bila wewe kumkemea,anapokutazama hakuoni wewe mdhaifu bali yuamwona YESU MWENYE NGUVU NA MAMLAKA,kwa kuwa umemvaa,wagalatia 3:27.unaweza kutoa pepo pasipokutaja jina la YESU,ukijua unaye YESU ndani yako na wewe ndani yake unaweza kuamrisha tu toka na hapohapo anatoka.kitu unafaa ujeu ni kuwa si wewe bali ni YESU KRISTO aliye ndani yako kwa njia ya ROHO MTAKATIFU ndiye anafanya kazi hizo zote john 14:20 na john 14:13-14.kila mtu atahukumiwa kwa kazi aliyofanya. ubarikiwe,kama kuna mahali hujanielewa au unataka kunielezea,basi karibu ndugu yangu.

 19. sungura
  tofauti yangu na wewe ni kidogo na pia ni kubwa.nakubali unaweza kuwa na haki na usitoe pepo,hi huja kwa sababu ya tofauti ya karama au vipaji.1corinthians 12:4-11,vipawa tofauti na roho ni yule mmoja.kumpokea yesu ndo kumpokea roho na kumpekea roho ndo kumpokea yesu,kwa sababu bwana ndiye roho,2corinthians 3:17,na tena john 14:18-20,23.unaona wazi kuwa ni yesu ndiye anaye kuja katika hali yake ya kiroho.wengi kwa kutoelewa husema twampokea yesu kwa kuombewa sala la toba na hiyo si kweli,wengini pia husema twampokea kwa njia ya ubatizo hi pia si kweli,ukibatizwa unamvaa yesu na ukijazwa roho mtakatifu ndo unampokea yesu,chunguza maandiko na utaona ni kweli.kwaivyo uwezo wa kutoa pepo tunapata tunapompokea{tukijazwa roho m},john 14:12-14.tukiomba chochote kwa jina lake atatenda,na tena anasema atakuja akae nasi yaani ndani yetu.john 14:23.kama kweli tumejengwa juu ya msingi ya mitume na manabii basi tufanye vile walifany,wtu wenyewe waamue kuvitumia wakiongozwa na roho mtakatifu—–

 20. Dauban,

  Kuna kitu ulisema hapa ngoja nikuoneshe:
  ”.wana wa sekewa hawakuwa na ROHO MTAKATIFU.kumaanisha hawakuwa na HAKI wala NGUVU ya kuweza kutoa mapepo.ndio sababu waliuzwa”

  Lakine tena umesema ”wana wa mungu ndo wanao haki ya kutumia hilo jina,na tunapata hiyo haki kwa kumpokea YESU KRISTO na kuamini JINA LAKE”

  Hapa umeongea vitu viwili tofauti. Ni kweli haki ya kutumia jina la Yesu tunaipata kwa kumpokea. Lakini suala la kumtoa pepo unaweza ukawa na hiyo haki na asitoke.

  Kwanza elewa kuwa kumpokea Yesu na kujazwa Roho mtakatifu ni vitu wilili tofauti. Si kila aliyempokea/aliyemwamini Yesu amejazwa Roho mtakatifu.
  Ndio maana wanafunzi wakaambiwa wasiondoke mpaka wapokee nguvu.

  Sasa uwezo wa kutimua mapepo hauji kwa kumpokea Yesu,ispoikuwa kwa kuwa na nguvu ya Roho mtakatifu.

  Nafikiri shida yako kubwa ni suala la kwa nini leo watu wanawaambia watu watumie vitu ambavyo wameviombea, wakati mitume hawakuwaambia watu ispokuwa watu wenyewe waliamua kutumia hivyo vitu.

  Kitu ambacho mimi sikikubali katika matuzi ya vitu, ni kule kuwauzia watu, na kuwaaminisha watu kuwa bila hivyo vitu mambo hayataenda. Kwa mfano mambo ya mfuta ya upako, maji ya upako, vitambaa vya upako(kama wengi waitavyo)
  Lakini suala la kwamba hivyo vitu hufanya kazi, liko wazi kwamba hufanya kazi.

  Suala la matumizi ni la kimaadili, na kila mtu atatoa hesabu ya jinsi alivyotumia talanta ambayo amepewa.

  Na shida yako kubwa nyingine ni uhusiano wa matumizi ya vitu na jina la Yesu.

  Labda jiulize kwanza kuwa, jina la Yesu lilitokaje ndani ya mtume Paul, hadi likaingia ndani ya vitambaa vya aliyokuwa vimegusa mwili wake? Paul hata hakuviombea hivyo vitambaa, afadhali hawa wa leo hata wanaviombea.

  Jiulize na haya maswali pia:

  Wewe unaaminije katika hili, je inawezekana pepo akamtoka mtu kwa kukuona tu wewe bila hata wewe kutaja jina la Yesu?

  Unaweza ukamkemea pepo kwa kusema tu ”pepo toka” bila kumalizia ‘kwa jina la Yesu na pepo akatoka kweli?

 21. Ndugu Sungura na Ndugu Dauban,

  Nimefwata vizuri mazungmuzo yenu wala sitayarudilia kwani kila mmoja amejieleza vizuri.

  Kinachowatofautisha ni uchambuzi wa lengo la yule mtu anaevitumia vitu pahali pa jina la Yesu Kristo. Pia ifahamike kama kwa kuvitumia hivi vitu aletuletea mada hakusema vinatumiwa kwa kudharua hilo Jina Kubwa. Nafikiri huyu mtu anavitumia kwa kujihukumu mwenyewe akiona kama yeye hastahili kuliita hilo Jina lililo kubwa kuliko majina yote, hapo akitafuta msaada kwa wale ambao anadhani wanamkomalia kiroho.

  Kwa mfano likiwa lengo la miujiza tu nafikiri kila mtu atakubaliana na Ndugu Sungura. Mtu anaetaka kupona anapotumia leso ya Paulo na kupata uponyaji pia kuwaponya wengine, amezitumia nguvu za Yesu Kristo hata pasipo kumfahamu wala kumwamini. Na kama Yesu anaruhusu ile ni kwa sababu anafahamu kama kuna utofauti mkubwa kati ya miujiza na wokovu. Nadhani mwenye mada anasema matumizi ya vitu kwa miujiza tu inayogusa mwili. Hiyo miujiza inaweza toka kwa Yesu ama kwa Ibilisi. Sasa maadam shida ya mhusika ni kupata muujiza tu (kupona magonjwa, kutajirika, ….) yeye hajali na mahala hizo nguvu zinatoka. Zitokapo kwa Ibilisi anadaka, zitokapo kwa Yesu anadaka.
  Lakini ikiwa ni wokovu au upako takatifu, hakuna kujiuliza mengi. Jina la Yesu tu kuipitia imani ya kwamba ni Mwana wa Mungu, aliyetufilia na akafufuka, sasa yupo mbinguni kuume kwa Baba. Hapa sasa ndipo Ndugu Dauban anasisitiza. Anyway ukishikilia kila kona yaani wokovu na miujiza utaona kama Ndugu Sungura hakukosea hio kona.
  Somo gani sasa kwa wakristo waliyookoka? Si vizuri kwa Mukristo kushabikia sana miujiza kwani Ibilisi naye anayo. Inampasa mulokole adumu katika maombi ili ahakikishe amepata muujiza utokao kwa Yesu Kristo. Sasa RM akituongoza kutumia mafuta, wala maji iliyovuviwa na upako wa Yesu, hapo hatuna ubishi kwani imetupasa kuacha mapenzi ya Yesu ndiyo yafanyike. Pia hatutamshurtisha kuitumia formula fulani. Ikiwa ni kwa kutaja Jina lake tu tatafanya, ikiwa tuna uhakika RM ametuambia kuyatumia maji au mafuta tutatumia. Kazi yetu siyo ya kumshurtisha Yesu bali kumtii.

  Mbarikiwe!

 22. sungura
  usome na hii pia,JOHN 1:12 yet to all who did recieve him,to those who believed in his name,he gave the RIGHT{HAKI} to become children of GOD.NIV.wana wa mungu ndo wanao haki ya kutumia hilo jina,na tunapata hiyo haki kwa kumpokea YESU KRISTO na kuamini JINA LAKE.na tena JOHN 14:23 mkinipenda mtashika amri zangu au{neno langu} na mmoja wa amri zake ni kuomba chochote kwa jina lake{YESU KRISTO} tena wakolosia 3:17 na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo fanyeni yote kwa JINA LA BWANA YESU mkimshukuru MUNGU BABA kwa yeye.

  Wote wanaotumia vitu vingine badala ya jina la Yesu kristo,hawana imani kwa hilo jina na sio wana wa Mungu na hawampendi yesu ndo sababu wamekataa kushika amri ya kuomba kila kitu kwa jina lake.tena matendo ya mitume 5:15 na 19:12.wagonjwa waliwekwa kando ya barabara,kivuli cha petro ikiwaguza wanapona,na watu walichukuwa nguo au leso zilizotoka mwilini mwa paulo,tunaona kuwa mitume hawakuambia watu watumie hivi vitu bali watu wenyewe waliamua kuvitumia.nasi tusiwaambie watu wavitumie.

 23. sungura
  kidogo unachanganya mambo,ebu nikupe mfano huu,ulikuwa ndani ya gari ya amri jeshe,akiwa na silaha zake zakivita,akatokea adui na wewe ukapiga kelele na kusema {adui yule!!!!!} naye akampiga risasi.ninachosema ni hii,kwa sababu ulikuwa pamoja na yule amri jeshi,ulipata haki na nguvu ya kumshautia yule adui na yeye kama mwenye mamlaka akampiga risasi akafa.sasa katika mambo ya kiroho,yesu haonekani,ukiliitia jina lake kwa imani na atende jambo,watu wataona ni wewe ndo umetenda hayo na wewe pia bila kujua utafikiria umetenda wewe kwa mamlaka uliopewa bila kujua kuwa yesu mwenye mamlaka yuko ndani yako na ndiye ametenda si wewe.soma JOHN 14:23 mtu akinipenda atashika amri zangu au neno langu—nasi tutakuja kwake na kukaa neye. JOHN 14:13-14,chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya,unaona kweli YESU akiwa ndani yetu,sisi hutamka na yeye hufanya,sasa wasiomini wenye kujivuna husema kuwa wanao mamlaka ya kutenda jambo,sisi tuna haki ya kuliitia jina la YESU kwa imani naye hutenda.

 24. Daubani,

  Huwa nina shida moja,kwamba hunisumbua sana kujadili na mtu ambaye wigo wake wa kufuatilia mambo yenye kumpa haki ya kusema anachokisimamia.

  Mamlaka ni haki ya kisheria ya kutumia nguvu uliyopewa/uliyonayo. Ukiwa na nguvu bila mamlaka huwezi kuitumia hiyo nguvu bila sheria/kanuni kukukatalia.

  Nilisema kuwa tumepewa mamlaka ya kutumia jina la Yesu na mwenye jina, lakini naona umenikosoa ukasema kuwa sisi tulichopewa ni nguvu na haki tu. Sijui hiyo umeitoa wapi.

  Mimi ya kwangu naitoa hapa; Luk 10:19 – I have given you authority to trample on snakes and scorpions and to overcome all the power of the enemy; nothing will harm you.-NIV

  Hawezi kutupa mamlaka bila kutupa nguvu ya kutekeleza utendaji wa hiyo mamlaka anayotupa. Na hapohapo bado nguvu hiyo na mamlaka ni vya kwake.

  Wanaoambiwa kuwa watapokea nguvu kutoka kwa Roho mt. ni hao ambao tayari walishapewa mamlaka ya kuwa na hiyo nguvu na kuitumia.
  Huwezi ukaitumia hiyo nguvu bila kuwa umepata kwanza mamlaka.

  Halafu usileta neno unaloliita la kufunuliwa ambalo halina ithibati katika neno la Mungu. kwa sehemu kubwa level ya jambo tunalojadili hapa ni ya kimaandiko zaidi kuliko kiufunuo. Nina haki ya kutoamini ufunuo wako kama hauna ithibati katika neno la Mungu lililoandikwa.

  Kumbuka tunajadili suala la kuhoji mapepo, na nimetaka ushahidi wa kimaandiko wa kwa nini mnasema hatutakiwi kuyahoji!

 25. sungura
  mimi nilikuelewa vizuri sana,ndo sababu nilitumia neno nguvu badala ya mamlaka,na bado nitakuelezea zaidi kama utaniruhusu.mtu anapo mwamini YESU KRISTO anajazwa roho mtakatifu,kwa huyo roho tunakuwa na{HAKI} tena roho mtakatifu hutupa NGUVU{POWER au UWEZO} wa kutumia hilo jina{sio MAMLAKA} na hilo jina lazima tuitamke kwa imani ndo tupate ushindi.wana wa sekewa hawakuwa na ROHO MTAKATIFU.kumaanisha hawakuwa na HAKI wala NGUVU ya kuweza kutoa mapepo.ndio sababu waliuzwa,paulo twamjua na yesu twamjua na nyinyi ni akina nani?.mamlaka ni yake anayetawala yaani YESU KRISTO.sisi twapata HAKI na NGUVU kutoka kwake aliye na mamlaka.usiseme ninakuhubiria ninatoa hoja yangu na vile nilivyo funuliwa,nimekuelezea kwa machache kama hujaamini basi lete yako,ninaisubiri kwa hamu ndugu sunguru.

 26. Dauban,

  Usitumie muda nwingi kunihubiria mimi, tumia muda huo kuchambua mada.

  Sijakwambieni kuwa hamjui mnachokiabudu, nilisema hamjui mnachokisema.

  Sikusema habari ya nguvu ya mwenye jina, nimesema Mamlaka ya mwenye jina au mamlaka ya jina kuwa ndani ya mtu.

  Kuna tofauti kati ya nguvu na mamlaka. Upako ni nguvu, mamlaka siyo upako.

  Na ukidhani natumia elimu ya dunia kusema ninachosema, hata hapo sijui kama unajua unachosema.

  Labda shangazwa na watu kuuza hivyo vitu,lakini si vitu hivyo kutumika. Siyo mara ya kwanza vitu kutumika, ukiona vinafanya kazi ujue vina uwezo wa jina la Yesu tayari kutoka kwa mtu viliyetoka kwake.

  Lakini pia kama unadhani nguvu ya mwenye jina iko ndani ya jina bila kuwa ndani ya aliyelibeba hilo jina, kawaulize wana Skewa walipojaribu kutumia nguvu iliyondani ya jina la Yesu. Walidhani kama wewe unavyodhani tu kuwa nguvu iko ndani ya jina la mwenye jina ( Yesu) na haiwi ndani ya mwenye kulitamka hilo jina. Nafikiri unajua kilichowapata!

  Karibu tujadili,

 27. wana wa Mungu songeni mbele.
  Tumieni hekima ya Yesu ktk kila jambo
  ili msiingie ktk mitego ya wana wa giza.
  ROHO MTAKATIFU ameshatutia ktk Kweli ya mambo yote.1 Yohana 2:27.

  Tusisumbuke na ulimwengu wa mwili.
  majibu halisi yako ktk ulimwengu wa roho.Cha msingi ni kuishi maisha ya kujitakasa ili macho na masikio ya rohoni yawe wazi usiku na mchana.

  Upumbavu wao unazidi kuwavua nguo
  mchana kweupe.Yesu anarejesha ufahamu wa wateule wake.SOMA 2 TIMOTHEO 3:9″…LAKINI HAWATAENDELEA SANA, MAANA UPUMBAVU WAO UTAKUWA DHAHIRI KWA WATU WOTE…..”

 28. Sungura,
  usidanganyike,tunajua tunachosema na tunajua MUNGU tunae mwabudu. Nimekubali kuacha kila kitu kinacho husiana na shetani,hata kama chaonekana kizuri nitakiacha ili nibaki na KRISTO YESU MWOKOZI WANGU. Mtu habebi nguvu za mwenye jina ila NGUVU ZA MWENYE JINA IKO NDANI YA JINA LAKE,na sisi tumeambiwa tulitumie jina lake YESU KRISTO kwa imani. Mapepo huhangaika mtu wa Mungu anapopita kwa sababu YA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU aliye ndani ya huyu mtu,si kwa sababu huyo mtu amebebu nguvu ya hilo jina.

  Nakuomba ndugu yangu sungura usome Bibilia na umuombe MUNGU akupe ufunuo na kweli wa neno lake,ukijidhania kuwa unajua kitu ndo bado haujajua,ukijiona mwenye hekima,mbele yeka MUNGU wewe ndiye mjinga. Kwaivyo muombe MUNGU akupe hekima itokayo juu ili upate kumjua vyema na upate wokovu wa kweli,sababu naona bado uko mbali sana ijapokuwa unajitahidi sana,ujue huwezi kumjua MUNGU kwa akili ya masomo yako ya kidunia.

  MUNGU AWABARIKI wote wanao jua kweli na kuifuata.

 29. Ndugu Dauban na shujaa wa taifa(japo silipendi hilo jina maana si jina halisi).

  Kwa sehemu kubwa hamjui mnachokiongea, hasa wewe Dauban.
  Hatuwezi kufanya jambo fulani ambalo ni sahihi ati kwa sababu tu shetani ameliiga. Kama ni hivyo tutaacha mambo mengi sana mazuri.

  Unapoona sentensi “kwa jina la” ujue kinachoongelewa ni mamlaka. Ni sawa na kusema kwa mamlaka ya. Sasa mamlaka haikai kwenye kutamka tu, bali inakaa ndani ya aliyeibeba. Ndio maana unaweza ukapita mahali mapepo yakalipuka bila hata wewe kutamka chochote.
  Na ukitamka jina bila kuwa na mamlaka ya mwenye jina ndani yako ni kutafuta balaa.

  Bless

 30. ndugu Dauban

  Barikiwa sana.INPUT zako zimehitimisha mada.Pamoja na kwamba
  wote tunatumia Bibilia lakini wajumbe
  wa shetani WAMEJIVUA NGUO katika
  matumizi ya hivi vitu.Wanafanya biashara haramu mchana kweupe.

  Wana wa Mungu tutumie jina la Yesu.
  Tukiweka imani zetu kwenye mafuta yenye upako wa mapepo tutazidi kuchukuliwa mateka.Tusikubali kuiga
  MAARIFA YA MASHETANI.

 31. Sisi tulio na ROHO WA YESU nivyema tuwe tofauti na wale walio na roho ya mashetani,yaani, kwa matendo yetu,kuomba kwetu na katika utumiaji ya majina au hivyo vitu lazima tuwe na tofauti. Kwahivyo ushauri wangu ni huu,kwa sababu shetani ameiga na kugeuza vitu vizuri vikaonekana kuwa vibaya,sisi tulio na ROHO WA YESU ni bora tumwachie hizo ambazo amechafua na tushikilie jina la YESU KRISTO ambalo hawezi kulichafua,na tulitumie kila mahali,kila wakati na kwa kila jambo tunalotenda iwe ni kwa tendo au kwa neno tufanye yote kwa JINA LA BWANA YESU tukimshukuru MUNGU BABA KWA YEYE, kama isemavyo maandiko pia katika waraka wa paulo kwa wakolosai 3:17.

 32. Cha msingi hapa sio utumiaji wa hivyo
  vitu au nani anatumiwa na Mungu kutoa
  hivyo vitu ili kuponya watu.

  cha msingi ni kujua uhalisia wa haya mambo katika ulimwengu wa roho.Maandiko yanadhibitisha kwamba mafuta, nguo na leso zilitumika kuponya kwa utukufu wa jina la Yesu.Leo wajumbe wa shetani wanatumia sana
  vitu hivi kwa utukufu wa shetani.Pasipo
  ufahamu na macho ya rohoni ni vigumu
  kuyatenganisha haya.ISAYA 42:18-20

  ROHO MTAKATIFU ndiye anayetafsiri mambo yote tunayoyaona ktk ulimwengu wa roho.Ni kazi kwetu kushirikiana na Roho wa Kristo.1 Yohana 2:27

  Wajumbe wa shetani wanatumia maji, mafuta, sabuni , nguo nk KUSAMBAZA
  MAPEPO.Mjumbe wa shetani anapoyaombea maji au nguo zako anawekeza mapepo ndani yako.Wanachokifanya kuvuta imani za wengi
  ili watu wengi zaidi WAENDELEE KUTOA
  SADAKA KWA SHETANI.

  Kama macho na masikio yako ya rohoni
  HAYAJAZIBWA AU KUBATILISHWA utajua uhalisia wa madhabahu unayoabudu na kama maji na mafuta
  yanatumika kwa utukufu wa Yesu utajua tu.mashetani huwa wanasimamia NENO
  kwa hila na werevu wa ibilisi.Na ndiyo maana HAWAWEZI KUJIFANYA WANASIMAMIA NENO MUDA WOTE.Ni lazima watumie vitu kusambaza mapepo yao.

  TUWE MAKINI ROHONI kwa sababu mengi yanayofanyika mwilini siyo Halisi.
  Mengi yanafanyika ili KUONGEZA MATEKA NA WACHACHE WANAOMWAMBIA MUNGU AWATOE KATIKA UTEKA.ISAYA 42:22.

 33. mengi togwa,
  tunakubali kuwa wakati wa mitume,leso na nguo zilizotoka mwilini mwa mitume zilitumika,lakini hawakuziuza wala hawakutoa amri hizo vitu vitumike,hao watu walikuwa wanavitumia kwa hiari yao,lakini wakati huu hizo vitu vyauzwa tena kwa faida kubwa sana,na maagizo tuliyo nayo sisi ni kutumia jina lake Bwana Yesu pekee,

 34. Kwa sababu watu wa dini wengi mnapenda maandiko kuliko uweza wa Roho Mtakatifu nami naomba niwaongezee maandiko! “Wakatoa pepo wengi,wakawapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa,wakawapoza”MARKO 6:13 Na pia “hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake,magonjwa yao yakawaondokea,pepo wachafu wakawatoka”Matendo ya mitume 19:12,Tuache ufarisayo ulimwengu wa roho ni zaidi ya yale unayofundishwa na dini yako,huu si wakati wa dini ni wakati wa Roho Mtakatifu kuliatamia kanisa kwa kuwa mambo ya rohoni hutambulikana kwa namna ya rohoni,MWAPOTEA KWA VILE HAMYAJUI MAANDIKO WALA UWEZA WA MUNGU.MATHAYO 22:29

 35. Gladys nina swali, hivi kwa mfano hivyo vitu wanavyogawa au kuuza kabla hawajagawa au kuuza wanaviombea kwa jina la Yesu halafu ndo wanawapa watu, kwani hapo kutakua na shida yoyote??

 36. Kinachotokea hapa ni imani ya mtu katika kile anachokiamini. Vitu vinavyotumika kama vinatumika vikitawaliwa na neno la Mungu mimi naona hakuna ubaya. Mtu ashikapo kitu na kuomba kwa jina la Mungu ni ishara tu ya utukufu na uchaji kwa Mungu wake.

 37. Sio sahihi.
  Kutumainia kitu chochote nje ya jina la Yesu ni sawa na kuitumainia tunguri ya kwa mganga wa kienyeji.
  Tuliookoka tumepewa jina moja tu, Yesu Kristo (wa Nazareti) ambapo kila aliitiaye jina hilo;
  1. Ataokolewa ( from any kind of disaster) Matendo2:21 na Rumi 10:13
  2. Ataponywa ( from any kind of disease or situation) Yoeli 2:32
  So majina mengine being it maji ya upako, mafuta ya mzeituni, vitambaa etc ni ubatili mtupu na kujilisha upepo.

 38. BWANA WETU YESU KRISTO alituagiza tuombe kwa jina lake,na tena mtume Paulo katika waraka wake kwa wakolosai 3:17 anasema,na kila mfanyalo kwa tendo au kwa neno fanyeni yote kwa jina la Bwana Yesu mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye,maana yake ni kuwa JINA LA BWANA YESU litumike kila mahali na kila wakati.wanaotumia vitu vingine au majina mengine wako nje ya maagizo ya BWANA WATU YESU KRISTO.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s