Nahitaji Maombi na Ushauri

Questions and clear strategy and solutions for business leadership with a straight path to success choosing the right strategic path with yellow traffic signs cutting through a maze of tangled roads and highways.

Bwana Yesu asifiwe!

Haja ya moyo wangu kwa Wakristo wenzangu hapa Strictly Gospel ni kuomba ushauri pamoja na kuhitaji muungane nami katika kuliombea suala hili.

Mimi ni kijana nimeokoka  na ni mzaliwa wa kwanza kwenye familia yetu na mzaliwa wa kwanza kiroho kwa sababu Mungu alianza kuniokoa mimi ijapokuwa nina ndugu zangu wameokoka lakini bado hawajapokea neema yakuweza kusimama na Kristo.

Lililonileta ni suala hili kwamba nipo kwenye vita na sijajua nifanye nini kwenye jambo hili lililonipata mwaka huu. 

Nyumbani kwetu tuna mdogo wetu wa kike ambaye ni mtoto wa mwisho. Tatizo lililojitokeza nilianza kuota ndoto juu ya mama yangu mzazi. Nilikuwa naota nawaona watu wanamuita majina mabaya sana. Nikiota hivyo mimi nakuwa nabishana nao ndotoni, nikiwakemea kuhusu maneno yao, lakini wao walikuwa wananishangaa sana.

Hapo mwanzo sikuwa naelewa nini kinaendelea. Lakini wakati nakaribia kurudi likizo nyumbani, kwani nilikuwa nipo muhula wa kwanza mwaka wa tatu namalizia masomo yangu ya shahada ya kwanza katika moja ya vyuo vikuu Tanzania, nilikuwa nasikia kuna wimbo wa injili wenye maudhui ya kumsihi Mungu anipe nguvu nisikate tamaa. Hapo sikuelewa kwa nini wimbo huu ulikuwa unakuja hasa asubuhi tu pale ninapoamka, unakuja kichwani. 

Ndipo niliporudi nyumbani nikakuta habari mbaya sana ambazo sikuzitarajia maishani. Nilianza sikia kwa watu baki ya kuwa mama yangu anamkuwadia (anamtafutia wanaume) mdogo wangu ambaye alikuwa ana umri wa miaka 17 kwa wakati huo. Yeye ni wa kike na wa mwisho kwa wanaume. Sababu ya mama kumkuwadia ni eti ili apate pesa ya kulipa madeni!

Kwa kweli kama mtoto mkubwa niliposikia habari zile nikaamua kuongea na mdogo wangu, mimi kama kama kaka, na kutumia mbinu za kisaikolojia kumhoji. Baada ya kumhoji dipo akaniambia habari zote ambazo zilinifanya nikaunganisha ndoto ile niliyoiota siku za nyuma na ule wimbo uliokuwa unanielekeza nimuombe Mungu anipe nguvu nisikatee tamaa. Pamoja na hayo nilisikia na mengine mengi sana kiasi kwamba yalinihuzunisha na yaliniumiza na kunifanya niingiwe na uchovu wa kiroho ambao umenigharimu sana roho yangu.

Mdogo wangu huyo sasa kawa mjeuri sana. Ameshatoroka nyumbani kama mara nne; tunamtafuta; tunamrudisha.

Huku napo baba yangu maisha yake ndiyo siwezi elezea maana hayampi Mungu utukufu. Kwa kifupi ni kwamba roho za uzinzi na uasherati zimeivamia nyumba yetu. Wazazi wangu sasa wametengana na baba yangu anataka kuoa mwanamke, tuseme msichana, ambaye kwa kukadiria nimempita umri au tumelingana. Vita vimepamba moto kama asingekuwa Mungu, chuoni ningefeli kwasababu kuna wakati nilikuwa nashindwa kabisa hata kusoma!

Sasa nalileta kwenu, ndugu zangu katika Kristo, mnishauri hapa nifanya nini. Sambamba na ushauri huo ninaomba mniombee ili Mungu aiponye familia yangu.

By C.P

Advertisements

7 thoughts on “Nahitaji Maombi na Ushauri

 1. Mungu mshindaji atusaidiaye kushinda na zaid ya kushinda, asimame upande wako kuitetea familia yenu.
  Lakini kubwa zaidi endelea kusimama katika neno msihi Mungu arejeze ule upendo wa mwanzo kwa wazazi wako.
  Funga, Omba, endelea kumlilia Mungu wa Isaka na Yakobo yeye sio dhalimu atatenda.
  Huenda ikawa ndio kipimo cha Imani yako kumbe unapopita Mungu anajitukuza, sikilia Imani kaka na Mungu ataiponya familia yenu.
  Mungu akubariki

 2. Waefeso 6:10-12 yasema, “Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Biblia inaeleza vizuri sana sitaki kuongeza neno juu ya hili, Simama katika maombi yote yanawezekana. Mwachie Mungu na utue mzigo huu kwake.

 3. Nashauri uende katika kanisa la Mkombozi Michungwani Mwanza kwa Nabii Malisa ili ukafunguliwe pamoja na familia yako, hizo ni roho zinazofuatilia familia,makanisa ya mkombozi yako Dar,Arusha,Kahama,Mwanza,Mbeya,Geita nk Mungu atakuponya katika kweli na Haki mama Joshua,

 4. Usikate tamaa, kaa katika maombi na Mungu atakupa suluhisho.Nakuombea ushindi katika Kristo Yesu!

 5. Hongera kwa ushindi ewe shujaa.
  Ni wakati wa kusimama kwa miguu yako ya kiroho.Mungu anataka kujitwalia utukufu katikati ya miba na
  nyoka.Usitishwe na kinachoendelea katika macho ya damu na nyama.Tafuta kulijua kusudi la Bwana katikati ya changamoto mnazopitia.Tafuta kujua mawazo na njia ambazo Mungu amewakusudia kupita katika haya yanayoendelea.ISAYA 55:8-9.

  simama katika nafasi yako kama Lango
  ili ubadilishe hiyo hali kupitia ulimwengu
  wa roho.Omba rehema kwa ajili yako
  na familia nzima alafu Roho Mtakatifu
  atakueza hatua inayofuata.Yeremia 14:7-9.

  Nakuona baada ya muda ukitokwa na
  machozi ya furaha.Ni urejesho kwa wale walio kubali kulipa gharama.ISAYA
  14:3.Roho Mtakatifu akupe kupambanua
  kati ya ushauri ulio hai na ushauri ulio kufa.Naungana kiroho na mchangiaji wa kwanza.Dhahabu inapopitishwa kwenye
  moto ndipo neema ya uvumilivu na hekima inapopambana na roho ya uongo
  na kukata tamaa.

 6. pole sana kilakitu kina mlango wakutokea hayo yataisha na mji utatulia kwajina la Yesu. Ninachokiona hapa kwanza uwezi ukapandishwa daraja bila kozi hiyo ni kozi yako ya kukupandisha daraja kiroho Mungu anataka akutumie iyo ndiyo kozi ya kwanza. wewe simamia huo wimbo uliokuwa unakuja kichwani ndiyo msaada wako mkuu. 1 wakorintho 10:12-13. 12 Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke. 13 Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s