Kanisa litanyakuliwa Wakati Gani?

Bioshock_rapture-wide

Bwana Yesu asifiwe!

Naomba kuuliza kwamba Kanisa litanyakuliwa KABLA ya kuanza kwa Utawala wa Mpiga Kristo au KATIKA kipindi cha Utawala wa Mpinga Kristo?

John Salum

Advertisements

34 thoughts on “Kanisa litanyakuliwa Wakati Gani?

 1. Hakuna unyakuliwaji wa kanisa maaana Kristo atarudi na kukuta kufufua wafu nao wale walio hai watasubiri wafu wafufuliwe na kuungana na Kristo mawinguni kama anavyoelezea mtume Paulo,. Swali kama wakinyakuliwa Kristo atakaporudi atawafufuaje au watamlaki vipi wakati walishakuwa naye mbinguni, tusome maandiko kwa umakini!

 2. Bwana YESU asifiwe. Kanisa litanyakuliwa mda wowote ule hata sasa na kabla ya dhiki kuu
  Bali kuja kwa YESU Mara ya pili ni baada ya dhiki kuu na kwaajiri ya ukumbozi kwa Yakobo(Israel).
  Hvyo basi chance kwa wamataifa ndo hii hapa tu ya unyakuo na pia YESU kuja Mara ya pili atakija na utisho wanamna ya kutisha mno haijawahi tokea na kwa ajiri ya vita sio mwaliko, atakuwa BWANA WA VITA. Pia atasimama juu ya mlima wa sayuni ambao hupo hata leo Israel nao utapasuka katikati.

  Wapendwa napenda kusema Unyakuo na Kuja YESU mara ya pili ni tofauti kwa wale inayowachanganya ningeomba msome

  ZEKARIA 12,13,14 kwakweli hapo ndo mtaelewa utafuti mkubwa na MUNGU awabariki.

 3. Anapokwambia Israeli wote wataokoka ni wana wa ile ahadi si kila mtu muisraeli kwa utaifa la sasa.

  MABAKI TU YA ISRAELI WATAOKOKA
  Warumi 9:27
  “Hesabu ya wana wa Israeli ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa.”

  Warumi 9:6
  “Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote waisraeli walio wa uzao wa Israeli.”

 4. Wapendwa, mbarikiwe sana na Bwana.
  Nimefuatilia mada hii kwa makini sana na kuona jinsi baadhi yetu tunavyoelewa juu ya kunyakuliwa kwa kanisa. Sina muda mzuri sana kwa sasa wa kuweza kutoa mchango wangu juu ya hili. Ninayo hamu sana ya kuchangia nitafanya hivyo nitakapopata wasaa mzuri. Somo hili lina maelezo mengi ambayo yakifuatiliwa kwa msaada wa araoho Mtakatifu kila mmoja ataweza kujua kanisa litanyakuliwa wakati gani.

  Kwa dokezo au kwa kifupi tu bila maandiko ni kwamba; kanisa litanyakuliwa kabla ya dhiki kuu. Dhiki kuu itawapiga wale ambao hawakutaka kumwamini Yesu. Mfano wa kujua hili ni kwamba, kwanza tunatakiwa kujua kuwa Mungu hana upendeleo na kama hana upendeleo, hawezi kuleta dhiki kuu hata kwa walio wake yaani watakatifu; eti washiriki pamoja na wenye dhambi!…. La hasha, Mungu hayuko hivyo. Unaweza sasa ukajiuliza, kwa nini hata sasa tunaonekana tupo katika dhiki kwa kukosa hiki au kile ikiwa ni pamoja na wakati mwingine kupoteza yale ambayo tunayapenda. Yanatutokea hayo ili kujaribiwa katika imani yetu, Mungu anataka ajue kwamba kweli tunamwamini au tupo kwa sababu ya yale yaliyomema kwetu? ndiyo maana hata ayubu alijaribiwa.

  Lakini dhiki kuu, si kwa ajili ya kujaribiwa, hiyo itakuwa ni adhabu kwa ajili ya waliomkataa Yesu.

  Tunaona nyakati za GHARIKA Nuhu na jamaa yake waliondolewa kwanza ndipo gharika ikaja kama adhabu kwa waliokuwa kunyume na Mungu. Wakati wa Sodoma na Gomora, Lutu na familia yake waliondolewa kwanza ndipo miji ile ikachomwa moto kama adhabu kwa waliokuwa kinyume na Mungu.

  Mungu asiyebadilika atafanya vivyo hivyo hata nyakati za unyakuo, hatawaadhibu waliofuata maagizo yake…Ni akina nani basi wanaelezewa kuwa siku hizo sisingalifupizwa asingeliokoka hata mmoja?

  Katika [Warumi 11:25-27 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao.] Ni kwamba; kuja kwa Yesu hasa ilikuwa ni kwa ajili ya wana wa Israel, hao ndio pia wanaoitwa wateule. Mungu asiye na upendeleo aliwafanya wana wa Israel wasimwamini Masihi yaani Yesu Kristo. Ili kuja kwake Masihi kusiwe bure aliwafanya mataifa [mimi nawewe] wapate neema ya wokovu. Hata hivyo pamoja na kutomwamini Yesu kwa wana wa Israel, sisi baada ya kunyakuliwa nao watapata neema na ufunuo na kuona kuwa kumbe yule waliyemkataa alikuwa ndiye Masihi waliyejua habari zake katika maandiko; hivyo nao watamlilia Mungu na wataokolewa kwa mujibu wa maandiko Warumi 11:25… Mambo haya pasipo roho wa Mungu ni vigumu sana kuyaelewa na matokeo yake tutajikuta tunatumia tu udhehebu yaani jinzi tulivyofundishwa na walimu wetu wa mwanzo.

  Kutokana na hayo niliyoyatoa kidogo tu, tunaweza kuanza kujua kwa sehemu ni kwa nini maandiko mengine yanasema mfano: [Mathayo 24:22-24, Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya WATEULE zitafupizwa siku hizo. 23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio WATEULE].

  Kumbe wateule wanaotajwa hapa ni wana wa Israel japo hawajamwamini Yesu mpaka wakati huu yeye aliyekuja nyakati zile. Hao ndio watakaookolewa kwa mateso yanayotajwa katika maandiko mengi tunayoyaona kama tatanishi. Kwa sehemu ugumu umewapata Israel mpaka utimilifu wa mataifa utakapowasili, kuwasili wa utimilifu wa mataifa ni ule unyakuo, watakapoona mataifa ambao siyo waisraeli lakini walimwamini Yesu wamenyakuliwa ndipo nao watasema; kumbe yule tuliyemkataa alikuwa ndiye. Ndipo hapo sasa wataanza kufurukuta upya ili wapate neema ya Mungu ili atawasamehe na kuwaokoa. Wataokolewa kwa njia ya dhiki ya nyakati hizo wakati sisi tumenyakuliwa. Lakini hata sasa sisi tulio katika Kristo tupo katika dhiki kwa kubezwa imani yetu katika Kristo lakini si ile dhiki kama ya wakati huo.

  Nilitaka niandike kidogo sana nimejikuta nimeandika yote haya niliyoyaandika, hata hivyo nadhani kwa muhtasari huu nimetoa mwanga kitogo ni kwa nini watu wengi wanachanganya mambo haya. Hata hivyo kama nilivyoahidi ninaomba tu neema ya Mungu nije nipate nafasi nitoe ufafanuzi zaidi kwa njia ya maandiko mengi, zaidi sana yanayoleta utata kama tulivyoona.

  Bwana awabariki wote na wote zidini kuishindania imani waliyokabidiwa watakatifu mara moja tu, Yuda 1:3

 5. MILE,
  Mimi nilikugundua mwanzoni kuwa wewe ni Miongoni mwa WALE wasemao, HAKUNA KUOKOKA Duniani.
  Unaona ulivyoonesha rangi zako kwa Maelezo ya MWISHO ya “Atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokoka”?
  Huu mstari , WASABATO wanapenda kuutumia kama uthibitisho wa kupitia kwenye Dhiki kuu.
  Usituletee Tafsiri POTOFU za Kidhehebu.
  Kama wewe ni MSABATO endelea kushikilia MAPOKEO ya wanadamu na Usitulete “Hybrid gospel”.
  UMEKWEPA kujibu maswali niliyokuuliza kwa sababu umezoea KUKARIRI MAFUNGU.
  Hapa SG ni INJILI HALISI na THABITI hivyo usituletee injili mfu.
  Wewe na dhehebu lako ndio mtakaopitia Dhiki kuu,wala usijali rafiki.

 6. Muuliza swali angejiridhisha muda mrefu kama kila mtu angemweleza Biblia inasemaje? Juu ya swali lake.

  Kwendana na swali la Muulizaji?mtoa mada anasema?

  Naomba kuuliza kwamba Kanisa litanyakuliwa KABLA ya kuanza kwa Utawala wa Mpinga Kristo au KATIKA kipindi cha Utawala wa Mpinga Kristo?

  2 Wathesalonike 2:1-3
  Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

  Ni kazi mmoja tu kufunuliwa Mpinga Kristo,anayetenda kazi.

  Paulo anatuambia habari ya kukusanyika mbele za Bwana mpaka yule muasi amefunuliwa,

  lakini biblia inatuambia:
  “atakayevumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka.

 7. MILE,
  usijifanye wewe ni wa ‘kiroho sana’ wala usijilinganishe na Bwana Yesu.Hapa SG si mahali pa ‘kupigia jaramba’ au mahali pa kuwanga’ng’aniza watu waukubali mtazamo wako wa UONGO..
  MAANDIKO uliyonukuu yapo Sahihi kabisa ila tafsiri yako ni POTOFU.
  Umekataa kujibu maswali halafu unajihesabia haki bure.
  JIBU KWANZA maswali uliyoulizwa kama Sijakuonesha maandiko yanayothibitisha kuwa Kanisa la Mungu aliye Hai(BIBI ARUSI WA KRISTO) halipitii kwenye Dhiki kuu.
  Hapa SG kuna kauli mbiu isemayo “INJILI HALISI NA THABITI” hivyo usiwe mjuaji kuliko NENO LA MUNGU.
  Hayo mafundisho yako ni ya “Wale” wasemao HAKUNA KUOKA DUNIANI.
  Hapa si mahali pa mzaha wala usifikiri wewe Unafahamu kila kitu.
  Hebu Jitathmini kwanza kabla kuongea.

 8. MILE,
  usijifanye wewe ni wa ‘kiroho sana’ wala usijilinganishe na Bwana Yesu.Hapa SG si mahali pa ‘kupigia jaramba’ au mahali pa kuwanga’ng’aniza watu waukubali mtazamo wako wa UONGO..
  MAANDIKO uliyonukuu yapo Sahihi kabisa ila tafsiri yako ni POTOFU.
  Umekataa kujibu maswali halafu unajihesabia haki bure.
  JIBU KWANZA maswali uliyoulizwa kama Sijakuonesha maandiko yanayothibitisha kuwa Kanisa la Mungu aliye Hai(BIBI ARUSI WA KRISTO) halipitii kwenye Dhiki kuu.
  Hapa SG kuna kauli mbiu isemayo “INJILI HALISI NA THABITI” hivyo usiwe mjuaji kuliko NENO LA MUNGU.
  Hayo mafundisho yako ni ya “Wale” wasemao HAKUNA KUOKA DUNIANI.
  Hapa si mahali pa mzaha wala usifikiri wewe Unafahamu kila kitu.

 9. MASHAHIDI 2 WAMEKUJA KUSEMA

  “Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba,ushuhuda wa watu wawili ni kweli.” YOHANA 8:17
  “..Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa” 1 Wakorintho 13:

  Hivyo Nawaleta kwenu Marko na Mathayo mashahidi wawili washuhudie kuwa kanisa litapitia ile dhiki kuu.

  “Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litaatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake. Na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wan chi hata upande wa mwisho wa mbingu.” Marko 13:24-27

  “Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”
  Mathayo 24:29-31

  Marko na Mathayo hawajapinga,ila wakristo wanapingana.

  mashahidi wote 2 wanasema;
  1.baada ya dhiki
  2.jua litatiwagiza
  3.mwezi hautatoa mwanga
  4.mbingu zatikisika
  5.mwana wa adamu ataonekana
  6.wateule watakusanywa

 10. Wayahudi walikuwa na tabia zifuatazo

  1.Kumshambulia mtoaji wa maneno,badala kulishambulia neno alilolitoa,ndio maana waliishia kumuua Yesu.
  2. Hawakuwa na hoja ya kumjibu Yesu kwa kutumia andiko.
  3.Walilazimika kutumia hasira kwa kuwa walishindwa kutoa wanayoelewa kwa watu kuthibitisha Yesu ni mwongo.
  4.Walimsubiri Yesu aongelee jambo ndio waseme…wakati wao walikaa kimya.
  5.Walijaa mambo yaliojaa mapokeo ya wanadamu ndio maana hawakutoa hoja zao bali kumshitaki mtu.
  6.Hawakuchagua maneno ya kuongea kuonyesha watu kuwa walitahiri midomo yao.
  7.hawakuonyesha kutahiri masikio yao,kwani hawakusikia wala kukubali yale ambayo wao hawakuamini hata kama yaliandikwa wazi katika maandiko.

  YESU NI NENO,NENO NI YESU….
  Yuda alimbusu Yesu aonekana na watu anamjali Yesu,ndivyo wakrsto wengi hulibusu neno kama Judas huku wakilisaliti.

  A)Nilijifunza kale kuwa mtu akikosa hoja ya kibiblia kukujibu, hukushambulia
  B)Mtu akikosa hoja hukuhamisha kwenye mada kuu kwa kukukushambulia wewe badala ya kuishambulia hoja uliyoitoa, ili either usichangie au uwe bored,au ukasirike.

  Hata mtu akasema atatoa fedha na dhahabu, hakuna atakae toa neno lililoandikwa watakatifu hawatapitia dhiki ile kuu.

  Karibuni mtoe hilo neno ndugu..mliotahiriwa kwa neno midomo yenu,mioyo yenu na masikio.

  Sisi waongo tutanyamaza mkitoa hilo neno.

  Karibuni ndugu msimamao juu ya mwamba mtufundishe waongo/yamkini tumesimama juu ya mchanga/mapokea ya wanadamu

 11. MILE,
  Hakika nimegundua UFAHAMU wako ni mdogo sana.
  Ndio maana nilikuuliza swali “Unaijua dhiki kuu?”
  Swali hilo hukulijibu.
  Pia nilikuuliza”Bwana Yesu Kristo alikuja duniani kufanya nini?”
  Hilo swali nalo kama kawaida yako hukulijibu.
  Hivyo,inaonekana wazi kuwa UMEVAMIA hapa SG na Kuleta MATANGO MWITU “mafundisho ya mashetani” ukifikiri utaweza kuwadanganya WAKRISTO. Bila shaka, kwa jinsi ulivyo na moyo mgumu hata unadiriki kutoa MAANDIKO yasiyo na Uhusiano na DHIKI KUU hata upewe MAANDIKO vipi huwezi kusaidika kwani umeshalishwa sumu.
  Umepoteza mwelekeo enenda ukajipange tena kwa UONGO Mwingine.

 12. Mile,

  Twende kwa utaratibu, nijibu maswali niliyokuuliza kisha tuendelee na hoja.

  Ukielewa nafasi ya dhiki kuu kutokea ndo utaelewa vema kuwa itawahusu akina nani.

  Hiyo mistari haijasema kuwa Kanisa litapitia dhiki kuu, ila imekuonesha kuwa kuna watu kutoka mataifa mbalimbali watapata wokovu wao kwa kupitia dhiki kuu.

  Ndo maana nimekwambia tufuate mtiririko wa mambo likiwamo kujua kwa nini kuwe na dhiki kuu!

  Ukienda unarukia tu mistari hatutafikia hitimisho makini!

  Twende sawa!

 13. WATU KUTOKA JAMAA,LUGHA NA TAIFA/KANISA WATAPITIA DHIKI KUU.

  SHUHUDIA MAFUNGU HAYA;

  Ufunuo 7:9-10

  9 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;

  10 wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.

  11 Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,

  12 wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina.

  13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi?

  14 Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.

  FUNGU LA 14
  LINATUHAKIKISHIA KUWA WATAKATIFU WATAPITIA DHIKI ILE ILIYO KUU.

 14. Mile,
  Inawezekana unachokisimamia hapa umekisoma tu toka mlengo wa wale wanaoamini kuwa kanisa litapitia dhiki kuu, lakaini hukutafuta uwiano toka kwa wale wenye mlengo wa pili.

  Kwanza maandiko uliyoyatoa ya kitabu cha Matendo 24:21 hayasemi unachodai yanasema.

  Pili, ni kweli kanisa limepitia/linapitia dhiki nyingi, lakini siyo dhiki kuu(Great Tribulation).

  Lakini ningependa kukuuliza mambo machache ili baadae tuendelee kujadili:

  1. Dhiki kuu kuu kusudi lake ni nini?
  2. Israel watampokea lini Kristo kama mwokozi wao?
  3. Kwa nini Neema na Dhiki kuu vifanye kazi pamoja?
  4. Nini tofauti ya ufufuo wa kwanza na ufufuo wa pili (First and second resurrection)?

  1 Thes 4:15 – 17 inasema:
  -15 According to the Lord’s word, we tell you that we who are still alive, who are left until the coming of the Lord, will certainly not precede those who have fallen asleep. 16 For the Lord himself will come down from heaven, with a loud command, with the voice of the archangel and with the trumpet call of God, and the dead in Christ will rise first. 17 After that, we who are still alive and are left will be caught up together with them in the clouds to meet the Lord in the air. And so we will be with the Lord forever.

  Kwa nini watafufuliwa waliolala katika Kristo na si watu wote waliokufa ili kuja kuungana na waliohai kumlaki Yesu?

  Twende point kwa point sasa!

 15. TUSIDANGANYIKE TUSOME MATENDO 14:22

  DHIKI NYINGI
  “wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.”
  MATENDO 14:22

  KIINGEREZA
  “Through many tribulations we must enter the kingdom of God.”
  (Acts 14:22)\

  DHIKI KUBWA YA SIKU ZA MWISHO,
  MATENDO 24:21
  Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe.

  22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.

 16. Fungu hili linatuhakikishia kuwa watakatifu watapitia dhiki kuu.

  “Lakini mara baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni;ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”

  Mathayo 24:29-31

  MWENYE MANENO YA KUTUNGA AIJIBU BIBLIA.

 17. FUNGU HILI LINATUHAKIKISHIA KUWA WATAKATIFU WATAPITIA DHIKI KUU.

  “LAKINI MARA BAADA YA DHIKI YA SIKU ZILE, JUA LITATIWA GIZA, NA MWEZI HAUTATOA MWANGA WAKE, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA; NDIPO ITAKAPOONEKANA ISHARA YAKE MWANA WA ADAMU MBINGUNI;NDIPO MATAIFA YOTE YA ULIMWENGU WATAKAPOOMBOLEZA, NAO WATAMWONA MWANA WA ADAMU AKIJA JUU YA MAWINGU YA MBINGUNI PAMOJA NA NGUVU NA UTUKUFU MWINGI.NAYE ATAWATUMA MALAIKA ZAKE PAMOJA NA SAUTI KUU YA PARAPANDA, NAO WATAWAKUSANYA WATEULE WAKE TOKA PEPO NNE, TOKA MWISHO HUU WA MBINGU MPAKA MWISHO HUU.”
  MATHAYO 24:29-31

 18. MILE,
  Hilo swali nilikuuliza baada ya kuona jinsi unavyotumia/Unavyotafsiri MAANDIKO vibaya.
  Sikulaumu kwani anayepaswa kulaumiwa ni mwalimu wako au dhehebu lako linalofundisha kuwa Bibi Arusi wa Kristo atapitia kwenye Dhiki kuu.
  Hayo ni mojawapo ya Mafundisho ya Mashetani kulingana na 1TIMOTHEO 4:
  MAANDIKO hayana Dosari ila tafsiri zako ni potofu.Pengine hujui nini maana ya dhiki kuu ndio maana unawajumlisha WAOVU na WAKRISTO na kwamba wote watapitia kwenye Dhiki kuu.
  Kama mmejianda kupitia kwenye dhiki kuu hilo ni juu yenu wala halihusiani na Kanisa la Mungu aliye hai.
  Nitarejea na MAANDIKO yanayoonesha kuwa WAKRISTO hawatapitia kamwe kwenye Dhiki kuu bali WASIOAMINI wao watapitia.
  SWALI;
  BWANA YESU alikuja Duniani kwa kusudi gani/kufanya nini?

 19. Mile,
  Be careful, kuna batton una-press zinalia off key.
  Kuna vitu unavichukulia juujuu na kudhani kuwa uko sawa lakini kumbe umechepuka!

  Katika ule mfano wa gharika ya Nuhu kuna kitu hujakiona :
  Subject katika hiyo paragrafu ni kuja kwa mwana wa Adamu
  (Yesu), kumefananishwa na kuja kwa gharika ya Nuhu.
  Gharika iliwakutiliza watu, kama ambavyo Yesu atawakutiliza watu.
  Kwa hiyo kilicho-take away watu kilikuwa ni gharika wakati wa Nuhu, na kitakachotake away watu wakati wa Yesu kitakuwa ni Yesu mwenyewe.

  LazimA uelewe Take away ya gharika ilikuwa ni kuwatake away watu kuwapeleka wapi.
  Kisha uelewe take awaya ya Yesu itakuwa ni kuwatake away watu kuwapeleka wapi, ndipo utaelewa mlinganyo wa huo mfano!

  Take away ya gharika is for destruction
  Take away ya Yesu is for safety

  Waliokuwa taken away wakati wa gharika ya Nuhu waliangamia( yaani maji yaliwatake away for destruction).

  Ulipoimiss point ni kwenye taking away ya Yesu, kule kudhani kwako kwamba sentensi ‘take away, inamaanisha kuchuliwa kwa ajili ya kuangamizwa, kwa kuwa ati waliokuwa taken away na gharika waliangamizwa, kwa hiyo na watakaokuwa taken away na Yesu wataangamizwa halafu wale waliachwa ndo watapona.

  Jesus will not take away people for destruction!!
  Here is the opposite; watakaokuwa taken away na Yesu ndo watakuwa wanawekwa mahali pa salama, na watakaoachwa ndo watakuwa shidani.

  The word Take away does not mean to set apart something for destruction!

  Ndo nimeanza kukufuatilia, nitakurejelea baadae!!

 20. Wakristo watapitia dhiki kuu

  MARKO 13:19,20
  19.Kwa maana siku hizo zitakuwa na dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe.

  20 Na kama Bwana asingalizikatiza siku hizo, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku hizo.

  2 Wathesalonike 2:1-2

  1 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.

  2 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

  Yesu yuko na kanisa mpaka ukamilifu wa dahari yaani mwisho wa dunia,Yesu hata acha hata chembe ya watu wake siku ya mwisho..kunyakuliwa kabla ya dhiki huonyesha kundi mmoja la walio nusu nusu wema na nusu nusu waovu kuachwa na kurudiwa baaadae,hilo si kweli.

  MATHAYO 28:19,20

  19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

  20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

 21. MILE,
  Kuna jambo sijalielewa vizuri kuhusu Kanisa la Bwana Yesu Kristo (Bibi Arusi).
  Unamaanisha kuwa Kanisa la Mungu aliye hai litapitia kwenye Dhiki kuu?
  Naomba unisaidie kwa hilo.

 22. wakati wa mwisho haionyeshi watu wema kuondoka kwanza kama wengine wanavyodhani ili kuwaacha wachafu (unyakuo) bali waovu kuharibiwa/taken away by death kwa mng’ao wa utukufu na walioachwa/waliopona mwonekano wake kukusanywa na malaika juu..Mungu wetu ni moto ulao
  MATHAYO 13:30
  Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
  Yesu katika Mathayo 24:37 Yesu anasema;
  kama wakati wa Nuhu mafuriko yakawachukua, ndivyo
  halafu anatoa mfano wa wawili,wakisaga mmoja kuchukuliwa,mmoja kuachwa,
  halafu wengine wakilala kitanda kimoja mmoja kuchukuliwa mmoja kuachwa.
  kumbuka Yesu amesema,kama wakati wa Nuhu: mafuriko yakawachukuwa..ndivyo itakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu
  1.PIMA NI KIPI KINACHUKULIWA/KIPI KINAACHWA?
  2.NINI KINACHOCHUKUA?
  Kundi mmoja ni bibi harusi wa shetani-MAUTI
  kumbuka kundi mmoja,ni bibi harusi wa Yesu-UZIMA

 23. Maneno Kuchukuliwa na Kuachwa yameandikwa hivi katika kiingereza;
  Taken away na Left behind
  Wakristo tumegeuza fundisho hili tukidhani kuwa taken away, ni kuwa unafaa kwa ufalme wa mbinguni…. Kumbe Left behind ndiye anayefaa.

  Matthew 24:37-42 …’But as the days of Noah were, so shall also the coming of the Son of man be. For as in the days that were before the flood they were eating and drinking, marrying and giving in marriage, until the day that Noe entered into the ark, and knew not until the flood came, and took them all away; so shall also the coming of the Son of man be. Then shall two be in the field; the one shall be taken, and the other left. Two women shall be grinding at the mill; the one shall be taken, and the other left. Watch therefore: for ye know not what hour your Lord doth come.’

  Yesu anatumia maneno;
  took them all away: kuchukuliwa
  shall be taken away and the other left.

 24. SCOFIELD KWA KUINGIZA MAWAZO YAKE MIAKA 200 ILIYOPITA KUWA KANISA LITANYAKULIWA KABLA MPINGA KRISTO HAJASIMAMA WAZI KUASI, AMBAYO KAMWE KANISA HALIKUWAHI KUYAFIKIRI AMEWAWEKA WENGI KATIKA MTEGO WA KUTOJIANDAA NA DHIKI KUU.

  BIBLIA IKO WAZI KWA WALE WALIO TAYARI KUISIKIA, NA HAIKO WAZI KWA WALE WANAOSIKIA MAPOKEO NA MANENO YA WATU.

  “LAKINI MARA BAADA YA DHIKI YA SIKU ZILE, JUA LITATIWA GIZA, NA MWEZI HAUTATOA MWANGA WAKE, NA NYOTA ZITAANGUKA MBINGUNI, NA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA; NDIPO ITAKAPOONEKANA ISHARA YAKE MWANA WA ADAMU MBINGUNI;NDIPO MATAIFA YOTE YA ULIMWENGU WATAKAPOOMBOLEZA, NAO WATAMWONA MWANA WA ADAMU AKIJA JUU YA MAWINGU YA MBINGUNI PAMOJA NA NGUVU NA UTUKUFU MWINGI.NAYE ATAWATUMA MALAIKA ZAKE PAMOJA NA SAUTI KUU YA PARAPANDA, NAO WATAWAKUSANYA WATEULE WAKE TOKA PEPO NNE, TOKA MWISHO HUU WA MBINGU MPAKA MWISHO HUU.”
  MATHAYO 24:29-31

  KUTOKA KATIKA BIBLIA MAMBO YAFUATAYO YATATUSAIDIA ILI MAWAZO YA SCOFIELD YANAYOENDA TOFAUTI NA BIBLIA YASIDANGANYE.

  1. BAADA YA DHIKI YA SIKU ZILE
  2. NDIPO ITAKAPOONEKANA ISHARA YAKE MWANA WA ADAMU MBINGUNI;
  3. MATAIFA YOTE YA ULIMWENGU WATAKAPOOMBOLEZA.
  4. NAO WATAWAKUSANYA WATEULE WAKE TOKA PEPO NNE,

 25. Kanisa litanyakuliwa kabla ya kuanza kwa utawala wa mpinga Kristo. Na mara Kanisa litakapoondoka tu mpinga Kristo ataanza kutawala. soma Wathesalonike 2:6-7.

 26. My brethren…
  I was doing my little research about end time prophecies. i found out something very interesting about “rupture” au unyakuo can be define as “taken away of church” which means taken out of the earth lakini hakuna neno linaitwa rupture au unyakuo kwenye bible. let me show you when the church is going to be taken away.

  “Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpaka yule ANAYEMZUI AONDOLEWE”( 2 Thesallonians 2:7)

  Kanisa ndo linazuia mpinga kristo asitokee…. kwa sababu hiyo basi lazima kanisa liondolewe duniani yaani Unyakuo halafu ndo ile miaka saba ambayo mpinga kristo ataweka agano na israel ndo itaanza…. baada ya miaka saba The King of Kings will return to destroy mpinga kristo, kwa hiyo church itachukuliwa kabla ya 7 years Tribulation haijaanza,

  Halafu ukisoma ufunuo kuanzia chapter 4 hadi chapter ya mwisho, matendo yote yanayotokea hapo kanisa litakuwa limeshaondolewa duniani soma kwa makini sana .

  Asanteni hako ndo kamchango kangu kadogo… May the Ancient of Days Bless you all, in Jesus Name.

 27. I dont really care about Pre- trib or Post-trib rupture, as long as i continue to believe in Jesus then heaven is mine.

 28. Wewe uliyeuliza kwamba, kanisa litanyakuliwa wakati gani” naomba utupe fungu katika biblia linalosemea kunyakuliwa kwa kanisa, ili ujibiwe inavyopasa.

 29. Reading 1 1 Thes 4:13-18

  We do not want you to be unaware, brothers and sisters,about those who have fallen asleep,so that you may not grieve like the rest, who have no hope.For if we believe that Jesus died and rose,so too will God, through Jesus,bring with him those who have fallen asleep.Indeed, we tell you this, on the word of the Lord,that we who are alive, who are left until the coming of the Lord,will surely not precede those who have fallen asleep.For the Lord himself, with a word of command,with the voice of an archangel and with the trumpet of God,will come down from heaven, and the dead in Christ will rise first.Then we who are alive, who are left,will be caught up together with them in the cloudsto meet the Lord in the air.Thus we shall always be with the Lord.Therefore, console one another with these words.

 30. Bwana Yesu asifiwe wapendwa wote
  napenda kutoa mchango kama ifuatavyo kanisa litanyakuliwa kabla ya kuanza utawala wa mpinga kristo ambao utadumu kwa kipindi cha miaka saba kwa nini kanisa kunyakuliwa. kanisa linanyakuliwa ili kuepusha na mateso ambayo yatakuwepo kuwatesa watu wote ambao hawamwini yesu kama Bwana na mwokozi katika maisha yao.( kukataa kuokoka)
  Yesu alikuja kumwokoa mwanadamu aliyepotea katiak dhambi leo watu wanapenda Dunia kuliko kupenda Yesu Biblia inasema mtu akipenda Dunia kupenda mungu hakumo ndani ya mtu huyo
  kupenda dunia inamanisha nini ni kuishi mbali na kweli ya neno la Mungu.kufanya dhambi kama uzinzi,wizi,ufisadi au matendo yote ya mwili Biblia inasema watu wa namna hiyo hawataulidhi ufalume wa mungu
  Wapendwa acheni ubishi juu ya neno la Mungu Biblia iansema kutakuwa na mateso ambayo hayajapata kutokea watu watatamani kufa kifo kitawakimbia kwa nini uje uangamie bila sababu ebu mwamini Yesu leo acha Dhambi wewe njoo kwa Yesu Yesu anakuita wewe

  Balikiwa sana

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s