Lijue Neno kwa ajili yako Mwenyewe!

biblia

Jitahidi (Jifunze) ili kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu,  mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa usahihi Neno la kweli (2 Timotheo 2:15),

Kwa wewe kuishi maisha ya furaha, na kuwa udhihirisho kamilifu wa mapenzi, haki, na utukufu wa Mungu, unatakiwa kulijua Neno wewe mwenyewe na kuishi kwa Neno. Wale wasiolijua Neno la Mungu ni kwa tabu sana wanaweza timiza ile shauku na mipango ya Mungu katika maisha yao. Neno la Mungu lilikufanya wewe (1 Petro 1:23), hivyo usipoishi kwa Neno, hautokuwa yule “wewe” Mungu aliyemtazamia, wala hautotimiza hatma Yake Kwako. Hii ndio sababu tunafundisha Neno na kuwatia moyo watoto wa Mungu kuwa wanafunzi wa Neno. Ni lazima ulijue Neno kwa ajili yako mwenyewe (lijue wewe mwenyewe).

 Usiishi katika viwango vya kudhania.  Usiache watu wakuhamasishe (wakushawishi) na mitazamo yao ya “kidini” kuhusu Mungu. Usikubali kwamba kitu fulani kinatoka kwa Mungu kwa sababu tu kinasikika kama chema, kizuri ama cha kidini.

Yesu Alisema katika Yohana 5:39, “Chunguzeni maandiko…” ; Paulo alisema katika 2 Timotheo 2:15, “Jitahidi (Jifunze) ili kujionesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukilitumia kwa usahihi Neno la kweli.” Neno la Mungu ni ufahamu wa Mungu uliodhihirishwa; ni mapenzi Yake katika maandishi na yaliyoelezewa kwa ajili yetu. Ni faida ya ajabu namna gani hii, kwamba unaweza jifunza Neno wewe mwenyewe, ukalielewa, na kuliishi! Ni baraka kuu.

Kipimo cha maisha yako ya kitukufu na ushindi kitakua ni, kiwango gani cha maanifa ya Mungu unacho, na ni kiasi gani unakitendea kazi. Si umekuwa Mkristo muda mrefu kiasi gani; bali ni unajua Neno vizuri kiasi gani na kulitumia. Shukurani kwa Mungu tunayo faida isiyolinganishwa ya uwepo wa Roho Mtakatifu ukaaoa ndani yetu, Ambaye Hutupatia uelewa wa Neno! Yeye Ndiye mtunzi wa maandiko; hivyo unapojifunza, unaweza kumtegemea Yeye ili kukuongoza, na kukupatia kuona katika mafumbo na siri za ki-Ungu.

 Lipatie Neno umakini na muda wako. Jifunze na uliwekee moyo wako. Kama unataka kuishi maisha yaliyopita ukawaida, ni kwa Neno, kupitia nguvu ya Roho Mtakatifu.

Imetafsiriwa kutoka kwa Mchungaji Chris Oyakhilahome

Advertisements

One thought on “Lijue Neno kwa ajili yako Mwenyewe!

 1. Ndugu mteule

  Makala hii inasisitiza jambo la kweli na muhimu mno.
  Hata hivyo natala utazame jambo hili kwa jicho lingine.Katika 2Tim 2:15 kuna
  maandiko yanasema …….UKILITUMIA
  KWA HALALI NENO LA KWELI.

  Kwahiyo tunapaswa kulielewa neno la Kristo na kulitumia KWA HALALI.Kuna
  watumishi wengi leo WANALITUMIA NENO LA MUNGU ISIVYO HALALI.
  Wanasisitiza kuhusu umuhimu wa kuliishi neno la Mungu lakini wakati huo
  huo wanalitumia kuwafanya watu wawe
  mateka wa shetani.

  Si kila anayesisitiza jambo jema ana lengo jema wakolosai 2:18.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s