Tuendelee Kuombea UCHAGUZI

3

Bwana Yesu asifiwe!

Wakati kampeni zinaendelea na tarehe ya Uchaguzi inazidi kukaribia unakumbushwa kuendelea kuuombea Uchaguzi Mkuu unaofanyika siku ya Jumapili ya Tarehe 25/10/2015.

Yako mambo mengi ambayo yanahitaji msaada wa Mungu. Wakati unaombea uchaguzi huu unaweza pia kukumbuka kuombea hafuatayo:

– Mungu awape afya njema wagombea wote hadi uchaguzi ukamilike.

– Mungu aepushe ajali za misafara ya kampeni.

– Hila zozote mbaya kinyume na uchaguzi zikadhihirike na kuharibiwa

-Hekima, maarifa na Uzalendo vikatawale kampeni ili kuepusha vurugu na mifarakano isiyo ya lazima!

Mungu akubariki unapoendelea kuombea Uchaguzi huu.

Advertisements

8 thoughts on “Tuendelee Kuombea UCHAGUZI

 1. watanzania tusisubiri kuomba pale a,bapo mambo yatakuwa yameharibika bali tutie bidii sasa hasa kwa siku hizi zilizobaki kuelekea kupata historia mpya ya tanzania

 2. Ukisoma Mithali 21:1 Moyo wa Rais upo katika mkono wa BWANA, na Mungu anao uwezo wa kuugeuza anakotaka. Pamoja na maombi tunayoendelea kuomba kwa ajili ya uchaguzi, ninaomba uende mbele kidogo kuomba kwa ajili ya watakaoshinda uchaguzi ili waweze kulitumikia kusudi la Mungu, Mungu awape washauri wenye hekima ya Mungu, watakaomshauri katika njia ya adili na ya baraka. Omba pia kwa ajili ya watakaoshindwa kwenye uchaguzi waweze kukubali matokeo na kutofanya hamaki wala kuhamasisha vurugu. MUNGU AKUBARIKI MPENDWA.

 3. Amina, ni kweli kabisa wapendwa tusimame tuombee uchaguzi huu, na hayo yote aliyoyasema mtoa mada hii, zaidi ya yote kuwa zaidi ni kuombea Mapenzi ya Mungu yatimizwe, kwa kuwa mapenzi yake kwetu ni mema kila siku, na yeye anasema mawazo anayotuwazia ni mema kila siku. Tunachotakiwa ni kuwa……haja zetu zijulikane mbele zake na tumwachie yeye ajibu, na tusijishughulishe na jambo lolote zaidi ya kuomba na kusali.
  Mungu ni mwema na atatuepusha na majaribu yote na atatupa kiongozi anayetufaa,
  Amina

 4. Juliana King, Mungu anaandikwa kwa herufi kubwa. unless kama unamaanisha mungu mwingine.

 5. Ndiyo nitapenda kufanya hivyo kwa taifa letu.Pia nilikuwa naomba maombi yenu Kama nitaweza kupata namba zenu za haponitafurahi zaidi Siwezi kuja huko tz nifike kwenye studio yenu mungu awabariki ×70 elfu nasikiliza radio safina masaa yote inanifundisha mengi ya kunua mungu wangu zaidi na zaidi Asante sana God bless

  Sent from my Samsung GALAXY S5

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s