MAONO JUU YA TANZANIA

tanzania

 

HAYA NDIYO MAONO NILIYOYAONA KWA NCHI YETU TANZANIA KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI.

Naliona bendera ya Taifa letu ikiungua na kutoa majivu kisha nikaona zaidi haya.

Najua wengine watadhihaki na wengine watatilia maanani.
(1)Naliona kiongozi mkubwa wa siasa mwenye mvuto mkubwa nchini akifariki Dunia siku chache kabla ya uchaguzi na kuzuka taflani kubwa nchini.Hii itagusa nchi nzima kuliko vifo vilivyotangulia.

Ni kiongozi wa juu wa chama chake,hupenda k ila kutoa maandiko mengi ya biblia akiwa kwenye majukwaa ya siasa(sijaruhisiwa kumtaja jina) nimeambiwa nimweleze na kumwombea na ntafanya hivo.

(2)Vifo sasa vitahamia kwa wanachama na washabiki wa vyama vya siasa,shetani atawaingia wengi nao watachukiana na kuuwana hovyo kila kona.
Si mpango wa mtu bali ni mpango wa shetani na wajumbe wake roho wachafu.

(3)Kutakuwa na uadui mkubwa wa watu na vyombo vya dola kiasi watu wengi hasa vijana hawatawaamini askari polisi na hivo wataamua kufanya majukumu ambayo yangefanywa na polisi na hivyo kuleta mgongano mkubwa,muda mfupi kabla ya kupiga kura na siku ya kupiga kura wataanza kutilia mashaka magari na nyumba za kulala wageni na nyumba za watu binafsi,watakagua bila kushirikisha polisi kwa madai ya kufichua njama za kuiba kura.Polisi wakiingilia patakuwa na mgongano mkubwa.

(4)Naliona kundi fulani likigomea kukubali matokeo ya Uraisi na hii italete shida sana nchini na hata wengine kuwa tayari kufa kwa ajili ya kutetea kile wanachokiita haki. Waliokataa matokeo walisema hata kama hatutawali basi tuunde serikali ya umoja wa kitaifa.

(5)Kwa mara ya kwanza naliona vyombo vikubwa Duniani vikitangaza kwamba Tanzania si kisiwa tena cha amani bali ni mojawapo ya nchi ya machafuko makubwa.
Nimeoneshwa hayo mara kwa mara na roho yangu imekuwa ikifadhaika sana kwa ajili ya nchi yangu Tanzania niipendayo sana.Nilikuwa siwezi yasema kwakuwa muda wa kuyasema ulikuwa haujafika.

Sasa nawasihi watanzania wenzangu tumwombe Mungu na kuomba rehema.
(2Nyakati 7 : 14).
Ahadi ya Mungu ni kwamba tukimuomba kwa dhati.
(a)Atatuma malaika wake kusimamia mchakato wa uchaguzi na kuleta usawa.
(b)Atawaadhibu yeye mwenyewe wale wote wenye nia mbaya na kuiharibu nchi.
(c)Atatupatia viongozi wanaostahili.
(d)Atailinda nchi na kuifunika kwa mbawa za amani.

*Unapoomba rehema ungama kwa ajili ya viongozi/wagombea wote wanaoenda kwa waganga na wachawi maana shetani hutumia mwanya huo kutaka kafara na damu za watu.
*Ingia katika maombi ya kufunga kuanzia sasa mpaka uchaguzi hasa tarehe 20 hadi 29 baada ya uchaguzi.
*Sina chama nachoshabikia bali namwombea kila mtanzania bila kujali itikadi yake.Ili uweze kuomba ipasavyo weka uvyama pembeni tuombe kwa mwelekeo wa utaifa na wala si uvyama.

*Sijayaandika haya kuwatisha watu bali nimesema niliyooneshwa ili wacha Mungu wameombe Mungu atuepushe na majanga hayo.

Je,uko tayari kufunga na kuomba Mungu atuepushe na haya yasitokee kwa nchi yetu Tanzania?

Apostle Mtalemwa Dionis 17th October 2015.

Advertisements

7 thoughts on “MAONO JUU YA TANZANIA

 1. Apostle Mutalemwa,
  Hayo uliyoyaona, hebu rudi tena magotini uyakague maana Mungu akikuonesha jambo ktk jinsi ya kutokea kwake, kama alivyomuonesha Nuhu jinsi dunia itakavyoangamizwa, hakuinuka na kuwaambia watu waingie ktk maombi ili Mungu alibadili jambo hilo bali aliendelea ktk Ono hilo na kutengeneza safina, vivyo Sodoma walitolewa; basi hebu lifafanue vizuri hilo ono lako, ulioneshwa ono kweli au ni ndoto zilizozaliwa ktk hofu?

 2. HE is God of mercy na fadhili zake ni za milele.Tunapoomba toba na kujinyenyekeza yeye ni MWAMINIFU na huiPONYA nchi.

  Tunamshukuru Mungu kwa Haki na Amani zaidi sana tunaomba ulinzi kwa kila liyemchagua kwa KUSUDI lake asimamie ufalme wa Mungu kuanzia udiwani,ubunge na uraisi.

  najifunza kitu …unapozidi kuomba sana roho ya kulalamika inatoka ndani yako maana hata linapokuja suala la kukusababisha ulalamike linabadilika kuwa prayer request.

  Mungu atupe kanisa nguvu,utayari ILI kusimama katika nafasi yetu. kanisa ndio tunabeba nchi ,ndio tunaamua Mungu atawale au la. kanisa tumefanywa kuwa kuhani wa Mungu.
  tukumbuke nafasi zetu…tusijisahahu tukaongea na kutenda kama wengine wasio mjua wala kumtumaini Kristu.

  SHALOM kanisa la Tanzania.

 3. Kwakua Mungu Wetu Ni Mungu Wa Rehema Na Fadhili Nyingi Na Mpango Wa Mungu Ni Thabiti Basi Naamini Mpango Wa Shetani Hauna Nguvu Katka Jina La Yesu Kristo! Amen.

 4. KATIKA JAMBO LA KUMSHANGAA MUNGU NI PALE NINYI WATUMISHI
  WAKATI WA MAONO MNAPOANGUKA KIFUDIFUDI NA KUWA MACHO HUKU MMEKATA PUMZI,HUKU MMEFUMBUA MACHO.

  “ASEMA, YEYE ASIKIAYE MANENO YA MUNGU, YEYE AONAYE MAONO YA MWENYEZI AKIANGUKA KIFUDIFUDI,AMEFUMBULIWA MACHO.”
  HESABU 24:4

 5. Sijaelewa vizuri jambo hili, mambo hayo uliyooneshwa yakitukia, je,si ni lazima yawe hivyo ulivyoyaona ili hiyo ndoto yako idhihirike! Au baada ya ndoto hiyo, ulioneshwa kwamba maombi na mfungo vyaweza kuligeuza jambo hilo?

 6. Nami nmepata msukumo wa kutubu, kufunga na kuomba kwa ajili ya Tanzania.. Asante mtumishi wa Mungu aliye Hai kutufahamisha.. Ubarikiwe

 7. Mungu Mwingi wa Rehema Atusamehe dhambi zetu zote na kutuepusha na janga hili linaloinyemelea nchi yetu. Mungu Akubariki wewe Mtumishi uliyeonyeshwa haya!

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s