Kupiga Kura kabla ya Kwenda Kanisani!

 

wpid-images.png

 

Bwana Yesu asifiwe mpendwa!

Kupiga kura ni HAKI ya msingi ya kila raia katika nchi yake kama ambavyo Tarehe 25/10/2015 Tanzania inakwenda kuchagua viongozi wapya kuanzia Rais wa nchi hadi Viongozi wa Ngazi za Mitaa!

Uchaguzi utfanyika Jumapili, siku mbayo inatumika na wengi kuwa ni siku yakukusanyika Kumuabudu Mungu na Kujifunza mambo mengine yahusianayo na mambo ya Kiroho!

Uchaguzi utaanza mapema asubuhi hivyo kuwahi ni vizuri ili kukamisha zoezi hilo lenye kuamua hatma ya nchi yetu!

SWALI: Je, Kuamka asubuhi na kwenda KUPIGA KURA KWANZA ndipo mtu aende Kanisani kuna ubaya wowote kwa Mkristo??

Advertisements

10 thoughts on “Kupiga Kura kabla ya Kwenda Kanisani!

 1. Pendael,

  Umetudanganya, kuna makosa mengi sana ya kiufundi kwenye chapisho lako. Wewe ndo hujui juu ya kile unachokisema kuliko wale unaowasema kuwa hawajui.

  Hujui maana ya kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake.
  Hujui maana ya sabato na matumizi yake, zaidi sana wewe ndo unaonesha kuwa unatukuza siku kuliko Mungu.

  Unasema habari za watu kutokuhoji kwa nini siku ya kupiga kura ni Jumapili, lakini hapa SG tulishajadili vizuri tu kuhusu hilo suala, wewe ndo hujafuatilia.

  Bila shaka wewe unaona suala la kupiga kura siyo sahihi, labda tupe maandiko ya kulithibitisha hilo ili tujui kama kweli unajua unachokisema.

  Ndo hivyo!

 2. Mathew Tambukwa,
  Umenena vyema ndugu yangu.
  Wapo watu “Wanaojiita” Wakristo wakati hawana sifa stahiki za Ukristo.
  Hebu tazama jinsi watu wasivyojitambua;
  1.Suala la kupiga kura wanaona ni sahihi, tena upigagi kura wenyewe ni siku ya Jumapili.
  2.Wanatetea kuwa, kuwahi kupiga kura ni sahihi badala ya kwenda Ibadani kwanza.
  Hawa wameshaona ibada zao hazina uungu ndani yake na mungu wao ni wa Dunia hii.
  3.Hawa “wanaojiita” Wakristo hawana hata chembe ya msimamo, bora Waislamu wana msimamo.
  Hawajawahi kuhoji, kwanini Serikali wamepanga Siku ya Jumapili iwe ni siku ya Kupiga kura.
  4.Wengine walibadilisha siku ya Ibada ikawa Jumamosi badala ya Jumapili na wakawa Wasabato bila kujua.
  5.Hawajui wanaabudu sanamu kama ulivyowaeleza!
  Ibada ya sanamu ni ibada ambayo unatanguliza/unaweka kitu fulani mbele kabla ya Mungu.
  Mfano mzuri; kupiga kura kabla ya kwenda ibadani ni ibada ya sanamu .
  MATHAYO 6:33
  ” Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”
  SWALI;
  Neno KWANZA katika mstari huu, humaanisha nini?

 3. Hakuna tatizo,timiza wajibu wako kikatiba na haki yako kiimani. Watanzania na tuongozwe na hekima ya kiMungu katika wakati huu muhimu!

 4. Ni mpango wa Mungu kila taifa lipate kiongozi. Kiongozi wa namna gani na lini apatikane ni mpango w Mungu.

 5. Anza na Ibada kwanza mambo mengine ndipo yafuate! Kwa kuwa utapewa mwongozo hata wa uchaguzi wako katika kupiga kura! Kitu unachokipa umuhimu wa kwanza ndicho unachokithamini. Mpe Mungu kipaaumbele ama sivyo waweza kujikuta kupiga kura imekuwa ibada ya sanamu kwako.

 6. Bwana Yesu asifiwe. Mimi sioni tatizo lolote kusali baada ya kupiga kura ila kutokana na tangazo kuwa siku hiyo hawataki watu wakae zaidi ya watatu pamoja karibu na kituo cha kupigia kura, hivyo inawezekana kanisa lako likawa karibu na kituo na waumini wakazidi zaidi ya watatu na kuonekana kama mkusanyiko huoni kama huko ni kutokutii sheria

 7. Bwana asifiwe mpendwa,Hakuna shida yoyote ya mukristo kwenda kanisani asubuhi na kwenda kwenye kura baada ya maombi kwa sababu ni vizuri kumwomba Mungu kabila kila kitu chochote.

  Tuzidi kumwomba Mungu wetu mkubwa Kwa kweli Mungu awabariki wahubiri wa safina . mimi najaribu kila njia kuomba na radio safina lakini tumetofautiana saa 8 lakini ndugu mpendwa mimi sijui nitawa shukuru namna gani kwa mafundisho yenu Mungu ni mkubwa sana nimeteseka sana katika maisha yangu bila kujua nina fanya nini,naitaji msada wenu sana Asante sana Mungu awabariki awazidishie ushindi kubwa mnoJuliana king longidu

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s